Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 605 | 606 | (Page 607) | 608 | 609 | .... | 1897 | newer

  0 0

  1
  Richard Rugimbana Mwenyekiti wa Chama cha Wanafunzi waliosoma katika shule ya (St Joseph Cathedral High School Alumn )kuanzia mwaka 1940 - 2014 akizungumza katika mkutano wao uliofanyika shuleni hapo jana wakati wa kikao chao kikilchojadili mipango mbalimbali ikiwamo kuanzisha mfuko wa Elimu utakaosaidia kuwasomesha wanafunzi wa shule hiyo wenye mahitaji maalum ikiwemo kuwapatia Scholaship katika vyuo mbalimbali.
  Chama hicho kinatarajiwa kuzinduliwa rasmi Septemba 26 kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam , Katika kufanikisha uzinduzi huo kadi maalum zimeandaliwa ambazo zitauzwa shilingi 50.000 kwa mtu mmoja , 100.000 kwa watu wawili na meza za watu kumi kila moja zitakazouzwa kwa kiasi cha shilingi 1.000.000. Katika Picha kushoto ni Katibu wa Chama hicho Bwa.Collins Rutenge.
  2
  Richard Rugimbana Mwenyekiti wa Chama cha Wanafunzi waliosoma katika shule ya (St Joseph Cathedral High School Alumn )kuanzia mwaka 1940 - 2014 akisisitiza jambo katika mkutano huo uliofanyika jana.
  3
  Mariam Ziaror mmoja wa wanachama hao akizungumza jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika jana (St Joseph Cathedral High School .
  4
  Chief Edward Makwaia akichangia jambo katika mkutano huo
  5
  Bw. Hassan Ndumbaro mmoja wa wanachama hao akizungumza jambo katika mkutano huo kutoka kushoto ni Leaticia Mukarasa, Mariam Zialr na Chief Edward Makwaia.
  6
  Dr. Zubeida Tumbo kutoka taasisi ya Room To Read Tanzania ambaye pia alisoma katika shule hiyo akichangia mawazo yake wakati wa mkutano huo.
  7
  Baadhi ya wanachama wakiwa katika mkutano huo
  9
  Mkutano ukiendelea.
  10
  Mkuu wa shule ya (St Joseph Cathedral High School )Sr. Theodeta Faustin akizungumza na wanachama hao wakati wa mkutano huo.
  

  0 0

    Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akikata utepe kuashiria kumkabidhi kijana Jonathan Tarimo (wa pili kulia), msaada wa Zizi jipya na Ng’ombe wawili wa maziwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha jana. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Baba mzazi wa kijana huyo, Clemence Tarimo na Mratibu wa Masoko wa Airtel wilaya ya Monduli, Polas Emmanuel. 
  1) Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akifafanua jambo kwa kijana Jonathan Tarimo (wa pili kulia), kabla ya kumkabidhi msaada wa Zizi jipya na Ng’ombe wawili wa maziwa, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha jana. Wanaoshuhudia ni Baba mzazi wa kijana huyo, Clemence Tarimo (kushoto) na maafisa wa Airtel wa Mikoa ya Arusha na Manyara.
   Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akimpongeza Jonathan Tarimo (wa pili kulia), baada ya kumkabidhi msaada wa Zizi jipya na Ng’ombe wawili wa maziwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha jana. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Baba mzazi wa kijana huyo, Clemence Tarimo, Mratibu wa Masoko wa Airtel wilaya ya Monduli, Polas Emmanuel na Meneja wa Airtel mkoa wa Manyara, Peter Kimaro.
  Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa tatu kushoto), akikabidhi Ng’ombe wa maziwa kwa kijana Jonathan Tarimo, ikiwa ni sehemu ya msaada wa Ng’ombe wawili wa maziwa na zizi jipya, alivyomkabidhi kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha jana. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Baba mzazi wa kijana huyo, Clemence Tarimo na Mratibu wa Masoko wa Airtel wilaya ya Monduli, Polas Emmanuel.
  Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto), akikabidhi Ng’ombe wa maziwa kwa kijana Jonathan Tarimo, ikiwa ni sehemu ya msaada wa Ng’ombe wawili wa maziwa na zizi jipya, alivyomkabidhi kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha jana. 

  AIRTEL Tanzania kwa kupitia mpango wake wa Airtel
  Fursa “Tunakuwezesha” imemkabidhi kijana Jonathan Clement mkazi    Migungani kata ya Mto wa Mbu wilaya ya Monduli mkoani Arusha ng’ombe wawili, banda la kisasa pamoja na mafunzo ya biashara   ambayo itamsaidia kuinua biashara yake ya ufugaji na kumuongezea kipato chake.
  Jonathan kijana mwenye umri wa miaka 21 na elimu ya kidato cha nne  amekabidhiwa mtaji huo ambapo awali alikuwa na ngomb’e wawili na banda  lililochoka  na  alikuwa na changamoto ya elimu ya ufugaji na madawa ya mifugo.
  Jonathan ameishukuru kampuni ya simu za mikononi ya Airtel kwa kumpatia msaada huo amesema  “biashara yangu ya ufugaji sasa itapiga hatua. Naamini miaka michache ijayo nitakuwa na mifugo mingi sana na soko langu la maziwa litakuwa kwa kasi. Na vile vile itaniwezesha kuinua familia na biashara yangu kwa ujumla”.

  “Hii ni bahati ya peke kwangu kutoka Airtel, kwani ni vijana wengi sana wanatamani kupata hivi nilivyovipata lakini hawakupata bahati hii. Nawahimiza vijana wengine wasikate tamaa na  wajitokeze kwa wingi kwani Airtel Fursa ipo kutuwezesha vijana”.

  Akizungumza baada ya makabidhiano, Meneja huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi, alisema “mpango huu ulibuniwa ili kuwawezesha vijana na kuwakwamua kiuchumi. Jonathan amepitia changamoto nyingi kufikia hapa alipo alianza na ngombe wa kukopeshwa kutoka kwa mjomba wake kwa makubaliano kwamba atakapopata ndama wa kwanza atakuwa wa kwake. Lakini leo hii tumemuwezesha kuwa na jumla ya ng’ombe watatu kwenye zizi lake”.
  “Airtel kupitia mradi wake wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” imempatia msaada huu Jonathan baada yakuridhishwa na hatua ya ufugaji pamoja na kuonyesha nia yakuwa mfugaji bora hapa nchini” alisema.

  Bayumi aliwataka vijana wachangamkie fursa hiyo na kuongeza kuwa mpango huu unawalenga vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 ambao watapokea misaada ya vifaa au thamani ili kuweza kutimiza malengo yao..
  “Program hii inahusisha vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini alisema.
  Ili kijana kushiriki au kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma
  ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:-
  Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. Pia wanaweza kutuma maombi yao
  kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com<mailto:airtelfursa@tz.airtel.com>. ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara. Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com

  0 0

  OFISI ya Makamu wa Rais inasikitika kuwepo kwa taarifa ambazo zimesambaaa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ataongea na vyombo vya habari kuhusu msimamo wake ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi.
    Tunaomba kuueleza umma wa Watanzania kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais hajapanga tukio lo lote la kukutana na waandishi wa habari na wala hana mpango wa kuzungumzia msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.
  Tunatumia nafasi hii kuwataka wale wote wenye tabia ya kuvumisha taarifa zisizo sahihi waache kufanya hivyo kwa kuwa ni kosa kisheria. Tunawaomba waandishi wa habari kufuata taratibu za kazi na kutafuta taarifa sahihi kwenye vyombo vinavyotambulika.
  Boniphace Makene
  Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais.

  0 0

  PRESS RELEASE” TAREHE 10.08.2015.

  ·         MTU MMOJA AUAWA KWA KUKATWA PANGA SHINGONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA WILAYANI KYELA.

  ·         MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KUTOKANA NA TUHUMA ZA WIZI.


  ·         MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MBOZI.

  ·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU KWA MAKOSA MBALIMBALI.
   
  KATIKA TUKIO LA KWANZA:
  MTU MMOJA MKAZI WA NSANSA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DAVID MWAKIPESILE (60) ALIUAWA KWA KUKATWA PANGA KICHWANI NA SHINGONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. 

  TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 09.08.2015 MAJIRA YA SAA 21:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA NSANSA, KATA YA NGONGA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.

  INADAIWA KUWA MHANGA ALIVAMIWA NA WATU HAO WAKATI ANARUDI NYUMBANI AKITOKEA KWENYE MATEMBEZI KISHA KUMJERUHI. MAREHEMU ALIFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA KWA MATIBABU.  

  CHANZO CHA MAUAJI HAYO INASADIKIWA KUWA NI IMANI ZA KISHIRIKINA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA AJILI YA MAZISHI. UPELELEZI UNAENDELEA PAMOJA NA MSAKO WA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILO.

  KATIKA TUKIO LA PILI:
  MTU MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA, JINSI YA KIUME, MIAKA KATI YA 20-27, ALIUAWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BAADA YA KUKAMATWA AKIWA AMEIBA PILIPIKI MC 811 AFJ AINA YA T-BETTER MALI YA THOBIUS ALLANUS YENYE THAMANI YA TSHS 1,800,000/=.

  TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 09.08.2015 MAJIRA YA SAA 19:45 USIKU HUKO ENEO LA UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.

   MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. UPELELEZI UNAENDELEA.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA. 

  AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO LA KWANZA KUZITOA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.


  KATIKA TUKIO LA TATU:
  MPANDA BAISKELI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MICHAEL KIBONA (55) MKAZI WA MLOWO ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LISILOFAHAMIKA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.

  AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 09.08.2015 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO KATIKA ENEO LA MLOWO, KATA YA MLOWO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA AJALI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. UPELELEZI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUMTAFUTA DEREVA ALIYEHUSIKA KATIKA TUKIO HILI.

  TAARIFA ZA MISAKO:
  WATU WATATU WAKAZI WA KIJIJI CHA MASIANO WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. SHAMLA MAHUNDOLA (20) 2. YUNGE LUHUNZA (25) NA WANGU D/O MKUWA (21) WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI UZITO WA KILO 09.
  WATUHUMIWA WALIKAMATWA KATIKA MSAKO MKALI ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 09.08.2015 MAJIRA YA SAA 08:30 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MASIANO, KATA YA CHOKAA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

  Imesainiwa na:
  [AHMED Z.MSANGI – SACP]
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
  

  0 0

   Kwaya Maalum ya Jangwani kutoka Shinyanga ikitumbuiza wakati wa Sherehe za Makambi ya Mtaa wa Kanisa la Waadventista Wasabato Manzes.
   Muhubiri Mkuu wa Sherehe za Makambi mtaa wa Manzese Mch. Idelphonce Tirumanywa akihutubia watu waliohudhuria sherehe hizo. Ujumbe Mkuu "Mtizame Yesu Ukaishi".
    Kikosi maalum cha vijana wadogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Manzese (Wavumbuzi) wakitembea kwa mwendo wa gwaride kuelekea jukwaani kwa ajili ya program maalum kwenye sherehe za makambi.
   Watoto wa Mtaa wa Manzese wakionesha program maalum jukwaani kwenye sherehe maalum za makambi ya Manzese.
   Baaadhi ya washiriki wa sherehe za makambi wakisikiliza kwa makini vipindi vinavyoendelea kwenye Makambi ya Mtaa wa Manzese.
    Mch. Amos Lutebekela (Kushoto) akimkabidhi zawadi ya shukrani mkufunzi wa vijana Bw. Chris Buhatwa wakati wa kuhitimisha sherehe za Makambi mtaa wa Manzese
   

   Baadhi ya wabatizwa wakipokelewa na wachungaji na wazee wakanisa wakati wa kuhitimisha sherehe za makambi.
   Mch. Idelphonce Tirumanywa akinyoosha mkono juu kuomba  wakati wa kufanya huduma maalum ya ubatizo kwa watu walioamua kujiunga na kanisa la waadventista wasabato ulimwenguni.

   Kwaya ya Angaza ikimwimbia Mungu siku ya kuhitimisha sherehe za makambi Manzese
   Picha zote na Sarah Reuben.

  Sherehe za Makambi kwa mwaka 2015 katika Mtaa wa Manzese zimemalizika kwa kishindo cha kubatiza waumini ishirini na saba (27) ambao wameamua kumpokea Yesu kwa kujiunga na kanisa la Waadventista Wasabato Manzese.

  Akizungumza na waumini wa kanisa hilo wakati wa kuhitimisha sherehe hizo mwishoni mwa wiki, Mchungaji Idelphonce Tirumanywa amesisitiza kuwa kanisa kuendelea kuwalea vyema waumini wapya waliojiunga na kanisa hilo. Mch. Tirumanywa pia ameendelea kuwaasa waumini wote wa kanisa la waadventista wasabato kuwa mfano bora kwa jamii kwa kuonesha matendo mema yatakayo warudisha watoto wa Mungu waliopotea nyumbani.

  “Ni wakati wakurudi nyumbani, dunia ipo kwenye hatari kubwa, tena kubwa sana. Tunapoishukuru serikali yetu kwa uhuru wa kuabudu, waadventista wasabato wote amkeni muumtangaze Mungu ili watoto wa Mungu waache dhambi na kurudi nyumbani”, alisistiza Mch. Tirumanywa.

  Sherehe za makambi ya mtaa wa Manzese yalihudumiwa na kwaya maalum kutoka Sauti ya Jangwani Shinyanga wakishirikiana na kwaya tatu (3) zinazounda mtaa huo yaani Angaza, Mbiu na Sauti ya Nyikani zote kutoka Dar es Salaam.
  

  0 0

   UKOSEFU  ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani. 

   Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

  Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

  Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
  Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :
  http://neemaherbalist.blogspot.com/2015/07/uhusiano-kati-ya-damu-na-tatizo-la.html


  Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.
  Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:
  i.                    Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema
  ii.                  Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )
  iii.                Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )
  iv.                 Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini
  v.                   Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema
  vi.                 Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.
  Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

  Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

  JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
  Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.
  Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. 

  Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :
  i.                    Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.
  ii.                  Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA)

  Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :
  1.      Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume
  2.      Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :
  i.                    Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.
  ii.                  Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana.  Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.
  3.      Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.
  Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :
  i.                    Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.
  ii.                  Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame
  iii.                Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.
  iv.                 Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

  DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
  Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:
  i.                    Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
  ii.                  Uume kurudi  ndani
  iii.                Uume  kusimama  ukiwa  legelege
  iv.                 Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

  TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
  Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :
  i.                    Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili
  ii.                  Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani
  iii.                Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege
  iv.                 Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

  BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU
  (Tsh. 80,000/=)
  MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  TABATA   MAKOKA    karibu  na SHULE  YA  SEKONDARI YA  MT. ANNUARITE.
  Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.

  Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI
  Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.
  Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

  MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.
  Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee  kwenye  blogu  yetu :
  www.neemaherbalist.blogspot.com

  0 0

  


  Ziito Kabwe  akiwa na mume  wa Chiku Abwao na Chiku Abwao  na kada wa ACT wazalendo.
  Zitto kabwe  akiwa na wapambanaji

  Zitto kabwe  akiwahutubia  wananchi wa jimbo la Iringa mjini

  Chiku  Abwao  akiwahutubia wananchi wa jimbo la Iringa mjini

  Mgombea udiwani wa kata ya Mvinjeni Abuu Majeck akimpongeza mgombea  ubunge jimbo la Iri nga mjini Chiku Abwao

  KIONGOZI  wa  chama  cha ACT Wazalendo amempongeza mbunge wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe (CCM)  kuwa ni miongoni mwa wabunge wa mfano kutokana na utendaji kazi  wake mkubwa badala ya maneno bila  vitendo.


  Huku aliyekuwa mbunge  wa  viti maalum mkoa  wa Iringa na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Taifa  Chiku Abwao akimtaka  mbunge  wa  jimbo la  Iringa mjini Mchungaji  Peter  Msigwa (chadema) kuwaeleza  wakazi  wa jimbo  hilo ndani ya  miaka  mitano ya  ubunge  wake  amefanya  nini zaidi ya maandamano  na kutukana  watu .

  Kauli   hiyo  waliotoa wakati  wa mkutano wa hadhara wa  kuwatambulisha   wagombea  ubunge  wa  jimbo la Iringa mjini na majimbo mengine ya  mkoa  wa Iringa na  kuwa siasa si maneno  matupu  siasa ni  kazi  zaidi ya  kuwakomboa wananchi   waliokuamini katika maendeleo .

  Alisema  Bw  Kabwe  kuwa mbali ya  kuwa  yeye  ni  ACT  wazalendo  ila hata acha  kuwazungumzia  baadhi ya  wabunge   waliofanya kazi nzuri ya  kuwatumikia  wananchi  wao na  miongoni mwa  wabunge hao ni pamoja na mbunge wa Ludewa Bw Filikunjombe kwani kazi aliyoifanya  jimboni inaonekana na kazi aliyoifanya  ndani ya  bunge katika  kupigania maendeleo ya  wana Ludewa na  Taifa  kila mtazania anatambua mchango  wake .

  Kwani  alisema  kuwa kati ya manho makubwa ambayo  Filikunjombe kama  makamu  wake  mwenyekiti  waKamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kamati liyoifanya  ni pamoja na  kuhakikisha ripoti ya Escrow inalindwa  pasipo  kuibiwa wakiwa wabunge  watatu ambao  walikesha  wakilinda  ripoti hiyo  isiibwe  na mawaziri  waliokuwa  wakizingira  jengo  walilokuwepo  ili  kuiba ripoti hiyo .

  '' Siku   ile  tulikesha na mashuka  yetu ya  kimasai  kuhakikisha  ripoti yetu  haiibwi ili  tuiingize  bungeni  na tukaiingiza  bunge  lakini  ile  ripoti hadi  leo kuna  mambo hayajamalizwa  kwani kampuni ya IPTL ambao  imenunuliwa na kampuni ya PAP ya  Singa  singa na kampuni   hiyo ya PAP hadi leo bado inapokea Tsh  bilioni 4 kila mwezi kutoka  Tanesco  hapo  wazalishe ama  wasizalishe'' alisema  Kabwe


  Alisema  kuwa kampuni  hiyo  asilimia 50  inamilikiwa na Seth Singa  singa na  asilimia 50  nyingine  zinamilikiwa na kampuni  inaitwa simba  Trust  iliyosajiliwa nje  ya  Tanzania  na  wamiliki  wake  hawafahamiki na  kuwa hizo ndizo  hoja ambazo  ACT wazalendo  wamejiandaa kutembea  nazo katika kampeni  ya uchaguzi mkuu .

  Kabwe  alisema  kuwa sakata  ya ECROW  bado  halijaisha kwani  bunge liliagiza mtambo wa IPTL  utaifishwe  ila hadi  leo bado kuna  kigugumizi katika  kuchukua hatua  juu ya suala   hilo la kampuni ya kitapeli  kuendelea  kulipwa mabilioni ya shilingi  hivyo  alisema kuwa haja ya chama cha  kati  kuingia Ikulu ili  kuweza kupambana na mafisadi  wa Richimond ambao leo  wamejificha katika mwamvuli wa UKAWA .

  Hivyo  alisema kuwa kila  sababu  wabunge kufanya kazi wanayotumwa na  wananchi  wao kwa uadilifu  badala ya  kuwa  wabunge wa maneno  bila  vitendo na kuwa wakati tukielekea katika  uchaguzi mkuu ni vema  wananchi  kuwapima  wabunge  wanaowachagua kwa  kueleza  wamefanya  nini majimboni  badala ya kuwa na mbunge  mpiga  kelele zisizo  za kimaendeleo kwa wananchi  wake .

  Kwa  upande  wake  mgombea  ubunge  wa ACT wazalendo   jimbo la  Iringa mjini Bi Abwao  ambae  amejiunga na  chama  hicho kutoka Chadema  alisema mbunge  wa  jimbo  hilo mchungaji Msigwa ajiandae  kukabidhi  jimbo   hilo kwa  ACT wazalendo kwani ameshindwa  kuwatumikia  wananchi wa  jimbo la Iringa mjini kazi  waliyomtuma bungeni .

  Alisema  kuwa kipindi  cha  miaka mitano ya  mbunge mchungaji Msigwa  jimboni hapo  hakuna  jipya ambalo amelifanya  zaidi ya  maandamano na  vurugu ambazo  wakazi  wa Iringa mjini hawajapata  kuziona na  kuwa atazunguka kila moja hadi nyingine  kuwaeleza  wananchi jinsi  ambavyo mbunge  huyo  alivyojaribu kuua nguvu  ya  vyama  vya  upinzani na  kushindwa  kuwajibika kwa wananchi  waliomchagua.

  0 0

  
    HALMASHAURI ya Wilaya ya Mufindi  Mkoani Iringa ni mingoni mwa  Wilaya saba nchini, zilizochaguliwa na shirika la kimataifa linaloshughulikia mazao ya viazi (CIP) kutekeleza mradi  wa uzalishaji wa viazi lishe vyenye asilimia kubwa ya vitamini “A” ukilinganisha na  aina nyingine ya vyakula kama Mboga, Matunda na Mizizi.

  Taarifa iliyotolewa na Afisa ya Habari na Mawasiliano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Ndimmyake Mwakapiso, imeeleza kuwa, viazi lishe hivyo ni aina ya viazi vitamu vyenye asilimia 90 ya vitamini A vinavyohitajika katika mwili wa binadamu ili kujenga ubongo wa watoto walio chini ya miaka 05, kuimarisha afya ya wajawazito pamoja na uwezo wa kuona kwa kila mwanadamu.  Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi  Mkoani Iringa ni mingoni mwa  Wilaya saba nchini, zilizochaguliwa na shirika la kimataifa linaloshughulikia mazao ya viazi (CIP) kutekeleza mradi  wa uzalishaji wa viazi lishe vyenye asilimia kubwa ya vitamini “A” ukilinganisha na  aina nyingine ya vyakula kama Mboga, Matunda na Mizizi.


  Katika kutekeleza adhima hiyo, mradi huo umeanza kutekekelezwa katika vikundi vya wakulima kwa kuotesha mbegu kwenye maeneo yenye miundombinu ya umwagiliaji yaliyopo katika viijiji vya Igomaaa na Lugolofu pamoja bustani zilizopo kwenye vijiji vya Lugema, Mabaoni na Makungu.
   
   Taarifa hiyo imeongeza kuwa mbegu zitakazozalishwa zitagawiwa kwenye vijiji 18 ambayo vimechaguliwa kutekeleza mradi huo kwa kipindi cha miaka mitatu na utekelezaji mara babada ya kwa kipindi cha mvua.

  Aidha, endapo Viazi hivyo vitazalishwa kwa wingi na kuongezwa thamani   vitaboresha  kipato kwa mkulima kwani soko lake linapatikana kwa urahisi huku vikiwa na uwezo wa kuzindikwa kwa utengenezaji wa Kripsi, Mkate, Chapati, Biskuti, Juisi na unga wa lishe.  Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi  Mkoani Iringa ni mingoni mwa  Wilaya saba nchini, zilizochaguliwa na shirika la kimataifa linaloshughulikia mazao ya viazi (CIP) kutekeleza mradi  wa uzalishaji wa viazi lishe vyenye asilimia kubwa ya vitamini “A” ukilinganisha na  aina nyingine ya vyakula kama Mboga, Matunda na Mizizi.

  0 0


  Mtumishi wa Nssf Mbeya Niah Almasi   akiwa na nyuso ya furaha baada ya  ya kufunga pingu za maisha na Jackline Bukuku  ndoa iliyofungwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika msikiti wa Forest jijini Mbeya na maulid iliyofanyika nyumbani kwa Bw.Harusi Brock T jijini hapa .
  Bw.Almasi na Mke wake Jackline katika ubora wao

  Baadhi ya watumishi wa Nssf Mbeya wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya mtumishi mwenzao kupata jiko ,(kushoto)Mr Maige  na Khadija Rashidi Shibobo.


  watoto wa madrasa wakisoma dua katika harusi ya Bw.Niah na Jackline nyumbani kwake Block T jijini Mbeya mwishoni mwa wiki..Picha Jamiimojablog.


  Aliyekuwa rais  wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA),Omari Ayub akiokoa jahazi kwa kugawa sahani za mpunga (Biliani)  

  0 0

  image (3)
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akitia saini kwenye kitabu cha wageni kwenye banda la maonesho la NHC lilikuwapo katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi kulikokuwa kukifanyika maonesho hayo ya Nane Nane kitaifa.
  image (5)
  Wateja wakipata maelekezo kutoka kwa maafisa wa mauzo wa Shirika la Nymba la Taifa kwenye maonyesho ya Nane Nane Kitaifa Ngongo, Lindi.
  image (7)
  Wateja wakipata maelekezo kutoka kwa maafisa wa mauzo wa Shirika la Nymba la Taifa kwenye maonyesho ya Nane Nane Kitaifa Ngongo, Lindi.
  image (9)
  Wateja wakipata maelekezo kutoka kwa maafisa wa mauzo wa Shirika la Nymba la Taifa kwenye maonyesho ya Nane Nane Kitaifa Ngongo, Lindi.
  image (11)
  image (13)image
  0I7A0544
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akihutbia wakazi wa Lindi kwenye uwanja wa Nane Nane Ngongo ambapo alihitimisha kilele cha sikukuu ya wakulima Nane Nane. Maonesho ya nane nane yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
  0I7A0550
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akihutbia wakazi wa Lindi kwenye uwanja wa Nane Nane Ngongo ambapo alihitimisha kilele cha sikukuu ya wakulima Nane Nane. Maonesho ya nane nane yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.

  0 0

  Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa kituo cha Redio cha EFM,  Denis Ssebo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu  kuendelea kufanyika kwa Tamasha la Muziki Bar kwa Bar baada ya kumalizika kwa tamasha hilo kwa awamu ya kwanza. Kulia ni Mtangazaji, Dina Marios.
   Mtangazaji, Dina Marios akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu  kuendelea kufanyika kwa Tamasha la Muziki Bar kwa Bar baada ya kumalizika kwa tamasha hilo kwa awamu ya kwanza. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa kituo cha Redio cha EFM,  Denis Ssebo.
  Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa kituo cha Redio cha EFM,  Denis Ssebo katika mkutano uliofanyika makao makuu ya EFM-Mikocheni jijini Dar es Salaam.
  Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

  BAADA ya kumalizika kwa Tamasha la musiku mnene Bar kwa bar awamu ya kwanza, na mashabiki kuomba Burudani hiyo iendelea tena, Uongozi Efm umekubali ombi hilo na sasa Tamasha hilo linarudi tena kwa kishindo likiwa  limeboreshwa kwakuongeza wigo wa kuwafikia watu wengi zaidi.

  Muziki mnene bar kwa bar awamu hii bila kuwasahamu wasikilizaji na mashabiki wa EFM katika wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala kwa umuhimu wake na Wilaya mpya katika mkoa wa Dar es salaam, Muziki mnene sasa utapelekwa pia katika mkoa wa Pwani.

  Maeneo ambayo wanatakiwa kukaa tayari  kwa Muziki mnene bar kwa bar utakaoporomoshwa  na Madjs wakali wa Efm, ni pamoja na Kibaha, Mlandizi, Mkuranga, Bagamoyo, Kisarawe,  Kigamboni na maeneo mengine mengi kwa ajili ya kuhakikisha tunakonga nyoyo za mashabiki wetu.

  Muziki Mnene bar kwa bar mwaka huu inatarajiwa kuanza rasmi tarehe 5/09/2015 . Lakini katika kuelekea huko efm imeanza na Muziki mnene bango katika sehemu yako ya biashara ambako bwana E anapita na ukiwa umeweka bango la EFM na unasikiliza matangazo yetu basi utapata kifurushi chenye zawadi kibao.

  Na kama ilivyokawaida yetu, mwishoni tutakuwa na Tamasha kubwa la hitimisho ambalo litafanyika jijini Dar es salaam ambalo safari hii limeboreshwa na kuongezwa vionjo vingi sana.


  “Ninawaomba wasikilizaji wetu wakae mkao wa kula maana tutawafikia na kuwamiminia Burudani ambayo pia itarushwa live kutoka eneo husika kupitia kituo chao cha 93.7 EFM. Njoo tuonane, tufahamiane na tuijenge Radio yetu efm ambayo kwetu Muziki unaongea”.

  LAKINI jambo la pili ambalo ndugu zangu wanahabari tungependa kuwajulisha ni kwamba katika kuhakikisha tunaendelea kukupa kilicho bora zaidi kupitia vipindi vyetu mbalimbali,sanjari na kuwa na watangazaji wenye ushawishi na uwezo mkubwa. leo hii tunamtambulisha kwenu mtangazaji Dina Marios ambaye wengi uwezo wake mnaujua na sasa ameungana na wenzake  wenye uwezo mkubwa katika familia ya Efm.

  Mwisho niwashukuru sana kwa mwitikio wetu na kwakuwa tumeendelea kushirikiana mara nyingi hivyo naomba tuendelee kushirikiana hivi hivi.  Asanteni sana kwakunisikiliza.


  0 0

    Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia wanachama na wafuasi wa CCM mkoa wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kumpokea,Dkt Magufuli aliwashukuru wanachama hao kwa kujitokeza kwa wingi na walimuahakikishia ushindi wa kishindo na wapema katika uchaguzi mkuu utakaofanyika hapo baadae mwaka huu.
   Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Husnain Murji akiwahutubia wana CCM nje ya ofisi ya CCM Mtwara na kuwaambia kuwa ushindi kwa CCM utakuwa wa kishindo .
   Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani akihutubia wakazi wa Mtwara  ambapo alihakikisha kuwa Mtwara itaongoza katika kumpigia kura nyingi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
   Wananchana na Wafuasi wa chama cha Mapinduzi (CCM),wakimshangilia  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli  alipokuwa akiwashukuru kwa kumpa udhamni na kujitokeza kwa wingi kumpokea,lakini pia alitumia nafasi hiyo kujitambulisha kwao na kuwaomba wajenge mshikamano na kuweka tofauti zao kando ili kukihakikishia ushindi chama cha CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika hapo baadae mwaka huu.
    Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli aakiwa katika picha ya pamoja na bbaadhi ya wa asisi wa chama hicho mkoani Mtwara na wananchama wengine katika picha pamoja nje ya ofisi za chama hicho mjini Mtwara..
   Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga baadhi ya Wanachama wa CCM nje ya ofisi za mkoani Mtwara,akirejea jijini Dar Es Salaam kuendelea na shughuli nyingine

   Mgombea mteule wa Urais kwa chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara,Ndugu Shaibu Akwilombe mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM mkoa wa Mtwara kuwashukuru Wanachama na wafuasi wa chama hicho kwa kujitokeza kwa wingi,na pia alitia saini vitabu vya wageni vya ofisi hiyo,kati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani pamoja na Naibu Waziri wa Fedha,ambaye pia aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Mwigulu Nchema,
    Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na wanachama na wafuasi wa chaa hicho nje ya ofisi za mkoa huo mjini Mtwara.
   Baadhi ya Wanachama na wafuasi wa chama cha CCM wakiwa wamekusanyika nje ya ofisi ya za mkoa huo mjini Mtwara,kabla ya kumsikiliza mgombea Urais wa chama hicho Dkt John Pombe Magufuli,ambaye alifika ofisini hapo kusaini vitabu na pia kuwashukuru wanachama huo kumdhamini na kujitokeza kwa wingi kumpokea.

  0 0


   Ofisa Mradi wa mpango wa kutekeleza  mkakati wa kupunguza  vifo vinavyotokana na ajali za barabarani kwa kusisitiza usalama  Barabarani unaosimamiwa kwa kushirikiana na  Bloomberg (BIGRS), Shirika la afya Duniani (WHO)  na Serikali ya Tanzania, Mary Kessi (katikati), akitoa mada kwenye semina hiyo iliyowajumuisha wanahabari na wadau wa sekta ya usafiri inayohusu  mpango huo wa utekelezaji wa mkakati huo.
   Mtaalamu Mwelekezi, Callie Long kutoka Canada akitoa mada kwenye semina hiyo. 


   Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Asah Mwambene akitoa mada kwenye semina hiyo.
   Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Mkaguzi wa Polisi Sokoni Deus (katikati), akitoa mada kwenye semina ya siku mbili ya wanahabari na wadau wa sekta ya usafiri Dar es Salaam leo asubuhi, inayohusu  mpango wa kutekeleza  mkakati wa kupunguza  vifo vinavyotokana na ajali za barabarani kwa kusisitiza usalama  Barabarani.
  Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye 
  semina hiyo.


  Semina ikiendelea.
  Mmoja wa wadau wa semina hiyo akichangia jambo.

  Na Dotto Mwaibale

  Mradi wa usalama barabarani kwa kushirikiana na  Bloomberg (BIGRS), Shirika la afya Duniani (WHO) na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa  umeanza kutoa mafunzo kdau wa sekta wa usafiri wakiwemo wanahari, wanasheria kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya ajali.

  Akizungumza Dar es salaam leo kwenye semina ya siku mbili  inayohusu mpango wa kutekeleza  mkakati wa kupunguza  vifo vinavyotokana na ajali za barabarani kwa kusisitiza usalama  Barabarani, Ofisa Mradi huo,  Mary Kessi alisema waandishi wamekuwa wakisubiri matukio ya ajali ndipo waripoti habari hizo jambo ambalo si lazima lisubiriwe na inachotakiwa ni kujenga mazoea ya kuandika habari za kufundisha jamii na watumiaji wa vyombo vya moto namna ya kuweza kuepuka kusababisha ajali.

  "Dhumuni la semina hii ni kujua jinsi ya kuripoti habari hizi za usalama barabarani ili kufikia walengwa kwa kuongea kupitia vyombo vyenu vya habari ili kuwapa ulewa watu wote' alisema  Kessi.

  Alisema kuwa mpango huo wa miaka mitano utaelekeza katika kupunguza ajali za barabarani  huku takwimu zinaonyesha ajali hizo zimekuwa zikiua watu milioni1.24 kila mwaka Duniani, kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya taifa huku kati ya hao 20 upata ulemavu kutokana na ajali.

  Alifafanua kuwa uzembe wa madereva usababisha ajali zinazoweza kuzuilika na kuzitaja sababu hizo kuu ni kutofunga mikanda ,kuendesha gari kwa kasi ,matumizi ya pombe kupita kiwango na kutoweka vizuwizi vya watoto.

  "Uendeshaji wa gari ukiwa umelewa ni kitu kibaya sana wengine wanaendesha gari huu wanachati na simu bila kujali kilichokua mbele wala nyuma yake"alisema

  Daktari wa Kitengo cha Maafa na Dharura wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,  Mery Kitambi,alisema Hospitali za mikoa zilizopo nchini hapa zimejaa majeruhu wa ajali pamoja na vifo vinavyo sababishwa na ajali hizo.

  Alisema waandishi wanatakiwa kuleta fikra mpya kwa  watumia wa vyombo hivyo vya moto ili wajue ni kiasi gani wanajiweka katika hatari na jinsi ya kuepuka hatari hizo.

  "Ukienda hospitali utawakuta majeruhi wa ajali ni wengi kuliko unavyo fikiria hivyo ni vyema wakajua kwa undani jinsi gani ya kuepuka ajali za kizembe"alisema Kitambi.

  Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Mkaguzi wa Polisi, Sokoni Deus, alisema wazazi wanatakiwa kuacha tabia ya kuwapa watoto walio chini ya miaka 18 kuendesha vyombo vya moto kwani usababisha ajali.


  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akitoa hotuba ya kuhitimisha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa kwenye viwanja vya Nane Nane Nzuguni Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.Picha na John Banda wa Pamoja Blog.
   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Margreth Mussa wa shule ya msingi Maria de Matias baada ya kushinda shindano la kuandika insha ya lishe na unyonyeshaji wakati wa sherehe za kilele cha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane Nane Nzuguni Mkoani Dodoma
   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akimkabidhi zawadi Bi. Lilian Simon mmoja ya wakina mama walionyonyesha watoto wao kwa kufuata maelekezo ya wataalamu na kuwezesha watoto wao kuwa na afya bora na kukua vizuri. 
   Kikundi cha ngoma za asili ya kigogo cha zepisa Hombolo kikitumbuiza wakati wa sherehe za kilele cha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane Nanne Nzuguni Mkoani Dodoma.
   Vijana wa bendi ya muziki ya Winners ya Mjini Dodoma wakionesha ufundi wa kusakata muziki wakati wa sherehe za kilele cha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane Nanne Nzuguni Mkoani Dodoma.
   Bi. Lilian Simon akiwa amembeba Mwanae Dorcas David (3)  akipongezwa na Vijana wa bendi ya muziki ya Winners alipotoa ushuhuda wa faida ya kumnyonyesha mtoto wake maziwa ya mama pekee hadi alipofikisha umri wa miezi sita na baadae kuendelea hadi miaka miwili wakati wa sherehe za kilele cha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane Nanne Nzuguni Mkoani Dodoma
   Bi. Judina Deus Malya akiwa na watoto wake mapacha Noel na Nance Malya (4) mara baada ya kutoa ushuhuda wa faida ya kuwanyonyesha watoto wake maziwa ya mama pekee hadi walipofikisha umri wa miezi sita na baadae kuendelea hadi miaka miwili wakati wa sherehe za kilele cha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane Nanne Nzuguni Mkoani Dodoma
   Baadhi ya Wananchi wa Dodoma waliofika kwenye viwanja vya Nane Nane Nzuguni wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo Chiku Gallawa (hayupo pichani) wakati akitoa hotuba ya kuhitimisha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa mwishoni mwa wiki.
   Picha ya pamoja baina ya mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa (katikati), viongozi wa Mkoa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na wamama walionyonyesha watoto wao kwa kufuata masharti ya wataalamu na watoto wao wenye afya bora baada ya kumalizika kwa Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa mwishoni mwa wiki kwennye viwanja vya Nane Nane Nzuguni Mkoani humo.
  Picha ya pamoja baina ya mkuu wa Mkoa wa Dodoma, viongozi wa Mkoa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambao kwa pamoja wameshirikiana katika maandalizi na  kufanikisha  Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa yaliyohitimishwa mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane Nane Nzuguni Mkoani humo.

  0 0

   Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo ataongoza vikao vya Kamati ya Maadili na Kamati kuu ya CCM vitakavyofanyika katika ukumbi wa White House Makao Makuu Dodoma.

  Alhaj Kimbisa amekanusha uvumi uliosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa ameihama CCM. Kushoto ni Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana   (picha na Freddy Maro).
   Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na KAtibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahmana Kinana baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo ataongoza vikao vya Kamati ya Maadili na Kamati kuu ya CCM vitakavyofanyika katika ukumbi wa White House Makao Makuu Dodoma. Picha na Freddy Maro


  0 0

  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za tume ya Taifa ya Uchaguzi kkugombea nafasi hiyo, kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mkurugenzi wa tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhan Kombwey, baada ya kukabidhiwa fomu za tume hiyo za kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Agosti 10, 2015. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif.

  MGOMBEA wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa amechukua fomu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ya kuwania nafasi hiyo leo Jumatatu Agosti 10, 2015.

  Msafara wa Mgombea huyo ulioanzia kwenye Ofisi za Chama cha Wananchi CUF Buguruni na kuishia kwenye Ofisi za CHADEMA Kinondoni Jijini Dar es salaam na kupelekea msongamano mkubwa wa watu ambao wengi wao ni wafuasi wakuu wa vyama vinavyounda UKAWA, na kufanya shughuli mbali mbali kusimama kwa muda wa takribani saa saba.  
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, wakati alipofika kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25, mwaka huu.
  Umati wa watu wakiwemo wafuasi wa vyama vya Siasa vinavyounda UKAWA ukiwa Umefurika kwa wingi kwenye Barabara ya Uhuru, Jijini Dar es salaam kumsindikiza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni, walipokuwa wakielekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25, mwaka huu. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwapingua maelfu ya wafuasi wa vyama vya Siasa vinavyounda UKAWA, jijini Dar es salaam, Augusti 10, 2015, walipokuwa wakielekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25, mwaka huu.
  Mh. Lowassa na Mh. Duni wakiwapungia maelfu ya wafuasi wa vyama vya Siasa vinavyounda UKAWA nje ya Makao Makuu ya Chama cha CUF, Buguruni jijini Dar.

  Sehemu ya Wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA wakiushangilia Msafara wa MGOMBEA wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa wakati akielekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25, mwaka huu.
  Buhuruni Rozana.
  MGOMBEA wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na
  Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif mara baada ya kuwasili kwenye Makao Makuu ya Chama cha CUF, Buguruni Jijini Dar es salaam.
  MGOMBEA wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Mh. Freeman Mbowe, huku Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif akishuhudia.


  Mh. Freeman Mbowe, Mh. Tundu Lissu na Mh. James Mbatia wakiwa kwenye magari yao wakati wakimsindikiza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni, walipokuwa wakielekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25, mwaka huu.
  Barabara ya Uhuru, Jijini Dar.
  Barabara ya Bibi Titi Mohamed, Jijini Dar.
  Barabara ya Uhio.
  Hakuna alietaka kupigwa na tukio hili.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwapingua maelfu ya wafuasi wa vyama vya Siasa vinavyounda UKAWA, jijini Dar es salaam, Augusti 10, 2015, walipokuwa wakielekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25, mwaka huu.  Mgombea mwenza wa Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwapungia wafuasi wa vyama vya Siasa vinavyounda UKAWA, jijini Dar es salaam, Augusti 10, 2015, walipokuwa wakielekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25, mwaka huu.


  0 0

  unnamed (69)
  .Miss Tanzania 2012, Brigite Alfred akizindua ujenzi wa bweni la Albino Buhangija mkoani Shinyanga.
  unnamed (70)
  Miss Tanzania 2012, Brigite Alfred akizungumza wakati wa uzinduzi wa taasisi yake ya BAF ambayo kwa kushirikiana na Junior Achievement (JA) huku lengo kuu likiwa ni kutoa elimu ya Ujasiriamali kwa albino Tanzania nzima. Kushoto ni Kaimu katibu Mkuu wa Jumuiya wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), Mohamed Chanzi.
  unnamed (71)
  Miss Tanzania 2012, Brigite Alfred akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Albino mara baada ya kuzindua mafunzo ya Ujasiriamali Makumbusho ya Taifa.
  ……………

  Taasisi ya Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred Foundation (BAF) kwa kushirikiana na Taasisi ya Junior Achievement (JA)  imeendeleza zoezi la kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa wajamii ya watu wenye albino nchini.Mafunzo hayo ya wiki mbili yalifunguliwa na mkuu wa mkoa wa Kigoma ambapo jumla ya albino 20 walifaidika na mafunzo hayo yaliyozinduliwa na mkuu wa mkoa wa Kigoma, kanali mstaafu Issa Machibya. Mbali ya watu wenye albino, washiriki wengine katika mafunzo hayo walikuwa wanawake na vijana.
   
  Machibya alitoa wito kwa taaisis nyingine kuiga mfano taasisi ya Brigitte na Junior Achievements ambayo mpaka sasa imetoa mafunzo kama hayo kwa vijana na akina mama 25,000.Mkuu wa mkoa huyo alisema kuwa mafunzo ya ujasiliamari ni muhimu kwa kila mtu na kupongeza juhudi za mrembo huyo ambaye mpaka sasa ametoa mafunzo kwa watu wenye albino 70. Kati ya hao 70, albino 50 walipata mafunzo jijini Dar es Salaam.
   
   “Haya ndiyo mambo muhimu ya kuigwa kwa jamii, taasisi ya Brigite imetoa elimu ambayo itawawezesha wahitimu kufanyakazi ya ujasiriamali na kujipatia kipato kwa jasho lako, nawapongeza sana na taasisi nyingine zifuate nyayo,” alisema Mashibya.Mratibu wa mafunzo hayo, Stanley Mosha alisema kuwa kwa kupitia BAF kwa sasa unaende vizuri na lengo lao ni kutoa mafunzo kwa watu wenye albino kila mkoa na wamepanga kutoa mafunzo kwa albino 300 nchi nzima kwa mwaka 2015.
   
  Mosha alisema kuwa lengo lao mafunzo hayo ni kuwawezesha kiuchumi vikundimbalimbali hususani vijana na wakinamama. Alisema kuwa hatua hiyo imetokana na mafanikio ya Brigitte katika mashindano ya urembo ya Dunia ya mwaka 2013  nchini Indonesia na kushika nafasi ya tatu kupitia taji la mrembo mwenye malengo baada ya kuonyesha dunia jitihada zake za kusaidia watu wenye ualbino nchini Tanzania.
   
  Alisema kuwa kuanzia hapo, Brigitte amekuwa Balozi wa watu kwa watu wenye ualbino Tanzania na kufanya shughuli mbalimbali za kuwasaidia mfano ujenzi wa bweni la kisasa lenye uwezo wa kuchukua idadi ya watoto 60, na uboreshaji  mazingira kituo cha Buhangija mkoani Shinyanga.
   
  “Nimefuraishwa na Mwitikio na ushirikiano walioonyesha kwa kutambua na kukubali kuliingiza kundi hili na kuweza kuungana na makundi mengine ya vijana katika program za ujasiriamali. Kulitambua na kulijumuisha kundi hili katika kuwajengea uwezo ni hatua kubwa inayowezesha kupanua wigo na juhudi za kuwezesha makundi ya vijana na wakinamama kiuchumi na tunaomba wadau wengine waungane nasi katika hili,” alisema Mosha.
   
  Kwa upande wake, Brigitte alisema kuwa ataendeleza mpango huo hapa nchini na anaamini atafikia lengo lake. “Nashukuru Junior Achievement kwa kuniunga mkono katika mpango huu ambao kwa sasa unapata mafanikio makubwa, naomba kuungwa mkono kwani jukumu hili ni la watanzania wote,” alisema Brigitte.

  0 0

  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kuongezeka kidogo kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Mei 2015 leo jijini Dar es salaam.Mfumuko wa Bei wa  bei kwa mwezi Julai ,2015 umefikia asilimia  6.4   kutoka asilimia 6.1 iliyokuwepo Juni 2015.


  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
  OFISI  ya Taifa ya Takwimu imetangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Julai 2015 na kusema kuwa umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.4  kutoka asilimia 6.1 iliyokuwepo mwezi Juni 2015.

  Hii inamaanisha kuwa  kasi ya upandaji wa bei ya  bidhaa na huduma kwa mwezi Julai 2015 imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya upandaji bei ya bidhaa na huduma  iliyokuwepo mwezi Juni mwaka 2015.  

  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam amesema kuongezeka huko kumesababishwa na kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula katika maeneo mbalimbali nchini.

  Amezitaja bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko huo kutokana na upandaji wa bei katika masoko kwa mwezi Julai 2015 kuwa  ni mchele kwa asilimia 27.9,mahindi asilimia 2.3, unga wa muhogo asilimia 9.2, nyama asilimia 4.5, samaki 12.2, na maharage asilimia 5.9.

  Kuhusu Fahirisi za Bei ambacho ni kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya binafsi hapa Tanzania, Kwesigabo  amesema zimeongezeka hadi kufikia 158.78  kutoka 158:12 za mwezi Juni.

  Amesema kuongezeka kwa fahirisi za bei kumechangiwa na ongezeko la bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula zikiwemo gesi ya kupikia kwa asilimia 3.7, mafuta ya dizeli 5.9, mafuta ya Petroli ailimia 4.9,  unga wa mahindi asilimia 2.5, ulezi asilimia 2.9, samaki asilimia 4.8, viazi vitamu asilimia 2.6 na ndizi za kupika asilimia 3.4.

  Kwesigabo amesema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za mlaji kwa mwezi Julai , 2015 umefikia shilingi 62 na senti 98 ikilinganishwa na kiasi cha shilingi 63 na senti 24  za mwezi Juni 2015. 

  “Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile kwa mlaji kwa mwezi Julai ,2015 na  umepungua  hii ina maana kuwa sasa mtu anahitaji kuongeza ziada ya shilingi 38 ili aweze kununua bidhaa na huduma sawa na zile alizokuwa na uwezo wa kuzinunua katika mwezi Juni"

  Kwa upande wa mfumuko wa Bei kwa nchi za Afrika Mashariki kwa mwezi Julai, 2015 Bw.Kwesigabo amesema kuwa una mwelekeo unaofanana , Kenya umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 6.62 na kutoka 7.03 mwezi Juni 2015 huku Uganda ikiwa na mfumuko wa Bei wa  asilimia 5.4  kutoka asilimia 4.9  za mwezi Juni, 2015.

  0 0

  Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Erasmus Rugarabamu kwa niaba ya Menejimenti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa akitoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya ambaye pia ni Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma kwa ushindi mnono alioupata katika kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kutafuta mgombea wa ubunge Jimbo la Mbinga Magharibi. Eng. Manyanya alishinda kwa kura 13,276 ambapo mshindi wa pili alikua na kura 3,466. Jumla ya wagombea walikua 10 ambapo tisa kati yao walikuwa ni wanaume.

   Awali Jimbo hilo lilikuwa nimeshikiliwa na hayati Capt. John Komba. Kwasasa imebaki hatua ya mwisho ya majina ya wagombea kupitishwa na Uongozi wa juu wa Chama kwa ajili ya kupeperusha bendera ya Chama  cha Mapinduzi majimboni katika uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu 2015. Uongozi na Watumishi wote wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa unamtakia kila la heri Eng. Manyanya katika safari yake hiyo na hatimae aweze kushinda katika Jimbo hilo. 

  Akitoa shukurani kwa niaba ya watumishi Katibu Tawala Msaidizi Kitengo cha Serikali za Mitaa Ndugu Albinus Mgonya alimpongeza Mkuu huyo wa Mkoa wa Rukwa kwa msukumo mkubwa wa maendeleo aliouweka katika kipindi cha uongozi wake hususani katika sekta ya elimu ambapo alianzisha Azimio la Kasense kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu mashuleni, Kuboresha afya ya mama wajawazito na watoto wachanga, usafi wa mazingira ambapo alianzisha kampeni ya Sumbawanga Ng'ara iliyozinduliwa na Mhe. Makamu wa Rais, Kampeni ya upandaji miti, kuboresha mazingira ya utalii katika maporomoko ya Mto Kalambo, kuboresha hali ya ulinzi na usalama katika Mkoa, Kuwaunganisha watumishi na viongozi katika kufanya kazi kwa pamoja n.k 

   
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa katika kikao kifupi cha kumpongeza baada ya kushinda katika kura za maoni Jimbo la Nyasa Magharibi kupitia CCM. Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Viongozi hao pamoja na watumishi kusimamia misingi aliyoiweka ya kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa, kufanya kazi kwa pamoja (team work) na kutekeleza majumu yao ya kila siku kwa ufanisi na ubunifu wa hali ya juu. Alisistiza kuwa maendeleo ya taifa la Tanzania hayataletwa tu kwa kutegemea vyama vya siasa bali kwa wananchi na wafanyakazi kutekeleza majukumu na wajibu wao ipasavyo kwa kuweka uzalendo mbele na kufanya kazi kwa bidii na uadilifu uliotukuka.   
   
   Katibu Tawala Msaidizi Kitengo cha Serikali za Mitaa Ndugu Albinus Mgonya akitoa Shukrani na Salamu za pongezi kwa niaba ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya kufuatia ushindi alioupata katika kura za maoni kutafuta mgombea wa CCM Jimbo la Mbinga Magharibi. Kwa sasa Mhe. Eng. Manyanya.
  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa

  0 0

   THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


   TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Joseph B. Masikitiko kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kabla ya uteuzi huo Ndugu Masikitiko alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo (TBS).

  Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Balozi mmoja na kuwabadilishia vituo vya kazi Mabalozi wawili kama ifuatavyo:

  (i)    Lt. Gen. Charles L. Makakala, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe. Kabla ya uteuzi huo Lt. Gen. Makakala alikuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College).
  (ii)Balozi Wilson Masilingialiyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi amehamishwa kwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Liberata Mulamula aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa. Atakuwa pia anaiwakilisha Tanzania nchini Mexico.

  (iii)                 Balozi Irene Kasyanjualiyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi kushika nafasi inayoachwa wazi na Balozi Wilson Masilingi.

  Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, Agosti 11, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Uteuzi na uhamisho huu unaanzia tarehe 07 Agosti, 2015.
  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.
  11 Agosti, 2015


older | 1 | .... | 605 | 606 | (Page 607) | 608 | 609 | .... | 1897 | newer