Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 592 | 593 | (Page 594) | 595 | 596 | .... | 1896 | newer

  0 0

  22
  Rais Jakaya Kikwete, akiwaaga baadhi ya Mashujaa waliopigana vita kuikomboa Tanzania.
  10
  Rais akiweka mkuki na ngao kwenye mnara wa Uhuru.
  11
  Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akirejea kwenye sehemu yake baada ya kuweka sime kwenye mnara.

  23
  Makamu wa Rais Dkt. Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Iddi na Spika wa Bunge Anne Makinda wakiondoka kwenye viwanja vya mnazi mmoja.
  242526
  Baadhi ya askari wa JWTZ waliopigana vita ya kuikomboa Tanzania.
  1
  Brass Bendi ya Jeshi ikiingia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kuanza Maadhimisho.Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO
  23
  Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa (JWTZ) , Luteni Jenerali Samweli Ndomba akisalimiana na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli baada ya kuwasili viwanja vya mnazi mmoja.

  4
  Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho akiwasili.
  5
  Spika wa Bunge la Jamhuri Anne Makinda akiwasili.
  6
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd.
  7
  Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwasili.
  8
  Rais Jakaya Kikwete akiwasili.
  9
  Rais Jakaya Kikwete akiwaongoza viongozi mbalimbali na wananchi kuimba wimbo wa Taifa.
  12
  Kiongozi wa Mabalozi akiweka shada la amaua.
  13
  Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Dkt. Didas Masaburi akiwa ameweka upinde na mshale kwenye mnara.
  14
  Mwenyekiti wa Tanzania Legion akiweka shoka kwenye mnara.
  15
  Baadhi ya wazee walioipigania Tanzania, viongozi wa dini na wageni waalikwa waliohudhuria.
  1617
  Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam sheikh Alhad Musa Salum akisoma dua.
  18
  Mchungaji Theophil Bolampete wa Kanisa Katoliki akiomba.
  19
  Mchungaji John Komoyo, akiomba.
  20
  Rais Jakaya Kikwete akiongoza viongozi mbalimbali kuimba wimbo wa Taifa baada ya Maadhimisho kukamilika.

  27
  Baadhi ya wananchi waliofika nje ya viwanja vya Mnazi Mmoja kushuhudia Maadhimisho.

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar Ndg Adila Hilal Vuai, akiutambulisha Ujumbe wa Madaktari Diaspora kutoka Washington walioletwa na Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Washington  wakali walipofika katika Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar walipofika hapo kutowa Elimu ya Afya ya Saratani ya Matiti na Mano, wakiwa Zanzibar kwa uwenyeji wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ)
  Rais wa Jumuiya ya Watanzania Washinton Ndg Iddi Sandaly akiutambulisha Ujumbe wa Madaktari 17 Diaspora, waliofika Zanzibar kutoa Tiba ya Maradhi ya Saratani ya Matiti, Kisukari na Meno akitowa maelezo wakati walipofika katik Chuo cha Elimu ya Afya Mombasa Zanzibar, na kutowa Elimu ya kutambua Saratani ya Matiti kwa Kinamama. na kutowa huduma ya uchunguzi wa Meno.
  Rais wa Jumuiya ya Wanawake Afrika Washington (Africa Womens Cancer Awereness Association ) Dr Ify Anne Nwabukwu, akiutambulisha ujumbe wa Madaktari wa maradhi mbalimbali waliowasili Zanzibar kwa ajili ya kutowa huduma kwa wananchi wa Zanzibar ikiwa ni kusaidia Wafrika wenzao walioko Afrika.
  Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar wakimsikiliza Dr Ify akitowa maelezo na kuwatambulisha Madaktari Diaspora aliofuatana nao. 
  Dr Ify Anne Nwabukwu akitowa Elimu ya tambua viashiria vya Saratani ya Matiti kwa wanafunzi hao wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar.
  Dr Ify akitowa mada kuhusiana na Saratani ya Matiti kwa Wanafunzi wa Chuo hicho hutoa Elimu ya Udaktari wa aima mbalimbali chuoni hapo.
  Dr Ify akionesha Mashine ya kupimia Saratani ya Matiti ya Kisasa inayoitwa MamaGram hutumika kucunguza viashiria vya Saratani ya Matiti kwa Wanachuo hao wakati akitowa Elimu ya Saratani ya Matiti jinsi ya kumgundua Mwanamke mwenye matatizo hayo. 
      Wanafunzi wa Chuo hicho wamepata fursa ya kuuliza mswali wakati wa Mafunzo hayo.
  Mmoja wa Madaktari hayo akitowa mfano hai kutokana na matatizo ya Saratani ya Matiti, kwa Wanachuo hao. 
  Daktari wa Meno Bi Queenate Ibeto akitowa elimu ya kutunza meno na kinga ya mane kwa Wanafunzi hao jinsi ya kuyatunza meno. wakati walipofika Chuoni hapo kutowa Elimu kwa Wanachuo hicho. 
  Daktari wa Meno Venessal Quitero akionesha moja ya tiba ya kunusuru meno kwa wanafunzi hao wakati wakitowa Elimu ya Utunzaji wa Meno na tiba yake.
  Mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar akionesha mafunzo ya utunzaji wa Meno kwa vitendo jinsi ya kupiga msuwaki inavyotakiwa kuweza kuimarisha meno kuwa imara.
  Dr Queenate Ibeto akionesha mfano ya vitendo kwa mmoja wa mnafunzi wa Chuo hichi jinsi ya utumiaji wa msuaki katika kupiga kwa Wanafunzi hao, wakati walipofika kutoa Elimu ya Afya kwa Wanafunzi wa Chuo hicho Mombasa Zanzibar. 
  Profesa Hailu na Dr Quintero wakifuatilia Mada zilizokuwa zikiwakilishwa kuhusiana na Saratani ya Matiti na Tiba ya Meno, kwa Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar Mombasa wakati walipofika katika Chuo hicho wakiwa Zanzibar kwa ajili ya kutoa Tiba ya Saratani ya Matiti Ugonjwa wa Kisukari na Meno.
  Dr Quintero ni mtaalamu ya Magonjwa ya Meno akifafanua moja ya swali lililoulizwa na Wanafunzi wa Chuo hicho. 
  Mwanafunzi wa chuo hicho akiuliza swali kuhusiana na baadhi ya Wananchi meno yao huwa na ukungu mweusi kwa wataalam hao
  Madaktari wa Diaspora wakigawa misuwaki na dawa za meno kwa wanafunzi hao baada ya kutowa Elimu chuoni hapo,
  Dr Silvia Dasi akitowa maelezo kwa wanafunzi hau jinsi ya kumgundua mwanamke mwenye matatiti ya Saratani ya Matiti wakati wakifanya mafunzo hayo kwa wanafunzi hao wanaochukua Elimu ya Afya ya binadamu,
  Dr Silvia Dasi akitowa maelezo kwa wanafunzi hau jinsi ya kumgundua mwanamke mwenye matatiti ya Saratani ya Matiti wakati wakifanya mafunzo hayo kwa wanafunzi hao wanaochukua Elimu ya Afya ya binadamu,  
  Dr Ify  akitowa Elimu ya Vitendo kugundua viashiria vya Saratani ya Matiti kwa Mwanamke akitowa mafunzo hayo ya mmoja wa mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar.
  Dr Ify akitowa Elimu ya Vitendo kugundua viashiria vya Saratani ya Matiti kwa Mwanamke akitowa mafunzo hayo ya mmoja wa mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar kulia Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar Ndg Adila Hilal Vuai,
  Madaktari Diaspora wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar baada ya kutoa Elimu kwao,
  DR Queenate Ibote akimfanyia uchunguzi wa meno mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar wakati walipofika Chuoni hapo kutowa Elimu kwa Wanachuo hicho.
  DR Queenate Ibote akimfanyia uchunguzi wa meno mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar wakati walipofika Chuoni hapo kutowa Elimu kwa Wanachuo hicho.
  DR Queenate Ibote akimfanyia uchunguzi wa meno mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar wakati walipofika Chuoni hapo kutowa Elimu kwa Wanachuo hicho.
  Madaktari wa Diaspora wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar wakiwa nje ya jengo la Chuo hicho katika Skuli ya Sekondari ya SHAA Mombasa Zanzibar. Picha na OthmanMapara.Blog  Zanzinews.Com

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma Zanzibar (CHAUMMA) Faki Salum Abdalla akitoa salamu za Chama hicho wakati wa Mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) wa kumtambulisha Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho katika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini Zabnzibar.
  Picha No. 2152- Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza mgombea nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia CHAUMMA katika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar.
   Baadhi ya Wanahabari waliohudhuria mkutano huo
    Katibu Mkuu wa CHAUMMA Ali Omar Juma akitowa wasfu wa mgombea nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama hicho katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar.
  Mgombea Kiti cha Rais wa Zanzibar kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma  (CHAUMMA) Mohd Masoud Rashid akijitambulisha na kueleza sera zake mbele ya waandishi wa habari katika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye Ulemavu  Kikwajuni, Mjini Zanzibar. (kulia) mgombea mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho Issa Abass na (kushoto) Katibu Mkuu Ali Omar Juma. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Znz.

  0 0

  Charles Magali akiwa ndani ya Kilimanjaro Studio zinazomilikiwa na Vijimambo Radio, Kwanza Production na NesiWangu Media
  Ijumaa ya Julai 24, 2015, mwigizaji na mwimbaji wa muziki nchini Tanzania Charles Magali alipata fursa ya kutembelea studio zetu zilizopo Beltsville Maryland. Hapo akazungumza nasi kwa ufupi,Karibu umsikilize akihojiwa na Mbunifu na Mtayarishaji wa kipindi hiki Dj Luke Joe na Mubelwa Bandio

  0 0

  MKURUGENZI wa Msama Promotions, Alex Msama  amewaita Maaskofu na viongozi wengine wa dini katika uzinduzi wa albamu tatu za mwimbaji nguli Bonny Mwaitege zinazotarajia kuzinduliwa Agosti 2 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

  Kwa  mujibu  wa  Msama  ambaye  ni  mdhamini  wa  uzinduzi  huo, Maaskofu watafikisha  ujumbe wa neno la Mungu  kwa karibu zaidi baada ya waimbaji kumaliza kazi yao jukwaani.

  Msama alisema uzinduzi huo unatarajia kusindikizwa na waimbaji mbalimbali wa Tanzania na nje lengo likiwa ni kufanikisha uzinduzi mahiri wa albamu hizo. Msama alisema pamoja na uzinduzi huo kusindikizwa na waimbaji mahiri pia, waimbaji chipukizi watamsindikiza Mwaitege ambaye hivi sasa anaendelea na mazoezi kuelekea uzinduzi huo.

  Aidha Msama alisema hivi sasa muimbaji huyo pia anamalizia kurekodi baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hizo katika majiji ya Mwanza, Arusha, Mbeya  na Nairobi. Msama alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa mashabiki wa muziki wa injili kujiandaa na uzinduzi huo ambao utakuwa ni wa aina yake.

  "Maandalizi makubwa kuelekea uzinduzi wa Mwaitege yameshafanyika, kilicho mbele ni uzinduzi wa hali ya juu, mashabiki wakae mkao wa kula," alisema Msama na kuongeza. "Uzinduzi wa Mwaitege utakuwa ni wa aina yake kwa sababu maandalizi yake kwa sababu yamefanywa kwa ustadi mkubwa, mashabiki watarajie kazi bora zaidi kutoka kwa muimbaji huyo," alisema.  

  Bonny Mwaitege anatamba na nyimbo mbalimbali kama Mama ni Mama, Mke mwema, Wakusamehe, Fungua Moyo wako, Njoo  uombewe na  Yesu yupo.

  0 0

  SAM_4394Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima aliyeshinda katika kura za maoni za kutafuta wabunge wa viti maalum mkoa wa Arusha kupitia jumuiya ya wazazi wa chama cha Mapinduzi ( CCM ).akizungumza katika mkutano wa chama cha mapinduzi jana mtaa wa kati (CCM MKOA)wakati wagombea 12 wa chama hicho walipofanya ziara ya kutembelea kila kata na  kujinadi kwa wananchi pamoja na wanachama wa chama hicho ambapo aliwataka wananchi wasirubuniwe na kama walipewa rushwa na mgombea yeyote wasimchague bali wamchague kiongozi sahihi wa kuleta mabadiliko ya kimaendeleo  katika jimbo la Arusha(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog) 
  SAM_4366Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalimaambaye alishinda katika   kura za maoni za kutafuta wabunge wa viti maalum mkoa wa Arusha kupitia jumuiya ya wazazi wa chama cha Mapinduzi ( CCM ).  ambaye pia ni Afisa masoko wa Triple "A",Mkurugenzi wa Phide entertainment akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Monaban yajijini Arusha,Philemon Mollel ambaye pia ni Mgombea Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM katika ofisi za (CCM Mkoa) jijini Arusha jana
  SAM_4398Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau akizungumza katika mkutano wa kuwanadi wagombea Ubunge kupitia chama cha mapinduzi mtaa wa kati jijini Arusha ambapo aliwataka wapambe wawagombea watulize mung'ari zao na kuacha tabia ya kukebihana huku akisisitiza wananchi kuchagua kiongozi bora.
  SAM_4363Kada maarufu wa chama cha mapinduzi ambaye pia  ni mfanyabiashara wa madini jijini Arusha Justine Nyari, anayeomba ridhaa ya ccm katika nafasi ya ubunge akiteta jambo na Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima  ambaye pia ni Afisa masoko wa Triple "A" na Mkurugenzi wa Phide entertainment kabla ya mkutano wao wa kujinadi kuanza
  SAM_4368Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima  ambaye pia ni Afisa masoko wa Triple "A"na Mkurugenzi wa Phide entertainment akibadilishana mawazo na wakili msomi Edimond Ngemela anayeomba ridhaa ya ccm katika nafasi ya ubunge
  SAM_4374Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima  ambaye pia ni Afisa masoko wa Triple "A" na Mkurugenzi wa Phide entertainment akiwa katika picha ya pamoja na watia nia nafasi ya Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM
  SAM_4376Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima  ambaye pia ni Afisa masoko wa Triple "A"na Mkurugenzi wa Phide entertainment, akisalimiana na mtia nia nafasi ya Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM Thomas Munisi ,ambapo Mwakitalima aliibuka  mshindi katika kura za maoni za kutafuta wabunge wa viti maalum mkoa wa Arusha kupitia jumuiya ya wazazi wa chama cha Mapinduzi ( CCM ).
  SAM_4372Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima  ambaye pia ni Afisa masoko wa Triple "A" akisalimiana na wadau ambao ni watia nia Ubunge na  Udiwani,kushoto ni Simba Salum anayeomba chama cha mapinduzi kumpitisha kuwania nafasi ya udiwani mtaa wa kati bondeni na kulia wakili msomi Edimond Ngemela anayeomba ridhaa ya ccm katika nafasi ya ubunge

  0 0

  SHIRIKA  la ndege la taifa (ATCL) limeupongeza utawala wa awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete huku likibainisha kuwa licha ya changamoto zilizo likabili shirika hilo katika kipindi cha awamu hiyo bado limefanikiwa kulinda hadhi yake sambamba na kuibua mipango inayolenga kuliibua upya shirika hilo.
  Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusiana na  utendaji wa shirika hilo katika kipindi hicho cha awamu ya nne, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Bw. Johnson Mfinanga aliitaja baadhi ya mikakati iliyoundwa juu ya msingi wa serikali ya awamu ya nne katika kuboresha zaidi huduma za shirika hilo.
   “Ni katika kipindi hiki cha awamu ya nne chini ya Rais Kikwete  ndio tuliweza kuanzisha safari zetu za kwenda visiwa vya Comoro na tumekuwa tukizidi kuongeza safari zetu zaidi kuelekea huko kwa kuwa tumebaini uamuzi huu umekuwa na tija kwa wananchi wa mataifa haya mawili,’’ alibainisha Bw. Mfinanga ambaye shirika lake kwa sasa limeongeza idadi ya safari zake kuelekea visiwa hivyo  kutoka mara tano hadi kufikia mara saba kwa wiki.
  Kwa sasa shirika hilo ndio shirika pekee la ndege hapa nchini linalotoa huduma zake kutoka Dar es Salaam kuelekea visiwa vya Comoro na hivyo kutoa fursa kwa wananchi wa mataifa hayo mawili  kuweza kuunganisha fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye mataifa hayo ikiwemo biashara, kwa mujibu wa Bw. Mfinanga.
  Zaidi Bw. Mfinanga alibainisha mpango wa shirika hilo wa kutambulisha safari zake za moja kwa moja baina ya visiwa vya Comoro na Zanzibar kabla ya mwisho wa mwaka huu kutokana na uhitaji mkubwa wa soko linachochewa na fursa za kibiashara baina ya visiwa hivyo.
  Aliongeza kuwa pamoja na mipango hiyo shirika hilo pia linaendelea kuboresha huduma zake kuelekea mkoani Mtwara na limekuwa likijivunia kuwa kiungo muhimu katika usafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoa huo ambao kwa sasa unajipanga kuchangamkia fursa ya uchumi wa gesi iliyovumbuliwa hivi karibuni.
  “Tumekuwa tukifanya safari zetu kuelekea mkoani Mtwara kwa kipindi kirefu sasa. Fursa ya gesi iliyoibuka mkoani humo inasababisha na sisi pia tujipange kwa kuangalia ni namna gani tutanufaika na fursa hiyo pia. Lakini pia tuna jukumu la kuhakikisha tunatimiza wajibu wetu kama shirika la taifa katika kukabiliana na mahitaji ya wananchi wa taifa hili,’’ alisema.
  Akizungumzia mipango ya shirika hilo katika kujipanua zaidi, Bw. Mfinanga alisema kwa sasa shirika hilo linaandaa mpango mkubwa wa miaka mitano ambao unatarajiwa kukamilika na kuwekwa wazi hivi karibuni.
  Kwa sasa shirika hilo linatoa huduma zake kuelekea mikoa ya Kigoma, Mtwara na visiwa vya Comoro kwa kutumia ndege yake aina ya CRJ-100  wakati ikiendelea kusubiri ndege yake nyingine aina ya De-Havilland Dash 8 Q300 inayoendelea na ukarabati mkubwa kwenye karakana ya shirika hilo iliyopo kwenye uwanja wa Kimataaifa wa Julius Nyerere (JNIA) , jijini Dar es Salaam.
  “Kukamilika kwa ukarabati wa ndege hiyo kutasaidia tuweze kurejesha huduma zetu kuelekea mikoa ya Mwanza, Tabora, Kilimanjaro na Mbeya,’’ alisema Bw Mfinanga.

  0 0

  Meneja Bidhaa wa benki ya Exim, Bw Aloyse Maro akiokota moja ya kura za wateja wakati wa kuchezesha bahati nasibu ya kwanza ya kampeni ya akaunti ya malengo inayoendeshwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Wanaoshuhudia ni pamoja na mwakilishi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Bw. Humudi Abdulhussein  (kushoto) na mmoja wa maafisa wa beki hiyo Bw George Musetti.

  Benki ya Exim Tanzania imeendesha  droo yake ya kwanza ya kampeni ya akaunti ya malengo inayolenga kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba miongoni mwa watanzania.

  Droo hiyo iliyosimamiwa na Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini iliendeshwa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam ikiwa ni droo ya kwanza kati ya sita zinazotarajiwa kuendeshwa katika kampeni hiyo.

  Akizungumza mara tu baada ya droo hiyo, Meneja bidhaa wa benki hiyo, Bw. Aloyse Maro alisema kampeni hiyo ilizinduliwa ikiwa ni sehemu ya jitahada za benki hiyo kuwapatia wateja wake faida zaidi sambamba na huduma bora.

  Alisema kwa kuanzia, washindi waliopatakina kupitia droo hiyo walifanikiwa kujitwalia zawadi za simu za kisasa aina ya iPhone 6 huku akitoa wito zaidi kwa wateja wa benki hiyo kuwa na mwitikio zaidi kwa kushiriki kwenye kampeni hiyo.

  “Pamoja na kutoa shukrani zetu kwa wateja wetu kutokana na mafanikio tunayoendelea kuyapata ni vema pia tuwe mrejesho wa mafanikio haya  kwao pia. Ni katika mazingira hayo ndio maana tumekuwa na utaratibu wa kutoa zawadi kwa wateja wetu ili kufurahi nao pamoja,’’ alisema Bw. Maro.

   Zaidi Bw. Maro aliwakumbusha wateja wa benki kuendelea kushiriki zaidi kwenye kampeni hiyo kwa kuwa bado wananafasi zaidi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi ya gari kwenye droo tano zilizosalia.

  “Kampeni hii inaendelea kwa kipindi cha miezi mitano na bado kuna zawadi zaidi kwa ajili ya washiriki ikiwemo zawadi kuu ya gari ambayo itakabidhiwa kwa mshindi mwishoni mwa kampeni hii. Hivyo tunaomba watu waendelee kushiriki zaidi,’’ alisema.
   Sambamba na zawadi hizo Bw. Maro aliongeza kuwa kampeni hiyo inatoa riba nzuri zaidi kwa wateja wanaofungua akaunti hiyo ya malengo.

  0 0

  Kama ambavyo aliweza kufanya vizuri na singo yake ya kwanza, msanii Galaxy anatarajia kuchomoka na wimbo wake mpya ‘mzuri tu’ ukiwa umeandaliwa na Man Walter chini ya studio za Combination sound hivi karibuni jijini Bongo.

  The smart boy Galaxy Ikanda akiwa maejipanga fresh kwa ujio wake mpya, alielezea sababu zinazompelekea kutumia muda wake mwingi kujipanga na sio kukurupuka “Muziki umekuwa na ushindani mkubwa sana kiasi inampelekea msanii makini kuongeza umakini  na ubunifu kwenye utendaji Otherwise unaweza kujikuta kila siku umesimama sehemu moja huendi mbele, kitu ambacho sikitarajii kulingana na jitihada nilizonazo”.

  Alisema “kinachoturudisha nyuma wasanii wengi ambao tunachipukia ni kutokuwa na nidhamu na kazi zetu wenyewa hata kwa wanaotusimamia (Managers), halikadhalika tuna pupa ya kutafuta shortcut kuyafikia mafanikio kirahisi bila kufanya juhudi, huku mi nasema ni kujidanganya”.

  Galaxy ambaye kwa sasa yuko hewani na wimbo unaojulikana kwa jina la ‘Tam Tam’ amewataka wasanii wenzake kuongeza jitihata kwenye ubunifu na kuepuka kuzihusisha Sanaa zao na maisha yao binafsi ‘KUTENGENEZA KICKI’ kwa maana haiwasaidii na hii inachangia kuudidimiza muziki wetu na Sanaa kwa ujumla.

  “sioni sababu ya msanii kutengeneza story ya uongo ili aweze kutoa wimbo wake, hii inaonesha dhahiri ni kutojiamini na sijawahi kuona imemsaidia msanii kwa kufanya hivyo wimbo ukapata umaarufu mwaka mzima, mara nyingi story za kutengeneza ili kutoa wimbo zikiisha na wimbo umeisha so zinaua muziki wetu kama vipi tukaze” – Galaxy.

  0 0

  Usili wa kwanza wa Dance 100% (2015) umefanyika kwa mafanikio makubwa Temeke jijini Dar es Salaam, ambapo makundi ya Team ya Shamba, The WT Group, WD, The Best Boys Kaka Zao na Team Makorokocho wameweza kushinda nafasi ya kuingia katika michuano kutoka wilaya ya Temeke.

  Makundi haya yamechuana vikali na mengine 6 yanayokamilisha idadi ya makundi 11, UNI 6 Crew, GMF Crew, TWC, Dar Crew, Noma Sana Crew, na Viga Stars yaliyojitokeza kuwania nafasi hiyo katika usajili huo wa kwanza.


  Mratibu wa mashindano hayo kutoka East Africa Television na East Africa Radio, Bi Happy Shame, amesema kuwa amefurahishwa na utulivu na amani ambayo wapenda burudani Temeke wameonyesha leo, huku pia kukiwa na vipaji mbalimbali kutoka makundi yaliyojitokeza katika usaili huo wa kwanza.


  Akizungumza baada ya kumalizika michuano ya usaili huo, mratibu wa Dance 100% kutoka BASATA, Kwerugira Maregesi, mbali na kufurahishwa na vipaji vilivyojitokeza, amekumbushia umuhimu wa makundi hususan yale yanayotarajiwa kushiriki usajili unaofuata, kuzingatia vigezo na masharti yaliyowekwa kujiwezesha kushinda, ikiwepo ubunifu katika mitindo ya kudansi, kuburudisha na muonekano, huku akishauri kupunguzwa kwa mitindo ya sarakasi na kuongezwa ladha katika upande wa dansi zaidi.


  Majaji Super Nyamwela, Queen Darleen na Shetta wametumia umakini nkubwa kuhakikisha wanatoa alama zinazostahili kwa mujibu wa vigezo kwa washiriki wote, huku burudani mbalimbali zikijiri zikishereheshwa kikamilifu na watangazaji rasmi wa Dance 100 kwa mwaka huu, T-Bway 360 na mrembo Maggie Vampire.


  Majaji pia kila mmoja kwa nafasi yake wametaka washiriki watakaoendelea kujitokeza kujipanga zaidi wakizingatia vigezo vilivyowekwa, ambavyo ndivyo wanavyovitumia kutoa maksi (alama) zitakazowawezesha kufikia ushindi.


  Usajili wa pili wa mashindano haya makubwa kabisa ya kudansi utafanyika katika viwanja vya Don Bosco Upanga siku ya Jumamosi Tarehe 01 Agosti 2015, ambapo makundi mengine matano yatasakwa kushiriki katika michuano hiyo kwa mwaka huu.


  Usikose kujionea kwa urefu yote yaliyojiri  pale TCC Chang'ombe katika mashindano ya usajili huo, kwa kutazama ting'a namba moja kwa vijana EATV, siku ya Jumamosi, kuanzia saa 12 na nusu jioni.


  East Africa Television na East Africa Radio inaleta Dance 100% kwa kupewa nguvu na mtandao wa Vodacom Tanzania na Coca Cola ambao ndio kinywaji rasmi cha dance 100% (2015).


  PICHANI JUU: Kati ya makundi matano yaliyopita kwenye usaili wa kwanza wa Dance 100% (2015) - Temeke. Kundi linaitwa 'The Best Boys Kaka Zao'
   Kutoka kushoto -Majaji wa mwaka huu kwenye Dance 100%  ni Super Nyamwela, Shetta na Queen Darleen wakiwa wanajumulisha matokeo ya washiriki kutoka Temeke.
   Shabiki wa kundi la 'Noma Sana' akiwa anajitayarisha kushangilia timu yake kwenye usaili wa kwanza Temeke kwenye Dance 100% (2015)
   Washiriki wa kundi la 'Noma Sana' mwaka huu kwenye Dance 100% wakiwa wanafanya yao viwanja vya TCC Changombe.
  Watangazaji rasmi wa Dance 100%, TBway 360 na Maggie Vampire wakiwa wanasherehesha kikamilifu huku burudani mbalimbali zikijiri TCC Changombe.

  0 0


  Dedicated, professional, eager to succeed, innovative and passionate are just some of the words used to describe Krantz Charles Mwantepele. He realized there was a deficiency and opportunity in Internet marketing but did not wait for changes, he made them happen. With no IT background, just a passion for news reporting, he has successfully
  created three blogs; Mwanaharakati Mzalendo blog, harakati 360 and  Mzalendo Times put as well as an application on Google Play Store for his Mwanaharakati Mzalendo blog. Mwanaharakati Mzalendo has been recognized in the country and in Africa as the one of the best political, news, educational and general blogs. MAN magazine correspondent, Lisa Baraba sat down with Krantz to find out who is the man behind the laptop; his journey, aspirations and the mark he has left in the blogosphere.

  Who prompted you to start your blog?

  I have always been interested in media and news reporting from my early stages. Throughout my ordinary and Advanced level studies, I have been involved with the school magazine and the school newsletter. In my school days I would go to the library, read on current issues and report it to my peers. Of course on the journey to starting Mwanaharakati Mzalendo I drew inspiration from bloggers like Michuzi and Haki Ngowi.

  I am sure you write with a purpose and a particular segment of the society. Tell me, who is a Mwanaharakati Mzalendo?

  Anybody and everybody is “Mwanaharakati Mzalendo” so to speak. Earlier on during my school days in seminary school I realized that many youth were not interested in current global affairs. So I set out my blog to capture the young person since I already had the content for the more mature section of society. Now there is something for everybody; the student, the working man/woman, the entrepreneur, for me and for you. We are all “Mwanaharakati Mzalendo”.

  We are more and more of an interest in many people on the internet and in blogging. I am curious with all these blogs around, what gives Mwanaharakati Mzalendo that edge above the competition?

  Key aspect is originality. I come up with my own content as opposed to taking it down and pasting in to my space. I have a friendly approach to the readers, giving out my contact information so they can give comments, feedback or stories they would like us to follow up on. Recently, I opened up an application with Google Play by the name of my blog. Look it up! We are objective and never post content that makes someone target to ridicule or hatred of any kind. We believe in hard hitting news that benefits our readers. We also give previews and references on our sites for more understanding.

  Discipline to post interesting topics frequently is often cited as one of the requirements to a successful blog. What other factors, in your opinion, can make a blog successful?

  Forming relationships with the readers, interactive posts tips on various subjects like love and life. I also have
  great communication with some other bloggers. The key is realizing that it is not about competition it’s about bettering yourself and accepting that you do not know everything. Every once in a while someone will beat you to that story. I do post the news to my readers but make sure to give them their due credit.

  Is it possible for someone to have a blog as his full time, income generating business or are blogs simply side projects that can earn people some extra income?


  Yes it is very possible. It has to be your passion and profession like with Kenyans and Nigerians. I blog on my own free time and I recently have hired two more individuals to assist me with Marketing and IT. 
  These two have degrees in their respective fields and earn incomes from the work they do on Mwanaharakati Mzalendo. Like all jobs it needs commitment to blogging all day and being on media as much as possible. You do not want to miss a
  thing in this business. Mwanaharakati Mzalendo has been known for breaking the news first. That’s how you do it.

  You have reputable companies advertising with your blog. How long did it take you to get the first company to advertise with you?

  Two years. It was after winning the Tanzania Blog Award for best political blog and first runner up for best news
  blog in 2012. It was a UK based company called Serengeti Clearers and Forwarders. In the beginning I offered them
  the space for free as a trial run, but after a month I started to receive commissions from them. They were impressed with the response.

  What are your future plans for your blog?

  To be recognized beyond national borders as an international blog. And it has already started with the nomination I received this year for the best educational and political blog from the African Blog Awards 2014. It takes me and this blog to another level. I am ecstatic.

  What advice do you give to anyone who would like to start a blog that generates income?

  Content; give people what they want with someone you are proud of. Professionalism; know what you are about
  and stick to it. Set goals as to what your blog is about and what it is for. Keep it fresh and always try to give it new looks every now and then. Love what you do and last but not least: creativity matters.


                       www.harakati360.blogspot.com
                       www.mzalendotimes.blogspot.com


    CREDIT ;http://www.manmagazine.co.tz

  0 0

  IMG_8896
  Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akielezea mantiki ya warsha ya wadau wa elimu kuhusu viwango vya umahiri wa Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu Tanzania iliyofanyika mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani mwishoni mwa juma.
  IMG_8887
  Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
  SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limesema litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na wananchi wenye uwezo mkubwa wa kuvumbua na kutumia elimu.

  Kauli hiyo imetolewa na Ofisa wa Unesco nchini Al Amin Yusuph wakati akizungumza na washiriki wa kongamano maalumu wa kupitia waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.

  Kongamano hilo ni moja ya mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China wenye lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.

  Mradi huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa ya Tehama na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.
  Ingawa kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vya Tabora na Monduli vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu ambavyo vitaingizwa.
  IMG_8817
  Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akifafanua jambo kwa wadau wa kongamano la kupitia kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini lililofanyika mjini Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa juma.


  Yusuph aliwataka wadau wanaoshiriki katika kongamano ambalo lilitarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki kutekeleza wajibu wao kwa makini kwa kuwa Watanzania wanasubiri maelekezo yao kufanikisha utoaji wa elimu ya Tehama yenye kuleta mwelekeo mpya wa matumizi kwa kulenga kuvumbua na kutumia elimu kwa manufaa ya taifa.

  Alisema UNESCO ipo tayari kuhakikisha kwamba Tanzania inazalisha wanafunzi ambao watakuwa na uwezo mkubwa katika Tehama ambao utaibua maendeleo endelevu.“Si kutoa walimu wazuri tu bali kuwezesha jamii , wanafunzi na waliopitia mafunzo hayo kuwa na namna mpya ya kufikiri na kuvumbua vitu vipya vya kujiendelea na kuendeleza taifa” alisema Yusuph.
  Alisema kimsingi elimu inatoa asilimia 5 lakini maisha yanatoa asilimia zilizobaki kama mtu atatumia vyema msingi wa maarifa aliyopewa.
  IMG_8793
  Jaco Du Toit, kutoka ofisi za Unesco kanda ya Nairobi akiendesha majadiliano ya maboresho ya vipengele mbalimbali vya waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu"UNESCO ICT Competency Framework for Teachers in Tanzania" wakati wa kongamano hilo lililomalizika mwishoni mwa juma mjini Bagamoyo.Alisema lengo la mradi huo ni kuwezesha wanafunzi na walimu wao kuongeza maradufu uwezo wao katika elimu.

  Naye Mratibu wa kitaifa wa Mradi Wa CFIT Kutoka UNESCO, Faith Shayo alisema kongamano hilo ni sehemu ya maandalizi ya mafunzo na matumizi ya maabara katika vyuo vya Monduli na Tabora katika kufunza Tehama ili kuboresha mafunzo na ufundishaji.

  “Leo tuko hapa Bagamoyo kwa ajili ya wadau kudiscuss ICT draft document (kujadili hati hii yenye draft ya mafunzo) ambayo ilipitiwa na watu watano kabla ya kuikabidhi kwa Wizara ya Elimu “ alisema Faith.
  IMG_8775
  Alifafanua kwamba Mradi huo ambao awali ulifadhiliwa na Benki ya Dunia na kukamilika mwaka 2011, haukuridhiwa kutumika hadi mwaka jana ulipokuja mradi wa CFIT ambao uliingizia upitiaji upya wa mradi huo na kuwezesha kuridhiwa kwa matumizi.

  Naye kiongozi wa timu iliyopitia awali katika mradi huo wa CFIT, Profesa Ralph Masenge amesema wataalamu waliohusika na upitiaji huo kabla ya kongamano walitoka Chuo cha Ualimu Tabora na kile cha Monduli,Chuo kikuu huria Tanzania na Chuo kikuu cha Dar es salaam.Alisema awali walipitia kuona mahitaji maalumu ya walimu kisha wakaja na mapendekezo ambayo sasa yanafanyiwa kazi .

  Alisema matatizo mengi ya elimu Tanzania yanatokana na uhaba wa vifaa vya elimu na ubora wa walimu.Alisema mradi huo utasaidia kutoa elimu bora kwa kuwa na walimu bora na vifaa bora kupitia Tehama. Alisema mradi huo utasaidia kuwezesha Tehama kutumiwa kama chombo cha kutumia wanafunzi hasa pale panapokosekana.Profesa Masenge alisema hatua waliyofikia ni hatua ya matayarisho na kwamba ni matarajio yao kwamba wakishafikisha hati hiyo kwa wizara masuala ya matumizi ya maabara yatakuwa yamekamilika.
  IMG_8849
  Pichani juu na chini ni washiriki wakiwasilisha mawazo yao wakati kongamano likiendelea kujadili masuala mbalimbali ya kuboresha waraka huo.
  IMG_8798
  IMG_8821
  IMG_8787
  Washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiwasilishwa.
  IMG_8842

  0 0

   Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Leticia Nyerere akinyanyua mikono ikiwa ni sehemu ya ishara ya kuondoka katika chama hicho na kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati alipokutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam.
   Mbunge wa Viti Maalum Chadema,Leticia Nyerere akifafanua jambo kwa waandishi habari juu ya kuondoka katika chama hicho.
   Waandishi wa habari wakifuatilia kwa umakini maelezo ya Mbunge wa Viti Maalum Chadema,Leticia Nyerere juu ya kuhama kwake katika chama hicho katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam. 
  Mwandishi akiuliza swali kwa Mbunge wa Viti Maalum Chadema,Leticia Nyerere ambaye leo alikutana na waandishi habari juu kuhama chama hicho na kurejea CCM katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam. 


  Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii.

  MBUNGE wa Viti  Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa  wa Mara ,Leticia Nyerere amengatuka rasmi leo katika chama hicho na kudai kuwa anarudi nyumbani katika chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini Dar es Salaam,Leticia amesema kuwa katika suala la kuhamia Chadema hakutafakari kwa kina labda angetafakari asingeweza kwenda huko.

  Amesema mchango wake unatambulika sasa anaweza kutumikia CCM nje  bila ya kuwa mbunge na kuweza kuleta maendeleo kutokana na uwezo wake katika masuala ya siasa.

  “Moyo wangu umekuwa ukisoneneka kutokana na kukaa Chadema na kuacha kukaa katika chama kilichonilea na kunisomesha hadi nje ya nchi ,sasa  nasema narudi  nyumbani kutumikia”amesema Leticia.

  Leticia amesema kwenda Chadema alifanya ujinga bila kutafakari na hawezi kulaumu dhamira yake mpya kurudi katika chama kilichompa makuzi yote na atatumikia CCM kwa kasi mpya na kuleta maendeleo chanya kutokana na kile ambacho amekuwa akitoa katika michango ya bunge.

  Amesema wapinzani wote wa zamani walikuwa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM)hivyo katika maamuzi yake ya kwenda Chadema hayakuwa  shahihi.

  0 0

   Maharausi wakikata keki kuashilia upendo katika hafla  iliyofanyika katika Ukumbi wa Danken House,Mikocheni jijini Dar es Salaam,
   Bwanaharusi Yahaya Kiyabo akimlisha keki Biharusi,Aisha Kirapo katika hafla iliyfanyofanyika katika ukumbi wa Danken  House,Mikocheni Jijini Dar es Salaam,
     Biharusi,Aisha Kirapo akimlisha keki Bwanaharusi Yahya Kiyabo katika hafla iliyfanyofanyika katika ukumbi wa Danken ,Mikocheni Jijini Dar es Salaam,
   Bwanaharusi Yahya Kiyabo akiwakabidhi baadhi ya Wafanyakazi wenzake wa Benki ya CRDB keki katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Dunken House,Mikocheni,jijini Dar es Salaam.
   Baadhi wa washiriki katika hafla hiyo wakisubiri keki katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Danken House,Mikocheni jijini Dar es Salaam.
   Mama mzazi wa bwanaharusi wakifurahia jambo kwa pamoja 
   Maharusi wakipeleka keki kwa wakwe hawapo pichani katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Dakan,Mikocheni ,jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha Taifa cha utalii, Rosada Musoma akizindua kwa kukata utepe kiota cha burudani cha Goldbar and Restaurant katika chuo cha Taifa cha Utalii kampasi ya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
  Mkurugenzi kitengo cha Biashara wa chuo cha Taifa cha Utalii (NCT),Neema Chololo Kusiga akizungumza mara baada ya uzinduzi wa kiota cha burudani cha Goldbar and Restaurant kilichopo katika chuo cha Taifa cha Utalii kampasi ya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
    Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha Taifa cha utalii, Rosada Musoma akizungumza mara baada ya kuzindua Goldbar and Restaurant katika chuo hicho mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa chuo cha Taifa cha Utalii kampasi ya Bustani.
   Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Chuo cha Taifa cha Utalii kampasi ya Bustani mara baada ya kuzindua Goldbar and Restaurant katika chuo hicho uzinduzi uliofanyika katika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 

    Wana kamati ya Maandalizi wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Afisa masoko wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Waheeda Mohamed.
   Vitu vipatikanavyo katika Chuo cha Taifa cha utalii kampasi ya Bustani jijini Dar es Salaam.
   Bendi kitumbuiza katika uzinduzi wa
  Goldbar and Restaurant katika chuo cha Taifa cha Utalii uzinduzi uliofanyika katika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   Mkurugenzi kitengo cha Biashara wa chuo cha Taifa cha Utalii (NCT),Neema Chololo Kusigaakiwa na mfanyakazi wa chuo hicho.

   Afisa Manunuzi Mkuu wa Masoko wa chuo cha Taifa cha Utalii,Elizabeth Kasawara akiwa katika pozi mara baada ya
  kiota cha burudani cha Goldbar and Restaurant katika chuo cha Taifa cha Utalii kampasi ya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha Taifa cha utalii, Rosada Musoma akiwa na wafanyakazi wa Chuo cha Taifa

  0 0

  Benki M yaadhimisha miaka 8 toka ilipoanzishwa, pichani ni naibu mkurugenzi mkuu wa Benki M Bi. Jaqueline Woiso katika mkutano na waandishi wa habari wikiendi hii katika ukumbi wa hoteli ya Hyatt Regency, kuelezea mafanikio waliyopata katika kipindi hicho cha miaka 8 , kulia ni mkurugenzi wa mawasiliano wa benki hiyo Bw. Allan Msalilwa.

  BANK M Tanzania plc leo inatimiza miaka 8 toka ilipoanzishwa July 27, 2007. Akiongea na waandishi wa habari, Naibu mkurugenzi mkuu wa benki hiyo Bi. Jacqueline Woiso alisema wanaadhimisha miaka minane yenye mafanikio makubwa, “mwaka 2007 tulifunga mwaka tukiwa na rasilimali zenye thamani ya TZS 32 billioni tu, na sasa tumefikia kiasi cha TZS 800 billioni. Tumekuwa tukifanya vizuri katika masoko kwa muda mrefu na tulifanikiwa kuanza kupata faida ndani ya miaka miwili (2) tu toka kuanzishwa kwa benki yetu. Kwa mwaka huu hadi kufikia June 2015 tumepata faida ya TZS 11.5 Billioni”.

   Alisema kuwa Benki hiyo ilianza na kiasi kidogo sana cha TZS 16 billioni hadi kufikia TZS 630 billioni, huku mtaji ukiwa pia umeongezeka kutoka TZS 6.5billioni hadi kufikia TZS 84 billioni kwa sasa huku idadi ya wafanyakazi pia imeongezeka kutoka 40 hadi 236, kwa uwiano wa asilimia 50% kati ya wanaume na wanawake.

  Kwa upande wa huduma kwa wateja, Bi woiso alisema kuwa Benki M imekuwa ni benki ya kwanza kutoa huduma masaa 12 kila siku kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa mbili usiku, siku 7 za wiki yaani Jumapili hadi Jumapili. “Pia tunatoa Garantii endapo tutazidisha muda tuliokubaliana kufanikisha miamala ya wateja, huduma hii inajulikana kama SSG (Service Standard Guarantee)” aliongeza.

  Benki hiyo pia imekuwa ikishiriki kwa kiasi kikubwa katika kusaidia jamii ikiwa ni moja ya sera kubwa za benki hiyo ambayo huiita Money@heart, alisema Woiso. “tunashirikiana na taasisi mbalimbali katika kufanikisha miradi mingi kwenye jamii katika sekta ya Afya, Elimu, Maji Utunzaji wa mazingirana pia kuwainua wajasiriamali na wasanii wa michoro ya asili nchini”.

   Pia alisema kuwa wamefanikiwa kupata tuzo mbalimbali za kimataifa ikiwemo tuzo ya benki bora ya biashara kwa mwaka 2015 iliyotolewa katika soko la hisa la London, Benki bora katika sekta ya biashara za makampuni Afrika Mashariki na Benki bora inayoshiriki katika maendeleo ya jamii Afrika Mashariki zilitolewa na Banker Africa.

  “Hatimaye tumefanikiwa kuwa chaguo bora katika benki zinazotoa huduma kwa makampuni nchini (Preffered Bank)”, alimalizia Bi Woiso.

  0 0   Katibu wa Mipango na Mikakati wa Chama cha ACT-Wazalendo, Habibu Mchange (kushoto), akimkabidhi kadi ya chama hicho, aliyekuwa mbunge wa Viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Iringa mjini, Chiku Abwao baada ya kuhamia rasmi ACT-Wazalendo Dar es Salaam leo mchana.
   Mbunge Chiku Abwao (kulia), akionesha kadi ya chama cha ACT-Wazalendo baada ya kukabidhiwa.
    Mbunge Chiku Abwao (kulia), akizungumza na wanahabari baada ya kukabidhiwa kadi ya chama cha ACT-Wazalendo.
  Wanahabari wakichukua taarifa hiyo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com

  0 0

   
   Mgeni rasmi Dk. Salim Ahamed Salim akizungumza katika ufunguzi wa Semina iliyoandaliwa na chuo cha Waislam Morogoro kuhusiana Utamaduni na Mirathi ya utamaduni iliyopo hapa nchini semina hiyo iliyohusisha viongozi mbalimbali na wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano katika hoteli ya lamada jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya utamaduni wa chuo cha kiislam Morogoro, Abdalla Bujra.
   Dk. Salim Ahamed Salim akizungumza na Mkurugenzi wa Taasisi ya utamaduni wa chuo cha kiislam Morogoro, Abdalla Bujra mara baada ya kumalizika kwa Semina inayozungumzia masuala ya utamaduni iliyofanyika katika hotel ya Lamada jijini Dar es Salaam leo.
   Mwenyekiti wa kigoda cha Mwalimu Nyerere Profesa Issa Shivji kichangia maada kuhusiana na mambo ya utamaduni na mambo ya kale jinsi yanavyochangia katika uchumi wa hapa nchini, katika semina iliyoandaliwa na Chuo cha Waislam Morogoro iliyofanyika katika hotel ya Lamada jijini Dar es Salaam leo.
   
   Wadau wa mambo ya utamaduni wakimsikiliza  Dk. Salim Ahamed Salim
  katika semina iliyoandaliwa na Chuo cha Waislam Morogoro iliyofanyika katika hotel ya Lamada jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanaosoma kozi ya Utamaduni ( Culture) waliohudhuria  katika semina iliyoandaliwa na Chuo cha Waislam Morogoro iliyofanyika katika hotel ya Lamada jijini Dar es Salaam leo.
   
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika semina iliyoandaliwa na Chuo cha Waislam Morogoro iliyofanyika katika hotel ya Lamada jijini Dar es Salaam leo.  
  Mwenyekiti wa kigoda cha Mwalimu Nyerere Profesa Issa Shivji akizungumza na Profesa Abdul Shariff kabla ya kuanza semina iliyoandaliwa na Chuo cha Waislam Morogoro iliyofanyika katika hotel ya Lamada jijini Dar es Salaam leo.  

  0 0

   Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi akipokea Madebe maalum la kuhifadhia takataka,Katika ni Mkurungenzi wa Usalama wa Chakula Kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Raymond Wigeng iliyofanyika katika eneo la wazi la Posta ya zamani leo Jiji Dar es Salaam.
   Mkurungenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi akitoa shukrani kwa uongozi mzima wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa kupokea msaada wa madebe ya kuhifadhia takataka ili zisizagae hovyo msaada huo umetolewa katika eneo la wazi Posta ya zamani leo Jiji Dar es Salaam.

  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia katika kikao hicho Kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) iliyofanyika katika eneo la wazi Posta ya zamani leo Jiji Dar es Salaam.
  Picha na Emmanuel Massaka

  0 0

  IMG_8896
  Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akielezea mantiki ya warsha ya wadau wa elimu kuhusu viwango vya umahiri wa Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu Tanzania iliyofanyika mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani mwishoni mwa juma.
  IMG_8887
  Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
  SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limesema litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na wananchi wenye uwezo mkubwa wa kuvumbua na kutumia elimu.

  Kauli hiyo imetolewa na Ofisa wa Unesco nchini Al Amin Yusuph wakati akizungumza na washiriki wa kongamano maalumu wa kupitia waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.

  Kongamano hilo ni moja ya mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China wenye lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.

  Mradi huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa ya Tehama na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.
  Ingawa kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vya Tabora na Monduli vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu ambavyo vitaingizwa.
  IMG_8817
  Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akifafanua jambo kwa wadau wa kongamano la kupitia kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini lililofanyika mjini Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa juma.
   
  Yusuph aliwataka wadau wanaoshiriki katika kongamano ambalo lilitarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki kutekeleza wajibu wao kwa makini kwa kuwa Watanzania wanasubiri maelekezo yao kufanikisha utoaji wa elimu ya Tehama yenye kuleta mwelekeo mpya wa matumizi kwa kulenga kuvumbua na kutumia elimu kwa manufaa ya taifa.
  Alisema UNESCO ipo tayari kuhakikisha kwamba Tanzania inazalisha wanafunzi ambao watakuwa na uwezo mkubwa katika Tehama ambao utaibua maendeleo endelevu.
  “Si kutoa walimu wazuri tu bali kuwezesha jamii , wanafunzi na waliopitia mafunzo hayo kuwa na namna mpya ya kufikiri na kuvumbua vitu vipya vya kujiendelea na kuendeleza taifa” alisema Yusuph.
  Alisema kimsingi elimu inatoa asilimia 5 lakini maisha yanatoa asilimia zilizobaki kama mtu atatumia vyema msingi wa maarifa aliyopewa.
  IMG_8793
  Jaco Du Toit, kutoka ofisi za Unesco kanda ya Nairobi akiendesha majadiliano ya maboresho ya vipengele mbalimbali vya waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu"UNESCO ICT Competency Framework for Teachers in Tanzania" wakati wa kongamano hilo lililomalizika mwishoni mwa juma mjini Bagamoyo.
  Alisema lengo la mradi huo ni kuwezesha wanafunzi na walimu wao kuongeza maradufu uwezo wao katika elimu.
  Naye Mratibu wa kitaifa wa Mradi Wa CFIT Kutoka UNESCO, Faith Shayo alisema kongamano hilo ni sehemu ya maandalizi ya mafunzo na matumizi ya maabara katika vyuo vya Monduli na Tabora katika kufunza Tehama ili kuboresha mafunzo na ufundishaji.
  “Leo tuko hapa Bagamoyo kwa ajili ya wadau kudiscuss ICT draft document (kujadili hati hii yenye draft ya mafunzo) ambayo ilipitiwa na watu watano kabla ya kuikabidhi kwa Wizara ya Elimu “ alisema Faith.
  IMG_8775
  Alifafanua kwamba Mradi huo ambao awali ulifadhiliwa na Benki ya Dunia na kukamilika mwaka 2011, haukuridhiwa kutumika hadi mwaka jana ulipokuja mradi wa CFIT ambao uliingizia upitiaji upya wa mradi huo na kuwezesha kuridhiwa kwa matumizi.

  Naye kiongozi wa timu iliyopitia awali katika mradi huo wa CFIT, Profesa Ralph Masenge amesema wataalamu waliohusika na upitiaji huo kabla ya kongamano walitoka Chuo cha Ualimu Tabora na kile cha Monduli,Chuo kikuu huria Tanzania na Chuo kikuu cha Dar es salaam.

  Alisema awali walipitia kuona mahitaji maalumu ya walimu kisha wakaja na mapendekezo ambayo sasa yanafanyiwa kazi.

  Alisema matatizo mengi ya elimu Tanzania yanatokana na uhaba wa vifaa vya elimu na ubora wa walimu.

  Alisema mradi huo utasaidia kutoa elimu bora kwa kuwa na walimu bora na vifaa bora kupitia Tehama.

  Alisema mradi huo utasaidia kuwezesha Tehama kutumiwa kama chombo cha kutumia wanafunzi hasa pale panapokosekana.

  Profesa Masenge alisema hatua waliyofikia ni hatua ya matayarisho na kwamba ni matarajio yao kwamba wakishafikisha hati hiyo kwa wizara masuala ya matumizi ya maabara yatakuwa yamekamilika.
  IMG_8849
  Pichani juu na chini ni washiriki wakiwasilisha mawazo yao wakati kongamano likiendelea kujadili masuala mbalimbali ya kuboresha waraka huo.
  IMG_8798
  IMG_8821
  IMG_8787
  Washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiwasilishwa.
  IMG_8842

older | 1 | .... | 592 | 593 | (Page 594) | 595 | 596 | .... | 1896 | newer