Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live

NEC YAONGEZA SIKU 7 ZA UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.

0
0
Mkurugenzi wa Idara  ya Daftri la Kudumu la Wapiga kura Dk.Sisti  Griah akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani leo katika ukumbi wa mikutano wa Tume ya uchanguzi, juu ya Tume ya Taifa ya uchaguzi kusogeza mbele siku saba ya  zoezi la Uboreshaji wa Daftali la Wapiga Kura katika Mikoa ya Kilimanjaro,Arusha ,Manyara na Mara Ambalo linatarajia kuanza Juni 16 mwaka huu.Kulia ni Mkurungenzi idara ya Elimu ya Mpiga kura Ruth Masham.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano wa mazungumzo ya kuongeza siku za uandikishaji wa Daftari la wapiga kura.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.)

BALOZI MAHIGA ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS.

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

ALIYEKUWA Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa,Dk.  Augustine Mahiga ametangaza nia ya kugombea urais ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), jijini Dar es salaam leo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Mahiga amesema maadili yamemomonyoka na kufanya kuwepo kwa rushwa na ufisadi.

Mahiga amesema ubadhirifu na ufisadi katika taifa kunahitajika kuwepo kwa mwelekeo katika kuweza kupambana na vitu hivyo ili maendeleo yapatikane kwa wananchi.

“Nikipata nafasi hii nitatumikia watu katika kuujenga uchumi imara kwa kila mwananchi kutokana na kuwepo kwa dira na kuondoa matabaka yanayotokana na ubadhirifu wa mali za umma”amesema Mahiga.

Amesema CCM itoe fursa, isifikie utawala wa watu wenye pesa hiyo sio dhamira ya CCM, na watu wanaotoa msaada uwe na kikomo chake.

Mahiga amesema katika kuweza kufikia uchumi wa kati kunatakiwa kupambana na rushwa na ufisadi, bila kufanya hivyo uchumi huo hautafikiwa.
Aliyekuwa Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Augustine Mahiga akizungumza wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam. kushoto ni Mke wa Aliyekuwa Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Augustine Mahiga, BI Elizabeth Julius Mahiga.
Baadhi ya waandishi wa habari na wananchi wakimsikiliza Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa,Dk Augustine Mahiga wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dar es Salaam leo.(Picha na Avila Kakingo).

HANSA GROUP SUPPORTS KIBAMBA PRIMARY SCHOOL- DAR ES SALAAM.

0
0
HANSA Group of Companies has business networks in Tanzania, Kenya, Zambia, South Africa, Uganda, DRC and India, just to name few. In Tanzania they have distributor ship of Mitsubishi, Fuso and Yokohama Tyres.

Hansa group in continuation with their endeavor in Corporate Social Responsibility (CSR) projects, particularly in the education sector, had donated TZS 67 million in 2014 for a learning facility in Kibamba for mentally handicapped Children.

Kibamba Primary school was built in the memory of Late Mr. & Mrs. J P Rajani, Hansa Group has pledged to support the school continuously by various means.

Last week … senior management representatives of HANSA Group visited the school to donate Lego Toys for kids and had enough time to enjoy with students and school teachersHANSA group is committed to support activities in the field of Education and Medical
Thanking you in advance,Reuben Richard,Manager – Marketing and Business Development.
02030401

WAZIRI BERNARD MEMBE AJINYAKULIA WADHAMINI WA KUTOSHA MKOA WA LINDI NA MTWARA.

0
0
Katibu wa CCM Mtwara mjini, Modesta Mwaya akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia), fomu zilizotiwa saini na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mtwara mjini, waliofika kwenye Ofisi hizo Juni 08.2015, kwa ajili ya kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.
Sehemu ya umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mtwara, waliofika kwenye Ofisi ya CCM Mtwara mjini Juni 08.2015, kwa ajili ya kutia saini fomu za kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia) akishangiliwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Lindi, mara baada ya kufika ofisi hapo akitokea mjini Dodoma.
 Umati wa wanachama waliojiokeza kumpokea Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe.
Mama Dorcas Membe akiwasalimia wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Lindi, wakati wakitia saini fomu za kumdhamini kwa ajili ya kuteuliwa kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, katika Ofisi ya CCM mkoani humo.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi, Ali Mtopa akiwasalimia wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Lindi, wakati wakitia saini fomu za kumdhamini kwa ajili ya kuteuliwa kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, katika Ofisi ya CCM mkoani humo.
Wanachama wakifuatilia kwa makini jinsi wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Lindi, wakati wakitia saini fomu za kumdhamini kwa ajili ya kuteuliwa kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, katika Ofisi ya CCM mkoani humo.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiwa na Mkewe Dorcas Membe mara baada ya kufika ofisi za CCM) Mkoa wa Lindi, wakati wakitia saini fomu za kumdhamini kwa ajili ya kuteuliwa kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akisalimia na wananchama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mtwara, waliofika kwenye Ofisi ya CCM Mtwara mjini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (wa pili kushoto) na mkewe Dorcas (kushoto) wakifuatilia kwa makini jinsi wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Lindi, wakati wakitia saini fomu za kumdhamini kwa ajili ya kuteuliwa kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiteta jambo na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Lindi, wakati wakitia saini fomu za kumdhamini kwa ajili ya kuteuliwa kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mtwara, waliofika kwenye Ofisi ya CCM Mtwara mjini, kwa ajili ya kutia saini fomu za kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.

MASHINDANO YA BAISKELI KUFANYIKA JIJINI DAR JUNI 14 MWAKA HUU.

0
0
 Mkuu wa mashindano ya Baiskeli na Barozi wa Umoja wa Ulaya Filiberto Sebregondi akizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani)katika ukumbi wa mikutano wa Ubalozi wa Ulaya jijini Dar es Salaam leo. kushoto ni Mratibu wa Msafara wa Mkuu wa Operesheni ya umoja wa Ulaya, Eric Beaume.
Naibu Mhamasishaji Mkuu wa Mfuko wa Fedha za Umoja wa Ulaya, Godlove Stephen akizungumza na waandishi wa habari hawapo hewani kuhusiana na mashindano ya baiskeli yatakayofanyika Juni 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam na kulia ni Mkuu wa mashindano ya Baiskeli na Barozi wa Umoja wa Ulaya Filiberto Sebregondi.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano wa watu walioongelea kuhusiana na mashindano yatakayofanyika jijini Dar es Salaam Juni 14 mwaka huu.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.)

DKT. BILAL AWASILI SHARM EL SHEIKH KUHUDHURIA MKUTANO WA TATU WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI YA UTATU WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC).

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Uwanja wa wa Ndege wa Kimataifa wa Sharm El Sheikh, jijini Sharm El Sheikh Cairo Misri, kwa ajili ya kuhudhuri Mkutano Mkuu wa tatu wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Soko la pamoja la nchi za Kusini mwa Afrika (COMESA) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Uchukuzi wa Egypt, Hossam Kamal, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sharm El Sheikh, jijini Sharm El Sheikh Cairo Misri, kwa ajili ya kuhudhuri Mkutano Mkuu wa tatu wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Soko la pamoja la nchi za Kusini mwa Afrika (COMESA) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Agenda ya mkutano huo ni kupokea taarifa ya majadiliano ya kuanzisha eneo huru la Biashara la Utatu wa EAC, COMESA na SADC.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Afrika Mashariki, Dkt. Harrison Mwakyembe, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sharm El Sheikh, jijini Sharm El Sheikh Cairo Misri, kwa ajili ya kuhudhuri Mkutano Mkuu wa tatu wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Soko la pamoja la nchi za Kusini mwa Afrika (COMESA) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa Uchukuzi wa Egypt, Hossam Kamal, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sharm El Sheikh, jijini Sharm El Sheikh Cairo Misri. Dkt. Bilal, amewasili Jijini Sharm El Sheikh kwa ajili ya kuhudhuri Mkutano Mkuu wa tatu wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Soko la pamoja la nchi za Kusini mwa Afrika (COMESA) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Picha na OMR 

ASKOFU CHARLES GADI AFANYA MAOMBI MAKUBWA NCHINI INDIA KUOMBA KUPUNGUA KWA JOTO.

0
0
 Askofu Charles Gadi  wa Huduma ya Good News for all Ministry akiwa katika matukio tofauti wakati akifanya maombi makubwa katika mji wa Hydrabad nchini India ili joto lipungue kwani tayari limekwisha uwa watu 2500 kutoka na kupanda hadi kufikia kiwango cha joto centgrade 50.

ASKOFU Charles Gadi  wa Huduma ya Good News for all Ministry akifanya maombi makubwa katika mji wa Hydrabad nchini India ili joto lipungue kwani tayari limekwisha uwa watu 2500 kutoka na kupanda hadi kufikia kiwango cha joto centgrade 50.

Akizungumza kwa njia ya simu na mtandao huu toka nchini humo alisema hali hiyo imetokana na maeneo kadhaa ya nchi hiyo kuwa na wimbi kubwa la upepo wa joto (heat wave) na kusababisha vifo hivyo.

"Habari hii kwetu si njema ndio maana nimeamua kuja kufanya maombi haya makubwa nchini humu na wenzangu kwani linatokana uharibifu wa mazingira ambapo hata huko nyumbani linaweza kutokea" alisema Askofu Badi.

Alisema watu waliokufa ni wengi, wazee, watoto na maskini ambao hawana uwezo wa kujikinga na wimbi hilo la joto kwani unahitaji uwe na viyoyozi 'Air conditioning' au maji baridi ya kujinyunyuzia wakati wimbi hilo la joto likipita.


Kutokana na hali hiyo sisi kama viongozi wa kiroho tumesukumwa na mungu kuja nchini humu kufanya maombi haya tukiamini mungu atatusaidia atukinge na joto hilo linalosababishwa na uharibifu wa mazingira.

Alisema maombi hayo yataambatana na utoaji wa misaada kwa waathiriwa wa joto hilo. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com simu namba 0712-727062)


 Askofu Charles Gadi  wa Huduma ya Good News for all Ministry akiwa katika matukio tofauti wakati akifanya maombi makubwa katika mji wa Hydrabad nchini India ili joto lipungue kwani tayari limekwisha uwa watu 2500 kutoka na kupanda hadi kufikia kiwango cha joto centgrade 50.
 Maombi yakiendelea.
Na Dotto Mwaibale

GLOBAL TV ONLINE : JOKATE AFUNGUKA KUHUSU BIDHAA ZA KAMPUNI YAKE

0
0

Morogoro yaanza maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. John Henjewele akifungua mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura yaliyofanyika Juni 5, 2015 Katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Kulia, ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Bi Azimina Mbilinyi.
Baadhi ya wajumbe wa mafunzo hayo wakila kiapo cha uaminifu katika utekelezaji wa zoezi ambalo liko mbele yao. Kushoto ni Hakimu Mkazi Bi. Agnes Ringo.
Bi. Sajira Mbaga ambaye ni Afisa kutoka tume ya Taifa ya Uchaguzi, akihojiwa nawaandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Baadhi ya vifaa vilivyowasili Mkoani Morogoro kwa ajili ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura. Picha na Andrew Chimesela .
Na Andrew Chimisela

Mkoa wa Morogoro umeanza maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba mwaka huu.

Maandalizi hayo yameanza jana kwa semina ya siku mbili inayotolewa kwa waratibu wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika ngazi ya Mkoa na Wilaya za Mkoa wa Morogoro.
Semina hiyo inalenga kutoa Elimu itakayowawezesha kutekeleza jukumu hilo katika kufanikisha zoezi hilo muhimu. Mafunzo hayo yatahusisha ujazaji  wa fomu zitakazotumika kwenye zoezi zima la uboreshaji la wapiga kura. 

Aidha, yatatolewa mafunzo kwa vitendo yatakayohusu jinsi ya kutumia kifaa cha kisasa yaani Biometric Voters Registration (BVR) kinachochukua alama mbalimbali za mpiga kura kwa lengo la kuondoa uwezekano wa mtu kujiandikisha zaidi ya mara mbili.

Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  Dkt. Rajabu Rutengwe kupitia hotuba iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa  Mhe. John Henjewele,  aliwataka wanasemina kujifunza kwa bidii na kuhakikisha wanajua utaratibu unaotakiwa kutumika katika kuboresha daftari hilo la kudumu la wapiga kura.

Dkt. Rutengwe alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa Mkoa wa Morogoro kujiandikisha katika vituo vyao mara muda utakapowadia wa kufanya hivyo. “Naomba kutoa wito kwa wananchi walio na sifa ya kuwa wapiga kura Mkoani hapa waweze kujitokeza ili wajiandikishe”. Alisema.
“Aidha, napenda kuwahakikishia kwamba Serikali Mkoani hapa imedhamiria kuhakikisha zoezi hili linafanyika kwa ufanisi mkubwa na kufanikiwa” Dkt. Rutengwe aliongeza.

Naye Bi. Sajira Mbaga, Afisa kutoka Tume ya Uchaguzi alisema, zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa Mkoa wa Morogoro, linatarajiwa kuanza kufanyika Juni 14 mwaka huu na kuongeza kuwa Tume hiyo inaendelea na jitihada za kuondoa changamoto zilizojitokeza kwenye zoezi hili katika Mikoa mingine ambapo zoezi hili limekwisha fanyika.

TANAPA to benefit from Chinese Academy of Sciences

0
0
Some of the TANAPA Management team posed in a group picture with a delegation from the Chinese Academy of Sciences after the official signing of the MoU between the two institutions.
Director General of Tanzania National Parks Allan Kijazi (right) and Executive Director of Sino-Africa Joint Research Centre, Chinese Academy of Sciences Professor Qing-Feng Wang signing Memorandum of Understanding between their institutions in Arusha yesterday.

Tanzania National Parks has signed a Memorandum of Understanding with the Sino-Africa Joint Research Centre, Chinese Academy of Sciences whereby the duo have agreed to work together for the mutual benefit of conservation sector in the country and particularly in National Parks.

Speaking during the official signing event, the Director General of TANAPA Allan Kijazi said that the MoU would boost and enhance higher education training through research, training, innovation, technological development and capacity building in areas of mutual interest.

Kijazi further mentioned that the two parties would exchange experience and resources in areas such as biodiversity conservation, effective utilization of bio- resource, water pollution control, and strategies for solving conflicts with communities, tourism and environmental protection.

On his part, the Executive Director of Sino-Africa Joint Research Centre, CAS Professor Qing Feng Wang commended the decision by TANAPA to enter into Mou with his institution believing that the move will assist TANAPA in managing better the National Parks.

Sino-Africa Joint Research Centre had already sponsored three staff from TANAPA to attend a short course on ecology in China last year and they have also offered three Masters degree Scholarships for TANAPA staff to be implemented soon.

LOWASSA ATIKISA MUSOMA, BUNDA NA TARIME

0
0
1
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akisalimiana wanachama wa CCM waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege Musoma mkoani Mara jana kwa ajili yakutafuta wanachama wakumdhani kugombea Urais.
  4
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akiwapungia mkono wanachama wa CCM waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege Musoma mkoani Mara jana kwa ajili yakutafuta wanachama wakumdhani kugombea Urais.
5
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akizungumza na wanachama wa Chama Chama Mpinduzi(CCM )nje ya Ofisi ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara baada wakati alipofika kwa ajili yakutafuta wanachama wakumdhani kugombea Urais.
6
 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akiweka shahada la maua kwenye Kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere Butiama baada ya kutembelea makazi ya Mwalimu wakati akiwa mkoni humo kwa ajili yakutafuta wanachama wakumdhani kugombea Urais.
3
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akiwasha  mshumaa kwenye Kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere Butiama baada ya kutembelea makazi ya Mwalimu wakati akiwa mkoni humo kwa ajili yakutafuta wanachama wakumdhani kugombea Urais.
7

KUPIGA PICHA WATENDA MAKOSA BARABARANI NI KUREKEBISHA TABIA

0
0
Baadhi ya magari yanayopigwa picha njiani na raia wema na mabalozi wa usalama barabarani yakifanya makosa na picha zao kutumwa kituo cha mawasiliano cha kikosi cha usalama barabarani
Baadhi ya magari yanayopigwa picha njiani na raia wema na mabalozi wa usalama barabarani yakifanya makosa na picha zao kutumwa kituo cha mawasiliano cha kikosi cha usalama barabarani,Baadhi ya magari yanayopigwa picha njiani na raia wema na mabalozi wa usalama barabarani yakifanya makosa na picha zao kutumwa kituo cha mawasiliano cha kikosi cha usalama barabarani
Baadhi ya magari yanayopigwa picha njiani na raia wema na mabalozi wa usalama barabarani yakifanya makosa na picha zao kutumwa kituo cha mawasiliano cha kikosi cha usalama barabarani
Na Augustus Fungo, Balozi wa Usalama Barabarani
HIVI karibuni imejitokeza njia mpya ya kusaidia kupambana na wimbi la ajali za barabarani, ambapo pamoja na faini kwa madereva wanaokiuka sheria za barabarani wamekuwa wakipigwa picha na baadaye picha hizo kuwekwa kwenye mitandao ya kijamii au magazetini na hata wakati mwingine kwenye televisheni. 
Mathalani katika mtandao wa facebook kundi la Mabalozi wa Usalama Barabarani maarufu kama, RSA wakishirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani hutumia mbinu hii kuwapiga picha wakiukaji wa sheria za barabarani kisha kuzituma katika Kituo cha Mawasiliano cha Usalama Barabarani (Traffic Control Center, TCC).
Kituo hiki huwatumia picha hizi ambazo pia ni ushahidi askari waliopo katika vituo mbalimbali barabarani, ili kuwezesha watuhumiwa kukamatwa na magari husika. Baada ya kukamatwa magari husika askari humwandikia faini mkosaji, kumpiga picha na kuituma kwenye kituo cha mawasiliano ya polisi (TCC) ambacho na chenyewe hutoa mrejesho kwa watoa taarifa. 
Picha hizo hatimaye kuwekwa kwenye mtadao wa facebook, hutumika kuandaa vipindi vya televisheni vya kuelimisha jamii mfano, ni kipindi cha ‘Aibu yako’ kinachorushwa na televisheni ya ITV na pia picha hizo huhifadhiwa na kikosi cha usalama barabarani kwa ajili ya kumbukumbu na rejea iwapo dereva husika atarudia kosa hilo.

Njia hii mpya ambayo inaitwa kutaja na kuaibisha, ama kwa kiingereza “Naming and Shaming” ni maarufu sana inayotumika si tu na nchi nyingi za Ulaya bali pia na mashirika ya haki za binadamu kama ‘Human Rights Watch’, hutumia kuyaaibisha mataifa yaliyokubuhu kwa ukiukaji wa haki za binadamu.
Saudi Arabia kupitia sheria yake ya makosa ya mtandao (Anti-cyber-crime law (Royal Decree No. M/17 dated 8 Rabi1 1428) imepitisha mbinu hii kama mojawapo ya adhabu. Mbinu kama hii hutumika pia katika nchi nyingi za Ulaya kuwaaibisha watu au makampuni yanayokwepa kodi. Moja ya makampuni yaliyowahi kuathirika na kadhia hii ni kampuni ya Kahawa ya Starbuck. Januari 15, 2015, serikali ya Uingereza iliwataja na kuwadhalilisha waajiri 37 wa Uingereza walioshindwa kulipa kima cha chini kwa wafanyakazi wao.
Hata hivyo, mwandishi James Meernick(2012), anaitaja njia hii kama chaguo kuu la mashirika mengi ya kimataifa katika kuhakikisha haki za binadamu zinazingatiwa.
Njia hii hutumika ikiaminika kwamba kumuweka mtu au taasisi hadharani ili aweze kujiona mwenyewe, aonwe na familia yake, marafiki zake, na hata waajiri wakati akitenda kosa inasaidia kumfanya mtu ajitafakari na kutorudia kosa au pia kuwafanya wanaomzunguka kumpa shinikizo la kufuata sheria au kuheshimu haki za wengine.
Baadhi ya magari yanayopigwa picha njiani na raia wema na mabalozi wa usalama barabarani yakifanya makosa na picha zao kutumwa kituo cha mawasiliano cha kikosi cha usalama barabarani
Baadhi ya magari yanayopigwa picha njiani na raia wema na mabalozi wa usalama barabarani yakifanya makosa na picha zao kutumwa kituo cha mawasiliano cha kikosi cha usalama barabarani
Pamoja na hayo baadhi ya wadau nchini wameipokea mbinu hii kwa hisia tofauti. Wengine wamedai kwamba ni kinyume cha sheria japokuwa hawajaweka kutaja ni sheria gani hasa inayokiukwa kwa kufanya hivyo; wengine wamedai ni kuingilia usiri(privacy) ya mtu bila kusema ni kwa vipi siri ya mtu inaingiliwa pale anapotenda kosa. Pia wameshindwa kuushawishi umma kuelewa je, mtu anapokuwa mathalani anatanua barabarani (matumizi mabaya ya barabara), au analipita gari pasiporuhusiwa au anakimbia kwa zaidi ya mwendo kasi wa 80 (speed) kinyume na sheria akakamatwa akapigwa picha ni kwa jinsi gani anadhalilishwa zaidi ya kuaibishwa?
Maana wakati anapigwa hiyo picha kwanza anakuwa ameshakubali kosa; pili, anakuwa hajavuliwa nguo wala kurushwa kichurachura, kupigwa au kufungwa pingu. Isitoshe wapinzani wa mbinu hii wameshindwa kuwashawishi Watanzania kuelewa iwapo kumpiga picha mkosaji barabarani ni kosa, inakuwaje au ni mara ngapi watuhumiwa wamekuwa wakipigwa picha wanapofikishwa mahakamani?
Je, ni mara ngapi kumekuwa na matukio mfano ya ujambazi na watuhumiwa wa ujambazi katika eneo la tukio au walipokamatwa vyombo vya habari vimekuwa vikiwapiga picha. Je, huku si kuvunja sheria? Itakumbukwa Kituo cha Luninga cha ITV na vingine nchini vimewahi kurusha kipindi maalumu kinachoonesha askari wanaodaiwa wanapokea rushwa, mbona hili halikusemewa? Ni mara ngapi polisi wamekuwa wakitoa picha wa watu wanaotafutwa kwa uhalifu (wanted), ni mara ngapi waajiri wamekuwa wakitoa picha za wafanyakazi wao waliofukuzwa kazi kwa makosa ya kutokuwa waaminifu? Iweje leo picha za wakosaji wa barabarani tu tutolewa ionekane wanadhalilishwa?
Wapo watu wametoa hoja kuwa dereva mkosaji ana maisha yake mengine eti yanaathirika kutokana na kupigwa picha. Kimsingi hoja hii haina mashiko kwakuwa lengo la mbinu ya kutaja na kuaibisha ni kumfanya muhusika aone aibu kwa upuuzi alioufanya na kuweza kujirekebisha. Dereva anayejua kuwa hiyo inaweza kumuharibia hadhi yake huko baadae atakuwa makini zaidi kutokiuka sheria za barabarani au kuchezea maisha ya watanzania wasio na hakia.
Gari za serikali, mashirika ya umma, miradi, na zinginezo haziko juu ya sheria. Bila kujali operesheni wanayofanya au lengo la safari yao hawapaswi kuvunja sheria, na endapo watakuwa wamevunja sheria kwa sababu ya kwenda kuhudhuria dharula husika, askari aliyesimamisha hilo gari akiridhika na sababu hiyo hata toza faini wala kupiga picha, kwa hiyo hakuna kitakachoathirika. 
Na endapo kuna hofu ya matumizi mabaya ya hizo picha, atakaye wajibika ni huyo anayetumia vibaya picha hiyo ili mradi tu picha halisi (original) ya tukio zima ipo na ndiyo itakayotumika kama ushahidi dhidi ya mtu aliyeitumia picha vinginevyo.
Ni ushauri wetu kuwa askari waendelee na mbinu hii ili wavunja sheria waaibike na kuweza kujirekebisha. Haiwezekani dereva amesomea amejaribiwa na kupewa leseni, anajua amebeba abiria kwenye gari lake halafu aendeshe kwa mwendo hatarishi, ayapite magari mengine kana kwamba amebeba viazi, au abiria ni mateka wake.
Faini peke yake hazi saidii. Binafsi ningependa hata siku moja mahakama imhukumu mkosaji kufagia barabara za Kariakoo kwa wiki zima badala ya kumpeleka jela hii ingesaidia zaidi kurekebisha watu. Kimsingi ipo haja kama taifa tuwe na adhabu mbadala. Na kwa kuwa hakuna sheria inayovunjwa kwa mtu kupigwa picha wakati akitenda kosa na kuwekwa hadharani, mbinu hii bado itaendelea kuwa sahihi ili wahusika waache kutenda makosa ambayo yanagharimu si tu maisha ya watanzania bali pamoja na uchumi wa nchi. Naimani Jeshi la Polisi ni Jeshi lenye ueledi na wataalamu mbalimbali hivyo litaendelea kubuni mbinu mbalimbali za kurekebisha tabia na kutekeleza sheria. Hii ndio imani yangu kwa taasisi hii muhimu nchini Tanzania, wananchi tushirikiane nao.
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu sote.

WIZARA YA ARDHI YAFANYA MABADILIKO KATIKA KODI YA ARDHI

0
0
Na Georgina Misama…MAELEZO…Dodoma



Serikali imekusudia kufuta milki za ardhi kwa wamiliki wanaokikuka masharti ya umiliki ikiwemo kutokulipa kodi ya ardhi kwa wakati.


Hayo yamesemwa na waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (MB) leo Bungeni Dododma wakati akiwasilisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kuwa huo ni mmoja wa mikakati ya Wizara yake katika kuimarisha uwezo wa kukusanya kodi.

Mhe. Lukuvi amesema baada ya Wizara yake kurekebisha viwango vya kodi inazokusanya inatarajia kukusanya shilingi bilioni 70 kwa mwaka.


Pamoja na kusudio hilo, Mhe. Lukuvi amesema mikakati mingine ambayo Wizara yake imedhamiria kuitekeleza ili kufikia lengo hilo ni pamoja na kutumia njia za kielektroniki kukusanya kodi ya pango la ardhi, ada na tozo mbalimbali.


Mikakati mingine ni kuhakikisha wamiliki wa mashamba na viwanja wanalipa kodi ya ardhi kupitia Benki, kushirikiana na Wizara ya Fedha kurejesha asilimia 30 ya makusanyo kwa wakati kwenye halmashauri kwa lengo la kuchochea ukusanyaji wa kodi ya ardhi kwa njia ya matangazo kwenye magazeti, redio, luninga na vipeperushi kulipa kodi kwa wakati.


Katika hotuba hiyo, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetangaza kuhuisha viwango vya kodi, ada na tozo mbalimbali ili wananchi wa kima cha chini waweze kulipa ada, tozo na kodi hizo.


Katika uhuishaji huo kwa mfano, kodi ya pango la ardhi imepunguzwa kwa wastani wa asilimia 30 na viwango vya vingine vinavyomgusa mwananchi wa kawaida kwa asilimia 50 au zaidi. 


Viwango vya tozo ya mbele (premium) itapunguzwa kwa asilimia 50 kuanzia mwaka wa fedha 2015/16 na tozo nyingine za sekta ya ardhi kwa asilimia 30. Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo yamepitishwa leo jioni.

SERIKALI KUTUMIA TEKNOLOJIA YA JENI KATIKA KUENDELEZA

0
0
2
Naibu Waziri, Wizara ya Ushirikiano wa Afika Mashariki, Mhe. Dkt. Abdullah Saadala, akijibu swali Bungeni Dodoma leo.3
Naibu Waziri, Wizara ya Kazi na Ajira, Mhe. Makongoro Nyerere (Mb) akijibu swali katika kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Dododma.
4
Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Martha Mlata (aliyesimama) akitoa hoja Bungeni Dodoma leo, akitaka Serikali itoe msimamo kuhusu mgogoro wa Ashanti na Wazawa katika migodi ya Mkoani singida.
5
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utawala Bora, Mhe. George Mkuchika, akijibu swali Bungeni Dodoma leo, la Mhe. Fakharia Shomar Khamis (Viti maalumu), aliyetaka kujua idadi ya viongozi waliofikishwa katika Tume ya Maadili kutokana na makosa ya ukiukwaji wa maadili.
6
Mbunge wa Vunjo, Mhe. Augustino Lyatonga Mrema (aliyesimama) akisalimiana na Mhe. Lekule Leizer (Mb), Loliondo, wakati akiingia Bungeni Dodoma leo

7
Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Esther Bulaya, akiuliza swali la nyongeza kuhusu matumizi ya vipodozi vyenye madhara kwa afya ya binadamu Bungeni Dodoma leo, katika kipindi cha maswali na majibu.
8
Naibu Waziri, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Stephen Kebwe (Mb) akijibu swali Bungeni Dodoma leo, la Mhe. Muhammad Ibrahim Sanya (Mji Mkongwe) aliyetaka kujua kuhusu jitihada za serikali katika kudhibiti kuingizwa kwa bidhaa za vipodozi vyenye madhara kwa matumizi ya binadamu.
9
Naibu Waziri, wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto Mhe. Pindi Chana (Mb) akijibu swali leo Bungeni Dodoma, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika kuhusu mpango wa Serikali kutumia teknolojia ya jeni katika kuboresha mbegu za mazao.
10
Mbunge wa Viti maalum, Mhe. Ana Abdallah akibadirishana mawazo na Mhe. Laidiana Mung’ong’o nje ya ukumbi wa Bunge, leo Dodoma.
11
Mbunge wa Kawe, Mhe. Halima Mdee (CHADEMA) kushoto, akiteta na Mbunge mwenzake, Mhe. Cecilia Paresso (CHADEMA) mara baada ya kikao cha Bunge leo, Dodoma.
Na. Georgina Misama…Maelezo…Dodoma
……………………………………………………………………
Serikali imeandaa mpango wa kuendeleza mazao ya pamba, muhogo, mahindi na migomba kwa kutumia utaalam wa uhandisi jeni.
Hayo yameelezwa bungeni leo na Naibu Waziri, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe Pindi Chana wakati akijibu swali kwa niaba ya Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, lilioulizwa na Mhe. Dkt. Henry Daffa Shekifu (Mb) Lushoto, aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kuanzisha kilimo cha mazao kwa kutumia utaalam wa jeni.
Mhe. Chana amesema kuwa, chini ya mpango huo, Serikali imeimarisha uwezo wa utafiti, Miundombinu ya maabara na mashamba maalum kwa aajili ya kufanya utafiti.
Amesema hata hivyo, utekelezaji wa mipango hiyo umeathiriwa na uwepo wa kipengele cha dhima kali katika kanuni za kusimamaia matumizi salama ya bioteknolojia ambacho kinalenga kuwajibisha utafiti wa mazao ya jeni endapo madhara yoyoyte yatatokea.
Amesema hata hivyo serikali kwa kuzingatia umuhimu wa manufaa ya uhandisi jeni katika kuleta mapinduzi ya kilimo, umefanya marekebisho ya kanuni hizo kwa kuondoa dhima kali katika utafiti ili kuwezesha kufanyika katika mazao ya kilimo.
Mhe. Chana amesema kuwa wataalam wetu wamejifunza utaalam huo na wanao uwezo wa kuitumia teknolojia hiyo, ambapo kwa mfano katika utafiti wa maabara, kwa kutumia uhandisi jeni, wameweza kugundua jeni katika muhogo ambazo zina ukinzani wa magonjwa ya batobato na michirizi kahawia ya muhogo.
Amesema kuwa, serikali itaendelea kuwaelimisha wananchi, kuhusu manufaa ya teknolojia ya uhandisi jeni katika kuleta maendeleo ya kilimo.

MJUMITA WAZINDUA WIMBO WA MKUHUMI ULIOIMBWA NA MPOTO, AFANDE SELE NA DAYNA

0
0
WATANZANIA wametakiwa kuwatumia wasanii katika kufikisha ujumbe wa masuala muhimu ya kijamii kwakuwa wasanii hao wanamvuto mkubwa kwa wananchi.

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa wimbo maalum wa kuhamasisha utunzaji wa mazingira  uliojulikana kama  ‘Mkuhumi’.

Wimbo huo ulioimbwa na wanamuziki wa kizazi kipya Seleman Msindi ‘Afande Sele’, Dayna Nyange pamoja na msanii nguli wa kughani mashairi Afrika Mashariki, Mrisho Mpoto maarufu kama ‘Mjomba’.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa wimbo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (Mjumita), Rahima Njaidi alisema, wameamua kuwatumia wasanii hao kwa kuwa ni rahisi kufikisha ujumbe kwa jamii.

Alisema lengo kuu la wimbo huo ni kuwahamasisha wananchi kutunza mazingira ili waweze kunufaika na Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na ukataji na uharibifu wa Misitu (Mkuhumi), kupitia fedha zinazotolewa na nchi zenye viwanda.

“Watu wengi tunapoenda kusikiliza muziki kuliko kusoma, kwa maana hiyo kama tungeweka elimu hii kwenye vipeperushi isingekuwa rahisi kwa watu wote kupata ujumbe, lakini tunategemea kupitia muziki huu tutawafgikia watu wengi,” alisema.

Alisema wimbo huo umetayarishwa chini ya usimamizi wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Mkuhumi ili kuwafikia wadau ili kwa pamoja waweze kuchukua tahadhari na kupunguza shughuli zinazochangia kutokea kwa mabadiliko ya tabia nchi.

“Kupitia wimbo huu jamii itapata uelewa utakaosaidia kuhamasisha jamiikutumia rasilimali za misitu kwa njia ya uendelevu na kujipatia faida,” alisema Njaidi.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni Mjumbe wa Kikosi kazi cha Mkuhumi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Julitha Masanja ambaye alipongeza kazi nzuri inayofanywa na taasisi hiyo ya Mjumita. 

“ Mjumita inapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote kwani inasaidia kutunza misitu ya asili ambayo imekuwa na changamoto kutokan ana shughuli za binadamu,”alisema Masanja.

Mjumbe wa kikosi Kazi cha Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na ukataji na uharibifu wa Misitu (Mkuhumi),Kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira,  Julitha Masanja (kushoto) akiwa ameshikilia CD na DVD alizozizindua jua ambazo zina nyimbo maalum wa Mkuhumi ambao hupambana na uharibifu wa mazingira Dar es Salaam jana. Pamojanae ni Mkurugenzi wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu (Mjumita), Rahima Njaidi
 Mjumbe wa kikosi Kazi cha Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na ukataji na uharibifu wa Misitu (Mkuhumi),Kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira,  Julitha Masanja akikabidhi DvD kwa wanahabari,
 Ofisa Mawasiliano wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili nchini, Bettie Luwuge akifafanua jambo juu ya mradi huo.
 Mtaalam wa IRA, Edmund Mabhuye akiwasilisha mada juu ya mabadiliako ya tabia nchi na ongezeko la hewa ukaa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (Mjumita), Rahima Njaidi akizungumzia uzinduzi huo Dar es Salaam leo.
Wanahabari n mbalimbali wa kifuatilia maelezo juu ya miradi ya hiyo ya uhifadhi mazingira.

watanzania milioni 21 wapatiwa dawa za magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele

0
0


Catherine Sungura, MOHSW- Arusha

Zaidi ya dozi milioni52 za dawa  zinazotibia magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ya matende, vikope, mabusha,minyoo ya tumbo, kichocho na usubi zimetolewa na Serikali kwa watanzania milioni 21 katika kipindi cha mwaka 2014.



Takwimu hizo zimetolewa jana jijini hapa na Katibu Mkuu wizara ya Afya na ustawi wa jamii Dkt Donan Mmbando katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa nne wa  kazi kati ya wizara hiyo na wadau wanaofadhili mpango huo iliyosomwa kwa niaba yake na mkurugenzi wa idara ya huduma ya kinga katika wizara hiyo Dkt.Neema Rusibamayila.


Dkt. Rusibamayila alisema katika kipindi cha mwaka 2014/2015, mpango huo ulifanikiwa kuwafikia watanzania katika wilaya 110 na mikoa 17 ya Tanzania ikiwemo wanafunzi katika ngazi za shule ya msingi  na watoto wenye umri wa kwenda shule.


Hata hivyo alisema katika kwa mwaka huu mikoa minne  zaidi inayokabiliwa na tatizo la magonjwa hayo  imelazimika kuongeza idadi ya mikoa katika mpango huo ikiwemo mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Simiyu, , Geita .



"Leo ikiwa tunakutana hapa tunajivunia kazi tuliyoifanya kwa kuwa tayari Takwimu zinaonyesha wilaya 6 hazihitaji dawa za matende ugonjwa huo umeshamalizika, ugonjwa wa trakoma tulifanya utafiti wa awali wilaya31 tumegundua ni wilaya moja tu ya Chunya Mkoani mbeya ndio imekuwa ikihitaji dawa ,Vilevile thathmini ya  trachoma iliyofanyika katika  wilaya 28  imeonyesha kuwa  wilaya 19 zimefaulu hivyo kutohitaji ugawaji dawa wakati 9 zitaendelea na ugawahji dawa  za Zithromax,"alisema.


Kwa upande wake Mratibu wa Taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutoka wizara ya Afya na ustawi wa jamii Dkt. Upendo Mwingira alisema mpango huo wa Serikali umekuwa na faida nyingi kuliko changamoto.


"Baadhi ya changamoto ni pamoja na  utoaji huduma kwa wagonjwa wanaohitaji upasuaji hasa kwa wale ambao wamekwisha athirika na magonjwa haya hasa vikope na matende, tunawasiliana na wadau wetu ili kuwapatia huduma hii, lakini pia kuna tatizo la uelewa ijapokuwa wengi wamekuwa waelewa baada ya kutumia mbinu mbalimbali za kuwaelimisha umuhimu wa zoezi tunalokuwa tunafanya,"alisema.


Kwa upande wake Kaimu mganga mkuu wa Mikoa wa Arusha Dkt. Omar Chande, alisema zoezi la ugawaji wa dawa za kuzuia maambukizi ya magonjwa hayo limeenda vizuri na matokeo yanaonyesha zaidi ya asilimia 85 ya  watoto wenye umri wa kwenda shule walipata dawa  za kichocho na minyoo mnamo mwezi Mei 2015.  utafiti wa awali umeonyesha kuwa wilaya zote zimeathiriwa na baadhi ya magonjwa hayo.


Alisema Mkoa wa Arusha unajipanga kutoa tiba ya upasuaji wa  ugonjwa wa trakoma kwa wakazi wa wilaya za Longido na Monduli sanjari na kuendelea na zoezi la ugawaji wa dawa kwa wilaya zingine tatu Julai mwaka huu.

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE BUKOBA VIJIJINI,KESHO KUUNGURUA WILAYA YA MISENYI MKOANI KAGERA.

0
0

Wananchi wa kijii cha Rukoma kata ya Rukoma wakiwa wamekusanyika wakimsilikiza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara jioni ya leo Bukoba vijijini. 

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana yuko katika ziara ya kikazi  katika mikoa ya Kagera , Geita na Mwanza akikagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 huku akihimiza uhai wa Chama akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara katika kata ya Rukoma,Bukoba vijijini mkoani Kagera
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na ujumbe wake wakipokelewa katika uwanja wa Katoro,kwenye mkutano wa hadhara Bukoba vijijini mkoani Kagera jioni ya leo.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Ndugu John Mongela akizungumza na wananchi na kuwaleza kuwa wasitishwe na mtu yeyote katika suala zima la kujiandikisa," asiwatishe mtu nendeni mkatumie haki yenu ya kikatiba mkajiandikishe katika daftari la wapiga kura katika kata ya Katoro Bukoba Vijijini na wala msiogope",alisema Mh.Mongella. 
 Mbunge wa jimbo la Bukoba Vijijini Mh Jason Rweikiza akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Katoro Bukoba Vijijini.
 Wananchi wa Katoro wakimsilikiza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo wilayani Bukoba Vijijini mkoani Kagera.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia Wananchi wa kijiji cha Katoro jioni ya leo wilayani Bukoba Vijijini,mkoani Kagera.
 Wananchi waliokusanyika katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Katoro wilayani Bukoba vijijini,mkoani Kagera jioni ya leo
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia Wananchi wa kijiji cha Katoro jioni ya leo wilayani Bukoba vijijini,mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto , Mbunge wa jimbo la Bukoba Vijijini Mh. Jason Rweikiza katikati  na  Novatus Nkwama Mwenyekiti wa CCM  Bukoba Vijijini wakishiriki kufukia mabomba katika mradi wa maji unaotekelezwa na serikali  katika kata ya Ibyera Bukoba vijijini wakati Katibu Mkuu huyo akiendelea na ziara yake katika jimbo hilo leo.

 Katibu Mkuu huyo yuko katika ziara ya kikazi  katika mikoa ya Kagera , Geita na Mwanza akikagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 huku akihimiza uhai wa Chama akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye Kikao cha kupokea taarifa ya chama na serikali na kuzungumza na halmashauri kuu ya  Wilaya,kabla ya kuendelea na ziara yake katika wilaya ya Bukoba Vijijini leo. Kinana amewataka viongozi wote kutokuwa na wagombea wao mioyoni katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, pia amewataka wapambe wa viongozi kuacha umbea wa kuuza maneno kutoka huku kwenda kule kwa sababu hali hiyo ni chanzo cha fitina miongoni mwa viongozi na wanachama.
Baadhi ya Wananchi wa Kemondo wakishangilia jambo
Wananchi wa Kemondo wakifuatilia yaliyokuwa yakijri kwenye mkutano wa hadhara,Bukoba vijijini mkoani Kagera.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika leo, katika mji mdogo wa Kemondo,Bukoba Vijijini mkoani Kagera .
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika leo, katika mji mdogo wa Kemondo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa chama katika wilaya ya Bukoba Vijijini, mkoani Kagera.

Wananchi wakimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na Ujumbe wake walipokuwa wakiwasili katika kijiji cha Rukoma,Bukoba vijijini mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua rasmi Ofisi ya CCM ya Kijiji cha Rukoma, wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoka ndani ya Ofisi ya CCM ya Kijiji cha Rukoma aliyoindua leo, wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera,kulai ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na kulia ni Mbunge wa Bukoba Vijijini Mh.Jason Rweikiza

KATIBU MKUU WA CHADEMA DKT. WILLIBROD SLAA ZIARANI BARANI ULAYA

0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa ameondoka nchini Jumamosi Juni 06, 2015 kuelekea Bara la Ulaya ambako atakuwa na ziara ya kikazi ya siku nane.
Akiwa ziarani Dk Slaa anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbali mbali wa nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU) ambapo pia atakutana na jopo la wataalamu wa masula ya uchumi kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika kupata mifumo sahihi na kujenga taasisi za kusaidia uwajibikaji na kusukuma maendeleo ya watu katika nchi za Afrika hususan zile zenye rasilimali nyingi kama Tanzania ili kuziepusha na kile ambacho kimezikumba nchi nyingi duniani yaani ‘laana ya raslimali’ (resource curse).

Aidha, akiwa na viongozi wa nchi za Ulaya, Dk Slaa atajadiliana nao kuhusu hali ya Demokrasia, utawala bora na hali ya haki za binadamu nchini hasa kwa kipindi hiki ambapo Watanzania wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba. Katika ziara hiyo, viongozi hao wa Ulaya watapata fursa ya kujadiliana na Dk. Slaa hali ya siasa kwa Ukanda wa Afrika Mashariki.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Dk. Slaa ameambatana na Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri, John Mrema na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Tumaini Makene.

Itakumbukwa kuwa Katibu Mkuu Dk. Slaa amekwensa ziarani barani Ulaya akiwa ametoka kufanya ziara ya kikazi katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Kagera, Mbeya, Rukwa na Katavi akikagua zoezi la uandikishaji wapiga kura kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Kwa mfumo wa BVR huku pia akiwahamasisha Watanzania wote wenye sifa za kupiga kura kuhakikisha wamejiandikisha. 

Alitumia pia ziara hiyo kukagua maandalizi ya chama katika maeneo mbalimbali kwa kushirikiana na vyama washirika wenza katika UKAWA kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Dk. Slaa atarejea nchini tarehe 15.06.2015.

Ali Kiba na Abdul Kiba watua VOA

0
0
Kushoto promota wa Ali Kiba Marekani Dickson Mkama a.k.a DMK , Ali Kiba , Abdul Kiba na Sunday Shomari.2.Kina Kiba wakiwa na Kushoto mtangazaji wa VOA Khadija Riyami , Mamu na kulia kabisa Mr.Tz akifuatiwa na mtangazaji  Idd Ligongo na baadhi ya mashabiki wao waliofika kuwaona.

TBL YAPATA USHINDI WA USALAMA NA USAFI WA MAZINGIRA

0
0
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mushi (kushoto), akikabidhi Cheti cha ushindi wa kwanza kwa Meneja Usalama na Mazingira wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda, kutambua mchango wa TBL kutunza mazingira, wakati wa kilele cha Wiki ya Mazingira, iliyofanyika Dar es Salaam hivi karibuni.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), baada ya kushiriki katika zoezi la usafi wa mazingira katika soko la Mchikichini, Dar es Salaam
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto) akishirikiana na wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika soko la Mchikichini, Dar es Salaam jana, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya mazingira, ambapo TBL imesaidia vifaa mbalimbali vya usafi kwa Manispaa ya Ilala. Kulia ni Meneja wa Kiwanda hicho, Bw. Calvin Martine.

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto) na Meneja wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Bw. Calvin Mushi wakisukuma toroli zenye  takataka, baada ya kufanya usafi katika soko la Mchikichini, Dar es Salaam jana, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya mazingira, ambapo TBL imesaidia vifaa mbalimbali vya usafi kwa Manispaa ya Ilala.

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto) akimuaga Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu baada ya kushiriki katika maadhimisho ya wiki ya usafi katika soko ya Mchikichini Dar es Salaam jana, ambapo TBL imesaidia vifaa mbalimbali vya usafi kwa Manispaa ya Ilala. Kulia ni Meneja wa Kiwanda cha Bia Tanzania Bw. Calvin Martine.

 Baadhi ya wafanyakazi wa Manispaa ya Ilala wakishiriki usafi katika soko la Mchikichini, Dar es Salaam jana, baada ya Manispaa hiyo kupewa vifaa mbalimbali vya usafi vilivyotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Mazingira.

Baadhi ya wafanyakazi wa Manispaa ya Ilala wakishiriki usafi katika soko la Mchikichini, Dar es Salaam jana, baada ya Manispaa hiyo kupewa vifaa mbalimbali vya usafi vilivyotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Mazingira.

Viewing all 46193 articles
Browse latest View live




Latest Images