Mkurugenzi wa kitengo cha Mauzo Mustapha Kapasi( kushoto) pamoja na Gaspa Mroso waakiongea na wateja wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembea wateja wake na kutoa elimu ya huduma zao ikiwemo Airtel Yatosha.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso akiongea na meneja wa Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembea wateja wake na kutoa elimu ya huduma zao ikiwemo Airtel Yatosha inayompa mteja, Simkadi moja, taifa moja na bei moja.
Meneja wa kitengo cha network, Emmanuel Luanda akisajili wateja kwenye huduma ya Airtel Yatosha wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembea wateja wake na kutoa elimu ya huduma zao ikiwemo Airtel
Yatosha mwishoni mwa wiki hii
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso Akibandika moja ya kipeperushi cha Airtel yatosha wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembea wateja wake na kutoa elimu ya huduma zao ikiwemo Airtel Yatosha inayompa mteja, Simkadi moja, taifa moja na bei moja.
Afisa Mauzo wa Airtel bi Theresia Kimaro Akiongea na wateja juu ya huduma ya Airtel yatosha wakati Airtel walioko Magomeni na kutoa elimu juu ya huduma mbalimbali ikiwemo ya Airtel yatosha.
========== ============ =========
AIRTEL YATOSHA YAENDA MIKOANI
* Uzinduzi wa huduma Yatosha wafanyika rasmi Mwanza , Kanda ya
ziwa waanza kupiga simu kwa gharama nafuu
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea kusambaza huduma ya
Airtel yatosha katika mikoa mbalimbali nchini baada ya kuzindua huduma
mpya ya punguzo la upigaji simu maarufu kama Airtel YATOSHA katika
mikoa ya kanda ya ziwa.
Airtel sasa imeanza kuitambulisha huduma hiyo kwa wadau na wateja
wake katika mikoa mbalimbali nchini ili waweze kunufaika nayo
Huduma ya Airtel Yatosha inamuwezesha mtumiaji wa mtandao wa Airtel
kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama ya chini kabisa na hivyo
kutokuwa na haja tena ya kubadilisha kadi ya simu pindi anapohitaji
kuongea na mtu wa mtandao mwingine.
Akionge wakati wa utambulisho wa huduma ya Airtel Yatosha kwa wadau
wa Airtel jijini Mwanza, Meneja wa kampuni hiyo kanda ya ziwa Ally
Maswanya alisema" Tumeamua kushusha gharama hizo kutokana na maagizo ya mamlaka ya mawasiliano ambayo iliagiza gharama za simu kushushwa kutoka shilingi 112 kwa dakika hadi shilingi 34.92.
kwa sasa huduma ya airtel yatosha ina punguzo la hadi asilimia 88 na inalenga kurahisisha mawasiliano kwa wateja wa hali zote kwa kuwawezesha kutumia kiwango kidogo cha fedha kupata muda wa maongezi wa kuanzia dakika 10 kupiga mitandao yote ,meseji bila kikomo na huduma ya internet".
Punguzo hilo la bei linatoa faraja kwa watumiaji wa mtandao huo kwa
kuwa litawawezesha kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho walikuwa
wakikitumia hapo awali. Aliongeza Maswanya.
Akiongea wakati wa halfa ya uzinduzi Mteja wa Airtel na mkazi wa
Mwanza Bi Agness Emmanuel alisema" Aritel yatosha sasa ndio suluhisho
la mawasiliano ya simu ya bei nafuu, tunashukuru Airtel kwa kutoa
vifurushi vingi na vya bei nafuu vinavyokidhi adha ya sisi wateja.
huduma hii itatuletea urahisi wa mawasiliano bila haja ya kuwa na simu
nyingi na usumbufu wa kuwa na line nyingi. Kwakweli Airtel yatosha
itakuwa ni mkombozi katika mawasiliano.
Kwa upande wake Bwana Brighton Maisel moja ya wateja waliohudhuria
uzinduzi huo alisema"ni kwa muda mrefu sasa mawasiliano ya simu za
mkononi kwenda mitandao mingine yamekuwa ya gharama za juu hivyo
nashukuru sana serikali kuweka sheria ya kupunguza bei kati ya
mitandaa na Airtel kwa kutii na kuja na Airtel yatosha ambayo sasa
inatuwezesha kuwasiliano kwa bei nafuu na wateja wote wa mitandao ya
simu za mkononi mingine"
Airtel wiki hii pia bado itaendelea kufanya uzinduzi wa huduma hii
katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Arusha, Dodoma ikiwa ni mwendelezo wa
kuwafikia watanzania na kuwaelimisha kuhusu huduma hii ya Airtel
Yatosha Kujiunga na huduma hii mteja anatakia kupiga *149*99# na kuunganisha moja kwa moja kwenye orodha ya huduma hii na kuchagua kifurushi anachokipenda na kuweza kujipatia dakika za maongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet.