Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 620 | 621 | (Page 622) | 623 | 624 | .... | 1897 | newer

  0 0  0 0

  Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa Mshindi wa Shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke Dennis Lwasai wakiwa na bango linalomwelezea mahindi huyo wakati walipojitokeza kumpokea wakati akirejea nyumbani kwao Mambogini Moshi.
   Mshindi wa TMT 2015 #mpakakieleweke Dennis Lwasai akiwasalimia wakazi wa mji wa Moshi waliokuwa wakimpongeza wakati akirejea kwao Mambo
   Wakiendelea kumpongeza
   Wakitoa Mkono wa pongezi kwa mshindi wakati akipita kuelekea nyumbani kwao
   Akipongezwa na wadau wake
   Kwa hisia huku akifurahi
   Alipokelewa hivi na vijana wenzie
   Kila Kona walijitokeza wadau kumpongeza
   Ndugu, Jamaa na marafiki wakimpokea mshindi wao na kumpongeza kwa kuibuka mshindi na kuiwakilisha kanda ya kaskazini vyema.


   Mama Mzazi wa Mshindi wa TMT 2015, Dennis Lwasai akimkumbatia mwanae na kumpongeza kwa kuibuka kinara wa TMT 2015 na kuondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania
   Mama mzazi wa mshindi wa TMT 2015 Dennis Lwasai akitoa maneno ya shukrani kwa vijana na watu waliojitokeza kumpokea Dennis wakati akirejea kwao Moshi hapo jana
  Dennis Lwasai mshindi wa shindano la tmt 2015 #mpakakieleweke akitoa maneno ya shukrani kwa vijana na watu wote waliojitokeza kumpokea mapema jana wakati akirejea nyumbani Kwao Moshi
  Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

  0 0

  IMG_4859
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (katikati) akimlaki Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia (kushoto) mara baada ya kuwasili katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha kufungua warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
  IMG_4862
  Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia (kushoto) akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dk. Tausi Kida (katikati) pamoja Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kuelekea sehemu maalum ya mapumziko kabla ya kuingia katika ukumbi wa mikutano.
  IMG_4869
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akifafanua jambo kuhusu warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na ESRF kwa mgeni rasmi (aliyeipa mgongo kamera) na meza kuu kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa mikutano.


  IMG_4966
  Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh. Hawa Ghasia akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya uwasilishaji wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya iliyofanyika jijini Arusha katika hoteli ya Ngurdoto.
  IMG_4954
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dk. Tausi Kida (katikati) pamoja Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakifuatilia kwa ukaribu hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani).
  IMG_4927
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
  IMG_4990
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 na Wakuu wa mikoa, wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa mikoa iliyofanyika katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
  IMG_5217
  Naibu Mkurugenzi Mkazi, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Amon Manyama akiwasilisha mada ya Mageuzi ya kiuchumi yanayoendelea: kuangalia zaidi ukaji wa uchumi wakati wa warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa kwa Wakuu wa mikoa, wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa mikoa katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
  IMG_5012
  Mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone (kushoto) wakifuatilia kwa umakini na viongozi wenzake wakati mada mbalimbali zizokuwa zikiwasilishwa kwenye warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa Wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa jijini Arusha.
  IMG_4900
  Pichani juu na chini ni Wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa waliohudhuria warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
  IMG_5009
  IMG_5019
  IMG_4807
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kushoto) katika picha ukumbusho na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa (katikati) na Mkuu wa wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Queen Mlozi (kulia).
  IMG_5123
  Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa (kushoto) katika picha ya ukumbusho na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema nje ya ukumbi wa mikutano Ngurdoto Mountain Lodge.
  IMG_5088
  Pichani juu na chini Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia na meza kuu katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa waliodhuria warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
  IMG_5095
  IMG_5110
  Mgeni rasmi na meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF).
  IMG_5077
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akiteta jambo na mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia mara baada ya zoezi la picha ya pamoja.
  Na Mwandishi wetu, Arusha
  SERIKALI imesema itazingatia ushauri uliotolewa katika Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania ya Mwaka 2014 iliyowasilishwa kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya katika warsha yao iliyofanyika Ngurdoto, Arusha.
  Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh. Hawa Ghasia wakati akifungua warsha yenye lengo la kujadili na kuielewa.

  Ripoti hiyo ambayo imejadiliwa kama “Mageuzi ya Kiuchumi kwa Maendeleo ya Binadamu” ilizinduliwa rasmi mwezi machi mwaka huu wa 2015 inawasilishwa kutokana na haja ya viongozi hao kutambua yaliyomo na namna ya kusonga mbele katika mipango ya baadae.

  Ripoti hiyo ambayo ni matokeo ya utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imelenga kusaidia kufahamu yaliyomo katika ripoti hiyo ili kuwawezesha viongozi hao kupata uelewa mpana juu ya dhana hii ya masuala ya Maendeleo ya Binadamu.

  Warsha hiyo imewezesha na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

  Ghasia alisema utafiti huo umelenga kuzijengea uwezo mamlaka za mikoa na serikali za mitaa ili kuziwezesha kutoa huduma bora kwa wananchi.

  Ripoti hiyo ambayo imezungumzia masuala ya mageuzi ya kiuchumi kwa Maendeleo ya Binadamu imetafakari kwa undani namna ya kufanya mageuzi ya kiuchumi katika taifa ili kuleta maendeleo ya Binadamu.

  Akizungumzia maendeleo alisema mwanzoni mwa karne ya 21, mataifa mengi ya kiafrika yalitengeneza Dira za Maendeleo kuwa mwongozo wa ujenzi wa uchumi na maendeleo.

  “Kwa upande wa taifa letu, Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025 inalenga katika kulifanya taifa letu kuwa nchi ya uchumi wa kati wenye kutegemea zaidi sekta ya viwanda na huduma.

  “ Kwa maneno mengine, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 inalenga siyo tu katika ukuzaji wa uchumi bali kubadilisha muundo wa uchumi; kwa miaka mingi uchumi wa Taifa letu umekuwa unategemea zaidi kilimo ambacho kina tija ndogo.” alisema Ghasia.

  Alisema kwamba Sera za Maendeleo ya taifa letu tangu uhuru zimekuwa zikiweka kipaumbele katika dhana ya Maendeleo ya Binadamu.
  “Kwa mfano, Azimio la Arusha la mwaka 1967, ambalo liliamua taifa lifuate mfumo wa ujamaa na kujitegemea lilielekeza kwamba sera, mipango na mikakati yote lazima zizingatie uboreshwaji wa maisha ya watu kwani lengo la maendeleo ni watu.” Alisema.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akizungumzia warsha hiyo alisema kwamba utafiti huyo uliofanywa na taasisi yake uliwezekana kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Idara ya uchumi), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali ya Zanzibar.
  Alisema Toleo hilo la Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania ya 2014 ni toleo la kwanza nchini.

  Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo hapa nchini na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, alizungumzia umuhimu wa mabadiliko ya kiuchumi ili taifa liwe la kipato cha kati.

  Alisema ipo haja kwa taifa hili kuhakikisha kwamba linatumia vyanzo vyake vya kifedha kubadilika kutokana na hali halisi ilivyo kwa sasa.
  Aidha alisema ipo haja ya kuzingatia mipango madhubuti ya kuondoa umaskini na kulinda mazingira, mambo ambayo yapo katika mpango mkakati wa Umoja wa Mataifa wa UNDAP wa maendeleo kuanzia mwaka kesho hadi 2021.

  0 0

  Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwasili Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa Kikosi namba 832 Ruvu JKT mkoani Pwani jana kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji mali. Kikosi hicho kilichaguliwa kuiwakilisha Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kuonyesha mafanikio ya majeshi nchini katika shughuli mbalimbali zikiwemo za uzalishaji mali ili kuinua uchumi wa taifa.
  Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenelari, Jacob Gedion Kingu, alikuwa mgeni rasmi katika ziara hiyo ya siku moja ya waandishi wa habari kutembelea kikosi hicho. Kingu alimwakilisha Mkuu wa JKT nchini.
  Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenelari, Jacob Gedion Kingu (kulia), akizungumza na wanahabari kabla ya kutembelea miradi mbalimbali inayofanywa na kikosi hicho.
  Mkuu wa Kikosi  832 Ruvu JKT, Luteni Kanali Charles Mbuge, akizungumza na waandishi wa habari wakati akimkaribisha Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenelari, Jacob Gedion Kingu kuzungumza na wanahabari katika ziara hiyo.
  Mkuu wa Kikosi  832 Ruvu JKT, Luteni Kanali Charles Mbuge (kushoto), akiwaelekeza wanahabari wakati walipofika uwanja wa gwaride kuona vijana wa kidato cha sita wanaopitia JKT kwa mujibu wa sheria wanavyofanya mazoezi ya gwaride la kuhitimu mafunzo yao ya miezi sita mapema mwezi ujao.
  Vijana wa kidato cha sita wanaopitia JKT kwa mujibu wa sheria wakionesha jinsi ya kukabiliana na adui kwa kutumia singe.
  Mary Raphael kutoka mkoani Singida  mmoja wa vijana hao waliopo katika kambi hiyo kwa mujibu wa sheria akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuonyesha jinsi ya kukabiliana na adui kwa kutumia singe.
  January Sungura (kulia), akizungumza na wanahabari baada ya kuonesha jinsi ya kukabiliana na adui kwa kutumia singe.


  Gelemaya Kibuga akizungumza na wanahabari.
  Dk. Meja Agustino Maile akiwaeleza wanahabari mambo yanafuatwa kabla ya kumnyoa mteja katika saluni ya kisasa iliyopo katika kikosi hicho kwa kuzingatia afya na kuepuka maambukizi ya magonjwa mbalimbali.
  Vijana wa mujibu wa sheria wakisubiri kunyolewa katika saluni hiyo.
  Unyoaji katika saluni hiyo ukiendelea.
  Rehama Hashim muuza wa duka katika kikosi hicho akiwaeleza wanahabari bidhaa zinazopatikana katika  duka hilo.
  Hapa ni eneo la kiwanda cha kushona nguo ambapo vijana wanaopitia jeshi hilo kwa mujibu wa sheria wanapata mafunzo.
  Wanahabari wakiangalia bweni lililojengwa kwa nguvu ya kikosi hicho kwa ajili ya kukabilana na uhaba wa vyumba vya kulala vijana hao.
  Wanahabari wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenelari, Jacob Gedion (katikati waliokaa mbele), pamoja na maofisa wa jeshi kutoka Makao Makuu ya JKT na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Maofisa Habari kutoka Idara ya Habari Maelezo.
  Vijana hao wakipiga kwata mbele ya wanahabari na mgeni rasmi.
  Vijana hao wakionesha onyesho la kuruka vikwazo.
  Onyesho la kuruka vikwazo likiendelea.
  Hapa wakiendelea kuruka vikwazo.
  Ni Gwaride bila ya kutumia bunduki.
  Wanahabari wakiangalia Intaneti iliyojengwa kwa nguvu ya kikosini hicho kwa ajili ya kusaidia wanafunzi kuona matokea yao pamoja na mambo mengine ya masomo yao.
  Vijana wakiwa katika intaneti hiyo.
  Wanahabari wakiangalia mradi wa kuku wa nyama uliopo katika kikosi hicho.
  Daktari wa Mifugo, Luteni  Ezekiel Mtani (kushoto), akiwaelezea waandishi wa habari kuhusu mradi wa kuku uliopo kikosini hapo.
  Kuku wanaofugwa kikosini hapo wakiwa katika banda maalumu.
  Wanahabari wakiangalia mabwawa ya samaki.
  Msimamizi wa mradi wa samaki katika kambi hiyo, Luteni Kelvin Ngodo (katikati), akitoa maelezo ya mradi huo kwa waandishi wa habari.
  Moja ya bwawa la samaki 
  Bwana shamba wa kikosi hicho, Ndabemeye Ludovick Rwikima (kulia), akizungumza na wanahabari kuhusu mradi wa shamba la matunda kikosini hapo.
  Bata maji wanaofugwa kikosini hapo wakiwa kwenye banda lao.
  Msimamizi wa mradi wa bata maji Rachel Muuta (kushoto), akitoa maelezo kwa wanahabari.
  Kilimo cha Vitunguu si Ilula pekee hata Ruvu JKT kinafanyika. Vijana wa JKT wakipalilia vitunguu. 
  Msimamizi wa shamba la vitunguu, Koplo Robert Eliezer (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kilimo cha vitunguu.
  Utunzaji Mazingira. Wanahabari wakiangalia shamba la miti iliyipandwa na viongozi mbalimbali katika kikosi hicho.
  Wanahabari wakiingia ulipo mradi wa usagishaji nafaka uliopo katika kikosi hicho.
  Shughuli za usagishaji nafaka ukiendelea. usagishaji huo unafanywa na vijana wa JKT kwa mujibu wa sheria.
  Wanahabari wakinagalia mradi wa usagishaji wa vyakula vya mifugo.
  Burudani mbalimbali zikiendelea kutolewa na vijana hao.
  Wanenguaji wa bendi ya JKT katika kikosi wakishambulia jukwaa.
  Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Luteni Kanali, Juma Sipe, akizungumza na wanahabari baada ya kumalizika kwa ziara hiyo ambapo aliwaomba wanahabari kuwa na ushirikiano na jeshi.
  Mwakilishi wa wanahabari hao, Mwanahabari Kibwana Dachi, akitoa neno la shukurani baada ya kumalizika kwa ziara hilo.(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com

  0 0

  TWAWEZA inatangaza uzinduzi wa midahalo iitwayo Mkikimkiki 2015. Midahalo hii imeanzishwa ili kutoa fursa na jukwaa kwa vyama vya siasa kunadi sera zao kwa wananchi. Aidha midahalo hii tawapa wananchi fursa ya kuwahoji na kuwapima wagombea na wataalamu wa vyama vikuu vya siasa.

  Mfululizo huu wa midahalo umekuja wakati muafaka. Utafiti ulidhaminiwa na Twaweza, uligundua kuwa wananchi 8 kati ya 10 wanafikiri kuwa wagombea ubunge (78%) na urais (79%) wanapaswa kuwa na midahalo ya pamoja. Mbali na mikutano ya hadhara ya kampeni, wananchi wana nafasi finyu sana ya kuwasikiliza na kuwahoji wagombea na vyama vya siasa kuhusu mitazamo, ilani na sera zao katika nyanja mbalimbali.

  Maswali ya wananchi na majibu ya hapo kwa hapo ni fursa muhimu kwa wote kupanua uelewa wa wote kuhusu sera na mipango hiyo.. 

  Wananchi wote wanakaribishwa kuwasilisha maswali yao kupitia mtandao na ujumbe mfupi wa simu (SMS). Vilevile, washiriki wa mdahalo na watazamaji wataweza kuuliza maswali wakati wa midahalo.

  Tumeandaa mfululizo wa midahalo minne itakayojikita kujadili ilani za vyama vikuu vitano vya siasa. Midahalo hii itahusu: utaifa; uchumi na kukosekana kwa usawa; huduma za kijamii hususan afya na elimu; na rushwa, utawala bora na uadilifu.

  Vyama vitano vya siasa tulivyochagua ndivyo vina wagombea wengi zaidi (ngazi ya ubunge na udiwani) kwenye uchaguzi mkuu ujao. Vimealikwa kutuma wataalam wao kushiriki midahalo itakayojadili maeneo haya muhimu. Wawakilishi hawa watahojiwa na jopo la wataalam wa sekta husika.

  Aidha, midahalo mitatu tofauti imepangwa kufanyika kwa ajili ya wagombea nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Urais wa Zanzibar na Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Kila mdahalo utachukua masaa mawili na nusu, na utarushwa moja kwa moja na Star TV na Radio Free Africa (RFA),  vyombo vya habari vya mshirika wetu, Sahara Media Group. Midahalo imeandaliwa na Compass Communications na kwenye mitandao ya kijamii itaratibiwa na Jamii Forums. 

  Ratiba ya midahalo ni kama ifuatavyo:

  Tarehe
  Mada
  Mshiriki
  30 Agosti 2015
  Utaifa
  Mdahalo wa masuala la utaifa kuhoji ilani za vyama
  6 Septemba 2015
  Mdahalo wa wagombea Urais wa Zanzibar
  20 Septemba 2015
  Elimu na Afya
  Mdahalo wa masuala la elimu na afya kuhoji ilani za vyama
  27 Septemba 2015
  Uchumi, ajira na usawa
  Mdahalo wa masuala la uchumi, ajira na usawa kuhoji ilani za vyama
  4 Oktoba 2015
  Mdahalo wa wagombea nafasi ya Makamu wa Rais
  11 Oktoba 2015
  Rushwa/uadilifu/ maadili
  Mdahalo wa masuala la rushwa na maadili kuhoji ilani za vyama
  18 Oktoba 2015
  Mdahalo wa wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

  Aidan Eyakuze, Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza amesema " Wakati huu wa kihistoria nchini Tanzania, ni vyema wananchi wakapata taarifa za kutosha kuhusu jinsi gani wagombea wa nafasi za uongozi wamepanga kushughulikia changamoto zetu. Twaweza na washirika wake imedhamini midahalo hii kuwapa fursa wananchi kuwahoji na kuwapima wagombea, pamoja na ilani na sera za vyama vinavyoomba ridhaa yao kuwaongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo."

  "Takwimu tulizokusanya kupitia utafiti wa Sauti za Wananchi na Uwezo, zinaonesha kuwa wananchi wameendelea kusisitiza mambo matatu," aliendelea Eyakuze. "Kwanza, wananchi wana hamu kubwa ya kuona serikali ikifanya kazi vizuri zaidi. Wananchi wengi waliodai kuwa wabunge wao hawakutekeleza ahadi za uchaguzi wanasema hawatawachagua tena wabunge hao. Pili, wananchi wametaja umaskini, na huduma duni za afya na elimu kama changamoto za msingi zinazowakabili. Tatu, licha ya changamoto hizi, wananchi wana matumaini makubwa kwamba maisha yao yataboreshwa na uongozi bora pamoja na juhudi zao. Kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu huu wa kipekee, ikiwa ni pamoja na kuwahoji wagombea, ni njia muhimu ya kuchochea mabadiliko chanya. Mkikimkiki 2015 inatoa fursa pana na ya bure kabisa kwa vyama vya siasa, pamoja na wagombea wao, kukutana na wapiga kura, na kunadi dira, vipaumbele and sera zao moja kwa moja. Tunatarajia ushiriki wao mzuri na wenye hamasa kubwa."

  Vyombo vya habari vinakaribishwa kushiriki lakini lazima wajiandikishe kabla ili kufanya hivyo. Tafadhali tuma barua pepe kwa pr@compass-tz.com au piga simu +255 768 129974. Hakutakuwa na posho zozote zitakazotolewa kwa washiriki.

  0 0


  image4
  Na Andrew Chale, modewjiblog
  (Dar es Salaam)-Ile shoo kubwa yamaonyesho ya mavazi ubunifu ya Tanzania katika kuibua vipaji vya wanamitindo chipukizi na models lililoandaliwa na kampuni ya Crown River Fame likijulikana kama Sanaa Fashion Show, linatarajia kufanyika Ijumaa hii ya Agosti 28, ndani ya ukumbi wa Mbezi Garden Hotel, ambapo pia kutakuwa na shoo kabambe kutoka kwa msanii wa THT, Msami.

  Akizungumza na mtandao huu Meneja Mradi wa Crown River Fame, Mr. Rahul anasema tayari taratibu zote zimeshakamilika na models pamoja na wabunifu wa mitindo wameshakamilisha kazi zao na kinachosubiriwa na shoo hiyo kabambe na ya aina yake kwa upande wa fashion show.

  "Tunataraji kuwa na Models zaidi ya 20, watakaonyesha mavazi ya ubunifu katika shoo hii ya Sanaa Fashion, na pia tunatarajia kuwa na wabunifu zaidi ya 15 wakiwemo wakongwe na wanaochipukia kwa maana 'Upcoming Desgners'.

  Ili kuleta mageuzi katika tasnia hii ya urembo na ubunifu, jukwaa hili la Sanaa Fashion Show, lina lengo kuu la kuinua models wanaochipukia 'Upcoming models' na pia kuendeleza tamaduni zetu kwa maana hiyo tumeipa jina la Sanaa.".

  Aidha, anabainisha kuwa, baadhi ya wabunifu wa mavazi watakaoshiriki kwenye kuvisha Models, katika show hiyo ni pamoja na Mama wa Mitindo nchini, Asia Idarous, Mohammed Abdul, Joyce na wengine wengi.

  Kwa upande wa kiingilio ni V.I.M ni Sh 20,000 huku V.I.P yenyewe ikiwa ni sh 40,000.
  Kwa upande wa wadhamini ni pamoja na MODEWJIBLOG, 8020Fashions, Shear Illusions, Mbezi Beach Garden, BR Production, MC na wengine wengi.
  Abdul AmadHusna Tandika akimfanyia make up, Model, Abdul-Amad katika duka la Shear Illusions Millenium Tower, jijini Dar es Salaam. Ikiwa tayari kwa maandalizi ya shoo hiyo ya kesho!
  Jonetha Peter
  Jonetha-Peter. akipakwa make up na mfanyakzi wa Shear Illusions, Agnes Rafael..


  Barnabas Lukindo
  Barnabas Lukindo akifanyiwa make up..
  Calisah Abdulhameed
  Calisah Abdulhameed akifanyiwa make up
  Husna Tandika wa Shearshen na Natasha Mohammed
  Husna Tandika akimpaka Natasha Mohammed model make up
  Calorine Benard
  Calorine-Benard. akifanyiwa make up
  Calorine Benard.jpge3
  DSC_0024
  DSC_0025

  0 0

  Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru.Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru.Baadhi ya wananchi na viongozi wa wafugaji wa kimasai wakifuatili mkutano Baadhi ya wananchi na viongozi wa wafugaji wa kimasai wakifuatili kutano
  Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru.Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru.Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru.Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru. Baadhi ya wanachama wa CCM wakimkabidhi zawadi katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu .
  Baadhi ya wanachama wa CCM wakimkabidhi zawadi katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu.  Anjela Kairuki mmoja wa wajumbe wa kamati ya kampeni ya taifa akizungumza katika mkutano wa mgombea mwenza,Anjela Kairuki mmoja wa wajumbe wa kamati ya kampeni ya taifa akizungumza katika mkutano wa mgombea mwenza.DSC_1605 Agrey Mwanri akizungumza na wapiga kura wakeAgrey Mwanri akizungumza na wapiga kura wake.Burudani kwa wananchi na mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara moshi Mjini.Burudani kwa wananchi na mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara moshi Mjini.Agrey Mwanri (kushoto) akifuraiya jambo na Bi. Ummy Mwalimu (kulia) kwenye mkutano wa B, Samia Suluhu,Agrey Mwanri (kushoto) akifuraiya jambo na Bi. Ummy Mwalimu (kulia) kwenye mkutano wa B, Samia Suluhu,[/caption] [caption id="attachment_61124" align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia jimbo la Hai.Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia jimbo la Hai.Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini. Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia jimbo la Hai.Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia jimbo la Hai.Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.Burudani kwa wananchi na mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara moshi Mjini.Burudani kwa wananchi na mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara moshi Mjini.[/caption] Na Joachim Mushi, Arusha CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kikifanikiwa kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kitahakikisha mgambo wa halmashauri ya jiji hawawasumbui kwa kamatakamata za wafanyabiashara ndogondogo ambao wengi wao ni akinamama pamoja na vijana. Kauli hiyo imetolewa leo na mgombea mwenza nafasi ya urais tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika mkutano uliofanyika uwanja wa Kilombero Jimbo la Arusha Mjini na kuhudhuriwa na umati wa wanaCCM na wananchi wengine.

   Akinadi ilani ya CCM alisema chama hicho kimeandaa utaratibu mzuri wa fursa kwa akinamama na vijana wanaofanya biashara ndogondogo hivyo itakuwa ni marufuku kwa mgambo wa jiji kukamata biashara za akinamama na vijana wanaojitafutia ridhiki mjini. "...Iwapo CCM itafanikiwa kuingia mjini naomba wale mgambo ambao uishi kwa kutegemea kukamata kamata bidhaa za akinamama watafute kazi nyingine ya kufanyanya...hatutaki mgambo wa kufanya kazi hizo ni marufuku,

  " alisema mgombea huyo mwenza wa CCM, Samia Suluhu. Alisema Ilani ya CCM imepanga kujenga viwanda vya kuchakata madini ili kuhakikisha vijana wanapata ajira na kuweza kukuza vipato vyao, na kufufua viwanda vilivyosimama kikiwemo cha 'General Tyre' ikiwa ni mpango wa kumaliza tatizo la ajira kwa vijana. Aidha alisema mpango mwingine ambao upo kwenye ilani ya CCM ni kushughulikia tatizo la mikataba ya ajira ya madereva wa magari madogo na makubwa, "..

  .Tukifanikiwa kuingia Ikulu kazi ya kwanza tutakayoipa Wizara ya ajira ni kuhakikisha inafanya kazi ya kushughulikia mikataba ya ajira kwa madereva wa magari madogo na makubwa," alisema Bi. Suluhu. Aliongeza Serikali ya CCM itaunda ufuko wa maji kuakikisha huduma za maji zinakuwa za uhakika kwani Mkoa wa Arusha unashughuli nyingi na idadi ya watu inakuwa kila uchao. Serikali ya CCM imepanga kushughulikia suala la rushwa na vitendo vya ufisadi, uzembe ili kuhakikisha kasi ya maendeleo inaongezeka. Awali kabla ya mkutano wa Arusha Bi. Suluhu alifanya mikutano katika majimbo ya Hai, Siha na Arumeru yaliyopo mikoa ya Kilimanjaro kabla ya kuingia Mkoani Arusha. Akiwa katika majimbo hayo mgombea aliinadi ilani ya CCM pamoja na kuwanadi wagombea ubunge na madiwani wa CCM wa maeneo hayo. Ambapo alisema Serikali ya CCM imepanga kuboresha huduma za afya, elimu, uwezeshaji wa vijana na akinamama ikiwa ni pamoja na kutenga shilingi milioni 50 kwa kila kijiji kwa ajili ya kuwainua akinamama na vijana. 

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Binagi Media Group George Marwa Binagi-GB Pazzo akionyesha Kitambulisho chake cha Kupigia Kura ikiwa ni katika Uzinduzi wa Kampeni yake ya KUHAMASISHA WATANZANIA WOTE kujitokeza Kupiga Kura 0ctoba 25 Mwaka huu kwa ajili ya Kuwachagua Viongozi watakaowatumikia. 
  Kampeni hiyo inafahamika kwa jina la "MTANZANIA PIGA KURA, EPUKA KULA KWA AJILI YA MAENDELEO YAKO".

  Katika Kampeni hiyo ambayo inaanza jana Agost 26, 2015 Wasomaji wa Mtandao huu pamoja na Wadau mbalimbali watapata fursa ya kutuma picha zao kwa ajili ya kuhamasisha zoezi zima la upigaji wa Kura pamoja na kuwa na uchaguzi wa Amani. Tuma picha yako kupitia Whatsupp namba +255 (0) 757 342 694 au Email binagimediagroup@gmail.com ukiambatanisha na ujumbe mfupi.

  Huu ndio ujumbe wa GB Pazzo juu ya Kampeni hii ya Piga Kura, Epuka Kura "Kwangu mimi Piga Kura, Epuka Kula ina maana kwamba mimi ambae ni mpiga kura napaswa kuweka maslahi yangu binafsi pembeni na kupiga kura kwa ajili ya manufaa ya Watanzania wote maana nikiendekeza kula leo kuna uwezekano wa kushinda njaa kwa miaka mitano ijayo".
  Binagi Media Group; Mtanzania Epuka Kula, Piga Kura Kwa Ajili Ya Maendeleo Yako"

  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akipewa maelezo ya ujenzi wa kituo cha kuwarekebisha watu walioathirika kwa matumizi ya dawa za kulevya huko Kidimni Wilaya ya Kati. Anayetioa maelezo hayo (aliyenyoosha mkono) ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dk. Omar Dad Shajak. Picha na Salmin Said, OMKR.

  MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesifu maendeleo mazuri ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha kuwarekebisha kitabia watu walioingia katika matumizi ya dawa za kulevya kinachojengwa Kidimni Wilaya ya Kati Unguja.


  Maalim Seif ameeleza hayo leo wakati alipotembelea ujenzi wa kituo hicho unaofadhiliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambao unakisiwa utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.6 na kujengwa na kampuni ya Alhilal ya hapa Zanzibar.

  Makamu wa Kwanza wa Rais amewahimiza wasimamizi, wajenzi na mafundi kuhakikisha wanaendelea na kasi hiyo hiyo, ili kuhakikisha jengo hilo linapatikana katika wakati muafaka.

  Akitoa maelezo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dk. Omar Dadi Shajak amesema jengo hilo litakapo kamilika litakuwa la ghora tatu na litaweza kutumiwa na watu wapatao 400 wanaume na wanawake.

  Amesema vijana watakao kuwepo katika kituo hicho mbali ya kupatiwa matibabu na ushauri wa kuondokana na matumizi ya dawa hizo haramu, pia watapatiwa mafunzo ya ujasiri amali katika karakana itakayo jengwa, ambapo pia kutakuwa na shamba kwa ajili ya kuwapatia mafunzo ya kilimo.

  Naye Mwakilishi wa kampuni ya ujenzi ya Alhilal, Hemed Nassor amesema ujenzi wa sehemu ya chini ya jengo hilo unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu, na jengo kamili linatarajiwa kuwa tayari katika kipindi kisichozidi miaka miwili ijayo.

  Katika ziara hiyo, Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad alifuatana na Waziri wa Nchi wa Ofisi yake, Fatma Abdul Habib Ferej, Katibu Mkuu Dk. Shajak na Naibu Katibu Mkuu, Dk. Islam Seif Salum.
  Khamis Haji, OMKIR

  0 0

  Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya A&T Brothers Co. Ltd Abdulmalik Mollel akuzungumza na wananchi juu ya Kuzuia kabisa mwendo kasi kwa magari makubwa barabara ya kutoka bandarini kuelekea ubungo kupitia ama Barabara ya Kilwa ama ile ya Mandela kwa wakati wote, na kuweka msisitizo wa alama za mwendo kasi katika barabara hizo kwakuwa pia imekuwa ikichangia kukosa umadhubuti wa breki pindi tatizo la ghafla linapojitokeza,  jana jiji Dar Salaam.
  Sehemu ya wananchi wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi Ambaye ni Mkurugenzi wa Kmpuni ya A&T Brothers co.Ltd Abdulmalik Mollel jana katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam.
  Wanafunzi wakitoa maelekezo kwa wananchi jinsi ya kutumia vifaa maalum vya kuzuia magari ili watembea kwa miguu wavuke barabara jana katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam.
  Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya A&T Brothers Co. Ltd Abdulmalik Mollel akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jana katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usala ma Barabarani Kanda ya Dar es Salaam.


   
  Mrakibu wa Jeshi la Polisi Chang'ombe Temeke akizungumza na waandishi wa habari juu ya kupungua kwa ajali kwa kiasi kikubwa katika Manispa ya Temeke jana katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabara Kanda ya Dar es Salaam.
   Kaimu Mwenyekiti Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Temeke Thabit Massa akizungumza na waandishi wa habari juu ya wananchi kutunza miundo mbinu ya barabara jana katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam.
  Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya A&T Brothers Co. Ltd Abdulmalik Mollel (mwenye suti nyeusi) akiwa pamoja na  Kaimu Mwenyekiti Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Temeke Thabit Massa wakipatiwa maelekezo na wanafunzi sehemu za makutano ya barabara zinazosababisha ajali  jana katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabara Kanda ya Dar es Salaam.
  Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya A&T Brothers Co. Ltd Abdulmalik Mollel akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi jana katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam.
   Mgeni Rasmi Ambaye ni Mkurugenzi wa Kmpuni ya A&T Brothers co.Ltd Abdulmalik Mollel na Kaimu Mwenyekiti Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Temeke akianga marabaada maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabara Kanda ya Dar es Salaam Picha na Emmanuel Massaka.
  ---
  HOTUBA YA MGENI RASMI UFUNGUZI WA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI MKOA WA KIPOLISI WA TEMEKE. TAREHE 26/8/2015 
  Ndugu; - Mkuu wa police Trafic mkoa wa Temeke (RTO). - Mwenyekiti usalama barabarani ndugu -Thabit - Mkuu wa Operesheni – Temeke , Mr Mchuya - Mkuu F.F.U – Mkoa polisi – Temeke - Ndugu kombe – mkuu wa kituo cha polisi- Chang`ombe - Viongozi mbalimbali wa kipolisi mkoa wa Temeke - Waalimu na wanafunzi wote mliohudhuria - Wadau wote mliohudhuria, mabibi na mabwana – Itifaki imezingatiwa 
  Baada ya kusikiliza na kuelewa kwa umakini changamoto mbalimbali zilizotolewa na baraza la watoto la usalama mkoa wa Temeke, pia wadau wa usalama barabarani ,yafuatayo naomba kuyarejea ili tuweze kuyapatia ufumbuzi wa mara moja kulingana na uwezo wangu na kwa ushirikiano wa Polisi mkoa huu na wadau wote kwa ujumla; Changamoto zinazosababisha kurudisha nyuma jitihada za kupunguza ajali ni pamoja na zifuatazo: 
  1. Kutokuwa makini kwa madereva waendeshao vifaa vya moto .

  2. Kutokuwa na elimu ya kutosha ya alama za barabarani kwa watumiaji ambao ni waenda kwa miguu au waendesha vyombo vya barabarani 
  3. Kutofuata alama za barabarani kwa watumiaji kama itakiwavyo 
  4. Wasimamizi wa usalama barabarani kutokuwa makini hasa hatua zinapotakiwa kuchukuliwa mara moja. Ndugu viongozi na wadau wote wa usalama mkoa huu na Taifa kwa ujumla, Rekodi zinajionyesha ni kwa jinsi gani tunavyopoteza ndugu na jamaa zetu kwa sababu ambazo zinazuilika,ikizingatiwa kuwa hawa tunaowapoteza kwa ajali hizi ni moja ya nguvu kazi ya Taifa hili. 

  Na wadau wameomba serikali iweze kuchukua nafasi ya kupunguza ajali hizi kwa kunusuru maisha ya watu, na hasa ikizingatiwa kauli mbiu ya mwaka huu “ENDESHA SALAMA- OKOA MAISHA”. 

  Ndugu wageni waalikwa, viongozi mbalimbali wa kipolisi,wanafunzi, waalimu na waandishi wa habari, Ikumbukwe kuwa serikali ni sisi tulioko hapa kwa kuwa ndio Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, Raisi wa nchi hii amewaamini viongozi hawa walioko hapa kusimamia jukumu hili maalumu la usalama mkoa huu wa Temeke. 

  Sina hofu kabisa na (RTO) wa Mkoa huu, kwani Temeke imepunguza ajali kwa asilimia hamsini (50%) kutoka 2014/2015 na hii inaonyesha jitihada na mikakati madhubuti inayofanywa kama ambavyo chati imeonesha, Nami kwa nafasi yangu kama mgeni rasmi leo, pia nikiwa mdau mkuu wa usafirishaji, ninashauri viongozi wafanye yafuatayo,ikiwa pia nitakuwa mstari wa mbele ktk kuhamasisha sekta binafsi zinazonihusu ili malengo yetu kwa pamoja yaweze kufikiwa; 

  1. Elimu itolewe mashuleni: Kikao cha wakuu wa shule, Afisa Elimu, Polisi na wadau wengine kiitishwe mara moja, ili yapitishwe maazimio ya elimu hii ya usalama barabarani, iwe ni yenye kutolewa kwa muendelezo katika kipindi chao wawapo masomoni. 

  2. Kiitishwe kikao cha wadau wa usafirishaji, viwanda,na watumiao vyombo hivi vya moto watokao ktk eneo la kimkoa kipolisi Temeke, ili washiriki katika kuchangia elimu hii kwa gharama za vitabu vyenye masomo hayo vipatikane kwa wanafunzi. 
  3. Vipindi vya siku za mpira uwanja wa Taifa: ninashauri muda wa kuanzia jioni saa moja, magari yote yaliyoharibika njiani yasiachwe kabisa bila kutolewa barabarani, 
  kwani waendesha pikipiki huwa wanashindwa kuyaona kwa wakati na kusababisha ajali zisizo na sababu na kuongezeka kwa vifo vya Raia wasiokuwa na hatia. 
  4. Elimu katika makundi maalum: Iendelee kutolewa na kuthibitishwa kwa vyeti hasa waendesha bodaboda na magari makubwa. 
  5. Mwendo Kasi:Kuzuia kabisa mwendo kasi kwa magari makubwa barabara ya kutoka bandarini kuelekea ubungo kupitia ama Barabara ya Kilwa ama ile ya Mandela kwa wakati wote,na kuweka msisitizo wa alama za mwendo kasi katika barabara hizo kwakuwa pia imekuwa ikichangia kukosa umadhubuti wa breki pindi tatizo la ghafla linapojitokeza,hivyo kupelekea ajali kutoepukika. 

  6. BREAKDOWN: Magari ya Breakdown yatumike kutoka polisi kwa zile gari ambazo zitakuwa zimepata matatizo ya kiufundi,na kusababisha uhatarishaji wa ajali kutokea,ziweze kuvutwa na kuwekwa nje ya eneo hatarishi na hasa vipindi vya usiku unapokuwa umeingia. 

  Mwisho ninawashukuru wageni waalikwa, wadau wote waliowezakuitikia wito wa kongamano hili,na sasa ninatamka Rasmi’ Kongamano la Wiki ya Nenda Kwa Usalama limefunguliwa.’ 
  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Temeke, ENDESHA SALAMA-OKOA MAISHA!! 
  Ni kwa ujenzi wa Taifa; Ndg. ABDULMALIK S. MOLLEL MGENI RASMI. A&T BROTHERS TRANSPORT CO.LTD

  0 0

   Wasanii wa SHIWATA wakigaiwa maeneo ya kujenga katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga.
  Wasanii wakipata maelekezo kutoka kwa mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib kabla ya kugaiwa nyumba zao katika awamu ya mwisho Agosti 8, mwaka huu,SHIWATA yazialika klabu, taasisi za michezo kujenga stadium, kumbi za burudani kijijini kwao Mkuranga,.
  Bado kuna ekari 290 bado hajizapata matumizi
  .Kila mwanachama kupewa robo hekari bure
  .Jella Mtagwa, Dua Said, Hamisi Kinye ni baadhi yao.


  Na Mwandishi Wetu
  MIAKA 15 imepita sasa kutoka wasanii na wanamichezo walipoungana na kuacha itikadi zao kwa kuanzisha kikundi cha kufanya maonesho ya pamoja, kusaidiana kwa hali na mali na kutafuta makazi ya pamoja ya kudumu.


  SHIWATA inayongozwa na Mwenyekiti Cassim Taalib katika kutimiza malengo hayo kutoka ianzishwe mwaka 2004 imekuwa ikiandaa matamasha mbalimbali katika ukumbi wa Star Light na Lamada mkoani Dar es Salaam na katika viwanja vya wazi kama vile Bandari Tandika na vingine kutika kuonesha sanaa ya wanachama wake.

  Baada ya SHIWATA kusailiwa Baraza la sanaa Taifa(BASATA) mwaka 2005 pia imesajiliwa na Mamlaka ya Leseni (BRELLA) kwa shughuli za kiuchumi ikiwa na dira ya kuwakomboa wasanii kuwa na maisha bora kupitia mtandao huu ifikapo mwaka 2015.

  Wasanii mbalimbali wa fani za maigizo, filamu, sarakasi, soka, bongo movie, muziki wa taarab,bongo fleva na kung Fu wamekuwa kivutio kikubwa kila yanapoandaliwa maonesho hayo.

  Kipindi chote ambacho maonesho hayo yakifanyika SHIWATA ilikuwa ikihaha kutafuta njia nyingine ya kuwaendeleza wasanii wake kwa kutafuta eneo la kujenga nyumba za makazi ya wasanii ya bei nafuu na kupata shamba ambalo litalimwa kwa pamoja.

  Mwenyekiti Taalib anasema katika jitihada za kutafuta maeneo zilianzisha msafara wa wasanii kutafuta eneo katika vijiji vya wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.


  Anasema katika jitihada hizo lilipatikana eneo la ekari 50 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe katika kijiji la Visegese ambalo uliingia dosari pale Serikali ya Wilaya ya Kisarawe iliyokuwa chini ya Mkuu wa Wilaya hiyo wakati huo, Hanifa Karamagi kuwagomea wasanii kumiliki eneo hilo ambalo mpaka sasa fedha zilizolipwa zaidi sh. mil. 4.1 hazijarejeshwa. 

  Kipindi hicho baadhi ya wasanii waliokuwa mstari wa mbele ni pamoja na marehemu Steven Kanumba,Mwanzo Mpango "King Kikii", Suzan Lewis "Natasha", waandishi wa habari akina Maulid Kitenge, Peter Mwenda, Spear Patrick,Isaac Gamba na wengine wengi.

  Taalib anasema baada ya kukwama kumilikishwa eneo hilo na Serikali ya Wilaya, jitihada za kutafuta eneo jingine ilianza na kufanikiwa kupata ekari 300 kwa ajili ya kujenga nyumba za makazi katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga mkoa huo huo wa Pwani.

  Anasema Mkuu wa wilaya ya Mkuranga wakati huo, Henry Clemence aliwapokea kwa mikono miwili wasanii hao na kukubali kubariki kupatiwa eneo hilo kulikofanywa na uongozi wa Serikali ya kijiji cha Mwanzega.

  "Jitihada ziliendelea a kutafuta mashamba ambayo wasanii watalima baada ya kuhamia kijijini na kufanikiwa kupata ekari 500 katika kijiji cha Ngarambe"anasema Taalib.

  Anasema SHIWATA ilianza kusafisha shamba hilo kwa gharama kubwa na kugawa ekari tano kwa kila mwanachama iliyependa kulima lakini walishindwa kuliendeleza kutokana na sababu mbalimbali kama vile ulinzi wa mazao kutokana na wanyama waharibu.

  Mwenyekiti  Taalib anasema wanachama waliogaiwa shamba hilo ni wale wanachama hai waliolipia ada zao na kulipa sh. 200,000 kila ekari moja na kuongezewa nusu ekari kila mmoja.

  Baada ya kugaiwa huko awamu ya pili ya kilimo kwanza katika shamba la Ngarambe ili kurahisisha baada ya kutumia mtambo wa kisasa (bulldozer) lililokodishwa kutoka Kampuni ya Willy Enterprises Ltd ya Dar es Salaam kwa gharama y ash. mil. 22 kusafisha ekari 200.

  "Ardhi hiyo ina rutuba kubwa na mazao yanayostawi eneo hilo ni mpunga, mahindi, mbaazi, viazi vitamu, ndizi, kunde, korosho, mtama na matunda kama embe, machungwa, matikiti maji na mafenesi"anasema Taalib.

  SHIWATA yenye wanachama zaidi ya 8,000 wa fani mbalimbali za sanaa za maigizo, mpira wa miguu, mpira wa wavu, netiboli, waigizai wa filamu, muziki wa dansi, muziki wa kizazi kipya, vijana na waandishi wa Habari wengi wao wameitikia ujenzio wa nyumba nafuu ambako mpaka Agosti mwaka huu nyumba 120 zimekwisha gaiwa.

  Mbali ya maonesho ya sanaa, ujenzi wa nyumba za bei nafuu za sh. 631,000 zilizojengwa kwa miti kuezekwa kwa bati ni sh. 631,000, nyumba za chumba kimoja za saruji za sh. 750,000, nyumba za chumba kimoja na sebule sh. 3.8 na nyumba za vyumba viwili na sebule sh. mil. 6.4.

  Serikali ya Wilaya ya Mkuranga ilikitambua rasmi kijiji hicho kwa kupeleka Mwenge wa uhuru Julai 21,2014 ukiongozwa kitaifa na Rachel Kassanda na wasanii zaidi ya 1,500 walijitokeza kupokea ugeni huo.

  Mkuu wa wilaya hiyo kipindi hicho alikuwa Mercy Sila ambaye aalitoa ushirikiano katika sherehe za uzinduzi wa kijiji hicho kwa kuchonga barabara ya kufika kijijini na SHIWATA iligharimia kulipa minazi, miembe na miti ya matunda ambayo barabara ilipita.

  Mwenyekiti pia anasema katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga wasanii wa fani ya filamu na tamthilia ilitengeneza filamu mbili ya kwanza ya kisufuria ambayo inaeleza maisha ya kawaida ya mtanzania na ya pili ya Ua Jeusi ambayo inaeleza ugonjwa hatari ambao bado haujajulikana ambazo zote zimeanza kurushwa kwenye vyombo vya habari.


  Filamu ya Kisufuria imetengenezwa na wasanii maarufu kama Lumole Matovole "Big", Ahmed Olotu "Mzee Chilo", Haji Mboto na katika filamu ya pili ya Ua Jeusi ni Mzee Msisi na mwigizaji maarufu Kenyata.

  Taalib anasema baada ya mafanikiop hayo changamoto iliwakuumba SHIWATA na wamiliki wa nyumba hizo kushindwa kuhamia kijijini jambo ambalo liliwalazimu kubuni njia nyingine ya kutoa ardhi nyiongine kwa ajili ya kulima bustani kwa wqale ambao watakuwa tayari kuhamia kijijini.

  Katika mpango huo mwanamichezo maarufu, Dua said aliyewahi kuchezea Simba na timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars", mchezaji wa zamani wa Yanga, Ramadhani Kampira na mwanamuzi mkongwe King Kikii kukubali kuhamia kijijini.

  Hata hivyo wasanii 21 walijitokeza kuuungana na wanamichezo hao kuhamia kijijini Mwanzega, Mkuranga na kupewa chakula, mbolea ya kulima bustani ya mbogamboga na wameanzisha kilimo cha kisasa cha pamoja kijijini hapo.

  Taalib anasema changamoto zinazoikabili SHIWATA mpaka sasa ni kutokuwa na vifaa vya kisasa vya kilimo kama vile matrekta kwa upande wa shambani, kutokuwa na barabara nzuri za kufika kijijini,kutokuwa na umeme, maji, kituo cha Polisi, shule na zahanati.

  "Mpaka sasa ardhi ambayo imetumika kwa ajili ya kujenga nyumba za makazi ni ekari kumi tu bado SHIWATA imebakiwa na hekari 290 ambazo zinahitaji uwekezaji wa klabu au taasisi kujenga viwanja vikubwa vya michezo mbalimbali kama mpira wa miguu, mpira wa wavu, riadha na michezo mingine inayohitaji maeneo makubwa" anasema Taalib.

  Anasema SHIWATA pia inawataka wanachama wake kuchangia fedha za ujenzi wa nyumba zao, shule hospitali na wengine wenye wanaotaka kuchangia ujenzi watapata robo hekari yaani miguu 35 kwa 35.

  Mwenyekiti Taalib anasema bado masharti ya kujiunga ni wale wale wanachama ambao ni wasanii, wanamichezo na wanahabari ambao wamejiunga na mtandao huo watapewa bure ardhi ya kujenga nyumba kutokana na uwezo wake.

  Anasema mgao wa nyumba hufanyika mara mbili kwa mwaka, kila mwezi Desemba na mwezi Juni.Katika mgawo wa mwaka huu uliofanyika Agosti 8, mwaka huu ambapo nyumba 16 ziligaiwa na kufikisha nyumba 120 mpaka sasa.

  Baadhi ya wacheaji wa zamani waliokabidhiwa nyumba zao ni mchezaji wa zamani wa timu ya Pan, Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania "taifa Stars, Jella Mtagwa, mcheaji wa zamani wa Simba, Dua Said  na kipa wa Yanga, Hamisi Kinye. 

  Kwa maelezo zaidi wasiliana na Ofisa Habari wa SHIWATA, Peter Mwenda 0715/0752 222677.

  0 0

  Mgombea Uras wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mbalizi mkoani Mbeya mapema leo asubuhi katika mkutano wa kampeni  maeneo ya Mbalizi wilaya ya Mbozi.
   Wanakijiji cha Kanga wakitazama picha ya mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt Jonh Pombe Magufuli wakati  mgombea huyo akielekea  Chunya kwenye mkutano wa kampeni.
  Wananchi wa Mbalizi wakiwa wamekusanyika wakimsikiliza mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt Jonh Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni uliofanya katika stendi ya mabasi Mbalizi
  Wafuasi na Washabiki wa CCM wakiwemo na Wananchi mbalimbali wakiwa wamefurika kwa shangwe kwa ajili ya kumsikiliza mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt Jonh Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mapema leo asubuhi kweny mkutano wa kampeni ndani ya wilaya ya Mbozi.
  Wananchi wakimsikiliza mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt Jonh Pombe Magufuli leo asubuhi wilayani Mbozi.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kufungua Barabara ya Wete- Gando na Wete-Konde katika Mkoa wa Kaskazini Pemba  katika ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa huo,(kushoto) Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Issa Haji Ussi,
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akifungua pazia kama ishara ya  kuifungua Barabara ya Wete- Gando na Wete-Konde katika Mkoa wa Kaskazini Pemba akiwa katika ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa huo,(kushoto) Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Issa Haji Ussi,
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Issa Haji Ussi (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk.Juma Malik Akili (wa pili kushoto) na Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban wakitembea katika  Barabara ya Wete-Gando baada ya kuizinduliwa rasmi juzi,katika katika ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo Mkoa wa Kaskazini Pemba.
   Baadhi ya Viongozi na Wafanyakazi wa Wizara ya Mindombinu na Mawasiliano wakiwa katika sherehe ya uzinduzi wa Barabara ya Wete-Gando,Wete-Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,sherehe zilizofanyika viwanja kijiji cha Ukunjwi. 


   Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein(kushoto) Waziri wa Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana, Wanawake na Watoto Bi.Zainab Omar Mohamed na Waziri wa Ardhi ,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban wakiwa sherehe za Uzinduzi wa Barabara ya Wete-Gando,Wete-Konde katika viwanja vya kijiji cha Ukunjwi Mkoa wa Kaskazini Pemba juzi,katika ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo Mkoa wa Kaskazini Pemba.
   Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Ukunjwi na Viongozi wakiwa katika sherehe za uzinduzi wa Barabara ya Wete-Gando,Wete-Konde zilizofanyika kijijini hapo Barabara iliyozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein juzi katika ziara ya kuzindua miradi mbali mbali ya Maendeleo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Viongozi na wananchi wa katika Kijiji cha Ukunjwi katika sherehe za uzinduzi wa Barabara ya Wete-Gando,Wete-Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba,akiwa katika ziara ya kuzindua miradi mbali mbali ya Maendeleo, [Picha na Ikulu.]

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho kikwete akiwa na Balozi mpya wa Tanzania nchini Uholanzi Mhe. Irene Florence Mwawa Kasyanju na Balozi mpya wa Tanzania nchini Zimbabwe Luteni Jenerali Charles Lawrence Makakala walipofika kumuaga Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 27,2015. 
   Rais Jakaya Mrisho kikwete akiwa na Balozi mpya wa Tanzania nchini Uholanzi Mhe. Irene Florence  Mwawa Kasyanju na Balozi mpya wa Tanzania nchini Zimbabwe Luteni Jenerali Charles Lawrence Makakala
  walipofika kumuaga Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 27,2015.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa Microfinance Bank Plc (NMB)  Bi Ineke Bussemaker baada ya kumwelezea kuhusu kadi ya MASTERCARD ambayo ni huduma mpya ya kisasa iliyoingizwa nchini na benki ya NMB wakati kiongozi huyo wa benki hiyo alipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaamleo Agosti 27, 2015

  Rais Jakaya Mrisho kikwete akiwa katika picha ya pamoja  na Mkurugenzi Mkuu wa Microfinance Bank Plc (NMB)  Bi Ineke Bussemaker pamoja na maafisa wa benki hiyo.

  0 0

   Baadhi ya Wanamichezo wa Michezo mbalimbali katika Wilaya ya Wete   wakiwa katika sherehe za Ufunguzi wa Kiwanja cha Baskatball na ugawaji wa Vifaa mbali mbali vya Michezo katika Nyumba za  Polisi Mess Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba jana.
   Baadhi ya Wanamichezo wa Michezo mbalimbali katika Wilaya ya Wete   wakiwa katika sherehe za Ufunguzi wa Kiwanja cha Baskatball na ugawaji wa Vifaa mbali mbali vya Michezo katika Nyumba za  Polisi Mess Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba jana.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akirusha mabofu kama ishara ya uzinduzi wa Kiwanja cha Basketball cha Polisi Mess Wete,ambapo pia aligawa vifaa mbali mbali vya michezo kwa Timu za Wilaya hiyo kwa michezo mbali mbali jana akiwa katika ziara Mkoa wa Kaskazini Pemba.


   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake katika sherehe za uzinduzi wa Kiwanja cha Basketball cha Polisi Mess Wete,kabla ya kugawa vifaa mbali mbali vya michezo kwa Timu za Wilaya hiyo kwa michezo mbali mbali jana akiwa katika ziara Mkoa wa Kaskazini Pemba.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi vifaa vya mchezo wa Karati khalfan  Suleiman wa Wete  katika sherehe za uzinduzi wa Kiwanja cha Basketball cha Polisi Mess na ugawaji wa vifaa kwa Timu mbali mbali za Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba jana akiwa katika ziara ya kikazi.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi vifaa vya mchezo wa Bad minton Ali Mwinyi Faki katika sherehe za uzinduzi wa Kiwanja cha Basket ball cha Polisi Mess na ugawaji wa vifaa kwa Timu mbali mbali za Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba jana akiwa katika ziara ya kikazi,[Picha na Ikulu.]

  0 0

   Balozi Mdogo wa China nchini, Zhang Biao akizungumza katika hafla fupi ya kuwaaga wanafunzi wanaokwenda kusoma nchini China hafla iliyofanyika ubalozi wa China  jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa  Sycilia Temu wakati wa kuwaaga wanafunzi 78 wanaokwenda kusoma nchini China  kwa ufadhili wa nchi ya China jijini Dar es Salaam jana.


   Balozi Mdogo wa China nchini, Zhang Biao akizungumza na mwakilishi wa mkuu wa chuo cha Kiislam cha Morogoro,Faraji Tamim katika hafla fupi ya kuwaanga wanafunzi wanaokwenda kusoma nchini China iliyofanyika ubalozi wa china jijini Dar es Salaam jana.  Mkufunzi wa katika chuo cha Kiislamu cha Morogoro akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa chuo cha Kiislamu cha Morogoro wanaoenda kusoma nchini China.


  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  SERIKAILI imesema  kuwa wanafunzi waliopata ufadhili wa kusoma nchini China wameweza kuleta mabadiliko nchini kutokana na kile ambacho wamekipata kutumia katika sehemu mbalimbali za kitaaluma.

  Hayo aliyasema Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa  Sycilia Temu wakati wa kuwaaga wanafunzi 78 wanaokwenda kusoma nchini China  kwa ufadhili wa nchi hiyo,amesema waliopata ufadhili wajitume na kuweza kuchangia  mabadiliko katika Nyanja mbalimbali ambazo zimewekwa kipaumbele  na serikali.

  Ufadhili huo katika Chuo cha Kiislam Morogoro (MUM) wanafunzi waliopata ufadhili ni 15 ambapo saba wanachukua  uzalmili na saba watasomea Lugha ya Kichina.

  Profesa , Sycilia amesema kuwa nchi ya China imepiga hatua kutokana na watu wake kujituma hivyo wanaopata ufadhili wanatakiwa kufanya hivyo na kuweza nchi kukua kiuchumi kutokana na elimu wanayoipata katika nchi hiyo.

  Aidha amesema kuwa serikali ya China imekuwa ikitoa kipaumbele katika serikali ya Tanzania kwa kutoa ufadhili hivyo  kwa wale wanaopata watumie fursa hiyo kwa kusoma kwa bidii kwani wahitaji wa ndani kutaka kusoma ni wengi.

  Kwa upande wa Balozi Mdogo wa China nchini, Zhang Biao  wanatambua ushirikiano kati Tanzania na China na kuona kuna umhimu wa kusukuma katika upande wa elimu kusoma na kuweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi kam ilivyofanya nchi yao.

  Amesema hadi sasa wametoa ufadhili kwa wanafunzi 1500 katika ngazi ya uzalimili na uzamivu ambapo wataendeleo kufadhili ili kuweza kufikia malengo  katika Nyanja mbalimbali.

  0 0

  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji wa Mbalizi  mkoa mpya wa  Songwe,katika mkutano wake wa kampeni uliohudhuriwa maelfu ya wananchi, Dr. John Pombe Magufuli amewaomba wananchi wa Mbalizi kummpa kura za ndiyo ili aweze kuongoza watanzania na kutatua matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii ya watanzania wa hali ya chini.

  Amesema ametumikia nchi hii kwa miaka 20 serikalini akiwa Waziri na amekuwa mkweli na muwazi ndiyo maana ameweza kuisimamia vizuri kila wizara au jukumu alilopewa na wakubwa wake akiwatumikia Watanzania na sasa anaomba nafasi ya urais ili aweze kutekeleza vyema jukumu lake la kuwatumikia Watanzania .

  Aliongeza kuwa ndiyo maana katika mchakato mzima wa kugombea urais ndani ya Chama cha Mapinduzi  alifanya kimya kimya na hakutumia fedha yoyote hivyo hakuna mtanzania yeyote anayemdai fedha ila anadaiwa utumishi uliotukuka wenye uaminifu, kujituma na kutetea maslahi ya watanzania na taifa kwa ujumla katika  taifa la Tanzania, Ameongeza kwamba ukitumia fedha kuingia madarakani na kununua madaraka ipo siku utawauza uliowanunua.  Wananchi waliokusanyika kumsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika stendi ya mabasi mjini Mbalizi wakishangilia huku wakipiga makelele kwamba anatosha na anafaa kuwa Rais na wameahidi kumpigia kura ya ndiyo.
  Wafuasi wa chama cha CCM na wananchi wakiwa wamekusanyika katika stendi ya mabasi mjini Mbalizi wakimsikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ambapo aliwahutubia na kuwaomba wampe kura ya ndiyo ili aweze kuwoangoza katika awamu ya tano.
   Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufulia akisisitiza jambo wakati akiwahutubia wakazi wa Mbalizi na kuendelea kusisitiza kuwa elimu itakuwa bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne,kuongeza maslahi ya walimu pamoja na jeshi la polisi.
  Wakazi wa mbalizi wakimsikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akimwaga sera za kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye kituo cha mabasi Mbalizi.
  Maelfu ya watu wakiwa na kiu kubwa ya kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha CCM mjini Mbalizi.

  Wananchi wa mji wa Chunya mjini wakishangilia ujio wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli katika viwanja vya Saba Saba Chunya mjini kwenye mkutano wa kampeni,ambapo Magufuli aliwahutubia wananchi hao na kuwaomba kura ya ridhaa ya kuwaongoza kwa kipindi kijacho cha awamu ya tano.


  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli,alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Makongorosi kuwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni.
  Wananchi wa Makongorosi wakimsikiliza kwa makini  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mjini hapo kwenye mkutano wa kampeni
  Wananchi wa Makongorosi wakimshangilia Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mjini hapo kwenye mkutano wa kampeni.  0 0

  indexG
  MUIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili anayetamba katika muziki huo, Upendo Nkone amekubali kushiriki katika Tamasha la Kuombea amani katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Nkone ni muimbaji wa kwanza wa Tanzania kukubali kushiriki katika tamasha la hilo la Amani linalotarajia kufanyika Oktoba 4.
  Msama alisema  wanaendelea na mchakato wa kuzungumza na waimbaji wengine ili kuwa na idadi kubwa ya waimbaji wa Tanzania sambamba na wengine kutoka nje.
  Msama alisema wanajipanga kualika waimbaji kutoka nchi tano za Afrika kwa lengo la kunogesha uzinduzi huo ili ujumbe wa neno la Mungu ufike kwa dhati.Aidha Msama alisema sambamba na waimbaji kutoka nje ya Tanzania pia wanajipanga kutangaza amani katika mikoa 10 ya Tanzania bara.
  “Tunaendelea na mikakati ya kufanikisha Tamasha hilo ambalo litakuwa ni la aina yake, hivyo wadau mbalimbali wasubiri tamasha hilo,” alisema Msama.
  Msama alisema Tamasha hilo litahudhuriwa na wadau mbalimbali kwa kushirikisha wanasiasa, viongozi wa dini mbalimbali na makundi mengine kama wasanii na wanamichezo

  0 0

  Ukiwa na haraka Mbweni JKT jiandae kupiga mbizi

  Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
  UPIGE mbizi,Ndivyo unavyoweza kusema msemo huu kama unahitaji kupita haraka haraka katika eneo la Mbweni JKT, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam, mahala panapojengwa daraja la kuvukia watu kwa miaka mitatu sasa, halina dalili za kukamilika hivi karibuni.

   Ni eneo tata,Ni eneo linalokera na kusumbua watu mno, Mbaya zaidi, ni eneo lililozunguukwa na majumba ya watu wenye ukwasi au ukubwa wa majina ya viongozi waliojenga katika eneo hilo. Eneo linalojengwa daraja hilo ni kwenye mkondo wa maji unaotokea baharini.
  Gari likivuka eneo la mkondo wa bahari, ambapo pia ndipo panapojengwa daraja hilo hatua chache mkono wa kulia kutoka gari linapopita, Maji yakijaa hapo hakuna kupita wala kuvuka.


  Kwa wanaofahamu tabia za mkondo huu wa bahari watakuwa wanaelewa, Na wasiofahamu ni kwamba, linakuwa na tabia za kujaa maji na kupungua kila wakati. Kwa mfano, mtu anaweza kupita saa tatu asubuhi akakuta hakuna maji mengi. Lakini dakika kadhaa mbele, maji mengi yanajaa kutokea baharini. Ukifanya makosa na  ukiwa na haraka ya kuendelea na shughuli zako, ndipo hapo unapopaswa upige mbizi.

  Hapa ndipo panapojengwa daraja hili.

  Itabidi uyavulie maji nguo ndipo upite, Na ikiwa unagari, huna budi kusubiri kwanza yapungue kama si kuisha kabisa maji hayo.

   Au utafute njia nyingine za kukufikisha eneo unaloelekea, ingawa njia hiyo inausumbufu mkubwa wa muda na gharama nyingine pia. Ni kutokana na hilo, serikali kwa kupitia Halmashauri ya Wilaya Kinondoni, inapaswa kuangalia kwa  jicho kuu eneo hili.

   Iangalie tatizo ni nini? Mbona daraja hilo halikamiliki kwa miaka mingi sasa, hakuna kinachoendelea, watu wanapata tabu, Mbaya zaidi ni eneo linalovutia na kusisimua, maana haiwezekani mtu kujenge nyumba kwa mamilioni ya pesa wakati njia ya kumfikisha kwake haieleweki eleweki. 

  Ni wazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni pamoja na DC Paul Makonda wanapaswa kuliangalia suala hili kwa kina.


  Kama serikali haina fedha za kukamilisha mradi huo iwachangishe wananchi wake, maana hii adha wanayokutana nayo ya kupiga mbizi si nzuri, kwani inapoteza muda, inadhalilisha pia.   Ikiwa mtu anasafiri nje ya nchi, anawahi uwanja wa ndege, anaweza kushindwa kusafiri kwa kuchelewa ndege yake kama atafika kwenye eneo hilo na kukuta maji yamejaa. 

  Ni aibu na fedheha kubwa, mtaa umezungukwa na majumba ya mamilioni ya pesa mtaa umezaja watu wengi wenye nazo, viongozi wakubwa, lakini njia wanayopita inapitika kwa vipindi vya maji kujaa na kuisha. 

  Hii haiwezekani Serikali iliangalie hili la mradi wa daraja la Mtaa Mbweni JKT, ambalo  linajengwa chini ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

  0 0

  KISAKALE CHA BIBI NYAMIHEMBE WA WAZARAMO NI CHIMBUKO LA UTANI WA WAZARAMO NA WANYAMWEZI.

  Benjamin Sawe-WHVUM
  HADITHI moja ya ajabu inayosimuliwa na wazee wa kizaramo ni ile ya Nyamihembe aliyolewa Unyamwezi,msimulizi mmoja alisema haikuwa Hadithi ya kweli, nayo ni hii, ( Hii ni Tanzu ya Fasihi simulizi)


  Mzee mmoja wa Kizaramo alikuwa na binti mzuri aliyeitwa Nyamihembe, mtoto wa kiti cha kwanza,(Mtoto wa kiti ni mwana Nyang’iti, ni utambulisho wa Mila na Desturi za baadhi ya Makabila ya Pwani, hutumika katika shuhuri zote za kimila za kurithisha vijana katika kundi la utu uzima) Baada ya kuvunja ungo akatokea Mnyamwezi mmoja akamposa, na kufunga pamvu(Harusi), kisha akapewa Bibi huyo akaishi naye. 

  Lakini Yule Mnyamwezi baadae alipendelea kurudi kwao unyamwezi pamoja na mke yule, basi akataka idhini kwa wazazi akakubaliwa,akaondoka Uzaramo na mkewe hadi kwao Unyamwezini.


  Walipokuwa kule wakajaaliwa watoto wengi wa kiume na wakike, waliishi kule Unyamwezi kwa miaka mingi hadi wale watoto wakawa watu wazima, wakaoa na kuolewa, wakazaa watoto kadha wa kadha waliokua wajukuu wa Nyamihembe.

  Lakini watoto na wajukuu wa

   Nyamihembe hawakupata bahati ya kufika Uzaramo tangu kuzaliwa kwao ila kila mara bibi Nyamihembe alikuwa akiwasimulia habari za Uzaramo kama hadithi tu.

  Nyamihembe aliishi kule hata akawa mzee (ajuza), maana hata wale wajukuu walizaa kisha wakajukuu, akawa na virembwe kadha wa kadha,wakati ule yule Mzazi mwezake Mnyamwezi Uzee ulimkithiri akafariki Dunia.   Nyamihembe akawa anatunzwa na wanawe na wajukuze, nae kila mara aliwausia akisema, ‘mimi nikifa msinizike hapa, mnipeleke kwetu Uzaramo mkanizike huko’.


  Mwanamke huyo aliishi kwa miaka mingi hata wale wanae wengine wakafariki dunia, yeye akabaki kama Mzimu, macho yake yalikwisha nguvu ya kuona  akawa kipofu,  nyama za mwili zikamkauka akabakiwa na mifupa na ngozi ikakunjana kunjana, hakujimudu kutembea, mvi zake zikapukutika zote, akabaki na Upara.


  Ajabu nyingine iliyotokea mwilini mwake ziliota Pembe mbili zilizotokeza katika paji la uso, baada  pembe hizo zikakua zikawa ndefu zilizo inama chini, Umbo alilokua nalo liliwaogofya watu, ila wale wajukuu zake ndio waliokuwa wakimuhudumia, maana ilibidi kila asubuhi kumuinua na kumtoa nje aote jua na jioni ni kumrejesha ndani na kumlaza kitandani.

   Alipokuwa anakalishwa chini zile pembe zilikuwa zinagusa ardhi na kujichomeka kama mikuki,wajukuu walipata taabu sana  kwa kumtunza ajuza huyo,baadaye mauti yalimkuta na kumuondolea taabu zake.

   Nyamihembe akaifariki Dunia.
   Basi, walipokuwa wakitangaza tanzia na kutayarisha mambo ya mazishi wale wajukuu hawakujali ule usia wake aliousia kwamba akifa akazikwe kwao Uzaramo,waliona nijambo lisilowezekana, maana kutoka Unyamwezi mpaka Uzaramo ni mwendo wa miezi miwili.

  Basi wakatayarisha mahali pa kuoshea maiti lakini walipojaribu kumuinua mfu yule  wakashindwa kabisa kwa maana alikuwa mzito sana wala hawakumudu kumjongeza hata kidogo, walifanya bidii kwa nguvu zao zote  wake kwa waume wakashindwa wakashangazwa na muujiza ule.


  Lakini baadae kidogo mjukuu mmoja alikumbuka usia na wimbo aliofundishwa na Bibi yake wakati wa uhai, maana mara mbili tatu Nyamihembe alimfundisha wimbo Mjukuu wake akamuhusia kuwa atakapokufa wanaomzika waimbe wimbo huo, naye atawaongoza njia ya kwendea Uzaramo katika nchi aliyozaliwa akazikwe huko.

  (Umuhimu wa kujiandikia Tarijima).

   Basi Yule mjukuu akawaeleza habari ile watu waliokuwapo nao wakanena, ‘Natujaribu kuimba wimbo huo na tutazame matokeo yake yatakuaje! lakini wengine wakasema, ‘pengine huenda Mfu akainuka kweli na kutuongoza njia ya kwenda kwao uzaramo, nasi wajibu wetu kumfuata, basi si bora kama tutatayarisha Chakula kwa matumizi yetu ya njiani kabla hatujaimba wimbo wenyewe’ kwa shauri hilo, wote wakakubaliana kutayarisha masurufu  ya njiani.

  Basi siku Ile wakalala bila kuigusa tena ile maiti, hata asubuhi yake kulipokucha tu wakakusanyika watu wengi waliokuwa na shauku ya kujua mazishi ya bibi Nyamihembe, yule mjukuu akawafundisha kiitikio cha Wimbo na yeye mwenyewe akaanza kuimba:

               ‘Nyamihembe tuhilike ukaye gwee!’

                 Nawenzake wakaitikia wimbo,

                  ‘Tuhilike kumwetu Zaramo’

                  Na maana yake:’Ewe Nyamihembe tuongoze nyumbani!’

                   Na waitikiao husema:’ Tuongoze kwetu Uzaramo.’


  Wimbo ule ulipoanza kuimbwa tu, ibra (ajabu) ikaanza tena kutokea, zile pembe zikaanza kunywea kidogo kidogo mpaka zikatoweka kabisa,kisha mwili wa Mfu ukaanza kutikisika, halafu mfu mwenyewe akasimama wima, watu wengine waliogopa wakaanza kukimbia  lakini wale wajukuu na ndugu wengine walibaki pale wakiendelea kuimba ule wimbo.

            Mara Nyamihembe naye akaimba :                     

                       ‘Mowana silawile behi niye,

                         Silawile behi m-m-m,

                         Ndawa Zaramo’.


  Na maana yake, ni (Tafsiri yake ‘Enyi watoto sikutoka karibu mimi, nimetoka Uzaramo.’) Nyamihembe alipokuwa akiimba hivyo mara akaanza kutembea kwa miguu yake kama kwamba mtu mzima mwenye nguvu. 

  Wajukuu na jamaa wengine wakamfuata, Msafara ukaanza pale kuelekea Uzaramo, ndugu wa marehemu, mume wa Nyamihembe waliuandama msafara huo,wengi wao walifuata ili kujua mwisho wa miujiza ile. 

  Lakini hakuna aliyesadiki kama mfu yule atawaongoza mpaka Uzaramo,basi Wimbo uliendelea kuimbwa na Nyamihembe aliendelea kuujibu Wimbo huo hali akiwa kiongozi wa msafara, alikuwa Kipofu, lakini ajabu kwamba alikuwa Kiongozi mwenye mwendo wa haraka bila kupotea njia. 


  Siku ile ya kwanza walisafiri mpaka Mchana upatao saa saba, kwa ghafla Nyamihembe akaanguka kando ya njia akajilaza kifudifudi akawa mfu tena,watu wakajua kuwa sasa ndio mwisho wa ajabu wa uhai wake, wakafanya shauri ya kumwinua ili wamchukue na kumrudisha nyumbani walikotoka ili wakamzike.

  Lakini walipojaribu kumwinua, wakashindwa kabisa maana alikuwa ameambatana na ardhi wala hawakuweza kumjongeza, kwa kuwa wote walikuwa wamechoka kwa njaa wakatua pale na kupika vyakula vyao wakala.

   Hata wakati wa alasiri, wakashauriana kuimba tena Wimbo ule labda Nyamihembe atainuka,basi walipoimba tu, Nyamihembe akasimama na kuimba wimbo wake mara akaongoza tena msafara,wakamfuata katika hali hiyohiyo ya kuimba mpaka jua lilipokuchwa Nyamihembe akaanguka kando ya njia akajilaza kifudifudi. Wafuasi nao walichoka kwa ule mwendo wa kutwa, basi wakafanya kambi mahali pale wakalala.

     

  Asubuhi kulipokucha, wale waliofuata msafara kwa upelelezi wa kujua mwisho wa ajabu ile wakarejea makwao. Lakini Wajukuu wa Nyamihembe pamoja na ndugu wachache wa mume wa Bibi Nyamihembe waliendelea katika safari. Nyimbo zikaimbwa kama kawaida na Nyamihembe akaongoza msafara.


  Mambo yaliendelea hivyo kama siku ya kwanza, nao walisafiri katika hali hiyo kwa muda wa Mwezi na nusu, hata safari ilipobaki mwendo wa siku tatu Nyamihembe hakufanya kituo tena wakati wa mchana isipokuwa alifululiza kusafiri na jioni akafanya kituo.


   Asubuhi moja waliposafiri hata mnamo saa tatu hivi wakatokea katika Kijiji chenye nyumba nyingi pamoja, kwa ghafla Nyamihembe akajitupa katikati  ya Uga, lakini badala ya kulala kifudifudi alilala chali.


    Watu wa Kijiji kile walistaajabishwa sana kuona Kizee ajuza kikifuatwa na jeshi la watu, kisha kimejitupa uwanjani kwao wale waliokuja na Nyamihembe waliendelea kuimba ule wimbo, lakini Nyamihembe hakuinuka tena, akawa kama mfu wa kawaida, maana amekwisha fika nyumbani kwake Uzaramo.

   Watu wa Kijiji wakakusanyika na kuwauliza habari wale wageni,wageni wakasimulia habari zote za Nyamihembe na jinsi hapo zamani alipopata kuolewa na Mnyamwezi, habari za wosia wake aliousia wakati alipokuwa hai na jinsi walivyo pata kuja naye mpaka pale.


   Basi kutokana na maelezo yale, Wazee wengi wa Kijiji kile walikumbuka nasaba yake, wengine wakasema,’huyu ni Shangazi yetu,’ wengine wakasema,’ huyu ni Nyanya yetu’ mradi Kijiji kile kilijaa ukoo wote wa bibi Nyamihembe. 

  Baada ya hivyo wakaleta kitanda wakaichukua maiti bila ya taabu yoyote, wakailaza juu ya kitanda na kuipeleka ndani, na wengine wakashughulika kuwapokea wageni waliotoka Unyamwezi.

    

  Siku ile watani wakaarifiwa na majirani wengine wakapelekewa Tanzia (Habari ya kifo inayopelekwa kutoka mbali) kuwa Nyamihembe Mwanamhembe alieishi Unyamwezi amerudi katika hali ya umauti na mazishi yake yatakuwa kesho,hapakuwa na kilio wakati ule, maana Nyamihembe alikuwa Tagala (mzee, kikongwe sana), mpaka Magharibi Bendebende (Ngoma ya kuashiria kifo cha mtu mkubwa) ikapigwa kuashilia kilio. 

  Wacheza Songwa na uzunguli (Ngoma zinazochezwa wakati wa maziko ya mtu mkubwa) wakahudhuria kama desturi hata Siku ya pili maandalizi ya mazishi yakafanyika, Nyamihembe akazikwa kwa heshima kubwa.


     Makala haya yanatufundisha kwamba fahari ya mtu ni kwao, (Makala haya yana vionjo vyote vya kidiaspora, yanatukumbusha ugenini ni matembezi, kwako ni maskani),yameandikwa kwa ushirikiano wa Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.


  Fanani wa Hadithi ni Mwaruka Ramadhani (1965) 

older | 1 | .... | 620 | 621 | (Page 622) | 623 | 624 | .... | 1897 | newer