Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

TAARIFA RASMI KUTOKA KWA KAMATI YA JUMUIYA NA USULUHISHI WA MIGOGORO

$
0
0
Kufuatia mgogoro  wa kisiasa, jaribio la kumtoa madarakani Raisi wa Jamhuri ya Burundi, Pierre Nkurunziza na maelfu ya wananchi wa nchi hiyo kukimbilia nchi jirani za Tanzania na Rwanda. Hali ya kambi zinazopokea wakimbizi zinaonekana kuelemewa na kupelekea kuhatarisha hali za wakimbizi hao.


Kutokana na hali hiyo, Bunge la Afrika ya Mashariki kupitia kamati yake ya Masuala ya Jumuiya na Usuluhishi wa Migogoro imeteua wajumbe watakaokwenda kutembelea kambi hizi zilizopo Kigoma-Tanzania na Mashariki mwa nchi ya Rwanda kwa madhumuni yafuatayo;


1.     Kujiridhisha na hali ya mazingira ya kambi hizo na kuangalia mipango kutatua mgogoro huo.

2.     Kuangalia na kutimiza jukumu la Bunge la Afrika Mashariki kupata suluhisho la kudumu la mgogoro ulioko sasa nchini Burundi.

3.     Kuwatemebelea na kuwafariji wananchi wote wa Burundi walioko kwenye kambi hizo.


Wajumbe wa kamati teule wamegawanyika katika makundi mawili, wajumbe watakaokwenda Kigoma-Tanzania wataongozwa na Mhe. Abdullah Mwinyi ambae ni menyekiti wa kamati hiyo na wajumbe watakaokwenda Mashariki mwa Rwanda wataongozwa na Mhe. Abubakar Zein.


Imetolewa na;

Mhe. Abdullah Mwinyi


(Mwenyekiti wa Kamati ya masuala ya Jumuia na Usuluhishi wa Migogoro)


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA KUAPISHWA RAIS WA NIGERIA LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Asha Bilal, wakiteremka kwenye Ndege walipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na mtoto Ernest Nkayala alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Asha Bilal, wakiwasili kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea shada la maua kutoka kwa Mtoto Elin Mwandobo alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ngoma za kabila la Kinigeria alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
(Picha na OMR). 

Serikali yatangaza kutenga bajeti zaidi kwenye tafiti za afya.

$
0
0
 Naibu wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi, Mh. Anne Kilango  akisisitiza jambo  mbele ya  Madaktari na wanafunzi wa udaktari kutoka Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) waliohudhuria Mkutano Mkuu wa tatu wa sayansi ya afya ulioandaliwa na chuo hicho  jijini Dar es Salaam jana. Kwenye mkutano huo wa siku mbili huku ukilenga  kujadili masuala ya tafiti kwenye sayansi ya afya, Mh. Kilango alimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Mohamed Gharib Billal.
 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anna Kilango (kulia) akijadiliana jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof.Ephata Kaaya, mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa tatu wa sayansi ya afya ulioandaliwa na chuo hicho  jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wanasayansi, Madaktari na wanafunzi wa udaktari kutoka  Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) wakifuatilia kwa umakini Mkutano Mkuu wa tatu wa sayansi ya afya ulioandaliwa na chuo hicho  jijini Dar es Salaam jana

Naibu wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi, Mh. Anne Kilango  amebainisha kuwa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2015/16 imeongeza fungu zaidi kwenye masuala ya utafiti hususani ule wa sayansi ya afya.

Mh. Kilango alitoa kauli jijini Dar es Salaam jana wakati akifungua  Mkutano Mkuu wa tatu wa sayansi ya afya ulioandaliwa na Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na kuhudhuliwa na mamia ya Madaktari na wanafunzi wa udaktari kutoka chuo hicho.

“ Ili taifa liweze kufanya vizuri kwenye sekta yoyote ile ni lazima tuwekeze zaidi kwenye masuala ya tafiti. Kwa kulitambua hilo napenda kuwataarifu kuwa hata kwenye bajeti yetu ya mwaka huu wa fedha tunatenga kiasi kikubwa cha rasilimali fedha kwa ajili ya kuwezesha tafiti hizi zikiwemo hizi za masuala ya afya,’’ alisema Mh. Kilango ambaye alimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Mohamed Gharib Billal.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof.Ephata Kaaya alisema kuwa kwa sasa taifa linahitaji zaidi tafiti za kiafya hususani kwenye magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo kisukari, shinikizo la damu na saratani.

“ Ni dhahiri kuwa kwa sasa magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza yamekuwa ni tishio kwa taifa. Kama wataalamu wa masuala ya afya tunaona kuja tija zaidi tukiwekeza katika tafiti zinazohusu pia magonjwa haya,’’ alibainisha.

Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kuhitimishwa leo ambapo zaidi ya tafiti 100 kuhusu maswala ya afya zitawasilishwa.

WAZIRI MKUU PINDA AHUTUBIA SHEREHE ZA MIAKA 25 WA TAWLA

$
0
0
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) baada ya kuhutubia katika sherehe za miaka 25 ya chama hicho kwenye viwanja vya  Karimjee jijini Dar es salaam Mei 30, 2015. Aliyekaa wapili kulia ni balozi wa Sweden nchini, Lennarth Hjelaker.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza wakati alipozindua Uandishi wa Wosia katiak sherehe za miaka 25 ya Chama cha Wanasheria Wananwake (TAWLA0 kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Mei 30, 2015.Kushoto ni balozi wa Sweden nchini, Lennarth Hjelaker
 7452  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi Mwanaidi Maajar baada ya kuhutubia katika sherehe za siku ya Wanasheria Wananwakde Tanzania Tawla , kwenye viwanja vya  Karimjee jijini Dar es salaam Mei 30, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Balozi wa Sweden Nchini, Lennarth Hjelaker baada ya kuhutubia katika sherehe za kuadhimisha miaka 25 ya Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kwenye viwanja vya  Karimjee  jijini Dar es salaam Mei 30, 2015.
   Baadhi ya wananchama wa Chama cha Wanasheria Wananwake (TAWLA) wakipita kwa maandamano mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika sherehe za miaka 25 ya TAWLA zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es slaam Mei 30, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

UMOJA WA WATANZANIA WALIOSOMA NCHINI AUSTRALIA WAZINDULIWA RASMI

$
0
0
 Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera Bw.Mathias Kabunduguru (aliyesimama) aliyemuwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi Mh. Celina O. Kombani (Mb) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) jijini Dar es Salaam leo. 
Baadhi ya Watanzania  waliosoma nchini Australia wakimsikiliza mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera Bw.Mathias Kabunduguru (kushoto) aliyemuwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi Mh. Celina O. Kombani (Mb) (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Watanzania  waliosoma nchini Australia wakimsikiliza mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera Bw.Mathias Kabunduguru (kushoto) aliyemuwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi Mh. Celina O. Kombani (Mb) (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) leo jijini Dar es Salaam.
Add caption
  Waziri wa Afya na Utalii wa Australia Mh. Dkt. Kim Hames akizungumza wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) jijini Dar es Salaam leo.
 Rais wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) Bw. Francis Mhimbila akizungumza wakati wa uzinduzi wa Umoja huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera Bw.Mathias Kabunduguru (aliyesimama) aliyemuwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi Mh. Celina O. Kombani (Mb) akizungumza na Watanzania walionufaika na ufadhili wa masomo nchini Australia.

Maadhimisho ya SIKU YA AFRIKA yafanyika Washington DC

$
0
0
Balozi wa Misri nchini Marekani Mhe. Mohamed Tawfik akiongea kufungua sherehe ya African Union iliyofanyika siku ya Alhamisi May 28, 2015 katika hotel ya JW Marriott, Washington DC
Balozi wa Morocco nchini Marekani Mhe. Rashad Bouhlal akiongea machahce.
Msemaji mkuu wa sherehe ya siku ya Afrika Mhe. Donald Tetelbaum.
Mchungaji Jesse Jackson akiongea kwenye sherehe ya siku ya Afrika.

Maureen Umeh mfanyakazi wa kituo cha luninga cha Fox News DC akisherehesha sherehe ya siku ya Afrika.
Mambalozi wa Afrika nchini Marekani wakiwa katika picha ya pamoja
Wageni waalikwa wakifuatilia hotuba.

Mkuu wa Utawala na Fedha mama Lily Munanka akisalimiana na Balozi wa Kenya nchini Marekani Mhe. Robinson Githae.

ZIARA YA MHESHIMIWA ALI HASSAN MWINYI JIJINI TEHRAN

ANDIKENI WOSIA KUEPUSHA MIGOGORO - WAZIRI MKUU

$
0
0
 WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka Watanzania wote nchini wajenge tabia ya kuandika wosia ili kuondoa matatizo ya mirathi pindi mume anapoaga dunia.

Ametoa wito huo leo mchana (Ijumaa, Mei 29, 2015) wakati akizindua kampeni ya kuandika wosia kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kushuhudia uandishi wa wosia mbele ya wakili, Waziri Mkuu alisema uandishi wa wosia ni suluhisho la migogoro mingi inayosababishwa na wanandigu ambao wakati mwingine wala hawakushiriki kuchuma mali wanayogombea.

“Kuandika wosia siyo uchuro kama ambavyo watu wengi wanadhani… ninatoa kwa Watanzania kuandoak wosia mapema kwani inasaidia kuondoa matatizo ya mirathi baada ya mmoja wao kuondoka duniani,” alisema.

“Mtua anapaswa kutamka mali nilizonazo ni kadhaa na endapo nitakufa mali hii apewe fulani, na hii fulani na nyingine fulani. Hati hii inapaswa kutunzwa kwa mwanasheria, benki au kwa Kabidhi Wasii. Tusipolifanya hili, matatizo yataendelea kuwakumba wajane na watoto walioachwa na marehemu,” alisema.

Aliipongeza TAWLA kwa kuchukua jukumu la kuhamasisha umma kuhusu suala la uandishi wa wosia lakini pia akawataka wanachama wa TAWLA wajikite zaidi kwenye kutetea haki za makundi maalum kama walemavu wa ngozi, vikongwe na watu kutoka makabila madogodogo. “Haya makundi yana shida zao ambazo hazifanani na watu wengine. Nendeni vijijini, mkatoe elimu, jueni changamoto wanazokabiliana nazo, wasikilizeni shida zao na muone ni njia gani mnaweza kuwasaidia,” alisema.

Akitoa mfano, Waziri Mkuu alisema katika kipindi cha miaka nane kuanzia mwaka 2006 hadi 2014, jumla ya vikongwe 2,219 waliuawa katika mikoa ya Geita, Simiyu, Mara, Kagera na Mwanza ambayo alisema yote iko Kanda ya Ziwa. “Mauaji haya yanasababishwa na imani potofu za kishirikina; jamii kuwa na uelewa mdogo wa sheria; ukosefu wa imani za kiroho; ukosefu wa elimu; na waganga wa kienyeji kupiga ramli,” alisema.
 
Alisema makabila madogo yanakabiliwa na matatizo ya ardhi ambayo ndiyo tegemeo lao kuu, vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi wanatishiwa usalama wa maisha yao bila sababu yoyote. “Nendeni mkatoe elimu zaidi kwa watu hawa ili tuwalinde wazee wetu, makabila madogo kama Wahadzabe na Wasandawe pamoja na ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi,” alisisitiza.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa TAWLA, Bi. Aisha Bade alisema chama hicho kimetumia wanasheria wanawake zaidi ya 200 na wasaidizi wa kisheria 400 (paralegals) kutoa msaada wa kisheria kwa watu mbalimbali ambao hawana uwezo kumudu gharama za kesi.

“Katika mwaka 2014, tumetoa msaada wa kisheria kwa watu zaidi ya 10,000 ambao hawana uwezo kumudu gharama za kesi kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini,” aliongeza.

Naye Balozi wa Sweden nchini, Bw. Lennarth Hjelmaker, akizungumza kwa niaba ya wadau wa maendeleo nchini alisema Serikali ya nchi hiyo ilitenga kiasi cha sh. bilioni 4 kusaidia mpango wa miaka minne wa chama hicho wa kuimarisha utawala bora, uwajibikaji na usawa wa kijinsia.

“Hadi sasa tumekwishatoa sh. bilioni 3.5 ambazo kati ya hizo, sh. bilioni 1.1 zimetumika kusaidia wanawake wapatiwe haki zao; sh. milioni 500 zimetumika kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya ili watoe huduma rafiki za afya ya uzazi kwa vijana na sh. milioni 700 zimetumika kutoa mafunzo kwa viongozi wa ngazi ya chini wanaohusika kutoa maamuzi. Kiasi cha sh. bilioni 1.2 kimetumika kuendeleza shughuli za chama,” alifafanua.

Pamoja na kutoa elimu kwa jamii na kutetea haki za akinamama na wasichana, Balozi huyo wa Sweden alisema kuna haja ya kuweka mkazo ili kuwafikia wanaume na wavulana wengi zaidi ili waweze kujirekebisha na kubadili tabia na mitazamo yao dhidi ya wanawake na wasichana.


IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
IJUMAA, MEI 29, 2015.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZUNGUMZA NA WATANZANIA WANAOISHI NCHINI NIGERIA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Watanzania wanaoishi Nchini Nigeria katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania mjini Abuja Nigeria leo May 29,2015.
 Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Mhe. Danniel Ole Njolai akimkabidhi zawadi ya saa iliyotolewa na Watanzania wanaoishi Nchini Nigeria Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, baada ya kuzungumza na Watanzania hao katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania mjini Abuja Nigeria leo May 29,2015.
 Baadhi ya Watanzania wanaoishi Nchini Nigeria wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokua akizungumza nao leo May 29,2015  katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania mjini Abuja Nigeria leo May 30,2015.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na  Watanzania wanaoishi Nchini Nigeria Baada ya kuzungumza nao katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania mjini Abuja Nigeria leo May 29,2015. (Picha na OMR).

RATIBA NA TAREHE MPYA ZA MoFLAVA ALL WHITE USA TOUR/PARTIES

$
0
0
ATANZANIA WAISHIO MAREKANI TUNAPENDA KUWAKUMBUSHA KUWA TOUR YA MoFLAVA ALL WHITE PARTY INAANZA HIVI KARIBUNI IN USA CITIES. TUNAOMBA USHIRIKIANO WENU AS WE BRING ENTERTAINMENT & GOOD TIME TO YOUR CITY OR CITY NEAR YOU. THIS IS THE UPDATED SCHEDULE FOR UPCOMING PARTY & CITIES

SATURDAY 06/06/2015  CINCINNATI OHIO
SATURDAY 06/20/2015  DALLAS TEXAS
SATURDAY  07/18/2015 (EID AL FITR)  HOUSTON TEXAS
SATURDAY  08/01/2015  WASHINGTON DC
SATURDAY  08/22/2015  WICHITA KANSAS
ATLANTA GA & COLUMBUS OHIO DATES TO BE ANNOUNCED SOON
 

IN LOVING MEMORY OF MZEE FELICIAN MAKWAIA

$
0
0
In Loving Memory of Mzee Felician Makwaia 1944 - 2013

Beloved Dad!
It has been two years now
since you responded to your Almighty’s call,
If we only knew it would be the last time
that we see you walk out the door,
We would give you a hug and kisses,
and call you back for one more.

A million times we needed you,
A million times we cried,
If love alone would have saved you,
You would have never died.

In life we loved you dearly,
In death we love you still,
In our hearts you will forever hold a place,
No one can ever fill.

A light from our household is gone,
A voice from our love is stilled,
A place in our vacant home,
Which never can be filled.

Some may think you are forgotten,
Though on earth you are no more,
But in our memory you are with us,
As you always were before.

It broke our hearts to lose you,
But you did not go alone,
A part of us went with you,
The day God called you home.

Your precious memories are for keepsakes,
with which we never part,
God has you safely in his keeping,
But we have you in our hearts and your Legacy will forever live on!

Deeply missed by your Loving Wife Mama Makwaia, your Children Stella, Frank, Robert and Christopher, In-laws, Grand-children, Neighbours, Friends and Relatives.

May you Rest in Peace Dad! Amen.

LOWASSA KUANZA "SAFARI YA MATUMAINI" MCHANA WA LEO JIJINI ARUSHA

$
0
0
Gari iliyombeba Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa ikipita nje ya uwanja wa Sheih Amri Abeid, jijini Arusha mapema leo asubuhi wakati akielekea kwenye Ofisi za CCM Mkoa. Mh. Lowassa anatarajia kulihutubia taifa mchana wa leo kwenye uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid, ikiwa ni sehmu ya kutangaza kwake nia yake ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na baadhi ya viongozi waliokuwepo kwenye ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha.Kulia ni Mkewe Mama Regina Lowassa.
Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole.
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa alieambatana na Mkewe, Mama Regina Lowassa pamoja na wanaCCM wengine.
Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole (hayupo pichani).

NEC YAKAMILISHA MAANDALIZI UBORESHWAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA KWA MIKOA 4

$
0
0
Maandalizi ugawaji wa mashine kwa ajili ya kuandikisha wanchi katika daftari la wapiga kura kwa Kanda ya 5 Tano kati ya Sita yamekamilika leo Mei 29, 2015 zaidi ya Biometric Voter Registration (BVR) zipatazo 1492 zinaanza kusambazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kuanzia mapema Alfajiri Kanda ya Tano ni Mikoa ya Mara, Arusha, Manyara na Kilimanjaro.

CCM WASHINDA NAFASI YA UENYEKITI MJI MDOGO WA HIMO.

$
0
0
Msimamizi wa Uchaguzi na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji akizungumza wakati wa kutangaza matokeo katika uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti wa mji mdogo wa Himo.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria katika uchaguzi huo kutoka vyama mbalimbali vya siasa.
Mwenyekiti wa mji mdogo wa Himo Hussein Jamal akizungumzamara baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo katika uchaguzi huo uliofanyika katika shule ya walemavu wa usikivu eneo la njia Panda.
Baadhi ya viongozi waliofika kushuhudia Uchaguzi huo.
Mkurugenzi wa wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji akitoa ufafanuzi katika uchaguzi huo.
Baadhi ya madiwani walioshiriki uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Moris Makoi akisalimia mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza wakati wa kufunga kikao cha uchaguzi huo.
Dc Makunga akipeana mkono na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Moris Makoi mara baada ya kuzungumza katika uchaguzi huo.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

MRATIBU MKAZI WA UN NCHINI NA WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI WATEMBELEA ENEO LA MAPOKEZI YA MUDA KWA WAKIMBIZI MJINI KIGOMA

$
0
0
IMG_0495
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) akiongozana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa tatu kushot0) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (katikati), Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wa pili kulia), Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner (kulia) mara tu baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma, eneo ambalo Wakimbizi wanapokelewa na kupewa huduma ya kwanza kabla ya kuelekea katika eneo maalum ya Nyarugusu, wilayani Kasulu mkoani Kigoma.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
IMG_0457
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akizungumza na wafanyakazi wa wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wanaoandikisha Wakimbizi wanaowasili kwenye uwanja wa Lake Tanganyika kabla ya kuelekea katika kambi ya Nyarugusu, iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
IMG_0468
Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner (kushoto) akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa tatu kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wa pili kushoto) walipotembelea uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
IMG_0504
Mmoja wa watoa huduma kwenye kituo cha muda cha Wakimbizi katika viwanja vya Lake Tanganyika akipuliza dawa ya kuua wadudu kwenye mifereji inayozunguka uwanja huo kwa ajili ya kujikinga na magonjwa mbalimbali ya milipuko ikiwemo Kipindupindu.
IMG_0512
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa pili kulia) akizungumza na baadhi ya Wakimbizi kutoka Burundi waliokuwa kwenye foleni ya kupanda mabasi kuelekea kambi ya Nyarugusu kwenye makazi maalum yaliyotengwa na Serikali ya Tanzania yanayohudumiwa na Shirika linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengi ya Umoja wa mataifa. Wanne kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez na wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole.
IMG_0440
Foleni ya Wakimbizi kutoka Burundi kuelekea kwenye mabasi maalum yaliyoandaliwa na Shirika la IOM kuwapeleka kwenye eneo maalum la kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

IMG_0524
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa pili kulia) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole wakishuhudia baadhi ya Wakimbizi wakipakia kwenye mabasi maalum yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la IOM tayari kuelekea katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
IMG_0525
IMG_0544
IMG_0550
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (aliyeipa mgongo kamera kushoto), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa pili kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole wakiagana na baadhi ya Wakimbizi wanaoelekea kwenye kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma kutokea katika kituo cha muda cha mapokezi na huduma za afya kilichopo katika viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma.
IMG_0475
Baadhi ya wakina mama na watoto zao wakiwa wamejipumzisha ndani ya viwanja vya Lake Tanganyika huku wakisubiri safari ya kuelekea katika kambi ya Nyarugusu, iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
IMG_0523
Wahudumu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa wakiwapulizia dawa maalum kwenye mikono na miguu kwa ajili ya kuua bakteria kabla ya kuingia ndani ya mabasi na kuelekea katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
IMG_0531
IMG_0536
IMG_0563
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) wakielekea kutembelea mabanda mbalimbali ya huduma za afya yaliyopo kwenye viwanja vya Lake Tanganyika yanayotoa huduma kwa Wakimbizi wanaowasili kabla ya kupekwa kambini.
IMG_0559
Pichani juu ni baadhi ya watoto wakipatiwa matibabu ndani ya kituo cha muda kabla ya kuelekea kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
IMG_0568
Wazazi na watoto wakiwa kwenye hema maalum, huku nwengine wakiwa kwenye dripu za kuongezewa maji mwilini.
IMG_0558
IMG_0569
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari wakisafisha mikono yao na kupuliziwa dawa maalum katika viatu mara baada ya kutembelea mahema yenye wagonjwa mbalimbali Wakimbizi kutoka Burundi wanaopatiwa matibabu kwenye kituo cha muda kilichopo kwenye viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma.
IMG_0578
Baadhi ya watoto wakijiliwa na kujifaraji kwa kucheza mpira katika kituo maalum cha kupokelea Wakimbi wanaotafuta hifadhi nchini Tanzania wakitokea nchini Burundi katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
IMG_0581
Pichani juu na chini ni familia za Wakimbi wakiwa wamejipumzisha kwenye kituo cha muda katika viwanja vya Lake Tanganyika huku wakisubiri safari ya kuelekea katika kambi ya Nyarugusi iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
IMG_0583
IMG_0500
Sehemu ya eneo la uwanja wa Lake Tanganyika.

Na Modewjiblog team
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe katikati ya wiki wametembelea eneo la mapokezi ya Wakimbizi kutoka Burundi lililopo katika viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma.

Walipofika katika eneo hilo la mapokezi waliojionea huduma mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo Shirika la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Shirika la kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Chakula duniani (WFP), Shirika la afya duniani (WHO) pamoja na Shirika la UNFPA linaloshughulikia mahitaji ya wanawake hasa wale waliokuwa wajawazito.
Wakimbizi wengi waliofika eneo hilo walikuwa na afya dhoofu kutokana na kusafiri kwa umbali mrefu.

Kutokana na hali hiyo baadhi yao ilibidi wapatiwe huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya makazi yaliyotengwa kwa Wakimbizi ikiwemo kambi ya Nyarugusu iliyopo katika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.

Hata hivyo kambi hiyo ya Nyarugusu ina uwezo wa kuchukua sio zaidi ya Wakimbizi 50,000 lakini sasa ina Wakimbizi zaidi ya 48,000 kutoka Burundi na 60,000 kutoka Jamuhuri ya watu wa Congo.

Aidha Waziri Chikawe alisema kuwa Serikali imetenga eneo maalum ambalo litajengwa kambi mpya itakayojulikana kama Nyarugusu B ambayo itakuwa ni mahususi kwa Wakimbizi kutoka Burundi.Mh. Chikawe alisema kuwa kambi hiyo itakamilika ndani ya miezi mitatu kutoka hivi sasa, ili kuwatenganisha Wakimbizi kutoka Congo na Burundi.

MWENGE WA UHURU WAKIMBIZWA WILAYA YA KINONDONI MKUU WA WILAYA ATANGAZA AJIRA YA PAPO KWA PAPO

$
0
0

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiwa ameubeba mwenge wa Uhuru baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto), akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda baada ya kumaliza mbio zake wilayani humo Dar es Salaam leo leo asubuhi. Mwenge huo ulianza mbio zake Wilaya ya Ilala na kuzindua miradi mbalimbali.
 Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum (kulia), akisalimia na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda.
 Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Kinondoni wakiwa wamejipanga foleni wakisubiri kuupokea mwenge wa Uhuru kabla ya kuanza mbio zake wilayani humo.
 Wakimbiza mwenge kitaifa.
 Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa (kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
  Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum akivuta pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ya mradi wa maji Mburahati Barafu na Kisiwani uliofadhiliwa na Jumuia ya Ulaya, Serikali ya Ubelgiji na Serikali ya Tanzania  wakati wa ukimbizaji wa mwenge huo Wilaya ya Kinondoni humo.
  Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum akivuta pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ya baabara tatu katika Shule ya Sekondari ya Makulumla. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Beatrice Mhina.
 Mwanafunzi Noel Mwita wa Shule ya Sekondari ya Makulumla, akiekeza namna ya kuchanganya madawa wakati kiongozi huyo wa mwenge, Juma Chum (wa nne kushoto), alipoweka jiwe la msingi za maabara katika shule hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Beatrice Mhina, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda
 Vijana wa hamasa wa wilaya ya Kinondoni wakitoa burudani mbalimbali wakati wa kuupokea mwenge huo ukitokea wilaya ya Ilala.
  Vijana wa hamasa wa wilaya ya Kinondoni wakitoa burudani mbalimbali wakati wa kuupokea mwenge huo ukitokea wilaya ya Ilala.
 Wananchi wa Mburahati wakiupokea mwenge huo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika eneo hilo.
 Vijana wa hamasa wakipamba hafla hiyo kwa kuonesha matukio mbalimbali.
 Mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’ akitoa ushuhuda wa jinsi alivyoacha matumzizi ya dawa ya kulevya mbe ya Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa kituo cha vijana walioathiriwa na dawa hizo katika Hospitali ya Mwananyamala.
 Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum, akimkabidhi Amina Mshana chandarua kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa malaria.
Wakimbiza mwenge wa Uhuru kitaifa,  Delina Simfukwe (kushoto) na Bakia Abdallah wakiteta jambo na mwanamuziki RehemaChalamila ‘Ray C baada ya kutoa ushuhuda kuhusu matumizi ya dawa za kulevya.
…………………………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ametoa ajira ya moja kwa moja kwa kijana Yusuf Mzitto mtaalamu wa masuala ya kompyuta ambaye alikuwa ameathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya  wa wilaya hiyo.
Makonda alitoa ajira kwa kijana huyo mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka huu. Juma Khatibu Mchum wakati wa uzinduzi wa kituo cha vijana walioathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya kilichozinduliwa na kiongozi huyo wa mbio za mwenge katika Hospitali ya Mwananyamala Dar es Salaam leo asubuhi.
“Kijana huyu mwenye elimu ya juu ya masuala ya kompyuta alikuwa ameathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya hivyo baada ya kuacha kutumia dawa hizo tumempa ajira katika ofisi yangu ili aweze kufanyakazi badala ya ujuzi wake kupotea bure” alisema Makonda.
Makonda alisema kuwa katika kuwawezesha vijana walioathiriwa na dawa hizo wamepatana na viongozi wa manispaa hiyo kuwa kila kampuni inayofanya shughuli za kijamii katika wilaya hiyo ili iweze kupata tenda ya kufanya kazi yoyote ni lazima itoe mchanganuo  kwanza wa utoaji wa nafasi ya ajira kwa vijana wa wilaya hiyo.
Alisema wamechukua hatua hiyo ili kutoa fursa ya ajira kwa vijana waliohamua kuachana na matumzi ya dawa za kulevya ambao hawana kazi hivyo kupitia  kakampuni hizo ziweze kuwasaidia vijana hao baada ya kupatiwa tenda na manispaa hiyo.
Alisema ili kuunga jitihada za Rais Jakaya Kikwete za kupambana na uingizaji wa dawa za kulevya ameanzisha mpango wa kukutana mara moja kila mwezi na vijana walioathiriwa na dawa hizo ili kubadilishana mawazo badala ya kuwatenga.
Makonda alisema vijana hao wengi wao ni wataalamu wa masula mbalimbali akimtolea mfano kijana aliyepewa ajira katika ofisi yake ambaye atawasaidia katika mambo mengine.
Akizungumzia mbio za mwenge katika wilaya yake kwa mwaka huu alisema umezindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi saba yenye jumla ya sh.5,079,153,972 ambapo kati ya fedha hizo sh.14,802,200 ni fedha kutoka serikali kuu, sh.2,672,992 kutoka katika Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni, sh.913,800,780 ni mchango wa wahisani na sh.1,477,978,000 ni michango ya wananchi.
Alitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa maji, ujenzi wa barabara, ujenzi wa baabara, ujenzi wa shule za Sekondari, ujenzi wa jengo la wazazi, ujenzi wa ofisi ya Kata na ujenzi wa nyumba ya walimu.
Alisema mwenge huo ulipata fursa ya kukagua miradi endelevu wa ugawaji wa vyandarua, mradi wa wanawake wajasiriamali, mradi wa vijana wajasiriamali watunzaji wa mazingira na mradi wa huduma za ukimwi.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Juma Khatibu Chum aliwataka watanzania wote bila ya kujali itikadi za vyama vyao kudumisha amani na utulivu wa nchi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.
Alisema amani ya nchi tusipo kuwa makini inaweza kuharibiwa kwa siku moja wakati imetafutwa kwa miaka mingi na aliwata vijana kuacha kutumia dawa za kulevya na kujikinga ma malaria ambayo yame kuwa yakiua watu wengi kuliko ukimwi. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera azindua zoezi la unywaji maziwa

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akizindua zoezi la unywaji wa maziwa kwenye maadhimisho ya wiki ya 18 ya maziwa ambayo kitaifa ilizunduliwa jana mjini Babati, kwa kuwapa maziwa wanafunzi wa shule ya msingi Babati.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera akizinduzi wa wiki ya 18 ya maziwa, ambapo kitaifa inafanyika Mjini Babati, kwa kumpa maziwa mkazi wa mji huo Magdalena Joseph ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ng'ombe wa maziwa ni fursa ya kiuchumi na lishe fuga kisasa.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera akizindua wiki ya 18 ya maziwa, ambapo kitaifa inafanyika Mjini Babati, kwa kumpa maziwa mkazi wa mji huo John Simon maziwa, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ng'ombe wa maziwa ni fursa ya kiuchumi na lishe fuga kisasa.


Wanafunzi wa shule ya sekondari Kwaraa ya Mjini Babati Mkoani Manyara, wakiimba jana kwenye uzinduzi wa wiki ya 18 ya maziwa ambayo kitaifa inafanyika mkoani humo, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ng'ombe wa maziwa ni fursa ya kiuchumi na lishe fuga kisasa.
 Wasanii wa kizazi kipya wa wakawaje wa Mjini Babati Mkoani Manyara, wakicheza jana kwenye uzinduzi wa wiki ya 18 ya maziwa kitaifa inafanyika mkoani humo, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ng'ombe wa maziwa ni fursa ya kiuchumi na lishe fuga kisasa.

MWANDISHI WA HABARI MWANDAMIZI ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UDIWANI KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA SONGEA MKOANI RUVUMA

$
0
0
Mwandishi wa Habari mwandamizi Bi. Celesencia Kapinga akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakata alipotangaza nia ya kugombea udiwani kata ya NDILIMALITEMBO Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).
 Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa pamoja na Mwandishi wa Habari wa gazeti la Majira ambaye ametangaza nia ya kugombea udiwani kata ya Ndilimalitembo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) . Habari na picha na Demasho.com.
..............................................................
WAKATI watu mbalimbali wameanza kujitokeza kutangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia vyama vya siasa mwandishi wa habari  Mwandamizi,  Mkoani  Cresensia Kapinga ametangaza nia ya kugombea udiwani kata ya Ndilima litembo manispaa ya Songea  Ruvuma.

Mwandishi huyo ametangaza nia yeke ya kuwania nafasi ya udiwani  mbele ya waandishi wa habari  kwenye ofisi za chama cha waandishi wa habari  Mkoa wa Ruvuma  zilizopo mtaa soko kuu mkoani  humo.
Amesema kuwa  kabla ya kutangaza nia amejipima na kujiona anaweza kuongoza kata baada ya kuwa  aligombea nafasi hiyo kupitia viti masalumu mwaka 2010 ambapo kura hazikutosha.

Akijibu masawali mbalimbali ya Waandishi wa habari amesema kuwa ameamua kugombea nafasi hiyo baaada ya kuona Changamoto mbalimbali zinazowakabaili Wananchi Katika Kata hiyo iliyokonje kidogo ya Manispaa  ya songea hazijafanyiwa kazi. 

‘Ziko Changamoto nyingi zinazowakabili Wananchi  wa Kata ya Ndilimalitembo bado hazijafanyiwa kazi,baadhi zikiwa ni Ukosefu wa Zahanati,Shule kukosa Vyoo na Wananchi kukosa soko la uhakika la kuuza mazao yao ambazo naamini  nikipata  nafasi ya kuwa Mwakilishi wao nitazishughulikia’anasema Bi. Cresensia Kapinga.

Anasema kuwa kuwa kutokana na  na taaluma yake ya uandishi wa habari ana uwezo wa kuingia Ofisi yoyote katika Manispaa ya Songea  na kuwasemea Wananchi wa  Kata hiyo hivyo anasema ni fursa  pekee ya Wananchi hao kumpa Fursa ya kuongoza Kata hiyo. Kwa upande wa Waandishi wa habari amesema kuwa  kwa kuwa yeye ni Mwanahabari atajitahidi kuwasema kwenye Baraza la  Madiwani  akiamini yapo mambo mengi yanashindwa kushughulikiwa ikiwemo posho zao.

Kwa upande wao Waandishi wa Habari wamepongeza hatua hiyo  na kutaka Waandishi wengine wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa kuwa Waandishi wamekuwa  wakinadi watu wengine wakati wapo baadhi yao wana uwezo wa kuongoza.

Mmmoja wa Waandishi hao Julius Konala anasema hatua hiyo ni ya kupongeza sana kwa kuwa imefunguia njia kwa Wanahabari wengine kugombea zaidi  na kuwata Wananchi  na Wanaccm kumuunga mkono  katika  azma yake ya kutaka kuwa  Diwani wa Kata ya Ndilimalitembo.

EDWARD LOWASSA ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS WA TANZANIA, JIJINI ARUSHA LEO

$
0
0
 Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
 Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola akisalima umati wa watanzania uliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, kumsikiliza  Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa (kulia).
 Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa, kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo.
 Mh. Lowassa akiwapungia wananchi.
 Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akihutubia katika mkutano wa hadhawa wa kutangaza nia yake hiyo,  kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo.
Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mkewe Mama Regina Lowassa wakati wa mkutano uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Mh. Edward Lowassa akipongezwa na baadhi ya Wabunge waliohudhulia mkutano huo, baada hotuba yake.

MKUU WA WILAYA KINONDONI PAUL MAKONDA AZINDUA MAONESHO YA 5 YA KAMPUNI YA EAG GROUP LEO JIJINI DAR.

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akikata utepe kuzindua maonyesho ya 5 ya Kampuni ya EAG Group Ltd yanayofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam,kutoka kushoto ni Msanifu majengo wa wizara ya Ardhi Julius Ndege na Mkurugenzi mkuu wa EAG group Ltd Imani Kajula.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akipewa maelekezo alipotembelea banda la DEGE Eco Village na  Mkurugenzi  na Afisa Masoko wa DEGE Eco Villag,Ashar Malik katika maonyesho ya 5 ya EAG Group Ltd yanayofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda Akimsikiliza Meneja masoko wa kampuni ya AVIC Internatinal Real Estate (T) Ltd, Linda Zhang alipotembelea maonyesho ya 5 ya kampuni  EAG Group Ltd yanayofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akionyeshwa namna mbalimbali za kujenga nyumba kwa kutumia vyuma na Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya PIVOTECH,Eric Chonjo  alipotembelea banda la Kampuni ya PIVOTECH katika aonyesho ya 5 ya kampuni  EAG Group Ltd yanayofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wananchi waliotembelea mabanda mbalimbali katika maonyesho ya 5 ya kampuni  EAG Group Ltd yanayofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika maonyesho ya 5 ya kampuni  EAG Group Ltd yanayofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images