Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 4 | 5 | (Page 6) | 7 | 8 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Marehemu Said Kilowoko enzi za uhai wake

  0 0
  KUWATUMIA WATAALAMU WA KITANZANIA WALIOKO UGHAIBUNI        (DIASPORA) NA NDANI YA NCHI KUJENGA UWEZO NA UFANISI WA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI MUHIMU ZA SERIKALI

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniainakusudia kuwatumia wataalamu wa Kitanzania walioko ndani ya nchi na wale walioko ughaibuni (Diaspora) katika kutekeleza mipango yake kadhaa yenye umuhimu kwa Taifa.


  Hapo awali, Serikali iliwatumia zaidi wataalamu kutoka nchi nyingine, ambapo kwa sasa lengo ni kuona kwamba wataalamu wa nchi nyingine wanatumika pale tu ambapo wataalamu wa Kitanzania walio ndani na nje ya nchi hawajapatikana kufanya kazi husika.


  Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali itapenda kupata wataalamu wa Kitanzania kwenye maeneo yafuatayo:-


  (i)                             Mfumo mzima wa utafutaji, uchimbaji, uongezaji thamani na usambazaji wa gesi asilia  na mafuta.

  (ii)                          Kuimarisha matumizi salama ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kuboresha utendaji wa Serikali na utoaji wa huduma kwa wananchi.

  (iii)                        Kuboresha utekelezaji wa malengo ya Serikali na kupima matokeo kupitia mfumo unaokusudiwa kuhakikisha tunapata matokeo  makubwa na ya haraka katika maeneo ya kipaumbele na kimkakati katika maendeleo ya Taifa.


  Wataalamu watakaojitokeza na kukubaliwa kufanya kazi Serikalini katika maeneo haya, watafanya kazi kwa mikataba ya muda mfupi, lakini inayoweza kuongezwa iwapo utendaji utaridhisha.


  Mwito unatolewa kwa Wataalamu wa Kitanzania popote walipo, ughaibuni au ndani ya nchi, kujitokeza na kuleta wasifu wao (CV’s) pamoja na maelezo ya kwa nini wanafikiri wao ni aina ya watu tunaowatafuta.  Tumia anuani ifuatayo:-


  Katibu Mkuu Kiongozi                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                           

  Ofisi ya Rais, Ikulu

  S.L.P. 9120

  DAR ES SALAAM.


  E.mail:chief@ikulu.go.tz


  0 0  0 0


  Mkurugenzi wa Maendeleo na Utamaduni wa Wizara ya Habari Bw. Herman Mwasoka (mwenye suti nyeusi) akimfariji Baba mzazi wa Marehemu Sajuki Mzee Juma Kilowoko alipofika nyumbani kwa marehemu kuhani msiba huo Tabata Bima jijini Dar.(Picha zote na Mo Blog).
  Mkurugenzi wa Utamaduni na Maendeleo wa Wizara ya Habari Bw. Herman Mwasoka akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Sajuki jijini Dar leo.
  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fisso akitia saini kitabu cha maombolezo ya Msiba wa Sajuki.
  Msanii mkongwe katika tasnia ya muziki wa Dansi na Rhumba Kikumba Mwanza Mpango almaarufu kama King Kiki akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Marehemu Sajuki Tabata Bima jijini Dar leo.
  Mzee King Kiki akiteta jambo na Mkurugenzi wa Utamaduni na Maendeleo wa Wizara ya Habari Bw. Herman Mwasoka (katikati) nyumbani kwa marehemu Sajuki jijini Dar leo. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fisso
  Wasanii mbalimbali na wakiendelea kuwasili nyumbani kwa Marehemu Sajuki Tabata Bima jijini Dar es Salaam. Pichani ni Msanii wa muziki Dokii (kushoto) sambamba na Mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa Mwisho Mwampamba na wasanii wengine.
  Mchekeshaji maarufu wa The comedy Masanja Mkandamizi akijifuta jasho kwa mbali akielekea msibani nyumbani kwa Marehemu Sajuki. Masanja alikuwa ni mmoja wa wahamishaji katika kuchangia pesa za matibabu ya marehemu Sajuki kwenda nchini India kupitia kipindi cha Luninga cha The Comedy kinachorushwa na Televisheni ya TBC.
  Baadhi ya waombolezaji wakiwa kwenye huzuni kutafakari kifo cha Sajuki.
  VIONGOZI WA SERIKALI WAKIWASILI: Mbunge wa jimbo la Segerea, Dar es Salaam, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (wa tatu kushoto) akiwa ameambatana na Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mh.Iddi Azzan wakipokelewa na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba na wasanii wengine wa filamu baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Sajuki kwa ajili ya kuhani msiba huo.
  Mkuu wa Itifaki Bw. Simon Simalenga wa Clouds Media akimuongoza Mh.Makongoro Mahanga sehemu maalum kwa ajili ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
  Mbunge wa jimbo la Segerea, Dar es Salaam, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akitia saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Sajuki.
  Mbunge wa Kinondoni Mh. Iddi Azzan naye aliangusha saini kwenye kitabu hicho.
  Mzee King Kiki akizungumza jambo na Waheshimiwa Wabunge kwenye msiba wa Sajuki Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.
  Waheshimiwa wakielekea nyumba ya jirani walikokusanyika baadhi ya waombolezaji na wasanii wa filamu nchini kwa ajili ya kuzungumza machache na kutoa Ubani.
  Katibu wa Fedha msibani hapo mchekeshaji maarufu Steve Nyerere akiwakaribisha waheshimiwa wabunge kuzungumza na hadhira ya waombolezaji (hawapo pichani).
  Mbunge wa jimbo la Segerea, Dar es Salaam, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akitoa salamu zake za rambimbi na kuahidi kuchangia shilingi 200,000/= kwa ajili ya kufanikisha shughuli za mazishi ya mpendwa wetu Marehemu Sajuki atakayezikwa Kesho Ijumaa katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
  Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mh. Iddi Azzani akielezea kwa majonzi alivyopokea taarifa za msiba wa Sajuki na kuahidi kushirikiana bega kwa bega na Wastara panapomajaliwa ya Mola katika malezi ya mtoto aliyeachwa na marehemu na kuwaasa wadau, ndugu, jamaa na marafiki kumsaidia Wastara kutokana na hali yake na amechangia kiasi cha Shilingi 500,ooo/= kufanikisha shughuli za mazishi ya marehemu Sajuki.
  Pichani Juu na Chini ni Umati wa waombolezaji ukisikiliza nasaha za waheshimiwa Wabunge (hawapo pichani) walipofika nyumbani kwa marehemu Sajuki kuhani msiba huo.
  Kazi ya kuosha vyombo si kina Dada tu, hata kina Kaka wanaweza pia....Pichani ni baadhi ya Watangazaji wa Clouds Radio wakiongozwa na Dina Marios kushiriki kuosha vyombo vilivyotumika katika msiba huo huku wakisaidiana na waombolezaji wengine.
  Mganga wa Jadi anayefahamika kwa jina la Dokta Manyaunyau (kushoto) sambamba na Msanii wa filamu nchini Cloud wakisikiliza mawaidha ya waheshimiwa wabunge (hawapo pichani).
  Mkuu wa Itifaki msibani hapo Bw. Simon Simalenga wa Clouds Media akimpokea Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete alipowasili nyumbani kwa marehemu Sajuki kwa ajili ya kuhani maeneo ya Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete akitoa pole baada ya kusaili kwa baadhi ya ndugu wa karibu wa marehemu Sajuki msibani hapo.
  Bw. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Baba mzazi wa marehemu Sajuki Mzee Juma Kilowoko nyumbani kwa marehemu Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Sajuki leo.
  Bw. Ridhiwani Kikwete akimpa maneno ya faraja Baba mzazi wa Marehemu Sajuki Mzee Juma Kilowoko.
  Bw. Ridhiwani Kikwete akitoa mkono wa pole kwa mke wa marehemu Sajuki Bi. Wastara (mwenye buibui).
  Bw. Ridhiwani Kikwete akimfariji mama mzazi wa Marehemu Sajuki alipofika nyumbani hapo kuhani msiba huo.
  Katibu wa fedha msibani hapo Steve Nyerere akitetea jambo na Bw. Ridhiwani Kikwete.
  Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Bw. Ridhiwani Kikwete kuzungumza machache na waombolezaji.
  Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete akizungumzia marehemu Sajuki na kuwataka wanawake kuiga mfano wa Maisha ya Sajuki na Wastara jinsi walivyokuwa wakiishi na Upendo mpaka Umauti ulipomkuta marehemu Sajuki na kuwasisitiza kuenzi yale yote mema aliyokuwa akifanya kipindi cha uhai wake na kuwamasisha Umoja na Mshikamano baina yao.
  Bw. Ridhiwani Kikwete naye alichangia Shilingi 500,000/= kwa ajili ya kufanikisha mazishi ya Mpendwa wetu Sajuki anayetarajiwa kuzikwa Kesho Ijumaa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
  Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya wasanii wa filamu wakisikiliza nasaha za Bw. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani).
  Marehemu Sajuki alikuwa kipenzi cha watoto na wakubwa pia. Pichani ni Umati wa watoto wanaokaa jirani na Nyumba ya Marehemu Sajuki wakiwa wamekusanyika huku wakionyesha majonzi na simanzi tele.

  0 0
 • 01/03/13--21:09: ATCL resumes Kigoma flights

 • AIR Tanzania Company Limited (ACTL) Acting Chief Executive Officer, Captain Milton Lazaro, speaks to journalists (not in picture) about the airline’s plans to resume Dar es Salaam- Kigoma daily flights on Thursday, 10th January this year after the services were suspended awaiting renovation of the Kigoma Airport. ATCL will deploy its Bombardier Dash 8-300 plane with a capacity of carrying 50 passengers to fly the route. Photo by correspondent.

  =======    ======  ========
  ATCL resumes Kigoma flights

  By Correspondent

  AIR Tanzania Company Limited (ACTL) resumes Dar es Salaam- Kigoma daily flights on Thursday, 10th January this year after the services were suspended awaiting renovation of the Kigoma Airport.

  Speaking to reporters in Dar es Salaam yesterday, the ATCL Acting Chief Executive Officer, Captain Milton Lazaro said the company will deploy its Bombardier Dash 8-300 plane with a capacity of carrying 50 passengers to fly the route after the company’s engineers certified to have completed major check-C repair it was undergoing.

  “We are now set to resume our Dar es Salaam- Kigoma flights on Thursday 10th January this year and we are also working on implementing our aggressive expansion plans which will see us flying to other destinations which we have not covered at the moment,” he said. Captain Lazaro mentioned that ATCL will soon fly to Tabora and Mpanda once renovation of those airport facilities are completed, hence giving their customers in various destinations a better most preferred airline service.

  “ATCL’s strategic plan to commence flights to Songwe Airport in Mbeya is in a better stage. We expect to start flying passengers to that destination on 20th of January this year as we were still waiting completion of renovation of the airport,” he said.

  According to him, after the launch of Mbeya route, the company will go ahead to start flights to Arusha via Zanzibar by the end of this month, which will be accompanied by flights to Mtwara. “I want to assure our esteem customers that our services are still the best and we offer a very competitive fare to the destinations we fly.

  The completion of this Check-C repair which has been carried out by our local engineers is a great step we have made in the aviation industry in Tanzania as we have proved that we can now offer such services to other airlines with no such capacity. We have already entered into agreement with some airlines who are seeking such services and we are ready to offer,” he said. He said the fact that the company’s engineers has successfully completed that kind of repair, ATCL will not only save money being used to send planes abroad for repairs, but also has helped the company to build its engineering capacity.

  Captain Lazaro said ATCL has plans to add three more planes before the end of this year, mentioning that they will go for Bombardier Dash 8 which are much bigger and with modern advanced technology.   

  0 0


  Hatua kuhusu matumizi ya dola milioni 164.6 za “mabomba ya mchina” na mikataba ya miradi ya sasa ya maji jijini Dar es salaam.


  Tarehe 3 Januari 2013 kwa kutumia kifungu cha 10 cha sheria ya haki, kinga na madaraka ya Bunge nimetaka Wizara ya Maji inipatie nakala ya ripoti ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam na maeneo ya Bagamoyo na Kibaha (Dar es salaam Water Supply and Sanitation Project-DWSSP) uliotekelezwa kati ya mwaka 2003 mpaka 2010 jijini Dar es salaam.


  Nimetaka ripoti hiyo ili kubaini matumizi ya dola milioni 164.6 zinazoelezwa kutumika katika mradi huo maarufu kama wa ‘mabomba ya mchina’ kwa kuwa mpaka sasa mwaka 2013 sehemu kubwa ya mabomba yaliyowekwa wakati wa mradi huo katika Jiji la Dar es salaam hayatoi maji huku kukiwa na upungufu katika uzalishaji, upotevu wakati wa usafirishaji, udhaifu katika usambazaji na tuhuma za ufisadi katika matumizi.


  Pamoja na kutaka ripoti ya utekelezaji wa mradi huo, nimetaka pia nakala ya ripoti ya ukaguzi wa kiufundi (technical Audit) uliofanywa na kampuni ya Howard Humphreys kuhusu mradi huo.


  Nimetaka pia kupatiwa ripoti za ukaguzi uliofanywa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Kampuni ya Maji Dar es salaam- DAWASCO (Dar es salaam Water Supply and Sewerage Company) na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka-DAWASA (Dar es Salaam Water Supply and Sewerage Authority) kwa mwaka miaka mitatu ya 2009/10, 2010/2011, 2011/2012 ili kuweza kufuatilia hatua zinazostahili kuchukuliwa.


  Aidha kwa kutumia kifungu hicho hicho cha 10 cha sheria ya haki, kinga na madaraka ya Bunge, katika barua yangu  kwa katibu wa Bunge niliyoiwasilisha leo tarehe 3 Januari 2013 nimetaka kupatiwa nakala za mikataba yote ya miradi inayotekelezwa hivi sasa ya maji katika Jiji la Dar es Salaam ili kuendelea kufanya kazi ya kibunge ya kuishauri na kuisimamia serikali kueupusha kasoro zilizojitokeza katika miradi ya miaka iliyopita kujirudia hivi sasa.


  Kati ya mikataba niliyotaka kupatiwa ni ile ya miradi ya miundombinu inayoendelea kujengwa na mikopo iliyopatikana kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu huyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa  Mpango Maalum wa Maji Dar es salaam 2011-2013 ambao uliwasilishwa katika Baraza la Mawaziri mwezi Machi 2011 na kuridhiwa kutekelezwa ukihitaji jumla ya shilingi bilioni 653.85; ambao utekelezaji wake unasuasua.


  Izingatiwe kwamba Jiji la Dar es salaam lina adha ya maji ya muda mrefu ambayo kila mkazi wa jiji hili ana wajibu wa kuhakikisha inapatiwa ufumbuzi hivyo mwaka 2013 utumike kuongeza msukumo wa uwajibikaji katika sekta ya maji ambayo ni muhimu kwa uchumi wa nchi na maisha ya wananchi.


  Pamoja na kuwa matokeo ya sensa ya mwaka 2012 kiwilaya na kimikoa bado hayajatangazwa, Jiji la Dar es salaam linakadiriwa kuwa na wakazi zaidi ya milioni nne; hivyo ni sawa na takribani asilimia kumi ya watanzania wote milioni 44.9 waliotangazwa.


  Upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es salaam miaka michache baada mwaka 1961 ulikuwa zaidi ya asilimia 68; hivi sasa miaka 51 baada ya uhuru tumerudi nyuma na upatikanaji ni kwa wastani asilimia 55 tu tena kwa mgawo.


  Pamoja na kero ya mgawo wa maji hali hii imesababisha ongezeko kubwa la bei ya maji kwa wananchi wa kipato cha chini wanaotegemea kupata maji kutoka sekta binafsi ambapo wanaonunua maji kwa madumu hununua bei ambayo ni takribani mara 15 ya bei ya mteja anayepata huduma ya maji ya bomba.


  Hali ni mbaya zaidi kuhusu uondoaji wa maji taka ambapo ni chini ya asilimia 10 tu ya makazi ndiyo yaliyounganishwa katika mtandao wa maji taka na hivyo kuleta uchafuzi wa mazingira hususani katika maeneo yasiyopimwa. Hata katika maeneo yaliyopimwa Jijini Dar es salaam mitandao ya maji taka haijakarabatiwa na kupanuliwa kwa wakati kwa kuzingatia ongezeko la watu suala ambalo lisipochuliwa kwa uzito unaostahili madhara yatatokea katika siku za usoni.


  Hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi na uondoaji wa maji taka zinapaswa kuchukuliwa kuhusu hali hii kwa kuzingatia kuwa idadi ya watu katika Jiji la Dar es salaam inaendelea kukua kwa kasi likiwa ni jiji la tatu kwa ongezeko kubwa la watu barani Afrika na la tisa duniani.


  Kwa nyakati mbalimbali katika kipindi cha kati ya mwaka 2000 mpaka 2010 Serikali imekuwa ikitoa ahadi za kumaliza tatizo la majisafi na majitaka katika Jiji la Dar es Salaam bila utekelezaji sahihi, kamili na wa haraka; hivyo uamuzi wa kutumia sheria ya haki, kinga na madaraka ya Bunge na kazi zingine za kibunge nitakazozifanya mwaka huu wa 2013 zitaongeza uwajibikaji katika sekta ya maji kwa manufaa ya wananchi na nchi kwa ujumla.


  Imetolewa mtandaoni tarehe 4 Januari 2013 na:


  John Mnyika (Mb)

  Jimbo la Ubungo

  0 0

   Waombolezaji wa Msiba wa Msanii wa Filamu hapa nchini,Marehemu  Sadick Juma Kilowoko wakibeba jeneza lenye mwili wake tayari kwa taratibu za kwenda Mazikoni,wakitokea Nyumbani kwa Marehemu Tabata Bima.Sasa hivi mwili wa Marehemu upo katika Msikiti wa Sheahk Adhir,Kariakoo kwa ibada ya Kusalia Mwili na baada ya Swala ya Ijumaa,Mwili utazikwa kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
  Mwili ukipakiwa kwenye gari.
  Dua ikisomwa kabla ya kuondoka na Mwili wa Marehemu kwenda mazikoni.
  Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania,Saimon Mwakifwamba akimpokea Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe alipokuwa akiwasili msibani hapo.
  Waombolezaji wakiwa Msibani mapema asubuhi hii.
  Pamoja na kwamba kulikuwa na Mvua kubwa lakini hakuna alitaka kuondoka msibani hapo mpaka pale mwili ulipoondoka kuelekea Msikitini kwa Kusalia na baadae kwenye Mazishi.
  Mwili ukiondoka nyumbani.

  0 0
  0 0


   Wafanyakazi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar wakifanya usafi katika maeneo ya Ofisi yao Rahaleo mjini Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za kuazimisha miaka 49 ya Mapinduzi Zanzibar ambapo kilele cha sherehe hizo ni January 12. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.


  0 0


   Meneja bidhaa na masoko Francis Ndikumwami akionyesha kipeperushi cha huduma ya SMS kichizi  wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo itakayowawezesha wateja wa Airtel nchini kutuma ujumbe mfupi wa sms kwa shilingi 1 kwa sms masaa 24 kwa siku 7 za wiki, kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Rahma Mwapachu  kushoto ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde. 
   Meneja Masoko wa Airtel Rahma Mwapachu akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuzindua huduma ya SMS kichizi ambapo wateja wa Airtel sasa wanaweza kutuma sma kwa gharama ya shilingi 1 kwa sms masaa 24 kwa siku 7 za wiki, katikati ni Meneja bidhaa na masoko Francis Ndikumwami na kushoto ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde
  Meneja bidhaa na masoko Francis Ndikumwami akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuzindua huduma ya SMS kichizi ambapo wateja wa Airtel sasa wanaweza kutuma ujumber mfupi (sms) kwa gharama ya shilingi 1 kwa sms masaa 24 kwa siku 7 za wiki, katikati ni na kushoto ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde na kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Rahma Mwapachu
  ==========   =========  =========

  Wateja wa Airtel sasa kutuma SMS kwa Shilingi Moja

  ·         Ujumbe mfupi utatozwa shilingi 1 badala ya shilingi 54 kwa sms
  ·         Sms kwenda mtandao wowote nchini

  3 January 2013, Airtel Tanzania kampuni ya simu inayoongoza kwa mtandao mpana na huduma bora na bei nafuu leo imetangaza bei mpya yenye  punguzo la gharama za kutuma ujumbe mfupi  ili kuwapati wateja wake urahisi na unafuu wa huduma ya ujumbe mfupi nchini.  Airtel imepunguza gharama za  sms kutoka shilingi 54 hadi shilingi 1 kwa kila sms. 

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa gharama mpya ya sms Meneja bidhaa na masoko Francis Ndikumwami alisema” Leo tunayofuraha kuzindua SmS Kichizi ofa ya peeke itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma ujumbe mfupi (sms) kwa gharama nafuu. 

  Hii ni ya kwanza kutoka Airtel ambapo tumewapatia na kuwawezesha wateja wetu nchi nzima kutuma ujumbe mfupi (sms) kwa gharama nafuu ya shilling 1 kwa kila ujumbe mfupi kwenda kwenye mtandao wowote masaa 27 siku 7 za wiki bila kikomo. sasa wateja wa Airtel watatozwa shilling 125 kwa ujumbe wa kwanza wa sms na zingine zitakazofuata zitatozwa gharama ya shilling moja kwa siku”.

  “SMS kichizi huduma ya ujumbe mfupi ni mwendelezo wa kutimiza dhamira yetu ya kutoa huduma bora, kuwapa wateja wetu uzoefu wa pekee katika huduma zetu za wateja na kutoza gharama nafuu. Airtel leo ndio mtandao ulioenea zaidi maeneo mengi nchini na kuwafikia watanzania wengi zaidi kupitia huduma zetu za Airtel money na internet yenye kasi zaidi nchini.” aliongeza Ndikumwami

  Gharama hizi mpya za ujumbe mfupi zitatozwa kwenda mitandao ya ndani ya nchini tu na ni  kwa wateja wa Airtel wa malipo ya awali nchini.

  Akiongea kuhusu muda wa huduma hii Francis Ndikumwami alieleza, Airtel tunawajali wateja wetu hivyo huduma hii ya SMS Kichizi sio promosheni ni huduma ya kudumu.

  Airtel bado inaendelea na promosheni yake ya msimu wa sikukuu ya Amka millionea ambapo wateja wengi nchini nzima wameendelea kujishindia pesa taslimu ambapo wateja zaidi ya 300 wameshajishindia jumla ya pesa taslimu zaidi ya shilling million 120 hadi sasa.

  0 0


  MCHAKATO WA MISS UTALII TANZANIA NGAZI ZA MIKOA WAKAMILIKA
  KAMBI RASMI YA FAINALI ZA TAIFA KUANZA JUMAMOSI WIKI IJAYO
  Fainali za mashindano ya Miss Utalii Tanzania na mchakato wa kuwapata wawakilishi wa mikoa katika Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania umekamilika katika mikoa yote ya Tanzania.

  Mikoa hiyo na majina ya warembo katika mabano ni Arusha(Rose Godwin),Dar es Salaam 3 (Irine Thomas), Dar es Salaam 1(Sophia Yusuph 21) ,Dar es Salaam 2(Ivon Stephen,21) ,Dodoma(Erica Elibariki,20), Geita (Jamia Abdul,19), Iringa(Debora Jacob Mwansepeta ), Kagera (), Kilimanjaro(Anna Pogaly,23), Kigoma ( Zena Sultan,18), Katavi (Asha Ramadhani,22), Lindi (Joan John,18), Mara(Doreen Bukoli,18), Mbeya (Dayana Joachim,19), Mwanza(Jessica Peter Rugalabamu,18), Mtwara (Halima Hamis Suleman,19), Morogoro ( Hadija Saidi,21), Manyara (Mary Chrysostom Rutta,18) Njombe (Paulina Renard Mgeni,20), Pwani (), Rukwa (Anganile Rogers Emmanuel ,22), Ruvuma( Furaha Amon Kinyunyu ,23), Singida (Neema Julius,20),  Simiyu (Flora Msangi,22), Shinyanga (Lightness Kitua,19),Tabora (Magreth Michael Malale,20 ),Tanga (Sarafina Jackson Chales,18),Vyuo Vukuu 1(Irine Richard Makoye,21), Vyuo Vikuu 2 (Hawa Nyange, 22)
  Washindi wa kwanza na wa pili wa kila mkoa watawakilisha mikoa yao, katika Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu,fainali ambazo zimepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu,katika Ukumbi wa Dar Live Dar es Salaam. Fainali za mwaka huu zitatanguliwa na kambi ya siku 21 ya washiriki wote itakayo kuwa katika Hoteli ya kitalii ya Ikondelelo Lodge Dar es Salaam.
  Maandalizi kwa ajili ya kuanza rasmi kambi ya Taifa yanaendelea na yamekamilika kwa zaidi ya 96%,tupo katika hatua za mwisho za kukamilisha Taratibu za Baraza La Sanaa la Taifa,ukiwemo kulipa ada ya shindano ya shilingi 1,500,00.00,kabla ya uzinduzi rasmi wa kambi utakao fanyika katika hoteli ya Ikondelelo, Kibamba Dar es Salaam,tarehe 8-1-2013.
  Washiriki wote watawania taji la Miss Utalii Tanzania 2012/13 .sambamba na tuzo 28 mbalimbali za heshima za Jamii, Elimu ya Jamii, Afya ya Jamii,Utalii, Utamaduni, Uchumi, Miundo Mbinu ya Utalii, Uwekezaji ,Madini na Maliasili mbalimbali za Taifa.
  Fainali za Taifa za mwaka huu ,zitakuwa ni za Tano tangu kusajiliwa rasmi na serikali na mamlaka za haki miliki za kutaifa na kimataifa mwaka 2002,katika kipindi hicho tumefanikiwa kutwaa mataji katika kila mashindano ya Dunia na kimataifa tuliyoshiriki,ambapo hadi sasa tunashikilia zaidi ya mataji matano ya Dunia na kumataifa. Mataji hayo ni pamoja na Miss Tourism World 2005- Africa, Miss Tourism world 2006-SADC, Miss Tourism World 2007-Africa,Model Of The World 2006-Personality, Miss Africa 2006-1STRunner Up na Miss Tourism World 2008-Internet.
  Asante,
  Erasto Gideon Chipungahelo
  Rais/Afisa Mtendaji Mkuu

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya msanii Sajuki leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam
   Jeneza lenye mwili wa marehemu Sadick Juma Kilowoko a.k.a Sajuki ukiwasili kwenye makaburi ya Kisutu,Upanga jijini Dar kwa ajili ya mazishi. 

   Baadhi ya watu waliofika kwenye mazishi ya marehemu sajuki jioni ya leo Kisutu,jijini dar.
   Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh Zitto Kabwe akifafanua jambo mbele ya baadhi ya Wanahabari kabla ya mazishi ya marehemu Sajuki,yaliyofanyika leo Kisutu jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na maelfi ya watu.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza jambo na Meya wa Wilaya ya Ilala,Mh Jerry Silaa ,shoto ni Rais wa Shirikisho la wasanii wa Filamu nchini,Simon Mwakifwamba akisikiliza .
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na baba mzazi wa marehemu Sajuki (pichani shoto) wakati wa mazishi ya msanii huyo  leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.Pichani kati Rais wa Shirikisho la wasanii wa Filamu nchini,Simon Mwakifwamba na mwisho kabisa Meya ya Wilaya ya Ilala,Mh Jerry Silaa.PICHA NA IKULU
   Mwandishi mkongwe wa  kampuni ya Uhuru Publications akiitafusta taswira murua kabisa kwenye mazishi ya marehemu Sajuki,yaliyoongozwa na Rais Kikwete mapema leo jioni kwenye makaburi ya Kisutu,Upanga jijini Dar.
  Baadhi ndugu jamaa na marafiki waliofika kwenye mazsishi ya marehemu Sajuki,wakisubiri mwili wake waupokee kwa ajili ya maziko.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja  na Mshauri Mkuu wa Kijeshi wa Umoja wa Mataifa Luteni Generali Babacar Gaye baada ya kuonana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.Kushoto Mbele ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mahadhi Juma Maalim, akifuatiwa na Mkuu wa Majeshi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange, na wa pili kulia ni Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi na wengine ni maafisa waandamizi katika JWTZ na Umoja wa mataifa.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mshauri Mkuu wa Kijeshi wa Umoja wa Mataifa Luteni Generali Babacar Gaye baada ya kuonana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.Kushoto Mbele ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mahadhi Mahadhi Juma Maalim, akifuatiwa na Mkuu wa Majeshi Tanzania  Jenerali Davis Mwamunyange, na wa pili kulia ni Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi na wengine ni maafisa waandamizi katika JWTZ na Umoja wa mataifa.

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  na Mshauri Mkuu wa Kijeshi wa Umoja wa Mataifa Luteni Generali Babacar Gaye baada ya kuonana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.Kushoto ni  Mkuu wa Majeshi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange. PICHA NA IKULU

  0 0


  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ' Sajuki' nyumbani kwao wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.

    Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ' Sajuki' nyumbani kwao wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo Januari 4, 2013. 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ' Sajuki' Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo ambako walienda kutoa pole leo Januari 4, 2013.PICHA NA IKULU.

  0 0


  Head of Primary Medical Centre Bwa. Siwawi Konteh (wa pili kulia) ambaye pia ni mratibu wa mradi wa Tuunganishe Mikono Pamoja ili kuokoa Afya ya Mama na Mtoto akizungumzia Malengo Makuu ya mradi huo kuwa ni kuongeza kiwango na matumizi ya Huduma ya Afya ya Mama Mjamzito na Watoto na kushirikiana na kujifunza kuhusu Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto. Kutoka kushoto ni Acting Medical Director wa Aga Khan Hospital Dr. Ambrose Chanji, Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib, Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Dr. Sebastian Ndege na Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu cha Hospitali hiyo Bw. Anis Nazrani.
  Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa kukabidhi magari ya kubeba wagonjwa kwa hospitali ya Aga Khan ambapo amesema vifo kadhaa vinavyotokea katika hospitali nyingi kwa sasa vinawahusisha akinamama na watoto wasio na hatia ambao hukosa huduma za awali za haraka zikiwemo usafiri na hivyo katika kujali hilo wametoa magari hayo.
  Aidha amesema Ndege Medics inashukuru kuwa sehemu ya mradi endelevu wa kujaribu kuokoa maisha ya akina mama na watoto ambao lengo lake ni kuchangia katika kuboresha afya ya uzazi wa mama na watoto wachanga katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Mwanza, Mbeya na Morogoro.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa magari ya kubeba wagonjwa kwa Hospitali ya Aga Khan ikiwa ni katika mradi wa kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto Tanzania
  Wakipongezana baada ya makabidhiano hayo.
  Mmoja wa wafanyakazi wa Ndege Medics akionyesha baadhi ya vifaa vilivyomo ndani ya magari hayo ya kisasa.
  Pichani Juu na Chini ni muonekano wa magari hayo ya kubebea wagonjwa kwa ndani yaliyotelwa kwa hospitali ya Aga Khan na NDEGE Medics kwa ajili ya mradi wa kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto Tanzania.
  Pichani Juu na chini ni baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege Medics, Hospitali ya Aga Khan na waandishi wa habari walioshuhudia tukio la makabidhiano hayo.

  Baadhi ya magari ya kubebea wagonjwa yaliyokabidhiwa rasmi leo kwa Hospitali ya Aga Khan jijini Dar ikiwa ni sehemu ya mradi Endelevu utakaohusisha Mikoa ya Mwanza, Dodoma, Iringa, Mbeya na Morogoro kwa ajili ya kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto.

  0 0


  0 0

   Pichani kati Mh.Amos Makalla  akifafanua jambo mbele ya wanahabari.
  Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Uwanja wa Taifa, Rish Moses Urio (kushoto) wakati Waziri huyo na baadhi ya wadau wa Mpira wa Miguu walipotembelea kujionea miundombinu mbalimbali ya Uwanja huo Dar es Salaam jana.

  0 0
 • 01/05/13--02:41: mdau anatafuta mchumba.

 • Natafuta Mchumba wa kuanza naye Maisha.
  Naitwa Fatma Ally ni mtanzania kutoka Zanzibar ila kwa sasa naishi hapa Doha,Qatar na ninafanya kazi na kampuni ya chakula hapa Doha,Ninatafuta mchumba wa kuanza naye maisha ya ndoa,ni lazima awe Muslim wa Tanzania bara au Zanzibar,mkweli na mcha Mungu,Sibagui langi wala kabila au kipato,awe na mapenzi ya dhali.
  Naomba tuwasiliane kwa email ifuatayo;

  0 0

   Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam. 

  Katika hotuba yake Mama Asha amewahasa vijana hususan wanafunzi hao waliohitimu masomo kutokukubali kutumika na watu wenye maslahi binafsi na kujikuwa wakisababisha uvunjifu wa amani. Aidha amewataka kutojihusisha na makundi yanayochochea uvunjifu wa amani bila kujitambua wafanyalo, badala yake amewambo kuwa wakipima kila wanaloambiwa kuwa linamaslahi na dini yao ama maslahi kwa jamii na taifa kwa ujumla. Picha Zote na www.sufianimafoto.blogspot.com
   Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita, Latifah Nuhu, wakati wa sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam. 
   Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita, Mwinga Gwao, wakati wa sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
   Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi zawadi mhitimu wa Kidato cha Sita, Zuhura Azmin, kwa kuwa mmoja kati ya waliofanikisha sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam. 
   Baadhi ya wahitimu wa kike wakiwa katika mahafali hayo leo.
   Baadhi ya wahitimu wa kiume, wakiwa katika mahafali hayo leo.
  Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita, Khadija Hassan, wakati wa sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
   Dua baada ya shughuli hiyo kukamilika.
  Mama Asha, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya wanafunzi wahitimu wa kidato cha sita, baada ya zoezi la kugawa vyeti kwa wahitimu. 

older | 1 | .... | 4 | 5 | (Page 6) | 7 | 8 | .... | 1897 | newer