Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 606 | 607 | (Page 608) | 609 | 610 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Shindano la kuibua na Kusaka Vipaji vya Kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambalo limedumu kwa takribani Miezi Minne hatimaye shindano hilo linakaribia kufika tamati mnamo tarehe 22 August 2015 huku Mshindi Mmoja Akiondoka Na Kitita Cha Shilingi Milioni Hamsini Za Kitanzania. 

  Na Washiriki waliofanikiwa kuingia Hatua ya Kumi bora watapata kifuta jasho huku wakiwa na mkataba mnono wa kufanya kazi na Kampuni namba moja ya Kutengeneza na Kusambaza filamu za Kitanzania ambao pia ndio waratibu wa Shindano Hilo la Tanzania Movie Talents (TMT) ya Proin Promotions Ltd.
  Shindano la TMT lilianza mapema mwezi wa Nne kwa kutafuta vipaji katika Kanda ya Ziwa ambapo usaili ulifanyika Mkoani Mwanza na kuhitimishwa Kanda ya Pwani Mkoani Dar Es Salaam kwa kupatikana Jumla ya Washindi 20 kutoka Kanda sita za Tanzania.
  Washindi wa kanda sita walipata fursa ya kuingia ndani ya mjengo wa TMT huku wakipatiwa mafunzo ya sanaa kutoka kwa Walimu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam huku mchujo ukiendelea na kupelekea kila wiki Washiriki wawili kuaga shindano, takribani wiki tano jumla ya washiriki 10 waliweza kuaga shindano hili ambalo limefikia hatua ya kuwapata washiriki 10 waliofanikiwa kuingia hatua ya Kumi bora huku wakingojea fainali itakayotoa mshindi wa kitita cha shilingi milioni hamsini za kitanzania
  Mpaka sasa washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya Kumi bora wanaendelea na kujifua Kwaajili ya fainali ambayo imebaki wiki moja tu kwa fainali hiyo kuliteka jiji la Dar huku hofu na presha zikiwapata Washiriki hao.
  Fainali ya TMT itafanyika Siku ya Jumamosi ya tarehe 22 August 2015 katika ukumbi wa makumbusho ya taifa karibu na Chuo cha IFM kwa viingilio vya shilingi Elfu 50 kwa VIP na Elfu 30 kwa viti vya kawaida.TMT 2015 inapigwa tafu na Precious Air, Cam gas, ITV na Radio One, Global Publishers, I-View Studio, Paisha na Hussein Pamba Kali

  0 0

  unnamed (85)

  Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati kuu ya CCM kilchofanyika katika ukumbi wa White house, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo.
  unnamed (86)
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo Agosti, 11, 2015 katika ukumbi wa Jengo la White House Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
  unnamed (87)
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo Agosti, 11, 2015 katika ukumbi wa Jengo la White House Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. 
  unnamed (88)
  Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Steven Wasira na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Adam Kimbisa wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma. 
  unnamed (89)
  Wajumbe wa Kamati Kuu, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Adam Kimbisa na Dk. Emmanuel Nchimbi, wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma.
  unnamed (90)
  Wajumbe wa Kamati Kuu, Dk. Maua Daftari na Samia Suluhu Hassan, wakibadilishana mawazo ukumbini, kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo mjini Dodoma. 
  unnamed (91)
  Mjumbe wa Kamati Kuu, Adam Kimbisa akiwasalimia wajumbe wenzake ukumbini kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma. Kutoka kulia ni Shamsi Vuai Nahodha, Zakia Meghji na Dk. Salim Ahmed Salim.
  unnamed (92)
  Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Zakiah Meghji na Dk. Asha-rRose Migiro wakibadilishana mawazo ukumbini kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCm leo mjini Dodoma.
  unnamed (93)
  Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Ameir Pandu Kificho akibadilishana mawazo na mjumbe mwenzake, Khadija Adood, kabla ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM kuanza leo mjini Dodoma.
  unnamed (94)
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akibadilishana mawazo na Mjumbe mwenzake wa Kamati Kuu, Zakiah Meghji kabla ya kikao cha Kamati Kuu kuanza leo mjini Dodoma. (Picha na Bashir Nkoromo)

  0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula akifungua Mkutano wa wadau wa mazingira unaohusu Miradi ya majaribio nchini wa Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) leo jijini Dar es salaam.
   Kiongozi wa wawezeshaji kutoka Asasi isiyo ya kiserikali ya Niras kutoka Finland inayosimamia Miradi ya majaribio nchini wa Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) Merja Makela akitoa mada wakati wa mkutano wa wadau wa mazingira kuhusu namna bora ya kuhifadhi mazingira na kuboresha usimamizi wa ardhi na kuongeza mapato kutoka kwenye misitu. Mkutano huo ambao umefanyika leo jijini Dar es salaam umeandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Norway.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula (kushoto) akifuatilia mada wakati wa mkutano wa wadau wa mazingira kuhusu namna bora ya kuhifadhi mazingira na kuboresha usimamizi wa ardhi na kuongeza mapato kutoka kwenye misitu. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu.
   Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa wadau wa mazingira unaohusu Miradi ya majaribio wa Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) nchini wakifuatilia mada wakati wa mkutano leo jijini Dar es salaam.
   Mhadhiri kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Pius Yanda akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Ubalozi wa Ufaransa mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa wadau wa mazingira leo jijini Dar es salaam.
   Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu (aliyevaa suti nyeusi) akiongea na baadhi ya waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa mkutano wa wadau wa mazingira leo jijini Dar es salaam.Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

  Na Jenikisa Ndile-MAELEZO
  Watanzania wameaswa kuzingatia namna bora ya kuhifadhi mazingira, upangaji wa matumizi bora ya ardhi na utekelezaji wa mipango ili kuleta tija na maendeleo endelevu nchini. 

  Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula leo jijini Dar es salaam alipokuwa akifungua Mkutano wa wadau wa mazingira unaohusu utekelezaji wa miradi ya majaribio ya Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) nchini.

  Bw. Sazi alisema kuwa mipango hiyo ya MKUHUMI inalengo la kuondoa umasikini kwa watanzania waishio vijijini ambao wapo karibu na hifadhi za misitu  inasimamiwa  na kutekelezwa  kwa kushirikiana na Serikari ya kijiji ili kuhakikisha mafanikio yanapatikana kwa kuzingatia utekelezaji na usimamizi wa sheria kupitia kamati za vijiji.

  Majaribio ya sera ya mazingira yamefadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Norway ili kuboresha na kushughulikia masuwala ya ardhi, misitu na kupunguza gesi joto kwa kuhimiza jamii kupanda miti kwa shughuli za maendeleo endelevu nchini.

  Mipango hiyo inatekelezwa katika wilaya za Sumbawanga, Lindi, Kilwa, Zanzibar, Pemba, Kigoma na Kondoa ambapo sera hiyo imewapa elimu ya kujenga utayari wa shughuli za MKUHUMA na kuwezesha ushiriki mpana wa wadau ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

  Kwa upande wake Kiongozi wa miradi ya majaribio ya MKUHUMI Merja Makela alisema kuwa taasisi yake imefanikiwa kutokana na kusimamia miradi hiyo ambayo imepokelewa na kutekelezwa kama ilivyopangwa katika maeneo husika nchini.

  Naye Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu alisema kuwa kwa tathmini iliyofanyika mwaka 2013, asilimia 55 ya ardhi ya Tanzania imefunukwa na misitu ambapo juhudi zinaendelea kufanyika kwa kuwaelimisha watanzania kuendelea kuitunza misitu hiyo kwa manufaa ya sasa na baadaye.


  0 0

  Katika kipindi cha JUKWAA LANGU wiki hii, tulijadili kuhusu kung'atuka uongozi kwa Prof Ibrahimu Lipumba na pia kukua kwa ufuasi kwa mgombea uRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Edward Lowassa.

  Pia, hotuba ya Zitto Kabwe huko Iringa, na mengine mengi
  Ungana na Dj Luke Joe (wa hapa), Rose Chitallah, Shamis Abdul (wa hapa) na Mubelwa Bandio (wa hapa) toka Kilimanjaro Studio, Beltsville Maryland na Jeff Msangi (msome hapa) kutoka Toronto Canada kujadili haya.

  Pia, kulikuwa na simu za wasikilizaji kadhaa
  KARIBU

  0 0


   Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC), Theodosia Muhulo Nshala, akizungumza na wanahabari katika kongamano hilo.
   Mwanaharakati wa masuala ya haki za binadamu, Gema Akilimali, akitoa mada kwenye kongamano la uhamashaji upigaji kura lililofanyika Dar es Salaam leo asubuhi. Kongamano hilo liloandaliwa mahususi kwa watu wa kundi maalumu liliandaliwa na Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC)
   Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo, Kuruthum Dindili (katikati), akizungumza na wanahabari katika kongamano hilo.
   Kongamano likiendelea.
  Kongamano likiendelea.
  Na Dotto Mwaibale

  WALEMAVU wenye mahitaji maalum wameonekana kusahaulika na serikali kwa kuwawezesha kufikia haki zao kama mchakato wa kupiga kura kutokana na kukosekana kwa miundombinu rafiki.

  Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam leo asubuhi  na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC), Theodosia Muhulo wakati wa mafunzo kwa wanawake walemavu wenye mahitaji maalum kuelekea uchaguzi.

  Lengo ikiwa ni ushiriki wa wanawake wenye mahitaji maalum katika kushiriki na kujitokeza  katika mchakato wa uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25,mwaka huu pamoja na kujenga na kukuza uelewa.

  "Kundi hili limesahaulika kwa serikali yetu hivyo kwa kuwapa semina hii kunawafanya wasionekane kutengwa na jamii ndiyo maana tumeona tuwaite na kuwaongezea uelewa wao katika kushiriki uchaguzi mkuu ikiwa ni pamoja na kushiriki,kuchagua na kuchaguliwa,"alisema

  Alisema serikali inapaswa kujua mahitaji ya walemavu kwenye michakato ya jamii,kwani hakuna sehemu maalum ya watu wa kundi hilo kwa kuwawekea miundombinu kama sehemu zenye ngazi ili kuweza kufika bila tatizo lolote.

  Muhulo alisema wanawake wanapaswa wajitokeze kupiga kura ili waweze kuchagua na kuchaguliwa kwa kumshagua rais, wabunge na diwani  ili waweze kuletewa maendeleo na mabadiliko  katika jamii zao na si kubaki nyuma.

  Kwa upande wake  Mbunge wa viti Maalum kupitia Umoja wa Wazazi nchini wa Chama cha Mapinduzi,Kuruthumu Dindili, alimpongeza rais Kikwete anayemaliza muda wake kwa kuwa ni mpenzi wa watu lakini walikosa wa kuwawakilisha bungeni kwani anaamini wangefaidika.

  "Kwa bunge lilikopita hatukuwa na mwakilishi bungeni wa kuweza kutusemea malalamiko yetu hasa kwa watu wenye ulemavu wa viungo  kwa maana wangekuwepo tungefaidika na mambo mengi sana, walikuwa wamekaa tu kimya bungeni wenzetu wananufaika wao...sisi walemavu hakuna tuanachokipata kupitia wao ndio maana tumeona tuingie na sisi kwenye mchakato,"alisema 

  Alisema wanapojitoa kugombea nafasi mbalimbali za kiuongozi wanaonekana ni kichekesho kwa wale wasiokuwa  walemavu na kuwabeza kwa kukosa fedha za kufanyia kampeni, aliitaka serikali kwa kutoa nafasi nyingi za wawakilishi walemavu  katika bunge lijalo ili kuwe na sauti nyingi za kuleta maendekeo ya kupata mahitaji ya kimsingi kuanzia ngazi za afya, elimu.


  Aidha semina hiyo ilihudhuliwa na Chama cha walemavu wa viungo(Chawata), Chama cha Walemavu wa Ngozi(Tas), Chama cha Wasioona (TLD), Chama cha Viziwi Wasioona(Tasodep), Chama cha wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi(Asbat) pamoja na Chama cha Afya na Akili(Tuspo).


  0 0

  Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Erasmus Rugarabamu kwa niaba ya Menejimenti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa akitoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya ambaye pia ni Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma kwa ushindi mnono alioupata katika kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kutafuta mgombea wa ubunge Jimbo la Mbinga Magharibi. Eng. Manyanya alishinda kwa kura 13,276 ambapo mshindi wa pili alikua na kura 3,466. Jumla ya wagombea walikua 10 ambapo tisa kati yao walikuwa ni wanaume.

   Awali Jimbo hilo lilikuwa nimeshikiliwa na hayati Capt. John Komba. Kwasasa imebaki hatua ya mwisho ya majina ya wagombea kupitishwa na Uongozi wa juu wa Chama kwa ajili ya kupeperusha bendera ya Chama  cha Mapinduzi majimboni katika uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu 2015. Uongozi na Watumishi wote wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa unamtakia kila la heri Eng. Manyanya katika safari yake hiyo na hatimae aweze kushinda katika Jimbo hilo. 

  Akitoa shukurani kwa niaba ya watumishi Katibu Tawala Msaidizi Kitengo cha Serikali za Mitaa Ndugu Albinus Mgonya alimpongeza Mkuu huyo wa Mkoa wa Rukwa kwa msukumo mkubwa wa maendeleo aliouweka katika kipindi cha uongozi wake hususani katika sekta ya elimu ambapo alianzisha Azimio la Kasense kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu mashuleni, Kuboresha afya ya mama wajawazito na watoto wachanga, usafi wa mazingira ambapo alianzisha kampeni ya Sumbawanga Ng'ara iliyozinduliwa na Mhe. Makamu wa Rais, Kampeni ya upandaji miti, kuboresha mazingira ya utalii katika maporomoko ya Mto Kalambo, kuboresha hali ya ulinzi na usalama katika Mkoa, Kuwaunganisha watumishi na viongozi katika kufanya kazi kwa pamoja n.k 
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa katika kikao kifupi cha kumpongeza baada ya kushinda katika kura za maoni Jimbo la Nyasa Magharibi kupitia CCM. Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Viongozi hao pamoja na watumishi kusimamia misingi aliyoiweka ya kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa, kufanya kazi kwa pamoja (team work) na kutekeleza majumu yao ya kila siku kwa ufanisi na ubunifu wa hali ya juu. Alisistiza kuwa maendeleo ya taifa la Tanzania hayataletwa tu kwa kutegemea vyama vya siasa bali kwa wananchi na wafanyakazi kutekeleza majukumu na wajibu wao ipasavyo kwa kuweka uzalendo mbele na kufanya kazi kwa bidii na uadilifu uliotukuka.   
   Katibu Tawala Msaidizi Kitengo cha Serikali za Mitaa Ndugu Albinus Mgonya akitoa Shukrani na Salamu za pongezi kwa niaba ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya kufuatia ushindi alioupata katika kura za maoni kutafuta mgombea wa CCM Jimbo la Mbinga Magharibi. Kwa sasa Mhe. Eng. Manyanya.

  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

  unnamed (95)
  Rais wa IBF Africa, Onesmo Ngowi (wa kwanza kulia) akizungumzia mapambano ya ngumi ya kulipwa yaliyopangwa kufanyika Novemba 28 jijini kwa ajili ya kutafuta fedha za uchangia watu wenye ulemavu wa ngozi(albino), wa pili kulia ni Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred na wa Rais wa TPBO Limited, Yasin “Ustadh” Abdallah.
  unnamed (96)
  Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred (wa pili kushoto) akiwa na viongozi wa juu wa ngumi za kulipwa nchini, Onesmo Ngowi (Rais wa IBF Africa, wa kwanza kushoto), Emmanuel Mlundwa (rais wa PST) na Yasin Abdallah (Rais wa TPBO-Limited) mara baada ya kutangaza mapambano ya ngumi ya kulipwa yaliyopangwa kufanyika Novemba 28 jijini kwa ajili ya kutafuta fedha kwa ajili ya kuchangia watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).
  ……………………………

  Shirikisho la Ngumi za kulipwa la Afrika (IBF Africa) kwa kushirikiana na Taasisi ya Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred Foundation (BAF) na kampuni ya Kango wameandaa mapambano ya ngumi ya kimataifa kwa kushirikisha mabondia nyota duniani.Mapmbano hayo yamepangwa kufanyika Novemba 28 kwenye ukumbi wa Mlimani City na lengo lake kubwa ni kutafuta fedha za kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).
   
  Rais wa IBF Africa, Onesmo Ngowi alisema kuwa siku hiyo imepewa jina la  “knock out albinos killers” (piga wanaua albino) ambapo bondia kutoka Denmark, Lolenga Mock atapigana na bondia nyota wa Zambia, Chioctha Chimwemwe  katika pambano la uzito wa super middle la  IBF continental Africa super.
   
  Pambano hilo limepangwa kuwa la raundi 12 na litafuatiwa na pambano lingine la kulipiza kisasi kati ya bondia kutoka Afrika Kusini, Phillip Ndou atakayepambana na Mtanzania, Ramadhan Shauri kuwania ubingwa wa IBF-Continental Africa welterweight  ambalo pia litakuwa la raundi 12.
   
  Bondia nyota wa Tanzania, Cosmas Cheka naye atapanda ulingoni kupambana na Gottlieb Ndokosho wa Namibia kuwania ubingwa wa IBF continental Africa super-feather.Mabondia wa Kenya, Geoffrey Munika na James Onyango nao wataingia ulingoni kupambana na mabondia kutoka china na Iran ambao watajulikana baadaye.
   
  Pia kutakuwa na pambano mengine ambayo yatawakutanisha mabondia wanawake, Lulu Kayage dhidi ya bondia atakayetangazwa baadaye kuwania ubingwa wa IBF Africa flyweight.“Lengo ni kutafuta fedha za kuchangia kununua vifaa maalum kwa albino na mpaka sasa maandalizi yanaenda vizuri, hii ni tukio kubwa sana kwa ngumi za kulipwa hapa nchini,” alisema Ngowi.
   
  Alisema kuwa wameamua kushirikiana na Brigitte kutokana na kutambua juhudi zake za kutetea albino baada ya kuwajengea bweni eneo la Buhangija, Shinyanga na taasisi yake kwa kushirikiana na Junior Achievements (JA) wanatoa elimu ya ujasiriamali kwa jamii hiyo.
   
  “Brigitte akiwa mwenye mashindano ya urembo ya dunia, 2012, aliweka rekodi ya kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya ‘urembo wenye malengo maalum” au Beuty with purpose”, alipeleka kazi yake ya ujenzi wa bweni la albino mkoani shinyanga, imetupa faraja sana na kuamua kumuunga mkono katika vita hiyo,” alisema.
   
  Brigitte alishukuru kuungwa mkono na kuomba wadhamini kujitokeza kusaidia shughuli hiyo ambayo baada ya ngumi, pia kutakuwa na mbio za marathon mkoani Kilimanjaro zenye lengo hilo hilo.“Tumeandaa mbio za Marathon mkoani Kilimanjaro wiki moja baada ya ngumi, mbali yam bio hizo, pia kutakuwa na zoezi la kupanda mlima Kilimanjaro, lengo ni kutafuta fedha na vile vile kutangaza utalii wetu, naomba makampuni yajitokeze,” alisema Brigitte.

  0 0

  kw1

  Afisa Habari wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Aristides Kwizela (Kushoto) akifuatilia burudani zilizokuwa zikitolewa na watoto wanaondaliwa na Baraza hilo kupitia programu ya ‘Sanaa kwa Watoto’ wakati wakitumbuiza kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii. Watoto hao wanatoka shule ya Msingi ya Msimbazi iliyoko Ilala jijini Dar es Salaam. Katikati ni Msanii wa filamu Honeymoon Mohamed na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na Stadi za wasanii Bi. Vick Temu.
  kw3
  Wasanii kutoka Kundi la Ngoma za Asili na Maigizo la Jivunie lenye makazi yake eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam wakionesha ufundi wao katika kuchenza ngoma za asili kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii.
  kw4
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA linalofanyika makao makuu ya Baraza hilo Ilala Sharif Shamba kwa mwezi mara mbili siku za Jumatatu.

  ………………………………………………………………….
  Na Mwandishi Wetu
  Wasanii nchini wametakiwa kurejesha kwa jamii sehemu ya faida wanayoipata kupitia kazi zao za Sanaa kwa kuwakumbuka watoto wenye mahitaji maalum ili kujijengea mtandao wa kudumu wa masoko, uhalali na taswira nzuri kwa jamii.

  Wito huo umetolewa mapema wiki hii na mtengeneza filamu wa Tanzania mwenye makazi yake nchini Marekani Bi. Honeymoon Mohamed wakati akiwasilisha mada kuhusu Filamu za Kitanzania na Masoko kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa inayoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

  “Wasanii wanaitegemea jamii kama chanzo cha mapato yao hivyo ni lazima wajenge utamaduni wa kurejesha kile kidogo wanachokivuna kutoka kwa jamii kupitia kusaidia watu wenye uhitaji maalum” alisema Honeymoon ambaye filamu yake ya Daddy’s Wedding imeshinda tuzo kwenye tamasha la kimataifa la filamu la Zanzibar (ZIFF) lililomalizika hivi karibuni eneo la Ngome Kongwe, Zanzibar.

  Aliongeza kwamba watoto wenye uhitaji maalum wanapata faraja na kuhisi kupendwa na jamii pale wanapotembelewa mara kwa mara na watu mbalimbali wenye umaarufu na nafasi kubwa katika jamii hivyo wasanii wetu hawana budi kuwa sehemu ya kujenga faraja hii kwa watoto hawa.

  Kwa mujibu wa Honeymoon wasanii wa Tanzania wako nyuma katika kuikumbuka jamii hususani kutembelea makazi ya watoto wenye uhitaji maalumu na kuchangia huduma mbalimbali zinazokuwa zinahitajika.“Watoto wenye utindio wa ubongo wako wengi, kuna wale wenye ulemavu wa ngozi na wengine wanaishi wakiwa yatima kwenye vituo mbalimbali lakini wasanii wetu wamekuwa wazito kuwakumbuka. Wasanii hawana budi kuyakumbuka makundi haya maana wako kwa ajili ya jamii” alisisitiza.

  Awali kabla ya uwasilishaji wa mada hiyo, watoto wanaoandaliwa kupitia programu ya BASATA ya ‘Sanaa kwa Watoto’ kutoka Shule ya Msingi wa Msimbazi iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam walitoa burudani mbalimbali za Sanaa wakisaidiana na Kikundi cha Sanaa cha Jivunie chenye maskani yake neo la Mbagala Manispaa ya Temeke.

  0 0


  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kuongezeka kidogo kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Mei 2015 leo jijini Dar es salaam.Mfumuko wa Bei wa  bei kwa mwezi Julai ,2015 umefikia asilimia  6.4   kutoka asilimia 6.1 iliyokuwepo Juni 2015.


  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.

  Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Julai 2015 na kusema kuwa umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.4  kutoka asilimia 6.1 iliyokuwepo mwezi Juni 2015.

  Hii inamaanisha kuwa  kasi ya upandaji wa bei ya  bidhaa na huduma kwa mwezi Julai 2015 imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya upandaji bei ya bidhaa na huduma  iliyokuwepo mwezi Juni mwaka 2015.  

  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam amesema kuongezeka huko kumesababishwa na kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula katika maeneo mbalimbali nchini.

  Amezitaja bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko huo kutokana na upandaji wa bei katika masoko kwa mwezi Julai 2015 kuwa  ni mchele kwa asilimia 27.9,mahindi asilimia 2.3, unga wa muhogo asilimia 9.2, nyama asilimia 4.5, samaki 12.2, na maharage asilimia 5.9.

  Kuhusu Fahirisi za Bei ambacho ni kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya binafsi hapa Tanzania, Kwesigabo  amesema zimeongezeka hadi kufikia 158.78  kutoka 158:12 za mwezi Juni.

  Amesema kuongezeka kwa fahirisi za bei kumechangiwa na ongezeko la bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula zikiwemo gesi ya kupikia kwa asilimia 3.7, mafuta ya dizeli 5.9, mafuta ya Petroli ailimia 4.9,  unga wa mahindi asilimia 2.5, ulezi asilimia 2.9, samaki asilimia 4.8, viazi vitamu asilimia 2.6 na ndizi za kupika asilimia 3.4.

  Kwesigabo amesema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za mlaji kwa mwezi Julai , 2015 umefikia shilingi 62 na senti 98 ikilinganishwa na kiasi cha shilingi 63 na senti 24  za mwezi Juni 2015. 

  “Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile kwa mlaji kwa mwezi Julai ,2015 na  umepungua  hii ina maana kuwa sasa mtu anahitaji kuongeza ziada ya shilingi 38 ili aweze kununua bidhaa na huduma sawa na zile alizokuwa na uwezo wa kuzinunua katika mwezi Juni"

  Kwa upande wa mfumuko wa Bei kwa nchi za Afrika Mashariki kwa mwezi Julai, 2015 Bw.Kwesigabo amesema kuwa una mwelekeo unaofanana , Kenya umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 6.62 na kutoka 7.03 mwezi Juni 2015 huku Uganda ikiwa na mfumuko wa Bei wa  asilimia 5.4  kutoka asilimia 4.9  za mwezi Juni, 2015.

  0 0

  Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.

  Waandishi wa habari wa kanda ya nyanda za juu Kusini wamepatiwa mafunzo ya nanma ya kuandika na kutangaza habari za uchaguzi ili waweze kutumia taaluma yao iifikie jamii

  Semina hiyo inaendeshwa kwa pamoja na shirika la utangazaji la Uingereza BBC na baraza la habari Tanzania MTC(Picha na Edwin Moshi wa Eddy Blog)

   Mwanahabari Gordon Kalulunga akichangia mada
   Mwanahabari Michael Katona akiwasilisha kazi waliyopewa kwa niaba ya kundi lake
   Mafunzo kwa vitendo yakiendelea
  Waandishi wa habari wa kanda ya nyanda za juu Kusini wamepatiwa mafunzo ya nanma ya kuandika na kutangaza habari za uchaguzi ili waweze kutumia taaluma yao iifikie jamii

  Semina hiyo inaendeshwa kwa pamoja na shirika la utangazaji la Uingereza BBC na baraza la habari Tanzania MTC(Picha na Edwin Moshi wa Eddy Blog)

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA NISHATI NA MADINI
  OFISI YA MADINI KANDA YA MASHARIKI   

   TANGAZO KWA UMMA
  KUIBIWA KWA STAKABADHI ZA SERIKALI
  (EXCHEQUER RECEIPT VOUCHER)

  Ofisi ya Madini, Kanda ya Mashariki Dar es Salaam inautangazia Umma kwamba, usiku wa Jumapili ya kuamkia tarehe 03-08-2015 wezi walivunja Ofisi ya Madini Kanda ya Mashariki iliyopo Upanga, Dar es Salaam na kuiba vitu mbalimbali vya Ofisi vikiwemo vitabu vya Stakabadhi za malipo ya Serikali.

  Katika tukio hilo, stakabadhi namba ERV 6361601-6361800, na ERV 6361201, 6361202, 6361203, 6361204 ziliibwa.

  Aidha, vitabu vipya vinane (8) vyenye Stakabadhi namba 6360201-6360400, 6360401-6360600, 6360601-6360800, 6360801-6361000, 6361001-6361200, 6361205-6361400, 6361401-6361600 na 6361801-6362000 viliibwa, kuharibiwa na kutupwa nje ya ofisi ya madini.

  Kwa taarifa hii, tunautangazia Umma kwamba stakabadhi zote zilizoibwa na kuharibiwa hazitumiki na malipo yote yatakayofanyika kupitia stakabadhi tajwa hapo juu yatakuwa ni batili.

  Tunaomba yeyote mwenye taarifa sahihi zitakazoweza kusaidia kukamatwa kwa wezi husika kutoa taarifa katika Ofisi ya Madini au kituo chochote cha Polisi kilichopo karibu.

  Imetolewa na:
  Kamishna Msaidizi wa Madini
  Kanda ya Mashariki – Dar es Salaam

  0 0
 • 08/11/15--22:30: MABADILIKO KUTOKA EDDY BLOG
 • Napenda kuufahamisha umma na wapenda habari nchini kuwa blog yangu ya EDDY BLOG kwa hivi sasa inapatikana kupitia link hii http://edwinmoshi.blogspot.com/ badala ya ile ya zamani. Napenda kuwaomba radhi kwa usumbufu mlioupata ila nawaomba tuungane pamoja kwa kubonyeza hapa http://edwinmoshi.blogspot.com/ ili uzipate habari motomoto kama ilivyokuwa mwanzoni

  Imetolewa na Ewin Moshi
  Mwandishi mkuu
  EDDY BLOG

  0 0


  0 0

   Meneja bidhaa wa Benki ya Barclays,Valence Lutegavya akizungumza wakati wa uzinduzi wa kadi ya ATM ya dola za kimarekani katika mkutano wa uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Bwana Kumaran Pather.
     Meneja bidhaa wa Benki ya Barclays,Valence Lutegavya akionyesha kadi ya ATM ya Dola za Kimarekani katikati ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays Tanzania, Bwana Kumaran Pather na wamwisho ni
  Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Vimal Kumar.
   Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Bwana Kumaran Pather, akitoa msisitizo juu ya faida za ATM kadi ya dola za kimarekani kwa wateja watakao zitumia kazi hizo wakati wa manunuzi ya bidhaa mbalimbali haoa nchini na kushoto ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Vimal Kumar.
  Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Vimal Kumar akifafanua juu ya matumizi ya ATM kadi za dola za kimarekani katika matumizi ya kawaida katika kununua bidhaa mbalimbali kwenye maduka yanayotumia kadi za ATM hapa nchini, katika mkutano wa uzinduzi kadi ya ATM ya dola, uliofanyika makao makuu ya benki jijini Dar es Salaam leo.
   
  BENKI ya Barclays hapa nchini imezindua kadi ya ATM ya dola hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays Tanzania, Bwana Kumaran Pather wakati akizungumza wakati wa uzinduzi, uliofanyika makao makuu ya benki jijini Dar es Salaam leo.

    alisema “wateja wa Barclays wenye akaunti ya Dola za kimarekani wataweza kutumia kadi hizo mpya wakiwa ndani na nje ya Tanzania kupitia huduma za VISA.”

  Kadi hizi mpya zimewekwa kwenye mfumo mpya wa teknohama ambao unawapa wateja usalama zaidi wanapofanya huduma zote za kibenki. Mteja atapata fedha za ndani atakapoitumia kadi hiyo akiwa nchini. Miamala yote ya nje ya nchi itafanyika kwa dola za Kimarekani tu.

  Pia amezitaja faida za Kadi za dola kutoka Benki ya Barclays hapa nchini,  Inarahisisha malipo ya bidhaa na huduma madukani, hotelini, vituo vya mafuta n.k. nchini na dunia nzima,Utakupo toa hela nje ya nchi kupitia ATM utapata noti za dola za kimarekani,
  Inakupa amani ya akili baada ya kukamilisha muamala kwa mtandao na pia inakupa nafasi ya kupata punguzo la bei mtandaoni unapotumia kadi ya matumizi ya Barclays.

  Aliendelea kusema “Barclays inawasaidia wateja kunufaika kwa kulenga kuwapatia uzoefu rahisi na kuwasikiliza mahitaji yao.” Barclays inazingatia kila wakati kuwapa wateja wake huduma timilifu za hali ya juu na kwa uzoefu wa hali ya juu.

  0 0

   Mkurungenzi Mtendaji wa kituo cha msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) Theosia Nshala akuzungumza kwenye mdahalo na wanawake wenye ulemavu (TAMAWA) juu ya taratibu mbarimbari za Uchanguzi hususani hari za mwanamke katika Uchanguzi hapa nchini katika mdahalo uliofanyika  Jijini Dar es Salaam.
   Mwanaharakati na Mtaaramu wa Jinsia na Haki za Binadam Gema Akilimali, akuzungumza kwenye mdahalo na wanawake wenye ulemavu(TAMAWA) juu Kuwajengea wanawake ufahamu na ujasiri wa kushiriki katika Uchanguzi kama wagombea,wapiga kura wafutiliaji na waangalizi katika mdahalo uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya   wanawake wenye ulemavu (TAMAWA) wakiwa katika mkutano leo Jijini Dar es Salaam.
   Picha na Emmanuel Massaka.

  0 0

   Bendi ya jeshi la polisi ikiongoza Maandamano ya siku ya vijana Duniani ,yaliyofanyika Agost 12 kila mwaka yaliyoanzia katika Shule ya Sekondari Jangwani na kuishia katika  viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
   Naibu Katibu  Mkuu wa Wizara ya habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo,Profesa Gabriel Ole Sante akizungumza  katika maadhimisho ya Siku ya Viajna Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,jijini Dar es Salaam.
   Vijana wakionyesha ujuzi wao katika mchezo wa sarakasi katika siku vijana duniani yaliyofanyika katika viwanja vya manzai mmoja leo jijini Dar es Salaam.

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Profesa Gabriel Ole Sante akipata maelekezo kutoka Afisa Maendeleo wa Vijana wa Wizara hiyo,Dora Meena katika maadhimisho ya Siku vijana Duniani yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo,Profesa Gabriel Ole Sante akipata maelezo katika banda la Asasi ya Vijana wa Umoja wa Matiafa (YUNA), katika maadhimisho ya Siku Vijana Duniani yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Vijana walioshiriki Maadhimisho ya Siku Vijana Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

  0 0

  Na Mwandishi wetu-MAELEZO-Dar es salaam

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(Pichani) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa michezo ya Wizara, Idara zinazojitegemea ,Wakala wa Serikali  na Ofisi za wakuu wa Mikoa (SHIMIWI) itakayoanza Jumamosi ijayo(15.8.2015) mjini Morogoro.

  Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Katibu Mkuu SHIMIWI Moshi Makuka, mashindano ya mwaka huu yatafanyika kwa wiki mbili.

  Amesema kuwa siku ya ufunguzi kutakuwa na michezo ya mpira wa miguu kati ya Elimu na Hazina kwa wanaume , mpira wa pete utazikutanisha timu ya Afya na Mambo ya Ndani.

  Makuka ameongeza kuwa siku hiyo pia kutakuwepo mchezo wa kuvuta kamba kati ya Wakala wa Jiolojia Tanzania na Mambo ya Nje  kwa wanaume na kamba kwa wananwake kati ya Ikulu na Bunge.

  Amezitaja timu zilizothibitisha kushiriki kuwa ni Ikulu, Utumishi, Waziri Mkuu, Afya, Ardhi, Elimu, Hazina, Kilimo,TAMISEMI, Mifugo, Maji, Afika mashariki, Maliasili, Mambo ya Nje, Mambo ya Ndani, Ulinzi, Nishati, Maendeleo ya Jamii, Viwanda, Uchukuzi, Ujenzi na Tume ya Mipango.

  Timu nyingine ni Mahakama, Tume ya Utumishi wa Umma, Bunge, Tume ya Kurekebisha Sheria, Tume ya Mahakama, Ukaguzi, tume ya ushirika , Wakala wa Jiolojia Tanzania, Wakala wa Ukaguzi wa Madini, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula, Mkoa wa Lindi, Katavi, Mwanza, Kagera, Rukwa, Dar es salaam, Mtwara, Iringa, Geita, Kigoma, Manyara , Arusha, Mara, na Tanga

  0 0

  Balozi wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing (katikati), akihutubia wakati akizindua kampeni ya kupambana na ujangili viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam leo asubuhi. Kampeni hiyo imeanzishwa na watu wa China kwa ajili ya kuunga jitihada za watanzania katika mapambano hayo ya kuwalinda wanyama dhidi ya ujangili hasa tembo.
  Balozi wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing (kulia), akimpa zawadi ya mpira kwa niaba ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kinondoni, Faudhia Eddy katika uzinduzi huo. Balozi huyo alitoa zawadi ya mipira kwa baadhi ya shule za Manispaa ya Kinondoni.
  Balozi wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing (kulia), akimpa zawadi ya mpira, Mwalimu Flora Lukali kutoka Shule ya Mount Pleasant kwa ajili ya shule hiyo.
  Balozi wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing akionyesha umahiri wa kuchezea mpira katika uzinduzi huo kabla ya kutoa zawadi ya mipira kwa baadhi ya shule za Manispaa ya Kinondoni.
  Wanafunzi wakiwa na vipeperushi vya bendera ya nchi ya china wakati wa uzinduzi huo.
  Wasanii wa kundi la makhirikhiri wakitoa burudani katika 
  uzinduzi huo.
  Wanafunzi wakiwa kwenye uzinduzi huo.
  Wimbo wa taifa ukiimbwa.
  Wanahabari wakichukua taarifa za uzinduzi huo.
  Wanafunzi ndani ya uzinduzi huo. 

  0 0

   Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

  Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
  Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :


  Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

  Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:
  i.                    Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema
  ii.                  Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )
  iii.                Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )
  iv.                 Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini
  v.                   Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema
  vi.                 Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.
  Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.
  Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

  JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
  Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.
  Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :
  i.                    Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

  ii.                  Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

  Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :
  1.      Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume
  2.      Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :
  i.                    Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.
  ii.                  Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana.  Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.
  3.      Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.
  Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :
  i.                    Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.
  ii.                  Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame
  iii.                Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.
  iv.                 Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume


  DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
  Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:
  i.                    Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
  ii.                  Uume kurudi  ndani
  iii.                Uume  kusimama  ukiwa  legelege
  iv.                 Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

  TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
  Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :
  i.                    Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili
  ii.                  Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani
  iii.                Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege
  iv.                 Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

  BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU
  (Tsh. 80,000/=)
  MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  TABATA   MAKOKA    karibu  na SHULE  YA  SEKONDARI YA  MT. ANNUARITE.
  Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.
  Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI
  Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.
  Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

  MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.
  Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee  kwenye  blogu  yetu :

  0 0

  Tanzania inaingia katika kipindi kigumu na cha muhimu sana kwenye historia yake. Ni kipindi ambacho kitasaidia kuamua muelekeo wa nchi kwa miaka mitano inayokuja. Mara nyingi ifikapo wakati wa uchaguzi kuna mambo mengi hubadilika. Biashara huanza kuwa ngumu kutokana na hofu miongoni mwa watu. Pia, ushiriki wa watu kwenye kampeni hufanya muda mwingi kutumika huko hivyo kutoa muda mchache kwenye shughuli kama kazi.
  Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, mwaka huu tutashuhudia mabadiliko makubwa sana, mabadiliko haya siyo tu aina ya watu wanaoshiriki kwenye kugombea nafasi mbalimbali, bali pia mfumo utakaotumika kwenye kampeni hadi upigaji kura. Mwaka huu tutashuhudia matumizi ya Tehama kwa kiwango kikubwa sana kwenye kampeni za uchaguzi na hata utangazaji na uchungaji wa matokeo ya chaguzi.Tutegemee kupata updates za matokeo ya kura toka kila kituo ndani ya dakika punde tuu wanapomaliza kuhesabu.

  Kwa chama chochote kinachotaka kufikia watu na hatimaye kushinda, ni ngumu kufanikisha hilo bila kutumia Tehama. kwa maneno mengine, Tehama ndiyo itakayoongoza uchaguzi wa mwaka huu. Tumeona mfano wa Obama mwaka 2008. Akiongozwa na kauli mbiu yake ya pamoja tunaweza (Yes we can) na matumizi ya mitandao, Obama aliweza kufikisha ujumbe kwa vijana wengi kama ilivyo sasa kwa Tanzania, na hatimaye kushinda uchaguzi wa kihistoria.

   Kwa Tanzania, tumeona jinsi gani vijana walivyo na chachu ya mabadiliko, tumeona ni jinsi gani vijana walivyokuwa wanakesha kwenye vituo vya kujiandikisha ili kupata kadi zao za kupigia kura. Ni vijana hawa ambao wamelala kwenye matumizi ya Teknolojia. Wao wanalala na Instagram, wanaamka na Twitter mchana wanashinda Whatsapp huki jioni wakitembelea Facebook. Iwe kwa kutumia komputa mpakato (Laptop) au kwa simu za mikononi. Haijalishi kijana huyu yupo kule kwetu Nyamwimbe au Mbezi Beach Goig, wote wanafikiwa na taarifa kwa uharaka wake.

  Mitandao ya kijamii, kama Facebook, Twitter, Whatsapp, Instagram nk itachukua nafasi ya kipekee kabisa mwaka huu. Nakumbuka, Uchaguzi wa mwaka 2010 mitandao kama Jamii Forums ilijizolea umaarufu sana, ila mwaka huu tutegemee mambo tofauti sana.
  Hebu tuangalie sababu zitakazosukuma matumizi ya Tehama kwa mazingira ya Tanzania.

  Tabia za Watanzania.

  Moja ya sifa kuu ya Watanzania, ni kutopenda kusoma makala ndefu,na sifa hii inaenda nchi nyingi Africa, ndiyo sababu kuna masihala wazungu husema, ukitaka kumnyima kitu muafrica, weka kwenye kitabu. Wengi hupenda picha na maelezo mache yaliyo rahisishwa (Summary). Kwenye kitabu chake cha How to Win Campaigns, Communications for Change, Chris Rose alisema, "Moja ya nguzo muhimu ya kushinda kampeni ni kuwajua unaowafanyia kampeni". 

  Kuwajua haimaanishi kuwajua kwa majina, la hasha, bali kitabia na kimazoea. Hii ni kwa sababu utahitaji kuwafikishia ujumbe utakaoeleweka na wao wawe tayari kuupokea halafu ndiyo waukubali.Na kama unataka kuwafikia Watanzania,  basi achana na makala ndefu, hawatosoma.


  Mitandao Jamii na Blogu nyingi zimejikita kwenye nadharia hii, Picha na ujumbe mfupi, na jinsi watu wanavyotazama au kuipenda (like) makala yako, ndivyo inavyozidi kuonekana. Kwe wengi wetu, hiki si kipindi tena cha kuongea logic, ni kipindi cha emmotion hivyo wagombea wanatakiwa kucheza na emottion za watu zenye kujenga.


  Uwingi wa Muda

  Ukweli usiopingika ni kuwa, wengi wa Watanzania wana muda mwingi wa kujadili mambo mbalimbali,(wengi hawana kazi, hasa vijana) hii inapelekea wengi wao kutokuwa busy kwenye shughuli wanazozifanya. Hivyo muda mwingi wamekuwa online wakitafuta habari, na kama vijana wanavyosema, uchaguzi ndiyo habari ya mujini.Na wao wameshaipata.
  Hivyo, kama wewe ni mmoja wa wagombea basi utahitaji kujikita sana kushibisha njaa hii ya habari wanaoitafuta kwa aina tofautitofauti.

  Uwezo wa kupambanua

  Kwenye ulimwengu wa Tehama, kuna lundo la taarifa, taarifa hizi zipo za kujenga na kubomoa. Leo hii tumeshuhudia kwenye mitandao ya Whatsapp taarifa jinsi zinavyozunguka tena kwa kasi ya ajabu. Na nyingi ya taarifa hizi si za kweli au hazijengi. Leo hii mtu anaweza kuamua kutunga taarifa na ndani ya dakika tano imeshasambaa nchi nzima bila kujali uhalali au umuhimu wake.

  Wengi wetu tumekuwa tukisambaza bila hata kumaliza kusoma au kutafakari. Hivyo, kwenye kipindi hiki cha ushaguzi tutegemee sana mafuriko ya habari zisizo na tija.

  Nimewahi kuongea na Kada mmoja wa chama fulani, akaniambia, Chama chetu kina wio mpana hadi vijijini sehemu ambazo wengi wa washindani wetu hawawezi kufika. Sikuongea mengi, nilimuambia kitu kimoja tu, ila Teknolojia imefika, hata kwa uchache wake. Na watu wa huko, wengi hawana hata huo muda wa kupoteza kupambanua, wao huamini wanachokipokea. Na moja ya nyenzo kuu kwenye kampeni ni kuwa midomoni au akilini mwa watu.Wengi hupiga kura kwa mkumbo.

  Tumeshaanza kuona matumizi makubwa ya Teknolojia,lakini, kampeni ni kama biashara, lazima uwe na uwezo wa kupima maendeleo na faida ya uwekezaji (ROI) ili kuepuka kuja kushangazwa siku ya mwisho. Kuna njia bora na thabiti za kutumia na kuongoza Teknolojia ili ije kuwa na manufaa makubwa kwenye kampeni yako. Tukutane kwenye makala ya pili nitakapoongelea matumizi bora ya Teknolojia kwenye Kampeni.
  Makala zaidi za IT Kibiashara, tembelea https://www.dudumizi.com/blog.html  
  Mkata Nyoni (MSc, IT Economics, ITIL)

older | 1 | .... | 606 | 607 | (Page 608) | 609 | 610 | .... | 1898 | newer