Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

TASWIRA MBALIMBALI KUTOKA KWENYE MKUTANO MKUU WA CCM MJINI DODOMA USIKU HUU

0
0
 Meza Kuu ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete tayari kwa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi unaoendelea usiku huu kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CCM wa Dodoma Convition Centre, uliopo njia ya Kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na aliekuwa Mgombea Urais na Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CCM wa Dodoma Convition Centre, uliopo njia ya Kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, Mjini Dodoma.
 Baadhi ya Wake wa Viongozi wakiwa kwenye Mkutano huo.
 Mmoja wa Wagombea Urais alieingia kwenye hatua ya tatu bora, Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya wajumbe wa Mkutano huo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Aliekuwa Mgombea Urais na Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM unaofanyika usiku huu kwenye Ukumbi wa Dodoma Convition Centre, uliopo njia ya Kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, Mjini Dodoma.
 Mmoja wa Wagombea Urais alieingia kwenye hatua ya tatu bora, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya Mabalozi walioalikwa kwenye Mkutano huo.

SEHEMU YA SHAMRA SHAMRA NDANI YA UKUMBI WAKATI WA MKUTANO MKUU WA CCM

0
0


SPORTS XTRA NDONDO CUP YAZINDULIWA RASMI, ABAJALO, FC KAUZU MUZIKI WAO..OGOPA SANA!

0
0
3Baada ya kuisubiri kwa muda mrefu burudani hii adimu! Sasa utamu umewadia!!

Msimu wa pili wa mashindano ya Sports Xtra Ndondo Cup chini ya udhamini wa Dr. Mwaka, Daktari bingwa wa masuala ya Afya ya uzazi na Tiba asilia kutoka kituo cha Foreplan Clinic, kilichopo Bungoni, Ilala, Dar es salaam umezinduliwa rasmi katika uwanja wa Bandari, Tandika, jijini Dar es salaam.

Mechi ya ufunguzi yenye mvuto wa aina yake imepigwa jana ikiwakutanisha mabingwa watetezi, Abajalo FC ya Sinza Dar es salaam dhidi ya timu iliyojizolea Umaarufu ya wauza mitumba wa Tandika, FC Kauzu na hadi dakika 90 zinamalizika wanaume hao wa ‘Shoka’ walitoka suluhu (0-0).
5Sports Xtra Ndondo Cup ni mashindano yenye heshima kubwa kwa sasa na kwa kulitambulia hilo, Mgeni rasmi alialikwa kufungua pazia ambaye ni Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF anayewakilisha mkoa wa Dar es salaam, Wilfred Kidau akiambatana na mwenyekiti wa chama cha soka cha Dar es salaam (DRFA), Almas Kasongo pamoja na mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Temeke (TEFA), Peter Muhinzi.
4
2Kwa wale ambao hawakushuhudia!, hakika mechi ya ufunguzi ilikuwa nzuri mno ikichagizwa na wachezaji wa ligi kuu wanaokipiga katika michuano hayo, mfano FC Kauzu walimtumia mshambuliaji hatari wa Kagera Sugar, Atupele Green na ngome ya ulinzi iliongozwa na beki wa Mbeya City, Juma Said Nyosso.
7Cha kufurahisha! FC Kauzu wanatumia jezi za Zambarao kama ilivyo kwa Mbeya City FC, hivyo Nyosso alionekana kama anakipiga katika kikosi hicho cha Juma Mwambusi. Abajalo FC wao walikuwa na mtu kama Paul Maona na nahodha wao George Kavila wanaokipiga Kagera.
8
Mashabiki zaidi ya Elfu tano walihudhuria mechi hiyo iliyojaa vitimbwi, mbembwe za kila aina na nimekuwekea baadhi ya picha zikionesha shamrashamra za mashabiki wa Sports Xtra Ndondo Cup Chini ya udhamini wa Dr. Mwaka.
6

FUATILIA MKUTANO MKUU WA CCM LIVE KUPITIA HAPA HAPA JAMVINI

0
0

MAANDAMANO YA AMANI YA WADAU WA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI YAFANYIKA LEO JIJINI DAR

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
IMEELEZWA kuwa nchi zilizoendelea ndio zinaongoza katika uharibifu wa mazingira kwa utumiaji wa Nuklia ,pamoja na uchimbaji wa Chuma hivyo zinawajibu kuwekeza katika mabadiliko tabia nchi kutokana na kuchangia hali hiyo .

Hayo ameyasema leo Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabia Nchi Tanzania (CAN),Sixbaty Mwanga wakati wa matembezi ya amani ya Mabadiliko ya Tabia ya Nchi yaliyofanyika  viwanja vya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Amesema mabadiliko ya tabia ya nchi yamezidi kukua kwa kasi kutokana na uharibuifu wa mzingira unaofanywa na binadamu kwa shughuli za kila siku  huku jitihada za kukabili mabadiliko hayo zikichukua asilimia ndogo.

Mwanga amesema malengo 17 ya maendeleo endelevu ya tabia ya nchi  ya mwaka 2015 -2030  kunahitaji viongozi kushughulikia katika vyanzo mbalimbali vya fedha katika kuweza kufikia malengo na  kushindwa kufanya hivyo kutakuwa na madhara ya ukame,njaa, vifo pamoja na mafuriko.

Aidha amesema kuna mikutano mbalimbali inakuja hivyo ni kila mtu kwa nafasi yake ashiriki katika kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi katika nchi iweze kuwa na uchumi imara.

 Wadau wa mabadiliko ya tabia ya nchi wakiwa pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya JKT Jitegeme wakihamasisha urtunzaji wa mazingira katika maandamano ya amani ya kupiga vita mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam leo.
 Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya JKT Jitegemee ya jijini Dar es Salaam wakiwa na mabango mbalimbali yenye jumbe tofautitofauti ili kuhamasisha yamii kuachana na uchafuzi wa mazingira ili kuokoa maisha ya watanzania kutokana na kuwa na majamba mbalimbali yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia  ya nchi, katika maandamano ya amani ya kupiga vita mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam leo.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya JKT Jitegemee wakiimba wimbo unaohamasisha utunzaji wa mazingira ili kuepukana na uchafunzi wa mazingira kwa njia mbalimbali, katika maandamano ya amani ya kupiga vita mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam leo.
Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabia Nchi Tanzania (CAN),Sixbaty Mwanga akizungumza na wadau wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia  ya nchi mara baada ya kuhitimisha maandamano ya amani yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam leo. 


Picha ya pamoja ya wadau mbalimbali wa kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi wakiwa na mabango ambayo yanahamasisha utunzaji wa mazingira pamoja na ujumbe wa kuokoa maisha ya jamii kwa kutunza mazingira, katika maandamano ya amani ya kupiga vita mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam leo. Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

NI DKT JOHN POMBE MAGUFULI KUIPEPERUSHA BENDERA YA CCM KITI CHA URAIS,AIBUKA NA ASILIMIA 87.1 YA KURA.

0
0





Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Dkt. John Pombe Magufuli kuwa ndie Mgombea Urais wa CCM


Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikumbatiana na Dkt. John Pombe Magufuli, mara baada ya kutangazwa kuwa ndiye Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, mchana huu hapa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Dodoma Convition Centre, Mjini Dodoma. Dkt. Magufuli ameibuka kidedea kwa jumla ya kura 2104, wakati wapinzani wake Amina Salum Ally, akiibuka na kura 253 na Dkt. Asha-Rose Migiro, akipata kura 59. Viongozi wakuu wameenda kwenye kikao hivi sasa cha kujua nani atakuwa Mgombea Mwenza wa Urais. hivyo tutaendelea kuwajuza zaidi, endelea kuwa jirani na Libeneke lako pendwa la Globu ya Jamii.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgombea Mwenza wake, Mh. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kumtangaza, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Dodoma Convtion Centre, Mjini Dodoma mchana huu.





 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Mgombea Mwenza wake, Mh. Samia Suluhu Hassan wakati akimtambuliasha kwa wanaCCM na Watanzania.


Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mh. Samia Suluhu Hassan akipongezwa na Spika wa Bunge, Mh. Anne Makinda pamoja na viongozi wengine. Kushoto ni Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda.


Ama kwa hakika hayawi hayawi sasa yamekuwa,Mchakato wa kumpata mgombea Urais ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM) umefanyika hatua kwa hatua na hatimaye kapatikana atakaipeperusha bendera ya CCM katika kiti cha Urais kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika hapo baadae mwaka huu.

Ni John Pombe Magufuli ambaye baada ya Wajumbe wa Mkutano mkuu wa chama hicho kupiga kura kwa wagombea Urais Watatu ambao ni Dkt John Pombe Magufuli ,Dkt Asha Rose Migiro na Balozi Amina Salum Ali.

Kura zilipigwa jana katika Mkutano mkuu wa chama hicho ndani ya ukumbi wa Convetion Center mjini Dodoma,na matokeo yake yametangazwa rasmi mapema leo asubuhi kuwa jumla ya kura zilizokuwa zimepigwa zilikuwa 2422,kura zilizoharibika zilikuwa 6 na kula halali zilipatikana 2416.

Katika kinyang'anyiro hicho Dkt Asha Rose Migiro alipata kura 59 ambayo ni 2%,Dkt John Pombe Magufuli alipata kura 2104 ambayo ni 87.1 % na Balozi Amina Salum Ali aliyepata kura 255 ambayo ni asilimia 10.5.

Kwa matokeo hayo,imetangazwa rasmi kuwa Dkt John Pombe Magufuli ndiye atakaibeba bendera ya CCM katika kuwania kiti cha Urais

UPDATES KUTOKA DODOMA: RAIS KIKWETE AFUNGA MKUTANO MKUU WA CCM MJINI DODOMA LEO, KUMTAMBULISHA MAGUFULI UWANJA WA JAMHURI JIONI HII

0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama, wakati wa kuufunga Mkutano huo jioni hii kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CCM (Dodoma Conveition Centre), uliopo Mjini Dodoma. CCM wanafanya mkutano mkubwa wa kumtambulisha Mgombea wao jioni hii kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwatambulisha Mgombea Urais wa  CCM, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mgombea Mwenza, Mh. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuufunga Mkutano huo.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin Mkapa akimkumbatia Dkt. John Pombe Magufuli wakati akimpongeza kwa ushindi alioupata.
Mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Mzee Pius Msekwa na Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Taswa FC, Kijitonyama kumenyana kesho uwanja wa bora kijitonyama

0
0


Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa FC) leo (Jumatatu) itacheza mechi maalum ya kirafiki dhidi ya timu ya Kijitonyama Veterans kwenye uwanja wa Bora, Kijitonyama.
Mechi hiyo imepangwa kuanza saa 10.00 jioni na imeandaliwa kwa lengo la kudumisha ushirikiano baina ya timu hizo mbili. Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary alisema kuwa wachezaji wote watafungua swaumu zao mara baada ya mchezo huo.
Majuto ambaye pia ni kiongozi wa Kijitonyama Veterans alisema kuwa timu hizo mbili zinauhusiano mkubwa na kila mwaka huwa wanacheza mechi ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na sasa imekuwa ni ‘mila’ yao.
Majuto alisema kuwa baadhi ya wachezaji wa Taswa FC pia ni wachezaji wa Kijitonyama Veterans kutokana na kukaa maeneo hayo. 
“Taswa FC na Kijitonyama Veterans zinauhusiano wa karibu sana, baadhi ya wachezaji wa Taswa FC ni wachezaji wa Kijitonyama Veterans kutokana na kukaa maeneo hayo na kushughulika katika shughuli za kila siku za timu hiyo, naamini mechi hii ya ‘futari’ itakuwa nzuri, ushindano na wachezaji kukaa pamoja baada ya kuisha na ‘kufungua’ pamoja,” alisema Majuto.
Kuhusiana na Kijitonyama Veterans, Majuto alisema kuwa timu hiyo imejipanga vilivyo ili kuhakikisha inatoka na ushindi katika mechi hiyo. Alisema kuwa siku ya Jumatano, Kijitonyama itacheza mechi na timu ya Kijitonyama United na baada ya mchezo watafuturu pamoja.
“Mbali ya mechi ya Taswa FC, pia tutacheza na timu ya vijana wetu inayoshiriki ligi daraja la pili Kanda ya Dar es Salaam kwa lengo la kuwapongeza kufikia hatua hiyo,” alisema.Alisema kuwa Kijitonyama Veterans itatumia mechi hiyo kuwapongeza wachezaji na makocha wao kwa lengo la kuwapongeza kufikia hatua hiyo.

SALASALA VISION GROUP WAKABIDHIWA HATI ZA HEKARI 250 HUKO FUKAYOSI BAGAMOYO PIA YAZINDUA TOVUTI.

0
0
Afisa Mtendaji Mkuu EAG Group Iman Kajula Wa Pili (kushoto) akipokea hati ya Kimila ya eneo walillonunua bagamoyo kwajili ya Jumuiya hiyo.
Jumuiya iliyoasisiwa na wakazi wa Kilima hewa Salasala jijini Dar es salaam likiwa na malengo ya kijamii na kiuchumi. Tangu kuasisisiwa SVG imetekeleza miradi Mingi kwenye eneo la Salasala ikiwemo kupanda miti zaidi ya 5,000, kutengeneza barabara, kutengeneza viwanja vya michezo na kulinda maeneo ya wazi, Ulinzi, kutengeneza gari la polisi na misaada ya miradi mbalimbali endelevu ikiwamo kujenga ofisi ya Serikali ya Mtaa Salasala
 
SVG haikuishia hapo, imeamua kwa dhati kuchochea maendeleo ya Wanachama wake. Mradi mkubwa uliotekelezwa ni pamoja na kununua hekari 250 huko Fukayosi Bagamoyo. Baada ya ununuzi huu mchakato wakupata hati ulifanywa na kufanikiwa kupata hati za kimila na kukabidhiwa kwa wanachama wa SVG ili kuanza kuendeleza maeneno hayo.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Afisa Aridhi wa Wilaya ya Bagamoyo Bw.Kibona aliipongeza SVG kwa kuwa kikundi kilicho makini na kutumia dhima ya umoja ni nguvu, alisema hati za kimila zina faida nyingi sana ikiwamo kutokuwa na kipindi cha ukomo ikilinganishwa na hati za kawaida.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa SVG Yahaya Banka alisema ‘’ SVG inalenga kuendelea kuwa chachu ya maendeleo kwa wanachama wake na familia zao. Tunaamini kwa kutumia nguvu ya umoja tunaweza kuleta maendeleo makubwa katika eneo letu tunaloishi pia kwa familia za wanachama’’

MDAU JOHN CHACHA AMPONGEZA DKT JOHN MAGUFULI KWA USHINDI WA KUIPEPERESHA BENDERA YA CCM KUWANIA URAIS

0
0

Mgombea uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi -CCM Dkt John Magufuli akipongezwa na mwandishi mwandamizi wa kituo cha ITV na Radio one John Chacha siku chache kabla ya Dkt Magufuli kuchukuwa fomu ya kutia nia kugombea nafasi ya Urais kupitia chama cha CCM,ambapo aliagana na mwandishi huyo akiwa njiani kuelekea mikoa ya Geita,Mwanza na Kagera.

Pichani ilikuwa ni nje ya ofisi za CCM makao makuu mjini Dodoma,John Chacha anamtakia kila lakheri na afya njema katika safari yake ya kuipeperusha bendera ya chama chake katika kuwania nafasi ya Urais katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika hapo baadae mwaka huu 2015.

Ofisi ya Kambi ya Upinzani Bungeni yaandaa futari wakati wa kikao cha ukawa jijini Dar es salaam

0
0
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Willibroad Slaa akishiriki futari iliyoandaliwa na Ofisi ya Kambi ya Upinzani Bungeni wakati wa kikao cha Viongozi Wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na wabunge wa umoja huo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu. Kushoto kwake ni Mbunge wa CUF, Ali Khamis Seif (Mkoani) na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa NLD Zanzibar, Ahmad Hemed. 
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Said Issa Mohamed (katikati) pamoja na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Ndelakindo Kessy (kushoto) huku wakishiriki futari iliyoandaliwa na Ofisi ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni wakati wa kikao cha Viongozi Wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na wabunge wa vyama vinavyounda umoja huo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu.
Baadhi ya Wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kutoka kushoto, Naomi Kaihula (Viti Maalum CHADEMA), Salum Baruan (CUF- Lindi Mjini) na Mohamed Habib Mnyaa wakishiriki futari iliyoandaliwa jana jijini Dar es Salaam na Ofisi ya Kambi ya Upinzani Bungeni, wakati wabunge wa vyama vinavyounda umoja huo waliposhiriki kikao cha Viongozi Wakuu wa UKAWA (Summit) kilichojadili mikakati mbalimbali ya maandalizi ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Said Issa Mohamed akijiandaa kuwamiminia uji baadhi ya wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakati wa kula futari. Wabunge hao walikuwa wakihudhuria kikao cha Viongozi Wakuu wa UKAWA kilichofanyika juzi jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu. Walioketi kutoka kushoto ni Seleman Bungala Bwege (CUF- Kilwa Kusini),Mohamed Habib Mnyaa (CUF-Mkanyageni) na Mama Riziki.
Wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakati wa kula futari.

TONY ELUMELU FOUNDATION HOSTS HISTORIC BOOTCAMP FOR 1,000 EMERGING AFRICAN ENTREPRENEURS FROM 51 AFRICAN COUNTRIES IN OTA, NIGERIA

0
0
TEEP 1
l-r:Benin Republic Prime Minister, Mr. Lionel Zinsou, Nigeria’s Vice President, Prof. Yemi Osinbajo, Founder, Tony Elumelu Foundation Mr. Tony Elumelu and Kaduna State Governor, Mallam Nasir El-Rufai at the $100 Million Tony Elumelu Entrepreneurship Programme (TEEP) boot camp for 1000 entrepreneurs from 51 countries across Africa, Ota, Ogun State, on Saturday July 11, 2015.
TEEP 2
l-r: Nigeria’s Vice President, Prof. Yemi Osinbajo, Founder, Tony Elumelu Foundation Mr. Tony Elumelu and Kaduna State Governor, Mallam Nasir El-Rufai at the $100 Million Tony Elumelu Entrepreneurship Programme (TEEP) boot camp for 1000 entrepreneurs from 51 countries across Africa, Ota, Ogun State, on Saturday July 11, 2015.
TEEP 3
As part of Tony Elumelu’s $100 million commitment to empowering African entrepreneurs, 1,000 Tony Elumelu Entrepreneurs, representing 51 African countries from the Tony Elumelu Entrepreneurship Programme (TEEP) Class of 2015, converged near Lagos, Nigeria for an intensive two-day bootcamp session, an unprecedented gathering of emerging African entrepreneurs, from 10-12 July, 2015. 


The entrepreneurs travelled from across the continent – from as far as Madagascar and Morocco – and convened in Ota, Nigeria for an entrepreneurship bootcamp made up of interactive sessions with successful entrepreneurs, political and business leaders, and an open mic session with the Founder, Tony O. Elumelu CON.

Gambian Badje Modou Lamin, whose business is in the agricultural sector, said, “The bootcamp has been a great experience. I have been able to exchange ideas with a number of entrepreneurs. This has really changed my perspective on Africa.”

Maalainine Mohamed Bouya, from Morocco, said: “The bootcamp has been a blast! Right from our journey from the airport down to the bootcamp, we have been discussing and sharing ideas among ourselves. Africa has huge potential.”

Nigerian Obinna Chukwu, said: “The bootcamp has been a wonderful experience – I have met people from all over Africa. It makes me proud of being a Nigerian. I thank Tony Elumelu and the Tony Elumelu Foundation for making this happen.”

Mr. Elumelu, the Chairman of Heirs Holdings, spoke on his life experiences and the principles that he learned from mentors, such as Chief Ebitimi Banigo, that he applied towards his own successful entrepreneurship journey. He answered an array of questions during a two-hour question-and-answer session, offering perspective on innovation, strategy, governance, financial management and decision-making.

He said: “Entrepreneurship is not a short-term journey and I am pleased that we can help these emerging leaders, as they seek to join me in transforming Africa. My commitment towards creating a thousand new entrepreneurs who can change Africa forever, has now become a reality. This is only the beginning.”

Vice President of Nigeria Professor Yemi Osinbajo, GCON, welcomed the entrepreneurs from across Africa and called on them to take advantage of the networks built in Ota to develop pan African investment and trade networks. According to Vice President Osinbajo, “This programme deserves all the commendation it is getting. Tony Elumelu has courageously put his money where his mouth is. Societies can’t develop without social entrepreneurs. I charge you to be little Elumelus and create opportunities for others.”

The Vice President was joined by other senior political leaders including Kaduna Governor Nasiru El Rufai, and Lionel Zinsou, the Prime Minister of Benin Republic.

Other speakers included Parminder Vir, OBE, CEO of the Tony Elumelu Foundation; Mo Abudu, Founder/CEO of Ebony Life TV; Nollywood screen icon Omotola Jalade-Ekeinde; Nimi Akinkugbe, CEO, Bestman Games; Rasheed Olaoluwa, CEO of the Bank of Industry; former SEC DG Arunma Oteh; inspirational coach Lanre Olusola; Martin Eigbike, Accenture Development Partnerships; governance expert Angela Aneke; playwright and producer Adewale Ajadi; Sam Nwanze, the Heirs Holdings Director of Finance and Investments; and David Rice, Director of the Africapitalism Institute. 

The Tony Elumelu Entrepreneurs of the TEEP Class of 2015 represent 51 African countries and territories. They cover all of Africa’s geopolitical regions - North, East, Southern, Central and West Africa – and major language blocs – Anglophone, Francophone, Lusophone, and Arabic Africa - as well as every state in Nigeria. They represent a diversity of sectors that range from agriculture to education to energy, fashion and ICT, emphasising Africa's potential. 

In his goodwill message to the visiting Tony Elumelu Entrepreneurs, Nigerian President Muhammadu Buhari, GCFR wrote, "I am proud that Nigeria (and a Nigerian) is taking the lead in this effort to promote self-worth, encourage entrepreneurship, create jobs, build and promote networks for intra-African trade, business collaboration and investment.

 Our Administration is committed to unlocking all such opportunities to restore dignity to our people. This programme is one example I hope others will emulate and I commend Tony Elumelu and his Foundation for their endeavor and leadership in this area. "

As he closed the bootcamp, Mr Elumelu challenged all the entrepreneurs by saying, "I want to go to Zambia when I am 80 years old and meet someone who shows me their manufacturing business or financial institution and tells me that it was built starting with $10k from Tony Elumelu. That's what this is about and that's what you owe me." He added, "The return I want from this $100 million investment is your success, because your success is Africa's success."

After the bootcamp, the Tony Elumelu Entrepreneurship Programme will focus on providing the seed capital and support for the entrepreneurs to put into practice the knowledge gained from the bootcamp and the 12 weeks of training carried out prior to the event. It will also continue to foster increased collaboration between them and the rest of the Tony Elumelu Entrepreneurship Network as it seeks to promote cross-border trade within the continent. The application portal will re-open on January 1, 2016 for emerging entrepreneurs across Africa to compete for places in the TEEP Class of 2016.

TUME YA MIPANGO YATEMBELEA MIRADI WA UMEME WA UPEPO SINGIDA

0
0
 Meneja wa Mradi, Mhandisi. Pascal Malesa akiwaonesha timu ya ukaguzi eneo linalokusudiwa kwa ajili ya mradi wa umeme wa upepo nje kidogo ya mji wa Singida, mbele yake ni kiongozi wa timu hiyo Mhandisi. Happiness Mgalula, ambaye ni Naibu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
 Meneja wa Mradi, Mha. Pascal Malesa akiwaonesha timu ya ukaguzi eneo linalokusudiwa kwa ajili ya mradi wa umeme wa upepo nje kidogo ya mji wa Singida.
 Mhandisi Malesa akitoa maelezo juu ya utendaji kazi wa mnara wa kupima upepo wa kampuni ya kuzalisha umeme wa upepo ya Wind East Africa Singida Wind Power katika kijiji cha Ihoro, Kata ya Kisaki, Singida mjini.
Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ikiwa chini ya mnara wa kupima kasi ya upepo katika kijiji cha Iroho, Kata ya Kisaki, Singida mjini. Mnara huo una urefu wa mita 60.
Meneja wa Mawasiliano wa Kampuni ya Wind East Africa Singida Wind Power Bw. Simon Magesa akionesha jinsi ambavyo kasi ya upepo inavyopimwa katika mnara wa upepo ambao tayari umewekwa na kampuni yake.

BALOZI LIBERATA MULAMULA AWAAGA TAMCO RASMI, ASEMA UMOJA NA MSHIKAMANO WAO NI MFANO WA KUIGWA NA JUMUIYA ZINGINE

0
0
Na Mwandishi wetu, Washington, DC
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula leo jioni siku ya Jumapili July 12, 2014 alijumuika na wanajumuiya ya Kiislam ya DMV (TAMCO) katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na jumuiya hiyo na kutumia fulsa hiyo kuwaaga rasmi.

Katika hotuba yake. Mhe. Liberata Mulamula  aliwakuwakumbusha alipokuja kwa mara ya kwanza kulitumikia Taifa kama Balozi wa Tanzania nchini Marekani , Jumuiya hiyo ndio iliyomkaribisha kwa mara ya kwanza hapa DMV na leo nimerudi tena kuagana nanyi rasmi. Mhe. Liberata Mulamula aliwashukuru TAMCO kwa ushirikiano na mshikamano wao na kuzitaka Jumuiya zingine za Watanzania ziige mfano wao kwani TAMCO ni jumiya ya Kiislam iliyoimara, isiyotetereka na yenye uongozi makini. Mhe. Balozi Liberata Mulamula aliushukuru uongozi wa TAMCO kwa kumkaribisha aje azungumze na Watanzania wanajumuiya ya TAMCO na kutumia fulsa hiyo kuwaaga rasmi.

Uongozi wa TAMCO ulimuzawadia Mhe. Balozi Liberata Mulamula zawadi na yeye kutoa mchango wake wa mwaka kwa jumuiya hiyo inayo wakubali Watanzania wote bila kubagua rangi, kabila wala dini.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislam ya Watanzania DMV (TAMCO)Ustadh Ally Mohamed akimlaki Mhe. Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulaula mara tu alipowasili kwenye ukumbi wa park iliyopo Silver Spring, Maryland nchini Marekani alipokuja yeye Mhe. Balozi akiambatana na mumewe Eng. George Mulamula (hayupo pichani) na mwanae Alvin Mulamula (kulia) kujumuika na wanajumuiya hao katika futari ya pamoja na kutumia futari hiyo kuwaaga rasmi. Picha zote na Kwanza Production na Vijimambo Blog.
 Mtunza fedha msaidizi wa TAMCO. Bi. Asha Hariz(kushotao) akiongozana na Mhe. Liberata Mulamula kuelekea ukumbini siku ya Jumapili July 12, 2015 siku Mhe. Balozi alipopata mwaliko wa Jumuiya hiyo wa kufuturu pamoja na kuwaaga rasmi.
Mwenyekiti wa TAMCO ustadh Ally Mohamed akiongea machache na baadae kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Balozi Liberata Mulamula kuongea na wanajumuiya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea na Wanajumuiya wa TAMCO na kuwaaga rasmi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Balozi Liberata Mulamula akikabidhi mchango wake wa TAMCO wa mwaka kwa mtunza fedha msaidizi ustadh Shamis Abdullah.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa mtunza fedha msaidizi wa TAMCO bi. Asha Hariz.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa mtunza fedha msaidizi wa TAMCO bi. Asha Hariz.
Picha ya pamoja

SOKO LA HISA WIKI HII JIJINI DAR ES SALAAM

0
0

Meneja Mradi na biashara wa soko la hisa hapa nchini, Patrick Msusa akizungumza na na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na kushuka kwa soko la hisa kwa asilimia 85.85 ukilinganisa na wiki iliyopita ambapo ziliuwa hisa 14,685 na kushuka kwa wiki hii hisa 2,1077 zilizouzwa.
 Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika ofisi za soko la hisa leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

DK.SHUKURU KAWAMBWA APATA MPINZANI JIMBO LA BAGAMOYO

0
0
 Mtangaza nia ya Ubunge Jimbo la Bagamoyo, Mathew 
Juma Salum Yangwe.
 Mtangaza nia ya Ubunge Jimbo la Bagamoyo, Mathew 
Juma Salum Yangwe (katikati), akizungumza na makada na wanahabari wakati akitangaza nia mjini Bagamoyo mkoani Pwani Pwani jana. Kushoto ni Meneja wa Kampeni wa Mtangaza nia huyo, James Mbuligwe na Katibu wa Sera na Mipango wa Mtangania huyo, Paul Kassanga.
Meneja wa  Kampeni wa Mtangaza nia huyo, James Mbuligwe (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
 Katibu wa Sera na Mipango wa Mtangania huyo, Paul Kassanga(kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.


 Mzee Abdallah Ngumbe akizungumza katika mkutano huo na wakati akimpa ushauri mbalimbali mtangaza nia huyo.
 Profesa Sameheni Kejeli akizungumza katika mkutano huo.
 Mzee Hussein Lugome akizungumza katika mkutano huo.
 Mama mzazi wa mtangania huyo, Mary Yungwe akiwasalimia makada wa CCM katika mkutano huo.
 Mtangaza nia huyo akipongezwa na vijana baada ya mkutano huo.
 Pongezi zikiendelea.
 Mkutano ukiendelea.



 Makada wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.
Mtangazania huyo akiwa na wadau wake.

Na Dotto Mwaibale
MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo ambaye pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa amepata mpinzani baada ya kijana mdogo kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mathew Yungwe kutangaza nia ya ubunge katika jimbo hilo.

Akizungumza na makada wa CCM na waaandishi wa habari mjini Bagamoyo mkoani Pwani jana, Yungwe alisema ameamua kugombea nafasi hiyo ili kusukuma maendeleo ya jimbo hilo ambayo yamekwama kwa muda mrefu.

"Wanaccm wenzangu na wazee wangu nimeamua kugombea nafasi hii ili niwatumikie kwani Bagamoyo naelewa vizuri na nitaendelea kuwa wilayani hapa ili tushirikiane katika mambo mbalimbali ya nmaendeleo" alisema Yungwe.

Yungwe alisema mambo atakayoyapa kipaumbele ni matatu, uchumi, Afya na Mawasiliano na kuwa hata penda aitwe mbunge bali aitwe mratibu na kuwa atakuwa na ofisi yake ya ubunge katika wilaya hiyo kwa lengo la kuwa jirani na wananchi zaidi.

Alisema maeneo mengine atakayoyafanyia kazi kwa kushirikiana na wananchi ni pamoja na kuinua uchumi wa jimbo hilo kupitia uvuvi, kuweka mipango mizuri ya kukusanya fedha kupitia viwanja vya michezo, utalii na mapato yatokanayo na uwekezaji na ujenzi wa soko la kisasa.

Alisema pia atashughulikia migogoro ya ardhi katika maeneo yote ya jimbo hilo yakiwemo ya Zinga na Pande ambayo inapunguza kasi ya maendeleo ya wananchi katika jimbo hilo.

Yungwe alisema kauli mbiu yake ni "Fikiri Tofauti, Badilika kwa Maendeleo Endelevu ya Bagamoyo.

Jimbo la Bagamoyo katika kpindi cha miaka 10 tangu mwaka 2005 hadi sasa lilikuwa likiongozwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com.

MWENYEKITI WA BAVICHA AMVAA MCHUNGAJI MSIGWA UBUNGE IRINGA MJINI

0
0

na fredy mgunda,iringa


MWENYEKITI wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), Leonce Marto amechukua fomu ya kuwania ubunge katika jimbo la Iringa kupitia chama chake hicho.

Amechukua fomu hiyo siku moja tu baada ya Rais Jakaya Kikwete kulihutubia na hatimaye kulivunja bunge la 10 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo uhai wake utakoma Agosti 20, mwaka huu.


Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, jimbo la Iringa Mjini limekuwa likiongozwa na Mchungaji Peter Msigwa ambaye pia alichaguliwa kupitia Chadema katika uchaguzi wa 2010.


Kwa kupitia taarifa yake aliyoisambaza kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii jana, Marto alisema;  “nawasalimu nyote wenye mapenzi mema na Taifa letu la Tanzania na wapenda mabadiliko na demokrasia za ushindani ndani ya vyama vya siasa kwa minajili ya katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 .”


 “Nianze kwa kuwashukuru watu wote  ambao kwa muda wa uhai wangu wameshiriki kwa namna moja ama nyingine kuniwezesha  kufika hapa nilipo . Pili nawashukuru viongozi , wanachama , wafuasi wa Chadema, ndugu,  jamaa na marafiki ambao kwa wingi wenu sitaweza kuwataja wote,” alisema.


Marto alisema ameamua kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Mchungaji Msigwa baada ya kupata msukumo wa ndani na nje ya chama.


Alisema kwa haraka katika fahamu zake aliona jambo hilo ni zito na la hatari kulinganisha na watu wanavyosema kwasababu kazi ya umma ni kazi inayohitaji dhamira safi, uadilifu, umahiri, weledi, kujali ya maisha ya watu na maendeleo yao na zaidi sana kupenda na kutathmini Taifa na watu wake.


Marto alisema ilimchukua muda kujiridhisha pasipo shaka na jambo hilo kama  anaweza kubeba wito huo wa kuwatumikia wananchi wa Iringa Mjini.


“Baada ya kutafakari kwa kina nilijipa mtihani wa kwanza wa kuzunguka nchi yetu na kukutana na jamii za watanzania. Kwa mantiki hiyo ninayafahamu kwa undani na kwa uhalisia wake maswala na matatizo muhimu yanayowakabili watanzania na wana Iringa Mjini,”alisema.


Marto alisema kwa kuwa anakidhi vigezo vya kikatiba, na kwa kuwa anaamini Mungu amempa karama ya uongozi ambayo watu wameiona na kumuomba agombee ubunge na kwa kuwa anayajua matatizo yanayowakabili watanzania na wana Iringa anayajua na yamemchosha kama yalivyowachosha watanzania wengine:


Na kwa kuwa Chadema kimejengwa kwenye mhimili na msingi mkuu wa Demokrasia pamoja na itikadi na falsafa yake ya Nguvu ya Umma na kwa kuwa anaamini viongozi bora wanapatikana kwa ushindani, kwa ujasiri wote aliopewa na Mwenyezi Mungu anatangaza rasmi kuomba ridhaa ya chama chake kugombea ubunge katika jimbo hilo.

MICHUANO YA KAGAME KUANZA JUMAMOSI

0
0
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 121
TAREHE 13 JULAI 2015
Michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa Kagame Cup) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya Jumamosi tarehe 18 Julai 2015 jijini Dar es salaam, kwa kushirikisha timu 13 kutoka nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na kati.

Mashindano ya CECAFA Kagame Cup ni mashindano makongwe barani Afrika ambayo yalianza mwaka 1967 kwa kushirikisha timu za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, na mwaka huu ni mashindano ya 40 tangu kuanza kwa michuano hiyo

Klabu ya Simba ndio timu inayoongzoa kwa kutwaa ubingwa huo mara sita (6) ikifuatiwa na Yanga, Gor Mahia zilizotwa mara (5), APR ya Rwanda ikiwa imetwaa ubingwa huo mara tatu (3). Yanga na Gor Mahia zina nafasi ya kufikia Simba SC endapo zitafanikiwa kutwaa Ubingwa msimu huu.

Mechi ya ufunguzi ufunguzi siku ya jumamosi uwanja wa Taifa itawaktanisha APR ya Rwanda dhidi ya Al Shandy ya Sudan saa 8 kamili mchana, KMKM kutoka Visiwani Zanzibar watacheza dhidi ya Telecom ya Djibout  uwanja wa Karume saa 10 jioni, huku wenyeji timu ya Yanga wakiwakaribisha Gor Mahia kutoka Kenya saa 10 jioni.

Kuelekea kwenye mashindano hayo, waandaji wa michuano hiyo CECAFA kwa kushirikiana na wenyeji Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya michezo hiyo, ambapo Uwanja wa Karume kiingilio kitakua shilingi elfu mbili (2,000) na uwanja wa Taifa kiingilio cha chini kitakua ni shilingi elfu tano (5,000) na kiingilio cha juu ni elfu 20,000 (20,000).

Timu zinazoshiriki michuano hiyo
Kundi A: Yanga (Tanzania Bara), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djibout), KMKM (Zanzibar), Khartoum-N (Sudan).
Kundi B: APR (Rwanda), Al-Shandy (Sudan),LLB AFC (Burundi), Heegan  FC (Somalia).
Kundi C: Azam FC (Tanzania), Malakia (Sudan Kusini), Adama City (Ethiopia) na KCCA (Uganda).

Michuano hiyo ya CECAFA Kagame Cup itaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha luninga cha Supersport.

UCHAGUZI TWFA
Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Soka cha Wanawake chini (TWFA) inatangaza kuwa wafuatao wamepita katika mchujo wa awali katika nafasi walizoomba kama ifuatavyo:
1.   Amina Ali Karuma  - Mwenyekiti
2.   Devotha John Marwa – Mwenyekiti
3.   Cecilia Makafu – Katibu Msaidizi
4.   Somoe Roberst Ng’itu – Katibu Msaidizi
5.   Debora Ernest Mkemwa – Mjumbe Kamati ya Utendaji
6.   Mwanaheri Kalolo – Mjumbe Kamati ya Utendaji
7.   Theresia Reginald – Mjumbe Kaamti ya Utendaji

Hivyo mtu yeyote mwenye pingamizi anaombwa aliwasilishe katika ofisi za TFF – Karume kuanzia tarehe 15/07/2015  mpaka 20/07/2015.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

UCHAKAVU WA MAJENGO YA SHULE TISHIO KWA WANAFUNZI

0
0

 Jengo la shule ya msingi Donyonaado.

 Na Woinde Shizza,Monduli
Wakati shule nyingi nchini zinafunguliwa baada kumalizika kwa likizo
Wanakijiji wa kijiji cha Donyonaado kilichopo wilaya ya Monduli mkoani
Arusha wameeleza wasi wasi juu ya uchakavu wa jengo la shule ya Msingi
Idonyonaado huenda linaweza kuanguka na kusababisha maafa kwa
wanafunzi.

Shule hiyo iliyoko umbali wa kilomita 64  kutoka Monduli mjini
iliyojengwa kwa udongo na mawe na wanakijiji waliojitoa haina milango
na madirisha hivyo wanafunzi kupata adha ya vumbi na baridi  kali hasa
kipindi cha mvua.

Wanakijiji hao wamesema kuwa  hali mbaya  ya miundombinu ya shule hiyo
imewafanya wazazi wengi kusita  kuwapeleka watoto mashuleni  hivyo
ameiomba serikali na mashirika binafsi yajitokeze kusaidia kutatua
changamoto hizo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Donyonaado ,Malulu Kutetei amesema kuwa licha
ya changamoto za shule hiyo bado wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa
nyumba bora za walimu pamoja na uhaba wa maji jambo linalokwamisha
maendeleo ya taaluma shuni hapo.

Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Wafugaji la Monduli
Pastodalist Development Initiative (MPDI) ,Erasto Sanare ameeleza
kusikitishwa na changamoto zinazoikabili shule hiyo hivyo kushiriki
katika  ujenzi wa shule ya kudumu ,ameieomba serikali isaidia shule
hiyo ambayo ni tegemeo kwa wafugaji.

Licha ya Jamii ya Wafugaji kuamka katika masuala ya elimu tofauti na
miaka iliyopita bado kuna mazingira duni ya elimu ikiwemo kukosekana
kwa shule za kutosha,miundombinu mibovu,uhaba wa maji na vifaa vya
kufundishia na nyumba za walimu

WATAKWIMU WA NCHI ZA AFRIKA WASISITIZWA KUZINGATIA WELEDI NA UWAZI

0
0
 Mwakilishi wa Benki ya Afrika (ADB) nchini Tanzania Tonia Kandiero akizungumza na washiriki wa Warsha  ya Kimataifa ya Watakwimu kutoka nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya kiingereza juu ya ushiriki wa ADB katika masuala ya Takwimu katika Bara la Afrika leo jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. albina Chuwa akiwakaribisha nchini Tanzania washiriki wa mkutano wa kimataifa wa Watakwimu kutoka nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya kiingereza leo jijini.Washiriki wa Warsha hiyo wanajadili na kubadilishana uzoefu kuhusu Pato la Taifa.
 Naibu Mkuu, Wizara ya Fedha Prof.  Adolf Nkenda akifungua warsha ya siku 5 ya watakwimu kutoka nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya kiingereza uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Washiriki wa Warsha hiyo ya kimataifa ya Watakwimu kutoka nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya kiingereza wakiwa katika picha ya pamoja leo jijini Dar es salaam.



Na.Veronica Kazimoto- Dar es salaam.
SERIKALI imesema kuwa itaendelea kuongeza uwazi katika matumizi ya takwimu zinazokusanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini ili kukidhi vigezo na malengo ya mfumo mpya uliowekwa na Umoja wa Mataifa wa mwaka 2008 wa upataji wa takwimu za pato la Taifa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha ya kimataifa ya siku 5 ya watakwimu kutoka nchi za Afrika zinazozungumza Kiingereza, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha Prof. Adolf Nkenda amesema kuwa Tanzania inaendelea kukusanya takwimu mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya watunga Sera na wananchi.

Amesema kwa kutambua na kuthamini mchango wa takwimu katika maendeleo, Serikali imeamua kuingiza takwimu za ubora wa mazingira na takwimu za matumizi ya simu za mkononi kwenye Pato la Taifa.

Amefafanua kuwa, mabadiliko hayo yataiwezesha Tanzania kuwa na takwimu zenye uhalisia kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanyika nchini na mchango wake katika Pato la Taifa.

Prof. Nkenda ametoa wito kwa washiriki wa warsha hiyo kuendelea kuzingatia weledi katika utekeleaji wa majukumu yao ili waweze kutoa takwimu sahihi zinazoonesha hali halisi ya tafiti zinazofanyika katika nchi zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)   Dkt. Albina Chuwa  akizungumza na washiriki wa Mkutano huo wa Kimataifa amesema kuwa Nchi za Afrika zinahitaji Takwimu sahihi ili ziweze kuendelea.

Amesema Tanzania imepiga hatua kwa kuweka kipaumbele katika shughuli mbalimbali za Takwimu ikiwemo kusaini mkataba wa Takwimu wa Afrika kuhusu kuongeza uwazi katika upatikanaji na matumizi ya takwimu  zilizopo kwa Maendeleo ya Taifa.

Ameeleza kuwa kupitia Mfumo mpya wa Umoja wa Mataifa wa kutengeneza Pato la Taifa wa mwaka 2008, Tanzania imefanikiwa kuingiza shughuli mbalimbali katika Pato la Taifa ambazo hapo awali hazikuwemo, zikihusisha shughuli za kitaalam za Sayansi na Teknolojia pamoja na sanaa.

Ili kufanikisha shughuli za takwimu Barani Afrika Dkt. Chuwa ameziomba Serikali zote za Afrika kuutumia na kuheshimu Mkataba wa Afrika wa Takwimu wa mwaka 2008 unaotoa kipaumbele katika uboreshaji wa shughuli za Takwimu.

"Napenda kutumia fursa hii kuziomba Serikali za Afrika kuzijengea uwezo Ofisi za Takwimu ili ziwe na uwezo wa kuzalisha takwimu za masuala mbalimbali kwa muda mfupi maana Takwimu ni sasa kwa ajili ya kukidhi mahitaji na matarajio ya wananchi", amesisitiza Dkt. Chuwa.

Aidha, ameongeza kuwa warsha hiyo ya siku 5 ambayo imewajumuisha watakwimu kutoka nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na baadhi ya nchi za Afrika Magharibi zikiwemo Ghana na Nigeria inalenga kuwajengea uwezo washiriki hao kwa kuwa na uelewa wa pamoja katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za Takwimu katika nchi zao.

Naye Mwakilishi wa Benki ya Afrika (ADB) nchini Tanzania Bi.Tonia Kandiero amewataka washiriki wa warsha hiyo kuzingatia mfumo uliowekwa wa upataji wa takwimu za Pato la Taifa ili kuwezesha uwepo wa takwimu sahihi za maendeleo ya nchi husika.

Amesema kuwa wingi wa washiriki wa warsha hiyo waliohudhuria kutoka nchi mbalimbali za Afrika ni ishara tosha kuwa nchi zao zinathamini mchango wa Takwimu katika kuleta maendeleo.

Amesema Benki ya Afrika ambayo yeye ni mwakilishi wake itaendelea kushirikiana na nchi za Afrika ili kuhakikisha kuwa Takwimu mbalimbali zikiwemo za Watu na Makazi, Pato la Taifa na nyinginezo zinapatikana kwa wakati na kuchangia maendeleo ya Afrika. 
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images