Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

TEMEKE WAMEONGEA- NATURE NDIYE MFALME!

0
0
Sir Kassim Juma Nature, kinara wa kundi la TMK Wanaume Halisi akiwanyooshea Mike mashabiki wake usiku wa kuamkia leo katika mchuano wa NANI MFALME ambapo mashabiki walimkubali kuwa Mfalme wao dhidi ya mahasimu wao, TMK Wanaume Family.
Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa mashabiki wa TMK Halisi, wakati wote vidole juu...TATU BILA, hata walipopagawishwa na nyimbo kali za TMK Family.
Mhe. Temba akicheza na mashabiki katika mpambano huo wa kukata na shoka
JB wa TMK Halisi akicheza na mashabiki wake pia
Sir Nature (kulia) na Doro..kazini
Mhe. Temba na Chege,,,kazini
..Inspector Haroun akiwa jukwaani akiwakilisha Gangwe Mob kivyake
..Inspector anapoamua kuvua viatu na kupiga shoo peku...
..Chezea Dar Live wewe!
Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa akionesha manjonjo yake mbele ya mpiga gitaa wake!
...dogo Lila kutoka kundi la Nature, akiwa ni member mpya wa kundi, akichana mistari vibaya mno....
...dogo Aslay wa TMK Family akiwaimbisha mashabiki
...Profesa jay nae alikuwepo kuwakilisha vilivyo game ya Hip Hop
DJ Jd alikuwepo kwenye mashine kucheza nyimbo za Prof jay na pia kuwaonesha Ma DJ chipukizi jinsi ngoma inavyochezwa!
........shooo wa Wanaume Family ikipamba moto
DJ JD alikuwa kama jaji pia, hapa akimtangaza Nature ndiye Mfalame kama mashabiki walivyoitikia.
...Nature akipungia mkono mara baada ya kutangazwa mfalme.
PICHA: Richard Bukos na Issa Mnally - GPL

TASWA FC, TASWA QUEENS ZANG'ARA MICHEZO YA PASAKA

0
0

 Mchezo ukiendelea japo uwanja ulikuwa ukisumbua kwa utelezi....
 Mafoto, akiondosha hatari.....
Timu ya soka na Netiboli za Waandishi wa Habari za michezo nchini, Taswa FC na Taswa Queens zimemaliza maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka kwa vishindo baada ya kuwatambia wageni wao, timu ya Kiliflora ya Arusha.
Katika mchezo wa soka, Taswa FC iliibuka kwa ushindi wa mabao 4-1 wakati katika mchezo wa netiboli uliochezwa kwenye uwanja huo huo, Taswa Queens iliyokuwa inacheza kwa mara ya kwanza baada ya miaka 18 iliibuka na ushindi wa mabao 28-8.
Taswa FC ilianza mechi hiyo kwa kasi na kufana mashambulizi ya mengi hata hivyo, washambuliaji wake, Julius Kihampa na Shafii Dauda walikosa mabao mengi ya wazi.
Katika mechi hiyo, kipa wa Taswa FC, Said Seif alikuwa ‘likizo’ kufuatia safu ya ulinzi chini ya Muhidin Sufiani, Fred Mweta, Sweetbert Lukonge, Fred “Chuji” Mbembela kuwa imara muda wote huku safu ya kiungo ilichezwa na Ali Mkongwe, Wilbert Molandi, Majuto Omary na Evarist Hagila kutotoa mwanya kwa Kiliflora kupenya na kupeleka mashambulizi.
Baada ya kosa kosa hizo, Taswa FC iliandika bao lake la kwanza katika dakika ya 24 kufuatia gonga safi za Majuto “Ronaldo De Lima” Omary na Ali Mkongwe kabla ya mpira kumfikia Hagila na kuuweka kimiani.
Bao hilo lilionekana kuwachanganya Kiliflora na kujikuta wakipachikwa bao la pili kupitia kwa Dauda baada ya pasi nzuri ya Wilbert Molandi aliyecheza vyema na Sweetbert Lukonge na kufanya timu hiyo kuongoza kwa mabao 2-0 mpaka mapumziko.
Taswa Fc ilifunga bao la tatu kupitia kwa Hagila baada ya pasi kupata pasi safi ya Fred Mbembela ‘Chuji’ na baadaye Dauda kufunga la bao la nne kufuatia ngazi nzuri ya Majuto.
Katika netiboli, ikiongozwa na Imani Makongoro aliyecheza nafasi ya (GS), Taswa Queens iliifunika kabisa Kiliflora Queens baada ya kuongoza kwa 16-3 hadi Mapumziko.
Wachezaji wengine wa Taswa Queens waliocheza mechi hiyo mbali ya Imani ni Oliver (mwananchi), Sada Ayoub,  Johari William, Elizabeth Mbassa, Shaarifa Mustapha wote wakitokea Business Times. Timu hiyo ilikuwa chini ya makocha, Amina Mussa (BTL) na Zainab Ramadhan (TBC).

NANI KUIBUKA MSHINDI WIKI HII KATIKA KIPINDI CHA 3 CHA GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE?

0
0
 Meneja wa kinywaji cha Guinness Davis Kambi(kulia) na mtangazaji wa kipindi cha Tamasha la michezo Amry Masare wakijadili na kufanya uchambuzi wa kipindi cha kwanza na pili cha Guinness Football Challenge jana katika kipindi cha Tamasha la michezo kinachorushwa na televisheni ya ITV.
Timu nne zitakazochuana katika kipindi cha tatu cha Guinness Football Challenge wiki hii. Kuanzia kushoto ni timu kutoka Kenya(wamevaa nyekundu), Tanzania –bluu, Uganda- kijani na nyeusi ni timu kutoka Kenya.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA NAIBU RAIS WA KENYA WILLIAM RUTO

0
0
 
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akipozi na familia ya  Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akiongea na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Mama Rachel Chebet, mke wa  Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.PICHA NA IKULU


======== =======  =======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 amekutana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto  ambaye alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.

Akiongea na mgeni huyo katika hoteli ya Seronera iliyoko katika mbuga ya wanyama ya Serengeti  mkoani  Mara, Rais Kikwete  amempongeza Mhe Ruto na Rais mteule wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, kwa ushindi wao kwenye uchaguzi mkuu nchini Kenya.

Mhe Rais pia alimueleza Mhe Rutto furaha yake pamoja na kuridhishwa  na jinsi  uchaguzi ulivyofanyika kwa amani katika nchi hiyo.

Alielelezea  matumaini yake ya kuwa  urafiki uliopo kati ya Tanzania na Kenya  utadumishwa  pamoja na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mhe Rutto, ambaye aliwasili mkoani  Mara wiki  iliyopita akiwa na mke wake na watoto, ameondoka  leo baada ya chakula cha mchana alichoandaliwa na mwenyeji wake.

BONDIA IDDY MKWERA AMGALAGAZA LUCAS NDULA MUHEZA TANGA

0
0

Bondia Iddy Mkwera akinyooshwa mkono juu baada ya kumgalagaza Lucas Ndula wakati wa mpambano wa mabondia wa Dar na Muheza Mkwera alishinda kwa pointi mpambano hou wa raundi sita uliotahalishwa kwa ajili ya kuinua mchezo wa ngumi Wilaya ya Muheza  na kusherekea sikukuu ya Pasaka.
Bondia Iddy Mkwela wa Dar es salaam kushoto akimshambulia vikali mpinzani wake Lucas Ndula wakati wa mchezo wao uliofanyika katika uwanja wa jitegemee Muheza Mkoa wa Tanga Mkwera alishinda kwa point 
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akiwa na mabondia wake walipotua katika wilaya ya Muheza Mkoani Tanga kwa ajili ya kwenda kuamasisha mchezo wa masumbwi katikati ni Iddy Nkwera na Martin Richard wote kutoka Dar es salaam.

Kocha wa mchezo wa ngumi Kimataifa Rajabu Mhamila 'Super D' wa tatu kushoto akiwa na mabondia Iddy Mkwera na Martn Richard baada ya kushuka katika gari kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi Wilaya ya Muheza wakati wa sikukuu ya Pasaka wakiwa na wapenzi wa mchezo huo katika stend kuu ya mabasi hayo.
Mabondia walio shiriki katika mpambano huo wakiwa katika picha ya pamoja
Kocha wa mchezo wa Masumbwi Wilaya ya Muheza Charles Muhiru 'Spins' akiwa na mgeni rasmi ambaye amefanikisha kuandaa mpambano huo Allan Augastino akisalimiana na mabondia kutoka Dar.
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' wa tatu kulia akiwa na baadhi ya mabondia waliocheza ngumi katika uwanja wa jitegemee muheza
Mabondia wakiwa na Super D.


Mabondia wa Kutoka Muheza wakionesha shoo ya masumbwi wakati wa kusherekea sikukuu ya Pasaka katika viwanja vya Jitegemee Muheza.

Mabondia wa Kutoka Muheza wakionesha shoo ya masumbwi wakati wa kusherekea sikukuu ya Pasaka katika viwanja vya Jitegemee Muheza
Bondia George Allen akinyooshwa mkono juu baada ya kushinda mpambano huo.

Bondia Lucas Ndula wa Muheza kushoto akioneshana uwezo wa kuoneshana uwezo wa kutupiana masumbwi na Iddy Mkwera wa Dar es salaam katika uwanja wa jitegemee muheza wakati wa sikukuu ya Pasaka Mkwera .

Baadhi ya Mashabiki waliojitokeza katika mpambano huo

Bondia Lucas Ndula wa Muheza kushoto akioneshana uwezo wa kuoneshana uwezo wa kutupiana masumbwi na Iddy Mkwera wa Dar es salaam katika uwanja wa jitegemee muheza wakati wa sikukuu ya Pasaka Mkwera.

Bondia Iddy Mkwera akinyooshwa mkono juu baada ya kumgalagaza Lucas Ndula wakati wa mpambano wa mabondia wa Dar na Muheza Mkwera alishinda kwa pointi mpambano hou wa raundi sita uliotahalishwa kwa ajili ya kuinua mchezo wa ngumi Wilaya ya Muheza  na kusherekea sikukuu ya Pasaka picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu

Bondia Iddy Mkwera wa Dar es salaam ameibuka mshindi baada ya kumgalagaza bondia Lucass Ndula wa Muheza wakati wa mpambano wa kuhamasisha masumbwi Wilayani Muheza uliochezwa wakati wa sikuku ya Pasaka katika uwanja wa Jitegemee

Mpambano ulioanza kwa ndula kuanza kwa kasi na kushangiliwa na wapenzi wengi katika raundi ya kwanza na ya pili upepo ulianza kumbadilikia raundi ya tatu baada ya kukata pumzi uku akitupa ngumi bila mpangilio wakati Mkwera akipanga mashambulizi na kupiga ngumi kali za kushitukiza zilizo mfanya Ndula kutulia

Raundi ya tano ilikuwa ni mfululizo wa makonde yaliyorushwa na Mkwera kwa ajili ya kumuhadhibu ndula ilipofika raundi ya sita na ya mwisho wa mchenzo ndula alipigwa upcat ambayo ilimchanganya na kufanya kuwa nje ya mchezo kwa kushika magoti

ambapo aliokolewa na kengele iliyoashilia kumaliza mpambano huo wa raundi sita na kufanya Iddy Mkwera kuibuka na ushindi wa point akipeperusha vema bendera ya Dar es salaam katika wilaya ya Muheza

Mfadhili wa mpambano huo ambaye aliwezesha kila kitu ikiwemo kupereka mabondia kutoka Dar pamoja na ulingo maarumu kwa ajili ya masumbwi  Allan Augastino ame haidi kurudia kufanya onesho hilo la wazi katika viwanja hivyo hivyo vya Jitegemee Muheza mkoa wa tanga wakati wa sikukuu ya Iddi na kuwataka wapenzi kujitokeza kwa wiki

Mpambano huo uliofanyika katika katika viwanja vya wazi vya Jitegemee iliwavuta wapenzi wengi wakiwemo watoto ,wanawake na vijana mbalimbali waliojitokeza kwa wingi

VILIO NA SIMANZI VYATAWALA JIJINI ARUSHA..WATU 17 WAPOTEZA MAISHA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI CHA MORAM

0
0

pic4
Wananchi wakiwa katika eneo la uchimbaji moram kata ya Moshono jijini Arusha wakiangalia zoezi la uokoaji ukiwa unaendela mara baada ya watu 17 kupoteza maisha  baada ya kufukiwa na kifusi hicho leo
pic6
Wanajeshi wakiwa wamebeba mwili wa marehemu juu ya machela mara baada ya kuutoa katika kifusi hicho mapema leo.
pic 1
pic5
Mbunge Lema akiwasili katika eneo hilo
Watu 13 wamefariki dunia baadaya ya kuangukiwa na kifusi cha Moram katika eneo la Moshono jijini Arusha  huku wengine 4 wahofiwa kupoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi hicho
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea leo jiji hapa majira ya saa 5:30 asubuhi baadaya ya mvua kubwa  kunyesha katika machimbo hayo ambayo inasemekana ndo chanzo cha tukio hilo
Hata hivyo vikosi mbalimbali vya uokoaji vilifika katika eneo hilo pamoja na  viongozi mbalimbali waliwasili katika  eneo hilo tayari kushuhudia hali halisi pamoja na kushiriki zoezi la uokoaji
Jamiiblog ilishuhudia kila baada ya dakika 5 maiti ilikuwa ikitolewa ndani ya kifusi hicho kilichokuwa kimewafunika wachimbaji hao,Pia majeruhi wawili walikimbizwa katika hospitali ya Mkoa Mt. meru pamoja na miili ya marehemu kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo
Mkuu wa Mkoa huu Magessa Mulongo alisema kuwa tukio hilo ni la kusikitisha na hivyo kuagiza machimbo yote ya mchanga kufungwa hadi hapo serikali itakapotoa amri ya kuendelea na shughuli za uchimbaji
Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki walifika katika eneo hilo kusaidia shughuli za uokoaji
Meya wa jiji hili Gaudence Lyimo alisema tukio kama hilo lilitokea mwaka 1997 ambapo watu 7 walipoteza maisha hivyo uongozi wa jiji uliwaagiza wachimbaji kutumia katapila badala ya mikono
Hata hivyo  wananchi waliishutumu vikali serikali kwa kushindwa kuboresha miundo mbinu ya eneo hilo kwa kuwa tukio kama hilo si mara ya kwanza kutokea hivyo walidai kuwa ni uzembe wa hali ya juu.
Zoezi la utambuzi wa miili unatarajiwa kufanyika kesho katika hospitali ya Mt.meru Jamiiblog inawapa pole ndungu jama na marafiki waliopoteza maisha katika tukio hilO
HABARI PICHA KWA HISANI YA http://jamiiblog.co.tz/

Serikali yashikilia msimamo wake sakata la Loliondo

0
0
SERIKALI     kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema haitabidili kamwe  maamuzi iliyotoa kuhusu Pori Tengefu la Loliondo, mkoani Arusha 
na kuwataka wanaharakati wanaochochea mgogoro wa ardhi katika eneo 
hilo kuacha mara moja.


Tamko hilo la serikali, limekuja muda mfupi baada ya watu mbalimbali 
kutoa maoni yao kwenye mitandao na vyombo vya habari kwamba uamuzi wa 
serikali kuhusu pori tengefu si sahihi. 
Tamko la serikali lilitangazwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, 
Balozi Khamis Kagasheki hivi karibuni kwamba, wameacha  kilomita za 
mraba 25,000 kwa ajili ya wananchi na serikali imechukua kilomita za 
mraba 15,00 kwa ajili ya kutunza rasilimali za nchi.

Alifanya hivyo kwa kwa mujibu wa Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya 
Mwaka 2009, Sehemu ya 16 Vifungu Na. 4, 5 na 6 na kwamba muda mrefu 
viongozi wa wizara wamekuwa wakikutana na wananchi na viongozi wa mkoa 
wa Arusha na Wilaya ya Ngorongoro kujua kero zilizopo ili zitatuliwe 
na ndio imewezesha serikali kufanya uamuzi alioufanya.

"Ukweli ni kuwa Waziri Kagasheki alifuata sheria alipotoa tamko kuhusu 
kupunguza eneo la pori tengefu la Loliondo kwa mujibu wa sheria 
inayompatia waziri mwenye dhamana uwezo wa kupitia upya mapori tengefu 
na kufanya marekebisho mbalimbali muhimu kwa manufaa ya wananchi bila 
kuathiri uhifadhi,"alisema George Matiko, ambaye ni msemaji wa wizara.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari jana, Matiko alisema tamko 
lilizingatia tafiti mbalimbali ikiwemo utafiti wa  Taasisi ya Utafiti 
wa Wanyamapori (TAWIRI) na mapendekezo ya tume mbalimbali zilizoundwa 
kuchunguza mgogoro wa Loliondo ikiwemo ya Waziri Mkuu iliyoundwa mwaka 
juzi.

Aliongeza kuwa eneo la kilomita za mraba 1,500 litaendelea kumilikiwa 
na wizara kwa mujibu wa sheria na kwa kutambua kuwa ni sehemu ya 
mazalia ya wanyamapori, mapito ya wanyamapori na vyanzo vikuu  vya 
maji kwa hifadhi mbalimbali ikiwemo Serengeti.

Alisisitiza ardhi iliyobaki baada ya kuondoa eneo la pori tengefu la 
Loliondo itasimamiwa na vijiji kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji 
Namba 5 ya Mwaka 1999 na wananchi watawezeshwa ili waanzishe Eneo la 
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) katika ardhi hiyo kwa manufaa 
yao.

"Tanzania inajali uhifadhi lakini pia inajali maslahi ya wananchi, 
ndiyo maana asilimia 25 ya eneo la nchi hii limehifadhiwa bila kuwepo 
migogoro. Hakuna migogoro kati ya wananchi na Serikali, kwa kuwa 
wananchi wanatambua umuhimu wa uhifadhi kwao na kwa vizazi vijavyo. 
Ndiyo maana wananchi wanachangia kwa kiwango kikubwa katika
kufanikisha uhifadhi,"alimaliza Matik

Article 10

0
0

MKUU wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu ameshauri kampeni aliyoianzisha wilayani humo yenye kauli ya 'Niache Nisome' kupambana na mimba kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa elimu, iwe taasisi na kufanya shughuli zake nchi zima.

Rweyemamu aliyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa habari hizi juu ya hali ilivyo kwa sasa ya matukio ya mimba kwa wanafunzi na kukatishwa masomo, vitendo ambavyo alivikuta vikishamiri eneo hilo hasa mwanzoni mwa mwaka jana kabla ya uteuzi wa nafasi hiyo.

Akizungumzia kampeni ya 'Niache Nisome' aliyoianzisha muda mfupi baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuiongoza wilaya hiyo, alisema kampeni yake imekuwa na mafanikio kwani licha ya matukio ya mimba kupungua wananchi wameipokea vizuri kampeni hiyo.

Alisema wananchi hasa baadhi ya wazazi wamekuwa wakiripoti matukio ya mimba na kutoa ushirikiano pale inapoitajika ili wavunjaji sheria kwa wanafunzi waweze kuadhibiwa kitendo ambacho hapo awali kilikuwa kigumu, na hata wengine kushirikia mikakati ya kuwaachisha masomo wanafunzi.

"Nina furahi kuwa muitikio wa kampeni ya 'Niache Nisome' katika maeneo mengi ya wilaya yangu imepokelewa vizuri, wananchi wanaanza kutambua umuhimu wa elimu na wanatoa ushirikiano kwa wale wachache wanaokwenda kinyume kwa kuwakatisha masomo wanafunzi hasa wa kike...jamii ya hapa wengi wao mwanzoni ilikuwa ni kitu cha kawaida mwanafunzi kulala nje pasipo idhini ya wazazi wake," alisema Rweyemamu akizungumza.

Akizungumzia utekelezaji wa kampeni hiyo Mkuu wa wilaya alisema licha ya kamatakamata iliyokuwa ikifanyika kwa wazazi, wanafunzi na watu waliyokuwa wakisababisha mimba kwa wanafunzi viongozi na watendaji anuai wa halmashauri hiyo walizunguka maeneo mengi na kutoa elimu juu ya umuhimu wa elimu kwa jamii zima.

"Tulikamatana sana mwaka jana kuanzia mwezi wa nane na kwa muda mfupi tulikuwa tuna watuhumiwa 80 wakiwemo wazazi, watu waliokuwa wakidaiwa kusababisha mimba kwa wanafunzi pamoja na wanafunzi wenyewe...mimi mwenyewe nilitembelea baadhi ya shule nikitoa elimu lakini baadaye walielewa licha ya uwepo wa changamoto kadhaa," alisema kiongozi huyo wa Wilaya ya Handeni.

Aidha akifafanua zaidi alisema ipo haja ya kampeni hiyo kugeuzwa taasisi na kuanza kufanya shughuli zake nchi nzima ili kampeni kama hiyo iweze kuyanufaisha maeneo mengi ambayo yamekuwa na mwamko duni wa elimu kwa jamii. Aliongeza kuwa faida ya kampeni hiyo haipiganii elimu kwa mtoto wa kike pekee kwani inagusa maeneo mengine pia kama miundombinu ya shule, vitendea kazi na vifaa vingine muhimu kwa shule kiujumla. 

Hata hivyo kiongozi huyo alisema licha ya kuanza kufanikiwa katika kampeni hiyo bado suala la ufauli katika shule za sekondari hasa kidato cha nne ni tatizo kutokana na ilivyokuwa hapo awali. Alisema matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana (2012) yalikuwa mabaya sana kwani Wilaya nzima ya handeni haikuwa na daraja la kwanza. 

"changamoto iliyobaki sasa ni ufaulu...matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka jana wilaya nzima ilikuwa na ziro 246, hatukuwa na daraja la kwanza kabisa huku tukipata wanafunzi 2 tu walio na daraja la pili," alisema Rweyemamu.

Mwezi Machi mwaka jana Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), kilifanya utafiti wa kihabari Wilayani Handeni kuangalia matukio ya mimba kwa wanafunzi na kubaini uwepo wa kesi nyingi za wanafunzi kutiwa mimba na kukatishwa masomo.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa kushirikiana na TAMWA 

wakazi wa morogoro waupokea vyema uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha

0
0

Pichani kushoto ni Meneja Mahusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel-Tanzania,Jackson Mmbando akimkabidhi fulana ya Airtel Yatosha pamoja na Muda wa maongezi kwa mmoja wa watumiaji wa huduma hiyo mara baada ya kueilezea vyema,kulia ni Meneja Mauzo wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel-Morogoro,Aluta Kweka.

Wakazi wa morogoro wakiendelea kujiunga na huduma ya Airtel yatosha kwa Kupiga *149*99#.
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya wa hip hop, kutoka kundi la Tip Top Conection ajulikanae kwa jina la Madee a.k.a Rais wa Manzese akiwarusha vilivyo wakazi wa mji wa Morogoro na wimbo wake wa “NANI KAMWAGA POMBE YANGU”,wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel  Yatosha ndani ya mji huo.Huduma hiyo itatambulishwa tena  hivi karibuni  kwa wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake.
Sehemu ya Umati wa watu waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha ndani ya mkoa wa Morogoro.
Wakazi wa morogoro walijitokeza kwa wingi jukwaani kujiunga na huduma ya Airtel yatosha kwa Kupiga *149*99#.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ney wa Mitego akitumbuiza mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Morogoro waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel  Yatosha ndani ya mji huo.Huduma hiyo itatambulishwa tena  hivi karibuni  kwa wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake.


Pichani kulia ni Meneja Mauzo wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel-Morogoro,Aluta Kweka akimkabidhi fulana ya Airtel Yatosha mmoja wa watumiaji wa huduma hiyo mara baada ya kueilezea vyema huduma hiyo mbele ya  umati mkubwa wa wakazi wa mji  huo na vitongoji vyke,shoto ni Msanii wa muziki wa kizazi kipya anaekuja juu katika miondoko ya hip hop hapa nchini aitwaye Stamina akishuhudia.

Pichani kulia ni Meneja Mahusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel-Tanzania,Jackson Mmbando akimkabidhi fulana ya Airtel Yatosha mmoja wa watumiaji wa huduma hiyo mara baada ya kueilezea vyema huduma hiyo mbele ya  wakazi wa mji  huo na vitongoji vyke,Katikati ni Msanii Nguli wa muziki wa kizazi kipya wa hip hop Fid Q akishuhudia tukio hilo.



Mmoja wa wasanii Mahiri katika  miondoko ya Hip Hop hapa nchini atambulikae kwa jina la Farid Kubanda a.k.a Fid Q  akiimba na mmoja wa mashabiki wa wakazi wa mji wa Morogoro wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel  Yatosha,uliofanyika kwenye kwenye uwanja wa shule ya msingi Sabasaba


Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature akiwa sambamba na baadhi ya wasanii wenzake wanaounda kundi la Wanaume TMK-Halisi wakiwarusha vilivyo wakazi wa mji wa Morogoro na Vitongoji vyake wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya  Airtel Yatosha ndani ya mji wa Morogoro jana jioni kwenye viwanja vya shule ya msingi Sabasaba.
Wasanii wa kundi la vichekesho liitwalo Kinoko lenye maskani yake Kinondoni jijini Dar wakitumbuiza mbele ya umati wa watu waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha ndani ya mji wa Morogoro jana jioni kwenye viwanja vya shule ya msingi Sabasaba.


Sehemu ya umati wa wati wakigombea fulana ya Airtel Yatosha mara baada ya huduma hiyo kuzinduliwa rasmi jana mkoani Morogoro.

Sehemu ya umati wa wakazi wa morogoro uliofurika kwenye uwanja wa shule ya msingi Sabasaba wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel  Yatosha wakishangilia,huduma hiyo itatambulishwa tena  hivi karibuni  kwa wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake.

KAMPENI YA TUPO PAMOJA YA SERENGETI PREMIUM LAGER ILIVYOFUNIKA WIKENDI YA PASAKA

0
0
 Timu nzima ya kampeni ya Tupo Pamoja wakigongesha chupa zao za bia ya Serengeti kuonesha upendo na kutakiana amani katika mafanikio, sasa tupo pamoja maskani kwako
   Washereheshaji wa kampeni ya Tupo Pamoja wakiwatambulisha mabalozi wa bia ya Serengeti
  Vijana wa kukimbiza mchakamchaka wa kampeni ya Tupo Pamoja wakifanya vitu vyao jukwaani.
 Mmoja wa wanenguaji akionyesha ujuzi wake katika kudansi.
 Mchakamchaka ulikua namna hii ndani ya Play Time Bar jijini Dar es Salaam
Hii ndiyo Serengeti Premium Lager!

TAARIFA YA KUPOROMOKA KWA JENGO LA GHOROFA JIJINI DAR- ES – SALAAM MTAA WA INDIRA GANDHI NA BARABARA YA MOROGORO

0
0
1. UTANGULIZI.

Sheria zinazosimamia masuala ya ujenzi mijini zilitungwa kwa mara ya kwanza mwaka 1920 wakati wa utawala wa Mwingereza. Sheria hizo zilijukana kama Kanuni za Miji (Township Rules, Cap.101) ambapo Kanuni za Ujenzi Mjini (Township (Building Rules) Cap. 101 zilikuwa sehemu ya Kanuni hizo. Sheria hizo pamoja na mambo mengine zililenga kusimamia shughuli zote za majenzi mjini. 

Aidha, Msimamizi wa sheria hizi zilikuwa Mamlaka za Miji, Manispaa na jiji ( kwa wakati huo) kwa sasa ni Majiji, Manispaa na Miji). Hata hivyo sheria hizi hazikuwa zinafanya kazi peke yake kwani mwaka 1968 Serikali ya Tanzania ilitunga sheria ya Wahandisi ( yaani the Engineers (Registration) Act,No.49/1968) na mwaka 1972 ilitungwa Sheria ya kusimamia Wasanifu Majengo ,Wakadriaji Majengo na Wakandarasi, Na.35/1972. Sheria zote hizo kwa pamoja zilikuwa zikisimamia shughuli zote za ujenzi mjini.

Kutokana na taratibu zilizokuwa zimezoeleka tangu huko nyuma usimamizi wa shughuli za ujenzi mjini zimeonekana kuwa mamlaka ya usimamizi ni Halmashauri ya Mji,Manispaa au Jiji husika na siyo wadau wengine. Kwa ujumla dhana hii sio sahihi hata kidogo. Kama tulivyoona hapo juu wadau katika sekta hii ni wengi ambao wanapaswa kusimamia shughuli zote za ujenzi pamoja na ubora wa kazi zinazofanywa na wakandarasi, watalaamu washauri kwa maana ya wahandisi na wasanifu majengo.Taarifa hii inakusudia kutoa ufafanuzi juu ya jengo la ghorofa kumi na sita lililokuwa linajengwa katika kiwanja Na……………………barabara ya Morogoro na mtaa wa Indira Gandhi jijini Dar es salaam kuporomoka siku ya tarehe 29/03/2013. 

2. Nini msimamo wa Sheria zinazosimamia Ujenzi Mjini.
Kama ilivyooneshwa hapo juu historia ya sheria zinazosimamia ujenzi mjini zilivyoanza na baadaye mabadiliko ya uchumi yalisababishwa kutungwa kwa sheria ya kusajili Wahandisi mwaka 1968 na baadaye sheria ya Wasanifu majengo ,Wakandarasi na Wakadriaji majengo.

Hivi leo sheria zote hizo hapo juu zilifutwa na kutungwa upya na kutoa majukumu ya msingi kwa kila mamlaka ( Mdau). 
Tukianza na Kanuni za Ujenzi Mijini Sura, 101 ilifutwa Mwaka 1994 kwa Sheria Na.8 /1994 (yaani the Law Revision Act, No.8/1994). Baada ya kufutwa sheria hii Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Nchini kote zilikaa kwa kipindi cha miaka 14 bila kuwa na sheria ya kusimamia ujenzi mijini mpaka zilipotungwa Kanuni za Miji chini ya Tangazo la serikali Na.242/2008 (the Local Government (Urban Authourities) (Development Control) Regulations, GN.No.242/2008).

Kanuni hizi zinaweka wajibu kwa Halmashauri kutoa kibali kwa mujibu wa Kanuni Na.124 kulingana na mchoro uliowasilishwa. 

Vilevile, kanuni hizi zinaweka wajibu Mhandisi au Msanifu majengo kuandaa hesabu ya uzito wa vyuma vitakavyotumika kujenga jengo husika hii ni kwa mujibu wa Kanuni Na.143.

Kwa mantiki hiyo Halmashauri si Mamlaka pekee ya usimamizi wa majengo makubwa ya umma na /au binafsi ambayo matumizi yake ni kwa ajili ya biashara au shughuli nyinginezo za kibinadamu.Taasisi zifuatazo ni mamlaka za usimamizi ambazo zimeanzishwa na sheria ya Bunge:-

1. Bodi ya Wasanifu Majengo ,Wakadriaji Majengo ni mamlaka iliyoanzishwa na Sheria Na.16/1997( the Architects and Quantity Surveyors (Registration) Act [cap.269 R.E 2002] na mwaka 2010 sheria hii ilifanyiwa marekebisho ambayo kimsingi hayakuathiri majukumu yake. Fungu la 4 la sheria hii linaweka majukumu kwa chombo hiki kufanya yafuatayo;-

• Kusimamia shughuli na utendaji kazi wa wasanifu majengo ,wakadriaji majengo pamoja na kampuni zinazofanya kazi ya utalaamu ushauri katika kusimamia miradi ya ujenzi; 

• Kuingia na kukagua shughuli zote za ujenzi unaofanyika hapa nchini kwa madhumuni ya kujiridhisha na kuhakikiksha kama kazi ya ujenzi inayofanyika inafanywa na mtu ambaye amesajiliwa na bodi na anazingatia taratibu,kanuni na sheria zote zinazosimamia ujenzi mijini; na 

• Kuhakikisha kuwa maeneo yote ambako ujenzi unafanyika kumewekwa mabango yenye kuonyesha jina na anwani ya mradi, jina la mteja (mmiliki) , watalaamu washauri kwa maana wasanifu majengo na wahandisi pamoja na mkandarasi endapo atakuwa hakufanya hayo atachukuliwa hatua za kisheria.

2. Bodi ya Usajili wa Wahandisi ni mamlaka iliyoanzishwa na sheria Na.15/1997(the Engineers Registration, Act [Cap.63 R.E 2002]. Fungu la 4 la sheria hii linaweka majukumu kwa chombo hiki kufanya yafuatayo;-

• Kufuatilia na kusimamia shughuli na utendaji kazi wa wahandisi ikiwa ni pamoja na kampuni zinazofanya kazi ya utalaamu ushauri wa usimamizi wa miradi ya majenzi mijini;

• Kuingia na kukagua shughuli zote za ujenzi unaofanyika hapa nchini kwa madhumuni ya kujiridhisha na kuhakikiksha kama kazi ya ujenzi inayofanyika inafanywa na mtu ambaye amesajiliwa na bodi na anazingatia taratibu,kanuni na sheria zote zinazosimamia ujenzi mijini; na 

• Kuhakikisha kuwa maeneo yote ambako ujenzi unafanyika kumewekwa mabango yenye kuonyesha jina na anwani ya mradi, jina la mteja (mmiliki) , watalaamu washauri kwa maana wasanifu majengo na wahandisi pamoja na mkandarasi endapo atakuwa hakufanya hayo atachukuliwa hatua za kisheria.

3. Bodi ya Wakandarasi [CRB] ni mamlaka iliyoanzishwa na sheria Na.17/1997( the Contractors Registration Act, [Cap.235 R.E 2002] Fungu la 4 la Sheria hii linaweka majukumu kwa chombo hiki kufanya yafuatayo;-

• Kusimamia shughuli na utendaji kazi wa Wakandarasi katika kujenga majengo imara na yenye kufuata viwango kwa mujibu wa michoro ya majengo hayo;

• Kuingia na kukagua shughuli zote za ujenzi unaofanyika hapa nchini kwa madhumuni ya kujiridhisha na kuhakikiksha kama kazi ya ujenzi inayofanyika inafanywa na mtu ambaye amesajiliwa na bodi na anazingatia taratibu,kanuni na sheria zote zinazosimamia ujenzi mijini; na

• Kuhakikisha kuwa maeneo yote ambako ujenzi unafanyika kumewekwa mabango yenye kuonyesha Jina na anwani ya mradi, jina la mteja (mmiliki) , Watalaamu washauri kwa maana wasanifu majengo na wahandisi pamoja na mkandarasi endapo atakuwa hakufanya hayo atachukuliwa hatua za kisheria.

4. Mamlaka nyingine ya usimamizi ni usalama mahali pa kazi (Occupational, Safety and Health Agency). Hiki ni chombo ambacho kinashiriki pia kusimamia miradi ya ujenzi mijini. Mamlaka hii hutoa kibali na kusajili mradi kama ambavyo mamlaka nyingine ambavyo zinafanya kwa kutoa “sticker”. 

5. Hitimisho.
Kama ilivyoonyeshwa hapo juu tumeona kwamba zipo sheria mbalimbali zenye kubainisha wadau wote wanaohusika na usimamizi wa majenzi mijini. Hivyo tunaomba ieleweke kwa umma kwamba Halmashauri ya Manispaa ya Ilala si mamlaka pekee ya usimamizi. Hii ni kwasababu muombaji wa kibali anapoomba na kukubaliwa baada ya kupitia michoro yake ambayo mara nyingi huwa imeandaliwa na Wasanifu na Wakadriaji majengo pamoja na “Structural Engineer” ambao wanasimamiwa na mamlaka zilizobainishwa hapo juu. Halmashauri huwa haina nafasi zaidi ya kitalaamu ya kusimamia katika masuala makubwa hasa ya vyuma na kiwango cha “material” yanayotumika katika ujenzi ; isipokuwa kufuatilia kama muombaji (mmiliki) anajenga kama ambavyo alionyesha katika michoro iliyopitishwa kwa mujibu wa mpango wa uendelezaji wa eneo husika.

______________________________ __
Imetolewa Na:
Mstahiki Meya 
katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani (1/04/2013),
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
Dar- es - salaam.

PASAKA GOSPEL FESTIVAL 2013 ILIVYOFANA MWANZA

0
0

Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula ambaye pia ni diwani wa kata ya Mkolani akifungua utepe wa gitaa kuashiria uzinduzi wa Studio mpya za kurekodi muziki za COSU Studio zilizozinduliwa ndani ya tamasha la Muziki lijulikanalo kama Pasaka Gospel Festival ambalo nalo limeanzishwa rasmi mwaka huu jijini  Mwanza.


Nesta Sanga ni moja kati ya waimbaji waliosisimua ndani ya Gospel Festival tizama watu wa Mungu walivyomzunguka wakiimba naye. 




Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula akifurahia yanayoendelea na Askofu Simeone Masunga wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Geita katika sherehe za Pasaka ndani ya Kusanyiko la Pasaka Gospel Festival lililofanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo kwaya mbalimbali na waimbaji toka pande nyingi nchini walihusishwa.


Mwimbaji wa nyimbo za injili anayetamba Afrika Mashariki na Kati Neema Mwaipopo akiiimba wimbo wa 'Raha jipe mwenyewe' na wakazi wa Mwanza waliofurika uwanja wa CCM Kirumba kwenye kusanyiko la Pasaka Gospel Festival 2013.


Waimbaji mbalimbali toka mikoa ya Dar es salaam, Manyara, Arusha, wakimpa sapoti mwimbaji Neema Mwaipopo kwenye kusanyiko la Pasaka Gospel Festival 2013 lililofanyika sikukuu ya Pasaka uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. 


Hapa raha ya ufufuko ilimvuvia kila mmoja.


Mwimbaji nesta Sanga  akiimba wimbo ujulikanao kwa jina Twendeni huku akipewa sapoti ya kutosha.
Sura za watumishi wa muziki wa Injili zikiranda huku na huko kudadisi yanayoendelea.


Ni cheki ya 500,000/= toka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Mkolani Investiment (katikati) Suleiman Nguvu kuchangia uboreshaji wa vitendea kazi ndani ya studio za kisasa za COSU Studio ndani ya Kusanyiko la Pasaka Gospel Festival 2013. Kushoto ni Mkurugenzi wa COSU Entertainment Fabian Fanuel (red tshirt) na Meneja wake Albert G. Sengo (kulia)


Wananchi hawakupitwa na shughuli za uwekaji kumbukumbu.

Jamani rahaaaaaaaa....Ndiyooooo....


Moja ya kwaya za jijini Mwanza zikihudumu.


Mwimbaji anayesisimua katika muziki wa injili akitamba na wimbo 'Zunguka' Enock Jonas akishusha upako...


Meza kuu ikijadili jambo.


Zunguka, zunguka, zunguka, zunguka eeeeeeeeeh!!!!!


Ilibidi muda usogee hata kiza kikaingia, tunamshukuru Mungu shughuli katika uwanja huu kwa kweli ilifana. Shukurani za dhati kwa Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula, Mbunge wa Monduli Edward Lowassa (twafahamu ni majukumu tu yamesababisha ukashindwa kuhudhuria), Mkurugenzi wa Sahara Media Group Dr. Anthony Diallo,  Michuzi Jr Blog na Kajunason Blog. 

WAZIRI wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe kuwa Mgeni rasmi Media Day

0
0

WAZIRI wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye bonanza la vyombo vya habari linaloandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA). Bonanza hilo litafanyika  Jumamosi wiki hii viwanja vya Sigara, Chang’ombe, Dar es Salaam kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa moja usiku likidhaminiwa na na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

Pamoja na mambo mengine, Waziri Mwakyembe atakabidhi zawadi za vikombe na medali kwa washindi mbalimbali watakaoibuka siku hiyo, pia atapata fursa ya kuzungumza na washiriki wa bonanza hilo.  Lengo la bonanza ni kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine, ili kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja na huwa linafanyika mara moja kwa mwaka, likiandaliwa na TASWA.

Bonanza hilo ambalo litahusisha wadau 1,500 kutoka vyombo mbalimbali vya habari litaambatana na michezo mbalimbali itakayohusisha vyombo vyote vitakavyoshiriki na pia kutakuwa na burudani ya muziki.

Tunataka bonanza la mwaka huu liwe la aina yake kuanzia mgeni rasmi, burudani, michezo na mambo mengine yawe ya kuvutia, ambapo Alhamisi Aprili 4,2013 saa tano asubuhi kutakuwa na mkutano na wanahabari mgahawa wa City Sports Lounge, Posta Dar es Salaam ambao ni maalum kutangaza makundi yatakayotumbuiza kwenye Media Day na tunatarajia makundi hayo nayo yatakuwepo kwenye mkutano huo.

Tunaomba vyombo vya habari ambavyo havijathibitisha ushiriki wao kwa njia ya maandishi vifanye hivyo kama vilivyoagizwa kwenye barua zao za mialiko, vinginevyo ushiriki wao hautathaminika.

Bonanza litaanza saa tatu asubuhi, ambapo baadhi ya michezo itakayoshindaniwa ni soka ya ufukweni, netiboli, wavu, mbio za magunia, mbio meta 100, kuruka kichura, kuvuta kamba, kucheza muziki na kuimba. 

Nawasilisha. 
Juma Pinto
Mwenyekiti TASWA
02/04/203

SUMATRA YATANGAZA VIWANGO VIPYA VYA NAULI YA MABASI NA DALADALA

0
0

DEATH ANNOUCEMENT

0
0



Airtel named most Socially Responsible Company in Niger

0
0
Airtel Niger’s Regulatory Director, Mr. Karimou Salifou, receives the award from Salifou Labo Bouche, Minister of Communication and New Technologies.

Bharti Airtel (“Airtel”), a leading telecommunications services provider with operations in 20 countries across Asia and Africa, has been named the Most Socially Responsible Company in Niger at the 3rd Edition of the National Excellence Awards Ceremony.

Airtel Niger was awarded by the independent organization for Management Excellence that rates organizations and individuals distinguishing themselves for exceptional achievements during the year.

Airtel Niger’s Regulatory Director Mr. Karimou Salifou, received the award on behalf of the Managing Director from Niger’s Minister of Telecommunications in the presence of government officials, corporate officials and civil society representatives.

Speaking after the ceremony, Mr Salifou said “This is in recognition of the tremendous contribution Airtel has made through its corporate responsibility in Niger, through the adoption and refurbishment of schools in underprivileged and remote areas of the country. We believe these investments, as with others we have made to better the lives of the communities in Niger, will help support some of the infrastructure needs in schools.”

He added: “We are also extremely humbled because this award recognizes what Airtel is doing in the 17 countries that we operate in across Africa, especially in the area of education. We believe this will go a long way in raising the literacy levels across the continent; we encourage more corporate organisations to join hands to help young students who we depend on for our future economic growth and development. ”

In awarding Airtel, it was noted that the company’s contribution to underprivileged children was highly appreciated by communities, government and the civil society.

According to the United Nation’s Development Programme (UNDP) index covering the years between 1980 and 2012, only 48 percent of the children in Niger are completing primary education, indicating a need for public-private partnerships in alleviating the challenge.

Tiemoko Coulibaly, CEO for the Francophone Africa Region at Bharti Airtel said : “ Our community engagement in the Francophone countries that we operate in appreciates that there are unique socio-economic challenges. This distinction recognizes Airtel’s efforts in trying to touch the hearts of the communities that we serve.”

TUZO ZA WANAWAKE WENYE MAFANIKIO TANZANIA

0
0
 Pichani kulia ni Waziri wa Maendeleo, Jinsia na Watoto Mh. Sophia Simba akiwa na mshindi wa Tuzo ya Mafanikio ya Maisha Bi. Marjorie Mbilinyi na rais wa Tuzo za wanawake wenye Mafanikio Tanzania Bi.Irene Kiwia wakati wa hafla hizo.
 Mshindi wa Tuzo ya Afya Dkt.Linda Ezekiel akipokea tuzo toka kwa Mwenyekiti wa bodi ya Hospitali ya Kairuki Bi.Kokushubira Kairuki
 Mshindi wa mwanamke bora wa mwaka Bi.Dina Marios akipokea tuzo toka kwa afisa wa Tigo Tanzania Bi.Woinde Shisael
 Mshindi wa Tuzo ya Mafanikio ya Maisha Bi. Marjorie Mbilinyi akipongezwa na mweyekiti wa kamati ya Tuzo za wanawake Bi. Sadaka Gandi 
 Washindi wa Tuzo wakiwa wamepozi kwenye picha ya pamoja.
=======  =======
WASHINDI WA TWAA 2013:

1.Kilimo-Emiliana Aligaesha
2.Sanaa na Utamaduni-Susan Luendo
3.Mshiriki Mdogo-Glory Matoi
4.Tuzo ya Mafanikio ya Maisha-Marjorie Mbilinyi
5.Habari na Mawasiliano_Vicky Ntetema
6.Afya-Dkt.Linda Ezekiel
7.Michezo-Joan Minja
8.Elimu-Ruth Meena
9.Tuzo ya Mwanamke wa Mwaka2012/13-Dina Marios
10.Ujasiriamali-Mary Kalikawe
11.Sayansi na Teknolojia-Regina Kapinga
12.Ustawi wa Jamii-Justa Mwaituka
13.Taaluma-Grace Rubambey



mgogoro wa ardhi sala sala,wananchi wamtaka waziri Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuingilia kati

0
0

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilimahewa Kata ya Salasala, Abdallah Mpondela akionesha eneo la wazi la serikali ambalo hutumiwa na wananchi wa eneo hilo kwa ajili ya michezo mbalimbali pamoja na shughuli za kijamii. Eneo hilo kwa sasa limevamiwa na mtu asiyefahamika anayedai kuwa ndie mmiliki wa kiwanja hicho ambacho kina  Ofisi ya Mtaa na Kata. (Na Mpiga Picha Wetu)


Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kilimahewa.

DAR ES SALAAM, Tanzania

WANANCHI wa Mtaa wa Kilimahewa Kata ya Salasala wamemtaka Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka kuingilia kati mgogoro wa kiwanja cha wazi cha serikali.

Akizungumza jana Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilimahewa Abdallah Mpondela alisema kuwa kiwanja hicho kimeingia katika mgogoro na mtu ambaye hafahamiki na kusema ndio mmiliki wa kiwanja hicho kukiwa kuna ofisi ya Mtaa pamoja na ofisi ya Kata hiyo.

Mpondela alisema kuwa mtu huyo ambaye anasema kiwanja hicho ni mali yake huku Manispaa ya Kinondoni imejenga ofisi katika eneo hilo ambapo katika ramani inaonyesha ni mali ya serikali.

Mwenyekiti pamoja na wananchi wamesema kuwa hawataweza kuachia kiwanja hicho kwenda katika mikono ya mtu mwingine kwa masilahi yake huku wakinanchi wakikosa eneo hilo linalotumika katika michezo na mikutano mikubwa.

Mpondela alisema kuwa mtu huyo alifikia kwenda mahakamani kwa kumshitaki Mwenyekiti wa Mtaa ambapo hajaweza kifika kizimbani kusimama katika kudai hicho kiwanja kuwa ni mali yake tangu ilipofunguliwa kesi na mtu huyo.

Wakili wa Kujitegemea wa Kutetea kiwanja hicho upande wa Mwenyekiti wa Kilimahewa Addo Mwasongwe alisema kuwa atahakikisha kiwanja hicho kinabaki katika mikono ya wananchi kwa shughuli za kijamii.

Mwasongwe alisema kuwa kazi yake ni kuona haki inatendeka kwa wananchi wa Kilimahewa kuenndeka kumiliki eneo hilo kutokana na ramani inavyoonyesha kuwa eneo la wazi la serikali.

utamu wa nyama choma.!

0
0

Naibu Spika kubariki Tamasha la Pasaka Dodoma

0
0
NAIBU Spika, Job Ndugai anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka Jumamosi Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa maandalizi kuhusiana na tamasha hilo la Dodoma yamekamilika na kwamba wasanii wanatarajiwa kuwasili mkoani humo leo wakitokea Iringa.

“Waliohudhuria matamasha ya Dar es Salaam na Mbeya wameona mambo mazuri na leo (jana) tunafanya vitu Iringa, hivyo tumempa heshima Naibu Spika kubariki tamasha letu la Dodoma, naamini mambo yatakuwa mazuri sana,” alisema Msama.

 “Ni matumaini yetu kwamba tamasha litakuwa zuri na kila mtu atafika kuja kuona kile ambacho wasanii wametuandalia,” alisema Msama na kuyataja makundi yatakayotumbuiza kutoka nje ya Tanzania kuwa ni kundi la Ambassadors of Christ ‘Kwetu Pazuri’ la Kigali, Rwanda.

Wasanii wengine wa nje ya Tanzania watakaotumbuiza tamasha hilo ni Sipho Makhabane wa Afrika Kusini, Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya.

Msama aliwataja wasanii wa Tanzania watakaopanda jukwaani leo kuwa ni Rose Muhando, Upendo Nkone,  Bonny Mwaitege, Upendo Kilahiro, John Lissu, kwaya ya Kinondoni Revival na kundi la Glorious Celebration.

“Kila msanii amepanga mambo yake kuwafurahisha Watanzania, naamini wengi watajitokeza na kushirikiana katika tamasha letu linalozidi kupanda chati mwaka hadi mwaka,” alisema Msama na kuongeza kuwa tamasha hilo litakamilika Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images