Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Bw. Suleiman Kova na Mkuu wa Mkoa huo Mhe saidi Meck Sadiki katika eneo la jengo lililoporomoka mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadcik akifafanua jambo kwa Rais Jakaya Kikwete muda mfupi mara baada ya kufika na kujionea hali halisi ya jengo la Ghorofa lililoporomoka mapema leo asubuhi na kupelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine 19 kujeruhiwa vibaya,kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Es Salaam,Mh Said cMeck Sadick shoto akiwa ameambatana na Rais Jakaya Kikwete muda mfupi mara baada ya kufika na kujionea hali halisi ya jengo la Ghorofa lililoporomoka mapema leo asubuhi na kupelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine 19 kujeruhiwa vibaya,kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge,Mh Mbatia muda mfupi mara baada ya kufika na kujionea hali halisi ya jengo la Ghorofa lililoporomoka mapema leo asubuhi na kupelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine 19 kujeruhiwa vibaya.,aidha shughuli za ukoaji zinaendelea kwani inadaiwa kuna watu wengi zaidi wamefunikwa na jengo hilo.
Rais Kikwete akiondoka eneo la tukio mara baada ya kujionea hali halisi ya tukio zima la kuanguka kwa ghorofa linalodaiwa kuwa na idadi ya ghorofa 15.
Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadick akifafanua jambo kwa Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.Dkt.ASha-Rose Migiro kuhusiana na tukio zima la kuanguka kwa jengo la Ghorofa mapema leo asubuhi,jijini Dar.
Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadick akipewa pole na Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.Dkt.ASha-Rose Migiro kuhusiana na tukio zima la kuanguka kwa jengo la Ghorofa mapema leo asubuhi,jijini Dar.
======= ====== =====
TAARIFA YA UHAKIKA KABISA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE INAELEZA KUWA JENGO MOJA LA GHOROFA 15 AMBALO NI SEHEMU YA MSIKITI WA SHIA ITHNAASHERI KATIKA MTAA WA INDIRA GHANDI KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM LIMEPOROMOKA MUDA MFUPI ULIOPITA
INAELEZWA KUWA MPAKA SASA WATU 19 WAMEOKOLEWA HUKU WAWILI WAKIWA WAMEPOTEZA MAISHA,NA JUHUDI ZA ZIADA ZINAENDELEA KUFANYWA ILI KUOKOA WENGINE WENGI WALIOFUKIWA NA KIFUSI HICHO.
MKUU WA MKOA WA JIJI LA DAR ES SALAAM,MH. SAID MECK SADICK PAMOJA NA VIONGOZI WENGINE MBALIMBALI WAPO ENEO LA TUKIO HIVI SASA AKISHIRIKIANA NA WADAU WENGINE WA VYOMBO MBALI MBALI VYA ULINZI NA USALAMA,KUHAKIKISHA UOKOAJI UNAFANYIKA KWA WAKATI.
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI DKT EMMANUEL NCHIMBI AMEWASILI PUNDE ENEO LA TUKIO NA INATARAJIWA KWAMBA HATA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE ATATEMBELEA SEHEMU HIYO WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA.
CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA JENGO HILO HAKIJAFAHAMIKA MPAKA SASA,KWANI KILA MTU YUPO KWENYE HEKAHEKA ZA UOKOAJI KAMA UONAVYO PICHANI.