Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

DKT MAGUFULI AREJEA JIJINI DAR BAADA YA KUJITAMBULISHA MIKOA KADHAA,APOKELEWA KWA KISHINDO

$
0
0
 Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Mji wa Bagamoyo (hawapo pichani) alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.Dkt Magufuli amejitambulisha vyema kila alikopita na kupokelewa kwa kishindo katika mikoa na vitongoji vyake aliyopita ikiwemo jijini Mwanza,Geita,dodoma,Morogoro,Pwani na jiji la Dar kwa ujumla.
 Wakazzi wa Bagamoyo wakimsikiliza Dkt Magufuli wakati alipokuwa akijitambulisha kwao na kuwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea,alipokuwa akitoka mkoani Dodoma kurejea jijini Dar jana jioni.
 Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Chalinze wakimsikiliza Mteule wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa nafasi ya Urais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi wa Chalinze alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
 Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chalinze,ambaye anawania tena nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete akiwasalimia Wananchi wa Chalinze na kumkaribisha Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru Wananchi wa Chalinze (hawapo pichani) pamoja na kujitambulisha kwao alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
  Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Chalinze wakimshangilia kwa mayowe Mteule wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa nafasi ya Urais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi wa Chalinze alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
   Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chalinze,ambaye anawania tena nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete pamoja na  Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli wakifurahia jambo mjini Bagamoyo,aliposimama mjini hapo kujitambulisha na kuwashukuru kwa kujitokeza kwao kwa wingi kumpokea,alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
 Mkazi wa Bagamoyo akifurahia jambo
 Wananchi wakimshangilia Dkt Magufuli (hayupo pichani) alipokuwa akijitambulisha kwao hapo jana mjini Bagamoyo.



KAMPUNI YA MAFUTA YA ENGEN HAPA NCHINI YAPATA MKURUNGENZI MPYA

$
0
0
 Mkurungenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Engen Tanzania, Mubita Akapelwa  akiwashukuru baadhi ya wafanyakazi wa kampunikwa ushirikiano walio uonesha wakati wa utendaji wake kazi katika hafla ya  kumuaga na kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji  Mpya wa Kampuni hiyo Paul Mhato iliyofanyika katika ukumbi wa Sea criff jijini Dar es Salaam. 
 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi MtendajiMpya wa Kampuni ya Mafuta ya Engen Tanzania, Paul Mhato akifurahia  jambo  katika hafra  ya kumkaribisha Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo na kumuaga Mkurungenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta Engen hapa nchini, Mubita Akapelwa   aliee maliza muda wakekatikati kulia ni Meneja Utawala Kampuni ya Mafuta Engin  Tanzania Shannel Sihuimba.
 Kushoto ni Mkurungenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Engen Tanzania, Mubita Akapelwa   aliemaliza muda wakeakipeana mkono wa shukurani na  Meneja Masoko wa Kampuni ya Mafuta EnginTanzania Shabaani Kajungilo.
 Mkurungenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Engen Tanzania, Mubita Akapelwa   aliemaliza muda wake  wa kufanya kazi katika kampuni hiyo (kushoto)akipokea zawadi kutoka kwa  Msaidizi wa Mkurungenzi wa  Kampuni ya Mafuta ya Tanzania ya Engen  Donathi Mbarara.
Mkurungenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya EngenTanzania, Mubita Akapelwa   aliemaliza muda wake  akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi  ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo.
  Picha na Emmanuel Massaka.

CHUO CHA WAISLAM MOROGORO WASHIRKI MAONYESHO YA VYUO VIKUU

$
0
0
Chuo cha  Waislam Morogoro kimeshiriki maonyesho ya vyuo vikuu yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam kilianzishwa mwaka 2005 na mpaka sasa kina miaka 10 kinatoa kozi mbalimbali kwa wanafunzi wanaojiunga katika chuo hicho.Afisa mahusiano wa chuo cha Waislam Morogoro, Ngaja Mussa akimwonyesha Mkufunzi mkuu wa chuo cha Waislam Morogoro, Faraji Tamim wakati wa maonyesho ya wiki ya vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu nyerere jinini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa chuo cha Waislam Morogoro wa Lugha ya Kichina katika chuo hicho, Sun Xiaofei akizungumza na wateja mbalimbali waliotembelea katika maonyesho ya vyuo vikuu vya hapa nchini na nje ya nchi.

 
Afisa Udahili Yahya Mhando akitoa maelekezo kwa watu waliotembelea katika banda la Chuo cha Waislam-Morogoro katika maonyesho ya wiki ya maonyesho ya vyuo vikuu yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa chuo cha Waislam Morogoro wa Lugha ya Kichina katika chuo  cha Waislamu Morogoro, Sun Xiaofei akitoa maelekezo kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Pugu walipotembelea katika maonesho ya wiki ya vyuo vikuu yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.

BASATA YAWATAKA WASANII WAFUATE TARATIBU WANAPOENDA NJE YA NCHI

$
0
0
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa nchini linawakumbusha wasanii wote nchini kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo wanapokwenda nje ya nchi kufanya maonesho au kushiriki shughuli yoyote ya Sanaa ili kuepuka matatizo na mikanganyiko mbalimbali inayoweza kujitokeza.

Kwa mujibu wa taratibu zilizopo, msanii yeyote anapokwenda nje ya nchi anapaswa kujaza fomu maalumu inayotolewa na BASATA na baadaye kupewa kibali bure (bila gharama yoyote) ambacho mbali na kueleza wapi msanii anaelekea kinaeleza kwa kina tarehe ya kuondoka kwa msanii na ile ya kurudi nchini.

Kutokana na kukua kwa sekta ya Sanaa nchini hususan muziki na filamu wasanii wengi wamekuwa wakipata fursa ya kwenda nje ya nchi kufanya maonesho na shughuli zingine za Sanaa hivyo suala la kufuata sheria, kanuni na taratizu za kupata vibali vya kwenda nje ya nchi ni muhimu sana ili kuhakikisha kwanza; safari zao zinakuwa na baraka ya moja kwa moja kutoka Serikalini, pili kusaidia upatikanaji wa takwimu sahihi za wasaniii wanaokwenda nje ya nchi, tatu usalama wa wasanii wetu na mwisho, kuwakabidhi bendera ya taifa kama ishara ya uwakilishi na ubalozi wa nchi yetu katika mataifa wanayoyatembelea.

MTOTO MWENYE KIPAJI CHA AJABU KUTOKA MAREKANI ATUA NCHINI LEO, KUFANYA KONGAMANO LA WATOTO NA WAZAZI KESHO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

MTOTO  mwenye kipawa cha ajabu katika kutoa ushauri  wa kujijengea uwezo wa kujiamini  anayezidi kujipatia umaarufu mkubwa duniani,  Lonnie Hudson  maarufu kama ‘King Nahh’(Pichani), ametua  jijini Dar es Salaam , leo.

King Nahh aliambatana na baba yake mzazi , Nyeeam Hudson  ambapo wapo nchini kwa mwaliko wa  taasisi isiyo ya kiserikali ya Wisdom Partners.

Kesho mtoto huyo atafanya  kongamano kubwa  la watoto na wazazi  katika Ukumbi wa Urafiki ambapo nia na madhumuni ni kuamsha hisia za  watu ambao wamekata  tamaa katika masuala mbalimbali na kukosa kujiamini katika maamuzi.

“Najisikia furaha kuja Tanzani. Ninaamini nina jukumu kubwa la kufanya hapa. Hususani  kwa watoto ambao bado hawaamini kuwa wanaweza kubadili hisia zao, kujiamini na  kushiriki katika masuala mazima ya maendeleo,” alisema.

King Nahh aliongeza kwamba, hisia za watu wengi hivi sasa zimelemaa kutokana na kuishia kulaumu  matatizo na vikwazo bila kutafuta suluhu ya matatizo yao.

“Kila mtu analaumu. Wa kwanza atalaumu, wa pili, wa tatu, wa nne, wa tano mpaka wa sita. Wote wanaishia kulaumu jambo moja. Wengine wanaamini kuwa hawezi kitu. Ila ukweli ni kwamba pale unapokuwa huwezi kitu kuna kitu unaweza kufanya. Jamii ibadilike. Iache kulaumu,”alisema mtoto huyo na kushangaza watu waliokwenda kumlaki.

Mkurugenzi wa taasisi ya Wisdom Partners, Cynthia Henjewelle, alisema kuwa dhamira kubwa ya kumleta mtoto huyo nchini ni kusaidia kubadili hisia za jamii hasa watoto ili waweze kujiona kuwa sehemu ya jamii.

“King Nahh ni miongoni mwa watoto wanaosifika hivi sasa duniani kutokana na  kipawa  alichonacho. Wazazi wawalete watoto kesho  Urafiki,  ili waweze kubadilishana mawazo. Pia wazazi wanakaribishwa kumsikiliza mtoto huyu kuanzia saa tano asubuhi,”alieleza Henjewele.

DR.MARY MWANJELWA USHINDI WA KISHINDO UBUNGE VITI MAALUM MKOWA WA MBEYA

$
0
0
Mgombea ubunge viti maalum mkoa wa mbeya Dr.Mary Mwanjelwa aibuka mshindi katika kura za maoni kutoka kwa wajumbe wa ccm mkoa wa mbeya na kupata ridhaa ya kulejea tena katika kiti  cha ubunge viti maalum mkoa wa Mbeya kwa ushindi wa kishindo wa asilimia 97 na kuwashinda wagombea kumi (10) kati ya kumi na moja (11) walio kuwa wakigombea na kutaka kuteuliwa na wajumbe wa ccm mkoa wa mbeya...Picha zote Na Fadhiri Atick, Mbeya.
Mshindi wa ubunge viti maalum kupitia chama cha mapinduzi mkoa wa mbeya Dr.Mary Mwanjelwa akiwashukuru wajumbe wa ccm mkowa wa mbeya mara baada ya ushindi katika uchaguzi wa kumpata mbunge viti maalum mkoa wa mbeya ulio fanyika tar:24-07-2015, katika ukumbi wa nyerere Musti jijini mbeya.

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA (PTA), YATOA SHILINGI MILIONI MBILI KUSAIDIA WANAHABARI WANAOPAMBANA NA UJANGILI NCHINI

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (PTA), Awadh Massawe akizungumza na wanahabari wakati akikabidhi hundi ya sh.milioni mbili kwa Taasisi ya Habari Development Association Dar es Salaam jana asubuhi. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (PTA), Awadh Massawe (kushoto), akikabidhi mfano wa hundi ya sh.milioni mbili kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Habari Development Association (HDA), Kunze Mswanyama (kulia), Dar es Salaam jana asubuhi kwa ajili ya kuandaa mafunzo ya kuwawezesha waandishi wa habari kujenga weledi wa kufanya tafiti na kuandika habari za kupambana na ujangili. Wa pili kushoto ni Ofisa Mwandamizi wa Mawasiliano wa TPA, Focus Mauki na Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo, Benard James.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Habari Development Association (HDA), Kunze Mswanyama (kulia), akizungumzia kuhusu mafunzo na umuhimu wa wanahabari katika kupambana na ujangili wa rasilimali za taifa kabla ya kukabidhiwa msaada wa sh.milioni 2 kutoka PTA. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa PTA, Awadh Massawe.
Kaimu Mkurugenzi wa PTA, Awadhi Massawe (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. Kushoto ni Ofisa Mwandamizi wa Mawasiliano wa TPA, Focus Mauki na Mkurugenzi wa Taasisi ya Habari Development Association (HDA), Kunze Mswanyama.


Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imetoa sh. milioni 2 kwa Taasisi ya Habari Development Association kwa ajili kuandaa mafunzo ya kuwawezesha waandishi wa habari kujenga weledi wa kufanya tafiti na kuandika habari za kupambana na ujangili.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Awadh Massawe alikabidhi hundi ya thamani ya fedha hizo kwa Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Kunze Mswanyama jijini Dar es Salaam jana.“Tunaunga mkono juhudi hizi za kupambana na ujangili,” alisema Massawe. 

Alisema TPA imefanya hivyo kwa kuwa nchi ina tatizo la uwindaji haramu hasa wa ndovu na usafirishaji wa pembe za ndovu na kulisababishia hasara taifa kupitia mipaka yake.

Alifafanua kuwa bandari ya Dar es Salaam ni sehemu ya mpaka wa taifa, hivyo lazima TPA iunge mkono juhudi za kuelimisha jamii na kuzuia uhalifu huo.

Massawe alisema kwa sasa wanatarajia kufunga kamera 400 za CCTV ili kuimarisha ulinzi na kuwa skana tatu zimeletwa bandarini kwa ajili yakuziongezea nguvu skana mbili zilizopo.

Pia, alisema wanatarajia kupata msaada wa mbwa maalumu wa ulinzi watakaotolewa na Serikali ya Marekani. Alisema TPA inaendelea kuwajengea uwezo wafanyakazi kimaadili ili kuendelea kufanya kazi kwa weledi na uaminifu kwa faida ya taifa.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Mswanyama alisema fedha walizopewa watazitumia kwa kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari 54  kwa masuala ya ujangili kupata weledi na kutafiti na kufichua ujangili. “Tunahitaji kujenga uwezo wa kupambana na ujangili  ili taifa liweze kunufaika nazo,” alisema. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)




Wafanye Watabasamu kutembelea kituo cha yatima Bagamoyo


PANJU AWATAKA WANANCHI KUTOKUNUNULIWA KWA SHILINGI ELFU KUMI

$
0
0
SAM_3941Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ya ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM akinadi sera zake mbele ya wanachama  jijini Arusha ili kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea wa ubunge jimbo la Arusha kupitia CCM.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_4058Mgombea Ubunge ambaye pia ni mwandishi wa habari Swalehe Kiluvia wakati akijinadi mbele ya wana CCM jijini Ausha

Mgombea ubunge kupita chama cha mapinduzi CCM Mustafa Panju ambaye pia ni mkurugenzi wa Bushback Safaris amewataka wananchi kuto uza kura zao kwa shilingi elfu kumi kwa kiongozi yeyote katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu.
 
Aliyasema hayo jana wakati akijinadi kwa wananchi na wananchama wa chama hicho, kata ya Baraa jijini Arusha uliohudhuriwa na watiani ubunge 12 jimbo la Arusha mjini

Panju alisema kuwa wana CCM wanatakiwa kuchagua kiongozi sahihi ambaye ataleta maendeleo kwa wanachama na wananchi kwa ujumla huku akionya kuwa lazima wanachama wa chama hicho waendeleze sera ya chama ambayo ni kudumisha amani ,upendo na mshikamano kwa Watanzania wote.

“Lazima tuwe wamoja, sisi ndio tunakiharibia chama na kusababisha makundi yanayoleta migawanyiko. Tuchague kiongozi mzuri ambaye ataleta maendeleo, pia tuache tabia ya kuuza kura zetu kwa bei ya shilingi 10,000, bora hata uuze kwa laki tano ili ununue walau godoro utakaa nalo kwa miaka mingi”

Alisisitiza kuwa chama hicho kitaimarika iwapo tu wanachama na viongozi watashirikiana na kuwa wamoja huku akidai kuwa katika hali ya migawanyiko chama kinaweza kufikia mahali pabaya.

Mgombea mwingine katika kinyang’anyiro hicho ambaye pia ni mwandishi wa habari Swalehe Kiluvia wakati akijinadi mbele ya wana CCM katika Kata za Levolosi, Baraa na Kimandolu alisema kuwa endapo atapata ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho atatumia uwezo wake wote aliojaaliwa na Mungu ili kubadilisha hali ya maisha ya wananchi na wapiga kura wa Arusha.

Alisema kuwa atakuwa mstari wa mbele kupiga vita rushwa ,uzembe na upotevu wa mali za umma hali itakayosaidia wananchi kupata hak yao.

BHALALUSESA ASISITIZA UMUHIMU WA UMAHIRI KATIKA TEHAMA

$
0
0
IMG_8834
Kiongozi wa kitaifa wa mradi wa CFIT, Prof. Ralph Masenge akimkaribisha mgeni rasmi Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa (hayupo pichani) kufungua kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu linalofanyika mjini Bagamoyo.
IMG_8915
Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa akisoma hotuba kwa niaba ya Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalusesa wakati akifungua rasmi kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu linalofanyika mjini Bagamoyo. Kulia ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.

Na Mwandishi wetu, Bagamoyo
KAMISHINA wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa amesisitiza haja ya kuhakikisha kwamba viwango vya umahiri vya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini vinakua vya juu kukidhi haja ya matumizi ya kufundishia na kujifunza nchini.

Alitoa kauli hiyo mjini hapa wakati akifungua kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu. Katika hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa alisema kwamba changamoto ya Tehama inaonekana wazi katika matumizi yake na hivyo wakufunzi lazima wawe mahiri.

"Duniani kote, sekta ya uchumi, fani mbalimbali, taasisi na hata mifumo ya maisha yanategemea sana matumizi ya Tehama kwa sasa. Kadhalika, maendeleo makubwa katika Tehama yamebadili namna mambo yanavyofanyika,” alisema.


Alisema kwa kuhakikisha kwamba kuna maendeleo ya kutosha ni vyema walimu kuwa na umahiri unaotakiwa kwani Tehama inachangamoto nyingi zinazotakiwa kuangaliwa ili kuweza kuitumia ipasavyo kuleta mabadiliko katika jamiii.

Aliwataka washiriki kuhakikisha kwamba wanapitia muswada huo kwa makini na kujazia maeneo yote ambayo wataalamu wameshindwa kumaliza na kusaidia kuweka mtaala huo vyema kwa mafunzo.

Kongamano hilo ambalo ni sehemu ya mradi wa kuimarisha uelewa kwa wanafunzi na wakufunzi vyuo vya walimu ili kuboresha matumizi ya Tehama katika mafunzo hasa masomo ya sayansi limeshirikisha wataalamu mbalimbali na kuendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na watu wa China.
Alisema kwamba serikali inatambua kuwa Tehama inaweza kutumika vyema katika kubadili na kuboresha mfumo wa elimu Tanzania.
Aidha alisema Sera mpya ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 inatambua umuhimu wa Tehama katika kuboresha viwango vya elimu nchini Tanzania.
Alisema moja ya malengo ya sera ni kuonesha mahitaji halisi ya Tehama nchini katika upande wa wataalamu na vifaa ili kufanikisha utoaji wa elimu hata ya masafa katika ngazi zote.
Kongamano hilo ni moja ya mradi wa China Funds in Trust Project (CFIT) wa UNESCO na serikali ya China wenye lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua tehama na kuitumia.
Mradi huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa ya Tehama na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.
Ingawa kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu vitaingizwa.
IMG_8909IMG_8842
Pichani juu na chini ni washiriki wa kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu wakati kongamano hilo likiendelea mjini Bagamoyo.
IMG_8843IMG_8831
Kiongozi wa kitaifa wa mradi wa CFIT, Prof. Ralph Masenge (kushoto) akijadili jambo na mgeni rasmi Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa (katikati). Kulia ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.
IMG_8826
Kiongozi wa kitaifa wa mradi wa CFIT, Prof. Ralph Masenge (kulia), akifurahi jambo na Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph (katikati) pamoja na Mratibu wa kitaifa wa mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo (kushoto) mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.
IMG_8928
Mgeni rasmi Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa (walioketi wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo inayomalizika leo mjini Bagamoyo.

WASIMAMIZI, WAHARIRI NA WADADISI WA UTAFITI WA AFYA YA MAMA NA MTOTO NA MALARIA WA MWAKA 2015,WAPEWA MAFUNZO

$
0
0
Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wasimamizi,wahariri na wadadisi wa utafiti wa afya ya mama na mtoto na Maralia yanayofanyika kwa siku 36 katika ukumbi wa YMCA mjini Moshi.
Baadhi ya wauguzi wanaoshiriki mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa YMCA mjini Moshi.
Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Takwimu ,Ephraim Kwesigabo akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo.
Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Zanzibar Halima Maulidi Saleh akiwa na ,Mganga mkuu wa Mkoa wa   Kilimanjaro,Andrewleon Qweker (katikati) na Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Hafidh Rajab wakifuatilia ufunguzi wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki.
Mkurugenzi wa Kinga ,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akizindua matokeo muhimu ya utafiti wa tathmini ya utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania 2015.
Mkurugenzi wa Kinga ,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Afya ,Zanzibar Halima Maulid Saleh  matokeo muhimu ya utafiti wa tathmini ya utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania 2015.
Mkurugenzi wa Kinga ,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akimkabidhi Mganga mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Andrewleon Qweker matokeo muhimu ya utafiti wa tathmini ya utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania 2015.
Mkurugenzi wa Kinga ,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akimkabidhi Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Hafidh Rajab  matokeo muhimu ya utafiti wa tathmini ya utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania 2015.
Mkurugenzi wa Kinga ,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akimkabidhi Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa ofisi ya taifa ya takwimu  Ephraim Kwesigabo matokeo muhimu ya utafiti wa tathmini ya utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania 2015.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Hafidh Rajab akitoa neno la shukrani wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo ambao ni wauguzi kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MCHUNGAJI NATSE AWAAGA JIMBO LA KARATU ,QAMBALA KUPEPERUSHA BENDERA YA CHADEMA

$
0
0
Mbunge mstaafu wa Jimbo la Karatu mkoa wa Arusha,Mchungaji Israel Natse akizungumza katika mkutano mkuu wa Jimbo hilo ambao ulifanya uchaguzi wa madiwani na Wabunge wa  Viti Maalumu mgombe Ubunge wa Jimbo la Karatu,katikati ni Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha,Kalisti Lazaro na Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Karatu,Thomas Darabe.
Mbunge wa Viti Maalumu wilaya ya Karatu,Cecilia Paresso akizungumza katika mkutano huo ambao alichaguliwa na wajumbe wanawake kuwania nafasi hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya hosteli ya KKKT Karatu na kumpongeza mch.Natse kwa kuamua kuachia nafasi wanachama wengine.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya hosteli ya KKKT Karatu na kumpongeza mch.Natse kwa kuamua kuachia nafasi wanachama wengine.
Mwanamke wa kwanza kuwahi kujitokeza kuomba ridhaa ya wanachama kumchagua kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Karatu,Fransisca Duwe akijinadi kwa wajumbe.
Willy Qamballa mmoja wa wagombea akijinadi kwa wajumbe
Aliyekua Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Karatu,Lazaro Maasay akiomba kura kwa wajumbe
Mshindi wa kura za maoni za Ubunge Jimbo la Karatu,Willy Qamballa akiwashukuru wajumbe baada ya kujizolea kura 217 na mpinzani wake wa karibu Lazaro alipata kura 84.
Mshindi wa kura za maoni za Ubunge Jimbo la Karatu,Willy Qamballa akifurahia na wafuasi wake baada ya kutangazwa mshindi.

LEMA KUPEPERUSHA BENDERA YA CHADEMA NA JOYCE MUKYA

$
0
0
SAM_4216Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akizungumza katika uchaguzi wa kumpata Mbunge pamoja na Mbunge viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA)jijini Arusha ambapo aliibuka kidedea kwa kura 255 sawa na asilimia 93.06% (Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_4210Mbunge viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Joyce John Mukya alipata kura 39 sawa na asilimia 73.6% katika kinyang'anyiro hicho hivyo kumfanya kuwa Mbunge wa viti maalum,aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuvunja makundi ili kuhakikisha chama kinashinda katika uchaguzi wa Urais,Ubunge na udiwani
SAM_4212Mgombea kupitia chama cha Demokrasia na maendelao (CHADEMA)Noel Olevaroya akizungumza mara baada ya kutangazwa kushika nafasi ya pili  kwa kupata kura 13 sawa na asilimia 4.74% katika kinyang"anyiro hicho ambapo aliwashukuru wajumbe wa mkutano huo na kuhaidi kumpa Mbunge Lema shilingi laki tano kwaajili ya kampeni ya kuhakikisha  chama hicho kinapata ushindi wa kishindo
SAM_4147Wagombea ubunge viti maalum Mkoa wa Arusha wakisubiria kuingia kujinadi kwa wajumbe wa mkutano.
SAM_4214Mgombea nafasi ya Ubunge,Nsajigwa Mwakatobe aliyepata kura 6 sawa asilimia 2.18% akiwashukuru wajumbe wa mkutano pamoja na wanachama wa chama hicho
SAM_4208PIPOOOOZ!Mgombea nafasi ya Ubunge viti maalum Grace Macha alipata kura 3 katika kinyang'anyiro hicho , akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo na kuhaidi kushirikiana nao
SAM_4142Wajumbe wa mkutano huo
SAM_4195Taswira  katika mkutano huo
SAM_4207
Mgombea nafasi ya Ubunge viti maalum Glory Bernad akishukuru katika mkutano huo
SAM_4201Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akisaini fomu ya uchaguzi,pembeni ni Mbunge wa Rombo na mwenyekiti wa uchaguzi huo Joseph Selasini
SAM_4194Mbunge wa Rombo na mwenyekiti wa uchaguzi huo Joseph Selasini akitaja washindi katka kinyang'anyiro hicho
SAM_4198Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiwa na mtoto wake aliyemkimbilia mara baada ya baba yake kutangazwa mshindi katika uchaguzi huo
SAM_4222Wajumbe wakimshangilia Mbunge viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Joyce John Mukya
SAM_4196
SAM_4152

Angalia Nyumbani Na Diaspora na David Kyungu-TBC1

MLEZI WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM BAYI AJITOSA KUWANIA UBUNGE

$
0
0
 Mlezi wa Jumuiya ya wazazi  wa CCM wilaya ya bahi  Hebron Kipiko (Mr.Kipiko) katika picha


Mlezi wa Jumuiya ya wazazi  wa CCM wilaya ya bahi  Hebron Kipiko (Mr.Kipiko)  ametangaza rasmi nia ya kugombea ubunge wa jimbo la Bahi lililopo mkoani Dodoma  na kusema kuwa anaamini  anauwezo wa kutekeleza kero na matatizo mbalimbali ya nao wakabili wananachi wa jimbo hilo.

Akizungumza na Libeneke la kaskazini blog ,  amesema kuwa ameona mambo mengi na matatizo mengi yanayo wakabili wananchi wa jimbo lake na pia   huu ndio wakati muafa kwake kuwatumiakia wana Bahi.

Kipiko alisema kuwa , wana wa  bahi  wananafasi sasa ya kuandika historia  ya aina yake kumchagu yeye kama mgombea kwani wameona tu baadhi ya mambo ambayo ameyafanya wakati alivyokuwa mlezi wa jumuiya ya wazazi wa ccm wilaya,  pia ni mmoja wa mzazi  mchapakazi mwenye uwezo wa kutetea na kuwasilisha hoja za kuleta maslahi kwa  Bahi  na taifa.

“Huu ni wakati wa wananchi wa Bahi  kuandika historia ya aina yake, sit u kwa kumchagua kwa ajili ya  kuwaongoza bali  ni Mzazi  mwenye uwezo wa kutetea hoja na maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla,”alisema Kipiko.

Kipiko  amekuwa ni mwananchi wa kwanza  kujitokeza kugombea jimbo la Bayi na ni mwana CCM wa  wa kwanza kujitokeza kuomba ridhaa ya chama kuteuliwa kugombea Ubunge kwa tiketi ya chama hicho.

Aidha aliainisha baadhi ya mambo ambayo atayatekeleza iwapo atapewa ridhaa  ndani ya chama na ndani ya jimbo kuongoza ,ambapo alisema jambo la kwanza alisema kuwa kumekuwa na tatizo la maji sana katika jimbo lake kitu ambacho ataanza nacho pindi tu atapewa ridhaa ,atajenga Zahanati ,shule ,atatengeneza barabara pamoja na kujenga hospitali


RAIS KIKWETE AMUAPISHA MKURUGENZI MPYA WA UCHAGUZI BW. KAILIMA RAMADHANI KOMBWEY JIONI HII IKULU

$
0
0
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo Julai 25, 2015.
 Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey akiweka sahihi kwenye hati baada ya kuapishwa kuwa kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo Julai 25, 2015.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi baada ya muapisha Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo Julai 25, 2015.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi vitendea kazi baada ya kumuapisha Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo Julai 25, 2015.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey baada ya kumuapisha kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo Julai 25, 2015.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo Julai 25, 2015. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Florens Turuka, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Jaji Hamid Mohamoud  Hamid, Rais Kikwete, Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Msajili wa vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi.
Rais Kikwete akiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi mpya Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey.
 ais Kikwete akisalimiana na mtoto wa Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey, Msemakweli (2)wakati wa hafla hiyo fupi. PICHA NA IKULU

MTANZANIA WAKWANZA MLEMAVU WA MACHO KUGOMBEA UBUNGE KAWE

$
0
0


Mungu ana mpango wake kwa kila aliemuumba,.Tanzania Imara inahitaji Kiongozi Mzalendo, Kutana na Mtanzania wa kwanza mlemavu wa macho kuthubutu kutia nia ya kugombea ubunge kawe.Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) ambapo anatetea haki na mahitaji ya Watanzania wenye ulemavu.2014  MPANJU AMON

Angalia Kipindi cha Nyumbani na Diaspora

WATIA NIA WA UBUNGE JIMBO LA MOSHI MJINI KUPITIA CCM WAJINADI MBELE YA WAJUMBE KATA YA MAWENZI

$
0
0
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini Priscus Tarimo akijinadi mbele ya wajumbe wa CCM kata ya Mawenzi.
Baadhi ya wajumbe wa Chama cha Mapinduzi kata ya Mawenzi wakiwasikiliza wagombea.
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Edmund Rutaraka akiomba kura mbele ya wajumbe wa CCM kata ya Mawenzi.
Baadhi ya wajumbe katika kata ya Mawenzi.
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Patrick Boisafi akiomba kura mbele ya wajumbe wa kata ya Mawenzi,
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini Chief Omary Mwaliko akiomba kura mbele ya wajumbe wa CCM kata a Mawenzi.
Omary Mwaliko akipongezwa na wanachama a chama hicho mara baada ya kutoa maelezo yake katika mkutano huo uliofanyika katika uwanja wa Hindu Mandal.
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Davis Mosha aijinadi mbele ya wajumbe wa CCM kata ya Mawenzi.
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Msohi mjini,Athuman Ramole maarufu kama Buni akiomba kura mbele ya wajumbe wa CCM kata ya  Mawenzi.
Baadhi ya wagombea wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Katibu msaidizi wa CCM wilaya ya Moshi Donatha Mushi mara baada ya zoezi la kujinadi mbele ya wajumbe kumalizika.
Watia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini wakiwa katika gari moja wakielekea katika kata nyingine kuomba kura.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

CHADEMA MOSHI MJINI WAMPITISHA JAFARY MICHAEL KUWANIA UBUNGE WA JIMBO HILO.

$
0
0
Wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Moshi mjini wakiwa katika mkutano maalumu wa kumchagua mtia nia atakaye peperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu nafasi ya Ubunge jimbo la Moshi mjini.
Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge anayemaliza muda wake,Philemoni Ndesamburoakizungumza wakati wa mkutano huo.
Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi mjini,Joel Makwaia akizungumza katika mkutano wa Chadema alipoalikwa kukiwakilisha chama chake.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilaya ya Moshi mjini,Leonard Buberwa akizungungumza akati wa mkutano wa kumpata mgombea wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini.
Watia nia katika nafasi ya Ubunge jimbo la Moshi mjini,Basil Lema,(kushoto) Jafary Michael (katikati) na wakili wa kujitegemea ,Elikunda Kipoko  wakiwa ukumbini kabla ya zoezi la uchaguzi kuanza.
Mbunge wa iti maalumu,Chadema,Lucy Owenya alikuwa ni miongoni mwa wagombea wa nafasi ya Ubunge aliyejitokeza kutetea kiti chake.
Wajumbe wa mkutano wakishangilia mara baada ya kutangazwa kwa matokeo.
Msimaizi wa Uchaguzi ,katibu wa baraza la wanawake mkoa wa Kilimanjaro ,Helga Mchomvu akitangaza matokeo katika uchaguzi huo ambao mgombea Basil Lema aliamua kujitoa kabla ya kura kupigwa.
Mtia nia aliyetangazwa mshindi Jafary Michael akiwa na mkewe katika ukumbi wa Umoja Hotel ambako uchaguzi huo ulifanyika.
Mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo aliyepata kura 9 ,Elikunda Kipoko akizungumza na kuwashukuru wajumbe kwa wale waliompigia kura .
Jafary Michael aliye chaguliwa na Chadema kupeperusha Bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba katika kuwania kiti cha Ubunge jimbo la Moshi mjini.
Michael aliyekuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,akimtambulisha mkewe mbele ya wapiga kura.
Mgombea wa nafasi ya viti maalumu ,Lucy Owenya akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo kwa kumuamini na kumchagua tena kupeperusha bendera ya chama hicho kupitia viti maalum.
Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro,Basil Lema aliyekuwa miongoni mwa wagombea kabla ya kujitoa akizungumza katika mkutano huo mara baada ya Jafary Michael mkutano huo kupitisha jina lake kuwa mpeperushaji wa bendera ya chama hicho katika jimbo la Moshi mjini.  
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images