Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 586 | 587 | (Page 588) | 589 | 590 | .... | 1897 | newer

  0 0

  IMG-20150715-WA0008
  Na Andrew Chale, Modewjiblog
  Bendi mpya ya muziki wa dansi ijulikanayo kama The Stars Band iliyo chini ya Anneth Kushaba inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Jumamosi ya Julai 18, siku ya Idd-Mosi ndani ya kiota cha Mzalendo Pub, Kijitonyama jijini Dar es Salaam huku ikitarajiwa kusindikizwa na mwanamuziki Barnabas pamoja na bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.

  Kiongozi wa Stars Band, Kushaba anasema kuwa, tayari wapo katika mazoezi mbalimbali na ‘crew’ nzima ya bendi hiyo ambayo inaunganisha wanamuziki wenye uzoefu mkubwa katika uimbaji, upigaji vifaa na kushambulia jukwaa ndani na nje ya Tanzania.

  “Wadau wa burudani ni nafasi ya kipekee kujitokeza kushuhudia uzinduzi wa bendi yao mpya iliyojaa kila aina ya burudani kuanzia uimbaji, kumiliki jukwaa na vyombo vilivyopangika.. burudani itakayoanza kuanzia saa moja jioni hadi majogoo” anasema Kushaba.

  Anaongeza kuwa, uzinduzi huo pia utapambwa na bendi ya Fm Academia ‘Wazee wa NGWASUMA na mwanamuziki Barnabas Classic huku kiingilio mlangoni kitakuwa sh 10,000. Kushaba anasema kuwa, miongoni mwa wanaounda bendi hiyo wapo wakali katika upande wa uimbaji kama Mao Santiago, Felly Kano, Alawy Junior, Khajanito (Khadija Maumivu) na Aneth Kushaba.

  Kwa upande wa vyombo bendi hiyo inaundwa na mpiga drum wa zamani wa Twanga Pepeta, James Kibosho akiwa pamoja na Zaid Sato (Base), Othuman Majuto, Sebastian na Denis ‘Keyboard’, pamoja na Chacha ‘Tumba’. Stars Band ndio inakuwa bendi ya kwanza ya dansi nchini kuja na mitindo mipya ya Utamaduni na bongo fleva (None stop!!) jukwaani.Stars Band pia baada ya uzinduzi huo itakuwa inapiga kila Jumamosi ndani ya kiota hicho cha Mzalendo Pub.

  0 0

  SAM_3817
  Katibu wa vijana umoja wa vijana  UVCCM wilaya ya Arusha mjini Jamali Khimji akimkabidhi fomu ya ubunge viti maalum Bi.Neema Kiusa(27)katika ofisi za umoja huo jijini Arusha, ahaidi kuinua vijana kiuchumi endapo atapata nafasi ya kuwa Mbunge wa vijana Mkoa wa Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
  SAM_3820
  Neema Kiusa(27) Mgombea ubunge viti maalumu kupitia  chama cha Mapinduzi ambaye pia ni mjumbe wa baraza la vijana wilaya ya Longido akionyesha fomu aliyochukua leo.
  SAM_3821
  Neema Kiusa(27)ambaye ni mgombea ubunge viti maalumu kupitia  chama cha Mapinduzi  akiwa na mumewe Andrea Shija, pia ni mama wa mtoto mmoja
  SAM_3824
  Neema Kiusa(27)Mgombea ubunge viti maalumu kupitia  chama cha Mapinduzi ambaye pia ni mjumbe wa baraza la vijana wilaya ya Longido akitoka katika ofisi za umoja wa vijana wa ccm mkoa wa Arusha baada ya kuchukua fomu

  Mgombea ubunge kupita kundi la vijana (UVCCM) Neema Kiusa  leo amechukua fomu ya kuwania nafasi ya ubunge viti maalumu Mkoa wa Arusha,ambapo amesema kuwa shauku yake kubwa ni kuwatumikia vijana kwa kutatua changamoto ya ajira.
   
  Neema ambaye pia ni mjumbe wa baraza la vijana Wilaya ya Longido alisema kuwa ndoto yake ya kuwatumikia vijana ni ndoto yake ya muda mrefu sana hivyo endapo atapata nafasi hiyo atashirikiana na vijana bega kwa bega kuleta maendeleo katika Mkoa wa Arushaa .

  Pia mgombea huyo alitoa shukrani kwa mume wake  anayempa ushirikiano mkubwa wa kufanikisha ndoto yake ya kutumikia vijana ambapo aliwataka wanaume wengine kuonyesha ushirikiano kwa wake zao endapo wataonyesha nia ya kuwania nafasi za uongozi.

  Kwa upande wake Katibu wa vijana UVCCM wilaya ya Arusha mjini Jamali Khimji amewataka vijana wa chama cha mapinduzi kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za nafasi za ubunge viti maalumu kundi la vijana katika mkoa wa Arusha
  Khimji alisema kuwa kijana anayetakiwa kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ni kijana wa kwanzia umri wa miaka 21-30 na awe ametimiza vigezo vya chama hicho

  0 0


   k
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na watanzania waishio  Switzerland katika hoteli ya Intercontinental jijini Geneva-Julai 16, 2015.
  mail.google.com9
  Watanzania waishio Switzerland.
  j
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa ofisi ya mwakilishi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa  Geneva jana baada ya kuzungumza nao na kisha kupata futari katika Hoteli ya Intercontinental jijini Geneva Uswisi.(picha na Freddy Maro)

  0 0

  bai1bai2
  Kabula Kalamu wa eneo la Lalanayo wilayani Mlele akitoka bombani kuteka maji   huku akiwa amembeba mgogongoni mwanae  Masunga Mayunga Jula 17, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
  bai3
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa amekalia oja ya madwati mapya ya plastiki yaliyowekwa kwenye moja ya madara ya shuley amsingi ya Kakuni  wilayni Mlele akiwa katika mapumziko mafupi kijijini kwake Kibaoni Julai 16, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  bai4
  Wanawake wa Kijiji cha Kibaoni wilayani Mlele wakielekea majumbani baada ya shughuli zao mbalimbali Julai 16, 2015. 
  bai5
  Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda akikagua ujenzi wa nyumba za walimu katika shule ya msingi ya Kakuni wilayani Mlele Julai 16, 2015. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  download (9)
  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini linawakumbusha wamiliki na waendeshaji wa kumbi za burudani kufuata sheria, kanuni na taratibu walizopewa kwenye vibali vyao vya uendeshaji wa kumbi.

  Wanaelekezwa kuhakikisha wanakuwa na vibali halali vya uendeshaji wa kumbi zao, kuzingatia muda wa matumizi ya kumbi, kuepuka kelele zinazosumbua kwenye maeneo maalum hasa makazi ya watu na kuhakikisha ulinzi na usalama wa maisha ya watu.

  Aidha, BASATA linawakumbusha wamiliki wote wa kumbi za burudani kwamba ni marufuku kukusanya watoto katika kumbi zao kupitia kile kinachoitwa ‘Disko Toto’ ili kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza.

  Uzoefu unaonesha kwamba, nyakati za sikukuu kama hizi wamiliki wa kumbi wamekuwa wakijisahau na kutamani kutengeneza faida katika biashara zao kiasi cha kuandaa disko kwa watoto hali mbayo imekuwa ikisababisha maafa makubwa ambayo yangedhibitika kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.

  BASATA kama mtoaji wa vibali vya kumbi za sherehe na burudani linasisitiza kwamba halitafumbia macho ukumbi wowote utakaokiuka maelekezo haya sambamba na kuruhusu maonesho machafu yenye kudhalilisha utu wa binadamu hasa yale yanayoonesha maungo ya ndani. Hatua kali na za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka maagizo haya.

  BASATA linawatakia wasanii na wadau wote wa Sanaa sherehe njema ya Eid El Fitr na yenye furaha tele.
  Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini
  Godfrey Mngereza
  KATIBU MTENDAJI

  0 0


  NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA   ACSEE 2015 EXAMINATION RESULTS  0 0

  Kiwanda cha saraji cha Lafarge kilichopo Mbeya. Kiwanda hiki ni maarufu kwa utengenezaji wa saruji, kokoto na zege.
  Wafanyakazi wa kiwanda cha saruji cha Lafarge kilichopo Mbeya wakiwa kwenye picha ya pamoja. Lafarge ni mdau mkubwa katika bishara ya Saruji, Kokoto na Zege.

  Kampuni mbili zinazoongoza katika sekta ya ujenzi hapa nchini, Lafarge S.A. na Holcim Ltd zimekamilisha muungano wao uliosubiriwa kwa muda mrefu na kuunda kampuni moja itakayo fahamika kwa jina la LafargeHolcim.

  Vigezo muhimu vya kukamilisha muungano huo vimeafikiwa hivi karibuni kufuatia ubadilishaji wa umiliki pamoja na kutolewa kwa hisa mpya za Holcim kwenda kwa wanahisa wa Lafarge.

  Wanahisa wa kampuni ya Holcim walipitisha azimio hilo la muungano katika mkutano mkuu uliofanyika Mei 8, 2015.   

  Wakati wa uzinduzi wa Kampuni hiyo, LafargeHolcim ilizindua pia nembo yake mpya ambayo itatambulisha ushirika baina ya kampuni zote mbili huku ikidhihirisha uongozi na nguvu mpya ya kampuni hiyo.

  Akizungumzia ubia huo, Mwenyekiti msaidizi wa bodi ya wakurugenzi LafargeHolcim Bw. Wolfgang Reitzle, alisema “Tukio hili la leo ni la kihistoria – sio tu kwa kampuni hizi mbili mama, bali kwa sekta nzima ya ujenzi kwa ujumla.

  LafargeHolcim ni kampuni yenye sifa za biashara za kipekee, ina sifa ya kuigwa katika sekta ya R&D na huwapa wateja wake bidhaa mbalimbali zenye ubunifu na zenye kuongeza thamani, huduma na ufumbuzi – kuanzia washika dau wadogo hadi makampuni makubwa na miradi migumu.”

  Naye Mwenyekiti msaidizi wa Bodi ya wakurugenzi wa LafargeHolcim, Bruno Lafont, alisema “Kampuni hii mpya imejengwa katika msingi mzuri wa historia ndefu na utamaduni wa Lafarge na Holcim na washirika wake. Muungano huu hauwaletei watanzania tu kampuni ya kimataifa, bali pia bidhaa zenye uwezo wa kipekee”.

  Hii ni habari njema kwa Tanzania kwani Lafarge ina uwepo mkubwa na ni mbia mkubwa katika kampuni ya Mbeya Cement, ambapo Serikali ya Tanzania na NSSF ni wabia wake pia.

  Akizungumza na wafanyakazi wa Lafarge Tanzania katika hafla ya chakula cha mchana, Ms Catherine Langreney, mkurugenzi mtendaji kwa nchi za Tanzania na Malawi, alisema “Nina Imani muungano huu utawezesha Lafarge Tanzania kuzalisha faida kubwa kwa wabia wake, wakati huo huo kuwa chachu ya ukuaji katika sekta ya Ujenzi na kuleta ufumbuzi mbali mbalimbali katika sekta yenye kubadilika kila siku”

  Bi. Langreney aliongezea kuwa: “Afya na Usalama wa watanzania ndio kiini cha biashara yetu hivyo tupo hapa kushughulikia mahitaji ya wateja wetu na hatimaye kuwa mshirika mzuri wa biashara”

  Mwezi April 2014 kampuni hizo mbili zilitangaza nia ya kuungana. Baada ya mazungumzo ya kina yaliyokuwa chanya na mamlaka husika kuafikiana, Kampuni hiyo mpya iliweza kupokea vibali vyote husika katika muda uliopangwa.  

  0 0

   
  Kada wa chama cha mapinduzi Emmanuel Barnabas Maro anayewania kuteuliwa na chama chake kugombea nafasi ya udiwani katika kata ya Kipawa wilayani Ilala jijini Dar akionesha fomu alizokabidhiwa leo na Katibu wa CCM wa kata ya Kipawa Amina Sebo hayupo pichani.

  0 0

  Timu ya watu 39 Wakiwemo wakurugenzi wa Taasisi na wakurugenzi kampuni mbalimbali za nchini Afrika Kusini walipotembelea shule ya sekondari ya Mazoezi Darajani iliyopo Marangu wilaya ya Moshi.
  Baadhi ya wanafunzi katika shule ya sekondari ya Mazoezi Darajani iliyopo Marangu mkoani Kilimanjaro wakiwa darasani.
  Wananfunzi katika shule ya sekondari Darajani wakiwa katika mkusanyiko tayari kupokea wageni waliotembelea shule hiyo.
  Mhifadhi katika Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro,KINAPA ,Charles Ngendo akiwatambulisha wageni kutoka Afrika Kusini mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Darajani.
  Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa,TANZANIA,(TANAPA) Allan Kijazi akiwa na ugeni kutoka nchini Afrika kusini walipotembelea shule ya sekondari ya Darajani iliyopo Marangu.
  Mkuu wa shule ya sekondari ya Darajani iliyopo Marangu,Mary Mlay akisoma taarifa ya shue hiyo mbele ya wageni waliotembelea shule hiyo.
  Katibu Tawala wilaya ya Moshi,Remida Ibrahim akizungumza wakati ugeni wa timu ya watu 39 ulipotembelea shule ya sekondari Darajani kwa lengo la kusaidia kununua taulo maalumu za wasichana waliopo mashuleni pindi wawapo katika siku zao za Hedhi.
  Mwanzilishi wa taasisi ya Imbumba Foundation ,Richard Mabaso ambaye taasisi yake inaratibu zoezi la upandaji Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia kununua taulo maalumu kwa wasichana walio mashuleni.
  Mwakilishi wa jiji la Ekurhuleni nchii Afrika Kusini,Lebo Modibe akikabidhi vipeperushi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa,Tanzania (TANAPA)Allan Kijazi ambavyo viligawiwa kwa wanafunzi wa shule hiyo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa ,Tanzania(TANAPA) Allan Kijazi akimshukuru Mwanzilishi wa taasisi ya Imbumba Foundation na Nelson Mandela Foundation kwa kuchangia msaada wa ununuzi wa taulo maalumu kwa wasichana waliopo mashuleni pindi wawapo katika siku zao za Hedhi.
  Katibu tawala wilaya ya Moshi ,Remida Ibrahim akikabidhi vipeperushi kwa walimu wa shule hiyo.
  Mcheza filamu maarufu wa nchini Afrika Kusini,Jacky Davnarain maarufu kama Rajesh wa tamthiliya ya Isidingo pia ni miongoni mwa wageni hao wanaopanda Mlima Kilimanjaro.


  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  SAM_3763
  Katikati ni Meneja Mahusiano shirika la The Foundation For Tommorow ,Anton Asukile akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Arusha juu ya Kampeni ya SHAMIRI inayolenga kuchangisha milioni 50 kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi ,kulia ni Meneja Programu wa masuala ya kijamii na afya Hedwiga Mchaki na kushoto ni Hilda Lema Mfanyakazi wa shirika hilo(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
  SAM_3747Meneja Programu wa masuala ya kijamii na
  afya  wa shirika la The Foundation For Tommorow Hedwiga Mchaki
  akifafanua jambo katika kikao na waandishi wa habari jijini Arusha
  SAM_3773 Hilda Lema mfanyakazi wa shirika hilo anasisitiza jamii kushiriki katika kampeni hiyo
  SAM_3742Taswira
  SAM_3803Mwanafunzi wa chuo kikuu Nicemary Phelix aliyewezeshwa na shirika la The Foundation For Tommorow kwa kusomeshwa kwanzia darasa la nne hadi sasa yupo elimu ya juu baada ya kupoteza wazazi wake wote, anaomba watanzania kuonyesha hisia zao katika kusaidia jamii yenye uhitaji na siyo kusubiria wafadhali kutoka nje ya Nchi.
   
  Shirika lisilo la kiserikali la The Foundation for Tommorow limezindua
  kampeni ya kuchangia SHAMIRI ya kusaidia elimu ya watoto wanaoishi
  kwenye mazingira magumu lengo ni kuchangisha kiasi cha shilingi
  milioni 50 zitakazowawezesha kupata elimu bora na kuondokana na
  mazingira yanayowakabili.
   
  Meneja Mahusiano wa shirika hilo Anton Asukile alisema hayo jana
  akizindua kampeni maalumu ya SHAMIRI inalenga kusaidia ustawi wa
  watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
   
  “Kampeni hii itawezesha kuinua uchumi wa kaya 40 za watoto wanaoishi
  katika mazingira hatarishi kupitia mradi wa WEZESHA KAYA pia
  itasaidia upatikanaji wa vifaa muhimu vya kujifunzia kwa watoto
  wapatao 112” Alisema Anton.
   
  Asukile ameiomba jamii ya Watanzania kushiriki katika kukabiliana na
  changamoto zinazoikabili jamii ili kuwakomboa watoto wanoishi katika
  mazingira hatarishi kwa kuchangia kampeni ya SHAMIRI.
  Alisema kuwa Watanzania wataweza kuchangia fedha hizo kwa njia ya simu
  katika kampeni hiyo imeanza rasmi mwenzi Julai na itahitimishwa
  septemba 25 mwaka huu.
   
  Meneja Programu wa masuala ya kijamii na afya Hedwiga Mchaki amesema kuwabaada ya kutoa misaada kwenye familia duni wameona ni vyema wakazipatia mafunzo ya ujasiriamali na mikopo ili waweze kujikwamua na kusomesha watoto wao pasipo kutegemea misaada.
   
  Hedwiga ameitaka jamii ya watanzania kuamka na kusaidia watoto yatima
  na wanaotoka kwenye familia masikini badala ya kusubiri mashirika
  kutoka nje yaje kutoa misaada.

  0 0

  Taarifa iliyotufikia chumba cha habari cha Globu ya Jamii hivi punde, inaeleza kuwa Mwanamuziki wa siku nyingi wa Muziki wa Dansi hapa nchini, Ramadhan Masanja "Banza Stone" amefariki dunia mchana huu nyumbani kwao Sinza karibu na Lion Hotel jijini Dar es salaam.

  TAARIFA ZAIDI ZITAWAJIA BAADAE KIDOGO.

  0 0

  Mwandishi wa Habari za Michezo na mdau wa maendeleo ya wilaya ya Handeni, Kambi Mbwana, mwenye fulana ya CCM, akikabidhiwa fomu ya kuwania Ubunge, Jimbo la Handeni Vijijini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Katibu Msaidizi wa CCM wilayani Handeni, Asha Muya, wilayani Handeni, mkoani Tanga. Kulia kwa Mbwana ni Jerome Mhando, mmoja wa wadau waliomsindikiza katika tukio la uchukuaji fomu ya kuwania nafasi ya kuwatumikia wana Handeni. Picha na Mpiga Picha Wetu.

  Kambi Mbwana ajitosa Ubunge Handeni Vijijini

  Na Mwandishi Wetu, Handeni
  MWANDISHI wa habari za michezo na mdau wa maendeleo wilayani Handeni, mkoani Tanga, amejitokeza rasmi katika mbio za kuwania ubunge jimbo la Handeni Vijijini kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).


  Makabidhiano hayo ya fomu yalifanyika mbele ya Katibu Msaidizi wa CCM wilayani Handeni, Asha Muya, ikiwa ni siku chache baada ya milango ya uchukuaji fomu za kuwania nafasi za Ubunge na udiwani kufunguliwa rasmi. Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Mbwana alisema kwamba ameamua kujitokeza katika mbio hizo za ubunge ili afanyie kwa vitendo yale aliyokuwa anayapenda, hususan katika suala zima la maendeleo, huku wachache wao wakishindwa kuelewa faida ya harakati zake, zikiwapo zile za kuitangaza Handeni kwa njia mbalimbali.

  Alisema wilaya yao imekuwa na changamoto kadhaa zinazohitaji nguvu za pamoja katika suala zima la shida ya kubwa ya maji, migogoro ya ardhi, ukosefu wa huduma bora za kijamii, hivyo kunahitajika jitihada na mipango ya pamoja kufanikishaji mambo hayo.

  “Nilikuwa kimya kwa siku kadhaa nikiangalia akina nani wapo katika mchakato wa kuhitaji nafasi ya kuwatumikia wananchi wa Handeni Vijijini na kusikitishwa na watu wasioishi huku na wasiokuwa na uchungu wala dhamira ya kuwakwamua wananchi wakijitokeza kwa wingi kuwania nafasi ya ubunge, inaonyesha wapo kwa maslahi yao zaidi.


  “Hii haiwezi kukubalika, ukizingatia kwamba wananchi wameendelea kuishi maisha ya mashaka kwa kukosa maji safi, elimu, afya, michezo, utamaduni na mambo mengine yanayopaswa kufanyiwa kazi kwa kushirikiana na watu wote, wakiwamo viongozi wa kisiasa, watendaji wa serikali na Watanzania kwa ujumla,” alisema Mbwana.


  Licha ya kuonekana mpya katika ulingo wa kisiasa hususan kwa nafasi ya ubunge, Mbwana anakumbukwa na kushukuriwa na wengi kutokana na mradi wake wa Tamasha la Handeni Kwetu linalofanyika kila mwisho wa mwaka, kuasisi Taasisi ya Handeni Kwetu Foundation, bila kusahau kuandika kitabu kinachojulikana kama Dira na Tumaini Jipya Handeni kilichopokewa kwa hisia tofauti, haswa kutokana na kilichoandikwa kwenye kitabu hicho.


  0 0

  Bi. Chikulupi Njelu Kasaka 
  Mgombea Ubunge Viti Maalum Vijana Mbeya Bi. Chikulupi Njelu Kasaka (Kushoto) akikabidhiwa Fomu ya Kuomba Ridhaa kuteuliwa kugombea Ubunge wa Viti maalum Vijana Mbeya na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Bi. Aida Mamu
   Kushoto ni Bw. Moses Mwakibinga Katibu wa Hamasa na Chipukizi Wilaya ya Chunya, Bi. Chikulupi Njelu Kasaka (Kushoto)  na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Bi. Aida Mamu Baada ya kukabidhiwa Fomu.

                    MFAHAMU BI. CHIKULUPI NJELU KASAKA


  *Anaitwa Chikulupi Njelu Kasaka.

  *Ni Mwanasheria (wakili) kitaaluma.


  *Ni mfanyakazi wa Bunge la JMT
  .
  *Sasa anawania Ubunge wa Viti-maalum (vijana).


  *WASIFU WA MGOMBEA: BI. CHIKULUPI KASAKA

  ELIMU:
  Chikulupi Kasaka ni mzaliwa wa Chunya na babu na Bibi ni wakazi wa Kijiji cha Mtanila katika Wilaya ya Chunya.

   Chikulupi alizaliwa mwaka 1986 na kuanza elimu ya msingi mwaka 1994 katika shule ya Chunya Kati. Chikulupi alimaliza elimu ya msingi Mkoani Tabora na kuchaguliwa kwenda shule ya Serikali ya Sekondari ya Wasichana Msalato iliyopo Dodoma ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha nne mwaka 2000-2004. Mwaka 2005-2007 alijiunga na Shule ya Serikali ya Sekondari ya Wasichana Loleza iliyopo Mkoani Mbeya. Alishaguliwa kijunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2007 kusomea Shahada ya Kwanza ya Sheria na kumaliza mwaka 2011. Mwaka 2013 alijiendeleza kwa kujiunga na mafunzo ya uanasheria kwa vitendo na kumaliza mwaka 2014 katika chuo kiitwacho Law School of Tanzania ambapo baadaye niliapishwa kuwa wakili.

  UZOEFU KATIKA UONGOZI:
  Chikulupi aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi akiwa anasoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alikuwa Mbunge katika Serikali ya wanafunzi - DARUSO.

   Chikulupi alichaguliwa mwaka 2009 kuwa Makamu wa Rais wa Umoja wa Wanafunzi wa Afrika Mashariki uitwao East Africa Community Students Union -EACSU.

   Pia alikuwa Afisa Mahusiano ya Umma katika Taasisi ya wanafunzi wa Sheria iitwayo University of Dar es Salaam Human Rights Association –UDHRA. Mwaka 2010 alishiriki mafunzo ya Uongozi kwa Vijana yaliyofadhiliwa na Shirika la Kijeruman liitwalo Friedrich Ebert Stiftung –FES.

   Pia mwaka 2014 alishiriki mafunzo ya Viongozi Vijana toka barani Afrika nchini Marekani ambao alisomea masomo ya Public Management katika chuo cha Howard kilichopo Washington. Pia nilipata fursa ya kukutana na Rais Barack Obama ambae ni mwanzilishi wa mafunzo haya.

  UZOEFU NDANI YA CHAMA/UVCCM:
  Chikulupi Kasaka alijiunga na CCM hasa katika jumuiya ya UVCCM mara tu baada ya kumaliza elimu ya sekondari 2006. 
  Alipokuwa anasomea Shahada ya Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alijikita katika shughuli mbalimbali za kuimarisha chama na mwaka 2010 alichaguliwa Mwenyekiti wa UVCCM tawi ya Abiyan-Chuo Kikuu. Na mjumbe wa Shirikisho la Vyuo Vikuu wanaCCM, Mkoa wa Dar es Salaam.

  KAZI:
  Mara baada ya kumaliza chuo kikuu Julai 2011 Chikulupi alifanya kazi katika Shirika la Wakimbizi katika Mradi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam uitwao International Migration Management Program (IMMP). 

  Mwaka 2012 aliajiriwa na Serikali kama Hakimu Mkazi daraja 2, katika Mahakama ya Mwanzo Makongorosi-Chunya, Mbeya. Mwishoni mwa mwaka 2012 nilijiunga na utumishi wa Chama Makao Makuu ya CCM Dodoma. 

  Nilipangiwa kufanya kazi za Chama katika Upande wa Bunge hasa za kisheria. Tangu kipindi hicho mpaka sasa Chikulupi anafanya kazi kama Msaidizi wa Katibu wa Wabunge wote wa CCM, Bungeni Dodoma.

  VIPAUMBELE:
  Chikulupi Kasaka anaomba ridhaa yako ili aweze kuwawakilisha vijana wa Mkoa wa Mbeya katika nafasi ya Uongozi wa Kitaifa kupitia ngazi ya Ubunge wa Viti Maalum-Vijana. 

  Kama mkazi wa Mbeya naamini vijana wa Mbeya wanauwezo, nguvu, bidii na jitihada katika shughuli zao za kila siku. Lakini mimi nitapigania kuwapatia vijana wa Mbeya fursa nyingi zaidi katika vipaumbele vifuatavyo: 

  ELIMU, AJIRA, MICHEZO, UTALII na AFYA.
  ANAOMBA UMUUNGE MKONO KWA FURSA ZAIDI KWA VIJANA WA MKOA WETU WA MBEYA.
  0 0

  Mwansheria na Kada wa Chama cha Mapinduzi, Emmanuel Makene (katikati) akiwa ameambata na mkewe Dk. Sarah Makene kurejesha fomu za kuomba ridhaa ya wana CCM Kinondoni kuteuliwa kugombea Ubunge katika Jimbo la Kinondoni. Anaepokea fomu hizo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe. Wengine ni wapambe wa mgombea huyo waliomsindikiza kurejesha fomu hizo leo.
  Emmanuel Tamila Makene ambae ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya na Katibu wa Usalama na Maadili taifa wa Umoja wa vijana (UVCCM) akisaini kitabu cha kurejesha fomu huku mkewe Dk Sarah Makene akimwangalia kwa makini na Katibu wa CCM Wilaya akikagua fimu. Dk Sarah Makene ni Daktari katika Hospitali ya Mwananyamala anaeshughulika na wagonjwa wa Ukimwi na wWaathirika na dawa za kulevya.
  Dk Sarah Makene ni Daktari katika Hospitali ya Mwananyamala anaeshughulika na wagonjwa wa Ukimwi na wWaathirika na dawa za kulevya, akipeana mkono na Katibu wa CCM Wilaya baada ya kupokea fomu za Muwewe.
  Makene akiwa na Mkewe Dk Sarah pamoja na rafiki yao baada ya kurudisha fomu.
  Makene akiwa na Mkewe Dk Sarah na marafiki zao baada ya kurejesha fomu.

  0 0


  0 0

  Shangwe na burudani za kutosha zinatarajiwa kufanyika katika sikukuu ya Eid hapo kesho mkoani Tabora panapo majaaliwa ya Mwenyezi Mungu. Mashabiki  mjini Tabora watarajiwa kufurahia onesho hilo katika maeneo mawili tofauti ambapo mchana itakuwa Bwalo la Polisi kuanzia saa 8 mchana na Usiku katika viwanja vya Muungano Mesi kuanzia saa 2 usiku.

  Wasanii wa kila nyanja wametua mjini hapo na kufanya mahojiano CG Fm Redio leo mchana; wasanii hao ni Kassim Mganga a.k.a tajiri wa mahaba, Ommy Dimpoz, Mkude Simba (Kitale) na rafiki yake Stan Bakora, Young Killer, na Baraka Da Prince.
  Eid_Tabora (8)
  Kassim Mganga akiwa CG Fm Redio, 89.5 The point of no Return
  Eid_Tabora (11)
  Ommy Dimpoz

  0 0

  Mtia nia wa ccm jimbo la ismani festo kiswaga akiwa katika ofisi za ccm jimbo la iringa vijiji
  akiwa na katibu wa ccm iringa vijijini

  NA MWANDISHI WETU,IRINGA.

  Baada ya zoezi la uchaguzi wa wagombea urais kukamilika katika vyama sasa zoezi limeanza kwa wabunge na madiwani ambapo hii leo Festo Kiswaga ambaye ameweka nia ya kugombea katika jimbo la isiman.


  Katika mkutano huo na waandishi wa habari KIswaga amekanusha uvumi uliokuwa umezagaa juu ya kuhongwa pesa mwaka 2010 ili kutogombea huku akidai kuwa alishindwa kwa haiki na si hongo ya mbunge aliyepo madalakani kwasasa huku akimzawadia ukuu wa wilaya.


  Ambapo pia ametumia mkutano huo ili kuujulisha uma juu ya maelengo yake ya kuchukua form katika wasifu wake amesema anadigree ya sayansi ya wanyama poli na kutumikia katika shirika la mbomipa na kuwatumikia wananchi wa misenyi mkoa wa kagera akiwa ni mkuu wa wilaya na sasa ni mkuu wa wilaya ya Nanyumbu huku akitumikia mashirika kama tanapa na chuo kikuu cha dar es-laam na kuteuliwa kuwa rais wa wa shirikisho vyuo vikuu vya umoja wa Afrika mashariki uliojumuisha vyou vikuu zaidi ya  400 katika nchi za Tanzania,Uganda,Kenya na Burundi.


  Akizungumzia kuhusu janga la njaa lililopo katika jimbo hilo amekiri kuwa anauzoefu juu ya utatuzi wa matatizo kama hayo kutokana na nyanja mbalimbali ambazo amepitia na pia amewataka wananchi wa ismani kumpa lidhaa yya kuwaongoza kutokana tatizo kama hilo amelikuta katika wilaya ya Namnyumbu na akafanikiwa kulitatua kwa asilimia 100%.


  Aidha amesema kutokana na jimbo hilo kukosa kiongozi mwenye uchungu kama yeye imepelekea kukosekana kwa huduma kama maji katika vijiji mbalimbali ikiwa jimbo hilo limefikisha miaka 20 ikiwa mashirika mbalimbali na serikali licha ya kuchangia lakini ukosefu wa maji umekuwa tatizo si kwa binadamu tuu bali hata kwa mifugo ambapo hupelekea wananchi kununua maji hadi kwa shiringi mia 500.


  Kwaupande wa wananchi waliohudhulia mkutano huo wamekiri kuwapo kwa tatizo hilo ambalo imekuwapo kwa miaka mingi sasa hali inyopelekea wananchi upeleka mifugo yao kunywesha usiku wa manane hali ambayo ineza kuhatarisha usalama wa mifugo hiyo.


  Nao kinamama wamekiri kuwa tatizo hilo limekuwa likiwaathiri kiuchumi kwakuwa hutumia muda mwingi katika kutafuta maji bila kufanya shughuli nyingine kwaajiri ya kujenga uchumi wao na wanchi.

  0 0

  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha Msanii wa muziki wa dansi Ramadhan Ally Masanja (Banza Stone) kilichotokea nyumbani kwao Sinza jijini Dar es Salaam leo mchana siku ya Ijumaa ya tarehe 17/07/2015 baada ya kuugua kwa muda mrefu. 

  Banza Stone ni msanii na mdau wa muda mrefu wa sekta ya Sanaa nchini. Amekuwa na mchango mkubwa katika kukuza muziki wa dansi nchini hasa katika kubuni miondoko mbalimbali ambayo ilikuja kupata umaarufu mkubwa. Moja ya mwondoko uliopata umaarufu mkubwa ni ule wa “Achimenengule” akiwa na Bendi ya Tanzania One Theatre (TOT).

  Mchango wake katika muziki wa dansi hasa katika kubuni na kutunga nyimbo zenye ubora, ujumbe na maadili kwa jamii hautasahaulika kamwe. Ni mwanamuziki aliyeacha misingi katika sekta ya muziki na alijitolea kwa kiasi kikubwa katika kuufikisha muziki wa dansi mahali ulipo leo.

  Itakumbukwa kwamba mnamo Julai 3, 2015 BASATA na Asha Baraka, Mkurugenzi wa African Stars Entertainment (ASET) walichukua juhudi za makusudi kwenda nyumbani kwa msanii huyu kufanya mashauriano na familia yake ikiongozwa na kaka yake Khamis Ally Masanja na hatimaye kwa pamoja kumrejesha tena hospitalini kwa ajili ya matibabu yake.
  Hata hivyo pamoja na juhudi hizo za kupigania uhai wake Mungu kampenda zaidi Msanii mwenzetu Banza Stone. Upendo wetu kwake umezidiwa na ule wa mwenyezi Mungu ambaye kimsingi wote tutarejea kwake. 

  Baraza, wasanii na wadau wote wa Sanaa hatuna budi kuendelea kuenzi mema yote aliyotuachia marehemu Banza Stone hasa katika kupenda kujitolea muda mwingi katika kukuza muziki wa dansi na sekta ya muziki kwa ujumla.

  Baraza linatoa pole kwa ndugu wa marehemu, shirikisho la muziki, wasanii na wadau wote wa Sanaa katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.
  Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Amen
  Godfrey Mngereza
  KATIBU MTENDAJI


  0 0

  Katibu Msaidi Ofisi ya CCM Wilaya ya Kaskazini a Unguja Ndg Shafi Hamad akimkabidhi Fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Mkwajuni Amini Salimini, baada ya kukamilisha taratibu zote za malipo na kutimiza masharti ya Chama cha Mapinduzi.
  Katibu Msaidi wa CCM Wilaya ya Kaskazini A Unguja akitowa maelezo kwa mgombea baada ya kumkabidhi fomu hiyo Ndg Amini Salimini.
  Mgombea wa Jimbo la Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini A Unguja  Amini Salimini akiwa katika picha ya kumbukumbu na familia yake baada ya kuchukua Fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni kwa tiketi ya CCM, akiwa katika Ofisi za CCM Gamba.

  Mtoto wa Komando Dk Salmin Amour Juma Amini Salimini achukua Fomu kogombea Jimbo la Mkwajuni Zanzibar akiwasili katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kaskazini A Gamba kwa ajili ya kuchukua Fomu kogombea Jimbo hilo, akisalimiana na Wananchi waliopo hapo. 
  Mama wa Amini Salimi Bi Khadija Kasimi akisalimiana na Katibu Msaidi wa Ofisi ya CCM Wilaya Kaskazini A Unguja alipofika katika Ofisi hizo kumshindikiza Mtoto wake kuchukua Fomu ya Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Zanzibar. 
  Katibu Msaidizi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Kaskazini Unguja Ndg Shafi Hamad akitowa maelezo kwa Mgombea kabla ya kumkabidhi fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Jimbo la Mkwajuni
  Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Amini Salimini akihesabu fedha kwa ajili ya kulipia Fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge kupitia CCM katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kaskazini Unguja Gamba.
  Amini Salimini akiwa katika picha ya pamoja na familia yake baada ya kuchukua Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Mkwajuni Zanzibar.Akionesha fomu yake baada ya kukabidhiwa kwa hutua za ujazaji 
  Amini Salimini akitoka katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kaskazini A Unguja baada ya kuchukua fomu hiyo akionesha kwa wananchi walioko katika eneo hilo.
  Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini A Unguja Amini Salimini akiwa na Mtoto wake wa Kwanza wakishikilia fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuiwakilisha CCM katika Jimbo la Mkwajuni Zanzibar. 
  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Amani Salimini akiomba dua katika makaburi ya Wazee wake huko Kidombo baada ya kuchukua Fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Zanzibar
  Amini Salimini akipata dua kutoka kwa Wazee wa Kijiji cha Kidombo Mkwajuni baada ya kuchukua Fomu ya Kugombea Ubunge wa Jimbu la Mkwajuni Zanzibar kupitia CCM

  0 0

  Meneja wa Bayport Mkoani Lindi, Jovin Mapunda, kulia, akimkabidhi kiasi cha Shilingi Milioni moja mshindi wa Kopa Bayport, Said Mkinda, katika droo iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Fedha hizo alikabidhiwa juzi. Jovin Mapunda. Picha zote kwa hisani ya Bayport Financial Services.

  Washindi wanne wa Kopa Bayport wakabidhiwa fedha zao
  Na Mwandishi Wetu, Dar es SalaamWATEJA wanne wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, walioshinda Sh Milioni Moja kila mmoja katika bahati nasibu ya Kopa Bayport, wataisherehekea vizuri Sikukuu ya Eid el Fitr, baada ya kukabidhiwa fedha zao jana. Wateja hao ambao ni Simion Ngassa (Iringa), Sisco Haule (Kigoma), Phelis Nziku (Arusha) na Said Mkinda (Lindi), ambao washindi wote hawa walikabidhiwa fedha zao kwa kupitia Ofisi za Mkoa za Taasisi ya Bayport zilizoenea nchi nzima.
  Mteja wa Bayport Phelis Nziku wa Arusha kushoto akikabidhiwa kiasi cha Sh Milioni moja baada ya kushinda bahati nasibu ya Kopa Bayport.

  Akizungumzia hatua ya makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Mauzo wa Bayport Financial Services, Charles Mgeta, alisema kwamba ni furaha yao kuona washindi wao wote wamepata haki zao kutokana na kushinda kwenye shindano la Kopa Bayport.
  Mteja wa Bayport akipewa fedha zake
  Alisema wanaamini wateja hao wataendelea kufurahia huduma za Bayport zinazotoa picha halisi ya namna gani taasisi yao ina lengo la kuwakomboa na kuwakwamua pia kwa kutoa huduma bora kwa ajili ya maendeleo ya watanzania wote. “Kama tulivyotangaza hapo awali kwamba tulikuwa na washindi wanne waliokopa Bayport na kushinda Sh Milioni Moja kila mmoja, hivyo tumekabidhi kwa kupitia mameneja watu katika maeneo waliyoshinda wateja hawa.

  “Tunawaomba wateja wetu na Watanzania kwa ujumla kuendelea kutuunga mkono ili tuwapatie huduma bora kama vile mikopo ya bidhaa, mikopo ya fedha taslimu bila kusahau Bima ya Elimu kwa Uwapendao, huku huduma ya ukopaji kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz ukiwarahishia wateja wetu kukopa kwa njia ya haraka popote walipokuwapo,” alisema Mgeta.

  Kwa mujibu wa Mgeta, promosheni ya Kopa Bayport imeanzishwa kwa lengo la kuwashukuru wote wanaokopa kwenye taasisi yao, huku wahusika wakuu wakiwa ni wale wanaokopa kwenye taasisi yao inayoongoza kwa huduma bora za kifedha.%

older | 1 | .... | 586 | 587 | (Page 588) | 589 | 590 | .... | 1897 | newer