Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

Barrick yatoa tuzo kwa wafanyakazi bora

$
0
0
Marco Zolezzi, afisa mwandamizi (Chief Operating Officer) wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold, akitoa zawadi ya tuzo ya mfanyakazi bora kwa mfanyakazi wa kitengo cha uchunguzi cha mgodi wa Bulyanhulu, Gilbert Kalisa, kwenye sherehe zilizofanyika Machi 21, 2013, kwenye mgodi huo.
Igor Gonzales, makamu wa rais mtendaji na afisa mwandamizi (Executive Vice President & Chief Operating Officer) wa kampuni ya Barrick Gold Corp. (kushoto), akitoa zawadi ya tuzo ya mfanyakazi bora kwa Godfrey Nyabuzoki, mfanyakazi wa kitengo cha ulinzi cha mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold kwenye sherehe iliyofanyika Machi 21, 2013. Godfrey na wafanyakazi wengine watano wa kitengo cha ulinzi cha mgodi huo walionesha ujasiri mkubwa kukabiliana na kundi kubwa la wananchi waliovamia mgodi huo mwezi Machi mwaka huu na wafanyakazi hao wakaweza kumuokoa mwenzao aliyeumia. Kulia ni makamu wa rais wa kampuni ya Barrick Gold Corp. anayeshughulikia masuala ya ulinzi, Mark Wall.

Lolence Kasekenya, mfanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (katikati) akiwa na zawadi yake ya mfanyakazi bora kwenye kitengo cha mahusiano ya jamii katika sherehe iliyofanyika kwenye mgodi huo tarehe 22 Machi 2013. Kulia ni Don Ritz, makamu wa rais mwandamizi wa kampuni ya Barrick anayeshughulikia usalama na uongozi na Kevin D'Souza, Mkurugenzi mwandamizi wa ABG upande wa mahusiano ya jamii na mazingira.


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA TUME YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA (COSTECH) KIJITONYAMA

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa maonyesho ya Kisayansi yaliyoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia, leo Machi 27, 2013

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Mkurugenzi wa Sayansi ya Uhai, Dkt. Flora Tibazarwa, wakati Makamu alipofanya ziara ya kutembelea katika maonyesho ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Kijitonyama leo Machi 27, 2013 kujionea maendeleo ya tume hiyo inayozalisha vijana wabunifu wa masuala ya kisayansi. Kushoto kwa Makamu wa Rais ni, Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa namna ya kutumia simu ya mkononi kuunganisha huduma ya mtumiaji simu ili kupata taarifa ya mkulima kutoka kwa Gwaliwa Mashaka wa Kampuni ya Spendid Amos, wakati Makamu alipofanya ziara ya kutembelea katika maonyesho ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Kijitonyama leo Machi 27, 2013 kujionea maendeleo ya tume hiyo inayozalisha vijana wabunifu wa masuala ya kisayansi. Kushoto kwa Makamu wa Rais ni, Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Mkurugenzi wa Sayansi ya Uhai, Dkt. Flora Tibazarwa, wakati Makamu alipofanya ziara ya kutembelea katika maonyesho ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Kijitonyama leo Machi 27, 2013 kujionea maendeleo ya tume hiyo inayozalisha vijana wabunifu wa masuala ya kisayansi. Kushoto kwa Makamu wa Rais ni, Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa.Picha na OMR 

SIRI YA KUUAWA ZITTO'-SIO KWELI -zitto kabwe.

$
0
0


SIRI YA KUUWAWA ZITTO .

Katika gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ‘ SIRI YA KUUAWA ZITTO YAFICHUKA’ na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza’. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa. Napenda kusema yafuatayo:
Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.
Pili, Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. 
Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya Zitto yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo.
Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. 
Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. CHADEMA sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.
Nne, Nawashauri viongozi wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.
--
Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Dar-es-Salaam
Jumatano, Machi 27, 2013.

RAIS KIKWETE AZINDUA TAARIFA YA UTAFITI WA VISAHIRIA VYA UKIMWI NA MALARIA MWAKA 2012

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akinyanyua juu vitabu baada ya  taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda',  Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata ukanda kuzindua rasmi taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Mhe William Lukuvi

 Wadau kutoka sekta mbalimbali wakiangalia matangazo ya kupiga vita UKIMWI na Malaria wakati wa uzinduzi rasmi wa taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipitia baada ya kuzindua rasmi  taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na kushoto kwake ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi, Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa.
 Meza kuu ikimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho akisoma taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa kuzindua rasmi  taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.

 Wadau kutoka sekta mbalimbali wakiangalia matangazo ya kupiga vita UKIMWI na Malaria wakati wa uzinduzi rasmi wa taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU.

Kesi za mimba kwa wanafunzi zapungua Handeni

$
0
0

 Mkuu wa Polisi Wilaya ya Handeni, Zuber Chembera akizungumza
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu
Ofisa Elimu wa Wilaya ya Handeni, Mgaza Muchiwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi

========  ========  ========

Na Thehabari.com, Handeni.

MATUKIO ya kesi za kuwatia mimba/kuwabaka wanafunzi yaliokuwa yameshamiri katika shule mbalimbali za msingi na sekondari wilayani Handeni sasa yameanza kupungua tofauti na ilivyokuwa awali. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Machi 2012 na Machi 2013 matukio ya mimba yanapungua.

Akizungumzia hali hiyo juzi Wilayani Handeni, Ofisa Elimu wa Wilaya, Mgaza Muchiwa alisema matukio ya mimba kwa wanafunzi yanapungua tofauti na miaka ya nyuma ambapo matukio ya utoro wa mimba kwa wanafunzi yalikuwa mengi. “Picha ya mwaka jana niliiona na tulikuwa tukifuatilia kwa karibu matukio ya kesi za mimba kwa wanafunzi…huwezi kufananisha na ilivyo sasa kunamabadiliko kwani matukio haya yamepungua,” alisema Muchiwa akizungumza na mwandishi ofisini kwake Handeni juzi.  
 
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Handeni, Zuber Chembera alithibitisha pia kupungua kwa kesi za mimba zinazofikishwa katika vituo vya Polisi ukilinganisha na hapo nyuma. Akifafanua zaidi kupitia taarifa za Dawati la Jinsia na Watoto Kituo cha Handeni, alisema hadi Novemba 2012 walipokea kesi 66 za matukio hayo lakini tangu hapo hadi Machi mwaka huu kesi hizo zimepungua kwa kiasi kikubwa.
 
Uchunguzi uliofanywa na www.thehabari hivi karibuni katika shule za sekondari Komnyang’anyo, Kileleni na Kivesa zote za wilayani Handeni umeonesha kupungua kwa matukio ya mimba kwa wanafunzi, huku walimu wakidai hali hiyo imechangiwa na kampeni ya ‘Niache Nisome’ iliyoanzishwa na Mkuu wa Wilaya mpya, Muhingo Rweyemamu.

“Kweli kampeni ya ‘Niache Nisome’ iliyoanzishwa na Mkuu wa Wilaya mpya imesaidia sana maana watu wameanza kuogopa kuwarubuni wanafunzi…hata wazazi na wanafunzi nao wanaogopa kuhusishwa katika kesi hizo hii imesaidia kupunguza matukio ya mimba,” alisema Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Komnyang’anyo Nadhiru Kinyama.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Rweyemamu Agosti 2012 alianzisha kampeni ya kupambana na watu waliyokuwa wakiwakatisha masomo wanafunzi kwa kuwatia mimba na kuwaozesha kwa kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wanafunzi na jamii juu ya umuhimu wa elimu wilayani humo. 
*IMEANDALIWA NA WWW.THEHABARI.COM KWA KUSHIRIKIANA NA TAMWA

Masanja Mkandamizaji apania Tamasha la Tumaini Jipya

$
0
0

MCHEKESHAJI maarufu na mwimbaji wa muziki wa Injili nchini, Emmanuel Mgaya, Masanja Mkandamizaji, amesema kuwa amejipanga imara kuhakikisha kuwa anafanya vitu vya aina yake katika onyesho la Tumaini Jipya, linalotarajiwa kufanyika mkoani Morogoro Machi 31, katika Uwanja wa Jamhuri na kushirikisha pia waimbaji mbalimbali nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Masanja alisema kuwa amejiandaa vyema kutangaza neon la Mungu kwa kupitia kipaji chake cha uimbaji wa muziki wa Injili, akiamini kuwa afya yake itakuwa njema na kuimba pamoja na wadau wao katika onyesho hilo la Tumaini Jipya.

Alisema ingawa anatamba sana katika ulingo wa uchekeshaji kwa kuwa na aina ya uzungumzaji na kufurahisha watu wengi, lakini makali yake hayaelezeki katika uimbaji wa muziki wa injili. “Nipo sawa kiafya na naamini Mungu atanibariki kila zuri kwa ajili ya kuimba pamoja kwenye tamasha hilo la Tumaini Jipya nikiwa na waimbaji wengine wenye makali ya aina yake.

“Itakuwa ni siku nzuri kwa siku ya Jumapili ya Machi 31 katika uwanja huo wa Jamhuri, hivyo naamini watu watakuja kwa wingi kulishuhudia neno likipenya masikioni mwao,” alisema Masanja Mkandamizaji.

Mbali na Masanja, wengine watakaofanya onyesho hilo ni pamoja na Martha Mwaipaja, Stara Thomas, Bahati Bukuku, Sifa John, Joseph Nyuki pamoja na vikundi mbalimbali vya kwaya vikitajwa kuwapo kwenye tamasha hilo la Tumaini Jipya litakaloanzia mkoani Morogoro.

MABONDIA ALBINUS NA HERBERT KUPIMA UZITO LEO

$
0
0

Mabondia kinda Albinus Felesianu wa Namibia na Herbert Quartey wa Ghana wanaogombea ubingwa wa dunia katika uzito wa bantam kwa vijana kesho, watapima uzito leo asubuhi katika ofisi za bodi ya mieleka na ngumi ya Namibia zilizoko katika eneo la katikati ya jiji la Windhoek, Namibia. 
Herbert_Quartey
         Herbert Quartey wa Ghana
 
Mpambano huo unategemewa kuwa na kila aina na hamasa kutokana na mabondia wote kuwa wajuzi wa kuzipiga katika maisha yao mpaka sasa. Mshindi wa mkanda huu ndiye atakayekuwa bingwa wa dunia kwa vijana katika uzito wa bantam. 
Wananchi wengi wa Namibia na kutoka katika nchi jirani kama Afrika ya Kusini, Zambia, Botswana na Angola wameshaingia katika jiji la Windhoek na tayari hoteli na nyumba nyingi za kulala wageni tayari zimeshajaa. 
Mpambano huu utafanyika katika hoteli maarufu ya Windhoek Country Club and Casino mahali ambapo ni wiki moja tu iliyopita kuliwako na hekaheka nyingine ya kugombea mkanda wa IBF wa kimataifa kati ya mabondia Immanuel“Prince” Naidjala (Namibia) na Lesley Sekotswe (Botswana) ambao walitoka sare. 
Mpambano huu utasimamiwa na Rais wa IBF Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowiambaye ni wiki iliyopita tu alikuweko tena mahali hapo kusimamia mpambano mwingine wa IBF. Rais Ngowi anaingia nchini Namibia leo akitokea nchini Ghana ambako alikuwa anasimamia mpambano wa ubingwa wa Afrika kati ya Frederick Lawsonna Isaac Sowah wote wa Ghana. 
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

ASASI YA VIJANA WA UMOJA WA MATAIFA TANZANIA KUKUSANYA MAONI YA MIKAKATI BAADA YA 2015

$
0
0
Mwenyekiti wa YUNA Asasi ya vijana ya Umoja wa Mataifa Lwidiko Edward akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati alipozungumzia mpango wa Asasi hiyo kukusanya maoni ya mikakati baada ya mwaka 2015. kulia ni Mwenyekiti wa Baraza kivuli la umoja wa Mataifa TIMUN -2013 Catherine Fidelis.

Kama tunavyofahamu, tunaelekea mwishoni mwa Malengo ya Maendeleo ya Kimilenia, Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa Tanzania imeanza harakati za majadiliano ya mikakati baada ya 2015 kati ya vijana kwenye zaidi ya mikoa sita nchini Tanzania. Mwaka huu, mkutano wa Baraza Kuu Kivuli La Kimataifa la Umoja wa Mataifa litafanyika Dodoma katika ukumbi wa bunge wa Pius Msekwa kuanzia tarehe 2 hadi 6 Aprili 2013 ikiwa na mada isemayo, “Malengo ya Maendeleo ya Kimilenia, kutazama mikakati ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi baada ya 2015”. 

Mkutano huu utashirikisha vijana 160 waliochaguliwa kutoka Tanzania bara na visiwani pamoja na vijana kutoka nchi mbalimbali duniani. Lengo letu kuu ni kuhakikisha kwamba sauti ya vijana inahusishwa katika ajenda za mashauriano ya Malengo ya Maendeleo ya Kimilenia na kuandaa ripoti ambayo itajumuishwa katika taarifa ya taifa itakayopelekwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Mkutano huu wa kimataifa utakuwa majadiliano ya mwisho ya vijana kabla ya kutayarisha taarifa ya mwisho.

Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa Tanzania inayofuraha kuwajulisha kwamba, mwaka huu Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano wa Baraza Kuu Kivuli La Kimataifa la Umoja wa Mataifa. Kwa miaka kumi na tano, Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa imekuwa ikiandaa mkutano wa Baraza Kuu Kivuli la Umoja wa Mataifa, ambapo washiriki hupata fursa ya kufanya kazi kama wanadiplomasia na hushiriki katika vipindi sawa na vile vya mashirika ya kiserikali. Washiriki hufanya utafiti kuhusu nchi fulani, hupata majukumu kama yale ya wanadiplomasia, hufanya utafiti wa masuala ya kimataifa, hujadili, huelimishana, hushauriana na hatimaye kupendekeza masuluhisho ya matatizo mbalimbali ya dunia.

Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa Tanzania inapenda kutumia fursa hii kukaribisha Watanzania wote kuungana mkono na vijana wa Tanzania watakavyokuwa wanatoa michango na mitazamo yao mikubwa na ya kimataifa katika suala la ajenda ya malengo ya maendeleo ya kimilenia baada ya 2015. Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa Tanzania pia inachukua nafasi hii kuwaomba mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali kuwa kipaombele katika kuwasaidia vijana wanaposhiriki katika nafasi hii ya pekee inayokusudia kuwaleta vijana wa Tanzania karibu na Umoja wa Mataifa pamoja na dunia kwa ujumla.

WAKENYA WAFURUKUTA GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE

$
0
0
 Mmoja wa waendesha kipindi cha Guinness Football Challenge Larry Asago.
 Washindi wa kipindi cha pili cha Guinness Football Challenge,Kepha Kimani kutoka Thika Kenya(kushoto) na Francis Ngigi kutoka Nairobi Kenya(kulia) katika picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi hicho Larry Asego and Flavia Tumsiime jana baada ya ushindi. 
=========  ========  ===============
TIMU YA KENYA YAPIGANIA NAFASI YA USHINDI KATIKA MASHINDANO GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™

* TIMU NNE SASA ZAINGIA KWENYE KIPINDI CHA TATU WIKI IJAYO *


Machi  28, 2013, Dar es Salaam; Jana usiku  kupitia televisheni  za ITV na Clouds TV mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ yalituonesha ni kwanini ushirikiano ni muhimu kwa  washiriki kuonyesha ujuzi wao. Francis Ngigi and Kepha Kimani kutoka Kenya walifanikiwa kuingia hatua ya mwisho  na kujipatia fedha za kimarekani  dola 3,000 shukrani kwa vipaji vyao na ushirikiano mzuri.


Francis na Kepha wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia  kitita cha fedha  za kimarekani hadi kufikia dola  250,000. Katika kipindi kijacho cha mashindano haya kinachorushwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne mpya zitaingia uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka mshindi  na kutambulika kama wachezaji na si tu mashabiki,watatakiwa kushinda na kuziwakilisha nchi zao katika mashindano ya Pan-African.


GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya  Endemol.  Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV.  Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku  ambapo  Clouds TV itarusha kipindi hicho  saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .


Tafadhali kunywa kistaarabu - Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.

Matamasha ya Airtel Yatosha kufanyika Nchi Nzima

$
0
0

 kiongozi wa Tip Top connection Bwana Madee  moja ya kikundi kitakachotumbuiza katika Matamasha ya Airtel Yatosha akiongea wakati wa uzinduzi wa Matamasha hayo yaliyofanyika katika ofisi za Airtel morocco, Matamasha haya yatawashirikisha wasanii wengine wakiwemo Fid Q,   Juma Nature,   Ney wa Mitego  na Stamina.Kulia Meneja Mauzo Airtel  Kanda ya Pwani  Raphael Daudi
Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiongea wakati akitangaza wa Airtel wa kufany Matamasha ya Airtel Yatosha katika mikoa mbalimbali ya Tanzania yenye lengo lan kutoa burudani sambamba na kuelimisha Jamii na wateja  wake kuhusu huduma za Airtel ikiwemo kuitambulisha huduma mpya ya Airtel Yatosha. Kulia Meneja Mauzo Airtel  Kanda ya Pwani  Raphael Daudi
===========  ==========  =======
Matamasha ya Airtel Yatosha  kufanyika Nchi Nzima
·         Tamasha la kwanza litafanyika Morogoro siku ya Jumapili na Jumatatu
·         Zaidi ya mikoa 6 kupata burudani kutoka kwa Wasanii wa kizazi kipya nchini
Airtel Tanzania leo imetangaza mpango wake wa kufanya matamasha ya Airtel Yatosha yenye lengo la kutoa burudani na kuwaelimisha jamii na wateja wake  juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Airtel ikiwemo huduma mpya Airtel Yatosha inayomuwezesha mteja kupiga simu kwenda mtandao wowote kwa gharama nafuu zaidi.
Akiongea wakati wa kutambulisha matamasha hayo, meneja uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando alisema “Airtel tumeamua kutoa burudani wakati wa msimu huu wa sikukuu ikiwa ni pamoja na kuitambulisha huduma yetu ya Airtel yatosha kwa watanzania,  tunaamini kwa kupitia matamasha yatakayofanyika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania wateja wetu na watanzania kwa ujumla watapata burudani na kupata nafasi ya kupata elimu juu ya huduma zetu Nyingi
“Safari yetu ya burudani za Airtel yatosha itaanza katika Mkoa wa Morogoro katika siku ya  Jumapili na Jumatatu ya Tarehe 31/3 na 01/04/2013,  Kuanzia Saa Tatu kamili Asubuhi mpaka saa Kumi na Mbili Jioni, pale katika viwanja vya Sabasaba.

Tutakuwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Fid Q,   Juma Nature,   Ney wa Mitego  na    Tip Top Connection. Kiingilio ni BURE , tunapenda kukukualika wewe na washikaji zako wote kuhudhuria katika tamasha hili la kwanza kabisa pale morogoro na utape burudani kabambe. Njoo na Kitambulisho chako ili uunganishwe na ufurahie ofa nyingi toka Airtel” aliongeza Mmbando

Naye kiongozi wa Tip Top connection Bwana Madee  alisema” kama kawaida tumejipanga kuwapa wateja wa Airtel na watanzania burudani ya Ukweli katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, tunaomba watanzania wajitokeze kwa wingi katika matamasha haya ya Airtel Yatosha. Mbali na sisi kutoa burudani itakuwa nafasi pia kwetu kuona vipaji mbalimbali vya mashabiki wetu ambao ndio wasanii nyota wa kesho hivyo tuwapa hamasa ya kujitokeza kwa wingi ili tuweze kuburudika pamoja.

Wasanii watakaoshiriki katika Matamasha maalumu ya Airtel yatosha watatumbuiza kwa vibao vyao mahiri kama vile Fid Q na kibao chake cha Sihitaji Marafiki na  Ney wa Mitego na kibao chake cha Nasema Nao huku Tip Top Connection wakiwakilisha na kibao chao cha Nani kamwaga pombe yangu
Airtel hivi karibuni imezindua huduma ya Airtel Yatosha inayomuwezesha  mtumiaji wa mtandao wa Airtel kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama ya chini kabisa na hivyo kutokuwa na haja tena ya kubadilisha kadi ya simu pindi anapohitaji kuongea na mtu wa mtandao mwingine.  Mteja anajiunga kwenye huduma hii kwa kupiga *149*99# 

Airtel Tanzania YATOSHA

EU Heads of Mission visit to mining operations and local authorities in Northern Tanzania March 26 and 27 2013

$
0
0

EU Heads of Mission visit to Mara, Mwanza and Shyinganga regions March 26-27,2013.
==========  ============= =====
EU Ambassadors visited Northern Tanzania on 26 and 27 March. The Ambassadors of the EU, BelgiumFinlandFranceIreland, the NetherlandsSweden, and the High Commissioner of the UK visited mining operations and local authorities in Kahama (Shinyanga) and North Mara (Mara) and met regional authorities and  stakeholders in Mwanza.

The ambassadors had discussions on the business environment and socio-economic developments in the areas that they visited. In the attached picture from left are Steve Kisakye (Corporate Community Relations Manager of African Barrick Gold), Ambassadors Sinikka Antilla   (Finland), Lennarth Hjelmaker(Sweden), Filiberto Cerinani Sebregondi (EU), Ad Koekkoek (Netherlands), Dianna Melrose (UK), Koen Adam (Belgium), Fionnuala Gilsenan (Ireland) and Marcel Escure (France) together with Deo Mwanyika (Vice President African Barrick Gold).  
 

Easter Greetings From GrooveBack...Join us This Saturday @ Nyumbani Lounge!!

bonanza la vyombo vya habari sasa kufanyika viwanja vya sigara-tcc chang'ombe.

$
0
0
 BONANZA la vyombo mbalimbali vya habari lililopangwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu viwanja vya Leaders Klabu likiandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), sasa litafanyika viwanja vya Sigara (TCC), Chang’ombe pia Dar es Salaam.

Uamuzi wa kuhamisha bonanza hilo umechukuliwa na sekretarieti ya TASWA kutokana na maombi ya waandishi wengi wa michezo kwa vile siku hiyo kuna mechi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika kati ya timu ya soka ya Azam na Barrack Young Controllers ya Liberia  itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam siku hiyo. Azam ni timu pekee ya Tanzania iliyobaki kwenye michuano ya Afrika kwa ngazi ya klabu baada ya Simba na Jamhuri ya Pemba kutolewa katika raundi ya awali.

Tunaamini kwa bonanza kufanyika Sigara itakuwa rahisi kwa wadau wetu kushiriki kwenye bonanza na wale wengine watakaohitaji kwenda uwanjani wafanye hivyo wakitokea Sigara kwa hakuna umbali mrefu na kisha warejee kujumuika na wenzao mpaka mwisho.

Tunawaomba radhi kwa mabadiliko hayo, lakini yakiwa na lengo la kujenga na kuwa pamoja na wenzetu wa Azam kuhakikisha tunashirikiana nao kwa namna mbalimbali siku hiyo.

Bonanza hili linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) likiwa na lengo la kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine pamoja na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari ili kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja.

Bonanza hilo ambalo litahusisha wadau 1,500 kutoka vyombo mbalimbali vya habari litaambatana na michezo mbalimbali itakayohusisha vyombo vyote vitakavyoshiriki na pia kutakuwa na burudani ya muziki kutoka katika moja ya bendi kubwa za muziki wa dansi hapa nchini, ambayo itatangazwa siku zijazo.

Nawasilisha

Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA

camera ya jiachie live ndani ya mabibo-ubungo jijini dar


Breaking News:Mbunge wa Chambani Salim Hemed Khamis,afariki dunia mchana huu.

$
0
0
Pichani ni Baadhi ya Maofisa wa Ofisi Ndogo ya Bunge,wakimsaidia kwa kumbeba Mbunge wa Chambani,Bwa.Salim Hemed Khamis,mara baada ya kuanguka ghafla hapo jana jijini Dar akiwa katika vikao vya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu ya haraka.
=======  ======  ======
Habari  zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chambani-Pemba, Salim Hemed Khamis,ambaye hapo jana alianguka ghafla jijini Dar Es Salaam alipokuwa akihudhuria vikao vya kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili, amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali hiyo ya Taifa ya Muhimbili,aidha chanzo cha habari hizi kimeongeza kuwa taratibu za kuusafirisha mwili wa Marehemu kuelekea Pemba kwa mazishi zinafanyika.Tutazidi kuwafahamisha zaidi kadiri ya habari zitakavyokuwa zikiingia.

Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema Peponi-Amin 


LOWASSA MGENI RASMI JUMAPILI HII KATIKA PASAKA GOSPEL FESTIVAL JIJINI MWANZA

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu ambaye ni Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa akiwa na Meneja wa COSU Entertainment Albert G. Sengo. 

Waziri Mkuu Mstaafu ambaye ni Mbunge wa jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa amethibitisha kuwa mgeni rasmi kwenye tamasha kubwa la muziki wa Injili lijulikanalo kama Pasaka Gospel Festival litakalo fanyika pasaka hii tarehe 31 march 2013, na kujumuisha waimbaji mbalimbali kutoka mikoa tofauti hapa nchini ikiwa ni pamoja na kwaya zaidi ya 15 za jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa COSU Entertainment Phabian Fanuel (kushoto) akifafanua jambo ndani ya studio za Afya Radio kuhusu tamasha la Pasaka Gospel Festival litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza tarehe 31/march 2013 ambapo mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Waziri  Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa.  Kulia ni mtangazaji wa Xtra Vaganza Mr. Credit.

Si wageni hao tu bali atakuwepo pia Meya wa jiji la Mwanza Mh. Stanslaus Mabula na wengine wengi waalikwa, hivyo wakazi wa Mwanza watashuhudia burudani ililoandaliwa kwa ubunifu wa hali ya juu ikishirikisha waimbaji wakubwa kama Enock Jonas (ZUNGUKA), na Neema Mwaipopo (RAHA JIPE MWENYEWE).


engine ni Nesta Sanga (JIANDAENI), Danni Safari, John Shahban, Jeska Julius, Isaya Msangi (SHETANI IMEKULA KWAKO), Danny Sanga kutoka Iringa, Tumaini Mbembela  kutoka Mbeya na mkoa wa Arusha utawakilishwa na Neema Munisi.


Kwaya za mkoa wa Mwanza ni nyingi za kutosha Anglican Vijana kwaya, EAGT City Centre kiufupi kwa zote zitaweka kambi kwenye shughuli yetu ya Uzinduzi Pasaka hii.


Jumatatu ya pasaka tutakuwa Geita uwanja wa CCM Katoro

Kiingilio kwa maeneo yote kitakuwa ni shilingi. 2000/= tu

Hivyo tunawakaribisha wote kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa COSU Entertainment Phabian Fanuel amesema kuwa hii imekuwa ni bahati ya kipekee kuweza kuweza kufikia hatua hii na ugeni huo mzito kwani maandalizi yote yamekwisha kamilika kwa asilimia 97 jambo la kumshukuru Mungu.

Kulia ni mtangazaji wa Xtra Vaganza Mr. Credit na kushoto anaonekana Dj. Sande.
Njooni tuzunguke kwani wema wa Mungu umetuzunguka. 


Ili ufanikiwe tizama na sikiliza wimbo huu 'UFANIKIWE'

TAASISI YA CATHERINE FOUNDATION DEVELOPMENT YATOA MISAADA YA KIJAMII KWA WAGONJWA NA WATOTO YATIMA ARUSHA LEO

$
0
0
Taasisi ya Maendeleo isiyo ya kiserikali ya Catherine Foundation ya jijini Arusha leo imetoa misaada mbalimbali ya vyakula kwa wagonjwa Hospitali ya Mt Meru na vituo viwili vya Yatima vya Faraja na Lohada Moshono vyopte vya jijini humo.

Catherine Foundation Develeppent inaongozwa na Mbunge wa Viti Maalum UVCCM Arusha, Catherine Magigie.

Misaada hiyo ya vyakula na sabuni pamoja na kuwatembelea wagonjwa kufanyika ikiwa ni sehemu ya kuwapa faraja wagonjwa na yatima hao waki huu wa kuelekea siku kuu ya Pasaka ili nawao wajisikie ni miongoni mwa jamii.
Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akimkabidhi  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Frida Mokit msaada wa mablanketi ya kujifunikia wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo.
Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akiwajulia hali wagonjwa waliolazwa Hospitali ya Mt. Meru ya jijini Arusha na kuwapa zawadi mbalimbali.

TAARIFA KWA UMMA

$
0
0


WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI UTALII NA MICHEZO ZANZIBAR SAID ALI MBAROUK AMEFANYA UTEUZI KWA KUMTEUA MRAJIS WA MICHEZO NA MJUMBE MMOJA WA BARAZA LA MICHEZO ZANZIBAR.

KATIKA UTEUZI HUO WAZIRI MBAROUK AMEMTEUA SAID MALIK JUMA KUWA MRAJIS WA VYAMA VYA MICHEZO AMBAYE ATASHIKA NAFASI HIYO KUANZIA LEO.

SAID MALIK JUMA AMBAYE NI MWANASHERIA KATIKA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI UTALII NA MICHEZO NI MWANATAALUMA WA SHERIA AKIWA NA SHAHADA MBILI ZA SHERIA.

AIDHA WAZIRI MBAROUK AMEMTEUA ULEDI JUMA WADI KUWA MJUMBE WA BARAZA LA MICHEZO ZANZIBAR.

ULEDI JUMA NI MKURUGENZI WA IDARA YA ELIMU YA MAANDALIZI NA MSINGI ANASHIKA NAFASI ILIYOACHWA WAZI NA MUSSA ABDULRABBI KUTOKA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI AMBAYE ALIJIUZULU HIVI KARIBUNI.

 IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR  

CRDB CHINA DESK YAZINDULIWA

$
0
0

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu akizungumza katika hafla hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa CRDB China Desk
 Balozi wa China hapa nchini, Lü Youqing akizungumza wakati wa uzinduzi wa CRDB Chine Desk.
 Baadhi ya wageni waalikwa
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei (kushoto) akiongozana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu na  Balozi wa China hapa nchini, Lü Youqing wakati wa hafla ya uzinduzi wa CRDB China Desk..

DAR ES SALAAM, Tanzania


MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei, amewataka wajasiriamali na wawekezaji wanaofanya biashara zao kati ya Tanzania na China, kuchangamkia fursa pana ya ukuzaji mitaji yao na pato kwa kutumia huduma mpya ya CRDB China Desk.


Dk Kimei aliyasema hayo jana wakati wa hafla ya uzinduzi wa China Desk, inayotolewa na CRDB, itakayo wahudumia wafanyabiashara, wajasiriamali na wawekezaji wanaofanyakazi zao baina ya mataifa hayo rafiki.

“China Desk, ni huduma yenye fursa inayoweza sio tu kusaidia kukuza mitaji na kutanua wigo wa maendeleo, bali kudumisha ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo baina ya China na Tanzania, ambao uliasisiwa karibia nusu karne iliyopita,” alisema Dk Kimei katika hafla hiyo.


Aidha, akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, aliiomba CRDB kuboresha utoaji wa mikopo ya riba nafuu kwa wajasiriamali wadogo na wa kati, ili kuharakisha ukuaji wa pato la Mtanzania na Taifa kwa ujumla.


Dk Nagu alibainisha kuwa, taasisi za kipesa nchini zina mchango mkubwa kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati kukuza pato lao, kama zitakuwa tayari kuwapa mikopo yenye masharti nafuu na riba ndogo, ili kusaidia harakati zao za kujikwamua na kukuza uchumi wa taifa.


“CRDB mnastahili pongezi kwa huduma hii, inayokuja wakati ambao Tanzania kama Taifa, lilimpokea rais mpya wa China, Xi Jinping katika ziara ya kikazi. Taasisi nyingine za kifedha zitambue umuhimu wa ushirikiano baina ya mataifa haya na kubuni huduma kama hizi,” alisema Dk Nagu.


Aliongeza kwamba, kwa kuwa harakati za kumkomboa Mtanzania zimeshika kasi, huku China ikijitoa kadri iwezavyo kuisaidia Tanzania, kuna haja huduma kama hizo za China Desk zikaambatana na mikakati endelevu ya kimandeleo, na taasisi nyingine nazo zinastahili kuiga.


Kwa upande wake, Balozi wa China hapa nchini, Lü Youqing, aliipongeza CRDB kwa kufuata nyayo za waasisi wa China na Tanzania, kiasi cha kubuni na kuzindua China Desk – dawati litakalowanufaisha wajasiriamali na wafanyabiara wa kila upande.


“Huduma hii ni harakati chanya inayofuata nyayo za waasisi wa ushirikiano baina ya China, Rais Mao Tse Tung na Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere. Vizazi na vizazi vitabaki kujivunia na kila mmoja atajisikia yu nyumbani anapokuwa katika moja ya nchi hizo,” alisisitiza Youqing. 
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live


Latest Images