Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

ACT–WAZALENDO WAMCHUKULIA FOMU YA URAIS PROF. MKUMBO

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
CHAMA Cha ACT-Wazalendo wamechukua fomu kwa ajili ya mgombea urais atakayepeperusha  bendera katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam baada ya kuchukua fomu ya urais,Katibu Mkuu wa Chama hicho,Samson Mwigamba amesema kamati kuu imempitisha Profesa Kitila Mkumbo kuperusha bendera katika uchaguzi utaofanyika mwishoni mwa Oktoba mwaka huu.
Mwigamba amesema kuwa wamejipanga katika kushinda uchaguzi huo kutokana na watu waliokupwepo katika chama hicho ni wazalendo wa vitendo.
Amesema kuwa watu amesema chama chao ni kidogo lakini wameweza kusimamisha wagombea wa ,Udiwani,pamoja na ubunge ambapo katika vyama vyote vilivyoanizisha kwa kipindi kifupi vilishindwa kufanya hivyo.
Aidha amesema wanamuamini Profesa Mkumbo kutokana na malengo ya uanzishaji wa chama hicho kwa kutoa mchango mkubwa hivyo lengo la chama limetimia.
Amesema ambao wanahamia katika Chama hicho watapimwa uadilifu wao katika kuweza kuwatumikia wananchi wanao wachagua katika nafasi mbalimbali.

ACT-Wazalendo wamechukua fomu kwa kuwa idadi ndogo kuliko vyama vyote na utulivu ulitawala katika ofisi za tume ya Tifa ya Uchaguzi (NEC).

 Mwakilishi wa chama cha ACT WAZALENDO na Katibu mkuu  wa chama ACT WAZALENDO, Samsoni Mwigamba akipewa maelekezo na Afisa tawala wandamizi wa Tume ya uchaguzi (NEC),George Baasha kuhusiana na vitu vinavyotakiwa kwenye uchaguzi mkuu pamoja na kampeni zitakazo anza hivi karibuni.
 Katibu mkuu  wa chama ACT WAZALENDO, Samsoni Mwigamba akimwakilisha Dkt. Kitika Mkumbo  kupokea fomu ya kugombea nafasi ya urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT WAZALENDO amechukua fomu hizo leo katika ofisi za Tume ya uchaguzi (NEC) leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu mkuu  wa chama ACT WAZALENDO, Samsoni Mwigamba akionyesha fomu ya kugombea nafasi ya urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT WAZALENDO  mara baada ya kupokea fomu hiyo katika ofisi za Tume ya uchaguzi (NEC) leo jijini Dar es Salaam.
  Katibu mkuu  wa chama ACT WAZALENDO, Samsoni Mwigamba akizungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi za Tume ya uchaguzi (NEC) leo jijini Dar es Salaam.

Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

EAC SECRETARY GENERAL CONCLUDES WORKING VISIT TO USA

$
0
0
  EAC Secretary General Amb. Dr Richard Sezibera with members of Kansas Department of Agriculture after a meeting the SG held with the Department.
 Amb Sezibera stresses a point during the meeting with Kansas State Governor Sam Brownback.

East African Community Secretariat, Kansas City, USA, August 17, 2015: The Secretary General of the East African Community, Amb. Dr. Richard Sezibera, concluded a three-day visit to the State of Kansas, United States of America.

During the visit, the Secretary General met and held talks with the Governor of the State of Kansas, Mr. Sam Brownback, as well as the Kansas Department of Agriculture. Amb. Sezibera and his counterparts held discussions on how EAC can work together with Kansas State in areas of Trade and Investment, Agriculture, Education and Pharmaceutical industries.

Speaking during the meeting with the Governor, Amb. Sezibera described the progress registered in various regional infrastructure projects, noting that while these projects were negotiated at regional level, implementation was often done by the Partner States.

The EAC Secretary General informed the Governor that the EAC is open to more structured discussions with the State of Kansas on improving business environment in the region, adding that a bilateral investment agreement framework between both parties was welcome.

In his remarks, Governor Brownback commended the Secretary General for his leadership and commitment in the East African integration. He said the State of Kansas was elated with the developments within the EAC and would continue keeping tabs on progress of the integration.

Meanwhile, Amb Sezibera also met the team from Kansas Department of Agriculture and held discussions with the department on various issues including how the EAC Partner States and the State of Kansas can work together towards the introduction of a Smart Agriculture Programme in East Africa.

BASATA YALIFUNGULIA SHINDANO LA MISS TANZANIA

$
0
0
                                          


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limelifungulia shindano la urembo la Miss Tanzania baada ya mwandaaji wake Kampuni ya LINO International Agency Limited kufuata taratibu, kuomba radhi na kuyafanyia kazi baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza na kutekeleza masharti aliyopewa.

Itakumbukwa kuwa mnano tarehe 22/12/2014 BASATA liliwaandikia barua LINO International Agency Limited ya kulisimamisha shindano la Miss Tanzania kwa miaka miwili (Mwaka 2015 na 2016) na kuwaagiza kujipanga upya na kurekebisha kasoro ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara.

Mapungufu yaliyobainishwa ni pamoja na; mosi, kutokufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za uendeshaji matukio ya Sanaa nchini, pili kutokuwasilisha nyaraka mbalimbali za shindano lake hususan mikataba ya washiriki. Tatu kutumia mawakala wasiosajiliwa na kupewa vibali vya BASATA.

Miongoni mjwa mapungufu ambayo Kampuni ya LINO imeyafanyia kazi ni kuanza mchakato wa usajili wa mawakala – BASATA na kufanyia marekebisho kanuni na taratibu za uendeshaji wa Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania. Aidha, LINO imewasilisha muundo wa kamati ya uendeshaji wa shindano yenye muelekeo wa kuzingatia jinsia.

Katika kuboresha na kurudisha hadhi ya shindano la Miss Tanzania, LINO International Agency Limited imepewa kibali cha muda kisichozidi miezi minne (4) kwa ajili ya maandalizi ya awali ikiwemo kukamilisha usajili wa mawakala katika ngazi zote husika.

BASATA linapenda kuwafahamisha wadau wote wa Sanaa hususan wale wa shindano la urembo la Miss Tanzania kwamba Kampuni ya LINO imetekeleza maagizo ya msingi iliyopewa kama masharti ya kufunguliwa. Na kwamba baada ya kufanyia kazi changamoto zilizokuwa zimejitokeza BASATA limeyafungulia mashindano ya Miss Tanzania kwa masharti ya kukamilisha changamoto zilizobakia.

Ni matarajio ya BASATA kwamba kampuni ya LINO itazingatia taratibu zote za uendeshaji wa matukio ya Sanaa nchini na kwamba haitarudia tena makosa yatakayopelekea kuliweka shindano hili katika hali ya kushuka hadhi na kuzua sintofahamu katika jamii.
Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini

Godfrey Mngereza
KATIBU MTENDAJI

WATATU WAIBUKA WASHINDI SHINDANO LA MUZIKI MNENE-KISARAWE

$
0
0


Jimmy Jiam akiwa na washindi wa Muzuki Mnene Bango  eneo la Kisarawe,Washindi hao walitokana na kuwenga bango la EFM katika sehemu zao mbalimbali  na kama wanavyoonekana tayari wamekabidhiwa zawadi zao.

NYAMAGANA DC AFUNGUA AIRTEL RISING STARS MWANZA

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akikagua timu wakati wa uzinduzi wa Airtel Rising Stars mkoa wa Mwanza jana.
 Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akiongea wakati wa uzinduzi wa Airtel Rising Stars mkoa wa Mwanza jana.

MKUU wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga jana Jumapili (Agosti 15) alifungua mashindano ya Airtel Rising Stars mkoa wa Mwanza na kuwambia vijana kuwa wanalo jukumu la kubadilisha matokeo ya timu za Tanzania hasa katika mashindano ya kimataifa ambapo Tanzania imekuwa haifanyi vizuri.


Akifungua mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars katika mkoa wa Mwanza, Konisaga alisema anaamini kuwa mkoa wa Mwanza umejaliwa kuwa na wachezaji wenye vipaji vya soka na ndio maana mwaka juzi uliibuka bingwa wa Airtel Rising Stars kwa upande wa wavulana. Amekitaka chama cha soka mkoa wa Mwanza (MZFA) kutumia mashindano ya Airtel Rising Stars kubaina wachezaji wazuri na kuwaendeleza.


Mkoa wa Mwanza ulivuma sana miaka ya themanini kupitia timu ya Pamba ambayo wachezaji wake kama vile Joram Mwakatika, Madata Lubigisa, John Mhina, Beya Simba, Raphael Paul na wengine wengi walikuwa moto wa kuotea mbali.


Mheshimiwa Konisaga ameipongeza kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuona umuhimu wa kuwekeza sehemu ya raslimali yao kwenye maendeleo ya mchezo wa soka kwa vijana. “Mashindano ya Airtel Rising Stars ni fursa nzuri. Ni vema timu mbalimbali za soka zikayatumia kupata vijana wenye vipaji na kuwaendeleza”, alisema.


Alisema mbali ya kuwa jukwaa la kutumia kubaini wachezaji wenye vipaji, Airtel Rising Stars pia yanawahamasisha vijana kushiriki mazoezi hivyo kuwa na afya njema na kuhudhuria darasani kama kawaida.


Konisaga aliwaambia vijana kwamba kwa dunia ya leo mpira ni chanzo cha ajira ya kutumainiwa kwa mamilioni ya vijana ambao wanaishi maisha mazuri kwa kuwa wanalipwa mishahara mizuri.


Aliwataka viongozi wa chama cha soka mkoa wa Mwanza kuchagua wachezaji wenye vipaji kuunda kombaini ya mkoa itakayoshiriki kwenye fainali za Taifa za Airtel Rising Stars jijini Dar es Salaam ambazo zinatarajia kuanza mwezi ujao.


Naye mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana (TFF) Ayoub Nyenzi aliwataka viongozi wa soka kuzingatia kanuni za mashindano hayo has suala la umri.  Mwenyekiti wa MZFA Jackson Songora amejinasibu kwamba mkoa wake una vijana wenye vipaji ambao bila shaka watatwaa ubingwa wa taifa mwaka huu.


Akizungumza kwenye hafla hiyo, Ofisa Masoka wa Airtel Tanzania Mkoa wa Mwanza Emmanuel Raphael amewashukuru wadau wote wa soka kwa kuyaunga mkono mashindano ya Airtel Rising Stars na kuyapa umuhimu yanaostahili.

INTERESTING FACTS YOU SHOULD KNOW ABOUT SWAHILI CULTURE IN TANZANIA

$
0
0
SWAHILI culture is one that is unique. It is the product of the influence of the Middle East, India and Persia on the coastal region . The coast of East Africa had a long history of trade that involved exchange of ideas and commodities. Also mixed marriages between of African women and Middle Eastern men created and cemented a rich Swahili culture.

Thus the diversity of Swahili culture was a result of the interaction of the coastal people with foreigners in ancient times around the small coastal strip in Dar es Salaam, Lamu, Zanzibar and Mombasa. It is very interesting for travelers and tourists since their uniqueness cannot be compared to other cultures in Africa. Jovago Tanzania mentions some peculiar features which make it distinctive.

Language - Swahili people use “Kiswahili” as their common language, it’s the language that binds people together. The interactions during the coastal trade and colonialism made the language grow by borrowing words from other languages.

Artifacts and crafts - Swahili people use various skills to express themselves in artistic forms which include furniture and architecture. The designs are said to be in form of geometry and the crafts specifically Kanga is quite enchanting. It is not just a rectangular piece of cloth but also an artifact of the Swahili culture.

Women with a khanga
Music - The outstanding emblematic music genre of the Swahili culture is taarab or taarab, which is mostly sung in the language. The melodies and orchestration have Arab and Indian influences.

During the 20th century,  several musical  styles have emerged in the Swahili world. A good example is the infusion of ‘Dansi’ derived from Congolese soukous (rumba) and some elements of  Afro-pop
Old taarab in Zanzibar

Food; Ugali and chips yai are the very popular food in most of tribes, Ugali can be eaten with stewed or roasted meat especially at home but chips yai is the easiest food to buy at restaurants.
Ugali

Recreation - Holiday celebrations are the most important forms of leisure, at the end of the year most people like to travel to their local village for the purpose of greeting their relatives and ancestors

But also, nowadays some families like to plan for tour instead of going to the village, popular places like Zanzibar, Arusha, Tanga, and Morogoro are great historical sites, and  Dar es Salaam for beaches and enjoying big hotels in town.

Time - This is very interesting, Swahili time can’t be compared with others, most tourists may get confused  by this, when Swahili people say it is 3 am that means it is actually 9am.

Greetings - The general greeting is ‘mambo, jambo, and habari’ and the reply is Salama, but for the Muslims like to use the Arabic world “Asalaam Aleikhum”. Nevertheless, children are supposed to greet their elders with respect by touching the forehead or kissing the elder’s hand.

Transport; Many people use bajaji , motorcycle or dalala for the public transport in Dar es Salaam, but also Tanga and Zanzibar like to use bicycle, and few of them use daladala .


Bajaji in Dar es Salaam.

IDARA YA UONGOZAJI NDEGE YA MAREKANI FAA YATOA MAFUNZO KWA WAONGOZA NDEGE BARANI AFRIKA

$
0
0
 Kaimu  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Wa Anga Tanzania (TCAA) Varrely Chanmlunga akimkaribisha Meneja Mipango  wa Kimataifa wa  Idara ya uya uongozaji wa Ndege wa Marekani (FAA) Michele Cappelle  wakati wa Warsha ya uongozaji  wa ndega  barani afrika  iliyoandaliwa na  Idara ya Anga ya Marekani  .Washa hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara  ya Uongozaji  wa Ndege ya Marekani (FAA) Tony Ferrante.
 Baadhi ya washiriki wa Warsha ya uongozaji wa Ndega  barani afrika  iliyoandaliwa na  Idara ya Anga ya Marekani (FAA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)leo  jijini Dar es Salaam wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa katika warsha hiyo.
 Kutoka (kushoto ) Kaimu  Mkurugenzi wa Idara ya hudumu toka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA ,Viola Masaku na Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Uongozaji ndege wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Said Onga wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa warsha ya uongozaji  wa ndege barani Afrika  iliyoandaliwa na Idara ya Anga ya Marekani  (FAA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAa,leo jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi wa Idara  ya Uongozaji  wa Ndege  nchini  Marekani (FAA) Tony Ferrante akitoa mafunzo ya uongozaji wa ndege wakati wa warsha iliyowashirikisha waoungozaji ndege kutoka barani afrika ,wakati wa warsha iliyoandaliwa na Idara ya uongozaji wa Ndege ya Marekani  na  TCAA ,leo jijini Dar es Salaam.  Wanao msikiliza kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Wa Anga Tanzania (TCAA) Varrely Chanmlunga, Meneja Mipango  wa Kimataifa wa  Idara ya uya uongozaji wa Ndege wa Marekani (FAA) Michele Cappelle  na  mtaalamu  wa mipango  wa idara ya uongozaji wa ndege  wa Marekani FAA,Rebecca Barthe
Washiriki wa warsha ya uongozaji wa ndege barani afrika wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa na Idara ya uongozaji wa ndege ya Marekani FAA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA,iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

WANACHAMA WA VYAMA VYA SIASA WAJITOKEZE KUWANIA NAFASI MBALI MBALI KUWANIA NAFASI NEC

$
0
0
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali

Iddi akikabidhiwa Fomu za kuwania nafasi ya Ujumbe wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar Jimbo la Mahonda kutoka kwa Afisa wa Uchaguzi
Wilaya ya Kaskazini B Ndugu Makame Pandu Khamis.

 Afisa wa Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini B Nd. Makame

Pandu Khamis akitoa maelezo kumpatia Balozi Seif ya namna ya ujazaji
wa fomu za kuwania Uwakilishi Jimbo la Mahonda Ofisini kwake Mahonda
Wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa wa Kaskazini Unaguja.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
akisalimiana na baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi mara baadaya kuchukuwa fomu za kuwania Uwakilishi Jimbo la Mahonda hapo Ofisi yaTume ya Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini B iliyopo Mahonda.

WANACHAMA mbali mbali wa Vyama vya Siasa Nchini walioomba na
kuthibitishwa na vyama vyao kuwania nafasi mbali mbali za uongozi
wameanza rasmi kujitokeza kuchukuwa fomu za kuwania kugombea nafasi
walizoomba katika  Ofisi za Tume ya Uchaguzi za Wilaya.

Zoezi hilo litalowashirikisha wagombea nafasi za Ubunge, Uwakilishi na
Udiwani linatarajiwa kuendelea hadi Tarehe 6 Septemba 2015 ambapo
wanaochukuwa fomu hizo watalazimika kujaza vipengele vyote vinne
vilivyomo kwenye Fomu hizo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikuwa
miongoni mwa wanachama kadhaa wa Chama cha Mapinduzi waliojitokeza
kuchukuwa Fomu hizo ambapo yeye ameamuwa kugombea nafasi ya Ujumbe wa
Baraza la Wawakilishgi Jimbo la Mahonda.
Balozi Seif alikabidhiwa fomu hizo mapema asubuhi na Afisa wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar {ZEC } Wilaya ya Kaskazini “B” Ndugu Makame Pandu
Khamis hapo ilipo ofisi hiyo Mahonda Wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa wa
Kaskazini Unguja.

Akikabidhi fomu hizo Afisa huyo wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Wilaya ya
Kaskazini B Ndugu Makame Pandu Khamis amethibitisha kwamba Balozi Seif
Ali Iddi ni Mgombea  halali wa kuwania nafasi ya Ujumbe wa Baraza la
Wawakilishi Jimbo la Mahonda kupitia CCM.

Nd. Makame alisema kwamba uhalali huo unatokana na Ofisi yake kupokea
barua rasmi kutoka Chama cha Mapinduzi { CCM } iliyoainisha na
kuthibitisha kwamba Balozi Seif Ali Iddi ameteuliwa na chama hicho
kuwania nafasi hiyo ya Uwakilishi kwenye Jimbo la Mahonda.

Afisa Uchaguzi huyo wa Wilaya ya Kakaskazini B alifafanua na kuwataka
wagombea wote watakaochukuwa fomu za kuwania nafasi hizo kutumia fursa 
ya kufika kwenye Ofisi hiyo kwa kupata ushauri zaidi wa namna ya
kujaza vyema fomu hizo licha ya kupatiwa maelezo ya awali wakati
wanapokabidhiwa.

Alisema hatua hiyo kwa kiasi kikubwa itatoa fursa pana ya kutatua
changamoyo zinazoweza kujitokeza  na  kuepukwa mapema ili kukidhi
matarahio yaliyopangwa na tume hiyo.

Balozi Seif Ali Iddi alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kitope kupitia chama
cha Mapinduzi kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita ambapo kutokana na
mabadiliko yaliyofanywa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar  jimbo hilo
limevunjwa na kuzaliwa majimbo mawili ya Mahonda na Kiwengwa.

JK AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM KWENYE OFISI ZA LUMUMBA LEO

$
0
0
 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu maalum kwenye ofisi za Makao Makuu ya Chama ,Ofisi Ndogo Lumumba,kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakatiwa na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakati wa kikao hicho.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana wakipitia baadhi ya ajenda kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa taarifa za mahudhurio ya kikao kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika kwenye ofisi za CCM Lumumba, jijini Dar es Salaam.
 Wajumbe wa Kamati Kuu wakipitia makabrasha yenye ajenda za kikao muda mfupi kabla kikao hakijaanza.












SERIKALI YAWATAKA MADEREVA WA BRT KUZINGATIA MAFUNZO.

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki akizungumza katika uzinduzi wa semina ya mafunzo ya madereva wa mabasi yaendayo haraka (BRT) leo jijini Dar es salaam,  juu ya kuanza kwa kipindi cha mpito cha mradi huo Oktoba mwaka huu, Semina itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu jijini Dar es salaam.
 Waziri Mkuu, tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na mgeni rasmi  Hawa Ghasia akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya madereva wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) waliokaa mbele, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki na kulia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi.
 Waziri Mkuu, tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na mgeni rasmi  Hawa Ghasia aliyeshika mkasi akikata utepe kuzindua mafunzo madereva wa mabasi yaendayo haraka (BRT) jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa mafunzo yayo ya madereva.
 Baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi hapa nchini  wakiwa na abiria katika basi la mwendo wa haraka jijini Dar es Salaam leo.
 Mgeni rasmi na Waziri Mkuu, tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na mgeni rasmi  Hawa Ghasia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi katika mradi wa mafunzo ya madereva wa mabasi ya mwendo wa haraka (BRT) jijini Dar es Salaam leo.
Moja ya mabasi yaendayo mwendo wa haraka yakiwa barabarani katikati ya jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii. 

Na Mwandishi wetu.

SERIKALI imewataka madereva walioanza kupata mafunzo ya kuendesha mabasi yatakayotumika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) kuzingatia mafunzo hayo ya kihistoria hapa nchini.


Mafunzo hayo yaliyoanza jana ni moja ya matayarisho ya kuanza kwa mradi huo katika kipindi cha mpito mwezi Oktoba mwaka huu.


Akifungua rasmi mafunzo hayo jana jijini Dar es Salaam, Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Hawa Ghasia aliwataka madereva hao kuyapokea kwa bidii na umakini mkubwa.


“Mafunzo haya yatawapa fursa ya kuweza kufanya kazi kwenye miradi mingine ya BRT kwani vigezo na mtaala wake ni wa kimataifa,” alisema wakati wa maadhimisho hayo katika eneo la Ubungo.


Waziri Ghasia aliieleza kwamba mafunzo hayo ni ya kihistoria hapa nchini kwani kwa mara ya kwanza watapatikana madereva wenye leseni za kimataifa na kuwa mafunzo hayo yatahusu pia namna ya kuhudumia wateja.


“Madereva hawa watajengewa weledi na nidhamu katika kazi yao ambayo kwa sasa inalalamikiwa sana na wananchi wakilalamikiwa kwa utovu wa nidhamu na kutotii sheria za barabarani,” alisema.


Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadiki alisema kuzinduliwa kwa mafunzo hayo ni ushahidi wa dhamira ya serikali kutatua kero ya usafiri na msongamano wa magari jijini humo kupitia mradi wa BRT.


“Mradi huu wa aina yake nchini na barani Afrika utatoa fursa mbalimbali za uwekezaji na biashara kwa sekta binafsi ambayo ndio msingi wa maendeleo ya nchi,” alisema.


Mafunzo hayo kwa madereva wazalendo yanafanyika baada ya kushinda usaili ulio endeshwa na wataalamu kutoka chuo cha ufundi stadi na mafunzo (VETA).


Jumapili iliyopita kampuni ya watoa huduma wa ndani wa mradi huo, UDA-RT iliendesha semina ya mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusiana na huduma za kipindi cha mpito za mradi huo.


Mradi huo wa awamu ya kwanza unahusisha ujenzi wa kilometa 20.9 za barabara maalum kutoka Kimara hadi Kivukoni; barabara ya Msimbazi kutoka Faya hadi Kariakoo-Gerezani na sehemu ya barabara ya Kawawa kuanzia Magomeni hadi eneo la makutano ya Morocco.

WAZIRI MEMBE APOKEA NAKALA ZA HATI ZA BALOZI WA INDIA

$
0
0
 Hon. Bernard Kamilius Membe, Minister for Foreign Affairs and International Cooperation receives Copies of Letters of Credence of H.E. Ambassador Sandeep Arya, the new High Commissioner of India to the United Republic of Tanzania.The Ceremony took place today in the Minister's Office in Dar es Salaam.
Hon. Membe (right) exchanges views with H.E. Arya.
Officials of the Ministry of Foreign Affairs take notes during the meeting. They are, from left: Thobias Makoba, Mkumbwa Ally and Emmanuel Luhangisa.
conversation in progress
The Deputy High Commissioner of India, Mr. Robert Shetkintong (Second left) and Ms. Deepa Sehgal, Second Secretary in the Mission (left) take notes during the meeting.
H.E. Arya presents a gift to Hon. Membe.
The Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Hon. Bernard Kamilius Membe today called for the resumption of Air India flights to Tanzania to further strengthen relations between Dar es Salaam and New Delhi.

Speaking after receiving copies of his credentials, Hon. Membe told the new Indian High Commissioner to Tanzania, H.E. Sandeep Arya, that revival of the historical communication link would stimulate trade between the two countries and facilitate easy movement of people.

It would also make it easier for people seeking medical attention in the Asian country. "India absorbs most of Tanzanians referred for treatment abroad and resumption of Air India flights will greatly ease their transition," he explained.

The Minister also urged the new envoy to support ongoing efforts to have India's Apolo chain of hospitals establish a center in Tanzania. He said apart from helping Tanzanians, the center could also carter for Tanzania's neighbors.

Hon. Membe said apart from health, Tanzania and India enjoyed robust cooperation in education and security sectors. Tanzania was also host to a sizable Indian community, which was law-abiding, he said.

Ambassador Arya undertook to push for resumption of Air India flights and expansion of economic cooperation between the two countries.
Photo By Reuben Mchome.

KATIBU KIONGOZI OMBENI SEFUE AFUNGUA KIKAO KAZI CHA WADAU WA KUCHOCHEA MAENDELEO

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue  akifungua kikao kazi cha wadau cha kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa kujenga na kuimarisha Stadi za kazi katika Sekta zinazochochea ukuaji wa  uchumi Tanzania
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Consolata Mgimba akizungumza katika kikao kazi cha wadau cha kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa kujenga na kuimarisha Stadi za kazi katika Sekta zinazochochea ukuaji Uchumi Tanzania. 
Washiriki wa kikao kazi cha wadau cha kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa kujenga na kuimarisha Stadi za kazi katika Sekta zinazochochea ukuaji Uchumi Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue. 
 Baadhi ya washiriki katika kikao kazi cha wadau cha kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa kujenga na kuimarisha Stadi za kazi katika Sekta zinazochochea ukuaji Uchumi Tanzania.

SIMBACHAWENE AKABIDHI NYARAKA ZA UFADHILI KWA WATANZANIA 22 KUSOMA MAFUTA, GESI CHINA

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini. George Simbachawene, akisisitiza jambo kwa wanafunzi kabla ya kuwakabidhi Nyaraka za Ufadhili kwa ajili ya masomo yao nchini China. 

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, (Kulia) akizungumza na  waandishi wa habari, baadhi ya Watumishi wa Wizara na wanafunzi  waliopata ufadhili wa  masomo katika ngazi za  Shahada za Uzamivu (Phd) na  Uzamili (Masters), katika masuala ya mafuta na gesi nchini China.
 Baadhi ya wanafunzi 22 waliopata nafasi za masomo ya shahada za Uzamili na Shahada ya Uzamivu wakimsikiliza kwa kwa makini Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.
 Waziri akiwakabidhi nyaraka za kusafiria na zenye maelezo baadhi ya wanafunzi waliopata ufadhili wa masoma katika masuala ya mafuta na gesi nchini China.Katikakati ni Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, James Andilile.


  Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene akiwakabidhi wanafunzi 22 wa Kitanzania Nyaraka za Ufadhili wa kusoma masuala ya mafuta na gesi nchini China.

Na Clinton Ndyetabula.                                                                

Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene, amewakabidhi Nyaraka za  Ufadhili na kuwaaga wanafunzi 22 wa Kitanzania wanaokwenda  masomoni nchini China,  kusoma masuala ya mafuta na gesi katika ngazi za Shahada za Uzamivu (Phd) na  Uzamili (Masters).


Akizungumza katika hafla ya kukabidhi Nyaraka hizo, Makao Makuu ya Wizara, Jijini Dar es Salaam, leo, Simbachawene amewataka wanafunzi hao kutumia fursa hiyo kusoma kwa bidii ili hatimaye waweze  kusaidia Taifa katika kuendeleza sekta ndogo ya gesi ikiwemo kuanzisha vyanzo mbadala vya nishati ya umeme , kuongeza usimamizi ili kuendana na kasi ya ukuaji wa sekta hiyo, na kusaidia katika kuondoa changamoto zinazoikabili sekta hiyo.


“Kama mnavyoelewa Wizara yetu ni miongoni mwa Wizara zilizo katika Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) katika sekta ya Nishati. Mpango huu unategemea kutoa matokeo makubwa ya haraka, na hili kutekeleza ipasavyo tunahitaji  wataalamu wazalendo waliobobea katika fani za ,mafuta na gesi asilia” alisema Simbachawene.


“Ni matumaini yangu kuwa mtatumia vizuri fursa mliyopata, mtajifunza kwa bidii na  kuiwakilisha nchi yetu vizuri na  kuleta  teknolojia  zitakazosaidia kupata ufumbuzi au mapendekezo  ya namna ya kutatua changamoto zilizopo katika sekta hii”alieleza Simbachawene.


Aidha, Waziri alitumia nafasi hiyo kuishukuru  Serikali ya Jamuhuri ya Watu  wa China kwa kuwawezesha Watanzania  kusoma masuala ya mafuta na gesi  tangu mwaka 2013 na kuongeza kuwa , serikali hiyo  imeahidi kuendelea kutoa ufadhili  kwa watanzania katika ngazi za Shahada ya Uzamivu na Uzamili hadi  ifikapo mwaka 2019.


Aidha, Simbachawene ameeleza kuwa, Wizara ilipokea jumla ya maombi 187 na kati yao, waombaji 33 waliokidhi vigezo walichunjwa na Serikali ya Watu wa China na kupatikana washindi 22.


Clinton Ndyetabula ni  Mwanafunzi  ambaye yuko katika Mafunzo ya Vitendo, Wizara ya Nishati na Madini.

MJUMITA: TUCHAGUE VIONGOZI WATAKAO TETEA USIMAMIZI ENDELEVU WA MISITU

$
0
0
Mtaalam wa Misitu ambae pia anafanya kazi na  Mama Misitu kupitia Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF), Cassian Sanga akiendesha mjadala wa mada ya kwanza ya usimamizi  endelevu wa rasilimali za misitu nchini.
******************
Na Father Kidevu Blog.

 Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (MJUMITA)  leo imeanza mkutano wake Mkuu wa Siku mbili ambao kwanza umeanza na Warsha ya siku moja ya wadau wote wa mtandao huo. Wajum,be na wadau wa Mjumita kesho Agosti 18, watafanya mkutano mkuu ambapo mambo mbalimbali yatajadiliwa huku Kauli mbiu ya mwaka huu katika Mkutano huo unaofanyika mkoani Morogoro ikiwa ni 'TUCHAGUE VIONGOZI WATAKAO TETEA USIMAMIZI ENDELEVU WA MISITU".

Mtandao huo umeandaa rasimu maalum ambayo wanakusudia kuigawa kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuwa katika mikutano yao ya kampenzi itakayoanza Agosti 22 mwaka huu nchini kote wananchi wasisite kuwauliza wagombea hao juu ya mstakabali wa rasilimali za misitu zilizopo katika maeneo yao  kwa kuzingatia kuwa misitu ni uhai kwa maisha ya mwanadamu.
Elias Monga, Meneja mradi wa MJUMITA akifafanua jambo wakati wa warsha hiyo.
 Hii ndio kauli mbiu ya Mujumita katika Mkutano wake wa 15 mwaka huu unaofanyika mjini Morogoro.
 Mmoja wa Maafisa Misitu akizungumzia mikakati ya uhifadhi misitu na namna bajeti Kuu ya Serikali inavyochangia fedha katika uendelezaji na usimamizi wa Misitu nchini. Maafisa Misitu kutoka Wilaya Mbalimbali wamealikwa kushiriki katika Warsha hiyo ambapo wamesema licha ya Halmashauri zao kutenga fungu kwaajili ya uendelezaji Misitu lakini hakuna fedha zilizoingizwa licha ya baadhi ya Halmashaurti kupata mapato mengi yatokanayo na misitu.
Mjumbe wa Bodi ya MJUMITA Kanda ya Mashariki, kutoka Kijiji cha Soga Kibaha Mkoani Pwani, Subira Juma akizungumza juu ya umuhimu wa kuwachagua viongozi walio na uwezo wa kutetea usimamizi endelevu wa Mazingira.
Mtoa mada ya ushiriki wa Wananchi katika Uchaguzi Mkuu utakao fanyika Oktoba 25,2015 Pasience Mlowe kutoka Kituo cha Haki za Binadamu, akiwasilisha mada hiyo kwa washiriki wa warsha hiyo.
Mjumbe wa Bodi ya Mjumita Mstaafu, Juliana Mwenda akifafanua jambo kuhusiana na mkakati huo wa kuwashirikisha wagombea na kuwajengea uwezo wa ufahamu juu ya umuhimu wa utetezi wa rasilimali za misitu  
Baadhi ya washiriki wakifuatikia warsha hiyo leo ambapo mada mbalimbali zilitolewa ikiwa ni pamoja na ushiriki wa Wananchi katika uchaguzio Mkuu 2015, Uchaguzi Mkuu na changamoto za wakulima wadogo wadogo na Umuhimu wa Kiongozi bora katika kuhamasisha matumizi endelevu ya rasilimali za misitu. SOURCE: Father Kidevu Blog

AIRTEL YAZAWADIA WATEJA WAKE MARA TANO ZAIDI MUDA WA MAONGEZI

$
0
0
Mkurugenzi  wa kitengo cha Mawasiliano wa Airtel Tanzania
Beatrice Singano, akiongea  na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi
wa ofa ya "Kamata Tano Zaidi" inayowawezesha wateja wa Airtel kupata
mara tano ya muda wa maongezi.



-Wateja kupata Bonus ya mara tano zaidi kwa kununua muda wa maongezi 
au kifurushi cha yatosha kupitia Airtel Money
-Wateja wote  wa malipo ya awali kufaidika

Dar es Salaam, Jumatatu Agosti 17, 2015, Kampuni ya simu za mikononi
ya Airtel leo imezindua ofa kabambe kwa wateja wake wa Airtel Money
ijulikanayo kwa jina la "Kamata tano Zaidi" itakayowawezesha wateja wa
Airtel kupata muda wa maongezi mara 5 zaidi pindi watakaponunua muda
wa maongezi au yatosha zaidi kupitia Airtel Money.

Akizungumza katika uzinduzi, Ofisa Mkuu wa Biashara wa Airtel ,
Arindam Chakrabarty alisema, kuanzishwa kwa bonus ya mara 5 zaidi  kwa
kununua muda wa maongezi kupitia Airtel Money ni katika juhudi za
Airtel  kuendeleza dhamira na azma yao ya kuwajali na kuwazawadia
wateja .

 "Lengo letu ni kutoa huduma nafuu, zenye ubora, tija na
zinazokidhi mahitaji ya mawasiliano kwa wateja wetu nchini kote. Nina
imani "Kamata Tano Zaidi" italeta uhuru wa kuwawezesha wateja wetu
kuwasiliana na familia zao,marafiki na hasa kuongeza ufanisi katika
biashara zao popote pale walipo . "

"Chakrabarty aliongeza kwa kusema, " tunawaahidi wateja wetu kupitia
huduma ya Airtel Money tutaendelea kuwapa huduma za kisasa na
kuwazawadia mara 5 ya matumizi yao kama bonus ya muda wa maongezi
itakayowawezesha kupiga simu kwenda namba yoyote ya Airtel kwa siku
hiyo".

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa AirtelTanzania, Beatrice
Singano, alisema, "Bonus ya mara 5 zaidi itapatikana kwenye aina zote
za manunuzi ya  muda wa maongezi yatakayonunuliwa  kwenye mfumo wa
Airtel Money kwa kupiga *150*60# na kuchagua namba 2. 

Muda wa maongezi 
utakaonunuliwa utajumlisha muda wa maongezi wa kawaida pamoja na 
vifurushi vyote vya Yatosha au Yatosha Noma. Bonus  ya mara 5 zaidi ya 
"Kamata Tano Zaidi" inayopatikana kwa kununua kupitia Airtel Money 
itadumu kwa muda wa masaa 24 toka muda uliponunuliwa, ili kuwatimizia 
wateja wetu mahitaji yao ya  mawasiliano.

TAMASHA LA 'DEMOCRACY IN DAR' LAFUNIKA JIJI, WAKAZI WAHAMASIKA KUJITOKEZA KUPIGA KURA OKTOBA 25, 2015

$
0
0
Wananchi waliojitokeza katika tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015. 
Msanii Msagasumu akimwaga sumu kwa wakazi wa Mbagala na Vitongoji vyake waliojitokeza katika tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.
Shangwe kila kona....
Wasanii wa Bongo Movie nao waliunga mkono harakati za Mabadiliko...
Mhe. Joseph Mbilinyi akiwa na Msanii wa Bongo Moive, Anti Ezekiel.
Wazee wa Isanga Family kutoka Mbeya nao hawakuwa nyuma kutoa ujumbe wao katika tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 
2015.



Msanii AT kutokea Zanzibar akimwaga burudani katika tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Joseph Haule “Professa J” (kulia) akiteta jambo na wasanii wenzake Kala Jeremiah (kushoto) na Ney wa Mitego (Kati) katika tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.
Show love ya wasanii...
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Kala Jeremiah akiwapa wananchi ujumbe katika tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.
Msanii Ney wa Mitego akitoa burudani katika tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.
Msanii Roma Mkatoriki akitoa burudani...
Msanii wa Bongo Movie Shamsa Ford nae alikuwepo kusapoti mabadiliko na kuwasisitiza wananchi wajitokeze kupiga kura.
Msanii wa Kizazi kipya, ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu  akitoa burudani tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.
Msanii Profesa Jay, ambaye ni mtia nia wa Ubunge kwa jimbo la Mikumi akiburudisha katika tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.
Msanii wa Kizazi kipya,  Juma Nature mtoto wa Mbagala akitoa burudani tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.
Wasanii Nguri wa Muziki wa Kizazi Kipya, Joseph Haule a.k.a Profesa Jay na Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu wakishow love mara baada ya kumaliza kuwapa elimu na burudani wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake.
Marafiki wakifurahi mara baada ya kumalizika kwa tamasha hilo.

CCM YATANGAZA UTEUZI WA WAGOMBEA WA MAJIMBO 11 YALIYOKUWA YAMEBAKIA

$
0
0
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo mchana,katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam kuhusiana na uteuzi wa wa wagombea Ubunge wa majimbo 11 nchini yaliyokuwa yamebakia

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa leo Agosti 17, 2015 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete imefanya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo 11 nchini yaliyokuwa yamebakia.

Wagombea Ubunge walioteuliwa na majimbo yao kwenye mabano ni:-


1.    Ndugu Jerry Slaa                                  -        (Ukonga) Dar es Salaam
2.    Ndugu Edward Mwalongo                      -        (Njombe Kusini) Njombe
3.    Ndugu Venance Mwamoto                     -        (Kilolo) Iringa
4.    Ndugu Raphael Chegeni                        -        (Busega) Simiyu
5.    Ndugu Edwin Ngonyani                         -        (Namtumbo) Ruvuma
6.    Ndugu Mohamed Mchengerwa               -        (Rufiji) Pwani
7.    Ndugu Norman Sigara                           -        (Makete) Njombe
8.    Ndugu Martin Msuha                             -        (Mbinga Vijijini) Ruvuma
9.    Ndugu Joel Makanyanga Mwaka             -        (Chilonwa) Dodoma

Imetolewa na:-


Nape Moses Nnauye,    
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
17/08/2015


MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALLY IDD ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA NHC

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akimuelekeza jambo Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd, ambaye alitembelea makao makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa kujua utekelezaji wa miradi ya Shirika hilo, anayeshuhudia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akimuelekeza jambo Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd, ambaye alitembelea makao makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa kujua utekelezaji wa miradi ya Shirika hilo, anayeshuhudia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi wakiangalia baadhi ya mabango walipotembelea makao makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa kujua utekelezaji wa miradi ya Shirika hilo.
Bwana Mohamed Sharif, Mtanzania ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Dubai Sports City, akisalimiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi, huku Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd wakiwasikiliza.



Bwana Mohamed Sharif, Mtanzania ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Dubai Sports City akimueleza Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd namna ujenzi wa jiji la la kisasa la NHC litakaloanza kujengwa Usa River, Arusha.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi wakiangalia baadhi ya mabango walipotembelea makao makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa kujua utekelezaji wa miradi ya Shirika hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Tuntufye Mwambusi akimwelekeza jambo Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd huku Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi na Bw Mchechu wakishuhudia.

KONGAMANO LA KWANZA LA SERIKALI MTANDAO LAFUNGULIWA ARUSHA

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma,Bw.Hab Mkwizu akifungua Kongamano la kwanza la Serikali Mtandao jijini Arusha leo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha(RAS)Addoh Mapunda akizungumza kwenye ufunguzi mapema leo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao,Dk Jabiri Bakari akizungumza kwenye kongamano la siku tatu jijini Arusha ambalo limewakusanya maafisa zaidi ya 600 kujadili mikakati ya kuongeza matumizi ya mtandao katika shughuli za kila siku.


Wajumbe wakifatilia mada kwa makini.
Wajumbe kutoka taasisi mbalimbali za serikali wakiwa kwenye kongamano hilo.

Jipatie Tsh 2,000 hadi Tsh 40,000 kwa Video kupitia Kisakuzi.com

$
0
0
Kisakuzi.com ni mtandao unaoonesha video za matukio mbalimbali yanayotokea nchini. Mtandao huu, unanunua video na kumuwezesha mtazamaji kujiongezea kipato chake. Kutokana na ubora au tukio la video yako, unaweza kupata kuanzia shilingi 2,000 hadi 40,000 kwa video moja.kisakuzi-video-tanzania Tunapokea video ambazo unazimiliki wewe, umeipiga kwa kutumia simu yako au kamera yako. Nirahisi. Upatapo video kama hiyo bila kujali ufupi wake unaweza kuituma kwenda Je, wajua kwa kutumia simu ya mkononi au kompyuta yako unaweza kujiongezea hela za ziada. Kutokana na ubora au tukio la video yako, unaweza kupata kuanzia shilingi 2,000 hadi 40,000 kwa video moja. Tunapokea videos ambazo unazimiliki wewe, umeipiga kwa kutumia simu au kamera yako mwenyewe. Nirahisi upatapo video kama hiyo bila kujali ufupi wake unaweza kututumia kwa njia zifuatazo:
Whatsapp namba +255 714 227 955
E-mail: kisakuzivideo@gmail.com
au pia unaweza uka- upload mwenyewe kwenye tovuti yetu ya www.kisakuzi.comkisakuzi-video-tanzania2 Mara baada ya video yako inapokubalika na kutumika kwenye tovuti yetu ya www.kisakuzi.com tutakulipa fedha yako ndani ya masaa 24. Changamkia fursa kwa kutumia simu yako ya mkononi na uweze kujiongezea kipato chako katika maisha. Kisakuzi inakuwezesha wewe kuwa boss wako mwenyewe. Pale utakapoona kituko au habari yenye mvuto changamka na urekodi video na tutumie. Video za kuchekesha, vituko, kusikitisha, kufurahisha na za kampeni za uchaguzi zinapendwa zaidi na watazamaji wetu.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live


Latest Images