Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 603 | 604 | (Page 605) | 606 | 607 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Mkurungezi wa Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA, Dk.Ally Simba akizungumza na waandishi wa habari juu ya semina ya kuwapiga brashi wa wasanii wa bongo Movie leo jijini Dar Dar es Salaam.
   Afisa Mwandamizi Mkuu wa Kitengo cha Watumiaji wa Huduma za Bidhaa za Mawasiliano wa TCRA,Thadeo Ringo akizungumza na baadhi na wasanii waliohudhuria semina hiyo hawapo pichani iliyoyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi  Makao Makuu,Kitengo cha Kuzuia Uhalifu ,Kamisheni ya Polisi Jamii,David Mwakalukwa akizungumza na wasaanii juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii katika semina ya wasanii iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Msanii Mkongwe wa Filam nchini,Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’ akichangia maada katika semina ya kuwanoa wasanii juu ya matumizi ya mitandao katika semina iliyoandaliwa na TCRA leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wasanii walioshiriki semina iliyoandaliwa na TCRA ,leo jijini Dar es Salaam.
  (picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa kilomita 60, hafla hiyo imefanyika jana Agosti 7 2015 mkoani Lindi.Wengine pichani ni Balozi wa Kuwait Jassem Ibrahim Al Najem,Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait, Abrahman Al- Hashim,Mkuu wa Mkoa wa Pwan, Eng. Evarist Ndikilo, wengine kushoto ni Waziri wa ujenzi Mhe.John Pombe Magufuli, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe.Mwantumu Mahiza.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazia Dkt.Jakaya Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali mara baada ya kufunguarasmi barabara ya Ndundu - Somanga.
   Rais Kikwete akimshukuru  Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait ,Abrahman Al Hashim mara baada kuweka jiwe la msingi wakati wa sherehe fupi zilizofanyika   kwenye kijiji cha Marendego ,wakati wa ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
   Rais wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa pamoja na mkewe Salma  Kikwete akimwagia maji mti wa kumbukumbu alioupanda baada ya ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga mkoani Lindi.
  Wafadhili wa ujenzi wa barabara ya Ndundu-Somanga, Balozi wa Kuwait Jassem Ibrahim Al Najim na   Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait ,Abrahman Al Hashim mara kwa pamoja wakishiriki kupanda mti wakati wa sherehe fupi zilizofanyika   kwenye kijiji cha Marendego ,wakati wa ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
   Rais Kikwete akiwasalimia na kuwaaga wananchi wa kijij cha Nangurukulu na kumtambulisha Mgomea Urais kwa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akielekea mkoani Lindi.
  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akijitambulisha kwa wakazi wa mji wa Nangukurulu,mara baada ya sherehe fupi za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga kukamilika mkoani Lindi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mgombea mteule wa Urais wa chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Marendengo Wilayani Kilwa mkoani Lindi kufungua barabara ya Ndundu-Somanga yenye urefu wa kilometa 6.Barabara hiyo imejengwa na Serili ya Tanzania kwa kushirikiana na Ufadhili wa Mfuko wa Kuwait pamoja na mfuko wa OPEC .
   Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa na  Mkuu wa mkoa wa Lindi,Mh.Mwantumu Mahiza mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Marendengo Wilayani Kilwa mkoani Lindi kushiriki ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga yenye urefu wa kilometa 6.Barabara hiyo imejengwa na Serili ya Tanzania kwa kushirikiana na Ufadhili wa Mfuko wa Kuwait pamoja na mfuko wa OPEC .
   Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa,Mh.Bernad Membe mara baada ya kuwasilia katika kijiji hicho  Marendengo,ambapo sherehe za uzinduzi wa barabara ya Ndundu-Somanga zilifanyika na mgeni Rasmi alikuwa ni Rais Dkt Jakaya Kikwete.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na wakulima na wananchi wa  mikoa ya Kanda ya Nyanda za juu kusini wakati akifunga maonesho ya sherehe za wakulima Nanenane katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Agost 8 ,2015b .Picha Jamiimojablog.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza katika sherehe hizo za wakulima Nanenaneb Kanda ya Nyanda za juu kusini katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
  wananchi na wakulima wa mikoa ya Kanda ya Nyanda za juu kusini wakimsikiliza Waziri Mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani)  wakati akifunga maonesho ya sherehe za wakulima Nanenane katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Agost 8 mwaka huu.
    
  Na EmanuelMadafa,Mbeya
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mchakato wa kumpata mgombea wa  urais kupitia chama cha mapinduzi  (CCM) umekwenda vizuri hivyo kwa wale wale ambao hawakufikia malengo nivema wakakubali  matokeo kwani ilikuwa lazima  mmoja apatikane.
  Amesema   busara nzuri ni kukubali matokeo hayo  badala ya kuhama chama kama walivyo fanya baadhi ya makada wengine wa chama hicho.
  Waziri Mkuu Pinda ametoa kauli hiyo mkoani mbeya wakati akifunga maadhimisho ya sherehe  za wakulima Nanenane kwa mikoa ya kanda za nyanda za juu kusini katika viwanja vya John Mwakangale.
  Amesema, katika mchakato wa kuomba nafasi ya urais wagombea walikuwa zaidi ya 40 lakini aliyekuwa akihitajika mmoja hivyo ni vema wengine ambao majina yao yaliondolewa kutokana na kutokidhi vigezo mbalimbali vya chama  wangekubali matokeo kuliko kuhama chama.
  Amesema yeye kwa upande wake ameridhika na mchakato huo hivyo haoni sababu ya kuondoka  ndani chama  hicho kwani ndicho  chama kilicho mfikisha hapo alipofikia sasa nakutumikia nafasi hiyo ya uwaziri Mkuu kwa miaka 8  hadi anakoma utumishi wake.
  Pinda amesema kama kuna mambo ya kusahishana atafanya hivyo akiwa ndani ya chama cha mapinduzi  kwani hata huko ambako wengine wamehamia hakuko salama na kunachangamoto nyingi hiyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kumchagua kiongozi bora atakaye wafikisha mahala pazuri.
  Hata hivyo, aliwataka wanachama wa CCM  kutambua kuwa sera nzuri za vyma ndizo zitakazo saidia kuwashawishi watu kukikubali chama hivyo hakuna sababu ya kuhama zaidi ni kuziboresha sera zilizopo ili watu wazipende na kuzikubali
  Katika hotuba yake waziri Mkuu Pinda amewataka viongoizi wa mikoa hiyo ya kanda za nyanda za juu kusini  kuhakikisha wanajikita katika kuwasaidia wakulima na wafugaji wadogo wadogo ili kuwainua kiuchumi badala ya kushughulika na wakulima wakubwa pekee.
  Amesema uchumi wa Tanzania unakuwa lakini bado hauendani na hali hali ya maisha ya watanzania hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kupigana na hali ya umasikini  sanjali na kuondoa utofauti  ya aliye nacho na asiye nacho.
  Hata hivyo waziri Mkuu Pinda amesema anajivunia katika kipindi cha utumishi ndani ya serikali ya rais kikwete  kwa kuweza kuinua sekta ya kilimo kwani nchi imeweza kupeleka tanni 500 za mahindi katika nchi jirani ya Ethiopia, Sudani tanni 500, Burundi tanni 500 , Malawi tanni 500 na nchi nyingine za jirani hivyo hii ni hatua kubwa sana .

  Waandishi wa habari wakiwa kazini.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi zawadi kwa washindi wa manesho hayo katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Agost 8 mwaka huu.  Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipotembelea baadhi ya mabanda ya waoneshaji katika sherehe hizo za wakulima Nanenane .

  0 0

  Kijana ABEL MACHANG'A, mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa Ukonga Mombasa Jijini Dar es Salaam, ambae anasumbuliwa na maradhi ya macho, akiwa amejipumzisha nyumbani kwao baada ya kuzungumza na waandishi wa habari ili kuomba msaada wa kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
    ..................................................................

  Kijana Abel mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa Ukonga Mombasa jijini Dar es Salaam anakabiliwa na maradhi ya macho na mishipa ya fahamu hali iliyosababisha apoteze uwezo wa kuona, na hivyo kuhitaji msaada wa wasamaria wema ili apelekwe nchini India kwa matibabu zaidi.

  Ama kweli kabla hujafa hujaumbika! Kijana ABEL MACHANG’A aliyezaliwa miaka 23 iliyopita alikuwa na uwezo wa kuona kama kawaida na alisoma mpaka kidato cha nne na baadaye kujiunga na elimu ya biashara katika chuo cha biashara cha CBE cha jijini Dar es Salaam.

  Lakini hivi sasa kijana huyo haoni tena baada ya kupata maradhi ya macho yaliyosababisha macho yake kuvimba na kutoka nje licha ya kupatiwa matibabu. 
  Baba wa kijana huyo amesema jitihada za kutibiwa nchini zimeonekana kutokuwa na mafanikio na kuomba wasamaria wema na mashirika mbalimbali yajitokeze kumsaidia kijana huyu gharama za matibabu takribani milioni Hamsini.

  Kwa yeyote atakayeguswa na maradhi ya kijana huyu, awasiliane na Chumba cha Habari Clouds Tv Mikocheni jijini Dar es Salaam au awasiliane na baba mzazi wa kijana huyo kwa namba 0713 275740 au 0784 275740.


  0 0

   Muonekano wa viwanja vya Mabano vilivyopimwa na Taasisi ya UTT-PID kwa ushirikiano na Halmashauri vilivyopo Manispaa ya Lindi.
  Zaidi ya viwanja 2,500 vilipimwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali kama vile Makazi, Biashara, Maeneo ya Umma na sehemu za kupumzika.  
   
   Akielezea Afisa Masoko Bi. Kilave Atenaka alisema kuwa kwa sasa wanaendesha huduma ya uuzwaji wa Fomu kwa ajili ya Viwanja, pia wanatarajia kuanza kuuza kwa umaa na taasisi mbali mbali miradi mipya ikiwemo wa Tundwi Songai – Kigamboni jijini Dar es Salaam na ule wa Kingorwila, Morogoro.
  Aidha Bi. Kilave alitumia wito huo kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi ndani ya banda hilo kujipatia elimu mbali mbali zitolewazo na taasisi hiyo hapa nchini.
  Toka kuanzishwa kwake Taasisi ya UTT-PID imejikita sana katika upimaji wa maeneno katika mikoa mbalimbali kwa kushirikiana na Halmashauri tofauti nchini. Miradi mikubwa kama ya Bukoba ambapo viwanja zaidi ya 5,000 vilipima kuuzwa, Halmashauri ya Sengerema kwa ushirikiano na Taasisi ilipima zaidi ya viwanja 1,200 na uuzaji pamoja na uwekezaji katika Miundombinu husika unaendelea kwa kasi. 

  Pia Taasisi imewekeza katika miradi binafsi kama vile eneo la Mapinga katika wilaya ya Bagamoyo huku ikatarajia uwekezaji mkubwa zaidi katika mikoa ya Morogoro , Arusha, Dar es Salaam, Maswa, Pwani, Maswa na Ruvuma.


  Maafisa Masoko wa UTT-PID, Bi Kilave Atenaka (katikati) na  Bi. Mary Minja (kwanza kulia) wakiongea na mteja aliyefika banda lao lililo chini ya wizara ya Fedha katika Maonyesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
  Afisa Masoko UTT-PID, Bi Kilave Atenaka akihudumia mteja katika banda lao lililo chini ya wizara ya Fedha katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
  Afisa Masoko UTT-PID, Bi Kilave Atenaka akihudumia mteja katika banda lao lililo chini ya wizara ya Fedha katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni  Mhe Paul Makonda alipowasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambako Wasani wa fani mbalimbali waliandaa hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Mhe. John Pombe Magufuli alipowasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambako Wasani wa fani mbalimbali waliandaa hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe January Makamba  alipowasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambako Wasani wa fani mbalimbali waliandaa hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Ruge Mutahaba, mratibu mkuu wa hafla  alipowasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambako Wasani wa fani mbalimbali waliandaa hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na wasanii  alipowasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambako Wasani wa fani mbalimbali waliandaa hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na msanii na kiongozi wa bendi Mapacha watatu  Jose Mara alipowasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambako Wasani wa fani mbalimbali waliandaa hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mona Lisa mmoja wa wasanii  walioratibu hafla alipowasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambako Wasani wa fani mbalimbali waliandaa hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na msanii JB  alipowasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambako Wasani wa fani mbalimbali waliandaa hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015. Kushoto kwa JB ni Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Mhe. John Pombe Magufuli
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo ya hafla itavyokuwa baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambako Wasani wa fani mbalimbali waliandaa hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na rasmi na  Wasanii wa fani mbalimbali katika  hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
   Wasanii wa fani mbalimbali wakimkaribisha JK katika  hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
    Wasanii wa fani mbalimbali wakimkaribisha JK katika  hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
    Wasanii wa fani mbalimbali wakimkaribisha JK katika  hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
    Wasanii wa fani mbalimbali wakimkaribisha JK katika  hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
    Wasanii wa fani mbalimbali wakimkaribisha JK katika  hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
    Wasanii wa fani mbalimbali wakimkaribisha JK katika  hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
    Wasanii wa fani mbalimbali wakimkaribisha JK katika  hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015

    Wasanii wa fani mbalimbali wakimkaribisha JK katika  hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
    Wasanii wa fani mbalimbali wakimkaribisha JK katika  hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
    Wasanii wa fani mbalimbali wakimkaribisha JK katika  hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
    Wasanii wa fani mbalimbali wakimkaribisha JK katika  hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
    JK akipata picha na Mgombea Ubunge Moshi Mjini Davies Mosha na mwendesha talk show Mboni Mashimba kwenye hafla ya Wasanii wa fani mbalimbali ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
   JK akisalimiana na msani Cassim Mganga
   Ommy Dimples akipata selfie na JK
   Wasanii wakipata selfie na JK
   Kila msanii aliomba selfie na JK
   selfie
   JK akipata selfie toka kwa
  Meza ya Mzee Yusuf na mkewe na wadau wakubwa wa muziki nchini
  Meza ya Mzee Walter Bgoya ya familia yake
  Meza ya Jose Mara na Kelvin Twissa
  Selfie zikiendelea
  JK na wakongwe Nyoshi el Sadat na Komando Hamza Kalala
  Kila kona selfie
  JK akiendelea kusalimiana na wadau wa sanaa 
  JK akipeana mikono na Joh Makini
  Selfie zimenoga meza ya kina Adam Mchomvu na Joh Makini
  Adam Mchomvu akitoa special thanks kwa Prezidaa
  JK akimsalimia Nikki wa Pili 
  Meza ya Fina Mango
  Jose Mara akinogesha shughuli. Huyu jamaa noma
  Diamond akitoa shukrani kwa niaba ya wasanii wenzie
  Jose Mara jukwaani katika Big Screen
  JK na King Majuto
  JK akiongea na King Majuto na Mzee Shilo
  JK akiwa na Bi Shakila Saidi
  Steve Nyerere akiwa kavamia meza kuu
  Steve Nyerere akiosha nyota
  Diamond akisalimia meza Kuu
  Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na mwimbaji nyota Patricia Hilary
  Mshindi wa Big Brother Africa Idriss Sultan akisalimia meza kuu
  Mshindi wa Big Brother Africa Idriss Sultan akisalimiana na Dkt Magufuli
  Mshindi wa Big Brother Africa Idriss Sultan akificha uso
  Mwanamuziki nyota Ali Kiba akitoa shukrani zake kwa JK
  Vanessa Mdee akiwa jukwaani
  Meza Kuu
  Dkt Magufuli na Nape Nnauye wakifanya mambo jukwaani
  JK akifurahi na wasanii
  JK akipongezwa na King Majuto kwa kusakata rhumba
  JK akipompongeza Dkt Magufuli kwa kupiga tumba kwa ustadi mkubwa
  JK akisalimiana na mwigizaji nguli Ray Kigosi
  Dkt Magufuli akisalimiana na Bashe
  JK na msanii wa Hip Hop mkongwe Fid Q
  JK akicheza na Vanessa Mdee
  Wasanii wakongwe wakiserebuka
  JK akifurahi na wasanii
  Furaha na vicheko vilitawala
  JK akisalimiana na Bushoke
  Dkt Magufuli akisalimiana na Bushoke
  MC Richie Mtambalike alinogesha vilivyo hafla hii
  Meza kuu wakishangilia baada ya JK kutangazwa Shujaa wa wasanii
  Nikki wa pili akionesha  zawadi ya picha waliyoandaa wasanii
  Nikki wa pili akionesha meza kuu zawadi ya picha waliyoandaa wasanii
  Nikki wa pili akimkabidhi JK  zawadi ya picha waliyoandaa wasanii.
  Nikki wa pili akimkabidhi JK  zawadi ya picha waliyoandaa wasanii huku Fid Q akimuonesha majina ya wasanii wote yaliyotengeneza mosaic ya picha hiyo
  Nikki wa pili akimkabidhi JK  zawadi ya picha waliyoandaa wasanii
  Dkt Magufuli akimpongeza Nikki wa Pili
  JK akiongea na wasanii
  Wasanii wakimsikiliza JK
  Wasanii wakimsikiliza JK
  Wasanii na wadau wakimsikiliza JK
  Wasanii wakimsikiliza JK
  Wasanii wakimsikiliza JK
  Wasanii wakimpongeza  JK
  Wasanii wakimpongeza  JK
  Wasanii wakimpongeza  JK
  Wasanii wakimpongeza  JK
  JK akiendelea kuongea 
  Wasanii wakimpongeza  JK

  0 0  0 0

  Mkurugenzi wa Global Link Education (GEL) ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Abdulmaliki Mollel akitoa maelezo katika semina ya kuwajengea uwezo wazazi na wanafunzi wanaokwenda kusoma Vyuo Vikuu vya India na China leo katika ofisi zao zilizopo viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
   Meneja Mkuu wa Global Link Education (GEL) ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, David Nsimba akitoa semina ya kuwajengea uwezo wanafunzi wanaokwenda kusoma Vyuo Vikuu vya India na China leo katika ofisi zao zilizopo viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
  Wanafunzi waliosimama wanakwenda kusoma katika vyuo vya China nao walipata fursa ya kuhuduria semina ya kuwajengea uwezo kuwajengea uwezo wa mazingira katika vyuo hivyo na jinsi ya kuanza safari yao Agosti 21, 2015. Semina hiyo ilifanyika ofisi za GEL zilizopo viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
  Meneja Mkuu wa Global Link Education (GEL) ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, David Nsimba akikabidhi Hati ya Kusafiria (passport) pamoja na visa kwa mmoja ya mwanafunzi wanaokwenda kusoma Chuo Kikuu nchini China, makadhiano hayo yalifanyika leo ofisi za GEL zilizopo viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya wazazi wakiwa na watoto wao wanaotarajia kwenda kusoma Vyuo Vikuu vya nchini India na China wakiwa katika semina ya kuwajengea uwezo iliyofanyika katika ofisi zao zilizopo viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka, GLOBU YA JAMII)
  …………………………………………………………………………..
  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Kampuni ya GLOBAL link Education (GEL) ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi leo imewapa semina zaidi wanafunzi 100 kwa wanaokwenda kusoma katika vyuo vya India na China katika kuwaandaa katika mazingira watakayokutana nayo kuanzia safari hadi kufika katika nchi hizo.
   
  Akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo katika nchi hizo, Mkurugenzi wa Global Link Education, Abdulmaalik Mollel amesema kufanya semina hiyo ni kuwaandaa wanafunzi jinsi ya kwenda kusoma katika vyuo na kuja kuendeleza nchi yao katika teknolojia mbalimbali.
   
  Amesema vyuo wanavyokwenda kusoma wanafunzi ni vyuo vyenye ubora wa elimu na sio majina ya vyuo yote hiyo ni kuandaa vijana katika soko la ajira uwigo mpana wa ndani na nje ya nchi au kujiajiri na kuleta mapinduzi katika nchi.
   
  Mollel amesema kuanzia Septemba hadi Novemba itakuwa ni kusafiri kwa wanafunzi ambao wamepitia Global Link Education kwenda katika vyuo vinavyofanya vizuri na baadhi ya wanafunzi wamefaulu vizuri katika madaraja yanayokubalika katika ajira duniani.
   
  Amesema Global Link Education wako katika utaratibu kuingia mkataba na makampuni mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wanaokwenda nje wakimaliza kuingia moja kwa moja katika soko la ajira ili kuondoa usumbufu kwa wanafunzi.
   
  Mollel amesema hadi kufikia Oktoba wanatakuwa wamepeleka wanafunzi zaidi 600 katika vyuo mbalimbali ambavyo Global Link ni wakala wa vyuo hivyo .Amesema waliokwenda India hadi sasa wamefikia 170 na bado wanaendelea kwenda na wanafunzi wengine zaidi 100 wanasubiriwa kutokana na kuwa katika Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
   
  Aidha amesema kuwa zaidi 100 wamepewa tiketi na visa katika vyuo vya nchi hizo ambayo kazi hiyo inafanywa na Global Link Education kwa kila hatua.Amewataka wazazi katika kipindi hiki kifupi walete watoto wao kutokana kuwepo kwa nafasi katika vyuo vya India na China kutokana na kuwepo kwa maombi maalum.Wazazi waliuliza juu ya kuharibikiwa kwa watoto katika vyuo vya nje ambapo Mkurugenzi wa Global Linki Education amesema kuharibikiwa huko kunatokana na wazazi kuwapa fedha nyingi za ziada na kufanya kujiingiza katika michezo michafu.

  Mollel amesema wazazi watoe fedha kutokana na hali halisi ya matumizi ya mwanafuzi katika chuo husika au kuweza kuuwasiliana na Global kwa kusahauri jinsi ya kuweza kudhibiti matumizi ya mtoto akiwa chuoni.

  Amesema kuwa wanafunzi hao wanakwenda ni watoto hivyo hawana udhibiti wa fedha hivyo lazima wazazi wawajue watoto matumizi yao.

  0 0

      5
  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janet Mbene akimkabidhi Vitanda vya Kujifungulia Katibu wa CCM wilaya ya Ileje kwa ajili ya Hospitali za wilaya hiyo.
  2
  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene,akionyesha baadhi ya vifaa vinavyotumika katika hospital ambavyo avimetolewa na Karemjee Foundation kwa ajili ya Hospital ya Ileje.
  4
  Mganga mkuu wa Wilaya ya ilje, akiangalaia sehemu ya msaada wa vitanda uliotolewa na Janet Mbene.
  1
  Mafundi wa Hospitala wakiunganisha kitanda cha kujifunguliwa kilicholetwa na Mh Janet Mben kwa ajili ya hospitalai za ieleje.

  0 0
 • 08/08/15--11:21: SIMBA DAY YAFANA JIJINI DAR
 •  Kikosi cha timu ya Sports Club Villa, kilichomenyana na Simba na kuangukia "pua" kwa kunyukwa bao 1-0
   Kikosi kipya cha Simba, kilichoinyuka Sports Club Villa


   Ben Kinyaiya, (kulia) wa timu ya wasanii, akiumiliki mpira mbele ya Imani Kajula
  Mashabiki wa Simba wakiishangilia timu yao.
  Aveva katika "ubora" wake
  Msemaji wa Simba, Haji Sunday Manara, ni mmoja wa watu "waliovunjwa mbavu" na Aveva
  Msemaji wa Simba, Haji Sunday Manara, (kushoto), akionyesha "kumbe wamo"


   RAIS wa klabu ya soka ya Simba, Evans Aveva, (pichani juu), jana alikuwa kama kocha wa Chelsea, Josse Morinho, kutokana na jinsi alivyokuwa akiwaelekeza wachezaji wa timu ya viongozi wa Simba dhidi ya timu ya soma ya wasanii wa bongo movie na bongo flava kwenye maadhimisho ya siku ya Simba almaarufu kama Simba Day.

  Aveva abaye alikuwa “kaulamba” yaani kapiga suti yake nyeusi, alikuwa ndio “kocha wa timu hiyo ya viongozi wa Simba.Akiwa amevalia suti nyeusi, hakuweza kutulia kwenye kiti, kila wakati alisimama na kuwaelekeza wachezaji wake kwa kunyoosha mikono na kufoka.
  Timu ya soka ya viongozi wa Simba iliibuka mshindi wa bao 1-0.


  Baada ya pambano hilo, lilifuatia tendo la kuwatambulisha wachezaji wapya wa Simba na benchi la ufundi kabla ya kuanza kwa pambano maalum la kirafiki baina ya timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam na wageni wao Sports Club Villa ya Uganda, katika pambano hilo la kirafikli, Simba iliibanjua Sports Club Villa "Jogoo" bao 1-0. Bao lililofungwa na Awadh Juma, kwenye dakika ya 45 ya kipindi cha lala salama.
   Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Hassan Dalali(kulia)

   Kikosi cha timu ya wasanii
   Kikosi cha timu ya viongozi wa Simba
   Aveva katika "ubora" wake


   JB akiwatoka wachezaji wa timu ya viongozi wa Simba
   JB akifuatilia jinsi wenzake wanavyopelekwa puta na timu ya viongozi wa Simba
   Kocha mkuu wa Simba, katika "ubora" wake

  Kocha Mkuu wa Simba, akizungumza jambo na mchezaji wake, Hamisi Kiiza Diego

   Mgeni rasmi, wa Simba Day, Mohammed Dewji "MOD", akisalimiana na mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassan Mgosi
   Mo akisalimiana na wachezaji wa timu ya Sports Club Villa ya Uganda


  Imani Kajula, (kulia), wa timu ya viongozi wa Simba, akijaribu kuutuliza mpira
  Mchezaji wa kiungo wa timu ya Wasanii JB, akiusaka mpira katikati ya uwanja
  Ibrahim Masoud, "Maestro" akipiga hesabu wakati wa pambano kati ya timu ya soka ya viongozi wa Simba na ile ya wasanii
  Mshambuliaji wa Simba, Khamisi Kiiza "Diego", (kulia), akijaribu kuupiga mpira huku akichungwa na msitu wa walinzi wa SSC Villa kutoka Uganda

  0 0  0 0

  1
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiongea na Maafisa Vijana na kuwataka kutumia elimu na ujuzi walioupata katika mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu katika kuisaidia serikali kutimiza dhamira yake ya kuwainua vijana kiuchumi, wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu kwa Maafisa Vijana jijini Arusha.
  2
  Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Prof Bonard Mwape akiwaeleza maafisa vijana kuhusu umuhimu wa kubadilisha fikra za vijana ili kuwawezesha kujiajiri kupitia mafunzo watakayowapatia ya ujasiriamali, wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu kwa Maafisa Vijana jijini Arusha.
  3
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiwakabidhi Baadhi ya Maafisa Vijana vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Ujasiriamali na ubunifu, wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu kwa Maafisa Vijana jijini Arusha.

  456
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akimueleza jambo Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Prof.Bonard Mwape wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu kwa Maafisa Vijana jijini Arusha.
  7
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga na Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Prof. Bonard Mwape wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Vijana na Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari na Chuo cha ESAMI.
  ………………………………………………………………………………………….
  Habari Picha na Hassan Silayo-MAELEZO ARUSHA
  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuweka mipango endelevu ya kuwasaidia vijana ili waweze kujiajiri na kuajiri wengine.
   Hayo yamesemwa leo Jijini Arusha na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga wakati akifunga mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu yaliyotolewa kwa Maafisa Vijana.Sihaba alisema kuwa kundi la vijana ni kundi kubwa lenye changamoto nyingi za kiuchumi na kijamii zinazopelekea kupunguza ufanisi katika uzalishaji mali kuanzia ngazi ya familia na taifa kwa ujumla.
   “Serikali inadhamira ya dhati ya kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia miradi mbalimbali ya kimaendeleo ili kuwafanya vijana waweze kujikimu kimaisha kwa kujiajiri au kuajiri wengine na hii inatokana na serikali kutambua changamoto zinazowakabili vijana ikiwa ni kundi muhimu katika jamii” Alisema Sihaba.
   Aidha Sihaba aliwataka Maafisa Vijana kutumia elimu na ujuzi walioupata katika mafunzo hayo katika kuisaidia serikali kutimiza dhamira yake ya kuwainua vijana kiuchumi na kulifanya kundi hilo kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.
   Naye Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Prof Bonard Mwape aliishukuru Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kuwapa nafasi ya kutoa mafunzo hayo kwa Maafisa Vijana watakayo yatumia katika kuwabadilisha fikra vijana na kuwafanya waweze kujiajiri kupitia ujasiriamali.
   Prof. Mwape aliongeza kuwa huu ni mwanzo wa mambo mazuri yanayokuja kwa ajili ya vijana na kwa ushirikiano na Serikali kupitia Wizara watahakikisha vijana wanakuwa wanakuwa sehemu muhimu katika jamii hasa katika shughuli za uzalishaji mali.
   Akizungumzia kuhusu faida za mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Arusha Bi. Hanifa Ramadhani alisema kuwa watatumia mbinu walizojifunza katika mafunzo hayo ili kukidhi mahitaji ya vijana na kuwawezesha kujiajiri kupitia ujasiriamali na kuwafanya kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali.
   Mafunzo hayo ya Ujasiriamali na Ubunifu yameandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) kwa lengo la kuwawezesha vijana kujiajiri na kuajiri wengine

  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizindua uvunaji wa matikiti maji kwa wakulima wa shehia ya Donge Muwanda.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizindua uvunaji wa matikiti maji kwa wakulima wa shehia ya Donge Muwanda.  Mkulima wa matikiti maji na pilipili boga Bw. Salum Khamis Kiregu akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais kuhusiana na changamoto zinazowakabili katika kilimo hicho.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa pamoja na badhi ya wakulima wa Donge Mchangani na Muwanda, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “A” (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Affan Othman Maalim (wa pili kushoto). Picha na OMKR.
                                   
  Na: Hassan Hamad (OMKR)
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesifu juhudi zinazochukuliwa na wananchi wa Donge katika kuendeleza kilimo cha matunda na mboga mboga.
  Amesema iwapo kilimo hicho kitawekeza mikakati imara, kinaweza kuwa mkombozi wa kweli kwa wakulima na kuweza kuweza kuongeza kipato chao.
  Maalim Seif ameeleza hayo wakati akizindua uvunaji wa matikiti maji na pilipili boga katika shehia za Donge mchangani na Muwanda katika Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja.
  Amesema katika siku za hivi karibuni, kilimo hicho kimepata mafanikio makubwa na kupunguza uagiziaji wa bidhaa hizo nje ya Zanzibar kutoka asilimia 80 hadi asilimia 20.
  Amefahamisha kuwa lengo la Serikali ni kuimarisha zaidi kilimo cha matunda na mboga mboga ili kuweza kukidhi soko la ndani na kuacha kuagizia bidhaa hizo kutoka nje ya Zanzibar.
  Amesema kinachohitajika hivi sasa ni kwa Serikali kuongeza mashirikiano na wakulima, ili kusaidia kuwatatulia kero zinazowakabili ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa maji pamoja na pembejeo.
  Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameiagiza Wizara ya Kilimo kupeleka mabwana na mabibi shamba wa kutosha katika shehia hizo za Mchangani na Muwanda, ili kusaidia utaalamu kwa wakulima hao na kuweza kuzalisha zaidi.
  Nae Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar Bw. Affan Othman Maalim, amesema tayari Serikali imeanza kufanya utafiti kujua maeneo ya kuchimba visima ili kuwasaidia wakulima hao kuondokana na tatizo la upungufu wa maji.
  Hata hivyo amewashauri wakulima hao kujikusanya pamoja ili kurahisisha miundombinu ya maji kuweza kuwafikia walengwa.
  Kuhusu tatizo la pembejeo, Bw. Affan amesema Wizara ya Kilimo inaandaa utaratibu wa kulipeleka suala hilo katika ngazi za juu, ili kuwawezesha wakulima wa matunda na mboga mboga kuweza kupatiwa ruzuku za pembejeo za kilimo kama wanavyopatiwa wakulima wa mpunga.
  Mapema mmoja kati ya wakulima hao Bw. Salum Khamis Kiregu, amemueleza Makamu wa Kwanza wa Rais kuwa licha ya mafanikio wanayoyapata, bado wanakabiliwa na tatizo la soko la kuuzia bidhaa hizo, na kuiomba serikali kuandaa mazingira bora ya soko kwa wakulima hao.
  Amesema hivi sasa wanalazimika kuuza bidhaa zao kwa bei ya chini kupitia kwa wafanyabiashara, jambo ambalo limekuwa likipunguza kipato chao licha ya kuzalisha bidhaa hizo kwa wingi.
  Bw. Kiregu ameeleza matatizo mengine yanayowakabili kuwa ni pamoja wadudu waharibifu na maradhi ya mimea, na kuwaomba wataalamu wa kilimo kuwa karibu na wakulima ili kusaidia kukabiliana na changamoto hizo.

  0 0

  SHINYANGA
  Mwandishi wa habari na mtangaaji wa Radio Free Africa William Bundala (KIJUKUU CHA BIBI K) ameshinda kura za maoni katika nafasi ya Udiwani katika kata ya Ulowa jimbo la Ushetu.

  Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa uchaguzi huo Sangoma amesema kuwa Bundala ameshinda nafasi hiyo kwa kupata kura 46 dhidi ya Wagombea wenzake Charles Bahati aliyepata kura 14 na Marco Matheo ambaye hakupata kura yoyote katika kinyang’anyiro hicho.

  Kuelekea uchaguzi mkuu Bundala alitangaza nia ya Kugombea Ubunge katika jimbo la Ushetu na udiwani katika kata ya Ulowa huku akisimamia kauli mbiu yake kuwa “Tunahitaji mawazo na nguvu mpya za vijana kuleta mabadiriko ya maendeleo”.

  Akiongea kwa njia ya simu akiwa jimboni Bundala amesema kuwa huu ni mwanzo na kuongeza kuwa kwa sasa anasubiri kura za maoni za ubunge ili kuchaguliwa kupeperusha bendera ya Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

  Sambamba na hayo Bundala amesema kuwa Tanzania ilipofikia kwa sasa inahitaji viongozi wazalendo wenye uchungu na rasilimali za wananchi na siyo kiongozi mwenye uchu wa madaraka anayetaka uongozi kwa rushwa.

  Kwa upande wao wagombea waliokuwa katika kinyang’anyiro hicho cha udiwani wamesema kuwa wameridhika na matokeo na kwamba lengo la CHADEMA ni moja kuleta mabadiriko katika jimbo la Ushetu na kata ya ulowa kwa Ujumla.

  Kwa sasa Bundala anasubiri kura za maoni za Ubunge zinazotarajiwa kufanyika wiki ijayo huku akiwa katika kinyang’anyiro hicho na watia nia wengine wawili ambao ni Mabula Nkwabi na John Kitibu ambaye alipata kura 45 katika kura za maoni za jimbo la Kahama Mjini katika uchaguzi ambao James Lembeli aliibuka mshindi.


  0 0

  Dkt John Pombe Magufuli kwa pamoja akicheza wimbo wa Adinselema uliokuwa ukiimbwa na wanachama hao mara baada ya kumpokea na kuamsha shamra shamra na shangwe za hapa na pale.Pichani kulia ni Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Mama Salma Kikwete akishuhudia.
  Mgombea Uraisi wa chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa kwa shangwe na shamra shamra kutoka kwa wanachama na wafuasi wa chama cha CCM waliokuwa wamekusanyika nje ya ofisi za CCM mkoa wa Lindi,alipofika kusaini vitabu,kuwashukuru na kujitambulisha kwao.
  Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Mama Salma Kikwete akizungumza jambo na Wanachama wa chama hicho nje ya Ofisi za CCM mkoa wa Lindi
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya wanachama wa CCM na wafuasi wa chama hicho waliofika kumlaki alipowasili kwenye ofisi hizo kwa ajili ya kusaini vitabu pamoja na kuwashukuru na kujitambulisha kwa wanachama hao mapema leo Agosti 8 2015.Dkt Magufuli amewataka wananchama hao kushikamanana kuwa wamoja katika kipindi hiki muhimu cha uchaguzi,ambacho anaamini kitaipatia ushindi chama CCM.
  Dkt John Pombe Magufuli akitia sahihi vitabu ndani ya ofisi ya CCM mkoa wa Lindi,pichani kati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa,Ndugu Ali Mtopa pamoja na 
  Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Mama Salma Kikwet.
  Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi,Ndugu Ali Mtopa,alipowasili kumkaribisha Mgombea Mteule wa chama cha Mapinduzi,Dkt John Magufuli aliyewasili kwenye ofis hizo kwa ajili ya kusaini vitabu pamoja na kuwashukuru na kujitambulisha kwa wanachama na wafuasi wa chama cha CCM
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi,Ndugu Ali Mtopa alipowasili  kwenye ofisi hizo kwa ajili ya kusaini vitabu pamoja na kuwashukuru na kujitambulisha kwa wanachama na wafuasi wa chama cha CCM mkoani humo mapema leo Agosti 8 2015
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu,Mama Salma Kikwete.Dkt Magufuli aliwasili kwenye ofisi hizo kwa ajili ya kusaini vitabu pamoja na kuwashukuru na kujitambulisha kwa wanachama na wafuasi wa chama cha CCM mkoani humo mapema leo Agosti 8 2015
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanachama wa chama hicho waliofika kumlaki alipowasili kwenye ofisi hizo kwa ajili ya kusaini vitabu pamoja na kuwashukuru na kujitambulisha kwa wanachama na wafuasi wa chama cha CCM mkoani humo mapema leo Agosti 8 2015
  "Karibu Bwana Magufuli..karibu sana Lindi" mmoja wa Wanachama akimkaribisha Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli mara baaada ya kuwasili katika ofisi za CCM mkoa wa Lindi  ambapo alisaini vitabu,aliwashukuru wanachama na wafuasi wa chama hicho pamoja na kujitambulisha kwao.
  Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa watoto waliofika kumlaki mgombea huyo.
  "Karibu Bwana Magufuli..karibu sana Lindi" mmoja wa Wanachama akimkaribisha Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli mara baaada ya kuwasili katika ofisi za CCM mkoa wa Lindi  ambapo alisaini vitabu,aliwashukuru wanachama na wafuasi wa chama hicho pamoja na kujitambulisha kwao. 
  Dkt John Magufuli akisalimiana na aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Mtama,kabla ya Mh.Bernad Membe,Ndugu Kassim Abdallah .

  0 0

  1
  Mtaalamu wa Kilimo Dkt.Kissa Kajigili akimpa maelezo ya kilimo bora cha mpunga kwa njia ya umwagiliaji wa kisasa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipotembelea maonesho ya nane nane yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
  2
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia moja ya matrekta katika viwanja vya maonesho Ngongo Mkoani Lindi wakati wa maadhimisho ya sherehe za wakulima Nanenane.
  4
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia muhogo uliolimwa kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo wakati wa maonesho ya kilimo yaliyofanyika katika viwanja vya Ngongo mjini Lindi wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima yaliyofanyika kitaifa mkoani humo.
  56
  Mjasiriamali Bi.Ashura Omary Mswazi akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete mafuta aliyokamua kwa mashine bora na kuyauza kupitia kampuni yake ya Kwadelo Investment wakati Rais alipotembea na kukagua baadhi ya mabanda ya maonesho katika viwanja vya Ngongo Mjini Lindi wakati wa sikukuu ya wakulima nanenane.(Picha zote na Freddy Maro)

  0 0

  unnamed 
  Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Antonino Kilumbi akiwa ameshika vikombe vya ushindi katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati kwa Mwaka 2015. Wengine ni Maafisa Washiriki wa Jeshi la Magereza wa Maonesho ya Wakulima ya Nane Nane Kanda ya Kati, Dodoma.
  …………………………………………………………………
  Jeshi la Magereza nchini limeibuka Mshindi wa kwanza kwa upande wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika Maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika katika Kanda ya Kasikazini(Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara), Kanda ya Magharibi(Mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga na Dar es Salaam) pamoja na Kanda ya Magharibi(Mikoa ya Tabora, Kigoma na Shinyanga) ambapo Jeshi la Magereza limeibuka kidedea katika upande wa Uzalishaji Taasisi za Serikali pamoja na Taasisi za Serikali upande wa Teknolojia na Maonesho Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
   
    Jeshi la Magereza ni Miongoni mwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi likiwa na jukumu lake la kuwahifadhi na kuwarekebisha Wafungwa wa aina mbalimbali wawapo Magerezani ili pindi wamalizapo vifungo vyao waweze kuwa raia wema katika jamii. Pia hushiriki kikamilifu katika Maonesho ya Nane Nane Kitaifa na Kikanda kwa lengo la kutoa elimu kwa umma kupitia shughuli zake mbalimbali za uzalishaji katika Sekta za Kilimo na Mifugo.


    Mbali na ushindi huo wa Kikanda, Jeshi la Magereza limeshiriki kikamilifu katika Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Kitaifa(Maarufu kama Nane Nane) katika Mkoa wa Lindi ambapo Jeshi hilo limeibuka Mshindi wa Pili kwa upande wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika Kilele cha Maonesho hayo huku Jeshi la Kujenga Taifa likibuka Mshindi wa Kwanza wa Jumla na Mgeni rasmi katika Kilele cha Maonesho hayo Kitaifa alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

   
    Kutokana na Ushindi huo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja amewapongeza Maafisa na Askari wote walioshiriki kikamilifu katika Maonesho hayo hadi kufanikisha ushindi huo na amewapa changamoto ya kuongeza bidii zaidi katika utendaji wao wa majukumu ya kazi ili katika Maonesho yajayo waweze kufanya vizuri zaidi.
   
    Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa Jeshi la Magereza kuibuka Mshindi wa kwanza kwa upande wa Taasisi za Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika Kikanda hapa nchini tangu Mwaka 2013.
   
    Maonesho ya Wakulima Nane Nane Kitaifa yamefunguliwa rasmi Agosti 04, 2015 na Waziri   Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Pinda ambapo kauli   mbiu ya Mwaka huu ni “Matokeo Makubwa Sasa” – Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo   ya Wakulima na Wafugaji.
                                       
   Imetolewa na Mrakibu Msaidizi wa Magereza,Lucas Mboje,                                      wa Jeshi la Magereza,   Agosti 08, 2015.


  0 0

  Kwa miaka mingi upatikanaji wa wataalamu wa Afya na matibabu ya uhakika unakabiliwa na changamoto kuu mbili inayowakumba wagonjwa wengi Tanzania.Watanzaniawamekuwa wakisafiri nje ya nchi kupata matibabu ya Figo na magonjwa yanayohusiana na kibofu. Hivyo wataalamu wawili waliobobea katika magojwa ya Figo na Kibofu kutoka Hospitali za Apollo walitembelea nchini Tanzania wakishirikiana na madaktari kutoka Hospital ya Hindu Mandal ili kuwafanyia uchunguzi, kutoa tiba na kutoa ushauri kwa wagonjwa mbalimbali Tanzania. 

  Dkt V. Rajagopal ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya njia ya mkojo na mfumo wa uzazi wa kiume na amekuwa mshauri mwandamizi wa magonjwa ya kibofu katika Hospitali za Apollo huko Hyderabad India tangu mwaka 1994. Dkt. Sanjay Maaitra ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya Figo kwa kutoa huduma za matibabu ya figo na magonjwa yanayoambatana na Figo ikiwa lengo kuu la ujio wao ni kuhakikisha wagonjwa wanapata uchunguzi sahihi bila kuingia gharama kubwa za kwenda nje ya nchi.
  Wagonjwa wanaosubuliwa na magonjwa yanayohusiana na figo pamoja na mkojo walihudhuria na kushiriki katika tukio hili.  Madaktari hao waliwafanyia wagonjwa uchunguzi kwa kupitia taarifa zao nyuma na kuzipitia upya, kutoa historia ya matibabu na kutoa ushauri wa matibabu na tiba kwa wagonjwa wapya waliojitokeza.
  Kama ilivyoelezwa hapo juu lengo la ujio wa madaktari hawa ni kupata taarifa za wagonjwa wote ambao walipata huduma za matibabu kutoka kwao iwe ndani ya nchi au katika Hospital za Apollo huko Hyderabad. Lengo la Dkt. Rajagopal na Sanjay Maitra ilikuwa ni kuangalia jinsi gani wagonjwa wao wamepata nafuu na kama wanahitaji vipimo zaidi na marekebisho ya tiba. Kwa mfano mgonjwa ambaye amepandikishwa figo anahitaji muda mrefu wa ushauri na uchunguzi wa mara  kwa mara. Ujio wa madokta hawa hapa nchini umekuwa jambo jema kwa kuwa umewarahisishia wagonjwa kupata matibabu kwa urahisi na uchunguzi wa muda mfupi. Endapo kama afya za wagonjwa zilitambulika kuzorota hivyo madaktari walipendekeza wapate vipimo zaidi katika Hospitali za Apollo, Hyderabad au Hospitali zozote zile.
  Taasisi ya Upandikizaji ya Apollo (ATI), ni sehemu ya Hospitali za Apollo ambayo niTaasisi kubwa na imara katika mpango wa upandikizaji figo duniani. Wanatoa huduma za uchunguzi wa figo, Ini, Upandikizaji figo,   upandikizaji wa ‘Corneal’ ‘GI’,  matibabu ya tumbo na huduma nyinginekwa watoto. Taasisi hii inatoa ushari mbalimbali, vipimo na tiba.
  Wakati wa ujio wa madaktari, tulipata fursa ya maohijiano na Dkt. V. Rajagopal pamoja na Dkt. Sanjay Maitra, tuliwauliza kama wameona mabadiliko yoyoteya afya Tanzania tangu walipokuja safari yao ya mwisho. 

  Pia madaktari hawa walitaja idadi ya wagonjwa ambao waliofika katika kliniki na kuona idadi kubwa kuongezeka kutokana na watu kutambua upatikanaji wa huduma hizo na mafanikio ya watu waliowahi kutibiwa na  kushauriwa na madaktari hao wa kimataifa wenye ujuzi mkubwa.  Hata hivyo Watanzania bado wanakosa njia za kupambana na magonjwa haya tangu mwanzo. Madokta walikuwa na maoni kwamba, mwamko utaongezeka kama watu wanatapata elimu ya kutosha kutoka kwa  madaktari juu ya uzuiaji wa magonjwa haya kwa kutambua dalili za mwanzo.
  Daktari. V. Rajagopal na SanjayMaitra walisisitiza umuhimu kuzuia magonjwa haya na pia kufanya vipimo mara kwa mara.  Waliendelea kusema kwamba magonjwa haya huwapata hasa watu wenye umri mkubwa lakini pia huweza kuzuilika. Watanzania wanatakiwa kuwa makini kutokana magonjwa mengi yanayotokana na figo hasa kwa watu wazima ni kutokana na Shinikizo la Damu, Kisukari, wingi wa Lehemu, kutofanya mazoezi, Ulaji mbaya pia utumiaji usio sahihi wa dawa hasa za kutuliza maumivu. Hivyo  husababisha  ulemavu wa figo. 
  Pia Dkt. Sanjay Maitra alitoa ushauri  ni vyema kuzingatia vipimo mara kwa mara kwani inasaidia watu kujua afya  zao.Alitoa mfano wa mtu mmoja,  ambaye  ni dereva mwenye ujuzi wa miaka hamsini na kipindi chote alikuwa anaumwa miguu na mwishowe aligundulika kuwa na kisukari kwa miaka kumi na tano. Pia mgonjwa huyo hakujua kuhusu shinikizo la damu wala hakuwa na walipompima walimgundua hana uwezo wa kuona vizuri. 

  Dkt. Sanjay Maitra aligundua kuwa ana ugonjwa wa kisukari. Pia kwa bahati mbaya pia watanzania wengi wanashabihiana na mfano huo kwa kuwa hawajui dalili mwanzo za magonjwa haya. Aliongeza kwa kusema kuwa ni muhimu kwa wao kutembelea kwani wameleta mwamko mkubwa.Pia Madokta hawa wametoa wito kwa Watanzania kupata taarifa zaidi juu ya kupambana na magonjwa haya ili kuishi kwa afya njema na maisha marefu.
  Tukio hili la madaktari kutembelea taasisi za afya hapa nchini  lengo ni kuleta ushirikiano katika huduma za afya na mafunzo kwa madaktari wa hapa nchini.  
  Dkt. Sanjay Maitraamesema ni jambo gumu na linahitaji hela nyingi  kwa wagonjwa kusafiri nje ya nchi, hivyo yeye ameona ni vyema kuweka muda ili kuja kutoa huduma  kwa ukaribu zaidi.  Anatumaini kwamba wagonjwa watatibiwa kwa urahisi hata wakiwa nje ya nchi.

  Lengo la ujio wao si kwamba kuwachukua wagonjwa na kuwatibia katika Hospitali za Apollo bali ni kuwapa ushauri sahihi na kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi ya matibabu. Mbali na suala la wagonjwa lakini tumeona pia wachache kati yao wataweza kwenda Apollo kama watahitaji matibabu.
  Alipoulizwa kuhusu watanzania watakachopata wakienda Hospitali za Apollo, Dkt. V Rajagopal alisema kwamba mpango wa Kimataifa wa Apollo ni kusaidia wagonjwa na washirika wao ili kurahisisha huduma za afya. 

  Pia wanatoa ratiba ya uteuzi, usafirishaji, na huduma za ukalimani kwani Hospitali za Apollo pia zinatoa huduma ya ukalimani kwa lugha ya Kiswahili ili kuwahudumia wagonjwa wanaotoka Kenya, Uganda na Tanzania kwa urahisi.  Hospitali za Apollo zinajulikana kwa kwenda mbali zaidi kuwafanya wagonjwa kuhisi unafuu.

  Mwaka 2014, Mji wa Apollo (Apollo Health City) Hderabad, ulipata tuzo ya heshima ya KIMATAIFA YA MATIBABU NA UTALII kutoka Jarida la  Kimataifa la Matibabu na Usafiri  kutokana na utoaji wa huduma bora kwa wateja.
  Hospitali za Apollo zinamfanya mgonjwa ajisikie kama yupo nyumbani kwani huwaandalia wagonjwavyakula vikuu kama ugali, ndizi mtori, ingawa wagonjwa wengi wa kiafrika wanapenda kujaribu vyakula vya kihindi. Pia mapishi yanaenda mbali zaidi kwa kuandaa chakula cha watoto na watu wazima. Chakula ni muhimu sana kwa wagonjwa ili kuwa na afya. Hospitali za Apollo zinaamini kwamba “kama tunafahamu chakula basi pia tunafahamu tamaduni husika”.

  Kuhusu Apollo:
  Mnamo mwaka 1993, Dkt. Prathap C. Reddy, mbunifu wa afya nchini India, alianzisha hospitali ya kwanza ya ushirika nchini India, Hospitali za Apollo Chenai. Kwa miaka mingi, Hospitali za Apollo zimeweza kukua kufikia moja ya shirirka kubwa la afya barani Asia likiwa na uwezo wa zaidi ya vitanda 8,500 ndani ya Hospitali 50, zaidi ya maduka 1350 ya dawa na zaidi ya kliniki za uchunguzi 100.  Pia hospitali za Apollohutoa huduma za matibabu kwa utaratibu wa kibiashara, huduma za bima za afya na kitengo cha tafiti za kitabibu kwa lengo la kufanya tafiti za magonjwa ya milipuko, seli shina za mwili na maumbile. Kuendeleza vipaji ili kumudu hitaji linaloongezekaa katika utoaji huduma za hali ya juu, Hospitali za Apollo zina jumlaa ya vyuo 11 vya madaktari pamoja na wauguzi. Mafanikio haya yamezifaidisha Hospital za Apollo kupata tuzo mbali mbali, ikiwa ni pamoja na tuzo ya kituo bora iliyotolewa na serikali ya India pamoja na kutambulika na tume ya pamoja ya kimataifa ( Hospitali saba za Apollo zinatambuliwa na kutunikiwa na tume ya pamoja ya kimataifa). Katika hesima nadra, serikali ya india ilitoa mhuli wa kumbukumbu wa kuutambua mchango wa Hospitali za Apollo Dkt. Prathap C Reddy,  alitunukiwa tuzo ya heshima ya Padma Vbhushan’ mnamo mwaka 2010. Ushirika wa Hospitali za Apollo kwa zaidi ya miaka 50, umeendelea kuboresha uongozi katika uvumbuzi wa kitabibu, huduma za kimataifa na maendeleo ya kiteknolojia. Hospitali zetu zimekuwa katika nafasi ya juu kimatifa katika huduma za kitabibu pamoja na utafiti.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye kilele cha sherehe za nane nane mkoani Lindi ambapo alizungumzia kukua kwa sekta ya kilimo na matumizi mazuri ya matrekata pamoaja na mbolea, pia kuanzishwa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo kwani itawasaidia sana wakulima lakini pia alikemea vitendo vya dhulma vinavyofanya na vyama vya ushirika kwa wakulima.Rais Dkt. Jakaya alitumia fursa hiyo kuwaaga wakazi wa mkoa wa Lindi.
   Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli akizungumzia miradi ya barabara iliyokamilika  mpaka sasa na iliyokuwa kwenye utaratibu wa kukamilishwa wakati wa kufunga sherehe za nane nane mkoani Lindi.

   Waziri wa Mambo ya Nje na Uusiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akizungumza masuala ya usalama wa mipaka yetu pamoja na mahusiano na nchi jirani kwenye kilele cha siku ya nane nane iliyofanyika Kitaifa mkoani Lindi.
   Vyombo vya habari vilikuwa vingi kuchukua matukio kwenye siku ya kilele cha sherehe za wakulima nane nane.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi kombe kwa mmoja wa washiriki wa Nane nane mkoani Lindi.
   Washindi wa jumla JKT wakiwa kwenye picha ya pamoja.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza tufe kuashiria kufunguliwa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania kwenye kilele cha sherehe za Nane Nane mkoani Lindi.

  0 0

     
  Mbunifu na Mmiliki wa Maduka ya Amina Design  Ambaye pia ni   Mentor wa Taasisi ya Manjano Foundation Amina Plummer Akitoa Mada kwenye Semina ya Kuwawezesha  Wanawake Kuwa Wajasiriamali kupitia Vipodoz Vya Luv Touch Manjano Iliyoandaliwa na Manjano Foundation Kwa Lengo la Kuwajengea Udhubutu Wanawake  Kufanya biashara pia namna ya Kujiwekea Akiba na Kutumiza Malengo yao. 

   Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa Miradi  ambayo itamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea umasikini wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha yake. Taasisi hii  limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd  Mama Shekhar Nasser (Katikati) Akiwa na Mbunifu Amina Plummer (Kushoto ) Pamoja Afisa Mtendaji Mkuu wa Women an Youth  Empowerment Program Kutoka Uganda Dada Remmie Male.
  Mbunifu na  Mmiliki wa maduka ya Amina Design Amina Plummer  ni mmoja kati ya Mentors 15 watakao wapa muongozo washiriki 30 wa mradi wa Manjano Foundation. Amina aliwapa somo la kujifahamu kama wajasiriamali chipukizi kuwa wasilimbuke pale ambapo mafanikio yanapo anza kuja. Aliwaeleza kuhusu umuhimu wa kujiamini, kumuamini Mungu, kuwakarimu wateja, kuweka akiba Akiwa Sambamba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Women an Youth  Empowerment Program Kutoka Uganda Dada Remmie Male
  Mbunifu  Amina Plummer  ni mmoja katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya washiriki wa Semina hiyo inayoandaliwa na Taasisi ya Manjano  Kupitia Bidhaa za Luv Touch Manjano.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd  Mama Shekhar Nasser na Mbunifu Amina Plummer  Pamoja Afisa Mtendaji Mkuu wa Women an Youth  Empowerment Program Kutoka Uganda Dada Remmie Male. Katika Picha ya Pamooja na Washiriki wa Semina hiyo.

older | 1 | .... | 603 | 604 | (Page 605) | 606 | 607 | .... | 1897 | newer