Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano na Masoko,Consitantine Magavila akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.kutoka kushoto ni msanii wa Bongo Fleva George Mdemu (Gnako),Afisa mipango wa kampuni ya Open Society Intiative for Eastern Africa(OSIEA),Adam Antony,Afisa Elimu NEC,Rose Malo pamoja na Snura Mushi(Snura).
Afisa Elimu wa NEC,Rose Malo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na vijana walioona umhimu wa kupiga kura na kuhamasisha vijana wengine kwa njia ya nyimbo,kutokana na mwaka huu kuwa ni mwaka wa Uchaguzi mkuu hapa nchini akizungumza katika ukumbi wa Idara ya habari maelezo jijini Dar es Salaam leo. kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano na Masoko,Consitantine Magavila na Afisa mipango wa kampuni ya Open Society Intiative for Eastern Africa(OSIEA),Adam Antony.
kutoka kushoto ni msanii wa Bongo Fleva George Mdemu (Gnako), Snura Mushi (Snura),Kala Masanja (Kala Jeremiah) pamoja na Boniventure Kabogo(Stamina) wakiimba kipande cha wimbo ambao utakuwa ukielimisha jamii kuhusiana na umhimu wa upigaji kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika Mkutano wa wanaohamasisha vijana kupiga kura katika uchaguzi mkuu mwaka huu.(Picha na Avila kakingo.)
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
VIJANA wamekuwa na changamoto ya kutoshiriki katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura na kushindwa kupata haki yake msingi ya kupiga kura katika chaguzi mbalimbali zinazofanyika nchini.
Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo Kampuni ya Mawasiliano na Masoko kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Shirika la Open Society International pamoja na wasanii mbalimbali wa muziki wameanzisha kampeni maalum kwa ajili ya kuhamasisha vijana kujiandikisha katika daftari la wapiga kura katika mikoa ambayo daftari hilo halijapita.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Idara ya habari Maelezo,Mmoja wa Wakurugenzi wa Mawasiliano na Masoko,Consitantine Magavila amesema kuwa kampeni hiyo wasanii mbalimbali wametengeneza nyimbo moja inayoenda kwa jina la Kuradili kwa ajili ya kuhamasisha vijana kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura na hatimaye kupiga kura.
Amesema wasanii walitunga nyimbo hiyo ni Gnako,Snura,Izo Biznez,Kala Jeremiah pamoja na Stamina ambao watapita kutumbwiza katika mikoa ya Dar es Salaam,Morogoro,Mwanza, pamoja na Shinyanga na hakuna kiingilio katika matamasha hayo yaliyolenga kufikia watu milioni nne wakiwemo vijana.
“Vijana wanaweza kuleta mabadiliko endapo watajitokeza katika kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura na hatimaye kupiga kura lakini tumeona fursa yetu ni kuwahamasisha waweze kufanya hivyo”amesema Magavila.
Nae Afisa Elimu NEC,Rose Malo,amesema kujitokeza na kampuni hiyo itasaidia vijana kuhaamasika kujiandikisha katika daftari la mpiga kura kutokana na ujumbe kutoka kwa vijana wenzao.