Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

GOLA KUWAONDOA WATOTO WA MITAANI JIJINI ARUSHA.

0
0
Afisa ustawi wa jamii na Maendeleo ya jamii jijini Arusha  Mwantumu Dossi
akitembelea mradi wa shamba la mahindi unaoendeshwa na taasisi ya Gola
Foundation jana katika kituo cha Kufikia watoto wa mitaani,katikati ni
Mkurugenziwa shirika hilo  Elisha Maghembe.
Habari Picha  na libeneke la kaskazini blog.
Mkurugenzi wa shirika lisilokua la kiserikali la Gola Foundation
,Elisha Maghembe amesema kuwa wameanza zoezi la  kuwaondoa watoto wa
mitaani walioko  jijini Arusha na kuwafikisha kwenye vituo maalumu vya
malezi lengo ikiwa ni kuwarudisha makwao pamoja na kuwapatia fursa ya
elimu waliyoikosa kwa muda mrefu.

Elisha alisema kuwa zoezi hilo limeanza mapema mwaka huu ambapo mpaka
sasa wamewakusanya watoto 25 na kuwapeleka katika kituo chao cha
malezi kilichopo wilaya ya Arumeru ambapo watoto watano walitambuliwa
na kuchukuliwa na wazazi wao.

Amesema kuwa watoto wa mitaani wanapokaa mtaani kwa muda mrefu
hujitumbukiza katika majanga ya matumizi ya madawa ya kulevya na
kufanya vitendo visivyofaa hivyo ameitaka jamii ishirikiane kutatua
tatizo hili ambalo ni janga kwa taifa.


“Tunapofika mtaani kuwaondoa watoto hawa wa mtaani tunakutana na
changamoto nyingi ikiwemo kukosa ushirikiano na watoto wenyewe na pia
wengine wanatumkishwa na ajira katika umri mdogo na baadhi ya watu
hivyo kufanya zoezi hilo kuwa gumu” Alisha Elisha

Afisa ustawi wa jamii na Maendeleo ya jamii jijini A Mwantumu Dossi
alifika katika kituo cha kufikia cha malezi ya watoto wa mtaani
kinachomilikiwa na Gola Foundation amesema kuwa Halmashauri ya jiji
itaangalia namna ya kushirikiana kutatua changamoto za watoto wa
mitaani.

“Tatizo la watoto wa mitaani ni tatizo sugu nimefika apa kujionea na
kama Jiji kuna mkakati Mahususi wa kuwaondoa watoto wa mitaani
utakaoanza 2015-2016” alisema Mwantumu

Mwenyekiti wa Baraza la watoto wilaya ya Arusha Hassan Omari alisema
kuwa juhudi za kuwaondoa watoto wa mitaani katika mazingira magumu na
hatarishi zinapaswa kuungwa mkono na kila mtu pamoja na serikali kwani
watoto ni taifa linalotegemewa kesho.

AMCO YASISITIZA MSHIKAMAO WA KIJAMII.

0
0
Na Swahilivilla Blog,  WASHINGTON DC.
 TANZANIANI muslim Community Washington DC na vitongoji vyake nchini Marekani (TAMCO) imesisitiza umuhimu wa umoja na mshikamao wa kijamii miongoni mwa wanajumuiya hiyo na Watanzania kwa ujumla wanaoishi katika maeneo hayo. 
Mwenyekiti wa Tanzanian Muslim Community Ndugu Ali Muhammed Shafi
 
Baadhi ya waumini wa  Tanzanian Muslim Community wakiwa katika mkusanyiko wa siku ya familia, ilioandaliwa rasmi na jumuiya hiyo,  Siku ya Jumapili June 6, waIslamu Washington DC.
Nyuma kabisa aliekuwa muasisi wa zamani wa Tanzanian Muslim Community in Washington DC (TAMCO) Bwana Yusuf Kalala akiwa na Shamis Alhatry, kushoto, Kulia ni Mwenyekiti wa ZADIA, pa moja na Mganga  katika sharehe ya familia Day Siku ya Jumamosi June 6, waIslamu Washington DC.
Baadhi ya waumini wa  Tanzanian Muslim Community wakiwa katika mkusanyiko wa siku ya familia, ilioandaliwa rasmi na jumuiya hiyo,  Siku ya Jumapili June 6, waIslamu Washington DC
Mwenyekiti wa Zanzibar Diaspora Association (ZADIA) Omar Haji Ally (kulia) akibadilishana mawazo na aliekuwa muasisi wa Tanzanian Muslim Community in Washington DC (TAMCO) Bwana Yusuf Kalala, kwenye sharehe ya familia Day Siku ya Jumapili June 6, waIslamu Washington DC (Picha zote na Abou Shatry).


Hayo yameeelezwa na Mwenyekiti wa TAMCO Ndugu Ali Muhammed Shafi alipokuwa akizungumza na Swahilivilla pembezoni mwa "Siku Ya Familia" iliyoandaliwa na Jumuiya hiyo, Siku ya Jumamosi June 6,  jijini Washington DC.
"Lengo kubwa la siku hii ni kuwakusanya pamoja wanachama wa jumuiya yetu na Watanzania wengine wanaoishi katika eneo hili hata kama si wanachama wa jumuiya yetu, kwa lengo la kusisitiza umuhimu wa Familia na mshikamano wa kijamii", alisema Ndugu Shafi, na kuongeza kuwa ni nafasi nzuri ya kujuana khususan kwa watoto.
Aliendelea kusema kuwa mkusanyiko huu ambao hufanyika mara moja kila mwaka una lengo pia la kufanya matayarisho ya mwezi Mrukufu wa Ramadhan, ambapo wanajumuiya huchangisha fedha kwa jili ya futari ya pamoja kwa mwezi mzima wa Ramadhani.
"Tayari TAMCO imeshaandaa kumbi maalum kwa ajili ya futari ya pamoja kwa muda wa mwezi mzima wa Ramadhani na matayarisho yote yameshakamilika, tunachosubiri ni kumkaribisha mgeni huyo Mtukufu" alisema Bwana Shafi, na kuwatolea wito wanajumuiya ambao bado hawajatoa ada zao za uanachama kufanya hivyo, ili kurahisisha na kufanikisha malengo ya jumuiya hiyo.
Akizungumzia malengo ya baadaye ya jumuiya hiyo, Bwana Shafi alisema kuwa wana lengo la kufungua madras kwa ajili ya watoto wanaoish Washington na maeneo ya karibu, ili kuhakikisha kuwa watoto wanapata elimu,malezi na mafunzo halisi ya Kiislamu.
Aliwatolea wito wanajumuiya kuitumia fursa ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa ajili ya kuongeza Ibada na Imani ndani ya mwezi huo na katika maisha kwa ujumla.
Siku Ya Familia ya TAMCO (TAMCO Family Day), hufanyika kila mwaka ambapo wanajumuiya hiyo na wengineo hukutanika pamoja kwa siku nzima, ambapo pamoja na mambo mengine, hutoa nafasi kwa watoto kucheza, kufurahi kujuana na kujenga urafiki tangu wakiwa wadogo.

Africa – A land worth exploring.

0
0
-->
26 May 2015: Africa Day 2015 is an opportunity to celebrate the development of the African continent as well as consider the various opportunities that it offers. This is according to Charles Brewer, Managing Director of DHL Express Sub-Saharan Africa (SSA), who not only believes that the continent offers vast opportunities but also that it is one of the last frontiers for economic growth and development.

Africa Day is the annual commemoration of the founding of the Africa Union (AU), and acts as a reminder of the continent’s rich culture, diversity as well as its resilience and the various developing economies on the continent.

Brewer explains that as DHL Express has been present in Africa for 37 years, the company has witnessed the turnaround from the ‘forgotten continent’ to ‘Africa Rising’, which has been an amazing and insightful experience.

“Despite the recent prediction by the World Bankthat economic growth in Sub-Saharan Africa will slow in 2015, the continent still remains relatively unexplored which indicates untapped opportunities in the region. We remain positive about Africa’s potential and believe that it’s time for the continent to focus on the opportunities, connect across the continent to leverage cross-border and global opportunities and grow as one.”

To meet the increased needs of the burgeoning middle class in the region, DHL Express has continued their aggressive expansion strategy in their efforts to make logistics more accessible. “With the rise of e-commerce, global markets are more attractive and accessible to individuals and local businesses, therefore we need to make sure that we are well positioned to cater to their needs. We currently have 3800 retail outlets across Sub Saharan Africa,” adds Brewer.

In the spirit of Africa Day, Brewer also points to one of the many projects conceptualized and implemented by DHL Express on the continent – DHL Africa as One - which highlights the company’s continuous commitment to investing in Africa.

 “As part of this epic journey, a team from DHL, the official logistics partner of Rugby World Cup 2015, is driving across Africa in three Land Rover Discoveries, while capturing every step of the journey, every person, every place and every pass on film, in photographs and words, and then sharing this content with Africa and the world. Part of the journey includes passing a single rugby ball from hand to hand through 45 African countries, over 11 months, from Cape Town and ending in London in September 2015.

We have passed the half way mark and the team is currently in Niger, en route to Chad. The tour is not just about rugby, but about showcasing Africa to the rest of the world and making an impact on the continent. In addition to the rugby clinics that take place as part of the journey, we are distributing over 500 000 units of stationery to young children and providing free eye tests for thousands of people, through our partnership with Mercy Ships.”

More than ever, global companies are now looking to expand into Africa and invest in its diverse markets and people. “DHL is committed to play a continued role in developing the continent through its investments and initiatives aimed at connecting Africa to the world,” concludes Brewer.
- Ends -

DHL – The logistics company for the world
DHL is the leading global brand in the logistics industry. DHL’s family of divisions offer an unrivalled portfolio of logistics services ranging from national and international parcel delivery, international express, road, air and ocean transport to industrial supply chain management. 

With more than 325,000 employees in over 220 countries and territories worldwide, they connect people and businesses securely and reliably, enabling global trade flows. 

With specialized solutions for growth markets and industries including e-Commerce, technology, life science and healthcare, energy, automotive and retail, a proven commitment to corporate responsibility and an unrivalled presence in developing markets, DHL is decisively positioned as “The logistics company for the world”.

DHL is part of Deutsche Post DHL Group. The Group generated revenues of more than 56 billion euros in 2014.

Media Distribution by Abel & Fernandes.

MABOMU YATAWALA CHUO CHA KAMPALA

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa Cha Kampala (KIU) leo wameandamana na katika chuo hicho kushinikiza warudishe fedha zao kutokana na kuanzisha kitivo ambacho hakitambuliki na mamlaka za nchi.

Mgomo huo umeanza majira ya saa tatu kwa baadhi wanafunzi kuwazuia wenzao wasiingie katika chumba cha mtihani na baada ya hapo wakaibuka na mabango kwenda katika ofisi za utawala wa chuo hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika chuo hicho,Rais wa Serikali wa Chuo Kikuu cha Kampala(Kiupeso),Elias Mbogho amesema kuwa maandamano hayo yametokana na baadhi ya wanafunzi waliohitimu ngazi ya cheti ya ufamasia kudai leseni na kuambiwa chuo hakitambuliki ndipo chanzo kiliazia hapo.

Mbogho amesema kuwa hatua mbalimbali zilishapita na kujiridhisha kuwa kinatambulika lakini wanafunzi wakitivo hicho wameendelea kuweka malumbano.

Afisa uhusiano wa chuo hicho ,Keneth Uki amesema kuwa mgogoro huo ulishapewa suluhu kwa kupitia hatua za mamlaka za serikali na kudhibitisha kutambuliwa chuo hicho.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Kimataifa Cha Kampala (KIU) wakiwa katika maandamano leo katika chuo hicho baada ya Kitivo cha Famasia kushindwa kutambulika na mamlaka mbalimbali.
 Askari wa Polisi wakiwa katika gari na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) waliowakamata katika maandamano hayo.
Rais wa  Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kampala (KIUPESO),Elias Mbogho akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maandamano yaliyofanyika leo katika hicho jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi,Jamal Mohamed.
 Wanafunzi wa KIU wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali.
 Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakiwa kazini  leo katika Chuo  Kikuu cha Kampala jijini Dar es Salaam.
 Mwanafunzi wa Chuo Kikuu  cha Kampala akiwa na majeraha katika maandano yaliyofanyika katika chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakiwa katika maandamano katika Chuo Kikuu  cha Kampala leo jijini Dar es Salaam.PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.

ZIARA YA RAIS KIKWETE NCHINI UHOLANZI.

0
0
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Watanzania waishio Uholanzi waliojitokeza kumlaki wakati akiwasili jijini The Hague, Uholanzi, leo Jumatatu Juni 8, 2015.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo na muhtasari wa ziara yake toka kwa Balozi wa Tanzania nchini Uholani Mhe Wilson  Masilingi baada ya kuwasili The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya mafuta ya Shell Bw. Ben van Beurden jijini the Hague, Uholanzi  leo Jumatatu Juni 8, 2015.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katikati wakati Waziri wa Zanzibar Mhe Ramadhani akigonganisha glasi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Mhe. Mark Rutte jijini The Hague  leo Jumatatu Juni 8, 2015.  Kushoto ni  Balozi wa Tanzania nchini Uholani Mhe Wilson  Masilingi.
Rais Jakaya Kikwete akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Mhe. Bert Koenders  jijini The Hague  leo Jumatatu Juni 8, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC Jaji Silvia Alejandra Fernandes de Gurmendi alipotembelea makao makuu ya mahakama hiyo jijini The Hague  leo Jumatatu Juni 8, 2015.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiwa  na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC Jaji Silvia Alejandra Fernandes de Gurmendi alipotembelea makao makuu ya mahakama hiyo jijini The Hague  leo Jumatatu Juni 8, 2015.
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Uholanzi Mhe Mark Rutte  jijini The Hague  leo Jumatatu Juni 8, 2015.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Mabalozi wa nchi mbalimbali za Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Uholanzi  jijini The Hague  leo Jumatatu Juni 8, 2015.

WATAALAM WA BIASHARA NA VIWANDA TANZANIA KUTEMBELEA CHINA KUSAKA FURSA ZA KIBIASHARA ZAIDI.

0
0

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dk Abdallah Kigoda (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 50 ya ziara Waziri Mkuu wa China Zhou Enlai nchini Tanzania zilizofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wa Kwanza kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Serikali ya Zanzibar, Mhe. Ali Juma Shamhuna, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Janet Mbene (wa pili kulia) na Balozi wa China nchini Tanzania Dk Lu Youqing (kulia). 

TIMU ya wataalam wa biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara na wafanyabiashara wengine wa nchini Tanzania wanatarajiwa kutembelea China baadaye Julai mwaka huu, ikiwa ni katika jitihada za kutafuta fursa za ki biashara ambazo zinaweza kutumika kuleta maendeleo nchini.

Hatua hiyo inakuja miezi michache baada ya ziara ya Rais Jakaya Kikwete nchini ambapo serikali ya China ilikubali kusaidia Tanzania katika maendeleo na uendeshaji wa Viwanda nchini.

Akizungumza wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 50 ya ziara Waziri Mkuu wa China Zhou Enlai nchini Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dk Abdallah Kigoda alisema kuwa kuna faida kubwa sana katika uchumi wa viwanda na jopo la watalaam hao wanaotarajiwa kutembelea nchi hiyo iliyopo Mashariki ya Mbali, litasaidia kutoa utaalam juu ya fursa za kibiashara ambazo zinaweza kutumiwa na Watanzania.

"Tutahakikisha kuwa mahusiano yetu haya kati ya China na Tanzania yanakuwa na manufaa pande zote mbili. Tumeendelea kukuza uhusiano mkubwa kati ya nchi hizi mbili na China, ambayo kwa sasa ipo kwenye safu ya nchi zenye nguvu zaidi kiuchumi duniani, imekubali ombi letu kutusaidia katika ukuaji  wa sekta ya viwanda," alisema Dk. Kigoda.

Dk Kigoda alisema uendeshaji mzuri katika sekta ya viwanda utasaidia kuinua uchumi wa watu nchini, ikiwa ukuaji wa biashara mpya na viwanda utajenga maelfu ya ajira mpya na kutoa fursa kwa watu wenye kipato cha chini kujiinua kiuchumi.

On hotuba yake, katika hafla hiyo, Balozi wa China nchini Tanzania Dk Lu Youqing alisema China imekuwa muwekezaji wa kigeni wa pili kwa ukubwa nchini Tanzania ikiwa imefikisha uwekezaji wa jumla ya dola za Kimarekani  bilioni 4 mwishoni mwa mwaka 2014.

"China pia ni mbia mkubwa wa biashara nchini Tanzania ikiwa na jumla ya biashara zenye thamani ya zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 4.3,” Balozi Dk. Youqing alisema.

Alibainisha kuwa Tanzania ni moja ya nchi tatu zilizopo kwenye mpango wa  China-Afrika wa ukuzaji wa Uwezo wa Ushirikiano katika Sekta ya Viwanda, huku Tanzania ni chachu ya kuonyesha mfano wa ushirikiano huo wa kirafiki wa China na Afrika.

"Kama rafiki wa kweli na mbia wa kuaminika wa Tanzania, China itazingatia nguzo za ushirikiano wa China-Afrika za ukweli, matokeo halisi, mshikamano na nia njema ambazo zilianzishwa na Rais Xi Jinping," alibainisha.

Balozi Dk Youqing alisema kuwa kutakuwa na uwekezaji zaidi wa China nchini Tanzania katika siku za  usoni hasa katika nyanja za miundombinu, mwanga/umeme na viwanda vikubwa na pamoja na habari na mawasiliano ya kisasa.

"Uwekezaji wa China nchini utazidi kuwa na manufaa makubwa kwa serikali ya Tanzania na watu wake kwa kulipa kodi na kutengeneza idadi kubwa ya ajira za wazawa," alisema.

WAZIRI BERNARD MEMBE ACHUKUA FOMU YA KUOMBA RIDHAA YA KUTEULIWA KUGOMBEA NAFASI YA URAIS 2015

0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe leo June 8, 2015 amechukua fomu za kuomba ridhaa ya kugombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma baada ya kutangaza nia hiyo jana (Jumapili). 
Waziri Membe akipokelewa fomu na Mkewe Dorcas mara baada ya kukabidhiwa fomu mjini Dodoma.  Alipokelewa na makada na wafuasi wa chama hicho mjini Dodoma baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Oganaizesheni, Seif Khatib ambapo baada ya kupokea fomu hiyo Membe alisema; “Ninafurahi kukabidhiwa fomu hii na nina hakika kutokana na kujipima na kujiona ninafiti nafasi hii kulinganisha na waombaji wengine ni lazima tubadilishe nchi yetu kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.”

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YAZINDUA HUDUMA ZA LESENI KWA NJIA YA MTANDAO- MAOMBI NA MALIPO YA LESENI KUFANYIKA KUPITIA MTANDAO

0
0
????????????????????????????????????
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akisoma hotuba ya uzinduzi wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao.????????????????????????????????????
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (katikati) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa huduma za leseni kwa njia  ya mtandao. Wa pili kutoka kulia ni Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Paul Masanja na wa kwanza kushoto  mbele ni Kamishna Msaidizi wa Madini- Kitengo cha Leseni, Mhandisi John Nayopa.????????????????????????????????????
Kamishna Msaidizi wa Madini- Kitengo cha Leseni, Mhandisi John Nayopa (Kulia)  akielezea mfumo wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao  unavyofanya kazi kabla ya kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Nishati na Madini, George  Simbachawene (wa pili kutoka kushoto, aliyekaa meza kuu).
????????????????????????????????????
Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Paul Masanja (Kulia) akielezea mafanikio  katika uboreshaji wa huduma za utoaji leseni kwenye uzinduzi huo.
????????????????????????????????????
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa nne kutoka kulia, waliokaa mbele); Kamishna wa Madini Nchini Mhandisi Paul Masanja ( wa tano kutoka kulia, waliokaa mbele) na Kamishna Msaidizi wa Madini- Kitengo cha Leseni, Mhandisi John Nayopa ( wa pili kutoka kushoto, waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini waliohudhuria uzinduzi huo.
????????????????????????????????????
Kikundi cha Ngoma za Asili cha Simba kutoka Dodoma (kushoto)  kikitumbuiza mbele ya  Waziri wa Nishati na Madini, George  Simbachawene (kulia katikati, aliyevaa koti la kahawia) kabla ya uzinduzi wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao uliofanyika mjini Dodoma.

…………………………………………………………………
Greyson Mwase na Samuel Mtuwa, Dodoma
Wizara ya Nishati na Madini imezindua mtandao utakaowezesha wachimbaji wa madini kutuma maombi ikiwa ni pamoja na kufanya malipo ya leseni za madini unaojulikana kwa jina la Online Mining Cadastre Transactional Portal (OMCTP).
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mtandao huo iliyofanyika mjini Dodoma, Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alisema kuwa lengo la mtandao huo ni kuwezesha shughuli za uchimbaji madini kufanyika katika uwazi na kukomesha rushwa.
Akielezea hatua mbalimbali katika uboreshaji wa huduma za leseni zilizopitiwa na Wizara Simbachawene alisema mwaka 1990 leseni zilishughulikiwa kwa njia ya mkono hadi kufikia mwaka 2005 ambapo Wizara ilianzisha mfumo wa kompyuta katika utoaji wa leseni uliojulikana kwa jina la MapInfo ambao bado ulitegemea uchambuzi kwa njia ya mkono.
Alisema ili kuboresha huduma ya utoaji wa leseni za madini, mwaka 2007 Wizara ilianzisha mfumo wa utoaji wa leseni za madini uliojulikana kama Mining Cadastral Information Management System (MCIMS) ambao uliwezesha ofisi za madini kuunganishwa kwa njia ya mtandao na kuwezesha uchambuzi wa maombi ya leseni kufanyika kwa njia ya kompyuta.
Alisema mfumo huo ulirahisisha sana upokeaji na uchambuzi wa maombi ya leseni na kurahisisha usimamizi wa leseni za madini.
Aliendelea kusema kuwa kupitia mfumo huo Wizara imeweza kupokea na kuchambua wastani wa maombi 1,400 ya leseni kubwa na 5,000 ya uchimbaji mdogo kwa mwaka.
Alisema mfumo huo umewezesha utolewaji wa wastani wa leseni 500 kubwa za madini na leseni zipatazo 1,500 za uchimbaji mdogo kila mwaka.
Waziri Simbachawene aliendelea kusema kuwa kuanzia mwaka 2010 Wizara iliendelea kuboresha mfumo wa flexicadastre chini ya Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali ya Madini (SMMRP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.
Alisisitiza kuwa maboresho hayo yalikuwa ni pamoja na kuwezesha uondoaji wa mlundikano wa maombi ya leseni, kuhuisha takwimu za leseni za madini na pia kuweka tovuti maalumu iliyowezesha wananchi kupata taarifa ya leseni za madini, maboresho yaliyochochea ari ya wananchi kufuatilia masuala ya leseni kwa njia ya mtandao, na kuweka uwazi katika usimamizi wa sekta ya madini kwa mujibu wa Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji Nchini (TEITI)
Aliongeza kuwa kufikia Mei, 2015 jumla ya leseni 3,500 za utafutaji mkubwa wa madini, leseni 14 za uchimbaji mkubwa wa madini, leseni 389 za uchimbaji wa kati na leseni 39, 921 za uchimbaji mdogo wa madini zilitolewa.
Alisisitiza kuwa kwa sasa Wizara imeamua kuboresha huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao kama utekelezaji wa agizo la serikali la kuhakikisha kuwa malipo ya serikali yanafanyika kwa njia ya kielektroniki.
Simbachawene aliongeza kuwa mfumo huo mpya utawawezesha wateja waliosajiliwa kutuma maombi, kuhakiki taarifa za leseni wanazomiliki, kutuma taarifa za utendaji kazi na kufanya malipo ya leseni na mrabaha kwa njia ya kielektroniki.
Alisema mfumo huu pia utawawezesha wateja kuoanisha ramani za maeneo ya leseni na ramani za kijiolojia zilizoandaliwa na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST)
Aidha, Waziri Simbachawene aliwataka wamiliki wa leseni na wananchi wote kwa ujumla kujisajili katika mfumo huo kwa kuwa lengo la Wizara ni kuhakikisha kuwa huduma zote za leseni zinakuwa kwa njia ya kielektroniki ifikapo Agosti 31, mwaka huu.
Pia aliwataka makamishna wa madini pamoja na watendaji wake kuhakikisha kuwa wanaweka utaratibu mzuri wa kuwasajili wachimbaji wadogo ili nao waweze kutumia huduma hizo la kielektroniki bila kikwazo.
Wakati huo huo akielezea faida za mfumo huo, Kamishna wa Madini Nchini Mhandisi Paul Masanja alisema kuwa mfumo huu unawawezesha wateja waliosajiliwa kutuma maombi, kuhakiki taarifa za leseni wanazomiliki, kutuma taarifa za utendaji kazi, kupata historia ya leseni zao, kuhuisha leseni zao, kuongeza ukubwa wa maeneo ya leseni zao na kufanya malipo ya leseni na mrabaha kwa njia ya kielektroniki.
Mhandisi Masanja aliongeza kuwa mfumo huu utawawezesha wamiliki wa leseni kuwa na usimamizi wa leseni zao kwani utakuwa ukimjulisha mmiliki wa leseni lini leseni yake inatakiwa kulipiwa na lini leseni yake itaisha
“Mfumo huu pia umesheheni takwimu mbalimbali za madini ikiwa ni pamoja na ramani za maeneo ya leseni na ramani za kijiolojia zilizoandaliwa na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST)” Alisema Mhandisi Masanja
Aliongeza kuwa, mfumo huu utawapunguzia mzigo watalam wa Wizara kwa kuwa wateja wenyewe wataingiza maombi ya leseni na hivyo wataalam kufanya uchambuzi kwa haraka zaidi na kupata muda wa kutosha kusimamia leseni zilizopo.
Alisisitiza kuwa mfumo huu umelenga kuondoa upotevu wa fedha za serikali kutokana na vitendo vya rushwa na makosa mengine ya kibinadamu.
Akielezea hatua iliyofikiwa ya usajili wa wateja katika mfumo huo, Mhandisi Masanja alisema tangu kuanzishwa kwa mfumo huo mwaka 2013 hadi sasa ni wateja 140 tu kati ya wateja wapatao 400 wamesajiliwa na wachimbaji wadogo 20 kati ya wamiliki wapatao 4,000 wamesajiliwa katika mfumo huo na kuwataka wadau wote waone umuhimu wa kujisajili na kutumia huduma hizi ili kuondoa matatizo ya ucheleweshaji wa kushughulikia maombi yao.
Mhandisi Masanja aliongeza kuwa kuanza kutumika kwa mfumo huu kunaiweka nchi ya Tanzania katika nchi chache za Afrika zilizo na mfumo wa kisasa wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao.

MFUMUKO WA BEI WAONGEZEKA NCHINI

0
0
1
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kuongezeka kidogo kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Mei 2015 leo jijini Dar es salaam.Mfumuko wa Bei  kwa mwezi Mei,2015 umefikia asilimia 5.3  kutoka asilimia 4.5 iliyokuwepo mwezi Aprili, 2015.
3
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo leo.
…………………………………………………………………..
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
 
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Mei 2015 umeongezeka hadi kufikia asilimia 5.3 kutoka asilimia 4.5 ya mwezi Aprili 2015 kutokana na kuongezeka kwa kasi ya upandaji wa bei ya  bidhaa na huduma katika maeneo mbalimbali nchini.

Mkurugenzi wa sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam amesema kuwa kuongezeka kwa mfumuko wa Bei nchini kumesababishwa na kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa za vyakula zinazotumiwa kwa wingi na kaya binafsi kwa mwezi Mei.

Amesema bidhaa za vyakula na zile zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko huo ni  Nyama,Choroko, Maharage,samaki, nyama,unga wa mihogo.

Kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni bei za mavazi ya wananume kwa asilimia 5.6, mavazi ya wanawake kwa asilimia 3.5, vyakula kwenye migahawa kwa asilimia 4.1 na huduma za malazi kwa asilimia 4.2.

Kuhusu Fahirisi za bei kwa maana ya namna bei zinavyopanda kutoka kipindi kimoja hadi kingine  kwa mwezi Mei zimeongezeka hadi kufikia 157.86  kutoka 157.21 za mwezi Aprili 2015 kutokana kuongezeka kwa bei ya  bidhaa za vyakula ambazo ni mahindi, unga wa mahindi, samaki wabichi, ndizi ,mbogamboga,viazi mviringo ,maharage na mihogo.

Kwa upande wa baidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa Fahirisi za bei kwa kipimo cha mwezi Kwesigabo amesema kuwa  Mafuta ya Dizeli ambayo yamechangia kwa asilimia 3.2 na na mafuta ya Petroli kwa asilimia 5.8.

Aidha,kwa upande wa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za mlaji kwa mwezi Mei , 2015 amesema umefikia shilingi 63 na senti 35 ikilinganishwa na kiasi cha shilingi 63 na senti 61 za mwezi Aprili 2015. 

“Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile kwa mlaji kwa mwezi Mei ,2015 na Aprili ,2015 umepungua, hii inamaanisha sasa mtu anahitaji kuongeza ziada ili aweze kununua bidhaa na huduma sawa sawa na zile alizokuwa na uwezo wa kuzinunua mwezi Mei”
Kwa upande wa mfumuko wa Bei wa mwezi Mei 2015 kwa nchi za Afrika Mashariki amesema kuwa una mwelekeo unaofanana , Kenya umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 6.87 na kutoka 7.08 mwezi Aprili,2015 huku Uganda mfumuko wa bei kwa mwezi Mei ,2015 ukiongezeka hadi asilimia 4.90  kutoka asilimia 3.60  za mwezi zilizokuwepo mwezi Aprili, 2015.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA TAMASHA LA BULABO KABILA LA WASUKUMA MKOANI MWANZA

0
0
6
Makamu wa Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akipiga Ngoma ishara ya Kuzindua Sherehe za  kimila za kabila la wasukuma zilizofanyika  kwenye kijiji  cha kisesaWilayani Magu Mkoa wa Mwanza jana.5
1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib  Bilal akisalimiana na Mwenyekiti wa Machifu wa Kisukuma Charles llago Kaphipa wakati wa sherehe za Kimila za wasukuma kwenye Tamasha la bulabo katika kituo cha bujoro Mkoani Mwanza Jana Tarehe 7/6/2015
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Dkt Mohammed Ghar Bilal  akishika jiwe la kutengenezea chuma wakati wa Uchifu kulia ni Mkurugenzi wa kituo cha Bujora Askofu Fabian Mkoja alipotembelea Maonyesho hayo Kijiji cha Kisesa wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza jana tarehe 7/6/2015 
3
Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akipata maelezo toka kwa Mkurugenzi wa kituo cha Bujora Askofu  Fabian Mkoja alipotembelea  Nyumba ya Mtemi wa kabila la wasukuma kwenye kituo cha  Bujora Mkoani Mwanza.4 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akiwapungia Mkono wananchi wa Kijiji Cha Kasesa wilaya ya Magu wakati alipowasili Uwanjani hapo kuzindua Tamasha la Kimila la wasukuma Mkoa wa Mwanza .

LOWASSA AZOA WADHAMINI 3,000 GEITA, CHATO NAKO APATA WA KUTOSHA

0
0
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa,(katikati), akipungia mkono maelfu ya wana CCM na wananchi wengine waliofika kwenye ofisi za CCM wilayani Geita Juni 8, 2015, kwa nia ya kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015; (Picha zote na K-VIS MEDIA)


Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge a Monduli, Mh. Edward Lowassa, akipokea fomu za udhamini za CCM baada ya ,kujazwa na wananchama wa CCM wilaya ya Geita, kwenye ukumbi wa CCM wilayani humo Juni 8, 2015. Mheshimiwa Lowassa, amedhaminiwa na jumla ya wanachama 3,000 wilayuani hapo
Wakazi wa wilaya ya Geita, wakiwa juu ya nyumba na juu ya mti (picha ya chini), ili kumuona Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa, alipowasili kwenye ofisi za CCM wilayani Geita, Juni 8, 2015 kuomba wana CCM wamdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015


Umati wa wana CCM waliofika kumdhamini Lowassa, na ananchi wengine waliofika walau kumuona wakiwa wamefurika nje baada ya ukumbi wa mikutano ofisi ya CCM wilayani Geita "kutapika" 


Waziri Mkuu a zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Losassa, akiwaaga wananchi na ana CCM waliofika kumdhamini kwenye ofisi za CCM wilaya ya Chato Juni 8, 2015.


Lowassa akiteremka kutoka ndani ya ndege, kwenye uwan ja mdogo wa mdege a mgodi wa Geita (GGM)

Lowassa, akiwapungia wana ccm waliofika kumdhamini baada ya kukabidhiwa fomu za udhamini zilizojazwa. Jumla ya wana CCM 3,000 walijitokeza kumdhamini

Wana CCM waliofurika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za chama hicho ilayani Geita, wakimshangilia Lowassa

Lowassa, akiondoka huku akiwa amezungukwa na umati wa watu nje ya ofisi za CCM wilayani Geita

UNGANA NA MWANDISHI SIMON KIVAMWO KUPAMBANA NA SARATANI YA UTUMBO

0
0


RAIS DK.SHEIN NA UJUMBE WAKE WATEMBELEA KAMPUNI YA MAGARI MERCEDES- BENZ

0
0
1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (watatu kulia) akiwa na ujumbe wake wakiapata maelezo kutoka kwa Adam Nowak M.A.Afisa  anaehusika na ufundi wakati walipotembelea katika Kampuni ya Magari ya Mercedes-Benz na kuangalia magari hayo yaliyotayari kwa kuingia sokoni Mjini Wurzburg nchini Ujerumani,[Picha zote na Ramadhan Othman,]
2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein   (katikati) na Mama Mwanamwema Shein (wa pili kulia) akiwa na ujumbe wake wakiangalia magari ya aina mbali mbali baada ya kupata maelezo kutoka kwa Adam Nowak M.A.Afisa anehusika na Ufundi wakati walipotembelea katika Kampuni ya Magari ya Mercedes-Benz na kuangalia magari hayo yaliyotayari kwa kuingia sokoni Mjini Wurzburg nchini Ujerumani.
3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein   (katikati) na Mama Mwanamwema Shein (wa pili kulia) pamoja na Viongozi waliofuatana nao katika ziara ya kikazi Nchini Ujerumani wakiwa na ujumbe wake wakiangalia mashine ya gari aina ya Mercedes -Benz na kupata maelezo kutoka kwa afisa anaehusika na ufundi Adam  Nowak M.A katika kampuni hiyo.
4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Adam Nowak M.A. Afisa anaehusika na ufundi  wakati alipotembelea katika Kampuni ya Magari ya Mercedes-Benz akiwa na ujumbe aliofuatana nao katika ziara ya kikazi nchini Ujerumani katika Mji wa Wurzburg ambaapo yapo tayari kwa mauzo.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendekeo ya Makazi Mh. William Lukuvi (MB) akitenda jambo na Watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mkuregenzi Mkuu wa Shirika hilo Bwn. Nehemiah Mchechu (kulia) na Meneja wa Shirika hilo Mkoa wa Dodoma, Bwn. Itandula Gambalagi.

0
0
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi (MB) akiwaonyesha waheshimiwa wabunge taarifa iliyoambatana na Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi yake kwa mwaka wa fedha 2015/16

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendekeo ya Makazi Mh. William Lukuvi (MB),  Bungeni  Dodoma leo Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2015/16

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendekeo ya Makazi Mh. William Lukuvi (MB)  akibadirishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bwn. Nehemiah Mchechu, baada ya kuwasilisha Bungeni  bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyimba na Maendeleo ya Makazi leo  Dodoma.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendekeo ya Makazi Mh. William Lukuvi (MB)  akitenda jambo na Watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mkuregenzi Mkuu wa Shirika hilo Bwn. Nehemiah Mchechu (kulia) na Meneja wa Shirika hilo Mkoa wa Dodoma, Bwn. Itandula Gambalagi.

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AENDELEA NA ZIRA YAKE WILAYANI MULEBA MKOANI KAGERA.

0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini.Prof Anna Tibaijuka pamoja na mkuu wa mkoa wa Kagera,John Mongella wakishiriki katika kazi ya utandazaji wa umeme wa REA katika shule ya sekondari ya Nyakatanga,jimbo la Muleba Kaskazini mkoani Kagera wakati wa ziara ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 pamoja kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi
 Umeme wa REA umesambazwa kwa kasi katika jimbo la Muleba Kaskazini,kama uonekanvyo katika nyumba hii katika kijiji cha Nshamba,wilayani Muleba mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Rushwa,jimbo la Muleba Kaskazini 
katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo na Diwani wa CHADEMA wa kata ya Mushabago,Respikius Feruz,baada ya kuhudhuria mkutano wa hadhara katika kijiji cha Rushwa,Diwani huyo alionekana kuvutiwa mno na maneno ya Ndugu Kinana na pia alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini,Mh.Charles Mwijage kwa kazi nzuri anayoifanya jimboni mwake.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana, akimshukuru mzee Mzee Abdulrajabu kwa kumzawadia zawadi baada ya kuhutubia wananchi katika kijiji cha Muleba mkoani Kagera. 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman  Kinana akikabidhi basikeli kwa ajili ya Makatibu wa CCM kata zilizopo jimbo la Muleba Kaskazini, baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara. Baiskeli hizo zimetolewa na Mbunge wa jimbo hilo Charles Mwijage (kulia).
 Katibu Mkuu wa CCM akikabidhiwa na Mbunge wa Muleba Kaskazini Mh.Charles Mwijage generata, kwa ajili ya kina mama wanaofanya shughuli za kilimo cha umwagiliaji.
  Vijana wanaofanya kazi katika mradi wa mabwawa ya kufugia samaki wa Ruhanga, katika Kijiji cha Izigo mkoani Kagera, wakiwa kazini leo .

 Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage akimpa maelezo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuhusu mradi wa mabwawa ya ufugaji samaki ya wajasiliamali, alipokagua mradi huo leo.  
Wananchi wa kijiji cha Izigo wakimshangilia  Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh Charles Mijage alipokuwa akiwahutubia katika mkutano huo.
 Wananchi wa kijiji cha Izigo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa hadhara.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahubia wananchi wa kijiji cha Izigo,Wilayani Muleba katika mkutano wa hadhara leo jioni.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akisisitiza jambo alipokuwa akiwahubia wananchi wa kijiji cha Izigo,Wilayani Muleba katika mkutano wa hadhara leo jioni.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (pili kulia) akikabidhi baiskeli kwa makatibu wa CCM wa Kata za jimbo la Muleba Kaskazini baada ya mkutano huo wa Izigo 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kulia) wakati akimtambulisha kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana, Mhariri wa zamani wa Tanzania Daima Asbert Ngurumo, ambaye alifika kwenye mkutano wa Katibu Mkuu huyo wa CCM  uliofanyika leo katika kijiji cha Izigo, wilayani Muleba.

 Sehemu ya jengo la ofisi hiyo ya CCM likiwa bando kukamilika
 Katbu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM Wilaya ya Muleba,anaetazama ni Mbunge wa jimbo la Muleba Kusini Mh.Prof Anna Tibaijuka.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana (haonekani pichani) akikagua na kupata maelezo kuhusiana na maendeleo ya mradi wa maji katika kata ya Nshamba wilayani Muleba mkoani Kagera,shoto ni Mkuu wa Mkoa wa kagera Mh.Jonh Mongella
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana (pili kushoto) akipata maelezo kuhusiana na maendeleo ya mradi wa maji katika kata ya Nshamba wilayani Muleba mkoani Kagera,shoto ni Mkuu wa Mkoa wa kagera Mh.Jonh Mongella
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwasalimia wananchi wa Kata ya Nshamba,wilayani Muleba mkoani Kagera.
 Wananchi wa Nshamba wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na ujumbe wake,wilayani Muleba.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipewa zawadi mbalimbali na wananchi wa Nshamba alipokuwa akondoka mara baada ya kumaliza kuwasalimia.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipata maelezo kuhusu mradi huo wa kompyuta kwa ajili ya wanafunzi kujifunzia masomo ya sayansi katika shule ya sekondari ya Nyakatanga. Kompyuta hizo zimetolewa na Mbunge wa Muleba Kaskazini Charles Mwijage (kushoto) na kulia ni Mbunge wa Muleba Kusini,Prof Anna Tibaijuka akishuhudia.

MBWA DOMO BAYA LAWAMANI KWA KUMTOROSHA BUNDI WA KAMANDA

0
0
Jumamosi ya 6 Juni 2015 inasemekana haikuwa nzuri katika kambi ya FFU -ughaibuni  baada ya msimu wa joto kuanza nchini ujerumani ,kikosi maalumu cha kuangalia wanyama kiliungana na Kamanda ras Makunja kumsaka Bundi wa  mkuu huyo wa Ngoma Africa Band,Bundi maarufu kwa jina la udi udi alichomoka katikabanda maalumu katika makao ya Ras Makunja marufu kama himaya ya Anunnaki Alien, Kutoroka kwa Bundi huyo kumesababishwa na mbwa wa kamanda aitwae  Kopro Dogi 

Domobaya, mbwa huyo anashutumiwa kwa kuwa mzembe na kuupiga kikumbo mlango wa banda la Bundi na kumfanya bundi kutoroka ,kamanda Ras Makunja aliwambia kikosi cha kuangalia wanyama kuwa "huyu mbwa si mlinzi mzuri siku hizi amekuwa na utoto sana !

Mbwa huyu tangu ampewe zawadi ya mpira watoto wa jirani yeye kazi yake ni kucheza na mpira mpaka kavunja banda la Bundi" Ras Makunja akilalamika na kudai kuwa huyu mbwa akiendelea  na uzembe nitamfuta kazi,Pia inasemekana midudu hiyo imetengewa eneo maalumu ktika himaya ya FFU-ughaibuni, Bundi huyo baadaye alirudi mwenyewe baada ya kutoweka kwa masaa kadha.

WARSHA YA VIJANA KATIKA MIPANGO YA MAENDELEO YA MKOA NA WILAYA YAFANYIKA JIJINI MWANZA

0
0
1Bw. Ramadhani Hangwa afisa kutoka UNFPA anaeshughulika na Program ya Idadi ya Watu na Maendeleo, akitoa neno kwa washiriki kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ili afungue semina hiyo.
2Mgeni Rasmi Bw. Ibrahim D. Kalengo, Mtakwimu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambae anamwakilisha Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, akitoa neno la ufunguzi kwa ajili ya warsha hiyo kuanza rasmi.
3Washiriki wa warsha kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita ambao ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo ya siku mbili inayofanyika katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza.
4Mwezeshaji  Dr. Deograsias P. Mushi ambae pia ni Mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mtafiti wa Ecom Research Group akishusha nondo kwa wanawarsha juu ya mambo mbalimbali yanayohusu ujumuishaji wa masuala ya vijana katika mipango ya Mkoa na wilaya.
5Washiriki wa warsha kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita ambao ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya wakimsiliza kwa makini mwezeshaji.
6Afisa kutoka UNFPA anaeshughulika na vijana Bi. Tausi Hassan, akiwashukuru washiriki kwa kuitikia wito na kushiriki kikamilifu warsha hiyo.
Tume ya Mipango kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) Tanzania, wameandaa warsha ya kuhamasisha na kujenga uwezo kwa watumishi wa Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu kujumuisha masuala ya vijana katika mipango ya Mkoa na wilaya.
Warsha hiyo inafanyika katika vituo vya Mwanza na Musoma. Katika kituo cha Mwanza warsha inafanyika tarehe 8 na 9 Juni 2015, kituo ambacho kinajumuisha Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita.
Washiriki wa warsha hii ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya.

FILAMU KUBWA YA MPANGO MBAYA YA TMT KURUSHWA MLIMANI CITY CINEMA 12.JUNE.2015.

0
0
ILE Filamu kubwa iliyoshirikisha wasanii mahiri kutoka Tanzania movie Talent Top Ten 2014(TMT) ipo tayari na inatarajia kuonyeshwa katika jumba la sinema la Mlimani City Cinema Tarehe 12.June. 2015 ni siku ya Ijumaa na itarfuka kwa siku tatu Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.


Sinema hiyo ambayo imeshirikisha wasanii wakali wenye elimu ya uigizaji kutoka kwa wakufunzi kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam imerekodiwa katika viwango vya kimataifa ndio maana inaanza kurushwa katika majumba ya sinema na kuingia sokoni katika Dvd siku ya Jumatatu tarehe 8.June 2015.

Filamu ya Mpango Mbaya ilitengenezwa baada ya shindano la kuibua vipaji kutoka mikoa mbalimbali kumalizika na kubaki na wasanii Bora 10 ambao walipata ofa ya kurekodi sinema hiyo ambayo imekidhi vigezo vya kimataifa ikiwa ni kampeni ya kampuni ya Proin Promotios kujenga mazingira wasanii kufika kimataifa.

Wasanii wanaofanya sinema hiyo kuwa ni ya kipekee ni Mwanaafa Mwinzago mshindi wa milioni 50, Isarito Isaya, Aneth Peter, Tishi Abdalah, Macdolnard Mapunda, Chiki Mchoma, Kaparata Mtawana wasanii wakali kibao wanaofanya vinzuri katika tasnia ya filamu Swahilihood.

Filamu ya Mpango mbaya kutoka kampuni ya Kizalendo ya Proin Promotions Ltd, imetayarishwa na Staford Kihore, na kuongozwa na Muongozaji mahiri wa kimataifa Karabani muandishi wa Muswada ni Novatus Nago Mugurusi ni kazi iliyojaa ujuzi wa kutukuka.

Sinema ya Mpango Mbaya itaingia rasmi katika soko katika mfumo wa Dvd na kusambazwa na kampuni ya usambazaji ya Proin Promotions ya jijini Dar es salaam, ambaye ndio mtayarishaji mkuu, kampuni iliyojitoa kuibuka nyota wapya kutoka popote walipo Tanzania.
 Ashi Abdalah katikati akiwa na wasanii Tmt 2014
Macdolnard Mapunda nae ni mmoja ya waigizaji katika filamu ya Mpango Mbaya ya TMT.

Mtoto mwigizaji,Mwanaafa Mwinzago akiwa ameshiriki katika Filamu ya Mpango mbaya ya TMT.

RAIS MSTAAFU, ALLY HASSAN MWINYI MGENI RASMI MASHINDANO YA MAGARI.

0
0
 Rais wa Chama cha Mashindano ya Magari Tanzania,Nizar Jivani akizungumza kuhusiana na mashindano ya magari katika hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam,mashindano yatakayofanyika Juni 12 mwaka, kushoto ni Mkurugenzi wa mashindano ya magari,Satnder Birdi na  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya gesi ya Oryx, Godfrey Frenarden.
 Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya gesi ya Oryx, Godfrey Frenarden, akizungumza kuhusiana na mashindano ya magari hayo na jinsi yatavyakuwa yanafanyiwa ukarabati baada ya mashindano hayo kulia ni  Rais wa Chama cha Mashindano ya Magari Tanzania,Nizar Jivani na  Mkurugenzi mkuu mtendaji  wa  Chama cha Mashindano ya Magari,Yusuf Ghor.
Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga akizungumza kuhusiana na watakavyokabiliana na usarama wa wananchi na Usalama wa barabarani wakati wa mashindano ya magari yatakayofanyika jijini Dar es Salaam na kumalizikia wilaya ya Kisarawe. Mkoani Pwani.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Oryx wakifuatilia kwa makini mkutano wa wadau wa Mashindano ya magari yatakayoanzia jijini Dar es Salaam.(Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)

Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
 Rais mstaafu, Ally Hassan Mwinyi kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya magari yatakayo fanyika Juni 12 hadi 14 mwaka huu kuanzia  katika hotel ya Sourthen Sun jijini Dar es Salaam na kuishia wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.

Hayo yamesemwa na Rais wa Chama cha Mashindano ya Magari Tanzania,Nizar Jivani wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Sourthen Sun jijini Dar es Salaam leo.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya gesi ya Oryx, Godfrey Frenarden amesema kuwa watakuwa wadhamini wa mashindano hayo ambayo yatafanyika Juni 12 mwaka huu.

Aidha Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga amewaasa wananchi kuchukua tahadhari katika mashindano hayo na kukaa mbali na barabara ambazo zinaweza kutumiwa na waendesha magari kwani mashindano hayo hayatafuata foleni za hapa jijini Dar es Salaam.

Pia amesema kuwa wanaoendesha magari ya mashindano hayo lazima wachukue tahadhari na kujikinga wao wenyewe katika mashindano hayo kwami kila mtu alinde usalama wake binafsi.

Mashindano hayo yatahusisha nchi tatu ambapo kila nchi itakuwa na waendesha magari ya mashindano wawili  kwa kila nchi, ikiwa madereva wa Tanzania, Uganda na Kenya.

WANAWAKE MUFINDI WAMWANGUKIA, MWENYEKITI WA UWT MUFINDI MARCELINA MKINI UBUNGE JIMBO LA MUFINDI KUSINI.

0
0
mwenyekiti wa UWT Mufindi na mjumbe wa NEC Taifa Bi Marcelina Mkini akiwapongeza  wanawake kwa kuonyesha kumkubali.
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi Bi Marcelina Mkini wa kwanza kushoto akiwa na mkuu wa wilaya ya Mufindi Mboni Mhita na mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa Bi Zainabu Mwamwindi wakati wa kongamano la wanawake wilayani Mufindi.

Na MatukiodaimaBLOG
 WAKATI joto  la uchaguzi  mkuu likiendelea  kushika kasi ndani ya chama  cha mapinduzi (CCM) kwa  wanachama  wake kujitokeza kutia nia ya kuwania urais ,ubunge na udiwani , umoja  wa wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Mufindi umemuomba mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi Marcelina Mkini kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Mufindi  kusini .


Wakizungumza mara baada ya  kumalizika kwa  kongamano la UWT wilaya ya Mufindi wajumbe wa kongamano  hilo  walisema  kuwa  toka nchi ipate  uhuru  wake  mwaka 1961  wilaya ya Mufindi mkoani Iringa haijapata  kuwa na mbunge mwanamke  hivyo kwa uchaguzi wa mwaka  huu lazima wanawake wachukue nafasi ya  kuongoza ubunge jimbo la Mufindi kusini ambalo kwa  sasa  linaongozwa na mbunge Mendrady Kigola (CCM).



Akizungumza kwa  niaba ya  wenzake mjumbe wa UWT Mufindi Bi Anna Nyamba kutoka  kijiji  cha Nyololo  alisema  kuwa wamevutiwa na utendaji kazi  wa mwenyekiti  wao Bi Mkini na  kuwa wamepata  kuwa na wenyeviti  wengi  wa UWT ndani ya wilaya ya Mufindi ila hawakuweza  kuifanya  jumuiya hiyo  kuwa hai kama  ilivyo  sasa .




Hivyo  alisema kazi nzuri  iliyoonyeshwa na mwenyekiti  huyo ndani ya UWT kuna  uwezekano mkubwa zaidi wananchi  wa  jimbo la Mufindi kusini iwapo  watamchagua kuwa mbunge  wa  jimbo  kasi ya maendeleo  inaweza  kuongezeka  zaidi .




Bi Nyambo  alisema  kipimo cha  utendaji wa mwenyekiti huyo ni katika nafasi yake ya  ujumbe  wa NEC Taifa  akiwakilisha  wilaya ya Mufindi japo kazi mbali mbali za  kimaendeleo alizozifanya kwa  kukiwezesha chama cha mapinduzi kuwa hai kupitia jumuiya  hiyo ya UWT ni kielelezo  tosha kuwa  iwapo atakubali  kugombea  ubunge na  kushinda nafasi hiyo sura  mpya ya maendeleo itaonekana katika  wilaya ya Mufindi.


" Sisi kama UWT Mufindi tutamuunga mkono mwanamke  mwenzetu ambae kazi zake  zimeonekana katika nafasi hii ya ubunge...leo jimbo letu halina barabara za uhakika na tunaopata shinda ni  wanawake na  watoto huduma za maji jimboni hakuna hivyo  tunataka kuwapa  wanawake watuongoze  "



Bi  Aida Kaduma mjumbe  kutoka  kijiji  cha Lufuna kata ya Mtwango alisema kuwa uwezekano  wa Marcelina  kuwatumikia  wananchi wa jimbo la Mufindi  kusini ni mkubwa kwani tayari kuna kazi nyingi za kimaendeleo ambazo amepata  kushirikiana na  wananchi  kuzitekeleza kama mwenyekiti  wa UWT wilaya  hiyo .




Alisema kwa upande wa kijiji chake shule ya msingi Lufuna ilikuwa haina  nyumba ya mwalimu mkuu ila kwa  jitihada  zake aliweza kuchangia bati  zote 40 za kuezekea nyumba  hiyo na  sasa nyumba  hiyo  imekamilika na mwalimu anaishi .




Pia  alisema mbali ya kusaidia sekta ya  elimu amepata  kuchangia taasisi mbali mbali za kiserikali na dini katika jimbo la Mufindi ambako amepata  kualikwa kama mgeni rasmi na  kuwa matumaini ya wanawake Mufindi  kusini ni kuona wanawake wanachukua nafasi ya ubunge .

 
Kwa  upande wake mwenyekiti  huyo Bi Mkini mbali ya  kuwapongeza wajumbe hao kwa ushawishi wao huo bado  alisema bado  anatafakari juu ya maombi hayo.



Japo  aliwataka  wanawake kwa mwaka  huu  kujitokeza kwa  wingi  kugombea nafasi za udiwani na ubunge katika wilaya  hiyo ya Mufindi ili  kuongeza chachu ya maendeleo na kuondoa  watu kujisahau katika nafasi zao.


Katika   kinyang'anyiro  cha kuomba  kuteuliwa  kugombea  ubunge ndani ya CCM mwaka 2010 jimbo la Mufindi  kusini  lilikuwa na wanachama 11 waliojitokeza  kuwania nafasi hiyo ambayo Bw Mendrady Kigola alishinda



Wengine waliojitokeza ni Thomas Bangu  ,Hassan  Kalinga , aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Benitho Malangalila , Faustine Mhapa ,Michael Mlonganile ,Mstapher Msovela ,Mary Ngailo ,Dr Alex Sanga, Marehemu Sprian Tweve na Marcelina Mkini




katika  kinyang'anyiro  hicho nafasi ya kwanza  ilichukuliwa na Kigola wakati nafasi ya  pili ilichukuliwa na marehemu Tweve na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Bi Mkini.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images