Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akitoa Mkono wa Iddi kwa wananchi mbali mbali waliofika viwanja vya Ikulu mjini Unguja leo katika kusherehekea Sikukuu ya Idd el Fitri,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Viongozi na Mashekhe waliofika Ikulu Mjini Unguja leo kwa madhumuni ya kupokea mkono wa Idd na kusoma Dua katika Sikukuu ya Idd el Fitri inayoadhimishwa Duniani kote,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akipokea salamu ya heshma ya gwaride maalum la kikosi cha Polisi FFU leo wakati wa Baraza la Idd katika Kusherehekea Sikukuu ya Idd el Fitri, Sherehe za Baraza Idd lilifanyika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za Baraza la Iddi el Fitri zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama bwawani Hotel Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
Baadhi ya Wake wa Viongozi na wananchi mbali mbali wakisikiliza hutuba ya Rais waZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein aliyoitoa leo katika kusherehekea Sikukuu ya Idd elFitri katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein(wa pili kulia) akijumuika na Viongozi na waislamu mbali mbali katika swala ya Suna ya Idd el Fitri iliyoswaliwa kitaifa leo katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
…………………………………………………….
Na RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhamed Shein amewataka wananchi wa Zanzibar kuyatumia mafunzo waliyopata katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kuendelea kupendana, kusaidiana na kuhurumiana.
Alisema katika kipindi chote cha mwezi wa Ramadhani wananchi waliongeza juhudi katika uchamungu na kutafuta radhi zake hivyo ametaka kuendeleza ut
amaduni wa kufanya mambo mema katika maisha ya kila siku.
Rais Ali Muhamed Shein alieleza hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi katika Baraza la Idd El Fitri lililofanyika Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar
Aliwashukuru masheikh, walimu na wanazuoni waliojitolea katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar kuendesha darsa na kutoa mawaidha juu ya njia bora ya kuitekeleza ibada ya saumu na kuhimiza mshikamano
Alisema tafauti za dini na itikadi za kisiasa visiwe chanzo cha kuleta mfarakano katika jamii na kila mtu anapaswa kuiunga mkono Serikali na kutoa mchango katika kuleta maendeleo.
Aliwataka viongozi wa siasa kwa upande wao kufanya siasa kwa kuzingatia misingi ya katiba na maadili ya vyama vyao na kwa mujibu wa sheria zilizowekwa za utawala bora.
Aliwakumbusha wanasiasa kwamba ni jukumu lao kushindana bila ya kulaumiana, bila ya kukejeliana na pia wanaweza kushinadana bila ya kudharauliana na kuhasimiana.
Dkt. Shein alisema vyama vya siasa vimeanzishwa na vitaendelea kuwepo kwa lengo la kushindana kwa sera na kuchochea maendeleo ya wananchi hivyo amewataka wanasiasa kuhubiri Umoja na amani katika vikao vyao.
“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa ni ushahidi unaotosha wa kuleta amani na maendeleo yanayokusudiwa, ”alisisitiza Rais wa Zanzibar.
Aliwataka viongozi wa kisiasa, dini, viongozi wa kijamii na wananchi wote kuona kuwa jukumu la kuhimiza utiifu wa sheria, kusimamia amani, utulivu na usalama wa nchi ni la watu wote.
“Zanzibar ni nchi yetu sote na Tanzania ni nchi yetu sote, hivyo sote ni wamoja na sote tunajukumu la kuishi kwa amani umoja na mshikamano”alieleza Dkt. Shein.
Aliwanasihi wananchi, hasa vijana kuendeleza amani na utulivu na kujiepusha na vitendo vitakavyopelekea kuvunja amani na umoja uliopo kwani hakuna mbadala wa amani inapotoweka.