Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

MKUU WA MKOA WA MWANZA AANZA KUSHUGHULIKIA SUALA LA LESENI ZIPATIKANE KILA WILAYA

0
0

WANAHABARI WAPEWA SEMINA KUHUSU MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

0
0
Kaimu Mkurugenzi Magonjwa Yasiyoambukiza wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Auson Rwehimbiza (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kwenye semina ya siku moja kuhusu magonjwa yasiyoambukiza. Kulia ni Meneja Mradi Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (TANCDA
Kaimu Mkurugenzi Magonjwa Yasiyoambukiza wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Auson Rwehimbiza (kulia), akimuelekeza jambo Ofisa Habari wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Catheline Sungura wakati wa semina hiyo.
Ofisa Habari wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Catheline Sungura (kushoto), akielekeza jambo kwenye semina hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye semina hiyo.

Semina ikiendelea.



Na Dotto Mwaibale

MAISHA ya watu katika nchi zinazoendelea, yapo hatarini kutokana na asilimia 50 ya magonjwa yasiyoambukiza kusababisha vifo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati wa semina ya magonjwa yasiyoambukiza iliyondaliwa mahususi kwaajili ya wanahabari yenye lengo la kukamilisha mkakati pamoja na mpango kazi 2015/2020, Kaimu Mkurugenzi Magonjwa yasiyoambukiza, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Auson Rwehimbiza aliyataja magonjwa yasiyoambukiza ni moyo na mishipa ya damu, kisukari, kansa na magonjwa sugu ya mfumo wa hewa.

Alisema magonjwa hayo yanazidi kuongezeka nchini hasa kwa jamii ya watu waishio mjini na kuongeza kuwa watu wazima wenye umri wa miaka 80 kuwa na magonjwa hayo kwa asilimia 1 hadi 3 na msukumo wa juu wa damu kwa asilimia 5 hadi 10.

"Tathmini ya mwaka 2012 iliyohusisha watu wazima katika wilaya 50, inaonesha viwango vya ugonjwa wa kisukari viliongezeka kwa asilimia 9, huku asilimia 27 kwa msukumo wa juu wa damu," alisema Dk. Rwehimbiza.

Alisema ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa utandawazi, ukuaji wa miji, kutofanya mazoezi ya mwili, ulaji usiofaa, utumiaji wa tumbaku pamoja na unywaji wa pombe kupita kiasi.

Aidha, alisema Tanzania ilianza kujihususha na magonjwa yasiyokuambukiza kuanzia mwaka 2009 hadi 2015, kwa kuandaa mpango mkakati na mpango kazi ambao ulihusisha utekelezaji wa mpango wa taifa wa kisukari kwa kushirikiana na chama cha wagonjwa wa kisukari nchini.  


"Hadi sasa utekelezaji wa mpango wa taifa wa kuanzisha  kliniki za magonjwa yasiyoambukiza umefikia asilimia 75 katika hospitali za mikoana wilaya na vituo vya afya,". Nakuongeza kuwa asilimia 75 ya elimu zinazotolewa na watoa huduma wa afya katika hospitali za mikoa, wilaya na vituo vya Afya.

Anaongeza kuwa, shirika la afya duniani WHO, liliandaa mpango mkakati ambao ulidhamiria kupunguza viwango vya sasa vya vifo vitokanavyo na magonjwa hayo kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2025 na kupendekeza mapendekezo ya hiari lengo ikiwa kufanikiwa kwa mkakati huo.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba -0712-727062)

January Makamba: Sigombea Kupambambana na Mtu bali Kupambana na Matatizo ya watanzania.

0
0
Mh Naibu wa waziri wa Sayansi na Teknolojia na Mtangaza nia kugombea nafasi ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, January Makamba anaendelea na Ziara yake ya Kusaka wadhamini katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.

Mgombea huyo leo alikua Singinda kuomba udhamini na kapata udhamini wa kutosha kwa wanachama wa CCM singinda, Mbali na hilo Mh January alizaliwa katika mkoa huo wakati baba yake mzee Yusuph Makamba akiwa mkoa huo kikazi.

Wanasinginda wamemsikiliza kwa makini Mh January na kuamini kuwa ni kija ambaye ataleta mabadiliko kutokana na majawabu yake juu ya kero mbalimbali ambazo zinawakabili watanzania walio wengi.

January Makamba aliwambia wanasinginda kuwa wananchi wanaitaji mabadiliko na wasipoyapata ndani ya CCM watayafuata nje ya CCM, kauli iliyosemwa na Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere, Makamba amewaeleza kuwa ili mabadiliko hayo  yatokee ni lazima wachague kiongozi wa aina yake ambaye akipanda jukwaani hana mzigo wowote wala hatotumia muda mwingi kujielezea lakini pia anaomba nafasi hiyo sio kwa ajili ya kumkomoa wala kupambana na mtu yeyote bali ameomba nafasi hiyo kupambana na matatizo pamoja na changamoto za watanzania.





KINANA NA NAPE WAONGOZA MAKUNDI YA VIJANA KUSHIRIKI JOGGING JIJINI MWANZA ASUBUHI HII.

0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wameongoza makundi ya vijana kutoka Shirikisho la Vyuo Vikuu pamoja na Machinga wa mjini Mwanza kukimbia mchakamchaka (jogging) kwa umbali wa zaidi ya kilometa 2,kuanzia Barabara ya Stesheni,kupitia barabara ya Posta,Kenyatta, Karuta,Lumumba maeneo ya Soko Kuu mpaka Stendi ya zamani Tanganyika.

Viongozi mbali mbali walishiriki mchakamchaka huo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Magessa Mulongo,Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Masoor na Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Ndugu Miraji Mtaturu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana akikimbia  mchaka mchaka (jogging)katika mitaa ya jiji la Mwanza ,wengine pichani ni Katibu wa CCM wilaya ya Nyamagana Mpanda(kushoto),Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Ndugu Miraji Mtaturu na wa mwisho kulia ni Mwenezi wa CCM mkoa wa Mwanza Magelepa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na vijana walioshiriki mchakamchaka (jogging) na kuwataka kuendelea kufanya mazoezi kwani yanasaidia kuimarisha afya na kujenga mwili.

WANAHABARI WAPEWA SEMINA KUHUSU MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

0
0
Kaimu Mkurugenzi Magonjwa Yasiyoambukiza wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Auson Rwehimbiza (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kwenye semina ya siku moja kuhusu magonjwa yasiyoambukiza. Kulia ni Meneja Mradi Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (TANCDA
Kaimu Mkurugenzi Magonjwa Yasiyoambukiza wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Auson Rwehimbiza (kulia), akimuelekeza jambo Ofisa Habari wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Catheline Sungura wakati wa semina hiyo.
Ofisa Habari wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Catheline Sungura (kushoto), akielekeza jambo kwenye semina hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye semina hiyo.
Semina ikiendelea.

Na Dotto Mwaibale
MAISHA ya watu katika nchi zinazoendelea, yapo hatarini kutokana na asilimia 50 ya magonjwa yasiyoambukiza kusababisha vifo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati wa semina ya magonjwa yasiyoambukiza iliyondaliwa mahususi kwaajili ya wanahabari yenye lengo la kukamilisha mkakati pamoja na mpango kazi 2015/2020, Kaimu Mkurugenzi Magonjwa yasiyoambukiza, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Auson Rwehimbiza aliyataja magonjwa yasiyoambukiza ni moyo na mishipa ya damu, kisukari, kansa na magonjwa sugu ya mfumo wa hewa.

Alisema magonjwa hayo yanazidi kuongezeka nchini hasa kwa jamii ya watu waishio mjini na kuongeza kuwa watu wazima wenye umri wa miaka 80 kuwa na magonjwa hayo kwa asilimia 1 hadi 3 na msukumo wa juu wa damu kwa asilimia 5 hadi 10.

"Tathmini ya mwaka 2012 iliyohusisha watu wazima katika wilaya 50, inaonesha viwango vya ugonjwa wa kisukari viliongezeka kwa asilimia 9, huku asilimia 27 kwa msukumo wa juu wa damu," alisema Dk. Rwehimbiza.

Alisema ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa utandawazi, ukuaji wa miji, kutofanya mazoezi ya mwili, ulaji usiofaa, utumiaji wa tumbaku pamoja na unywaji wa pombe kupita kiasi.

Aidha, alisema Tanzania ilianza kujihususha na magonjwa yasiyokuambukiza kuanzia mwaka 2009 hadi 2015, kwa kuandaa mpango mkakati na mpango kazi ambao ulihusisha utekelezaji wa mpango wa taifa wa kisukari kwa kushirikiana na chama cha wagonjwa wa kisukari nchini.  


"Hadi sasa utekelezaji wa mpango wa taifa wa kuanzisha  kliniki za magonjwa yasiyoambukiza umefikia asilimia 75 katika hospitali za mikoana wilaya na vituo vya afya,". Nakuongeza kuwa asilimia 75 ya elimu zinazotolewa na watoa huduma wa afya katika hospitali za mikoa, wilaya na vituo vya Afya.

Anaongeza kuwa, shirika la afya duniani WHO, liliandaa mpango mkakati ambao ulidhamiria kupunguza viwango vya sasa vya vifo vitokanavyo na magonjwa hayo kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2025 na kupendekeza mapendekezo ya hiari lengo ikiwa kufanikiwa kwa mkakati huo.

PPF YASAIDIA SHULE YA SEKONDARI IDODI-IRINGA MIFUKO 220 YA SARUJI

0
0
Mifuko ya saruji  220 yenye thamani ya Zaidi Tsh milioni 3.
Meneja wa kanda ya nyanda za juu kusini wa PPF Bw. Ephrahim Mwaikenda  akimkabidhi msaada wa saruji mifuko 220 yenye thamani ya Zaidi Tsh milioni 3 kwa  Mkuu wa shule ya Sekondari Idodi, Christopher Mwasomola  kwaajili ya kujengea majengo yaliyoungua moto katika shule ya Sekondari Idodi iliyopo tarafa ya Idodi mkoani Iringa.

USHIRIKI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KWENYE MAONYESHO YA 39 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DARES SALAAM

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
 TANGAZO KUHUSU USHIRIKI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII  KWENYE MAONYESHO YA 39 YA  BIASHARA YA KIMATAIFA YA DARES SALAAM
  1. Wizara ya Maliasili na Utalii inashiriki kwenye Maonyesho ya 39 ya  Biashara ya Kimataifa ya Dares Salaam (Saba Saba) yatakayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius.K.Nyerere,  Barabara ya Kilwa kuanzia tarehe 28 Juni hadi 8 Julai, 2015.
  2. Karibu kwenye Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii ujionee na kuelimika kuhusu shughuli za Utalii,  Ufugaji Nyuki, Uhifadhi wa Misitu, Malikale na Wanyamapori.
  3. Safari za kutembelea Hifadhi za Mikumi na Saadani kwa gharama nafuu zitakuwepo
  4. Aidha, Wizara itachezesha bahati nasibu ambapo mshindi atazawadiwa safari ya kwenda kutembelea Hifadhi ya Mikumi au Saadani.
  5. Pia, Utapata fursa ya kuwaona wanyamapori hai kama vile Chui, Mamba, Nyoka, Ndege wa aina mbalimbali pamoja na mfalme wa pori SIMBA.
Karibuni Wote
“Unganisha Uzalishaji    na Masoko ”




WATOTO WAKICHEZA SEHEMU HATARISHI

0
0
 Watoto wakiwa katika moja ya michezo wakiwa na hatari ya katatwa na vitu vyenye nnja kali kwakuwa wanatembea bila kuvaa viatu.
Watoto wakijaribu kuruka ukuta bila mafanikio.
 Hali si shwari kwa watoto hawa ambao walikua wakitaka kujaribu kuruka ukuta na kutokufanikisha lengo lao.

WAFANYAKAZI WA WIZARA OFISI YA RAIS ZANZIBAR NA VIONGOZI WASHIRIKI FUTARI YA PAMOJA IKULU ZANZIBAR

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Maalim Seif Sharif Hamad alipowasili viwanja vya Ikulu jana kuhudhuria katika futari ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara zilizo chini ya Ofisi ya Rais.
????????????????????????????????????Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)  na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Maalim Seif Sharif Hamad wakiwa  katika futari ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara zilizo chini ya Ofisi ya Rais,(kushoto) Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.
????????????????????????????????????Viongozi mbali mbali wa Wizara zilizo chini ya Ofisi ya Rais wakiwa katika futari ya pamoja iliyotayarishwa jana katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.
????????????????????????????????????Wafanyakazi wanawake wa Wizara mbali mbali wa Wizara zilizo chini ya Ofisi ya Rais wakiwa katika futari ya pamoja iliyofanyika jana katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar,ambapo Viongozi Wakuu wa Nchi walihudhuria ambao ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,Makamo wa Kwanza wa Pili  wa Zanzibar  Balozi  Seif Ali Iddi.
????????????????????????????????????Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar pia walijumuika katika futari ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara zilizo chini ya Ofisi ya Rais,iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar jana,
????????????????????????????????????Wafanyakazi wanawake wa Wizara mbali mbali wa Wizara zilizo chini ya Ofisi ya Rais wakiwa katika futari ya pamoja iliyofanyika jana katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar,ambapo Viongozi Wakuu wa Nchi walihudhuria ambao ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,Makamo wa Kwanza wa Pili  wa Zanzibar  Balozi  Seif Ali Iddi.

KILICHO BORAA ZAIDI

0
0
 Hali hapa itakuwa ngumu katikati ya barabara na  ni eneo la mistari ya pundamilia nani avuke na asivuke naona sasa wote wameona wavuke.
 Wazee wa kuchagua chagua wakiwa katika harakati za kupata kilicho boraaaa zaidi na ni saizi yake.
Magari yakiwa katika hospitali yake na madaktari wakiwa katika shughuri ya kuyaweka sawa ili yaweze jongea kama mengine.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.)

RAIS KIKWETE KATIKA HAFLA YA MIAKA MIWILI YA KUTAWAZWA KWA POPE FRANCIS KUWA KULIONGOZI WA KANISA KATOLIKI DUNIANI

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla kwenye sherehe za kuadhimisha miaka miwili ya kutawazwa Papa Francis kuwa Kiongozi wa kanisa katoliki nchini jana jioni kwenye makazi ya balozi huyo jijini Dar es salaam
Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla qkihutubia kwenye sherehe za kuadhimisha miaka miwili ya kutawazwa Papa Francis kuwa Kiongozi wa kanisa katoliki nchini jana jioni kwenye makazi ya balozi huyo jijini Dar es salaam
Rais Kikwete akigonganisha glasi na Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla na Muadhama kardinali Polycarp Pengo kwenye sherehe za kuadhimisha miaka miwili ya kutawazwa Papa Francis kuwa Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani  jana jioni kwenye makazi ya balozi huyo jijini Dar es salaam.
Meza Kuu wakati wa hafla hiyo.
rais Kikwete, Waziri Membe,  Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla na  Kaimu Mufti wa Tanzania Sheikh abubakar Zubeiry kwenye sherehe hizo.

RAIS WA ZANZIBAR DK.ALI MOHAMED SHEIN AFUNGA BARAZA LA NANE LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

0
0
????????????????????????????????????Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikagua gwaride maalum la Kikosi cha Polisi akiongozwa na SP Ali Abdalla Kitole wakati wa Ufungaji wa Baraza la Wawakilishi la nane huko Chukwani jana Nje ya Mji wa Unguja. Picha na IKulu.
????????????????????????????????????Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake ya ufungaji wa Baraza la nane la Wawakili wa Zanzibar jana,huko Chukwani Wilaya ya Magharibi Unguja,
????????????????????????????????????Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitia saini kitabu cha wageni alipofika katika Ofisi za Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi  jana alipohudhuria kulifunga Baraza la nane la Wawakilishi la Zanzibar,
????????????????????????????????????Mpambe wa Baraza la Wawakilishi Mohammed Bilali akiwaongoza Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar  Pandu Ameir Kificho, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ambaye ndio mgeni rasmi, pamoja na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Yahya Khamis Hamadi wakiingia katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi  wakati Ufungaji wa Baraza hilo la nane jana.
????????????????????????????????????Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar  Pandu Ameir Kificho alipokuwa  akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na wajumbe wa Baraza hilo pamoja na kulifunga rasmi  Baraza  la nane la Wawakilishi katika ukumbi wa  Baraza Chukwani jana,
????????????????????????????????????Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibarwakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipozungumza nao katika ufungaji rasmi wa baraza hilo la nane la Wawakilishi jana Chukwani Wilaya ya magharibi Unguja,
????????????????????????????????????Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ambao ni Mawaziri wa Wizara mbali mbali akiwepo Mwansheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipozungumza nao katika ufungaji rasmi wa baraza hilo la nane la Wawakilishi  jana Chukwani Wilaya ya Magharibi Unguja.
????????????????????????????????????Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipozungumza nao katika ufungaji rasmi wa baraza hilo la nane la Wawakilishi jana Chukwani  Wilaya ya Magharibi Unguja.
????????????????????????????????????Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ambao ni Mawaziri wa Wizara mbali mbali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipozungumza nao katika ufungaji rasmi wa baraza hilo la nane la Wawakilishi jana Chukwani Wilaya ya Magharibi Unguja.
????????????????????????????????????Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ambao ni Mawaziri wa Wizara mbali mbali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipozungumza nao katika ufungaji rasmi wa baraza hilo la nane la Wawakilishi jana Chukwani   Wilaya ya Magharibi Unguja,
????????????????????????????????????Watendaji wa Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi Unguja wakimsikiza Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufungaji wa Baraza la nane la Wawakili wa Zanzibar jana.
????????????????????????????????????Watendaji wa Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi Unguja wakiwepo na wawakilishi wa Ofisi za Ubalozi na Mashirika ya Kimataifa wakimsikiza Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufungaji wa Baraza la nane la Wawakili wa Zanzibar jana.
????????????????????????????????????Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Pandu Ameir Kificho(katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbali mbali na Wajumbe wa Baraza hilo baada ya kulifunga rasmi Baraza la nane Wawakilishi  jana huko Chukwani Wilaya ya  Magharibi Unguja.

CHADEMA MOSHI VIJIJINI WARUDISHA FOMU ZA KUWANIA UBUNGE NA UDIWANI.

0
0
Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Moshi vijijini,Godlisen Maramia akipokea fomu kutoka kwa Deogratius Mushi ya kuwania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi vijijini wakati liporudisha katika ofisi za chama hicho zilizopo Majengo.
Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Moshi vijijini ,Godlisen Maramia akimpongeza mtia nia Deuogratius Mushi kwa uamuzi wa kuingia katika kinya'ng'anyiri cha kuwania nafasi hiyo.
Mushi akipongezwa na makada wengine wa Chadema waliofika kumsindikiza ofisnini hapo.
Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Moshi vijijini,Godlisen Maramia akipokea fomu toka kwa Tally Kisesa ya kuwania Ubunge wa viti maalumu katika jimbola Moshi vijijini.
Mtia nia wa nafasi ya Udiwani katika kata ya Kindi,kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Michael Kirawira akirejesha fomu ya kuwania nafasi hiyo katika ofisi ya Chadema kata ya Kindi.
Wananchi wa kata ya Kibosho Magharibi wakimlaki Mgombea wa nafasi ya Ubunge Deo Mushi ambaye pia ametangaza kuwania nafasi ya Udiwani katika kata hiyo.
Mgombea wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi vijijini,Deogratius Mushi,akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuasili katika kata hiyo.
Deo Mushi ambaye pia ni mwenezi wa Chadema wilaya ya Moshi vijijini ,akizungumza na baadhi ya wananchi katika kata ya Kibosho Magharibi .
Baadhi ya wananchi waliohudhuria kikao hicho.
Deo Mushi akizungumza.
Mbali na kuwania nafasi ya Ubunge ,Deogratisu Mushi pia amerudisha fomu ya kuwania nafasi ya udiwani katika kata ya Kibosho Magharibi  na hapa akikabidhi kwa Mwenyekiti wa Chadema katika kata hiyo Kikas Mmasi.
Mwenyekiti wa Chadema katika kata ya Kibosho Magharibi Kikas Mmasi akizungumza katika kikao hicho mara baada ya kupokea fomu ya Deo Mushi. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

KOMBE LA MEYA SHINYANGA 2015 LAZINDULIWA,TIMU 18 KUCHUANA, MSHINDI KUONDOKA NA ZAWADI NONO!

0
0
Mashindano ya Kombe la Meya Shinyanga 2015 (Pepsi Meya Cup 2015) yamezinduliwa rasmi leo na mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga.

Mashindano hayo ambayo yameandaliwa na mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam na kudhaminiwa na kampuni ya Vinywaji baridi ya  Pepsi (SBC Tanzania Ltd) yanashirikisha timu 17 za kata zote za manispaa hiyo na timu ya polisi Shinyanga.

Mashindano ya Kombe la Meya Shinyanga yakihusisha mpira wa miguu yataendelea kufanyika hadi tarehe 25,Julai 2015 na yatakuwa yanafanyika siku tatu kwa wiki yaani Ijumaa,Jumamosi na Jumapili.

Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo ataondoka na kitita cha shilingi milioni moja na laki tano,kombe na medali ya dhahabu,wa pili shilingi milioni moja,kombe dogo na medali ya fedha na wa tatu shilingi laki tano,kombe dogo na medali ya shaba.

Malunde1 blog ilikuwepo wakati wa uzinduzi huo,Kadama Malunde,ametuletea picha kutoka eneo la tukio....
Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akizungumza wakati wa ufunguzi wa Pepsi Meya Cup Shinyanga 2015,ambapo alisema lengo la mashindano hayo ya mpira miguu kwa vijana yatakayoshirikisha timu 18 za manispaa ya Shinyanga ni kwa ajili ya burudani,ajira na kusaka vipaji kutoka kwa vijana katika manispaa ya Shinyanga.
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh alisema mashindano hayo yatakuwa yatafanyika kwa muda wa mwezi mmoja na yatafanyika mara tatu kwa wiki katika viwanja vitatu vya Shycom,Kambarage na Polisi mjini Shinyanga.
Mashindano hayo yameanza leo Juni 26,2015 yatafikia tamati Julai 25,2015
Meza kuu wakiwa eneo la tukio.
Meneja mauzo wa Kampuni ya vinywaji baridi Pepsi kanda ya Ziwa Seni Makwaya akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kombe la Meya Shinyanga 2015 ambapo alisema katika mkoa wa Shinyanga ndiyo mara ya kwanza kwa kampuni ya Pepsi kudhamini mshindano ya meya,ingawa huu ni mwaka wa tatu nchini Tanzania tangu waanze kudhamini mashindano ya namna hiyo.
Meneja mauzo  wa kampuni ya vinywaji baridi SBC Tanzania Limited (Pepsi) bwana Promod  Nair akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kombe la meya Shinyanga 2015 ambapo alisema wameamua kudhamini mashindano hayo ili kuinua vipaji kutoka kwa vijana katika manispaa ya Shinyanga.
Meneja mauzo kampuni ya Pepsi mkoa wa Shinyanga bwana Benson Tweve akizungumza katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambapo alizitaka timu za Stand United na Mwadui FC kutumia fursa ya mashindano hayo ya Meya Cup kuchukua vijana wenye vipaji kwa ajili ya kuinua mkoa wa Shinyanga kimichezo.
Mgeni rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kombe la Meya Shinyanga 2015,ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka vijana wa Shinyanga kutumia fursa ya mashindano hayo kuonesha vipaji vyao kwani michezo ni ajira.
Mgeni rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro akikabidhi vifaa vya michezo kwa afisa mtendaji wa kata ya Masekelo yenye Timu ya Masekelo fc iliyocheza mechi ya ufunguzi na Ngokolo fc kutoka kata ya  Ngokolo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza katika mchezo wa mbio za baiskeli  Kulwa Ntyuki uliofanyika mjini Shinyanga wakati wa ufunguzi wa kombe la meya Shinyanga.
Mgeni rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro akikabidhi vifaa vya michezo kwa afisa mtendaji wa kata ya Ngokolo.

Waamuzi wa mchezo wa ufunguzi wakikagua wachezaji wa timu ya Masekelo FC na Ngokol0 FC.
Mgeni rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine akikagua timu ya Masekelo FC kabla ya mechi ya ufunguzi kati ya Masekelo FC na Ngokolo fc haijaanza katika uwanja wa mpira wa Shycom Mjini Shinyanga .
Mgeni rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine akikagua timu ya Ngokolo fc kabla ya mechi ya ufunguzi kati ya Masekelo fc na Ngokolo fc haijaanza katika uwanja wa mpira wa Shycom Mjini Shinyanga.
Waamuzi wa mchezo wakiwa uwanjani.
Mgeni rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine akizungumza na wachezaji wa timu ya Ngokolo fc  na  Masekelo fc na Ngokolo FC
Mgeni rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro akijiandaa kupiga penati huku meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akiwa golini.
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akihangaika golini baada ya kufungwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Mechi kati ya Masekelo fc na Ngokolo fc ukiendelea ambapo hadi mwisho wa mchezo,Masekelo fc bao 2,na Ngokolo fc bao 2.
Wakazi wa Shinyanga wakishuhudia mechi.
Wengine walipaki na baiskeli zao uwanjani kujionea kilichokuwa kinajiri uwanjani.
Mchezo unaendelea.
Tunafuatilia kinachoendelea....
Wachezaji wa Masekelo fc wakishangilia goli lao la kwanza.

Wakazi wa Shinyanga wakiwa juu ya ukuta wakifuatilia mechi.
Tunafuatilia mechi......
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam(mwandaaji wa Kombe la Meya Shinyanga 2015) akiteta jambo na  Meneja mauzo  SBC Tanzania Limited Pepsi bwana Promod  Nair( wadhamini wa kombe la meya Shinyanga 2015).
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akiteta jambo na msimamizi wa kituo cha Shycom bwana Geofrey Tibakenda,na mratibu wa Kombe la Meya bwana Paul Mganga,ambaye ni mkurugenzi wa Myklay Entertainment(katikati). 

Picha zote na Kadama Malunde.

RAIS JAKAYA KIKWETE, MAKAMU WAKE DKT. BILAL WAWAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MBUNGE WA GEITA, VIWANJA VYA KARIMJEE, DAR.

0
0
  Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 
 Rais Jakaya Kikwete, akiifariji familia ya marehemu Max, wakati wa  shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiifariji familia ya marehemu Max, wakati wa  shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Picha na OMR.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete,  akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 
 Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Makamu wa Dkt. Bilal, wakati walipokuwa katika shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max, zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Bilal, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na baadhi ya Viongozi wakijumuika na waombolezaji katika shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max, leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Juni 27, 2015 kwa ajili ya kushiriki shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max.

WAJUMBE BODI YA FILAMU WATEMBELEA MIUNDOMBINU YA KAMPUNI YA UTENGENEZAJI FILAMU YA PROIN

0
0
 Mjumbe wa Bodi ya Filamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bi.Vicensia Shule(wa kwanza kutoka kushoto) akimwuliza  jambo Mwenyekiti wa makampuni ya Proin Bw,Johnson Lukaza(hayupo pichani) leo jijini Dar es salaam walipotembelea kujionea  miundombinu ya kampuni hiyo.Kutoka kulia ni Makamu mwenyekiti wa  wa Bodi iyo Bw.Sylvester Sengerema na katikati ni  Bw.Bishop Hiluka.
 Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi,Joyce Fissoo akichangia jambo wakati walipotembelea miundombinu ya Filamu ya Makampuni ya Proin.Bi Fissoo ametoa wito kwa makampuni yanayotengeneza Filamu Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ili kuimarisha Tasnia ya Filamu na kusaidia katika kupambana na Changamoto mbalimbali.
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Bw,Johnson Lukaza akimwonyesha Katibu mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi,Joyce Fissoo  moja ya Kazi walizotengeneza na kuingia Sokoni,Pia aliiomba Serikali kusaidia kuweka sheria kali zitakazo zuia wizi wa Filamu nchini.
Wajumbe wa Bodi ya Filamu Tanzania wakifurahia jambo na Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin Bw,Johnson Lukaza(wa tatu kutoka kushoto) walipotembelea miundombinu ya kutengenezea filamu ya Kampuni iyo eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam.Wajumbe hao walijionea jinsi Filamu inavyotengenezwa na pia walitembelea eneo kampuni iyo wanapojenga Studio ya kutengenezea Filamu.

MAMIA YAMUAGA MWANDISHI KAMUKARA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema), Freeman  Mbowe akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama hicho,Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Hamis Kagasheki (katikati)akiwa na viongozi wa Chadema ,Kushoto ni  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema), Freeman  Mbowe na Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama hicho,Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema) ,Freeman  Mbowe akiteta jambo na Mkurugenzi wa Hali Halisi Publisher wachapishaji wa Mawio na Mwanahalisi Online,Sued Kubenea wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Reginard Mengi akipeana mkono Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema) ,Freeman  Mbowe wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Chadema ,Dk Wilbroad Slaa akiteta jambo na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginard Mengi wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya waombolezaji wa kuaga mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam. 
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Reginard Mengi akitoa hishima za mwisho  wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Chadema ,Dk Wilbroad Slaa akitoa hishima za mwisho  wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wafanyakazi wa Kampuni ya Free Media wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima na Sayari wakiwa katika huzuni wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.  
Safari ya kuelekea Kagera kwaajili ya maziko ya  Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.) 

Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii.
MAMIA wamejitokeza katika kuaga mwili wa aliyekuwa Mhariri wa Mawio na Mwanahalisi online  ,Edson Kamukara aliyefariki mwishoni wiki na anatarajiwa kuzikwa  Juni 29 mkoani Kagera.

Wakizungumza wakati wa kuaga kwa aliyekuwa Mhariri wa Mawio na Mwanahalisi online  ,Edson Kamukara  wamesema ni pigo kwa tasnia ya habari kutokana na kuwa na kusimamia kitu anachoamini kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari .

Akizungumza juu ya kifo chake ,Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema kifo cha kamukara ni pigo kutokana na kuwa na msimamo wa bila kuyumbusha na bahasha.

“ Ni bora kuishi kwa kusimama kwa muda mrefu kuliko kuishi kwa kupiga magoti kwa muda mfupi hiyo ikiwa ni kuangalia kutumia kalamu kwa wanyonge bila masilahi ya wanasiasa”amesema Mbow.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP.Reginard Mengi amesema Kamukara alikuwa jasiri katika kufanya mbambo yake kwa kusimamia misingi ya habari na alikuwa hangalii fedha.

“Fedha angekuwa Kamukara anaiangalia basi angekuwa tajiri kwani alikuwa ni mtu kusimamia misingi ya habari kwa ajili ya wanyonge”amesema Mengi.

MWENYEKITI WA CCM RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM jijini Dar es salaam leo.

January Makamba na Safari ya Kusaka wadhamini mkoa wa Manyara, Babati

0
0
Mh January Makamba Jana baada ya Kumaliza Singinda alielekea Mkoa wa Manyara, Babati kuomba udhamini na kuzungumza na Wanachama pamoja na Wakazi wa Babati juu ya dhamila yake ya kuomba nafasi ya kuongoza Tanzania.

Mh January alipokelewa vizuri sana na wakazi Babati na akapewa udhamini wa kutosha. January makamba akizungumza na wanababati alisema kuwa Urais sio kama Ngoma ya Mdundiko unaingia na kuifaita unapofika mbele unajikuta haujui umefikaje na haujui jinsi ya kurudi, kabla ya kuomba nafasi hiyo inabidi ujiulize maswali katika nafsi yako na ujilishe kuwa unaweza, kwanza ujiuliza je unamajawabu mapya ya kutatua changamoto za watanzania?
 Vijana wa Bodaboda Babati waliojitokeza kumpokea Mh January Makamba wakiwa katika msafala kuelekea Ofisi za CCM Babati.

Mh January Makamba akisalimiana na wakazi pamoja na wanachama wa CCM waliojitokeza kumsikiliza Babati.

Shekhe akitoa dua kabla ya zoezi zima la Mh January Makamba kuzungumza na wakazi wa Babati

Askof Pia akitoa neno na kumuombea January Makamba katika safari yake ya kutaka kuiongoza Tanzania.

Mh January Makamba akivishwa Shuka na moja ya Mzee wa Babati kwa mira pamoja na desturi za Babati 










Mh January Makamba akimtambulisha Mke wake kwa wakazi wa Babati.

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM HAJI OMAR KHEIR AZUNGUMZA NA WAANDISHI

0
0
 Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum Haji Omar Kheir alienyoosha mikono akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mradi wa Uwekaji Kamera za kiusalama katika mji wa Zanzibar Ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar.
 Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa ITV Farouk Karim wakwanza kushoto akiuliza maswali katika mkutano wa Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum Haji Omar Kheir  na Waandishi wa Habari akielezea mradi wa Uwekaji Kamera za kiusalama katika mji wa Zanzibar Ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar.
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum Haji Omar Kheir akifafanua jambo katika Mkutano na Waandishi wa Habari akizungumzia mradi wa Uwekaji Kamera za kiusalama katika mji wa Zanzibar Ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar.
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images