Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA JIJINI MBEYA LEO KWENYE MKUTANO WA KAMPENI WA CCM


Rais Kikwete amjulia hali Bwana Charles Kizigha

$
0
0
KIZ1
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mwandishi wa habari Mkongwe wa magazeti ya Serikali ya Daily News na Sunday News Bwana Charles Kizigha nyumbani kwake Mbezi Beach jijini Dar es Salaam jana jioni.Aliyesimama kulia ni mtoto wa mwandishi huyo wa habari Mhe.Angela Kizigha ambaye ni Mbunge wa Afrika Mashariki.Rais Kikwete alimtembelea Bwana Kizigha nyumbani kwake baada ya kupata taarifa kuwa ni mgonjwa(picha na Freddy Maro) 
KIZ2KIZ4

sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali mpya ya Abdalla Mzee

$
0
0
3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa Wananchi jana wakati sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali mpya ya Abdalla Mzee iliyopo Mkoani Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba akiwa katika ziara ya Moahuo kufungua miradi ya maendeleo.
,[Picha na Ikulu.]
2
Waziri wa Afya Rashid Suleiman akisalimiana na Wananchi wakati wa Sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi mpya wa Hospitali ya Abdalla Mzee pia kumkaribisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kutoa hutuba yake katikasherehe hiyo jana,
4
Balozi Mdogo wa China nchini Tanzania anayeishi Zanzibar Xie Yunliang akitoa salamu zake kwa wananchi na Viongozi wakati wa sherehe za  uwekaji wa jiwe la msingi Ujenzi mpya wa Hospitali ya Abdalla Mzee inayojengwa na Kampuni kutoka China Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipoweka jiwe la msingi  katika ziara ya  kufungua miradi ya maendeleo.
1
Baadhi ya wananchi wa Mji na Vitoji vya Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba wakiwa katika sherehe za Uwekaji wa jiwe la Msingi wa ujenzi mpya wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani inayojengwa na kampuni kutoka China jiwe hilo lililowekwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein jana.

WAANDISHI HABARI WA ZANZIBAR WAPATIWA MBINU BORA ZA KURIPOTI HABARI ZA UCHAGUZI MKUU.

$
0
0
 X2
Mwandishi Mkongwe wa Tasnia ya Habari Tanzania ambae pia ni Mkurugenzi wa Internews Tanzania Valerie N. Msoka akifafanua kitu kwa wandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya kuripoti uchaguzi Mkuu.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
X4
Mkurugenzi wa Shirika la Internews kanda ya Afrika Ian Noble akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari juu ya kuripoti habari za Uchaguzi, alipotembelea katika mafunzo hayo huko ukumbi wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Weles Mjini Zanzibar.
X1
Afisa Mwandamizi Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan (aliesimama)akifahamisha kitu katika mafunzo ya siku tano yalimaliza jana Agosti 28 yaliyoandaliwa na Shirika  la Habari la Marekani  Internews  kwa waandishi wa Habari wa Zanzibar katika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye Ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
X3
Badhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo juu ya kuripoti Habari za Uchaguzi Mkuu wakisikiliza nasaha zilizotolewa na Mkurugenzi wa Internews Tanzania Valerie N. Msoka (hayupo pichani) katika mfunzo yaliofanyika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar.
05
Mkurugenzi wa Shirika la Internews kanda ya Afrika Ian Noble (wakatikati) katika picha ya pamoja na washiriki na wasimamizi wa mafunzo hayo (kulia) aliekaa ni Afisa Mwandamizi Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan na kushoto ni Mwandishi Mkongwe wa Tasnia ya Habari Zanzibar Salim Said Salim.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

MBUNGE WA LUDEWA DEO FILIKUNJOMBE APINGWA KUPITA BILA KUPINGWA MCHAKATO WA UCHAGUZI MKUU

$
0
0
 Mgombea Ubunge Jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Msambichaka Mkinga (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akipinga kupitishwa bila kupingwa mgombea mwenzake wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Deo Filikunjombe na kudai kulikuwa na hujuma. Kulia ni Wakili wake, Paulo Kalomo.
  Mgombea Ubunge Jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Msambichaka Mkinga, akionesha fomu namba 10 ambazo alikabidhi kwa Msimamizi wa Uchaguzi. 
 Wakili wake, Paulo Kalomo, akizungumza katika mkutano huo kuhusu sheria inavyoelekeza.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
……………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
 
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Msambichaka Mkinga amepinga vikali kupitishwa bila kupingwa mgombea mwenzake wa jimbo hilo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Deo Filikunjombe na kudai kulikuwa na hujuma.
 
Mkinga alitoa malalamiko hayo mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam jana na kueleleza kuwa sababu zilizotolewa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo kuwa hakupeleka fomu namba 10 hazikuwa na ukweli wowote.
 
“Nilipofika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Ludewa nilisaini na kukabidhi tamko la kuheshimu na kutekeleza maadili ya uchaguzi ya mwaka 2015 (fomu namba 10) na baada ya kusaini nilimkabidhi msimamizi wa uchaguzi pamoja na fomu namba 8B,picha, stakabadhi ya malipo ya dhamana ambapo vilihakikiwa na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Gervas Lupembe” alisema Mkinga.
 
Mkinga alisema katika jambo lisilo la kawaida msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo hilo hakubandika kwenye ubao wa matangazo tamko hilo na alipomfuata msimamizi huyo kumuulizia msaidizi wake Lupembe alikiri kupokea na kuziwasilisha kwa kiongozi wake ili kutia saini ambaye naye alikiri kuzipokea lakini wakati ana bandika tamko hilo la Mgombea wa CCM fomu hiyo hakuiona.
 
Alisema katika pingamizi alilowekewa dai mojawapo ni kutokuwepo  tamko hilo kwenye fomu zake hali inayoonesha wazi kuwa kulikuwa na mchezo mchafu uliofanyika ili kumpitisha Filikunjombe bila kupingwa.
Mkinga alisema kuwa kuwaondoa wagombea kwa sababu zisizo za msingi ni kuiminya demokrasia na kuirudisha nchi nyuma kwani kunaweza kusababisha kukosa viongozi wazuri na kubakia na viongozi wasiofaa na wasiotaka kushindanishwa kwa kuwapa nafasi wananchi ya kumchagua kiongozi wanayemtaka.
 
Mgombea huyo alisema kutokana na sintofahamu hiyo alimuomba msimami wa uchaguzi wa jimbo hilo kutupiliambali pingamizi lililotolewa dhidi yake na mgombea mwenzake ambapo anasubiri majibu baada ya kuandika barua ya malalamiko.

MAGUFULI AMJULIA HALI NA KUMPA POLE MEYA WA JIJI LA MBEYA MH ATHANAS KAPINGA BAADA YA KUPATA AJALI

$
0
0
 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu John Pombe Magufuli akimjulia hali na kumpa pole aliyekuwa Meya wa jiji la Mbeya Mh.Athanas Kapunga aliyepata ajali wilayani Momba mkoani Mbeya wakati wa mbio za maandalizi ya Kampeni hivi karibuni,Mh Kapunga amelazwa kwenye chumba maalum cha wagonjwa  mahututi (ICU) katika hospitali ya Rufaa mjini humo.
 Mmoja wa Wauguzi walioko kwenye chumba maalum cha wagonjwa  mahututi (ICU),akimpa maelezo mafupi Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu John Pombe Magufuli alipokwenda kumjulia hali n kumpa pole aliyekuwa Meya wa jiji la Mbeya Mh.Athanas Kapunga aliyepata ajali wilayani Momba mkoani Mbeya wakati wa mbio za maandalizi ya Kampeni hivi karibuni.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya Wauguzi walioko katika chumba maalum cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Rufaa Mbeya,mara baada ya kumjulia hali na kumpa pole aliyekuwa Meya wa jiji la Mbeya Mh.Athanas Kapunga aliyepata ajali wilayani Momba mkoani Mbeya wakati wa mbio za maandalizi ya Kampeni hivi karibuni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Meya Mama Kapinga mara baada ya kutoka kumjulia hali na kumpa pole aliyekuwa Meya wa jiji la Mbeya Mh.Athanas Kapunga aliyepata ajali wilayani Momba mkoani Mbeya wakati wa mbio za maandalizi ya Kampeni hivi karibuni.

 PICHA NA MICHUZI JR-MBEYA

TAMASHA LA KUOMBEA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU KUFANYIKA OKTOBA 4 MWAKA HUU.

$
0
0
 Muandaaji wa matamasha hapa nchini Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na maandalizi ya tamashala kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu. pia amesema kuwa katika tamasha hilo litahuzuliwa na watu mbalimbali akiwemo mwimbaji mahili wa nyimbo za Injili hapa nchini Rose Mhando pamoja na Solomoni mwimbaji wa nyimbo hizo Solomon Mkubwa ameyasema hayo katika ofisi zake zilizopo kinondoni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya tamasha la kuombea amani,Beno Chelele.


Muandaaji wa matamasha hapa nchini Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na maandalizi ya tamashala kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu. Pia amewaomba watanzania kumuunga mkono katika tamasha hilo litakalofanyika Oktoba 4 mwaka huu  jijini Dar es Salaam.

VIJANA WATANO U-15 WAELEKEA AFRIKA KUSINI

$
0
0

BUNGE LA WATOTO WA SHULE ZA MSINGI MKOANI MANYARA WAFANIKIWA KUWARUDISHA WATOTO WA MITAANI SHULE

$
0
0

Abdallah Waziri - ambaye ni mmoja wa watoto wa mitaani aliyerudishwa shule kwenye kikao cha leo.
Abdallah Waziri, Asia Mtibua na Mwalimu Gaudensia Igoshalimo wakimkaribisha Abdallah Waziri shuleni.
Mmoja wa wajumbe akitoa maoni yake katika kikao  cha bunge katika shule ya oysterbay mkoani manyara.
Mbunge Nasri Selemani akifuatilia hoja kwa makini wakati kikao cha bunge la watoto likiendelea katika shule ya oysterbay mkoani manyara.


 Mbunge Nasri Selemani ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa nyumbani na sasa kwa jitihada za bunge amerudishwa shuleni,,akichangia hoja.
Mtangazaji wa Kipindi cha Tafakari Time Benedicta Mrema akizungumza na Abdallah Waziri na kumkabidhi mchango wa shilingi 57,800 aliochangiwa kwa ajili ya kumuwezesha mahitaji ya shule.
Raisi wa Bunge la watoto Oysterbay, Manyara - Sarah David akitoa hotuba ya ufunguzi wa bunge la watoto katika shule ya oysterbay mkoani manyara.
Wabumbe wa Bunge la watoto Oysterbay Manyara akishangilia hoja.
Wajumbe a Bunge la watoto Oysterbay Manyara akishangilia hoja.
Waliosimama, Abdallah Waziri, Asia Mtibua na Mwalimu Gaudensia Igoshalimo wakimkaribisha Abdallah Waziri shuleni.
MTANDAO wa  Marafiki wa Elimu Babati (BADENET) ulianzishwa mwaka 2012 chini ya uongozi wa Asia Mtibua, mtandao huu ulianzishwa kwa lengo la kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli za elimu pamoja na kuanzisha kituo cha kupashana habari.


Moja ya mafanikio ya BADENET ni kuanzishwa kwa Bunge la Watoto katika shule ya msingi Osterbay mkoani Manyara, bunge hili lilianzishwa kwa lengo la kuwaleta pamoja watoto waliopo shuleni na ambao wapo nje ya shule ili waweze kujadili masuala ya elimu ikiwa ni pamoja na kutafuta njia za kuweza kusikilizwa wao kama watoto. 

Bunge hili la watoto linajumuisha wajumbe 43 (26 wasichana na 17 wavulana) na hukutana mara 1 kwa kila mwezi. Mpaka sasa jumla ya watoto wa mitaani 19 wamerudishwa shuleni na wanasoma, wapo wanaoingia asubuhi na wengine mchana.


Leo hii Bunge la watoto Oysterbay mkoani Manyara limekutana kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili  watoto wa mitaani “Chokoraa” ili kuzungumza namna ambavyo watawawezesha  watoto hao kupata fursa ya elimu kama watoto wengine waliopo shuleni. 

Katika kikao cha leo bunge limefanikiwa kumrudisha shuleni mtoto Abdala Waziri ambapo alichangiwa na wabunge, marafiki wa elimu na walimu jumla ya shilingi 57,800 ili zimuwezeshe kununua mahitaji muhimu ya shule.


Mkakati wa bunge la watoto katika shule ya msingi Osterbay ni kuhakikisha kuwa kila mbunge anamrudisha shuleni mtoto yoyote ambaye yuko mtaani na kuhakikisha wanafurahia fursa ya kupata elimu ambayo ni haki yao ya msingi.

Timu ya Tafakari Time, kipindi kinachorushwa kila siku ya alhamisi kupitia ITV ilishiriki kikao cha leo kwa lengo la kujifunza uendeshwaji wa shughuli za bunge hili la watoto.

MABALOZI IRENE MKWAMA WAZUNGUMZA NA RAIS WA ZANZIBAR

$
0
0
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uholanzi Irene Florence Mkwama alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uholanzi Irene Florence Mkwama alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Mpya wa Jamhuri ya watu wa Algeria Belabed Saad alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi kwa Rais leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Balozi Mpya wa Jamhuri ya watu wa Algeria Belabed Saad alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi kwa Rais leo,[Picha na Ikulu.]

MAFUNZO KUHUSU HUDUMA ZA LESENI ZA MADINI KWA NJIA YA MTANDAO YAANZA RASMI KANDA YA KUSINI

$
0
0
 Mtaalam kutoka  Kitengo cha Leseni, Wizara ya Nishati na Madini, Charles Gombe akielezea hatua za Wizara katika  kuboresha huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal; OMCTP) kwa wachimbaji wa madini (hawapo pichani) mjini Mtwara. Lengo la mafunzo hayo lilikuwa ni kuwapa uelewa  wachimbaji wa madini kuhusu  huduma hiyo pamoja na kuwasajili.
 Baadhi ya wachimbaji wadogo  wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini (hawapo pichani).
 Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Aidan Mhando akifungua mafunzo  kuhusu huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao yaliyoshirikisha wachimbaji wa madini kutoka katika mkoa wa Mtwara.
 Mwenyekiti wa Chama cha  Wachimbaji wa Madini kutoka Mkoa wa Mtwara (MTWAREMA), Festo Balegele akifafanua jambo katika mafunzo hayo.
 Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Aidan Mhando ( wa pili kutoka kushoto, waliokaa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.
 Mtaalam kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mtwara, Juma Namuna akielezea umuhimu wa wachimbaji wa madini kujiunga na mfuko huo  ili kunufaika kwa kupata mikopo.


 Mtaalam kutoka  Kitengo cha Leseni, Wizara ya Nishati na Madini, Pendo Elisha akielezea faida za kujiunga na huduma ya leseni za madini kwa njia ya mtandao katika mafunzo hayo.
 Mchimbaji mdogo wa madini ya chumvi, Hussen Abdalah akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
 Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Aidan Mhando ( wa nne kutoka kushoto, waliokaa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na  wataalam wa Wizara  ya Nishati na Madini na wachimbaji wa madini kutoka Lindi walioshiriki mafunzo ya huduma ya leseni  za madini kwa njia ya mtandao yaliyofanyika mjini Lindi.
Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Paul Mtulo akiweka mitambo sawa kwenye  gari la matangazo la Wizara kabla ya kuanza kwa kampeni ya kuhamasisha wachimbaji  wa madini kujiunga na huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao mjini Lindi.



Na Greyson Mwase, Mtwara

Ofisi ya Madini, Kanda ya Kusini yenye ofisi zake mjini Mtwara imeanza kutoa huduma za leseni  za utafutaji na  uchimbaji  wa madini  ndani ya  siku moja  tofauti na ilivyokuwa awali.


Hayo yalisemwa na Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Aidan Mhando  katika mafunzo  kuhusu  huduma za leseni za madini kwa njia  ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal; OMCTP) yaliyoshirikisha wachimbaji wa madini mkoani Mtwara.


Mhando alisema kuwa awali maombi yalikuwa yakichukua muda mrefu kutokana na changamoto mbalimbali  ikiwemo ya  mtandao na kuongeza kuwa ofisi yake imeboresha mtandao na kuanza kutoa leseni ndani ya siku moja.


Alisema ofisi yake ina uwezo  wa kushughulikia ombi moja  la leseni ndani ya nusu saa iwapo mwombaji  atakuwa amekamilisha  vigezo vyote vinavyotakiwa.


Alieleza kuwa tangu huduma ya mtandao iboreshwe ofisi ya madini imekuwa na uwezo wa kushughulikia maombi  20 kwa siku  tofauti na awali ambapo ilikuwa inachukua muda mrefu.


Akielezea mikakati ya ofisi yake katika utekelezaji wa mfumo mpya wa utoaji wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao, Mhando alisema ofisi imejipanga kwa zoezi  la kuhakikisha kuwa wateja wake wote wanaingizwa katika mfumo huu na kunufaika na huduma hiyo.


Aliongeza kuwa ili kuwafikia wachimbaji wa madini ya chumvi ambao idadi yako kubwa ni wazee, ofisi yake imeweka utaratibu  wa kuwatembelea kwenye maeneo yao  ya kazi, kuwapa elimu  pamoja na kuwasajili kwenye mfumo huu.


Akielezea  faida za mfumo mpya wa huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao Mhando alisema kuwa mfumo utawawezesha wamiliki wa leseni za madini kupata taarifa za leseni zao   wakati wowote pamoja na kufanya malipo ya leseni zao kwa njia ya mtandao yaani M-Pesa, Airtel Money na Tigo Pesa.


“Mfumo huu utapunguza migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara kati ya wachimbaji na kuondoa dhana ya kwamba kuna upendeleo kwenye  utoaji wa leseni za madini.” Alisema Mhando.

SHUKURANI ZA CCM KWA KUJITOEKEZA KWA WINGI SANA KWENYE MIKUTANO

SEHEMU YA HOTUBA YA MWAKYEMBE (VIDEO)

MSD YAZINDUA RASMI TAARIFA YAKE YA MWAKA 2013/2014 (ANNUAL REPORT)

$
0
0

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa MSD, Profesa Idris Ali Mtulia (kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa taarifa ya MSD ya mwaka 2013/2014 uliofanyika Ofisi za MSD Keko jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani.
 Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Johnson Mwakalitolo, akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, Profesa Idris Ali Mtulia, akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mkurugenzi wa Tehama  wa MSD, Issaya Mzolo, akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo.
Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kushoto), akizingumza kwenye uzinduzi huo. Kulia ni Meneja wa Uhasibu wa MSD, Sako Mwakalobo.
Keki ya Birthday ya Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani katika muonekano.
Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani (kushoto), akikata keki hiyo aliyoandaliwa na wafanyakazi wenzake wakati wakimpongeza kutimiza miaka 55 ya kuzaliwa kwake. Kulia ni Katibu Muhtasi wa Mkurugenzi wa MSD, Doreen Josia. Wafanyakazi hao waliamua kumpongeza Mwaifwani baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa ripoti hiyo.
Mwaifwani akimlisha keki, Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja wa MSD, Edward Terry.


Hapa ni zamu ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, Profesa Idris Ali Mtulia akilishwa keki.
Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja wa MSD, Edward Terry, akimlisha keki, Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani.
Hapa Katibu Muhtasi wa Mkurugenzi MSD, Dinah Dileya (kushoto), akilshwa keki.
Ofisa Uhusiano wa MSD, Benjamin Massangya (kulia), akigawa ripoti hiyo kwa wafanyakazi wa MSD.
Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kushoto), akizingumza kwenye uzinduzi huo.
Wafanyakazi wa MSD, wakifuatilia uzinduzi huo.
Wafanyakazi wa MSD, wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Ni furaha tupu katika uzinduzi huo na hafla ya wafanyakazi hao kumpongeza Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani kutimiza miaka 55 tangu azaliwe.
Viongozi wa MSD wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Hii ni timu ya wajumbe walioandaa ripoti hiyo ya mwaka 2013/2014. 'Big Up wajumbe kwa kazi nzuri'

Na Dotto Mwaibale
BOHARI ya Dawa (MSD) imezindua rasmi taarifa yake ya mwaka 2013/2014 (Annual Report), ambayo ilizinduliwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa MSD, Profesa Idris Ali Mtulia.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa taarifa hiyo, Profesa Mtulia alisema kupanda kwa huduma za usambazaji dawa, upatikanaji wa dawa kutoka asilimia 55 hadi 85 ni jambo la kujivunia.

Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani alisema mpango wa MSD kwa sasa ni kuanzisha maduka ya dawa ambayo yataendeshwa na MSD ambapo kwa kuanzia hivi karibuni litazinduliwa mkoani Mbeya na baadae itafuatia mikoa Kanda za  Dar es Salaam, Mwanza na Moshi.

WAANDISHI HABARI WA ZANZIBAR WAPATIWA MBINU BORA ZA KURIPOTI HABARI ZA UCHAGUZI MKUU.

$
0
0
 Afisa Mwandamizi Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan (aliesimama) akifahamisha kitu katika mafunzo ya siku tano yalimaliza jana Agosti 28 yaliyoandaliwa na Shirika  la Habari la Marekani  Internews  kwa waandishi wa Habari wa Zanzibar katika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye Ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
 Mwandishi Mkongwe wa Tasnia ya Habari Tanzania ambae pia ni Mkurugenzi wa Internews Tanzania Valerie N. Msoka akifafanua kitu kwa wandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya kuripoti uchaguzi Mkuu.
 Badhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo juu ya kuripoti Habari za Uchaguzi Mkuu wakisikiliza nasaha zilizotolewa na Mkurugenzi wa Internews Tanzania Valerie N. Msoka (hayupo pichani) katika mfunzo yaliofanyika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar.
 Mkurugenzi wa Shirika la Internews kanda ya Afrika Ian Noble akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari juu ya kuripoti habari za Uchaguzi, alipotembelea katika mafunzo hayo huko ukumbi wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Weles Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Shirika la Internews kanda ya Afrika Ian Noble (wakatikati) katika picha ya pamoja na washiriki na wasimamizi wa mafunzo hayo (kulia) aliekaa ni Afisa Mwandamizi Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan na kushoto ni Mwandishi Mkongwe wa Tasnia ya Habari Zanzibar Salim Said Salim.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

UKAWA WAZINDUA KAMPENI ZAO JANGWANI JIJINI DAR

$
0
0
Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema kupitia Ukawa, Mh Edward Lowassa akiongea na wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa katika viwanja vya Jangwani mapema leo.Mh Lowassa amesema kipaumbele chake kimoja wapo ni Elimu huku akisisitiza kuwa kampeni zao zitakuwa ni za busara na hekima bila kutumia matusi.
Mke wa Mgombea Urais kupitia Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Mama Regina Lowassa akitoa salamu kwa wakazi wa Jiji la Dar Waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za Ukawa katika viwanja vya Jangwani leo.
Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Duni Haji akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa Kampeni za Ukawa leo katika viwanja vya Jangwani
Mwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar Waliojitokeza katika uzimduzi wa Kampeni za Ukawa zilizofanyika Jangwani leo.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mh Freeman Mbowe (wa kwanza kulia) akiwa na wagombea urais kwa Upande wa Zanzibar na Upande Wa Bara na mgombea mwenza bara wakionyesha Kitabu chao cha Ilani ya Uchaguzi mwaka 2015 katika uzinduzi wa kampeni za ukawa uliofanyika katika viwanja vya jangwani.

Halima Mdee akihutubia
 
 Wagombea Ubunge katika majimbo ya Dar Es Salaam wakitambulishwa mbele ya wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa leo zilizofanyika katika Uwanja wa Jangwani.
 Mgombea ubunge wa jimbo la Kisarawe kwa tiketi ya CUF Kingwendu akisikiliza hotuba ya mgombea urais kwa tiketi ya Chadema chini ya Mwamvuli ya Ukawa
 Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Mh James Mbatia akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar Waliojitokeza leo katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa jangwani jijini Dar
 Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu, Mh Fredrick Sumaye akihutubia wakazi wa jiji la Dar waliofika katika viwanja vya Jangwani wakati wa uzinduzi wa kampeni za Ukawa
 Umati wa watu waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za Ukawa katika viwanja vya jangwani leo
 Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema na Mgombea Mwenza wakiwaaga watanzania waliojitokeza katika viwanja vya jangwani katika uzinduzi wa kampeni za Ukawa
Moja ya kifaa cha Kisasa kabisa aina ya Drone ambacho kilikua kikitumika kupiga picha kutoka anagani ambacho kimekuwa kivutio kikubwa kabisa kwa wakazi wa jiji la Dar Es Salaam leo katika viwanja vya jangwani .Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

MAGUFULI AZIDI KUCHANJA MBUGA,AWATAKA WANANCHI WAWEKE IMANI KUBWA KWAKE NA KUMPA KURA NYINGI ZA USHINDI

$
0
0
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Njombe mjini katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa saba saba.Magufuli amesema akichaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano ataendeleza juhudi zake za kujenga barabara kwa kiwango cha lami,amesema dhamira yake aliokuwa nayo ya Uwaziri wa Ujenzi katika kujenga barabara za lami katika maeneo yote hapa nchini.

Amesema tangu kupewa kuwa waziri wa ujenzi ameweza kujenga barabara  zaidi kilomita 7000 nchi nzima,ambapo ilipelekea kuongeza kuongeza pato la mfuko wa barabara kutoka bilioni 73,3 hadi kufikia bilini 866 kwa mwaka huu hivyo ameahidi akiwa rais atajenga zaidi barabara za lami.

Dkt MAGUFULI ambae anaendelea na mikutano ya kampeni za Urais mikoa ya nyanda za juu kusini , amelalamikia udanganyifu wa baadhi ya mitandao ya kijamii  na baadhi ya vyombo vya habari kuripoti  kuwa amelazwa wodi ya wagonjwa mahututi katika hospitali ya mkoa wa mbeya wakati sio kweli.

Aidha pia Magufuli  amewaomba wananchi waweke imani kubwa kwake kwa  kumpa kura nyingi  zitakazomwezesha kuwa raisi wa awamu ya tano,na kIsha alipe fadhira hizo kwa kutatua kero zinazowakabili hasa wananchi wenye kipato cha chini.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Joh Pombe Magufuli akipeana mkono na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara,Ndugu Phillip Mangula mara baada ya kumkaribisha mgombea huyo jukwaani kuwahutubia wananchi wa njombe na kuzinadi sera za chama chake na kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara,Ndugu Phillip Mangula akiwashukuru wananchi wa Njombe waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa sabasaba mjini humo,ambapo pia Ndugu Mangula alimkaribisha mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kuwahutubia wananchi wa njombe na kuzinadi sera za chama chake na kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano
 Wananchi wa Njombe wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa sabasaba mjini Njombe.
 Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM na Mgombea Ubunge wa jimbo la Kyela,Mh Harrison Mwakyembe akiwahutubia wananchi wa Njombe jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
 Waanchi wakishangilia jambo kwenyemkutano wa kampeni wa CCM.

 Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Wanging'ombe Mh. Gerson Lwenge kwa wananchi wa Makoga ndani ya wilaya hiyo ya Wanging'ombe
 Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM mgombea Ubunge wa jimbo la Wanging'ombe Mh. Gerson Lwenge kwa wananchi wa Makoga ndani ya wilaya hiyo ya Wanging'ombe kwa ajili ya kuwaambia wananchi ni namna gani wataiongoza Tanzania katika awamu ya tano. 
  Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Makete Dkt Norman Msigala kwa wananchi wa Makoga ndani ya wilaya hiyo ya Wanging'ombe
 MKutano wa Kampeni ukiendelea. 
 Wananchi wakisikiliza sera za mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,hayupo pichani alipowahutubia jioni ya leo mjini Njombe. 
 Wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Wananchi wakiwa na mabango yao ya kumsifu na kumkaribisha mgombea Urais wa CCM Ndugu John Pombe Magufuli,mara baada ya kufunga barabara alipokuwa akipita katika kijiji cha Mgagala akielekea mkoani Njombe kwenye mkutano wa kampeni
 Wananchi na Mabango yako
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Makoga katika wilaya ya Wanging'ombe mapema leo mchana.
 Wananchi  wa kijiji cha Ikonda wakimsikiliza Dkt Magufuli 
 Bango .



MABALOZI WAZUNGUMZA NA DK.ALI MOHAMED SHEIN.

$
0
0
????????????????????????????????????
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uholanzi Irene Florence Mkwama alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais leo.????????????????????????????????????
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uholanzi Irene Florence Mkwama alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais leo,
????????????????????????????????????
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Mpya wa Jamhuri ya watu wa Algeria Belabed Saad alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi kwa Rais leo,
????????????????????????????????????
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Balozi Mpya wa Jamhuri ya watu wa Algeria Belabed Saad alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi kwa Rais leo.

RAIS KIKWETE AZINDUA KAMPENI YA MAMA ONGEA NA MWANAO

$
0
0
w1
Wasanii wa Filamu nchini Wema Sepetu na Steven Nyerere wakimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam kuzindua Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao illi aipigie kura CCM.Kampeni hiyo imeratibiwa na Wasanii wa filamu wakuongozwa Wema Sepetu na Steven Nyerere.w2
Msanii wa Filamu Bi.Wema Sepetu akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete tuzo maalum kwa kutambua mchango wake katika kulinda na kuthamini kazi za wasanii nchini ambapo katika kipindi chake cha uongozi wamepata manufaa makubwa.Wema alikabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya  baadhi wasanii wa filamu na Muziki nchini wanaoshiriki katika kampeni ya Mama Ongea na Mwanao yenye lengo la kuwahimiza wanawake kuwahimiza watu kuipigia kura CCM kwa kuwachagua wagombea wake katika uchaguzi mkuu mwaka huu.w5w6
w3
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao.(picha na Freddy Maro)

BANK OF AFRIKA TANZANIA YAKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 210 KUSAIDIA MATIBABU YA WOTOTO WANAOZALIWA NA MIGUU ILIYOPINDA

$
0
0
  Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa nchini Bw. Ammishadai Owusu-Amoah akimkabidhi Ofisa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT mfano wa hundi wenye ya dola za kimarekani 100,000 kwa ajili ya matibabu ya watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda. Nyuma ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassani Mwinyi na Mwenyekiti wa Bodi ya Bank of Afrika Mwanaidi Majaar.
 Balozi Mwanaidi Majaar,Mwenyekiti wa Bodi Bank of Afrika akihutubia wadau mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo. Balazo anasema BOA wamejizatiti kurudisha kwa jamii wanayoihudumia na harambee ya kutibu watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda ni moja ya mafanikia ya taratibu wao.
 Matembezi ya hisani ya pamoja yaliyoandaliwa na BOA na CCBRT hospitali kutoka Leaders clup mpaka CCBRT kuadhimisha kilele cha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya matibabu ya watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mh. Ali Hasssan Mwinyi akihutibia na kupongeza kwa dhati juhudi zilizofanya na zinazoendelea kufanywa na  Bank of Africa kwa kujali jamii na kuhusia wadau wengine pia kuiga mfano wa BOA
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mh. Ali Hasssan Mwinyi akimsalimia mtoto aliyeshiriki katika matembezi hayo.
Matembezi ya hisani  kuadhimisha kilele cha ukusanyaji fedha yakiendelea kueleka hospital ya CCBRT

NA  FRANCIS DANDE

RAIS wa Awamu ya Pili, Ali Hssan Mwinyi, jana aliongoza  matembezi ya hisani ya kilometa tatu kutoka Leaders Club, Kinondoni hadi Hospitali ya CCBRT Msasani kwa ajili ya kuchangia  matibabu ya watoto waliopinda miguu.

Matembezi hayo yaliyodhaminiawa  na Benki ya Afrika - Tanzania, lengo kuu lilikuwa ni kukusanya dola za marekani laki moja kwa madhumuni ya kugharamia watoto wenye miguu iliyopinda nchini kote. Ilikuwa ni kilele cha kampeni ya  ukusanyaji wa dola za Marekani laki moja iliyozinduliwa mwezi Aprili mwaka  huu.
Kupatikana kwa fedha hizo kutawezesha  CCBRT kutoa matibabu ya gharama nafuu kwa watoto  400 wenye ugonjwa wa kupinda miguu nchini kote,ilikuyabadili  maisha  yao na kuwa  ya kawaida.
Akizungumzia kuhusu tukio hilo jana,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya  Benki ya Afrika – Tanzania, Mwanaidi Maajar, alisema: “Benki ya Afrika – Tanzania imedhamiria kurejesha kwa jamii kile  inachopata  kwa kuwa inaendesha  shughuli  zake, kwa kuchangia mahitaji mbalimbali ya jamii husika. Tumeona umhimu wa kuhimiza  usaidizi katika suala hili jema, kwa kuwa  CCBRT inatoahuduma kawa jamii maskini kwa kuondoa vikwazo mbalimbali ili jamii husika iweze  kupata  matibabu,” alisema Mwanaidi .

Aidha , Ofisa Mendaji mkuu wa CCBRT,Erwin Telemans alisisitiza: “ CCBRT inatoa shukrani za pekee kwa  Benki ya Afrika –Tanzania kutokana na ukarimu wao katika kipindi chote  cha kampeni hii. Maisha ya  a mamia ya  watoto wenye ugonjwa wa kupinda miguu watapona kwa uhakika kutokana na matibabu watakayopatiwa na CCBRT, na hatutaweza kuya badili maisha  ya watoto hao bila  kupata msaada kutoka kwa washirika wetu wakarimu kama Benki ya Afrika – Tanzania.”
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images