Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 619 | 620 | (Page 621) | 622 | 623 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kupitia Chama cha Mapinduzi ,Samia Suluhu Hassan alipowasili uwanja wa Majengo mjini Moshi kwa ajili ya mkutano wake wa kampeni wa hadhara.
  
  Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika mkutano wa kampeni ya Mgombea Mwenza wa Chama cha Mapinduzi alifanya mkutano wake katika uwanja wa Majengo mjini Moshi.
  


  
  Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi,Samia Suluhu Hassan akiwatambulisha wagombea Ubunge katika majimbo matatu ya Moshi mjini (Dais Mosha),Vunjo(Innocent Shirima)na Moshi vijijini (Dkt Cyril Chami).
  Mgombea Ubunge jimbo la Vunjo ,Innocent Shirima akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Majengo mjini Moshi.
  Mgombea Mwenza wa Urais ,Samia Suluhu Hassan akimtamburisha mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini ,Davis Mosha wakati akimuombea kura wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Majengo mjini Moshi.
  Mgombea Mwenza wa Urais ,Samia Suluhu Hassan akimtamburisha mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi vijijini Dkt Cyril Chami wakati akimuombea kura wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Majengo mjini Moshi.
  Mgombea Mwenza wa Urais ,Samia Suluhu Hassan akimtamburisha mgombea Ubunge katika jimbo la Vunjo ,Innocent Shirima wakati akimuombea kura wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Majengo mjini Moshi.
  Mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Davis Mosha akizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Urais ,Samia Suluhu Hassan aliyeanzia kampeni zake mkoani Kilimanjaro.
  
  Mgombea Mwenza wa Urais,Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Majengo mjini Moshi.
  
  
  Wagombea Ubunge wa majimbo ya Moshi mjini,Vunjo na Moshi vijijini wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais,Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa majengo mjini Moshi.
  Baadhi ya wanachama wa Chaa cha Mapinduzi  katika mkutano ho.
  Wagombea wa nafasi ya Udiwani katika jimbo la Moshi mjini.
  Baadhi ya wanachama wa chama cha Mapinduzi.
  Mgombea Udiwani kata ya Miembeni ,Bw Juma ,akizungumza kwa niaba ya madiwani wenzake.
  Baadhi ya wanachama wa CCM mkoa wa Kilimnajrao,

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

   Mwenyekiti wa Jumuiya  ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA),Eliud Sanga  ( kati kati) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa(LAPF), akibadilishana mawanzo na  Katibu mkuu wa  TSSA, Meshack Bandawe, ( kulia) ambaye pia ni Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa ,  Augosti 24, mwaka huu mjini Morogoro  baada ya mwenyekiti huyo kufungua mafunzo kwa wafanyakazi wa mbalimbali wa mifuko yote ya hifadhi ya jamii chini inayounda  Jumuiya hiyo ( kushoto) ni Ofisa Matekelezo wa Mfuko wa PSPF Makao makuu Dar es Salaam.

  Na John Nditi, Morogoro
  JUMUIYA ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA) umewataka vijana wanaoajiriwa katika mifuko inayounda jumuiya hiyo kuingiza mawazo mapya ya ubunifu  katika  kubuni mbinu mbadala za vivutio ili kukubalika katika soko  katika maeneo ya vijijini ambako huduma hizo  hazijawafikia watu wengi.

   Hayo yalisemwa na Mwenyekiti  wa TSSA,  Eliud Sanga , Augosti 24,mwaka huu , wakati alipofungua mafunzo ya siku tano kwa wafanyakazi mbalimbali wa kutoka mifuko yote ya hifadhi ya jamii chini inayounda  Jumuiya hiyo . 

   Alisema kuwa,  soko bado ni kubwa la kutatafuta wanachama walio nje ya ajira isiyorasmi kuwaingiza katika mifuko hiyo hivyo ni vyema  wakaanza kuelekeza nguvu zao katika kutafuta wanachama  maeneo ya vijijini ambako kuna idadi kubwa ya wananchi wanaohitaji huduma zao.

    Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa hifadhi ya wafanyakazi wa Serikali za Mitaa(LAPF), alisema si jambo jema kuendelea   kulumbuna na  kugombania wanachama katika maeneo ya mijini kwani soko bado ni kubwa maeneo ya vijijini ambapo kuna ajira binasfi na isiyo rasmi. 

   Alisema  endapo vijana wasomo wanaoajiriwa katika mifuko hiyo wanaingiza mawazo mapya na ubunifu wao , kila mfuko utakuwa na hazina kubwa ya wanachama kutokana na  kuwafikia wananchi wanaoishi katika maeneo ya vijijini ambao ni wakulima na wafugaji wenye uwezo wa kuchangia mifuko hiyo.

  Mwenyekiti huyo wa TSSA , alisema  kutokana na mifuko hiyo kujikita katika maeneo ya mjini imekuwa ikitoa huduma hiyo kwa asilimia nne pekee  na endapo itaongeza juhudi za kuwafikia watu wa maeneo ya vijijini inaweza kufikia zaidi ya asilimia 96.

  Alisema , kuna kundi kubwa la wakulima,wafugaji na waendesha bodaboda ambao mifuko hiyo inapaswa  kwenda kuhamasisha  kujiunga na kuchangia huduma hizo za  hifadhi ya jamii  na pia kuangalia namna ya kutangaza mafao hayo. 

  Naye  Katibu Mkuu wa TSSA, Meshack Bandawe, alisema  malengo ya kuanzisha Jumuiya hiyo ni kufanya kazi kwa pamoja na kwa lengo moja ili kuhakikisha sekta ya hifadhi ya jamii inaimarishwa ili kuingiza Watanzania katika mifuko hiyo na waweze kunufaika nayo.

  Mafunzo hayo ya siku tano  yanawashirikisha wafanyakazi  kutoka mifuko ya NSSF, PPF, LAPF, GEPF,NHIF na ZSSF na yamelenga kuwagengea uwezo wa ufahamu mkubwa juu ya madhumuni, malengo , umuhimu na misingi ya sekta ya hifadhi ya jamii ili kuboresha utendaji wao wa kazi katika sekta ya hifadhi ya jamii ili kuwafanya watanzania wengi wafaidike.

  Bandawe ambaye pia ni Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa,alisema kuwa kupitia Jumuiya hiyo sasa wataanza kuwaelimisha wananchi wote walioko rasmi katika soko ajira na wale wasio rasmi waweze kukingwa na mifuko ya hifadhi ya jamii .

  Alisema kuwa wanaangalia namna ya kuiboresha mifuko hiyo kwa kupata uzoefu jinsi mifuko hiyo inavyofanya kazi katika nchi za Afrika mashariki  ambayo imekuwa ikisaidia sana wananchi hasa wanaoishi katika maeneo ya vijijini.

  Katibu mkuu huyo  alisema,  kupitia mafunzo hayo wanaangalia namna ya kupata wanachama ambao ni Watanzania wanaoishi nje ya nchi kuweza  kuchangia kwenye mifuko hiyo wakiwa huko huko na wale wanaoishi maeneo ya vijijini.

  0 0

  Bwana E Mr Jimmy Jiam wa EFM akipozi na mshindi wa EFM Muziki Mnene Bango eneo la Sinza, jijini Dar Es Salaam. Mshindi huyo alionekana akiwa anasikiliza 93.7 EFM na pia alikuwa ameweka stika ya EFM kwenye sehemu yake ya kazi. 
  Mshindi mwingine wa EFM Muziki Mnene Bango akiwa na furaha baada ya kukabidhiwa zawadi na bwana E wa EFM. Dada huyo alikuwa ameweka stika ya EFM kwenye sehemu yake ya biashara eneo la Magomeni, jijini Dar Es Salaam.
  Bwana E Mr Jimmy Jiam akionekana anapozi na kumpa zawadi ya T-shirt ya EFM  mshindi wa EFM Muzuki Mnene Bango. 
  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi tawi la benki ya First National la Mbezi Beach jana jijini Dar es salaam huku akiambatana na Balozi wa Heshima wa Djibouti Said Shamo na Mkuu wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha. 
  Mkuu wa Bidhaa na Huduma za Mitandao, Silvest Arumasi akimpa maelekezo Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda mara baada ya kufungua rasmi tawi la benki ya First National la Mbezi Beach jana jijini Dar es salaam. Pembeni yake ni Balozi wa Heshima wa Djibouti Said Shamo.
  Mkuu wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha akiongea machache wakati wa ufunguzi rasmi tawi la benki ya First National la Mbezi Beach jana jijini Dar es salaam.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akitoa shukrani zake za pekee kwa benki ya First National kwa kuendelea kufungua matawi yake pembezoni mwa mji wa Dar es Salaam ambapo alisema ni jambo la faraja sana pale mteja anapofuatwa alipo na si kila siku kukimbilia kufungua benki katikati ya mji.  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa pili toka kulia) akiwa na Balozi wa Heshima wa Djibouti Said Shamo ( kwanza kulia) pamoja na viongozi wa benki ya First National. Kulia ni Mkuu wa Huduma za Rejareja, Francois Botha na Mkuu wa Bidhaa na Huduma za Mitandao, Silvest Arumasi.


  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiongea machache na mmoja ya kiongozi wa Benki hiyo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya First National na wageni waliohudhuria uzinduzi huo.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda  akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akifanyiwa mahojiano na waandishi wa habari. -- Ikiwa ni sehemu ya mkakati wake kuwafikishia Watanzania wengi zaidi huduma za kibenki na kukuza uchumi, First National Bank imefungua tawi Mbezi Beach na kufanya idadi ya mtandao wa matawi yake kufikia nane. 

   Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi hilo jipya lililopo Shamo Towers Mbezi, mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja wa benki hiyo Francois Botha amesema leo kwamba ufunguzi wa tawi hilo ni sehemu ya mkakati wa kufikisha huduma za kibenki katika maeneo yote muhimu ya jiji la Dar es salaam na nchi nzima na kuinua uchumi wa Watanzania kupitia huduma mbalimbali kama mikopo ya nyumba na mikopo kwa wafanyabiashara wadogo,wa kati na wakubwa.

   “Mara kwa mara tunafikiria mbinu mpya za kutuwezesha kutoa huduma inayowapa unafuu wateja wetu kwa kupeleka huduma hiyo karibu na makazi pamoja na biashara zao. Tawi hili litarahisisha huduma kwa wateja wetu wanaoishii Mbezi na maeneo ya jirani ambayo yana biashara nyingi zinazokua kwa kasi,” alisema Botha.

   Mkuu wa kitengo cha bidhaa na huduma za kidigitali wa First National Bank, Silvest Arumasi, alisema kuwa kutokana na ukuaji wa kasi wa jiji la Dar es salaam benki hiyo imeona umuhimu wa kuhakikisha huduma za kisasa za kibenki zinawafikia watu wengi zaidi.

    “Tunataka kuhakikisha tunatoa mchango muhimu katika kuendeleza sekta ya fedha nchini na tumepanga kuendelea kuanzisha huduma mpya zenye ubunifu na za kitaalamu hapa nchini,” alisema Arumasi. Tawi hilo lililofunguliwa Mbezi Beach Shamo Towers litatoa huduma za kibenki mahususi kukidhi mahitaji ya watumiaji huduma pamoja na wafanyabiashara katika eneo hilo.

  0 0

   Meneja Malipo ya Akaunti za Mishahara wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Amos Lyimo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa droo ya pili ya kampeni ya akaunti za mishahara iitwayo ‘Mcheza Kwao’ jijini Dar es Salaam leo. Jumla ya washindi 35 walijishindia zawadi mbalimbali zikiwemo nyongeza ya pesa katika akaunti zao ya hadi asilimia 50. Kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Mrisho Millao na kulia ni Meneja wa Akaunti Maalumu wa benki hiyo, Deogratius Kibodya. 
  Meneja wa Akaunti Maalumu ya Benki ya Taifa ya Biashara(NBC), Deogratius Kibodya (kulia) akizungumza kwa simu na mmoja wa washindi wa kampeni ya akaunti za mishahara ya NBC iitwayo ‘Mcheza Kwa’ wakati wa droo ya pili iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.  Jumla ya washindi 35 walijishindia zawadi mbalimbali zikiwemo nyongeza ya pesa katika akaunti zao ya hadi asilimia 50. Kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Mrisho Millao na Meneja Malipo ya Akaunti za Mishahara wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Amos Lyimo.

  0 0

  Baadhi ya Maafisa kutoka Mgodi wa Buzwagi wakifatilia mashindano hayo wakati wa ufunguzi, kutoka kushoto ni Bwana, Jamal Rwambol, (Security Operations Section Leader),George Mkanza-(Sustainability Manager), Amos John – (Commercial Manager and Acting Mine General Manager), Bahati Mwambene-Community relations section Leader na Magesa Magesa-(Stakeholder engagement & communications officer)
  Bwana Jamal Rwambol Security Operations Section Leader wa mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo.
  Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Amos John  akizungumza wakati  wa uzinduzi wa mashindano hayo.


  Mgeni Rasmi Kaimu Meneja wa Mgodi wa Buzwagi akikagua timu ya Star boys wakati wa mechi ya ufunguzi.
  Baadhi ya timu zinazoshiriki katika mashindano hayo zikiwa katika picha ya pamoja wakati wa ufunzi wa ligi hiyo.
  Kikosi cha Timu ya Majimaji kutoka kata ya Mwendakulima.
  Kikosi cha Timu ya Star Boys.
  Baadhi ya timu zinazoshiriki mashindano hayo kwa uoane wampira wa miguu na Soka. 
  Bwana Amos John Kaimu meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi akifunga goli kuashiria kufungua michezo hiyo.
  Moja kati ya hekaheka wakati wa mechi ya ufunguzi ambapo timu ya majimaji yenye jezi ya njano iliibuka kidedea dhidi ya Star boys baada ya kuitandika bila huruma goli tatu kwa moja (3-1)
  


  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini aliyekuwa mkoani Shinyanga.

  Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi kupitia idara yake ya mahusiano ya Jamii imezindua mashindano ya mpira wa miguu na ule wa pete, kwa timu kutoka kata ya Mwendakulima wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
  Ligi hiyo ambayo imepewa jina la Mahusiano Cup, ikiwa na ujumbe wa Kuhamasisha masuala ya Usalama, Mahusiano na Maendeleo baina ya wenyeji na mgodi wa Buzwagi itahusisha timu tisa za mpira wa miguu na timu nane za mpira wa pete, ambapo kupitia ligi hiyo itaundwa timu moja ya kata ambayo itakuwa ikishiriki ligi za wilaya.
  Akizindua ligi hiyo Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Amos John amesema, kupitia mashindano hayo ambayo yamelenga kujenga mahusiano baina ya Mgodi na wenyeji kwa kuimarisha usalama na kuhamasisha shughuli za maendeleo miongoni mwa jamii.
  Aidha kaimu meneja huyo amewaasa vijana hao kuonyesha uwezo mkubwa wakati wote wa mashindano kwani kupitia michezo hiyo baadhi ya vijana watakaofanya vizuri watachaguliwa kuunda timu ya kata hiyo ambayo itakuwa ikishiriki michezo mbalimbali kwa ngazi ya wilaya.
  Awali Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Bwana  Julius Masubo Kambarage  ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada ambazo imekuwa ikifanya katika kuhamasisha na kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo michezo.
  “Sisi kwetu kupata mashindano kama haya ni fursa ya pekee sana katika kuhakikisha shughuli za michezo katika halmashauri yetu zinatekelezwa. Tutakacho kifanya kwa sasa ni kuhamasisha hizi timu zisajiliwe ili baadae ziweze kushiriki mashindano makubwa kwa sababu miongoni mwa hawa vijana wapo wenye vipaji vikubwa ila ni fursa tu hawajapata” Alisema Kambarage.
  Kwa Upande wake Mratibu wa Mashindano hayo ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Buzwagi Bwana Bahati Mwambene amezitaja timu zinazoshiriki mashindano hayo kuwa ni Tembo,Star Boys,Shehena, zote kutoka mtaa wa Chapulwa. Timu nyingine amezitaja kuwa ni Majimaji, Unity, Budushi, za mtaa wa Mwendakulima, na nyingine ni Israel, Busalala na Miembeni zote hizi ni kutoka mitaa ya Busalala na Mwime.
  Aidha Bwana Mwambene amesema kabla ya Kuanza kwa mashindano hayo timu zote zimekabidhiwa vifaa mbalimbali vya michezo kama vile seti za jezi kwa timu zote pamoja na mipira, ambavyo amesema pamoja na zawadi za washindi vimegharimu zaidi ya shilingi za kitanzania milioni ishirini na mbili na laki sita.
  Ligi hiyo ambayo inafanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mwendakulima imeanza tarehe 23 mwezi wa nane na inatarajiwa kumalizika tarehe 05 mwezi wa tisa ambapo mshindi wa kwanza kwa kila mchezo atajinyakulia kikombe pamoja na pesa taslimu laki tatu, huku mshindi wa pili akiondoka na laki mbili na nusu na mshindi wa tatu akiondoka na shilingi laki mbili.
  

  0 0

  Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi wakwanza kushoto akitoa maelezo juuya haki za binaadamu  kwa mujibu wa Uislam wakati alipokuwa akifunguwa Mafunzo ya Haki za Binaadamu na kuwatambulisha wasaidizi wa Sheria kwa Viongozi wa Dini, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Harusi Miraji na mwisho Jina Mwinyi Waziri Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma na Sheria.
  Sheikh Thabit Nooman Jongo kutoka Afisi ya Mufti Zanzibar akiwafahamisha jambo washiriki wa mafunzo ya Haki za Binaadamu katika Ukumbi wa Mazsons Hotel mjini Zanzibar

  Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar         26/08/2015.
  Mashekhe na Walimu wa Madrasa wametakiwa kuwashajihisha Wananchi ili waepuke kujiingiza katika makundi yanayoweza kuvunja amani katika kipindi hiki cha Mchakato wa Uchaguzi Mkuu nchini.

  Hayo yameelezwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi alipokuwa akifunguwa mafunzo ya Haki za Binaadamu yaliyoandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar na kufanyika katika ukumbi wa Mazsons Hotel,Shangani Mjini Zanzibar.

  Amesema Masheikh na Walimu hao ndio Wasimamizi wakuu katika maeneo mbalimbali ikiwemo Miskitini, Madrasani na hata ndani ya Nyumba zao kwani kufanya hivyo kutawasaidia kuepuka Uvunjifu wa Amani ni.

  “Tofauti za dini, jinsia, cheo na Kabila sio njia za ukiukwaji wa Sheria ndani ya Nchi yetu bali zitumike katika kutii sharia kwa kila raia”,alisema Shekh Kaabi.

  Nae Shekh Thabit Nooman Jongo kutoka Afisi ya Mufti Zanzibar amewataka Walimu na Mashekhe wenzake kuwa mstari wa mbele katika kusimamia juu ya ukumbusho huo kwani kufanya hivyo ni kutekelaza majukumu yao.

  Aidha amewataka Masheikhe na Walimu  hao kuchukuwa juhudi za hali ya juu na kutumia maneno ya hekima, busara na unyenyekevu ili waweze kufanikiwa malengo waliyokusudia.

  Hata hivyo amesema kuwa wakati wanapotoa hutuba zao ndani ya Misikiti na Madrasa ziwe ni zenye kujenga amani kwani kufanya hivyo ni kuzitii sheria zilizowekwa katika nchi yao.

  Kwa upande wao Washiriki wa mafunzo hayo wamesema watayafanyia kazi bila ya kinyongo na kuyafikisha katika maeneo yao kama walivyoagizwa na Viongozi wenzao.

                  IMETOLEW NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

   Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto Mhe.Dkt  Pindi Chana (Mb) akiangalia baadhi ya machapisho yanayohusiana mbinu za malezi na makuzi ya watoto kabla ya kufungua semina ya siku mbili ya matokeo ya utafiti wa malezi na makuzi ya familia nchini iliyofanyika Hotel Protea Courtyard, jijini Dar es salaam.
  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii  Jinsia na Watoto  (Mhe. Dkt  Pindi Chana (Mb) akifungua rasmi   Kongamano la siku mbili la wadau wa familia wanaokutana kupokea matokeo ya utafiti wa malezi na makuzi ya watoto katika familia lililofanyika hotel Protea jijini Dar es salaam, tarehe 26/8/2015.

  Kauli mbiu ni ‘FAMILI BORA TAIFA IMARA AULI MBIU’.
  Kulia; Naibu Waziri Mhe.Dkt  Pindi Chana (Mb)akisikiliza maelezo ya utangulizi ya Kongamano la Utafiti wa Malezi na Makuzi  ya Watoto katika Familia (kushoto) ni Kaimu Katibu Mkuu  wa wizara hiyo Bibi Nuru Millao aliyeongozana na Mhe. Naibu Waziri katika ufunguzi wa kongamano la kitaifa la familia katika hotel ya Protea, jijini Dar es salaam tarehe 26/8/2015
   Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Utafiti wa Malezi na Makuzi ya Watoto katika Familia wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Mhe. Dkt. Pindi Chana (MB hayupo pichani) katika Hotel ya Protea Courty yard jijini Dar es salaam tarehe 26/08/2015.

  0 0

    Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto), akimkabidhi kijana Prisca George Chilumba, msaada wa vifaa mbali mbali vya saluni ya wanawake kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye sehemu yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Ligula, Manispaa ya Mtwara jana. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew Masatu (wa pili kushoto) na rafiki wa Prisca. 
   Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto), akimkabidhi kijana Prisca George Chilumba, msaada wa vifaa mbali mbali vya saluni ya wanawake kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye sehemu yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Ligula, Manispaa ya Mtwara jana. Anayeshuhudia (katikati) ni Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew Masatu.
   Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto), akifafanua jambo baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbali mbali vya saluni ya wanawake kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, kwa kijana Prisca George Chilumba (kulia), katika hafla fupi iliyofanyika kwenye sehemu yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Ligula, Manispaa ya Mtwara jana. Anayeshuhudia ni Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.
   Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa pili kulia), akimpongeza kijana Prisca George Chilumba, baada ya kumkabidhi msaada wa vifaa mbali mbali vya saluni ya wanawake kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye sehemu yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Ligula, Manispaa ya Mtwara jana. Wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa Airtel.


  KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa imemuwezesha mjasiriamali Prisca George Chillumba ambaye ni mmiliki wa biashara ya saluni mkoani Mtwara. Prisca amenufaika na mradi huu kwa kupatiwa vitendeakazi mbalimbali vitakavyomuwezezesha kupanua wigo wa idadi ya huduma zitatakopatikana katika saluni yake. 

  Akikabidhi vifaa hivyo meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi amesema, sambamba na kuongeza idadi ya huduma zitakazopatikana katika saluni ya Prisca, vifaa hivi vitamuwezesha kuhudumia wateja wengi Zaidi kwa wakati mmoja, jambo ambalo litamuwezesha Prisca kuajiri vijana wenzie ili kuendeleza biashara na kukuza kipato chake.

  Bi Bayumi amesema, mpango huo wa kuwawezesha wajasiriamali unawapatia vitendeakazi vijana wajasiriamali ili kuwaongezea kasi ya maendeleo ya kibiashara vijana  hawa ambao tayari wameshachukua hatua na kuanza kujishughulisha na biashara ndogondogo.

   Lengo likiwa ni kurudisha sehemu ya mapato yake kwa jamii katika njia inayoleta tija.

  “Sisi kama Kampuni ya mawasiliano tumeona ni vizuri kushirikiana na wajasiriamali na hasa vijana ili kuhakikisha tunawawezesha na kukuza mitaji yao ya biashara kwa mafunzo na vifaa” alisema meneja huyo.

  Awali akipokea msaada huo Bi Prisca ameshukuru kwa vifaa hivyo na kuahidi kuendeleza zaidi biashara hiyo ili kutimiza ndoto zake za kuwa mfanyabiashara mkubwa.

  “Siamini kama naweza kufikia malengo yangu katika biashra hii, naahidi kuongeza juhudi na kutumia vyema msaada huu ili kuhakikisha nakuza na kuendeleza biashara yangu lakini pia nitatoa fursa kwa viajana wenzangu” Alisema Priscar.

  Kampuni ya simu ya Airtel inazunguka nchi nzima kukutana na vijana kwa lengo la kuwapa elimu ya ujasiriamali na kisha kutoa uwezeshaji kwa vijana ili waweze kukuza mitaji yao.

  0 0

  BASATA yaipongeza Kamati ya Miss Universe Tanzania
  Na Mwandishi wetu
  Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limeipongeza kampuni ya Compass Communications Tanzania kwa kufanya mashindano bora ya Miss Universe hapa nchini.

  Kauli hiyo imetolewa na  Mratibu wa mashindano ya Miss Universe Fausta Magoti wakati wa kufanya tathimini ya mashindano ya mwaka jana ambapo, Caroline Benard aliibuka mshindi.

  Magoti alisema kuwa pamoja na kampuni ya Compass kuanza kushiriki katika mashindano ya Miss Universe mwaka 2007, waliweza kufanya vyema na kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake.

  Mbali ya kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, Magoti alisema kuwa wameridhishwa sana na utendaji wa kamati hiyo kwa kuteua majaji ambao wamekuwa wakiwatangaza washindi ambao ni mfano bora kwa tabia kwa jamii.

  “Washindi wenu hawana kashfa katika jamii, mmeendesha mashindano yasiyokuwa na malalamiko, kwa kwa kweli mnahitaji kupongezwa pamoja na kupata changamoto nyingi kutoka kwa wadhamini,” alisema Magoti.

  Alitoa wito kwa waandaaji kupanua wigo wa mashindano yao na kuyafanya katika mikoa mingi ili kujitangaza zaidi. “Najua changamoto kubwa ni kuapata wadhamini, tunaomba mjitahidi ili kuyatangaza zaidi mashindano yenu, Basata tumeridhishwa na utendaji wenu, tunataka mfanye bora zaidi ya hapa,” alisema.

  Mrembo Flaviana Matata ambaye alimaliza katika hatua ya sita bora katika fainali za mashindano ya mwaka 2007, kwa sasa amekuwa akifanya vyema nje ya nchi katika sekta ya maonyesho ya mavazi au wanaminitindo.

  “Ni mashindano bora ambayo kwa kweli yametuvutia sana, tunaomba muongeze bidii ili kuyaboresha zaidi kwani mashindano haya kwa sasa ni makubwa na warembo wengi wanayaulizia jinsi ya kujiunga nayo,” alisema.
  Mkurugenzi wa Compass Communications ambaye pia ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai aliishukuru Basata kwa usimamiaji bora wa mashindano katika sekta ya sanaa nchini na kusema kuwa watajiathidi kuongeza wigo wa washiriki kaika mashindano ya mwaka huu.

  Maria alisema kuwa pamoja na changamoto zote wanazokabiliana nazo, bado wanahitaji msaada kutoka Basata ili kupata wadhamini.
  “Basata ni chombo cha serikali, mnaweza kutusaidia kupata wadhamini hata kwa Wizara ya Maliasili na Utalii, sisi tunatangaza jina la nchi na utalii pia, tunaamini kupitia kwenu, tunaweza kupata sapoti kubwa kutoka wizara hiyo, Bodi ya Utalii (TTB) na mamlaka ya zake kama Tanapa.

  0 0

   Kamanda Mpinga, akishiriki dua ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini, baada ya mazoezi yao timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kirafiki na timu ya Kamati ya Amani ya Mkoa wa Arusha unaotarajia kuchezwa mwezi ujao jijini Arusha na ule wa kirafiki kati yao na timu ya Mabalozi hivi karibuni. Kamanda Mpinga alifika kuwatembelea wachezaji hao kujionea maendeleo ya mazoezi yao. 
    Kamanda Mpiga akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini ya Mkoa wa Dar es Salaam,baada ya mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo asubuhi kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Kamanda Mpinga alifika kuwatembelea wachezaji hao kujionea maendeleo ya mazoezi yao.


   5:- Kamanda Mpinga, akisalimiana na walimu wa timu hiyo, baada ya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi. 
   6 hadi 10:- Kamanda Mpinga akisalimiana na wachezaji wa timu hiyo baada ya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
   Mchungaji wa Kanisa la Penuel Healing Ministry Ubungo Kibangu, Mch. Alphonce Temba (kulia) akimramba chenga Mchungaji wa Kanisa la KKKT Mashariki ya Pwania, George Fupe, wakati wa mazoezi yao yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi kwa ajili ya kujiandaa na michezo kadhaa ya kirafiki kwa ajili ya kuimarisha amani na mshikamano kwa watanzania.
   Ustaadh Sale  (katikati) akimiliki mpira katikati ya mabeki wa timu pinzani, wakati wa mazoezi ya timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa dini yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi kwa ajili ya kujiandaa na michezo kadhaa ya kirafiki kwa ajili ya kuimarisha amani na mshikamano kwa watanzania. 

  Picha ma www.sufianimafoto.com

  0 0
 • 08/26/15--05:47: TANZIA
 • Ndg.Robert Gondwe wa Dar es Salaam,anasikitika kutangaza kifo cha kaka yake Geofrey Boardington Gondwe kilichotokea jana(25.08.2015).

  Ataangwa kesho(27.08.2015) kwake Kunduchi saa 6 mchana na Mazishi yatafanyik makaburi ya kinondoni saa kumi jioni

  0 0  Na Mwandishi Wetu ,
  Kutokea kwa ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa (CHD) kunatazamwa kwa usawa kwa duniani kote, pamoja na kutofautiana kati ya mikoa na nchi kutokana na maumbile, mazingira na mabadiliko ya kiepijenetiki.

   Takriban watoto 8 kati 1000 wanaozaliwa wakiwa hai wanazaliwa na CHD duniani kote. Takwimu hii kwa ujumla inaaminika zaidi. Hata hivyo, kutokana na ukosefu wa takwimu sahihi katika bara la Afrika, watoto walioathirika na CHD barani Afrika inaweza kuwa wengi sana.

  Watoto wenye ugonjwa wa moyo wanaweza kuonesha dalili wakati wa kuzaliwa. baadhi ya dalili hizi ni pamoja mtoto kubadilika rangi na kuwa wa bluu, mtoto kupumua kwa kasi, jasho nyingi, kuvurugika kwa mapigo ya moyo, kushindwa kula ambapo husababisha kushindwa kuongezeka uzito na mtoto kupata maambukizi katika mfumo wa upumuaji mara kwa mara. 

  Wakati mwingine, hii inaweza kugundulika kwa kuhakikisha unamuona daktari wa watoto wachanga mara kwa mara. Tatizo lolote katika moyo linaweza kubadilisha namna moyo unavyosikika. Sauti hizi zisizo za kawaida zinaweza kugunduliwa na daktari kwa kusikiliza kutumia kifaa maalumu cha ‘stethoskopu’. Kuna baadhi ya matukio ambapo vichanga na watoto wadogo wanakuwa wakizimia, kuonyesha kwamba wako katika hali ya kushindwa kwa mizunguko upumuaji.

  Watoto, hasa walio chini ya umri wa siku 28 na vichanga ambao wako chini ya umri wa mwaka mmoja hawachukuliwi kama vijana, hivyo kuwafanyia upasuaji moyo kwao ni changamoto. Inapaswa kuzingatiwa kuwa moyo wa mtoto anapozaliwa unakuwa na ukubwa wa ngumi yake. Kutokana na muundo wake unaochanganya, watoto wachanga hukabiliwa na kiwango kidogo cha ufanyaji kazi wa moyo na hivyo kupata uharibifu kwa viungo vingine muhimu ikiwa ni pamoja na mapafu, figo na ini. Hivyo, kwa asili upasuaji wa moyo ni mgumu zaidi.

  Kutokana na ugumu wa upasuaji kwa mtoto, Dkt. Neville A.G Solomon Mshauri, Upasuaji wa Moyo kwa Watoto & Watu Wazima na Mkuu wa Idara ya Upasuaji Moyo kwa Watoto wa Hospitali ya Watoto Apollo, Chennai anaona kwamba mbinu zinazojumuisha mambo mbalimbali zitumike ili kuwa na mafanikio. Ili kufanya kwa usahihi upasuaji na marekebisho bila kuharibu miundo yoyote muhimu, mpasuaji ni muhimu kuusimamisha moyo wa mtoto, kukata usambazaji wa damu kwenye moyo na kukausha damu yote ili aweze kuona vema miundo ya ndani. Pamoja na utaratibu huu mgumu, wakati wa upasuaji ni wa muhimu na makini sana. Ugumu huongezeka kadiri upasuaji unapochukua muda mrefu. Ni muhimu kwa timu nzima kufanya kazi katika hali ya maelewano kwa lengo la pamoja la kuokoa maisha.


  Wakati mtoto anapohisiwa kuwa na ugonjwa wa moyo hatua ya awali ya kuchunguza hili ni kwa kufanya vipimo kama vile kuchukua X-ray ya kifua na ECG ambapo husaidia kuthibitisha uchunguzi. Mionzi ya sauti ya moyo (ECG) mara nyingi husaidia katika uchunguzi. Hii itatoa taarifa za kutosha kwa ajili ya mtaalamu na / au mpasuaji wa moyo na kuamua namna matibabu yanavyopaswa kufanyika. Kama vipimo vya ziada au zaidi vinahitajika, takwimu hizi zinaweza kupatikana kwa njia za uchunguzi kama wa kutumia katheta ya moyo na ‘anjiografia’, CT na MRI ‘anjiogramu’ ya moyo.

  Uboreshaji wa hatua hizi za uchunguzi umeongezeka ubora wa upasuaji kwa watoto. Daktari mpasuaji au mtaalamu wa moyo sasa utakuwa na mwongozo wa pande tatu za ugonjwa wa moyo kabla ya utekelezaji wa wake. Hii inatoa mpango bora wa upasuaji usiokabiliwa na matatizo wakati wa upasuaji na kwa hiyo matokeo ya upasuaji kuwa bora zaidi na yenye mafanikio zaidi.

  Kuna tiba kadhaa ambazo zinapatikana kwa sasa. Baadhi ya hizi ni pamoja na mbinu ya kutumia matundu madogo na upasuaji wa moyo kwa kuufungua na kuufunga. Mbinu ya matundu huweza kukamilika kwa siku moja tu na hii inaweza kufanywa na wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu wa magonjwa ya moyo kwa watoto. Utaratibu huu unahitaji kupatikana kwa vifaa vinavyowezesha  kuipata  mashimo midogo ya moyo ambayo imefungwa na valvu na kujificha ndani sana. Kwa mbinu hii  mtoto hapati maumivu ya kukatwa. Utaratibu huu hauhitaji  mashine ya upumuaji kuwekwa au mtoto kuwekwa katika chumba maalumu cha wagonjwa mahututi mtoto anaweza kupona kwa haraka zaidi na kurudi shule na hata kushiriki katika michezo.

  Namna  nyingine za matibabu ambazo zinaweza kutumika kwa watoto wenye hali mbaya zaidi ya moyo ni ile ya kuufungua na kuufunga moyo yaani (upasuaji). Upasuaji huu unaweza kufanywa kwa watoto wachanga wenye umri wa masaa manne hadi matano au wenye gramu 800. Kutokana na utata wa hali hii, umuhimu wa kutumia timu shirikishi unasisitizwa zaidi. Hata mtaalamu wa upasuaji awe mjuzi sana, atahitaji msaada kutoka kwa timu.

  Watu kadhaa wanahusika katika mchakato huu. Wauguzi wanashiriki katika kuwahudumia watoto ambao wamefanyiwa upasuaji wa moyo. Madaktari wa watoto wanashiriki kuwahuduma baada ya upasuaji kama vile kudhibiti maumivu, kudhibiti maambukizi na msaada wa kisaikolojia na teknolojia ya kisasa inaruhusu usahihi zaidi katika uchunguzi. Hii ni sehemu muhimu zaidi kuhakikisha maisha ya mtoto yanaendelea.

  Kwa mujibu wa Dkt Neville A.G Solomon wa Hospitali ya Watoto Apollo, Chennai, kinga ni bora kuliko tiba. Kuna njia nyingi ambazo mtu anaweza kujaribu na kuzuia ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa. Kliniki (ya mjamzito) kupata kipimo maalumu kitaalamu ‘echocardiography, ambacho hutumika kuchunguza moyo wa mtoto akiwa ndani tumbo la mama.

   Daktari bingwa wa Moyo unaweza kutambua kasoro za moyo mapema wiki ya kumi na nane ya ujauzito. Kwa hiyo ‘echocardiogram’ itawezesha wazazi kufanya maamuzi sahihi juu ya mustakabali wa mtoto kama kuna kasoro zilizogundulika katika moyo.

  Njia nyingine ambayo inaweza kuzuia au kupunguza hatari kwa kuepukana ndoa kati ya ndugu wa damu, kwa mama kuacha kutumia baadhi ya madawa, na kuepuka mionzi wakati wa ujauzito huweza kumfanya mtoto kuzaliwa na kasoro katika moyo na pia mama kuepuka maambukizi. Njia ya kawaida ya kuepuka ugonjwa wa baridi yabisi katika moyo wa mtoto ni kwa kupatiwa matibabu ya maambukizi katika  koo kwa wakati kwa kutumia antibiotiki.

  Timu ya wataalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto Hospitali ya Apollo Chennai inaona fahari kubwa kupambana dhidi ya maradhi ya moyo kwa watoto duniani kote. Hii imewezekana kutokana na uvumbuzi mashine za mawimbi ya sauti zinazobebeka na za ukubwa wa kompyuta ndogo (mpakato). Hii Inawawezesha kufika sehemu za mbali zaidi duniani na kuchunguza kasoro na magonjwa ya moyo.

  Baada ya upasuaji ingawa watoto wengi hutibiwa kikamilifu bado watahitaji ufuatiliaji kwa miaka ijayo. Baadhi wanaweza kuhitaji kurudiwa upasuaji hata hivyo wengi hawatahitaji dawa tena na kuwa na uwezo wa kuendelea na maisha ya kawaida kama watoto wengine. Wataweza wa kuishi wakiwa afya kwa muda mrefu maishani bila matatizo.

  Inachangiwa na:
  Dk Neville A.G Solomon
  Mshauri, Mtaalamu Upasuaji wa Moyo kwa Watoto & Watu Wazima na Mkuu wa Idara ya Upasuaji Moyo kwa Watoto
  Hospitali ya Watoto Apollo, Chennai.

  0 0

  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  akizungumza jambo na mlemavu wa miguu ndugu Joseph,mkazi wa kijiji cha Lwasho wilaya ya Momba,ambapo alimuahidi kumletea baiskeli ya kutembelea.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  akiombewa na Watawa wa kijiji cha Lwasho,mara baada ya kumaliza mkutano wa kampeni katika kijiji cha Lwasho,wilaya ya Momba.

  Palikuwa hapatoshi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchana wakati mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipowasili katika viwanja hivyo na kuwahutubia wananchi.
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tunduma waliofurika kwa wingi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma,mkoa wa Mbeya mapema leo mchana,kwenye mkutano wa kampeni wa kuwaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano,ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika Oktoba 25  mwaka huu.

  Palikuwa hapatoshi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchana wakati mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipowasili katika viwanja hivyo na kuwahutubia wananchi.
   Maelfu ya Wananchi wa Tunduma waliojitokeza  kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika uwanja wa shule ya msingin Tunduma mkoani Mbeya.

     Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya,Mh.Abbas Kandolo alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Nzoka Wilaya ya Momba mkoani humo,pichani kati ni Mgombea Ubunge wa jimbo la Mbozi Mh Godfrey Zambi.

  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mgombea Ubunge wa jimbo la Ileje Mh.Janet Mbene,mara baada ya kuwasili wilayani humo kuhutubia mkutano wa kampeni.
  Wananchi wakiwa wamefurika katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchama kumsikiliza mgombea urais wa CCM akimwaga sera zake kuwaomba Watanzania wamchague na kumpa ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano.
  Wananchi wa wilaya ya Ileje wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa katumba,Ileje mjini wakimshangilia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa kampeni wilayani humo.

  0 0  MISATAN to sharpen Bloggers & Editors’ skills on RTI, Election Reporting

  By Gasirigwa GS


  The Media Institute of Southern Africa (MISA) Tanzania Chapter in association with the Centre for ICT Policy promotion in Africa (CIPESA) will tomorrow train a selected number of bloggers and editors on Right to Information with special focus on this year’s general election.


  Editors and bloggers will be taught on the safest ways to access information and report responsibly during campaigns and the entire election period. Attention will be directed to the Cyber crime and the Statistics Acts which are already in effect and have dire consequences on media practice.


  Participants will also be introduced to ‘The Broadcasting Services (Content) (The Political Party Elections Broadcasts) Code 2015’ which was gazetted on June 26, 2015. Bloggers, SMS pollsters, and broadcasters in general will seriously be affected by this Code. The Code was developed by the Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA).


  About 20 selected Dar es Salaam-based editors and bloggers have confirmed to take part in this one-day workshop, scheduled for tomorrow Thursday the 27thof August at Kebbys Hotel in Dar es Salaam.


  Similar training was held two weeks ago in Mwanza and drew participants from Geita, Mara and Mwanza itself. The Mwanza training specifically targeted journalists who basically cover rural areas.


  MISATAN and CIPESA believe that the media needs to responsibly serve the public in a way that will provoke positive engagement and subsequent improvement in the political administration of the country.


  0 0

  Afisa Wa Elimu Zanzibar Bw Suleiman Yahya Ame kulia, akionesha makala ya kitabu.
  Na Abou Shatry Washington DC
  Jumuiya ya Wazanzibari waishio Nchini Marekani (ZADIA), imepongezwa kwa kusaidia gurudumu la maendeleo ya Elimu visiwani Zanzibar.
  Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Zanzibar Bw. Suleiman Yahya Ame wakati wa kupokea mchango wa vitabu vya Ufundi na Mafunzo ya Amali uliotolewa na ZADIA kwa ajili ya shule za ufundi visiwani humo.
  Akizungumza kama mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika mjini Zanzibar, Bw. Ame pia aliwashukuru Wanadiaspora hao kwa kuendeleza juhudi za kujenga jamii iliyoelimika Zanzibar.
  Aliendelea kusema "Tukiwa na mahitaji makubwa ya vitabu katika shule zetu, vitabu hivi vimewasili katika wakati mwafaka, na tunashukuru kwa msaada huu", na kungoeza kuwa juhudi kama hizi zitasaidia kuigeuza Zanzibar kuwa jamii inayojitosheleza kiajira.Alizitolea wito shule zilizofaidika na vitabu hivyo kuvitumia vizuri kwa lengo la kuisaidia Zanzibar kufikia malengo yake ya kielimu.
  Bwana Ame alimalizia kwa kuitolea wito ZADIA kupanua zaidi mfumo wa misaada yake ya kielimu na kujumuisha ujenzi wa madarsa na vitabu vya taaluma nyengine ambazo Zanzibar ina upungufu mkubwa, kama vile taaluma ya Fedha na nyenginezo.
  Naye Mwenyekiti wa ZADIA Bwana Omar Haji Ali, alisisitiza azma ya Jumuiya yake ya kuendeleza juhudi za kusaidia maendeleo Zanzibar.
  Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na mwakilishi wa ZADIA Zanzibar Bwana Mussa Shehe kwenye hafla ya makabidhiano ya vitabu hivyo, Bw. Ali alisema "ZADIA, tangu kuanzishwa kwake imekuwa msitari wa mbele katika harakati za kusaidia maendeleo Visiwani Zanzibar katika nyanja tofauti"
  Aliendelea kutamba kwa kusema kuwa, "Kwa vile ZADIA inaelewa kuwa daima maadui wakubwa wa maendeleo ya jamii wamekuwa wakivinjari kuzorotesha maendeleo hayo, basi jeshi letu siku zote liko imara kupambana na maadui hao ambao ni maradhi, ujinga na umaskini, na kuhakikisha kuwa milele hawatothubutu kujaribu kuyachokoza maendelea ya Wazanzibari.
  Aidha, Bwana Ali alisisitiza kuwa msaada huo wa vitabu siyo mwisho wa juhudi za ZADIA katika kusaidia sekta ya Elimu Zanzibar, bali ni mwendeleo wa mapambano dhidi ya adui ujinga.
  Alielezea matumaini yake kuwa msaada huu utakuwa ni changamoto kwa jumuiya nyengine za Wazanzibari ulimwenguni kushiriki katika kusaidia maendeleo Zanzibar.
  Bwana Omar aliwashukuru WanaZaida wote walioshiriki katika kufanikisha msaada wa vitabu hivyo, pamoja na shirikika la Goodheart-Willcox la nchini Marekani kwa ukarimu wao.Hafla hiyo ya makabidhiano ya vitabu, pia ilihudhuriwa na maofisa wa ngazi za juu kutoka Wizara ya Elimu Zanzibar, Maofisa wa Idara ya Diaspora katika Ofisi ya Rais wa Zanzibar, wawakilishi wa Vyuo vilivyokusudiwa kufaidika na msaada huo pamoja na wawalikishi wa vyombo mbalimbali vya habari vilioko Zanzibar.

  0 0

   
  Katibu wa taswa mkoa wa Arusha Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha la waandishi Agosti 29 uwanja wa kheikh Amri abeid mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Arusha, Filex Ntibenda,  kati kati mwenyekiti wa taswa mkoa Arusha, Jamila omar, Meneja matukio ya kampuni ya bia nchini TBL Chris Sarakana ambao wadhamini wakuu, na makamu mwenyekiti wa taswa Arusha, Andrea Ngobole
  .Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda,anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la 10 la vyombo vya habari  vya mkoa wa Arusha. ambalo litafanyika Agosti 29 katika uwanja wa sheikh Amri Abeid.

  Akizungumza na waandishi wa habari Palace hoteli   mwenyekiti wa TASWA mkoa wa Arusha, Jamila Omar  na Katibu wa TASWA Arusha,  Mussa Juma walisema maandalizi yote muhimu yamekamilika ikiwepo ujio wa timu ya TASWA kutoka jijini Dar es Salaam.
  Omar alisema Kauli mbiu ya Mwaka huu ya Tamasha hilo ni kuwa,Uchaguzi bila vurugu inawezekana na   timu zitachuana katika michezo ya Soka, mbio zamagunia, kuvuta kamba, kukimbiza kuku na mpira wa pete.
  Alisema mdhamini Mkuu wa Tamasha hilo ni Kampuni ya Bia nchini(TBL), ambapo wadhamini wengine ni TANAPA, Faidika, Mega Trade Investment,na SBC(T) Ltd.
  Omar aliwataja wadhamini wengine kuwa ni, Shilika na nyumba nchini(NHC), Kampuni ya Tanzanite One,Coca cola na Big Expedition.
  Akizungumzia tamasha hilo, Afisa matukio ya TBL Arusha, Chris Sarakana aliwataka wanahabari na wakazi wa mkoa wa Arusha kujitokeza na kuahidi TBL itaendelea kushirikiana na wanahabari.

  Awali Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha,Mussa Juma alitaja timu nyingine zitakazoshiriki ni TASWA Arusha, AJTC. Habari Maalum,Radio 5, Radio ,Faidika,Mj radio, Arusha one na ORS kutoka mkoa wa Manyara.
   Alisema kabla ya Tamasha wanahabari watatembelea hifadhi ya Taifa ya Arusha vile vile  kiwanda cha Bia nchini(TBL) mkoa wa Arusha na viwanda vya Mega Trade na Pepsi  mkoani hapa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya bonanza hilo

  0 0

   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu, akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM, uliofanyika leo katika stendi ya daladala maarufu kwa jina la Samunge, jijini Arusha leo
   Sehemu ya umati wa wananchi waliofurika kwenye mkutano huo jijini Arusha leo
   Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Ummy Mwalimu akimuombea kura mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo jijini Arusha
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Hawa Ghasia, akimuombea kura mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo jijini Arusha
   Mbunge wa Afrika Mashariki, Angela Kizigha, akimuombea kura mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo jijini Arusha

   Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda Kijiko, akimuombea kura mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo jijini Arusha
   Wananchi wakishangilia katika mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika jijini Arusha leo
   Wananchi wakiwa na bango wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika jijini Arusha leo
   Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika jijini Arusha leo
   Wananchi wakiwa na bago la kuonyesha imani kwa mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassani, katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo jijini Arusha.
   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu, akipokea kadi ya CUF kutoka kwa kada wa Chama hicho Sheikh Khalid Abubakar, aliyeamua kuhamia CCM wakati wa mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo jijini Arusha.
   Wananchi wakiwa na bango la kiutakia ushindi CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, wakati wa mkutano wa kampeni wa CCM, uliofayika leo Usa River, Arumeru mkoani Arusha leo
    Msafara wa Mgombea Mwenza wa Rais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, ukiwa njiani mkoani Arusha leo kuendelea na kampeni mkoani.
   Wananchi wakimlaki kwa furaha mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, alipowalisi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro.
    Kijana katika jimbo la Hai, Kilimanjaro akishangilia kiaina, Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan, alipowasili kwenye mkutano huo.
   Kina mama wakijimwayamwaya kumkaribisha Mama Samia kuhutubia mkutano wa hadhara leo katika jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro
  Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, Danstan Mallya katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Hai, Machame mkoani Kilimanjaro, leo
   Kinamama wakimlaki Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipowasili katika kuhutubia mkutano wa hadhara katika Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro leo.
   Kinamama wakimlaki Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipowasili katika kuhutubia mkutano wa hadhara katika Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro leo
  Mgombea ubunge jimbo la Siha kwa tiketi ya CCM, Aggrey Mwanri akimwaga sera, wakati wa mkutano wa kampeni za CCM wa Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika katika jimbo hilo leo
   KIMBUNGA: Baadhi ya wananchiwaliohudhuria mkutano wa hadhara wa Mgombea Mwenza a Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, katika kijiji cha Oloiwa, Kata ya Donyomorwa, Jimbo la Siha, wakijaribu kukifukuza kwa vidole kimbunga kipite nje ya mkutano, baada ya kimbunga hicho kilichoambatana na vumbi kali, kutokea ghafla wakati mkutano huo ukiendelea.
   Kinana Mama wakimtuza Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu, katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kijiji cha Oloiwa, jimbo la Siha leo
   Mgmbea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi mgombea ubunge jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro, Aggrey Mwanri katika mkutano huo leo
   Wananchi wa Usa River wakiwa wamejipanga kandoni mwa barabara, kumlaki Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan alipowasili kuhutubia mkutano wa kampeni leo katika eneo hilo la Usa River Arumeru mkoani Arusha leo
   
   Wananchi wakiwa wamefurika kwenye mkutano huo wa Usa River, Arumeru Mashariki mkoani Arusha leo
   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wananchi leo katika Viwanja vya Usa River, jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0

  Ndg.Robert Gondwe wa Dar es Salaam,anasikitika kutangaza kifo cha kaka yake Geoffrey Boardington Gondwe kilichotokea jana(25.08.2015).

  Ataangwa kesho(27.08.2015) kwake Kunduchi saa 6 mchana. Mazishi yatafanyika katika   makaburi ya Kinondoni saa kumi jioni.

  Sisi tulimpenda, lakini BWANA alipenda zaidi. Jina lake BWANA na lihimidiwe...
  AMINA!

  0 0

  Kamanda Mpinga, akisalimiana na walimu wa timu hiyo, baada ya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi
   Mchungaji wa Kanisa la Penuel Healing Ministry Ubungo Kibangu, Mch. Alphonce Temba (kulia) akimramba chenga Mchungaji wa Kanisa la KKKT Mashariki ya Pwania, George Fupe, wakati wa mazoezi yao yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi kwa ajili ya kujiandaa na michezo kadhaa ya kirafiki kwa ajili ya kuimarisha amani na mshikamano kwa watanzania.
   Ustaadh Saleh  (katikati) akimiliki mpira katikati ya mabeki wa timu pinzani, wakati wa mazoezi ya timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa dini yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi kwa ajili ya kujiandaa na michezo kadhaa ya kirafiki kwa ajili ya kuimarisha amani na mshikamano kwa watanzania.
   Shoot on target.....
   Kamanda Mpinga, akishiriki dua ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini, baada ya mazoezi yao timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kirafiki na timu ya Kamati ya Amani ya Mkoa wa Arusha unaotarajia kuchezwa mwezi ujao jijini Arusha na ule wa kirafiki kati yao na timu ya Mabalozi hivi karibuni. Kamanda Mpinga alifika kuwatembelea wachezaji hao kujionea maendeleo ya mazoezi yao. KWA PICHA ZAIDI BOFYA READ MORE

   Kamanda Mpinga, akishiriki dua ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini, baada ya mazoezi yao timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kirafiki na timu ya Kamati ya Amani ya Mkoa wa Arusha unaotarajia kuchezwa mwezi ujao jijini Arusha na ule wa kirafiki kati yao na timu ya Mabalozi hivi karibuni. Kamanda Mpinga alifika kuwatembelea wachezaji hao kujionea maendeleo ya mazoezi yao.
   Kamanda Mpiga akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini ya Mkoa wa Dar es Salaam,baada ya mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo asubuhi kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Kamanda Mpinga alifika kuwatembelea wachezaji hao kujionea maendeleo ya mazoezi yao.
   Kamanda Mpinga, akisalimiana na walimu wa timu hiyo, baada ya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
   Kamanda Mpinga, akisalimiana na walimu wa timu hiyo, baada ya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
   Kamanda Mpinga, akisalimiana na walimu wa timu hiyo, baada ya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
   Kamanda Mpinga, akisalimiana na walimu wa timu hiyo, baada ya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
   Kamanda Mpinga, akisalimiana na walimu wa timu hiyo, baada ya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
   Hapa ni mapande tu kama Yaya Toure.....
  Mchungaji Simon (kulia) akimfinya Ustaadh Saleh. Picha zote na www.sufianimafoto.com

older | 1 | .... | 619 | 620 | (Page 621) | 622 | 623 | .... | 1897 | newer