Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 579 | 580 | (Page 581) | 582 | 583 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Kikosi kamili cha timu ya Wazalendo kabla ya mchezo wa fainali.
  Kikosi kamili cha Himo fc kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali .
  Katibu Mwenezi wa chama cha NCCR -Mageuzi ,Stanley Temba akiwa ameongozana na katibu wa Vijana wa chama hicho katika jimbo la Vunjo  Danieleson Shayo wakisalimiana na wachezaji wa timu zote mbili kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali.
  Waamuzi wa mchezo huo,Kabwe Korona,Beda Lyimo na Nassib wakizungumza na manahodha wa timu hizo.
  Benchi la ufundi la timu ya Wazalendo likongozwa na raia wa Kigeni.
  Heka heka ndani ya uwanja .
  Baadhi ya Mashabiki waliofika kushuhudia mchezo huo wa fainali.
  Mmoja wa Shabiki wa timu ya Himo fc ,Mzee Rashid aliyekuwa kiutio katika mchezo huo hasa kutokana na midadi aliyokuwa nayo wakati mchezo ukiendelea.
  Mchezo huu ulikuwani burudani kwa wakazi wa mji wa Himo wa jinsia zote.
  Huyu hakuweza kufahamika mara moja kama alikuwa ni Shabaiki wa moja ya timu zilizokuwa zikicheza.
  Licha ya mchezo kuendelea bado uwanjani kulionekana kuwepo kwa kuku wakiendelea kutafuta chakula.
  Hata hivyo mchezo huo uliingia Dosari baada ya kutokea kwa vurugu zilizopelekea mchezo kuvunjwa.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Mkuu wa kituo cha Kulelea Watoto yatima cha Al-Madina, Bi. Kulthum Juma akizungumzia kuhusu kituo hicho pamoja na kutoa shukrani kwa kampuni ya Multichoice Tanzania kwa kuendelea kukisaidia kituo cha hicho ambacho kina takribani watoto 68 na pia kituo hicho kipo eneo la Tandale kwa Tumbo jijini Dar.
  Ustadhi Mashaka Salim akitoa neno.
  Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania, Peter Fauel akichukua chakula wakati wa kuwafuturisha watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Al-Madina kilichopo Tandale kwa Tumbo, Wa pili kutoka kulia ni Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo.
  04
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi, akitoa huduma ya chakula kwa watoto yatima hii ikiwa ni njia mojawapo ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
  Baadhi ya Watoto yatima, Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania pamoja na viongozi wa kituo hicho cha Al-Madina wakichukua chakula katika futari iliyoandaliwa na kampuni ya Multichoice Tanzania.


   
  Baadhi ya Watoto yatima, Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania pamoja na viongozi wa kituo hicho cha Al-Madina wakijumuika katika futari hii ikiwa ni moja wapo ya kutoa msaada katika vituo mbalimbali hapa nchini.
  Meneja wa Fedha wa Multichoice Tanzania, Francis Senguji akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Kampuni ya Multichoice Tanzania kwa waliofika na kujumuika nao katika futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Multichoice Tanzania.

  0 0

   Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman na ujumbe wake pamoja na maafisa wa bunge wakiingia Bungeni tayari kwa hotuba ya mwisho ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma Alhamisi Julai 9, 2015
  Marais wastaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa na Mawaziri wakuu wastaafu Dkt Salim Ahmed Salim, Jaji Joseph Sinde Warioba, Mhe. Frederick Sumaye na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na maafisa waandamizi jeshini na serikalini wakiwa wamesimama wakati viongozi wakiingia bungeni.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akiingia bungeni.
   Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali akiingia katika ukumbi wa Bunge.
   Spika Anne Makinda akimuongoza Rais Kikwete kuingia bungeni.
   Rais Kikwete akiingia bungeni huku akishangiliwa na wabunge.
   Rais Kikwete akiingia bungeni.
   Rais Kikwete na Spika Makinda wakielekea kuchukua nafasi zao.
   Sehemu ya ukumbi wa bunge wakati Rais Kikwete akiingia.
  Waheshimiwa wabunge
   Sehemu ya maafisa waandamizi wa bunge.
   Rais Kikwete akianza kuhutubia wabunge.

   Sehemu ya maafisa waandamizi wa bunge.
   Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake.
   Waheshimiwa wabunge wakiwa wametulia kumsikiliza Rais Kikwete.
   Sehemu ya wageni mashuhuri wakifuatilia hotuba.
   Sehemu ya wabunge.
   Wake wa viongozi, watoto wa Rais Kikwete na maafisa mbalimbali.
   Sehemu ya Mabalozi .
   Wabunge wakifuatilia hotuba.
   Wabunge wakifuatilia hotuba.Continue reading →

  0 0

   Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw.Raymond Mushi akifungua mafunzo ya wasimamizi wa uandikishaji wa Wananchi katika Daftari la Kudumu la wapiga kura kupitia mfumo wa BVR litakalofanyika Julai 16 hadi 25 mwaka huu.
  Picha na 3 Wasimamizi wa uandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga
  kura katika jiji la Dar es salaam wakiwa katika mafunzo hayo.
   
  Na. Aron Msigwa - Dar es salaam.
  Serikali imesema kuwa zoezi la uandikishaji wa wananchi katika Daftari
  la Kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo wa BVR katika jiji la Dar
  es salaam litafanyika kama ilivyopangwa kuanzia Julai 16 hadi 25 mwezi
  huu kwa mafanikio makubwa kutokana na maandalizi mazuri yaliyofanywa
  na Tume ya uchaguzi kwa kushirikiana na Manispaa za mkoa huo.

  Akizungumza wakati ufunguzi wa Mafunzo ya siku 2 ya wasimamizi wa
  uchaguzi wa mkoa huo leo jijijini Dar es salaam, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
  Dar es salaam na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw.Raymond Mushi amesema
  lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wasimamizi wa Manispaa hizo
  ili zoezi la uandikishaji wa wananchi katika daftari
   la kudumu la wapiga kura katika jiji la Dar es salaam lifanyike kwa
  kiwango cha hali ya juu na kuzuia makosa yaliyojitokeza katika maeneo
  mengine nchini.

  Amewataka wasimamizi hao kufanya kazi kwa viwango na weledi wa hali ya
  juu ili kuzuia malalamiko kutoka kwa wananchi kwa kuhakikisha kuwa
  kila raia mwenye sifa anaandikishwa katika daftari hilo.

  Amesema kuwa wananchi wote watakaofika kwenye vituo kujiandikisha
  wahakikishe kuwa wana taarifa muhimu kuhusu uraia wao pia wahakikishe
  kuwa wanafuata taratibu zilizowekwa na Tume ili waweze kuandikishwa.

  "Natoa wito kwa wananchi wote waliokidhi viwango vya kupiga kura
  na wale watakaofikisha umri wa kupiga kura ifikapo 25 Oktoba 2015
  wajitokeze kwa wingi maana wote wataandikishwa"

  Amesisitiza.
  Aidha, amewataka wasimamizi hao kufanya kazi kwa weledi, kutoa
  ufafanuzi na elimu kwa wananchi pale inapobidi wakati wa ukusanyaji wa
  taarifa zao na kuepuka kutumia lugha ya
   kuudhi ili kazi hiyo iwe rahisi na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza
  kwa wingi katika kujiandikrsha na kuepuka vitendo vya vurugu na siasa
  zinazoweza kuleta machafuko katika vituo vya uandikishaji,

  Ametoa wito kwa baadhi ya wanasiasa watakaofika kujiandikisha kwenye
  daftari la kudumu kuepuka kuingilia zoezi hilo kwa kuwa wao sio
  watumishi wa Tume ya uchaguzi.

  "Kuna maeneo nchini baadhi ya wanasiasa wamekuwa chanzo cha
  kusababisha vurugu kwenye vituo vya uandikishaji, wao kama raia wanalo
  jukumu la kufika kujiandikisha na kuangalia watu wanaojiandikisha kama
  sehemu ya haki na wajibu wao kufuatilia ufanisi wa zoezi hilo na sio
  kuingilia kazi za wataalam wa Tume"

  Kwa upande wake Afisa TEHAMA Mwandamizi kutoka Tume ya Uchaguzi Bw. Joseph Mally, Afisa Amesema kuwa Mafunzo hayo ya siku 2 yaliyohusisha wasimaizi 36 wa uchaguzi ngazi ya jimbo kwa manispaa zote tatu Ilala, Kinondoni na Temeke ambao nao watatoa mafunzo hayo
   kwa wasimamizi wa Kata 36, ujazaji wa Fomu na matumizi ya mashine za BVR.

  Amesema wao kama Tume ya Uchaguzi watahakikisha kuwa wanatembelea
  vituo vyote vya uandikishaji ili kukabiliana na changamoto mbalimbali
  zitakazojitokeza.

  Aidha kwa kuzingatia wingi wa idadi ya watu katika jiji la Dar es
  salaam kutakuwa na mashine 3500 zitakazofanya kazi katika vituo 1000
  huku kukiwa na wataalam zaidi ya 600 waliopatiwa mafunzo kwa lengo la
  kukamilisha kazi hiyo na kukabiliana na changamoto zilizojitokeza
  katika maeneo mengine.

  "Kwa upande wa Tume tunaendelea kujipanga ili kuhakikisha kuwa
  changamoto zilizotokea katika maeneo mengine hazitokei, tunatoa wito
  kwa wananchi watakaofika kwenye vituo kuandikishwa wawe wamekidhi
  vigezo vilivyowekwa kulingana na vielelezo vya uraia, na umri"
  Amesema.

  Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo kutoka Manispaa za Temeke,
  Ilala na Kinondoni wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati
   wa mafunzo hayo wamesema kuwa mafunzo hayo ya siku 2 yanawajengea
  uwezo wa kuelewa namna ya kuandikisha wapiga kura, ujazaji wa fomu
  ,uelewa wa sifa za mtu anayestahili kuandikishwa na matumizi ya
  mashine za BVR.

  0 0


  STAR TV NEWS CLIPPS

  Benki ya Dunia yatoa ripoti yake juu ya mwelekeo wa uchumi nchini huku ikibainisha changamoto kadhaa katika ukusanyaji mapato. http://youtu.be/hrfyJhtxZ2o


  Wizara ya mali asili na utalii yaweka mikakati ya kukabiliana na uharibifu wa misitu ambao umekuwa ukiliingizia taifa hasara kubwa kwa mwaka. http://youtu.be/0MAjFbS_mqI


  Madiwani wa halmashauri ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro wamtaka Mkurugenzi halmashauri hiyo kuwachukulia hatua kali baadhi ya watendaji wa kata na vijiji kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za maendeleo. http://youtu.be/ImrVg0_YwsY


  TBC NEWS CLIPPS

  Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya yapongezwa kwa kuvuka lengo la kupanda miti zaidi ya million katika kipindi cha nwaka mmoja uliopita.http://youtu.be/IDfZsp0w6Lo  Wadau wa vyama vya siasa na tume ya uchaguzi Zanzibar wanatarajiwa kutiliana saini ya maadili ya uchaguzi ili waweze kukubaliana kwa pamoja masuala muhimu ya uchaguzi huo. http://youtu.be/kEhWeNc-Qm0  Kamati kuu ya CCM inakutana mjini Dodoma kwa ajili ya mchakato wa mchujo wa wagombea wa nafasi za uraisi. http://youtu.be/_yJWnG7ppKI  Spika Anne Makinda awaasa wabunge kurejea katika misingi ya umoja na utulivu nchini huku akisifu yaliyo fanywa na Raisi Kikwete. http://youtu.be/qP6FF55yMi4  Wananchi watakiwa kujitokeza kwa wingi katika uandikishaji wa BVR katika mkoa wa Dar es Salaam unao tarajiwa kuanza julai 16 mwaka huu. http://youtu.be/DZ4odFYSAo4  CH10 NEWS CLIPS  Tume ya taifa ya kudhibiti Ukimwi yajivunia katika kusaidia kupima afya za wananchi zaidi ya 2000 katika viwanja vya sabasaba. http://youtu.be/apUcaDxqPb4  Halmashauri ya manispaa ya Temeke yasema imefanikiwa kukusanya mapato ya ndani katika miaka 4 iliyopita kutoka shilingi billion 12 kwa mwaka hadi billion 31. http://youtu.be/vPm5B3U3Ew0  Raisi Kikwete atoa rai kwa vyama vya siasa kuweka ahadi ya kuwezesha uchaguzi mkuu kuwa huru na wa haki kwa kuzingatia maadili ya uchaguzi. http://youtu.be/GR5_IiSYfOM  Raisi Kikwete aridhia kugawanya mkoa wa Mbeya na kuwa mikoa 2 huku pia akiridhia kuanzishwa kwa wilaya kadhaa nchini. http://youtu.be/0Hl-uJ1LJ4U  Kada mkongwe wa CCM Kingunge Ngombare Mwiru aitahadharisha CCM, kufuatia kauli za viongozi wake huku akimkosoa Nape Nauye.  http://youtu.be/hvQuGnxncwQ  Mama mmoja mkazi wa Morogoro awaomba watanzania kumsaidia kiti kwa ajili ya mtoto wake alijifungua akiwa mlemavu. http://youtu.be/bmOtMl3mZnY  Vibanda kadhaa vya wafanyabiashara katika eneo la Ubungo Kibangu vyateketea kwa moto baada ya moto kulipuka kwenye godawn. http://youtu.be/nK8mls45QqA  AZAM TV NEWS CLIPPS

  Tanzania yaonekana kuwa moja ya nchi barani Afrika iliyofanikiwa katika sekta ya mawasiliano huku suala la ajira likiwa bado changamoto kubwa.http://youtu.be/erTH7rh8RkU  Idara ya uhamiaji ya Tanzania yakiri uwepo idadi kubwa ya watanzania wanao uza passport zao za kusafiria kwa tama ya pesa huku zikitumika katika uhalifu. http://youtu.be/ReaKw8_cfMo  Wananchi watoa rai kwa viongozi wa ngazi za juu wakiwaomba kuteua kiongozi aliye bora kwa watanzania. http://youtu.be/XFn2i2qz4W8  Katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha Mapinduzi azungumzia mchakato wa uteuzi wa mgombea huku akitanabaisha hali jinsi ilivyo. http://youtu.be/GWZnjL8LRXA


  Joto la uchaguzi ndani ya CCM katika nafasi ya Uraisi laendelea kupanda kwa kasi huku wagombea wa nafasi hiyo wakitoa ya moyoni. http://youtu.be/_C5lpnaWJTU

  0 0
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhem Meru ( kulia) akiwa  na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Miradi la Ujerumani  la  Giz  nchini Tanzania,  Dkt. Sussane Grimm  ( kushoto)    wakitia saini  hati  ya Makubaliano  ya kusimamia na kuendeleza Maliasili nchini. Hafla hiyo fupi ilifanyika Jijini Dares Salaam, Makao Makuu  ya  Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House.


   Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhem Meru ( kulia) akiwa   na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la  Miradi la Ujerumani  la Giz  nchini Tanzania,  Dkt. Sussane Grimm  ( kushoto)    wakibadilishana  hati  ya Makubaliano  ya usimamizi na uendelezaji wa  Maliasili nchini. Hafla hiyo fupi ilifanyika Jijini Dares Salaam, Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House.


  Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la Miradi  la   Ujerumani  la Giz la  nchini Tanzania imetia saini  hati ya  makubaliano na  Serikali ya Tanzania kupitia  Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuendeleza na kusimamia Maliasili zilizopo nchini.

  Hati hiyo ya Makubaliano   imesainiwa   na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhem Meru na  Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Giz  nchini Tanzania,  Dkt. Sussane Grimm .

   Utiaji saini huo umefanyika  Jijini Dares salaam,  Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House,  na kushuhudiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori , Bw. Herman Keryaro pamoja na baadhi ya  Maafisa  wa Wizara hiy.

  Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la Miradi  la   Ujerumani  la Giz  nchini Tanzania imeongeza kiasi cha Euro million tatu  sawa na billion kumi  kwa pesa za Kitanzania katika kusaidia usimamizi wa kiufundi ikiwemo  uanzishwaji wa Mamlaka ya Wanyamapori nchini Tanzania ( TAWA) .   Pia Makubaliano hayo yatadumu kwa muda wa  miaka mitatu katika kusimamia na kuendeleza Maliasili nchini.

  Uhusiano   kati ya Serikali ya Ujerumani  kupitia Shirika la Miradi  la   Ujerumani  la Giz  nchini Tanzania  na  Serikali  ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ulianza mwaka 2014.

  Pia  Shirika la Miradi  la   Ujerumani  la Giz  nchini Tanzania imekuwa   ikishirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia  Wizara ya Maliasili na Utalii katika kipindi cha mpito cha Uanzishwaji wa Mamlaka ya Wanyamapori ( TAWA)  katika kuwandaa watumishi  kufanya kazi katika Mamlaka hiyo 

  0 0
 • 07/10/15--01:53: TANZIA
 • MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI, MENEJIMENTI NA WAFANYAKAZI WOTE WA KAMPUNI YA UWEKEZAJI YA UTT (UTT-AMIS) WAMEPOKEA KWA HUZUNI KUBWA HABARI YA KIFO CHA ALIYEKUWA MWENYEKITI MUASISI WA DHAMANA YA UWEKEZAJI TANZANIA (UTT) (2003-2009)

  IKUMBUKWE, MAFANIKIO YA UTT AMIS, UTT PID NA UTT MICROFINANCE NI KUTOKANA NA MISINGI BORA YA UONGOZI ALIYOWEKA WAKATI WA KIPINDI CHAKE. NI DHAHIRI, UTT-AMIS NA SEKTA NZIMA YA MASOKO YA FEDHA NA MITAJI ITAMKUMBUKA BALOZI MULOKOZI KWA MCHANGO WAKE MKUBWA. 

  MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI AMEN.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Bank Of Africa Tanzania (BOA), Ammish Owusu Amoah akizungumza katika hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake na kufanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Bank Of Africa Tanzania (BOA), Ammish Owusu Amoah akizungumza katika hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake na kufanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Bank Of Africa Tanzania (BAO), balozi Mwanaidi Maajar akizungumza wakati wa hafla iliyoandaliwa na benki ya BOA kwa ajili ya kufuturisha wateja wake katika hoteli ya Serena Dar es Salaam. 
   Wateja wa benki ya BOA wakipata futari katika hoteli ya Serena.
   Wafanyakazi wa BOA wakijumuika na wateja wa benki hiyo kupata futari.
   Wateja wa Bank Of Africa Tanzania wakipata futari.
   Mkurugenzi Mkuu wa Bank Of Africa Tanzania (BOA), Ammish Owusu Amoah (katikati) akipata futari katika hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake.
  Sehemu ya wateja waliofika katika hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na Bank Of Africa Tanzania kwa ajili ya wateja wake.

  0 0

  The ‘composition’ challenge discussed on ‘UBISHI’

  Released July 10, 2015  One of the great opportunities that we have in accelerating the fortunes of this great country is addressing, what I like to refer to as, our ‘composition’ challenge; what kind of people make up our populous, in particular our youth, in terms of skills, competencies and values. 


  If you are making strides in life and form part of the top echelons of society, the plight of the bottom of the food chain may not be of particular interest to you – think again! 


  Irrespective of its composition, the broad bottom will always carry the narrow top.  The masses, at large, are either consumers of the products that keep our companies running and or are the ones casting the votes that inform who will lead our country. 


  Are you still not interested in the plight of broad bottom?

  I reflect briefly on this in this week’s Ubishi Talk Show series, visit or https://youtu.be/fo7Jm2KpkZ4or www.magavilla.com/videoswhere you can view my other videos.

  Regards,

  Magavilla, Costantine aka Kifimbo
  Twitter/Instagram: cmagavilla FB/Linkedin: costantine magavilla.

  0 0


  0 0

  KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye, akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo asubuhi Julai 10, 2015. 

  Nape amesema, leo hii majina matano ya makada wa chama hicho walioomba kuteuliwa na CCM kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yatajulikana, na kufuatia majina matatu ya makada hao ambayo yatapelekwa mbele ya Mkutano Mkuu utakaofanyika Jumamosi Julai 11, 2015. 

  Nape amesema vikao vyote vinaanza leo saa nne, na hakuna kikao chochote kilichokwisha fanyika ikiwa ni pamoja na kile kinachozungumzwa sana na vyombo vya habari yaani kikao cha kamati ya maadili ya chama hicho ambacho ndicho kinachokata majina na kutoa mapendekezo Kamati Kuu. 

  Alipoulizwa ucheleweshwaji huo umetokana na nini, Nape alisema "Nyote mmeshuhudia, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, amekuwa na kazi nyingi katika kipindi cha siku mbili hizi na hivyo asingeweza kusimamia vikao hivyo kama ilivyotarajiwa ingawa amedokeza kuwa "wakubwa" hao walikuwa wakikutana kwa majadiliano na wadau kingawa hakueleza ni wadau gani.
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa White House, Mjini Dodoma leo Julai 10, 2015.

  0 0

  ·         ORIGINAL KOMEDI WAWA KIVUTIO

  Siku ya PSPFiliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF ilifana na kuvutia mamia ya wananchi waliotembelea maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yaliyomalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
  Siku hiyo ni maaluma kwa ajili ya kutoa elimu ya Mfuko wa PSPF kwa umma ili waweze kupata uelewa mpana wa sekta ya Hifadhi ya Jamii hususan bidhaa na huduma zinazotolewa na PSPF, kwa mwaka huu, PSPF ililenga kuhimiza watanzania kujiunga na Hifadhi ya Jamii kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari unaoendeshwa na PSPF.

  Kwa mujibu wa takwimu zilizipo zaidi ya asilimia 90 ya watanzania hawapo katika Hifadhi ya Jamii, hivyo jukumu kubwa la siku ya PSPF mwaka huu ni kuhakikisha watanzania wengi wanajiunga na PSPF, jambo hilo lilifanikiwa kwani zaidi ya watu 500 walijiunga na PSPF katika maonesho ya sabasaba ya mwaka huu.

  Siku hiyo ilitumika kuwahamasisha wanachama wa PSPF kuwa na utaratibu wa kuhakiki taarifa zao mbalimbali ikiwawemo, historia ya michango, historia ya pensheni, kufuatilia mafao, kujisajili katika Mfuko na pia PSPF ilikuwa ikitoa vitambulisho vipya kwa wanachama wake.

  Katika kunogesha siku ya PSPF, Mfuko uliwaalika, Balozi wa PSPF Mjomba Mrisho Mpoto, waigizaji wote wa kikundi cha Original Komedi na Mboni Masimba mtangazaji na mwaandaaji wa kipindi cha The Mboni Show kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha TBC, kwa udhamini wa PSPF.

  Baadhi ya wageni mashuhuri waliotembelea banda la PSPF wakati wa maonesho hayo ni pamoja na Mheshimiwa Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Pinda, Waziri Mkuu, Mheshimiwa Gaudentia Kabaka, Waziri wa Kazi na Ajira, Mheshimiwa Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi, Mheshimiwa Shaaban Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na wengine wengi.

  Kwa mwaka wa pili mfululizo Mfuko wa Pensheni wa PSPF umekuwa ukitenga siku maalum wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam (sabasaba) kwa ajili ya kutoa elimu juu ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii na huduma zinazotolewa na PSPF.

   Msanii mahiri wa kughani mashairi Mrisho Mpoto akiwa ameambatana na baadhi ya wasanii wa kundi la Original Komedi walipokuwa wakikatiza viunga vya saba saba.
   Baadhi ya wasanii wa kikundi cha Original Komedi wakionesha mbwembwe zao

   Baadhi ya wadau wakiendelea kujiunga na mfuko huo wa PSPF ndani ya viunga vya saba saba.

  0 0

  Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabia ya NCH I(CAN) ,Sixsbaty Mwanga akizungumza na waandishi  wa habari (hawapo pichani)  katika mkutano wa mabdiliko tabia nchi katika kuelekea mkutano wa viongozi utaofanyika nchini Addis Ababa,Ethiopia uliofanyika leo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 
  Baadhi ya waandishi wakifatilia taarifa Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabia ya NCHI(CAN) ,Sixsbaty Mwanga hayupo pichani katika mkutano uliofanyika leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

   Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii

  VIONGOZI nchini wametakiwa kushiriki katika mkutano wa mabadiliko ya tabia ya nchi utakaofanyika Julai 13 na 16 Addis Ababa Ethiopia.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi (CAN),Sixsbaty Mwanga amesema mkutano huo ni muhimu kutokana hali iliyopo sasa katika mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuongezeka ukame ,njaa pamoja na mafuriko, hivyo viongozi wanaweza kushawishi mkutano katika kuongeza bajeti katika eneo hilo katika kukabiliana na majanga hayo.

  Amesema fedha ya kuweza kupambana na mabadiliko hazitoshi kufikia mwaka 2020, Tanzania kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi itatumia Trilioni mbili  kwa mwaka kutokana na ambayo itakuwa imefikia katika mabadiliko ya tabia.

  Mwanga amesema fedha za mabadiliko ya tabia ya nchi zinatakiwa ziwekwe wazi ili kusaidia wananchi kuweza kupata msaada pale panapotokea majanga ya ukame na mafuriko na waketi mwingine fedha hizo zinapotea na kushindwa kutatua matatizo yanayotokana  na mabadiliko hayo .

  Amesema mikutano iliyopita haikuwa na changamoto ya tabia ya nchi lakini sasa tatizo limezidi kukua kutokana na hali iliyopo kufikia mwaka 2020 vifo vitakuwa vya kila siku vinavyotokana na mabadiliko hayo.

  Amesema katika malengo 17 ya maendeleo endelevu ya masuala ya tabia ya nchi yanatakiwa kuangaliwa kwa katibu katika kila kpengele katika kuweza kukabili hali hiyo.

  Hata hivyo CAN inatarajia kufanya maandamano  ya matembezi  amani Julai 12 ambayo itashirikisha zaidi ya wadau 400 wa mazingira kushiriki na kupaza sauti, na matembezi hayo yataanzia katika chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) na kuishia katika kiwanja cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  0 0

   Mkurugenzi wa Chama cha Wanasayansi vijana wa Tanzania, Dk.Kamugisha Gozibert  akizungumza na waandishi wa habari(hawapo picha) kuhusu onesho la  Young Scientists Tanzania (YST) kwa mwaka wa 2015 na kueleza kuwa onesho ilo litafanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia tarehe 5 hadi 7 August 2015 ambapo wanafunzi wataweza kuonesha tafiti za kisayansi na kitekinologia zilifanywa na wanafunzi wa sekondari kwa takribani mwaka mmoja.
   Mwakilishi wa Ubalozi wa Ireland nchini, Brian Nolan akizungumza jambo wakati wa utangazaji rasmi wa Onesho la Young Scientists Tanzania (YST) kwa mwaka wa 2015 ambao wa wameamua kuwa wadhamini wa Onesho ilo.
   Vice President, Policy and Corporate AffairsJohn Ulanga akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kususu udhamini wao katika onesho la Young Scientists Tanzania (YST) kwa mwaka wa 2015 ambapo mwaka huu wamedhamini kiasi cha Dolla  laki mbili (200,000) pia wanadhamini wanafunzi wote kwa kwenda kusoma chuo chodhote kwa wale watakaoshinda kwenye onesho la mwaka huu.
  Waandishi wa habari wakiendelea kuchukua matukio  0 0

  DSC00136

  Meneja wa NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Singida, Alli Amanzi msaada wa mashuka 200 kwa ajili ya hospital ya mkoa mjini hapa.(Picha na Nathaniel Limu).
  DSC00132
  Mkuu wa wilaya ya Singida,Alli Amanzi (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja Mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoa wa Singida, Agnes Chaki (katikati) muda mfupi kabla Meneja NHIF hajakabidhi mashuka 200 kwa hospitali ya mkoa mjini hapa.Kushoto ni Afisa uthibiti ubora wa huduma NHIF mkoani hapa, Dk.Edwin Mwangajilo.

  Na Nathaniel Limu, Singida
  HOSPTALI ya mkoa wa Singida iliyopo mjini hapa,inakabiliwa na uhaba mkubwa wa mashuka kitendo kinachochangia wagonjwa kutumia mashuka yao binafsi wakati wote wanapokuwa wamelazwa hospitalini hapo.

  Hayo yamesemwa na Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Henry Mgetta, wakati akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya msaada wa mashuka 200 yaliyotolewa msaada kwa hospitali ya mkoa na mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoani Singida.Alisema hospitali hiyo yenye vitanda 300 vya kulaza wagonjwa,inakabiliwa na uhaba wa mashuka 2,400 na magodoro 230.

  “Hali ni mbaya mno,shuka 100 tulizonazo,ni chakavu na kwa ujumla nazo hazifai kwa matumizi ya binadamu.Wagonjwa wanaolazwa inawalazimu kutumia shuka zao binafsi jambo ambalo halikubaliki”,alisema Dk.Mgetta. Alisema mbali na uhaba wa shuka na magodoro,hosptali hiyopia ina uhaba wa vitanda na hasa kwenye wodi ya wazazi, kitendo kinachochangia wajawazito wanne watumie kitanda kimoja.

  “Natoa wito kwa wadau mbalimbali,waangalie uwezekano wa kuisaidia kwa hali na mali hospitali yetu hii na vituo mbalimbali,ili viweze kutoa huduma bora inayokidhi mahitaji ya wananchi”’alisema Dk.Mgetta. Kwa upande wake Meneja wa NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki,alisema kuwa wametoa msaada huo wa mashuka hayo baada ya kuombwa na serikali ya wilaya ya Singida.

  Alisema majukumu ya NHIF,ni pamoja na kuhakikisha vituo vya kutolea huduma za afya zinajitosheleza kwa kuwa na mahitaji yote muhimu kwa kutoa misaada na vile vile mikopo ya kununulia dawa,vifaa tiba na uboreshaji wa majengo.

  “Nina imani kituo cho chote cha afya,zahanati na hospitali,kinapokuwa na vitanda,mashuka na mambo mengine muhimu kwa wagonjwa wanaolazwa,kitendo hicho kitakuwa kinawajengea mazingira mazuri ya kuendelea na matibabu bila usumbufu wo wote”,alifafanua meneja huyo.

  Chaki alisema NHIF itaendelea kutoa misaada mbalimbali kadri uwezo utakavyoruhusu kwa lengo la kusaidiana na serikali katika kuboresha utoaji wa huduma za afya.

  0 0

  IMG_20150620_094935
  Refugees at the Nyarugusu Camp receive the Oral Cholera Vaccine. (c) UNICEF Tanzania/2015/Thomas Lyimo.

  Last week the Oral Cholera Vaccine, OCV, was administered at the Nyarugusu Refugee Camp, in Kigoma Region, Tanzania, to over 106,000 refugees from the Congo and – more recently – Burundi, out of an estimated camp population of 120,000 (children under the age of one were not vaccinated, hence the discrepancy in numbers). Medicins Sans Frontiers (MSF), who administered the vaccine, administered to Muslims observing Ramadan after sundown. We had been concerned whether the whole eligible community would receive the vaccine – and they did!

  This is a significant event not only for the huge numbers of people who have been given the vaccine but also because it’s the first time the OCV has been administered in an emergency situation in Tanzania Mainland. Previously we simply relied on WASH (water, sanitation and hygiene) interventions, by sensitizing the people on good practices to help prevent diseases. However, given that refugees are still arriving from Burundi, this compromises our WASH interventions as facilities are no longer sufficient to meet the growing numbers. What makes OCV special is that it can help to fill this gap easily and quickly.

  I’m a Health Specialist at UNICEF and as such my part in the OCV campaign has been to support the social mobilization task force – which is a key aspect of the campaign’s success. In the camp, in partnership with the Tanzanian Red Cross Society, we have trained 121 health information volunteers – community workers from the refugee community. They conduct household visits providing key messages not only on the OCV, but also cholera prevention through appropriate hand washing at critical times, and safe latrine use.


  0 0

   Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga akiwasalimia kwa kuonesha vidole baada ya kuzikagua timu za Foma na Mtongani katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya mpira wa miguu ya timu za Bodaboda ya Mpinga Cup, Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam leo.Lengo la mashindano hayo yaliyoshirikisha timu 108 ni kutoa elimu ya usalama barabarani kwa Bodaboda. Kushoto kwake ni Msimamizi wa mashindano hayo, Mrakibu Msaidizi wa Polisi,Mbunja Matibu. (PICHA NA RICHARD  MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
  Mchezaji wa timu Foma (kushoto) akiwania mpira na mchezaji wa timu ya Mtongani.
  Ni heka heka katika lango la timu ya Foma.

  0 0
 • 07/10/15--08:24: Bonanza la Masauni Cup
 • Mchezaji wa Zamani wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Salum Bausi akiikagua timu ya Kilimani wakati wa mchezo wao wa mwisho na timu ya Miembeni uliofanyika katika uwanja wa malindi Zanzibar timu ya Miembeni imeshinda 3--0
  Mchezaji wa Zamani wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Salum Bausi akiikagua timu ya Miembeni wakati wa mchezo wao wa mwisho na timu ya Kilimani uliofanyika katika uwanja wa malindi Zanzibar timu ya Miembeni imeshinda 3--0
  Kocha Bausi akiwa na Kiongozi wa TAYI Adaya, wakifuatilia michuano ya Bonaza la Masauni Cup linalofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja usiku. Timu ya Miembeni ishinda 3--0.

  Mchezaji wa timu ya Kilimani akiruka kihuzi cha mchezaji wa timu ya Miembeni wakati wa mchezo wao wa kumaliza mzunguko wa kwanza na kuingia nusu fainali ya Bonaza hilo.
     Wachezaji wa Miembeni na Kilimani wakiwa katika hartakati za kuzuiya mpiwa katika mchezo wao wa Bonaza.uliofanyika katika viwanja vya malindi mnazi mmoja.


  Mashabiki wa timu ya Miembeni Watoto wa Kidedea wakishangilia timu yao ilipoandika bao la tatu na la mwisho katika mchezo huo wa Bonaza la Kombe la Masauni Cup

  Mchezaji wa timu ya miembeni akimzuiya chezaji wa timu ya Kilimani wakati wa mchezo wao wa Bonaza uliofanyika katika viwanja vya malindi usiku jana timu ya Miembeni imeshinda 3--0
  Mchezaji wa timu ya Kilimani akimpita mchezaji wa timu ya Miembeni katika mchezo wa kuwania Kombe la Bonaza la Masauni Cup linalofanyika katika viwanja vya malindi mnazi mmoja Zanzibar timu ya miembeni imeshinda 3--0.,

  0 0

  Kamanda wa Jimbo la Chumbuni UVCCM Ndg Ussi Salum Pondeza Hanjad akikaribisha wageni wake katika futari aliowaandalia Wananchi wa Chumbuni ikiwa ni kawaida yake kila mwaka hujumuika na Wananchi hao katika futari katika mwezi mtukufu wa ramadhani.
  Wananchi wa Chumbuni wakijumuka katika futari ilioandakliwa na Kamanda Hamjad katika viwanja tawi la CCM Muembemakumbi Zanzibar.
                  Wananchi wakijumuika katika futari ilioandaliwa kwa ajili yao.


  Mzee wa Chumbuni akitowa shukrani wakati wa hafla hiyo ya futari ilioandaliwa na Kamanda wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza.
                   Mzee wa Muembemakumbi akisoma dua baada ya hafla hiyo ya futari.  0 0

   Mkurugenzi wa  Masoko na bidhaa wa Huawei ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini Jaco Van Zyl akielezea matumizi  simu  mpya ya Huwei P8 wakati wa  hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika klabu ya Country nchini Afrika ya Kusini.
  Maofisa waandamizi wa kampuni ya Huawei wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya uzinduzi wa simu ya kisasa ya P8 uliofanyika katika klabu ya Country mjini Johanessburg nchini Afrika ya Kusini.
  Mkurugenzi wa  Masoko na bidhaa wa Huawei nchini Afrika Kusini Yudi Rambaran akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa simu  mpya ya P8 katika klabu ya Country nchini Afrika ya Kusini wengine pichani kutoka kulia ni maofisa waandamizi wa kampuni hiyo ambao ni Chris Chetty ,Cameron Perumal,Charlene Munillal na Jaco Van Zyl.
   Wafanyakazi wa kampuni ya Huawei wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya uzinduzi wa simu ya kisasa ya P8 uliofanyika katika klabu ya Country mjini Johanessburg nchini Afrika ya Kusini.
   Maofisa waandamizi wa kampuni ya Huawei wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya uzinduzi wa simu ya kisasa ya P8 uliofanyika katika klabu ya Country mjini Johanessburg nchini Afrika ya Kusini.
  Shamra shamra zilitawala katika ukumbi wa klabu ya Country wakati wa uzinduzi huo.

older | 1 | .... | 579 | 580 | (Page 581) | 582 | 583 | .... | 1897 | newer