Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

TANGAZO KWA UMMA.

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

JESHI LA POLISI TANZANIA



JESHI LA POLISI TANZANIA LINAWAJULISHA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2014, KIDATO CHA NNE MWAKA 2014 NA JKT MWAKA 2015 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI KUWA WANATAKIWA KURIPOTI KWA MAKAMANDA WA POLISI WA MIKOA TAREHE 28/08/2015 KWA AJILI YA MAANDALIZI YA USAFIRI WA KWENDA SHULE YA POLISI TANZANIA

TAREHE 29/08/2015.


KILA MMOJA ATATAKIWA KUWA NA NAULI YA KUMWEZESHA KUSAFIRI TOKA MAKAO MAKUU YA MKOA ANAKOANZIA KUSAFIRI HADI SHULE YA POLISI MOSHI NA ATAREJESHEWA NAULI ATAKAPOFIKA CHUONI BAADA YA KUWASILISHA TIKETI YA SAFARI. AIDHA TAREHE YA MWISHO YA KURIPOTI CHUONI NI TAREHE 05/09/2015 NA ATAKAYERIPOTI BAADA YA HAPO HATAPOKELEWA.


AIDHA VIJANA HAO WATALAZIMIKA KUFIKA SHULENI WAKIWA NA VITU VIFUATAVYO :

1.VYETI VYAO VYOTE VYA MASOMO (ORIGINAL ACADEMIC CERTIFICATES/RESULT SLIP PAMOJA NA LEAVING CERTIFICATES) KIDATO CHA NNE, SITA NA VYUO.

2.VYETI HALISI VYA KUZALIWA (ORIGINAL BIRTH CERTIFICATES). HATI YA KIAPO CHA KUZALIWA HAITAKUBALIKA.

3. MASHUKA MAWILI RANGI YA BLUU BAHARI (LIGHT BLUE)

4.CHANDARUA CHENYE UPANA FUTI TATU

5.NGUO ZA MICHEZO (TRACK SUIT NYEUSI,T-SHIRT BLUE NA RABA)

6.PASI YA MKAA.

7.NDOO MOJA.

8.PESA ZA KULIPIA BIMA YA AFYA KIASI CHA SHILINGI ELFU HAMSINI NA MIA NNE TU (50,400/=).

9.PESA KIDOGO YA KUJIKIMU.


ZINGATIA: KWA MUJIBU WA KANUNI ZA SHULE YA POLISI NI MARUFUKU KUFIKA SHULENI NA SIMU YA MKONONI. ATAKAYEPATIKANA NA SIMU ATAFUKUZWA SHULENI HAPO. SHULE ITAELEKEZA NA KUSAIDIA KUFANYA MAWASILIANO.

MAJINA YA WAHITIMU YANAPATIKANA KUPITIA TOVUTI www.policeforce.go.tz au WAFIKE OFISI YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Imesainiwa na:

 [AHMED Z. MSANGI – SACP]


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

NAIBU WAZIRI WA MAJI, AMOS MAKALLA AITIMISHA ZIARA YAKE YA SIKU TATU KATIKA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO YA UJENZI WA MAJI MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia), akisalimiana na Afisa Ugavi Mkuu wa Bohari Kuu ya Maji, Datus Bahati mara baada ya kuwasili Bohari Kuu ya Maji wakati wa ziara yake ya siku tatu ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji katika mkoa wa Dar es Salaam inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) ambapo aliitimisha ziara hiyo Agosti 27, 2015 kwakukagua miradi iliyopo daraja la mpiji na Kerege na maungio ya maji ya wazo.
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Bohari Kuu ya maji iliyoko Boko jijini Dar es Salaam wakati ziara yake ya siku ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji katika mkoa wa Dar es Salaam inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA).
DSC_0085
Afisa Ugavi Mkuu wa Bohari Kuu ya Maji, Datus Bahati akisoma taarifa ya utekelezaji wa kazi za Bohari Kuu ya Maji kwa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (hayupo pichani).
????????????????????????????????????????????????????????????????????????
Kushoto ni Meneja Usimamizi Uendeshaji na Mazingira DAWASA, Modesta Mushi, Afisa Ugavi Mkuu wa Bohari Kuu ya Maji, Datus Bahati (kulia) pamoja na Wakandarasi wa miradi hiyo na maofisa kutoka Wizara ya maji na waandishi wa habari wakimskiliza Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla wakati akizungumza (hayupo pichani).


????????????????????????????????????
Baadhi ya watu waliohudhuria ziara hyo wakimsikiliza kwa umakini Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla wakati akizungumza.
IMG_2809
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Bohari Mkuu wa Wizara ya Maji, Crepn Balamu, jinsi mita za kisasa kutoka Uturuk zinavyofanya kazi ambapo amesema kazi yao ni kuingiza na kuwauzia mamlaka za maji katika miji nchini, kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA), Mary Mtukula.
DSC_00733
Kutoka kulia ni Bohari Mkuu wa Wizara ya Maji, Crepn Balamu akimpa maelezo Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla vifaa vya kuunganisha maji wakati wa ziara yake ya siku ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji katika mkoa wa Dar es Salaam inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA)
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla na ummbe wake wakishuudia maungio mapya ya maji yaliopo Kerege Bagamoyo mbapo yamekamilika kwa asimilia 95.wakati wa ziara yake ya siku ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji katika mkoa wa Dar es Salaam inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA)
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????Muonekano wa maungio ya maji .
IMG_2872
Wakiangali maungio ya maji katika mto Mpiji Bunju.
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla na ujumbe wake wakiwasili katika eneo la Wazo tayari kuangalia maungio ya maji.
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla na ujumbe wake wakiangalia maungio ya maji katika eneo la wazo jijini Dar es Salaam Agosti 27, 2015 wakati wa ziara yake ya siku ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji katika mkoa wa Dar es Salaam inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA).
????????????????????????????????????
SIKU YA PILI YA ZIARA
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla na ujumbe wake wakiwa katika eneo Kigamboni jijini Dar es Salaam katika visima vya Kimbiji na Mpera,akizungumza baada ya kutembelea maeneo hayo ambapo alisema ameridhishwa na uchimbaji wa visima hivyo visima 6 vimekamilika bado 14 kati ya visima 20 vinavyotakiwa katika mradi huo.Waziri alikuwa katika ziara yake ya siku ya pili Agosti 26, 2015 .
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akijione mashine ya kunyonya maji kutoka kisimani.
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akipata maelezo mara baada ya kufika katika kisima kilichokamilika cha Kisarawe 11 chenye urefu wa mita 415.
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla hapa wakijionea mashine ya usafishaji wa kisima eneo la Kisarawe 6 kilichochimbwa kwa urefu wa mita 473.
???????????????????????????????????? 
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akipata maelezo.
Picha zote na Alex John.

ALLIANCE, MARSH MABINGWA AIRTEL RISING STARS MWANZA

$
0
0
 Nahodha wa timu ya Alliance Academy Ally Hamisi (kushoto) akikabidhiwa
kombe na Mwenyekiti wa Soka Mkoa wa Mwanza (MZFA)Bw. Jackson Songora 
baada ya kutwaa ubingwa wa U-17 Airtel Rising Stars mkoa wa Mwanza 
upande wa wavulana jana.
Nahodha wa timu ya wasichana ya Marsh Meriany Kimbuya (kushoto)
akikabidhiwa na kombe na Meneja Masoko wa Airtel Kanda ya Ziwa Bw.
Emmanuel Raphael baada ya kutwaa ubingwa wa U-17 Airtel Rising Stars
mkoa wa Mwanza upande wa wasichana jana.

TIMU  ya wavulana ya Alliance Academy ya jijini Mwanza jana imetwaa
uchampioni wa michuano ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya
Aitel Rising Stars kwa kuwafunga Misungwi Academy 3-1 kwenye uwanja wa
CCM Kirumba.

Kwa upande wa wasichana timu ya Marsh ndio iliyotawazwa mabingwa kwa
kushinda timu ya TSC kwa magoli 3-2 katika mchezo mkali uliovuta hisia
za watamazaji waliojitokeza kushuhuduia mtanange huo.

Akikabidhi vikombe kwa washindi, Mwenyekiti wa soka mkoa wa Mwanza Bw.Jackson Songora amewataka wachezaji waliochaguliwa kuiwakilisha Mwanza vyema kwenye fainali za Taifa za Airtel Rising Stars zinatarajiwa


kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 11 hadi 21. Songora
alisema kwamba kikosi kilichochaguliwa kitaanza mazoezi Jumamosi.

Naye Meneja masoka wa Airtel kanda ya Ziwa Emmanuel Raphel
alizipongeza timu zote kwa kushiriki na kuwaasa wachezaji kulinda na
kuviendeleza vipaji vyao ambavyo ni hazina kwa taifa. Aliseema lengo
lilikuwa ni kuibua vipaji na kuwaasa vijana ambao hawakuchaguliwa
kutokata tama na badala yake wajinge kufanya vizuri mwakani.
Kukamilika kwa michuano hiyo jijini Mwanza ndio kunafunga pazia la
Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa iliyoanza kutimua vumbi mwezi
uliopita.

Hivi sasa kombaini za mikoa zilizochaguliwa kuwakilisha mikoa yao
zinajiandaa kwa fainali za taifa na mwenyekiti wa soka la vijana wa
shirikisho la mpira nchini Bw. Ayoub Nyenzi amesema kuwa maandalizi ya
michuano hiyo yamekamilika.

 Mashindano ya Airtel Rising Stars ambayo mwaka huu yanashirikisha
mikoa ya Ilala, Kinondoni, Temeke, Morogoro, Mbeya, Mwanza na Arusha
inatarajiwa kuingia kwenye hatu nyeti ya fainali za Taifa iliyopangwa
kufanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, kuanzia Septamba 11

hadi 21.

MICHUANO YA WAVU YAANZA KURINDIMA ARUSHA

$
0
0
 Picha ikionyesha wachezaji wa timu ya pentagone ya jijini Arusha
Iliovaa bluu ikiwa inacheza na wachezaji wa timu ya Tanga katika
MICHUANO yamchezo wa wavu klabu Bingwa Taifa inaendelea kutimua vumbi jijini hapa ambapo timu ya mchezo wa wavu ya Tanga iliibuka kidedea kwa kuifunga timu ya pentagoni seti 3-1.
 wachezaji wa timu ya pentagoni wakiwa wanamsikiliza mwalimu.





picha zote na woinde shizza,Arusha

MICHUANO yamchezo wa wavu klabu bingwa taifa inaendelea kutimua vumbi jijini hapa hukuikizishuhudia timu shiriki zikichuana vikali kwa kuonyesha ubabe.

Katika ufunguzi  wa michuano hiyo timu za Pentagone na Flowers za
jijini Arusha zilifungua mashindano hayo ambapo zilifanikiwa kumaliza
 mchezo kwa timu ya Pentagone kuibuka na ushindi wa seti3-0 dhidi ya wapinzani wao.


Michezo mingine ilichezwa kwa wanaume ambapo ilizikutanisha timu ya  Dodoma ambayo iliibuka na ushindi wa  seti 3-0, dhidi ya Tanga, Karatu  walishinda seti 3-0 dhidi ya Flowers  hukukwa upande wa wanawake timu ya Dodoma ilichabangwa jumla ya seti 3-0 na wenzaoTanga. 

Mashindano hayo  yaliyoandaliwa na chama cha wavu
Tanzania(TAVA)  kwa Kushirikiana na chama chawavu mkoa Arusha
(AVA) yamekutanisha,mikoa mitatu pekee ambayo ni Arusha, Dodoma na Tanga
 huku vilabu sita kutoka mikoa hiyo ndivyo vinaonyeshana
ushindania mbavpo ni Pentagone klabu, Flowers Arusha, Karatu, JKT Mbweni ya Dar es salaam na Dodoma na Tanga vikiwakilishwa na timu mbili za wanaume na wanawake kilamoja.


Makamu Mwenyekiti wa chama cha wavu Tanzania (TAVA) Muharini Mchume alisema kuwa  mikoa mingine imeshindwa kushiriki kutokana na sababu mbalimbali za kwao kwani zilithibitisha kuja lakini hazikuweza kufika .

“Baadhi ya vilabu viliweza kutupa taarifa ya kushindwa kuja kwao katika mashindano hayo ikiwemo vilabu vya  jeshi na magereza ambavyo  vilitupa sababu yakuwa katika masuala ya ulinzi na usalama.
alifafanua Mchume.

Aidha alieleza zawadi mbalimbali zikiwemo medali na vikombe zawadi  hizo zitatolewa kwa washindi na kuongoza kuwa  Mabingwa watetezi wa michuano hiyo ya wavu mwaka 2014  timu ya Magereza kwa wanawake kutoka jijini Dar es salaam.

MAMA SAMIA KATIKA UBORA WAKE KATIKA MAJIMBO YA MONDULI NA LONGIDO MKOANI ARUSHA

$
0
0
 Wananchi wakiwa wamejawa hamasa kwa nyimbo na nderemo wakati Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassam, alipowasili kwenye Uwanja wa mkutano wa kampeni za CCM leo, katika jimbo la Monduli mkoani Arusha.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassa, akiwa na Kina mama wa Jamii ya Kimasai, baada ya kuwasii kwenye uwanja wa mkutano wa hadhara, eneo Namanga, Longido mkoani Arusha, leo
 Mbunge wa Longido anayemaliza muda wake, Lekule Laizer akihutubia kabla ya mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, kwenye uwanja a mkutano wa hadhara, eneo Namanga, Longido mkoani Arusha, leo
  Mgombea jimbo la Longido kwa tiketi ya CCM, Dk. Steven Lumomo (kushoto), akisalimia wananchi baada ya kutambulishwa na Mbunge wa jimbo hilo anayemaliza mda wake, Lekule Laizer, katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika katika jimbo hilo leo
  Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassa, akihutubia wananchi wa kwenye uwanja wa mkutano wa kampeni, eneo Namanga, Longido mkoani Arusha, leo
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu, akiwasikiliza kina mama waiokuwa wakichota maji katika eneo la mtaa wa madukani, Longido mkoani Arusha.
 Kijana akishangilia wakati mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipowasili eneo la Madukani, Longido mkoani Arusha leo kuhutubia mkutano wa kampeni.
 Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi, akimtambulisha mke wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, aliyehamia Chadema, wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan kwenye Uwanja wa Madukani, Longido mkoani Arusha leo.
 Mbunge anayemaliza mda wake, katika jimbo la Longido, Lekule Laizer, akimnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo, Dk. Steven Lemomo katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Madukani, Longido mkoani Arusha leo.
 Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika eneo la madukani, Longido mkoani Arusha
 Mbunge wa Afrika Mashariki, Angela Kizigha (kulia) akizungumza na Kina Mama wa Jamii ya Kimaai baada ya mkutano wa Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, uliofanyika eneo la madukani, Longido mkoani Arusha
 "MWAKA HUU MTAISOMA NAMBA" Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassani akimwambia Mgombea Udiwani wa Chadema, Anna Oloiwa, aliyefika kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza huyo, uliofanyika eneo la Madukani, Longido mkoani Arusha leo
 
 Kina mama na mabinti wa jamii ya kimasai wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu uliofanyika jimbo la Monduli, mkoani Arusha leo
 Wananchi wakijimwayamwaya kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu uliofanyika jimbo la Monduli, mkoani Arusha leo
 
 Aliyekuwa ameomba kugombea Ubunge jimbo la Monduli lakini kura zake zikawa hazikutosha, Mchungaji Amani Silanga, akionyesha aina mbili tofauti za Kadi za Chadema, wakati wa mkutano wa kampeni za Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan leo katika jimbo hilo mkoani Arusha. Amani amedai kuwa wakati Chadema kadi ya kwanza ya Chadema ilikuwa ya  rangi ya bluu na nyeusi tu, lakini miaka kadhaa baadaye ilibadilishwa na kuchanganywa na rangi nyekundu baada ya kulazimishwa na Chama cha Freemason cha uingereza ili chama hicho kupatiwa fedha.


 Wananchi wa jimbo la Monduli wakiinua mikono kula kiapo cha kumchagua mgombea Urais wa CCM, Dk. John Magufuli na mgombea Ubunge wa jimbo hilo Melock Sokoine, katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Hiyo ilikuwa kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan.
Sasa na mimi nitaitwa Samia Ole Suluhu" alisema mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika vazi la Kimasai baada ya kuzawadiwa na Kina Mama wa kabila hilo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Monduli mkoani Arusha.
 Mgombea Ubunge jimbo la Monduli kwa tiketi ya CCM, Melok Sokoine akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan uliofanyika kwenye jimbo hilo leo
 Wagombea wa Udiwani katika kata mbalimbali jimbo la Monduli wakiinua mikono kusalimia wananchi walipotambulishwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo mkoani Arusha leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wake wa Kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Monduli mkoani Arusha leo
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwaaga wananchi baada ya kuhutubia mkutano wake wa Kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Monduli mkoani Arusha leo. 

PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

NEC YAKABIDHI POLISI MAJINA YA WATU 52,078 WALIOJIANDIKISHA ZAIDI YA MARA MOJA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

$
0
0
 Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kailima Ramadhan (kushoto), akimkabidhi Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Benedict Wakulyamba orodha ya majina 52,078 ya watu waliojiandika katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR zaidi ya mara mbili Dar es Salaam leo, kwa ajili ya uchunguzi na baadae hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika.
 Masanduku ya BVR yakiwa yamehifadhiwa Bohari ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
 Mkurugenzi wa Idara ya Daftari la mpiga kura, Dk. Sisti Cariah (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu hatua waliyoifikia kuhusu daftari hilo na shughuli mbalimbali zinazoendelea kufanywa na NEC kuelekea uchaguzi mkuu.
 Mtaalamu wa Tehama wa NEC, Fatuma Mkanguzi akiwaelezea wanahabari jinsi mfumo wa Tehama unavyofanyakazi.
 Fundi, Francis Skale akiwa kazini.


 Mafundi wa NEC wakiendelea na kazi.
 Mtaalamu wa mfumo wa ulinzi wa NEC, Adolf Kinyelo akitoa maelekezo ya jinsi ya mfumo huo unavyofanya kazi.
 Wanahabari wakichukua taswira mbalimbali kuhusu NEC inavyofanyakazi zake na hatua waliyofikia kuelekea uchaguzi mkuu. 
Picha hii ni baadhi ya watu waliojiandikisha zaidi ya mara mbili katika daftari hilo.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imelikabidhi jeshi la polisi orodha ya majina ya watu zaidi ya 52,000 ambao wamebainika kujiandikisha zaidi ya mara moja kwenye daftari la kupigia kura kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR), akiwemo Diwani wa Kata ya Kimara, Pascal Manota (Chadema).

Idadi hiyo ilibainishwa Dar es Salaam leo na Mkurugenzi wa NEC, Ramadhan Kailima wakati wa ziara na waandishi wa habari katika bohari ya utayarishaji wa vitambulisho vya kupigia kura kwa mfumo wa BVR.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi orodha ya majina hayo kwa Jeshi la Polisi, Kailima alisema watu hao watachukuliwa hatua kisheria kwani kujiandikisha zaidi ya mara moja ni kosa kisheria huku akiwatoa hofu wananchi waliojiandikisha na kutoonekana majina yao.

"Mchakato wa kutoa majina ni suala ya kisheria kwa sababu ukiangalia kifungu namba cha sheria ya uchaguzi namba 11 (a) kinasema baada ya kuboresha daftari tume itaweka wazi majina hayo ili watu waweze kupitia, lakini kifungu namba 23 cha sheria hiyo hiyo kinasema, iwapo mtu hataliona jina lake kwenye daftari anapaswa atoe taarifa kwa mkurugenzi wa uchaguzi au ngazi ya halmashauri ili taarifa zake ziweze kufanyiwa marekebisho,"alisema

Akizungumzia namna ya kupiga kura kwa walemavu wasioona, Kailima alisema hadi sasa wapo kwenye mchakato wa kuleta vifaa vya kupigia kura kwa kundi hilo ili kuwe na usiri wakati wa upigaji kura na kuepusha watu kupiga kura zaidi ya mara moja.

"Ijumaa (leo) mtashuhudia tukifanya maridhiano ya mwisho na kundi hilo, tumewashirikisha kwenye kikao chetu cha ndani na tukawapa wenyewe kazi ya kwenda kubuni aina ya karatasi za kupigia kura na tumewapa uhuru ambapo tutakubaliana nao na tuone mahitaji yao wenyewe kwa wale wanaojua kusoma maneno yao na wasioweza wapige kura,"alisema.

Kwa upande wa Msimamizi wa Kitengo cha Kufanya Marekebisho ya 'BVR Kit' na Kuchakata data, Aguta Obala alisema tuhuma za vitambulisho feki vilivyokamatwa hivi karibuni si ya tume ya uchaguzi.

"Hizo taarifa sina uhakika kwa sababu sijaona kama taarifa zinafanana na za hapa tume, lazima wahakikishe wametoa taarifa za vitambulisho hivyo kwenye BVR Kit ipi,"alisema.

Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Benedict Wakuryamba baada ya kupokea orodha hiyo alisema baada watu hao na taarifa zao zitafanyiwa upelelezi na kufikishwa mahakamani endapo atakutwa na hatia.

Naibu Katibu Mkuu wa Teknlojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wa NEC, Dk. Sisti Cariah alisema kwa kutumia mfumo wa BVR ni vigumu mtu kujiandikisha zaidi ya mara moja kwani mfumo huo ni rahisi kumgundua huku akibainisha kurekebisha kasoro ndogo ndogo. 

Manota ajibu tuhuma

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili kuhusu kutuhumiwa kujiandikisha zaidi ya mara moja, Manota alisema tuhuma hizo si za kweli na kwamba alijiandikisha mara moja ambapo jina lake katika kitambulisho hicho halikuonekana vizuri.

Alisema kutokana na hali hiyo ilimpasa arudie kujiandikisha upya katika kituo hicho hicho huku ikiwa muda ni tofauti kutokana na msongamano wa watu katika mchakato wa uandikishaji.

"Nilipojiandikisha mara ya kwanza jina langu lilififia kwenye kitambulisho na hapo ndipo nilipoomba nijiandikishe tena ambapo nilivua koti na kupiga picha," alisema na kuongeza kuwa muandikishaji huyo alishindwa kurekebisha data 'edit'.

Manota alisema baada ya kujiandikisha upya kitambulisho cha awali alikiacha na kwamba kitambulisho hicho kipo halmashauri ya manispaa hiyo huku akiamini hiyo ni siasa na kumpigia kampeni.

Rufaa za ubunge 

Katika hatua nyingine, NEC imesema hadi kufikia jana rufaa za wagombea ubunge na udiwani katika maeneo mbalimbali nchini zilikuwa zimefikia 60.

Pia, imesema hadi kufikia Agosti 30 ya wiki ijayo rufaa 31 zitakuwa zimetolewa uamuzi, hivyo tume itakuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumzia hilo.

Akizungumza na gazeti hili, Mkurugenzi wa NEC, Ramadhan Kailima alisema rufaa za ubunge zilikuwa 31 na udiwani 29 lakini zinaweza kuongezeka .

Hata hivyo, alitoa mwito kwa vyama ambavyo vitaona havikuridhika na matokeo kwa njia moja ama nyingine katika maeneo waliyogombea kuwasilisha rufaa zao tume hiyo kutokana na kutoridhishwa na wakurugenzi wa uchaguzi katika maeneo yao.

Alisema miongoni mwa chama kilichowasilisha rufaa zake tume ni ACT -Wazalendo ambacho kinalalamikia wagombea wake kutotendewa haki.

TABORA WANUFAIKA NA MAFUNZO YA ULINGO – TANZANIA WOMEN CROSSPARTY PLATFORM (TWCP)

$
0
0
Mwenyekiti wa Kikundi cha Maigizo cha Kirumba Sanaa Group kilichopo Jijini Mwanza Katumba Khalid Maduwa akiwa na Kitambulisho chake cha Kupigia Kura.

Maduwa ambae pia ni Mshereheshaji (Mc Katumba) na Mtangazaji wa 99.4 Radio Metro Fm, ameungana na Binagi Media Group katika Kampeni yake ya Kuwahamasisha Watanzania waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura kujitokeza kwa wingi katika kuwachagua viongozi bora wa kuwatumikia na si bora viongozi ambao wakati mwingine huchaguliwa kutokana na kutoa rushwa. Kampeni hiyo inaitwa "PIGA KURA, EPUKA KULA".

"Napenda kuwaasa Watanzania wenzangu kuwa tunahitaji uchaguzi wa Amani na Haki bila uvunjifu wa Amani. Tupige kura ili tuwachague viongozi sahihi kwa ajili ya Maendeleo ya Taifa letu". Anasema Maduwa.
Bonyeza HAPA Kufahamu Zaidi.

2015-07-24 22:07 GMT+03:00 Mkala Fundikira :
ULINGO WA WANAWAKE WANASIASA – Tanzania Women Crossparty Platform (TWCP) ni shirika lisilo la kiserikali lililoendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watia nia wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu katika nyadhifa mbalimbali za uongozi wa nchi ikiwa ni kuchangia kutoa elimu inayolenga kuleta usawa kama haki msingi ya Mtanzania. 
Mafunzo hayo yamedhaminiwa na UNWomen.

Mafunzo hayo yamewanufaisha walengwa husika kwa kujipatia elimu hiyo huku wawezeshaji wakiwa ni Hilda Stuart Dadu na Emmiliana Msaguka waliohakikisha wanawafikia watiania katika mkoa wa Tabora na kuendesha mafunzo hayo pale Student Center.
t-wcp (2)
Wanufaika na watia nia za kugombea nafasi mbalimbali na wa vyama tofauti tofauti wakifuatila mafunzo hayo yaliyotolewa na Hilda Stuart Dadu kutoka TWCP
t-wcp (3)
Watia nia wakichukua kumbukumbu za mafunzo hayo mapema leo hii
t-wcp (4)
Miongoni mwa wanufaika wa mafunzo hayo akifuatilia jambo kwa umakini.
t-wcp (5)
Wakati mafunzo yakiendelea na maswali yakiulizwa kwa ufafanuzi zaidi kutoka kwa wawezeshaji.


t-wcp (6)
Hilda Stuart Dadu wa ULINGO (aliyesimama) akisisitiza jambo wakati mafunzo yakiendelea.
t-wcp (1)t-wcp (7)t-wcp (8)
Hawa, mgombea wa ubunge wa viti maalumu kwa tiket ya Chadema akiuliza swali kwa muwezeshaji .t-wcp (12)
t-wcp (11)
Muwezeshaji Emmiliana akitoa zoezi kwa wanafunzi wake ili kukazia zaidi kile walichofundishwa na kukifanya kwa vitendo.
t-wcp (13)
Miongoni mwa wanakundi wakijadiliana jambo baada ya kupewa zoezi na muwezeshaji wa mafunzo.
t-wcp (10)
t-wcp (9)

Picha ya pamoja ya wanufaika wa mafunzo ya ULINGO na wawezeshaji wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo watia nia za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Mafunzo hayo yamekuja wakati huu ambao ndiyo haswa muda mwafaka wa uchaguzi mkuu wa ngazi za udiwani, ubunge na Urais.

LOWASSA AHUTUBIA BARAZA LA WANAWAKE WA CHADEMA LEO JIJINI DAR

$
0
0
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono baadhi ya Wanawake wanachama wa CHADEMA, waliokuwa wamefurika kwa wingi nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam leo Agosti 27, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwasalimia baadhi ya Wanawake wanaounda Baraza la Wanawake wa Chadema, waliokuwa wamefurika kwa wingi nje ya Jengo la LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam, wakati walipowasili kwa kuhutubia Baraza hilo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Mh. Halima Mdee akizungumza na Umati wa Kinamama wa Chama hicho, uliokuwa umefurika kwa wingi nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam leo Agosti 27, 2015, kabla ya kufanyika kwa Mkutano wa Baraza hilo, uliohutubiwa na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.
Mke wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akiwasalimia Wanawake wa Chama hicho waliokuwa wamefurika kwa wingi nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam leo Agosti 27, 2015, kabla ya kufanyika kwa Mkutano wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWICHA).




Wakinamama hao wakimshangilia Mh. Lowassa na Babu Duni wakati walipowasili Ukumbini hapo.
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia akiwasalimia kina mama hao ambao walikosa nafasi ndani ya Ukumbi na kuamua kukaa nje.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwasalimia kina mama hao.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza machache wakati akiwasalimia maelfu ya Wanawake wanaounda Baraza la BAWICHA, waliokuwa wamekaa nje ya jengo la LAPF kutokana na kukosa nafasi ndani ya Ukumbi huo. Mh. Lowassa alilazimika kusimama na kuwasalimia kinamama hao kabla ya kuingia Ukumbini kulihutubia Baraza hilo.
Mh. Lowassa na Ujumbe wake wakiwasili Ukumbini.
Salam kwa Wajumbe.
Baadhi ya Wadau wa Sanaa ya Filamu nchini waliokuwepo kwenye Mkutano huo wa BAWICHA.
Shangwe Ukumbini.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, akiteta jambo na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea Mwenza, Dkt. Juma Haji Duni, wakati wa Mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Uliofanyika leo Agosti 27, 2015.
Mmoja wa Kinamama wanaowakilisha Watu wenye ulemavu akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Mh. Halima Mdee  akifatilia Hotuba ya Mama anaewakilisha Watu wenye Ulemavu.
Mh. Kaihula na Kinamamam wenzake wakifatilia Mkutano huo.
Viongozi wa Kuu.
Keki ya Siku ya Kuzaliwa kwa Mh. Lowassa iliyotolewa na Baadhi ya Washanii wanaomuunga Mkono.
Mmoja wa Wasanii wa Filamu nchini, Jacqueline Wolper akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokea Keki ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kutoka kwa Msanii wa Filamu nchini, Aunt Ezekiel.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimpongeza Msanii wa Filamu nchini,  Jacqueline Wolper.
 Jacqueline Wolper akizungumza kwa niaba ya wenzake.
Mke wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akitoa hotuba yake mbele ya Wanawake wa Chama hicho waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam leo Agosti 27, 2015, wakati wa Mkutano wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWICHA).
Mh. Lowassa katika tabasamu.
Babu Duni akifatilia jambo kwa umakini.
Mh. Mbowe na Mh. Lowassa wakiteta jambo.
Mh. Mbatia na Mh. Silima wakiteta.
Taswira mbali mbali katika Mkutano huo.
Mh. Lowassa akimpongeza Mkewe kwa hotuba nzuri aliyoitoa.
Msanii na Muziki wa Injili, Florah Mbasha akitoa burudani.



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, akitoa hotuba yake, kwenye Mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Uliofanyika leo Agosti 27, 2015, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam.


Mh. Mbatia akizungumza.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni, akitoa hotuba yake, kwenye Mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Uliofanyika leo Agosti 27, 2015, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa ,akitoa salamu ya Chama kabla ya hotuba yake, kwenye Mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Uliofanyika leo Agosti 27, 2015, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimueleza jambo, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Mh. Halima Mdee wakati akilihutubia Baraza hilo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa ,akitoa hotuba yake, kwenye Mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Uliofanyika leo Agosti 27, 2015, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam.


BALOZI WA MISRI AMUAGA RAIS KIKWETE IKULU

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kuagana na Balozi wa Misri anayemaliza muda wake Mhe.Hossam Moharram Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakiagana  na Balozi wa Misri  anayemaliza muda wake Mhe.Hossam Moharram Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
(picha na Freddy Maro)

HESLB YAWATAKA WAOMBAJI MIKOPO KUREKEBISHA TAARIFA ZAO

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 ambao fomu za maombi zimegundulika kuwa na upungufu na kuwataka kufanya marekebisho kabla au ifikapo tarehe 11 Septemba mwaka huu (2015).


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi hiyo leo (Ijumaa, Agosti 28, 2015), jumla ya fomu za waombaji wa mikopo 7,788 kati ya 68,445 zilizopokelewa na kuhakikiwa zimegundulika kuwa fomu zina upungufu na kuwataka waombaji kusoma majina yao katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz).


Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. George Nyatega, (Pichani) waombaji ambao fomu zao zimegundulika kuwa na upungufu wanatakiwa kurekebisha kabla au ifikapo tarehe 11 Septemba mwaka huu (2015).


“Baada ya kusitisha uombaji wa mikopo kwa njia ya mtandao kwa mwaka wa masomo 2015/2016, Bodi ilianza kufanya uchambuzi wa maombi yote yaliyopokelewa na kugundua kuwa maombi 7,788 ya mikopo yanakosa taarifa muhimu,” inasomeka taarifa hiyo.

  

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, taarifa muhimu zinazokosekana ni pamoja na sahihi za waombaji, nakala za vyeti vya kuzaliwa vya waombaji, sahihi na picha za wadhamini na baadhi ya fomu za maombi kutosainiwa na wanasheria na maafisa wa serikali za mitaa kama maelekezo yanavyotaka.


“Bodi inawataka waombaji wa mikopo ambao fomu zao za maombi zimegundulika kuwa upungufu, kufika wao wenyewe katika ofisi za Bodi zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam ili kufanya marekebisho katika fomu hizo,” imesisitiza taarifa hiyo na kuongeza kuwa majina waombaji wanaotakiwa kufika katika ofisi za Bodi yanapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz).


Aidha, Bodi ya Mikopo imewakumbusha waombaji wa mikopo kuwa waangalifu na kuchukua tahadhari dhidi watu wasio waaminifu ambao wanaweza kutumia zoezi hilo kuwadai fedha.


HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu.

 Aidha, jukumu jingine la Bodi ni kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 wakati Serikali ilipoanza kukopesha wanafunzi.

WADAU WA MAENDELEO YA VIWANDA WATANGAZA VYEMA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI

$
0
0
 Naibu katibu mtendaji kutoka Ofisi ya Rais Tume ya Mipango anayesimamia klasta ya Miundombinu na huduma, mhandisi Happiness Mgalula akitoa hotuba katika mkutano uliowahusisha ujumbe wa wadau wa maendeleo ya viwanda kutoka Tanzania  na ujumbe wa  wawekezaji kutoka nchini China.
Wajumbe wa mkutano wakiwa wanafuatilia kwa makini mada zinazowasilishwa katika mkutano wa wadau wa maendeleo ya viwanda.
 Naibu katibu mtendaji kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango anayesimamia klasta ya bishara  za kimataifa na mahusiano ya uchumi, Bw. Paul Sanagawe akihutubia wajumbe wa kikao ambao ni wadau wa maendeleo ya viwanda kutoka China na Tanzania.
 Wajumbe wa mkutano wakifuatilia mada inayotolewa na Mkurungenzi wa viwanda kutoka wizara ya viwanda na biashara mhandisi Elli Pallangyo.
Mkurungenzi wa viwanda kutoka wizara ya viwanda na biashara mhandisi Elli Pallangyo akitoa mada kwa wajumbe wa mkutano.
 Mkurugenzi mtendaji wa sekta binafsi nchini Bw. Godfrey Simbeye akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano ambapo aliisifu serikali kwa kujitahidi kuweka mazingira mazuri ya biashara kwa sekta binafsi.


Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji Tanzania (CTI) Bibi Juliet Kairuki akitoa mada katika mkutano kati ya wadau wa maendeleo ya viwanda kutoka China na Tanzania.
 Picha ya pamoja kati ya wadau wa maendeleo ya viwanda kutoka Tanzania na ujumbe wa wawekezaji kutoka nchini China.
 Wajumbe wa mkutano wakisikiliza kwa makini hotuba kutoka kwa Naibu katibu mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango, Mhandisi Happiness Mgalula wakati wa mkutano.
Wajumbe wa mkutano wakiwa wanasoma kwa makini baadhi ya nyaraka katika mkutano huo.
 Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania (CTI) Bibi Juliet Kairuki (kulia) akibadilishana mawazo na kaimu mkurugenzi wa NDC bw. Mlingi Mkucha nje ya ukumbi wa mkutano.
Wajumbe wa mkutano wakiwa wanasikiliza kinachoendelea ndani ya mkutano wa wadau wa maendeleo ya viwanda.

Na Adili Mhina.
Wadau wa maendeleo ya viwanda nchini wametumia vyema fursa ya kutangaza na kuwashawishi wawekezaji wa kigeni kutoka nchini China kuwekeza katika maeneo muhimu yatakayohimiza maendeleo ya viwanda na kupunguza umaskini miongoni mwa wananchi.

Hayo yametokea katika mkutano wa siku mbili mfululizo kati ya wadu wa maendeleo ya viwanda kutoka serikalini, sekta binafsi nchini pamoja na ujumbe wa wawekezaji kutoka nchini China uliomalizika jana. Mkutano huo ulioandaliwa na kituo cha kimataifa cha kupunguza umaskini cha nchini China, Mfuko wa maendeleo wa China-Afrika kwa kushirikiana na kituo cha uwekezaji Tanzania na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ulibeba ujumbe usemao, “punguza umaskini kupitia maendeleo ya viwanda”.

Katika hotuba yake kwa niaba ya katibu mtendaji wa Ofisi ya Rais Tume ya mipango, naibu katibu mtendaji anayesimamia klasta ya miundo mbinu na huduma mhandisi Hapness Mgalula alisema Mkutano huo umekuja wakati muafaka ambapo Tanzania ipo katika maandalizi ya kuandaa mpango wa maendeleo wa miaka mitano (2016/17-2020/21) ambao umebeba dhima ya kuendeleza uchumi wa viwanda.  “mkutano huu sio kwamba tu umekuja wakati muafaka lakini pia ni muhimu kwa sababu miongoni mwa yatakayojadiliwa hapa yatatumika katika kuboresha huo mpango”, alisema Mgalula.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC), bi Juliet Kairuki aliueleza ujumbe kutoka China kuwa kuwa Tanzania kuna maeneo mbali mbali ya uwekezaji ambayo yanaweza kuleta tija kubwa kwa Taifa pamoja na wawekezaji. 

 Alisisitiza zaidi kwa wawekezaji hao kuwekeza katika kujenga viwanda nchini ili kuondokana na usafirishaji bidhaa ghafi kwenda nchi za nje. Miongoni mwa maeneo aliyoyawekea msisitizo katika uwekezaji wa ujenzi wa viwanda ni pamoja na;  ubanguaji wa korosho, usindikaji wa mbegu za mafuta, utengenezaji wa nguo, ngozi, utengenezaji wa nyama bora na maziwa.

Alisisitiza kuwa pamoja na kuwa  uwekezaji wa ujenzi wa viwanda katika maeneo hayo utasaidia kukuza ajira kwa wanachi  vilevile utasaidia kuongeza thamani ya bidhaa zinazotoka nchini kwenda kuuzwa nchi za nje. “kwa sasa bidhaa nyingi zinauzwa zikiwa ghafi na hii inafanya kuuza bidhaa bei ya chini wakati kama tukifanikiwa kujenga viwanda na kuuza bidhaa za viwandani thamani ya mazao yetu itaongezeka na italeta faida upande wa serikali na vilevile kwa muwekezaji,”.

Nae mkurugenzi wa viwanda kutoka wizara ya viwanda na biashara mhandisi Elli Palangyo aliwahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania ni sehemu salama kwa uwekezaji hivyo yeyote anayekuja kuwekeza ajue kuwa yupo katika eneo salama na lenye tija kibiashara.

 Alieleza kuwa Tanzania ina faida nyingi za kuwavutia wawekezaji ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa amani na utulivu wa taifa toka kipindi cha uhuru, uwepo wa maliasili za kutosha kama vile madini na gesi asilia, upatikanaji wa ardhi ya kutosha na yenye rutuba kwa ajili ya kilimo,  kuwepo kwa bahari inayotumika kupitisha bidhaa mbalimbali hususani kwenye nchi zisizo na bahari, na zingine nyingi.

Kwa upande wa Zanziabar Mkurugenzi wa uwekezaji  kutoka mamlaka ya uwekezaji vitega uchumi Zanzibar  (ZIP) Nasriya Nassor alieleza wadau kuwa Zanzibar ina fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta za utalii, uvuvi, kilimo pamoja na maeneo mengine kama huduma za kifedha, usafirishaji, nishati pamoja na huduma mbalimbali za jamii.

Wawekezaji hao kutoka nchini China walionesha kuridhishwa na uwepo wa fursa mbalimbali zilizopo nchini na kueleza kuwa katika kutimiza azma ya kupunguza umaskini kupitia maendeleo ya viwanda Tanzania, China ina jukumu kubwa hususani katika kutoa mawazo, uzoefu, elimu, fursa na kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.

EU KUTUMA WAANGALIZI 128 KWAAJILI YA UCHAGUZI MKUU UTAKAOFANYIKA OKTOBA MWAKA HUU

$
0
0
Katibu Mkuu  wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula, na Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania, Mhe. Filiberto Sebregondi, wakibadilishana Hati ya Makubaliano ya kuruhusu waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kuingia nchini kufuatilia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.
Hati hiyo ya makubaliano imesainiwa leo, 28-08-2015, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo.
 Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Filiberto Sebregondi, akisaini Hati ya Makubaliano ya kuruhusu waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kuingia nchini kufuatilia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula, naye akisaini Hati hiyo.
Zoezi la kusaini likiendelea.
Katibu Mkuu,Balozi Mulamula akisisitiza jambo, huku Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, wakifuatilia kwa makini mazungumzo hayo.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga,(kulia) akizungumza katika hafla hiyo ya kusaini hati ya Makubaliano ya kuruhusu waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kuingia nchini kufuatilia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.
Bi. Mindi Kasiga akiwatambulisha waandishi wa Habari, waliohudhuria hafla hiyo (hawapo pichani).
 Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Filiberto Sebregondi, akijibu maswali ya Waandishi wa habari. 


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari.
Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe.Filiberto Sebregondi, akiagana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula, muda mfupi mara baada ya kusaini hati hiyo.

NA REUBEN MCHOME.
Umoja wa Ulaya (EU) utatuma timu ya waangalizi yenye wajumbe 128 nchi nzima katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 25 Oktoba 2015. 

Hayo yalibainishwa wakati wa uwekaji saini wa Makubaliano ya awali ya kuruhusu timu hiyo kati ya EU na Serikali ya Tanzania uliofanyika kwenye Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tarehe 28 Agosti 2015. 

Uwekaji saini huo umefanywa na Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na kwa upande wa EU ulifanywa na Mhe. Filiberto Ceriani Sebregondi, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania.


Akizungumza baada ya uwekaji saini wa Makubaliano hayo,  Balozi Sebregondi alieleza kuwa EU imekuwa ikituma timu hiyo kwa nchi washirika ambazo zina historia nzuri ya demokrasia. Aidha, nchi hizo zina dhamira ya dhati ya kukuza mahusiano na EU kwa kuruhusu waangalizi wafanye majukumu yao katika hatua zote za uchaguzi kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa uchaguzi unakuwa wa haki na huru.


Balozi Sebregondi aliendelea kueleza kuwa timu kama hiyo ambayo wajumbe wake wanakuwa Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya, ilitumwa katika uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo iliutangaza kuwa ni huru na haki.   Timu pia ilitoa ushauri na maelekezo ya namna ya kufanya maboresho katika hatua mbalimbali za uchaguzi.

Kwa upande wake, Balozi Mulamula aliikaribisha timu hiyo kuja Tanzania na alisema kuwa  jukumu la Wizara yake ni kuratibu na kuhakikisha kuwa wajumbe wa timu hiyo wanatekeleza majukumu yao kama ilivyokubalika kwenye Makubaliano ya Kimataifa. Aliongeza kuwa maelezo ya undani wa shughuli ya timu hiyo wakati wa uchaguzi yatatolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ambao pia watasaini makubaliano ya utekelezaji wa kazi ya timu hiyo. 

Taasisi zingine za Kimataifa zinazotarajiwa kutuma timu za uangalizi wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 ni pamoja na Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR).

NSSF YASHIRIKI KWENYE MKUTANO WA MWAKA WA WADAU WA KOROSHO MKOANI LINDI LEO

$
0
0
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF limeshiriki kwenye mkutano wa Wadau wa Korosho unaofanyika kwenye Hoteli ya Peace Beach Mkoani Lindi,mkutano huo utakaofanyika kwa Siku mbili mfululizo utahusisha wadau wa Korosho kutoka Tanzania nzima.

Katika Mkutano huo ambao NSSF imepata nafasi ya kutoa  mada imewahimiza wadau hao waweze kujiunga na NSSF ili waweze kupata mafao bora yatolewayo na mfuko huo, Mafao hayo yakiwemo Matibabu bure, Kuumia Kazi, Uzazi kwa Kina mama , Mikopo kwa wanachama na Mengineyo.



Akiongea katika Mkutano huo Meneja wa NSSF Mkoa wa Mtwara , Stanley Milanzi amewaambia wadau huo kupitia Mpango wa NSSF Wakulima Scheme wakulima wa Mkoa wa Mtwara wamepata karibia Shilingi bilioni mbili kama mikopo kutoka NSSF.
 
Meneja Kiongozi wa Masoko na Uhusiano  wa NSSF, Eunice Chiume(wa tatu Kushoto)  akiwa na Kaimu Meneja Mkoa wa Lindi, Jumbe Dona (wa pili Kushoto), Afisa  Matekelezo Kuruthum Yusufu ( Wa kwanza Kushoto), Afisa Mwandamizi wa Uhusiano Salim Kimaro (wa tatu Kulia), Afisa Uendeshaji Muandamizi Abasi Cothema (wa pili Kulia) na Afisa Mafao wa Mkoa wa Lindi Paschal Mushi (Wa kwanza Kulia) kwenye mkutano wa Wadau wa Korosho unaofanyika leo katika hoteli ya Peace Beach Mkoani Lindi.
Maofisa wa NSSF wakiwasaidia wadau wa Korosho kujaza fomu za uanachama ili waweze kujiadikisha kujiunga na NSSF.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii (NSSF), Mkoa wa Mtwara, Stanley Milanzi akitoa mada kwa wadau wa zao la Korosho kwenye mkutano wa mwaka wa wakulima wa korosho uliofanyika leo mkoani Lindi.

Meneja Wa NSSF Mkoa wa Mtwara, Stanley Milanzi  akiwaelekeza wadau wa Korosho jinsi ya kujaza fomu za NSSF ili waweze kujiandikisha na NSSF.
 Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii (NSSF), Mkoa wa Mtwara, Stanley Milanzi akitoa mada kwa wadau wa zao la Korosho kwenye mkutano wa mwaka wa wakulima wa korosho uliofanyika leo mkoani Lindi.

RAIS KIKWETE ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA ZA WALIOPATWA NA AJALI YA MOTO

$
0
0
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Said Meck Sadik kufuatia vifo vya watu tisa wa familia moja ya Bwana Masoud Matal vilivyotokea alfajiri ya tarehe 27 Agosti, 2015 kwa ajali ya moto.


Wanafamilia hao wakiwemo watoto watano walipoteza maisha baada ya nyumba yao iliyoko katika Mtaa wa Gulam, eneo la Buguruni Malapa katika Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam kuungua na kuteketea kabisa kwa moto.  Baba wa familia, Bwana Masoud Matal alisalimika kwa vile hakuwamo katika nyumba hiyo wakati ikiungua.


“Nimepokea kwa mshtuko mkubwa na nimesikitishwa mno kutokana na taarifa za kupoteza maisha kwa watu tisa wa familia moja ya Bwana Masoud Matal baada ya nyumba yao kuunguzwa na kuteketezwa kabisa na moto alfajiri ya tarehe 27 Agosti, 2015”, amesema kwa huzuni Rais Kikwete akiomboleza vifo vya wanafamilia hao.


“Kwa hakika hili ni pigo kubwa kwa Bwana Masoud Matal, lakini namuomba awe mvumilivu kwa machungu yote ya kupotelewa ghafla na familia nzima, lakini  yote amwachie Mwenyezi Mungu muweza wa yote”, ameongeza kusema Rais Kikwete.


Katika salamu zake hizo, Rais Kikwete amemwomba Mheshimiwa Sadik kumfikishia Salamu zake za rambirambi na pole nyingi kwa Bwana Masoud Matal kutokana na msiba huo mkubwa uliompata, na amesema anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema azipokee na kuzilaza Mahala Pema Peponi Roho za Marehemu wote, Amina.


Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu – Dar es Salaam.

28 Agosti,2015



MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI YAFANYIKA MKOA WA KIPOLISI TEMEKE

$
0
0
 Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya Usalama Barabarani, Thabeet Massa akimkaribisha mgeni rasmi katika mazimisho ya wiki ya nenda kwa Barabarani  yaliyofanyika katika viwanja vya Mwembe yanga Temeke jijini Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkowa wa Temeke, Endrew Satta akihutubia wananchi juu ya kuendesha  kwa usalama ili kuokoa maisha katika wiki ya nenda kwa Barabarani iliyofanyika katika Mwembe yanga Temeke jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke, Endrew Satta akiwakabidhi vyeti baadhi ya madereva wa bodaboda waliofuzu mafuzo ya Pikipiki katika wiki ya nenda kwa Barabarani iliyofanyika katika viwanja vya Mwembe yanga Temeke jijini Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkowa wa Temeke, Endrew Satta akitembelea mabanda ya maonyesho ya wiki ya nenda kwa usalama Barabarani iliyofanyika katika viwanja vya Mwembe yanga Temeke jijini Dar es Salaam leo.
Umoja wa waendesha  Pikipiki  Temeke (UWAPITE) wakiwa kwenye picha ya pamoja katika vianja vya Mwembeyanga katika maazimisho ya wiki ya nenda kwa usalama Barabarani.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

MAMA SAMIA AKAMUA LEO MBULU NA BABATI

$
0
0
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa mikutano wa Mbulu mjini mkoani Manyara.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa mikutano wa Mbulu mjini mkoani Manyara.
 Mgombea ubunge jimbo la Mbulu Vijijini, kwa tiketi ya CCM, Fraten Maasai, akiomba kura baada ya kutambulishwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan  katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa mikutano wa Mbulu mjini mkoani Manyara.
Umati wa wananchi waliohudhuria  mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, leo  kwenye Uwanja wa mikutano wa Mbulu mjini mkoani Manyara.

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiingia kwenye  mkutano wake wa kampeni uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa mikutano wa Mbulu mjini mkoani Manyara.
 Kijana akionysha bango la kumfagilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, kwenye mkutano wa kampeni za CCM za Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa mikutano wa Mbulu mjini mkoani Manyara.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa mikutano wa Mbulu mjini mkoani Manyara.
 Mgombe mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akimsalimia kijana Augustine Male, mwenye ulemavu, ambaye alihudhuria mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza huyo, leo Mbulu Mjini.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Karatu, kwa tiketi ya CCM, Wilbard Lorri, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika kijiji cha Mbulumbulu katika jimbo hilo.
 Mwananchi akiwa na mabango ya kuwafagilia mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli na Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika leo, Mbulu mjini.
 Wananchi katika Kijiji cha Mbulumbulu, wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipowasili kufanya mkutano wa kampeni katika eneo hilo leo
 Kina mama wakimzawadia mavazi, Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni katika kijiji cha Mbulumbulu, wilayani Karatu, mkoani Arusha.
 Wananchi wakiwa wamezuia msafara wa mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, katika eneo la Karatu mjini, Mama Samia ambapo alilazimika kuwasalimia, wakati akiwa njiani kwenda  Mbulu leo
 
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akiwasalimia wananchi waliosubiri msafara wake kkwenye makutano ya mkoa wa Arusha na Manyara, wakati akitoka Arusha kuingia Manyara
 Wananchi wakiwa wamezuia msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika eneo la Magugu, wilayani Bbati mkoani Manyara leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

TWIGA KUFUNGUA DIMBA NA IVORY COAST

$
0
0
TIMU ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inayotarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa mwezi Agosti kuelekea nchini Congo-Brazzavile kwenye Fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) imepangwa kufungua dimba na timu ya Wanawake ya Ivory Coast Septemba 6, 2105.
Twiga Stars iliyoweka kambi kisiwani Zanzibar kwa takribani mwezi mmoja sasa, itacheza mchezo wake pili Septemba 9, dhidi ya Nigeria kabla ya kumalizia mchezo wake wa mwisho hatua ya makundi dhidi ya wenyeji Congo-Brazzavile Septemba 12, 2105.
Jumla ya timu nane za Wanawake kutoka Barania Afrika zinashirki fainali hizo ambazo ni Nchi za Afrika Kusini, Cameroon, Ghana, Misri (wamejitoa) kundi B, na wenyeji Congo-Brazzavile, Ivory Coast, Nigeria na Tanzania kutoka kundi A.
Timu mbili za juu kutoka kila kundi zitafuzu kwa hatua ya nusu fainali.

WHO YATOA MSAADA WA DAWA ZA KUTAKASA MAJI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii Dk Donan Mmbando  akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kwa kulishukuru shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kwa kutoa msaada wa Dawa za kutakasa maji (Water Guard ) leo jiji Dar es Salaam kulia ni Mwakilishi wa shirika la Afya Ulimwenguni hapa Nchini Dk Rufaro Chatora.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii Dk Donan Mmbando leo jiji Dar es Salaam
 Mwakilishi wa shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) hapa Nchini Dk Rufaro Chatora akimkabidhi msaada huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Donan Mmbando  leo jiji Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Donan Mmbando  akimkabidhi Mgaga Mkuu wa Serikali, Dk.Grace Magembe  msada huo ulio tolewa na shirika la Afya Ulimwenguni leo jijini Dar es Salaam
( Picha na Emmanuel Massaka)

MAGUFULI AHIDI KUANZISHA MAHAKAMA YA MAFISADI NA WALA RUSHWA IWAPO ATACHAGULIWA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

$
0
0
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni ya kuwaomba ridhaa Watanzania ya kuwaongoza katika awamu ya tano.

Dkt Magufuli amesema kuwa serikali atakayoingoza atakapopata ridhaa ya kuingia Ikulu,itazifanya huduma za Afya kuwa bora na kuwabana wahudumu wa afya wenye tabia ya kuchukua dawa na kuziuza kwa watu binafsi.

Magufuli ambaye yupo katika mikoa ya Nyanda za juu kusini katika kampeni ya kusaka nafasi ya kuwa raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,amesema suala la afya litakuwa moja ya ajenda zake muhimu atakapoingia madarakani.

Katika hatua nyingine Dkt Magufuli amewaleza wananchi kuwa iwapo watampa ridhaa ya kuiongoza Tanzania,atahakikisha anaanzisha mahakama maalumu ya Mafisadi na Wala rushwa.
 Mbunge wa zamani wa jimbo la Kyela Mzee John Mwakipesile akimpigia debe Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt  John Pombe Magufuli wakati mgombea huyo alipofika jimboni humo kuomba kura za wananchi ili wamchague kuwa rais.Mzee Mwakipesile amesema kuwa anamuunga mkono Dkt Magufuli na atahakikisha anashiriki kikamilifu kuhakikisha mgombea huyo anaibuka na ushindi kwa kishindo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kyela Dkt Harrison Mwakyembe akimpigia debe Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya jionu ya leo.
  Naibu Waziri wa Fedha Mh Mwigulu Nchemba akihutubia katika  mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya,ambapo Mwigulu aliwaomba wananchi hao waliojitokeza kwa wingi kumpigia kura za ndio Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli na hatimae aweze kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano kwa sababu ana sifa zoto za kuongoza nchi.
 Maelfu ya Wananchi waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya Nzovwe Mbeya jioni ya leo,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli aliwahutubia wananchi hao.
 Naibu Waziri wa Fedha Mh Mwigulu Nchemba akihutubia katika  mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya,ambapo Mwigulu aliwaomba wananchi hao waliojitokeza kwa wingi kumpigia kura za ndio Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli na hatimae aweze kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano kwa sababu ana sifa zoto za kuongoza nchi.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni ya kuwaomba ridhaa Watanzania ya kuwaongoza katika awamu ya tano,Magufuli amewaambia wananchi hao kuwa atahakikisha  huduma za afya zinaimarishwa ipasavyo,katika suala la Elimu Magufu aliwaeleza Wananchi kuwa iwapo watamchagua katika nafasi hiyo ya Urais atahakikisha elimu kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne itatolewa bure,aidha pia amewataka Watanzania kuwa wamoja katika kuhakikisha wanailinda na kuitunza amani iliyopo nchini. 
 Wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya. 
 Wafuasi na wapenzi wa chma cha CCM wakishangilia 
Maelfu ya Wananchi waliokusanyika katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo.
 Jicho la samaki katika ubora wake kwenye mkutano wa kampeni za CCM katika viwanja vya Nzonvwe mjini Mbeya.
 Mmoja wafuasi wa chama cha chadema ambaye aliikabidhi kadi yake kwa Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli na kutanganza kuhamia chama cha CCM,katika mkutano wa kameni uliofanyika katika uwanja wa Tandale,Tukuyu mjini wilayani Rungwe
 Baadhi ya Wananchama kadhaa wa Chadema wakiwa katika picha ya pamoja na Dkt Magufuli mara baada ya kutangaza rasmi kukihama chama hicho na kujiunga na ccm
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi waliokuwa wamefika katika uwanja wa Tandale mjini Tukuyu kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Baadhi ya wananchi wa mji wa Kiwila wakiwa wamefunga barabara wakitaka kumsikiliza na kumuona mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli aliyekuwa akipita kuelekea wilayani Kyela kwenye mkutano wa kampeni.
 Heka heka za wafuasi wa CCM
 Wananchi wa Kyela wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika uwanja wa John Mwakangale mjini Kyela,kwa ajili ya kumsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwenye mkutano wake wa kampeni mjini humo.
 Dkt Magufulia akiwahutubia wananchi wa Kyela mjini Ipinda
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa jimbo la Kyela kwa  wananchi wa mji wa Ipinda wilayani Kyela wakati alipofika katika mji huo kufanya mkutano wa kampeni, Dr. John Pombe Magufuli amewaomba wananchi wa Kyela kumpa kura za ndiyo Dr. Harrison Mwakyembe ili  aweze kumtumia mara atakapochaguliwa na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

 Dkt Magufuli akiwapungia wananchi wa Tukuyu mjini alipowasili mjini humo kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni.
 Wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni 
 Mh.David Mwakyusa akimwombea kura mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwa wananchi ili apate ridhaa ya kuwatumikia wananchi akiwa Ikulu.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tukuyu mjini kwenye kutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tandale mjini gumo jioni ya leo.

MISS TANZANIA YAPATA MWENYEKITI MPYA.

$
0
0
Mwenyekiti Mpya wa Mashindano ya Miss Tanzania Juma Pinto akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni msemaji wa kamati hiyo na Miss Tanzania namba 2 mwaka 2006 Jokate Mwegelo.


Allen Mhina Na Ally Daud – Maelezo

Kamati inayosimamia mashindano ya Miss Tanzania Lino International Agency imepata Mwenyekiti na wajumbe wapya watakaoandaa ,kuratibu na kusimamia mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.

Akiwatambulisha wajumbe hao mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania iliyomaliza muda wake  Hashim Lundenga amesema  kuwa kamati  mpya ndiyo itakayowajibika na shughuli zote zilizokuwa zikifanywa na kamati ya awali.

Amesema kamati hiyo itafanya kazi zake kwa kuzingatia sheria na vigezo vyote vya kimaadili ili kuepuka  ukiukwaji wa taratibu za mashindano hayo.
 “Hatutamvumilia mwanakamati yeyote atakayevunja miiko ya mashindano haya, sisi tutakuwa nyuma tukiangalia kwa umakini”, amesema Bw. Lundenga.

Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa kamati hiyo  Juma Pinto ametoa pongezi za dhati kwa kamati iliyomaliza muda wake na kuhaidi kukubaliana na mfumo unatumika kuratibu  mashindano hayo .

“Namshukuru  Lundenga kwa  kunikabidhi nafasi hii ya mwenyekiti wa kamati ya miss Tanzania,  naahidi kuratibu mashindano haya kwa kuzingatia vigezo na masharti yaliyowekwa ili kamati yangu iweze kukidhi haja ya mashindano haya”. Amesema. 

Naye Msemaji Mkuu wa kamati hiyo na aliyekuwa Miss Tanzania namba mbili  mwaka 2006 Jokate Mwegelo, ametoa rai kwa wasichana wa kitanzania wajitokeze kushiriki mashindano hayo kwa kuonesha vipaji walivyonavyo na kupata ajira. 

Mwishoni mwa mwaka  jana Mashindano  ya Miss Tanzania  yalikumbwa na mtafaruku wa ukiukwaji wa maadili na vigezo vya mashindano na kulazimika kusimamishwa kwa muda na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).
.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images