Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live

SIHABA NKINGA:Tutaendelea na jitihada za kuwawezesha vijana kama kundi muhimu katika jamii


INTRODUCING New VIDEO | Isaya - Asia

ZAWADI MASHINDANO YA JIMBO LA VUNJO (MBATIA CUP 2015) HADHARANI.

$
0
0
Baadhi ya viongozi wa Chama cha NCCR-Mageuzi jimbo la Vunjo akiwa katika hafla fupi ya kutangaza zawadi kwa washindi wa mashindano ya Mbatia Cup 2015.
Mmoja wa Waratibu wa Mashindano ya Mbatia Cup 2015 yanayofanyika katika jimbo la Vunjo,Danielson Shayo akizungumza wakati wa kutangaza zawadi kwa washindi.
Baadhi ya iongozi wa timu zinazoshiriki mashindano hayo.
Msaidizi wa Mbunge James Mbatia ,Hamis Hamis akizungumza katika hafa fupi ya utambulisho wa zawadi kwa washindi wa mashindano hayo yaliyofikia hatua ya nusu fainali.
Kikundi cha sarakasi kikitoa burudani wakati wa hafla hiyo .
Kikosi cha timu ya Wazalendo ambacho kimefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali.
Kikosi cha timu ya Himo fc kilichofanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali.
Moja ya heka heka wakati timu hizo zikitafuta nafasi ya kucheza hatua ya Nusu fainali.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.



Na Dixon Busagaga,Moshi.
KAMATI ya Mashindano ya Kombe la jimbo la Vunjo maarufu kama Mbatia Cup 2015 imetenga zaidi ya kiasi cha sh Mil 6 kama zawadi kwa washindi wa mashindano hayo yanayoingia hatua ya nusu fainali pili leo
Zawadi zilizotengwa ni pamoja na sh Mil 2,Kombe kubwa,Medali za Dhahabu na mipira mitatu kwa mshindi wa kwanza,Sh Mil 1,Kombe la kati,Medali za fedha na Mipira miwili kwa mshindi wa Pili huku mshindi wa tatu akipata Sh 500,000,Ngao,Medali za Shaba na Mpira mmoja.
Mwenyekiti wa kamati hiyo,Danielson Shayo alisema mbali na zawadi hizo kwa washindi,kamati pia imepanga kutoa zawadi za Jezi kwa timu nane ambazo zitafanikiwa kuigia hatua ya nane bora.
“Mshindi wan ne pia tumemuandalia zawadi ya Mpira ,mbali na jezi ambazo itakuwa imepata wakati wa kufanikiwa kuingia hatua ya Nane bora,lakini pia kuna zawadi kwa Mchezaji bora,Mfungaji bora,mlinda mlango bora,timu yenye nidhamu na kocha bora”alisema Shayo.
Shayo alisema mashindano hayo yatakayotumia viwanja vitano vya Chuo cha Ualimu,Marangu,Njia Panda,Kahe Magharibi ,Himo Polisi na Ifati yamepangwa kuchezwa kwa mtindo wa mtoano .

RAIS KIKWETE AZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI SAFI MKOANI LINDI,AWAAGA WANANCHI WA LINDI

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji safi katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji safi katia\ka Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.

 Sehemu ya Chotea kama inavyoonekana pichani katika mradi mkubwa wa maji safi katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi,mradi huu ukikamilika utaweza kutoa lita milioni 750 ambapo utakuwa umetosheleza mahitaji ya maji, kwa sasa wakazi wa Manispaa ya lindi wanapata lita milioni 250 na mahitaji yao ni lita milioni 500.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ujenzi wa mradi wa maji safi uliopo Ng'apa mkoani Lindi.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali ,Wahisani na Wakandarasi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji safi wa halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Ng'apa waliojitokeza kwa wingi kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa mradi wa maji safi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wananchi wa kata ya Matopeni kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba za walimu.
Manispaa ya Lindi ina mpango wa kujenga  nyumba kumi (10) za gharama nafuu za walimu kwa mwaka 2015/2016.
 Wananchi wa kata ya Matopeni wakimsikiliza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete wakati akizungumza  kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba za walimu.Mradi huo ambao upo kwenye halmashauri 7 za mkoa wa Lindi  na ambapo katika kata ya Matopeni kwenye shule ya Msingi Mtuleni zimeanza kujengwa nyumba mbili.
 Waziri wa Ujenzi na Mgombea wa Urais kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Abdallah Ulega pamoaja na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Yahaya Nawanda.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa shule ya msingi Mtuleni mara baada ya kumaliza kukagua  mradi wa ujenzi wa nyumba za walimu, Wengine pichani ni Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli, Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutokea Wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa .
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli wakiwasalimia wananfunzi wa Shule ya Msingi Mtuleni mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za walimu shuleni hapo.

MEMBE AMUUNGA MKONO MAGUFULI,AMKUBALI KUWA NI MCHAPA KAZI

LOWASSA AHUDHULIA MKUTANO WA BARAZA KUU LA CHAMA CHA WANANCHI CUF JIJINI DAR LEO

$
0
0
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwapungua Wanachama na Wafuasi wa Vyama UKAWA waliofurika kwenye Makao Makuu ya CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akikumbatiana na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kabla ya kuelekea kwenye Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF. 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na Wenyeviti wenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia na Dkt. Emmanuel Makaidi wakitembelea kuelekea Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakiwapungia wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakati wakielekea kwenye Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF. Wengine walioambatana nao ni Wenyeviti wenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia na Dkt. Emmanuel Makaidi.

Umati wa Watu ukiwapokea Viongozi wao.
 Sehemu ya Wafuasi na Wanachama wa Chama cha Wananchi CUF, wakiwa wamejipanga Barabarani tayari kwa kumlaki, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, alipokuwa akielekea Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
 Wanachama wa Chama cha Wananchi CUF wakifurahia Ugeni huo.
 Sehemu ya Viongozi wakuu wanaounda UKAWA, wakiongozwa na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR - Mageuzi, Mh. James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi, wakimsuburia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.
Umati nje ya Makao Makuu ya CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakati wakielekea kwenye Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.

Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwasili kwenye Makao Mkuu ya CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR - Mageuzi,Mh. James Mbatia  akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Tundu Lissu akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi akimpongeza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa mara baada ya kuhutubia.
Wakielekea kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Mh. Magdalena Sakaya wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Chama hicho, uliofanyika August 9, 2015, kwenye Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.

MESSAGE FROM MS IRINA BOKOVA, DIRECTOR-GENERAL OF UNESCO, ON THE OCCASION OF INTERNATIONAL DAY OF THE WORLD’S INDIGENOUS PEOPLES, 9 AUGUST 2015

$
0
0
Irina_Bokova1
Director-General of UNESCO, Ms Irina Bokova.

International Day of the World’s Indigenous Peoples is the perfect opportunity to emphasize indigenous peoples’ vital contribution to the implementation of sustainable solutions for tackling development challenges, from the management of natural resources to the fight against climate change.

Promoting the cultures, the languages and the knowledge of indigenous peoples is an essential part of UNESCO’s action. We know that respecting knowledge systems and local languages – including those of indigenous peoples – is one of the conditions for successful inclusive, equitable school systems, in which everyone can learn and show their potential. It is central to achieving the implementation of the quality education for all (EFA) goals and is fully integrated into the declaration adopted at the World Education Forum held in May 2015, in Incheon, Republic of Korea. The declaration advocates inclusive and equitable, quality education and life-long learning opportunities for all by 2030. 

We must better transmit and promote indigenous peoples’ cultural diversity and scientific knowledge, which are forces for renewal and innovation for the whole world. UNESCO is thus working to have culture fully recognized as an enabler and a driver of inclusive and sustainable development. The cultural diversity of indigenous peoples, be it artistic traditions, music, craftsmanship or contemporary art, represents an infinite source of dignity, identity and cohesion, whose full potential we are far from having unleashed. 

Local and indigenous knowledge also plays a crucial role in the fight against environmental risks. We must further integrate this knowledge into the world’s scientific corpus, warning systems and our collective environmental conscience. Such is the goal of UNESCO’s programmes for the promotion of indigenous knowledge systems and the respect for indigenous peoples’ rights to maintain, control, protect and develop their traditional knowledge. 

This reservoir of know-how and expertise contributes to the world’s beauty and wealth and can make all the difference in our attempts to safeguard it. Prior to the twenty-first session of the Conference of the Parties to the United Nations Framework Convention on Climate Change (COP21) in December 2015, UNESCO will host a conference devoted to indigenous peoples’ lessons in resilience to climate change. By listening to how indigenous peoples mobilize and adapt, all of humanity can be strengthened.

MISA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU MZEE SAMUEL LUANGISA NEW YORK NCHINI MAREKANI.

$
0
0
Mchungaji Butiku akiongoza misa ya shukurani na arubaini ya marehemu Mzee Samuel Luangisa iliyofanyika siku ya Jumamosi Aug 8, 2015 Mount Vernon, New York na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki kutoka kila pembe ya Marekani.
Mrs Luangisa, mke wa marehemu akifuatilia misa.
Wanafamilia wakifuatilia misa.
Wajukuu wa marehemu wakifanya onesho la kumenzi babu yao.
Mtoto wa marehemu Mao Luangisa akitoa salamu za shukurani.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania New York Hajji Khamis akiongea machache huku akisisitiza upendo na mshikmano kwenye Jumuiya za Watanzania hususani zile zilizopo nje ya Tanzania kwani kwa kufanya hivyo Jumuiya zitakua imara.
Mchungaji Butiku akiongoza misa.
Wakati wa maakuli. Kwa picha zaidi bofya HAPA

MAONYESHO YA NANE NANE NI SHAMBA DARASA – PINDA

$
0
0

download (6)


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema maonyesho ya siku ya wakulima nchini maarufu kama Nane Nane ni sawa na shamba darasa ambalo washiriki na wananchi wanapata fursa kujifunza mambo mapya kila mwaka.

“Maonyesho ya Nane Nane ni shamba darasa kubwa, nimetembelea mabanda mengi na kubaini kuwa sasa hivi kuna fikra mpya ambazo hazikuwepo wakati wa maonyesho ya mwaka jana,” alisema.

“Maonyesho haya yana umuhimu mkubwa kwani yanatoa fursa kwa wananchi wanaokuja uwanjani kupata ujuzi na maarifa mapya ili waone kwa namna gani wanaweza kuboresha uzalishaji wa mazao au mifugo yao,” aliongeza.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumamosi, Agosti 8, 2015), wakati akiwahutubia wakazi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini alipokuwa akifunga Maonesho ya Wakulima ya Nanenane kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Aliwataka viongozi wa Jumuiya ya Wakulima Tanzania (TASO) ambao ni waandaaji wa maonyesho hayo, wabadili mtazamo wao na mwakani (2016) waweke utaratibu wa kufanya tathmini ya maonyesho hayo kwa kuwahusisha zaidi wakulima na kuwapa nafasi ya kuelezea jinsi walivyonufaika na maonyesho hayo.

Aliwataka pia Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa wanaoshiriki maonyesho hayo nao pia wapewe fursa ya kuelezea jinsi walivyonufaika na maonyesho na kwa kiasi wamesaidia kuwapelekea wananchi wanaowaongoza ujuzi na maarifa hayo.


“Mnapaswa mjiulize ni kwa kiasi gani mmewasaidia wakulima na wafugaji huko vijijini kutumia teknolojia mnazozipata huku kwenye maonyesho. Kama viongozi mnapaswa muwapelee elimu ya kubadili maisha ya mvuvi, mkulima au mfugaji, bila kufanya hivyo, sisi tutabakia kuwa wakubwa tu na hatutasawasaidia wanachi wetu,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amesema hawezi kuhama Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuwataka waliohama baada ya kubwagwa kwenye kinyang’anyiro cha kugombea urais, wajiulize iwapo wataihama nchi wakishindwa kufanikisha malengo yao huko walikohamia.

 “Tulijitokeza wengi kuchukua fomu, watatu wakashindwa kurejesha fomu, wakawa wamejitoa wenyewe. Tulibaki 38 tuliorejesha fomu na kati ya hao wapo waliopita na wengine wakawekwa pembeni. Mimi pia nikawekwa pembeni. Ninaamini kazi tuliyokwenda kuifanya tumeifanya vizuri, tena vizuri sana”.

“Sasa hapa katikati nilikaa kimya kidogo, watu wakaanza kusema kwenye mitandao… Oooh mbona mzee yuko kimya! Au naye anataka kuhamia kule. Sasa niseme nimeachwa huku kwa hiyo nifanyaje? Nihame niende wapi? Hivi, ukihama huku huko unakohamia ukishindwa utahamia wapi tena? Au ndiyo utahama nchi?” alihoji huku akishangiliwa.

Waziri Mkuu alisema CCM ina Ilani yenye sera nzuri, na ndicho chama kinachopaswa kuaminiwa na Watanzania katika Uchaguzi Mkuu ujao na kuongeza kuwa anayo imani na sera ya CCM, hana mashaka kuwa chama hicho kitapata ushindi mnono kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Waziri Mkuu aliipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa jitihada zake katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu, ikiwemo uandikishaji wapigakura ambao wamevuka malengo yaliyowekwa awali.

“Licha ya changamoto nyingi zilizoibuka tangu kuanza kwa uandikishaji wapiga kura nchini kupitia mashine za Biometric Voters Register(BVR), Tume imeandikisha zaidi ya wapiga kura milioni 24 na imevuka malengo yaliyowekwa awali ya kuandikisha watu milioni 22,” alisema.

RAIS KIKWETE AZINDUA KIVUKO CHA MV MAFANIKO NA KUWEKA JIWE LA MSINGI WA NYUMBA ZA MAKAZI NHC MKOANI MTWARA LEO

$
0
0

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Ndugu Nehemia Mchechu akizungumza jambo na Rais  Dkt Jakaya Kikwete mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30za makazi zinazojengwa  na NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,Kulia ni Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais mteule wa chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli wakiondoka eneo la tukio mapema leo mchana
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Ndugu Nehemia Mchechu akizungumza jambo na Rais  Dkt Jakaya Kikwete mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30za makazi zinazojengwa  na NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,Kulia ni Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais mteule wa chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli wakiondoka eneo la tukio mapema leo mchana.

 Sehemu kivuko hicho kilichozinduliwa Rais Dkt Jakaya Kikwete mapema leo mkoani Mtwara.
 Naibu Waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi Mh.John Pombe Magufuli kabla ya uzinduzi wa Kivuko cha Mv Mafanikio mkoani Mtwara mapema leo mchana
 Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais Jakaya Kikwete kabla ya uzinduzi wa kivuko cha Mv Mafanikio mkoani Mtwara mapema leo mchana,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mh.Fatma Salum Ali.
 Rais Dkt Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Fedha,Mh Mwigulu Nchemba ambaye pia alihudhuria sherehe hizo fupi uzinduzi wa kivuko cha Mv Mafanikio mkoani Mtwara mapema leo mchana
 Rais Kikwete akizindua rasmi kivuko cha MV Mafanikio kwenye pwani ya mji wa Mtwara kitachofanya safari kutokea Msemo kuelekea Msangamkuu muda huu mkoani Mtwara.
  Rais Dkt.Jakaya Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kivuko cha Mv Mafanikio kwenye pwani ya mji wa Mtwara kitachofanya safari kutokea Msemo kuelekea Msangamkuu muda huu mkoani Mtwara.Kivuko cha MV Mafanikio kina uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3

  Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwa ameambatana Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli mara baada kushuka kwenye kivuko cha Mv Mafanikio katika kata ya Msanga Mkuu-Mtwara vijijini mara baada ya kuzinduliwa na Rais Jakaya Kikwete,kivuko hicho kina uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi wa Msanga Mkuu-Mtwara vijijini waliofika kwenye uzinduzi wa kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3.
 Baadhi ya wananchi wa Msanga Mkuu-Mtwara vijijini wakishangilia jambo mara baada ya kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3 kuzinduliwa na Rais Dkt Jakaya Kikwete mapema leo mchana mkoani Mtwara.
Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi,Dkt Jonh Pombe Magufuli akizungumza jambo mbele ya wananchi wa Msanga Mkuu-Mtwara vijijini baada ya uzinduzi wa  kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3,Dkt Magufuli amesema kuwa Rais Jakaya Kikwete katika utawala wake ndani ya maiaka kumi amefanikiwa kujenga vivuko vipya 15 na vingine 7 vimekwishakarabatiwa na vinafanya kazi mpaka sasa
 Rais Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza jambo mbele ya wananchi wa Msanga Mkuu-Mtwara vijijini kuzindua kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3
 Bango la mradi huo
 Mkuruegenzi Mkuu wa NHC,Nehemia Mchechu akizungumza jambo mbele ya mgeni rasmi Rais Dkt Jakaya Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na wananchi kwa ujumla katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30 za makazi zinazojengwa  na NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,
 Rais Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi  katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30 za makazi zinazojengwa  na NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Ndugu Nehemia Mchechu pamoja na Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais mteule wa chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akishuhudia tukio hilo.

PICHA NA MICHUZI JR-MTWARA

MAISHA ya sasa. Ni kukimbiza DEATHDAY kuliko kuikimbia BIRTHDAY

$
0
0
Na Mubelwa T Bandio
MAISHA. Nimejifunza kuwa hayako sawa. Na naamini huo ndio usawa wake, kwani humu tuishimo hakuko sawa.
Hivyo, haitakuwa sawa kwa maisha kuwa sawa katika "uwanja" usio sawa kwa waishimo.
Na...
Najua nililoanza nalo na nitakaloendeleza halitaeleweka sawa, na huo ni udhihirisho wa usawa wetu, ambao nao hauko sawa.
Leo, Agosti 10,  ninapoadhimisha mwaka mwingine katika maisha yangu, naitumia siku hii KUAKISI maisha yangu kuliko kusherehekea.
UKWELI ni huu...

Unasoma hapa kwa kuwa "umekua" na kufikia umri wa kusoma na kuelewa. Huu ni umri wa kusherehekea ama kuadhimisha siku kadhaa za kuzaliwa kwako. Na, kama unasoma hapa, jambo moja ninaloweza kukuhakikishia ni kuwa UTAKUFA.

Kwa hiyo, kama wanadamu, haya mawili yanakuwa ya lazima. Ukizaliwa, utakufa. Tofauti ya maisha yetu ipo katikati ya haya mawili.
Kama nilivyowahi kuandika, kuwa UTAKUMBUKWA KWA DESHI YA MAISHA YAKO (rejea hapa),Maishani, nimehudhuria BIRTHDAY(s) na MISIBA mingi tu, na kote nimejifunza mengi kuhusu maisha yetu ya sasa, tuyatakayo na namna tunavyojitahidi kuifikia TAMATI yetu.

Labda funzo kuu nililowahi kushiriki nanyi ni lile nililoliandika HAPA Agosti 22, 2011 baada ya kuhudhuria msiba wa Dada yetu hapa Washington DC.
Maisha yetu ya sasa yanaonekana kuwa ya mchakamchaka, twayakimbiza matumaini na (katika hali ya kushangaza) hata siku zaonekana kuwa fupi kuliko awali.Kabla hujajipanga, ni kesho, ni juma lijalo, ni mwezi ujao na mwaka bila kukamilisha mengi uliyoamini ungependa kuyakamilisha katika muda uliojipangia.

Ninapoangalia miaka hii niliyoishi, naiona kuwa mingi sana. Si kwa kuwa nimeishi mingi kuzidi wote, bali kwa kuzingatia ni mara ngapi nimekuwa nikiamini nimefika mwisho wa uhai.Nakumbuka kusoma makala ya Kaka Eric Shigongo, iliyosema kuuona mwaka mpya ni nafasi ya ziada. Na naamini katika hilo.

Mara kadhaa (na ni zaidi ya moja) nimekuwa kwenye nafasi ya kuona kama kesho ilikuwa mbali na isiyofikika kwangu nikiwa hai. Siku ambayo hunijia akilini zaidi juu ya hilo, ni HII Lakini leo wasoma niandikalo.
NI NAFASI YA ZIADA katika kuikimbiza "siku ya mwisho"

Nikirejea kwenye kichwa cha bandiko hili,fikra kwamba maisha yetu ya sasa ni kama kuikimbiza kesho kuliko kuifikiria leo na hata jana, kunatufanya tuonekane kuyawaza yajayo kuliko tulikotoka.Ni hili linalonifanya niamini kuwa, maisha yetu ya sasa yamewekeza katika yajayo. Na kama nilivyoeleza kabla, jambo pekee ambalo sote tuna hakika nalo, ni kifo.

Na ndio maana nikasema, MAISHA ya sasa. Ni kukimbiza DEATHDAY kuliko kuikimbia BIRTHDAY

Anyway!
Nisijesahau kujitakia EARTHday njema.
Najua fika kuwa hongera na shukrani za maisha yangu nazipokea kwa sababu ni Mungu aliyeniweka hai mpaka sasa.Na ndiye aliyenipa WAZAZI wangu ambao sina ninanloweza kueleza kuhusu nafasi yao maishani ikalingana na walilotenda.

Labda jambo moja tu, kwamba walinibariki na NDUGU ambao uwepo wao umekuwa kama egemeo la kukua kwangu. Hawa ndugu wameniwezesha kuambatana na JAMAA ambao kwa muongozo wa ndugu, wameniwezesha kuwa nilivyo. Si unakumbuka kuwa Twachagua maongezi, maongezi yachagua mawazo na mawazo yatuchagulia jamii? (Isome hapa)
Nina maRAFIKI ambao wananisaidia katika kukua kwangu. Hawa nawajumusha na wale wanajiona kama maadui kwangu, ambao mara nyingi wamenifanya kujitahidi kukamilisha mambo ili wasipate la kusema.
Hahahahahaaaaaaaaaaaaaaaa
Kipekee, namshukuru mke wangu mpenzi Esther na wanangu Paulina na Annalisa kwa kuwa wavumilivu kwenye harakati zangu (nyingine hazielewekagi yaani).
 
Hahahaaaaaaaaaaaaaa
Ni siku nyingine ya kukumbuka kuzaliwa kwangu. Nalikaribia hitimisho la maisha, na nikilijongelea, najitahidi kukamilisha dhumuni yangu ya kuwa humu duniani.

Mungu akubariki na kuonyeshe namna muafaka ya kutenda kila lililo jema, kadhi uikaribiavyo.
 

MADEREVA WA BODABODA WAENDELEA KUSAJILIWA KWENYE MFUMO MAALUM WA KUMBUKUMBU

$
0
0

 Waendesha bodaboda mkoani Mbeya wakiwa katika maandamano kuelekea kwenye Uwanja wa CCM Iromba kwenye uzinduzi wa mradi wa kuwasajili na kuwapatia sare maalumu za kuwatumbua.



 Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mh. Nyerembe Mnase akihutubia hadhira kubwa ya waendesha bodaboda katika uzinduzi wa mradi wa kuwasajili katika mfumo wa kumbumbuku pamoja na kuwapatia sare maalumu.



 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni ya Matangazo na Masoko ya Alternative Communications Bw. Edward Mgaya akizungumza na hadhira kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa kuwasajiri waendesha bodaboda mkoani Mbeya.



 Meneja wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kanda ya Nyasa Bw. Minja akitoa salam za kampuni hiyo kama mdhamini wa mradi wa kuwasajili waendesha bodaboda katika mfumo maalumu wa kumbukumbu.


Ule mchakato kabambe wa kuwasajili waendesha bodaboda katika mfumo maalum wa kumbukumbu (database) na kuwakabidhi sare umeendelea kushika kasi ambapo wakati utekelezaji ukiendelea jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita uzinduzi wa mradi huo umefanyika kwa mbwembwe kubwa jijini Mbeya ambapo maelfu ya waendesha bodaboda jijini humo walijitokeza kwa shamrashamra tele kuuzindua mradi huo.

Uzinduzi huo wa aina yake uliofanyika katika Uwanja wa CCM Iromba jijini Mbeya, ni mwendelezo wa mchakato unaofanywa na kampuni ya mawasiliano, masoko na matangazo ya Alternative Communication ya jijini Dar es Salaam, ikishirikiana na jeshi la polisi na kudhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, lengo likiwa kuwasaidia waendesha bodaboda na abiria wanaotumia usafiri huo kutambulika kwa urahisi inapotokea wamehusika katika matukio ya kihalifu.

Akiuzindua mradi huo mgeni rasmi katika tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mh. Nyerembe Mnase, aliwapongeza waendesha bodaboda hao kwa namna walivyoupokea mradi huo, na ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuakikisha wanawapa chama cha UWABOM chumba kimoja cha ofisi katika soko jipya la kimataifa la Mwanjelwa, na kwamba mradi wa kuwatambua bodaboda utausaidia uongozi wa jiji kupata takwimu sahihi, wakati ambapo jiji hilo linaandaa mkakati wa kuwatafutia eneo la viwanja vya ujenzi kwa ajili ya waendesha bodaboda. 

“Kwa hatua mliyofikia, tutawatafutia eneo la viwanja vya ujenzi ili muendelee zaidi kwa kuwa na makazi bora. Lakini nawasisitiza muendelee kuwa watii wa sheria barabarani, na kuwafichua wale wasio waaminifu wanaoshiriki katika vitendo vya kihalifu nyuma ya mgongo wa bodaboda.” Alisema. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Alternative Communication Bw. Edward Mgaya, aliwamwagia sifa waendesha bodaboda wa mkoani Mbeya kwa namna walivyofanikiwa kwa kiwango kikubwa kuutekeleza mradi huo, hadi kufikia hatua ya kufungua SACCOS ya wanachama wa Chama cha Wamiliki na Waendesha Bodaboda na Bajaj mkoani humo (UWABOM). 

Naye Katibu wa UWABOM Bw. Msumba Mdesa, katika risala kwa mgeni rasmi, uliushukuru mradi huo wa kuwasajili na kupewa sare, na kuongeza kuwa sare hizo zimewafanya wafanikiwe kujenga mshikamano wenye nia ya kujikwamua kwenye janga la umasiki, na wanachama kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kutii sheria bila shuruti.

Mradi wa kuwasajili waendesha bodaboda na kuwapatia sare maalum umekuja kufuatia madai kuwa baadhi yawaendesha bodaboda wasio kuwa waaminifu hujihusisha katika matukio ya kihalifu au kutumiwa na wahalifu kuvunja amani na kupotea bila ya kutambulika.

Kupitia mradi huu waendesha bodaboda waliosajiliwa pia watapata faida ya kupewa huduma ya bima ya afya, mafunzo ya usalama barabarani na  Ujasiriamali, huku kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ambayo ndio wadhamini wa mradi, ikiwa imewatengea bodaboda kifurushi maalumu cha simu ambacho kina dakika 30 za maongezi, sms 500 na mb 100 za intanet kwa gharama ya shilingi 500 tu, na kikidumu kwa muda wa mwezi mmoja.

RADIO 5 YASHINDA NAFASI YA KWANZA MAONYESHOA YA NANENANE ARUSHA

$
0
0
SAM_4950Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera Mahusiano na Uratibu Dkt.Mary Nagu akiwa anamkabidhi kikombe Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya mara baada yakituo cha Radio5 kutangazwa washindi wa kwanza kwa upande wa Radio na wapili katika sekta nzima ya mawasiliano katika kilele cha sherehe za sikukuu ya Wakulima nanenane na maonyesho ya kilimo Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika katika uwanja wa maonyeshoThemi Mkoani Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_4952Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya wa Radio 5 akiwa ameshikilia kikombe walichoshinda katika maonyesho ya nanenane
SAM_4977Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya akiwa na timu yake ya ushindi mara baada ya kituo hicho kutangazwa washindi wa kwanza kwa upande wa Radio na wapili katika sekta nzima ya mawasiliano katika kilele cha sherehe za sikukuu ya Wakulima nanenane na maonyesho ya kilimo Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika katika uwanja wa maonyeshoThemi Mkoani Arusha

ALHAJ MWINYI: FUNDISHENI SAYANSI KWA KISWAHILI

$
0
0
 Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akisisitiza jambo wakati akifungua Maonyesho ya 5 ya Sayansi kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Young Scientists Tanzania (YST) Dk. Gosbert Kamugisha akimtambulisha Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwa Balozi wa Kenya nchini Tanzania Chirau Ali Mwakwere kabla ya kufungua maonyesho hayo mwishoni mwa wiki.

Na Daniel Mbega wa brotherdanny.com
RAIS mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, amewataka walimu katika shule za msingi na sekondari kutumia lugha ya Kiswahili kufundisha sayansi, kwani lugha hiyo inaeleweka vizuri.

Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya Tano ya Sayansi kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini jijini Dar es Salaam jana, Alhaj Mwinyi amesema Kiswahilini lugha inayoeleweka vizuri, si kwa wanafunzi tu,bali hata kwa watu wengine, hivyo ni vyema walimu wakaweka mkazo katika kuitumia kwenye masomo ya sayansi.

“Nimepita kwenye maonyesho haya, baadhi ya wanafunzi walikuwa wananiuliza ‘tukueleze kwa Kiswahili au kwa Kiingereza’, nikasema tumieni lugha yoyote tu. Wengine wamenieleza Kiingereza na wengine Kiswahili.
Balozi wa Kenya nchini, Chirau AliMwakwere (wa pili kushoto) na Balozi wa Ireland nchini, Fionnuala Gilsenan wakisikiliza kwa makini maelezo ya wanafunzi walioshiriki maonyesho hayo. Nyumaya Balozi Gilsenan ni Dk. Gosbert Kamugisha, Mkurugenzi Mtendaji wa Young Scientists Tanzania. 

MWIGULU NCHEMBA APANGA KIKOSI CHA USHINDI CHA CCM.


USHINDI WA VETA KATIKA MAONESHO YA KILIMO (NANENANE) KITAIFA

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kusini Mashariki, Bw. Joseph Kibehele kikombe cha ushindi baada ya VETA kuibuka Mshindi wa Kwanza katika eneo la Taasisi za Mafunzo na Utafiti kwenye Kilele cha Maonesho ya Kilimo (Nanenane) kitaifa,  iliyofanyika viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi, tarehe 8 Agosti, 2015.
 Wafanyakazi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wakiwa katika picha ya pamoja kufurahia ushindi baada ya VETA kuwa Mshindi wa Kwanza kwenye eneo la Taasisi za Mafunzo na Utafiti katika kilele cha Maonesho ya Kilimo (Nanenane) Kitaifa, kwenye viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi. Aliyeshika kikombe ni Mwenyekiti wa Bodi ya VETA Kanda ya Kusini Mashariki, Br. Sixtus Luoga.
 Wafanyakazi wa VETA wakishangilia kikombe cha ushindi baada ya VETA kutunukiwa Ushindi wa Kwanza kwenye eneo la Taasisi za Mafunzo na Utafiti katika kilele cha Maonesho ya Kilimo (Nanenane) Kitaifa, kwenye viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi.

MAISHA YA SASA, NI KUKIMBIZA DEATHDAY KULIKO KUIKIMBIA BIRTHDAY

$
0
0
Na Mubelwa  Bandio
MAISHA. Nimejifunza kuwa hayako sawa, na naamini huo ndio usawa wake, kwani humu tuishimo hakuko sawa.

Hivyo, haitakuwa sawa kwa maisha kuwa sawa katika "uwanja" usio sawa kwa waishimo.
Na...
Najua nililoanza nalo na nitakaloendeleza halitaeleweka sawa, na huo ni udhihirisho wa usawa wetu, ambao nao hauko sawa.

Leo, Agosti 10,  ninapoadhimisha mwaka mwingine katika maisha yangu, naitumia siku hii KUAKISI maisha yangu kuliko kusherehekea.
UKWELI ni huu.....

Unasoma hapa kwa kuwa "umekua" na kufikia umri wa kusoma na kuelewa. Huu ni umri wa kusherehekea ama kuadhimisha siku kadhaa za kuzaliwa kwako.

Na, kama unasoma hapa, jambo moja ninaloweza kukuhakikishia ni kuwa UTAKUFA.

Kwa hiyo, kama wanadamu, haya mawili yanakuwa ya lazima. Ukizaliwa, utakufa, tofauti ya maisha yetu ipo katikati ya haya mawili.

Kama nilivyowahi kuandika, kuwa UTAKUMBUKWA KWA DESHI YA MAISHA YAKO (rejea hapa).

Maishani, nimehudhuria KUMBUKUMBU ZA KUZALIWA WATU MBALIMBALI  na MISIBA mingi tu, na kote nimejifunza mengi kuhusu maisha yetu ya sasa, tuyatakayo na namna tunavyojitahidi kuifikia tamatuti yetu.

Labda funzo kuu nililowahi kushiriki nanyi ni lile nililoliandika hapa Agosti 22, 2011 baada ya kuhudhuria msiba wa Dada yetu hapa Washington DC.
Maisha yetu ya sasa yanaonekana kuwa ya mchakamchaka, twayakimbiza matumaini na (katika hali ya kushangaza) hata siku zaonekana kuwa fupi kuliko awali. 

Kabla hujajipanga, ni kesho, ni juma lijalo, ni mwezi ujao na mwaka bila kukamilisha mengi uliyoamini ungependa kuyakamilisha katika muda uliojipangia.

Ninapoangalia miaka hii niliyoishi, naiona kuwa mingi sana, si kwa kuwa nimeishi mingi kuzidi wote, bali kwa kuzingatia ni mara ngapi nimekuwa nikiamini nimefika mwisho wa uhai.

Nakumbuka kusoma makala ya Kaka Eric Shigongo, iliyosema kuuona mwaka mpya ni nafasi ya ziada, na naamini katika hilo.

Mara kadhaa (na ni zaidi ya moja) nimekuwa kwenye nafasi ya kuona kama kesho ilikuwa mbali na isiyofikika kwangu nikiwa hai, siku ambayo hunijia akilini zaidi juu ya hilo, ni  hii..

Lakini leo wasoma niandikalo.
NI NAFASI YA ZIADA katika kuikimbiza "siku ya mwisho"
Nikirejea kwenye kichwa cha bandiko hili,fikra kwamba maisha yetu ya sasa ni kama kuikimbiza kesho kuliko kuifikiria leo na hata jana, kunatufanya tuonekane kuyawaza yajayo kuliko tulikotoka.

Ni hili linalonifanya niamini kuwa, maisha yetu ya sasa yamewekeza katika yajayo na kama nilivyoeleza kabla, jambo pekee ambalo sote tuna hakika nalo, ni kifo.

Na ndio maana nikasema, maisha ya sasa,ni kukimbiza DEATHDAY kuliko kuikimbia BIRTHDAY.

Nisijesahau kujitakia EARTHday njema.
Najua fika kuwa hongera na shukrani za maisha yangu nazipokea kwa sababu ni Mungu aliyeniweka hai mpaka sasa. 

Na ndiye aliyenipa WAZAZI wangu ambao sina ninanloweza kueleza kuhusu nafasi yao maishani ikalingana na walilotenda.

Labda jambo moja tu, kwamba walinibariki na NDUGU ambao uwepo wao umekuwa kama egemeo la kukua kwangu. Hawa ndugu wameniwezesha kuambatana na JAMAA ambao kwa muongozo wa ndugu, wameniwezesha kuwa nilivyo. 

Si unakumbuka kuwa Twachagua maongezi, maongezi yachagua mawazo na mawazo yatuchagulia jamii? (Isome hapa)
Nina maRAFIKI ambao wananisaidia katika kukua kwangu. Hawa nawajumusha na wale wanajiona kama maadui kwangu, ambao mara nyingi wamenifanya kujitahidi kukamilisha mambo ili wasipate la kusema.

Hahahahahaaaaaaaaaaaaaaaa
Kipekee, namshukuru mke wangu mpenzi Esther na wanangu Paulina na Annalisa kwa kuwa wavumilivu kwenye harakati zangu (nyingine hazielewekagi yaani)

Hahahaaaaaaaaaaaaaa
Ni siku nyingine ya kukumbuka kuzaliwa kwangu. Nalikaribia hitimisho la maisha, na nikilijongelea, najitahidi kukamilisha dhumuni yangu ya kuwa humu duniani.

Mungu akubariki na kuonyeshe namna muafaka ya kutenda kila lililo jema, kadhi uikaribiavyo.

NCCR-MAGEUZI WAANZA KUSHAMBULIA JIMBO LA VUNJO,WAWATAMBULISHA WAGOMBEA WA NAFASI YA UDIWANI

$
0
0
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi taifa ,Hemed Msabaha akizungumza wakati wa mikutano wa kutamburisha wagombea wa nafasi ya udiwani inayofanyika katika jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya viongozi wa NCCR-Mageuzi jimbo la Vunjo wa kiwa katika moja ya mikutano hiyo kata ya Makuyuni.

Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi taifa na Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia ,Bw Hamis Athuman akitoa salamu za mwenyekiti huyo wakati wa mkutano wa utamburisho wa wagombea wa nafasi za udiwani kupitia chama hicho.

Baadhi ya wakazi wa kata ya Makuyuni wakiwasikiliza viongozi wa chama hicho.(hawako pichani).

Aliyekuwa kada wa Chama cha TLP,Stanley Temba akiwa ameibukia katika jukwaa la NCCR-Mageuzi akizungumza katika moja ya mikutano ya Utamburisho wa wagombea wa nafasi ya Udiwani katika kata zilizoko ndani ya jimbo la unjo.
Aliyekuwa Diwani kupitia chama cha TLP,Yolanda Lyimo akizungumza katika jukwaa la chama cha NCCR-Mageuzi.
Yolanda Lyimo akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya njia Panda.

Baadhi ya wananchi katika jimbo la Vunjo wakiitikia salamu za vyama vinavyounda UKAWA.

Kikundi cha sarakasi kikitoa burudani katika mikutano hiyo.
Baadhi ya wananchi katika kata ya Njia Panda wakifuatilia mkutano wa hadhara uliolenga kumtamburisha mgombea wa nafasi ya udiwani katika kata hiyo.
Baadhi ya wananchi katika kata ya Njia Panda.
Viongozi wa chama cha NCCR-Mageuzi wakicheza mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Njia Panda.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.


BONDIA LULU KAYAGE AIBUKA KIDEDEA AFRIKA YA KUSINI

$
0
0

BONDIA wa Kike Lulu Kayage mwishoni mwa wiki iliyopita alibuka kidedea nchini Afrika ya kusini baada ya kumdunda vibaya   Lizbeth Sivhaga wa nchini humu huu ni mpambano wake wa kwanza Lulu kucheza nje ya nchi na kufanikiwa kushinda kwa T.K.O ya raundi ya pili mchezo uho ulioanza kwa kasi ya mashambulizi ya uku na kule kila mmoja kutaka kumpiga mwenzie raundi za awaliata hivyo ilivyofika raundi ya pili bondia Lulu Kayage alimwelemea sana mpinzani wake kwa makonde mfululizo na wasaidizi wake kumuokoa kwa kumtupia taulo hivyo kusababisha Lulu kushinda T.K.O ya raundi ya pili.

ushindi wa Llulu Kayage ulichagizwa na kocha maarufunchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambapo siki mbili kabla ya kuondoka nchini alimzawadia vifaa mbalimbali vya mchezo wa masumbwi na kumwaidi ushindi kwa asilimia zote.

bondia huyo anatarajia kurudi nchini agost 11 kwa ajili ya maandalizi ya mapambano yake mengine ya kimataifa wakati uho uho bondia Ramadhani Shauri amepoteza mpambano wake kwa kupigwa K.O ya raundi ya nne na bondia mzoefu Philip Ndlovu wa Afrika ya Kusini ambapo mpambano uho wa raundi nane ulijikuta ukisha katika raundi ya nne.
Bondia Lulu Kkayage akiwashukuru mashabiki walio udhulia kwa kuwapigia magoti na kuwapungia mikono baada ya kumchakaza bondia Lizbeth Sivhaga wa Afrika ya Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita Picha na SUPER D BOXING NEWS


Refarii akiwa katikati uku akiwashika mikono mabondia Llulu Kayage na Lizbeth Sivhaga wa Afrika kusini kwa ajili ya kutangaza mshindi Lulu alishinda kwa TKO ya raundi ya pili kushoto ni Yassini Abdallah
Picha na SUPER D BOXING NEWS.
Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' akimnyoosha mkono juu bondia Lulu Kayage baada ya kuibuka mshindi.

 
Yassin Abdallah 'Ostadh' akimwinua juu mkono baada ya kushinda kwa T.K.O ya raundi ya pili.


TPDC YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE LINDI

$
0
0

 Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Mhe. Hawa Ghasia (MB) (kulia), akiweka sahihi alipotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania katika Wiki ya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) eneo la Ngongo, Mkoani Lindi.
 Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Mhe. Hawa Ghasia (MB) (kulia), akipokea zawadi kutoka Meneja wa Mawasiliano TPDC, Bi. Marie Msellemu (kushoto) alipotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika Wiki ya Maonesho ya Wakulima (Nanenane).
 Mhandisi wa Petroli, Yusufu Risasi, (kulia) akitoa maelezo ya kitalaam kwa watu waliotembelea banda la Shirika la Maendeleo Petroli Tanzania kujionea shughuli zinazo fanywa na Shirika la TPDC

  Afisa Masoko wa TPDC, Elias Mziray (kulia), akitoa maelezo ya shughuli za Shirika kwa Wananchi waliotembelea banda la Shirika katika Wiki ya Maonesho ya Wakulima.
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live




Latest Images