Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 580 | 581 | (Page 582) | 583 | 584 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC) kinachoendelea hivi sasa kwenye Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM, Mjini Dodoma. Kikao hiki kinapitia majina yote 38 ya Watangaza nia ya kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, ambapo majina matano yatapatikana baada ya kikao hiki.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM - Zanzibar, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM - Bara, Mzee Phillip Mangula (kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, DODOMA.
  Sehemu ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakiwa kwenye Kikao cha kupitia Wagombea wanaowania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia CCM, ambapo majina matano yatapatikana katika kikao hiki na kupelekwa kwenye Mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM ili kupata majina matatu yatakayokwenda kupigiwa kura kwenye Mkutano Mkuu.
  Baadhi ya Wapigapicha za Habari wakichukua taswira ya Wazee wa Kamati ya Ushauri wa Chama.
  Wazee wa Kamati ya Ushauri ya CCM ikiongozwa na Rais Mstaafu awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu awamu ya tatu, Mh. Benjamin Mkapa, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Mzee Pius Msekwa, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mh. Aman Abeid Karume, Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Cleopa Msuya pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim.

  0 0

  Waandishi wa Vyombo mbali mbali vya habari nchini Tanzania walioweka kambi kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma kwa ajili ya kutoa taarifa za vikao mbali mbali vinavyopendelea ili kumpata mgombea Urais wa Mwaka 2015 kupitia chama hicho.

  UPDATES:kamati ya maadili ya tayari imemaliza kikao chake, kikao cha Kamati Kuu kinaendelea sasa kuwapata wagombea 5 watakaopelekwa NEC kupata 3.Ni mapumziko sasa wajumbe wa Kamati Kuu wameenda kufuturu kisha watarudi tena kuendelea na kikao.

  0 0


   Madaktari  bingwa kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakimfanyia  upasuaji  mgonjwa  katika hosptali ya Wilaya ya Bariadi mkoani  Simiyu Zowezi  hilo lina endelea katika  hosptali ya Wilaya ya Bariadi hadi sasa zaidi ya watu 480
  Bingwa wa magonjwa ya moyo Dokta Tatizo Wane akimpima mgonjwa kwa kutumia mashine ya kisasa inayojulikana kama ECHOCARDIOGRAM Machine Zowezi  hilo lina endelea katika  hosptali ya Wilaya ya Bariadi hadi sasa zaidi ya watu 480.
   Wakazi wa mji wa Bariadi na maeneo  ya  jirani wakisubiri huduma za matibabu za madaktari  bingwa kaitka hosptali ya Wilaya ya Bariadi mkoani  Simiyu


  0 0

  Waandishi wa Vyombo mbali mbali vya habari nchini Tanzania na nje walioweka kambi kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma kwa ajili ya kutoa taarifa za vikao mbali mbali vinavyopendelea ili kumpata mgombea Urais wa Mwaka 2015 kupitia chama hicho.
  UPDATES:  Kikao cha  Kamati Kuu ya CCM   kimemalizika hapa Dodoma na Nape Nnauye akiongea na wanahabari hivi punde amesema kikao kimaeenda vyema kabisa na kumalizika vizuri - ila majina hatoyataja sasa. Hadi kesho saa nne asubuhi.... 
  Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete(wa pili kushoto) akiongoza kikao cha Kamati Kuu Maalum cha CCM mjini Dodoma, Kikao hicho kitachuja majina ya wagombea na kupata majina matano(5) .
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa taarifa fupi ya wajumbe waliohudhuria kikao cha Kamati Kuu Maalum ambapo wajumbe 28 walihudhuria kati ya 32.
  Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakipitia baadhi ya makabrasha wakati wa kikao cha Kamati Kuu Maalum (Picha na Adam Mzee)

  Vijana wa CCM wakipakia mikoba yenye makabrasha ya mkutano maalum wa CCM Taifa 2015 unaotarajiwa kuanza baadaye leo  katika ukumbi mpya wa Dodoma Convention Centre mjini Dodoma  uliozinduliwa juzi.

  0 0

  Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mbando , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Utafiti cha Magonjwa ya Binadamu cha Taifa (NIMR), Dk. Julius Massaga wakizinduwa kitabu cha utafiti kitakachosaidia uboreshaji mfumo wa huduma za afya, uandaaji wa ajenda za kitafiti juu ya utafiti wa mifumo wa afya wa magonjwa ya kifua kikuu na maleria na pamoja na magonjwa ya kitropiki (NTD). Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mbando , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Utafiti cha Magonjwa ya Binadamu cha Taifa (NIMR), Dk. Julius Massaga wakizinduwa kitabu cha utafiti kitakachosaidia uboreshaji mfumo wa huduma za afya, uandaaji wa ajenda za kitafiti juu ya utafiti wa mifumo wa afya wa magonjwa ya kifua kikuu na maleria na pamoja na magonjwa ya kitropiki (NTD).Mwanasayansi, mtafiti na mshauri wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk. Olumide Ogundahunsi ambaye alishiriki kufanikisha kitabu cha utafiti kitakachosaidia uboreshaji mfumo wa huduma za afya, uandaaji wa ajenda za kitafiti juu ya utafiti wa mifumo wa afya wa magonjwa ya kifua kikuu na maleria na pamoja na magonjwa ya kitropiki (NTD). Kulia ni Ofisa Mwakilishi wa Shirika la UNDP na Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk. Bwijo Bwijo. Mwanasayansi, mtafiti na mshauri wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk. Olumide Ogundahunsi ambaye alishiriki kufanikisha kitabu cha utafiti kitakachosaidia uboreshaji mfumo wa huduma za afya, uandaaji wa ajenda za kitafiti juu ya utafiti wa mifumo wa afya wa magonjwa ya kifua kikuu na maleria na pamoja na magonjwa ya kitropiki (NTD). Kulia ni Ofisa Mwakilishi wa Shirika la UNDP na Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk. Bwijo Bwijo.Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha utafiti kitakachosaidia uboreshaji mfumo wa huduma za afya, uandaaji wa ajenda za kitafiti juu ya utafiti wa mifumo wa afya wa magonjwa ya kifua kikuu na maleria na pamoja na magonjwa ya kitropiki (NTD) wakifuatilia mada anuai. Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha utafiti kitakachosaidia uboreshaji mfumo wa huduma za afya, uandaaji wa ajenda za kitafiti juu ya utafiti wa mifumo wa afya wa magonjwa ya kifua kikuu na maleria na pamoja na magonjwa ya kitropiki (NTD) wakifuatilia mada anuai.

  Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha utafiti kitakachosaidia uboreshaji mfumo wa huduma za afya, uandaaji wa ajenda za kitafiti juu ya utafiti wa mifumo wa afya wa magonjwa ya kifua kikuu na maleria na pamoja na magonjwa ya kitropiki (NTD) wakifuatilia mada anuai. Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha utafiti kitakachosaidia uboreshaji mfumo wa huduma za afya, uandaaji wa ajenda za kitafiti juu ya utafiti wa mifumo wa afya wa magonjwa ya kifua kikuu na maleria na pamoja na magonjwa ya kitropiki (NTD) wakifuatilia mada anuai.
  Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mbando akizungumza na wanahabari mara baada ya kuzinduwa kitabu cha utafiti kitakachosaidia uboreshaji mfumo wa huduma za afya, uandaaji wa ajenda za kitafiti juu ya utafiti wa mifumo wa afya wa magonjwa ya kifua kikuu na maleria na pamoja na magonjwa ya kitropiki (NTD). Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mbando akizungumza na wanahabari mara baada ya kuzinduwa kitabu cha utafiti kitakachosaidia uboreshaji mfumo wa huduma za afya, uandaaji wa ajenda za kitafiti juu ya utafiti wa mifumo wa afya wa magonjwa ya kifua kikuu na maleria na pamoja na magonjwa ya kitropiki (NTD).Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Utafiti cha Magonjwa ya Binadamu cha Taifa (NIMR), Dk. Julius Massaga akizungumza na wanahabari mara baada ya uzinduzi wa kitabu cha utafiti wa Uandaaji wa ajenda ya kitafiti juu ya utafiti wa mifumo wa afya wa magonjwa, kifua kikuu na maleria na magonjwa ya kitropiki. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Utafiti cha Magonjwa ya Binadamu cha Taifa (NIMR), Dk. Julius Massaga akizungumza na wanahabari mara baada ya uzinduzi wa kitabu cha utafiti wa Uandaaji wa ajenda ya kitafiti juu ya utafiti wa mifumo wa afya wa magonjwa, kifua kikuu na maleria na magonjwa ya kitropiki.Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mbando , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Utafiti cha Magonjwa ya Binadamu cha Taifa (NIMR), Dk. Julius Massaga wakizinduwa kitabu cha utafiti kitakachosaidia uboreshaji mfumo wa huduma za afya, uandaaji wa ajenda za kitafiti juu ya utafiti wa mifumo wa afya wa magonjwa ya kifua kikuu na maleria na pamoja na magonjwa ya kitropiki (NTD). Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mbando , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Utafiti cha Magonjwa ya Binadamu cha Taifa (NIMR), Dk. Julius Massaga wakizinduwa kitabu cha utafiti kitakachosaidia uboreshaji mfumo wa huduma za afya, uandaaji wa ajenda za kitafiti juu ya utafiti wa mifumo wa afya wa magonjwa ya kifua kikuu na maleria na pamoja na magonjwa ya kitropiki (NTD).

  KITENGO cha Utafiti cha Magonjwa ya Binadamu cha Taifa (NIMR) leo kimezinduwa kitabu cha utafiti kitakachosaidia uboreshaji mfumo wa huduma za afya, uandaaji wa ajenda za kitafiti juu ya utafiti wa mifumo wa afya wa magonjwa ya kifua kikuu na maleria na pamoja na magonjwa ya kitropiki (NTD). 

  Akizinduwa utafiti huo leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mbando mwakilishi wa katibu mkuu huyo alisema utafiti huo umefanywa kwa nguvu ya pamoja kati ya Shirika la UNDP, Shirika la Afya Duniani (WHO), Watu wa Japani na Serikali ya Tanzania kupitia Kitengo cha Utafiti cha Magonjwa ya Binadamu cha Taifa (NIMR). Alisema kitabu hicho cha utafiti kimeangalia masuala gani muhimu yanayotakiwa kufanyiwa utafiti, kutambua na kutatua vitu vinavyotatiza mfumo wa afya kutotoa huduma inayostahiki na kwa mafanikio kwa wagonjwa au walengwa. 

  "..'Kitabu kimeangalia ni masuala gani muhimu ya kuboreshwa ili kusaidia kuboresha mfumo wa huduma za afya, huku ukipewa jina la 'Uandaaji wa ajenda ya kitafiti juu ya utafiti wa mifumo wa afya wa magonjwa, kifua kikuu na maleria na magonjwa ya kitropiki ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele hapo awali," alisema Dk. Mbando katika hotuba yake iliyosomwa na mwakilishi wake. 

  Alisema licha ya changamoto zinazoikabili sekta ya afya, mpango wa afya wa taifa umebaini vikwazo vitatu vikuu ambavyo vimekuwa changamoto katika kufikia malengo ya utoaji huduma bora kiufasaha ambapo alivitaja vikwazo hivyo hivyo kuwa ni pamoja na miundombinu ya afya, mgawanyiko wa watumishi wa afya na mfumo wa uongozi wa idara ya afya. Aliongeza kuwa pamoja na hayo suala zima la kikwazo cha upatikanaji wa bajeti ya kutosha katika eneo zima la shughuli za afya. 

   Hata hivyo licha ya changamoto hizo alisema Serikali imepata mafanikio kwa ujumla katika sekta ya afya, kwani kumekuwepo na mafanikio katika kupunguza vifo vya watoto wachanga na vifo kwa wajawazito, pia kupungua kwa kiasi kikubwa kwa vifo kwa watoto chini ya miaka 5 ambapo vifo vimepungua kutoka 137/1000 hadi 81/1000. fungua Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Utafiti cha Magonjwa ya Binadamu cha Taifa (NIMR), Dk. Julias Masaga akizungumza alisema mradi huo wa utafiti umefanywa sasa ili kuangalia kitu gani kipya ambacho kinaweza kusaidia kuzuia magonjwa ya kifua kikuu (TB), maleria na pamoja na magonjwa ya kitropiki (NTD). 

   "...Tumetafuta njia mpya ambazo zitasaidia kuzuia, watafiti wetu wamekaa kwa makundi matatu wakaangalia ni matatizo gani yanayokwamisha huduma hizi, lengo likiwa ni kupunguza matatizo ya kiafya na pia kuangalia namna ya kutatua. Tumefanya sasa ili kuangalia kitu gani kipya ambacho kinaweza kusaidia kuzuia haya magonjwa," alisisitiza Dk. Masaga katika hotuba yake. 

   Alisema pamoja na tafiti hizo hali halisi inaonesha ugonjwa wa maleria kwa sasa unapungua ikiwa ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo pia mabadiliko ya tabia nchi, huku ugonjwa wa kifua kikuu ukichochewa na ugonjwa wa Ukimwi. "Awali tulifanikiwa kwenye kifua kikuu ila kwa sasa umeanza kurudi ukichangiwa na ugonjwa wa Ukimwi na tafiti kama hizi zinatusaidia zaidi namna ya kukabiliana," alisema Dk. Masaga akizungumza na wana habari mara baada ya uzinduzi wa kitabu cha utafiti. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0

  unnamed (6)
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto) akisaini mkataba wa mkopo wa sh. Biloni 223 kwa niaba ya Serikali Tanzania ambapo makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Balozi Ufaransa nchini Malika Berak.
  unnamed (7)
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano mara baada ya kusaini ambapo hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Balozi Ufaransa nchini Malika Berak.
  unnamed (8)
  Balozi Ufaransa nchini Malika Berak akisistiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya kusaini mkataba wa mkopo wa sh. Biloni 223 kwa Serikali ya Tanzania ambapo makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua.
  unnamed (9)
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mkataba wa mkopo wa sh. Biloni 223 kwa niaba ya Serikali  ambapo makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dar es salaam.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
  ………………………………………………………………………….
  Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
  Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) imesaini makubaliano ya mkopo nafuu wenye thamani ya Sh. bilioni 223 za Kitanzania ambazo ni sawa Euro milioni 93 kwa ajili ya uboreshaji wa sekta ya maji na umeme nchini.
   
  Makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dar es salaam ambapo kwa upande wa Tanzania Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua amesaini kwa niaba ya Serikali na kwa upande wa Serikali ya Ufaransa imewakilishwa na Balozi wake nchini Malika Berak na Mwakilishi wa AFD Yves Boudot.
   
  Dkt. Mwinyimvua amesema kuwa fedha hizo kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa  zimetolewa kwa ajili ya kutiasaini mikataba mitatu ili boresha upatikanaji wa huduma za jamii.
   
  Mkataba wa kwanza unahusisha sekta ya maji ambao wenye thamani ya Euro milioni 40 utakaosaidia kuboresha huduma ya uzalishaji maji, utunzaji maji safi na salama pamoja na kuboresha huduma ya maji taka nchini katika maeneo ya mijini na vijijini.
   
  Dkt. Mwinyimvua alisisitiza kuwa mkataba wa pili una thamani ya Euro milioni 53 kwa lengo la uboreshaji wa sekta ya umeme nchini ambapo vituo 10 vilivyo chini ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na vitanufaika na mkopo huo ili kutakarabati mtandao wa miundo mbinu ya umeme na kukabiliana na upotevu wa umeme nchini.
   
  Vituo hivyo vitakavyokarabatiwa ni Chalinze, Mlandizi, Same, Tabora, Mbeya, Mufindi, Dodoma, Mwanza na Bukoba pamoja na Mkongo wa Taifa.Na mkataba wa tatu unahusisha mkataba wa Tanzania na Ufaransa wa mwaka 1998 ambao ni umekuwa wa muda mrefu ili kuendana na hali ya sasa ambapo yametokea mabadiliko mengi ambayo yanapaswa kuendana na wakati.
  Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kudumisha ushrikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili.
   
  Ushirikiano wa Tanzania na Ufaransa katika miradi ya maji na umeme  umekuwa na tija kwa wananchi kijamii na kiuchumi tangu miaka ya 2009 ambapo Shirika la AFD lilitoa zaidi ya sh. Bilioni 628.

  0 0

  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari usiku huu nje ya ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma, mara baada ya kumalizika kwa Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilichokaa kupitisha majina matano ya wagombea Urais yatakayopelekwa kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM kujadiliawa hapo saa nne asubuhi. Nape hakutaja majina ya wagomea hao waliopita kwenye tano bora, kwa kuseka atataja asuhuhi. 
  Muda mfupi baada ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari, walitoka wajumbe watatu wa Kamati Kuu ambao ni Dkt. Emmanuel Nchimbi, Mh. Sophia Simba na Mh. Adam Kimbisa ambao walizungumza na waandishi wa habari juu ya walichokizungumza kwenye kikao hicho, ambapo wao walisema wamegomea makubaliano ya majina yaliyopitishwa kwenye kikao hicho kwa madai kwamba Kikao kikekiuka tararibu za uchujaji wa majina hayo. kwani yalijadiliwa majina machache tu na kupitishwa kwenda tano bora, lakini nao hawakuyataja majina hayo.

  0 0

   Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari asubuhi hii nje ya Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma, akithibitisha taarifa iliyokuwa ikizagaa mitandaoni ya Wagombea Urais walioingia katika hatua ya tano bora, ambao aliwataja kuwa ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Mh. Bernard Membe, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh. January Makamba pamoja na Balozi Amina Salum Ali. Majina hayo yanapelekwa kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kujadiliwa na kupatikana matatu yatakayopelekwa kwenye Mkutano Mkuu na kupatikana moja ambaye ndie atakuwa Mgombea Urais.

  Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa nje ya Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma leo.

  0 0

    Wananchi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa katika harakati za kutafuta mahitaji kuelekea sikukuu ya kuhitimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
   Mzigo ukishushwa tayari kwa kuuzwa.
  Msongamano wa magari  katikati ya kariakoo jijini Dar es Salaam.
  Hapa ni maongezi ya biashara na kununua tuu.
  Hapa ni hatari zaidi kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam maeneo ya mtaa wa Congo.
  Picha zote na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  JAMII imetakiwa kutambua mahitaji ya watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea  katika kubaini  changamoto zao katika maisha wanayoishi na kuweza kuguswa kutoa msaada.
  Hayo ameyasema leo Mhasibu Mwandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Idara za Serikali na Mabalozi,Wema Mbaga wakati akitoa msaada wa kituo Khilati Kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam,amesema kuwa wanatambua umhimu wa kutoa msaada kwa makundi maalumu wakiwemo watoto wanaolelewa katika vituo.
  Amesema kuwa watoto wanachangamoto nyingi katika ukuaji wao ikichangiwa na kuondokewa na wazazi wao hivyo wanahitaji faraja kutoka kwa jamii katika kuweza kufikia ndoto zao.
  Wema amesema watu wengine wanawajibu kuwakumbuka watoto katika katika kipindi hiki cha kuelekea Siku Kuu ya Idd El-Fitri kuwaza kupata mahitaji yao.
  Vitu walivyotoa ni Magodoro ,Daftari,Kalamu ,vyenye thamani y ash.milioni 1.5 ambapo ni sehemu ya mchango wao.
  Mkurugenzi wa Kituo hicho ,Khadija Hussein  amesema kutuo kinachangamoto ya eneo kwani eneo waliopo watoto wanalipia kodi pamoja na matatizo ya chakula.
  Amesema watu wenye uwezo watembelee kituo hicho na kuona mahitaji yao ili waweze kusaidia katika kulea watoto hao ambao wako 65.
  Mhasibu Mwandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Idara za Serikali na Mabalozi,Wema Mmbaga akitoa akikabidhi msaada kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Watoto Yatima cha  Khayrat  Kilichopo ,Kigogo,Khadija Hussein katika hafla iliyofanyika kituo hicho ,jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Kituo cha Watoto Yatima cha  Khayrat,Khadija akizungumza na waandishi wa habari juu ya msaada walioupata katika hafla iliyofanyika kituo hicho ,jijini Dar es Salaam.
   Mhasibu Mwandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Idara za Serikali na Mabalozi,Wema Mmbaga akizungumza na waandishi wa habari juu ya msaada walioutoa katika kituo cha kulele watoto yatima cha Khayrat, katika hafla iliyofanyika kituo hicho ,jijini Dar es Salaam.  
  Sehemu ya watoto katika kituo cha Khayrat wakiwa na daftari zilizotolewa na NSSF Mkoa wa Idara za Serikali na Mabalozi katika hafla iliyofanyika kituo hicho ,jijini Dar es Salaam. 

  0 0

   Watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam wakiwa wamekaa katika kituo hicho mara baada ya Chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA),kuwatembelea na kufuturu pamoja nao katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
  Wanachama wa  Chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA) wakichukua Futari kwaajili ya kuwagawia watoto wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam jana.
  Mfanyakazi wa Wanachama wa Chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA),akiwawekea Futari kwaajili ya kufutari pamoja na watoto wa kituo cha watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo vingunguti jijini Dra es Salaam jana.
   
   Watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini wakifutari pamoja na wanachama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA) walipo futuru pamoja na watoto hao katika kituo cha Mwana jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Kituo cha watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam, Mohamed Wage akiwashukuru wanachama wa Chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA),walipoamua kutembelea kituo cha mwana.
  Mwakilishi wa  Chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA), Stella Manongi(wa kwanza kushoto) akizungumza na watoto wa kituo cha Mwana (hawapo pichani) mara baada ya kufutari na watoto hao.
  Pia wanachama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA), walitoa msaada wa vitu pamoja na fedha tasilimu na baadi ya vyakula ambavyo vitawasaidia watototo hao kwa siku zijazo kama inavyoonekana wakivitoa vitu hivyo kwenye gari.
  Mwakilishi wa chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA) akimkabidhi vitu mbalimbali Mkurugenzi wa Kituo cha watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam, Mohamed Wage, Mara baada ya Kufutari pamoja na watoto hao.
  Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

  0 0

   Kazi zikiendele katika mitaa mbalimbali ya Kariakoo jijini Dar es Salaam ikiwa na matengenezo ya fremu mbalimbali.
  Nondo zikiwa katwa kwaajili ya kutengeneza fremu katika mtaa wa Congo ,Kariakoo jijini Dar es Salaam.
  (Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)

  0 0


  mail.google.com

  0 0

  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari jioni hii juu ya kilichofanyika kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM, ambapo amesema kuwa sasa NEC inapiga kura kupata majina matatu yatakayopelekwa kwenye Mkutano Mkuu unaotarajiwa kufanyika Usiku wa leo majira ya saa tatu, kwenye Ukumbi wa Dodoma Convetion Centre.

  0 0

  Mtangaza nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini ,Edmund Rutaraka akiwasili katika ofisi za Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro,kwa ajili ya kikao na wajumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho wa wilaya chenye lengo la kutangaza azma yake ya kugombea Ubunge katika jimbo hilo.
  Mwenyekiti wa Makatibu, wa CCM,Kilimanjaro Nemes Kaingirila Maufi akizungumza wakati wa kikao malumu cha kutangaza nia kilichoitishwa kwa ajili ya Naibu kamanda wa vijana wilaya ya Moshi mjini na Mjumbe wa NEC wa chama hicho,Edmund Rutaraka (kulia) kutangaza nia ya kugombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini.
  Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya  CCM wilaya ya Moshi mjini wakifuatilia mkutano huo.
  Naibu Kamanda wa Vijana wa CCM Manispaa ya Moshi na mjumbe wa NEC ,Edmund Rutaraka akizungumza na wajumbe wa Halmshauri kuu  CCM ya wilaya ya Moshi mjini 
  Mtia nia Edmund Rutaraka pia ametumia maji ya kunywa kutangaza Nia yake hiyo baada ya wajumbe wote walioshiriki mkutano huo kugaiwiwa yakiwa na lebo maalumu yenye maandishi pamoja na picha yake.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akimuongoza Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum na wadau wa mfuko huo kupakua futari iliyoandaliwa na PPF Kanda ya Temeke kwa wadau wake, Dar es Salaam
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akizungumza na wadau wa mfuko huo baada ya kupata futari iliyoandaliwa na PPF Kanda ya Temeke, Dar es Salaam juzi. Wengine kutoka kulia kwake) ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, Mwakilishi wa Sheikh wa Wilaya ya Temeke, Sadi Msati na Msaidizi wa Sheikh Ahad Musa, Athumani Mkambaku.

   Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akitoa shukrani zake baada ya futari hiyo
   Sheikh Alhadi, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Erio.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akimkabidhi Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, alhad Mussa Salum zawadi iliyotolewa na mfuko huo Kanda ya Temeke kwake baada ya kupata futari iliyoandaliwa na PPF Kanda ya Temeke, Dar es Salaam

  Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF na wafanyakazi wa Mfuko huo, wakipakua futari iliyoandaliwa na PPF Kanda ya Temeke kwao, Dar es Salaam 

  0 0

   Balozi Amina Salum Ali
   Dkt John Pombe Magufuli
  Dkt Asha Rose Migiro.

  Pichani ni majina matatu ya wagombea kiti cha Urais kwa chama cha CCM,yaliyopitishwa jioni ya leo na Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM,ambapo kati ya hayo majina matatu kupitia Mkutano Mkuu wa CCM unaotarajiwa kufanyika usiku huu utaibua jina la mtu mmoja tu ambaye  atatambulika kuwa ndiye mgombea kiti cha Urais kupitia chama hicho cha CCM

  0 0


   
  Na Woinde Shizza,Arusha
  Ukosefu wa Chakula sheleni hususan zile zinazomilikiwa na serikali
  umetajwa kuwa chanzo kikubwa kinasababisha wanafunzi kutoroka
  mashuleni na kwenda kujitafutia chakula hali inayoathiri taaluma na
  maendeleo ya elimu nchini.  Mwanakijiji wa kijiji cha Arkata  Kipara Ngine amesema kuwa watoto
  wengi wamekua wakitoroka shuleni kwa kukosa chakula hivyo kupelekea
  idadi ndogo ya mahudhurio  mashuleni.

  Kipara ameihasa saerikali kwa kushirikiana na mashirika binafsi pamoja
  na wazazi kuhakikisha upatikanaji wa chakula  katika sahule ya msingi
  Arkata iliyopo wilaya ya Monduli mkoani hapa.

  Mwenyekiti wa Kamati ya  Shule Kipi Alarosi  amesema kuwa licha ya
  changamoto ya utoro bado shule hiyo inakabiliwa na uchakavu wa majengo
  na upungufu wa madarasa hivyo ameiomba jamii na wapenda maendeleo
  wajitokeze kuiwezesha shule hiyo iweze kufanya vizuri kitaaluma.

  “Shule haina madirisha na majengo yamechakaa mvua ikinyesha inaingia
  mpaka darasani watoto hawasomi vizuri hata kipindi cha jua vumbi
  linajaa darasani “ Alisema Mwenyekiti.

  Mkurugenzi wa Shirika la wafugaji Monduli Pastoralist Development
  (MPDI) Erasto Sanare  amesema kuwa baada ya kupokea ombi la shule hiyo
  watatua fedha za ukarabati wa  madarasa ya shule hiyo ili kuwajengea
  watoto mazingira bora.

  Alisema mwamko wa jamii ya wafugaji katika masomo umekua kwa kiasi
  kikubwa  mashirika na watu binafsi yakijitoa kusaidia kutatua
  changamoto zao ili watoto wa wafugaji wapate elimu bora.

  0 0


   Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Segerea,  Steve Massaburi akiwa Hospitali ya Aga-khan leo akiendelea na matibabu.
  Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Segerea,  Steve Massaburi akiwa Hospitali ya Aga-khan leo akiendelea kuuguza majeraha baada ya kujeruhiwa kwa mapanga nyumbani kwake Segerea jijini Dar es Salaam jana na watu wasiojulikana. Kushoto anayemuhudumia ni jamaa yake Martin Pemba.

  Na Dotto Mwaibale

  WATU wasiojulikana wamejeruhi kwa mapanga Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Segerea Steve Massaburi usiku wa kuamkia juzi nje ya nyumba yake alipokua akirejea kutoka matembezini.

  Kwa mujibu wa Steve aliyelazwa katika Hospitali ya Aga khan, watu hao wapatao wanne wakiwa na Pikipiki, walimvamia majira ya saa tatu usiku nje ya geti la nyumba anayoishi na kuanza kumshambulia huku yeye akijaribu kupambana nao.

  Steve ambaye ni mtoto wa Meya wa Jiji la Dar es salaam Dk. Didas Massaburi, alisema wakati watu hao wakimshambulia walikuwa wakisema wazi wazi kuwa lengo lao ni kumuona hagombei nafasi ya udiwani katika Kata hiyo ya Segerea baada ya yeye kuonyesha nia ya kutaka kugombea nafasi hiyo.

  “Walikuwa wakiniambia kuwa wewe si unautaka udiwani sasa utaugombea ukiwa kitandani au kaburini, hapa hakuna na umaharufu wa mtu kwa kuwa kila mtu anaitaka nafasi hiyo” alisema Massaburi.

  Alisema wakati akiendelea kupambana na watu hao alikuwa akipiga kelele jambo lililowafanya watu hao kumuacha na kasha kukimbia huku yeye akiwa amelala chini damu zikimtoka sehemu za shavuni kutokana na panga alilopigwa.

  Pamoja na sehemu ya shavuni, watu hao pia wamemjeruhi sehemu mbalimbali za mkono wake wa kushoto alipokuwa akijaribu kuzuia panga kumdhuru sehemu za usoni.

  “Kelele nilizopiga ndizo zilizonisaidia kwa kuwa ziliwafanya watu watoke katika majumba yao kuja kunisaidia wakati huo huo watu hao wakikimbia kwa kutumia pikipiki zao mbili walizokuwa wamekuja nao” aliongeza.

  Alisema kwa sasa hali yake inaendelea vizuri  tangu alipofikishwa hospitalini hapo jana huku akishonwa nyuzi zaidi ya ishirini katika taya lilipigwa na panga na watu hao. (Imeandaliwa na mtandao wa www.
   


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Momba Richard Mbeho kushoto kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya leo tarehe 11 Julai 2015 tayari kwa kuanza mbio zake za siku nne Mkoani Rukwa. Mwenge wa Uhuru utatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Tsh. bilioni 11. 
  Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akishika Mwenge wa Uhuru ulipowasili  Mkoani Rukwa leo tarehe 11 Julai 2015.

   Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mkutano Mkoani Rukwa wakiwa wamebeba bendera ya taifa kwa ajili ya kuipeleka na kuipeperusha eneo la makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Mbeya kwenda Mkoa wa Rukwa.
   Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Erasmus Rugarabamu akishika mwenge wa Uhuru baada ya kuwasili Mkoani Rukwa leo.
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Juma Khatibu Chum akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi mradi wa maji ya mserereko katika kijiji cha Kamnyazia Wilayani Sumbawanga leo katika ziara ya mbio za mwenge wa Uhuru Mkoani Rukwa.
  Sehemu ya wananchi wakishuhudia mwenge wa Uhuru Mkoani Rukwa leo.
  
  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)

older | 1 | .... | 580 | 581 | (Page 582) | 583 | 584 | .... | 1897 | newer