Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 550 | 551 | (Page 552) | 553 | 554 | .... | 1898 | newer

  0 0


  0 0

  IMG_0820

  Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (katikati) wakiwasili kwenye ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kabla ya ziara ya kuelekea katika kijiji cha Chasimba kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF katika wilaya ya Bagamoyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

  Na Modewjiblog team, Bagamoyo.

  SERIKALI ya Hispania imetoa shilingi bilioni 3.1 kusaidia miradi ya maendeleo ya jamii nchini ambayo mingine inatekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, TASAF.

  Fedha hizo zimetolewa kupitia mfuko wa maendeleo endelevu (SDGF) zilizotolewa kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya shughuli zake hapa nchini. Mashirika hayo ni Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ,Shirika la Umoja wa Mataifa la watoto (UNICEF) , Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu (UNFPA), na Shirika la Kazi Duniani( ILO).

  Hayo yamesemwa katika ziara ya Balozi wa Hispania nchini, Luis Cuesta Civis na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika kijiji cha Chasimba kilichopo wilayani Bagamoyo, Pwani jana. 

  Ziara yao ilikuwa ya kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF katika wilaya ya Bagamoyo. Bagamoyo ni miongoni mwa wilaya nane zilianza kupokea fedha za TASAF na kuonekana kuleta mabadiliko makubwa katika jamii. Hata hivyo moja ya shughuli wanazofanya wakazi wa Chasimba ni kilimo wakiwa na pato la sh 350,000 kwa mwaka. Huduma za jamii zinazopatikana katika vijiji hivyo ni pamoja na shule ya msingi, barabara inayopita kijiji ni hapo na zahanati.

  Wakati wa utekelezaji wa awamu ya pili ya TASAF jamii ya Chasimba ilijenga madarasa matatu na ofisi ya walimu. Miradi hiyo ilizinduliwa mwaka 2007 na kukamilika mwaka 2008. Katika miradi hiyo TASAF ilichangia 30,415,471.

  Aidha kijiji cha Chasimba ni miongoni mwa vijiji 17 ambavyo vinatekeleza mradi wa CB-CCT toka mwaka 2008/2009. Katika kipindi hicho wamepata ruzuku ya jumla ya sh 28,325,400.
  Pia kijiji hicho kina kaya 197 zinazonufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III (PSSN) ambapo tayari wamepewa ruzuku ya shilingi 43,227,190 katika mikupuo 9.
  Akizungumza kijijini hapo Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliishukuru serikali ya Tanzania na Hispania kwa kufanikisha shughuli hiyo nzito ya kusaidia jamii kukabiliana na umaskini.
  IMG_0803
  Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez wakisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo.
  “ Tunashukuru serikali ya Tanzania na Hispania kwa kushirikiana kusaidia wananchi wa Tanzania kukabiliana na umaskini. Kwa kufanyakazi na watu wa hali ya chini kabisa miradi hii imewezesha familia kupeleka shule watoto wao, kushiriki katika mipango ya uwekaji wa akiba na kuongeza kipato. Jukumu letu la pamoja ni kuondoa umaskini Tanzania” alisema Alvaro.
  Naye Balozi wa Hispania Luis amesema kwamba serikali ya Hispania inaamini katika kusaidia kupambana na umaskini kwa kusaidia jamii kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

  Alisema wataendelea kufanya hivyo kupitia Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo yanafanyakazi kwa kushirikiana na serikali za mikoa na mitaa ambazo ndizo ziliopo karibu na wananchi husika. Alisema kwamba wanaamini mradi wa kunusuru kaya maskini unafanya wajibu wake kwa kuwafikia wananchi maskini sana.

  Alisema mradi huo ni moja ya miradi inayoonesha umuhimu wa kufanyakazi pamoja kati ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa na nchi wahisani.
  Kijiji cha Chasimba pia kinafanya kazi za ujenzi mbalimbali kuanzia Machi 23, mwaka jana. Kazi hizo ni pamoja na ujenzi wa barabara ya kilomita 1.1 ya Chasimba-Kiegea. Aidha kumekuwepo na mafanikio makubwa tangu kuanza kwa mradi wa PSSN kijijini hapo.

  Alisema kumekuwepo na ongezeko la wanafunzi wanaoandikishwa na kuhudhuria shule, aidha madarasa matatu yamejengwa na ofisi ya mwalimu. Akizungumzia mafanikio Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga alisema kuna mabadiliko makubwa katika maisha ya watu kutokana na utekelezaji wa miradi hiyo katika kijiji.

  Aidha wananchi wa Chasimba wamepata ushawishi mkubwa wa kushiriki katika miradi ya maendeleo ndio sababu ya mafanikio yanayoonekana.
  Kwa mujibu wa taarifa zilizopo mradi wa kunusuru kaya maskini umesaidia watoto kwenda shuleni wakiwa wametimiziwa mahitaji yao yote.
  Aidha mradi huo umeweza kufanikiwa kufanya watu wapendekwenda kiliniki na kuangalia afya za mama na watoto.
  Aidha familia zilizopewa fedha sasa wamebadilisha namna ya mfumo wa kupata lishe na kuwa na uhakika na lishe.
  Aidha ujira kutokana na kazi unaotarajiwa kutolewa ni jumla ya dola za Marekani 15,991 wakati gharama za vifaa na ufundi ni dola za Marekani 5,328.
  Jumla ya kaya 197 zitashiriki katika miradi ya ujenzi kwa kipindi cha miezi minne na utaendelea kwa miaka miwili katika kipindi hicho hicho.
  IMG_0824
  Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kulia), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mahali (katikati) wakielekea kwenye ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kupokea taarifa ya mradi wa TASAF katika wilaya ya Bagamoyo.
  IMG_0838
  Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mahali (wa pili kushoto) akifafanua jambo kwenye mkutano wa kupokea taarifa ya maendeleo ya miradi ya TASAF katika wilaya ya Bagamoyo kwa wadau wa maendeleo waliotembelea wilaya hiyo kukagua miradi inayofadhiliwa na Tasaf. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez sambamba na Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (wa pili kulia) na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa wilaya ya Bagamoyo, Hilda Gadi.
  IMG_0854
  Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga akizungumza kwenye mkutano mfupi wa kupokea taarifa ya miradi inayofadhiliwa na TASAF wilayani Bagamoyo. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Bi. Hilda Gadi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mahali (katikati), Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (wa pili kulia) pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.
  IMG_0873
  Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Bi. Hilda Gadi akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi wa TASAF wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika wilaya ya Bagamoyo mbele ya wadau wa maendeleo.
  IMG_0894
  Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis akizungumzia ufadhili wa serikali yake kusaidia miradi ya maendeleo ya jamii nchini ambayo mingine inatekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, TASAF.
  IMG_0924
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza katika mkutano huo ambapo aliishukuru serikali ya Tanzania na Hispania kwa kufanikisha shughuli ya kusaidia jamii kukabiliana na umaskini ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Malengo ya Millenia (MDG's).
  IMG_0855
  Baadhi ya wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wa TASAF wakishiriki kwenye mkutano huo.
  IMG_0861
  IMG_0860
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo.
  IMG_0948
  Picha ya pamoja mara baada ya mkutano.
  IMG_0954
  Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (katikati) akijadiliana jambo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mahali (kushoto).
  IMG_0967
  Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kulia) akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Bi. Hilda Gadi. Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mahali.

  0 0


   Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amina Salum Ali.
   viti vikiwa tupu baada ya kuahirishwa kwa mdahalo huo.
   Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amina Salum Ali (kulia), akizungumza na wadau mbalimbali waliofika kwa lengo la kuwasikiliza wagombea hao ambao hawakufika.
  Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amina Salum Ali, akitoka ukumbini katika Hoteli ya Hyatt Recency Kilimanjaro baada ya kuahirishwa kwa Mdahalo wa waliotangaza nia ya kugombea urais kupitia chama hicho kushindwa kuhudhuria Dar es Salaam juzi. Wagombea hao walioshindwa kuhudhuria mdahalo huo ni Mwigulu Nchemba, Samuel Sitta, January Makamba, Lazaro Nyalandu  na Frederick Sumaye.

  Dotto Mwaibale
  WATANGAZA nia watano wa kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliokuwa wahudhurie mdahalo ulioandaliwa na Umoja wa Maofisa Watendaji Wakuu (CEOrt), walishindwa kuhudhuria mdahalo huo bila ya kuwa na sababu za msingi ambapo mgombea pekee Amina Salum Ali ndiye aliyejitokeza.

  Wagombea walioshindwa kuhudhuria mdahalo huo wametajwa kuwa ni Samuel Sitta, Mwigulu Nchemba, Lazaro Nyalandu, Frederick Sumaye na January Makamba.

  Mdahalo huo ulikuwa uonyeshwe moja moja na Kituo cha Televisheni cha Azam na Clouds TV ulihudhuriwa na watu mbalimbali na maandalizi yake yalikuwa yamekamilika.

  Kuharishwa kwa mdahalo huo kuliwasikitisha wadau mbalimbali waliokuwa wamefika kushiriki wakisema kwamba wagombea hao hawakupaswa kufanya hivyo ukizingatia kuwa wote ni kutoka chama kimoja cha CCM.

  Akizungumzia kuahirisha mdahalo huo, Mwenyekiti wa Mdahalo huo Ali Mafuruki hawakupata maelezo yoyote kutoka kwa wagombea ya kuto hudhuria.

  Mtangaza nia pekee aliyefika kwenye mdahalo huo uliokuwa ufanyike ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro, Amina Salum Ali alisema amesitika sana kwa wenzake kwa kutofika.

  Alisema midahalo kama hiyo ni ya muhimu na ina afya hasa katika wakati huu wa mchakato wa uchaguzi wa viongozi ambapo wagembea hawapaswa kutukanana bali kuelewana na kila mmoja wao kuzungumza kile anacho kiamini kwa maslahi ya taifa.

  "Midahalo kama hii ilikuwa ni  fursa kwa watangania kwani wananchi walitaka kujua tofauti kati ya mgombea huyu au yule lakini ndio hivyo wenzangu hawajakuja najisikia vibaya" alisema Ali.

  Alisema anashukuru kupata uwanja wa kujiunga na wenzake hasa vijana katika kinyang'anyiro hicho ingawa amewatangulia kufanya kazi na kuyafahamu mambo mengi.

  Ali alisema kwamba katika suala la kuinua uchumi haiwezekani kufanya jambo hilo kwa haraka ni vizuri kwanza  vitu vikaweka sawa na kuwe na sera za kuweza kushawishi kwani hivi sasa kila jambo linakwenda kwa utaratibu.

  Alisema yeye anafahamika sana na amefanyakazi Zanzibar na nje ya nchi na anauzoefu mkubwa ndio maana akaona anaweza kuongoza taifa iwapo jina lake litapitishwa kugombea nafasi hiyo.

  Alisema kiongozi anayehitajika ni yule ambaye anaweza kusimamia kwa moyo wa dhati masuala ya gesi na uwekezaji katika maeneo mbalimbali ambapo yeye anaweza kutokana na uzoefu wake kwani anajua sheria na sera.

  Watangania hao walioshindwa kuhudhuria mdahali huo baadhi yao walisema wameshindwa kufika baada ya kukosa nafasi kutokana na kuwa katika mchakato wa kwenda mikoani kutafuta wadhamini wa kuwajazia fomu za kugombea nafasi hiyo na wakaahidi wapo tayari kuhudhuria mdahalo utakaoandaliwa wakati mwingine. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

  0 0

  Mbunge wa viti maalumu Lucy Owenya (Chadema)akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kibosho Kilima kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali katika mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015. 
  Mratibu a mashindano hayo Charles Mchau  akisalimiana na wachezaji.
  Mgeni rasmi katika fainali hiz katibu wa Chadema kanda ya kaskazini Aman Golugwa akisalimiana na wachezaji.
  Mbunge Lucy Oweya akiwa ameambatana na mgeni rasmi Aman Golugwa mara baada a kukagua timu hizo.
  Mgeni rasmi katika mashindano ya Lucy Owenya Cup yaliyoshirikisha timu za jimbo la Moshi vijijini,Aman Glogwa akizungumza na timu zilizoingia fainali za Kibosho Kindi na Kibosho Kilima.
  Manahodha wa timu hizo mbili wakipeana mikono kusalimiana.
  Timu ya Kibosho Kindi wakiomba Dua.
  Timu ya Kibosho Kilima wakiomba Dua.
  Waamuzi wakiwa katika picha ya pamoja na manahodha wa timu hizo mbili.
  Timu ya Kibosho Kindi  katika picha ya pamoja.
  Timu ya Kibosho Kilima katika picha ya pamoja.
  Baadhi ya mashabiki waliohudhulia mchezo huo.
  Mchezo ukiendelea.
  Moja ya timu iliyoshiriki mashindano hayo Sangiti Sekondari wakifuatilia mchezo wa fainali.
  Meza kuu wakifurahi mara baada ya mwamuzi kupuliza kipyenga cha mwisho ambapo timu ya Kibosho Kindi iliibuka na ushindi wa bao 3 kwa 1.
  Mashabiki wa timu ya soka ya Kibosho Kindi wakifurahia ushindi huo.
  Mashabiki wa timu ya soka ya Kibosho Kindi wakichukua taswira na muandaaji wa mashindano hayo.
  Baadhi ya timu zilizoshiriki mashindano hayo.
  Mdhamini wa mashindano hayo Lucy Owenya akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mashindabo hayo na bingwa kupatikana.
  Mgeni rasmi katika mashindano hayo Katibu wa Chadema Kanda ,akizungumza wakati wa kufunga rasmi mashindano hayo na kukabidhi zawadi kwa washindi.
  Mgeni rasmi ,Golugwa akikabidhi cheti kwa Mbunge Lucy Owenya kama ishara ya chama hicho kuthamini mchango wake katika kukuza vipaji vya vijana kupitia michezo.
  Mgeni rasmi Aman Golugwa akikabidhi zawadi ya kikombe kwa nahodha wa timu ya Kibosho Kindi mara baada ya kufanikiwa kutwaa kikombe hicho kwa mara ya kwanza katika mashindabo ya Lucy Oweya Cup. 2015.
  Mashabiki wa timu ya Kiboshi Kindi wakifurahia na kikombe chao.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akilakiwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vijana, waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa mjini Songea jana, baada ya kuwasili mkoani Ruvuma kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000. Picha zote na John Badi
    Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akisoma moja ya mabango yenye ujumbe mbalimbali yaliyobebwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vijana, waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa mjini Songea jana, baada ya kuwasili mkoani Ruvuma kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati) akilakiwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliofika kumpokea nje ya Ofisi ya CCM Mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea jana, baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000.
    Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiwapungua mkono wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi, waliofurika nje ya Ofisi ya CCM Mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea jana, baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000.
   Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Odo Mwisho akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe, fomu zilizotiwa saini na wanachama wa CCM mkoani humo, waliofika kwenye Ofisi hizo jana, kwa ajili ya kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe, akizihakiki fomu zilizotiwa saini na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, kwa ajili ya kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo, Odo Mwisho (wa pili kulia),  katika Ofisi za chama hicho mjini Songea jana, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Ruvuma, waliofika kwenye Ofisi ya CCM zilizopo mjini Songea jana, kwa ajili ya kutia saini fomu za  kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (watatu kushoto), akipongezwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Ruvuma, waliofika kwenye Ofisi ya CCM zilizopo mjini Songea jana, kwa ajili ya kutia saini fomu za  kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000. Wa pili (kushoto) ni Mkewe, Mama Dorcas Membe
  Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Ruvuma, wakimwombea dua maalum Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto), kwa ajili ya kumtakia kheri katika safari yake ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kupata wadhamini kutoka mkoa huo jana. Wa pili (kushoto) ni Mkewe, Mama Dorcas Membe.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na viongozi wa dini ya kiislam wa Mtwara mjini jana jioni, wakati wa dua maalum iliyoandaliwa na viongozi hao kwa ajili ya kumtakia kheri katika safari yake ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Aliyekaa (kushoto) ni Sheikh wa Mkoa wa Mtwara, Dk. Nurdin Abdallah Mangochi. Picha zote na John Badi.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (mwenye shati la kijani), akiagana na baadhi ya viongozi wa dini ya kiislam wa Mtwara mjini jana jioni, baada ya dua maalum iliyoandaliwa na viongozi hao kwa ajili ya kumtakia kheri katika safari yake ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  0 0

   Makamu wa rais Mohammed Ghalib Bilal akikaribishwa na Katibu Mkuu wa wizara ya uchukuzi Dk. Shaban Mwinjaka wakati alipotembelea banda  TCAA wakati wa maadhimisho ya wiki ya mazingira yaliyofanyika hivi karibuni mkoani Tanga.
   Baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)wakipanda mti ofsini kwao  Banana Ukonga jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira  iliyofanyika hivi karibuni  kitaifa mkoani Tanga.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dk. Shaban Mwinjaka akiwa kwenye picha ya pamojana wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) wakati alipotembelea banda la hilo wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Mazingira yaliyofanyika hivi karibuni Mkoani Tanga.
   Wanafunizi wa shule  za msingi mbalimbali mkoani Tanga waliotembelea kwenye banda la Mamlka ya Usafiri wa Anga Tanzania ,(TCAA) wakigawiwa vipeperushi vyenyenujumbe mbalimbali na Mkurugenzi mazingira wizara ya Uchukuzi Tumpe Mwaijunde  wakati maadhimisho ya wiki ya Mazingira mkoani Tanga.
  Wanafunzi wa shule za msingi mkoani Tanga wakiwa kwenye banda la TCAA wakijionea mambo mbalimbali yaliyokuwa yakionyweshwa hapo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira yaliyofanyika mkoani hapo.

  0 0

  KAMPUNI  ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy Tanzania Ltd imekabidhi msaada wa jengo lenye nyumba mbili za wahudumu wa afya wa Zahanati ya Nangurukuru ikiwa ni jitihada za kuisaidia Serikali kupunguza vifo vya akinamama na watoto katika eneo la Nangurukulu na vijiji vya jirani.

  Akikabidhi majengo hayo jana kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Meneja Uwajibikaji kwa Jamii wa Kampuni ya Pan African Energy Tanzania Ltd, Andrew Kashangaki alisema lengo kubwa la misaada wanayotoa ni kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika wilaya ambazo wanafanyia kazi zao.

  Alisema kuwa madhumuni ya msaada wa ujenzi wa nyumba hizo mbili waliozijenga kwenye Zahanati ya Nangurukuru ni kuimarisha mahusiano mazuri na jamii inayowazunguka maeneo ambayo wanafanyia shughuli zao.

  Aidha Kashangaki alisema mradi huo wa ujenzi wa nyumba za waganga umegharimu zaidi ya milioni 458 za fedha za Kitanzania na zimejengwa kisasa ambapo zinauwezo wa kubeba familia nne za watumishi wa Zahanati ya Nangurukuru hali ambayo itasaidia.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Abdulah H. Ulega akipokea nyumba hizo alisema msaada huo utapunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya akinamama wajawazito na watoto eneo hilo ambapo awali vilikuwa vinatokana na huduma za afya kuwa mbali na makazi ya akinamama hao.

  "...Ni kweli kwamba bado tunatatizo kubwa la vifo vya akinamama na watoto eneo letu na vifo hivi vinachangiwa na tatizo la kukosekana kwa huduma za afya karibu...kama inavyoeleza sera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kusogeza huduma za kijamii karibu na wananchi.

  Aliongeza kuwa Wilaya ya Kilwa kwa sasa inajitahidi kuhakikisha suala hilo lakuendelea na ujenzi wa zahanati zaidi unafanya vizuri. "...Na moja ya mafanikio yetu ni ujenzi wa Zahanati ya Nangurukuru na nyingine tano tunazijenga, awali ilikuwa kati ya Vijiji 90 vya Wilaya yetu vilivyokuwa na huduma za afya vilikuwa 43, lakini ndani ya miaka mitatu tumejitahidi kuunga mkono juhudi za wanakijiji walipoanza mchakato wa ujenzi wa zahanati kwenye vijiji vyao," alisema Mkuu wa Wilaya.

  Kwa upande wao baadhi ya wakazi waliohojiwa katika hafla hiyo ya makabidhiano walisema ujenzi wa nyumba ya watumishi wa zahanati ya Nangurukuru utawasaidia sana kihuduma za afya eneo hilo kwani awali wananchi walikuwa wakilala barabarani wakati mwingine usiku wakisafiri kutafuta huduma za afya.

  Mwenyekiti wa Kitongoji cha Dodomezi, Mwanahawa Hamis alisema uzinduzi wa jengo la zahanati hiyo utawasaidia hasa akinamama ambao walikuwa wanapoteza maisha njiani kutokana na kutembea umbali kufuatilia huduma za afya.

  Naye Mwanawetu Mshamu Mkazi wa Kitongoji cha Dodomezi, mbali na kukabidhiwa jengo la makazi ya watumishi wa afya aliiomba Serikali isaidie kuboresha barabara zinazotumiwa na wakazi wa eneo hilo ili kuondoa changamoto ya usafiri kwa wagonjwa wanaokuja kuhudumiwa.

  Kampuni ya Pan African Energy Ltd kwa mwaka 2015 inatarajia kutumia takribani shilingi bilioni 550 kwa ajili ya kusaidia maendeleo na misaada ya huduma za kijamii katika maeneo ambayo wanaendesha shughuli zao.

  Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Abdallah Ulega akiishukuru Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy kwa kuamua kuleta misaada kwa jamii ambayo ni ya msingi hasa Hospitali pamoja na jengo la Wauguzi lililokabidhiwa katika kijiji cha Nangurukuru wilaya Kilwa
  Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za Jamii wa Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy, Andrew Kashangaki (mwenye fulana nyekundu) akimkabidhi mfano wa funguo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Abdallah Ulega(wa pili kushoto) la jengo la Wauguzi la Zahanati ya Nangurukuru wilayani Kilwa. Wa kanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Peter Malekela, wapili kushoto ni Mbunge wa Kilwa Kusini, Suleman Ally Bungara 'Bwege' na wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilwa Mzee Ally Mtopa.
  Meneja Uwajibikaji na Huduma za Jamii wa Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy, Andrew Kashangaki akizungumza jambo wakati wa kukabidhi jengo la Wauguzi katika kituo cha Afya cha Nangurukuru wilayani Kilwa
  Mwenyekiti wa Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy nchini Tanzania, Patrick Rutabanzibwa akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi(hawapo pichani) kwa kuamua kutoa misaada mbalimbali ya jamii , mradi huu wa nyumba za Wauguzi zilizojengwa na nguvu ya wananchi pamoja na msaana mkubwa wa Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy katika maendeleo ya jamii.
   Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilwa Mzee Ally Mtopa akizungumza jambo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy wakifuatilia jambo wakati wa kukabidhi jengo la Wauguzi
  Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy nchini Tanzania, Patrick Rutabanzibwa (wa tatu kutoka kulia) akimkabidhi funguo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Abdallah Ulega hii ni kuonesha ishara ya kukabidhiwa kwa jengo hilo la wauguzi
  Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Abdallah Ulega akipata maelezo baada ya kukabidhiwa nyumba ya Wauguzi iliyojengwa na Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy nchini Tanzania
  Kikundi cha nyimbo za asili kikitoa burudani
  Wakazi wa kijiji cha Nangurukuru nao hawakuwa nyuma wakati wa kukabidhiwa jengo la wauguzi
  Waandishi wa habari wakiwa kazini.

  0 0
 • 06/10/15--05:09: NIAMBIE LIVE SHOW EP 4.
 • Omby Nyongole, Henry Kente na Salma Moshi
  Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE
  Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu kwenye mitandao ya kijamii. Pia kupata Tip ya siku / wiki kusaidia kuboresha maisha yako.
  Ni Niambie Live....
  KARIBU

  0 0

   Gulio la Airtel Smartphone lililofanyika  Mlimani City wikiendi iliyopita.
  Baadhi ya Wateja waliofika katika Mlimani City kujipatia Ofa kabambe inayotolewa na Kampuni ya simu ya Airtel na Huawei  katika banda la  Mlimani City jijini Dar Es Salaam  wiki iliyopita. Gulio linalomuwezesha mteja kujishindia zawadi mbali mbali pale anaponunua simu ya Huawei.

   


  Airtel Bazaar Gulio lililoanza wiki iliyopita pale Mlimani City siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili litaendelea tena wiki hii kutoa ofa kabambe za simu za kisasa. Wiki hii Bazaar la Airtel na Huwawei ni pale Kibo Complex Tegeta na Mlimani City kuanzia saa tatu na nusu Asubuhi hadi saa moja usiku siku zile zile za Ijumaa Jumamosi na Jumapili.


  Huu ndio wakati wako wewe kujismartifonisha kwa simu kali kwa gharama nafuu ikiambatana na Bando la bure la mwaka mzima la Airtel.


  Bazaar hili sio lakukosa kwani linamwaga ofa ambazo huwezi kupata popote zaidi ya Airtel.

  0 0

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  SIKU moja baada ya kambi rasmi ya Upinzani Bungeni kumlipua mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama kwa madai ya kufanya udalali na ufisadi katika uporaji wa ardhi ya wananchi ,mkuu huyo amejitokeza
  mbele ya wanahabari na kukanusha tuhuma hizo.

  Katika utetezi wake Gama alirejea kauli yake aliyoitoa miaka sita iliyopita ya kuwa yeye ni msafi huku akiitupia mzigo halmashauri ya wilaya ya Rombo tuhuma za kiasi cha sh Mil 500 zilizotajwa kutolewa wawekezaji wa Kichina kama fidia kwa wananchi katika ardhi
  kilipojengwa kiwanda cha kutengeneza Saruji.

  Alisema tuhuma zilizotolewa Bungeni dhidi yake si za kweli na kwamba ni za kisiasa huku akitaja sababu ya kuibuliwa kwa tuhuma hizo kuwa ni kutokana na juhudi zake za kupambana na Pombe haramu katika wilaya ya Rombo pamoja na Urejeshwaji wa wafanyabiashara katika soko la kati la mjini Moshi.

  “Nataka niwaambie hii ni siasa,zipo issue nyingi zilizochangia kuibuka kwa haya mambo ,lakini nawaambieni mbili tu,Issue ya kwanza Pombe Rombo,na msimamo wangu juu ya Pombe Rombo ndio imeza hii,la pili ni soko la Moshi mjini,watu wana agenda zao kwenye soko hilo ,wananchi wamerudi pale ,imewaumiza watu.”alisema Gama.

  “Watu walitaka Pombe ya Gongo iharalishwe,mimi nimesema hadharani anayetaka pombe ya Gongo ihararishwe si mwenzetu mu mshughulikie kwa maana si mwenzetu sasa hili limeleta nongwa”aliongeza Gama.

  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akizungumza na wanahabari (hawako pichani) juu ya tuhuma zilizoibuliwa bungeni dhidi yake.
  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akiwa na mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga katika mkutano huo na wanahabari.
  Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali ya habari mkoani Kilimanjaro.
  Akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma hizo ,Gama amekiri mtoto wake aliyetajwa kwa jina la Mayunga Leonidas Gama kuhusika katika uanzishaji wa kiwanda hicho huku akihakikisha kiwanda hicho kinajengwa katika mkoa wa Kilimanjaro badala ya Bagamoyo kama walivyo pendelea
  wawekezaji hao.

  “Kiwanda cha saruji kinachojengwa pale Rombo, nilikuwa na uwezo wa kukipeleka popote ninapotaka mimi, lakini mimi binafsi ndiye niliyefanya juhudi kiwanda kile kijengwe Kilimanjaro, mimi binafsi na wala sio mtu mwengine, nimefanya juhudi hizo kwa lengo la kuongeza
  ajira kwa wananchi na kuinua uchumi wa mkoa huu”, alisema Gama .  “Historia ya Kiwanda hiki iko wazi, na  nililipeleka hadi kwenye kikao cha ushauri wa mkoa (RCC),nanaomba nieleweke kwamba, ni juhudi zangu na za mtoto wangu, nilitamka kwenye kikao kile na wala sikuficha, mtoto wangu ambaye ametajwa yeye ana rafiki yake wa kichina, wala si
  kweli kwamba hii kampuni mimi nimekwenda kuichukua China kwa gharama za serikali” aliongeza Gama.

  Alisema katika kikao hicho (RCC), Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, Mbunge wa Vunjo, Dkt. Augustino Mrema na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, walishiriki katika kikao hicho na kwamba baada ya mvutano ndipo makubaliano yakawa kiwanda kijengwe wilaya ya Rombo .

  “Toka siku ile mimi kama mkuu wa mkoa nikakabidhi madaraka wilaya yaRombo,kwa hiyo shughuli zote za ujenzi ,shughli zote za kutafuta viwanja ziifanywa na halmashauri ya wilaya ya Rombo na sio Gama”alisema Gama.

  Alisema waliolipa fidia na kununua viwanja ni halmashauri ya wilaya na hata eneo kilipojengwa kiwanda hicho ni mali ya halmashauri ya wilaya ya Rombo na si cha mwekezaji kama inavyoelezwa .

  “Nimeelezwa kweye tuhuma kuwa nimepewa milioni 500,hii ni hadithi ya kisiasa ,sijapokea kiasi hicho cha fedha wala sikijui,hata hizo hisa 20,000 nilizoambiwa ninazo kwa kweli sina ,kama ningekuwa nazo ni haki yangu kwa sabau sijavunja sharia lakini sin ahata hisa moja.”alisema
  Gama.

  “Swala mtoto wangu kuwa na hisa si dhambi na ni haki yake kisheria,kwa
  sababu yeye ndiye aliyewatafuta hao watu na ni rafiki zake ,wala si
  mimi niliyewaleta kama amenunua hisa huko ni hiari yake,mimi sina hisa
  kama Gama,sijapokea milioni 500 kama gama,mimi si dalali na kama ni
  udalali wa ardhi hiyo itakuwa ni halmashauri ya wilaya ya Rombo na si
  gama.”alisema Gama.

  Alipoulizwa endapo kama halmashauri ya wilaya ya Rombo itakuwa inamiliki sehemu ya hisa katika kampuni hiyo kutokana na utolewaji wa ardhi yake ,Gama alisema wenye majibu ni halmashauri ndio watakuwa wanajua ni mikataba gani wameingia na wawekezaji hao.

  Kuhusu eneo la Uwekezaji wa soko la Lokolova, Gama alisema ameshangazwa na kauli za kuwa yeye ni fisadi wa ardhi katika eneo hilo wakati makubaliano ya kuanzishwa kwa soko la kimataifa na ji mdogo wa kibiashara ulipitishwa katika kikao cha RCC ambacho pia Mbunge wa Vunjo, Dkt. Augustino Mrema alihudhuria na kusifia mpango huo.

  Sakata la Kiwanja cha Mawenzi, Gama alisema yeye kama mkuu wa Mkoa, alichokifaya ni kuishauri Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kufuata Sheria za umilikishwaji wa Ardhi ili kuepusha Halmashauri kufilisiwa kwa kukiuka taratibu.

  Juzi wakati akiwasilisha bungeni maoni ya kambi rasmi ya upinzani kuhusu bajeti yay a wizara ya ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi kwa mwaka wa fedha 2015/2016,msemaji mkuu wa kambi hiyo Halima Mdee
  alimrushia tuhuma Gama za kuhusika katika kutumia fedha za serikali kwenda nchini China kutafuta watu wawili wanaotajwa kama wawekezaji.

  Katika taarifa hiyo Mdee alidai katika hali isiyo ya kawaida nay a kushangaza watu hao katika ardhi iliyokwisa lipiwa fidia kwa fedha za umma ,ilianzishwa kampuni binafsi ya Jun Tu Investment International Company Ltd .

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania (BOA), Masia Mushi (kulia), na Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa ya Uendelezaji wa Ardhi ya AVIC, Liu Dexiang, wakisaini mktaba wa makubaliano ya mikopo na uuzaji wa nyumba za bei nafuu kupitia BOA jijini Dar es Salaam jana, zilizojengwa na kampuni hiyo eneo la Somangira, Kigambini jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania (BOA), Masia Mushi (kulia), na Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa ya Uendelezaji wa Ardhi ya AVIC, Liu Dexiang, wakibadilishana hati za mktaba wa makubaliano ya mikopo na uuzaji wa nyumba za bei nafuu kupitia BOA jijini Dar es Salaam jana, baada ya kusaini leo, zilizojengwa na kampuni hiyo eneo la Somangira, Kigambini jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwanasheria wa BOA, Patrick Malewo na kushoto ni Mwansheria wa AVIC, Li Jiayin.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa (BOA), Masia Mushi, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa pamoja na Kampuni ya Kimataifa ya Uendelezaji wa Ardhi ya AVIC, kuhusu mradi mkubwa wa mikopo nafuu ya nyumba zilizojengwa na kampuni hiyo, zilizopo eneo la Somangira, Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambao utawanufaisha watanzania hususani wateja wa benki ya BOA, ambao ulisainiwa rasmi jana. Katikati ni Naibu Meneja Mkuu wa AVIC, Liu Dexiang na kushoto ni Mwanasheria wa kampuni hiyo, Li Jiayin.
   Viongozi wa Bank of Africa (BOA) kwa pamoja na viongozi wa Kampuni ya Kimatiafa ya Uendelezaji wa Ardhi (AVIC), wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu kusainiwa kwa mkataba wa makubaliano ya mikopo nafuu uuzaji wa nyumba zilizojengwa ka kampuni hiyo, zilizopo eneo la Somangira, Kigamboni, Dar es Salaam. Hafla ya kusaini mktaba huo ilifanyika leo.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa (BOA), Masia Mushi, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kuhusu mkataba wa pamoja na Kampuni ya Kimataifa ya Uendelezaji wa Ardhi ya AVIC, wa mikopo nafuu ya nyumba zilizojengwa na kampuni hiyo eneo la Somangira, Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambao utawanufaisha watanzania hususani wateja wa benki ya BOA, kabla ya kusainiwa mkataba huo rasmi jana. Kushoto kwake ni Mwanasheria wa benki hiyo, Patrick Malewo.

  0 0

  Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudentia Kabaka (Kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah Moshi (Kushoto) wakifuatilia majadiliano kwenye Mkutano wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) unaofanyika Geneva, Uswizi. Mada Kuu katika Mkutano huo ambao umehudhuriwa na wajumbe zaidi ya 2000 kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni ni Mchakato wa Kurasimisha Sekta Isiyo Rasmi na Mchango wa Ujasiriamali wa Kati na Mdogo katika Kutengeneza Ajira. Waziri Kabaka aliuhutubia Mkutano huo tarehe 8 Juni, 2015 chini ya Uenyekiti wa Balozi wa Tanzania nchini Uswisi Mh. Mero.

  0 0

   Balozi wa India Debnath Show akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa makampuni ya GEM, Rangaswame Veeramani  katika mkutano wa wafanyakazi wa India wanaowekeza Tanzania, mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam leo.
   Mkurugenzi  wa utawala wa TCCIA Francis Lukwaro akizungungumza na baadhi ya waandishi wa habari kuhusiana na thamani ya shilingi ya Tanzania inavyoshuka na kusababisha wawekezaji kuja kuwekeza hapa nchini leo katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Taasisi ya sekta binafsi hapa nchini Loics Accaro akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kumalizika mkutano wa wawekezaji wa  China katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.
    Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wawekezaji uliofanyika katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam..(PICHA NA EMMENUEL MASSAKA.)

  0 0


  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiwapungia mkono wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na wananchi waliofika kumpokea nje ya Ofisi ya CCM Mkoa wa Mbeya leo June 10, 2015 baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho. Picha zote na John Badi.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati) akilakiwa na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na wananchi waliofika kumpokea nje ya Ofisi ya CCM Mkoa wa Mbeya leo June 10, 2015, baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati) akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na wananchi waliofika kumpokea nje ya Ofisi ya CCM Mkoa wa Mbeya leo Juni 10, 2015, baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.

  0 0

   WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesisitiza kuwa tarehe ya mwisho (deadline) iliyotolewa na Serikali ya kusimamia ujenzi wa maabara za shule za sekondari iko palepale na akawataka watendaji wa Halmashauri na Mikoa kuhakikisha wanatimiza agizo hilo.

  Ametoa wito huo leo mchana (Jumatano, Juni 10, 2015) wakati akizungumza na watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Waratibu wa Elimu wa Wilaya na Mikoa waliohudhuria ufunguzi wa mashindano ya UMISSETA NA UMITASHUMTA kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

  Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mashindano hayo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, alisema Serikali bado haijalegeza msimamo wake. “Tarehe 30 Juni 2015 bado iko palepale… Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya simamieni shughuli za ujenzi ili zikamilike kwa wakati,” alisema.

  Alisema mbali na maabara, Serikali bado inakabiliwa na changamoto ya kumaliza tatizo la uhaba wa madawati. Alizitaka Halmashauri ziendelee kutenga fedha kila mwaka pamoja na kushirikiana na taasisi zinazosaidia jitihada za Serikali kupunguza tatizo hilo ili kuhakikisha tatizo hilo linakwisha nchini.

  Waziri Mkuu pia alitumia fursa hiyo kuzungumzia tatizo la mipaka ya shule na utunzaji wa  mazingira ya shule na kuwataka Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Wilaya wasimamie suala hilo na kuhakikisha maeneo hayo yanapimwa na kupatiwa hati. “Simamieni maeneo yote ya shule yapimwe na yawe na hati miliki. Lakini wakati wa ujenzi wa shule zetu hakikisheni ramani za shule zinazingatia kuwepo kwa viwanja vya michezo ili wanafunzi waweze kufanya mazoezi na kucheza.


  Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa vitabu, Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kila mwanafunzi awe na kitabu kimoja kwa kila somo ifikapo mwaka 2016. “Hata hivyo, hivi sasa katika shule za msingi uwiano umefikia kitabu kimoja kwa wanafunzi watatu (1:3) ikilinganishwa na kitabu kimoja kwa wanafunzi saba (1:7) ilivyokuwa mwaka 2005,” alisema.

  Akizungumza na washiriki wa mashindano hayo kutoka kanda 12 za Tanzania Bara na Zanzibar, Waziri Mkuu aliwataka watambue kwamba michezo siyo mahali pa ugomvi bali michezo inataka nidhamu na uadilifu. “Mashindano siyo ugomvi bali ni fursa ya kujenga mshikamano, tumieni fursa hii kujenga dhamira ya kweli ya kutaka kufanya vizuri zaidi katika michuano ijayo,” alisisitiza.

  Alisema washiriki wa mashindano hayo wamekutanishwa kutoka mikoa mbalimbali, na kwamba watapimwa siyo tu katika michezo, bali katika masuala mengine ikiwemo uadilifu, usafi, kuzingatia maelekezo na nidhamu. “Baadhi ya wanamichezo wana mahitaji maalum, hivyo tuoneshe upendo kwao ili wajisikie nao kushiriki katika mashindano haya,” alisisitiza.

  Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki michezo hiyo, Waziri wa Nchi (OWM – TAMISEMI), Bibi Hawa Ghasia alisema mashindano hayo ni ya tano kufanyika kitaifa tangu yalipofufuliwa mwaka 2000.

  Akitoa mchanganuo wa mashindano hayo, Waziri Ghasia alisema mashindano hayo yanayofanyikia Butimba, wilayani Nyamagana yataendeshwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itahusisha mashindano ya UMISSETA yaliyoanza Juni 8, 2015 na yanatarajiwa kumalizika Juni 20, mwaka huu.

  “Awamu ya pili itakuwa ni ya mashindano ya UMITASHUMTA ambayo inatarajiwa kuanza Juni 22, 2015 na kukamilika ifikapo Julai 4, 2015. UMISSETA inajumuisha washiriki 1,755 wakati UMITASHUMTA itashirikisha wanamichezo 1,000,” alisema Waziri Ghasia.

  (mwisho)

  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  DODOMA.
  JUMATANO, JUNI 10, 2015.

  0 0

   DAUDI YASSINI AKIMKARIBISHA MKUU WA WILAYA YA MUFINDI, MBONI MHITA KATIKA UWANJA WA WAMBI MJINI MAFINGA WAKATI WA FAINALI YA MASHINDANO YA MUUNGANO.
   MKUU WA WILAYA YA MUFINDI, MBONI MHITA AKIKAGUA TIMU KABLA YA MCHEZO
  MGENI RASMI KATIKA FAINALI HIZO, MKUU WA WILAYA YA MUFINDI, MBONI MHITA AKIWA KATIKA PICHA MOJA NA MABINGWA  WA MUFINDI CUP TIMU YA MKOBA.


  0 0

   DAUDI YASSINI AKIMKARIBISHA MKUU WA WILAYA YA MUFINDI, MBONI MHITA KATIKA UWANJA WA WAMBI MJINI MAFINGA WAKATI WA FAINALI YA MASHINDANO YA MUUNGANO.
   MKUU WA WILAYA YA MUFINDI, MBONI MHITA AKIKAGUA TIMU KABLA YA MCHEZO
  MGENI RASMI KATIKA FAINALI HIZO, MKUU WA WILAYA YA MUFINDI, MBONI MHITA AKIWA KATIKA PICHA MOJA NA MABINGWA  WA MUFINDI CUP TIMU YA MKOBA.


  0 0


  Bendi ya African Stars maarufu kama Twanga Pepeta leo (Ijumaa Juni 12) itafanya onyesho maalum la kumtambulisha mwanamuziki maarufu nchini Ali Choki na wengine waliorejea kwenye bendi hiyo.
  Onyesho hilo litafanyika usiku katika ukumbi wa Da West Park, Tabata.  Mratibu wa onyesho hilo Joseph Kapinga wa Keen Arts na Bob Entertainment amesema kuwa onyesho hilo pia litakuwa ni la vunja jungu kabla ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
  Kapinga alisema pia Choki atatumia onyesho hilo kutambulisha nyimbo zake mpya ambazo ni “Kichwa Chini” na “No Discussion”.  Wanamuziki wengine ambao watatambulishwa pamoja na Choki ni mnenguaji wa bendi hiyo Super Nyamwela na mpiga kinanda Victor Mkambi. Choki na Nyamwela wametokea kwenye bendi ya  Extra Bongo wakati Victor Mkamba ametokea bendi ya Ruvu Stars.  Kwa upande wake Ali Choki alisema kwenye onyesho hilo litakuwa ya aina yake kwani atapiga nyimbo zote alizizowahi kupiga akiwa na Twanga Pepeta kabla hajahamia bendi ya Extra Bongo.  Baadhi ya nyimbo hizo ni “Kisa Cha Mpemba,” “Fainali Uzeeni,”  “Umbea Hauna Posho,” “Jirani,” “Password,” “Kuolewa,” “Busu la 2005,” “Busu la Kufunga Mwaka,”  “Aminata” na zinginezo.

  Naye Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka amesema onyesho ya leo litakuwa ni kama zawadi kwa wakazi wa Tabata na vitongoji vyake, kwani itakuwa onyesho la mwisho la bendi hiyo kabla mfungo wa Ramadhani.

  0 0

  WAANDAAJI wa Tamasha la Pasaka wamesema kuwa DVD ya onesho la Miaka 15 ya tamasha hilo lililofanyika Aprili mwaka huu ipo mtaani.
   
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kuwa DVD imeonesha shughuli nzima ya tamasha hilo lililofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na mgeni rasmi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
   
  “Nawaomba mashabiki wa muziki wa Injili ambao walikuwa wakiniulizia kuhusiana na DVD hiyo kwamba sasa ipo mtaani na ni jukumu lao kuitafuta katika maduka yetu.
   
  “Wale waliohudhuria tamasha hilo na wale ambao hawakuhudhuria wote watambue kuwa sasa wanaweza kuona tamasha hilo wakiwa sebuleni kwao,” alisema Msama.
   
  Alisema tamasha la mwaka huu lilikuwa tofauti na matamasha mengine yaliyopita kwani liliendana na sherehe za miaka 15 tangu waanze tamasha hilo.
   
  Alisema DVD hiyo inaonesha waimbaji wote mahiri waliohudhuria na kwamba ana matumaini makubwa mashabiki watakuwa na kumbukumbu kubwa ya shughuli hiyo.Waimbaji mbalimbali wa ndani na nje walishiriki tamasha la mwaka huu akiwemo Mwingereza, Ayobami David na Rebecca Maloppe wa Afrika Kusini.
   
  Mwaka huu Tamasha la Pasaka lilitimiza miaka 15 tangu kuasisiwa kwake na Kampuni ya Msama Promotions ya Dar es Salaam, ambapo limekuwa likijiongezea umaarufu na kukubalika zaidi kutokana na ubunifu wake wa kufanya maadhimisho ya Sikukuu za Pasaka na Krismasi kwa umahiri na mguso wa kiroho kupitia matamasha hayo.

older | 1 | .... | 550 | 551 | (Page 552) | 553 | 554 | .... | 1898 | newer