Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 585 | 586 | (Page 587) | 588 | 589 | .... | 1898 | newer

  0 0

  ????????????????????????????????????
  Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akizungumza na vijana  ambao hawana ajira  wenye elimu tofauti  katika viwanja vya Leadres jijini Dar es salaam, ambapo amekutana na vijana hao  ili kuzungumza nao kwa ajili ya kutatua tatizo lao lao la ajira . 

  DC Makonda amesema lengo la kuwaita vijana hao ilikuwa ni kuwakutanisha  wafahamiane na wabadilishane mawasiliano lakini pia wataunda vikundi vyao kulingana na taaluma zao na kila kundi litaandika miradi ipatayo mitano ili tuweze kuifanyia kazi kwa kuwatafutia mitaji au ufadhili baada ya miradi yao kubuniwa ,

  Ameongeza kwamba mpango huu utapunguza vijana kukaa bila kazi na kuingia katika vishawishi vya mimba kwa wasichana na na matukio yasiyo mema katika jamii. kama vile uhalifu na mengine mengi.

  Lakini pia amesema kuna makampuni mengi yameahidi kuchukua vijana wenye uwezo wa kufanya kazi kwani kwa kuwaunganisha vijana hao litakuwa ni jambo rahisi kupata wafanyakazi wa kuajiri , ikiwa ni pamoja na kuchukua vijana watakaofanya kazi kwa kujitolea na baada ya kuonyesha uwezo kazini wao wataajiriwa na mashirika au taasisi husika.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
  ????????????????????????????????????
  Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akizungumza na vijana hao kwenye viwanja vya Leaders
  ????????????????????????????????????
  Baadhi ya vijana wakiwa katika mkutano huo.
  ????????????????????????????????????
  ????????????????????????????????????
  Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari kutoka kituo cha televisheni cha Chanel Ten.

  0 0

  Wananchi na Wafuasi wa chama cha Mapinduzi CCM wakiwapokea kwa shangwe Mgombea Urais kwa tiketi ya chama hicho Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea mwenza Mh.Samia Suluhu Hassan mapema asubuhi hii mara baada ya kuwasili mjini Unguja -Zanzibar kujitambulisha kwa chama na Wananchi kwa ujumla.
   Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwa kwenye gari la wazi pamoja na mgombea mwenza Mhe.Samia Suluhu Hassan kwenye mitaa ya Michenzani Zanzibar.

  Mhe. Magufuli aliwasili Zanzibar kwa lengo la kutambulishwa kwa wanachama wa CCM Zanzibar akiongozana na mgombea mwenza Mhe.Samia Suluhu Hassan ambapo wote kwa pamoja walipata kuwasalimia wananchi wa Zanzibar kwenye viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
   Maelfu ya watu wakiufuata msafara wa mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Mhe. John Pombe Magufuli aliyeongozana na mgombea mwenza Mhe. Samia Suluhu Hassan.
   Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akivishwa skafu na chipukizi wa CCM Zanzibar mara baada ya kuwasili Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
   Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu na chipukizi wa CCM nje ya jengo la Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.


   Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akisalimiana na wazee maarufu wa Zanzibar
   Mhe. Magufuli akiwasili kwenye kaburi la muasisi wa Mapinduzi na Rais wa Kwanza wa Serikali Mapinduzi ya Zanzibar ,Hayati Sheikh Abeid Amani Karume
   Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John P.Magufuli pamoja na mgombea mwenza Mhe. Samia Suluhu Hassan wakiomba dua mbele ya kaburi la Hayati Abeid Aman Karume muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar.


   Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Wageni kwenye Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.

   Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Magufuli nje ya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kwenye sherehe fupi ya kutambulishwa wagombea wa CCM kwa wanachama wa CCM.
    Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mgombea Mwenza Mhe. Samia Hassan Suluhu.
   Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Mhe. John Magufuli akiwasalimu wananchi waliojitokeza kwenye sherehe fupi za kumtambulisha kwenye viwanja vya Afisi Kuu CCM Zanzibar.

   Kila mtu alitaka kumgusa.
   Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Zanzibar waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya Afisi Kuu Zanzibar kwenye sherehe fupi ya kumtambulisha kwa wanachama pamoja na mgombea mwenza Mhe. Samia Suluhu Hassan,kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM(Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe.Ali Mohamed Shein.
   Wananchi wakishangilia.
   Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akihutubia wakazi wa Zanzibar waliojitokeza kwa wingi kushuhudia sherehe fupi za kutambulishwa kwa wagombea wa nafasi ya Urais kwa kupitia CCM kwenye viwanja vya Afisi Kuu.


   Mgombea mwenza wa nafasi ya Urais Mhe. Hassan Suluhu Hassan akizungumza kwenye sherehe fupi za utambulisho nje ya Afisi kuu ya CCM Zanzibar.
   Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli akiwasalimu wakazi wa Zanzibar waliojitokeza kwa wingi kwenye sherehe za kumtambulisha yeye na mgombea mweza kwenye viwanja vya Afisi Kuu Zanzibar.
   Wakazi wa Zanzibar wakimsikiliza mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Magufuli kwenye viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
   Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na mgombea wa ueais kwa kupitia CCM Dk.John Magufuli.

  0 0

   Meneja wa TTCL Mkoa wa Mbeya, James Mlaguzi akisoma taarifa ya msaada uliotolewa na kampuni hiyo katika shule ya Sekondari Luswisi.
   Mbunge wa Ileje aliyemaliza muda wake,Aliko Kibona akitoa shukrani kwa niaba ya  wananchi wa Kata ya Luswisi kwa kampuni ya TTCL kutokana na msaada waliopokea.
   Mbunge Aliko Kibona pamoja na Meneja wa TTCL wakikabidhiana mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu.
   Mbunge na Meneja wakipongezana baada ya kukabidhiana Saruji na Mbao.
   Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Luswisi wakifurahia msaada uliotolewa na TTCL.

   Wanafunzi wakisaidia kushusha mifuko ya saruji iliyotolewa na kampuni ya TTCL.
   Watumishi wa TTCL Mbeya wakijadiliana jambo kabla ya kuanza makabidhiano ya msaada wa saruji na mbao katika shule ya sekondari Luswisi.
   Baadhi ya wanakijiji waliojitokeza kupokea msaada huo.
   Watumishi wa TTCL Mbeya wakimsikiliza Mbunge alipokuwa akitoa shukrani kwa  niaba ya wananchi.

    Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Luswisi, Mseven Ndangalaakielezea furaha yake baada ya kupokea msaada wa saruji na mbao kutoka TTCL.
   Ngoma za asili zikiendelea kutoa burudani katika hafla ya kukabidhiana msaada wa saruji na Mbao. 

  *************
  KAMPUNI ya simu ya TTCL imetoa msaada wa saruji na mbao katika Shule ya Sekondari ya Luswisi iliyopo Kata ya Luswisi Wilaya ya Ileje mkoani Mbeya kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mbili za Walimu na chumba kimoja cha darasa.
  Kampuni hiyo ilitoa msaada wa mifuko 100 ya saruji na mbao vyenye thamani ya shilingi Milioni tatu ikiwa ni kupunguza changamoto inayowakabili Walimu wa Shule hiyo ambayo inawalimu 22 huku ikiwa na Nyumba moja iliyokamilika ambayo anaishi Mkuu wa Shule.
  Wakizungumza baada ya kupokea msaada huo baadhi ya Walimu hao wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Shule, Mseven Ndangala, alisema Walimu wanaishi katika wakati mgumu kwani asilimia kubwa wamepangishwa na wanakijiji sehemu ambayo ni mbali na eneo la shule.
  Alisema Walimu wengi wamepanga umbali wa kilomita 7 kutoka shuleni hivyo hulazimika kukodi pikipiki kuwapeleka na kuwarudisha shule kwa gharama ya shilingi 6000 kwa siku hali inayowarudisha kwenye umaskini na kupunguza ari ya kufundisha kutokana na kutumia gharama kubwa kwenye usafiri.
  Aliongeza kuwa hivi sasa kuna walimu wapya watano ambao kwa mazingira yalivyo hawataweza kupanga kutokana na ukosefu wa fedha na kuwalazimu kuishi walimu wote watano kwenye chumba kimoja hali inayoonesha kuwakatisha tama kuendelea kufundisha shuleni hapo.
  Awali akikabidhi msaada huo, Meneja wa TTCL Mkoa wa Mbeya, James Mlaguzi, alisema Kampuni ilipata maombi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Ileje, Aliko Kibona kwa ajili ya kusaidia kupunguza adha hiyo jambo ambalo lilikubaliwa na hatimaye kuwafikishia.
  Alisema kampuni imejipanga kuhakikisha mwishoni mwa mwaka huu inapeleka huduma za mawasiliano vijijini ili kuwawezesha wakulima kutafuta masoko ya mazao yao kwa njia za mtandao.
  Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ileje aliyemaliza muda wake, Aliko Kibona aliwashukuru kampuni ya TTCL Hususani Afisa mtendaji Mkuu Dk. Kazaula Kamugisha kwa kumkubalia ombi lake ili kuhakikisha walimu wanakuwa na mazingira mazuri ya kufundishia kwa kuwajengea nyumba nzuri.
  Aidha alitoa wito kwa Watendaji wa vijijini na Kata kuhakikisha wanasimamia vizuri msaada huo kwa kuhakikisha unafanya kazi zilizokusudiwa ili kuwaridhisha waliotoa misaada na hivyo kuwafanya wawe na moyo wa kujitolea katika kipindi kingine.
  Aliongeza kuwa ni wajibu wa Wabunge, wadau na wananchi kuhakikisha wanatumia kila njia wanatengeneza mazingira mazuri ya Walimu kuwa na ari kubwa ya kufundisha kuliko kuitegemea Serikali kwa kila kitu.


  0 0

   Mkuu wa Matawi wa Benki ya Exim, Bi Elizabeth Mayengo (wa pili kulia) na Meneja Mahusiano wa benki hiyo, Bi. Violet Bikoche (wa pili kushoto) wakibadilishana mawazo na baadhi ya wateja wa benki hiyo wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
   Baadhi ya wateja wa Benki ya Exim wakishiriki futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan jijini Dar es Salaam  hivi karibuni.
  Mkuu wa Matawi wa Benki ya Exim, Bi Elizabeth Mayengo (kulia) akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

  0 0

  1
  Naibu katibu Mkuu wa Chadema tawi la zanzibar Salum Mwalim akielezea maswala mbalimbali kuhusiana na hali ya Usalama kuelekea katika Uchaguzi mkuu katika hafla ya utiaji Saini waraka wa maadili ya Uchaguzi kwa vyama vya Siasa Grand Palas Zanzibar
  2
  Baadhi ya Wajumbe wa vyama vya Siasa waliohudhuria katika hafla ya utiaji Saini waraka wa maadili ya Uchaguzi kwa vyama vya Siasa Grand Palas Zanzibar. 
  3
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya ZEC Nassor Khamis Mohammed akifafanua baadhi ya mambo katika hafla ya utiaji Saini waraka wa maadili ya Uchaguzi kwa vyama vya Siasa Grand Palas Zanzibar.
  4
  Naibu Katibu Mkuu wa ATC-Wazalendo Juma Said Sanani akitia saini waraka wa maadili ya Uchaguzi kwa vyama vya Siasa Grand Palas Zanzibar.
  5
  Mwakilishi wa CCM Hafidh Ali akitia saini waraka wa maadili ya Uchaguzi kwa vyama vya Siasa Grand Palas Zanzibar. 
  6
  Naibu katibu Mkuu wa Chadema tawi la zanzibar Salum Mwalimakitia saini waraka wa maadili ya Uchaguzi kwa vyama vya Siasa Grand Palas Zanzibar.

  0 0

  Kada wa Chama cha Mapinduzi,Octavian akimtambulisha mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Davis Mosha kwa wakazi wa Moshi waliofika katika uwanja wa Mashujaa.
  Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Davis Mosha akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa mjini Moshi.
  Baadhi ya wananchi waliofika katika mkutano huo.
  Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Davis Mosha akisalimiana na wakazi wa Moshi waliofika katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa.


  Baadhi ya wakazi wa mji wa Moshi mjini wakiwa katika uwanja wa Mashujaa katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mtangaza nia wa nafasi ya Ubunge wa jimbo la Moshi mjini ,Davis Mosha.
  Mtangaza nia ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Davis Mosha ,akiwa na meneja kampeni wake Voctor (kushoto kwake pamoja na Goodluck Moshi.
  Baadhi ya makada waliofika katika uwanja huo.
  Msanii wa filamu Tanzania Stephen Mengere maarufu kama Steve Nyerere alikuwa ni mmoja wa makada wa chama hicho waliofika kutoa hamasa katika mkutano  huo uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa.
  Baadhi ya kina mama waliofika katika mkutano huo.
  Baadhi ya vijana wakiwa na mabango yao waliofika katika mkutano huo.
  Wasanii wa Bongo Movie walipamba mkutano huo.
  Baadhi ya wananchi wa Moshi mjini waliofika katika mkutano huo wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali.
  Davis Mosha akizungumza na waandishi wa habari marabaada ya mkutano wake wa kutangaza nia.
  Mtia nia wa nafasi ya Ubunge Davis Mosha akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara mjini Moshi waliofika katika mkutano huo.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  download
  Tunaelekekea kipindi hiki cha kusherehekea sikukuu ya Eid-El-Fitr na ambapo wananchi wenye imani ya kiislam na hata madhehebu mengine hutumia muda huo kwenda kuabudu pamoja na muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya starehe, Jeshi la Polisi nchini linatoa wito kwa wananchi wote kuwa makini na kusheherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.

  Jeshi la Polisi nchini linapenda kuwaondoa hofu wananchi kuwa, limejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wanasherehekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu. Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote.

  Aidha,  tahadhali zichukuliwe kwa wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara ikiwemo maderera na watembea kwa miguu, kuwa makini kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kwenda mwendo kasi na kutumia vilevi wawapo kazini.

  Jeshi la Polisi linaendelea kuwasisitiza wananchi kutoa taarifa haraka kwenye vyombo vya dola juu ya kitu chochote ama mienendo ya watu watakaowatilia shaka mahali popote kwani taarifa hizo za haraka zitasaidia kuzuia uhalifu kabla haujatokea.

  Vilevile wananchi wachukue tahadhari watokapo kwenye makazi yao, wasiache nyumba wazi ama bila mtu na endapo italazimika basi ni vema watoe taarifa kwa majirani zao kwa ajili ya usalama.
  TUNAWATAKIA WATANZANIA WOTE SIKUKUU NJEMA YA EID –EL-FITR 
  Imetolewa na: Advera John Bulimba-SSP
  Msemaji wa Jeshi la Polisi
  Makao Makuu ya Polisi.

  0 0

  unnamed
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dkt. Ibrahim Mzengi wakati aliposoma taarifa fupi ya mkoa huo baada ya Waziri Mkuu kuwasili Mpanda mkoani Katavi kwa mapumziko mafupi  Julai 15, 2015. Kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Emmanuel Kalobelo.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  0 0


  1

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania, Lennarth Hjelmaker, wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 16, 2015 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
  2
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania, Lennarth Hjelmaker, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 16, 2015 alipofika kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.

  0 0

  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets with South Centre Executive Director Martin Khor in Geneva this afternoon .President Kikwete is in Geneva to attend the High Level Panel on the Global Response to Health crises.
  The Chairman of the High Level Panel on the Global Response to Health crises President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with Celso Amorim a panel member from Brazil during one of the consultative sessions held at World Health Organization(WHO) Headquarters in Geneva this morning. (photos by Freddy Maro)

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya Kushoto akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Ibrahim Msengi Mwenge wa Uhuru baada ya kumaliza ziara yake Mkoani Rukwa na kuanza ziara zake Mkoani Katavi tarehe 15 Julai 2015. 
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (wa nne kulia mbele) na wakimbiza mwenge kitaifa na kimkoa wakiukimbiza Mwenge wa Uhuru kwa ajili ya kuukabidhi Mkoani Katavi tarehe 15 Julai 2015 baada ya kumaliza ziara yake Mkoani Rukwa.
   Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta (wa kwanza mbele) na wakimbiza Mwenge kitaifa na kimkoa wakiukimbiza Mwenge wa Uhuru Wilayani Nkasi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi wa maji katika Kijiji cha Kalundi Wilayani humo tarehe 14 Julai 2015. 
  Moja ya mtambo wa kisasa wa umwagiliaji katika shamba la umwagiliaji la Ntatumbila Wilayani Nkasi. Mradi huu wa shamba la umwagiliaji na mifugo lina ukubwa wa hekta 1,000 na linamilikiwa na kuendeshwa na wazawa ambapo mpaka kukamilika kwake utagharimu fedha za kitanzania shilingi bilioni 46.
  Miongoni mwa wamiliki wa shamba hilo na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa ndugu Juma Khamis Chum wakipiga picha ya pamoja na Mwenge wa Uhuru mara baada ya uzinduzi wa mradi wa umwagiliaji katika shamba hilo la Ntatumbila Wilayani Nkasi.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

  0 0

  ????????????????????????????????????
  Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akisalimiana na Diwania wa Kata ya Bwilingu Bw, Ahmed Masser wakati alipowasili katika eneo la mkutano uliofanyika mji mdogo wa Chalinze jana ukiwa na lengo la kuelezea utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM uliofanywa na Mbunge huyo kwa kipindi cha mwaka mmoja katika huduma za Afya, Elimu, Maji, Miundombinu, Uchumi, Michezo na amaendeleo mengine ya kijamii.

  Mh. Ridhiwania Kikwete ametanganza rasmi jana katika mkutano huo nia yake ya kutetea jimbo la Chalinze ambapo leo mchana anatarajiwa kuchukua fomu katika ofisi za CCM wilaya ya Bagamoyo tayari kwa kuanza mchakato wa kuwania tena ubunge wa jimbo la Chalinze ili kuendeleza yale aliyokwishayaanza kutekeleza katika kipidi cha mwaka mmoja alipokuwa madarakani.
  ????????????????????????????????????
  Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akisalimiana na wananchi mbalimbali wakati alipowasili katika eneo la mkutano mjini Chalinze.
  ????????????????????????????????????
  Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akizungumza jambo na Katibu wake Bw. Idd Swala huku Diwani wa Kata ya Bwilingu Ahmed Nasser akisikiliza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Bw.ndugu Majid Mwanga.
  ????????????????????????????????????
  Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ndugu Majid Mwanga.


  ????????????????????????????????????
  Diwani wa Kata ya Bwilingu Ahmed Nasser akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze jana.
  ????????????????????????????????????
  Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ndugu Majid Mwanga akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze jana.
  ????????????????????????????????????
  Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akizungumza na wananchi mjini Chalinze wakati alipotangaza nia yake ya kutetea tena ubunge wa jimbo hilo.
  ????????????????????????????????????
  Wananchi wa Chalinze wakimsikiliza Ridhiwania Kikwete mbunge wa jimbo hilo hayupo pichani wakati alipokuwa akitangaza nia yake ya kutetea tena kiti cha ubunge wa jimbo la Chalinze.
  ????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi kadi msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho. Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi kadi msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi aliyekuwa Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi, Deo Meck alipotangazwa kujiunga na chama hicho rasmi leo jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi aliyekuwa Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi, Deo Meck alipotangazwa kujiunga na chama hicho rasmi leo jijini Dar es Salaam.Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi kadi na katiba msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho. Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi kadi na katiba msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa akizungumza na waandishi wa habari leo alipowapokea baadhi ya wanachama wapya wa ACT-Wazalendo. Kushoto ni Katibu wa Kampeni na Uchaguzi, Mohamed Masaga na kulia ni Deo Meck mwanachama mpya wa ACT Wazalendo. Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa akizungumza na waandishi wa habari leo alipowapokea baadhi ya wanachama wapya wa ACT-Wazalendo. Kushoto ni Katibu wa Kampeni na Uchaguzi, Mohamed Masaga na kulia ni Deo Meck mwanachama mpya wa ACT Wazalendo.
  Msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' akizungumza na waandishi wa habari alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho. Msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' akizungumza na waandishi wa habari alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.[/caption] MSANII maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' amejiunga na chama kipya cha siasa cha ACT Wazalendo. Frank amejiunga na chama hicho leo jijini Dar es Salaam akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM). Katika hafla hiyo ya utambulisho kiongozi mwingine ambaye ni Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi, Deo Meck pia amejiunga na chama cha ACT Wazalendo na kukabidhiwa kadi za chama hicho. Akiwakabidhi kadi za ACT-Wazalendo, Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa leo Makao Makuu ya ACT alisema wamewapokea wanachama hao wapya kwa mikono miwili na wapo tayari kushirikiana nao ndani ya chama hicho. 
  Alisema kuna idadi kubwa ya vigogo kutoka vyama vingine ambao tayari wameomba kujiunga na chama chao na taratibu zinafanywa kutambulishwa. "...tendo hili la leo la kuwakaribisha vijana hawa ni mwanzo wa kuwatambulisha wanachama mbalimbali wakiwemo wabunge na viongozi wa vyama waliojiunga nasi baada ya kuvunjwa kwa Bunge. Tayari tunao baadhi ya watu waliokuwa wabunge na wameshajiunga nasi na mchakato wa kuwatambulisha unaendelea katika maeneo mbali mbali nchini," alisema Mtemelwa. Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimtambulisha aliyekuwa Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi, Deo Meck alipotangazwa kujiunga na chama hicho rasmi leo jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimtambulisha aliyekuwa Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi, Deo Meck alipotangazwa kujiunga na chama hicho rasmi leo jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_59599" align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kwenye mkutano wa ACT Wazalendo. Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kwenye mkutano wa ACT Wazalendo.[/caption] Akizungumzia mchakato wa uchukuaji fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho, Mtemelwa alisema Julai mosi mwaka huu Chama Cha ACT-Wazalendo kilifungua rasmi pazia la uchukuaji fomu za kugombea nafasi mbalimbali zikiweno za Udiwani, Ubunge na Urais. Alisema tangu kuanza kwa uchukuaji huo wa fomu kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wanachama kuchukua fomu na hadi sasa kuna baadhi ya majimbo na kata zina watia azma kuanzia wanne mpaka tisa jambo ambalo alidai ni faraja kwa ACT Wazalendo.

   "Kati ya majimbo 265 yakiwamo majimbo mapya 26 yaliyoongezwa hivi karibuni na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), ACT-Wazalendo tumeshakuwa na waweka azma zaidi ya mmoja katika majimbo 226 kwa nchi nzima na tunaamini mpaka kufikia mwisho wa uchukuaji fomu ndani ya Chama majimbo yote 265 yatakuwa yanawatia azma mbalimbali wanaosubiri kupitishwa na chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu," aliongeza Naibu Katibu Mkuu huyo wa ACT Wazalendo. 

   Alibainisha kuwa kichama mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu kwa nafasi ya udiwani ni julai 24, kwa nafasi ya Ubunge mwisho ni Julai 31 na kwa nafasi ya Urais mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Agosti Mosi, 2015. "Kwa ngazi ya Taifa Halmashauri kuu itakutana Agosti 13 kwa ajili ya kuteua jina la mgombea Urais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na kupendekeza majina ya wagombea Urais kwenye mkutano mkuu. Agosti 13, Mkutano mkuu utamchagua mtu atakayepeperusha bendera ya Chama cha ACT Wazalendo katika mbio za urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania." 

  "Hivi karibuni tumepokea taarifa kutoka katika miji ya Tarime na Rorya Mkoani Mara kuwa kuna watu wanapita na kutangaza kuwa Chama chetu kimezuiwa kushiriki Uchaguzi kwa muda wa miezi sita. Tumebaini lengo la upotoshaji huu ni kuwakatisha watanzania tamaa juu ya ukuaji wa Chama Cha ACT-Wazalendo pamoja na dhamira yake nzuri ya kuirudisha nchi katika misingi iliyoachwa na hayati Mwalimu Julius Nyerere. 

   "Tunawataarifu wananchi kuwa Chama chetu kitashiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu kwa kuweka wagombea wa nafasi zote na Chama hakitakuwa tayari kuona sehemu yoyote ya nchi mgombea wa CCM anapita bila kupingwa," alisisitiza Naibu Katibu Mkuu huyo wa ACT Wazalendo. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0


   Amiri wa Jumuiya ya Answari Suna Tanzania, Shekh. Juma Omari Poli (kulia), akiswalisha Swala ya Iddi katika viwanja hivyo.
   Shekh Hamid Abdallah, akitoa mawaidha wakati wa ibada ya Swala ya Idi katika Viwanja vya Jangwani Dar es Salaam leo.

  Waumini wa dini ya kiislam wakiwa kwenye ibada hiyo.
   Waumini wa madhehebu ya Anwar-Suni wakiswali katika viwanja hivyo.

  0 0

   The United Nations High Commissioner for Refugees UNHCR Mr.Antonio Guterres welcomes to his Geneva office President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete The President paid a courtesy call on him today and held talks on the influx of Refugees in Tanzania
    The United Nations High Commissioner for Refugees UNHCR Mr.Antonio Guterres introduces President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete to him some of his senior staff members.
  The United Nations High Commissioner for Refugees UNHCR Mr.Antonio Guterres and President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete shake hands when the nlatter paid a courtesy call on him today and held talks on the influx of Refugees in Tanzania. Photos by Freddy Maro

  0 0

  Mkuu wa Matawi wa Benki ya Exim, Bi Elizabeth Mayengo (aliyesimama) akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi.
   Mkuu wa Hazina Benki ya Exim Bank Tanzania, Bw. George Shumbusho akitoa neon la shukrani kwa wateja na wageni waalikwa wa benki hiyo waliohuzuria hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan jijini Dar es Salaam juzi. 
   Mkuu wa Huduma za rejareja kutoka benki ya Exim Tanzania, Bw. Raul Singh (wapili kulia waliosimama)na Meneja wa benki hiyo tawi la Samora Bi. Hawa Msangi (wa kwanza kutoka kulia) wakibadilishana mawazo na baadhi ya wateja wa benki hiyo wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi.
  Meneja wa Benki ya Exim tawi la Namanga jijini Dar es Salaam, Bi. Anna Wesiwasi (aliyesimama) akizungumza na baadhi ya wateja na wageni waalikwa wa benki hiyo waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan jijini Dar es Salaam juzi.

  0 0

  Kiwanda cha saraji cha Lafarge kilichopo Mbeya. Kiwanda hiki ni maarufu kwa utengenezaji wa saruji, kokoto na zege.
  Wafanyakazi wa kiwanda cha saruji cha Lafarge kilichopo Mbeya wakiwa kwenye picha ya pamoja. Lafarge ni mdau mkubwa katika bishara ya Saruji, Kokoto na Zege.

  Kampuni mbili zinazoongoza katika sekta ya ujenzi hapa nchini, Lafarge S.A. na Holcim Ltd zimekamilisha muungano wao uliosubiriwa kwa muda mrefu na kuunda kampuni moja itakayo fahamika kwa jina la LafargeHolcim.

  Vigezo muhimu vya kukamilisha muungano huo vimeafikiwa hivi karibuni kufuatia ubadilishaji wa umiliki pamoja na kutolewa kwa hisa mpya za Holcim kwenda kwa wanahisa wa Lafarge.

  Wanahisa wa kampuni ya Holcim walipitisha azimio hilo la muungano katika mkutano mkuu uliofanyika Mei 8, 2015.  

  0 0


   Baadhi ya washiriki wakiwa kazini katika kutengeneza filamu mfupi
   Baadhi ya washiriki wakiwa makini huku sura zao zikiwa na majonzi na wasiwasi juu ya washiriki gani wanaooaga shindano kwa wiki hii.
   Baadhi ya watazamaji waliojitokeza katika kushuhudia mtanange wa washiriki wanaaga mashindano katika wiki hii na kushuhudia wanaoingia katika jua la utosi
   Walimu wa Washiriki wa Shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke kutoka Kushoto Ni Mwl Issa na Dkt Mona Mwakalinga wakifuatilia kazi ya wanafunzi wao katika kipindi cha TMT 2015 #mpakakieleweke
   Majaji wa Shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke wakifurahia show ya washiriki wa TMT waliobahatika kuendelea na shindano hilo mara baada ya washiriki wengine kuaga mashindano hayo kutokana na kura kutotosha.
   Mahosti wa Kipindi cha TMT 2015 #mpakakieleweke wakifurahia kazi yao wakati wa kipindi cha TMT kinachorushwa kila jumapili saa tatu na nusu usiku kupitia kituo cha ITV
  Baadhi ya washiriki wa TMT 2015 #mpakakieleweke wakiwa mbele ya majaji tayari kwa kutaja waliongia hatua ya jua la utosi.
  Na Josephat Lukaza.
  Shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke limeingia hatua nyingine tena mara baada ya washiriki wengine kuaga shindano hilo . Katika hatua hiyo ya mchujo hali imezidi kuwa ngumu kwa washiriki kutokana na shindano kuwa gumu kwao kila wiki. Mpaka sasa jumla ya washiriki wanne wameshaaga shindano hilo huku mchuano ukiwa mkali kwa washiriki waliobakia.
  Ili kuweza kumbakiza mshiriki umpendae unachotakiwa kufanya ni Kumpigia kura kadri uwezavyo ili kumnusuru na kuaga shindano ambalo limejizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya Nchi ya Tanzania kutokana na ubora wake na uwajibikaji na ubunifu wa shindano hilo
  Jinsi ya kumpigia kura mshiriki umpendae unachotakiwa kufanya ni Kuandika ujumbe mfupi wa Maneno TMT ikifuatiwa na namba ya mshiriki halafu tuma kwenda namba 0784 36 77 38.
  Kufahamu ni nani na nani wameaga shindano hili kwa wiki hii basi usikose kufuatilia kipindi cha TMT 2015 #mpakakieleweke kupitia kituo cha runinga cha ITV kila siku ya Jumapili saa tatu na nusu usiku.
  Shindano la TMT limepigwa Tafu na I-View Studio, Precision Air, Global Publishers, Paisha, Cam Gas, Radio One na ITV pamoja na Pepsi

  0 0

   Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Lusajo Willy akijaza akiwa na fomu yake mara baada ya kuchukua katika Ofisi Kuu ya CCM wilaya ya Kinondoni leo. 
   Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Lusajo Willy akichukua fomu ya kuwania jimbo hilo kutoka kwa Katibu wa CCM wilaya ya Kinondoni, Othuman Salum Shesha  jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
   Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Lusajo Willy akichukua fomu ya kuwania jimbo hilo kutoka kwa Katibu wa CCM wilaya ya Kinondoni, Othuman Salum Shesha  jijini Dar es Salaam. 
   Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Lusajo Willy akipeana mkono na Katibu wa CCM wilaya ya Kinondoni, Othuman Salum Shesha.
   Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Lusajo Willy akijaza fomu. 
   Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Lusajo Willy akijaza fomu. 
   Katibu wa CCM wilaya ya Kinondoni, Athuman Salum Shesha akitoa maelezo muhimu kwa mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Lusajo Willy akijaza fomu. 
    Katibu wa CCM wilaya ya Kinondoni, Athuman Salum Shesha akikabidhi fomu kwa mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Lusajo Willy. 
  Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Lusajo Willy akisalimiana na wadau mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Kinondoni. 
    Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Lusajo Willy akiwa na wapambe waliomsindikiza kuchukua fomu ya kuwania ubunge jimbo la Kinondoni.


  0 0


   Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba(Kushoto) akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili ofisini kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akimueleza Dkt. Ally Yahaya Simba (Kushoto) umuhimu wa kuendelea kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya mawasiliano,alipomtembelea leo ofisini kwake.
    Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga na kumhakikishia kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi ya Taifa hasa katika kuiendeleza Sekta ya Mawasiliano Nchini.
   1-    Watendaji wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (mwenye suti nyekundu) alipotembelewa na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba (kulia kwa Katibu Mkuu) aliyeteuliwa kushika nafasi ya Prof. John Nkoma aliyemaliza Muda wake.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwaeleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Hawapo pichani), walipotembelewa na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba.Kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Raphael Hokororo
   Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiagana na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba(kushoto) Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

older | 1 | .... | 585 | 586 | (Page 587) | 588 | 589 | .... | 1898 | newer