Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 541 | 542 | (Page 543) | 544 | 545 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Baadhi ya uchafu uliokuwa katoka fukwe ya Bahari inayoizunguka Hoteli ya Double Tree by Hilton ya jijini Dar.
  Mkurugenzi mkuu wa Hotel ya Double Tree by Hilton nchini Tanzania, Bw.Ian Mclachan (wa pili kutoka kushoto) akifanya usafi katika ufukwe wa Bahari inayoizunguka Hoteli ya Double Tree huku akishirikiana bega kwa bega na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Hoteli ya Double Tree By Hilton, Bw. Yehia Elmansoury (wa kwanza kushoto).
  Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Double Tree by Hilton, Bw. Florenso Kirambata(kushoto) akifanya usafi wa mazingira katika fukwe inayoizunguka hoteli hiyo ya jijini Dar es Salaam huku akiwa pamoja na mmoja wa wafanyakazi wa hoteli hiyo.

  Wafanyakazi wa hoteli ya Double Tree ya jijini Dar es Salaam wakifanya usafi maeneo yote yanayoizunguka hoteli hiyo
  Wafanyakazi wa hoteli ya Double Tree ya jijini Dar es Salaam wakiongozwa na Mkurugenzi mkuu wa Hotel ya Double Tree by Hilton nchini Tanzania, Bw.Ian Mclachan (wa kwanza kulia) wakiwa na mifuko ya uchafu katika picha ya pamoja mara tu ya kumalizika kwa usafi uliofanyika kwenye fukwe zinazoizunguka Hotel hiyo.
  Wafanyakazi wakiweka uchafu kwenye gari la kubebea taka mara baada ya kumaliza kufanya usafi
  Viongozi na wafanyakazi wa Hoteli ya Double Tree by Hilton ya jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya Hotel hiyo mara baada ya kumaliza kufanya usafi. Picha na Geofrey wa Pamoja Blog

  0 0

  Naibu Katibu mkuu wa Chadema Taifa upande wa Zanzibar Salum Mwalimu akizungumza wakati wa mahafali ya Chaso mkoa wa Kilimanjaro yaliyofanyika katika shule ya sekondari Majengo.

  Naibu katibu mkuu Chadema Zanzibar,Salum Mwalimu akitunuku yeti kwa wanafunzi wana tarajia kumaliza elimu ya chuo kikuu ambao ni wanachama wa Chaso mkoa wa Kilimanjaro.
  Baadhi ya wanachama wa Chaso  kutoka vyuo mbalimbali mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katimsikiliza Naibu katibu mkuu wa Chadema taifa,upande wa Zanzibar Salum Mwalimu wakati wa sherehe za umoja huo.
  Wakili wa kujitegemea Elikunda Kipoko (katikati) akisikiliza kwa makini hotuba ya Naibu katibu mkuu Zanzibar ,Salum aliyoitoa wakati wa mahafali ya kuhitimu kwa wanafunzo wa vyuo vikuu ,wanachgama wa Chaso. 
  Mbunge wa Viti maalum Lucy Owenya (Chadema) katikati akiwa na Diwani wa kata ya Longuo ,Raymond Mboya (Kushoto) na kulia kwake ni aliyekuwa katibu wa Chadema wilaya ya Moshi vijijini.Aquiline Chuwa .
  Aliyekuwa katibu wa Chadema wilaya ya Moshi vijijini,Aquilene Chuwa akizungumza katika mahafali hayo.
  Naibu katibu mkuu Chadema Zanzibar,Salum Mwalimu akitunuku yeti kwa wanafunzi wana tarajia kumaliza elimu ya chuo kikuu ambao ni wanachama wa Chaso mkoa wa Kilimanjaro.
  Mratibu wa Chaso aliyemaliza muda wake ,Ibrahim Chotola  akizungumza wakati akiaga nafasi hiyo rasmi na kukabidhi kwa mratibu mpya wa Chaso mkoa wa Kilimanjaro.
  Chotola akifanya utambulisho wa mratibu mpya wa Chaso mkoa wa Kilimanjaro Malijoel Mali.
  Mratibu mpya wa Chaso mkoa wa Kilimanjaro ,Malijoel Mali akitoa salamu ya chama chake mara baada ya kukabidhiwa rasmi mikoba ya kufanya shughuli za Umoja huo. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.  0 0

  Benki ya Exim Tanzania imezindua kampeni maalum ya kuhamasisha wateja wake kufungua akaunti ya amana ya malengo (Fixed Deposit Account) ikiwa sehemu ya mpango wa benki hiyo kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba miongoni mwa watanzania.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma lililopita, Meneja Bidhaa wa Benki hiyo, Bw Aloyse Maro alisema lengo kuu la kampeni hiyo ni kukuza utamaduni wa kuweka akiba hapa nchini ili kuongeza tija kwenye maendeleo ya taifa.

  "Kampeni hii ina lengo la kukuza utamaduni wa kuweka akiba hapa nchini.Viwango vya ushindani vinavyotolewa na benki yetu ndio chachu ya mafanikio kwenye kampeni yetu hii kwakuwa kupitia akaunti hii wateja wetu wataweza kunufaika zaidi kwa kupata kiasi kikubwa cha faida mrejesho kutoka kwenye akaunti zao,’’ alibainisha Bw. Maro.

  Katika jitihada za kuonyesha dhamira ya benki hiyo katika kuhamasisha zaidi ufunguaji wa akaunti hiyo, Bw. Maro aliongeza kuwa kampeni hiyo itaambatana na zawadi za kila mwezi kwa wateja watakaokuwa wanafungua akaunti hiyo.

  "Zawadi hizi za kila mwezi ni pamoja na simu aina ya iphone. Pia tunatarajia kutoa zawadi ya gari kama tuzo kuu '' alitangaza meneja huyo kwa majigambo.

  Bw.  Maro alisisitiza zaidi kuwa Benki hiyo inadhamira ya dhati katika kuhakikisha kwamba wateja wake wanapata huduma na bidhaa bora zaidi za kibenki huku pia akitumia fursa hiyo kuwashawishi wateja wa benki hiyo kufika au kuwasiliana na matawi ya benki hiyo ili kupata maelezo zaidi kuhusu kampeni hiyo.

  0 0

  Naibu balozi bi Maura Mwingira akitoa pole kwa watoto wa Mzee Luangisa, Bi Maura Mwingira kwa niaba ya balozi alipata nafasi ya kuongea machache mbele ya Watanzania waliojitokeza kwenye misa hiyo ya kumuombea marehemu mzee Luangisa pamoja na kuaga mwili wake tayari kwa safari ya kwenda nyumbani Bukoba Tanzania kwa mazishi.
  Mtoto wa marehem Kwame akitoa wasifu wa mzee Luangisa wasifu huo uliwatoa machozi watu kutokana jinsi mzee Luagisa alivyokuwa mtu mwenye moyo wa kutoa kwakile alichonacho bila kuchagua wala kuhoji.
  Mchungaji akiongoza misa mbele ya Watanzania wa New York na miji ya karibu na New York.
  Watoto wa marehem wakiwa na sura za udhuni ya kuondokiwa na baba yao mpendwa ambae alikuwa nguzo ya familia hii pendwa.
  Watu wakiaaga mwili wa mzee Luangisa pamoja na misa iliyofanyika jumamosi ya tarehe 30 mwezi wa 5. Kwa picha zaidi nenda soma Hapa.

  0 0

  Mwenyekiti Mpya wa mji mdogo wa Himo,Hussein Jamal akiwasili katika ukumbi wa King size katika mji wa Himo kwa ajili ya sherehe ya kupongezwa baada ya kufanikiwa kushinda kiti hicho.
  Baaadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi waliofika katika sherehe ya pongezi kwa mwenyekiti wa mji mdogo wa Himo.
  Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya mji wa Himo wakiwa katika sherehe hizo.
  Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi vijijini Miriam Kaaya akizungumza wakatio wa sherehe za kumpongeza mwenyekiti wa mji mdpgo wa Himo ,Hussein Jamal.
  Kamanda wa Uhamasishaji wilaya ya Moshi Vijijini Hassan Hussein,akizungumza wakati wa sherehe hizo.
  Mjumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi kutoka wilaya ya Kinondoni,
  Mzee Shayo maarufu kama King size akimpongeza naibu kamanda wa jumuiya ya Vijana wilaya ya Moshi vijijini ,Innocent Melecky  kwa uamuzi wake wa kutangaza nia ya kutaka kugombea jimbo la Vunjo.
  Viongozi wakiimba nyimbo za pongezi .
  Mwenyekiti mpya wa mji mdogo wa Himo ,Hussein Jamal akizungumza na wananchi waliofika katika sherehe za pongezi zilizofanyika katika ukumbi wa King size uliopo mji mdogo wa Himo. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Afya na ustawi wa jamii Dk. Donan Mbando akiwa kwenye picha ya pamoja na madaktari na viongozi wa chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi cha Muhimbili (MUHAS)  mara baada ya kufunga mkutano mkuu watatu wa sayansi ya afya uliondaliwa na chuo hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Kushoto kwake ni Makamu mkuu wa MUHAS, Prof. Ephata Kaaya. 
   Katibu Mkuu Wizara ya Afya na ustawi wa jamii Dk. Donan Mbando akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa udaktari, madaktari na viongozi wa chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi cha Muhimbili (MUHAS)  mara baada ya kufunga mkutano mkuu watatu wa sayansi ya afya uliondaliwa na chuo hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya na ustawi wa jamii Dk. Donan Mbando akiagana na baadhi ya wanafunzi wa udaktari kutoka chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi cha Muhimbili (MUHAS)  mara baada ya kufunga mkutano mkuu watatu wa sayansi ya afya uliondaliwa na chuo hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

  SERIKALI imewaomba watafiti wa masuala ya afya hapa nchini kuhakikisha kwamba wanaibua hoja mpya zitakazosaidia kuleta mabadiliko kwenye sera za kitaifa zinazohusu sekta hiyo muhimu. Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Katibu Mkuu Wizara ya Afya na ustawi wa jamii Dk. Donan Mbando mara tu baada ya kufunga mkutano mkuu watatu wa sayansi ya afya uliondaliwa na chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi cha Muhimbili (MUHAS).


  “Kwa sasa taifa linashuhudia ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaosumbuliwa na magonjwa yasiyoyakuwa ya mbukiza kama vile kisukari, shinikizo la damu na kisukari. Kwa bahati mbaya sana vituo vyetu vingi vya afya havijaandaliwa vizuri kukabiliana na magonjwa haya kwasababu sera zetu wakati zinaandaliwa hazikujika zaidi kwenye magonjwa yasiyoyakuwa ya kuambukiza na ndio maana tunahitaji mabadiliko kwenye hili,’’ alisema Dr. Mbando.


  Dr. Mbando alizataja sababu kubwa zinazochangia ongezeko la magonjwa hayo kuwa ni pamoja na matumizi ya pombe kupita kiasi, aina ya vyakula vinavyotumiwa na watanzania hususani wale wanaoishi maeneo ya mijini, kutokufanya mazoezi pamoja na uvutaji wa sigara. Aidha aliiongeza kuwa kwa sasa serikali ipo kwenye mpango wa kuandaa mkakati  wanne wa huduma za afya hapa nchini (health care financing strategy) utakao muwezesha kila mtanzania kuwa na bima ya afya. 

  “Kwa sasa ni asilimia 20 tu ya watanzania ndio wanamiliki bima za afya zinazotolewa na shirika la bima ya afya la taifa na mashirika binafsi na hivyo kufanya asilimia 80 ya watanzania kuishi bila kuwa na uhakika wa masuala ya tiba….hili tumelianza tayari,’’ alibainisha.

  Kuhusu mlipuko wa ugonjwa wakipundupindu kwenye mikoa ya kagera na kigoma uliosababishwa na kuingia kwa wakimbizi kutoka Burundi, Dr. Mbando alisema kwa sasa serikali kwa kushirikiana na Wananchi, wadau wa maendeleo na asasi zisizo za kiraia wanapambana kuhakikisha tatizo hilo linakwisha.


  Akizungumza kwenye mkutano huo Makamu mkuu wa MUHAS, Prof. Ephata Kaaya alisema kwa sasa taifa linahitaji zaidi tafiti za kiafya hususani kwenye magonjwa yasiyo ya kuambukiza na ndio sababu mkutano huo ulijikita zaidi kujadili tatizo hilo. 

  “Kama wataalamu wa masuala ya afya tunaona kuna haja kubwa tukiwekeza katika tafiti zinazolenga kuibua changamoto na suluhisho kwenye magonjwa haya,’’ alisema. Mkutano huo wa siku mbili ulihudhuriwa na washiriki zaidi ya 300 wakiwemo madaktari, viongozi na wanafunzi wa udaktari kutoka MUHAS na vyuo vingine vya afya.  0 0

  Muwakilishi wa Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa TBS Joseph Masikitiko  katika Hafla ya maamuzi ya fomu za shindano la mamashujaa wa Chakula Bi. Stella E. Mrosso wa kwanza kushoto, wa pili kutoka kushoto ni Tusfaye Legesse Obole President's Delivery Bureau, Manager Agriculture Productivity na  Mratibu wa Programu kutoka Care International in Tanzania Maureen Kwilasa ambaye ni Mkuu wa mahabara ya Chakula TBS akifungua rasmi hafla hiyo ya kuanza kuzihakiki fomu hizo .
   Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea juu ya shindano la Mama shujaa wa Chakula .
   Mratibu wa Programu kutoka Care International in Tanzania Maureen Kwilasa akisisitiza jambo wakati wa Hafla hiyo
   Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiwashukuru TBS , Majaji pamoja na washiriki ambao ndio watazipitia fomu hizo kabla hazijafika kwa majaji.

   Mkuu wa maabara chakula TBS Stella E. Mrosso aliye Mwakilisha Mgeni rasmi katika hafla hiyo akimkabidhi rasmi fomu za shindano la mama shujaa wa chakula  Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster kwa ajili ya kuanza kufanya maamuzi.

   Vijana wenye fani mbalimbali  kutoka vyuo vikuu na taasisi mbalimbali  wakiwa katika mchakato kwa kuzipitia Fomu zote za maombi ya kushiriki shindano la mama shujaa wa Chakula 2015
   Hafla ikiwa inaendelea 
  ****
  Shindano la mama shujaa wa chakula limeingia katika hatua mpya baada ya zoezi la kukusanya fomu za washiriki kutoka mikoa mbalimbali nchini kupitiwa na majaji kwa ajili ya mchujo ambapo washiriki 18 watapatikana kisha baadaye 15 bora ambao wataingia kijijini kwa ajili ya mchakato wa kugombea nafasi ya mama shujaa wa chakula mwaka 2015.

  zoezi la kusahihishwa fomu  limezinduliwa mapema leo hii na mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TBS, Joseph Masikitiko ambaye ni Mkuu wa Maabara na Chakula TBS, Bi. Stella Mrosso akiwa sambamba na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Oxfam Tanzania, Jenny Foster na majaji watakaopitia zoezi zima la mchujo wa fomu hizo.

   Akizungumza na wageni waandishi wa habari katika uzinduzi huo Mkuu wa Maabara na Chakula, Bi. Stella Mrosso alilisifu shirika la Oxfam kuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za wanawake, umiliki wa ardhi na kuhamasisha uzalishaji wa chakula kwa wazalishaji wadogo wadogo.

  Bi. Stella alisisitiza kuwa kila mzalishaji anapaswa kuzalisha bidhaa bora ili kushindana na soko la ndani na la nje huku akifafanua kuwa kwa kupitia SIDO, TFDA na Wizara ya Afya, wazalishaji wadogowadogo watakuwa na uwezo wa kupata kibali kutoka TBS bure na kuongeza kuwa wakina mama nchini watumie shindano la mama shujaa wa Chakula kama chachu ya kujitokeza kwa wingi katika mashindano yanayofuata huku wengine wakijifunza uzalishaji bora kupitia mashindano hayo.

  0 0

  New Picture (7)
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Vangimembe Lukuvi akikata utepe kuzindua ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Mjini Kahama. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Felix Maagi
  New Picture (2)
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi(aliyevaa miwani) akiweka jiwe la msingi katika nyumba zilizojengwa na NHC Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
  1
  Hizi ni miongoni mwa nyumba 50 za gharama nafuu zilizojengwa na NHC katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula katika halmashauri ya Mji Kahama mkoani Shinyanga. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Mh.William Vangimembe Lukuvi ameweka jiwe la msingi katika nyumba hizo.
  New Picture (4)
  Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC Bw. Haikamen Mlekio akitoa maelezo kwa Waziri Lukuvi kuhusu hatua zilizofikiwa katika mradi wa nyumba 50 zinazojengwa na NHC Wilayani Kahama ulioanza kujengwa mwezi Januari mwaka 2015 na kutarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2015.
  New Picture (5)
  Waziri Lukuvi akitizama michoro ya mradi wa nyumba 50 utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.1 unaotekelezwa na NHC Wilayani Kahama.
  New Picture (8)
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akikagua majengo ya nyumba 50 zinazojengwa na NHC eneo la Bukondamoyo Wilayani Kahama akiambatana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Felix Maagi (kushoto)


  New Picture (1)
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Mh.William Vangimembe Lukuvi akiwasili kuweka jiwe la msingi zilizojengwa na NHC eneo la Bukondamoyo Mjini Kahama.
  New Picture (3)
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akielekea kwenye ya mfano ili kuikagua na kukata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Mjini Kahama.
  New Picture (9)
  Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Felix Maagi akitoa maelezo kwa Waziri Lukuvi baada ya kukagua moja ya majengo hayo 50 yaliyojengwa na NHC eneo la Bukondamoyo Wilayani Kahama.
  New Picture (11)
  Meza Kuu- Waziri Lukuvi akitazama kikundi cha ngoma wakati alizindua nyumba za gharama nafuu za NHC Mjini Kahama lengo likiwa la kupendezesha mandhari ya miji yetu, kupandisha hadhi ya maeneo lakini pia kuwapatia wananchi wa kipato cha chini nyumba bora na gharama nafuu
  New Picture (12)New Picture (15)
  Kundi la sanaa la Makhirikhiri la Kahama wakitoa burudani
  New Picture (16)
  Mkuu wa Wilaya ya Kahama Bw. Benson Mpesya akizungumza eneo la Bukondamoyo na kulipongeza Shirika la Nyumba la Taifa kwa kujenga nyumba za kisasa na imara na kutoa msaada wa mashine za kufyatulia matofali katika halmashauri za wilaya nchini.
  New Picture (17)
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC,, Bw. Felix Maagi akizungumza eneo la Bukondamoyo ambapo alisema halmashauri zitakazotoa ushirikiano na kuwa tayari kununua nyumba ndizo zitazojengewa nyumba na NHC.Bw. Felix Maagi, alisema pia kuwa mradi huo umetengeza ajira za moja kwa moja 290, ajira shirikishi 145 na makazi ya watu 300.
  New Picture (18)
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini William Lukuvi akiwahutubia wakazi wa Kahama katika eneo la mradi wa nyumba 50 zilizojengwa na NHC katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula Wilayani Kahama.Alizitaka Halmashauri za Wilaya kupima maeneo ya Miji na kuyagawa kwa wananchi kwa utaratibu unaotakiwa ili kuondoa migogoro ya ardhi na kuweka mipango miji vizuri.
  New Picture (19)
  Mbunge wa Jimbo la Kahama Mh. James Lembeli akizungumza katika eneo la mradi ambapo aliwataka wakazi wa Kahama kuchangamkia fursa ya nyumba hizo kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ya kibiashara katika eneo hilo ili fedha za watu watakaoishi hapo zisitoke nje ya eneo hilo.
  New Picture (20)
  Waziri William Vangimembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wealiohudhuria uzinduzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Bukondamoyo Mjini Kahama.
  New Picture (21)
  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh. William Lukuvi akiondoka eneo la tukio akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Felix Maagi
  New Picture (22)
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akiagana na Mbunge wa Jimbo la Kahama Mh. James Daudi Lembeli mara baada ya kuzindua nyumba za gharama nafuu eneo la Bukondamoyo.

  0 0
   THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  Telephone: 255-22-2114512, 2116898
  Website : www.ikulu.go.tz              

  Fax: 255-22-2113425


  PRESIDENT’S OFFICE,
        STATE HOUSE,
                1 BARACK OBAMA ROAD,  
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Rais Kikwete aanza ziara ya nchi tatu Ulaya.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Juni Mosi, 2015 ameanza ziara rasmi ya wiki moja katika nchi tatu za Ulaya kwa mwaliko wa viongozi wa nchi hizo.

  Rais Kikwete ambaye aliondoka nchini usiku wa jana, Jumapili, Mei 31, 2013 baada ya kumaliza kuendesha Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Burundi ameanzia ziara yake katika Finland ambako atakaa kwa siku tatu.               

  Baadaye, Rais Kikwete atatembelea nchi za Sweden na Uholanzi kabla ya kurejea nyumbani.

  Katika Finland, Rais Kikwete miongoni mwa mambo mengine kesho Jumanne, Juni 2, 2015, atafanya mazungumzo rasmi ya Kiserikali na Rais wa nchi hiyo na baadaye atatembelea Bunge la nchi hiyo ambako atafanya mazungumzo na Wabunge.

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.  1 Juni, 2015

  0 0

  Mgeni Rasmi kwenye halfa ua Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Pamoja na Vipodozi Pendwa Vijulikanavyo kama Luv Touch Manjano Mke wa Waziri Mkuu Mh Tunu Pinda Akitoa Hotuba yake katika Uzinduzi huo .Katika Hotuba yake Mh Mama Pinda Alisema amefurahishwa sana Kwa Mwanamke wa Kitanzania Kuanzisha Bidhaa amabyo imeweza kushindana na Bidhaa kama hizo kutoka mataifa Mengine.Halfa hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.Hafla hiyo ya uzinduzi ilifunguliwa na mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania mama Tunu Pinda. 

  Alizindua rasmi kwa soko la Tanzania poda ya luvtouch Manjano, rangi ya awali (foundation), na rangi ya mdomo (lipstick) na walio hudhuria hafla hiyo walipata nafashi ya kushuhudia thamani ya bidhaa hizo, aina ya urembo na viwango vya ubora vinvyoshinda hoja zote na kuthibitisha kuwa bidhaa za hapa nchini zinaweza kushindana na bidhaa za kimataifa. Wanawake wengi walipata fursa ya kujaribu moja ya bidhaa hizo na waliweza kununua bidhaa za LuvTouch Manjano ukumbini.

  Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar Akisisitiza Jambo kwenye Halfa Hiyo.Mh Balozi Majaar Alisisitiza Umuhimu wa Kumsomesha Mtoto wa Kike Pamoja na Kuwawezesha Kiuchumi.Balozi Majari alisiistiza Jamii ya Kitanzania Kuachana na Kasumba ya Kuwanyanyapaa Watoto wa Kila pia Kutokuwawezesha na Akasema mtoto wa Kike akipewa Fursa ya Kupata Elimu na Kuwezeshwa Wanawake Wanaweza .

  Hafla hiyo pia ilihusisha kuzindua Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa miradi na programu ambazo zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea umasikini wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha yake. Shirika hili limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu.

   Shear illusions ilikusanya wanawake takriban 450 wa Kitanzania kusherehekea miaka 10 ya safari ya kumfurahisha kila mwanamke, pamoja na kuzindua kipodozi pendwa cha LuvTouch Manjano iliyobuniwa na Shekha Nasser, mmiliki wa Shear illusions. Pamoja na uzinduzi huo, alizundua pia kitabu cha muongoza kwa kina mama kuonyesha jinsi ya kujipodoa kitaalam kwa kutumia nyenzo na vipodozi sahihi.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser Katikati akiongea Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda (Kulia) Pamoja na Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar
  Balozi wa Manjano Foundation Irene Paul Wakati wa Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Pamoja na Uzinduzi wa Vipodozi Pendwa vya Luv Touch.
  Balozi wa Manjano Foundation Irene Paul (Kulia) Akiwa n Mtoa Mada katika Halfa hiyo Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda
  Msanii aliyetumbuiza Kwenye Halfa Hiyo Brian Mugenyi akitoa Burudani ya aina yake kwenye Halfa hiyo iliambatana na Uzinduzi wa Vipodozi vya Luv Touch 
  Wageni waalikwa walioshiriki katika halfa ya Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation
  Mshereheshaji wa Halfa Hiyo Ndugu Angela Bongo akiwa na Msanii aliyetumbuiza Kwenye Halfa Hiyo Brian Mugenyi 
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser wa Pili Kushoto akiwa Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda wa Pili Kulia Pamoja na Watoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar na Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda.
  Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda Katikati Pamoja Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser wa Kushoto na Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda. 
  wageni walikwa

  0 0

  1 
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Fatma Ali akizungumza na wananchi kabla ya kuzindua mpango wa kupeleka madaktari Bingwa katika mikoa ya pembezoni ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa kusafiri umbali mrefu kwenda kufuata huduma hizo katika hospitali kubwa,
  2
  2. Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Raphael Mwamoto, akitoa maelezo kuhusu mpango wa Madaktari Bingwa wanaopelekwa mikoani na Mfuko huo.
  3
  Baadhi ya wakazi wa Mtwara wakisubiri huduma za madaktari Bingwa,
  4
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Fatma Ali akiwa katika picha ya pamoja na madaktari Bingwa baada ya kuzindua rasmi huduma ya madaktari Bingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara,
  ..........................................................................................................
  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF unaendelea na mpango wake wa kupeleka madaktari Bingwa katika mikoa ya pembezoni ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa kusafiri umbali mrefu kwenda kufuata huduma hizo katika hospitali kubwa. 

   Mpango huo pia unalenga kuwajengea uwezo wa kiutendaji madaktari walioko katika hospitali za mikoani ambao watafanya kazi pamoja na madaktari bingwa hao.Madaktari waliokwenda Mtwara ni pamoja na wagonjwa ya akinamama,m magonjwa ya ndani, bingwa wa upasuaji na bingwa wa dawa za usingizi.Zoezi hilo litadumu kwa muda wa siku sita.

  Akizindua zoezi hilo Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Bi. Fatma Ali amewahimiza wananchi wa mkoa wa Mtwara kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF ili kuujengea uwezo zaidi Mfuko huo kupeleka huduma za kibingwa katika mikoa mingi zaidi.

  0 0

   Jaji Antony Bahati enzi za uhai wake.
   Waombolezaji wakiweka sahihi kitabu cha maombolezo.
  Mwili wa Jaji mstaafu Antony Bahati ukiwasili nyumba kwake Oysterbay ambapo mazishi yanafanyika leo Juni 2 katika makaburi ya Kinondoni. 
  Mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani.
   Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa Jaji mstaafu, Antony Bahati nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam. Mazishi ya jaji Bahati yanafanyika leo Juni 2 katika makaburi ya Kinondoni. (Picha na Francis Dande)
   Baadhi ya waombolezaji.
   Ndugu na jamaa wakiwa nyumbani kwa marehemu jaji mstaafu Antony Bahati.
   Waombolezaji wakiwasili nyumbani kwa marehemu.
   Watoto wa marehemu wakiwa na huzuni mara baada ya mwili kuwasili nyumbani.
   Mwili ukiwa umehifadhiwa nyumbani.

  0 0

   Muonekano wa viwanja vya Mabano vilivyopimwa na Taasisi ya UTT-PID kwa ushirikiano na Halmashauri vilivyopo Manispaa ya Lindi.
  Baada ya kupima na kufanikiwa kuuza viwanja zaidi ya 2,500 katika fukwe za Mabano na Mmongo kwa ushirikiano na Manispaa ya Lindi, Mradi huo umeingia katika hatua ya upanuzi wa barabara kuu na za mitaa ndani ya mradi ambapo kwa ushirikiano huo zaidi ya Shilingi Billion 1 zinatarajiwa kutumika mpaka kukamilika kwake.
  Mradi huo mkubwa zaidi nchini katika upimaji wa viwanja Manispaa ya Lindi ulifadhiliwa na Taasisi ya UTT-PID utekelezaji wake ulianza mapema mwaka 2013 na sasa uaandaji wa hati kwa wanunuzi upo katika hatua ya mwisho baada ya kila mteja wa kiwanja kufanikiwa kuweka saini kwa hati zao katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Lindi kwenyewe.
   Uchongaji wa hatua za awali wa Barabara ukiendelea katika eneo la Mradi. Ujenzi wa barabara hizi unatarajia kukamilika kabla ya wanunuzi kuuanza ujenzi wa makazi yao katika eneo la mradi.
  Uwekezaji huo ukiendelea pia Taasisi hiyo kwa ushirikiano huo na Halmashauri ya Lindi inatarajia kuingia katika awamu ya pili ya Mradi wa upimaji viwanja katika fukwe hizo ambapo zaidi ya viwanja elfu tano vitapimwa na kuuza kwa wananchi wote. Utekelezaji wa awamu ya pili bado upo kwenye hatua za awali na unatarajia kuuanza ndani ya mwaka huu 2015.
   Viwanja vya Mabano na Mmongo vipo katika fukwe nzuri na vikipata upepo mwanana kutoka bahari ya Hindi.
  Toka kuanzishwa kwake Taasisi ya UTT-PID imejikita sana katika upimaji wa maeneno katika mikoa mbalimbali kwa kushirikiana na Halmashauri tofauti nchini. Miradi mikubwa kama ya Bukoba ambapo viwanja zaidi ya 5,000 vilipima kuuzwa, Halmashauri ya Sengerema kwa ushirikiano na Taasisi ilipima zaidi ya viwanja 1,200 na uuzaji pamoja na uwekezaji katika Miundombinu husika unaendelea kwa kasi. Pia Taasisi imewekeza katika miradi binafsi kama vile eneo la Mapinga katika wilaya ya Bagamoyo huku ikatarajia uwekezaji mkubwa zaidi katika mikoa ya Morogoro , Arusha, Dar es Salaam, Maswa, Pwani, Maswa na Ruvuma.
   Upanuzi huu wa barabara utafanyika mpaka kwenye fukwe kuwapa nafasi wakazi wa eneo husika kutembelea maeneo ya fukwe hizo
  Zaidi ya viwanja 2,500 vilipimwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali kama vile Makazi, Biashara, Maeneo ya Umma na sehemu za kupumzika. (Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog).

  0 0


  Na DixonBusagaga.Moshi.

  MAMLAKA ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA) inakusudia kuongeza bei ya kutoa huduma za maji kwa watumiaji wake ,lengo likiwa ni kutaka kuendelea kufanya maboresho katika utolewaji wa huduma hiyo.


  Kwa mujibu wa ombi Na,TR-W-15-008 kutoka Muwsa kwenda Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji(EWURA) Mamlaka ya maji safi na maji  taka mjini Moshi imetaka kuongeza beo ya huduma zake kwa mwaka 2015/2016 HADI 2017/2018.


  Mabadiliko ya bei hiyo inayopendekezwa itawahusu makundi mbalimbali ya watumiaji wa huduma hiyo hususani wale wa majumbani,Taasisi,Biashara ,Viwanda na wale wa kwenye Vioski.


  Mapendekezo mapya ya bei ya utolewaji wa huduma hiyo kutoka kiasi cha sh 495 kwa  Uniti moja ya ujazo wa maji ilivyo sasa hadi kufikia 710 katika kipindi cha mwaka 2015/2016 na kiasi cha sh  746 kipindi cha mwa 2016/2017 kwa wateja wa majumbani na taasisi.


  Kwa upande wa Biashara ,Muwsa imependekeza bei ya huduma hiyo kuwa ni kiasi cha sh  839 kwa uniti moja kipindi cha 2015/2016,n ash 881 kipindi cha mwak 2016/2017 kutoka kiasi cha sh 585 katika ,kipindi cha mwa 2014/2015.


  Eneo jingine ni kwa watumiaji wa viwandani ,ambao Muwsa imepndekeza bei ya huduma kuwa ni kiasi cha sh 947 katika kipindi cha mwaka 2015/2016 hadi kufikia kiasi cha sh 994 mwaka 2016/2017 kutoka 660 za sasa.


  Nao wamiliki wa vioski  bei iliyopendekezwa ni kiasi cha sh 696 katika kipindi cha mwa 2015/2016 hadi kufikia 731 katika kipindi cha mwala 2016/2017 kutoka kiasi cha sh 485 bei ya sasa.


  Kutokana na hali hiyo mamlaka ya udhibiti wa wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeandaa mkutano na wananchi wa manispaa ya Moshi ili kutoa maoni yao juu ya ongezeko la bei za huduma za maji .


  Mkutano huo unatarajia kufanyika June 4 mwaka huu ,kuanzia majira ya saa 4 asubuhi , katika ukumbi wa Hindu Mandal uliopo jirani kabisa na kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha mjini Moshi.


  Mgeni rasmi katika mkutano huo anatazamiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama.  0 0


  KWA MARA YA KWANZA SHOW YA AINA YAKE KATI YA WANA NDUGU WAWILI ALI NA ABDU KIBA ITAFANYIKA WASHINGTON DMV,JUMAMOSI HII PALE FIRE STATION 1, 8131,GEORGIA AVENUE,DOWN TOWN SILVER SPRING,VIP PACKAGE ZINAPATIKANA,FREE PARKING

  0 0

  Gari maalum kutoka Nchini Uganda lililobeba Mwili wa Mzee Samwel Ntambala Lwangisa ukiingia Bukoba. Na Faustine Ruta, Bukoba
  Mwili wa Marehemu Samuel Ntambala Luangisa uliwasili usiku wa kumkia leo katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera. Mauti yalimkuta akiwa Nchini Marekani na maziko yake itakuwa kesho jumatano june 3,2015. Wakati wa Uhai wake Marehe Samwel Luangisa aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Mkoa wa Kagera (ukiitwa ziwa magharibi), Aliwahi pia kuwa mbunge wa Bukoba Mjini, Meya wa Bukoba na Diwani wa Kata ya Kitendaguro hadi mauti yalipomkuta.
  Mtoto wa Marehemu Bi. Murungi
  Kulia ni Mbunge wa Bukoba Mjini Mh. Khamis KagashekiNi majonzi na huzuni.

  0 0


  Leo ni zamu ya Profesa Sospeter Muhongo kutangaza nia ya kuombwa kugombea urais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, kurithi mikoba ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Profesa Muhongo anatangaza nia yake leo Mjini Musoma, kwenye Ukumbi wa Open University Hall, kuanzia saa 10 jioni.

  0 0

  1
  Mijiolojia wa Wizara ya Nishati na Madini, Assa Mwakilembe akizungumzia sekta ya madini  nchini kabla ya kumkaribisha  Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje  ili aweze kufungua mafunzo kwa wataalam wa Wizara. Mafunzo hayo yaliyoshirikisha Makamishna Wasaidizi kutoka Ofisi za Madini Nchini  na kufanyika Bagamoyo mkoani Pwani, yanatolewa na Taasisi ya  Sayansi na Mazingira kutoka  India, lengo likiwa ni kubadilishana  uzoefu na kuwapa uelewa katika usimamizi wa mazingira kwenye migodi.
  2
  Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje kutoka  Wizara  ya Nishati na Madini akifungua mafunzo yaliyoshirikisha Makamishna Wasaidizi kutoka Ofisi za Madini Nchini yanayoendelea mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
  3
  Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje kutoka  Wizara  ya Nishati na Madini (wa kwanza kushoto, waliokaa mbele) pamoja na washiriki wengine wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa na wataalam kutoka  Taasisi ya  Sayansi na Mazingira kutoka Nchini India (hawapo pichani) katika mafunzo kuhusu usimamizi wa mazingira migodini yanayoendelea mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
  4
  Sehemu ya wataalam kutoka Idara ya Madini iliyopo chini ya  Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini mada kuhusu usimamizi wa mazingira kwenye migodi katika nchi  ya India iliyokuwa inawasilishwa na mtaalam mwelekezi kutoka  Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Sujit Kumar Singh (hayupo pichani) kwenye mafunzo  hayo.
  5
  Mtaalam kutoka  Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Srestha Banerjee akiwasilisha mada katika mafunzo hayo.
  6
  Mtaalam mwelekezi kutoka  Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Sujit Kumar Singh akisisitiza jambo katika mafunzo hayo.
  7
  Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje kutoka  Wizara  ya Nishati na Madini (wa tatu kutoka kushoto, waliokaa mbele), Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara  ya Nishati na Madini,Mhandisi  Gideon Kasege ( wa pili kutoka kulia, waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo  hayo.

  Na Greyson Mwase, Bagamoyo
  Taasisi zinazohusika na usimamizi wa sheria na kanuni za mazingira zimetakiwa kushirikiana kwa karibu zaidi ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa mazingira migodini na kuepuka mwingiliano wa majukumu.
  Wito huo umetolewa na Kamishna Msaidizi wa Madini – Ukaguzi wa Migodi Mhandisi Ally Samaje katika mahojiano maalum kwenye mafunzo yanayohusisha Makamishna Wasaidizi wa Madini, Wakaazi kutoka Wizara ya Nishati na Madini Tanzania na wataalam kutoka India yanayoendelea mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
  Mhandisi Samaje alitaja taasisi hizo kuwa ni pamoja na Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Wizara ya Maji, Wizara ya Maliasili na Utalii (Misitu) na kuongeza kuwa taasisi hizo zimekuwa zikishirikiana katika masuala muhimu yahusuyo madini hususan katika masuala yenye kuhitaji uelewa wa pamoja.
   Wakati huo huo akizungumza kwa kutumia mfano wa nchi ya India, mtaalam mwelekezi kutoka Taasisi ya Sayansi na Mazingira kutoka Nchini India, Sujit Kumar alisema kuwa India ina taasisi nyingi mbalimbali zinazohusika katika usimamizi wa kanuni na sheria za mazingira hali inayopelekea ugumu katika usimamizi wa sheria na kanuni hizo.
  “ Matokeo yake kila taasisi inaona kuwa sheria na kanuni zake za mazingira ni bora na sahihi na kuwataka wawekezaji wa madini kuzifuata, hivyo kupelekea ukaguzi wa migodi kuwa mgumu.” Alisisitiza Singh.
   Naye mtaalam muelekezi kutoka Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Srestha Banerjee akizungumzia jinsi ya kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa kutumia mfano wa nchi ya India alisema kuwa ili wachimbaji wadogo waweze kufanikiwa kupata leseni wanatakiwa kuunda vikundi vidogo vidogo na kuomba leseni ya pamoja na kuanza kumiliki vitalu.
  Banerjee alishauri serikali kuendelea kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa  kuwapatia ruzuku kwani wana mchango mkubwa sana katika pato la nchi kupitia sekta ya madini.
   Alisisitiza kuwa elimu ni muhimu kwa wachimbaji wadogo kwa kuwa wengi hawana elimu hali inayopelekea kuchimba katika mazingira hatarishi na kutokea kwa ajali za mara kwa mara migodini.
   Ili kuhakikisha kuwa wananchi waishio karibu na migodi wananufaika na rasilimali za madini, Banerjee alipendekeza kuanzishwa kwa mifuko ya madini ambapo fedha zinazolipwa kama kodi na wawekezaji zitawanufaisha wananchi wote.
   Alisema kuanzishwa kwa mifuko itakayowanufaisha wananchi kutachochea maendeleo katika ngazi ya halmashauri na wananchi kuondokana na dhana kuwa hawanufaiki na rasilimali za madini.
   Aliongeza kuwa fedha hizo zinaweza kutumika katika uboreshaji wa huduma za jamii kama vile maji, umeme, miundombinu, afya pamoja na kusomesha wakazi kupitia elimu za madini.

  0 0
 • 06/02/15--05:03: TANGAZO LA KIFO

 • unnamedKamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara kuanzia Mwaka 1996 hadi 2002, Onel E. Malisa kilichotokea leo Alfajiri tarehe 2 Juni, 2015 katika Hospitali ya Dar Group, Jijini Dares Salaam.
  Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Familia ya Marehemu linaendelea kuratibu taratibu zote za kuaga na mazishi ya marehemu. Hivi sasa msiba upo nyumbani kwake Kinyerezi, Jijini Dar es Saalam. Aidha taarifa kamili kuhusiana na msiba huu mtaendelea kufahamishwa baada ya mipango yote kukamilika.

  Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi;
  AMINA

  0 0

  1 (2)

  Raymond Mhenge Mtaalam wa Biashara za Kimataifa wa Kampuni ya PESAEXPO akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Kebbys Mwenge jijini Dar es salaam wakati alipoelezea kuhusu maonyesho hayo yanayotarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi wa tisa jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni Sunday Mashele Mkurugenzi Mwenza Kampuni ya Exclusive Media na Godie Gervas Mkurugenzi wa Exclusive Media
  1
  Godie Mashelle Mkurugenzi wa Exclusive Media akisisitiza jambo katika mkutano huo kutoka kulia ni Eric Fussi Mkurugenzi Mwenza Qutub Grobal Limited na Sunday Mashele Mkurugenzi Mwenza Kampuni ya Exclusive Media.

  Exclusive Media (T) Ltd ikishirikiana na Qutub Global Ltd imeandaa maonyesho makubwa yaTaasisi na asasi za kifedha nchini Tanzania yajulikanayo kama Pesa Expo.

  Maonyesho hayo yanatarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi wa tisa jijini Dar es salaam.
  Pesa Expo itahusisha Taasisi na asasi mbali mbali za kifedha Kama
  1. Mabenki
  2. Saccos
  3. Makampuni ya bima
  4. Makampuni yanayotoa huduma za Mikopo (Microfinance)
  5. Makampuni yanotoa huduma za fedha za kieletroniki
  6. Mifuko ya hifadhi ya jamii
  7. Makumpuni yanoyotoa huduma za kutuma fedha
  8. Soko la hisa na madalali wake
  9. Makampuni yanayotoa huduma za ushauri wa kifedha
  10. Taasisi zisizo za Faida zinazotoa Elimu kuhusu mambo ya fedha (NGOs)
  Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa watanzania wana ufinyu wa elimu ya kutosha juu ya huduma nyingi za kifedha zitolewazo nchini pamoja na faida zake.Lengo kuu la Pesa Expo ni kuwakutanisha watoa huduma za kifedha pamoja na watumiaji wao na wananchi kwa ujumla.
  Pesa Expo inapenda kuchukua nafasi hii kutoa wito kwa asasi zote za kifedha nchini kushiriki maonyesho hayo.

  Tayari baadhi ya makampuni yamesha thibitisha ushiriki wao hivyo tunaendelea kutoa wito kwa wale ambao bado hawajathibitisha kuendelea kujitokeza na kuthibitisha ushiriki wao katika maonyesho haya Pesa Expo itatoa fursa mbali mbali kwa makampuni shiriki kama vile
  Kufanya mauzo ya moja kwa moja Kutangaza huduma zao mpya Kutoa elimu ya huduma za kwa wananchi Kuboresha mahusiano yao na wateja Kuboresha mahusiano baina ya makampuni shiriki Kubadilishana mawazo na wajasiriamali na wananchi
  Kufanya tafiti ya bidhaa zao Kujitangaza nk

  Pesa Expo ni maonyesho endelevu yatakayokuwa likifanyika kila mwaka likianzia Dar es salaam na kuzuunguka mikoa mbali mbali nchini. Kwa hiyo tunawakaribisha Taasisi na asasi zote za kifedha na wadau wote wa masuala ya fedha nchini na wananchi kwa ujumla kuweza kushirikiana nasi kuweza kufanikisha maonyesho haya.

older | 1 | .... | 541 | 542 | (Page 543) | 544 | 545 | .... | 1898 | newer