Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46327 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZARI WA MAJI ATEMBELEA MAMLAKA YA MAJI MWANZA

$
0
0
NAIBU waziri wa maji Amos Makalla ametembelea Mamlaka ya maji jiji la Mwanza kwa kutembelea chanzo cha maji, kituo cha kutibu maji, ujenzi wa jengo la ofisi za mamlaka, mfumo wa majitaka na mkutano wa bodi na wafanyakaziKatika mkutano na bodi na wafanyakazi amewataka kutoa  huduma kwa wateja kwa kiwango cha juu ikiwemo kusikiliza matatizo ya wateja na kuyashughulikia kwa wakati.

Aidha ameitaka menejimenti kuhakikisha mkandarasi wa kujenga mradi mkubwa wa kuboresha huduma ya maji jiji la Mwanza hususan maeneo ya miinuko ananza kazi novemba kama ilivyopangwa.

Mradi huo mkubwa unagharimu shilingi bilioni 110 na ni ushirikiano wa serikali ya Tanzania. Shirika la maendeleo la Ulaya na ufaransa
Kukamilika kwa mradi huu kutamaliza tatizo la maji jiji la Mwanza.

 Bi Mary Matunge mtalaam wa urekebishaji mita akimweleza jambo naibu waziri wa maji.
 Naibu waziri maji akipokea maelezo kutoka kwa mhandisi Davis Fute kuhusu majitaka.
 Naibu waziri maji akihutubia bodi na watumishi.
 
Mhandisi Stanley Mwasawale akimweleza naibu waziri wa Maji ujenzi wa jengo la mamlaka ya maji mwanza litakalogharimu shilingi bilioni 3.6


TFDA YATOA TAHADHARI YA KUWEPO KWA VIPODOZI VYENYE VIAMBATO VILIVYOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Hiiti Sillo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya TFDA Dar es Salaam leo, wakati akitoa tahadhari ya uwepo katika soko wa vipodozi vyenye viambato vilivyopigwa marufuku na Serikali. Kulia ni Mkurugenzi wa Dawa  na Bidhaa Nyongeza, Fimbo Mitangu.
 Mkurugenzi wa Dawa  na Bidhaa Nyongeza, Fimbo Mitangu (kushoto), akizungumza katika mkutano huo huku akionesha moja ya kopo lenye kipodozi vilivyopigwa marufuku. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Uendelezaji Huduma wa TFDA, Chrispin Severe 
 Mkurugenzi wa Usalama wa chakula, Raymond Wigenge (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Maabara wa TFDA, Charys Ugullam (kulia), wakiwa kwenye mkutano huo na wanahabari.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.



1.            MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) ni Wakala wa Serikali ulio chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wenye jukumu la kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa aina ya chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.

2.            TFDA inautaarifu umma kuwa kupitia mfumo wake wa ufuatiliaji ubora na usalama wa bidhaa kwenye soko, imebaini uwepo wa vipodozi vyenye viambato vilivyopigwa marufuku aina ya “steroids” zinazojulikana kitaalam kama “clobetasol propionate”, “hydrocortisone” na “triamcinolone”.

3.            Jumla ya Vipodozi aina tofauti 36 vya jamii ya krimu (creams) na losheni (lotion) vimebainika kuwa na viambato hivyo vilivyopigwa marufuku baada ya kufanya uchunguzi wa kina wa matoleo 57 yaliyochukuliwa kwenye soko na viwanda vilivyotengeneza.

4.            Vipodozi hivyo vimetengenezwa na makampuni manne (4) yaliyoko hapa nchini na kiwanda kimoja (1) kilichoko nje ya nchi kama ifuatavyo:-

Na.
Jina la kiwanda
Idadi ya vipodozi
Idadi ya matoleo
1.
Chemi & Cotex Industries Limited - Dar es Salaam
6
7
2.
Mamujee Products Limited - Tanga  
11
20
3.
Tanga Pharmaceutical & Plastics Limited - Tanga
15
24
4.
Tridea Cosmetics Limited - Dar es Salaam
3
5
5.
Johnson & Johnson (Pvt) Ltd, Rattray Road, East London, South Africa
1
1

Jumla
36
57

5.            Steroids aina ya “clobetasol propionate”, ‘hydrocortisone’’ na “triamcinolone” hutumika kama dawa kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi yajulikanayo kitaalam kama eczema, herpes labialis, psoriasis, contact dermatitis, alopecia areata, vitiligo, lichen sclerosus, lichen planus na mycosis fungoides. Steroids hizi hazitakiwi kutumika zaidi ya wiki mbili na lazima mgonjwa apate ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa hizi.

6.            Baadhi ya madhara yanayotokana na kutumia dawa hizi ni pamoja na muwasho na kuvimba kwa ngozi (allergic contact dermatitis), ngozi kuwaka moto (burning sensation), ngozi kukatikakatika (skin cracking), ngozi kubabuka (fissuring) ngozi kukosa chembembe aina ya melanin inayoleta kinga na hivyo kuifanya ngozi kuwa nyeupe isivyo kawaida (hypopigmentation), madhara kwenye mifupa (osteoporosis), kizunguzungu (dizziness), ngozi kukauka (skin dryness), shinikizo la damu kwenye macho (glaucoma), vinyweleo vya ngozi kupata athari (folliculitis), kuwashwa mara kwa mara (excessive itching, pruritus, erythema and irritations), vidole kufa ganzi (numbness of fingers), ngozi kusinyaa (skin atrophy) na ngozi kubanduka (skin peeling/maceration). Madhara mengine ni pamoja na ngozi kuwa nyekundu (skin redness), kusikia kichefuchefu (nausea), kichwa kuuma (headache), kushindwa kupata usingizi (insomnia), kutoka jasho jingi (sweating), kupata chunusi kubwa kwenye ngozi (acne), kuchoka (fatigue), kuongezeka uzito (weight gain), mapigo ya moyo kutoenda sawa (uneven heartbeats) na kuona maluweluwe (blurred vision).

7.            Kufuatia hali iliyojitokeza na kwa kuzingatia madhara yanayoweza kusababishwa na matumizi ya steroids kwa muda mrefu, TFDA imechukua hatua zifuatazo:

a.      Kuzuia kwa muda wa miezi sita (6) utengenezaji wa vipodozi aina ya krimu, losheni na jeli kwenye viwanda vinne (4) vilivyohusika.
b.      Kuwaelekeza wenye viwanda vilivyohusika kuviondoa vipodozi vilivyokutwa na steroids kwenye soko na kuviteketeza kwa gharama zao wenyewe.
c.       Kufuta usajili wa vipodozi 31 vilivyokuwa vimesajiliwa.
d.     Kuwaelekeza Mameneja wa Ofisi za Kanda za TFDA kufanya ukaguzi katika maeneo yao kwa kushirikiana na Ofisi za Halmashauri ili kuondoa katika soko vipodozi vyote vilivyohusika.

8.            Pamoja na hatua hizo, TFDA inatoa maelekezo yafuatayo:-

a.      Wananchi wote wasitumie vipodozi husika kwa kuwa vina madhara ya kiafya. Wananchi wanaaswa kuangalia lebo za vipodozi walivyonavyo majumbani na wakiona vina majina yaliyoainishwa waache kutumia vipodozi hivyo mara moja.
b.      Wasambazaji na wauzaji wote kurudisha vipodozi vilivyohusika kwa watengenezaji au kwa waliowauzia ili hatua za uteketezaji ziendelee.

9.            TFDA inaendelea kufuatilia vipodozi vingine vyote ili kujiridhisha na ubora na usalama wake kwa watumiaji. Vile vile itaendelea na kazi yake iliyopewa ya kulinda na kudumisha afya ya jamii kwa kuhakikisha bidhaa aina ya chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba zinazotengenezwa hapa nchini au kuingizwa kutoka nje ya nchi ni bora, salama na zenye ufanisi unaotakiwa.

10.        TFDA itawachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaojihusisha na uvunjaji wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219 na inawaomba wananchi wote kuendelea kutoa taarifa pale wanapobaini uwepo wa bidhaa (chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba) duni au bandia kwenye soko la Tanzania. 

ORODHA YA VIPODOZI VILIVYOBAINIKA KUWA NA VIAMBATO VILIVYO PIGWA MARUFUKU



Na.
Jina la kipodozi
Namba ya usajili
Toleo
Tarehe ya kuishamatumizi
Sehemusampuliilipochukuliwa
Aina ya kiambatokilichokutwa

Chemi&Cotex Industries Limited, Dar es Salaam
1.    
Lovely Body Cream - Lemon
TAN15 CP 0095
12&16
Feb-18
Kwenye soko&Kiwandani
ClobetasolProprionate
2.    
Baby Soft Body Lotion
Haijasajiliwa
08
Dec-16
Kwenye soko
ClobetasolProprionate
3.    
Siri Moisturizing  Cream- Cocoa Butter
TAN13 CP 3118
26
Jan-18
Kiwandani
ClobetasolProprionate
4.    
Siri Moisturizing  Cream- Lemon
TAN13 CP 3120
03
May- 18
Kiwandani
ClobetasolProprionate
5.    
Lovely Body Cream - Lemon
TAN15 CP 0094
16
Mar-18
Kiwandani
ClobetasolProprionate
6.    
Lovely Body Cream - Papaya
TAN15 CP0096
10
May-18
Kiwandani
Hydrocortisone

Mamujee Products Limited, Tanga
7.    
Beauty Care Aloe Vera Beauty Cream
Haijasajiliwa
00283
Sep-15
Kwenye soko&Kiwandani
ClobetasolProprionate
8.    
BOSS Hand & Body Lotion
TAN 15 CP 0300
10/0077258

WATAALAM WA TEHAMA NCHINI TANZANIA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA MAADILI, WELEDI NA UBUNIFU

$
0
0
1
Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.HAB Mkwizu akifungua mkutano wa kwanza wa mwaka wa Serikali Mtandao leo jijini Arusha.Zaidi ya wataalam wa TEHAMA 500 kutoka Wizara, Idara, Wakala,Taasisi, Halmashauri wako jijini Arusha kujadili mafanikio na changamoto za Serikali mtandao.
2
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt.Jabiri Bakari akitoa ufafanuzi kuhusu Serikali Mtandao kwa washiriki wa Mkutano wa kwanza wa Serikali Mtandao unaofanyika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha leo.
4
Mtaalam wa masuala ya Serikali Mtandao kutoka nchini Singapore Bw.Tan Kim akiwasilisha mada kuhusu Umuhimu wa Serikali mtandao kwa washiriki wa Mkutano wa kwanza wa Serikali mtandao unaofanyika jijini Arusha leo
5
Wataalam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kutoka maeneo mbalimbali nchini wakifuatilia Masuala mbalimbali wakati wa mkutano wa kwanza wa mwaka wa Serikali mtandao unaofanyika jijini Dar es salaam.
Picha na Aron Msigwa.
………………………………………………………………..
Na. Aron Msigwa -MAELEZO .ARUSHA.
Serikali imewataka watalaam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) walio katika utumishi wa umma kote nchini kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili, weledi na ubunifu ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za serikali kwa njia ya mtandao  katika maeneo mbalimbali na kuondoa malalamiko yanayotokana na utoaji wa huduma   usiokidhi viwango.
 
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Arusha na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.HAB Mkwizu wakati akifungua Mkutano wa kwanza wa mwaka wa Serikali mtandao wa Maofisa TEHAMA kutoka Wizara, Idara,Wakala na Taasisi mbalimbali za Serikali.
Amesema Watumishi wa umma wasipotimiza wajibu wao kikamilifu wanasababisha malalamiko kwa wananchi na kuifanya Serikali kushindwa kufikia malengo iliyojiwekea.
 
“Ni muhimu wote mtamtambue kuwa utumishi wa umma imara hujenga serikali na Taifa imara, utumishi wa kufanya kazi kwa mazoea na kusukumwa  hauna tija kwa taifa letu” Amesema.
 
Ameongeza kuwa ili kufikia malengo ya kuimarisha utawala bora na kuongeza tija na ufanisi Serikali imekuwa ikisisitiza matumizi ya TEHAMA ili kuimarisha mawasiliano ya haraka, yenye uhakika na salama ndani ya taasisi mbalimbali za Serikali; kuanzia kwenye Wizara, Mikoa hadi ngazi za Halmashauri pamoja na Balozi mbalimbali nje ya nchi.
 
 Amefafanua kuwa katika  kupanua wigo wa upatikanaji wa taarifa muhimu na kuimarisha usalama wa Serikali na raia wake Serikali imeendelea kujenga na kuongeza uwezo wa kupambana na majanga kwa kutumia teknolojia.
 
Aidha, amesema   Serikali kwa kutambua mchango wa TEHAMA inaendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zikiwemo za baadhi ya mifumo  kutokuongea, kutowasiliana na kutobadilishana taarifa kati ya taasisi na taasisi pia rudufu ya mifumo ambapo kila taasisi inakuwa na juhudi za kipekee katika kusimika na kutumia miundombinu ya TEHAMA ambayo ingeweza kutumiwa na zaidi ya taasisi moja pamoja na changamoto ya mifumo kuwa na viwango vya usimikaji tofauti.
 
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao ( e Government Agency) Dkt. Jabiri Bakari awali akiwakaribisha Wataalam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano waliohudhuria Kongamano hilo amesema  kuwa katika kuimarisha uwazi na upatikanaji wa Takwimu huria, Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya TEHAMA  ili  kuwawezesha wananchi kupata huduma zinazotolewa na Wizara na Taasisi kwa njia ya mtandao.
 
Amesema kuwa Serikali inaendelea kufanya vizuri katika kufanikisha lengo kubwa la kufikisha huduma kwa wananchi na kuongeza kuwa mpango wa  Serikali uliopo sasa ni kuwa na mfumo mmoja utakaowezesha taarifa zote za wananchi kuwa katika sehemu moja.
 
 Akizungumza kuhusu mkutano huo  Dkt.Jabiri amesema kuwa washiriki zaidi ya 500 kutoka taasisi mbalimbali za Serikali watapata fursa ya kujadili  masuala mbalimbali ya ushirikiano katika kutekeleza jitihada za Serikali Mtandao nchini pamoja na Kutafuta ufumbuzi wa changamoto za serikali mtandao zilizopo nchini ili kuleta  maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Aidha, wataalam wa TEHAMA wa Tanzania waliohudhuria kongamano hilo watapata fursa ya kujifunza kutoka kwa wataalam wengine wanaohusika na Serikali Mtandao kutoka nchi zinazofanya vizuri katika eneo la Serikali mtandao zikiwemo India na Singapore.
 
 Ameongeza kuwa katika mkutano huo mada mbalimbali zitajadiliwa zikijikita  katika usimamizi wa Serikali Mtandao nchini Tanzania, Hali ya miundombinu  ya Serikali mtandao na Utekelezaji wa Mpango wa Uendeshaji wa Serikali kwa uwazi.
 
Mada nyingine zitahusu uimarishaji wa uwazi na Mfumo wa Takwimu huria nchini Tanzania na uimarishaji wa huduma za Serikali kupitia simu za mkononi na mifumo inayotumika kutoa huduma kwa wananchi.
Naye Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Bw.Agostin Mapunda akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha amesema kuwa Matumizi ya TEHAMA katika shughuli za Serikali yamerahisisha utendaji wa kazi na kuboresha maisha ya wananchi.
Amesema sasa wananchi wanaweza kupata huduma mbalimbali zikiwemo za upataji wa hati za ardhi kwa haraka zaidi kupitia mifumo ya TEHAMA iliyoanzishwa na serikali.
Ameongeza kuwa ni vema mabadiliko hayo yakaendelezwa kutokana na umuhimu wake katika kufanikisha utendaji wa Serikali, kupunguza muda na kuokoa gharama!
“Tuko kwenye njia sahihi ya kuufanya utendaji wa Serikali kupata mafanikio kupitia mtandao, hali hii tunaona imepunguza matumizi na gharama kubwa waliyokuwa wanaipata wananchi kufuata huduma ambazo sasa zimerahisishwa kupitia mtandao”
Amefafanua kuwa wananchi sasa wanaweza kulipia ankara zao za umeme, maji na huduma nyingine kupitia simu zao za mkononi jambo ambalo hapo awali halikuwepo

KAMPUNI YA HUAWEI YASAIDIA KATIKA ELIMU NA TEKNOLOGIA HAPA NCHINI

$
0
0
Balozi wa China nchini Tanzania Dr.Lu Youqing (katikati) akipata maelekezo kuhusu bidhaa za Huawei wakati wa mkutano wa watanzania waishio uhaibuni (Tanzania Diaspora).Kushoto ni Afisa mahusianao na habari,Jimmy na kulia ni Meneja wa bidhaa na huduma wa Huawei hapa nchini, Joseph Lyimo Huawei walikua ni wazamini wakuu wa mkutano huo ulifanyika jijini Dar es salaam katika hoteli ya Serena  Augost 14 mwaka huu.

  Dr.Lu Youqing lieleza kuwa sasa hivi China na Tanzania wana ushirikiano mzuri ambapo China imekuwa ikisaidia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa kuwawezesha watanzania waliopo nchini China.

 Mbali na hayo wamekuwa wakisaidia Tanzania kwa njia nyingi moja wapo kwa makampuni ya nchi yao kuwekeza nchini Tanzania.

 Huawei ni moja ya kampuni hizo ambapo ina wafanyakazi wengi watanzania na imekuwa ikisaidia watanzania katika mambo mengi ya kielimu na kiteknolojia na kupelekea kukuza uchumi wa tanzania.
 Balozi wa China nchini Tanzania Dr.Lu Youqing akiwa kakatika picha ya pamoja na mameneja wa Huawei,wa kwanza kutoka  kushoto ni Jane Wang Jin afisa masoko wa Huawei na wa pili kutoka kushoto ni Mr.Jimmy Afisa mahusiana na mawasiliano akifuatiwa na mama Mulamula. Wengine ni wafanyakazi wa Huawei Tanzania. Hii ilikua katika mkutano wa watanzania waishio ughaibuni (Diaspora).
 Huawei Tanzania walikua moja ya wadhamini wa kongamano hili la siku mbili ambapo kampuni ya Huawei walionyesha jinsi Kamera za CCTV zinavyofanya kazi katika lango kuu la kuingilia katika kongamano  hilo ambapo kamera hizo zilionyesha vyema jinsi ya kumwona mtu ambaye anaweza kufanya uharifu wowote mahali pale.
Pia Huawei walikuwa na redio za 4G ambazo walikuwa wakizionyesha katika mabanda kabla na baada ya wanatanzania waishio ughaibuni kuingia na kutoka kujionea vifaa hivyo vinavyofanya kazi.
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete,akiwapongeza kampuni ya Huawei kwa kuwapatia cheti cha kudhamini kongamano la watanzania waishio ughaibuni ambapo kampuni ya huawei iliwakilishwa na Meneja wa Huawei hapa nchini, Jimy Jinglio.
 China imekua na ushirikiano mzuri na Tanzania na imetoa kipaumbele kwakufadhili kongamano la wanaDiaspora nje ya nchi kwa kuwapatia elimu na vitu vingine. 
Mbali na Hapo China imewekeza mambo mbalimbali nchini Tanzania hasa katika Elimu na Teknologia.
Waziri wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,Bernad Membe akipewa maelekezo na Mhandisi wa teknologia wa kampuni ya Huawei hapa nchini,Lameck Mangu mara baada ya kutembelea banda la maonyesho la HUWAWEI. HUWAWEI wakiwa na moja ya kampuni zilizodhamini mkutano uliowakutanisha watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Waziri wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,Bernad Membe amwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kufungua mkutano uliowakutanisha watanzania waishio ughaibuni uliofanyika  katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizingumza na watanzania waishio Ughaibuni,(Diaspora) kuhusiana na watanzania hao kuwekeza hapa nchini na kupenda kwao katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) wa wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,Rosemary Jain ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkutano huo uliowakutanisha watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya Serena  jijini Dar es Salaam.
Msanii wa nyimbo za bongo freva,Peter Msechu akiwaongoza watanzania waishio Ughaibuni maarufu kama Diaspora kuimba wimbo wa Taifa  katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.


 Watanzania waishio ughaibuni maarufu kama Diaspora wakisikiliza watoa maada hawapo pichania katika mkutano uliowakutanisha  uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Meneja wa sheria wa mamlaka ya uhifadhi katika hifadhi ya Ngorongoro, Julius akaibebe akiwaasa watanzania waishio ughaibuni kuwekeza hapa nchini hasa katika buga za wanyama ili kuchangia uchumi wa nchi hapa nchini aliyasema hayo katika mkutano uliowakutanisha watanzania waishio ughaibuni(Diaspora) uliofanyika jana na leo katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa  kampuni ya Choice Coffee.co.tld, Rose Swai akizungumza na wanadiaspora waishio ughaibuni kuwekeza kwenye viwanda vinavyotengeneza bidhaa mbalimbali kwa kutengeneza vifaa vya kuhifadhia(Packeging product) vitu mbalimbali kwa wajasiliamali hapa nchini ili waweze kupata masoko kwa urahisi aliyasema hayo katika kutano uluiwakutanisha watazania waishio ughaibuni uliofanyika katika hoteli ya serene jijini Dar es Salaam.




 Waziri wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Bernad Membe akiwa katika picha ya pamoja na watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) mara baada ya mapumziko ya mkutano uliowakutanisha watanzania hao ulifanyika katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam.
(Picha na Avila Kakingo Globu ya Jamii)

WANACHAMA WA MFUKO WA BIMA YA AFYA WA NHIF KUTIBIWA KATIKA HOSPITALI YA JESHI LA JWTZ

$
0
0
 Kaimu Mkurungenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Michael Mhando na Mkuu wa Huduma za Matibabu Jeshini,Brigedia Denis Raphael wakitia saini Mkatamba wa Ushilikiano leo katika Makao Mkuu ya Jeshi Jiji Dar es Salaam.
Kaimu Mkurungenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Michael Mhando na Mkuu wa Huduma za Matibabu Jeshini,Brigedia Denis Raphael wakibadilishana hati za makubaliani leo katika Makao Mkuu ya Jeshi Jiji Dar es Salaam.

WANACHAMA kutibiwa katika hospitali za jeshi,

Mfuko wa Taifa  wa Bima ya Afya (NHIF) umeingia mkataba na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambapo wanachama wa mfuko huo na wategemezi  wao watapata huduma za matibabu katika hospitali  za jeshi nchini kote.


Mkataba huo wa miaka mitatu uliosainiwa jana unalenga kupanua wigo wa vituo vya matibabu na kuanzisha ushirikiano wa kihistoria baina ya pande mbili hizo.


Akizungumza wakati wa kutia saini mkataba huo Mkuu wa Huduma za Afya Jeshini Brigedia Denis Raphael Janga,  amesema amepokea kwa furaha mkataba huo kwa kuwa utawapa nafasi ya kutoa huduma bora kwa kundi kubwa la wanachama wa NHIF ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikosa huduma katika vituo vya jeshi vilivyo karibu nao.


Ameahidi kushirikiana kwa karibu na uongozi wa NHIF ili kuhakikisha wanachama na wategemezi wao wanapata vipimo na dawa wakati wote watakapokwenda kwenye vituo hivyo.


Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Michael Mhando amesema NHIF kwa muda mrefu fursa ya kufanya kazi na JWTZ katika sekta ya matibabu na kwamba mkataba huo unafungua historia mpya ya ushirikiano baina ya taaisi hizo wa kujenga nchi kwa pamoja.


Amesema ili kuhakikisha kuwa mkataba huo unakuwa na manufaa kwa pande zote mbili Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya utaandaa mafunzo maalumu kwa watoa huduma wa vituo vya jeshi ili kuhakikisha kuwa kunakuwa na uelewa wa pamoja wa namna ya kuhudumia wanachana wa NHIF watakaokwenda kupata huduma katika vituo hivyo.


Mhando ameongeza kuwa NHIF itaendelea kushirikiana na uongozi wa JWTZ ili kukamilisha taratibu za kiutawala zitakazowawezesha wanaejeshi na familia zao kujiunga na kunufaika na matibabu kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.


Aidha ameushauri uongozi wa JWTZ kutumia fursa ya mikopo ya vifaa tiba, ukarabati na dawa na vitendanishi inayotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuhakikisha kuwa vituo vya matibabu vinavyomilikiwa na JWZT vinakuwa na mazingira mazuri na vitendea kazi vinavyotakiwa.


Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lina vituo vya matibabu vya ngazi mbalimbali zaidi ya kumi na nane nchini kote.

UKAWA WATANGAZA MAJIMBO WALIYOGAWANA KATIKA UCHAGUZI MKUU

$
0
0

 Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi,  Nderakindo Kessy (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho, Ilala Dar es Salaam jana, wakati akitangaza majimbo yaliyochini ya vyama vinavyounda Ukawa ambayo vyama hivyo vitasimamisha wagombea wao katika uchaguzi mkuu. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha NLD, Masudi Makunjunga.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Shaweji Mketo (wa pili kulia), akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari. Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha NLD, Masudi Makunjunga, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi,  Nderakindo Kessy na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika.
 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, akizungumza katika mkutano huo.
 Viongozi wa vyama hivyo wakiwa meza kuu.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.


Na Mwandishi Wetu


UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umetangaza mgawanyo wa majimbo yake 253 huku majimbo mengi yakienda Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).


Taarifa ya mgawanyo wa majimbo ilitolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Dk. Nderakindo Kessy jana katika ofisi kuu za chama hicho Ilala jijini Dar es Salaam.


Kessy alisema baada ya majadiliano ya muda mrefu kuhusu kuachiana majimbo ya ubunge, vyama vinavyounda Ukawa vimefanikiwa kuachiana majimbo ili kuhakikisha wanakiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM), madarakani.


Alisema mgawanyo wa majimbo hautahusiana na mgawanyo wa kata za kugombea udiwani na mwongozo wa kuachiana kata ndiyo utatumika katika kuamua namna ya kugombea kata.


“Tunapenda kuchukua nafasi hii kuwatangazia Watanzania majimbo ambayo hadi leo (jana), tumekubaliana kuachiana kuwa ni majimbo 253 na majimbo 12 tutawaambia Jumatano au Alhamis kwani kuna mambo hayajakaa vizuri,” alisema.


Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Mkoa wa Mara majimbo yote wameachiwa Chadema ambayo ni Rorya, Tarime Mjini, Tarime Vijijini, Musoma Vijijini, Butiama, Bunda Mjini, Mwibara, Musoma Mjini na Bunda Vijijini.


Kessy alisema Mkoa wa Simiyu ambao una majimbo saba, majimbo sita wamepewa Chadema ambayo ni Bariadi, Maswa Magharibi, Maswa Mashariki, Kisesa, Meatu, Itilima na Jimbo la Busega atasimama mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF).


“Mkoa wa Shinyanga majimbo yote sita wameachiwa Chadema na sababu ya msingi ni wao kuwa na mizizi ambapo ni majimbo ya Msalala, Kahama Mjini, Kahama Vijijini, Shinyanga Mjini, Kishapu na Ushetu na Mkoa wa Mwanza ni Ukerewe, Magu, Nyamagana, Buchosa, Sengerema, Ilemela, Misungwi yameenda Chadema na Kwimba na Sumve CUF,” alisema.


Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema Mkoa wa Geita majimbo yote yaliachiwa Chadema, ambayo ni Bukombe, Busanda, Nyang’wale, Chato na Mbogwe, Mkoa wa Kagera katika majimbo tisa Chadema imeachiwa majimbo sita ambayo ni Karagwe, Kyerwa, Bukoba Mjini, Muleba Kaskazini, Muleba Kusini na Biharamulo na Nkenge, Ngara yakiachwa kwa NCCR-Mageuzi na Jimbo la Bukoba Vijiji likiachwa kwa CUF.


Mkoa wa Mbeya Jimbo la Lupa, Songwe, Mbeya Mjini, Kyela, Rungwe, Busekolo, Mbozi Mashariki, Momba, Mbeya Vijijini, Vwawa na Tunduma yote yameachiwa Chadema na Jimbo la Ileje NCCR-Mageuzi.      


“Iringa, Jimbo la Ismani, Kalenga, Mufindi Kaskazini, Iringa Mjini, Kilolo, Mufindi Mjini Chadema itasimamisha wagombea na Mufundi Kusini NCCR-Mageuzi, ambapo Mkoa wa Njombe majimbo yote yameachwa Chadema ambayo ni Njombe Kaskazini, Lupembe, Wanging’ombe, Makete, Ludewa na Makambako,” alisema Kessy.


Kessy alisema Mkoa wa Rukwa wamekubaliana kuwaachia Chadema, ambapo ni majimbo ya Nkasi Kusini, Kwela, Nkasi Kaskazini, Sumbawanga Mjini na Kalambo, huku Mkoa wa Tanga CUF wameachiwa majimbo nane ambayo ni Handeni Mjini, Handeni Vijijini, Pangani, Tanga Mjini, Bumbuli, Mlalo, Lushoto na Mkinga. Chadema wameachiwa majimbo manne ambayo ni Kilindi, Muheza, Korogwe Mjini na Korogwe Vijijini. 


Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema Mkoa wa Kilimanjaro majimbo saba imeachiwa Chadema ambayo ni Rombo, Same Magharibi, Same Mashariki, Moshi Vijijini, Moshi Mjini, Hai na Siha ambapo Vunjo NCCR-Mageuzi wameachiwa na Jimbo la Mwanga likibakia hadi Alhamis.


Mkoa wa Arusha alisema Chadema wameachiwa majimbo yote ambayo ni Arumeru Mashariki, Arumeru Magharibi, Arusha Mjini, Longido, Monduli, Karatu na Ngorongoro halikadhalika Mkoa Manyara Jimbo la Simanjiro, Mbulu Vijijini, Hanang, Babati Mjini, Babati Vijijini, Kiteto na Mbulu Mjini.


Aidha, Kessy alisema Mkoa wa Dar es Salaam, Jimbo la Ubungo, Kawe, Ukonga, Ilala na Kibamba Chadema itasimamisha wagombea na Kinondoni, Jimbo la Temeke na Mbagala CUF itasimamisha wagombea huku majimbo ya Segerea na Kigamboni yakibakia kiporo hadi Alhamisi wiki hii.


Alisema Mkoa wa Pwani majimbo ya Bagamoyo, Kisarawe, Mkuranga, Mafia, Rufiji Utete na Rufiji Kibiti majimbo hayo yameachiwa CUF na Majimbo ya Chalinze, Kibaha Mjini, Kibaha Vijijini yakiachiwa Chadema.    


Mkoa wa Morogoro Jimbo la Kilosa na Morogoro Kusini Mashariki CUF watasimamisha wagombea huku majimbo ya Mikumi, Morogoro Kusini, Kilombero, Mlimba, Mvomero, Ulanga Magharibi, Ulanga Mashariki na Morogoro Mjini yatakuwa chini ya Chadema.


“Mkoa wa Dodoma Jimbo la Kondoa Mjini, Kondoa Vijijini, Chemba yameachwa kwa CUF, Jimbo la Kibakwe na Mtera wameachiwa NCCR-Mageuzi na Dodoma Mjini, Kongwa, Bahi na Chilonwa Chadema itasimamisha wagombea.


Kessy alisema Mkoa wa Singida majimbo yote saba yameenda Chadema ambayo ni Iramba Magharibi, Iramba Mashariki, Singida Kaskazini, Singida Mashariki, Singida Magharibi, Manyoni Magharibi na Manyoni Mashariki. 

Kwa Mkoa wa Tabora Jimbo la Bukene, Nzega Vijijini, Igalula, Kaliua Tabora Kaskazini na Tabora Mjini watagombea CUF na Nzega Mjini, Igunga, Urambo, Ulyankulu, Manonga na Sikonge Chadema watasimamisha wagombea.


Alisema Mkoa wa Katavi majimbo yote sita ya Mpanda Mjini, Mpanda Vijijini, Katavi, Nsimbo na Kavuu. Mkoa wa Kigoma Jimbo la Buyungu, Mhambwe, Kasulu Mjini, Kasulu Vijijini, Kigoma Kusini na Manyovu NCCR-Mageuzi itasimamisha wagombea na Kigoma Kaskazini na Kigoma Mjini Chadema itasisimamisha wagombea wa ubunge.


Mkoa wa Ruvuma Jimbo la Tunduru Kaskazini, Namtumbo na Tunduru Kusini Chama cha CUF watasimamisha wagombea na majimbo ya Peramiho, Mbinga Magharibi/Nyasa, Mbinga Mashariki/Mbinga, Songea Mjini na Madaba, na Mbinga Mjini NCCR-Mageuzi itasimamisha mgombea.


“Mtwara Jimbo la Newala Mjini, Newala Vijijini, Tandahimba, Mtwara Vijijini, Nanyamba na Nanyumbu CUF itasimamisha wagombea huku majimbo ya Lulindi, Masasi na Ndanda wakiachiwa Chama cha National League Democratic (NLD),” alisema Kessy.


Kessy alisema Mkoa wa Lindi Ukawa kwa ujumla wao wamekubaliana kuwaachiwa CUF katika majimbo yote ambayo ni Mtama, Kilwa Kaskazini, Kilwa Kusini, Lindi Mjini, Ruangwa, Nachingwea, Liwale na Mchinga.

Mketo


Akizungumzia uamuzi huo, Kaimu Naibu Katibu Mkuu CUF, Shaweji Mketo alisema mgawanyo huo umezingatia mambo makuu matano ambao ni kuhusu mbunge aliyeko tangu waka 2010, nafasi ya chama katika uchaguzi huo wa 2010, nafasi ya udiwani, uchaguzi wa Serikali za Mitaa na nguvu na mtandao wa chama hadi sasa.


Mketo alisema lengo la Ukawa si kugawana majimbo kama inavyotafsiriwa ila ni kugawana kwa vigezo ili kuhakikisha wanapata ushindi wa jumla na kushinda uchaguzi ujao.


Makujunga


Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa NLD, Masudi Makujunga alisema chama chao kipo pamoja kuhakikisha kuwa mabadiliko ya kisiasa, kijamii yanatokea ndani ya nchi wakati huu.


“Lengo si ufahari katika kugawana majimbo, lengo letu ni kuhakikisha kuwa mabadiliko yanapatikana na sisi NLD tupo tayari kushiriki katika mabadiliko hayo kwenye sehemu husika,” alisema.


Mnyika


Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alisema jitihada za Ukawa zipo katika hali nzuri hivyo wao watahakikisha kuwa wanakuwa wamoja hadi kufikia hatima yao ambayo ni kushinda uchaguzi na kuongoza nchi.


Alisema kilichofanyika ndio makubaliono ya viongozi wao hivyo wana Ukawa wote wanapaswa kukubaliana na hali hiyo ili Taifa liweze kusonga mbele kwa maslahi ya wananchi na wapenda mabadiliko.


Aidha, Mnyika aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kutoa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa maelekezo ya kuvitaka na wagombea wao kurejesha fomu Agosti 19, mwaka huu huku ikiamini kuwa sheria inataka mchakato huo kukamilika Agosti 21.


Mnyika aliitaka NEC kutoa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa wanajeshi watatu ambao wanahusika na mfumo wa teknolojia ya habari katika tume hiyo jambo ambalo ni kinyume cha taratibu za tume hiyo.


Mnyika alisema iwapo tume itakuwa kimya itakuwa imethibitisha taarifa hizo ambazo kimsingi zinachochea vurugu na hofu kwa washiriki wa uchaguzi huo.


Ukawa uliasisiwa wakati wa Bunge Maalumu la Katiba mwaka 2014, lengo likiwa kuunganisha nguvu kwa ajili ya kusimamia na kutetea maoni ya wananchi yaliyowasilishwa kupitia rasimu ya pili ya Katiba iliyotayarishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.


Umoja huo ulihusisha wabunge kutoka vyama mbalimbali vya upinzani na baadhi ya wabunge kutoka kundi lililojulikana kama la 201ambapo baadaye, ulibaki na wabunge na viongozi kutoka vyama vya NLD, NCCR – Mageuzi, CUF na Chadema.


Lowassa


Wakati huo huo, Mgombea urais wa Chadema, Edward Lowasa amelakiwa na maelfu ya watu mjini hapa na kusema yeye ni muumini wa muungano wa serikali tatu na si mbili, ikiwa ni kuhitimisha mchakato wake wa kutafuta wadhamini Zanzibar.


Akihutubia maelfu ya wanachama wa vyama vinavyounda umoja huo na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Demokrasia Kibanda Maiti mjini Unguja, alisema wanaosema yeye si muumini wa serikali tatu ni wazushi na wapuuzwe.


Lowassa alisema alikuwa muumini wa mfumo huo tangu alipokuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu katika miaka ya 90. Alisema wanaosema yeye ni muumini wa serikali mbili na hawezi kubadilika hawamjui.


Alisema yeye na wenzake waliwahi kupendekeza jambo hilo katika vikao vya chama na serikali kwa lengo la kuimarisha muungano, lakini ilishindikana kutokana na viongozi wengi wa CCM kuwa na woga wa mabadiliko.


“Hali hii ya uwoga wa viongozi wengi wa CCM haikuja bure bali ni kutokana na mfumo wa chama hicho ila wanasahau mwalimu aliwahimiza kuwa Watanzania wanahitaji mabadiliko, na kwa mujibu wa Baba wa Taifa kama watayakosa ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM,” alisema.


Lowassa aliongeza, “fursa ya mabadiliko imekuja kupitia Ukawa na ninawaomba Watanzania tuitumie vyema na kuionesha CCM kuwa nchi hii inaweza kuwa na mabadiliko bila ya ubabe wala vitisho.”


Kabla ya mkutano huo alipokelewa na wafuasi wa vyama hivyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume mjini Zanzibar kisha msafara wake ulioongozwa na mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.


Alisema muungano kati ya iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar ni watu wa pande hizo mbili, hivyo kuna umuhimu wa kuwepo kwa maridhiano yatakayoondoa manung'uniko miongoni mwa wananchi wa pande hizo jambo ambalo atalisimamia kwa nguvu zake.


“Umaskini wa nchi hii una sababishwa na watu kutojiamini kwa baadhi ya watendaji wa serikali na kutosimamiwa kikamilifu kwa sheria za nchi, miongozo na maamuzi yanayofikiwa ktika vikao vya kitaifa jambo ambalo tukiwa timu moja mimi, babu Duni (mgombea mwenza) na Maalim Seif (mgombea urais wa Zanzibar) tutawapeleka mchaka mchaka ili kuleta maendeleo kwa kasi kubwa na ya ajabu,” alisema.


Aidha, mgombea huyo alikosoa hatua ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) ya kumvua ukamanda wa vijana taifa, muasisi wa Tanu na CCM, Kingunge Ngombare Mwiru na kuitaja hatua hiyo kuwa ni kukiuka haki ya kikatiba ya kutoa maoni na kwamba laana za kiongozi huyo zitakishukia chama hicho.


“Watu makini hamuwezi kukubali kumpoteza mtu kama Kingunge eti kwa sababu alitoa maoni yake hadharani kuhusu jambo la kweli. Wamesahau kuwa mzee huyu ndiye aliyekinusuru chama kisisambaratike wakati Ujamaa ulipokuwa umesambaratika ulimwenguni na yeye kuwa ndiyo msemaji mkuu wa chama. Jambo hili linaashiria mwisho wa zama za CCM na laana za kitendo hicho ni lazima ziwashukie na hawatakuwa na wa kumlaumu,” alisema Lowassa. 


Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na Chadema katika ardhi ya Zanzibar, mgombe mwenza wa Lowassa, Juma Duni Haji aliwaomba wananchi wa Zanzibar kuwaunga mkono na kuwapa ridhaa itakayowawezesha kuwaunganisha wananchi wa Tanzania kuelekea katika umoja na maridhiano.  


Maalim Seif


Akihutubia hadhara hiyo,  Maalim Seif alivitahadharisha vyombo vya dola kusimamia ulinzi wa raia na mali zao kwa haki bila ya upendeleo kutokana na kuwepo kwa taarifa za vitendo vinavyoashiria uvunjwaji wa sheria alivyodai vinafanywa na CCM.


“Wenzetu hawa wamekuwa mabingwa wa kuhubiri amani wanapokuwa majukwaani lakini wanaposhuka huwa ndiyo wavunjaji wakubwa wa amani kwani kuna taarifa kuwa wagombea wetu wa ubunge na udiwani katika Jimbo la Shauri Moyo na Wadi ya Kidatu wamevamiwa na kunyang'anywa fomu zao za kusaka wadhamini. Hali hii haiashirii kuwa kuna nia njema,” alisema.

 

Mapema aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambaye alijiunga na Chadema, Khamis Mgeja aliwataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kuiunga mkono Ukawa kwa kuwa ndiyo yenye uwezo wa kukidhi matakwa ya Wazanzibar na Watanzania.


Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwashukuru wananchi wa Zanzibar na CUF kwa kumridhia aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho na Waziri wa Miundombinu, Duni Haji kujiunga na Chadema hatua iliyomuwezesha kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Lowassa.


“Kumekuwa na vitisho dhidi ya watumishi wa vyombo vya dola kuwa mtaachwa pindi mkiwaunga mkono wagombea wa Ukawa, ninawatoa hofu kuwa mtaendelea kuwepo hata baada ya CCM kuondoka kwa sababu nyinyi mpo kwa mujibu wa sheria,” alisisitiza Mbowe na kuahidi kustawisha maslahi yao pindi Ukawa ikishinda.


Mbatia


Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema kupitia umoja wao wamewaagiza wanasheria wa vyama vinavyounda Ukawa kunakili matukio yote ya ukiukwaji wa haki binadamu vitakavyofanywa na watendaji au viongozi wa CCM ili waweze kuwafungulia kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita-The Hague. 




“Hatutavumilia aina yoyote ya uharamia ambayo itafanywa na mtu au taasisi ili kuvuruga harakati za Ukawa kuleta mabadiliko kupitia uchaguzi mkuu ujao, tumewaagiza wanasheria wetu kunakili kila tukio linaloashiria hali hiyo na tutamfikisha kila aliyehusika au atakayehusika kuhujumu matakwa ya demokrasia yasitekelezwe,” alisema.(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

Kipindi cha Jukwaa Langu Agosti 17 2015

$
0
0
Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Katika kipindi hiki utasikia mjadala wetu na wageni Jeff Msangi toka Toronto Canada na Darmatus Nambai aliyehudhuria studio kuhusu DEMOKRASIA na MABADILIKO kuelekea uchaguzi nchini Tanzania
KARIBU

EWURA FAMILY DAY ILIVYOFANA DAR

$
0
0
 Watoto wa familia za wafanyakazi wa wakishindana kukimbiaMamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Ewura kufurahi pamoja na familia zao (Ewura Family Day) kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam
 Wafanyakazi wa Ewura wakiwa katika picha ya pamoja na familia zao
 Wakiwa katika mchezo wa Wavu
 Wakishindana kukimbia huku wakiwa kwenye magunia
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi (kulia) akishiriki na wakurugenzi wenzie kushindana kuvuta kamba na wafanyakazi wa Ewura wakati wa siku ya wafanyakazi wa Ewura kufurahi na familia zao kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam juzi.

 Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), wakishindana katika mchezo wa kuvuta kamba wakati wa siku ya kufurahi na familia zao kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi (wa tatu kushoto) akishiriki kucheza mpira wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Ewura kufurahi pamoja na familia zao kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam
 Waliovaa fulana za bluu wakishindana soka na waliovaa njano

 Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo (kulia) akishiriki na wenzie katika shindano la kukimbiza kuku
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi akifurahia zawadi ya kuku aliyemkamata katika shindano la kufukuza kuku wakati wa siku ya wafanyakazi wa Ewura kufurahi na familia zao kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam juzi.


 Mwanafunzi Charles Daud ambaye ni mmoja wa watoto wa wafanyakazi wa Ewura akishangilia baada ya kushinda shindano la kufukuza kuku
 Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Ngamlagosi akikabidhi kikombe kwa mmoja wa washindi wa michezo iliyofanyika siku hiyo
 Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Ngamlagosi (kulia) akipokea kikombe kwa niaba ya wakurugenzi walioshinda katika mchezo wa kuvuta kamba
 Ngamlagosi akifurahia zawadi hiyo
 Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Ngamlagosi akikabidhi zawadi ya kikombe kwa nahodha wa timu ya ilivaa fulana ya njano  iliyoishinda  ya bluu katika shindano la kuvuta kamba
 Wafanyakazi na familia zao waliovaa fulana ya njano wakishangilia baada ya kukabidhiwa kikombe hicho
 Mfanyakazi wa Ewura Rachel Kiula akifurahia kupata zawadi ya kikombe aliyopata baada ya mfanyakazi pekee aliyeshiriki katika michezo mingi iliyochezwa siku hiyo.
 Baadhi ya washindi wa michezo mbalimbali wakishangilia huku wakiwa na zawadi zao

 Sasa ni wakati wa msosi


 Kijana mchekeshaji Comedian akiwa kazini baada ya watu kupata msosi
 Sasa ni wakati wa watoto kufurahi


 Wafanyakazi wa Ewura na familia zao wakipata ushauri nasaha kuhusu masuala ya kulinda  afya zao
Wafanyakazi wa Ewura na familia zao wakiwa katika picha ya pamoja

CCM YATANGAZA KAMATI YA KAMPENI ZAKE

Benki ya Exim Tanzania yaadhimisha miaka 18 ya kuanzishwa kwake.

$
0
0
 Afisa  Mtendaji Mkuu wa benki ya Exim Tanzania akizingumza na baadhi ya wafanyakazi  pamoja na wateja wa benki hiyo wakati wa hafla fupi iliyoaandaliwa na benki hiyo  kuadhimisha miaka 18 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa juma lililopita.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo  wakifurahia kwa pamoja wakati wa hafla fupi iliyoaandaliwa na benki hiyo  kuadhimisha miaka 18 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa juma lililopita
 Meneja Mwandamizi wa Benki ya Exim Tanzania tawi la Exim Tower, Bi Rose Kanijo (wa tano kulia) akiwaongoza wawakilishi wa wateja wa benki hiyo Bw. Geofrey Mihaambo (wan ne kulia) na Bi. Usha Kakad (wa tatu kulia) kukata keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili maadhimisho ya miaka 18 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa juma lililopita.Wanaoshuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
Meneja Mwandamizi wa Benki ya Exim Tanzania tawi la Exim Tower, Bi Rose Kanijo (wa tano kulia) akiwaongoza wawakilishi wa wateja wa benki hiyo Bw. Geofrey Mihaambo (wan ne kulia) na Bi. Usha Kakad (wa tatu kulia) kukata keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili maadhimisho ya miaka 18 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa juma lililopita.Wanaoshuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.


Exim Bank imeadhimisha miaka 18 tangu kuanzishwa kwake huku uongozi wa benki hiyo ukiahidi kuboresha zaidi huduma zake hasa katika kipindi hiki ambacho sekta benki imetawaliwa na ushindani mkubwa.

Benki hiyo iliyoanza kutoa huduma zake mwezi Agosti,1997 ikiwa na tawi moja jijini Dar es Salaam kwa sasa ina jumla ya matawi 30 hapa nchini  na matawi saba nje ya nchi huku pia rasilimali yake ikitajwa kuwa na thamani ya sh. trilioni 1.1 hadi kufikia mwezi juni mwaka huu.

Akizungumza hivi karibuni kwenye hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha baadhi ya waafanyakazi na wateja wa benki hiyo, Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw Selemani Ponda alisema mafanikio hayo kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na ukweli kuwa benki hiyo inafanya kazi chini ya bodi ya wakurugenzi iliyo imara.

“Siku kama ya leo miaka 18 iliyopita ndio benki yetu ilianzishwa. Leo benki ya Exim imesaidia ukuaji wa biashara  ndani na nje ya nchi na tunashukuru kuona kwamba baadhi ya wateja wetu wameweza kuhudhuria hafla hii ili tusherehekee pamoja siku hii muhimu,’’ alisema.

Kwa mujibu wa Bw. Selemani mbali ya kuwa na idadi kubwa ya matawi ndani na nje ya nchi pia imefanikiwa kuwa na mashine za kutolea fedha 57 hapa nchini, vituo vya mauzo zaidi 250 na kwa sasa ina matawi kwenye mikoa 16 hapa nchini ambayo yanahudumia takribani wateja 180,000.

“Miaka yote tumekuwa tukiitumia siku hii pia kutathmini ubora wa huduma zetu kwa wateja na ndio maana tumekuwa tukiendelea kufanya vizuri kila siku. Uhodari wa wafanyakazi wetu imekuwa pia imekuwa ni chachu kwenye mafanikio haya,’’ alibainisha bw. Ponda.

Kwa mujibu wa Bw. Ponda, benki hiyo ndio benki ya kwanza hapa nchini kufungua matawi yake nje nchi ambapo kwa sasa imefungua matawi yake visiwa vya Comoro na nchini Djibouti.

Ngoma Africa band na Mama wa Mitindo Asia Idarous-Khamsin wanogesha hafla ya kongamano la Diaspora hoteli ya Serena jijini Dar es salaam

$
0
0
Ngoma Africa band yenye makazi yake nchini Ujerumani na Mama wa Mitindo Asia Idarous-Khamsin walivyonogesha hafla ya Kongamano la Pili la Diaspora lililofanyika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam Agosti 15, 2015 ambapo Ngoma Africa band walituma CD yenye nyimbo kali mbili za kumuaga Rais Kikwete na Mama wa Mitindo alifanya onesho maalumu la mavazi ya Kiafrika.

VILABU VYA UN VYA ELIMU YA JUU VYAZIMISHA SIKU YA VIJA DUNIANI.

$
0
0

2
Mwenyekiti wa vilabu vya UN vya Elimu ya juu Zanzibar Ali Kombo Hassan akisoma risala ya vijana wa vilabu UN katika Mkutano uliofanyika Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
1
Mlezi wa vilabu vya UN vya Elimu ya juu Zanzibar Dkt. Muhd Makame Haji akiwakaribisha wageni walikwa katika Mkutano wa kuadhimisha siku ya vijana Duniani uliofanyika huko Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
3
Mjumbe wa vilabu vya UN vya Elimu ya juu Khadija Salum Khamis akitoa hutuba yake kuhusu madhara yanayopatikana kutokana na vurugu za uchauzi, katika Mkutano wa kuadhimisha siku ya vijana Duniani.
4
Afisa elimu ya wapiga kura kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar Juma Sanifu Sheha akitoa mada juu ya ushiriki wa vinaja katika uchaguzi wa Amani katika Mkutano wa kuadhimisha siku ya vijana Duniani uliofanyika huko Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
6Afisa programu ya maendeo ya Vijana mfuko wa idadi ya watu wa Umoja wa Mataifa ofisi ya Zanzibar Aoife Spengeman akitoa shukrani kwa vijana mara baada ya kumaliza kwa Mkutano huo (kushoto) Mratibu wa vilabu vya UN Zanzibar Maalim Ame Haji Vuai.
5
Baadhi ya Vijana wa vilabu vya UN vya Elimu ya juu wakimskiliza kwa makini mtoa mada Juma Sanifu kutoka Tume ya Uchaguzi (hayupo pichani) wakati akiwasilisha.Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar.

ATCL yarejesha safari zake kuelekea Mwanza.

$
0
0

 Abiria wakipanda kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Taifa, Air Tanzania (ATCL) aina ya CRJ-200 tayari kuelekea Mwanza katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Jumamosi jioni baada ya shirika hilo kurejesha safari zake kati ya Dar es Salaam na Mwanza baada ya kusimamisha safari hizo tangu mwezi Agosti mwaka jana. Shirika hilo litafanya safari zake kati ya majiji hayo mawili mara mbili kwa siku katika siku zote saba za wiki.
 Abiria wakishuka toka kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Taifa, Air Tanzania (ATCL) aina ya CRJ-200 katika uwanja wa ndege wa Mwanza Jumamosi jioni baada ya shirika hilo kurejesha safari zake kuelekea jijini Mwanza baada ya kusimamisha safari hizo tangu mwezi Agosti mwaka jana. Shirika hilo litafanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Mwanza mara mbili kwa siku katika siku zote saba za wiki.
Abiria wakipanda kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Taifa, Air Tanzania (ATCL) aina ya CRJ-200 tayari kuelekea jijini Dar es Salaam katika uwanja wa ndege wa Mwanza Jumamosi jioni baada ya shirika hilo kurejesha safari zake kati ya Dar es Salaam na Mwanza baada ya kusimamisha safari hizo tangu mwezi Agosti mwaka jana. Shirika hilo litafanya safari zake kati majiji haya mawili mara mbili kwa siku katika siku zote saba za wiki.

 SHIRIKA  la ndege la taifa (ATCL) limerejesha safari zake kuelekea mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya mpango wa shirika hilo kupanua huduma  kwa wateja wake hapa nchini.

Safari ya kwanza ya shirika hilo kuelekea mkoani Mwanza ilifanyika mwishoni mwa juma lilopita kwa kukutumia ndege yake aina ya CRJ- 200, baada ya safari hizo kusimama tangu mwezi Agosti mwaka mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Uwanja wa ndege wa Mwanza, Kaimu Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Bi Lily Fungamtama alisema uamuzi wa kurejesha safari hizo umezingatia mahitaji ya wateja wa shirika hilo.

“Tumepokea maombi mengi kutoka kwa wateja wetu wakiwemo wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kwa kuhusisha majiji haya mawili. Kwa kuwa ATCL ni shirika mama la ndege hapa nchini tukafanya kila jitihada kuhakikisha tunarejesha safari zetu kuelekea jijini Mwanza,’’ alibainisha Fungamtama huku akiongeza kuwa shirika hilo litafanya safari zake  mara mbili kwa siku katika siku zote saba za wiki.

Alisema ili kukabiliana na ushindani wa kibiashara dhidi ya mashirika mengine ya ndege yanayofanya safari zake kuelekea mkoani humo, shirika hilo limewekeza zaidi kwenye ubora wa huduma zake sambamba na kutoa huduma zake kwa gharama nafuu.

Akizungumzia na waandishi wa habari mara tu baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Uwanja wa ndege wa Mwanza mmoja wa abiria waliosafiri na ndege hiyo Bw. Bakari Hamidu mbali na kushukuru kurejeshwa kwa huduma hiyo pia alionyesha kuridhishwa kwake na ubora wa huduma unaotolewa na wahudumu wa shirika hilo.

“Nimefurahishwa sana na kurejeshwa wa huduma hii na zaidi nimefurahishwa na huduma nzuri zinazotolewa kwa abiria na wafanyakazi wa shirika hili. Kwa hilo lazima niwapongeze,’’ alisema Bw. Hamidu.

Pamoja na kurejesha safari hizo za mkoani Mwanza, shirika hilo pia kwa sasa linatoa huduma zake kuelekea mikoa ya Kigoma, Mtwara na visiwa vya Comoro kwa kutumia ndege yake aina ya CRJ-100.

“Tunatarajia mambo yatakuwa mazuri zaidi baada ya kukamilika kwa ukarabati wa ndege yetu nyingine aina ya De-Havilland Dash 8 Q300 inayoendelea na ukarabati mkubwa kwenye karakana iliyopo kwenye uwanja wa Kimataaifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam,’’ aliongeza Fungamtama.

Bayport yaanzisha huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na bajaj

$
0
0
Mratibu wa Bima kutoka Bayport Financial Services, Ruth Bura, katikati akizungumza katika uzinduzi wa huduma mpya ya Bima ya Magari, pikipiki na Bajaj kwa kushirikiana na Kampuni ya NIKO Insurance. Kulia ni Meneja Uendelezaji wa Biashara wa NIKO Insurance, Jabir Kigoda na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Niko, Mannaseh Kawoloka.

Na Mwandishi Wetu, Dar es SalaamTAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo, imezindua huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na bajaj, ikiwa na lengo la kurahisisha masuala ya usafiri kwa wateja wao ili kukwamua zaidi. Kuanzishwa kwa huduma hiyo mpya kumetajwa kuwa kutachangia kwa kiasi kikubwa wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri waliokuwa wakishindwa kulipa bima kwa wakati na wakati mwingine mteja kupata ajali hali ya kuwa hana huduma ya bima inayoweza kumlinda.
Oparesheni Meneja wa Bayport Financial Services, Charles Mgeta, kushoto akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya Bima ya Magari, pikipiki na bajaj. Anayefuata ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NIKO Insurance, Mannaseh Kawoloka.
1. Afisa Mtendaji Mkuu wa NIKO Insurance, Mannaseh Kawoloka katikati akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na bajaj inayoendeshwa na Taasisi ya Bayport Financial Services. Kulia kwake ni Mratibu wa bima hiyo, Ruth Buran a kushoto kwake ni Meneja Oparesheni wa Bayport, Charles Mgeta. Picha zote na Mpiga Picha Wetu. 
Wakati shughuli ya uzinduzi wa huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na bajaj kutoka Bayport Financial Services kwa kushirikiana na NIKO Insurance ukiendelea Makao Makuu ya Bayport leo asubuhi.
Meneja Madai wa Niko Insurance, David Mshuza, akiafuatiwa na Cecilia Peter na Lester Chinyang'anya. 

Akizungumza leo asubuhi jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Bima hiyo kutoka Bayport Financial Services, Ruth Bura, alisema huduma yao wanayoshirikiana na NIKO Insurance ina lengo kubwa la kumrudisha mteja wao (mkata bima), katika hali aliyokuwa nayo kabla ya kupata ajali hiyo.

Alisema mara kadhaa baadhi ya Watanzania wamekuwa wakikimbizana na askari wa usalama barabarani kwa sababu hawana bima kwenye vyombo vyao vya usafiri, ila kwa kupitia huduma yao mpya, sasa kila mtu anaweza kujiunga na bima kwa njia rahisi, wakiamini kuwa ni sehemu yao ya kuhakikisha wateja wao wanakuwa kwenye usalama ili watimize wajibu wao kufanya kazi na kukuza uchumi wao na wa Tanzania kwa ujumla.

“Ili mtu aweze kujiunga na huduma yetu ya Bima kutoka Bayport Financial Services, kwanza anatakiwa kujaza fomu yetu ya mkopo na ile fomu ya udhibitisho wa bima, bila kusahau nyaraka za umiliki wa gari lake ili tujiridhishe na umiliki wake.

“Baada ya hapo, gari lake litapigwa picha tano kila pembe, ikiwa ni nyuma na mbele na kwenye injini na tukimaliza hatua hiyo, mteja wetu atapatiwa mkataba wa bima pamoja na ‘sticker’ kuonyesha kuwa yupo kwenye bima, huku huduma hiyo ikiwa ni rahisi kwa sababu gharama za bima kwa mwaka ni kuanzia Sh 354,000 pamoja na VAT,” Alisema.

“NIKO tunajisikia faraja kubwa kushirikiana na wenzetu Bayport Financial Services kutoa huduma bora na kiwango cha juu, hususan kwa kupitia huduma hii mpya ya bima ya magari, tukiamini kuwa itawafanya Watanzania wote watembee kifua mbele, maana ile presha ya kukimbiana na watu wa usalama barabarani itakuwa imepatiwa ufumbuzi,” alisema Kigoda.

Bayport Financial Services ni taasisi ya kifedha inayotoa huduma mbalimbali za mikopo ya fedha, mikopo ya bidhaa, bila kusahau mradi wa mikopo ya viwanja vya Vikuruti unaoendelea na kuwafanya Watanzania watembee kifua mbele, huku taasisi hiyo ikifanikiwa kuwa na matawi 80 Tanzania Bara, hivyo kutoa huduma bora na kwa njia rahisi kwa kupitia matawi yao au mtandao wao wa www.kopabayport.co.tz.

Naye Meneja Uendelezaji wa Biashara wa NIKO Insurance, Jabir Kigoda, alisema kuwa huduma hiyo ni nzuri na rahisi inayoweza kuwanufaisha wateja na Watanzania wote, hivyo wanapaswa kuichangamkia ili kuwaweka katika usalama wao na wa vyombo vyao vya usafiri.

TAMASHA LA MICHEZO LA WAANDISHI WA HABARI ARUSHA KUTIMUA VUMBI AGOSTI 29

$
0
0
..Meneja masoko na mauzo wa Kampuni ya Mega Trade  Edmundi Rutaraka, akimkabidhi hundi ya Ts 1.5 Milioni Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha,Mussa Juma kwa ajili ya tamasha la  10 waandishi wa habari mkoa wa Arusha, Manyara na Dar es salam na wadau wa habari ambalo litafanyika Agoust 29 uwanja wa sheikh Amri Abeid, hafla hiyo ilifanyika jana, Palace Hoteli Jijini.
 
habari na libeneke la kaskazini blog
Tamasha la 10 la vyombo vya habari  na wadau wa habari mkoa wa Arusha, linatarajiwa kufanyika Agosti 29 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa kushirikisha timu nane ikiwepo  timu ya TASWA kutoka jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Palace Hotel , Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo mkoa wa Arusha(TASWA-Arusha), Mussa Juma, alisema tayari maandalizi muhimu yamekamilika.


Juma alisema Tamasha hilo linaloandaliwa na TASWA na kampuni ya Arusha Media.mdhamini Mkuu ni Kampuni ya Bia nchini( TBL) kwa miaka 10 sasa, litashirikisha michezo ya Soka, Mpira wa pete, kuvuta kamba na kukimbiza kuku.


"tunapenda kutangaza rasmi tamasha la 10 ya TASWA Arusha litafanyika Agosti 29 na kauli mbiu yetu ni Uchaguzi Mkuu bila vurugu inawezekana"alisema


Alisema katika Tamasha hilo, ambalo litashirikisha pia timu za wafanyakazi wa kampuni ya bia nchini(TBL) Taasisi na Faidika na kampuni ya Pepsi litaandamana na ziara ya wanahabari kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha.

Nahodha wa timu ya TASWA Arusha, Ramadhani Siwayombe akikabidhiwa jezi kwa ajili ya tamasha la waandishi wa habari na wadau wa habari mkoa wa Arusha ambalo litafanyika Augosti 29 Sheikh Amri Abeid, anayemkabidhi ni Filbert Masele meneja mikopo ya wafanyakazi wa FAIDIKA na Meneja wa FAIDIKA mkoa wa Arusha Eliya Mlay hafla hiyo, ilifanyika Palace hotel 

Wakizungumza katika kikao hicho, Meneja wa Masoko wa kampuni ya Mega Trade Edmund Rutaraka, Meneja masoko wa kampuni ya SBC(T) Lalit Sharma na Meneja wa Faidika Arusha,Eliya Mlay walisema wamedhamini Tamasha hilo ili kuendeleza michezo.




Rutaraka alisema kampuni yao kwa miaka mitano sasa inadhamini tamasha hilo na wanajivunia mafanikio makubwa.


Tamasha hilo, limedhaminiwa na kampuni ya bia nchini(TBL) Kampuni ya Mega Trade,Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA),Shirika la Nyumba nchini (NHC) Kampuni ya SBC(T) Ltd,Mamlaka hifadhi Ngorongoro(NCAA), Taasisi ya FAIDIKA na Tanzanite One.

Makamu Mwenyekiti wa TASWA Arusha, Adrea Ngobole alisema wadhamini wengine wa Tamasha hilo watatangazwa karibuni sambamba na zawadi na mgeni rasmi.

 Meneja wa masoko na mauzo wa Kampuni ya SBC(T) Lalit Sharma, akimkabidhi mipira Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha, Mussa Juma kwa ajili ya Tamasha la kumi la waandishi wa habari mkoa wa Arusha,Manyara na Dar es Salaam na wadau wa habari, ambalo litafanyika Agoust 29 uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
 Makamu Mwenyekiti wa TASWA mkoa wa Arusha,Andrea Ngobole, akipokea  vikombe kutoka kwa Filbert Masele meneja mikopo ya wafanyakazi wa FAIDIKA na Meneja wa FAIDIKA mkoa wa Arusha Eliya Mlay jana Palace Hotel  kwa ajili ya tamasha la waandishi wa habari na ambalo litashirikisha pia wafanyakazi wa taasisi hiyo, ambalo litafanyika Augost 29 uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Wadhamini na viongozi wa TASWA Arusha, wakiwa kwenye kikao na waandishi wa habari kuelezea Bonanza la vyombo vya habari na wadau wa habari mkoa wa Arusha,ambalo litafanyika Augosti 29 uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

NAIBU WAZIRI SILIMA AONGOZA MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU NA PEMBE YA AFRIKA KATIKA MAPAMBANO YA KUZUIA NA KUDHIBITI UZAGAAJI WA SILAHA HARAMU (RECSA), ZANZIBAR LEO

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akitoa hotuba fupi ya kuwakaribisha nchini wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) kabla ya kufungua kikao cha wajumbe hao kinachofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar. Lengo la kikao hicho ni  kujadili masuala mbalimbali ya jinsi ya Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan Kusini, Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania.
 Wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) wakiwa katika chumba cha mkutano wakijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan ya Kusini, Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania. Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani) ndio Mwenyekiti wa Baraza hilo, hata hivyo katika Mkutano huo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia meza kuu) anamuwakilisha katika kikao hicho. 
 Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini, Pereira Ame Silima (kulia) akiwa na  Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Uganda ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Balozi James Baba (katikati) na Mjumbe wa Baraza hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Usalama wa Ndani nchini Rwanda, Balozi Munyabagisha Valeus, wakisoma taarifa za masuala mbalimbali ya jinsi ya Kupambana ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan Kusini, Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania. Baraza hilo limekutana katika Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar leo.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Nchi nchini, Pereira Ame Silima (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza hilo ambalo nchi zake wanachama ni Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan Kusini, Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania. Wajumbe hao wamekutana katika Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar leo.

Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.


MFUKO WA PENSHENI WA PSPF, TPB KWA KUSHIRIKIANA NA PROPERTY INTERNATIONAL LIMITED WAZINDUA MPANGO WA KUWAKOPESHA VIWANJA WANACHAMA WA MFUKO HUO

$
0
0
 WAZIRI wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais, (anayeshughulikia masuala ya Muungano), Samia sSuluhu Hassan,(wapili kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Sabasaba Moshingi, (wakwanza kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Property International Ltd, (PIL), Abdulkarim Haleem, (watatu kulia), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji, Gabriel Silayo, (wane kulia), wakiwa wamekamata mwamvuli ikiwa ni ishara ya umoja, kwenye uzinduzi wa mpango wa kukopesha viwanja wanachama wa PSPF ambapo TPB itaratibu ukopeshwaji huo kwa kutoa fedha. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam Jumanne Agosti 18, 2015.

 Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano), Samia Suluhu Hassan, akitoa hotuba

 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Gabriel Silayo, akitoa hotuba yake

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, TPB, Sabasaba Moshingi, akitoa hotuba yake

 Msanii wa muziki wa majigambo, Mrisho Mpoto, ambaye pia ni balozi wa PSPF, akitoa burudani kwenye hafla hiyo.

 Mh. Samia Suluhu Hassa, akimpongeza Silayo baada ya kutoa hotuba yake. Wanaoshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi,(kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa PIL, Abdulkarim Haleem.

NA K-VIS MEDIA
 MFUKO wa wa Pensheni wa PSPF kwa kushirikiana na  Benki ya Posta Tanzania, TPB, na Taasisi ya Property International Ltd leo Agosti 18, 2015 wamezindua mpango maalum wa kutoa mikopo ya viwanja kwa wanachama wa mfuko huo katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Hyatt Regency.

Lengo la mkopo huu wa viwanja ili kuwawezesha wanachama wa mfuko huu kumiliki viwanja vilivyopimwa na vilivyo halali kwa mujibu wa taratibu za nchi. Nia ni kwenda sambamba na dira ya PSPF ambayo ni kutoa huduma bora zenye ushindani katika sekta ya Hifadhi ya  Jamii kwa wateja wa PSPF, na pia kuitikia mwito wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),walioagiza Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii kutoa mafao kwa fomula iliyo sawa kwa watumishi wote. Hivyo kuanzia wakati huo Mifuko ya Hifadhi inapaswa kushindana kwa ubora wa huduma na vivutio vingine kwa wananchama na wananchama watarajiwa.

Ni dhahiri kuwa kila Mtanzania anahitaji kuwa na makazi bora ya kudumu, hivyo mpango huu unaozinduliwa leo hii ni mpango mzuri sana hasa kwa Watanzania wengi ambao hawana uwezo wa kutoa fedha taslimu. Utaratibuu huu wa kuwakopesha utawanufaisha wengi  na hatimaye kufikia kauli mbiu ya Serekali yetu ya kuhakikisha Maisha bora kwa kila Mtanzania.

Mfuko wa Penshini wa PSPF umeendeleza ushirikiano wake mzuri na Benki ya Posta Tanzania, ambapo kama mnavyofahamu ushirikiano wao ulianzia kwenye utoaji wa Mikopo kwa Wastaafu, Mkopo wa Elimu na Mkopo wa kuanzia Maisha kwa wanachama wapya. Jitihada hizi zote ni katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wanachama wake, na pia katika kuonesha imani kwa Benki ya Posta, ambayo huduma zake bora zinapatikana kote nchini. Mahusiano haya na Property International Ltd yanazidi kujenga mahusiano haya kwa maslahi ya wanachama na Watanzania kwa ujumla.

Wanachama wa PSPF waliochangia Mfuko kwa kipindi kisichopungua miezi sita wanasifa zote za kuweza kukopa viwanja hivi, na watapaswa kulipa ndani ya miaka mitatu. Wanachama walio katika mpango wa Uchangiaji wa Hiari pia watafaidika na mkopo huu. Wanachama wote wa Mfuko wa Hifadhi wa PSPF wanakaribishwa sana kupata mkopo huu maalum kwa ajili yao.


 Mgeni Rasmi, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PSPF

 Mgeni rasmi, Samia, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TPB


  1.  Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PIL

Moshingi, (kushoto), akibadilishana mawazo na Meneja Masoko wa PIL Zohra Moore, (kulia
 Mh. Samia, (kulia), akisindikizwa na Silayo, wakati akiondoka ukumbi wa Hotel ya Hyatt, baada ya hafla hiyo
Moshingi (kulia), akisalimiana na Mh. Samia Suluhu Hassan, wakati akiwasili kwenye hafla hiyo

MAKALLA ATEMBELEA MIRADI YA MWAUWASA JIJINI MWANZA LEO

$
0
0
 Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla akikagua mradi wa majisafi katika Kituo cha Majisafi cha Capri Point, akiwa pamoja na Mkurugenzi wa MWAUWASA, Inj. Anthony Sanga.
 Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla akiwa kwenye mradi wa majitaka katika Kituo cha Kusukuma Majitaka cha Makongoro.

 Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla akiambatana na Meneja Msaidizi wa Operesheni ya Tiba ya Maji (Sanitation Operation), Inj. Salim Lossindilo katika mradi wa tiba ya maji (sanitation) Butuja, unaopokea majitaka kutoka Makongoro na kuyatibu na kutumika kwa ajili ya matumizi mengine.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla akiwa pamoja na Bodi ya MWAUWASA, wafanyakazi wa MWAUWASA na maafisa wa Wizara ya Maji alipotembelea ofisi ya MWAUWASA, Capri Point.

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla leo ameendelea na ziara yake Kanda ya Ziwa kwa kutembelea miradi ya Mamlaka ya Majisafi na Mazingira, jijini Mwanza (MWAUWASA) na kukagua utekelezaji na maendeleo ya miradi ya maji mkoani Mwanza.


Aidha, Mhe. Makalla aliweza kujionea ujenzi wa jengo jipya la MWAUWASA, Isamilo na kuzungumza na wafanyakazi wa MWAUWASA katika hafla fupi ya kuwazawadia wafanyakazi waliofanya kazi kwa uaminifu kwa zaidi ya miaka 15 katika ofisi za MWAUWASA zilizopo Capri Point.

STARS KUONDOKA NCHINI JUMAMOSI

$
0
0
Afisa habari wa TFF,Baraka Kizuguto.
TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajiwa kuondoka nchini siku ya jumamosi usiku kuelekea Muscat Oman, kucheza mchezo wa kirafiki kabla ya kuunganisha kuelekea Istambul Uturuki kwa kambi ya wiki moja.
Taifa Stars imepata mwaliko wa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Oman tarehe 24 Agosti, 2015 usiku, ambapo baada ya mchezo huo timu itasafiri kuelekea nchini Uturuki katika jiji la Istambul.
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Oman (OFA) liliomba kucheza mchezo wa kirafiki na Taifa Star kabla ya kuwavaa Turkemebistan katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia Septemba 03, 2015 kwa bara la Asia, ambapo kocha wake mkuu Mfaransa Paul Leguen aliomba kucheza na vijana wa Charles Mkwasa kujiandaa na mechi hiyo.
Mara baada ya mchezo huo Taifa Stars itaelekea Istambul katika mji wa Kocael hoteli ya Kartepe kwa kambi ya wiki moja, ikiwa nchini Uturuki Stars inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki kabla ya kurejea nchini kucheza na Nigeria Septemba 05, 2015 mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika.
Kocha mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa anatarajiwa kutoa orodha ya kikosi chake cha wachezaji 22 mwishono mwa wiki watakaosafiri kuelekea nchini Uturuki kwa kambi ya hiyo ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria.
Mshambuliaji Adi Yussuf anayechezea klabu ya Mansfield Towny ya Uingereza alitarajiwa kujiunga na timu nchini Uturuki, lakini kutokana na majeruhi aliyoyapata hivi karibuni katika michezo ya ligi, uongozi wa Mansfield umeomba mchezaji huyo kutojiunga na timu ya Taifa kwa ajili ya kupata mataibabu zaidi.
Adi aliumia wiki iliyopita katika mchezo dhidi ya Nottingham Forest ambapo kwa sasa anaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa klabu hiyo, na pindi atapokuwa fit atapata nafasi ya kujumuika na kuitumika timu ya Taifa ya Tanzania.

UTAFITI WA AFYA YA UZAZI NA MTOTO NA MALARIA KUANZA RASMI

$
0
0
 Mgeni rasmi, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Dkt. Ahmed Makuwani kutoka Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii akiwahutubia Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akielezea umuhimu wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
 Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu akitoa maelezo ya awali wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
 Baadhi ya Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Mgeni rasmi, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Dkt. Ahmed Makuwani kutoka Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 mara baada ya kufunga mafunzo ya utafiti huo wilayani Moshi, Kilimanjaro. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).


Wito umetolewa kwa viongozi wote wa Serikali katika Ngazi zote na wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano kwa Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria utakaoanza rasmi tarehe 21 Agosti, 2015.
 
 Wito huo uletolewa leo na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Ahmed Makuwani wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika wilayani Moshi, Kilimanjaro.
 
"Ninawaomba Wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Wadadisi, Wasimamizi na Wahaririwatakaoshiriki zoezi la kukusanya Takwimu za Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015 ili kupata taarifa muhimu na sahihi kwa ajili ya kupanga Mipango na Sera endelevu za Sekta ya Afya katika nchi yetu, amesema Makuwani".
 
Dkt. Makuwani amesema kuwa taarifa zitakazokusanywa kwa wananchi kwa ajili ya  utafiti huo zitakuwa ni siri na zitatumika kwa shughuli za Kitakwimu tu na wala hazina uhusiano wowote na Uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.
 
kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema utafiti huu wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015  unalenga kukusanya taarifa nyingi za sekta ya afya zinazotumika katika kutathmini malengo mbalimbali na pia kusaidia katika kupanga mikakati mipya.
 
Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa mara nyingine tena inafanya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015 ambao kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2010. Utafiti huu utaanza rasmi tarehe 21 Agosti, 2015 kwa nchi nzima na utamalizika mwishoni mwa Mwezi Februari 2016.
Viewing all 46327 articles
Browse latest View live




Latest Images