Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 589 | 590 | (Page 591) | 592 | 593 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mkurugenzi wa Taasisi ya kinamama wa Kiafika inayohusika na ugonjwa wa Saratani ya matiti Bi. Ify Nwabuku(kushoto) akizungumza na wakina mama (hawapo picha) wakati wa utoaji wa matibabu bure kwa wakina mama katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar. Kushoto ni Bi Asha Nyang'anyi ambaye ni mwanakamati wa ustawi wa jamii na maendeleo ya kiuchumiwa jumuiya ya Watanzania DMV.

   Wakina mama wakimsikiliza kwa makini Bi. Ify Nwabuku wakati akitoa maelezo juu ya upimaji wa Saratani kwa wakina mama waliofika kupima afya zao katika hospitali ya Mwananyamala zilizokuwa zikitolewa na Jumuiya ya Watanzania DMV pamoja na  washirika wao walioamua kutoa huduma za kitabibu na madawa bure.
   Dk. George Quintero(kushoto) kutoka Marekani akimtibu meno mtoto Living Andrew aliyeshikwa na mama yake huku akisaidiana na Dk. Emilton Ndashau(kulia) wakatia wa utoaji wa uduma bure iliyodhaminiwa na Jumuiya ya Watanzania DMV pamoja na  washirika wao katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar.
   Dk. Somtochukwa Agunwah(kushoto) kutoka Marekani akimtibu mmoja wa mama aliyekuwa anaumwa jino katika hospitali ya Mwananyamala huku akisaidiwa na Dk. Kilechi Nwankwo(kilia) kutoka Marekani pamoja na Dk. Kisumo Armogaston.
   Dk. William Desdery ambaye ni daktari wa macho akimtibu mmoja wa wakina mama waliofika katika hospitali ya Mwananyamala jijini dar kwa ajili ya matibabu yanayotolewa bure na Jumuiya ya Watanzania DMV pamoja na  washirika wao.
  Dk. Sharon Sagoo akipima dawa zilizotolewa na Jumuiya ya Watanzania DMV pamoja na  washirika wao  kwa ajili ya kupewa mgojwa waliokuwa wanaumwa katika hospitali ya Mwananyamala 
   
   Dk. Jummy Amuwo akihakiki madawa
   Hizi ni baadhi ya Dawa zilizotolewa na Jumuiya ya Watanzania DMV pamoja na  washirika wao kwa ajili ya wagonjwa wa Hospitali ya Mwananyamala na pia zinatolewa bure.
  Rais wa Jumuiya ya Jumuiya ya Watanzania DMV, Bw. Iddi Sandaly(kustoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Bi. Adama Gibateh(katikati) pamoja na Kushoto ni Bi Asha Nyang'anyi ambaye ni mwanakamatiwa ustawi wa jamii na maendeleo ya kiuchumiwa jumuiya ya Watanzania DMV.

  0 0

   MKURUGENZI Mkuu wa kwanza wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha Mshomba, akiwasilisha mada wakati wa warsha iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa Wahariri kwenye Hoteli ya Court Yard jijini Dar es Salaam, Julai 22, 2015.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Irine Isaka, akifungua warsha hiyo
   Mhariri Shemax Ngahamera akizungumza kwenye warsha hiyo
   Mhariri wa vipindi wa ITV/Radio One, Steven Chuwa, (kulia), na Mhariri Mtendaji wa EFM, Scolastica Mazula, wakipitia mada zilizokuwa zikitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF
   Mhariri Mshiriki wa gazeti la Nipashe, Ramadhan Mbwaduke, akiuliza swali
   Mhariri gazeti la Serikali, Sunday News, Ichikaeli Maro, akizungumza wakati wa warsha hiyo
   Baadhi ya Wahariri wakinukuu yaliyokuwa yakielezwa kwenye warsha hiyo
   Mhariri Anold Victor, akiuliza swali

   Mhariri mkongwe, Mzee Yasin Sadick, akifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye warsha hiyo
   Baadhi ya Wahariri, wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa juu ya kazi na huduma zitolewazo na WCF
  Mhariri  wa kujitegemea Mzee Wence Mushi akiuliza swali.


  0 0

  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mjini Ndg Juma Fakhi Chum akifungua mkutano wa Kampeni ya Wagombea Ubunge Uwakilishi na Udiwani Jimbo la Kikwajuni Zanzibar katika Tawi la CCM Majumba ya Mjeru kikwajuni. 
  Mwenyekiti wa Mkutano wa Kampeni Mussa Rajab akiongozi mkutano huo wa wagombea katika Tawi la CCM kikwajuni kwa mjeru.
  Wananchi wa kikwajuni wakiwasilikiza wagombea wao wakati wakijinadi katika Tawi la CCM kikwajuni
  Wagombea Uwakilishi na Ubunge wakiwa katika tawi la CCM Kikwajuni wakiwa katika mkutano wa kampeni ya kuwania Ubunge na Uwakilishi wakijinadi kwa Wananchi wa Tawi la Kikwajuni kwa Mjeru
  Wagombea Uwakilishi na Ubunge wakiwa katika tawi la CCM Kikwajuni wakiwa katika mkutano wa kampeni ya kuwania Ubunge na Uwakilishi wakijinadi kwa Wananchi wa Tawi la Kikwajuni kwa Mjeru

  Wagombea Uwakilishi na Ubunge wakiwa katika tawi la CCM Kikwajuni wakiwa katika mkutano wa kampeni ya kuwania Ubunge na Uwakilishi wakijinadi kwa Wananchi wa Tawi la Kikwajuni kwa Mjeru
  Wagombea Uwakilishi na Ubunge wakiwa katika tawi la CCM Kikwajuni wakiwa katika mkutano wa kampeni ya kuwania Ubunge na Uwakilishi wakijinadi kwa Wananchi wa Tawi la Kikwajuni kwa Mjeru
  Wagombea Uwakilishi na Ubunge wakiwa katika tawi la CCM Kikwajuni wakiwa katika mkutano wa kampeni ya kuwania Ubunge na Uwakilishi wakijinadi kwa Wananchi wa Tawi la Kikwajuni kwa Mjeru
  Mgombea Uwakilishi katika Jimbom la Kikwajuni Saleh Ali Abdalla akitangaza sera zake endapo atachaguliwa wakati ukampeni hiyo 
  Mgombea Ubungeb Jimbo la Kikwajuni Ndg Abbulkarim Abrazak Mukrim akijinadi kwa  Wananchi waliofika kuwasikiliza wakati wa kampeni ya kuwania kuchaguliwa kuwakilisha Jimbo hilo 
  Wazee wa Kikwajuni wakifuatilia mkutano wa kampeni ya Wagombea Ubunge na Uwakilishi na Udiwani katika Jimbo la Kikwajuni Zanzibar.
  Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Mahmuod Mohammed Mussa akitetea Kiti chake cha Uwakilishi katika mkutano wa kampeni ya kuwania tena Kiti hicho
  Mwanamke pekee aliyejitokeza kugombea Ubunge katika Jimbo la Kikwajuni Nuru Mohammed Ahmeid akitowa sera zake wakati wa kampeni hiyo kwa wananchi wa Tawi la CCM kikwajuni kwa mjeru. 
  Mgombea Ubunge Ndg Mohammed Ali Ahmeid akitangaza sera kwa mara ya pili kugombea nafasi hiyo uchaguzi uliopita kura zake hazijatosha amejitokeza tena kuomba ridhaa za Wananchi wa Kikkwajuni kugombea nafasi hiyo 
  Kocha Msoma akiwa katika hali ya utulivu akifuatilia sera za Wagombea wa Uwakilishi na Ubunge katika Jimbo la Kikwajuni wakati wa kampeni za kuwania nafasi hiyo uliofanyika katika tawi la CCM Kwamjeru kikwajuni. 
  Aliyekuwa Mwakilishi wa Rahaleo Mhe Nassor Salum Jazira akiwania nafasi ya Uwakilishi Jimbo la Kikwajuni baada jimbo lake kuunganishwa na kikwajuni kuwa Jimbo moja akiomba ridhaa za Wananchi wa kikwajuni kumpa kura.
  Mwananchi wa kikwajuni akimuulizac swali kuhusiana na timu ya kutembe kushindwa kuwalipia faini ya shilingi milioni moja ZFA, Na kujibu timu hiyo yeye ndiyev aliyeipandisha kwa kununua daraja na yeye ni mlezi wa timu za jimbo hilo wakati huo.  
  Mgombea Ubunge Ndg Mussa Shaal Chum akitangaza sera kwa kuwakomboa Vijana na kuwatetea kupata ajira na kuweza kupitisha miswada ya Sheria kwa umakini kutokana na yeye ni mwanasheria akitowa sera hizio wakati wa mkutano wa kampeni. kuwania nafasi hiyo
  Mgombea nafasi ya Uwakilishi katika Jimbo la Kikwajuni Ndg Said Shaban Said, akijinadi katika mkutano huo wa kampeni ya kuwania nafasi hiyo katika jimbo la kikwajuni Zanzibar 
  Mwananchi wa kikwajuni akimuuliza suala kuhusiana na kujipanga vipi kuliongoza jimbo hilo endapo atapata ridhaa za wananchi
  Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Eng Hamad Yussuf Masauni, akimwa sera zake wakati akitetea nafasi yake ya Ubunge wakati wa mkutano wa kampeni katika tawi la CCM Kikwajuni kwa mjeru wakati wa zoezi la kampeni likiendelea katika jimbo hilo. 
  Wazee wa Kikwajuni wakifuatilia mkutano wa kampeni ya Wagombea Ubunge na Uwakilishi na Udiwani katika Jimbo la Kikwajuni Zanzibar.
  Wananchi wakifuatilia kampeni hizo za uchaguzi wa Udiwani Ubunge na Uwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar, uliofanyika katika Tawi la CCM Kikwajuni kwa Mjeru.
  Wagombea wa Ubunge Uwakilishi na Udiwani wakisoma dua na Viomgozi wa mkutano wa kampeni baada ya kumalizika kwa mkutano huo.  Na OthmanMapara.Blog  Zanzinews.Com.

  0 0  0 0

   Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Willibroad Slaa akiwa kwenye gari katika msafara wa mapokezi kwa ajili ya mkutano wa hadhara wa kuwatambulisha Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya waliohamia Chadema wakitokea CCM jana jijini Mwanza.
   Msafara ukiendelea kuelekea uwanjani sasa
  Mbunge wa Jimbo la Kahama, mkoani Shinyanga, James Lembeli (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, John Mnyika, wakiwapungia wananchi mikono walipokuwa kwenye msafara wa mapokezi ya Viongozi Wakuu wa Chama hicho wakiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya mkutano mkubwa wa hadhara.

  0 0


  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji cha Kimataifa (International Trade Centre UN-Agency) inafanya Maandalizi ya Kongamano la Diaspora (Tanzania Diaspora & SMEs Partnership Conference 2015). Kongamano husika litafanyika hapa Dar es Salaam, kuanzia tarehe 13 hadi 15 Agosti 2015 katika Hoteli ya Serena. Kongamano hilo litakuwa la pili kufanyika hapa nchini na litahusisha Diaspora na Wadau wa hapa Tanzania.
   Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Rais na Utawala Bora – Zanzibar na Ofisi ya Waziri Mkuu ndio Wadau Wakuu katika Maandalizi ya Kongamano hili.
  Kongamano la mwaka huu lina Kauli Mbiu, ‘Creating Linkages between Diaspora and Local SMEs in Tanzania’ na Dhumuni lake ni kuhamasisha Ushiriki wa Diaspora katika kukuza Biashara Ndogo na za Kati hapa nchini. Kongamano la mwaka huu pia litahusisha Mikoa ya Tanzania ambapo Mikoa itapata fursa ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Mikoani.
  Kongamano hilo linatarajiwa kufunguliwa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufungwa na Mhe. Dr. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
   Aidha, katika kuhitimisha kilele cha Kongamano hilo, Diaspora wanatarajiwa kufanya ziara Zanzibar tarehe 15 Agosti 2015, ikiwa ni sehemu ya mwaliko maalum kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
   Pamoja na Shughuli za Ufunguzi na Kilele, Matukio muhimu yatakuwa ni Maonesho ya Kibiashara, Majadiliano ya Mada kuhusu Ushirikishwaji wa Diaspora kwa Maendeleo ya Nchi hususan SMEs, uwekezaji Mikoani n.k.
   Kongamano hilo litahudhuriwa na Watanzania Wanaoishi Ughaibuni (Diaspora) na wale waliorejea hapa nchini na Wadau wa Maendeleo kutoka hapa nchini.
   Wizara ya Mambo ya Nje inawakaribisha kushiriki nasi katika Kongamano hilo. Tafadhali tembeleeni tovuti ya (www.tzdiaspora.org)kupata taarifa muhimu hususan kuhusu Ada za Ushiriki, fursa za Kufadhili na namna ya kujisajili.

  Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam

  21 Julai, 2015


  0 0

  Msafara wa Magari na Pikipiki wa mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Mwanga kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi Wakili wa kujitegemea,Youngsevier Msuya ukitoka eneo la Njia Panda kuelekea wilaya ya Mwanga kwa ajili ya zoezi la Urejeshaji wa fomu.
  Msafara wa Mtia nia ,Wakili wa kujitegemea,Msuya ukipita katika maeneo mbalimbali ya mji wa Mwanga wakati mtia nia huyo akirejesha fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Mwanga.
  Mtia nia wa nafasi ya Ubunge jimbo la Mwanga kupitia chama cha NCCR-Mageuzi ,Wakili wa kujitegemea ,Youngsevier Msuya akisalimia wakati msafara wake ukipita katika maeneo mbalimbali ya mji wa Mwanga.
  Mtia nia wa Ubunge,Wakili wa kujitegemea,Msuya akisalimiana na wanachama wa chama cha NCCR-Mageuzi waliofika kumpokea wakati akirejesha fomu za kuwania nafasi hiyo katika jimbo hilo.
  Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi ,Marry Msuya akifanya utamburisho wa wageni waliofika katika kushuhudia urejeshwaji wa fomu hizo.
  Baadhi ya wananchma wa chama cha NCCR -Mageuzi wakiwa ndani ya ukumbi wa ofisi za chama hicho wilayani Mwanga.
  Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi taifa,Hemed Msabaha akitoa salmau kwa wananchama waliofika katika zoezi hilo.
  Baadhi ya wanachama wa chama hicho.
  Mtia nia Msuya akizungumza na wanachma walikokuwa ndabi ya ukumbi wa ofisi za Chama hicho .
  Mke wa mtia nia Msuya,akisalimia ndani ya ukumbi huo mara baada ya kutamburishwa.
  Kutokana na idadi kubwa ya wananchi waliofika katika ofisi hizo kushuhudia zoezi la urejeshwaji wa fomu uliofanywa na mtia nia Msuya ,iliwalazimu wananchi wengine kubaki nje ya ukumbi ambapo mtia nia huyo pia alitoka nje kuwahutubia.
  Baadhi ya wananchi waliofika katika kushuhudia zoezi hilo.
  Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Mwanga kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi ,Wakili wa kujitegemea ,Youngseier Msuya akikabihi fomu kwa Mwenyekiti wa Chama hicho jimbo la Mwanga,Marry Msuya.
  Mtia nia Msuya akiwa katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na wananchi waliofika katika kumsindikiza kurejesha fomu.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Wanafunzi wa Darasa la Saba (Adolph Kolping English Medium Primary School) wametembelea kiwanda cha Kagera Sugar kilichopo Bukoba na kujionea utengenezaji wa Sukari ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao.

  Kiwanda cha Sukari cha Kagera tayari kilishaanza kuzalisha ziada ya sukari inayohitajika katika soko la sukari Nchini hali inayopelekea kuweza kupunguza tatizo la upatikanaji wa sukari Tanzania na Nchi za jirani zinazotumia sukari kutoka kiwandani hapo.

  Kiwanda hicho cha Sukari cha Kagera kiko katika sehemu Kaskazini Magharibi ya Tanzania (karibu na mpaka wa Tanzania na Uganda) kilibinafsishwa na Serikali kwa sekta binafsi mwaka 2001. Malengo ya ubinafsishaji yalikuwa kuboresha upanuzi wa masoko ya ndani na kikanda, uwekezaji wa kisasa, upanuzi na ukarabati na majengo ili kuhakikisha shughuli za kiundeshaji zinaboreshwa.

  Daraja la Mto Kagera.

  Mto wa Kagera ni kati ya mito inayounda mto wa Nile pia ni mto mkubwa kabisa wa kuingia ziwa la Viktoria Nyanza. Inaanza Burundi inapounganika mito ya Nyawarongo na Ruvuvu ikiendela 400 km hadi kuingia ziwa la Victoria Nyanza. 

  Mto wa Kagera ukielekea kaskazini ni mpaka kati ya Tanzania na Rwanda; pale inapogeuka kuelekea mashariki karibu na mji wa Kikagati ni mpaka kati ya Tanzania na Uganda. Sehemu ya mwisho wa njia yake inaingia kabisa ndani ya eneo la Tanzania hadi kufika Viktoria Nyanza kama 40 km kaskazini za Bukoba. Jina la Mto wa Kagera umekuwa pia jina la mbuga ya wanyama ya Akagera National Park huko Rwanda na pia la Mkoa wa Kagera katika Tanzania.
  Wanafunzi wa hao wa darasa la saba walipata nafasi wakapita Darajan hapo na kuweza kujionea taswira kamili ya Daraja hilo. Wengi wa Wanafunzi hao walikuwa hawajawahi kupita hapo. Habari na Picha na Faustine Ruta, Bukoba

  Picha ya pamoja ikapigwa
  Wengi wakafurahia!


  Wanafunzi wakitokelezea pamoja na Mwalimu wao wakati wa safari hiyo

  Wakiingia Eneo la lango kuu la Kiwanda hicho cha Kagera Sugar. Mbele ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo
  Rev. Sr. Merceline Masha. Habari na Picha na Faustine Ruta, Bukoba
  Wanafunzi hao waliongozwa na Walimu wao katika Ziara hiyo
  Mfanyakazi wa Kiwanda cha Kagera Suagar Bw. Moses Mwanga akitoa maelezo kwa Wanafunzi hao juu ya Kiwanda hicho akianzia Historia fupi ya kiwanda tangu kilipoanzishwa na Baba wa Taifa mwaka 1982 hadi kilipobinafsishwa mwaka 2011 na mpaka sasa.Kisomo kikiendelea...Bw. Moses Mwanga akitoa ufafanuzi juu ya aina ya Miwa inayolimwa katika Mashamba yao.
  Miwa ikitolewa Shambani upimwa na kumwagwa eneo hili na kisha uongozwa kwa mashine ndani ya kiwanda.
  Wanafunzi wakijionea hatua ya pili baada ya kukatwa katwa miwa bila kukamliwa na kisha kwenda hatua nyingine.
  Wafunzi wakiendelea kujionea shunghuli mbalimbali ndani ya kiwanda hicho.

  Sehemu ya Jiko
  Wanafunzi wakipata kuonja sukari hiyo inayopatika hapo kiwandani baada ya kujionea tangu Miwa inatoka shambani mpaka uundwaji wake!

  Bw. Moses Mwanga akiwa ndani ya Maabara ya Kiwanda hicho akitoa maelezo kwa Wanafunzi, Habari na Picha na Faustine Ruta, Bukoba
  Mkuu wa Shule Rev. Sr. Merceline Masha akiwaongoza Wanafunzi

  Maji kutoka Mto Kagera ufikia eneo hii na kuchujwa kwa Mitambo na kuwa salama na tayari kwa kutumia kwa shughuli mbalimbali kiwandani hapo.
  Kutenganisha Tope na maji
  Mwisho waliweza kukutana na kuuliza maswali ya hapa na pale na kujibiwa mtaalam Bw. Moses Mwanga.

  0 0

  `Aliekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki mkoani Arusha,Joshua Nassari akizungumza namna alivyotekeleza ahadi zake katika kipindi kilichopita wakati wa mkutano Mkuu wa Jimbo uliofanyika kwenye Mji mdogo wa Usa River ambao  alichaguliwa bila kupingwa ili kupeperusha bendera ya Chadema katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

  Wanachama wa Chadema wakipiga kura za maoni kwaajili ya kumchagua mgombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki katika Mji Mdogo wa Usa River,Joshua Nassari alipata kura 387  na kura 2 za hapana.

  Wanachama wa Chadema wakifurahia jambo katika mkutano huo

  Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini ambaye alikua Mbunge wa Chadema jimbo la Karatu mkoa wa Arusha,Israel Natse(kulia)na Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha,Kalist Lazaro wakimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari(kati)baada ya kutangazwa mshindi.

  0 0

  IMG_7871

  Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mipango ya maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez.
  UMOJA wa Mataifa umetaka vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa kuhakikisha vinatoa taarifa zao kwa usahihi kuhusu maandalizi ya uchaguzi na uchaguzi wenyewe.

  Kauli hiyo imetolewa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa Dar es salaam, kufuatia taarifa iliyochapishwa na jarida moja kwamba UN inataka kujitoa katika kusaidia mandalizi ya uchaguzi nchini Tanzania.

  Aidha alisema kwamba si kweli kuwa Umoja wa Mataifa haujaridhishwa na mwenendo wa maandalizi ya uchaguzi nchini Tanzania na kwamba Umoja huo utaendelea kushirikiana na serikali na vyombo vingine vya uchaguzi kuhakikisha uchaguzi unakwenda vyema.

  Indian Ocean Newsletter ya Julai 10 mwaka huu ilichapisha habari iliyoandikwa na kichwa cha habari “State is facing electoral commissions negligence” na kusema kwamba Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mipango ya maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez, haridhishwi na mwenendo wa maandalizi ya uchaguzi na uchaguzi wenyewe na kutishia kuondoa msaada wa mamilioni unaoratibiwa na UNDP kutoka kwa wahisani mbalimbali.

  Aidha Julai 15, 2015, mtandao wa Jamii Forum ilitafsiri habari hiyo kwa Kiswahili na kuitawanya kwa wasomaji wake.

  Ukweli ulivyo
   
  Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini hajawahi kukutana wala kuzungumza na watu wa Indian Ocean Newsletter .
  Aidha taarifa zilizotolewa na kijarida hicho na tafsiri yake iliyowekwa mtandao wa kijamii wa Jamii Forums hazikujengwa katika ukweli.
  Pia Umoja wa Mataifa utaendelea kufanyakazi na mamlaka za Tanzania na wananchi wake na kuwa Uhusiano kati ya Umoja wa Mataifa na mamlaka za uchaguzi nchini Tanzania na Jumuiya ya kimataifa inayofadhili mradi wa DEP unawasilisha mahusiano muhimu miongoni mwa wadau mbalimbali wanaotaka kuwapo na uchaguzi huru na wa amani.
  Alisema katika makubaliano kuna kamati ya mradi inayojumuisha wadau wote na ina wajibu kuongoza na kutoa mwongozo wa utekelezaji mradi huo kimkakati.
  Maamuzi ya mradi huo hufanywa na kamati hiyo na kamati ya ufundi ya mradi iliyopo Bara na Zanzibar.
  Kutokana na ukweli huo Umoja wa Mataifa unavitaka vyombo vya habari vya kitaifa na Kimataifa kuhakikisha kwamba inatoa taarifa za ukweli na za usahihi kipindi hiki cha maandalizi na uchaguzi wenyewe.
  [caption id="attachment_141105" align="aligncenter" width="595"]Biometric Voter Registration (BVR)  Machines operator, Kheri Mkali attends Rebeca Kimu at Bunju A in Dar es Salaam yesterday during the trial registration. PHOTO|VENANCE NESTORYBiometric Voter Registration (BVR) Machines operator, Kheri Mkali attends Rebeca Kimu at Bunju A in Dar es Salaam yesterday during the trial registration. (LIBRARY PHOTO|VENANCE NESTORY).[/caption]
  Background
  The Democratic Empowerment Project is a three year project launched on the 12th of March 2013 and is directly executed by UNDP with UN Women and UNESCO through a donor basket fund. It follows two previous electoral support projects in Tanzania: the Electoral Assistance Project of 2005 and the Election Support Project of 2010.

   The USD 25m project has four main components, namely, a) supporting legal and institutional reforms; b) support improvement of Electoral Management body’s capacities(NEC and ZEC); c) promote inclusive participation in political and electoral processes, and d) support national peace infrastructures. More specifically, the project has been supporting both NEC and ZEC to improve their institutional capacity both in the context of the conduct of the voter registration process (but not the provision of the BVR kits which is the government’s responsibility) and the preparations for the 2015 general elections. DEP’s support has included technical and advisory services, staff training, voter education and stakeholder engagement. Such stakeholders include the Office of the Registrar of Political Parties, political parties, media, civil society and groups representing women, youth and people with disabilities. So far DEP has supported and implemented most of these activities either directly or via cooperation agreements with the electoral management bodies who execute specific activities directly in line with their mandate.
  Issued by: The Office of the UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative – Mr. Alvaro Rodriguez
  For more information, please contactHoyce Temu-UN Communications Specialist at hoyce.temu@one.un.org or Aine Mushi, UN Coordination Specialist at aine.mushi@one.un.org
  Below is the Indian Newsletter article in French

  0 0
  0 0

   Mkuu wa Wilaya  ya Busega Mkoani Mwanza Bw. Paulo Mzindakaya , akimpa mkono wa shukurani Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB Bw. Waziri Barnabas(kulia), baada ya kukabidhi  madawati 240 yenye thamani ya shilingi milioni .... yaliyotolewa na benki ya NMB ukiwa ni msaada kwa  Shule za Msingi Nyashimo na Nasa Wilayani Busega pamoja na Sukuma na Simakitongo Wilaya ya Magu ili kupunguza uhaba wa madawati katika shule hizo. Kila shule imepata madawati sitini.
   Mkuu wa Wilaya  ya Musoma Mkoani Mara Bw. Zelothe Stephen , akimpa mkono wa shukurani Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB Bw. Waziri Barnabas(kushoto), baada ya kukabidhi  madawati 330 yaliyotolewa na benki ya NMB ukiwa ni msaada kwa  Shule za Msingi Bwai, Kiriba, Chanyahuru na Busumi pamoja na shule ya Sekondari Kiriba zilizopo Musoma vijijini ili kupunguza uhaba wa madawati katika shule hizo. Kila shule imepata madawati hamsini na tano.

  Wanafunzi wa shule ya Msingi ya Kwibara wakiwa wameki kwenye madawati waliyokabidhiwa na NMB.


  0 0

  DSC_0263Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro (kulia) akifafanua jambo kwa wandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wandishi wa habari akielezea kampuni hiyo ilivyoweza kusaidia sanaa kwa Tanzania na Afrika. Kushoto kwake ni CEO wa ZIFF, Prof. Martin Mhando.
  Na Andrew Chale.
  Shirika la ndege la Fastjet limeendelea kupanua wigo wake kwa kuanzisha ‘rout’ zaidi za safari zake ikiwa ni kuunganisha Afrika kuwa moja.

  Kwa mujibu wa Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro anasema kampuni hiyo inatarajia kuizindua rasmi safari zake kwa kwenda, Malawi.
  “Julai 27, Fastjet tutazindua rasmi safari ya kutoka Dar es Salaam-Lilongwe Malawi. Hii inakuwa ni ‘rout’ yetu ya tano katika safari zetu za Kimataifa ndani ya Afrika lengo ni kufikia nchi mbalimbali za Afrika.” Anabainisha Lucy Mbogolo.

  Hata hivyo anabainisha kuwa, wanaendelea kutoa elimu mbalimbali kwa wateja wao juu ya huduma ya Fastjet Ambayo imeendelea kuwa bora zaidi kila kukicha huku akisisitiza kwa wateja kufanya ‘booking’ mapema pamoja na kuzielewa sheria na taratibu za usafirishaji wa anga.

  Awali Fastjet ilianzia na safari za ndani za kusafirisha abiria ‘rout’ za Mwanza – Dar, Kilimanjaro – Dar na Mbeya – Dar sasa hivi wamevuka mipaka zaidi kwa nchi za Afrika zikiwemo, kati ya Dar – Johannesburg, Dar – Lusaka, Dar – Harare,Dar – Entebbe nah ii inayotarajiwa kuzinduliwa wiki ijayo ya Dar-Lilongwe.

  Aidha, Lucy Mbogoro alibainisha kuwa Fastjet itaendelea kusaidia kukuza sekta ya sanaa nchini na Bara la Afrika kwa kuwaunganisha wadau wa sekta hiyo ikiwemo wasanii wa filamu, muziki na sanaa kwa ujumla.

  Lucy Mbogoro anasema hayo ambaapo kwa mwaka huu ni mwaka wa pili mfululizo wakiendelea kudhamini tamasha la Filamu za nchi za majahazi maalufu kama ZIFF. DSC_0311Mwanamuziki wa Kimataifa, Moussa Diallo kutoka Mali (kushoto), akifafanua jambo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wandishi wa habari. Kulia kwake ni Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro ambao wamedhamini tamasha hilo kwa mwaka wa pili mfululizo kwa upande wa usafirishaji.. DSC_0328Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro akizungumza na waandishi wa habarimuda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano huo.. (Picha zote na Andrew Chale, modewjiblog).fastjetmoja ya ndege za Fastjet kama inavyoonekana pichani.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
    JESHI LA POLISI TANZANIA

  “PRESS RELEASE” TAREHE 23.07.2015.

  ·    MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MBARALI.

  ·        JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA POMBE KALI NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU.

  KATIKA TUKIO LA KWANZA:

  MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE KATIKA SHULE YA SEKONDARI MSHIKAMANO ILIYOPO KATIKA WILAYA YA MBARALI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GIDION MPUGI (20) MKAZI WA UHAMBULE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.618 CQH AINA YA MITSUBISHI FUSO ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA FRANK EVARISTO NYOTA (36) MKAZI WA UBARUKU.

  TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 22.07.2015 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAJEN, KATA YA IGURUSI, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA NA UPELELEZI UNAENDELEA.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE VYA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO MVYA MOTO IKIWA NI PAMAOJA NA KUFUATA NA KUZINGATIA SHERIA, ALAMA NA MICHORO YA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


  KATIKA TAARIFA ZA MISAKO:
  JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA MAKUNGURU JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AGATHON SANGA (18) AKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI AINA YA DOUBLE PUNCH KATONI 04, BOSS KATONI 02 NA CHARGER KATONO 01.

  MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 22.07.2015 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO KATIKA MAENEO YA KABWE, KATA YA MAANGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.

  KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LIMEKAMATA VIPODOZI MBALIMBALI VILIVYOPIGWA MARUFUKU NCHINI BAADA YA KUFANYA MSAKO KATIKA NYUMBA MOJA HUKO KATIKA MAENEO YA ITEZI, KATA YA ITEZI, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA  MKOA WA MBEYA.

  KATIKA MSAKO HUO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 22.07.2017 MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI, VIPODOZI AINA YA BUTA SOAP PIECE 50, EXTRA CLAIR PIECE 18 NA CAROLOGHT PIECE 12 VILIKAMATWA BAADA YA MTUHUMIWA KUWAONA POLISI NA KUKIMBIA NA KUVITELEKEZA VIPODOZI HIVYO. MSAKO MKALI UNAENDELEA KUMTAFUTA MTUHUMIWA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA UINGIZAJI/USAMBAZAJI NA UUZAJI WA POMBE KALI NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU NCHINI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

  Imesainiwa:
  [AHMED Z. MSANGI – SACP]
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

  0 0

  Mshereheshaji katika Kongamano la Tamasha la 20 la Utamaduni wa Mzanzibar Otman Mohd (Makombora ), akitoa maelezo mafupi ya kongamano litakavyokuwa katika Ukumbi wa Suza mjini Zanzibar.
   Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Tamasha la 20 la Utamaduni wa Mzanzibar wakisikiliza kwa makini mada inayowasilishwa katika Ukumbi wa Suza mjini Zanzibar.
   Katibu mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar Bimwanahija Ali Juma ambae ni mgeni rasmi akitoa hotuba ya ufunguzi wa Tamasha la 20 la Mzanzibari katika Ukumbi wa Suza mjini Zanzibar.
   Mtoa mada Bimwanahamisi Hamadi akiwasilisha mada ya Athari za Utalii katika kuendeleza  Utamaduni katika Tamasha la 20 la Mzanzibari katika Ukumbi wa Suza mjini Zanzibar.
  Mmoja kati ya washiriki wa Tamasha la 20 la Mzanzibari Abdalla Alawi akichangia mada iliowasilishwa katika Tamasha hilo  katika Ukumbi wa Suza mjini Zanzibar.

  PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0


   Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Rajab Luhwavi akimkaribisha  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  awasalimie wananchi,awashukuru na kujitambulisha kwa wananchi hao waliokuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM Manyoni mkoa wa Singida.
    Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  akiwasalimia wananchi waliokuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM Manyoni mkoa wa Singida. 
    Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli(kulia) akisalimiana na aliyekuwa Mbunge wa Nzega Vijijini Dk. Hamisi Kigwangala
   Hussein Bashe ambaye ametia nia ya kugombea ubunge jimbo la Nzega Mjini akisalimiana na Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli mjini Nzega.
   Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasalimu wakazi wa Nzega kwenye mkutano uliofanyika nje ya ofisi ya CCM wilayani hapo, ambapo aliwaambia Wananchi kuwa amefarijika na mapokezi mazuri na amewaahidi kurudi tena wakati wa kampeni zitakapoanza..
    Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisaini vitabu vya  wageni Ofisi za CCM ndani ya mji wa Manyoni  mkoani Singida alipokuwa akipita kuwashukuru Wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea na kujitambulisha kwao akiwa anatokea jimboni kwake Chato akirejea jijini Dar kwa njia ya barabara.
   Wananchi wa Igunga wakiwa na Bango lao wakimkaribisha Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili maeneno hayo kuwashukuru na kujitambulisha kwao akiwa anatokea jimboni kwake Chato akirejea jijini Dar kwa njia ya barabara.

  Wananchi wa Ikungi wakiwa wamelizunguka gari la Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli na kufunga barabara wakimtaka awasalimie tu ndipo aendelee na safari yake.


  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akitoa hotuba wakati wa kumuaga Balozi wa Ubelgiji ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe. Adam Koeler huku Balozi huyo (wa kwanza kulia waliketi) na wageni waalikwa wakimsikiliza. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Julai, 2015. Katika hotuba yake Balozi Kasyanju alimsifu Balozi Koeler kwa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Ubelgiji.
  Balozi Koeler pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine wakimskiliza Balozi Kasyanju wakati wa hafla fupi ya kumuaga Balozi Koeler.
  Balozi Koeler nae akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga. Katika hotuba yake Balozi huyo aliishukuru Serikali ya Tanzania  kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chote alichokuwepo hapa nchini  na kusifu ukarimu wa Watanzania.


  Balozi Kasyanju kwa pamoja  na Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Congo (DRC), Mhe. Juma Halfan Mpango na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodrigues wakimsikiliza Balozi Koeler (hayupo pichani) akihutubia.

  Balozi Sokoine nae akizungumza machache wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Koeler.

  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bunndala (katikati) akiwa na wageni waalikwa wengine wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini.

  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (katikati) akiwa na Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Mhe. Egon Kochanke (kushoto) pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Felister Rugambwa wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji.

  Balozi wa Ireland hapa nchini, Mhe. Fionnuala Gilsenan (kulia) akiwa na Bw. Rodrigues (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Maulidah Hassan wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji.

  Wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.

  Bi. Kasiga ambaye alikuwa msheheshaji (MC) katika hafla hiyo akiwakaribisha  Mabalozi na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
  Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Kasyanju (kushoto) na Balozi Koeler (kulia) pamoja na wageni waalikwa wakimsikiliza Bi. Kasiga ambaye haonekani pichani.

  Juu na Chini ni Maafisa Mambo ya Nje wakifuatilia matukio kwenye hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji.

  Balozi Koeler akiteta jambo na Balozi Sokoine.

  Balozi Kasyanju, Balozi Koeler na wageni waalikwa wakitakiana afya njema.

  Balozi Koeler akifurahia zawadi ya picha ya kuchora ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro aliyokabidhiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Kasyanju huku akitamka kuwa "nitarudi Tanzania kuja kupanda Mlima Kilimanjaro".

  Balozi Koeler akimshukuru Balozi Kasyanju kwa zawadi hiyo nzuri.
  Picha ya Pamoja.

  0 0

   Waziri Mkuu,Mizengo Pinda  akifafanua jambo kwa kutumia  kompyuta ndogo (Ipad) wakati alipozungumza  na wanafamilia wa Mzee Katinda wa kitongoji cha Tupindo wilayani Mlele akiwa katika mapumziko mafupi nyumbani kwake  Kibaoni, Katavi julai 22, 2015.
   Watoto  wa familia ya  mzee Katinda wa  Kitongoji cha Tupindo wilayani Mlele  wakicheza ngoma ya Kisukuma mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda .   Mheshiiwa Pinda yuko katika mapumziko mafupi kijijini kwake Kibaoni, katavi.
  7027  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana  na  wasichana wa Kisukuma  nyumbani kwa Mzee Katinda kwenye kitongoji cha Tupindo wilayani  Mlele  akiwa  katika mapumziko mafupi  nyumbani kwake Kibaoni, Katavi   Juai 22, 2015.
    Mke wa Waziri Mama Tunu Pinda  akiwaonyesha picha mbalimbali alizopiga vijana wa kabila la Kisukuma aliokutana nao nyumbani kwa Mzee  Katinda katika kitongoji cha Tupindo wilayani Mlele  ambako yeye na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wako katika mapumziko mafupi  kijijini Kibaoni. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  

  0 0
 • 07/23/15--02:43: Article 4
 • HIP-HOP-FESTIVAL


  0 0

   Meneja Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo (kulia), akimkabidhi Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, DCP, Mohamed Mpinga, mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 124, 6. za kudhamini upimaji wa afya za madereva wa masafa marefu nchini na kugharamia mafunzo kwa waendesha Bodaboda 300 wa Mkoa wa Tanga, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama itakayofanyika mkoani Tanga Agosti 3-7 mwaka huu. Kushoto ni Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani, .Hafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam.
   Meneja Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo (kulia), akimkabidhi Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, DCP, Mohamed Mpinga, mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 124.6, za kudhamini upimaji wa afya za madereva wa masafa marefu nchini na kugharamia mafunzo kwa waendesha Bodaboda 300 wa Mkoa wa Tanga, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama itakayofanyika mkoani Tanga Agosti 3-7 mwaka huu. Kushoto ni Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani, Johansen Kahatano.Hafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam.
   Kamanda Mpinga akitoa shukrani kwa TBL kwa udhamini huo. Kulia ni Emma Oriyo wa TBL   Baadhi ya maofisa wa Trafiki wakishuhudia makabidhiano hayo

  Kamanda Mpinga akimshukuru Meneja Mawasiliano na Mambo ya Nje wa TBL, Emma Oriyo kwa udhamini huo wa TBL.

older | 1 | .... | 589 | 590 | (Page 591) | 592 | 593 | .... | 1898 | newer