Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

MWANDISHI WA HABARI MWANDAMIZI AKIMWAGA SERA ZAKE WAKATI ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UDIWANI KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA SONGEA MKOANI RUVUMA


KATIBU MKUU WA CCM KOMREDI KINANA AHANI MSIBA WA MAREHEMU MHE.SAMUEL LUANGISA MJINI BUKOBA LEO

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitia saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo ya Marehemu Jaji Mstaafu Samuel Luangisa nyumbani kwake kwa marehemu Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera.Marehemu Luangisa ni miongoni  mwa Waasisi wa Taifa na katika vipindi tofauti tofauti alikuwa mkuu wa Mkoa wa Ziwa Magharibi (Kagera),Mbunge na Meya wa Manispaa ya Bukoba pamoja na nyadhifa nyingine.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Jaji Mstaafu Samuel Luangisa mapema leo asubuhi nyumbani kwake kwa Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera.
Katibu Mkuu Ndugu Kinana na baadhi ya maofisa wa chama na ndugu na jamaa wa marehemu wakishiriki sala ya pamoja na kumuombea marehemu Mzee Samuel Luangisa nyumbani kwake Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera
Katibu Mkuu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitia saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo ya Marehemu Mh. Samuel Luangisa nyumbani kwake mapema leo asubuhi,Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera.

PICHA NA MICHUZI JR-BUKOBA.

LOWASSA ASHIRII JUBILEE YA MIAKA 50 YA SEMINARI YA MTAKATIFU KALOLI LWAHANGA, HUKO NGARA

$
0
0

Waziri Mkuu Mstaafu, na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, (wapili kushoto), akiwa na Askofu  wa Jimbo Katoliki la Lulenge Ngara, mkoani Kagera, Severine Niwemuguzi baada ya kuzindua jiwe la msingi kuashiria maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50, Seminari ya Mtakatifu Kaloli Lwahanga Katote Jimbo Katoliki la Lulenge Ngara, Jumamosi Juni 6, 2015.



Waziri  Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa, akisalimiana na Askofu  wa Jimbo Katoliki la Lulenge Ngara, Severine Niwemuguzi, baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege Biharamulo Mkoani Kagera kwa ajili ya kusherekea Miaka 50 ya Seminari ya Katote



Lowassa, akiwasha kompyuta baada y kuzindua chumba cha mafunzo ya Kompyuta katikaKuadhimisha Jubilei ya Miaka 50 Seminari ya Mtakatifu Kaloli Lwahanga Katote Jimbo Katoliki la Lulenge Ngara mkoani KageraJumamosi Juni 6, 2015. Kushoto ni  Askofu  wa Jimbo Katoliki la Lulenge Ngara, Severine Niwemuguzi


SHEIKH SHARIFU MSOPA ATOA OFA YA MAOMBI KWA VIONGOZI NA WANANCHI KUTUMIA MAFUTA MAALUMU TOKA GUBA YA UAJEMI KUWAPAKA

$
0
0
 Sheikh Sharifu Msopa akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo Hoteli ya Shamoloon iliyopo Sinza kuhusu maombi hayo maalumu.
  Sheikh Sharifu Msopa (kulia), akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo Hoteli ya Shamoloon iliyopo Sinza kuhusu maombi hayo maalumu. Kshoto ni Sheikh Maulana Salim.
 Sheikh Maulana Salim (kushoto), akizungumza na wanahabari katika mkutano huo.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali na bloggers 
wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

SHEIKH Sharifu Msopa ametoa ofa kwa viongozi na wananchi nchi nzima ya kuwafanyia maombi pamoja na kuwapaka mafuta maalumu ya uponyaji kutoka Guba ya Uajemi.

Sharifu Msopa ametoa ofa hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, ambapo alisema walengwa zaidi ni watu maskini, viongozi mbalimbali wale waliotangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu.

Alisema lengo la maombi hayo ambayo hayachagui dini ni kuwapata viongozi waliochaguliwa na mungu ambao wataliongoza taifa wakiwa na hofu ya mungu.

"Maombi tutakayofanya hayambagui mtu na dini yake kwani tumekuwa tukitoa huduma hii ya maombi bure kwa kushiriana na wenzetu wa kristo na tayari baadhi ya viongozi tumeanza kuwafanyia maombi  na yule aliyetayari awasiliane nasi" alisema Sharifu Msopa.

Msopa alisema suala hilo la imani ni muhimu sana hasa katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu na kuwa lengo kubwa ni kuona nchi inapata viongozi waliobora na si bora viongozi kupitia maombi yao.

Alisema baada ya kufanyiwa maombi mtu husika atapakwa mafuta ya ajabu kutoka Guba ya Uajemi ambayo yananguvu ya kuondoa mikosi, uchawi na kumletea bahati muombewaji.

Alisema hivi sasa wapo katika maombi ya mwezi mzima ya kuwaombea, viongozi wa siasa serikali, wafanyabiashara, maskini na makundi mengine ili wapate neema hiyo.

Msopa alisema anaamini kuwa kupitia maombi kiongozi mzuri atapatikana kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge na urais na kuwa mara baada ya mtu husika kupakwa mafuta hayo kama atakuwa na uchawi, nuksi na mambo mengine yatamtoka kwa njia ya kuharisha, kutapika na kumfanya awe huru.

Alisema maombi hayo anatarajia kuyafanya nchi nzima kwa kukutana na makundi ya watu mbalimbali wakiwemo wanafunzi.

Alisema kwamba maombi kama hayo amekuwa akiyafanya katika nchi mbalimbali duniani na yamewasaidia watu wengi kutoka dini zote za kikrito na waislamu na amekuwa akiyafanya bure. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

CHADEMA WAIKUNA ARUSHA

$
0
0
 Profesor Jay akihamsisha wananchi kujitokeza kwenda kujiandikisha "NDUGU ZANGU WANA WA ARUSHA NA TANZANIA KWA UJUMLA TUJITOKEZE KUJIANDIKISHA ILI TUJIHAKIKISHIE UHURU WA KWELI NA SIO MATUMAINI"
 Mbuge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari amewataka watanzania kutambua muda wa mateso waliyoyapata kwa Miaka Mingi sasa yamefikia ukomo,"Njia pekee iliyobaki ndugu zangu ni kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la Mpiga kura"
Pia ametambulisha AMBULANCE 2 alizo zitoa kwenye jimbo lake
Mbuge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari akitambulisha  AMBULANCE 2 alizo zitoa kwenye jimbo lake
 umati wa wananchi waliouthuria katika mkutano huo wa chadema jana jijini Arusha
Mjumbe wa Kamati kuu na Mbunge wa Viti Maalum Mh Grace Kiwelu amewataka Wanawake kuwa Chachu ya mabadiliko kwa Taifa letu."MUDA WA KUDANGANYWA KWA KANGA UMEPITA TUJITOKEZE KUJIANDIKISHA ILI OCTOBER TUPATE UHURU WA UHAKIKA,WANAWAKE TUKIAMUA TUNAWEZA"

Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema ambaye pia ndiye aliyeteuliwa na Chadema Kanda Ya Kaskazini kuwa kiongozi wa kampeni za Hamasa ya kujiandikisha kanda ya kaskazini amewaambia wananchi wa Arusha kuwa safari ndio imeanza sasa kuelekea majimbo yote 33 ya kanda ya kaskazini kuhakikisha Watanzania wanajiandikisha kwa wingi ili October tufanye maamuzi sahihi

Mbunge wa Rombo Joseph Selasini" WATANZANIA WENZANGU HUU NDIO MUDA MUAFAKA WA KILA MMOJA WETU KUJIANDIKISHA ILI IKIFIKA OCTOBER TUWE TUNAFANYA MAAMUZI YA UHAKIKA NA SIO SAFARI YA MATUMAINI"

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Manyara Mh Pauline Gekul awatakwa Watanzania kujiandikisha na kuhamasishana kwa wingi wetu kwa kutumia simu mitandao ya kijamii vikao vya kijamii ili ifikapo October tuiondoe CCM madarakani.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Mh Cecilia Daniel Paresso amewataka Vijana na Akina Mama kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha ili ikifika October waweze kufanta maamuzi ya UHAKIKA na sio ya maamuzi ya MATUMAINI

 
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Mh Rebecca Mgodo amewataka wananchi kusoma nyakati"NDUGU ZANGU MIAKA YA MATESO KWA WATANZANIA SASAS IMEFIKA MWISHO, TWENDENI KWA UMOJA WETU TUKAJIANDIKISHE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURATUITOE CCM MADARAKANI"-Mgodo

Mwenyekiti wa Chadema Kanda Ya Kaskazini Mh Israel Natse akiwaongoza viongozi na Wabunge wa Chadema Kanda ya Kaskazini kuingia uwanjani huku wakiwapungia wanachama na wapenzi wa Chadema waliofika uwanjani vya kilombero (PICHA NA WOINDE SHIZZA)

Mwonekano WA MRADI WA VIWANJA VYA MIKOPO MAENEO YA VIKURUTI

$
0
0
Huu ndio muonekano mzuri unavvyoonekana maeneo ya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani kunapoendeshwa mradi wa viwanja vya mikopo kwa watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali. Picha na Mpigapicha wetu.

KAAZI KWELI KWELI

Wakazi wa Jiji la Dar Wajitokeza kwa wingi kushiriki Shindano la TMT 2015

$
0
0
 
 Baadhi ya wafanyakazi wa TMT wakiwahudumia watanzania waliojitokeza kwaajili ya kushiriki shindano la TMT 2015 kwa furaha 
Baadhi ya washiriki wakisubiria kuingia kwa majaji tayari kwa kuonyesha uwezo wao wa kuigiza
Baadhi ya vijana waliojitokeza kwaajili ya usajili wa kushiriki shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 #mpakakieleweke wakisikiliza maelekezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya Proin Promotions Ltd ambao ni waendeshaji wa shindano hilo katika viwanja vya makumbusho ya taifa jijini Dar Es Salaam.
 Baadhi ya washiriki waliojitokeza kwaajili ya kuonyesha viapji vyao vya kuigiza katika shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 #mpakakieleweke wakisubiri kuingia kwa majaji tayari kwa Kuanza kuonyesha vipaji vyao katika Ukumbi wa Makumbusho ya taifa uliopo jijini Dar Es Salaam mapema leo
 Baadhi ya washiriki wakianza kuonyesha yao kabla ya kuingia kwa majaji tayari kwa kuonyesha uwezo wao wa kuigiza
Wakichukua fomu za usajili kwaajili ya kushiriki shindano la TMT 2015
Washiriki wakiwa kwenye foleni..Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA BOHARI YA KUHIFADHI MAFUTA YA GBP MKOANI TANGA

$
0
0
1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Kituo cha kupokelea mafuta cha Kampuni ya GBP, wakati alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea Jeti ya kupokelea mafuta na Bohari ya kuhifadhia mafuta ya kampuni hiyo, wakati alipokuwa katika ziara yake ya siku moja mkoani Tanga jana Juni 5, 2015.
Picha zote na OMR
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka katika eneo hilo baada ya kukagua kituo hicho cha kupokelea mafuta cha Kampuni ya GBP, mkoani Tanga jana.
4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoizana na baadhi ya viongozi wa Kampuni ya GBP, wakati akielekea kukagua Bohari ya kuhifadhia mafuta ya Kampuni ya GBP, alipokuwa katika ziara yake ya siku moja mkoani Tanga jana.
5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya GBP, Badar Seif Sood, (wa pili kulia) wakati alipotembelea Bohari ya kuhifadhia mafuta ya kampuni hiyo, kwenye ziara yake ya siku moja mkoani Tanga jana.
6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka katika eneo hilo, akiongozana na Mkurugenzi wa ya GBP, Badar Seif Sood (kushoto), Waziri wa Mazingira wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Binilith Mahenge na baadhi ya viongozi, baada ya ukaguzi wa Bohari ya kuhifadhia mafuta ya Kampuni ya GBP, mkoani Tanga jana.
7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkurugenzi wa Kampuni ya GBP, Badar Seif Sood, baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua Bohari ya kuhifadhia mafuta ya kampuni hiyo, jana mkoani Tanga.

NYALANDU ATANGAZA NIA KUGOMBEA URAIS

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na wananchi mkoani Singida baada ya kutangaza nia ya kugombea nafasi ya urais kwenye Uwanja wa Namfua leo. (Picha na Loveness Bernard).
Umati wa watu ukimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu baada ya kutangaza nia ya kugombea nafasi ya urais kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida leo. (Picha na Loveness Bernard)
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (kushoto) akiwa na mkewe Faraja kabla ya kuzungumza na wananchi mkoani Singida wakati wa kutangaza nia.

SENENE JERO KWA KIGANJA KIMOJA CHA MKONO MJINI BUKOBA.

$
0
0
 Baadhi wachuuzi wa kitowea maarufu kwa wakazi wa Bukoba,kiitwacho senene,wakiwaandaa tayari kwa kuwauza kwa wateja wao,ambapo hupima kwa kiganja cha mkono kwa kiasi cha shilingi 500.
 Kijana akiandaa senene wake kwa ajili ya chakula,kama alivyokutwa na Camera ya Globu ya Jamii nje ya soko la Bukoba mjini,ambako Senene hao hupatikana na kuuzwa kwa wingi. 
Wachuuzi wa kitoweo cha Senene wakimuuzia mteja wao,ambapo hupima kwa kiganja na kuuzwa 500 .
 Wengine wanauwaza wakiwa bado hai kama hivi
Baadhi ya akina mama wakiwa kwenye ujasiliamali wao biashara ya mbogamboga nje ya soko la Bukoba mjini,mapema leo mkoani Kagera.

PICHA NA MICHUZJI JR-BUKOBA

MHESHIMIWA BERNALD MEMBE ANAWAALIKENI KESHO, JUNE 7, 2015 KUMSIKILIZA ATAKAPOKUWA ANATANGAZA NIA YA URAIS

DKT. BILAL AONGOZA WANANCHI KWENYE MAZISHI YA MBUNGE WA JIMBO LA UKONGA MAREHEMU EUGENE MWAIPOSA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha kumbukumbu kufuatia kifo cha Mbunge wa Ukonga Marehemu Eugene Maiposa kabla ya mazishi yake yaliyofanyika leo Juni 06, 2015 nyumbani kwake Ukonga Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima ya mwisho kwenye Jeneza lenye Mwili wa aliyekua Mbunge wa Ukonga Marehemu Eugene Mwaiposa aliyefariki Ghafla nyumbani kwake Dodoma juzi, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo Juni 06, 2015 nyumbani kwake Ukonga Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la Maua kwenye Kaburi la aliyekua Mbunge wa Ukonga Marehemu Eugene Mwaiposa wakati wa mazishi yake yaliyofanyika nyumbani kwake Ukonga Dar es salaam leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia ya Mbunge wa Ukonga Marehemu Eugene Mwaiposa baada ya mazishi yake yaliyofanyika nyumbani kwake Ukonga Dar es salaam leo Juni 06, 2015. (Picha na OMR)

LOWASSA ATUA ZANZIBAR

$
0
0

Waziri Mkuu wa zamaninaMbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowasa, (kulia), akipokewa na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mjini Unguja, Borafia Silima Juma, wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mkoa wa Mjini, Unguja Jumamosi usiku, Juni 6, 2015. Mh.  Lowassa, yuko Zanzibar kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015. (Picha na K-VIS MEDIA)


Mh. Lowassa, akifurahia jambo na Mzee Borafia, mara baada ya kuwasili kisiwani Zanzinzibar, akitokea Mwanza.

Wazirti Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mjini, kisiwani Unguja, Zanzibar, Borafia Silima Juma, (kulia), na aliyekuwa Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba, Simai Mohammed Jumamosi usiku Juni 6, 2015 mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar. Mh.  Lowassa, yuko Zanzibar kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015

Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, (kushoto), akiwasalimia wakereketwa wa CCM, waliofika kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, Jumamosi usiku Juni 6, 2015. Mh.  Lowassa, yuko Zanzibar kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015

Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, (kushoto), akiwasalimia vijana wa Kimasai, waliofika kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, Jumamosi usiku Juni 6, 2015. Mh.  Lowassa, yuko Zanzibar kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015

Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, (aliyevaa suti), akiondoka uwanja wa ndege wa Kitaifa wa Zanzibar, muda mfupi baada ya kuwasili huku akipokewa na wakereketwa wa CCM, waliofika kumlaki Jumamosi usiku Juni 6, 2015. 2015. Mh.  Lowassa, yuko Zanzibar kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015

Mh. Lowassa, akiongozana na Mbunge wa Kigoma Mjini, Mh. Peter Serukamba, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar Jumamosi Juini 6, 2015.

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA ALIVYOUNGURUMA LEO BUKOBA MJINI.KESHO KUWASILI WILAYA YA MULEBA.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia Mkutan wa hadhara leo, kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Bukoba, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na ilani ya Uchaguzi ya CCM.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mh.John Mongella akiwasalimia Wananchi na na  Wanachama wapenzi wa CCM,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Mashujaa,mkoani Kagera.
 Baadhi ya Wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano huo wa hadhara. 
  Wanannchi wakisikiliza kwa makini
  Mbunge wa Bukoba mjini Hamis Kagasheki (kushoto) akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Bukoba mkoani Kagera.
 Wananchi wa mji wa Bukoba mjini na wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia jambo wakati Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pichani katikati alipokuwa akizungumza
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mashujaa mjini Bukoba leo, akiwa katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana mkoani Kagera.
  shangwe na shamra shamra zilikuwepo katika mkutano huo
 Wanafuatilia kwa makini
Baadhi ya Wananchi wa Bukoba mjini na vitongoji vyake wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa ukihutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana jioni ya leo katika uwanja wa Mashujaa,mjini Bukoba mkoani Kagera
 Anafuatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana jioni ya leo katika uwanja wa Mashujaa,mjini Bukoba mkoani Kagera.
 Baadhi ya waendesha piki piki maarufu kama bodaboda wakiushangaa msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ulikuwa ukielekea kushiriki na kukagua miradi mbalimbali. 

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizungumza na wafanyabiasha wa soko la Kashai,lakini pia alipata wasaaa wa kuwasalimia wafanyabiashara hao.


 Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh. John Mongela pamoja na Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Mh. Khamis Kagasheki 
Ujenzi wa uwanja wa ndege wa mjini Bukoba  ukiwa katika hatua za mwisho kukamilika 
 atibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na Meneja wa uwanja wa Ndege wa Bukoba Bw. Julius Mulungwana wakati akikagua ujenzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba wakati akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza uhai wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoani Kagera ambapo leo aliuwa katika jimbo la Bukoba mjini, Kinana yuko katika ziara ya mikoa ya Kagera, Geita na Mwanza akingozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM. 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza risala aliyosomewa wakati alipokagua chanzo cha maji safi huko kata ya Nshambwa,mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akijadiliana na jambo na Mbunge wa jimbo mjini Mh.Hamis kagasesheki mara baada ya kukagua mashine ya maji
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata taarifa ujenzi wa jengo la Wagonjwa wa nje (OPD),Hospitali ya wilaya.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa sambamba na wananchi  akishiriki katika utengenezaji wa barabara kwa njia ya kujitolea katika kijiji cha Nyanga,mkoani Kagera
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiri ujenzi wa Zahannati ya kata Nyanga.
Ndugu Kinana akizungumza na akina mama wajasiliamali mara baada ya kukizindua kikundi chao.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi wakandarasi wa kampuni ya TechnicfabEngeneering Limited inayojenga mradi huo wa maji mjini Bukoba.


WAGOMBEA URAIS CCM WAPO HURU KUSHIRIKI MIDAHALO - KINANA

MAALIM SEIF AHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKA KIBANDAMAITI, ZANZIBAR

$
0
0
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wafuasi na wapenzi wa chama hicho katika viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba akiwahutubia wafuasi na wapenzi wa Chama hicho katika viwanja vya Kibandamaiti mijini Zanzibar.
Wafuasi na wapenzi wa chama cha wananchi CUF wakifuatilia mkutano wa hadhara wa CUF katika viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad ambaye ni mgombea Urais wa Chama hicho, akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad na mkewe Mama Awena Sinani Massoud, wakiwa kwenye jukwaa kuonesha furaha zao baada ya kuteuliwa kuwa mgombea urais wa Zanzibar.
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akipokelewa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar, baada ya kuwasili akitokea Dar es Salaam ambako aliteuliwa Rasmi kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF mwaka 2015.
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Zanzibar.
.(picha na Salmin Said, OMKR).

Na: Hassan Hamad (OMKR).
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema anakusudia kuifanya Zanzibar kuwa visiwa vya fursa za biashara na ajira kwa wananchi.

Maalim Seif ambaye tayari Chama chake kimeshamteua rasmi kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015, ameeleza hayo katika viwanja vya Kibandamaiti, wakati akihutubia mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho kwa ajili ya mapokezi ya mgombea huyo. Amesema Zanzibar inazo fursa nyingi za kuweza kunyanyua kipato cha wananchi, na kwamba ataweka kipaumbele katika kuziibua na kuziendeleza fursa hizo.

Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema katika kujenga mazingira bora ya uwekezaji, ataisimamia ipasavyo Mamlaka ya vitega uchumi, ili kuondosha vizingiti vinavyokwamisha uwekezaji nchini.

Amefahamisha kuwa wapo wafanyabiashara wengi wa ndani na nje ya nchi wenye nia ya kuwekeza miradi mikubwa ya kiuchumi, lakini wamekuwa wakipata usumbufu, jambo ambalo ameahidi kulishughulikia muda mfupi baada ya kuingia madarakani.

Sambamba na hilo, Maalim Seif amesema iwapo atachaguliwa kuiongoza Zanzibar, atahakikisha kuwa Zanzibar inakuwa na shirika lake la ndege ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, ili kurahisisha shughuli za kibiashara ikiwemo Utalii. Amesema hatua hiyo itakwenda sambamba na uboreshaji wa huduma za viwanja vya ndege, ambavyo vitaweza kutoa huduma bora kitaifa na kimataifa.

Aidha amesema chini ya uongozi wake iwapo atapata ridhaa ya kuongoza nchi baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015, ataitangaza Zanzibar kuwa bandari huru, sambamba na kujenga bandari mpya itakayotoa huduma bora kwa mwambao wa Afrika Mashariki.

Katika hatua nyengine Maalim Seif amesema anakusudia kuongeza viwango vya mishahara kwa wafanyakazi wote, pamoja na kuzingatia maslahi ya wastaafu na wazee wasiojiweza.

Akizungumzia kuhusu mafuta, Maalim Seif amesema anakusudia kuanzisha Wizara ya Mafuta na Gesi ili kurahisisha uchimbaji wa nishati hiyo, itakayoondosha hali ya umasikini katika visiwa vya Zanzibar.
Maalim Seif pia alizungumzia hali ya amani na utulivu nchini, na kueleza kuwa amani ya kweli itapatikana iwapo vyombo vinavyohusika vitatoa haki kwa wananchi wote.

Mapema akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, amesema Baraza Kuu la Uongozi la CUF limeshawika kumuidhinisha Maalim Seif kuwa mgombea Urais wa Zanzibar, kutokana na uwezo na nia ya dhati ya kuwatumikia wazanzibari.

Amesema viongozi waliopo madarakani wana dhamana na wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu ujao unafanyika katika hali ya amani, sambamba na kuheshimu maamuzi ya wananchi katika uchaguzi huo.

Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania Wanaosoma Wuhan-China (WUTASA) yaaga wenzao waliomaliza masomo

$
0
0
Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania Wanaosoma Wuhan-China (WUTASA) imefanya sherehe ya kuwaaga wenzao waliomaliza masomo yao. Sherehe hiyo ilihudhuriwa pia na Wanajeshi wa Jeshi la Wanachi (JWTZ) Kikosi cha Maji wanaosoma kozi fupi za uhandisi katika chuo cha jeshi cha uhandisi kilichopo Jijini Wuhan.









WANANCHI WA MKOA WA LINDI WAJITOKEZA KWA WINGI USIKU WA SHAMRA SHAMRA ZA TWENDE NA MEMBE

$
0
0
 Shamra shamra za kutangaza nia ya kuwania urais zaendelea kunoga mjini Lindi ambapo leo June 6 kuamkia June 7, 2015 ambapo Mheshimiwa Bernard Membe atakuwa anatangaza nia ya Kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2015. Wananchi wamejitokeza kwa wingi huku msanii mzee Yusuph na kikundi cha ngoma ya Deda wakitoa burudani ya kijadi.
 Wananchi waliojitokeza katika Shamra Shamra za kumpokea kesho Mheshimiwa Bernard Membe wakati atakapotangaza nia ya Urais 2015.


Mfalme wa Muziki wa taarabu Mzee Yusuph akitoa burudani katika shamra shamra hizi.
 Vijana wa Mzee Yusuph wakitoa burudani.
Mbunge wa Mchinga Mheshimiwa Said Mtanda (wa pili toka Kushoto) akicheza na wananchi waliojitokeza katika shamra shamra hizo.
kikundi cha ngoma ya Deda kikitoa burudani ya kijadili katika kudumisha mila.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi  Mzee Alli Mohamedi Mtopa (kushoto) akicheza na baadhi ya wananchi waliofika eneo la tukio.

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI, PAUL MAKONDA ACHANGIA MILIONI MOJA KUSAIDIA KUUNDA UMOJA WA MSASANI JOGGING CLUB

$
0
0
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, amewataka vijana waliopo katika shirikisho la umoja wa Jogging wa Kata ya Msasani kuunda umoja ambao utawasaidia kupata fursa mbalimbali.

Makonda alitoa mwito huo wakati akizungumza na wana jogging waliopo kwenye shirikisho hilo kutoka katika kata hiyo wakati wa hafla ya kutimiza miaka mitatu tangu ianzishwe Msasani Jogging.

"Naomba fanyeni mchakato wa kuanzisha Kamati ya Uchumi na Mipango na muuanzishe umoja wenu uliosajiliwa, utawasaidia kupata mikopo na sisi kama serikali tutawapa kazi kama za kukusanya takataka, ulinzi na nyingine nyingi" alisema Makonda.

Alisema Manispaa ya Kinondoni imetenga zaidi ya sh. bilioni 2 kwa ajili ya vijana na wanawake fedha zitakazo tolewa kupitia makundi mbalimbali yaliyosajiliwa.

Alisema fedha hizo zipo kwa ajili ya shughuli mbalimbali na kuwa kwa awamu ya kwanza zitatolewa sh.milioni 100.

Katika kusaidia mchakato wa kuanzisha umoja huo, Makonda alitoa sh. milioni 1 na Diwani wa Kata hiyo, Christina Kirigiti alitoa sh. 300,000 papo hapo. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akizungumza na wana jogging wa Kata ya Msasani Dar es Salaam leo asubuhi kwenye hafla ya kutimiza miaka mitatu tangu ianzishwe Msasani Jogging Club.
 Viongozi mbalimbali meza kuu. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kunduchi Kwanza Jogging, Asia Mohamed, Katibu Msaidizi wa Msasani Jogging, Alhaji Seif Muhele, DC Makonda, Diwani wa Kata ya Msasani, Christina Kirigiti, Mwenyekiti wa Msasani Jogging Club, Mohamed Hassan na Makamu Mwenyekiti, Pili Ndumba.
 Diwani wa Kata ya Msasani, Christina Kirigiti (kulia), akihutubia katika hafla hiyo.
  Diwani wa Kata ya Msasani, Christina Kirigiti (kushoto), akizungumza na Kiongozi wa Msasani Jogging, Abubakar Simon.
 Wana jogging wa Msasani Club wakimsikiliza DC Makonda.


 Madaktari wa Msasani Jogging wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kulia ni Swalehe Mohamed Akida na Tatu Hamisi.
 DC Makonda (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wanamsasani Jogging Club.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoki Paul Makonda akiondoka baada ya kuhudhuria hafla hiyo na kuhutubia.
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images