Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

MAOFISA WA JESHI LA RWANDA,GHANA WATEMBELEA TBL DAR

$
0
0
 Mpishi wa Bia wa kampuni hiyo, Kelvin Nkya, akiwapatia maelezo maofisa wa majeshi ya Rwanda na Ghana, kuhusu idara mbalimbali za uzalishaji walipotembelea kiwanda cha bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam hivi karibuni. Maofisa hao waliongozwa na maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo akiwapatia maelezo ya awali maofisa hao wa kijeshi kutoka nchi hizo mbili.
 Maofisa wakiwa idara ya upishi wakipata maelezo ya jinsi bia inavyopikwa kisasa kwa kutumia kompyuta
 Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Orio (kushoto) akisalimiana na maofisa wa jeshi la Rwanda na Ghana waliofika kutembelea utendaji wa kampuni hiyo, Dar es Salaam hivi karibuni.
 Mpishi wa Bia wa TBL, Kelvin Nkya akiwapatia maelezo maofisa hao namna bia inavyopikwa kwa kutumia kompyuta.
 Maofisa hao wakiangalia kwenye kompyuta jinsi bia inavyopikwa
 Baadhi ya maofisa wakijaza majina yao kwenye kitabu cha wageni TBL
 Brigedia Jenerali  Jean Jacques Mupenzi kutoka Jeshi la Rwanda, akimkabidhi zawadi Meneja wa Kiwanda cha Bia cha TBL Dar es Salaam, Calvin Martine baada ya kutembelea kiwanda hicho.
 Baadhi ya maofisa wakitembelea kiwanda hicho, idara ya packaging
 Meneja wa Kiwanda cha TBL Dar es Salaam, Calvin Martine akimpatia zawadi Brigedia Jenerali  Jean Jacques Mupenzi kutoka Jeshi la Rwanda

 Maofisa wakipata maelezo katika idara ya uchachuaji bia
Maofisa hao wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa TBL baada ya kumalizika kwa ziara hiyo.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA

Mwenjuma Magalu: TAMWA imerejesha ndoto zangu kielimu

$
0
0


Mwanafunzi, Mwenjuma Magalu.

Bibi Amina Mohamed mlezi wafamilia ya mwanafunzi Mwenjuma Magalu akifanya mahojiano na mwanahabari Joachim Mushi, kijijini Msasa,wilayani Handeni
========  ========  ===
Na Thehabari.com, Handeni

“BAADA ya kumaliza darasa la saba nilichaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari, lakini sikufanikiwa kuendelea na elimu hiyo kutokana na uwezo wa mzazi wangu mmoja (mama) ambaye alishindwa kumudu gharama zilizokuwa zikihitajika kwa wakati…,”ndivyo anavyoanza kusimulia Mwenjuma Magalu akizungumza Kijijini Msasa, Wilaya ya Handeni.

Magalu anasema furaha zote alizokuwa nazo mwaka 2011 baada ya kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Komnyang’anyo, iliyopo kijijini Msasa Wilaya ya Handeni zilikuwa zikiyeyuka kadri siku zilivyokuwa zikikaribia kufunguliwa kwa shule za sekondari.

Anasema hadi shule zinafunguliwa mama yake alikuwa hajakamilisha vitu vilivyokuwa vikihitajika shuleni ikiwa ni pamoja na fedha ya ada ya kuanzia shule. Kijana huyo ambaye alikuwa akiishi na mama yake pamoja na wadogo zake wawili walitelekezwa na babayao miaka kadhaa iliyopita kijijini hapo baada ya baba huyo kudai anakwenda kutafuta maisha nje ya kijiji chake.

 Hata hivyo kwa kuonesha ana uchu na elimu kijana Magalu hakumuachia mamayake jukumu la kuitafuta ada peke yake, naye alifanya vibarua huku na kule kijijini Msasa kwa kuamini huenda angelipata kitu na kufanikiwa kuingia shuleni. Lakini ilishindikana kwake kutokana na uduni wa kipato kwa mamayake, kwani fedha ambayo mara nyingine Magalu aliipata kwenye vibarua ililazimika kununua chakula. Hii ilikuwa ni changamoto nyingine kwa familia ya kijana huyo mdogo.

Baada ya ndoto za kujiunga na shule kutoweka bila mafanikio, Magalu aliamua kufanya vibarua na kampuni ya Kichina iliyokuwa ikitengeneza barabara ipitayo karibu na kijijini chao. Magalu anasema ndoto yake ya shule ilikuja kurejeshwa na utafiti wa kihabari uliofanywa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Machi 2012 kwa kushirikiana na waandishi wa habari.

“Baada ya kufanya mahojiano na mwandishi wa habari aliyekuja kijijini kwetu Msasa na kumweleza hali halisi, kilio change kilisikika kwawasamaria na kujitokeza kuisaidia familia yetu…kwa sasa nimepata ufadhili wa kusomeshwa hadi kidato cha nne,” anasema Magalu.

Mwenjuma Magalu ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Komnyang’anyo muda mfupi baada ya kupata ufadhili wa masomo akiwa bado na furaha alijikuta anaingia katika mtihani mwingine wa maisha baada ya mamayake mzazi kufariki dunia.


Hata hivyo baada ya utafiti wa kihabari kufanyika kijijini Msasa Wilaya ya Handeni na taarifa za mtoto huyo kushindwa kujiunga na elimu ya sekondari kwa kile mamayake (kwa sasa marehemu) kutokuwa na uwezo kuripotiwa, alijitokeza mfadhili wa kugharamia masomo yake ambaye hadi sasa anafanya hivyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi akiwa shuleni Komnyang’anyo, mwanafunzi huyo aliishukuru TAMWA kwa kuibua tatizo la familia yao kwa umma na kupatikana kwa mfadhili ambaye amemrudisha masomoni licha ya familia yao kutelekezwa.

Kwa upande wake bibi wa mtoto huyo (Amina Mohamed) ambaye aliachiwa familia hiyo baada ya kufariki kwa mwanaye, anamshukuru mfadhili wa mjukuu wake. “Binafsi nawashukuru sana hao (TAMWA) waliopaza sauti hadi mjuu wangu kurudi shuleni…hii kwetu ilikuwa ni ndoto kwetu maana mtoto mwenyewe alikuwa amekata tamaa kabisa kurudi shuleni na alikuwa kaanza kufanya vibarua mitaani huku wenzake wakiendelea na shule,” anasema bibi huyo. Bibi huyo anafafanua kuwa kwa sasa bado familia hiyo inahitaji msaada wa huduma hasa baada ya mwanaye (mama wa familia hiyo) kufariki dunia mwaka jana na kumuachia watoto wake.

Anasema yeye ndiye aliyebaki kulea familia hiyo baada ya mtoto wake kufariki. Lakini kwa sasa hali ya afya yake si nzuri, licha ya uzee alionao amepimwa na kubainika ni mgonjwa wa TB ambapo ameanza kutumia dawa hivyo kwa hali yake ameshauriwa kupumzika.

Anasema baada ya kushauriwa na daktari kupumzika, mzigo wa malezi ya familia sasa umejikuta ukielekea kwa mjukuu wake Mwenjuma ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Komnyang’anyo.  Kwa mujibu wa maelezo aliyoyatoa katika uchunguzi uliofanywa tena juzi na mwandishi wa makala haya bibi huyo anabainisha kuwa mjukuu wake anamzigo mkubwa.

“Nasema anamzigo mkubwa kwa kuwa sasa anatakiwa kutekeleza majukumu ya shule na nyumbani kama yeye ndiye mlezi wa familia…namuhurumia sana lakini sina cha kufanya. Anaporudi shuleni anatakiwa kutafuta chakula cha familia, yeye pia ndiye mpishi, mchota maji na ndiye mkulima,” anamzigo mzito kweli ndiyo maana wakati mwingine nalazimika kuingilia licha ya afya yangu.

Muhingo Rweyemamu ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, anasema tatizo la uduni wa maisha kwa familia katika wilaya hiyo lipo kwa kiasi kikubwa. Anabainisha kuwa kwa sasa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni haina mfumo maalumu kwa ajili ya kusaidia moja kwa moja familia kama hizo.

Anasema kinachofanyika ni kuhamasisha ndugu, jamaa na marafiki kuendelea kutoa msaada kwa familia ambazo zimekuwa katika wakati mgumu kimaisha na kuitaji msaada. “Kwa ujumla tunatoa elimu ya kuhakikisha wazazi wanazaa watoto ambao wanaweza kuwamudu kimatunzo…wajua wakati mwingine umasikini katika familia hizi huchangiwa na wanaume kuzaa bila mpangilio, unakuta mwanaume anakuwa na familia zaidi ya moja wakati hana kipato cha kumudu familia hizo,” anasema Rweyemamu.

Anasema kwa kuwa hili limesha jitokeza wamejipanga kuziwezesha shule kufanya uzalishaji wa kilimo ili wanafunzi waanze kupata chochote wawapo shuleni, halmashauri imepata vocha takribani 300 ambazo zitasaidia upatikanaji wa pembejeo kwa shule zitakazokuwa zikizalisha mazao kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi kama chakula wawapo shuleni mchana.

Halmashauri pia imejipanga katika uhamasishaji kilimo kwa familia pamoja na uwezeshaji katika nyanja anuai ili kukabiliana na janga la njaa pamoja na ugumu wa maisha kiujumla.

Diamond aitikisa bukoba,apokelewa kama mfalme.!

$
0
0

Pichani ni baadhi ya wakazi wa mji wa Bukoba wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumlaki nyota wa muziki wa kizazi kipya kwa sasa (bongofleva),hapa nchini,Nassib Abdul a.k.a Diamond mara alipokuwa akiwasili mkoani humo kwa maonesho yake kadhaa ambayo yalifana na kupokelewa vyema.Picha zaidi bofya hapa

hongera kwa mdau mwenzetu dinah marios

Msami; Mwalimu wa kucheza kutoka THT aliyewapa ubingwa madansa wa Marekani

$
0
0


Ukizungumzia makundi yanayofanya vizuri kwenye uchezaji wa muziki hapa nchini, huwezi kuacha kuwataja THT. Pamoja na kuwa ndio walioleta mageuzi kwenye tasnia ya kucheza miziki hapa nchini, hasa kwa kuchanganya miziki ya asili na ya kizazi kipya, kituo hicho bado kimeendelea kuzalisha wachezaji wengi wa miziki hapa nchini.


Kikiwa ni kituo maarufu kwa kuzalisha vipaji vya kuimba pia,THT inaaminika kuwa kituo kikubwa kabisa cha sanaa ya burudani chenye mafanikio makubwa hapa nchini.  Wakati historia ya wacheza muziki hapa nchini ina chimbuko la muda mrefu, kwa THT,Msami Giovani, ndie mtu ambaye anatajwa sana katika kusaidia mafanikio ya kituo hicho.

Msami, ambaye alijiunga kituoni hapo kama mchezaji, lakini kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha katika kucheza ndipo alipochaguliwa kufundisha wenzake. Toka wakati huo hajawahi kurudi nyuma, na ameendelea kujijengea jina kwa kuwaandalia wanamuziki wengi wa hapa nchini mtiririko wa show zao.

Msami ambaye ana umri wa miaka 24, anasema alianza kupenda kucheza akiwa na umri mdogo na alivutiwa na Michael Jackson pamoja na miziki ya kikongo. Msami ameshiriki mashindano ya kucheza mashindano mengi hapa nchini kama Cheza Tanzania, Dance La Fiesta, Malta Guiness Street Dance na Mkali wa Temeke.

Zaidi ya kushiriki kwenye kucheza Msami pia ameshiriki kuandaa mtiririko, au choreagraphing kwa kiingereza, ya matamasha makubwa hapa nchini kama FIESTA, KILLI MUSIC AWARDS, MISS TANZANIA, VISA2DANCE, na mengine mengi.  Kwa mwaka huu umeanza kwa hatua nyingine kubwa katika maisha yake ya kazi na sanaa. Msami alipata fursa ya kipekee kwa kwenda Marekani kufundisha kundi la madansa ambao wanaruka na kamba na kucheza pia, ikifahamika kama Fusion kwa kiingereza.

Kundi hilo alilofundisha Marekani kwa wiki tatu, limeshinda ubingwa wa dunia katika kipengele cha kucheza na kuruka kamba. Akizungumzia mafaniko hayo makubwa, Msami alisema anamshukuru Mungu kwani hayo ni mafanikio makubwa kwa mtanzania wa kawaida kufundisha madansa Marekani, lakini pia kuweza kuwapa ubingwa wa dunia.

‘Kujituma na kujifunza kila siku ndio msingi mkubwa wa mafanikio yangu, kwani toka nilipoanza kucheza niliamini nitafika mbali katika sanaa hii’ anasema Msami. Kundi hilo alilolifundisha Msami, la Hot Dog USA, linadhaminiwa na kampuni ya One World, One Rope ambao walishawahi kuja hapa nchini miaka mitatu iliyopita kuendesha kambi ya kuruka kamba kwa ajili ya Watanzania.

Msami anasema akiwa Marekani alipata fursa ya kufundisha makundi kumi tofauti ya muziki lakini mkazo ukiwa kundi la Hot Dog USA. Akizungumzia mipango yake, Msami anasema ana mpango wa kuandaa kikundi cha wacheza muziki na kuruka kamba hapa nchini ili kikashiriki mashindano ya dunia hapo baadaye.

‘Unajua Fusion, yaani kucheza na kuruka kamba sio mchezo maarufu hapa nchini, hivyo kwa kushirikiana na wadau nina mpango wa kuufikisha mbali’ anasema Msami.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA SIKU TATU WA MWAKA KUHUSU TAFITI ZA SERA NA MAENDELEO WA REPOA DAR

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, baada ya kuufungua mkutano hio, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Picha na OMR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia washiriki wa mkutano wakati akifungua ramsi mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa meza kuu na baadhi ya viongozi, wakati akifungua ramsi mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba, akichangia wakati wa mkutano mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umefunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakiwa ukumbini humo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua ramsi mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Kunduchi Beach, kufungua ramsi mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, baada ya kuufungua mkutano huo ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.

picha za tukio la tamasha la pasaka dar na mbeya.

$
0
0


Bon Mwaitege muimbaji nguli wa muziki wa ijnili hapa nchini akikonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa Injili Mkoani Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine wakati wa tamasha la Pasaka katika Jijiji hilo,ambalo liliandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion.
Pichani kati ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Mbeya kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt.Marry Mwanjelwa akiwapungia mkono baadhi watu waliofika kwenye tamasha la pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa Sokoine,mkoani Mbeya.
Waimbaji wa Muziki wa Injili kutoka Kigali Rwanda,maarufu kama kwetu pazuri wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu MHE,Mizengo Pinda aliekuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la Pasaka uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema,Freeman Mbowe,na Mke wake Dk Lilian Mbowe wakifuatilia tamasha la Pasaka2013  kwenye jukwaa la wageni wa heshima kwenye  uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Muimbaji wa Injili wa kimataifa kutoka Afrika ya Kusini Sipho Makabane akikonga na kuburudisha nyoyo za wapenzi wa Muziki wa Injili Jijini Dar es salaam wakati wa tamasha la Pasaka kwenye uwanja mpya wa Taifa,fuatilia hapa kwa matukio zaidi ya tamasha la pasaka 2013 linaloendelea katika mikoa ya Iringa Dodoma na Mwanza.

Upendo Nkone akifanya vitu vyake kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya na wimbo wake Upendo wa Yesu wanizunguka.


Maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam wakifurahia tamasha la Pasaka 2013 kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Waimbaji wa nyimbo za Injili wakiwasili kwenye uwanja wa Sokoine tayari kwa kutumbuiza kwenye muendelezo wa tamasha la pasaka.
Mwenyekiti wa tamasha la Pasaka,ambae pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Alex Msama,akishuka kwenye uwanja wa ndege wa Songwe akiwa sambamba na waimbaji wa muziki wa injili waliotumbuiza kwenye tamasha la muendelezo wa pasaka mkoani Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine.

WOMEN IN BALANCE KITCHEN PARTY GALA APRIL 2013

$
0
0


Wanawake na wasichana wa Dar es salaam na mikoa ya jirani Kitchen party gala ipo on tayari.

Mwaka jana ile ya mwisho ya mwezi wa kumi tulifanyia Diamond jubelee VIP hall na ukumbi ulishona sana sana.Kulikuwa na mapungufu kadhaa ambayo sitapenda yajirudie
 this time.Najua ni mara chache shughuli kukosa upungufu fulani lakini kulirudia kosa ndio kosa zaidi.

Sasa mwaka huu tumepata ukumbi mpya kabisa upo ndani ya jengo la GOLDEN JUBELEE.Hili jengo ni jipya lipo pembeni ya jengo la PPF Tower mjini kabisaaa.

Ukumbi huo unaingiza watu 1000 tu na ndio idadi tunayoitaka siku hiyo.
Service zao ni za kihoteli kabisa na wao ndio wataserve kila kitu.Ukumbi huu uko chini ya JB Belmonte hotel hivyo wao ndio watatoa huduma za chakula.Chakula chetu kitakuwa kwenye hadhi ya starter,main course na desert.
Hivyo tumeona tuadvance ili kukidhi mahitaji yako ya kihuduma,mazungumzo yetu ya siku hiyo na burudani.

Na kwasababu tumeadvance kihuduma na shughuli kwa ujumla  kiingilio chetu this time kitapanda kitakuwa Tsh 40,000/= Ukumbi una vyoo vingi vipya na visafi na wa hadhi ya kimataifa.Pia najua kina mama ndio waandaaji wa shughuli mbalimbali za kifamilia,marafiki,ukoo mje muone ukumbi huu mpya.Hawa wana kumbi 4 katika jengo hili hili.Unaoingiza watu 1000,600,400 na 150 mkuje muone maana tunapata taabu sana ya kumbi  hasa kama unataka maeneo ya town.
Tutakuwa na wasemaji wa ndani na nje ya Tanzania.
DRESS CODE:Tusisahau dress code yetu ya siku hiyo imekuwa inspired na bendera ya nchi yetuTanzania.

TAREHE:Kparty gala itakuwa jumamosi ya tarehe 27 april 2013.Kuanzia saa tano asubuhi mpaka kumi na mbili jioni.
 Kwa lolote piga namba hii 0787583132 na 0657442255.

ASANTENI

Ognaniser
Dina Marios
!

MSHINDI WA TIGO ASCEND Y200 ALEJEA

$
0
0


Mshindi wa promosheni ya Ascend Y200 Fred Mgaya aliyejishindia zawadi ya kugharamiwa na Tigo gharama zote za kutembelea miji mikubwa nchini China akiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK Nyerere leo (jana)

Promosheni ya Tigo ya Ascend Y200 ilizinduliwa rasmi mnamo mwezi Oktoba mwaka 2012 ambayo inamuwezesha mteja kununua smartphone yenye kiwango na hadhi ya juu aina ya 'Ascend Y200' kwa punguzo la hali ya juu.

Jumla ya washindi wawili walipatikana ambao ni Bw. Fred Mgaya mwanafunzi wa Kcmc Moshi na Bw. Simon Richard mkazi wa Ubungo Dar es Salaam, washindi hao walitembelea vivutio mbalimbali kwa nusu siku jijini Guangzhou na mapumziko ya siku nzima katika milima ya Lotus nchini humo.

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE E3-WINNER

$
0
0
 Watangazaji wa kipindi cha Guinness Football Challenge Larry Asego(kulia) na Flavia Tumsiime(kushoto).
 Washindi wa kipindi cha Tatu cha Guinness Football Challenge,Kenneth Kamau(kulia) na Wills Ogutu (kushoto) wote wanatoka Nairobi Kenya, katika picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi hicho Larry Asego na Flavia Tumsiime.
======  ======  ====

TIMU YA PILI KUTOKA KENYA KUTINGA FAINALI ZA PAN-AFRICAN


Katika sehemu ya tatu jana usiku kupitia televisheni za ITV na Clouds TV, mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ yalionesha ni jinsi gani utulivu unavyosaidia katika mashindano ambapo timu kutoka Kenya ilifanikiwa kuzitoa timu nyingine za Tanzania, Uganda na timu nyingine kutoka Kenya . 

Kenneth Kamau na Wills Ogutu walishinda katika mikwaju ya penati na kufikia hatua ya mwisho katika ukuta wa pesa wa Guinness ambapo walifanikiwa kulenga matundu manne na kupata fedha za kimarekani dola 5,500. Kwa bahati mbaya walishindwa kulenga tundu la mwisho na hivyo kupelekea kupoteza dola 2,500 na kuondoka na fedha za kimarekani taslimu dola 3,000.

Kenneth na Wills wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia  kitita cha fedha  za kimarekani hadi kufikia dola  250,000. Katika kipindi kijacho cha mashindano haya kinachorushwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne mpya zitaingia uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka mshindi  na kutambulika kama wachezaji na si tu mashabiki,watatakiwa kushinda na kuziwakilisha nchi zao katika mashindano ya Pan-African.


GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol.  Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV.  Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku  ambapo  Clouds TV itarusha kipindi hicho  saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .


Tafadhali kunywa kistaarabu - Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.

TAARIFA YA MSIBA.

$
0
0
MDAU Said Mdoe amefiwa na  dada yao kipenzi Fatma Mdoe  (pichani) aliyefariki  ghafla jana (Jumatano) saa 10 jioni, msiba uko nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach, jirani na Dr Hizza.

Mazishi ni leo Alhamisi saa 10 Alasiri katika makaburi ya Kisutu, DSM. Msafara wa kutoka Mbezi kuelekea makaburini utaanza saa 8.30 mchana ili kukabiliana na adha ya foleni.


Mungu amlaze mahali pema peponi-Amen. 

Mwanafunzi kidato cha pili 'abebeshwa' mzigo wa kulea familia

$
0
0


 Kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Komnyang’anyo, Nadhiru Kinyama akizungumza na mwandishi wa Thehabari.com

Mwanafunzi Mwenjuma Magalu (16), mstari wa pili kulia wa Shule ya Sekondari Komnyang’anyo
===========   ======== =======
Na Thehabari.com, Handeni

MWANAFUNZI wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Komnyang’anyo, Mwenjuma Magalu (16) amejikuta akibeba mzigo wa kulea familia baada ya familia hiyo kutelekezwa na babayake.

Mwanafunzi huyo anayeishi katika Kijini cha Msasa amejikuta katika hali hiyo ngumu baada ya mama yake mzazi, Hadija Magalu kufariki dunia ambaye ndiye aliyekuwa akiihudumia familia hiyo baada ya mzazi mwenzake (mumewe) kuitelekeza miaka minne iliyopita.

Mama huyo (Hadija Magalu) alifariki dunia Agosti, 2013 kwa matatizo ya uzazi na kuiacha familia hiyo ya watoto watatu aliyokuwa akiihudumia chini ya ulezi wa mamayake mzazi, Bibi Amina Mohamed.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni kijijini Msasa, mwanafunzi Magalu alisema amelazimika kuilea familia hiyo baada ya bibi yake aliyeachiwa familia hiyo kuugua ugonjwa wa TB na kushindwa kuendesha shughuli za kilimo na nyinginezo kuisaidia familia hiyo.

“Bibi ndiye aliyekuwa akitupikia, tutafutia chakula na tulikuwa tukishirikiana naye hata kulima…lakini kazi hizo zote kutokana na afya yake hawezi kuzifanya, ninalazimika kuzifanya mwenyewe. Japokuwa nipo shuleni lakini natakiwa kujua tutakula nini tunapata wapi pesa ya chakula na shughuli nyingine za familia,” alisema Magalu akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Alisema familia yao hutegemea kilimo lakini wakati mwingine hulazimika kwenda kutafuta vibarua vya kufanya ili kupata pesa ya kula yeye pamoja na bibi yake. Aidha aliongeza kuwa wadogo zake wawili ambao awali alikuwa akikaa nao amelazimika kuwapeleka kwa mjomba wake baada ya kuona hali ni ngumu. Hata hivyo alisema wajomba zake nao hali yao ni ngumu hivyo wanashindwa kuhudumia familia hiyo.

Akizungumzia hali ya maisha ya familia hiyo Bibi. Amina Mohamed ambaye kwa sasa ni mgonjwa wa TB alikiri mwanafunzi huyo kuwa na majukumu mazito ya familia ambayo awali alikuwa ameyabeba yeye baada ya mwanaye kufariki dunia.

“Kweli mtoto huyu anaelemewa na malezi ya familia hii lakini sina cha kufanya kwa kuwa mimi ni mgonjwa wa TB na nimeshauriwa nisifanye kazi kwa sasa, hivyo kuanzia kupika, kulima shambani na hata kutafuta cha kula anafanya yeye baada ya kurudi shuleni,” alisema bibi huyo.

Mwanafunzi huyo ambaye anasomeshwa na msamaria mmoja aliyejitokeza baada ya familia yao kushindwa kumlipia ada amewaomba watu walioguswa na maisha ya familia hiyo kumsaidia.

Akizungumza hivi karibuni Kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Komnyang’anyo, Nadhiru Kinyama alikiri hali ngumu kwa kijana huyo kutokana na mazingira ya familia yao na kuongeza anahitaji kusaidiwa hata fedha za kujikimu na gharama zingine za masomo.

habari picha za vurugu za SAKATA LA KUGOMBEA KUCHINJA LAZUSHA BALAA TUNDUMA.

$
0
0

Hii ndiyo hali halisi ya Mji mdogo wa Tunduma leo (jana) kuanzia asubuhi.



Matairi yanachomwa katikati ya barabara



Mambo hayo 




Mwandishi wa Mbeya yetu pamoja na waandishi wenzake walipata shida sana kufika mji wa Tunduma walikutana na vikwazo vingi sana lakini wananchi walikuwa waelewa waliwasaidia kutoa magogo na matairi ili wapite wakapate habari





picha zote kwa hisani ya Mbeya Yetu Blog

Airtel Rising Stars Awamu ya tatu kuanza mwishoni mwa mwezi huu

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayofanya kazi pamoja na kampuni ya Samsung zimesaini makubaliano ya kushirikiana kudhamini mashindano makubwa Afrika kwa vijana wa chini ya miaka 17. 

Katika mkataba huo wa mamilioni ya dola, Samsung pia itakuwa mtoaji rasmi wa vifaa vya mawasiliano kwenye mpango huo wa mashindano maarufu kama Airtel Raising Star (ARS) unaoendeshwa na Airtel. 

Airtel inatoa huduma za mawasiliano kwa simu za mkononi kwenye nchi 20 barani Asia na Africa huku Samsung ikiwa ni miongoni mwa makampuni makubwa ya vifaa vya kisasa vya elektoniki. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam leo, Airtel imefanya kazi kwa karibu sana na taasisi za elimu kwenye nchi 17 zinazozungumza Kiingereza na Kifaransa ambapo kwa kupitia mashindano hayo ya soka ya Airtel Rising Stars yamefanikiwa kushirikisha zaidi ya timu 18,000. ambapo vijana wa kike na wa kiume wapatao 400,000 barani Afrika walishiriki katika mashindano hayo ya Airtel Rising Star. 

 Mwaka jana mashindano haya ya Airtel Rising Stars yalionekana kukua kwa asiliamia 65 na kuna kila dalili kwa mwaka huu kukua zaidi,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Airtel Makao Makuu. 

Mkakati huo wa kukuza soka barani Afrika unaungwa mkono kwa dhati na klabu kubwa za England; Arsenal FC na Manchester United ukiwa na lengo la kuibua na kukuza vipaji vipya vya vijana wa Kiafrika. “ARS imefikia kuwa chanzo kizuri cha wachezaji wapya wa timu za mataifa mbalimbali huku pia wengine wakijiunga na klabu zinazoshiriki ligi kuu barani humu. Afrika ina vijana wengi zaidi duniani. 

Uwiano wa vijana barani humu ni mkubwa kuliko mabara yote kwani takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 60 ya Waafrika zaidi ya bilioni moja ni vijana,” alisema George Ferreira, Makamu wa Rais wa Samsung Electronics, Africa. 

Akizungumzia ushirikiano huo, Andre Beyers, Ofisa Masoko Mkuu wa Airtel Africa alisema: "Ushirikiano huu utapanua wigo wa biashara na kuyawezesha mashindano ya ARS kufikia malengo yake.” 

Msimu ujao wa Airtel Rising Stars ukiwa ni wa tatu tangu kuanzishwa kwake utaanza mwishoni mwa mwezi huu. Moja kati ya matunda ya mashindano haya ya Airtel ni Priscilla Okyere, binti aliyeibuka kutoka ARS na sasa ni nahodha wa timu ya taifa ya wasichana chini ya miaka 17 ya Ghana. Aliiongoza timu hiyo kunyakua medali ya fedha kwenye mashindano ya Dunia ya FIFA Under-17 kwa wanawake mwaka jana huko Azerbaijan.

Kikao kazi cha Ushirikiano kuhusu kuandaa Mkakati wa Pamoja wa namna ya kushughulikia masuala ya Jinsia katika Sekta ya Madini.

$
0
0
 Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Tanzania Bw.Phillipe Poinsot akiongea wakati wa ufunguzi
 Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Tanzania Bw. Philipe Poinsot, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba na Mkurugenzi Mtendaji wa UN-Women Kanda ya Afrika Mashariki na Pembe ya Pwani katika kikao.
 Baadhi ya Washiriki wa kikao hicho wakifuatilia ufunguzi rasmi
Washiriki wa kikao wakimsikiliza Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi

======  =======  =========

Mainstreaming Gender into Extractive Industry: Sophia Simba


By Asteria Muhozya


Achieving the development gains that extractive industries promise in particular for women depends on understanding and managing the risks involved, while coming up with innovative policy responses to ensuring active and fair engagement of women.


Hon Sophia Simba Minister of Community Development Gender and Children said that, It is a high opportunity to promote women’s participation in the natural gas industry in terms of education and skills as these will help women entrepreneurs to be able to take advantage of opportunities presented to potential contractors in the natural gas industry.


Sophia Simba was addressing during the 2013 partnership dialogue ‘A gender Responsive Industry in Africa’ today convened at Hyatt Regency Hotel in Dar es Salaam, organized by UN-women and Publish What You What Organization, where participants from Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan, Ethiopia and UN-Women UK are participating in a two days working session..


Hon. Simba explained that, despite of creation of jobs and generatation of wealth, extractive industry has not been enjoyed equally by all members of society while at the same time cases extractive industries have been associated with negative and social and environmental negative effects to local communities.


“ We are here today to understand who is benefiting, who is being impacted negatively and what actions are required to ensure equitable sharing of benefits and opportunities among women and men’ Simba said


Hon. Simba pointed out that, number of World reports show that less 10% of extractive industries labour forces are women which shows that women need to be empowered to become active actors in industry activities.


Presenting welcoming remarks Phillipe Poinsot Tanzania– UNDP country Director said, for a country to successed in human development for extractive, appropriate legistrative framework, well functioning institutions and strong progmammes that drive the needs should be in place. He also added that, extractive industry expects to operate in good governance, accountability, transparency, and in gender sensitive manner.


Also Christine Musisi UN-Women Regional Director said the two days workshop will focus on Gender Dimensions in the Extractive Industry Sector, Status of Transparency and Accountability in the Extractive Industries, The African Mining Vision Action Plan. She also added that, generally UN- Women is obliged to focus on issues of Women Economic Empowerment, Ending Violence against Women, Engaging women in peace and security process, centralizing gender equality to national development processes and has mandatory power to coordinate and ensure the equality issues are fully addressed in UN-System and practiced by member states. 


Mazishi ya Advocate Nyaga Mawalla - Nairobi 03 April 2013

$
0
0

  Picha kwa hisani ya Kwa hisani ya Jamii forums.

SHAMBA ZURI LINAUZWA BAGAMOYO

$
0
0
Shamba lenye ukubwa wa heka moja na nusu linauzwa maeneo ya Kiromo, Bagamoyo, liko jirani na Kiromo View Resort kwenye barabara kuu iendayo Bagamoyo mjini, kiasi cha 10 tu. Lina kibanda cha vyumba vinne, linafaa kwa uwekezaji wa shughuli mbalimbali za kibiashara, kwani liko barabarani kama picha zinavyoonesha. Bei T.Shs 95 milioni tu.
MWENYE NIA THABITI YA KUNUNUA, PIGA SIMU: +255 657 803139

kazi kweli kweli mujini..!

ziara ya rais wa china nchini Tanzania yaleta mafanikio mengi kwa zanzibar.

$
0
0

Imeelezwa kuwa ziara ya Rais wa China nchini Tanzania imeleta mafanikio mengi kwa Zanzibar ikiwa ni pamoja na Makampuni ya Kichina kupanga kuwekeza katika sekta tofauti Zanzibar.

Balozi Mdogo wa China anayefanya kazi Zanzibar Bi Chen Qiman ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Mazizini kuhusiana na matokeo ya ziara ya Rais Jinping aliyofanya karibuni nchini Tanzania. Amesema Zanzibar imeweza kunufaika moja kwa moja na zira hiyo ikiwa ni pamoja na kusainiwa Miradi mitatu ya maendeleo kwa ajili ya Visiwa vya Unguja na Pemba.

Bi Chen amesema Rais wa China pia amemualika Rais Shein kwenda China kwa ziara ya kikazi ambapo pia atapata fursa zaidi ya kupanga mambo mengi ya kimaendeleo nchini huko. Ameongeza kuwa Ziara hiyo inayotarajiwa kufanyika mwaka huu itakuwa fursa adhimu kwa Rais Shein kujifunza mengi na kukuza mahusiano zaidi kati ya Zanzibar na Jamhuri ya China.

Akizungumzia mikakati iliyowekwa na China ya kuisadia Zanzibar Bi Chen amesema Ofisi yake itaendelea kuitangaza Zanzibar katika nchi yake ili kuwavutia Wananchi wa China kuja kutembelea Zanzibar na kuimarisha Sekta ya Utalii. katika kufanikisha hilo Bi Chen ameshauri Wazanzibari kuijifunza Lugha ya Kichina ili kurahisisha mawasiliano iwapo Wageni hao watakuja kutalii nchini hapa.

Mikakati mingine waliyoipanga ni pamoja na kuyahamasisha Makampuni kufanya uwekezaji katika Viwanda vya kusindika Matunda na kuwekeza katika Bahari jambo ambalo litasaidia sana maendeleo na kupunguza ukosefu wa Ajira. Ziara ya Rais Jinping nchini Tanzania aliyoifanya karibuni imezidi kuimarisha mahusiano mema kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya China ambapo katika ziara hiyo jumla ya Miradi 17 ya kimaendeleo iltiwa saini.

Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar.

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

WAZIRI SAMIA SULUHU AENDELEA NA ZIARA YAKE ZANZIBAR LEO

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Muungano Samia Suluhu Hassan akionyeshwa aina mbali mbali za Passpoti ambazo zinatumika hapa Nchini na Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji Passpoti na Ukaazi Haji Hamza Khamis wakati wa Ziara ya kutembelea Taasisi za Muungano zilizopo Zanzibar [Picha na Ali Meja]
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan  akionyeshwa Vibali vya Ukaazi Nchini na Mkuu wa Kitengo cha kuzalishia Passpot na Ukaazi Haji Hamza wakati wa Ziara ya kutembelea taasisi za Muungano ziliopo Zanzibar. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiuliza jambo kwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Mwinchumu  Hassan Salum  kwenye chumba cha Kutunzia Kumbu kumbu za Nyaraka za Kuzaliwa wakati wa Kuomba passpoti Nchini
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images