Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

MAKATIBU WA CCM MKOA WA ARUSHA WAPEWA PIKIPIKI NA JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA ARUSHA

$
0
0
SAM_3542Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Arusha na Mbunge wa Africa Mashariki  Mh.Bernard Murunya amabye alikuwa mgeni rasmi katika tukio la kukabidhi pikipiki,akimkabidhi moja ya Pikipiki kwa katibu jumuiya ya wazazi Wilaya ya Arusha Rehema Mohamed jana katika makao makuu ya chama  hicho jijini Arusha, jumla ya pikipiki saba zilikabidhiwa kwa Wilaya saba katika Mkoa wa Arusha huku Mwenyekiti wa Taifa  Abdalah Bulembo pamoja Baraza kuu Taifa wakifanya jitihada za kupatikana kwa Pikipiki hizo,katikati ni Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_3532Makatibu wa Wilaya saba katika Mkoa wa Arusha wakiwa katika pikipiki zao
SAM_3529Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau akiwa anatoa maelekezo ya namna pikipiki hizo kutumika kwa uangalifu huku akiongeza kuwa endapo mtumishi atahamishwa kwenda sehemu nyingine basi atalazimika kuhama na pikipiki yake na akiweza kutunza vema baada ya miaka minne atazawadiwa kwa bei nafuu.
SAM_3536Katibu jumuiya ya wazazi Wilaya ya Arusha mjini Rehema Mohamed akiwa na furaha baada ya kukabidhiwa pikipiki jana jijini Arusha

SAM_3517 Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau akisoma risala fupi kwa mgeni rasmi ambapo katika risala yake alisema kuwa ugawanyi wa pikipiki hizo saba ni juhudi za Mwenyekiti Taifa Abdalah Bulembo pamoja na Baraza Kuu la Wazazi Taifa ,Tukio hilo ni la Jumuiya ya wazazi Nchi nzima la kuwakabidhi Makatibu wa Wilaya zote 161 pikipiki kwaajili ya kurahisisha utendaji wa kazi na kuboresha suala zima  la usafiri ikiwa ni kuimarisha Chama cha Jumuiya zote
SAM_3528Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Arusha na Mbunge wa Africa Mashariki  Mh.Bernard Murunya akijaribu moja ya pikipiki alizokabidhi

DOGO JEMBE AHOJI NANI ANAFAA KUWA RAIS

$
0
0
TANGU  mgombea mwenye umri mdogo zaidi kutangaza nia ya kutaka kuwa rais wa Tanzania, Dogo Jembe amejikuta akipambana na upinzani mkali toka kwa wananchi wengi hasa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao wengi wamekuwa wakimtaka arudi shule huku wengine wakimshambulia kuwa anatumiwa na mmoja ya wanasiasa.

Mara baada ya kuzongwa na waandishi wa habari waliomuuliza anachukuliaje maoni ya wananchi kuhusu nia yake ya kuutaka urais amelazimika kuitisha mkutano na waandishi wa habari ambapo ameongea kwa hisia akihoji kama hawamtaki yeye ni nani hasa wanaona anafaa. Tazama video hii.

WAZIRI WA UTALII NA MALIASILI MHE. LAZARO NYALANDU AFUNGUA MKUTANO WA UHIFADHI WA WANYAMAPORI TANZANIA

$
0
0
  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akisalimiana na baadhi ya wadau wa masuala ya uhifadhi na utalii wakati alipofungua mkutano wa majadiliano kuhusu uboreshaji wa mfumo wa usimamizi na uendeshaji Maeneo ya Jumuia ya Hifadhi ya Wanyamapori Tanzania (WMA), ulioanza jana jijini Arusha.
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akifuatilia majadiliano wakati wa mkutano wa      wadau na viongozi wa Maeneo ya Jumuia ya Hifadhi ya Wanyamapori nchini (WMA), ulioanza jana jijini Arusha.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akizungumza na wadau na viongozi wa Maeneo ya Jumuia ya Hifadhi ya Wanyamapori nchini (WMA), ulioanza jana jijini Arusha kujadili uboreshaji mfumo wa usimamizi na uendeshaji jumuia hizo.
 
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akisalimiana na mdau wa masuala ya utalii na uhifadhi nchini, Willy Chambulo, muda mfupi baada ya kufungua mkutano wa majadiliano kuhusu uboreshaji wa mfumo wa usimamizi na uendeshaji Maeneo ya Jumuia ya Hifadhi ya Wanyamapori Tanzania (WMA), ulioanza jana jijini Arusha.
KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO KATI YA WIZARA NA WMAs
UKUMBI WA NAURA SPRINGS, ARUSHA,
TAREHE 2 & 3 JULAI, 2015.

Mhe. Mahmood Mgimwa - Naibu Waziri,Wizara ya Maliasili na Utalii;
Dkt. Adelherm Meru         - Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii;
Bw. Herman Keraryo        - Mkurugenzi, Idara ya Wanyamapori;
Dkt. Simon Mduma            - Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Utafiti wa
                                           Wanyamapori;

Dkt. Freddy Manongi        - Mhifadhi Mkuu, Mamlaka ya Hifadhi ya
                                           Ngorogoro; 

Bw. Allan Kijazi                - Mkurugenzi Mkuu, Hifadhi za Taifa;
Mwenyekiti, Muungano wa Jumuiya Zilizoidhinishwa;
Wakurugenzi/ Wawakilishi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali
(USAID, WWF, FZS, AWF, WCS);
Viongozi wa Maeneo ya Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori;
Wawakilishi kutoka Sekta binafsi;
Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii;
Maafisa Wanyamapori wa Wilaya;
Mabibi na Mabwana.

Napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wote katika mkutano huu muhimu unaolenga kutathmini ustawi na changamoto zilizojitokeza/zinazojitokeza katika usimamizi wa shughuli za uhifadhi kwenye Maeneo ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori “Wildlife Management Areas” (WMAs) nchini.

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana  
Sera ya wanyamapori ya mwaka 1998 kwa mara ya kwanza nchini ilielekeza kuanzisha dhana ya ushirikishaji wa jamii katika uhifadhi wa wanyamapori. Dhana hii inatoa fursa kwa wananchi kushiriki katika uhifadhi kwa kutenga maeneo ya ardhi ya vijiji ili kusimamia na kunufaika moja kwa moja kupitia rasilimali ya wanyamapori. Utekelezaji wa dhana hii ulianza rasmi mwaka 2003 na hadi sasa maeneo ya WMAs 21 zenye ukubwa wa kilometa za mraba 36237.7 yameidhinishwa na kutangazwa katika gazeti la serikali. Aidha, maeneo mengine 17 ya WMA yapo katika hatua mbalimbali za uanzishwaji.

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana 
Kwa miaka 12 ya utekelezaji wa dhana hii tumeshuhudia mwamko katika jamii kushiriki katika kiuhifadhi, na wao kujipatia manufaa ikiwemo ajira, kipato katika ngazi ya jumuia, vijiji husika na kuchangia katika miradi ya maendeleo katika sekta za elimu, afya, maji. Pamoja na mafanikio haya bado kumekuwepo na changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika utekelezaji wa dhana hii nchini. Hivyo mkutano huu ni mwendelezo wa matokeo ya tuliyojifunza wakati wa kutekeleza dhana ya kushirikisha jamii katika uhifadhi kwa kuwaleta pamoja wadau muhimu na wataalamu ili kubadilishana uelewa, uzoefu, matokeo ya tafiti, na kutoa fursa ya mjadiliano rasmi yenye malengo kujitathimini mahali tulipotoka, tulipo na  tunapotakiwa kwenda.

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana 
Naomba nijikite katika changamoto chache lakini muhimu ambazo mimi kama Waziri mwenye dhamana nimeziona katika kutekeleza majukumu yangu ambayo ningependa kupitia mkutano huu uziangalie kwa kina na kutusaidia kutoa ushauri wa kuandaa maelekezo ya kisera yatakayoweza kutoa majibu kama ifuatavyo:
1.   Kuchangia uboreshaji wa utawala bora katika rasilimali za wanyamapori na matokeo ya jamii na uhifadhi wa wanyamapori, ikiwa pamoja na kuhakikisha utawala bora kulingana na maslahi na haki za jamii (muingiliano wa mamlaka kati ya viongozi wa wilaya, vijiji na wale wa jumuiya/WMA na mgongano wa maslahi).
2.   Migogoro inayotokana na uwekezaji katika maeneo ya WMA mfano MBOMIPA.
3.   Mgogoro unaotokana na gharama za watalii katika hoteli na loji zilizopo ndani ya hifadhi za Taifa na zile zilizopo ndani ya WMAs zinazopakana.
4.   Uwiano wa mgawanyo wa mafao yatokanayo na uwekezaji katika maeneo ya WMAs kati ya Jumuiya/WMA, Serikali kuu, halmashauri za wilaya na vijiji wanachama.
5.   Matumizi ya fedha/mapato zinazotokana katika WMA na katika vijiji kutofanya kazi zitarajiwa.
6.   Ucheleweshaji wa mgao wa fedha unaotakiwa kupelekwa katika WMAs kutoka Serikalini.

Wageni Waalikwa Mabibi na Mabwana, 
Mkutano huu ambao ni wa kwanza kufanyika na kukutanisha Wizara, Jumuiya Zilizoidhinishwa na Wawezeshaji wa WMAs ni fursa muhimu ambayo ikitumika ipasavyo na kwa nia njema itatoa suluhisho lkwa changamoto nilizozianisha hajo juu. Hivyo natoa wito kwa washiriki wa mkutano huu kuhakikisha fursa hii haipote bali itoe tija katika ustawi wa dhana ya kushirikisha jamii katika uhifadhi endelevu na wenye manufaa kwa jamii.

Wageni Waalikwa Mabibi na Mabwana 
Mwisho lakini sio kwa umuhimu napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wawezeshaji katika uanzishaji na uendeshaji wa WMA. Kipekee nitambue michango iliyotolewa na  USAID, WWF, FZS, AWF, WCS, KfW, BTC, DANIDA, GTZ (GIZ) na AFRICARE. Aidha, ninawashukuru USAID, AWF na WWF kwa ufadhili wao katika kufanikisha mkutano huu. Ni matumaini yangu kuwa mkutano huu utaleta tija inayokusudiwa ili kuhakikisha kuwa shughuli za uhifadhi katika WMA zinaendeshwa kwa ufanisi.

Natangaza rasmi Mkutano huu umefunguliwa.

WAHARIRI KATIKA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI WAFURAHIA ZIARA KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA KISIWA CHA SAANANE.

$
0
0
Baada ya safafri ya takribani dakika 10 hatimaye Wahariri na Wanahabari wakawasili hifadhi ya Taifa ya Saaanane.
Baadhi ya Wahariri na Waandishi wa habari wakiwa katika Boti maalumu kwa ajili ya safafri ya kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane jijini Mwanza.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa ,TANAPA,Pascal Shelutete alikuwa ni miongoni mwa wahifadhi walioongoza kundi hilo la Wahariri na Wanahabari kuelekea hifadhi ya Saanane.
Safari ya kutembelea maeneo mbalimbali katika hifadhi hiyo ilianza.
Wahariri walipata maelezo katika maeneo tofauti tofauti.
Wakati mwingine katika mapitio ndani ya Hifadhi hiyo,wahariri na wanahabari walilazimika kupita kwa staili ya kutambaa.
Wengine walihitaji pia msaada ili waweze kuvuka kwa baadhi ya  maeneo .
Baada ya safari ya muda mrefu ,ndipo wakafika katika jiwe la kuruka na kuamua kupumzika.
Mazoezi ya kuruka yakaanza sasa.
Mhariri wa Channel ten Esther Zeramula akionesha umahiri katika kuruka katika eneo hilo.
Mhariri Jackton Manyerere pia hakua nyuma kuonesha umahiri wake.
Mhariri Mniku Mbani pia .
Wengine tukapata picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu.
Safari ya kurudi ikaanza kwa kundi la kwanza la Wahariri..
Wakati huo kundi la pili ndio lilikuwa likiwasili katika eneo hilo.
Baada ya kufika taswiraz zikaanza kuchukuliwa ,kama inavyoonekana hapa mhariri Dulinga akimchukua taswira mhariri Theofily Makunga.
Pozi za picha nazo hazikuwa mbali kwa baadhi ya wahariri.
Picha zaidi muelekeo wa ziwani.
Wahariri wakaoneshana umahiri katika kuruka .
Kama iliyokuwa kwa kundi la kwanza hawa nao wakapata picha ya pamoja.
Kisha safari ya kurudi ikaanza  huku wakifurahia Mandhari ya ziwa Victoria.

Na Dixon Busagaga wa Globuya Jamii Kanda ya Kaskazinia aliyeko jijini Mwanza.

NHC yanyang’anya mashine za kufyatulia matofari baada ya Halmashauri za Mikoa baada ya kushindwa kutumia fursa hiyo

$
0
0
● Mkoa wa Katavi na Rukwa washindwa kutumia fursa ya msaada huo● NHC yanyang’anya mashine Halmashauri za Mikoa hiyo● Zatakiwa kuomba upya mashine hizo na kuunda vikundi imara Katika kuhakikisha kuwa rasilimali za umma zinatunzwa, kutumika ipasavyo na kuhakikiwa, NHC imeendelea kuwakagua vijana waliopewa msaada wa mashine za kufyatulia matofali yatakayowezesha wananchi kujijengea nyumba za gharama nafuu katika Halmashauri zote za Mikoa ya Katavi, Mbeya na kukamilika Mkoani Iringa. 

Kwa ujumla, vijana wana ari ya kutosha ingawa wana changamoto zinazohitaji msukumo wa Halmashauri zao, hasa za masoko ya matofali yao pamoja na mtaji wa kuwawezesha kuendelea na uzalishaji wa benki ya matofali ya kuuzia wananchi. Katika ziara ya NHC Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya hizo wameomba NHC isiwanyang’anye mashine na wameahidi kuwapa vijana mikopo na kuwasaidia malighafi za kuwawezesha kutengezea matofali hayo ikiwemo mchanga, sementi na udongo maalum kwa kazi hiyo. 

Hata hivyo, Mikoa ya Rukwa na Katavi muitikio wa vijana na Halmashauri hizo ukiacha Halmashauri ya Mlele ambayo inafanya vizuri, umekuwa hafifu sana na Shirika limelazimika kuzinyang’anya Halmashauri hizo mashine na kuzitaka kuomba upya kama bado wana azma ya kutumia mashine hizo kujiletea maendeleo ya kuwa na nyumba bora na kukuza ajira kwa vijana wao. Fuatilia yaliyojiri katika uhakiki huo katika picha.
New Picture (1) 
Kikundi cha ‘Mshikamano’ katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje kikimsikiliza Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC BW. Muungano Saguya akiwaelezea namna ya kukuza ujuzi na kutumia Halmashauri zao kuongeza ufanisi wa kazi alipowatembelea nakusaidia kuondoa changamoto zinazowakabili. Vijana hao wameshapewe eneo la muda la kuendesheea shughuli zao na wameanza kutengeneza tofali kwa ajili ya kuwauzia wanmanchi.
New Picture (2)
Hii ndiyo hali iliyojitokeza Mkoani Katavi katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda pale NHC ilipolazimika kuzitwaa mashine ilizotoa msaada kwa vijana ili waweze kujiajiri. Kikundi hiki cha Mpanda Hotel ni mojawapo ya vikundi vilivyonyang’anywa mashine Mkoani Katavi na Rukwa kwa Halmashauri sita za Mikoa hiyo ukiacha Mlele inayofanya vizuri, kushindwa kuzitumia mashine hizo ipasavyo. Halmashauri hizo zimetakiwa kuomba upya mashine hizo na kuunda vikundi imara baada ya kubainika kuwa vikundi vya awali vilundwa kisiiasa.
New Picture (3)
Kikundi cha vijana cha ITIMBA kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini kikimsikiliza` Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Kasibi Saguya alipowatembelea ili kujuwa changamoto zinazowakabili. Kikundi hicho kimeshapata kazi za watu binafsi na shule ili kuwajengea majengo mbalimbalia na hivyo kupata fedha za kujiendeleza. Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini imekubali kuwapa vijana hao ardhi na maeneo ya kufanyia kazi.
New Picture (4)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Bw. James Milanzi akimsikilza Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya alipofika Ofisini kwake kukumbusha wajibu wa Halmashauri za Wilaya wa kusaidia vijana ili waweze kutengeneza matofali ya kujengea nyumba za gharama nafuu na kujipatia ajira. Halmashauri hiyo imepiga marufuku ukataji miti kwa ajili ya kuchoma matofali na badala yake wananchi wametakiwa kutumia matofali rafiki wa mazingira yanayozalishwa kwa kutumia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana katika Halmashauri zote nchini.

New Picture (5)
Kikundi c ha “CHAPAKAZI” Wilayani Mbarali kikiwa kinamsikiliza Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya alipowatembelea kujuwa changamoto zinazowakabili.Halmashauri ya Mbarali imesaidia vijana vifaa na maeneo ya kutengenezea matofali hayo na vijana wamehamasika baada ya kuhakikishiwa soko la tofali zao.
New Picture (6)
Kikundi cha “JITEGEMEE NA CALVARY “ Wilayani Tukuyu kikiwa tayari kumsikiliza Meneja wa Huduma kwa Jamiii wa NHC Bw. Muungano Saguya alipowatembelea ili kujuwa changamoto zinazowakabili. Kikundi hicho kimeishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Tukuyu kwa kuwapa eneo la kufanyia kazi na masoko ya tofali wanazatengeneza. Kushoto ni Meneja wa NHC Mkoa wa Mbeya Bw. Anthony Komba.
New Picture (7)
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Ubisimbali Jesiwande alipokutana na timu ya NHC na kuchangia hoja ya namna ya kuondoa changamoto za ajira zinazowakabili vijana nchini. Halmashauri hiyo ambayo vijana wake hawajafanya vizuri imeapa kuwapa vijana wake mikopo na kuwatafutia masoko ya matofali yao.
New Picture (8)
Kikundi cha “Umoja wa matofali imara” Wilayani Iringa Vijijini ambacho kimeshajenga jengo kubwa la kibiashara kwa kutumia mashine kilichopewa msaada na NHC kilipata fursa ya kutembelewa na ujumbe kutoka NHC na kupewa msasa na hamasa ya kuendelea kujiletea maendeleo kwa kutumia mashine hizo.
New Picture (9)
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Bi. Sikitu Mwemsi (kulia) akiomba timu ya NHC iliyofanya mazungumzo naye Ofisini kwake kuwapa muda badala ya kuwanyang’anya mashine walizopewa baada ya Halmashauri hiyo kususua kuwasaidia vijana na kusimamia vikundi vyao. Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC ameipa Halmashauri hiyo mwezi mmoja kujiweka sawa na vijana wake kuanza kutumia kikamilifu mashine walizopewa msaada na NHC.
New Picture (10)
Timu ya NHC na Maofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo ikiwa eneo linalotumiwa na kikundi cha vijana cha “Muungano Vijana Kilolo”kilichopewa msaada wa mashine na NHC ambapo walikagua kazi za vijana hao (hawapo pichani) ambapo Wilaya hiyo imeamua kuwapa mkopo vijana hao ili wawe na benki kubwa ya matofali.
New Picture (11)
Kikundi cha vijana cha “Umoja wa Wafyatua matofali” kilichopo katika Kata ya Mkwawa Manispaa ya Iringa kikiwa kimeanza kazi ya kutengeneza matofali kilipotembelewa na timu ya NHC kuona kazi zao. Hiki ni kikundi kinachofanya vizuri katika Manispaa hiyo yenye vikundi vinne vya vijana waliopewa msaada wa mashine na NHC za kufyatulia matofali ya kufungamana.. UMOJA WA WAFYATULA MATOFALI MANISPAA YA IRINGA
New Picture
Kikundi cha SHIDEPHA ambacho kilipewa mafunzo ya namna ya kutumia mashine za kutengeneza matofali ya kufungamana na NHC kikiwa imara na timu ya NHC iliyowatembelea na kuamua kuwaongezewa uwezo kwa kupewa mafunzo na vifaa vya kufanyia kazi. Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC baada ya kuona juhudi zao aliamuru waongezewe mashine mbili ili wasonge mbele na Halmashauri imekitambua kikundi hicho.

WAZIRI MKUU PINDA ATEMBELEA BANDA LA PSPF,AVUTIWA NA NAMNA WATU WALIVYOHAMASIKA KUJIUNGA NA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda akijadiliana jambo na Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Abdul Njaidi (katikati) na Gasper Lyimo jana alipotembelea banda la PSPF katika maonesho ya 39 ya sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Mheshimiwa Pinda alifurahishwa na juhudi za PSPF za kuhakikisha idadi kubwa ya watanzania wanaingia katika hifadhi ya jamii.

 Mhadisi Alli Shanjirwa akitoa maelezo kwa mmoja wa wateja waliotembelea katika banda ya PSPF katika maonesho yanayoendelea katika viwanja vya maonesho ya biashara vya kimataifa vya Mwalimu Nyerere.

  Baadhi ya wananchi wakipata maelezo kutoka kwa maafisa wa PSPF walipotembelea banda la PSPF.

 Maafisa wa PSPF Rahma Ngassa (kushoto) na Colleta Mnyamani wakitoa maelezo kwa wateja waliotembelea banda la PSPF katika  maonesho ya 39 ya kamataifa ya Dar es Salaam, yanayoendelea jijini  Dar es Salaam.

Maafisa wa wakitoa maelezo kwa wateja waliotembelea banda la PSPF katika  maonesho ya 39 ya kamataifa ya Dar es Salaam, yanayoendelea jijini  Dar es Salaam.

CHUO KIKUU CHA IRINGA ZAMANI TUMAINI KESHO KUADHIMISHA SIKU YA UTALII NA UTAMADUNI MAADHIMISHO YATAFANYIKA KATIKA CHUO HICHO.

$
0
0
 
 MHADHILI WA CHUO KIKUU CHA IRINGA JIMSON SANGA 
 
 baadhi ya majengo ya chuo kikuu cha iringa zamani tumaini
 
  baadhi ya majengo ya chuo kikuu cha iringa zamani tumaini

Na Fedy Mgunda,Iringa



Chuo kikuu cha IRINGA ZAMANI TUMAINI kesho kinatarajiwa kuadhimisha siku ya utalii wa kitamaduni  katika chuo hicho.


Akizungumza na blog hii mkuu wa kitengo cha utalii cha chuo  hicho MHADHILI WA CHUO KIKUU CHA IRINGA JIMSON SANGA amesema kuwa wameamua kuadhimisha siku hiyo ili kuwakumbusha wananchi juu ya kuuezi utamaduni wao na kuacha kuiga tamaduni za kigeni.


Aidha SANGA amesema kuwa chuo hicho kimekuwa kikifundisha elimu ya utalii ndani ya chuo tu sasa imefika wakati wa kutoka na kuifikia moja kwa moja  jamii ambayo haina elimu hiyo.


“Tunaona wakina mama ntilie wanauza vyakula ya kitamaduni lakini hawana wateja kwa sababu wanashindwa kutoa huduma ya kuridhisha kwa wateja hata hivyo mama ntilie wengine hutoa huduma kwa kutofata mazingira ya kiafya”.alisema SANGA


Ameongeza kuwa watanzania  wengi hatuna tabia ya kuupenda utamaduni wetu au kuipenda asili yetu tunaona wananchi wengi wanapenda kuiga utamaduni wa kigeni hivyo tunatakiwa kuuenzi utamaduni wetu.


SANGA amemalizia kwa kuwataka wanachi wajitokeze siku ya jumamosi ili kujionea vitu mbalimbali ya kitamaduni.


Kwa upande wao WANAFUNZI WA CHUO HICHO hasa wanaosomea masomo ya maliasili na utalii wamewataka wananchi wa mkoa wa iringa kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hao.

AIRTEL YAKABIDHI FUTARI KWA WATOTO YATIMA KATIKA VITUO VITATU MKOANI DAR ES SALAAM.

$
0
0
 Meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia) akiongea na wawakilishi wa vituo vitatu vya watoto yatima baada ya kukakabidhi msaada wa vyakula mbalimbali vya mfungo wa Ramadhani kwa wawakilishi wa vituo vya kulelea watoto waliokatika mazingira magumu. Vituo vilivyopata msaada huo ni pamoja na  Almadina cha Tandale, Dogodogo cha Kigogo na Hisani cha Mbaga .wakishuhudiwa na baadhi ya watoto waishio katika vituo hivyo, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Airtel kupitia mpango wake wa huduma kwa jamii imeanza kutoa futari kwa vituo mbali mbali hapa nchini.
 Meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia) akimkabidhi  bibi Kurudhumu Yusuph Juma mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Al- Madina (wa pili Kulia) msaada wa vyakula mbalimbali kwa ajili ya
mfungo  wa Ramadhani wakishuhudiwa na walezi wa vituo vingine vya Dogodogo kilichopo Kigogo  bw, Ditufu Ally (tatu Kulia) na Kituo cha Hisani kilichopo Mbaga bw. Twaha Kambaya (kushoto)  katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Airtel kupitia mpango wake wa huduma kwa jamii imeanza kutoa futari kwa vituo mbali mbali hapa nchini.
 Meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia) akimkabidhi  bw. Twaha Kambaya  (kushoto)   mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Hisani kilichopo Mbagala msaada wa vyakula mbalimbali kwa ajili ya  mfungo huu wa Ramadhani wakishuhudiwa na baadhi ya watoto wa vituo hivyo na mlezi wa kituo cha Al- Madina bi  Kurudhumu Yusuph Juma (kati) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.



Meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel, Hawa Bayumi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto waishio katika vituo vya kulelea watoto walio katika mazingira magumu wakati wa hafla ya kuwakabithi msaada wa vyakula kwaajili ya mfungo wa Ramadhani iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, vituo vilivyopata msaada ni pamoja na  Almadina cha Tandale, Dogodogo cha Kigogo na Hisani cha Mbagala Dar es salaam.

MEDIA CAR WASH FOR CANCER KUFANYIKA KESHO JULAI 4, 2015 LEADERS DAR ES SALAAM

FINLAND NA TANZANIA KUSHIRIKIANA KIBIASHARA

$
0
0
 Mkurugenzi wa biashara ya ndani mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania (TANTRADE), Edwin Rutagarutwa akizungunza  katika semina ya kibiashara iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu nyerere jijini Dar es Salaam  leo. Kuhusiana na  wigo wa biashara hapa nchini na nchi ya Finlan.
 Mwenyekiti wa mkutano na Ushirikishaji  wa ubalozi wa Finland,Siv Ahlberg katika akizungunza  katika semina ya kibiashara iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam  jana, kuhusiana na historia ya Finland pamoja na njia za kibuiashara za nchi yao.
 Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel akiuliza swali kuhusiana na utoaji elimu kwa wananchi kuhusiana na masual;a ya kibiashara kati ya wafinland waliopo hapa nchini na Watanzania.
 Mkurugenzi mtendaji Global Education Link, Abdulmalik Mollel akizungumza na  Balozi wa Finland hapa nchini, Sinikka Antila mara baada ya mkutano uliokuwa ukishirikisha masuala ya biashara kati ya wafanyabiashara hapa nchini na wafinland, na Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link, David Nsimba.
Mkurugenzi mkuu mtendaji wa kampuni ya 3disius International , Afrodisius Sabuni akichangia  maada katika kuhusiana na kinga ya mjasisliamali wa kitanzania kwenye kutoa taarifa za kibenki kwa wawekezaji wa kigeni iko na imara kwa kiasi gani na inaulinzi wa kutosha katika jamii, katika semina ya kibiashara iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu nyerere jijini Dar es Salaam  jana. 
Baadhi ya wadau wa biashara waliohudhuria katika mkutano unaoshirikisha wadau wa biashara wa hapa nchini na wafinland.

NEC NA VIONGOZI WA VYAMA VYASIASA ,WAJADILI MAADILI YA UCHAGUZI WA RAIS,WABUNGE NA MADIWANI

$
0
0
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji  Mstaafu Damiani Lubuva akizungumza wakati wa mkuato wa kujadili maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
 Mkurugenzi wa uchaguzi, Julius Mallaba akizungumza leo katika mkutano wa kujadili maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
  Baadhi ya viongozi wa vyombo vya siasa wakifuatilia kwa umakini katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
 Kamishina wa Polisi, Mussa Ali Mussa akizungumza kuhusiana na usalama kipindi cha kampeni na uchaguzi mkuu katika mkutano wa kujadili maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
Katibu Mkuu wa chama cha Tanzania Labour Part(TLP), Nancy Mrikalia akichangia maada katika mkutano wa kujadili maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
 
Na Avila kakingo, Globu ya jamii.
TUME ya uchaguzi NEC  wakishirikiana na viongozi wa vyama  vya siasa wakutana kujadili  maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ikiwa tunaelekea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika  Oktoba mwaka huu.

 Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji  Mstaafu Damiani Lubuva, Kwenye ufunguzi wa mkutano wa tume na viongozi wa vyama vya siasa kuhusu maadili ya uchaguzi leo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji  Mstaafu Damiani Lubuva amesema kuwa kupiga kura ni haki ya msingi na ya kikatiba kwa kira raia wa Tanzania hivyo uchaguzi unatakiwa uwe wa haki, uhuru, uaminifu na wakuaminika.

Lubuva amesema kuwa  maadili yanayojadiliwa yahahusu zaidi  vyama vya siasa, wagombea wote, serikali pamoja na tume ya uchaguzi pia  kila chama na wagombea wanatakiwa kuheshimu na kutekeleza sheria za uchaguzi,kanuni na maadili na sheria nyingine za nchi katika kipindi cha kampeni kuanzia siku moja baada ya uteuzi hadi siku ya uchaguzi Oktoba mwaka huu.

Pia ametoa wito  kwa wanasiasa wote kuwaelimisha wafuasiwao kuondoka vituoni nara  baada ya kupiga kura ili kuepusha msongamano wa vitendo vingine vinavyoweza kuchochea kuvunjika kwa amani.

Kwa upande wa jeshi la polisi wametoa wito kwa wagombea wote watakao wania nafasi mbalimbali wafanye kampeni zake kipindi wakati kuna mwanga na si usiku ili kuepuka matatizo mbalimbali yatakayojitokeza.

Wanne wajishindia mamilioni ya Bayport

$
0
0
Zoezi la kuchezesha droo hiyo ya Kopa na Bayport likiendelea. Washindi wanne walijishindia Sh Milioni 1,000,000 kila mmoja.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo kushoto, akizungumza jambo kwenye heka heka ya droo ya kutafutwa washindi wanne wa shindano la Kopa na Bayport linaloendeshwa na Taasisi hiyo. Aliyefungwa kitambaa usoni ni Meneja wa Bayport Financial Services, Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala. Kulia ni Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo. Washindi hao wanne kila mmoja amejishindia Sh Milioni 1,000,000 baada ya kukopa kwenye taasisi hiyo ya kifedha nchini.

Wateja walioshinda katika bahati nasibu yetu na maeneo watokayo kwenye mabano ni pamoja na Simion Ngassa (Iringa), Sisco Haule, (Kigoma), Said M Mkinda (Dar es Salaam) na Phelis Nziku ambapo wote kila mmoja watakabidhiwa kiasi hicho cha pesa kutoka Bayport Financial Services. Naye Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo aliipongeza Bayport Financial Services kwa kuendelea kubuni mambo yanayoweza kuwapatia mwanga wateja na Watanzania kwa ujumla.

“Hii ni bahati nasibu nzuri na rahisi kuchezwa na kila mtu, maana haina vigezo zaidi ya mtu kuingia kwenye droo kama atakuwa amekopa tu, iwe kwenye mtandao wao au kufika katika tawi la ofisi yao yaliyoenea sehemu mbalimbali za Tanzania Bara,” alisema Ngolo, huku akiwataka Watanzania kuendelea kunufaika na huduma mbalimbali za Bayport. Huduma zinazotolewa na Bayport ni pamoja na mikopo ya fedha, mikopo ya bidhaa mbalimbali kama vile vifaa vya ujenzi, bodaboda, injini ya boti, pembejeo za kilimo, zikiwa ni miongoni mwa huduma zinazorahisisha maisha kwa Watanzania wote.

KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA RUKWA NDUGU ERASMUS RUGARABAMU AFUNGUA RASMI MAFUNZO YA SIKU SITA YA WALIMU WAKUU NA WARATIBU ELIMU KATA

$
0
0
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Erasmus Rugarabamu akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku sita ya Walimu Wakuu Shule za Msingi na Waratibu Elimu Kata juu ya muongozo wa uendeshaji wa shule (School Management Tool Kit) pamoja na usimamizi wa ufundishaji wa kusoma, kuandika na kuhesabu leo tarehe 03 Julai 2015. 

Mafunzo hayo yanayoendeshwa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu yanafanyika Mkoani Rukwa katika Chuo cha Ualimu Sumbawanga ambapo jumla ya washirikia 200 kutoka Halmashauri mbili za Manispaa ya Sumbawanga na Sumbawanga Vijijini wameshiriki kwenye awamu hii ya kwanza ya mafunzo. Mafunzo haya ni sehemu ya mpango wa BRN wenye lengo la kuinua ubora wa elimu nchini.
 Ndugu Nicholaus Moshi ambae ni Mratibu wa Programu ya Mafunzo ya Waalimu Kazini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza katika Semina hiyo. Ndugu Moshi ni mmoja ya wawezeshaji wakuu katika Mafunzo hayo.
 Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo.
 Mkuu wa Chuo cha Ualimu Sumbawanga Bi. Witnes Maeda akitoa nasaha zake katika mafunzo hayo.
Mmoja ya washiriki akitoa neno la shukurani kwa niaba ya washiriki wote.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

KATIBU MKUU KIONGOZI ,BALOZI OMBENI SEFUE ATEMBELEA MAONESHO YA 39 VIWANJA VYA M.J.NYERERE JIJINI DAR

$
0
0
 Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Fedha alipotembelea katika banda hilo katika maonesho ya 39 yanayofyanyika katika Viwanja Vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) leo jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha,Ingiahedi Mduma.

Katibu Mkuu wa Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue  akisalimiana Afisa Habari wa Shirika la Taifa la  Bima( NIC),Mwanaidi Shemheta alipotembelea banda hilo katika maonesho ya 39 katika Viwanja vya Mwalim Nyerere (Sabasaba) leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi akisaini Kitabu cha wageni katika banda la Shirika la Taifa la Bima (NIC) alipotembelea Maonesho ya 39 yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (Saba saba) leo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akipata maelekezo katika Mfuko wa Pensheni wa PSPF alipotembelea maonesho ya 39 yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (Saba saba) jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akipata maelezo kutoka Afisa Masoko Mwandamizi wa GEPF,Violeth Nyakunga  alipotembelea maonesho ya 39 yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar esalaam leo. 
Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akipata maelekezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa ajira ,Masoko na Utafiti  wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA)Julius Mjelwa  alipotembelea katika maonesho ya 39 yanayofanyika katika viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akipata maelekezo kutoka kwa  Mwalimu wa Umeme   wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA),Majollo Mwigowe, alipotembelea katika maonesho ya 39 yanayofanyika katika viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam. (picha zote na Chalila Kibuda wa Globu ya Jami).

SIMBA SPORT CLUB YAZINDUA HUDUMA MPYA YA SIMBA NEWS

$
0
0
Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva (katikati) Akizungumza katika Uzinduzi Huo Akiwa na   Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya EAG Group LTD Imani Kajula (Kushoto) Pamoja na Meneja Uendeshaji wa Premier Mobile Solutions, Bi Lulu Ramole.

Simba Sports Club kwa kushirikiana na Kampuni ya Tigo Tanzania zimezindua huduma ya ujumbe mfupi ijulikanayo kama ‘SIMBA NEWS’, ambayo lengo lake nikuwapatia wateja wa Tigo taarifa zinazoihusu klabu ya Simba popote walipo nchini.

Huduma hii mpya inajulikana kama ‘SIMBA NEWS’. Njia hii ni rahisi na yenye ufanisi yenye kuifanya dunia ijulikane kwa wateja wake. “Pamoja na kasi yaukuaji wa Tehama, Tigo inaelewa umuhimu wakutoa taarifa kwa wateja wake, ndiyo maana leo, tunajisikia fahari kuzindua huduma hii iliyotengenezwa vizuri ya SIMBA NEWS nawashirika wetu wa klabu ya SIMBA, EAG Group LTD pamoja na Premier Mobile Solutions (PMS), ilikuendelea kuwapa wateja wetu taarifa zinazohusu masuala ya sasa huku wakifurahia habari mpya zinazohusu klabu,”alisema meneja wa mawasiliano ya kibiashara Jacqueline Nnunduma.

Lengo letu si tu kuwapatia wateja wetu taarifa kiurahisi zaidi, lakini pia kuwapatia taarifa hizo kwa wakati na zenye uhakika kutoka vyanzo vya michezo vyenye kuaminika,” aliongeza Nnunduma.

Akizungumza kwa niaba ya Klabu ya Simba,Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva alisema, “Tunaamini ubunifu huu bila shaka utawawezesha mashabiki wote wa Simba na wa soka kwa ujumla ambao pia ni wateja wa Tigo kupata habari mbalimbali za klabu ya Simba kupitia simu zao za mkononi”.
Tunawahimiza mashabiki wetu kujiunga na huduma hii kupitia Tigo ili waweze kupata nakufurahia habari mbalimbali kutoka klabu ya Simba. Aliendelea Aveva.


Akiongea katika tukio hilo Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya EAG Group LTD Imani Kajula ambao ni washauri na watekelezaji wa shughuli za kibiashara na masoko katika klabu ya Simba, alisema “Tunatarajia kuendelea kuwapatia mashabiki wa Simba huduma za kisasa kwa kutumia teknolojia zisizokuwa na usumbufu wa aina yeyote kupitia wadau wanaoaminika ndani ya Tanzania”.

Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa Premier Mobile Solutions, Bi Lulu Ramole alisema kuwa huduma hii imetengenezwa ili kuwawezesha wateja kupata habari za papo kwa papo naaliongeza kuwa huduma ipo katika mfumo wa vifurushi vya Combo / BUNDLE PACK ambapo wateja wa Tigo watakuwa wakilipia mara moja kwa siku na kupokea kiwango cha chini cha habari nne (04) na habari mpya za kila siku zina zohusu klabu ya Simba.

Huduma pia itamruhusu mteja aliyejiunga kujitoa kwenye huduma hii wakati wowote akitaka bila vikwazo vyovyote na pia kwenye huduma hii kutakuwepo na neon kuu “MSAADA”kwa ajili ya kusaidia juu ya maswali mbalimbali ya nayo ulizwa mara kwa mara na wateja wakati wakifurahia huduma.

Ili kujiunga na huduma hizi unatakiwa kutuma neon kuu SIMBA kwenda 15460. Utakapo jiunga tu mteja atapokea habari kutokana na neon analolituma kila siku na atatozwa kiasi cha shilingi za kitanzania 150 kwa siku. Na ili kujitoa kwenye huduma mteja atahitaji kutuma neno ONDOA SIMBA kwenda 15,460.

WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA AKUTANA NA WAJASIRIMALI WA ASALI KATIKA VIWANJA VYA M.J NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,akipata maelekezo ya asali alipotembelea banda la asali katika maonesho ya 39 yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Wajasiriamali wa bidhaa ya asali  ndani ya maonesho ya 39 yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

CHADEMA YAANDAA KONGAMANO LA WAZEE, KUFANYIKA KESHO HOTELI YA BLUE PEARL UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Hashim Juma Issa (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu kongamano litakalo wakutanisha wazee wote bila kujali itikadi za vyama vyao litakalo jadili mustakabali wa taifa kuelekea uchaguzi mkuu litakalofanyika  kesho ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Makamu  Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Suzan Lymo, akizungumza katika mkutano huo.
 Baadhi ya wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano huo.
 Baadhi ya wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano huo.




Na Dotto Mwaibale

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeandaa 
kongamano la wazee ambalo litafanyika Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam kesho.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo mchana 
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la chama hicho, Hashim Juma Issa alisema kongamano hilo litawahusisha wazee wote nchini bila ya kujali itikadi za vyama vyao.

Alisema dhima kubwa ya kuanzisha kongamano hilo ni kuwapa elimu wazee bila kujali itikadi zao za kisiasa  hasa katika kipindi hiki cha  kuelekea uchaguzi mkuu. 

"Wazee wengi wamekuwa hawafahamu nini majukumu yao kama wazee lakini kongamano hili litakuwa ndiyo chanzo kikubwa cha 
kuwafahamisha wazee majukumu yao hasa katika wakati huu wa 
kuelekea uchaguzi," alisema Issa.

Alisema kila mtu anafahamu  binadamu huwa anapitia hatua muhimu za maisha nazo ni utoto,ujana na utu uzima hivyo hamna budi wazee hawa kuelewa lengo kuu katika katika uchaguzi mkuu huo kuwa katika mstari ulinyooka. 

"Kumekuwa na tabia ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwatumia wazee kwa ujanja tena hasa wakiwa na matatizo na kuwabagua wa vyama vingine lakini sisi katika kongamano hili hatutobagua mzee wa chama chochote katika kongamano hili kwani wazee wote ni hazina,"alisema

"Hakuna asiyefahamu kuwa kwa sasa nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu ambao uchaguzi huu utakuwa ni mkubwa na wa aina yake hivyo kwa kuwaita wazee hawa itakuwa ni muendelezo wa kupata hekima zao kama wazee"alisema.

Issa alisema katika uchaguzi mku wazee wana jukumu kubwa la 
kuhakikisha kushiriki kikamilfu katika zoezi zima la kujiandikisha na kupiga kura ipasavyo.

Alisema hatua hiyo haina budi kuwasahawisi watoto na watu wakubwa na wajukuu kushiriki kwa ukamailifu katika tukio hili kwani kila mtu anahitaji mabadiliko katika nchi.

Hata hivyo Issa alisema wazee pia wana jukumu kubwa la kutatua 
migogoro ,kushawisi na kusimamia maadili lengo likiwa ni uthubutu wa kukemea viongozi wanaopata madaraka kwa njia ya rushwa na ufisadi.

Alisema wanahitaji wazee watakaosimama kidete na kupaza sauti zao katika kukemea maovu na watenda maovu bila kuona haya.

Alisema katika kongamano hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Wilbroad Slaa huku mada mbalimbali zitatolewa na Mabere Marando pamoja na viongozi wa dini ili kuwapa elimu wazee kutokana na maadili ya nchi kumomonyoka kwa kiasi kikubwa.

NEC YATOA MWALIKO WA WAANGALIZI WA NDANI WA UCHAGUZI MKUU .

$
0
0

 Na Jovina Bujulu.

Taasisi na Asasi mbalimbali zimetakiwa kutuma maombi kwenye ya  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa ajili ya kusimamia uchaguzi mkuu utatarajia kufanyika mwezi oktoba mwaka huu.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tume hiyo leo jijini Dar es salaam, imezitaka taasisi na asasi zenye nia ya kuwa waangalizi wa Uchaguzi Mkuu ujao kuwasilisha maombi yao katika ofisi ya NEC kuanzia  Julai 5 hadi Oktoba 6 mwaka huu.


Taarifa hiyo imeongeza kuwa waombaji wanatakiwa kuwalisha maombi yao yakiwa na anuani kamili ikiwemo ya makazi ya taasisi na asasi husika , mahali inapofanyia kazi, shughuli zake na sehemu ambayo taasisi inataka kuendeshea shughuli za uangalizi.


Mambo mengine yanayohitajika katika maombi hayo ni idadi ya wafanyakazi wa taasisi husika na taarifa zao binafsi na pia taasisi iambatanishe vivuli vya nakala cheti za usajili na Katiba ya Taasisi husika.


Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa Mamlaka ya kusajili waangalizi wa ndani kwa mujibu wa sehemu ya IV na V ya kanuni ya uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani.



Uchaguzi Mkuu wa kuwamchagua  Rais , Wabunge na Madiwani  unatarajiwa kufanyika nchini kote Oktoba 25 mwaka huu.

SIMBA SPORT CLUB YAZINDUA HUDUMA MPYA YA SIMBA NEWS

$
0
0
Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva (katikati) Akizungumza katika Uzinduzi Huo Akiwa na   Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya EAG Group LTD Imani Kajula (Kushoto) Pamoja na Meneja Uendeshaji wa Premier Mobile Solutions, Bi Lulu Ramole.
Simba Sports Club kwa kushirikiana na Kampuni ya Tigo Tanzania zimezindua huduma ya ujumbe mfupi ijulikanayo kama ‘SIMBA NEWS’, ambayo lengo lake nikuwapatia wateja wa Tigo taarifa zinazoihusu klabu ya Simba popote walipo nchini.
Huduma hii mpya inajulikana kama ‘SIMBA NEWS’. Njia hii ni rahisi na yenye ufanisi yenye kuifanya dunia ijulikane kwa wateja wake.

 “Pamoja na kasi yaukuaji wa Tehama, Tigo inaelewa umuhimu wakutoa taarifa kwa wateja wake, ndiyo maana leo, tunajisikia fahari kuzindua huduma hii iliyotengenezwa vizuri ya SIMBA NEWS nawashirika wetu wa klabu ya SIMBA, EAG Group LTD pamoja na Premier Mobile Solutions (PMS), ilikuendelea kuwapa wateja wetu taarifa zinazohusu masuala ya sasa huku wakifurahia habari mpya zinazohusu klabu,”alisema meneja wa mawasiliano ya kibiashara Jacqueline Nnunduma.
Lengo letu si tu kuwapatia wateja wetu taarifa kiurahisi zaidi, lakini pia kuwapatia taarifa hizo kwa wakati na zenye uhakika kutoka vyanzo vya michezo vyenye kuaminika,” aliongeza Nnunduma.
Akizungumza kwa niaba ya Klabu ya Simba,Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva alisema, “Tunaamini ubunifu huu bila shaka utawawezesha mashabiki wote wa Simba na wa soka kwa ujumla ambao pia ni wateja wa Tigo kupata habari mbalimbali za klabu ya Simba kupitia simu zao za mkononi”.
Tunawahimiza mashabiki wetu kujiunga na huduma hii kupitia Tigo ili waweze kupata nakufurahia habari mbalimbali kutoka klabu ya Simba. Aliendelea Aveva.
Akiongea katika tukio hilo Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya EAG Group LTD Imani Kajula ambao ni washauri na watekelezaji wa shughuli za kibiashara na masoko katika klabu ya Simba, alisema “Tunatarajia kuendelea kuwapatia mashabiki wa Simba huduma za kisasa kwa kutumia teknolojia zisizokuwa na usumbufu wa aina yeyote kupitia wadau wanaoaminika ndani ya Tanzania”
Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa Premier Mobile Solutions, Bi Lulu Ramole alisema kuwa huduma hii imetengenezwa ili kuwawezesha wateja kupata habari za papo kwa papo naaliongeza kuwa huduma ipo katika mfumo wa vifurushi vya Combo / BUNDLE PACK ambapo wateja wa Tigo watakuwa wakilipia mara moja kwa siku na kupokea kiwango cha chini cha habari nne (04) na habari mpya za kila siku zina zohusu klabu ya Simba.
Huduma pia itamruhusu mteja aliyejiunga kujitoa kwenye huduma hii wakati wowote akitaka bila vikwazo vyovyote na pia kwenye huduma hii kutakuwepo na neon kuu “MSAADA”kwa ajili ya kusaidia juu ya maswali mbalimbali ya nayo ulizwa mara kwa mara na wateja wakati wakifurahia huduma.
Ili kujiunga na huduma hizi unatakiwa kutuma neon kuu SIMBA kwenda 15460. Utakapo jiunga tu mteja atapokea habari kutokana na neon analolituma kila siku na atatozwa kiasi cha shilingi za kitanzania 150 kwa siku. Na ili kujitoa kwenye huduma mteja atahitaji kutuma neno ONDOA SIMBA kwenda 15,460.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA JENGO JIPYA LA OFISI YA TTCL, PEMBA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi ya TTCL, wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Julai 3,2015 Wilayani Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi ya TTCL, Wilayani Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba, leo.
 Baadhi ya wawakilishi wa makampuni na Mashirika waliohudhuria hafla hiyo, wakimsikiliza Makamu wa Rais.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kuhusu ramani ya Jengo hilo la TTCL, kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi ya 'Quality Buildin Contractors Ltd', Khamis Ally Shaibu,  wakati wa hafla fupi ya uwekaji wa Jiwe la Msingi katika Jengo jipya la Ofisi ya TTCL,  iliyofanyika leo Wilayani Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba. Kulia kwa Makamu ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa.
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images