Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 545 | 546 | (Page 547) | 548 | 549 | .... | 1904 | newer

  0 0

  Q-Chilla baada ya kuwa kimya kwa Muda Mrefu na Pia mambo yake Kubadilika, Sasa amerudi tena katika Muziki na Safarii hii ameamua kufanya kazi yaani Muziki Biashara, Akizungumza wakati wa kupreview video yake Mpya ya For U amesema kuwa kwa sasa amerudi rasmi katika Muziki na Amebadilika Tofauti na Mwanzoni alivyokuwa pia ametoa Shukran Nyingi sana kwa QS ambaye anasimamia kazi zake za kimuziki kwa sasa, Video ya For You imefenywa na Director Adam Juma Nchini Afrika ya Kusini, Kwa Upande wa Adam amesema kuwa Video hii ameifanya kwa mapenzi na ameomba wasanii kuthamini vitu vyao vya nyumbani na ameahidi kufanya kazi na msanii yeyote ambaye atakuwa tayari kikubwa kazi iwe nzuri. by www.harakatizabongo.com Angalia video hii ya Q Chilla For You au MdogoMdogo kisha kama unacomment yeyote unaweza kuacha hapo chini....
  d

  0 0

   AFISA UHUSIANO MWANDAMIZI WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF ,ABDUL NJAIDI AKITOA HOTUBA WAKATI WA UZINDUZI WA ASASI YA HIFADHI YA JAMII, ILIYOANZISHWA NA WANAFUNZI WA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM). UZINDUZI HUO ULIDHAMINIWA NA PSPF.
   WANAFUNZI WA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM) WAKIFATILIA UZINDUZI WA ASASI YA HIFADHI YA JAMII ULIODHAMINIWA NA PSPF.
   RAIS WA KWANZA WA ASASI YA HIFADHI YA JAMII, BW. HASSAN ABDULRAHMAN AKIZUNGUMZA WAKATI WA UZUNDUZI WA ASASI HIYO,UZINDUZI HUO ULIDHAMINIWA NA PSPF.

   MKURUGENZI WA UTAFITI, TATHIMIN NA SERA WA MAMLAKA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII, ANSGAR MUSHI   (WA TANO KUTOKA KUSHOTO) AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WANAFUNZI WA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA AMBAO NI WANACHAMA WAAZILISHI WA ASASI YA HIFADHI YA JAMII, WA NNE KUTOKA KUSHOTO NI DR. ABDALLAH SAQWARE NA WA NNE KUTOKA KULIA NI ABDUL NJAIDI, AFISA UHUSIANO MWANDAMIZI WA PSPF. PSPF NDIO WALIKUWA WADHAMINI WAKUU WA UZINDUZI HUO.
   MKURUGENZI WA UTAFITI, TATHIMIN NA SERA WA MAMLAKA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII ANSGAR MUSHI,    AKITOA HOTUBA WAKATI WA UZINDUZI WA WA ASASI YA HIFADHI YA JAMII ILIYOANZISHWA NA WANAFUNZI WA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM) NA KUDHAMINIWA NA PSPF.
  MKURUGENZI WA UTAFITI, TATHIMIN NA SERA WA MAMLAKA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII ANSGAR MUSHI    AKIKATA UTEPE KUASHIRIA UZINDUZI WA WA ASASI YA HIFADHI YA JAMII , KILICHOAZISHWA NA WANAFUNZI WA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM) KULIA NI ABDUL NJAIDI AFISA UHUSIANO MWANDAMIZI WA PSPF.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa mapema leo katika uwanja wa shule ya msingi Nyakanazi,Wilayani Biharamulo  mkoani Kagera,ambapo pia aliwasalimia wananchi wa kijiji hicho tayari kwa kuanza ziara rasmi mkoni humo.Kinana yupo Mkoani humu kwa ziara ya kikazi ya siku kumi ya Kukagua utelekezwaji wa Ilani ya chama cha CCM ya mwaka 2010 pamoja na kuimarisha chama na kusikiliza matatizo ya wananchi.
  Kinana akisalimiana  baadhi ya Wananchi wa Nyakanazi mapema leo,alipopita kuwasalimia.

  katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa ameambatana Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (aliyebeba mtoto),wakiwasalimia wananchi wa kijiji cha Nyakanazi,wilayani Biharamulo mkoani Kagera
  Wananchi wa kijiji cha Nyakanazi pamoja na wapenzi/washabiki wa chama cha CCM wakishangilia kwa ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Taifa,Ndugu Kinana mkoani Kagera.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwasalimia Wananchi wa kijiji cha Nyakanazi pamoja na wapenzi/washabiki wa chama cha CCM waliofika kumsikiliza mapema leo asubuhi,mkoani humo.Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya maofisa wa chama hicho wako ziarani kanda ya ziwa kwa siku 28 za  Kukagua utelekezwaji wa Ilani ya chama cha CCM ya mwaka 2010 pamoja na kuimarisha chama na kusikiliza matatizo ya wananchi.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na wafuasi wa chama hicho wakikatiza kuelekea kwenye mkutano wa ndani na pia kuzungumza na kundi la Wafugaji

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na ujumbe wake akikatika kwenye moja ya soko katika kijiji cha Nyakanazi,Wilayani Biharamulo mkoani Kagera mapema leo asubuhi,akielekea kwenye mkutano wa kupokea taarifa za Chama na serikali pamoja na kuyasikiliza makundi ya Wafugaji kuhusiana na matatizo waliyonayo.

  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
  WATANZANIA wameendelea kuvichangamkia viwanja vya mkopo vinavyotolewa na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, vilivyopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani.

  Kuchangamkiwa kwa viwanja hivyo kumekuja siku chache baada ya kuzindua huduma mpya ya mikopo ya viwanja hivyo kutoka Bayport, ikiwa ni ishara nzuri na njia ya kuwapa fursa Watanzania ya kumiliki nyumba.

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema watu wengi wamekuwa wakituma maombi ya kuomba kupewa viwanja hivyo, tangu huduma hiyo ilipozinduliwa rasmi.

  Alisema kwamba baadhi ya watu walioonyesha nia ya kuvipata viwanja hivyo pamoja na kutuma maombi yao, pia wamekuwa wakitembelea eneo kulipokuwa na viwanja hivyo ili wajiridhishe kwa ajili ya kujipatia viwanja hivyo vinavyokopeshwa kwa minajiri ya kuwakwamua Watanzania, ukizingatia kuwa ardhi inapanda thamani siku hadi siku.

  “Jana (juzi) zaidi ya watu 82 wamekwenda Vikuruti, Kibaha kujionea eneo lenyewe na kuchagua viwanja wapendavyo, ikiwa ni mwendelezo mkubwa wa wananchi wanaotuma maombi ya kukopa viwanja vya Bayport, wakichukua fomu bure z kwa kupitia matawi yetu yaliyoenea nchi nzima, bila kusahau kwenye matawi ya Bank of Afrika (BOA).

  “Huduma hii ni murua kwa Watanzania wote, tukiamini kuwa ni sehemu ya kuwapatia wananchi urahisi wa kumiliki vitu vyenye thamani ikiwamo ardhi wanayoweza kuitumia kwa mambo mengi, ikiwa nyumba za kuishi na za biashara, huku thamani ya viwanja vikianzia Sh 1,400,000 na kuendelea kwa viwanja vyenye ukubwa tofauti vya kujenga nyumba za kuishi na biashara kama vile shule, vituo vya afya, nyumba za kulala wageni na hoteli,” alisema Cheyo.

  Cheyo alisema nafasi ni chache, maana maombi yanafanyika kwa siku (20), kuanzia Mei 22 hadi Juni 10, huku fomu za maombi zikipatikana katika matawi yao yote ya Bayport Financial Services na matawi ya bank of Africa (BOA), ambapo malipo ya awali yakianzia Sh 150,000 na yatakuwa yakilipwa kwa akaunti yao ya Bayport iliyopo BOA.

  Kwa mujibu wa Cheyo, fomu ya maombi na nakala ya malipo ya awali yarejeshwe katika matawi BOA au ofisi za taasisi ya Bayport zilizoenea nchi nzima na baada ya Juni 10, mteja atatakiwa kulipia kiwanja kwa fedha taslimu au mkopo kutoka kwenye taasisi yao huku watumishi wa umma na wa kampuni binafsi wakiweza kukopeshwa kiwanja na kukabidhiwa hati miliki ndani ya siku (90) watakapokamilisha mkopo wao.

  Hawa ni miongoni mwa Watanzania waliohamasika kutembelea katika viwanja vilivyokuwa kwenye mradi wa Vikuruti kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, ambavyo vinatolewa kwa wananchi kwa mkopo. Wakopaji ni watumishi wa umma, kampuni binafsi na wajasiriamali.
  Eneo la viwanja vya Vikuruti vinavyoonekana huku barabara ikionekana pichani.

  0 0
 • 06/05/15--03:27: Article 13


 • 0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Memba (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Adam Mayingu, baada ya kikao cha waheshimiwa Mabalozi.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (wa tatu kulia) akimpongeza Costantin Martin, Meneja Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF baada ya kutoa mada kwa waheshimiwa mabalozi.

  Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Balozi John Haule akipata maelezo juu ya PSPF kutoka kwa Meneja Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF Costantina Martin.
  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe. Peter Kallaghe akijaza fomu ya Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, anayeshuhudia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Abdul Njaidi.


  Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe. Radhia Msuya akijaza fomu ya Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, wanaoshuhudia ni Maafisa wa PSPF, Hadji Jamadaly (katikati) na Zuhura Lwamo.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) kipata maelezo juu ya michango katika PSPF kutoka kwa Afisa wa PSPF Easter Jorry.

  Meneja Mawasiliano, Masoko na Uenezi, Costantin Martin akitoa mada ya Mfuko kwa waheshimiwa mabalozi wa Tanzania wanaiwakilisha katika nchi mbalimbali.


  Hivi karibuni Mfuko wa Pensheni wa PSPF ulitoa semina kwa waheshimiwa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.

  Katika semina hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Ramada, jijini Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF Costantina Martin alipata fursa ya kutoa mada juu ya PSPF.

  Mada ya meneja huyo wa PSPF ilijikita katika maeneo yafuatayo; historia ya PSPF, wanachama wa PSPF, Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, mpango wa lazima, mafao yatolewayo na PSPF, mikopo itolewayo na PSPF, kikokotoo cha mafao, uwekezaji, huduma kwa wateja, utunzaji wa kumbukumbu kwa wanachama, mafao yaliyolipwa kwa wastaafu, wastaafu na thamani ya Mfuko.

  Baada ya mada hiyo waheshimiwa mabalozi walihamasika na uimara wa Mfuko na hatimaye wengi kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa Hiari

  Kiwango cha uchangiaji katika mpango wa uchangiaji wa hiari ni kuanzia shilinghi 10,000/- au zaidi. Michango itawasilishwa moja kwa moja kupitia akaunti ya benki au wakala wa malipo wa M-Pesa, Tigo-Pesa, Airtel-Money au Maxmalipo.

  PSPF ilianzisha mpango huu ili kuhakikisha kila mtanzania anafaidika na Hifadhi ya Jamii, PSPF kupitia mpango wake wa Uchangiaji wa Hiari tumeendelea kusajili watanzania na wasio watanzania ambao wanaishi nchini katika mpango huu, pia tunatoa huduma hii hata kwa watanzania wanaoishi nje ya Tanzania, lengo hapa ni kuhakikisha kila mtanzania anakuwa salama katika Hifadhi ya PSPF. Lengo la mpango huu ni kupanua wigo wa wanachama kwa kuandikisha wananchi waliojiajiri au kuajiriwa katika sekta rasmi na isiyo rasmi.

  0 0


  TAMASHA la Jambo Fashion Affair linatarajia kufanyika leo Jijini hapa na kushirikisha wabunifu wa ndani pamoja na wasanii kutoka Jijini Arusha na mikoa mbalimbali.

  Akizungumzia  maandalizi ya tamasha hilo linafanyika leo, Augustine Namfua  ambaye ni Mwenyekiti wa Jambo Festval alisema wamaejiandaa vizuri kuhakikisha wananchi wataohudhuria wanapata burudani ya ubunifu wa mavazi sambamba na muziki.

  Alisema wabunifu mbalimbali watakuwepo kama An Nisa, Fatma Naeem, Martin Kadinda ,Wanyoke Lewis, iheartz Collection, Ankara By Chimzy, Fabilouskitenge, Zakia Collection, gLushaju Clothing, Florinyah Designs ,Martin Mukiwa na wengine ambao wataonyesha aina mbalimbali za mavazi. 

  Namfua alitumia nafasi hiyo kuwasihi watanzania hususan wakazi wa Jiji la Arusha kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo ambalo linafanyika leo Viwanja vya Allliance Franc’aise Arusha na kiingilio kikiwa ni h, 20,000 kwa kila mtu.

  “Tamasha hili tunalifanya kwa mara ya nne na wasanii mbalimbali pamoja na wabunifu wa mavazi wataonyesha ubunifu wao katika tamasha hili hivyo ni vyema watu wakajitokeza kwa wingi kwani mbali na maonyesho ya mavazi pia kutakuwa na burudani za aina mbalimbali sambamba na vinywaji”.

  Naye Meneja Mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd, Edmund Rutaraka alisema kampuni hiyo ndio wadhamini wa tamasha hilo na pia watatoa huduma mbalimbali za vinywaji ili kufanikisha tamasha la ubiifu huku Mkurugenzi wa Alliance Francaise kutoka Arusha, Ga’’ele Lapostolle akisema taasisi yao imeamua kushirikiana na wahusika wa tamasha hilo ili kukuza utamaduni wa watanzania sambamba na ubunifu wa mavazi pamoja na muziki ambao ni ajira kwa vijana.

  Naye mmoja kati ya wanamuziki kutoka Jijini arusha ambaye atashiriki katika tamasha hilo na kukonga nyoyo za washiriki wa tamasha hilo, Elisha Simon maarufu kama Hisia aliwasihi wakazi wa Ausha kujitokeza kwa wingi kuona vipaji vya wasanii pamoja na mavazi yatakayoonyeshwa katika tamasha hilo.

  0 0

   Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam(DCP), Simon Sirro Akizungumza na waandishi wa habari juu ya Operesheni inayoendelea ya kuwasaka wahalifu wa makosa mbalimbali katika mkutano uliofanyika Ofisi za kanda maalumu ya Polisi jijini Dar es Salaam leo.

   Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam(DCP),Simon Sirro akiwaonesha Bastola yenye namba za usajiri 05532 baadhi ya  waandishi wa habari hawapo pichani.


  Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam(DCP), Simon Sirro akiwaonesha picha za kontena llililo kamatwa maeneo ya Kibamba.


  Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam(DCP) Simon Sirro Sirro akiwaonesha Pembe za Ndovu zilizo kamatwa maeneo ya Kimara Suka katika oparesheni  ukaguzi wa magari.
   Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam(DCP),Simon Sirro akiwaonesha baadhi ya  waandishi hawapo pichani ,Bunduki  aina ya (SMG) iliyofutwa namba zake ikiwa na risasi 10l


  Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam(DCP),Simon Sirro Sirro akiwaonesha Bastola bandia  katika Operesheni inayoendelea ya kuwasaka wahalifu wa makosa mbalimbali.PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.

   Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya uhalifu ikiwa ni pamoja na unyang’anyi wa kutumia silaha. Watuhumiwa wamekamakwa katika matukio tofauti jijini Dar es Salaam kufuatia oparesheni kali inayoendelea ya kuwasaka wahalifu wa makosa mbalimbali.


  Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 03/06/2015 majira saa 08:00HRS  maeneo ya Tabata Kinyerezi mtaa wa Kibaga askari wa kikosi kazi (TASK FORCE) walimkamata mtuhumiwa  HEMED S/O HASSAN MRISHO @ BUDA, Miaka 31, Mfanyabiashara, Mkazi wa Tabata Kinyerezi, akiwa na Bunduki aina ya SMG iliyofutwa namba zake ikiwa na risasi 10. 

  Mtuhumiwa alikamatwa kufuatia taarifa toka kwa msiri kuwa anajihusisha na uhalifu wa kutumia silaha. Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mtuhumiwa HEMED S/O HASSANI akishirikiana na wenzake ambao wanasakwa, wanajihusisha na unalifu wa kutumia silaha. Atafikishwa mahakamani mara uchunguzi utakapokamilika.  Katika tukio lingine, mnamo tarehe 01/06/2015 majira ya saa 02:00 huko maeneo ya Tegeta Mashimo ya Kokoto, Polisi walifanikiwa kukamata risasi 49 za bunduki aina ya Short Gun zikiwa katika mfuko wa Rambo baada ya kuwakurupua vijana wanaokaa katika vijiwe vya mashimoni hayo.


  Hii ni kufuatia kundi la vijana wanaokadiriwa kufikia kumi wakiwa na mapanga na silaha nyingine za jadi kuvamia nyumba ya VERONICA D/O SABATH MAMBOYA na kuiba vitu mbalimbali vikiwemo vitambulisho, TV, Laptop na Pesa taslim TSHS. 300,000/=. Baada ya tukio mlalamikaji alitoa taarifa kituo cha polisi Kawe na ufuatiliaji ulianza mara moja. Polisi walifanikiwa kuwakamata vijana watatu ambao walionyesha vijiwe vya vijana wenzao.

  Wakati polisi wakijiandaa kuwakamata walikurupuka na kukimbia ndipo polisi walifanya upekuzi wa eneo hili na kufanikiwa kupata risasi hizo zikiwa katika mfuko wa plastiki maarufu kama “mfuko wa Rambo”. Watuhumiwa waliokamatwa ni pamoja na

  1.   RAMADHANI S/O NUHU, Miaka 20,  Mkazi wa Kiwangwa.

  2.   ABED S/O SALUM, Miaka 18, MKAZi wa Kibaoni.

  3.   HANIF S/O HAMIS, Miaka 19, MKAzi wa Tegeta.


  KUKAMATWA KWA ROLA 15 ZA NYAYA ZA UMEME PAMOJA NA WATUHUMIWA SABA.

           Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum limefanikiwa kukamata kontena lenye namba 00LU2876031 likiwa na rola 15 za nyaya (zenye thamani ya shilingi 150,000,000/= milioni mia moja na hamsini) zilizoibwa tarehe 26/02/2015 zikiwa zinasafirishwa kuelekea mkoani Kagera kwa ajili ya mradi wa umeme vijijini (REA). Baada ya wizi wa kontena hilo kesi ilifunguliwa kituo cha Polisi Buguruni na watuhumiwa watano walikamatwa na kufikishwa mahakamani.

  Wakati upelelezi ukiendelea ndipo tarehe 25/05/2015 Polisi Buguruni walipokea taarifa toka kwa msiri kwamba huko maeneo ya Kibamba mtaa wa Kibwegele wilaya ya Kimara Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kuna kontena limefichwa katika kiwanda cha kutengeneza matofali.


  Askari wa kikosi kazi walifika eneo la tukio na kukuta kontena hilo lenye namba 00LU2876031 na walimhoji mlinzi wa eneo ili kupata mmiliki wa eneo na kontena hilo. Ilipofika saa 23:55hrs mmiliki wa eneo hilo aitwaye DONESIA D/O AIDAN @ KIFYOGA, Miaka 40, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mbezi Makabe ambaye ni mtuhumiwa wa sita.


  Taratibu zilipokamilika kontena hilo lilifunguliwa ndipo zilipokutwa rolla za nyaya zipatazo 15 kati ya 17 zilizokuwepo katika kontena hilo siku lilipokuwa linasafirishwa. Tarehe 27/05/2015 majira ya saa 00:30hrs maeneo ya Kimara mwisho alikamatwa mtuhumiwa mwingine wa saba PROSPER S/O MTEI, Miaka 43, Mfanyabiashara  na upelelezi unaendelea ili aweze kuunganishwa na watuhumiwa wengine katika kesi ya msingi.


  KUKAMATWA KWA BASTOLA MOJA NA MAGANDA YA RISASI

  Mnamo tarehe 28/05/2015 majira ya saa 23:00hrs maeneo ya Kiwalani Minazi Mirefu Kata ya Ilala WIlaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Polisi walifanikiwa kukamata silaha Bastola yenye nambari 05532 pamoja na maganda mawili ya risasi aina ya SMG katika eneo la tukio baada ya majambazi kuitelekeza mara walipozingirwa na wananchi waliotaka kuwakamata.


  Majambazi hao walikuwa wamefanya tukio la uporaji maeneo ya vingunguti wakitumia pikipiki mbili ambapo moja ina namba za usajili MC610 ABU aina ya Boxer rangi nyekundu ambayo pia waliipora kwa mtoa taarifa. Aidha katika tukio hilo pia majambazi hao walimpiga mtoa taarifa na kitako cha bunduki waliyokuwa nayo kisha kumpora pikipiki hiyo na pesa taslim shilingi 300,000/= Hata hivyo majambazi hao walifanikiwa kutoroka. Polisi kwa kushirikiana na wananchi waliweza kuikamata pikipiki hiyo.


  KUKAMATWA KWA VIPANDE 20 VYA PEMBE ZA NDOVU.

           Katika oparesheni iliyoendeshwa tarehe 25/05/2015 na idara ya INTERPOL jijini Dar es Salaam ya kukamata magari, madawa ya kulevya na uhalifu mwingine. Ilipofika majira ya saa 18:00hrs maeneo ya Kimara Suka ambapo kutokana na foleni ya magari iliyosababishwa na ukaguzi wa magari katika zoezi hilo alishuka kijana mmoja mwenye umri kati ya miaka 39- 45 kwa dhumuni la kukodi pikipiki.


  Katika hali isiyokuwa ya kawaida baada ya kuwaona askari wa unifomu kijana huyo alitupa kifurushi alichokuwa nacho na kukimbia. Askari walilichukua hilo furushi na kulipekuwa na kukuta kuna meno ya tembo vipande ishirini pamoja na nguo kuku. Kielelezo kilipelekwa kituo cha Polisi Mbezi na kufunguliwa jalada la uchunguzi KMR/PE/67/2015.


  KUKAMATWA KWA MLIPUKO, VIFAA VYA KUVUNJIA, DAWA ZA KULEVYA PAMOJA NA MTUHUMIWA.

  Tarehe 04/06/2015 majira ya saa 10:00hrs maeneo ya Chamazi ulifanyika msako mkali wa kupambana na uhalifu na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa MICHAEL S/O KASAMBALE, Miaka 28, Mkazi wa Chamazi akiwa na mlipuko mmoja na vifaa vya kuvunjia. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika. Aidha mtuhumiwa huyo amekamatwa na kete kadhaa za madawa ya kulevya.


  KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA AKIWA NA BASTOLA BANDIA

  Polisi wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa JACOB S/O NATHANIEL MWETA, Miaka 30, Mfanyabiashara, Mkazi wa Kimara ambaye alikuwa anaitumia kutishia watu kisha kupora. Mtuhumiwa ame kiri kuhusika katika matukio kadhaa ya unyang’anyi hasa katika maeneo ya Tegeta na Kunduchi jijini Dar es Salaam.


  MAFANIKIO MENGINE YA OPARESHENI INAYOENDELEA JIJINI DAR ES SALAAM.


           Aidha, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na oparesheni ya kupambana na uhalifu katika jiji la Dar es Salaam na kufanikiwa kukamata vitu vifuatavyo:

  1.   Mitambo mitano (5) ya kutengeneza pombe ya moshi (Gongo)

  2.   JUmla ya lita mia mbili (200) za pombe ya Moshi (Gongo)

  3.   Gunia mbili za banghi.

  4.   Kupatikana na Mirungi box moja (1).

  5.   Kete kadhaa za madawa ya kulevya.

   

   
  SIMON SIRRO – DCP

  KNY. KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
  DAR ES SALAAM 

  0 0

   Ofisa Uhusiano wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), Jafarri Malema (kushoto), akizungumza na wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo (hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu shughuli zinazofanywa na Rita na umuhimu wa cheti cha kuzaliwa. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa Rita, Grace Kyasi.
   Ofisa Uhusiano wa Rita, Grace Kyasi akizungumza katika mkutano na wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo.
  Wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo wakiwasikiliza maofisa wa Rita walipokuwa wakizungumza nao.  Dotto Mwaibale
  WANANCHI wametakiwa kuwa na vyeti vya kuzaliwa kwani vina umuhimu katika maisha ya kila siku ndani na nje ya nchi.

  Mwito huo umetolewa na Ofisa Uhusiano wa Wakala wa  Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), Jafarri Malema wakati  akizungumza na wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu shughuli zinazofanywa na Rita na umuhimu wa kuwa na cheti cha kuzaliwa. 

  "Cheti za kuzaliwa ni msingi wa mafanikio ya kila mmoja wetu na ni muhimu kuwa nacho" alisema Malema.

  Alisema Rita imekuwa ikifanya shughuli za usajili wa vizazi,vyeti vya kuzaliwa, kuandika wosia, kusajili ndoa na talaka na udhamini kama mali za umma na ile isiyokuwa na mwenyewe.

  Alisema faida ya kuandika wosia unasaidia kuepusha watoto, mke au mume kunyang'anywa mali pale kinapotokea kifo na inawezesha kumchagua msimamizi wa mirathi.

  Alitaja faida nyingine ya kuandika wosia kuwa ni kuepusha migongano katika familia, ndugu au jamaa na kuwa unampa uhakika wa maisha bora ya baadae warithi wa mali waliziachiwa.

  Alisema jambo linalofanyika baada ya kufariki kwa mtu aliyeandika wosia mmoja wa mashahidi anatakiwa kwenda kutoa taarifa Rita ambapo taratibu za wosia kuwasilishwa mahali husika hufanyika.

  Naye Ofisa Uhusiano wa Rita, Grace Kyasi alisema umuhimu wa kuwa na cheti cha kuzaliwa ni mkubwa kwani ni nyaraka pekee yenye mamlaka kisheria kuthibitisha tarehe na mahali mtu alipozaliwa na ni nyaraka muhimu kwa kila mwananchi kwani hutumika kupata huduma nyingine za msingi kama elimu, afya na makazi.

  Alisema cheti cha kuzaliwa kinawawezesha watoto kujiunga na elimu ya msingi na sekondari na kuwawezesha kupata nafasi ya masomo ya elimu ya juu pamoja na mikopo ya masomo.

  0 0

  MAELFU ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM, na wakazi wengine wa jiji la Mwanza, leo Ijumaa Juni 5, 2015, walifurika kwa wingi kwenye ofisi za CCM wilaya ya Nayamagana na ile ya Ilemela, wengine wakitaka kumuona na kupeana mikono na wengine kwa nia ya kumdhamini Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edwrad Lowassa, alipofika jijini Mwanza kutafuta wana CCM wa kumdhamini katika safari yake ya Matumaini. (Kuwania urais wa Tanzania kupitia CCM.  Madereva texi, waendesha bodaboda, na hata wafanyakazi na wasafiri kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, waliacha shughuli zao kwa muda ili walau wamuone mtangaza nia huyo wa nafasi ya jurasi kupitia CCM.  Lowassa alichukua fomu, za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania, Alhamisi Juni 4, 2015 pale makao makuu ya CCM, na safari yake ya kusaka wadhamini ilianza “chap chap” pale pale Dodoma, na Mwanza ndio kituo cha kwanza nje ya Dodoma, ambacho Lowassa, ameanza kampeni yake ya kusaka wadhamini.  Picha ni, Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, ambaye tayari amechukua fomu za kuomba CCM imteue kuwania urais, Edwrad Lowassa, akipungia mkono maelfu ya wanachama wa chama hicho na wananchi wengine baada ya kupata wadhamini kwenye ofisi ya CCM wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza Ijumaa Juni 5, 2015. (Picha na K-VIS MEDIA)  Lowassa, akipokea fomu za wadhamini ambazo tayari zimejazwa na wana CCM wilaya ya Ilemele, kutoka kwa Katibu wa CCM wilayani humo, , Loti Olele Mtui Lazaro

  Mmoja wa madereva Texi, akionyesha bango la kumuunga mkon o Lowassa, katika safari ya matumaini 2015

  Lowassa, akipokea fomu zilizojazwa na wadhamini ambao ni wanachama wa CCM, kutoka kwa Katibu wa CCM wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza, Elias Mpanda

  Mwanachama mkongwe wa CCM, Mzee Rutaraka, akitoa salamu zake kwa niaba ya wazee jijini Mwanza

  Watoto wa Chipukizi kutoka Chama Cha Mapinduzi, jijini Mwanza, Marie Kighei Joseph, (wapili kulia) na Sarafina Magabe, wakimkabidhi zawadi ya maua ikiwa ni ishara ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwnza, Ijumaa Juni 5, 2015, ili kuomba wadhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuwania urais wa Tanzania kuputia CCM
  Lowassa, akiteremka kutoka ndani ya ndege baada ya kuwasili jijini Mwanza kuomba wadhamini.
  Wananchi waliokuwa na kiu ya kumuona Lowassa, walilazimika kupanda juu ya viti kutokana na msongamano wa watu waliofurika kwenye mitaa jirani na odfisi za CCM wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza Ijumaa Juni 5, 2015.
  Wasafiri na wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa Mwanza, waliacha shughuli zao ili walau wapate kumuona Lowassa, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwnaza Ijumaa Juni 5, 2015, tayari kutafuta wadhamini.
  Lowassa, akionyesha fomu ambayo tayari imejazwa na wadhamini wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza

  0 0

   mkurugenzi wa Phide Entertainment and tours akiwa na watangazaji wa Triple A fm  katika uzinduzi huo

   Crew ya anPhide Entertainment d tours siku ya uzinduzi wa double mint last week. ‪#‎Team‬ getbusy $ Phide entertainment -Event organisers#
   Yaani ukitembelea jiji la Arusha usiache kufika katika kiota hiki kipya ni paukweli balaa sio pakukosa  ndio habari ya mjini kwa sasa   Dj maarufu wa Triple A fm wanamuita dj Nass akiwa navimwana wa ukweli wanaopatikana ndani ya kiota kipya  kijulikanacho kwa jina la  double mint
   mkurugenzi wa Phide Entertainment and tours dada Phide au unaweza kumuita King Ian akiwa ndani ya Red capeti ndani ya uzinduzi huo
   wadau mbalimbali waliuthuria katika uzinduzi huo
   wageni waalikwa  wakiwa ndani ya kiota hicho cha double mint

  Bendi ya malindi ndio ilihusika katika swala zima la kutoa burudani hapa ilikuwa ikiendelea kuangusha sebene(picha kwa hisani ya libeneke la kaskazini blog


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga leo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mazingira wa Ofisi yake, Dkt. Julius Ningu, wakati alipotembelea kwenye banda la maonyesho la Ofisi ya Makamu wa Rais, kwenye Sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamano, mkoani Tanga, leo Juni 5, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya mshindi wa tatu katika usimamizi wa usafi wa mazingira, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga leo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu utunzaji wa nyaraka kutoka kwa Mkurugenzi wa Msaidizi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Lupi Mwaikambo, wakati alipotembelea kwenye banda la maonyesho la Ofisi ya Makamu wa Rais, kwenye Sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamano, mkoani Tanga leo

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea mabanda wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga leo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mtoa huduma wa dawa za asili, Karunde Amadi, wakati alipotembelea kwenye banda wafanyabiashara za dawa asili, kwenye Sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamano, mkoani Tanga  leo .
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi zawadi ya Pikipiki kwa mmoja kati ya washindi.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Filamu ya Mamba wa Zigi, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga, leo Juni 5, 2015. Kushoto kwake ni Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Binilith Mahenge, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, Samia Suluhu. Picha na OMR

  0 0

  Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Balozi Dk. Mohamed Maundi akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la chuo hicho ikiwa ni sehemu ya madhimisho ya siku ya mazingira Duniani. (Picha na Francis Dande)
   Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Balozi Dk. Mohamed Maundi akimwagilia maji mti wa kumbukumbu alioupanda katika eneo la chuo hicho ikiwa ni sehemu ya madhimisho ya siku ya mazingira Duniani. 
   Naibu Mkurugenzi wa Mipango Utawala na Fedha wa Chuo cha Diplomasia, Dk. Bernard Achiula akipanda mti wa kumbukumbu wakati wa maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani ambapo walipanda miti na kufanya usafi katika eneo la chuo hicho. 
  Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia, Nice Munissy (kulia) akiwaongoza wenzake kupanda mti ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Kanda ya Ziwa Bwa.Mugisha Murshad wakati alipokuwa akitoa malalamiko ya wafugaji kwa ukatili wanaofanyiwa na askari wa wanyamapori katika mapori mbalimbali ya hifadhi kanda ya ziwa.

  Mwenyekiti huyo alisema kuwa wafugaji wamekuwa wakifunga safari kwenda mkoani Dodoma kwa ajili ya kuonana na mawaziri wahusika akiwemo, Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dk.Titus Kamani , aliyekuwa Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka na Waziri Mkuu Pinda.

  Pia alisema wamefanya vikao kati yao na wakuu wa wilaya za mkoa wa Kagera pamoja na Mkurugenzi wa Wanyamapori lakini hakuna kilichoifanikiwa zaidi ya kupewa tarehe ya kwamba ufumbuzi utapatikana.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma taarifa ya vikao 17 vilivyofanyika kati ya Wafugaji hao (pichani)  na viongozi mbalimbali  wa Serikali,kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa mgogolo wao dhidi ya Askari wanyama pori lakini hakuna maamuzi ama suluhisho lililopatikana.Kinana amekutana na wafugaji hao mapema leo katika kijiji cha Nyakanazi wilayani Biharamulo na kutoa kero zao kwake juu ya manyanyaso wanayofanyiwa na askari wa wanyamapori.

  Alisema kuna mambo mawili yamemsikitisha, moja watu kutumia mwavuli wa sheria kufanya mambo yao binafsi kwani hakuna Serikali inayoweza kutumbukiza ng'ombe kwenye shimo.

  "Wizi ,rushwa ndicho kinachoonekana ndani yake, kwa maelezo yenu kuna baadhi ya watendaji wameamua kuchukua sheria mkononi mwao.Wanachukua milioni 10 za mfugaji na kisha zinakwenda kwenye mifuko yao,"alisema.

  Alisema lazima akiri, Serikali nayo imelegea mno katika kuchukua maamuzi, kwani amehesabu vikao ambavyo wafugaji wamekaa na viongozi wa ngazi mbalimbali za juu serikali vipatavyo 17 lakini hakuna ufumbuzi na badala yake ni maneno, maneno tu.

  Alisema kama wameshindwa kutatua matatizo ya watu ni vema wakaa kando maana mishahara wanalipwa na marupurupu wanapewa lakini kushughukulikia matatizo ya watu imekuwa ngumu.

  "Watu wameuawa, ng'ombe wamekufa, ng'ombe wameporwa.Hii haiwezekani na kwamba matatizo yote yanayohusu wanyamapori wenye mamlaka ni Wizara ya Maliasili na Utalii.

  "Niombe mambo mawili yafanyike, ng'ombe waliokamatwa warudishwe kwa wafugaji na pili kesi zilizopo mahakamani zifutwe na wenye mamlaka ya kuzifuta ni Serikali maana ndio waliofungua kesi,"alisema Kinana.
  Baadhi ya wafugaji wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati alipokuwa akizungumza nao katika kijiji cha Nyakanazi Wilayani Biharamulo mkoani Kagera.Kwa mujibu wa wafugaji hao wameeleza kuwa wilaya zote zilizopo Mkoa wa Kagera na hasa Wilaya ya Ngara , wafugaji wamekuwa wakipata mateso makubwa pindi mifugo yao inapokamatwa kwenye pori la Kimisi ambapo ng'ombe wamekuwa wakipigwa risasi na wengine kuingizwa kwenye shimo refu lenye tope linalojulikana kwa jina la Gwantanamo.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Kanda ya Ziwa Bwa.Mugisha Murshad wakati alipokuwa akimuonyesha eneo linalotumika kuhifadhi mifugo yao mara inapokamatwa na kuwa eneo hilo ni dogo na halina chakula cha mifugo wala maji jambo ambalo hupelekea mifugo kufa kwa wingi.
  Mmoja wa wafugaji akimuonesha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana eneo ambalo mifugo inayokamatwa hupelekwa hapo na kuwekwa kwa muda mrefu bila maji wala chakula na matokeo yake mifugo hufa,iwapo mwenye mifugo hiyo hakwenda kuikomboa kwa gharama itakayokuwa imetajwa,ambayo wafugaji hao wamekuwa wakiilamimikia 
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akioneshwa eneo ambalo mifugo ya Wafugaji ilikuwa ikikusanywa eneo hilo na kuacha kwa muda mrefu bila chakula wala maji na hatimae kupoteza uhai,jambo ambalo wafugaji hao wameona ni kitendo cha uonevu na unyanyasaji mkubwa,kwani kwa kukamatwa mifugo yao wamekuwa wakitozwa fedha nyingi kuikomboa mifugo yao,hivyo wameomba Ndugu Kinana kusikiliza kilio chao cha mda mrefu.

  0 0

   Twaha Sultan akionyesha mpira anaotumia kwa ajili ya kujisaidia hali ambayo inampa maumivu makali pamoja na kupata gharama kubwa ya kubadilisha mpira kila baada ya wiki tatu.
    Mama mdogo wa Sultan, Sarha akionyesha uvimbe unaomsumbua mtoto Twaha sultan.
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Sitti Tanzania Foundation, Sitti Mtemvu akizungumza baada ya kukabidhi msaada wa shs laki mbili kwa ajili ya kusaidia matibabu yake. 
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Sitti Tanzania Foundation, Sitti Mtemvu (kushoto), akimkabidhi msaada wa sh. laki mbili, Sarha Magamba, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kusaidia matibabu ya mtoto, Twaha Sultan (17), mkazi wa Kipawa Karakata (katikati), ambaye ana uvimbe wa kilo nne na nusu mgongoni.Yeyote atakayeguswa na tatizo la mtoto huyo anaweza kuwasiliana na mlezi wake kupitia namba ya simu  0713970491. 

  Mwenyekiti wa Taasisi ya Sitti Tanzania Foundation, Sitti Mtemvu (kushoto), akimkabidhi msaada wa sh. laki mbili, Sarha Magamba, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kusaidia matibabu ya mtoto, Twaha Sultan (17), mkazi wa Kipawa Karakata (katikati), ambaye ana uvimbe wa kilo nne na nusu mgongoni.Yeyote atakayeguswa na tatizo la mtoto huyo anaweza kuwasiliana na mlezi wake kupitia namba ya simu  0713970491. 
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Sitti Tanzania Foundation, Sitti Mtemvu akiwasili nyumbani kwa mtoto Twaha Sultan Kipawa Karakata jijini Dar es Salaam ambapo alikabidhi msaada wa fedha kwa ajili ya matibabu ya mototo huyo anayekabiliwa na uvimbe mgongoni. Uvimbe huo unakadiliwa kufika kilo nne na nusu na kuweza kumuathiri mtoto huyo katika masomo yake kutokana na kushindwa kwenda shule. Yeyote atakayeguswa na tatizo la mtoto huyo anaweza kuwasiliana na mlezi wake kupitia namba ya simu  0713970491.
   Mama Mdogo wa mtoto Twaha sultan (17), Sarha Magamba mkazi wa Kipawa Karakata akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matatizo uvimbe wa ajabu katika mgngo wake mtoto sultan ambaye anahitaji kufanyiwa upasuaji. 
   Twaha Sultan akionyesha mpira anaotumia kwa ajili ya kujisaidia hali ambayo inampa maumivu makali pamoja na kupata gharama kubwa ya kubadilisha mpira kila baada ya wiki tatu.

    Mama mdogo wa Sultan, Sarha akionyesha uvimbe unaomsumbua mtoto Twaha sultan.
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Sitti Tanzania Foundation, Sitti Mtemvu.

  0 0

  Zanzibar Telecom (Zantel) started its operations in Zanzibar in 1999 as a subsidiary of Emirates Telecommunications Corporation (Etisalat) and extended its footprint to the Mainland of Tanzania in 2005.


  Zantel is a joint venture between Etisalat and Government of Zanzibar with current shareholdings of 85% and 15%, respectively. On 4th June 2015, Etisalat has agreed to sell its stake in Zantel to Millicom International. 

  The Government of Zanzibar and Etisalat have both been active participants during the sale process. The key objective of the sale process has been to secure a long-term future for Zantel, its employees and the brand.

  The sale is subject to regulatory approval by the Tanzanian Communication Regulatory Authority and the Fair Competition Commission. After the sale closes, Millicom International will have an 85% shareholding in Zantel and the Government of Zanzibar will remain with 15%.

  As the transaction is only a change in one of Zantel’s shareholders, it will not affect Zantel customers. Zantel services will continue as normal and Zantel will honour its commitment to its other stakeholders.

  0 0

   Sehemu ya Mandhari ya mji wa Bukoba kama uonekanavyo pichani,mbele yake ni moja ya kisiwa kiitwacho Misira
   Sehemu ya katikati ya mji wa Bukoba kama uonekanavyo jioni ya leo.

   Sehemu ya mji wa Bukoba kama uonekanavyo pichani

  0 0


  0 0


  0 0

  1
  Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiweka jeneza la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa kwenye nyumba yake ya milele. Mazishi hayo yamefanyika leo Juni 05, 2015 katika kijiji cha Kidia, Old Moshi Mkoani Kilimanjaro.
  2
  Jeneza la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa likiwa tayari limewekwa kwenye nyumba yake ya Milele.
  3
  eneza la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa likiwa tayari limewekwa kwenye nyumba yake ya Milele.
  4
  Askofu Mstaafu Dkt. Martin Shayo wa Diyosisi ya Kasikazini akiweka akiongoza Ibada Maalum ya mazishi ya Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa ambaye amefariki Juni 2, 2015 katika Hospitali ya Dar Group, Jijini Dar es Salaam(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi ka Magereza, John Casmir Minja.
  6
  Gadi Maalum ya Maofisa wa Jeshi la Magereza wakitoa heshima kwa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu, Onel Malisa katika Gwaride la mazishi yake.
  7
  Kabuli la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa likiwa limepambwa na mashada ya maua baada ya mazishi.
  8
  Umati wa watu waliojitokeza katika mazishi ya Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa.
  9
  Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa pili kushoto) akiimba wimbo kwenye Ibada Maalum ya kumuombea kheri Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa baada ya shughuli za mazishi kukamilika(kulia) ni Mchungaji Frank Machanga kutoka Jimbo la Kasikazini(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

older | 1 | .... | 545 | 546 | (Page 547) | 548 | 549 | .... | 1904 | newer