Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

Zantel yatoa msaada wa kisima cha maji kwa watoto yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania

$
0
0
 Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Evans Tegete akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhiwa kisima kwa ajili ya kituo chake kutoka kwa kampuni ya Zantel. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Paul Makonda akizungumza wakati wa kukabidhi kisima kwa kituo cha Watoto Wetu Tanzania. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Zantel, Pratap Ghose.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizindua kisima cha maji kilichojengwa na kampuni ya simu ya Zantel kwa ajili ya kituo cha Watoto Wetu Tanzania.
 

Kampuni ya simu ya Zantel leo imetoa msaada wa kisima cha maji kwa watoto yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania,ikiwa na lengo la kumaliza tatizo la maji na kuhakikisha  upatikanaji wa maji safi na salama kwa takribani watoto 70 wa kituo hicho.
Tatizo la maji ni moja ya matatizo sugu katika mkoa wa Dar es salaam pamoja na Tanzania kwa ujumla hivyo msaada huu ni wa muhimu kwa watoto wa kituo hicho.
Kisima hicho kilichokabidhiwa leo kitatoa maji safi na salama na yaliyotayari kwa matumizi ambayo yatawasaidia watoto kuepukana na maradhi yanayosababishwa na maambukizi ya maji yasiyo salama na machafu.
Akizungumza wakati wa makadhiano, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Zantel, Pratap Ghose alisema kampuni ya Zantel imekuwa siyo tu ikitoa huduma bora na zenye unafuu kwa wateja wake bali pia imekuwa ikifanya jitihada za kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwenye jamii inayoizunguka

‘Kampuni yetu inalenga kugusa maisha ya wananchi wanaotuzunguka, na ndio maana tumeamua kutoa msaada huu wa kisima ili kiweze kukisaidia kituo hiki kumaliza moja ya matatizo yaliyokuwa yanawakabili kwa muda mrefu’ alisema Pratap.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mheshilmiwa Paul Makonda, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika shughuli ya makabidhiano, aliipongeza kampuni ya Zantel kwa msaada huo akisema ni ishara inayofaa kupongezwa.

‘Ustawi wa watoto na vijana ni jambo muhimu katika jamii, hivyo nakipongeza kituo hiki kwa kazi kubwa wanayofanya, na pia kampuni ya Zantel kwa kulikumbuka kundi hili muhimu katika jamii, na ninatoa wito kwa makampuni mengine kushiriki na kusaidia kituo hiki’ alisema Makonda.

Kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilianzishwa mwaka 2001, kwa lengo la kuhakikisha watoto wasio na wazazi au walezi wanapata matunzo na elimu bora.

Akitoa neno la shukurani Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania,Evance Tegete alisema awali kituo kilikuwa na tatizo kubwa la maji, lakini sasa shukrani kwa Zantel tatizo hilo limemalizika.

‘Awali tulikuwa tunategemea maji kutoka DAWASCO ambayo upatikanaji wake si wa uhakika,tunawashukuru Zantel wameweza kutusaidia kutatua tatizo hili’ alisema Tegete.

Nyalandu akabidhiwa magari 50 na pikipiki maalum 30 kupambana na ujangili

$
0
0

NY1
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Balozi wa China nchini, Lu Youqing, wakikata utepe wakati wa makabidhiano ya msaada wa magari 50 na pikipiki maalumu 30 kwa ajili ya kusaidia vita dhidi ya ujangili. Pembeni ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Adelhelm Meru. Makabidhiano hayo yamefanyika jana katika Makao Makuu ya wizara hiyo mjini Dar es Salaam.
NY2
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Balozi wa China nchini, Lu Youqing, wakikata utepe wakati wa makabidhiano ya msaada wa magari 50 na pikipiki maalumu 30 kwa ajili ya kusaidia vita dhidi ya ujangili. Pembeni ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Adelhelm Meru. Makabidhiano hayo yamefanyika jana katika Makao Makuu ya wizara hiyo mjini Dar es Salaam.
NY3
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Balozi wa China nchini, Lu Youqing, wakijaribu kuendesha pikipiki maalumu zitakazotumika kwenye vita dhidi ya ujangili. Serikali ya China imekabidhi msaada wa magari 50 na pikipiki hizo 30 pamoja na vifaa vingine kutokana na kuridhishwa na jitihada za serikali.
NY4
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Balozi wa China nchini, Lu Youqing na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Adelhelm Meru, wakiwa kwenye picha ya pamoja na askari wa wanyamapori wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo mjini Dar es Salaam, jana.

DKT JOHN POMBE MAGUFULI ATIKISA JIMBONI KWAKE ,WANANCHI WAIBUA SHANGWE KILA KONA YA MJI

$
0
0
  Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga Wananchi wa Chato waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kumaliza kujitambulisha na kuwashukuru kwa kiasi kikubwa kwa kuchaguliwa kwake katika nafasi ya kupeperusha bendera ya chama chake kuwania nafasi ya Urais .
  Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli.
  Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Chato na vitongoji vyake waliokuwa wamekusanyika kwenye kituo cha mabasi wilayani humo wakishangilia kwa  furaha kubwa mara baada ya Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli kujitambulisha kwao.
 Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Chato na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumlaki Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo na shamra shamra za mapokezi kurindima kila kona wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli,huku wengine wakiwa wamebeba mabango kama hivyo pichani.

   Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara),Ndugu Rajab Luhwavi akiwasalimia wanachama wa CCM pamoja na Wananchi waliofika kumlaki Dkt Magufuli jioni ya leo katika kituo cha mabasi cha zamani ndani ya wilaya hiyo.
 Ilikuwa ni shangwe tu jioni ya leo ndani ya Wilaya ya Chato ambako ndiko nyumbani kwa Mbunge na  Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli. 

   Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji  wa Katoro mkoani Geita alipokuwa akipita njiani kuelekea wilayani Chato.Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli mkoani humo wananchi walijitokeza kwa wingi kila baada ya kilometa kadhaa na kuziba barabara wakita kumuona Dkt Magufuli na kumpongeza kwa kuchaguliwa kwake na chama cha CCM.
 Mwananchi akiwa amekumbwa na joto la furaha mara baada ya kumuona Dkt Jonh Magufuli akiwa na msafara mzima wakielekea jimboni kwake Chato mkoani Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh.Magesse Mulongo akiwasalimia wananchi wa Chato jioni ya leo,kabla ya kumkaribisha Dkt John Magufuli aliyewasili mjini humo jioni ya leo akitokea mkoani Mwanza akijitambulisha kwa wananchi na kuwashukuru.
 Dkt Magufuli akizungumza jambo kwa maelfu ya wakazi wa mji wa Chato jioni ya leo
 Dkt Magufuli akifurahia jambo mbele ya umati wa watu,mara baada ya kujitambulisha kwao.
   Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru wakazi wa mji huo kwa kujitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli.

 Maelfu ya Watu walijitokeza kumlaki Dkt Magufuli jioni ya leo mjini Chato

UBUNGE VITI MAALUM VIJANA BUKOBA;ANTU MANDOZA AJITOSA KUCHUKUA FOMU

$
0
0
Mgombea Ubunge Viti Maalum Vijana Bukoba Bi. Antu Mandoza(Kulia) akirejesha Fomu ya Kuomba Ridhaa kuteuliwa kugombea Ubunge wa Viti maalum Vijana Bukoba katika ofisi za umoja huo Mjini Bukoba, ahaidi kuinua Vijana Kiuchumi endapo atapata nafasi ya kuwa Mbunge wa Vijana.(Habari Picha na Faustine Ruta/bukobasports).Mcheza kwao hutunzwa, Vijana wazidi kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi. Binti Antu Mandoza mwenye kuonekana kuwa na umri miaka 22-25 Amerudisha Fomu za kuwania nafasi ya Ubunge Vijana Viti Maalumu kupitia CCM. Kwa Mahojiano mafupi ameongelea jinsi anavyopanga kuinua Maisha ya Vijana kwa kuwatengenezea Fursa na mbinu mbalimbali za kujiajiri pia kuwaonya kutokukubali kutumika vibaya na MAKUNDI ya Kisiasa tunapoelekea Uchaguzi kwani ni wajibu wetu Vijana kuilinda Amani yetu. Mgombea huyo pia amesema kuwa shauku yake kubwa ni kuwatumikia Vijana kwa kutatua changamoto ya Ajira na pia ametoa ahadi ya kushirikiana na Vijana bega kwa bega kuleta maendeleo katika Mkoa wa Kagera.
Binti Antu Mandoza akiweka sawa Kumbukumbu zake katika kitabu mbele ya karani Bi. Jasinta Benedicto wa Umoja wa Vijana Kagera.

Dada Antu Mandoza akiwa kwenye Ofisi za Umoja wa Vijana BukobaMgombea Ubunge Viti Maalum Vijana Bukoba Dada Antu Mandoza (kulia) akiptia Fomu yake ya Kuomba Ridhaa kuteuliwa kugombea Ubunge wa Viti maalum Vijana. Kushoto ni Bi. Jasinta Benedicto karani wa Umoja wa Vijana Kagera.
Mgombea Ubunge viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi dada Antu Mandoza akitoka katika ofisi za umoja wa vijana wa ccm Mkoa wa Kagera baada ya kuchukua fomu

ACACIA YATUMIA MILIONI 400 KUJENGA MAABARA SHINYANGA

$
0
0
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi,Mhandisi Philbert Rweyemamu(kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi Josephine Matiro wakati wa uzinduzuzi wa jengo la Maabara katika shule ya Sekondari Ngokolo lililojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Buzwagi.
Jengo la Maabara lililojengwa kwa ufadhili wa Mgodi wa Kuchimba Dhahabu wa Buzwagi katika shule ya sekondari Ngokolo iliyopo wilani Shinyanga.
Baadhi ya wanafunzi katika shule ya sekondari Ngokolo iliyopo wilayani Shinyanga wakishuhudia uzinduzi rasmi wa vyumba vya Maabara uliojengwa kwa ufadhili wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi ,Maabara itakayotumik kwa ajili ya kujifunzia masomo ya Sayansi.
Add caption
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi,Mhandisi Philbert Rweyemamu akizungumza na waandishi wahabari mara baada ya kukabidhi majengo ya Maabara hizo.
Baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Shinyanga waliojitokeza kushuhudia makabidhiano ya Maabara hizo.
Mkuu wa wilaya Shinyanga Bi Josephine Matiro akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia kukabidhiwa kwa maabara hizo ambazo zimejengwa kwa msaada wa Kampuni ya Kuchimba Dhahabu ya Acacia kupitia Mgodi wa Buzwagi.
Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais na Mbunge wa Shinyanga Mjini Mh. Steven Masele akitoa maneno ya shukurani kwa kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Acacia kwa msaada wa ujenzi wa maabara kwa baadhi ya shule za sekondari katika manispaa ya Shinyanga
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama na kamati za shule zilizonufaika na msaada huo wakifuatilia kwa makini hotuba mbalimbali kutoka kwa viongozi wa wilaya.
Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini wakizungumza na mbunge wa Shinyanga mjini juu ya utekelezwaji wa agizo la Rais Dr Jakaya Kikwete la kuhakikisha kila shule inakuwa na maabara ya sayansi.
Afisa miradi ya maendeleo ya jamii wa mgodi wa Buzwagi Moses Msofe akiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi Josephine Matiro na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais wakati walipokuwa wakikagua miradi hiyo kabla ya kukabidhiwa rasmi.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Philbert Rweyemamu akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi Josephine Matiro jengo la maabara la shule ya Sekondari ya Mazinge ambalo limejengwa kwa ufadhili wa kampuni yaKuchimbaDhahabu ya Acacia. Anayepiga makofi ni mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mh Steven Masele.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini aliyekuwa mkoani Shinyanga.

Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Acacia kupitia mgodi wake wa Buzwagi imetumia zaidi ya shilingi Mil 400 kukamilisha miradi minne ya ujenzi wa vyumba vya maabara katika Shule za sekondari za Mazinge, Kizumbi, Ngokolo na Old Shinyanga zote za Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza wakati wa kukabidhi maabara hizo, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Philbert Rweyemamu amesema, Acacia imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo yote ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya kampuni ya kufanya uchimbaji unaojali na hususani kwa kutekeleza miradi katika maeneo yanayozunguka migodi ya Acacia.
Kukamilika kwa miradi hii kunatajwa kuwa kutasaidia katika kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa wataalamu wa sayansi katika maeneo mbalimbali hapa nchini “Matumaini ya Kampuni ya Acacia ni kuona Tanzania inapata wataalamu wengi katika fani za Sayansi, ambao watasaidia katika maendeleo ya taaluma hii” Alisema Injinia Philbert Rweyemamu.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mjini Bi Josephine Matiro ameupongeza Mgodi wa Buzwagi kwa namna ambavyo umekuwa ukishirikiana na wananchi wa Shinyanga katika kukamilisha miradi mbalimbali. “ Wananchi wetu wengi ni wa kipato cha chini, msaada huu mlioutoa ni mkombozi kwao lakini pia kwa watoto wetu maana mmetutengenezea mazingira mazuri ya watoto wetu kusoma na hapana shaka hawa watabadili hali ya maisha yetu na kuwa mazuri pindi watakapohitimu masomo yao” Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni naibu Waziri ofisi ya makamu ya rais Mh. Steven Maselle amesema uwepo wa wawekezaji hapa nchini umekuwa ni chachu ya maendeleo, kutokana na ushiriki wao katika kutekeleza miradi mbalimbali ambayo imekuwa ya manufaa kwa jamii.
Mbali na utekelezwaji wa ujenzi wa maabara hizi za manispaa ya Shinyanga, katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita  Acacia ilikabidhi pia maabara nyingine kwa Shule ya Sekondari Kinaga katika wilaya ya Kahama ambapo mradi huo uligharimu shilingi milioni mia moja na sitini pamoja na nyumba 3 kwa waathirika wa tukio la mvua za Mwakata zenye thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania milioni mia moja.
Acacia kupitia Mgodi wake wa Buzwagi Pamoja na migodi  mingine ya Bulyanhulu na North Mara itaendelea kushirikiana na jamii zinazotuzunguka katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa  jamii na hasa katika maeneo ya afya, elimu, barabara, maji, pamoja na utoaji wa elimu  ya ujasiliamali kwa vikundi mbalimbali. Injinia Philbert Rweyemamu.
Mwisho.

Harambee ya ujenzi wa Kanisa la KKKT mkoani Rukwa – yafana

$
0
0
1
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akijadiliana jambo na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa (katikati) na Askofu Ambele Mwaipopo wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, wakati wa harambee ya ujenzi wa Kanisa la KKKT mkoani Rukwa. Katika harambee hiyo Nyalandu, aliyekuwa mgeni rasmi alichangia sh. Milioni 100. Harambee hiyo ilifanyika jana usiku katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.
23
ASKOFU Ambele Mwaipopo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, akimkabidhi zawadi mbalimbali zilizotolewa na waumini wa kanisa hilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, wakati wa harambee ya kuchangia kanisa.
4
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, akimkabidhi zawadi maalumu aliyopewa na Papa Francis XIV, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ikiwa ni ishara ya kuthamini mchango wa sh. Milioni 100 alioutoa kuchangia ujenzi wa kanisa mjini Sumbawanga.

8
5
WAUMINI wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), waliohudhuria harambee hiyo wakishangilia kwa furaha baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, kutangaza kuchangia sh. Milioni 100 kusaidia ujenzi wa kanisa jipya la KKKT mjini Sumbawanga.
6
9
7
BAADHI ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), waliohudhuria harambee hiyo wakimsikiliza mgeni rasmi kwenye hafla hiyo, Waziri wa Maliasi na Utalii, Lazaro Nyalandu (hayupo pichani), wakati akihutubia.

HIVI NDIVYO MAGUFULI ALIVYOPOKELEWA KWA KISHINDO JIMBONI KWAKE CHATO

MAMA SALMA AWASILI NAIROBI KUHUDHURIA MKUTANO WA WAKE WA MARAIS WA AFRIKA KUHUSU KANSA YA MATITI,SHINGO YA KIZAZI NA TEZI DUME.

$
0
0
s1
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa binti Esther Wanjiru anayelelewa katika Kituo cha watoto cha Mama Ngina huko Nairobi muda mfupi  baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya tarehe 19.7.2015.  Mama Salma yupo nchini Kenya kuhudhuria Mkutano wa 9 wa wake wa Marais wa Nchi za Afrika unaozungumzia masuala ya kansa Barani Afrika.
s2
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitia saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta huko Narobi tarehe 19.7.2015. Aliyesimama nyuma kulia ni Mheshimiwa Korere Sarah, Mbunge wa Jimbo la Laikipya katika Mkoa wa Rift Valley aliyekuja kumpokea rasmi.
s3
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiambatana na Mheshimiwa Korere Sarah  wakipata mapumziko mafupi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta kabla ya kuelekea hotelini walikopangiwa.
s4
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Ndugu John Haule akisalimiana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati alipowasili kwenye Hoteli ya Intercontinental iliyoko Nairobi tarehe 19.7.2015 kuhudhuria mkutano wa siku tatu wa wake wa Marais wa Afrika utakaozungumzia magonjwa ya kansa ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume.
s5
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Mke wa Rais wa Kenya Mama Margret Kenyatta wakati wa tafrija ya kuwakaribisha kwenye mkutano wa 9 wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika unaozungumzia masuala ya kansa ya matiti, shingo ya kizazi na tezi dume. Tafrija hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Intercontinental jijini Nairobi tarehe 19.7.2015.
s6
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Madame Lordina Draman Mahama, Mke wa Rais wa Ghana wakati wa tafrija ya kuwakaribisha iliyofanyika kwenye Hoteli ya Intercontinental jijini Nairobi tarehe 19.7.2015.
s7
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mke wa Rais wa Niger Dkt. Lalla Malika Issofou Mahammadou wakati wa tafrija ya kuwakaribisha wajumbe wa mkutano wa 9 wa wake wa Marais wa Africa wanaokutana Nairobi kuzungumzia kansa ya matiti, kizazi na tezi dume.
s8
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mke wa Rais wa Namibia Mheshimiwa Monica Geingob wakati wa tafrija kwa wajumbe wa mkutanon wa 9 wa wake wa Marais wa  nchi za Afrika tarehe 19,7.2015.       PICHA NA JOHN LUKUWI

KADA WA CCM ASSENGA ATANGAZA NIA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KILOMBERO

$
0
0
as1
Kada wa CCM Abubakar Assenga akitangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Kilombero, mbele ya ummati wa wananchi waliofurika katika Uwanja wa mpira wa  Asante Afrika, Ifakara katika jimbo hilo mkoani Morogoro, jana. Picha na Bashir Nkoromo.
as2
Mchezaji wa timu ya Lumemo Ashir Mtenge (kushoto), akipambana na Juma Ngulukila wa timu ya Kining’ina, timu hizo zilipomenyana katika mechi ya fainali ya Kombea la Assenga, katikaUwanja wa Asante Afrika, Ifakara katika jimbo la Kilombearo mkoani Morogoro, jana. Lumemo ililala kwa bao 6-0. Picha na Bashir Nkoromo

KALUNDE BAND KATIKA UBORA WAO, WAFANYA KWELI KLABU YA GMB MBEZI

$
0
0
????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa bendi ya Kalunde Deo Mwanambilimbi akiimba wakati bendi hiyo ilipotumbuiza katika klabu ya GMB Mbezi jijini Dar es salaam Maarufu kwa Mbaga katika siku ya pili ya sikukuu ya Idd , kulia ni mwanamuziki Bijuu wa bendi hiyo.
????????????????????????????????????
Wanamuziki wa bendi hiyo wakiimba katika onesho hilo lililofanyika kwenye klabu ya GMB Mbezi jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????????????????????????????????????????
Mwanamuziki Debora Nyangi wa pili kutoka kulia mwimbaji na Meneja wa bendi hiyo akioongoza waimbaji wenzake wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitumbuiza jana kwenye klabu ya GMB Mbezi.

????????????????????????????????????
Mwanamuziki wa bendi hiyo Bijuu akiimba huku wanenguaji wakifanya vitu vyao.
????????????????????????????????????
Mwanamuziki wa bendi ya Kalunde Gringo Junior kushoto akishoo Love na wadau wa bendi hiyo Teddy Mwanambilimbi katikati na Fina Mwanambilimbi kulia.
????????????????????????????????????
Gringo Junior akifanya vitu vyake jukwaani.
????????????????????????????????????
Wangenguaji wa bendi hiyo wakifanya vitu vyao jukwaani.

THE STARS BAND YAZINDULIWA RASMI SIKU YA EID MOSI NDANI YA MZALENDO PUB HUKU IKISINDIKIZWA NA BENDI YA FM ACADEMIA PAMOJA NA BARNABA

$
0
0
Mkurugenzi wa The Stars Band, Aneth Kushaba akijitambulisha kwa mashabiki wakenm  pamoja na azungumza na wapenzi wa bendi mpya ya The Stars Band wakati wa uzinduzi yeye binafsi alisema hawezi kusema yaliyopita bali wapenzi wa bendi hiyo wategemee makubwa kutoka kwenye bendi hiyo iliyozinduliwa siku ya Idd Mosi ndani ya kiota cha Mzalendo Pub
Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Felly Kano akionesha mambo yake kwenye stage hii yote ni wakati anajitambulisha kwa mashabiki wa bendi waliofika kwenye uzinduzi wa bandi hiyo
Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Seghito mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangozi akijitambulisha kwa kuonesha uwezo wake kwenye stage wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo uliofanyika katika kiota cha Mzalendo Pub jijini Dar.
Mwimbaji wa Bongo Flava, Barnaba Elias aka Barnaba akiimba moja ya nyimbo zake huku akisindikizwa na waimbaji wa Bendi ya The Stars kutshoto ni Seghito na kulia ni Prince.
Waimbaji wa Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma' ambao ni  Jesus(wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Patcho Mwamba(wa pili kutoka kushoto),  Pablo Masai (katikati), Mulemule(wa pili kutoka kulia) pamoja na 33 wote wakiimba kwa pamoja wakati wa uzinduzi wa bendi mpya ya The Stars katika kiota cha Mzalendo Pub




Mpiga Drums na pia ndiye meneja wa Bendi, Kibosho akijitambulisha kwa kuone uwezo wake katika Drums
 Mpiga la Gitaa katika Bendi ya The Stars, Othuman Majuto akionesha ujuzi wake kwenye stage wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo
   Mpiga la Gitaa la Base katika Bendi ya The Stars, Zaid Sato (Base) akionesha mambo yake kwenye stage
  Mpiga la Keyboard katika Bendi ya The Stars,  Sebastian akionesha maujaja yake
  Mpiga la Keyboard katika Bendi ya The Stars, Denis akifanya ya kwake
 Mwimbaji wa Bendi ya The Stars,  Alawy Junior akijitambulisha rasmi wakati wa Uzinduzi wa Bendi hiyo Mpya iliyojaa vipaji vya ukweli
Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Prince ambaye aliwavutia walembo wengi kutokana na sauti yake wakati wa kujitambulisha wakati wa uzinduzi wa Bendi hiyo.
Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Mao Santiago akijitambulisha kwa kuimba sebene moja matata ilikuwa ni hatari

Mwimbaji wa Bongo Flava, Barnaba Elias aka Barnaba akiendelea kutoa burudani ndani ya kiota cha Mzalendo Pub wakati wa Uzinduzi wa Bendi mpya ya The Stars iliyozinduliwa siku ya Idd - Mosi
wimbaji wa Bongo Flava, Barnaba Elias aka Barnaba akiimba sambamba na  Mwimbaji wa Bendi ya The Stars,  Alawy Junior wakati wa uzinduzi wa sendi mpya ya The Stars 
Waimbaji wa Bendi ya The Stars wakiimba kwa pamoja wakati wa Uzinduzi wa Bendi hiyo ndani ya Kiota cha Mzalendo Pub, KIjitonyama jijini Dar
Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Seghito  (wa pili kutoka kushoto) akiimba moja ya nyimbo zinazobaba katika dunia hii huku akisindikizwa na waimbaji wenzake amabo ni Felly Kano(wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Bendi, Aneth Kushaba( wa pili kutoka kulia) pamoja na Prince (wa kwanza kulia)
RAIS wa bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma', Nyoshi El Sadat akiimba kwa hisia kali wakati wa uzinduzi wa bendi ya The Stars iliyofanyika kwenye kiota cha Mzalendo Pub siku ya Idd-Mosi
Wakati wa uzinduzi wa Bendi ya The Stars ilikuwa ni funika mbayaaaaa maana  Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma ilifanya ya kwao
Waimbaji wa Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma wakiongozwa na Totoo Kalala(wa kwanza kusoto) pamoja na MP 3 (wa kwanza kuli) wakiendelea kutoa burudani huku wakisindikizwa na waimbaji pamoja na wanenguaji wa bendi hiyo
Ni burudani kwenda mbele
Wanenguaji wa bendi ya  Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma wakiendelea kutoa burudani wakati wa uzinduzi wa bendi mya ya The Stars
Waimbaji wa Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma wakiongozwa Rais wa bendi hiyo, Nyoshi El Sadat wakiendelea kutoa burudani wa wapenzi wa bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma pamoja naThe Stars Bandi
Mwimbaji wa Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma wakiongozwa, Totoo Kalala(wa kwanza kusoto) akiendelea kuimba huku akisindikizwa na wanenguaji wa bendi hiyo
Burudani ikiendelea 
Waimbaji wa Bendi ya The Stars wakendelea kutoa burudani wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo uliofanyika siku ya Idd Mosi katika kiota cha Mzalendo pub
Wakiendelea kucheza kwa furaha wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo
Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Felly Kano(wa pili kutoka kulia) akiimba kwa hisia kali huku akisindikizwa na na waimbaji wenzake ambao ni Mao Santiago(wa kwanza kushoto), Seghito (wa pili kutoka kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Bendi ya The Stars, Aneth Kushaba
Mkurugenzi wa Bendi ya The Stars, Aneth Kushaba(kushoto) akiimba na Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Felly Kano ambao kwa pamoja wameamua kuitumia fursa walioipata kupitia vipaji vyao vya kuimba.
Waimbaji wa Bendi ya The Stars wakiendelea kutoa burudani mbele ya mashabiki wao (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo uliofanyika siku ya Idd Mosi atika kiota cha Mzalendo Pub jijini Dar
Mkurugenzi wa Bendi ya The Stars, Aneth Kushaba(kushoto) akiimba na Mwimbaji mwenzake wa Bendi ya The Stars, Seghito wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo
Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Mao Santiago( wa pili kutoka kushoto) akiendelea kuimba sebene za nguu uku akisindikizwa na waimbaji wenzake ambao ni Seghito(wa kwanza kushoto), Felly Kano (wa pili kutoka kulia) pamoja na Alawy Junior(wa kwanza kulia)
Ndani ya Bendi mpya ya The Stars ni full burudani na sio chenga
The Stars Band wakiendelea kutoa burudani
Mwimbaji wa Bendi ya The Stars,  Alawy Junior(kushoto) akiimba sambamba na Mkurugenzi wa Bendi ya The Stars, Aneth Kushaba(kushoto) wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo uliofanyika siku ya Idd-Mosi katika kiota cha Mzalendo Pub, Kijitonyama jijini Dar
Ndani ya bendi ya The Stars ni full raha hapa waimbaji wa bendi hiyo wakionesha moja ya style yao kwa mashabiki waliofika kwenye uzinduzi huo
Mashabiki wa Bendi ya The Stars wakiendelea kuserebuka na ngoma za bendi hiyo wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo
Waimbaji wa Bendi ya The Stars wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo
Wazee wa kusababisha hara za mziku zinakua poa kutoka katika bendi ya The Stars wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Bendi mpya ya muziki wa dansi ijulikanayo kama The Stars Band iliyo chini ya Aneth Kushaba imezinduliwa rasmi siku Jumamosi ya Julai 18, siku ya Idd-Mosi ndani ya kiota cha Mzalendo Pub, Kijitonyama jijini Dar es Salaam huku ikisindikizwa na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Barnabas pamoja na bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.

MSIGWA APATA RIDHAA YA WANANCHI KUONGOZA MIAKA MITANO MINGINE KITI CHA UBUNGE IRINGA MJINI.

$
0
0
Mhe. Joseph Mbilinyi mbunge wa Mbeya akiunguruma kwenye mkutano huo wa wananchi wa Iringa wa kumpa ridhaa Mbunge wao Mhe. Peter Msigwa kugombea tena kwa miaka 5 katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu.
Mbunge wa Mbeya Mhe. Joseph Mbilinyi (sugu) watatu toka kushoto akiteta jambo na Mhe/ Peter Msigwa Mbunge wa Iringa katika mkutano wa kumpa ridhaa Mbunge Mhe. Peter Msigwa kugombea ubunge kwenye jimbo hilo kwa miaka 5 ijayo kwa tiketi ya chama chake, CHADEMA.
 Msanii wa Bongo Flava Roma Mkatoliki akinogesha mkutano huo.
Mwimbaji wa nyimbo za injili Flora Mbasa akiimba moja ya nyimbo zake kwenye mkutano huo uliofanyika leo Jumapili July 18, 2015 mjini Iringa.

Bongo Star search (BSS) yatoa sita bora jijini Mwanza

$
0
0
Vipindi vya Bongo Star search vimeanza kwenda hewani, na siku ya jana imeruka episode ya kwanza kuonyesha mchujo jinsi ulivyoenda mpaka kubakiwa na Top 6 (pichani) ya washiriki kutoka Mwanza ambayo itajumuika na washindi wa mikoa iliyosalia.

Kipindi kitakuwa kinaruka kila siku ya Jumapili, saa tatu kamili kwenye vituo vya televisheni vya Clouds Tv na Star Tv na marudio yake; Kwa Clouds Tv ni Jumanne saa tano kamili asubuhi pamja na Alhamisi saa nane kamili mchana; Kwa StarTV ni Alhamisi saa tisa na nusu mchana.

MAOFISA WA JWTZ WATEMBELEA KIWANDA CHA TBL DAR

$
0
0
 Maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),walio kwenye mafunzo wakitembelea Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam.
 Meneja Uhusiano wa TBL,Edith Mushi akisalimiana na Mkufunzi wa Kozi ya Eme, Kapteni Erasto Kalinga.
 Maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzaniaa (JWTZ),walio kwenye mafunzo wakitembelea Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam
 Meneja wa Afya na Usalama mahali pa kazi wa TBL, Renatus Nyanda akitoa maelezo kwa maofisa hao jinsi ya kuzingatia usalama watakapotembelea kiwanda hicho.
 Maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),walio kwenye mafunzo wakitembelea Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam
 Maofisa hao wakipata maelezo kuhusu upishi wa bia kiwandani hapo
 Mtaalamu wa Ubora wa Bia wa TBL, Lydia Soi akitoa maelezo kuhusu jinsi wanavyozingatia ubora wa bia zinazotengenezwa kiwandani hapo
 Maofisa wakipata maelezo jinsi bia inavyochachuliwa
 Maofisa wakitembelea kitengo cha ufungashaji wa bia

 Mpishi Mwandamizi wa Bia wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) Dar es Salaam, Elikana Ngosha akiwapatia maelezo Maofisa wa Jeshi walio kwenye mafunzo waliotembelea kiwanda hicho
 Maofisa wakiangalia mitambo kiwandani
Maofisa wa JWTZ na TBL wakiwa katika picha ya pamoja

KALUNDE BAND KATIKA UBORA WAO, WAFANYA KWELI KLABU YA GMB MBEZI

$
0
0
????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa bendi ya Kalunde Deo Mwanambilimbi akiimba wakati bendi hiyo ilipotumbuiza katika klabu ya GMB Mbezi jijini Dar es salaam Maarufu kwa Mbaga katika siku ya pili ya sikukuu ya Idd , kulia ni mwanamuziki Bijuu wa bendi hiyo.
????????????????????????????????????
Wanamuziki wa bendi hiyo wakiimba katika onesho hilo lililofanyika kwenye klabu ya GMB Mbezi jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????



????????????????????????????????????
Mwanamuziki Debora Nyangi wa pili kutoka kulia mwimbaji na Meneja wa bendi hiyo akioongoza waimbaji wenzake wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitumbuiza jana kwenye klabu ya GMB Mbezi.
????????????????????????????????????
Mwanamuziki wa bendi hiyo Bijuu akiimba huku wanenguaji wakifanya vitu vyao.
????????????????????????????????????
Mwanamuziki wa bendi ya Kalunde Gringo Junior kushoto akishoo Love na wadau wa bendi hiyo Teddy Mwanambilimbi katikati na Fina Mwanambilimbi kulia.
????????????????????????????????????
Gringo Junior akifanya vitu vyake jukwaani.
????????????????????????????????????
Wangenguaji wa bendi hiyo wakifanya vitu vyao jukwaani.

UHUSIANO KATI YA UGONJWA WA KISUKARI NA TATIZO LA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME.

$
0
0
Ugonjwa  wa  kisukari  ni  miongoni  mwa  vyanzo  vikuu  vya  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.
Asilimia  kubwa  ya  wagonjwa  wa   kisukari  wanakabiliwa  na  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.

Unajua  ni  kwa  nini  wanaume  wenye  kisukari  wanasumbuliwa  pia  na  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  ?

JIBU  NI  RAHISI  SANA, NALO  NI  KWA  SABABU  KUNA  UHUSIANO  MKUBWA  SANA  KATI  YA  UGONJWA  WA  KISUKARI  NA  TATIZO  LA  UKOSEFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kabla  hatuja  fahamu  kuhusu  uhusiano  uliopo  kati  ya  ugonjwa  wa   Kisukari  na  tatizo   la  ukosefu wa nguvu  za  kiume  ni  vyema  tukafahamu  kwanza   kuhusu  SAYANSI  YA  NGUVU  ZA  KIUME.

Sayansi  ya  nguvu  za  kiume, itatuwezesha  kufahamu  kuhusu  mechanism  ya  nguvu  za  kiume. Itatusaidia  kujibu  maswali  muhimu  kuhusu  nguvu  za  kiume  kama  vile: KITU  GANI  KINAFANYA  UUME  USIMAME ?  KITU  GANI  KINAFANYA  UUME  USISIMAME  ? KITU  GANI  KINAFANYA  UUME  USIMAME  KWA  MUDA  MREFU  ?   KITU  GANI  KINAFANYA  UUME  USISIMAME  KWA  MUDA  MREFU ? KITU  GANI  KINAFANYA  UUME  USIMAME  UKIWA  IMARA  KAMA  MSUMARI  ? KITU GANI  KINAFANYA  UUME  USIMAME  UKIWA  LEGELEGE ?   nakadhalika.
Kufahamu  kuhusu  SAYANSI  YA  NGUVU  ZA  KIUME, tafadhali  tembelea  link  hii  hapa  chini :
http://neemaherbalist.blogspot.com/2015/07/uhusiano-kati-ya-damu-na-tatizo-la.html

Baada  ya  kufahamu  kuhusu  SAYANSI  YA  NGUVU  ZA  KIUME, sasa  tunaweza  kufahamu  kuhusu  UHUSIANO  ULIOPO  KATI  YA  UGONJWA  WA  KISUKARI  NA  TATIZO  LA  UKOSEFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Ukisoma  vizuri  kuhusu  SAYANSI  YA  NGUVU  ZA  KIUME  utagundua  kuwa  SUALA  LA  NGUVU  ZA  KIUME  NI  SUALA  LA  KIMFUMO.
Mambo  makuu   muhimu  katika  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  ni
  • Ubongo  imara  na  wenye  afya  njema
  • Mishipa  imara  ya  kusafirishia  damu   mwilini
  • Mfumo  imara  na  wenye  afya  wa  usafirishaji  damu  mwilini.
  • Mishipa  na  misuli  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema
  • Pamoja  na  uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyo  katika  ubongo  ( nerves),mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  ( spinal  cords )  pamoja  na  mishipa  & misuli  ya  kwenye  uume.
Ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume  ni  lazima   mfumo  wa  mwili  wake  uwe  na  mambo  yote  matano  yaliyo  tajwa  hapo  juu .
Kukosekana   ama  kuwa  na  hitilafu  katika    lolote  kati  ya  mojawapo  kayi   mambo  yaliyo  tajwa  hapo  juu  kutamfanya  mwanaume  huyo  apungukiwe  na  nguvu  za  kiume.
Hitilafu  ama  kukosekana  kwa  zaidi  ya  jambo  moja  kati  ya  mambo  yaliyo  tajwa  hapo  juu, kutamfanya  mhusika  awe  katika  risk  ya  kupungukiwa  nguvu  za  kiume  maradufu.

JINSI  UGONJWA  WA  KISUKARI  UNAVYO  SABABISHA  UKOSEFU  NA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Ugonjwa  wa  kisukari, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, unafanya   mambo  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanadamu:
  • Unashambulia  na  kudhoofisha  mishipa  ya  ubongo.
  • Unashambulia  na  kudhoofisha  mishipa  inayo  safirisha  damu  mwilini  ( Blood  Vessels )
  • Unashambulia  na  kudhoofisha  mishipa  na  misuli mbalimbali  iliyopo  katika  sehemu  mbalimbali  za  mwili  wa  mwanadamu  ikiwemo  mishipa   na  misuli  ya  kwenye  uume.

Mishipa  ya  ubongo  ( nerves ), mishipa  ya  damu  ( Blood  Vessels ), pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume, ni  vitu  muhimu  sana  katika   MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Kudhoofishwa  kwa  vitu  hivi  muhimu, husababisha  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.
Hii  ndio  sababu  kuu  inayo  wafanya  wagonjwa  wa  kisukari  kusumbuliwa  na  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.

TIBA  YA  UKOSEFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME  KWA  MGONJWA  WA  KISUKARI.
Ili  mgonjwa  wa  kisukari  aweze  kupata  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, ni  lazima   apate  pia  tiba   itakayo  saidia  ku- control  sukari  kwenye  damu   yake.
Hivyo  basi ,  tiba  ya  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  inatakiwa  kwenda   sanjari  na  tiba  ya  ku - control  sukari  kwenye  damu  ya  mgonjwa.
Hii  ina  maana  kuwa,   ili  tiba  ya  nguvu  za  kiume  kwa  mgonjwa  wa  kisukari  iweze  kufanya  kazi  barabara, ni  lazima  mgonjwa  huyo, pamoja  na   kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume , apate  pia  tiba  ya  sukari.
TIBA  HII  HAIPONYESHI  TATIZO  LA  KISUKARI, ISIPOKUWA  INASAIDIA  KU –CONTROL  SUKARI KATIKA  DAMU  YA  MGONJWA  NA  HIVYO   KUISAIDIA  TIBA  YA  NGUVU  ZA  KIUME  KUFANYA  KAZI  VIZURI.

Dawa  Ya  Nguvu  Za  Kiume  Kwa  Mgonjwa  Wa  Sukari :  Dawa  asilia  ya  JIKO  ni dawa  ambayo  inasaidia  kutibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la  nguvu  za  kiume  kwa  watu  wote, ikiwemo  wagonjwa  wa  kisukari.  ( WAGONJWA  WA  KISUKARI  NI LAZIMA  WATUMIE  DAWA  YA  JIKO , PAMOJA  NA  DAWA  YA  KU-CONTROL  SUKARI  MWILINI  )
Kufahamu  zaidi  kuhusu  dawa  ya  JIKO  na  namna  inavyo  fanya  kazi. Tafadhali  tembelea :
http://neemaherbalist.blogspot.com/2015/07/uhusiano-kati-ya-damu-na-tatizo-la.html

TIBA   YA   KU-CONTROL  SUKARI  MWILINI
Zipo   dawa  mbalimbali  za  asili  zinazoweza  kutumika , kutibu  tatizo  la  kisukari. Lakini  miongoni  mwa  dawa  hizo, dawa  asilia  zifuatazo  zimethibitika  kuwa  na  uwezo  mkubwa  sana  wa  ku-control   kiwango  cha  sukari  kwenye  damu.
Kufahamu  kuhusu  dawa  asilia  zinazo  saidia  ku-control  kiwango  cha  sukari  mwilini, tafadhali  tembelea :
http://neemaherbalist.blogspot.com/2015/07/jitibu-kisukari-presha-shinikizo-la.html

JINSI  YA  KUPATA  TIBA  YA  NGUVU  ZA  KIUME  KWA  WAGONJWA  WA  KISUKARI.

Kama  wewe   una tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume   unao  tokana  na  ugonjwa  wa  kisukari, unatakiwa  kutumia  DAWA  YA  JIKO  pamoja  na  TIBA  YA ASILI  INAYO  SAIDIA  KU-CONTROL  KIASI  CHA  SUKARI  MWILINI.

Kupata  dawa  hizo  wasiliana  na  duka  la  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC.

Tunapatikana  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  TABATA  MAKOKA  , karibu  na  Shule  ya  Sekondari ya  Mt., Annuarite  .
WASILIANA   NASI   KWA  SIMU   NAMBA   0766  53  83  84.
Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu, tunawapelekea  dawa  mahali  walipo
( DELIVERY )
Kwa  wateja  wa  mikoani, tunawatumia  dawa  kwa  usafiri  wa  mabasi. Kwa  wateja  waliopo  Zanzibar  tunawatumia  dawa  kwa  usafiri  wa  boti  na  kwa  wateja  waliopo  ughaibuni, tunawatumia  dawa  kwa   njia  ya  DHL  au  POSTA.


 www.neemaherbalist.blogspot.com

DC WA KINONDONI, PAUL MAKONDA AZINDUA KISIMA CHA MAJI SAFI KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA WATOTO WETU TANZANIA KILICHOJENGWA NA KAMPUNI YA SIMU YA ZANTEL.

$
0
0
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose (katikati), akimkaribisha  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda wakati akiwasili kwenye hafla ya kuzindua kisima cha maji safi katika Kituo cha Watoto Yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka Dar es Salaam jana.
DC Makonda akisaini katika kitabu cha wageni katika kituo hicho.
Mmoja wa vijana wa kituo hicho akiigiza igizo kuonesha changamoto zinazowakabili watoto waishio katika mazingira hatarishi.
Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Evans Tegete (kulia), akizungumza katika hafla ya kuzindua kisima hicho. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose na  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.


Naibu Mkurugenzi wa Kituo hicho, Theobard Bubelwa (kulia), akiteta jambo na Chief Commerial Officer wa Zantel, Sukwinder Bajwa wakati wa hafla hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Watoto wa kituo hicho na wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Watoto wa kituo hicho wakitoa burudani.
DC Makonda akipokea risasi ya watoto wa kituo hicho.
Vijana wa kituo hicho wakitoa burudani.
DC Makonda akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alitoa ahadi ya kuwasomesha baadhi ya wanafunzi wa kituo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, akifungua pazia wakati akizindua kisima cha maji katika Kituo cha Yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka Dar es Salaam jana. Kisima hicho kimejengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Simu ya Zantel.
DC Makonda akifungua bomba kuashiria uzinduzi wa kisima hicho.
Hapa DC Makonda akimtwisha maji mmoja wa wanafunzi wa kituo hicho baada ya kukizindua.
DC Makonda akimkabidhi kitabu, mtoto Yusla Omari kwenye uzinduzi huo.
DC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na timu nzima ya kituo hicho.


Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Simu ya Zantel jana ilitoa msaada wa kisima cha maji kwa watoto yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania,ikiwa na lengo la kumaliza tatizo la maji na kuhakikisha  upatikanaji wa maji safi na salama kwa takribani watoto 70 wa kituo hicho.
Tatizo la maji ni moja ya matatizo sugu katika mkoa wa Dar es salaam pamoja na Tanzania kwa ujumla hivyo msaada huu ni wa muhimu kwa watoto wa kituo hicho.

Kisima hicho kilichokabidhiwa jana kitatoa maji safi na salama na yaliyotayari kwa matumizi ambayo yatawasaidia watoto kuepukana na maradhi yanayosababishwa na maambukizi ya maji yasiyo salama na machafu.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo , Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zantel, Pratap Ghose alisema kampuni ya Zantel imekuwa siyo tu ikitoa huduma bora na zenye unafuu kwa wateja wake bali pia imekuwa ikifanya jitihada za kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwenye jamii inayoizunguka


‘Kampuni yetu inalenga kugusa maisha ya wananchi wanaotuzunguka, na ndio maana tumeamua kutoa msaada huu wa kisima ili kiweze kukisaidia kituo hiki kumaliza moja ya matatizo yaliyokuwa yanawakabili kwa muda mrefu’ alisema Pratap.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika shughuli ya makabidhiano hayo, aliipongeza kampuni ya Zantel kwa msaada huo akisema ni ishara inayofaa kupongezwa.


‘Ustawi wa watoto na vijana ni jambo muhimu katika jamii, hivyo nakipongeza kituo hiki kwa kazi kubwa wanayofanya, na pia kampuni ya Zantel kwa kulikumbuka kundi hili muhimu katika jamii, na ninatoa wito kwa makampuni mengine kushiriki na kusaidia kituo hiki’ alisema Makonda.


Kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka jijini Dar es Salaam kilianzishwa mwaka 2001, kwa lengo la kuhakikisha watoto wasio na wazazi au walezi wanapata matunzo na elimu bora.


Akitoa neno la shukurani Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania,Evance Tegete alisema awali kituo kilikuwa na tatizo kubwa la maji, lakini sasa shukrani kwa Zantel tatizo hilo limemalizika.



‘Awali tulikuwa tunategemea maji kutoka DAWASCO ambayo upatikanaji wake si wa uhakika,tunawashukuru Zantel wameweza kutusaidia kutatua tatizo hili’ alisema Tegete. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com.

KADA WA CCM ASSENGA ALITAKA JIMBO LA KILOMBERO

$
0
0
 Kada wa CCM, Abbakar Assenga akitangaza nia ya kugombea Ubunge jimbo la Kilombero mkoani Morogoro, mbele ya umati wa wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kining'ina, Ifakara, leo
 Msanii wa muiziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba, akizungumza na umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo wa Kada wa CCM, Abubakari Assenga (kushoto) aliyetangaza nia ya kugombea Ubunge jimbo la Kilombero kwenye mkutano huo
 Ali Kiba akiwapa hi, umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo wa Assenga kutangaza nia ya kuwania ubunge, jimbo la Kilombero mkoani Morogoro,  kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kining'ina, Ifakara, leo baada ya mechi ya fanali ya Kombe la Assenga iliyofanyika kwenye Uwanja wa Asante Afrika, Ifakara
 Mchezaji wa timu ya Lumemo Ashir Mtenge (kushoto), akipambana na mchezaji wa Kining'ina  Juma Ngulukila, timu hizo zilipoemnyana katika mechi ya fainali ya Kombe la Assenga, kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kining'ina, Ifakara mkoani Morogoro leo.  Kining'ina iliibuka bingwa wa kombe hilo baada ya kuicharaza Lumemo mabao 6-0 katika mechi hiyo.


 Mchezaji wa timu ya Lumemo Ashir Mtenge (kushoto), akipambana na mchezaji wa Kining'ina  Juma Ngulukila, timu hizo zilipoemnyana katika mechi ya fainali ya Kombe la Assenga, kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kining'ina, Ifakara mkoani Morogoro leo.  Kining'ina iliibuka bingwa wa kombe hilo baada ya kuicharaza Lumemo mabao 6-0 katika mechi hiyo.
 Wachezaji wa Kining'ina wakishangilia bao la tano dhidi ya Lumemo wakati wa mechi hiyo

 Msanii wa muziki, Ali Kiba, akifuatilia mechi ya Lumemo na Kining'ina ya fainali ya Assenga Cup kwenye Uwanja wa shule ya Msingi Kining'ina, Ifakara, mkoani Morogoro, mwishoni mwa mechi hiyo, kada wa CCM, Aboubakar Assenga alitangaza nia kuwania Ubunge jimbo la Kilombero
 Ali Kiba na Assenga wakiwa kwenye mechi hiyo
 Mashabiki wakiwa kwenye mechi hiyo ya fainali ya ssenga Cup, kenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kining'ina, Ifakara mkoani Morogoro.
 Wachezaji wa timu ya Kining'ina wakijinasibu baada ya kuibuka mabingwa wa Assenga CUP kwenye mechi hiyo
Wananchi wakishangilia wakati Kada wa CCM, Aboubakar Assenga alipokuwa akitangaza nia kuwania Ubunge jimbo la Kilombero katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Kining'ina, Ifakara.
 Ali Kiba akimpa zawadi mchezaji bora katika mechi hiyo
Aboubakar Assenga akikabidhi zawadi ya pea moja ya jenzi, alipogawa jozi moja ya jezi kwa timu zote zilizoshiriki michuano ya Assenga Cup
Ali Kiba akitoa zawadi  kwa nahodha wa timu ya Lumamo Cup, Hamza Ali baada ya timu hiyi kuibuka mshindi wa pili katika fainali za kombe la Assenga.
Ali Kiba akikabidhi zawadi ya kitita cha fedha kwa nahodha wa timu ya Kining'ina, Mohammed Abeid, baada ya timu hiyo kuibuka bigwa wa michuano ya Assenga, baada ya tmu hiyo kuizaba mabao 6-0 timu ya Lumamo katika mechi ya fainali kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kining'ina, Ifakara. Kushoto ni Kada wa CCM Aboubakar Assenga ambaye baadaye alitangaza nia kuwania ubunge jimbo la Kilombero
Msanii Ali Kiba akiwasili kwenye Uwanja wa Michezo, kumpiga tafu Kada wa CCM, Abubakari Assenga, ambaye alikuwa akitangaza nia kuwania Ubunge jimbo la Kilombero, katika mkutano uliofanyika Mang'ula mkoani Morogoro.
Msanii Alikiba akinena na wananchi alipompa tafu, Kada wa CCM, Abubakari Assenga, ambaye alikuwa akitangaza nia kuwania Ubunge jimbo la Kilombero, katika mkutano uliofanyika Mang'ula mkoani Morogoro.
Baadhi ya wadau wakiwa kwenye mkutano huo, kushoto ni Zainabu Bakari kutoka Umoja wa Vijana wa CCM.
Mtoto na karanga zake akiwa kwenye mkutano huo
Alikiba akiwasha moto kwa kuwashindanisha vijana kucheza muiziki wake kwenye mkutano huo
Baada ya kunogewa, Ali Kiba akaamua na yeye kusakata muziki na vijana hao aliokuwa akiwashindanisha.
Mama akishangilia kwa nguvu zake zote, Kada wa CCM, Abubakar Assenga alipokuwa akitangaza nia kuuwania ubunge jimbo la Kilombero katika mkutano huo uliofanyika Mang'ula.
Vijana wakiwa wamepanda kwenye mti kuhakikisha wanamuona Assenga wakati akitangaza nia kwenye mkutano huo
Assenga aakiwasalimia wananchi alipowasili katika mkutano wke wa kutangaza nia ya kugombea ubunge, uliofanyika Mang'ula
Kada wa CCM, Abubakar Assenga akiwahutubia wananchi alipotanagaza nia kuwania ubunge jimbo la Kilombero, katika mkutano uliofurika wananchi hao katika eneo la Mang'ula
Assenga akishauriana jamabo na Mweneyekiti wa CCM
Assenga akishauriana jambo na Kijana wa CCM Zainabu bakari
Abubakari Assenga, ambaye alikuwa akitangaza nia kuwania Ubunge jimbo la Kilombero, akiwa na Ali Kiba jukwaani mwishoni mwa mkutano huo uliofanyika Mang'ula mkoani Morogoro. 
PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO, KILOMBERO

BALOZI SEIF AFUNGUA MKUTANO KWA NIABA YA RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN, WA KUIMARISHA MASUALA YA USHIRIKIANO KATIKA AMANIUSALAMA NA MAENDELEO KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI UNAOFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
Vijana wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa ufunguzi wa mkutano huo kulia  Ali Hamad Suleiman na Rukaiya Rashid Kombo. uliofanyika katika ukumbi wac hoteli ya Zanzibar Beach Resorty Mazizini Zanzibar na kufunguliwa na Balozi Ali Ali Iddi kwa niaba ra Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, 
Viongozi wa meza kuu wakisimama wakati wa kuimbwa kwa wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa mkutano huo uliowashirikisha Marais Wastaaf, Viongozi wa Dini na Vijana kutona Nchi za Afrika Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resorty Mazizini Zanzibar.
Viongozi wa Dini wakisimama wakati wa kuimbwa kwa wimbo wa Taifa wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Saleh Omar Kabi akisoma Dua wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.


Kiongozi wa Dini ya Kikristo akiuombea Mkutano huo wakati wa ufunguzi wake katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifungua Mkutano huo wa Kuimarisha Masuala ya Ushirikiano katika Amani Usalama na Maendeleo kwa Nchi za Afrika Mashariki kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, uliowashirikisha Marais Wastaaf Viongozi wa Dini na Vijana uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk Amani Karume mwenyeji wa Mkutano huo wa Kuimarisha Masuala ya Ushirikiano katika Amani Usalama na Maendeleo kwa Nchi za Afrika Mashariki, akizungumza wakati wa ufunguzi katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resorty Mazizini Zanzibar, uliowashirikisha Marais Wastaaf, Viongozi wa Dini na Vijana. 
Waziri Mkuu Mstaaf wa Kenya Mhe Raila Omolo Odinga akihutubiwa mkutano huo wakati wa ufunguzi wake katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar 
Rais Mstaaf wa Zambia Mhe Rupia Banda akihutubia mkutano huo wakati wa ufunguzi wake uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, ulifunguliwa na Balozi Seif Ali Iddi kwa Niaba yake.
                 Viongozi washiriki waalikwa wa Mkutano huo wakifuatilia hutuba ya ufunguzi.
Washiriki wa mkutano huo wakifuatili ufunguzi wa mkutano huo katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort mazizini Zanzibar.












OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAENDESHA MAFUNZO YA UTAFITI WA AFYA YA UZAZI NA MTOTO NA MALARIA TANZANIA, 2015 MOSHI, KILIMANJARO.

$
0
0
Na: Veronica Kazimoto, MOSHI
AFYA ya Uzazi na Mtoto ni viashiria vizuri vinavyoonyesha maendeleo ya uchumi na kijamii na vinaainishwa na utoaji endelevu wa huduma za afya nchini.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Kinga, Dkt. Neema Rusibamayila kutoka Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii wakati akifungua rasmi mafunzo ya Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 yaliyofanyika Moshi, mkoani Kilimanjaro.

"Kutokana na umuhimu wa viashiria hivyo, Serikali kupitia Mpango wake wa Afya ya Uzazi na Mtoto imefanya juhudi za ziada katika kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na matatizo ya uzazi na vifo vya watoto wachanga nchini", Amesema Dkt. Rusibamayila.

Dkt. Rusibamayila amesema kuwa vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi vimeendelea kupungua ambapo kwa mwaka 2012 kulikuwa na vifo 432 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa hai ikilinganishwa na vifo 454 kwa kila watoto waliozaliwa hai 100,000 iliyopatikana kwenye Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa mwaka 2010.

Vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka vifo 51 kati ya watoto 1,000 waliozaliwa hai kama ilivyopatikana kutoka kwenye Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa mwaka 2010na kufikia vifo 45 kati ya watoto 1,000 waliozaliwa hai kwa mwaka 2012.

Aidha, Dkt. Rusibamayila ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mafunzo hayo amewaasa washiriki hao kufanya kazi yao kwa weledi ili kuhakikisha kuwa Serikali inapata takwimu sahihi za  Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015 kwa ajili ya kupanga maendeleo.

Pamoja na ufunguzi wa mafunzo hayo, Mgeni rasmi huyo amezindua matokeo muhimu ya Utafiti wa Tathmini ya Utoaji wa Huduma ya Afya Nchini wa mwaka 2014/2015.

Matokeo ya utafiti huo yanaonyesha kuwa, vituo saba (07)kati ya kumi (10)vinatoa huduma zote za msingi za afya yaani tiba kwa watoto, chanjo pamoja na ufuatiliaji wa mwenendo wa ukuaji wa mtoto.

Aidha, huduma za matibabu kwa watoto wagonjwa zinapatikana kwa asilimia 98   katika vituo vyote vinavyotoa huduma za afya Nchini, pia zaidi ya vituo vinane (8) kati ya kumi (10)nchini vinatoa huduma za chanjo kwa watoto.

Kwa huduma za kisasa za uzazi wa mpango zinapatikana kwa asilimia 80 ya vituo vyote vinavyotoa huduma za afya, ikilinganishwa na asilimia 76 kwa utafiti wa namna hii wa mwaka 2006.

Aidha,  kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2014/2015 karibu vituo vyote vya Serikali (sawa na asilimia 97) vinatoa huduma za uzazi wa mpango ikilinganishwa na asilimia 35 ya vituo binafsi vya kibiashara na asilimia 41 ya vituo vinavyomilikiwa na asasi za kidini.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ephraim Kwesigabo amesema utafiti huu wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015  unalenga kukusanya taarifa nyingi za sekta ya afya zinazotumika katika kutathmini malengo mbalimbali na pia kusaidia katika kupanga mikakati mipya.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa mara nyingine tena inafanya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015 ambao kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2010. Utafiti huu utaanza rasmi mwishoni mwa mwezi Agosti, 2015 kwa nchi nzima yaani Tanzania Bara na Visiwani.

 Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kinga, Dkt. Neema Rusibamayila kutoka Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii akiwahutubia washiriki wa mafunzo ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 yaliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
 Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu akitoa maelezo ya awali wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 yaliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 yaliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.


 Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kinga, Dkt. Neema Rusibamayila kutoka Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii akizindua matokeo muhimu ya Utafiti wa Tathmini ya Utoaji wa Huduma ya Afya Nchini wa mwaka 2014/2015 wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 yaliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.



 Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kinga, Dkt. Neema Rusibamayila kutoka Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii akionyesha kijitabu cha matokeo muhimu ya Utafiti wa Tathmini ya Utoaji wa Huduma ya Afya Nchini wa mwaka 2014/2015 wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 yaliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images