Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

TPA YAWAWEZESHA WAANDISHI WA HABARI WANAOPAMBANA NA UJANGILI

0
0
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa shilingi milioni mbili kwa Taasisi ya Habari Development Association kwa ajili kuandaa mafunzo ya kuwawezesha waandishi wa habari kujenga weledi wa kufanya tafiti na kuandika habari za kupambana na ujangili.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Awadh Massawe alikabidhi hundi ya thamani ya fedha hizo kwa Mkurugeni wa taasisi hiyo, Bw. Kunze Mswanyama jana jijini Dar es Salaam.

“Tunaunga mkono juhudi hizi za kupambana na ujangili,” alisema Bw. Massawe mjini hapa.
Alisema TPA imefanya hivyo kwa kuwa nchi ina tatizo la uwindaji haramu hasa wa ndovu na usafirishaji wa pembe za ndovu na kulisababishia hasara taifa kupitia mipaka ya taifa.

Alifafanua kwamba bandari ya Dar es Salaam ni sehemu ya mpaka wa taifa, hivyo lazima TPA iunge mkono juhudi za kuelimisha jamii na kuzuia uhalifu huo.

“Tunazidi kuimarisha ulinzi katika bandari kwa kuwa ni sehemu ambayo bidhaa haramu zinaweza kupitishwa,” alisema.

Alifafanua kuwa kwa sasa wanatarajia kufunga kamera 400 za CCTV ili kuimarisha na kuwa skana tatu zimeletwa banadarini kwa ajili yakuziongezea nguvu skana mbili zilizopo.

Pia alisema wanatarajia kupata msaada wa mbwa maalumu wa ulinzi watakaotolewa na serikali ya Marekani. 

Alisema TPA inaendelea kuwajengea uwezo wafanyakazi kimaadili ili kuendelea kufanya kazi kwa weledi na uaminifu kwa faida ya taifa.

Mkurugenzi wa Habari Development Association, Bw. Mswanyama alisema fedha walizopewa watazitumia kwa kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari 54 wa maswala ya ujangili kupata weledi na kutafiti na kufichua ujangili.

“Tunahitaji kujenga weledi zaidi wa kupambana na ujangili wa rasirimali zetu ili taifa liweze kunufaika nazo,” alieleza.

Alisema taasisi yao inaundwa na waandishi wa habari wanaoandika habari za kupambana na ujangili na rasirimali nyingine katika mbunga mbalimbali zikiwemo za Sadani, Serengeti, Mikumi na Selou.

 
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), Bw. Awadhi Massawe katikati akizungumza wakati alipokuwa akikabidhi hundi ya shilingi milioni mbili(2m/-) kwa Taasisi ya Habari Development Association, kwa ajili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo  waandishi wa habari kufanya tafiti na kuandika habari za kupambana na ujangili nchini. Taasisi hiyo inaundwa na waandishi wa habari wanaoandika habari za ujangili kwa kina. Kulia ni Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Bw. Kunze Mswanyama na kushoto ni Ofisa Mawasiliano Mwandamizi wa TPA, Bw. Focus Mauki.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), Bw. Awadhi Massawe kushoto akimkabidhi hundi ya shilingi milioni mbili (2m/-) Mkurugeni wa Taasisi ya Habari Development Association, Bw. Kunze Mswanyama kwa ajili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kufanya tafiti na kuandika habari za kupambana na ujangili. Taasisi hiyo inaundwa na waandishi wa habari wanaoandika habari za ujangili kwa kina.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONESHO YA 10 YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA VYUO VYA ELIMU YA JUU NCHINI.

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kufungua  rasmi Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam.  Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mvumbuzi wa mashine ya kuchujia maji safi, Dkt. Askwar Hilonga, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la Chuo Kikuu cha Nelson Mandela, katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha, Atilio Raphael (kushoto kwake) na William Sambera (kulia) kuhusu Kompyuta ya mezani waliyoibuni maalum kwa ajili ya kufundishia somo la Kompyuta, wakati Makamu alipotembelea Banda la Chuo hicho katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 :- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha, William Sambera (kulia) kuhusu Kompyuta ya mezani iliyobuniwa maalum kwa ajili ya kufundishia somo la Kompyuta, wakati  Makamu alipotembelea Banda la Chuo hicho katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akioneshwa Plastiki zilizotengenezwa  kwa kutumia Mahindi kutoka kwa Mkurugenzi wa Chuo cha The United African University Of Tanzania (UAUT) Chang Kilee, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la Chuo hicho katika Maonesho ya 10 ya  Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya Mashine ya 3D Printer iliyobuniwa nchini Korea na inayotumika kufundishia wanafunzi wa IT wa Chuo cha 'The United African University Of Tanzania' (UAUT), wakati alipotembelea banda la maonesho la Chuo hicho katika Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Chuo hicho, Chang Kilee, akimpa maelezo kuhusu Mashine hiyo. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja kati ya mashine za kufanya miamala za Max Malipo, huku akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko wa Kampuni hiyo, Machungu Msama,  wakati alipotembelea banda lao la maonesho katika Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tunguu Zanzibar, Hadi Mohamed  (kushoto) na baadhi ya wanafunzi wake, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la Chuo hicho kwenye Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja baadhi ya walimu, viongozi na wanafunzi wa Vyuo Vikuu.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja baadhi ya walimu, Kung Fu na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Udom.
 Dkt. Bilal, akisalimiana na mmoja wa Walimu wa Chuo cha Liaoning Shi hua, Liju Shi, wakati alipotembelea katika Banda lao.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Baadhi ya Wahadhiri na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
 Baadhi ya Wahadhiri na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
 Baadhi ya Wahadhiri na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
 Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDOM, wakitoa burudani ya mchezo wa Kung Fu, wakati wa ufunguzi huo.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDOM, wakitoa burudani ya mchezo wa Kung Fu, wakati wa ufunguzi huo.

RAIS JAKAYA KIKWETE KUWA MGENI RASMI KUMBUKUMBU YA MASHUJAA

0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa zitakazofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.Bw. Sadiki amefafanua kuwa shughuli zote katika viwanja vya Mnazi Mmoja zitaanza saa mbili Asubuhi na kumalizika saa sita mchana, pia wananchi watakaohudhuria kumbukumbu hiyo watapata fursa ya kushuhudia matukio yatakayokuwa yananendelea uwanjani hapo kupitia Luninga kubwa zitakazokuwepo katika maeneo yote muhimu ya uwanja.

Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika mazoezi katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho ya sherehe za Kumbukumbu ya Mashujaa.Picha na Aron Msigwa.

RAIS JAKAYA KIKWETE MGENI RASMI MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA!

Na.Aron Msigwa - MAELEZO.
23/7/2015. Dar es salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Kikwete anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa itakayofanyika Julai 25, 2015  Katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa maandalizi ya maadhimisho hayo leo jijini Dar es salaam,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki amesema maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika jijini Dar es salaam kuwakumbuka na kuwaenzi mashujaa waliojitoa muhanga kupigania uhuru na ukombozi wa Taifa la Tanzania,kulinda na kudumisha amani na utulivu wa nchi.

Amesema Maadhimisho hayo yatapambwa na Gwaride la Kumbukumbu litakaloandaliwa na vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),Polisi ,Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Aidha, amesema  kutakuwa na  Mizinga salama itakayopigwa, uwekaji wa silaha za asili na maua kwenye mnara wa kumbukumbu, Kutakuwa na sala na Dua kutoka kwa viongozi wa Madhehebu mbalimbali ya dini hapa nchini.

Bw. Sadiki amefafanua kuwa shughuli zote katika viwanja vya Mnazi Mmoja zitaanza saa mbili Asubuhi na kumalizika saa sita mchana ambapo wananchi watakaohudhuria kumbukumbu hiyo watapata fursa ya kushuhudia matukio yatakayokuwa yananendelea uwanjani hapo kupitia Luninga kubwa zitakazokuwepo katika maeneo yote muhimu ya uwanja.
  
Ameongeza kuwa siku hiyo baadhi ya barabara katika jiji la Dar es Salaam zikiwemo  Lumumba ,Uhuru na Bibi Titi zitafungwa kwa muda ili kuhakikisha usalama wa watumiaji wa barabara hizo watakaohudhuria maadhimisho hayo .

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ametoa ufafanuzi kuhusu changamoto zinazoendelea kujitokeza za kusuasua kwa zoezi uandikishaji wa wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura katika mfumo wa BVR jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Manispaa za jiji la Dar es Salaam wanaendelea kushughulikia matatizo mbalimbali yaliyojitokeza katika siku ya kwanza na ya pili katika baadhi ya vituo hususani baadhi ya mashine za BVR kushindwa kufanya kazi vizuri.

Akizungumzia baadhi ya malalamiko yanayotolewa na wananchi hasa tatizo la uchelewaji wa waandikishaji kufika katika vituo walivyopangiwa kwa wakati amesema kuwa Serikali ianaendelea kuchukua hatua ili kukomesha tabia hiyo.

Amewaagiza Wakurugenzi wa Manispaa zote za jiji la Dar es Salaam kuwachukulia hatua watumishi hao wazembe kwa kuwafuta kazi ili kuepusha madhara na vurugu zinazoweza kuepukika na uongeza kuwa kazi ya uandikishaji wananchi inatakiwa kuanza saa 2 asubuhi mpaka saa 12 jioni kila siku kwa tarehe zilizopangwa.

Kuhusu taarifa za uwepo wa baadhi ya watendaji kuwaingiza waandikishaji wasiohusika kusimamia zoezi hilo Mkuu wa Mkoa huo amewataka watendaji hao kuacha mara moja tabia hiyo ili kuepuka kuvuruga zoezi hilo na kwamba hatua kali za kisheria  zitachuliwa dhidi yao.

Pia amevitaka Vyama vya siasa kuacha kutumia mwanya huo kuweka bendera au kuvaa mavazi yanayoashiria kampeni za siasa ili kuepusha vurugu.

SERIKALI YAZINDUA KAMATI YA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA USALAMA ZA WATU WENYE UALBINO

0
0
 Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro akiizundua Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Kamati hii imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliitoa wakati alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto meza kuu ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi, na kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi akiwafafanulia jambo wajumbe wa Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini. Kamati hiyo ambayo ni ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliitoa alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu, imezinduliwa leo na Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati meza kuu) kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Mwenyekiti wa Chama cha Albino nchini (TAS), Ernest Kimaya akimshukuru Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati meza kuu), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (kulia meza kuu), kwa msaada wao ambao umesaidia matukio ya utekaji na mauaji ya albino kupungua kwa kiasi kikubwa. Pia alisema Kamati iliyozinduliwa itaongeza nguvu zaidi katika kukabiliana na changamoto ambazo zinawakabili za usalama wao nchini. Kushoto meza kuu ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi. Kamati hiyo ilizinduliwa na Waziri Dk. Migiro kwa niaba ya Waziri Chikawe, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
 Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (kulia), na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu mara baada ya kupokelewa Waziri huyo katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ili azindue Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Kamati hiyo imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipoitoa alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (wanne kulia-mstari wa mbele), Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (katikati), na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (watatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa uzinduzi wa Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini. Kamati hiyo ilizinduliwa na Waziri Migiro kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Hata hivyo Kamati hiyo imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipoitoa alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  

KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

MAMA SALMA AWASILI MALAYSIA NA KUTEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGENEZA TRENI CHA SMH RAIL MJINI KUALA LUMPUR

0
0
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa watoto wa wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Malaysia mara baada ya kuwasili kwenye Hoteli ya Royale Chulan iliyopo Kuala Lumpur, Mji Mkuu wa Malaysia tarehe 23.7.2015.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Mkurugenzi Mkuu wa SMH Rails Bwana Narayanan Kuppusamy mara baada ya kuwasili kwenye karakana ya treni iliyoko Kuala Lumpur nchini Malaysia Tarehe 24.7.2015.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa Mke wa Mkurugenzi Mkuu wa SMH Rails Mama Lakshmi Narayanan ikiwa ni ishara ya kumkaribisha kutembelea karakana ya treni na mabehewa huko Malaysia tarehe 24.7.2015.

 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa SMH Rail Bwana Narayanan (kulia) na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima kushoto) wakielekea kwenye jengo la karakana ya reli ili kujionea shughuli mbalimbali za matengenezo ya vichwa vya treni na mabehewa tarehe 24.7.2015.

 Mke wa Rais na Ujumbe wake wakitembelea sehemu mbalimbali zinahusika na matengenezo ya injini za treni na mabehewa.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitia saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye karakana ya SMH Rail huku Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Bwana Narayanan Kuppusamy akishuhudia.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika moja ya mabehewa ya abiria yaliyokarabatiwa na kampuni ya SHM Rail na yanayotumika kubeba abiria mijini.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete pamoja na ujumbe wake wakipiga picha ya pamoja na mwenyeji wake Bwana Narayanan na baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo mbele ya behewa lililokamilika na tayari kwa kubeba abiria.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi ya picha Mkurugenzi Mkuu wa SMH Rail Bwana Narayanan mara baada ya kutembelea karakana ya treni ya kampuni hiyo huko Kuala Lumpur Malaysia tarehe 24.7.2915.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake baada ya kutembelea karakana ya injini za treni na mabehewa ya kampuni ya SHM  huko Malaysia tarehe 24.7.2015.
  Mkurugenzi Mkuu wa SHM Rail Bwana Narayanan Kuppusamy akitoa neon la shukrani kwa ujio wa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kutembelea karakana ya treni huko Kuala Lumpur nchini Malaysia tarehe 24.7.2015
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongozana na Mwenyeji wake Bwana Narayanan baada ya kumaliza shughuli ya kutembelea karakana ya treni.

WATIA NIA CCM WAENDELEA NA ZIARA YA KUJITAMBULISHA KATIKA KATA MBALIMBALI JIMBO LA ARUSHA MJIN

0
0
SAM_4061Mtia nia ya ubunge kwa CCM Philemon Mollel akizungumza katika mkutano wa kujinadi mbele ya wana CCM wa kata ya Sinoni jijini Arusha ili kuomba ridhaa yakuteuliwa na chama chake kuwania ubunge wa jimbo la Arusha katika uchaguzi wa mwezi Oktoba Mwaka huu.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_4098Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ya ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM akinadi sera zake mbele ya wanachama wa chama hicho katika kata ya Sakina jijini Arusha ili kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwamgombea wa ubunge jimbo la Arusha kupitia CCM.
SAM_4041Mtia nia ya ubunge kupitia CCM mwanasheria Victor Njau akimwaga sera zake mbele ya wana CCM wa kata ya Sinoni jijini Arusha ili kuomba ridhaa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa mwezi Oktoba mwaka huu.
 
 
SAM_4116Wanachama na waasisi wa CCM wa kata ya Sakina jijini Arusha wakisikiliza kwa umakini sera zinazotolewana watia nia ya ubunge wa jimbo la Arusha walipokua wakijinadi kwao ili kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chaa chao kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
SAM_4177Kada wa CCM Mosses Mwizarubi anayeomba ridhaa yakuteuliwa na chama chake kuwania ubunge wa jimbo la Arusha akisisitiza jambo katika mkutano wa kujinadi uliofanyika katika kata ya Ngarenaro jijini Arusha.
SAM_4059Mtia nia ya ubunge wa jimbo la Arusha kupitia CCM Hamis Migire akijieleza mbele ya wanachama wa CCM wa kata ya Sokon One jijini Arusha ili kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea wa kiti hicho kupitia CCM.
SAM_4157Mmoja wa wanachama wa CCM wa kata ya Sakija jijini Arusha ambaye hakujulikana jina lake mara moja akipitia kwa umakini kipeperushi chenye maelezo binafsi na mikakati ya kazi za ubunge cha mtia nia ya ubunge wa chama hicho Mustafa Panju wakati wa mkutano wa kujinadi wa watia nia hao uliofanyika katika kata hiyo.
SAM_4140Team kanitangaze wakifuatilia hotuba za watia nia ya ubunge kupitia CCM katika kata ya Elerai jijiniArusha 
SAM_4175Hapa ni sehemu ya wananchi wakifatilia hotuba mbalimbali za watiania nafasi ya Ubunge
SAM_4155Wananchi waliojitokeza kuwasikiliza watia nia Ubunge CCM katika kata ya Ngarenaro jijini Arusha.

BALOZI WA AFRIKA KUSINI ASHIRIKI KUFANYA USAFI MHIMBILI

0
0
 Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini, Thami Mseleku akifanya usafi katika Wodi (A) ya Watoto iliyopo katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI),ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela.
Muunganishi wa Makazi katika Umoja wa Mataifa,Alvaro Rodriguez (wa kwanza kutoka kushoto),Balozi wa Afrika Kusini nchini,Thami Mseleku (wa pili) wakiwa na baadhi ya wawakilishi wakipokea misaada kwa niaba ya walezi wengine.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI),Dkt.Othman Kiloloma akizungumza na waandishi wa habari juu ya msaada waliopokea kutoka kwa Umoja wa Mataifa,,ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela.
Baadhi ya wadau wakiendelea na usafi katika sehemu ya maadhimisho ya  ya siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela. 

 
 Baadhi ya washiriki waliofanya usafi hospitali ya  Mhimbili Wakiwa katika picha ya pamoja. 
PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.

WATANZANIA WATAKIWA KUANGALIA UBORA WA ELIMU YA VYUO VIKUU VYA NJE NA SIO MAJIMA-MOLLEL

0
0
Na Mwandishi Wetu
Watanzania wametakiwa kuangalia ubora elimu katika vyuo vya nje na sio kuangalia majina ya vyuo hivyo ili ukuweza kupata wataalamu wataosaidia nchi kupata maendeleo.

Hayo aliyasema jana,Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link,Abdulmaliki Mollel katika maonesho ya  Elimu ya Vyuo Vikuu vya Ndani na Nnje ya nchi yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Mollel amesema yeye akiwa wakala wa vyuo vikuu vya nje anatambua vyuo walivyoenda watanzania kusoma hawakumuangusha kutokana na kujituma kwao pamoja na mazingira rafiki ya kusomea katika vyuo hivyo.

Amesema watu wanaokwenda katika vyuo kwa kuangalia majina wanarudi na kuwa hawana msaada wa elimu walioipata nje na kulazimika nchi kuchukua wataalam kutoka nje wenye uwezo kutokana na vyuo vyao na kuacha watanzania waliopata elimu katika vyuo vyenye majina lakini havina elimu bora.

Mollel amesema kuna vyuo vingi nje lakini suala la kuangalia ubora wa elimu inayotolewa na mazingira ya kusomea kutokana na baadhi ya watu waliosoma wamekuwa wakiiga utamaduni mwingine na kuingiza nchini na kushindwa kuendana na utamaduni wa ndani na kusababisha kukosa ajira.

Mollel amewataka watanzania kutumia Global Education Link katika kuweza kuwapa vyuo bora ambavyo itasaidia vijana kupata elimu bora kutokana na uwezo wa vyuo husika.

Aidha amesema Global Education Link imekwenda mbali zaidi kwa baadhi ya vyuo vya nje kuingiza kozi katika vyuo vya ndani ikiwemo kozi ya Petrol ,Gesi.

Amesema  anafanya kazi na vyuo 10 vya nje ambavyo vinazalisha elimu bora yenye kumsaidia mtanzania katika kuweza kuongeza uwezo wa kitaalam katika nchi.
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa shirika la taifa la bima (NIC), Sam Kamanga akipata maelezo kutoka kwa afisa masoko mwandamizi wa shirika la taifa la bima (NIC),Joyce Mswia katika maoneho ya wiki ya elimu ya vyuo vikuu katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Da es Salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa Global Education  Link akiwapa maelezo wananchi alipotembelea banda la Global Education  Link katika maoneho ya wiki ya elimu ya vyuo vikuu katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Da es Salaam.
Wanafunzi wakipata maelekezo walipotembelea  maoneho ya wiki ya elimu ya vyuo vikuu katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Da es Salaam.

Tabora Wanufaika na Mafunzo ya ULINGO – Tanzania Women Crossparty Platform (TWCP)

0
0
ULINGO WA WANAWAKE WANASIASA – Tanzania Women Crossparty Platform (TWCP) ni shirika lisilo la kiserikali lililoendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watia nia wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu katika nyadhifa mbalimbali za uongozi wa nchi ikiwa ni kuchangia kutoa elimu inayolenga kuleta usawa kama haki msingi ya Mtanzania. Mafunzo hayo yamedhaminiwa na UNWomen.

Mafunzo hayo yamewanufaisha walengwa husika kwa kujipatia elimu hiyo huku wawezeshaji wakiwa ni Hilda Stuart Dadu na Emmiliana Msaguka waliohakikisha wanawafikia watiania katika mkoa wa Tabora na kuendesha mafunzo hayo pale Student Center.
t-wcp (2)
Wanufaika na watia nia za kugombea nafasi mbalimbali na wa vyama tofauti tofauti wakifuatila mafunzo hayo yaliyotolewa na Hilda Stuart Dadu kutoma TWCP
t-wcp (3)
Watia nia wakichukua kumbukumbu za mafunzo hayo mapema leo hii
t-wcp (4)
Miongoni mwa wanufaika wa mafunzo hayo akifuatilia jambo kwa umakini.
t-wcp (5)
Wakti mafunzo yakiendelea na maswali yakiulizwa kwa ufafanuzi zaidi kutoka kwa wawezeshaji.
t-wcp (6)
Hilda Stuart Dadu wa ULINGO (aliyesimama) akisisitiza jambo wakati mafunzo yakiendelea.
t-wcp (1)t-wcp (7)t-wcp (8)
Hawa, mgombea wa ubunge wa viti maalumu kwa tiket ya chadema akiuliza swali kwa muwezeshaji t-wcp (12)
t-wcp (11)
Muwezeshaji Emmiliana akitoa zoezi kwa wanafunzi wake ili kukazia zaidi kile walichofundishwa na kukifanya kwa vitendo.
t-wcp (13)
Miongoni mwa wanakundi wakijadiliana jambo baada ya kupewa zoezi na muwezeshaji wa mafunzo.
t-wcp (10)
t-wcp (9)
Picha ya pamoja ya wanufaika wa mafunzo ya ULINGO na wawezeshaji wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo watia nia za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Mafunzo hayo yamekuja wakati huu ambao ndiyo haswa muda mwafaka wa uchaguzi mkuu wa ngazi za udiwani, ubunge na Urais.

SERIKALI YAZINDUA KAMATI YA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA USALAMA ZA WATU WENYE UALBINO

0
0
????????????????????????????????????
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro akizundua Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Kamati hii imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliitoa wakati alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto meza kuu ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi, na kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu.
Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
????????????????????????????????????
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi akiwafafanulia jambo wajumbe wa Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini. Kamati hiyo ambayo ni ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliitoa alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu, imezinduliwa leo na Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati meza kuu) kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu.
3
Mwenyekiti wa Chama cha Albino nchini (TAS), Ernest Kimaya akimshukuru Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati meza kuu), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (kulia meza kuu), kwa msaada wao ambao umesaidia matukio ya utekaji na mauaji ya albino kupungua kwa kiasi kikubwa. 

Pia alisema Kamati iliyozinduliwa itaongeza nguvu zaidi katika kukabiliana na changamoto ambazo zinawakabili za usalama wao nchini. Kushoto meza kuu ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi. Kamati hiyo ilizinduliwa na Waziri Dk. Migiro kwa niaba ya Waziri Chikawe, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo.

4
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (kulia), na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu mara baada ya kupokelewa Waziri huyo katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ili azindue Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. 

Kamati hiyo imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipoitoa alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam.
5
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (wanne kulia-mstari wa mbele), Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (katikati), na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (watatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa uzinduzi wa Kamati itakayoshughulikia changamoto za usalama za watu wenye Ualbino nchini. Kamati hiyo ilizinduliwa na Waziri Migiro kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. 

Hata hivyo Kamati hiyo imeundwa kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipoitoa alipokutana na viongozi wa Chama cha Albino nchini (TAS), Machi 5, mwaka huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam

KIOTA KIPYA CHA MARAHA CHA JOZI LOUNGE CHAZINDULIWA MSASANI VILLAGE JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Kiota Kipya Cha Maraha kimezinduliwa Kimezinduliwa Jijini Dar es Salaam jana Jiioni. Kiota hicho Jozi Lounge, inapatikana Pande za Msasani Village, jirani kabisa na Shule ya Msingi Msasani.
 Mmiliki wa Jozi Lounge, Dismass Massawe (kushoto)  akifungua   Champaign wakati wa uzinduzi wa kiota hicho.  Hafla hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali ambao walikunywa na kucheza mpaka majogoo.Hiyo ndiyo habari ya Mujini.
Mmiliki wa Jozi Lounge, Dismass Massawe (kushoto)huku meneja wake ni Nick Rawlings(Mzungu anayefungua Champaign).
 Sehemu ya Counta ya kiota hicho cha Jozi.
Wadau wakipiga picha kabla ya kuzama ndani kwenye kiota cha maraha.
 DJ mkali anaeporomosha muzic wa hatari

 Wadau kutoka Kampuni ya Executive Solution ya jijini Dar es salaam ambao ndio walikuwa waratibu wakuu wa uzinduzi huo wakishow love.
 Ilikuwa ni hatari kuyarudi magoma mwanzo mwisho. Hakuna kulala wala kuchoka ndani ya Jozi Lounge

KOMBE LA KAGAME; YANGA YAIFUNGA KMKM 2-0

0
0
 Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akimtoka beki wa KMKM, Khamis Ali Khamis wakati wa mchezo wa Kombe la Kagame uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshinda 2-0.
 Deus Kaseke akiwatoka wachezaji wa KMKM.
 Golikipa wa timu ya KMKM ya Zanzibar, Nassor Abdulla Nassor akiokoa moja ya hatari langoni mwake wakati timu yake ilipopambana na Yanga katika mchezo wa Kombe la Kagame.
Donald Ngoma (kulia) akiwania na beki wa KMKM, Khamis Ali Khamis.
Mashabiki wa Yanga wakishangilia timu yao.

UZINDUZI WA KAMPENI YA WAZAZI NIPENDENI AWAMU YA PILI WAFANYIKA VIWANJA VYA MWEMBE YANGA TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
 Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Neema Rusibamayila kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo Dk. Seif Rashid  (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  kampeni ya Wazazi Nipendeni awamu ya pili  katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam leo mchana. Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Anna Bodipo Memba na wa pili kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magema. 
 Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Anna Bodipo Memba (kulia), akitoa hutuba yake kwenye uzinduzi huo.
 Mshauri wa masuala ya Afya ya Jamii kutoka Taasisi ya HBC, Mdadike Thabit (kulia), akimuelekeza jambo mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Neema Rusibamayila wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya watoa huduma kabla ya kufanyika uzinduzi huo.
 Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupata huduma za afya ya jamii kwenye uzinduzi huo.
 Wanamuzi wa bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia 
wakitoa burudani.
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magema akizungumzia mikakati ya Afya ya Jamii katika mkoa huo.



 Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Neema Rusibamayila, akitoa hutuba yake ya uzinduzi.
 Watoto nao walikuwepo kwenye uzinduzi huo.
 Mwanamuziki Juma Nature akitoa burudani kwenye uzinduzi huo.
 Wananchi walioshiriki uzinduzi huo.
Kiongozi wa kundi la muziki la Wanaume Family, Chege (kulia), akishambulia jukwaa katika uzinduzi huo.
Msanii wa kundi la utamaduni la HD Entertainment la Mbezi Beach, Michael Kamugisha, akiwa ameruka juu wakati wa kundi hilo lilipokuewa likitoa burudani katika uzinduzi huo.


Na Dotto Mwaibale

TANZANIA imeweza kufikia lengo la milenia namba 4 la kupunguza vifo vya watoto kwa theluthi mbili kutoka vifo 152 hadi 54 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa hai.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Neema Rusibamayila kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo Dk. Seif Rashid wakati akizindua kampeni ya awamu ya pili ya Wazazi Nipendeni katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam leo mchana.

Alisema pamoja na kutofikia lengo la melenia namba 5 la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa robo tatu kufikia vifo 193 kwa kila vizazi hai laki moja, taarifa za umoja wa mataifa za mwaka 2014 zinaonyesha kuwa Tanzania imeweza kupunguza vifo hivyo toka 770 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 1990 hadi kufikia 410 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2014.

"Sababu zinazosababisha watoto waliochini ya miaka mitano kupoteza maisha ni kuharisha, nimonia na malaria na kuwa zinachangia takribani asilimia 50 ya vifo vya watoto hao waliochini ya miaka mitano" alisema Dk.Rusibamayila.

Alisema utapiamlo nao ni tatizo linalochangia vifo vya watoto hao kwani takwimu za mwaka 2010 zinaonyesha kuwa kiwango cha udumavu ni asilimia 42 kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano.


Dk.Rusibamayila aliongeza kuwa vifo vya watoto wachanga havijapungua kwa kasi inayoridhisha na vinachangiwa na wale watoto wanaozaliwa njiti, kushindwa kupumua vizuri mara baada ya kuzaliwa na maambukizi ya bakteria. 

HUDUMA YA UPASUAJI WA WATOTO WENYE UGONJWA WA KICHWA KUJAA MAJI NA MGONGO WAZI YAZINDULIWA RASMI MKOANI KAGERA KATIKA HOSPITARI YA RUFAA YA MKOA

0
0
Na Faustine Ruta, Bukoba
Shirika lisilokuwa la serikali la Friends of Children with Cancer Tanzania (FOCC TZ) lazindua rasmi huduma ya upasuaji wa watoto wenye ugonjwa wa vichwa kujaa maji na mgongo wazi mkoani Kagera katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa ambapo jumla ya watoto arobaini wenye tatizo hilo wanatajiwa kufanyiwa upasuaji kuanzia Julai 25-26, 2015. 


Mkurugenzi wa shirika la FOCCTZ Bw. Walter Miya katika uzinduzi huo alisema kuwa baada ya kutoa matangazo kupitia redio za jamii mkoani Kagera kwa muda wa siku mbili wameweza kupata watoto 70 wenye tatizo la vichwa kujaa maji na mgongio wazi kutoka katika wilaya zote saba za mkao wa Kagera na nje ya mkoa. 


Bw.Walter alisema watoto walioweza kufikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwa msaada wa shirika lake ni 40 na watoto 30 wameshindwa kufika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo wazazi kutokuwa na uwezo wa kuwasafirisha watoto hao, pia changamoto ya wananchi kuwa na imani potofu ya kuwa watoto hao wamerogwa.

Huduma hiyo inatolewa mkoani Kagera na shirika la Friends of Children with Cancer Tanzania wakishirikiana na Madaktari wataalam wa upasuaji huo kutoka Hospitali ya Rufaa ya Bugando pia kutoka katika kitengo cha Muhimbili Orthopaedic Instutite (MOI) kilichopo Hospitali ya Rufaa ya Taifa Muhimbili.

Daktari Gerald D. Mayaya kutoka idara ya upasuaji Hospitali ya Rufaa Bugando akielezea chanzo cha tatizo la ugonjwa wa kichwa kujaa maji na mgongo wazi alisema kuwa ni mishipa ya kusafirisha maji kichwani kuziba na kichwa huanza kuvimba ambapo kuna watoto huzaliwa na ugonjwa huo pia wengine upatwa na ugonjwa huo wakiwa tayari wamezaliwa na watu wazima pia hupatwa na ugojwa huo.
Lengo la kutoa huduma hiyo katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kagera ni kupunguza gharama kwa wazazi wenye watoto wenye tatizo hilo badala ya kwenda Bugando na muhimbili wapate huduma hiyo karibu na maeneo yao. Pia kutoa ujuzi kwa wataalam wa haspitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera ili wawe wanatoa huduma hiyo katika hospitali hiyo. Alisema Mkurugenzi wa shirika la FOCCTZ Bw. Walter. 


Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella baada ya kuzindua huduma hiyo na kutembelea wodi ya watoto wenye tatizo la vichwa kujaa maji na mgongo wazi alisema amejifunza mambo mengi maana mwanzo alijua kuwa ugonjwa huo kwa watoto huzaliwa nao kumbe hata mara baada ya kuzaliwa au mtu mzima anaweza kupatwa na ugonjwa huo.


Mhe Mongella alitoa wito elimu kutolewa kwa wingi ili wananchi waweze kujua kuwa ugonjwa huo unatibika ili wazazi na walezi waweze kuwaleta watoto wenye tatizo hospitali ili wakatibiwe. Pia aliwashukuru Shirika la FOCCTZ kwa kuzindua huduma hiyo ambayo aliita huduma takatifu kwani inaokoa maisha ya watoto walio wengi.

Wito, Mhe. Mongella alitoa wito kwa wananchi wenye uwezo kuweza kushirikiana na shirika hilo ili kuchagia huduma hiyo kuokoa maisha ya watoto. Pia alitoa wito kwa Wanahabari wa mkoa wa Kagera na Tanzania kwaujumla kuelimisha jamii juu ya tatizo hilo ili liweze kupunguzwa kwa kiasi kikubwa.

Naye Vaileth John Makula (32) mzazi wa Gib Philimoni kutoka Wilaya ya Karagwe alilishukuru Shirika la FOCCTZ kuleta huduma hiyo Kagera maana anasema kuwa mwanae Gib alizaliwa katika hali ya kawaida na baada ya miezi minne tatizo la kuvimba kichwa lilianza na alimpeleka mtoto wake katika hospitali teule ya Wilaya Nyakahanga alikoambiwa ampeleke Bugando ambako hakumpeleka kwa kukosa nauli. Mama Gib alishukuru na alisema ana imani na madaktari hao kuwa watamponya mwanae Gib.
Madhara ya ugonjwa wa kichwa kujaa maji na mgongo wazi unaweza kusababisha upofu wa macho, mtoto kutojiweza kabisa kutumia muda wote akiwa amelala tu, pia huathiri ubongo, na wakati mwingine husababisha vifo kwa watoto.

Kwa takwimu alizotoa Bw. Walter alisema kwa kila watoto 1000 wanaozaliwa duniani watoto 2 huzaliwa na tatizo la kichwa kujaa maji, kwa nchi ya Tanzania watoto wote wanaozaliwa kwa mwaka watoto 4580 huzaliwa au hupatwa na ugonjwa huo ambapo kila watoto 1000 wanaozaliwa watoto 3 huwa na tatizo hilo.
Shirika la Friends of Children with Cancer Tanzania lilianzishwa mwaka 2013 tayari limeweza kuwahudumia watoto 300 katika nchi nzima ya Tanzania na malengo yake ni kuendele kupunguza ukubwa wa tatizo kwa kuanzisha kambi za upasuaji kama walivyofanya mkoani Kagera.
Mganga Mfawidhi wa Haspitalia ya Rufaa ya mkoa wa Kagera Dk. Juma Nyakina aliwashukuru shirika la FOCCTZ na liwahakikishia kuwa hospitali yake ipo tayari kwa kuwawekea mazingira mazuri wataalamu hao na kuandaa vitendanishi ili waweze kuifanya kazi yao kwa ufanisi mkubwa pia alisema wataalam wa hospitali hiyo wapo tayari kujifunza na kupata ujuzi huo.

TTCL yaunganisha Ofisi na Kanda za MSD kwenye Mkongo

0
0
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akionesha orodha ya wateja wanaopata huduma ya mkongo toka kampuni hiyo kwenye tableti yake, alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL kwenye hafla ya kukabidhi mradi wa huduma ya mkongo kwa Bohari ya Dawa nchini (MSD) leo jijini Dar es Salaam. Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akionesha orodha ya wateja wanaopata huduma ya mkongo toka kampuni hiyo kwenye tableti yake, alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL kwenye hafla ya kukabidhi mradi wa huduma ya mkongo kwa Bohari ya Dawa nchini (MSD) leo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania inayotolewa na kampuni ya TTCL. Ofisi za Kanda za MSD zimeunganishwa na Makao Makuu na huduma za mkongo wa mawasiliano ili kufanya kazi zake kwa haraka na ufanisi zaidi. Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya  mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania inayotolewa na kampuni ya TTCL. Ofisi za Kanda za MSD zimeunganishwa na Makao Makuu na huduma za mkongo wa mawasiliano ili kufanya kazi zake kwa haraka na ufanisi zaidi.Baadhi ya maofisa wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na Bohari ya Dawa Nchini (MSD) pamoja na wageni waalikwa wakiwemo wanahabari wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) unaotolewa na kampuni ya TTCL. Baadhi ya maofisa wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na Bohari ya Dawa Nchini (MSD) pamoja na wageni waalikwa wakiwemo wanahabari wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) unaotolewa na kampuni ya TTCL.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kulia) akisaini hati ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD), kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani akishuhudia kabla ya kukabidhiwa. Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kulia) akisaini hati ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD), kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani akishuhudia kabla ya kukabidhiwa.Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (kushoto) akisaini hati ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) leo Makao Makuu ya Ofisi za MSD Dar es Salaam, kulia ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akishuhudia. Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (kushoto) akisaini hati ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) leo Makao Makuu ya Ofisi za MSD Dar es Salaam, kulia ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akishuhudia.Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (wa tatu kushoto waliokaa) na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (wa pili kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa kampuni ya Simu Tanzania na Bohari ya Dawa Nchini katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania na kampuni ya TTCL. Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (wa tatu kushoto waliokaa) na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (wa pili kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa kampuni ya Simu Tanzania na Bohari ya Dawa Nchini katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania na kampuni ya TTCL.[

/caption] KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) leo imekabidhi mradi mkubwa wa Mkongo wa Mawasiliano ambao umeyaunganisha matawi yote ya Bohari ya Dawa Nchini (MSD) na Makao Makuu ili kufanya kazi zake kwa haraka na kwa ufanisi. Hafla ya kukabidhi mradi huo imefanyika leo Makao Makuu ya Ofisi za MSD zilizopo jijini Dar es Salaam. Akikabidhi mradi huo, kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura, Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania, Peter Ngota alisema kampuni hiyo inajisikia fahari kufanikiwa kuunganisha ofisi zote za kanda za MSD na Makao makuu kupitia mkongo wa mawasiliano ambao ni salama na wauhakika katika utendaji wa kazi. Alisema MSD ni moja ya wateja wake wakubwa ambao wameunganishwa kihuduma kupitia mkongo wa mawasiliano ambao ufanisi wake ni mkubwa na salama kwa wateja tofauti na teknolojia nyingine za mawasiliano. 

Alisema huduma za mkongo wa mawasiliano zinazotolewa na TTCL kwa wateja wake ni salama na zenye ubora katika ufanisi jambo ambalo limevuta idadi kubwa ya wateja kuongezeka kila uchao. Alisema kwa sasa TTCL inatoa huduma hizo kwa makampuni ya simu, taasisi mbalimbali za umma na binafsi, mabenki, hospitali kadhaa, vyombo vya habari, wateja binafsi pamoja na mataifa kama Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Zambia na nchi ya Malawi. 

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani alisema MSD ilianza kufungiwa mawasiliano ya mkongo Mwezi Mei, 2011 kwa kuunganisha ofisi za makao makuu na baadaye ofisi mpya za mauzo zilizopo Muleba zilizounganishwa mwaka 2013. Alisema MSD ilifanya uamuzi wa kuhamia kwenye teknolojia ya Mkongo baada ya kuona uwepo wa matatizo makubwa yaliyokuwepo katika teknolojia ya awali ambayo ni waya wa jadi yaani shaba ambayo pia ilitolewa na kampuni ya TTCL. 

"...Bohari ya Dawa iliamua kuhamia katika teknolojia hii baada ya kufanya utafiti wa kina na kuona faida ambazo zinaweza kupatikana kwa kutumia teknolojia hii (mkongo) na hivyo kuachana na matatizo yanayosababishwa na teknolojia ya shaba. Hii ina maana mkongo unaweza kubeba habari zaidi na kwa ubora mkubwa kuliko waya wa shaba," alisema Mwaifwani. 

Alisema kwa sasa MSD imeanza kupata mafanikio makubwa baada ya kuanza kutumia huduma za mkongo na tayari TTCL imeyaunganisha Ofisi 10 za MSD ambazo ni Kanda nane (8) pamoja na vituo viwili vya mauzo; alizitaja Kanda zilizounganishwa ni pamoja na Dar es Salaam, Moshi, Iringa, Mbeya, Mwanza, Tabora, Dodoma, Mtwara, Muleba, Tanga, Makao Makuu ya Muda Jamana na Ofisi za Keko Mwanga. 

"...Tunasema kwamba Bohari ya Dawa imedhamiria kuokoa maisha ya Watanzania kwa kutumia teknolojia ya Mkongo yenye kasi zaidi, usalama, na gharama nafuu zaidi katika kuhakikisha dawa zenye ubora zinamfikia kila Mtanzania kwa wakati na kupunguza kero ya kusubiri huduma zetu kwa muda mrefu kwani sasa huduma zinapatikana kwa wakati kwa kuwa teknolojia inayotumika ni ya kisasa na yenye ubora wenye kukidhi viwango vinavyohitajika na bohari ya dawa," alisema Mkurugenzi Mkuu, Mwaifwani. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

PHIDESIA MWAKILIMA AIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI WA UBUNGE WA VITI MAALUM KUPITIA TIKETI YA JUMUIYA YA WAZAZI CCM

0
0
http://2.bp.blogspot.com/-RCy23A0BZXU/VXGrU4TGNzI/AAAAAAAAPCU/JU7jwGuH2Mw/s1600/11390351_860026487378599_5734199586013076232_n.jpg
 katika picha ni mwanadada  Phidesia Mwakilima

Na Woinde Shizza,wa libeneke la kaskazini blog
Mkurgenzi wa kampuni ya Phide Intataiment ambaye pia ni meneja masoko wa  kituo cha redio Triple A ya Arusha, Phidesia Mwakilima, ameibuka kidedea kwenye uchaguzi wa mbunge viti maaluimu kupitia jumuia ya wazazi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha.


Phidesia Mwakilima, amepata kura 18 na kuwashinda, Aimbora Nnko, aliyepata kura 6, Angela Mwanri kura 4 na Anna John kura 2 ,uchaguzi huo umefanyika ukumbi wa ccm, mkoa.


Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo katibu wa jumuia ya wazazi mkoa, wa Arusha, Mayasa Kimbau, amewataka wale ambao kura zaohazikutosha kutokukata tamaa bali wajipange kwa chaguzi zingine ndani ya chama.

Akawataka wanawake wasiwe wanyonge kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi bali wawe mstari wa mbele kujitokeza kila uchaguzi utakapotokea

KANALI MSTAAFU ISAAC MWISONGO ALIYEKUWA KAMBI YA LOWASSA AKUBALI KUMUUNGA MKONO DKT MAGUFULI

0
0

DIAMOND PLATNUMZ NA MASANJA WATUA MOSHI KUSHUSHA BURUDANI LEO

0
0
 Mwanamuziki Naseeb Abdul almarufu kama Diamond Platnumz akisalimia warembo baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro International Airport (KIA).



Shindano la Miss Kilimanjaro Ambassador 2015 linafanyika usiku wa leo katika viwanja ya Kili Home Resort kuanzia saa mbili usiku likiambatana na burudani za muziki wa kizazi kipya ambapo wasanii mbalimbali watatumbuiza akiwemo Diamond Platnumz na burudani ya Uchekeshaji kutoka kwa Masanja Mkandamizaji.

Rais Kikwete aongoza Mahafali National Defence College

0
0
mail.google.com
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi na medali ya dhahabu ya mwanafunzi bora katika kozi ya tatu ya National Defence College(NDC) Brigedia Jenerali Aloyce Damian Mwanjile wakati wa mahafali iliyofanyika chuoni huko Kunduchi jijjini Dar es Salaam.
Picha na Freddy Maro
mail.google.com
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange baada ya kutunuku vyeti na zawadi kwenye mahafali ya kozi ya tatu ya National Defence College iliyofanyika Kunduchi jijini Dar es Salaam leo ambapo jumla ya wanafunzi  42 walihitimu masomo yao.
mail.google.comC
Amiri Jeshi Mkuu ,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja n wahitimu wa kozi ya Tatu ya Chuo Cha Ulinzi wa Taifa(National Defence College NDC) Kunduchi jijini Dar es Salaam julai 24, 2015.Aliyeketi Pembeni ya Rais kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange na liyeketi pembeni ya Rais Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Gaudence Salim Milanzi.

Rais Kikwete amfariji Nehemia Mchechu

0
0
k modified
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Marehemu John Edward Mchechu ambaye ni baba wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) Bwana Nehemia Mchechu. Rais Kikwete alikwenda nyumbani kwa Mkurugenzi huyo Mbezi Beach jana kumpa pole kufuatia kifo cha Baba yake aliyekuwa anaugua ugonjwa wa kiharusi.Kulia aliyesimama ni Mtoto wa Marehemu Bwana Nehemia Mchechu.
mail.google.com
Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akiifariji familia ya marehemu John Edward Mchechu Mbezi beach Dar es Salaam jana jioni.aliyeketi wapili kushoto ni mtoto wa Marehemu ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bwana Nehemia Mchechu.(picha na Freddy Maro)
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images