Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 612 | 613 | (Page 614) | 615 | 616 | .... | 1897 | newer

  0 0

                   Ni katika suala la uanzishaji viwanda ili kukuza uchumi.
    
  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda (Pichani)amesema Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) haina kuweka mkakati utakaohakikisha kuwa nchi wanachama zinakuwa na mpango mahsusi wa kuendeleza viwanda kama ambavyo imekubaliwa kwenye kikao chao kilichomalizika leo.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Agosti 18, 2015), wakati akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza mkutano wa 35 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini Gaborone, Botswana.

  “Jumuiya ya SADC kupitia sekretarieti yake itabidi iweke mkakati maamlu wa kufuatilia kama nchi wananchama imeandaa mapango wa kuendeleza viwanda kulingana na makubaliano yaliyofikiwa kwenye kikao cha leo,” alisema Waziri Mkuu ambaye ameshiriki kikao hicho kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete.

  Alisema yeye binafsi amefurahishwa na kupitishwa kwa azimio la uendelezaji wa viwanda katika nchi za SADC kwani unaendana na juhudi za Serikali ya Tanzania za kukuza uchumi kupitia uendelezaji wa viwanda vya usindikaji.

  “Nimefurahi kwa sababu azimio hili linaendana na mpango wetu wa kuendeleza viwanda wa mwaka 2015/2016 hadi 2020/2021. Sisi tumelenga viwanda vya kusindika mazao ya wakulima, wavuvi na wafugaji… kwa hiyo naamnini tutaenda vizuri na mpango mzima wa Jumuiya hii,” alisema.

  Kuhusu madeni ya michango kutoka kwa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo, Waziri Mkuu alisema Tanzania iko kwenye hatua nzuri ya ulipaji michango hiyo. “Jana nilipofika niliulizia suala hilo, nikaambiwa kwamba Tanzania imekwishalipa kwa kiwango cha kuridhisha. Nilitoa wito wakamilishe kulipa hiyo michango iliyobakia kwenye maeneo husika,” aliongeza.

  Mapema, Waziri Mkuu Pinda alisoma salamu maalumu mbele ya wakuu wa nchi na washiriki wa mkutano huo zaidi ya 500, zikiwa ni salamu maalum za kuwaaga zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete. Rais Kikwete anamaliza muda wake mwishoni mwa mwaka huu na hatapata nafasi nyingine ya kushiriki kikao cha wakuu wa nchi.

  Kikao kijacho kimepangwa kufanyika Agosti, 2016 nchini Lesotho ambapo Mfalme Letsie Mswati wa III alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wakuu wa nchi wanachama kwenye mkutano huo.

  Katika hatua nyingine, wakuu wa nchi  za Jumuiya ya SADC wamechangua Rais Ian Khama Seretse Khama kuwa mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo.

  Katika kikao hicho waliazimia kuendeleza mapambano dhidi ya magonjwa ya Kifua Kikuu, Malaria na kuazimia kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwenye nchi wanachama.

  Mbali na kusisitiza utunzaji na uhifadhi wa mazingira, waliazimia pia kila nchi itekeleze mpango wake wa kilimo ili kuwa na akiba ya kutosha hasa ikizingatiwa hali ya ukame ambayo imezikumba nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na kuashiria uhaba mkubwa wa chakula.

  Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea nchini leo jioni.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMANNE, AGOSTI 18, 2015.

  0 0

  al4
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifunguaMfereji ikiwa ni ishara ya kuzindua Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni leo katikaviwanja vya Mnara wa Mbao Kilimani Wilaya ya Magharibi A Unguja (katikati) Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni  Hamad Yusuf Masauni.
  al5
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimtwisha ndoo ya maji Fathiya Khamis Husein (Suza)baada ya kuzindua Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni leo katika viwanja vya Mnara wa Mbao Kilimani Wilaya ya Magharibi A Unguja.

  al1

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) huko Bavuai Migombani Mkoa wa Magharibi Unguja leo alipofika kuzindua Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni
  al2
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuzindua  Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni leo katika  Kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) huko Bavuai Migombani Mkoa wa Magharibi Unguja,(kutoka kushoto) Nd,Abdalla Suleiman  Mkuu wa Kituo cha maendeleo ya Vijana (Tanzania Youth ICON) na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni  Hmad Yusuf Masauni.
  al3
  Wafanyakazi wa Mamlaka ya maji ZAWA wakiwa katika sherehe za uzinduzi wa Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni leo uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika Mnara wa Mbao Kilimani Wilaya ya Magharibi A Unguja
  al6
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo wakati alipotembelea mabanda ya maeonesho ya kazi mbali mbali katika kituo cha Maendeleo ya Vijana Mwembe madema leo akiwa katika ziara ya kuzindua Mradi wa Maji na Kituo hicho katika Jimbo la Kikwajuni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
  al7
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha maendeleo ya Vijana (Tanzania Youth ICON) Nd,Abdalla Suleiman  (kulia)wakati alipotembelea kituo hicho Mwembe Madema kuona maendeleoya kazi mbali mbali zinazofanywa na vijana wa Jimbo la Kikwajuni  sambamba na uzinduzi wa Mradi wa Maji safi na Salama katika Jimbo hilo leo.
  al8
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheinalipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Maji safi na Kituo cha maendeleo ya Vijana (Tanzania Youth ICON) huko Mwembe madema Jimbo la Kikwajuni leo.
  al9
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Maji safi Jimbo la Kikwajuni samba mba na  Kituo cha maendeleo ya Vijana (Tanzania Youth ICON) huko Mwembe madema leo.

  0 0
 • 08/18/15--07:23: Article 2
 • JESHI  la Polisi  Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatarajia kuzindua mashindano ya michezo mbalimbali kwa lengo la kuwashirikisha wananchi  wa  rika zote  na  itikadi  mbalimbali 
  yatakayojulikana“KAMISHNA KOVA CUP”.

   Madhumini ya mashindano haya ni  ni  Kuwaunganisha wananchi wenye itikadi mbalimbali ili kupitia mashindano  haya  watakaoshiriki  watajifunza  masuala  ya usalama, uzalendo  na kuzingatia utaifa kwa madhumuni ya kuwashirikisha kikamilifu katika ulinzi wa nchi na kudumisha amani  na  utulivu  katika  jiji  la  Dar  es  Salaam  na  mikoa mingine.

  Lengo lingine ni  Kuishirikisha jamii  kuondokana na dhana ya kutenda uhalifu wa aina mbalimbali kama vile ujambazi, matumizi ya aina mbalimbali ya  madawa ya kulevya,  wizi katika mitandao,uzururaji, na kukaa katika vijiwe bila kazi.

  Pia  Kupitia michezo mbalimbali, jamii itafaidika kupata elimu juu ya umuhimu wa jukumu la msingi la kushiriki katika ulinzi na usalama  wa  nchi  hii,  itakuwa  ni  fursa  nzuri  kujua madhara ya kujihusisha na vitendo vya uhalifu.

  Katika michezo watajifunza kujenga au kuimarisha mahusiano mema baina ya Jeshi la Polisi na  jamii  kwa  ujumla  kupitia  dhana  ya  Polisi  Jamii itatekelezwa kwa vitendo.

  0 0

   WAZIRI wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais, (anayeshughulikia masuala ya Muungano), Samia sSuluhu Hassan,(wapili kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Sabasaba Moshingi, (wakwanza kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Property International Ltd, (PIL), Abdulkarim Haleem, (watatu kulia), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji, Gabriel Silayo, (wane kulia), wakiwa wamekamata mwamvuli ikiwa ni ishara ya umoja, kwenye uzinduzi wa mpango wa kukopesha viwanja wanachama wa PSPF ambapo TPB itaratibu ukopeshwaji huo kwa kutoa fedha. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam Jumanne Agosti 18, 2015.

   Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano), Samia Suluhu Hassan, akitoa hotuba.

   Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Gabriel Silayo, akitoa hotuba yake

   Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, TPB, Sabasaba Moshingi, akitoa hotuba yake

   Msanii wa muziki wa majigambo, Mrisho Mpoto, ambaye pia ni balozi wa PSPF, akitoa burudani kwenye hafla hiyo.

   Mh. Samia Suluhu Hassa, akimpongeza Silayo baada ya kutoa hotuba yake. Wanaoshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi,(kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa PIL, Abdulkarim Haleem.

  NA K-VIS MEDIA
   MFUKO wa wa Pensheni wa PSPF kwa kushirikiana na  Benki ya Posta Tanzania, TPB, na Taasisi ya Property International Ltd leo Agosti 18, 2015 wamezindua mpango maalum wa kutoa mikopo ya viwanja kwa wanachama wa mfuko huo katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Hyatt Regency.  Lengo la mkopo huu wa viwanja ili kuwawezesha wanachama wa mfuko huu kumiliki viwanja vilivyopimwa na vilivyo halali kwa mujibu wa taratibu za nchi. Nia ni kwenda sambamba na dira ya PSPF ambayo ni kutoa huduma bora zenye ushindani katika sekta ya Hifadhi ya  Jamii kwa wateja wa PSPF, na pia kuitikia mwito wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),walioagiza Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii kutoa mafao kwa fomula iliyo sawa kwa watumishi wote.

   Hivyo kuanzia wakati huo Mifuko ya Hifadhi inapaswa kushindana kwa ubora wa huduma na vivutio vingine kwa wananchama na wananchama watarajiwa.  Ni dhahiri kuwa kila Mtanzania anahitaji kuwa na makazi bora ya kudumu, hivyo mpango huu unaozinduliwa leo hii ni mpango mzuri sana hasa kwa Watanzania wengi ambao hawana uwezo wa kutoa fedha taslimu. 

  Utaratibuu huu wa kuwakopesha utawanufaisha wengi  na hatimaye kufikia kauli mbiu ya Serekali yetu ya kuhakikisha Maisha bora kwa kila Mtanzania.

  Mfuko wa Penshini wa PSPF umeendeleza ushirikiano wake mzuri na Benki ya Posta Tanzania, ambapo kama mnavyofahamu ushirikiano wao ulianzia kwenye utoaji wa Mikopo kwa Wastaafu, Mkopo wa Elimu na Mkopo wa kuanzia Maisha kwa wanachama wapya.

   Jitihada hizi zote ni katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wanachama wake, na pia katika kuonesha imani kwa Benki ya Posta, ambayo huduma zake bora zinapatikana kote nchini. Mahusiano haya na Property International Ltd yanazidi kujenga mahusiano haya kwa maslahi ya wanachama na Watanzania kwa ujumla.  Wanachama wa PSPF waliochangia Mfuko kwa kipindi kisichopungua miezi sita wanasifa zote za kuweza kukopa viwanja hivi, na watapaswa kulipa ndani ya miaka mitatu. Wanachama walio katika mpango wa Uchangiaji wa Hiari pia watafaidika na mkopo huu. Wanachama wote wa Mfuko wa Hifadhi wa PSPF wanakaribishwa sana kupata mkopo huu maalum kwa ajili yao.

   Mgeni Rasmi, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PSPF.

   Mgeni rasmi, Samia, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TPB.

  Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PIL.
  Moshingi, (kushoto), akibadilishana mawazo na Meneja Masoko wa PIL Zohra Moore, (kulia)
   Mh. Samia, (kulia), akisindikizwa na Silayo, wakati akiondoka ukumbi wa Hotel ya Hyatt, baada ya hafla hiyo.
  Moshingi (kulia), akisalimiana na Mh. Samia Suluhu Hassan, wakati akiwasili kwenye hafla hiyo.

  0 0

  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi,katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam kuhusiana na uteuzi wa kamati ya Kampeni  kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015,ambayo itaongozwa  na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na  Wajumbe

  Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa jana Agosti 17, 2015 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete imekamilisha kazi ya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo mawili ya Singida Mashariki na Kiteto.

  Wagombea ubunge walioteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika majimbo hayo ni pamoja na Ndugu Jonathan Njau (Singida Mashariki) na Ndugu Emmanuel Papian John (Kiteto).

  Aidha Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Kamati ya Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. Wajumbe wa Kamati hiyo ni kama ifuatavyo;-
  1.
  KAMATI YA KAMPENI YA CHAMA CHA MAPINDUZI
  1. Ndugu Abdulrahman Kinana - Mwenyekiti
  2. Ndugu Rajab Luhwavi - Makamu Mwenyekiti - Bara
  3. Ndugu Vuai Ali Vuai - Makamu Mwenyekiti - Z'bar
  4. Ndugu Sofia Simba
  5. Ndugu Mohamed Seif Khatib
  6. Ndugu Asha-Rose Migiro
  7. Ndugu Samwel Sitta
  8. Ndugu Nape Nnauye
  9. Ndugu Mwigulu Nchemba
  10. Ndugu Harrison Mwakyembe
  11. Ndugu January Makamba
  12. Ndugu Amina Makillagi
  13. Ndugu Christopher Ole Sendeka
  14. Ndugu Stephen Wasira
  15. Ndugu Abdallah Bulembo
  16. Ndugu Hadija Aboud
  17. Ndugu Mohamed Aboud
  18. Ndugu Lazaro Nyalandu
  19. Ndugu Issa Haji Ussi
  20. Ndugu Waride Bakari Jabu
  21. Ndugu Mahmoud Thabit Kombo
  22. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
  23. Ndugu Maua Daftari
  24. Ndugu Stephen Masele
  25. Ndugu Pindi Chana
  26. Ndugu Shaka Shaka
  27. Ndugu Makongoro Nyerere
  28. Ndugu Bernard Membe
  29. Ndugu Sadifa Juma Khamis
  30. Ndugu Antony Diallo
  31. Ndugu Livingston Lusinde
  32 . Ndugu Ummy Mwalimu


  Imetolewa na:-
  Nape Moses Nnauye,

  KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
  ITIKADI NA UENEZI

  18/08/2015

  0 0


   Afisa Mkuu wa Biashara wa Airtel Tanzania, Arindam Chakrabarty
  (kushoto), Kamishna Msaidizi wa Wizara ya Fedha, Ridhiwan Masudi
  (kulia) na Mkurugenzi wa Afb Tanzania, Wayne Stocks  wakionyesha bango
  kama ishara ya uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo kwa mawakala wa
  Airtel Money ijulikanayo kama ‘Timiza Mikopo kwa Wakala’, katika hafla
  iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
   Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya
  akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo kwa mawakala 
  wa Airtel Money ijulikanayo kama ‘Timiza Mikopo kwa Wakala’, katika 
  hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kulia) ni
  Mkurugenzi wa Afb Tanzania, Wayne Stocks, Kamishna Msaidizi wa Wizara
  ya Fedha, Ridhiwan Masudi na Afisa Mkuu wa Biashara wa Airtel
  Tanzania, Arindam Chakrabarty.
  3) Afisa Mkuu wa Biashara wa Airtel Tanzania, Arindam Chakrabarty
  akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo kwa mawakala 
  wa Airtel Money ijulikanayo kama ‘Timiza Mikopo kwa Wakala’, katika 
  hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kulia) ni
  Mkurugenzi wa Afb Tanzania, Wayne Stocks na Kamishna Msaidizi wa
  Wizara ya Fedha, Ridhiwan Masudi.
  Baadhi ya mawakala wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
  uzinduzi wa huduma ya Timiza Mkopo kwa wakala, huduma itakayowawezesha
  kupata mikopo isiyo ya dhamana kupitia huduma ya Airtel Money.

  Airtel yatoa Mikopo kwa Mawakala wa Airtel Money
  *          Mikopo isiyo na dhamana
  *          Zaidi ya mawakala 20,000 kunufaika
   KAMPUNI ya simu za mkononi
  ya Airtel kwa kushirikiana na Afb Tanzania imezindua huduma ya mikopo
  kwa wateja wa Airtel Money ijulikanayo kama "Timiza Mkopo kwa Wakala",
   itakayowawezesha  mawakala wa Airtel Money nchini nzima kupata mikopo
  isiyo na dhamana ya kuanzia shilingi 50,000 hadi 500,000.

  Akiongea wakati wa uzinduzi, Afisa Mkuu wa Biashara Airtel , Bwana
  Arindam Chakrabary alisema" Airtel inatambua kuwa mawakala wetu
  wanatafuta fursa ya kukuza biashara zao na kuongeza mitaji. Na leo
  tunayo furaha kuzindua huduma ya kwanza Tanzania na Afrika "Timiza
  Mkopo kwa Wakala" mikopo isiyo na masharti mahususi kwa mawakala wetu.

  Huduma hii ya mikopo kwa mawakala  itawanufaisha mawakala zaidi ya
  20,000 nchi nzima,  na tunaamini mikopo hii itasaidia kukuza biashara
  za mawakala wetu , kuwaongezea faida zaidi na hatimaye kuboresha
  upatikanaji wa huduma za kifedha"

  Chakrabarty aliongeza kwa kusema" Mwaka jana tulizindua huduma ya
  Timiza kwa wateja wetu nchini nzima,  ambayo kwa sasa ina zaidi ya
  wateja milioni 7 wanaoweza kupata mikopo ya haraka isiyo na masharti
  kwa urahisi , mikopo ambayo inawasaidia kutatua changamoto za kijamii
  na kiuchumi.

   "Timiza Mkopo kwa Wakala" itatoa kwa mawakala wetu wa
  Airtel Money uhuru wa kupata mikopo ya  haraka isiyo na masharti bila
  kupitia njia ndefu zakupata mikopo katika mfumo wa kawaida. Tunaamini
  huduma hii inatasaidia na kuwawezesha mawakala wa Airtel Money kupata
  fedha za kutatua mahitaji yao ya muda mfupi na mrefu wakati wote.

  Aliongeza
  Naye Msimamizi  Mkuu Afb Tanzania, Rwebu Mutahaba, amesema  " Mawakala
  wanapata mikopo kulingana na matumizi yao ya simu ndo mana tumeweza 
  kuwaamini na  kuwapatia mikopo isiyo na masharti.  Lengo kubwa ni 
  kuwapatia watu fulsa ya kupata huduma ya kisasa na kibunifu ambayoa 
  haijawahi kutolewa kabla. 

   Afb Tanzania tunajivunia ushirika huu na 
  Airtel ambao umetuwezesha kutoa suluhisho kwa wateja wa Airtel , 
  mikopo kwa mawakala ni moja ya huduma nyingi za kibunifu tulizonazo na 
  tunazopanga kuzindua katika mienzi ijayo nchini Tanzania".

  Timiza Mkopo kwa Wakala" ina viwango na riba tofauti zenye marejesho
  ya ndani ya siku saba, wiki mbili au mwezi mmoja. 

  Kiasi cha kukopa
  kitategemeana na matumizi simu ya wakala na jinsi anavyorudisha mkopo
  wake kwa wakati. Mteja atakapo rudisha mkopo wake ndani ya siku 7,14
  au 28 mojakwamoja atawezeshwa kupata mkopo mwingine.

   Inachukua dakika 
  moja kwa mteja kujaza fomu ya kuomba mkopo kupitia simu yake  na kisha 
  mara baada ya kujaza pesa zinawekwa kwenye akaunti yake ya Airtel 
  Money hapohapo".

  alisema Mutahaba 
  Kwa upande wake, kwa niaba ya Katibu Mkuu, Kamishna Msaidizi Wizara ya 
  Fedha, Bwana Ridhiwan Masudi alisema"  sisi kama Serikali 
  tumefurahishwa na hatua walioichukua Airtel katika kuboresha mfumo 
  rasmi wa kifedha kupitia huduma ya Airtel Money.  Tunafurahi  kuona 
  huduma ya Airtel Money  ikikuwa kwa haraka na kuwafaidisha watanzania 
  wakawaida hususani wanaoishi katika maeneo ya pembe zoni mwa nchi.

  Napenda kuchukua fulsa hii kuwaomba Airtel waendelee kuleta bidhaa na
  huduma za kibunifu ili kuweza kuipatia jamii huduma bora za
  mawasiliano na kukuza zaidi huduma za kifedha."

  Mawakala wa Airtel Money wanaweza kujipatia mikopo kwa kupiga
  *150*60#, na kuchagua 4  ili kupata orodha ya mikopo kwa wakala , na
  kisha kuingiza namba ya simu na namba ya siri  na baada ya hapo
  wataunganishwa kwenye orodha ya mikopo ya Timiza.

  0 0

   Daktari Hafidh Ameir toka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) akitoa elimu juu ya umuhimu wa kupima afya kwa wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Semina iliyofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
     Mfanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marcelina Henry akichukuliwa vipimo vya shinikizo la damu na Muuguzi toka Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, Asma Msimbe wakati wa zoezi la kupima afya kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
     Bwana Ponela John wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akichukuliwa vipimo vya urefu na Bwana John Joseph wa Timu ya Wataalamu waliofika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ajili ya kupima afya za wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
  Mfanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bi. Radhia Said akichukuliwa vipimo vya urefu na Bwana John Joseph wa Timu ya Wataalamu waliofika Wizara hapo kwa ajili ya kuendesha zoezi la kupima afya za wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam. 

  0 0

  Aliyekuwa  mgombea wa nafasi ya Urais Monica Mbega jukwaani  akimwombea  kura  mgombea  urais wa  CCM na mgombea  ubunge jimbo la Iringa mjini Frederick Mwakalebela (aliyekaa katikati kulia) leo  baada ya  mwakalebela  kuchukua  fomu ya ubunge
  Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Bw  Abeid Kiponza  (kulia) akimtambulisha mgombea  ubunge jimbo la Iringa mjini Frederick Mwakalebela  leo
  Monica Mbega  akimwombea  kura  mgombea  ubunge jimbo la Iringa mjini leo
  Monica  Mbega  akimpongeza  Mwakalebela
  Monica  Mbega  akijiandaa kumsalimia Kiponza.

  Mwakalebela  akizungumza na  wana CCM leo.
  Mgombea udiwani wa kata ya Mtwivila Bw Jose Mgongolwa (kulia) akitambulishwa na Mwakalebela.

  Mgombea  udiwani Bw Chatanda  kulia  akitambulishwa na Mwakalebela
  Mwakalebela akimtambulisha Ibrahim Ngwada (kulia) mgombea udiwani kata ya Mshindo
  Mgombea  udiwani  wa  kata ya Mvinjeni akitambulishwa
  Mgombea  udiwani wa kata ya Mkimbizi Bi Farida Mpogole  akitambulishwa na Mwakalebela
  Mwakalebela  akimtambulisha mgombea udiwani wa kata ya Gangilonga Bw Nicholina Lulandala
  Mwakalebela  akimtambulisha mgombea udiwani wa Kwakilosa Bw Himid Mbata (kulia)
  Mwenyekiti  wa CCM wilaya ya  Iringa mjini Bw Abeid  Kiponza  akimtambulisha  mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia  CCM Bw  Frederick Mwakalebela (kushoto)

  Na Matukiodaima BLog.
  ALIYEKUWA mmoja  kati ya  wagombea  wa nafasi ya  urais  kupitia  chama  cha mapinduzi (CCM) na mbunge  wa zamani wa jimbo la  Iringa mjini Bi  Monica  Mbega amesema  kuwa mbali  ya kuwa  yeye  alikuwa ni mmoja kati ya  walioomba kuteuliwa  kuwania nafasi ya  urais na  jina lake  kukatwa bado hana  kinyongo na mteuliwa  wa CCM Dr  John Magufuli kwani anamkubali kwa  asilimia 100 kuwa ni chaguo la watanzania kama  ilivyo  kwa mgombea  ubunge  wa CCM jimbo la Iringa mjini Bw  Frederick Mwakalebela .

  Mbega  ambae  alikuwa ni mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini kwa  vipindi  viwili kati ya   mwaka 2000  -2010 alitoa kauli  hiyo  leo   wakati akizungumza na  wanachama  wa CCM katika  viwanja  vya CCM wilaya ya  Iringa mjini wakati  wa mgombea  mteule wa  ubunge  jimbo hilo la Iringa mjini Bw Mwakalebela  kutoka  kuchukua fomu  kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini kwa ajili ya  kuwania  ubunge kupitia  CCM.

  Alisema  kuwa katika  mchakato wa ndani ya  chama wa  kuwania kuteuliwa  kugombea  Urais yeye  alikuwa ni kati ya  wanachama zaidi ya 40  waliojitokeza kuchukua fomu akiwemo Dr. Magufuli na  kuwa baada ya  vikao  vya  juu vya  chama  kukamilisha taratibu za  kumpata  mgombea mmoja hakuwa na kinyongo  cha  kuhama  chama  wala kukaa nyuma katika mambo ya chama na ndio maana ameamua  kurejea nyumbani kwake  ili  kuungana na  wana CCM kurejesha  jimbo  hilo kwa  CCM na  kuwapigia kampeni wagombea wote wa CCM akiwemo mgombea  wa nafasi ya urais Dr  Magufuli na madiwani pia.

  "Kweli  nawapongeza  sana wananchi  wa  Iringa mlinipa udhamini wa kutosha  wakati wa mchakato wa kuomba  kuteuliwa  kuwa mgombea  Urais wa CCM nilipata  watu 45 kati ya 35  waliokuwa  wakihitajika kweli ni  watu  wengi  sana na baada ya  mchakato  jina langu halikupitishwa na jina la mwenzetu Dr Magufuli ndie  aliyeteuliwa na kazi  yetu ni  kumuunga mkono kwani  kati ya  watu wote  41  ni nafasi mmoja pekee ndio ilitakiwa ....hivyo hakuna haja ya  kuwa na kinyongo kwa  kuhama  chama chetu "

  Mbega  aliwataka  wana CCM jimbo la Iringa mjini kuweza kuunganisha  nguvu  zao kwa mgombea  ubunge Bw Mwakalebela ili  kuweza kulikomboa  jimbo  hilo na  kuhakikisha mgombea Urais na madiwani   wa CCM wanapata  kura  za  kishindo  zaidi katika  jimbo la Iringa mjini .

  Alisema  kwa  wanachama wa CCM ambao  waligombea nafasi mbali mbali na kura  kutotosha katika nafasi  walizoomba wanapaswa  kuvunja makundi  yao na  kuunganisha nguvu  zao kwa wale  walioshinda  ili  kufanya kazi ya  kujenga  chama badala ya  mtu .

  Hata  hivyo  alisema kwa upande  wake atapambana kwa nguvu  zote  kuhakikisha chama kinapata ushindi mkubwa katika  jimbo  hilo la Iringa mjini na kudai  kuwa  kazi kubwa  iliyopo mbele kwa  wana CCM ni kujenga utamaduni  wa  kusamehe na kusonga  mbele.

  Katibu  wa  CCM wilaya ya  Iringa mjini Elisha Mwampashi akimkaribisha  mwenyekiti  wa CCM wilaya ya Iringa mjini Bw Abeid Kiponza  kumtambulisha rasmi mgombea  ubunge wa jimbo  hilo ,alisema  kuwa ni  lazima  watanzania na  wananchi  wa jimbo la Iringa mjini  kuwapuuza  wale  wote  wanaohama  CCM mara  baada ya  kushindwa katika  kura  za maoni na kuwa watu hao  hawana mapenzi  mema na Taifa  bali  wapo kwa ajili ya maslahi yao  zaidi .

  Mwampashi  alisema kuwa kinachoshangaza ni kuona UKAWA  ambao  walikuwa mbele  kupinga vitendo  vya ufisadi na kumtuhumu  wazi wazi waziri  mkuu mstaafu Edward  Lowasa  kuwa  si  mtu msafi  leo  wamempokea na kuwa mgombea  wao wa nafasi ya urais jambo ambalo  watanzania  wanapaswa  kujiuliza  juu ya mwenendo wa UKAWA katika Taifa  hili.

  Mwenyekiti  wa CCM Iringa mjini Bw  Kiponza  alisema kuwa kazi kubwa ya CCM jimbo la Iringa mjini ni  kulikomboa jimbo  hilo  kutoka kwa aliyekuwa mbunge  wa  jimbo  hilo mchungaji Peter  Msigwa (chadema) ambae hakuna  maendeleo  yoyote  aliyoyaleta katika  jimbo  hilo kwa kipindi  chote cha miaka  mitano  zaidi ya wana Iringa  kusababishiwa kupigwa mabomu na lugha  zisizofaa majukwaani .

  Hivyo  alisema wana Iringa wanayosababu ya  kusema basi kuendelea  kukosa maendeleo na  kufanya maamuzi  sahihi ya  kukirejesha  chama cha mapinduzi madarakani kwa kumchagua mchapa kazi Bw  Mwakalebela ambae  kwa  muda  wake  mfupi  wa ukuu  wa wilaya ya wanging'ombe kazi kubwa amepata  kuionyesha na hivyo ni zamu ya  wana Iringa  kushuhudia maendeleo  hayo kwa  kumchagua  kuwa mbunge  wa  jimbo  hilo .

  " Toka  ameondoka  Mbega mwaka 2010  kwa  kuanzisha  miradi ya barabara na maji ya JR hakuna mradi  ulioendelea  chini ya  ubunge wa Msigwa  zaidi ya maandamano na mabomu kila  wakati na kupinga  wananchi  kushiriki katika shughuli za kimaendeleo"

  Kwa  upande  wake mgombea  huyo wa ubunge  jimbo la Iringa mjini Bw  Mwakalebela  alisema kuwa  chini ya ilani ya  CCM serikali imefanikiwa  kuleta maendeleo  kila kona ya nchi hii na hadi sasa  wapo  wanaopinga  kuwa akili ndogo haiwezi  kutawala akili kubwa ila ukweli upo  wazi  kwa  wana Iringa  kuona kasi  kubwa ya miradi ya maendeleo  iliyoletwa na CCM inayoongozwa na wenye akili ndogo kama  mbunge wa  jimbo  hilo anavyojinasibu majukwaani na kuwa haja ya  wananchi kumhoji mwenye akili kubwa ni ahadi gani aliyoahidi ambayo amepata  kuwatimizia  wananchi  wake .

  Mwakalebela  alisema  kuwa ni  wakati mzuri kwa wana Iringa  kupima akili ndogo na kubwa katika maendeleo na  sio katika majukwa  ya  siasa na mwisho wa  siku shughuli  za maendeleo  zinasimama na wananchi kushuhudia maandamano kila uchwao .

  Alisema  kuwa  iwapo  wananchi  wa Iringa  watamchagua kuwa mbunge wa  jimbo  hilo Octoba 25 mwaka  huu  wawe na matumaini mapya ya  kimaendeleo   ikiwa ni pamoja na  kuanzisha mfumo mzuri wa  kuwakomboa  wanawake na vijana  kiuchumi kwa  kuwapa  mikopo nafuu.

  0 0
 • 08/19/15--06:30: MUZIKI MNENE BANGO BOKO
 • Jimmy Jiam akiwa na washindi wa Muzuki Mnene Bango  eneo la Kisarawe. Washindi hao walitokana na kuwenga bango la EFM katika sehemu zao mbalimbali  na kama wanavyoonekana tayari wamekabidhiwa zawadi zao.


  0 0

  Na Benedict Liwenga, MAELEZO.
  SERIKALI imekanusha taarifa zilizojitokeza kwenye Vyombo vya habari yakiwemo magazeti na mitandao ya kijamii kwamba Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kitafanya mkutano hadhara Uwanja wa Taifa Dar es Salaam tarehe 22 Agosti, 2015.

  Akizungumza na vyombo vya habari jana, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene alisema serikali haijatoa ruhusa kwa chama chochote cha siasa kutumia uwanja wa taifa kwa ajili ya shughuli za kisiasa.

  Alikiri kwamba ni kweli kwamba CHADEMA waliiandikia Wizara tarehe 12 Agosti, 2015 kutaka kutumia uwanja wa taifa katika uzinduzi wa kampeni lakini ombi lao lilikataliwa kwa maelezo kwamba uwanja ule kwa mazingira ya sasa hauruhusiwi kutumika kwa ajili ya mihadhara ya vyama vya siasa.

  “kwa kipindi haturuhusu uwanja wa taifa kutumika kwa mihadhara ya kampeni za vyama vya siasa. Uamuzi huu unalenga kuweka uwanja katika mazingira rafiki ya michezo na kuepuka athari zozote zinazoweza kujitokeza kutokana na mihemuko ya kisiasa” alisema Bwana Mwambene.

  Mwambene ameeleza kuwa, Serikali imeamua uwanja huo ubaki kwa ajili ya kufanyia shughuli zake za msingi za kimichezo ili kuepuka mihemuko na athari yoyote inayoweza kujitokeza kutokana na hamasa za kisiasa.

  “Ni kweli kwamba tulipata barua ya Chadema kuomba Uwanja kutumika kwa ajili ya mhadhara ya kisiasa wa CHADEMA hasa kuzindua Kampeni zao kwenye Uwanja tayari tumeshawaandikia kuwaarifu kuwa Uwanja ule hauwezi kutumika kwa ajili ya shughuli zozote za kisiasa” alisema Bwana Mwambene.

  Alisema vyama vyovyote vitakavyoomba kutumia Uwanja ule kwa shughuli za kisiasa havitaruhusiwa.
   Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) akikanusha kuhusu Chadema kutumia Uwanja wa Taifa kuzindua kampeni zake siku ya tarehe 22 Agosti, 2015 jijini Dar es Salaam. Kanusho hilo lilitolewa katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) uliopo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa kutoka Serikalini kuhusu Chadema kutumia Uwanja wa Taifa kuzindua kampeni zake siku ya tarehe 22 Agosti, 2015 jijini Dar es Salaam. Kanusho hilo lilitolewa katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) uliopo jijini Dar es Salaam.
  PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA.

  0 0  0 0


  mwendaPichani: Bi. Janet Sosthenes Mwenda

  Na Andrew Chale, Modewjiblog
  (Dar es Salaam). Mmiliki na Mweneshaji wa kipindi cha 'Ongea na Janet' Bi. Janet Sosthenes Mwenda kwa sasa anakuja na ujio mpya wa kipindi kinachoelezea masuala ya kuwalinda Watoto kwa kutoa elimu kiitwacho ‘Tuwalinde Watoto Wetu’ ambacho kinatarajiwa kuonekana kupitia kituo cha televisheni cha Clouds Tv na baadae pia ndani ya chaneli za Dstv.

  Tuwalinde Watoto Wetu, kipindi kipya na cha kwanza kwa upande wa televisheni (Tv ambacho kinawatetea watoto moja kwa kwa moja kikiielimisha Jamii jinsi ya kumthamini mtoto, kumlinda na jamii kubadili mtazamo juu ya kundi hili kwa ujumla wake.

  Sote tunaamini kuwa, Watoto ambao baadae ndio huja kulijenga Taifa wameonekana ni wadhaifu wanaoshindwa kujitetea hasa pale wanapofanyiwa vitendo vya kikatili, baadhi ya watoto hawa wamebaki na vilema vya kudumu na baadhi wamepoteza maisha kwa mateso na kujiona wakosaji katika dunia hii.

  "Watoto wetu wengi wameathirika kisaikolojia inafika mahali wanaona kama wao kufanyiwa ukatili ni sehemu ya maisha yao. Wengine wamebaki na makovu na ulemavu na wengine hata wamepoteza maisha!" Anasema Janet

  Swali: Unafikiri hali ya usalama ya watoto imepungua?
  Jibu: Sana! Unyanyasaji wa majumbani umeongezeka, ukiacha kupigwa, kutengwa na kupewa majina si yao, kwa mfano kuna wazazi wanawaita watoto wao nyau, mbwa, ng'ombe na mengine yanayofanana na hayo lakini pia wimbi la watoto wetu kubakwa limeongezeka, na wabakaji hawatoki mbali, wanatoka kwenye familia hizohizo, wajomba, akina baba wadogo, walinzi, wafanyakazi na hata wapo akina baba wanaowabaka watoto wao wa kuwazaa! mbaya zaidi hawa watoto huwa wanapata vitisho vikali wasiseme, lakini hata ikigundulika kesi inamalizwa kifamilia bila kujali madhara aliyoyapata mtoto

  Lakini pia swala la watoto kutelekezwa limekuwa kubwa, akina baba wamesahau wajibu wao juu ya familia zao, baba anapotelekeza familia hawa watoto wanaathirika na vitu vingi kuanzia afya, elimu na hata kisaikolojia ndio hapo zao la watoto wa mitaani linapokuja au la ajira za utotoni

  Swali: Kwanini umefikiria kufanya kipindi kama hiki?
  Jibu: (tabasamu) Nafikiri ni Mungu tu ameniongoza kufanya hivi, nikirudi nyuma, kama unakumbuka nikiwa Radio One pamoja na vipindi vingine, nilikuwa naendesha kipindi kilichokuwa kinatoa elimu juu ya kupinga mtoto kuishi katika mazingira magumu, kilikuwa ni kipindi kilichoigusa jamii moja kwa moja na kuleta mabadiliko kwenye jamii.

  Binafsi licha ya kuwa muongozaji wa kipindi lakini pia niliguswa moja kwa moja, wakati mwingine nilikuwa napata shida kuongoza kipindi,unakuta unamhoji mtoto,anaelezea njia ngumu alizopitia au anazopita hadi inafika mahali anaanza kulia ,akianza kulia nami udhaifu moyo unaniingia naweka mziki ili nimbembeleze na wakati mwingine nilikuwa nafeli, namimi machozi yananitoka. Ilikuwa inaniuma na siku nzima kwangu haiwi nzuri tena,


  Nilipotoka pale, kazi nyingine niliyoipata(Under the same Sun) nayo ililenga watoto moja kwa moja, hawa walikuwa ni watoto wenye Albinisim. Kitendo cha watoto wengi kutelekezwa au kutaliwa na wazazi wao kilikuwa kinaniumiza sana na kama haitoshi wengine wakawa wanauawa kitendo hiki kinaniumiza zaidi na ninakikemea kutoka moyoni.

  Kama hiyo haitoshi, pamoja na kuamua kujiajiri nikaitwa tena na kampuni ya True vision ambao wanashirikiana na Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto nikafanye tena vipindi vya watoto. Hapa sasa ndipo nilipoona Mungu anataka nifanye kitu cha ziada juu ya watoto,siku moja nikajikuta najiuliza kwanini nisifanye kipindi cha TV ili watu waone kinachoendelea? kama ni kusikia wanasikia kila siku na wanasoma habari za watoto zisizopendeza kila siku,sasa umefika wakati watu waone kwa macho. 
  Nikafanya research,nikagundua hakuna kipindi cha aina hii kwenye Tv yoyote hapa nyumbani Tanzania nikaona bora nianzishe kitu kama hiki,nikiamini na wenzangu wataniunga mkono baadae na wao kutoa elimu kupitia Runinga baada ya Radio na Magazeti.
  Swali:Hiki kipindi kitarushwa TV gani?
  Jibu: Clouds TV, nashukuru Mungu nilipoenda na kipindi changu kilipokewa kwa mikono miwili na hiyo ikanipa moyo zaidi na kuona nimefanya uamuzi sahihi lakini pia baadae kitaruka kupitia DSTV
  Swali: Tulikuzoea kwenye "Ongea na Janet" ,sasa unarudi na "Tuwalinde watoto wetu" vipi kuhusu Ongea na Janet umekiua?
  Jibu: (kicheko) sijakiua,kipo na kitarudi msimu wa tatu October,nilichokifanya ni kuangalia,kipi nikipe uzito kwanza, nikaona watoto wamesahaulika katika matatizo yao hasa kwa upande wa Tv,hata ikitokea habari mbaya hata iwe ni ya kuogofya lakini haitatangazwa kwa muda mrefu au kufuatiliwa kwa undani. Nimeona ni jukumu langu na kama nilivyosema nina sauti inayonisuta na najiona mwenye kosa kuchelewa kulifanya hili,nahisi nadaiwa na hawa watoto na huko kote nilikopitishwa nilikuwa naambiwa ni jukumu langu kuielimisha jamii kuhusu thamani ya mtoto na ulinzi wake.
  Swali: Una lolote la kumalizia?
  Jibu:Ndio, hiki kipindi ni muhimu sana kwa wakati tuliopo,hatuwezi kuwa na Taifa bora kama hatujatengeneza msingi huku chini,vitendo vingi vibaya wanavyofanyiwa watoto vinakuja kuzaa Taifa lenye hasira,chuki,visasi na dharau. Hii inatokana na ukatili aliofanyiwa mtoto,na mtoto huyu akakua na maumivu ambayo anapokuwa mkubwa anajikuta analipiza kwa wengine,au kwa kujua au kwa kutokujua,kwa mtindo huu tusitegemee kuwa na Taifa lenye upendo, wote tunajua pasipo na upendo pana chuki na mazalio ya chuki tunayafahamu.Pamoja na hayo tusitegemee watoto hawa baadae waje kuwa wazazi bora,haitawezekana.Hivyo nawaomba sana wananchi wakiangalie hiki kipindi ili waone na kujua hali halisi ya mambo ambayo wengi bado hatufahamu juu ya usalama wa watoto wetu,itasaidia kutubadili sisi sote na kufanya yafaayo kwa watoto wetu
  Mmiliki-na-Mweneshaji-wa-kipindi-cha-Ongea-na-Janet-Bi.-Janet-Sosthenes-Mwenda.Janet Mwenda
  Janet Sosthenes Mwenda ni Mmiliki na Mweneshaji wa kipindi cha 'Ongea na Janet Tv Show' ni mwanahabari mwenye taaluma ya Utangazaji na uandaaji wa vipindi mbalimbali kupitia vipindi mbalimbali vya Radio na Tv huku akiwa ni miongoni mwa watangazaji waliojizolea umaarufu mkubwa kutokana na vipindi vyake vya tv na radio kwa muda mrefu sasa.
  “..KAA TAYARI KWA UJIO WA KIPINDI HIKI KIPYA, UNGANA NA JANET KUWALINDA WATOTO WETU!”
  Dada Janet Sosthenes Mwenda wa Ongea na Janet akicheza mpira na watoto.Jenet akicheza mpira na watoto katika moja ya shughuli za kijamii ...

  0 0
 • 08/19/15--06:44: DIVAS PARTY GALA TANGAZO
 •  Siku zimeisha event yetu itafanyika tarehe 30th August nazidi kuwaomba support yenu ya kunitangazia kwenye blogs zenu na kunirushia mitandaoni tuweze kufanikisha hili na mwenye uwezo wakutusaidia kuuza tickets anipigie namba 0658021981 nitamgawia na tutaelewana asijali
  Samahani kwa usumbufu naomba mtumie attached burner ambayo ina logo ya TBN.

  Natanguliza shukurani sana sana kwa uongozi wote wa TBN na wanachama kwa ujumla
  TBN oyeeeeeee!!!!!

  0 0

   Jaji Mkuu wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Roy Sarungi akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo Katika ofisi za Proin Promotions Ltd juu ya mchakato mzima wa fainali ya TMT itakayofanyika tarehe 22 August 2015 Katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Posta kwa kiingilio cha Shilingi Elfu Hamsini (50000) kwa viti maalumu na shilingi elfu thelathini (30000) kwa viti vya Kawaida.Mshindi katika fainali hiyo itaondoka na kitita cha Shilingi milioni hamsini (50,000,000) za Kitanzania.
  Meneja Mradi wa Tanzania Movie Talents (TMT) Saul Mpock akiongea kuhusu jinsi Fainali hiyo itakavyorushwa ,moja kwa moja (live) kupitia Kituo Cha Runinga cha ITV pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii , Vilevile amewashukuru wadau wote ambao wameweza kuipiga tafu TMT kwa mwaka huu na kuhaidi kuendelea kukushirikiana nao kwa njia moja au nyingine.
   Meneja Bidhaa wa Paisha Godfrey Fataki ambao ndio wadhamini wakuu wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 akiongelea juu ya wao kushawishika kuamua kuidhamini Paisha mara baada ya kuona kuna umuhimu mkubwa wa kuinua sekta ya filamu nchini huku akisisitiza Wananchi kutumia app ya paisha katika Simu zao kwaajili ya kuweza Kujipatia bidhaa mbalimbali kutoka kwenye makampuni mbalimbali ambayo yanapatikana ndani ya app hiyo ya Paisha.
  Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 itafanyika mnamo tarehe 22 August 2015 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kuanzia saa moja na nusu usiku huku fainali hiyo ikirushwa live kupitia kituo cha ITV pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile blogs.

  Fainali hii itakuwa ya kipekee na ya aina yake kutokana na burudani zitakazokuwepo na kuwafanya watazamaji kuendelea kuvutiwa kuangalia shindano hilo mpaka mshindi atakapopatikana na kuibuka na Milioni 50 za Kitanzania huku washiriki wa kumi waliofanikiwa kuingia hatua ya kumi bora wataweza kutengeneza filamu ya pamoja huku wakinufaika na filamu hiyo kuanzia kutengeneza hadi kuuzwa.

  Tiketi za fainali zinapatikana Makumbusho ya Taifa Posta, Kwenye Maduka yote ya Hussein Pamba Kali, Dar Live Mbagala, Shear Illusion Mlimani City na Millenium Tower na Tausi Fashion Mlimani City.

  Shindano la TMT limedhaminiwa na Paisha huku wakisaidiwa na Pepsi, Camgas, Precision Air, ITV/Radio, Global Publishers, I-View Studio, Hartman Barbershop, Van Maria Boutique, Hussein Pamba kali, Data Vision International

  0 0

   Wawezeshaji na Wadhamini wa shindano la Tanzania Movie Talent (TMT),Jaji Mkuu,Loy Sarungi(wa kwanza kutoka kushoto),Jaji katika shindano hilo Single Mtambalike(wa kwanza kutoka kushoto),Meneja Mawasiliano na Masoko wa Proin Promotion,Josephat Lukaza,Meneja Bidhaa wa Paisha,Godfrey Fataki na Meneja Masoko wa ITV,Ernest Dilli wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talent (TMT) litakalofanyika Agosti 22 katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
   Meneja Mawasiliano na Masoko wa proin Promotion,Josephat Lukaza akizungumza na Wanahabari kuhusu Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talent (TMT) litakalofanyika Agosti 22 katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
   Meneja Mradi wa Proin Promotion,Saul Mpock akizungumza juu ya Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talent (TMT) litakalofanyika Agosti 22 katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
  Jaji katika shindano hilo, Single Mtambalike akizungumza na Wanahabari katika mkutano uliohusu Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talent (TMT) litakalofanyika Agosti 22 katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

  0 0

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI         
  KAMATI 
  ya uchaguzi DRFA inaelekeza kamati ya uchaguzi ya TEFA kufanya uchaguzi wa viongozi,jumapili tarehe 23/08/2015 katika ukumbi wa JKT kama ilivyopangwa kufanyika hapo awali.
  Kamati pia inapenda  kuutarifu umma kuwa mchakato huu una Baraka zote kutoka TFF,hivyo uingiliaji wowote unakwenda kinyume na ibara ya 6(1)ya kanuni za uchaguzi za TFF 2013 na ibara za 52(6) na 56(6)(a) za katiba ya TFF ambazo zinaelekeza kuwa majukumu ya uchaguzi yapo chini ya kamati ya uchaguzi.
  Itakumbukwa uchaguzi huo uliokuwa ufanyike jumapili ya tarehe 16,08,2015 uliahirishwa na kamati ya uchaguzi ya Tefa licha ya shirikisho la TFF kuagiza ufanyike,na hivyo mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi DRFA wakili Rashid Saadallah akaitaka kamati hiyo ya TEFA kumuandikia barua kueleza sababu ya kuahirisha uchaguzi huo.
  baada ya kupitia sababu hizo,ndipo DRFA ikatoa majibu kwa kuelekeza uchaguzi huo sasa kufanyika jumapili hii.
  KOZI YA MAKOCHA LESENI ‘C’ ILIYOANDALIWA NA  DRFA SASA YAIVA,WADAU WAOMBWA KULIPIA  ADA ZAO  MAPEMA.
  kozi ya ukocha leseni C inatarajiwa kufanyika kuanza tarehe 28. 08. 2015,katika ukumbi wa TFF Uwanja wa Karume, ambapo washiriki wanakumbushwa kulipia ada zao za ushiriki ambayo ni shilingi  TZS 250,000.
  Katika kzoi hiyo inategemewa kuwepo na madarasa mawili ya wanafunzi 30 kila darasa.
  NB;NIMEAMBATANISHA NA MAJINA YA WASHIRIKI HAPO CHINI.
  IMETOLEWA NA CHAMA CHA SOKA DAR ES SALAAM DRFA

  Omary Katanga mkuu wa Habari na Mawasiliano DRFA

  0 0  0 0

  Baadhi ya Wajasiriamali wakiwa katika maonyesho ya bidhaa mbalimbali kwenye kongamano la wajasiriamali lililofanyika Hoteli ya Mbezi Garden mapema mwaka huu. Kongamano la namna hiyo linatarajiwa kufanyika Septemba 26, 2015 jijini Mwanza  Ukumbi wa  Benki Kuu (BoT), Capripoint.

  Na Dotto Mwaibale

  WAJASIRIAMALI  zaidi ya 250 wanatarajia kuonyesha bidhaa zao mbalimbali katika kongamano la mafunzo ya ujasiriamali litakalofanyika jijini Mwanza.

  Akizungumza na Dar es Salaam leo, Mratibu wa kongamano hilo, Getrude Kilyabusebu alisema lengo la kongamano hilo ni kutoa mafunzo ya ujasiriamali ili kuwajengea uwezo wajasiriamali hao.

  "Wajasiriamali hao katika kongamano hilo watapata fursa ya kuonesha bidhaa zao mbalimbali na pia watapata mafunzo ya jinsi ya kukuza mitaji yao na mbinu zingine za biashara" alisema Kilyabusebu.

  Alisema makongamano ya namna hiyo yamekuwa yakiwasaidia wajasiriamali hao kujuana na kubadilishana uzoefu wa kibiashara na utengeneza wa bidhaa zao zikiwemo mbinu za ufugaji na kilimo.

  Alisema mafunzo hayo utolewa na wataalamu waliobobea katika shughuli za ujasiriamali na matunda ya mafunzo ya  makongamano hayo yamewanufaisha wajasiriamali  wengi wajasiriamali.

  Kilyabusebu alisema kongamano hilo lililoandaliwa na  Jumuiya ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (Tanzania Business Entrepreneurs Women) lita Septemba 6, 2015 jijini Mwanza  katika ukumbi wa Benki Kuu (BoT) Capripoint.

  Mratibu huyo alisema kuwa pamoja na mambo mengine kila mshiriki atalazimika kuchangia gharama kidogo ili kufanikisha kongamano hilo ambapo katika mafunzo na chakula atatakiwa kulipia sh.30,000, meza ya kuuzia bidhaa na kuzitangaza sh. 20,000 na mafunzo na meza sh.50,000.

  Kilyabusebu alitumia fursa hiyo kuwaomba wajasiriamali wa kanda ya ziwa kuweza kushiriki katika kongamano hilo ambalo ni muhimu kujifunza stadi za kazi zao.

  Kwa maelezo zaidi kuhusu kongamano hilo unaweza kupiga simu namba  0754032589 /0756334078/0673032589.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com


  0 0

  2

  Bw. Alferio Nchimbi Katibu wa Chama cha Mchezo wa Baseball na Softball Tanzania akikabidhi vifaa vya michezo kwa wachezaji wa timu ya mchezo huo ya Tanzania inayotarajia kuondoka kesho kuelekea nchini Uganda kwa ajili kambi ya mafunzo ya Meja League Base Ball Training Camp For Tryout (MLB) yatakayofanyika kuanzia tarehe 23-25 Agosti 2015 ambapo wachezaji watakaochaguliwa kutoka katika kambi hiyo watakwenda nchini Afrika Kusini kwa kwa mafunzo ya wiki mbili na baadaye wachezaji watakaochaguliwa kutoka kambi ya mafunzo ya Afrika Kusini watakwenda katika mafunzo kama hayo nchini Marekani kwa ajili ya kupata mafunzo zaidi ya mchezo huo na Scholarship ya kusoma nchini humo
  Wachezaji waliochaguliwa katika timu hiyo ya taifa kwenda nchini Uganda ni Abdallah Abdallah kutoka Shule ya Sekondari ya Al Muntazir, Pius Cheka kutoka Sekondari ya Kibasila, Martin Cosmas kutoka Sekondari ya Azania, Juma Fikiri na Leodgar Leonidas kutoka sekondari ya Azania. Timu zitakazoshiriki katika mafunzo hayo ni Tanzania, Kenya na Uganda.

  Katika Picha kutoka kushoto ni Mwalimu Marck Hatia , Juma Fikiri, Martin Cosmas na Leodgar Leonidas wachezaji wa timu hiyo waliopokrea vifaa hivyo kwa niaba ya wenzao.
  3

  0 0

    Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akikabidhiwa fomu za uteuzi kwa nafasi ya ubunge na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Olliver Vavunge.
  Mbunge wa Jimbo la Mchinga Said Mtanda akipokea fomu za uteuzi kwa nafasi ya ubunge na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Olliver Vavunge.
    Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akisalimina na wananchi waliojitokeza kumsindikiza kwenda kuchukua fomu za uteuzi wa ubunge za Tume ya Taifa ya Uchaguzi .Nape Nnauye ndie  mgombea aliyependekezwa na Chama Cha Mapinduzi kugombea jimbo la Mtama mkoani Lindi.
   Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Katibu Mwenezi wa kata ya Namangare Mzee Evod  nje ya ofisi za CCM mkoa Lindi,muda mfupi kabla ya kwenda kuchukua fomu za uteuzi wa ubunge za Tume ya Taifa ya Uchaguzi
    Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akizungumza na kamati ya siasa ya mkoa pamoja na wagombea ubunge wa CCM kutoka majimbo yote ya mkoa wa Lindi kabla ya kumsindikiza kwenda kuchukua fomu za uteuzi wa ubunge za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
    Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akitoka kwenye ofisi za CCM mkoa wa Lindi akiongozana na Said Mtanda kuelekea kwenye Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Lindi kuchukua fomu za uteuzi wa ubunge za Tume ya Taifa ya Uchaguzi
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye ndiye mgombea wa CCM jimbo la Mtama pamoja na Said Mtanda anayegombea kwa jimbo la Mchinga wakiwasili kwenye ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Lindi kuchukua fomu za uteuzi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

older | 1 | .... | 612 | 613 | (Page 614) | 615 | 616 | .... | 1897 | newer