Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi lafanyika

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu akifungua mkutano wa  baraza la wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Dar es Salaam mapema leo.
Baadhi ya Wajumbe wa  Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi wakiwa katika mkutano wa baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Dar es Salaam mapema leo.
 

Watanzania walionufaika na Ufadhili wa Masomo nchini Japan waagwa

$
0
0
 Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Watanzania walionufaika na ufadhili wa masomo wa mpango wa ABE Initiative  wakati wa hafla fupi ya kuwaaga  iliyofanyika nyumbani kwake mapema jana
Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw. HAB Mkwizu (wa sita kutoka kulia) na Balozi wa Japan nchini Bw. Masaharu Yoshida (wa tano kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na watanzania wakionufaika na ufadhili wa mpango wa ABE Intiative baada ya hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika nyumbani kwa Balozi huyo mapema jana. Wengine ni Maofisa kutoka Utumishi na JICA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ateua wajumbe wa Bodi ya KADCO na RAHCO

Waziri Membe atembelea mabanda ya maonesho wakati wa Kongamano la Diaspora

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (kushoto) akipata maelezo kuhusu na matumizi ya Gesi Asilia, Miradi na manufaa yake kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Bw. James Mataragio (kulia) alipotembelea banda la shirika hilo wakati wa Kongamano la Watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) .
Waziri Membe akionyeshwa na Bw. Mataragio eneo bomba la gesi asilia lilipopita kwenye Mchoro wa Ramani ya Tanzania uliopo mbele yao.
Waziri Wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa katika picha ya pamoja na Bibi Dorcas Membe (kushoto), Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. James Mataragio (Kulia), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Diaspora, Bi Rosemary Jairo (wa pili kutoka kulia) na Watumishi kutoka katika shirika hilo.
Waziri Membe na Mkewe Mama Dorcas wakipata maelezo juu ya matumizi ya radio calls kutoka kwa  Bw. Sunji wa Kampuni ya Huawei nchini alipotembelea banda la Kampuni ya hiyo wakati wa Kongamano la Diaspora.
Waziri Membe (wa kwanza kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) nchini, Bi. Matilda Nyallu. Kushoto kwa Mhe. Membe ni Balozi Mulamula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Balozi Mulamula (katikati) akielezea jambo kwa Waziri Membe (kushoto).
Waziri Membe akisalimiana na mmoja wa  Washiriki wa Kongamano la Pili la Diaspora,Bw. William Malecela. Kulia ni Balozi Mulamula na katikati ni Bi. Suzani Mzee kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Bi. Rosemary Jairo (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Itifaki, Bw. James Bwana (wa pili kutoka kushoto)na Maafisa Mambo ya Nje Bw. Batholomeo Jungu ( kulia) na Bw. Amosi Tengu ( kushoto). Picha na Reginald Philip.

Bodi ya Mikopo kuendelea kutekeleza majukumu yake ili kuinua sekta ya elimu

Kongamano la Diaspora na Wajasiriamali likiendelea kwa siku ya pili jijini Dar es Salaam

$
0
0
Chukwu-Emeka Chikezie akiongoza moja ya mdahalo katika kongamano la Diaspora, Balozi wa Marekani nchini Mhe. Mark Childress kwa pamoja na Bw. Ali Mufuruki, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maafisa Watendaji Wakuu nchini, Bw. Richard Miles, Mwakilishi wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Marekani nchini na Dkt. Silencer Mapuranga, Mchumi kutoka ITC.
Balozi wa Marekani nchini, mhe. Childress akichangia mada kuhusu mabadiliko ya kiuchumi Tanzania wakati wa Kongamano la Diaspora.
Bw. Miles nae akichangia wakati wa mjadala kuhusu mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania na namna ya kuwashirikisha wafanyabiashara wadogo na wakati katika maendeleo ya nchi.
Balozi Mulamula akizungumza wakati wa mjadala huo .
Balozi wa China nchini, Mhe. Lu Youqing akiwasilisha mada kuhusu Mapinduzi ya Viwanda nchini na wajibu wa Diaspora katika ukuaji wa SME's
Balozi Lu akiwasilisha mada yake.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula kwa pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uswisi, Mhe. Modest Mero wakimsikiliza Balozi wa China nchini (hayupo pichani) wakati akiwasilisha mada
Washiriki wakifuatilia mada kutoka kwa Balozi wa China
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. Hemed Mgaza akiwa na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia, Dkt. Bernard Achiula wakisikiliza kwa makini uwasilishwaji wa mada wakati wa kongamano la Pili la Diaspora.
Mada zikitolewa
Maafisa Mambo ya Nje wakijadili jambo 
Timu ya Waandishi wa kumbukumbu za mkutano kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakinukuu taarifa mbalimbali wakati wa Kongamano la Diaspora ili kuweka kumbukumbu za tukio hilo sawasawa
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo akizungumza wakati wa kongamano hilo
Mada zikiendelea kutolewa wakati wa kongamano hilo 
Washiriki wa kongamano .Picha na Reginald Philip

MGOMBEA WA CHAMA CHA WAKULIMA ACHUKUA FOMU YA URAIS LEO

$
0
0
  Afisa Uchanguzi Mwandamizi Deogratus Nsawagwanko akimkabidhi fomu Mngombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupiti chama cha wakuliama (AFP), Omari Mohamed Sombi leo katika ofisi za Tume ya uchaguzi  jijini Dar es Salaam.
Afisa Uchanguzi Mwandamizi, Rafiki Kiravu akitoa  maelekezo kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia  Chama cha Wakuliama (AFP), Omari Mohamed Sombi kabla ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo leo  katika ofisi za Tume ya uchaguzi (NEC) jijini Dar es Salaam.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia  chama cha wakuliama (AFP), Omari Mohamed Sombi akionesha fomu ya kuwania nafasi hiyo hapa nchini  akiwonesha waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kuchukua fomu hiyo katika ofisi za tume ya uchanguzi (NEC) leo jijini Dar es Salaam.

(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.)

TAARIFA MUHIMU KUTOKA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI


IDADI YA WANAFUNZI WANONUFAIKA NA MIKOPO YAZIDI KUONGEZEKA

$
0
0
Na Jenikisa Ndile
Idadi ya wanafunzi  wanaopata  mikopo kutoka   Bodi ya Mikopo  kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imekuwa imeongezeka mwaka hadi mwaka na kusaidia kuongeza idadi ya watanzania wanaopata elimu ya juu.


Katika mwaka wa masomo wa 2005/2006 Bodi ya Mikopo ilitoa mikopo kwa  wanafunzi 42,729 iliyogharimu sh.  bilioni 56.1  na mwaka wa masomo wa 2014/2015 bodi ya mikopo ilitoa mikopo kwa wanafunzi 98,000 iliyogharimu shilingi bilioni 345.


Hayo yalisemawa leo na Kaimu Mkurugenzi  Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka bodi hiyo Cosmas Mwaisobwa wakati akizungumza na waandishi wa  habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (MAELEZO) kuhusu mafanikio ya  bodi hiyo katika kipindi hicho.


Alisema kwa kipindi hicho chote  wamekuwa na sheria mbalimbali ilioanzishwa kwa kuwapa jukumu la ukusanyaji wa madeni ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ambayo ilianza kutolewa tangu mwaka 1994/1995 kupitia iliyokuwa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia wakati huo Serikali haikukusanya madeni kutoka kwa wanufaika hadi pale bodi  ilipoanza kazi rasmi mwaka 2006/2007.


Aliongeza kuwa taasisi hiyo imekuwa  na mafanikio makubwa kulinganisha na hapo awali kwani kwa kipindi cha miaka kumi tumeongeza ufanisi katika matumizi ya teknolojia  ya habari na mawasiliano (TEHAMA)  kwa lengo la kuomba mikopo kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa uombaji wa mikopo  wa (OLAMS)

Aidha  bodi hiyo  imeendelea kukua kwa kasi kutokana na idadi ya watumishi kutoka tisa hadi kufikia watumishi 135 mwaka huu,ongezeko hilo limesaidia bodi kuwa na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake.


Bodi hiyo imewawezesha wateja wake  kupata huduma katika maeneo manne ambayo ni  Arusha, Mwanza, Dodoma, na Zanzibar ili kupata huduma za kibodi kwa ukaribu zaidi.


Mwaisongwa   aliwahakikishia wateja  hao  wataendelea kuwanufaisha waombaji na kutambua kuwa mikopo ya wanafunzi  wa elimu ya  juu ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya uchangiaji wa elimu ya juu na ni muhimu kurejesha mikopo ili kuwezesha mfuko huo  kuwa endelevu.


Taasisi hiyo iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria namba  9 ya mwaka 2004 na kuanza rasmi julai 2005 yenye lengo la kutoa mikopo kwa wanafunzi i wa elimu ya juu,utoaji na ukusanyaji wa mikopo ili kufanya mfuko wa mikopo kuwa endelevu.

ZIARA YA NAIBU WAZIRI MAJI AMOS MAKALLA MJINI GEITA

$
0
0
NAIBU waziri wa maji Amos Makalla leo ametembelea mradi  unaotekelezwa kwa ushirikiano wa serikali na mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) wa uboreshaji huduma ya maji kwa mji wa Geita, Mradi huu unagharimu fedha sh 10 bilioni ambao kukamilika kwake kutaongeza huduma ya upatikanaji maji kutoka asilimia 13 iliopo sasa hadi  kufikia asilimia 57.

Kwa mujibu wa tathmini ya kazi iliyofanyika mradi huu unatarajiwa kukamilika  mwishoni mwa mwezi august mwaka huu na naibu waziri wa maji ameagiza wahakikishe wananchi wanapata maji wiki ya kwanza mwezi ya mwezi septemba na si vinginevyo.
NAIBU waziri wa maji,Amos Makalla akikagua kazi za uchimbaji mitaro, ulazaji wa mabomba na ukaguzi wa tanki leo katika mji wa Geita
 NAIBU waziri wa maji Amos Makalla akitembele maeneo mbalimbali yaliyo na mabomba ya maji.

Mkuu wa mkoa wa Geita Fatma Mwasa akimpokea naibu waziri maji Amos Makalla.

SUGU, NATURE, PROFESSA J KUFANYA SHOO YA KUHAMASISHA MASHABIKI KUPIGA KURA OKTOBA 25, 2015

$
0
0
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Kala Jeremiah akiongea na waandishi wa habari ili kuwaelezea onyesho lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015. Pembeni ni Joseph Haule “Professa J”, Juma Kassim “Sir Nature” pamoja na Msagasumu.
 Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Joseph Haule “Professa J” akionyesha msisitizo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya onyesho lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015. 
 Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Juma Kassim “Sir Nature” akionyesha msisitizo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya onyesho lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25.
Tanzania Oyeeeee! Tanzania Oyeeee! ndiyo wasanii hawa walivyokuwa wakitia msisitizo.
 Baadhi ya wasanii watakaowasha moto Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.
Mwandishi wa habari wa Times Fm, akifanya mahojiano na Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Joseph Haule “Professa J”.

Wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya na baadhi ya nyota wa Bongo Movie watafanya onyesho la bure Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25.
Wasanii hao wataongozwa na Mbunge wa Mbeya mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi “Sugu” na nyota wengine kama Juma Kassim “Sir Nature”, Joseph Haule “Professa J” na Kara Jeremiah.
Wengine ni watakaopanda jukwaani siku kuanzia saa 8.00 mchana ni Msaga Sumu, Baba Haji na waigizaji nyota wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper na Auntie Ezekiel.
Akizungumza jijini jana, Professa J alisema kuwa sababu kubwa ya kufanya onyesho hilo ni kutoa elimu kwa mashabiki wao kuhusiana na zoezi la upigaji kura kuchagua viongozi bora wan chi hii wataodumu kwa miaka mitano.
Professa alisema kuwa wanataka kutoa mwamko kwa mashabiki wao kushiriki kwa wingi katika zoezi hilo ili kutumia demokrasia yao kumchagua kiongozi wanayemtaka.“Tumejiandaa vilivyo kutoa elimu, lengo ni kuwahamasisha mashabiki wetu kufanya kile wanachokiona kinafaa ili kutimiza malengo yao ya kikatiba,” alisema Professa J.Alisema kuwa mbali ya Dar es Salaam, onyesho hilo pia litafanyika katika mikoa mengine mbalimbali.
Akizungumza katika mkutano huo, Nature aliwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kupata elimu hiyo ambayo wasanii wameamua kuitoa.“Hii siyo kampeni ya kisiasa, sisi ni wasanii tumeamua kujitolea kufanya kazi ambayo wasanii wengi duniani wameifanya, lazima tutumie kazi yetu kutoa elimu kwa mashabiki ili wajue wajibu wao katika mambo mbali mbali pamoja na uchaguzi mkuu,” alisema Nature.

SUGU, NATURE, PROFESSA J KUFANYA SHOO YA KUHAMASISHA MASHABIKI KUPIGA KURA OKTOBA 25, 2015

$
0
0
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Kala Jeremiah akiongea na waandishi wa habari ili kuwaelezea onyesho lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015. Pembeni ni Joseph Haule “Professa J”, Juma Kassim “Sir Nature” pamoja na Msagasumu.
 Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Joseph Haule “Professa J” akionyesha msisitizo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya onyesho lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015. 
 Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Juma Kassim “Sir Nature” akionyesha msisitizo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya onyesho lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25.
Tanzania Oyeeeee! Tanzania Oyeeee! ndiyo wasanii hawa walivyokuwa wakitia msisitizo.
 Baadhi ya wasanii watakaowasha moto Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.
Mwandishi wa habari wa Times Fm, akifanya mahojiano na Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Joseph Haule “Professa J”.
Na Mwandishi Wetu.
Wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya na baadhi ya nyota wa Bongo Movie watafanya onyesho la bure Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25.
Wasanii hao wataongozwa na Mbunge wa Mbeya mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi “Sugu” na nyota wengine kama Juma Kassim “Sir Nature”, Joseph Haule “Professa J” na Kara Jeremiah.
Wengine ni watakaopanda jukwaani siku kuanzia saa 8.00 mchana ni Msaga Sumu, Baba Haji na waigizaji nyota wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper na Auntie Ezekiel.
Akizungumza jijini jana, Professa J alisema kuwa sababu kubwa ya kufanya onyesho hilo ni kutoa elimu kwa mashabiki wao kuhusiana na zoezi la upigaji kura kuchagua viongozi bora wan chi hii wataodumu kwa miaka mitano.
Professa alisema kuwa wanataka kutoa mwamko kwa mashabiki wao kushiriki kwa wingi katika zoezi hilo ili kutumia demokrasia yao kumchagua kiongozi wanayemtaka.
“Tumejiandaa vilivyo kutoa elimu, lengo ni kuwahamasisha mashabiki wetu kufanya kile wanachokiona kinafaa ili kutimiza malengo yao ya kikatiba,” alisema Professa J.
Alisema kuwa mbali ya Dar es Salaam, onyesho hilo pia litafanyika katika mikoa mengine mbalimbali.
Akizungumza katika mkutano huo, Nature aliwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kupata elimu hiyo ambayo wasanii wameamua kuitoa.
“Hii siyo kampeni ya kisiasa, sisi ni wasanii tumeamua kujitolea kufanya kazi ambayo wasanii wengi duniani wameifanya, lazima tutumie kazi yetu kutoa elimu kwa mashabiki ili wajue wajibu wao katika mambo mbali mbali pamoja na uchaguzi mkuu,” alisema Nature.

LAPF YAMWAGA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU YA MANISPAA YA KINONDONI

$
0
0
 Meneja Masoko Kanda ya Pwani, Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Manispaa ya Kinondoni. Vifaa vilivyotolewa na mfuko huo ni jezi seti 30, mipira 30 pamoja na viatu jozi 30. (Na Mpiga Picha Wetu)
Meneja Masoko Kanda ya Pwani, Yessaya Mwakifulefule (kushoto), akimkabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 5 mjumbe wa bodi ya timu ya Manispaa ya Kinondoni, Abbas Tarimba. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya timu hiyo, Yusuph Mwenda zilizotolewa na mfuko huo kwa ajili ya timu hiyo. 
Meneja Masoko Kanda ya Pwani, Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi jezi Mwenyekiti wa Bodi ya timu soka ya Kinondoni, Yusuph Mwenda zilizotolewa na mfuko huo kwa ajili ya timu hiyo. Wanaoshuhudia ni wajumbe wa Bodi ya timu hiyo, Abbas Tarimba (kulia) na Mtemi Ramadhani (wa pili kushoto).

AIRTEL FURSA YAANDAA SEMINA YA DARAJA LA MAFANIKIO KWA VIJANA MJINI MTWARA

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Salum Ally akifungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana.
 Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi akizungumza wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana.
 Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew Masatu akitoa mada kuhusu fursa mbalimbali zinazoweza kuwakwamua vijana kiuchumi, wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana.

 Mkufunzi kutoka Mpango wa Anzisha na Boresha Biashara yako (SIYB) ulio chini Shirika la Kazi Duniani (ILO), Fidelis Madaha akitoa mada wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Salum Ally (kulia), akijadiliana jambo na vijana walionufaika na fursa za Airtel (kutoka kushoto), Iddy Salum Chilumba, Godfrey Frank Manjavila na Prisca George Chilumba baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa pili kulia) na Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew Masatu.

SEKTA BINAFSI YASAINI HATI YA UADILIFU

$
0
0
Na Lilian Lundo, MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete  (Pichani)amezipongeza sekta binafsi kwa kukubali kusaini hati  ya ahadi ya uadilifu  katika harakati za mapambano dhidi ya rushwa na utovu wa nidhamu.

 Rais alisema hayo katika wakati akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa hati hizo zinazojumuisha sekta ya Umma na  Binafsi katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Katika hafla hiyo,  Mhe. Rais alisaini hati tatu ambazo ni Hati ya ahadi ya uadilifu ya Viongozi wa Umma, hati ya ahadi ya uadilifu ya Utumishi wa Umma na hati ya uadilifu ya Sekta Binafsi. 

“Ushiriki wa sekta binafsi katika hati hii utasaidia kuleta mabadiliko ya kuwa na mwenendo wa kimaadili ya mapambano dhidi ya rushwa” alisema Mhe. Kikwete.

Rais Kikwete alisema kuwa badala ya wananchi na sekta binafsi kulalamika pembeni ni vyema kuwasilisha malalamiko yao katika sehemu husika ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

 Aidha, Rais aliongeza kuwa baadhi ya sekta binafsi  zimekuwa zikiombwa na kutoa rushwa ili kupewa  upendeleo wa kupata  tenda serikalini, hivyo kwa kusaini hati   hiyo ya ahadi ya uadilifu kutaondoa mianya ya  upokeaji na utoaji rushwa katika sekta hiyo.

Hati ya ahadi ya uadilifu inakumbusha Makampuni, Viongozi na Watumishi wa Umma juu ya wajibu wao wa kuzingatia kanuni za maadili na mapambano dhidi ya rushwa nchini.

Wazo la kuwa na ahadi ya uadilifu liliibuliwa katika maabara ya Mpango wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambapo ilionekanakuwa rushwa bado ni tatizo katika uendeshaji wa shughuli za Umma na Binafsi hususani utoaji huduma kwa umma na biashara.

MTOTO WA CHINI YA MIEZI SITA HAWATAKIWI KUNYWESHWA MAZIWA YA NG'OMBE-TFNC

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
IMEELEZWA kuwa Mtoto chini ya mwezi hatakiwi kunywa maziwa yeyote isipokuwa ya mama yake, kutokana na maziwa ya ng’ombe  kuwa mazito na hayawezi kumsaidia mtoto katika kukua kwake.

Hayo ameyasema mtaalam wa lishe  wa Taasisi ya Chakula  lishe  nchini (TFNC),Neema Joshua wakati wa semina ya waandishi wa habari ya kuwajengea uwezo wa masuala ya Lishe,amesema maziwa ya ng’ombe wa yanatumika tu pale hakuna namna ya kuweza kupata maziwa mengine.

Amesema watoto chini ya miezi sita wanahitaji maziwa kwa mama na anatakiwa kupewa kila muda katika kuweza kumjenga mtoto kiakili.

Neema amesema katika suala la utapiamlo liko katika viwango vya juu ambapo mwaka 2010 ilikuwa na asilimia 42 hadi sasa imefikia asilimia 34.7 kwa takwimu za mwaka 2014.

Aidha amesema kuwa wale ambao wananyonyesha wakapata mimba akiwa ananyonyesha anaweza  kuuendelea kunyonyesha mtoto na bila kuathiri mimba nyingine.

Amesema wakati akinyonyesha huku ana mimba nyingine anatakiwa karibu na kujifungua miezi miwili aache kwa ajili ya kuupa mwili nguvu kwa mtoto atakayezaliwa na baada ya hapo anaendelea kunyonyesha wote wawili kwa kwanza akifikisha miwili ndipo anaweza kukoma.

CCM YAKANUSHA UVUMI WA HABARI YA MGOMBEA WAKE WA URAIS DKT JOHN MAGUFULI KUAHIDI KUGAWA KOMPYUTA KWA WALIMU NCHINI

$
0
0
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama hicho,Lumumba jijini Dar,kuhusiana na madai ya kauli inayodaiwa kutolewa na Mgombea wa Urais wa Chama hicho Dkt John Magufuli kuwa kupitia Ilani yake ya chama atatoa kompyuta kwa Walimu nchi nzima iwapo CCM itapita madarakani,habari ambazo Nape amezikunusha vikali na kusema hayo ni maneno ya uzusihi na kuwa Dkt Magufuli hajawahi kutamka maneno hayo popote pale.

 Nape Nnauye akionesha kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambayo imepitishwa jana Agosti 13,2015 katika Mkutano wa Chama hicho uliofanyika jana mjini Dodoma na inatarajiwa kuzinduliwa Agosti 23,mwaka huu katika uzinduzi wa Kampeni.Nape amefafanua kuwa kauli yoyote iliyotoka kwa chama hicho ikidaiwa imetoka katika Ilani  ya chama cha CCM,siyo ya kweli,kwani Ilani hiyo itazinduliwa wakati wa uzinduzi wa kampeni Agosti 23" alisema na Nape kwa msisitizo.
  Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo wa CCM mapema leo jijini Dar


NA BAKARI ISSA WA GLOBU YA JAMII.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekanusha uvumi ulioenea sehemu mbalimbali kuwa Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya Chama hicho,Dkt.John Pombe Magufuli amewaahidi Walimu kuwapa Kompyuta kama CCM itapita madarakani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama hicho,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye amesema kauli hiyo siyo ya kweli na haikutolewa na Mgombea huyo wa Urais,Dkt.Magufuli.

Hatahivyo,Nape amesema kauli hiyo imetolewa kwa nia mbaya kuonyesha Chama cha Mapinduzi kimeanza ziara ya kampeni mapema.

Amesema watu walioinukuu kauli hiyo wamesema imetoka katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho,Nape amesema " Ilani ya Uchaguzi ya CCM imetoka jana Agosti 13,2015 katika Mkutano wa Chama uliofanyika jana mjini Dodoma na inatarajiwa kuzinduliwa Agosti 23,mwaka huu katika uzinduzi wa Kampeni,hivyo kauli yoyote iliyotoka kwa chama hicho ikidaiwa imetoka katika Ilani yetu ya Uchaguzi,hiyo siyo ya kweli,kwani Ilani hiyo itazinduliwa wakati wa uzinduzi wa kampeni Agosti 23" alisema na Nape kwa msisitizo.

Kuhusu msimamo wa Chama cha Mapinduzi kwa wanachama wanaohama chama hicho,Nape amesema wanachama hao wanahama kwa mapenzi yao binafsi wengine wamehama kwa sababu ya kushindwa katika kura za maoni za chama.

RAIS KIKWETE AZINDUA HATI ZA AHADI YA UADILIFU KWA VIONGOZI, WATUMISHI WA UMMA NA SEKTA BINAFSI IKULU JIJINI DAR ES ES SALAAM LEO

$
0
0
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini Hati za Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi, Watumishi wa Umma na Sekta binafsi akishuhudiwa na viongozi wa taasisi na sekta hizo leo Agosti 14, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiikabidhi baada ya kuweka saini Hati za Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi, Watumishi wa Umma na Sekta binafsi akishuhudiwa na viongozi wa taasisi na sekta hizo leo Agosti 14, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam
 Hati za Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi, Watumishi wa Umma na Sekta binafsi zikioneshwa huku zikishuhudiwa na viongozi wa taasisi na sekta hizo leo Agosti 14, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam
 Mwenyekiti wa Business Roundtable Ali Mufuruki na Mkuu wa Brela wakisaini kwa niaba ya sekta binafsi na za umma Hati za Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi, Watumishi wa Umma na Sekta binafsi akishuhudiwa na viongozi wa taasisi na sekta hizo leo Agosti 14, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam. 

MGOMBEA URAIS WA UKAWA ALIVYOTAMBULISHWA JIJINI MBEYA JANA

$
0
0
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa akiwapumbia maelfu ya wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini  Mbeya jana Agosti 14, 2014. Mh. Lowassa na Mgombea mwenza wake Dkt. Juma Haji Duni, walikuwa jijini humo kwa ajili ya zoezi la kutafuta wadhamini wa Tume na kutambulishwa kwa wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu" akimueleza jambo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa, wakati akiwahutubia wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini  Mbeya jana Agosti 14, 2014.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dkt. Juma Haji Duni akiwahutubia maelfu ya wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini  Mbeya jana Agosti 14, 2014.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe akipunga mkono pamoja na wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini  Mbeya jana  Agosti 14, 2014.

KUONA PICHA ZAIDI

TaSUBa watambulisha rasmi Tamasha la 34 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo

$
0
0

DSC_0016Mwenyekiti wa Kamati kuu wa tamasha la 34 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Bw. John Mponda (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) katika ukumbi wa MAELEZO mapema leo 8.14.2015. Wengine ni Mwalimu Christa Kombo ambaye ni Mwenyekiti wa Maonyesho (kulia) na kushoto ni Bw. Frank Sika ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Majukwaa na Ufundi wa tamasha hilo ambalo linatarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu (Picha zote na Andrew Chale wa modewjiblog).

TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO
(TaSUBa)
945988442748510035_tangazo_html_mb1ecfee
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU .TAMASHA LA 34 LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO.

Tamasha la kimataifa la sanaa na utamaduni Bagamoyo liliasisiwa mwaka 1981 na Chuo cha Sanaa Bagamoyo ambacho kwa sasa ni Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo. Lengo kuu la Tamasha kwa wakati huo ilikuwa ni kuwapa nafasi wanafunzi wa chuo cha sanaa kuonyesha kwa vitendo yale waliojifunza kwa mwaka mzima kwa kuwashirikisha wakazi wa Bagamoyo, baada ya Tamasha hilo kufanikiwa uongozi wa chuo uliamua tamasha hilo lifanyike kila mwaka kwa kushirikisha Vikundi mbalimbali vya ndani na nje ya nchi ili kubadilishana Uzoefu na hivyo kujizolea umaarufu ndani na nje ya Tanzania.

Tamasha la kimataifa la sanaa na utamaduni Bagamoyo mwaka huu litafanyika kwa mara ya 34 kuanzia tarehe 21-27 Septemba katika kumbi na viunga vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ambao ndio wenyeji na waandaaji wa tamasha hilo kongwe Tanzania.

Tamasha la mwaka huu linabeba Kauli mbiu isemayoSANAA NA UTAMADUNI KATIKA UCHAGUZI HURU NA WA AMANI’Aidha kutakuwa na mada ndogondogo zitakazotolewa kupitia kongamano na warsha zitakazohusu Haki za binadamu, Rushwa na kupinga Mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).

Tamasha la mwaka huu litahusisha Ngoma za Asili, Maigizo, Sarakasi, Mazingaombwe, Muziki wa kisasa na asili, Sanaa za Ufundi na bidhaa mbalimbali.Hadi sasa jumla ya vikundi 48 kutoka ndani na nje ya Tanzania vimethibitisha kushiriki,ambapo vikundi 43 ni kutoka ndani ya Tanzania na vikundi 5 kutoka nchi za Kenya, Namibia, Afrika Kusini, Korea na Congo.

Hadi kufikia sasa hakuna mdhamini yoyote aliyejitokeza kudhamini Tamasha hili na hii imepelekea vikundi kujigharamia na TaSUBa kugharamia Uendeshaji,hivyo Taasisi inatoa wito kwa wadau mbalimbali wa sanaa,Makampuni,Taasisi za serikali na zisizo za serikali kujitokeza kudhamini tamasha hili muhimu kwa mustakabali wa sanaa na utamaduni wa Mtanzania.
Kwa yeyote anayehitaji kuchangia tamasha hili anaombwa awasiliane na Kamati ya maandalizi kwa mawasiliano hapo chini.

Mtendaji Mkuu, TaSUBa, S.L.P 32, BAGAMOYO, Tanzania, Simu.: 0255 023 2440149
Barua pepe: bagamoyofest@gmail.com, Tovuti: www.tasuba.ac.tz
Namba za Simu: +255(0) 754 310 425, +255(0) 787 542 242 na +255(0) 655 840 405
ASANTENI.
___________
JOHN MPONDA
M/KITI WA TAMASHA
14/8/2015
DSC_0029Mwenyekiti wa Kamati ya Maonyesho wa TaSUBa, Mwalimu Christa Kombo akifafanua jambo juu ya tamasha hilo kwa mwaka huu litakavyokuwa huku mambo mbalimbali yakiwa yamezingatiwa ikiwemo ubora wa vikundi na wasanii kutoka ndani na nje. Ambapo pia aliweza kufafanua juu ya maadili ya Sanaa katika tasnia ya burudani kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani). anayemfuatia ni Mwenyekiti Kamati Kuu ya Tamasha hilo la 34, Bw. John Mponda.
DSC_0040Mwenyekiti wa Kamati ya Majukwaa na Ufundi wa TaSUBa, Frank Sanga akielezea idadi ya vikundi vitakavyoshiriki na namna TaSUBa ilivyojipanga katika kuboresha utamaduni kupitia tamasha hilo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani)..
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images