Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 538 | 539 | (Page 540) | 541 | 542 | .... | 1897 | newer

  0 0

  KWA mara ya kwanza baada ya miaka mingi, ukumbi wa Mango Garden, ulioko Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kupitisha wikiendi bila burudani yoyote, leo usiku ‘utawaka moto’ wakati Yamoto Band na Mashauzi Classic zitakapotoa shoo kabambe hapo.
  Wasanii wa yamoto band.

  Ni onyesho ambalo limeteka hisia za mashabiki wa muziki kutokana na ukweli kuwa vikundi hivyo viwili havijawahi kukutana katika katika onyesho la pamoja, ukiondoa yale matamasha yanayoshirikisha wasanii wengi.

  Kesho, Ijumaa,  Malaika Band ambao hupiga hapohapo Mango Garden, kila Ijumaa, watakuwa Arusha mjini wakitoa burudani.
  Mwimbaji na Kiongozi wa Kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhani 'Isha Mashauzi'.

  Vilevile,  Twanga Pepeta ambao hupiga Mango Garden kila Jumamosi, wasanii hao Jumamosi hii watakuwa Wenge Garden Ukonga.  Bendi ya FM Academia ambayo huibuka Mango Garden na kufukia viraka vya bendi zilizopata dharura ya kuhama ukumbi, Ijumaa hii itakuwa Polisi
  Kilwa Road wakati Jumamosi itakuwa Leaders Club katika tamasha la Nyama Choma.

  0 0

   Dr. Fatma Mrisho, Executive Director for Tanzania Commissions for AIDS (TACAIDS), joined by Former President Hon. Benjamin Mkapa (centre) and The Managing Director of AngloGold Ashanti - Geita Gold Mine Mr. Terry Mulpeter and Mr. Simon Shayo Vice President of Sustainability and their colleagues during the launch of Kilimanjaro Challenge 2015 campaign in Dar es Salaam. TACAIDS received a cheque worth two hundred million so as to facilitate the eradication of HIV and AIDS in Tanzania.
   DC of Geita, Hon. Manzie Mangochie receive TZS 100M on behalf of Geita District Hospital from the Former President Hon. Benjamin Mkapa and The Managing Director of AngloGold Ashanti - Geita Gold Mine Mr. Terry Mulpeter and Mr. Simon Shayo Vice President of Sustainability during the launch of Kilimanjaro Challenge 2015 campaign in Dar es Salaam.
   The Former President Hon. Benjamin Mkapa and The Managing Director of AngloGold Ashanti - Geita Gold Mine Mr. Terry Mulpeter and Mr. Simon Shayo Vice President of Sustainability at AngloGold Ashanti - Geita Gold Mine during the launch of Kilimanjaro Challenge 2015 campaign in Dar es Salaam.
  Some of the participants joined by the Former President Hon. Benjamin Mkapa and The Managing Director of AngloGold Ashanti - Geita Gold Mine Mr. Terry Mulpeter and Mr. Simon Shayo Vice President of Sustainability at AngloGold Ashanti - Geita Gold Mine during the launch of Kilimanjaro Challenge 2015 campaign in Dar es Salaam.

  0 0


  0 0

  Na Ali Issa Maelezo Zanzibar.                                                           


  Naibu waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mahamoud Thabiti Kombo amesema bodi ya Chakula, Madawa na Vipodozi inajenga maabara ya kisasa  ya uchunguzi wa madawa , chakula na vipodozi ambayo itakuwa na ubora wa Kimataifa.  Hayo ameyasema leo huko Baraza la Wawakilishi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Mhe. Jaku Hashimu Ayoub aliyetaka kujua kwamba bodi ya Chakula, Madawa na Vipodozi ni taasisi muhimu kwa afya za binaadamu, kwanini Wizara haifikirii kuipa ruzuku na lini watawapa ruzuku hizo.  Alisema ruzuku  ya bodi hiyo itapatiwa katika bajeti ijayo na zaidi ya  milioni 70 zimetengwa kuipa bodi hiyo ili kuyafikia mahitaji yao  ikiwa pamoja na ujenzi huo wa maabara.“Hivi sasa bodi wana tengeneza laborali ya kisasa inayoweza ushindani kuvipima vyakula vinavyoingia nchini”,alisema Naibu Waziri huyo.  Aidha Naibu Waziri huyo alisema kuwa hakuna ruhusa ya chakula, dawa na vipodozi kuingia dukani bila ya bodi hiyo kuvifanyia uchunguzi wa kimaabara na pale vitu hivyo vinapobainika kuwa ni vibovu ndio bodi huchukua jukumu la kuviangamiza.“Inapobainika kuwa chakula, Madawa na vipodozi ni vibovu basi mmiliki hupigwa faini kwanza na baadae hulazimika alipie kazi ya uangamizaji”, alisema Mahamoud.  Wakati huo Naibu Waziri huyo kwa niaba ya Waziri wa Afya alitoa tarifa fupi ya dharura juu ya ukosekanaji wa maji katika Hospitali ya Mnazi Mmoja ambayo ilileta usumbufu mkubwa hospitalini hapo.Hata hivyo alisema huduma hiyo tayari imeshapatiwa ufumbuzi kwa ushirikiano na mafundi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar ambapo huduma hiyo  inapatikana bila ya usumbufu.


  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO- ZANZIBAR 

  0 0

  ASILIMIA 61 ya ardhi nchini imeharibika kutokana uharibifu wa mazingira ya ardhi  katika vyanzo vya mbalimbali na kusababisha kuzama kwa baadhi ya viziwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

  Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira,Mhandisi Binith Mahenge wakati akitangaza maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani  yatakayofanyika Juni 5 mwaka  huu mkoani Tanga.  Mahenge amesema Juni 5 ya kila mwaka iliamuliwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1972 kuwa Siku ya mazingira duniani kutokana na kuonekana baadhi  ya vyanzo vinapotea kutokana na uchafuzi mazingira.

  Amesema mikoa ambayo imekuwa kame kutokana na uharibifu wa mazingira ni Dodoma,Shinyanga,Geita,Singida,Simiyu na Kilimanjaro huku kasi yaukataji miti ikiwa inaongezeka na kufikia hekta 400, 000  kupotea kila mwaka nchini. Waziri huyo ameunga mkono kwa Kampuni ya simu za mikononi Airtel kuungana kuadhimisha siku ya mazingira kwa kuchangia kutoa elimu kwa njia ujumbe mfupi.

  Afisa Mawasiliano na Matukio wa Airtel,Dangio Kaniki,amesema watatoa
  ujumbe mfupi kwa ajili ya kutoa elimu kwa katika kuhamasisha utuzaji
  wa mazingira na kutaka makampuni mengine yajitokeze kuunga juhudu za
  utuzaji wa mazingira. Dangio,amesema ujumbe mfupi wataotoa katika utuzaji wa mazingira katika maadhimisho hayo ni zaidi ya Sh.milioni 90 ambazo Airtel ingepata kutokana na kutuma ujumbe huo.
    Afisa Usalama na Mazingira wa Airtel, Mazoya Ncheye (katikati) akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Binilith Mahenge msaada wa moja ya fulana zilizotolewa na Airtel Tanzania, kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yatafanyika Juni 1-5 mwaka huu, mkoani Tanga, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.
  Afisa Usalama na Mazingira wa Airtel, Mazoya Ncheye (kushoto)akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa RaisDk. Julius Ningu msaada wa moja ya fulana zilizotolewa na Airtel  Tanzania, kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayokitaifa yatafanyika Juni 1-5 mwaka huu, mkoani Tanga, katika haflafupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wanaoshuhudia ni AfisaUhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa pili kushoto) na(kulia) ni Meneja Uthibiti wa Airtel, Calvin Simba
    Afisa Usalama na Mazingira wa Airtel, Mazoya Ncheye (wa pili kulia)   akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Mhandisi Angelina Madete msaada wa moja ya fulana zilizotolewa na Airtel Tanzania, kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yatafanyika Juni 1-5 mwaka huu, mkoani Tanga, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Mazingira, Dk. Binilith Mahenge (wa pili kushoto) na (kulia) ni Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. George Nyatega (mwenye tai) akipokea tuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti (RAAWU) - Tawi la HESLB Bw. Deodatus Mwiliko kutambua uongozi wake bora katika HESLB tangu ilipoanzishwa mwaka 2005. Wengine ni viongozi wa RAAWU-HESLB Bw. Luhano Lupogo na Bi. Octavia Selemani. Picha: HESLB

  Watumishi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wametakiwa kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuondokana na malalamiko kutoka kwa wanafunzi.

  Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. George Nyatega ametoa wito huo mara baada ya kukabidhiwa tuzo na Chama chaWafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti (RAAWU), tawi la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

  Akiongea katika hafla fupi ya kukabidhi ngao hiyo, Mwenyekiti wa RAAWU Tawi la HESLB Bw. Deodatus Mwiliko alisema RAAWU, Tawi la HESLB imeamua kumkabidhi Mkurugenzi mtendaji huyo ngao hiyo kutokana na kujali na kuboresha mazingira ya kufanya kazi kwa watumishi wote wa HESLB.

  Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema amepokea tuzo hiyo kwa niaba ya menejimenti anayoingoza na wafanyakazi wote na kuwataka watumishi wa HESLB kutoridhika na ufanisi uliopo na badala yake waongeze juhudi.

  “Ninapokea hii ngao kwa niaba ya menejimenti na wafanyakazi wote kwa sababu sifanyi kazi peke yangu,” alisema Bw. Nyatega leo (Alhamisi, Mei 28, 2015) katika makao makuu ya HESLB jijini Dar es Salaam.

  “Ninawapongeza kwa kufanya kazi kwa ufanisi, lakini pia muongeze juhudi katika utoaji wa huduma kwa wanafunzi ili pasiwe na malalamiko,” amesema Bw. Nyatega.

  HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu. Tangu kuanzishwa kwake, Bw. Nyatega amekuwa Mkurugenzi Mtendaji wake.

  0 0

   Mwigizaji wa Origino Komedi ,Mjuni Sylivery(Mpoki,nyani Mzee),akipewa maelekezo ya kuendesha Trekta mara Baada kukabidhiwa ufunguo wake na  Fundi Mkuu wa Kampuni ya Farm Equip Tanzania , Yunusu Nsekela wakati wa kukabidhiwa Matrekta kwaajili ya kilimo jijini Dar es Salaam leo
   Mwakilishi wa muigizaji Josef Shamba(Vengu),ambaye hakuweza kufika kupokea Trekta lake kwa sababu ya Maradhi yanayomsumbua akipokea ufunguo kutoka kwa  Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink jijini Dar es Salaam leo.
   Mwakilishi wa muigizaji Josef Shamba(Vengu),ambaye hakuweza kufika kupokea Trekta lake kwa sababu ya Maradhi yanayomsumbua akipokea ufunguo kutoka kwa  Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink jijini Dar es Salaam leo.
   Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink  akisalimiana mara baada ya akimkabidhi ufungua wa Trekta lake Mwigizaji wa Origino Komed, Isaya Mwakilasa(Wakuvanga) jijini Dar es Salaam leo.
    Mwigizaji wa Origino Komedi ,Mjuni Sylivery(Mpoki,nyani Mzee) akishukuru kwa niaba ya waigizaji wa kundi la Origino Komedi  mara baada ya kukabidhiwa Funguo za Matrekta ya Kilimo jijini Dar es Salaam leo, kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink,Isaya Mwakilasa(Wakuvanga ),Lucacy Mhavile(Joti) na kulia ni Alex Chalamila(Mackregani).
    Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink akizungumza na Vijana wa Kundi la Origino    Komedi mara baada ya kuwakabidhi funguo za Matrekta ya kilimo jijini Dar es Salaam leo.
   Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink , katika picha ya pamoja waigizaji wa kundi la Origino  Komedi na nyuma yao ni Matrekta ambayo wamekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza katika makabidhiano ya Matrekta ya Kilimo kati ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink na Waigizaji wa kundi la Origino Komedi, leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Matrekta ya Kilimo ambayo waigizaji wa Kundi la Original Comedi wamekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam. Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.


  Na Avila kakingo,Globu ya Jamii.
  WAIGIZAJI wa kindi cha Origino Komedi  wamewaasa vijana kutumia vipaji vyao ili kutengeneza maisha yao kuwa  mazuri na sio kufikiri kuwa vijana wengi hushikwa mkono na mtu ili kufanikiwa.


  Hayo yamesemwa na kundi la waigizaji wa Origino Komedi wakati wa kukabidhiwa Matrekta ya Kilimo aina ya Sonalika kutoka kampuni ya Farm Equip Tanzania jijini Dar es Salaam leo.


  Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink amesema kuwa  vijana  wameamua kufanya jambo la maana kwa jamii ,"kwani wamenunua matrekta kwa ajili ya kilimo,vijana wengi wamekuwa wakinunua magari ya kifahari  bila kujua kunakesho na keshokutwa kwa maendeleo yao",alisema Bwa Arif.


  Nae Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amewapongeza vijana wa kundi hilo kuwa kufanya maamuzi sahihi na ya maendeleo kwa kununua Matrekta hayo kwaajili ya kilimo,amesema kuwa uamuzi wao ni mzuri hata kwa jamii kwani pia kwa namna moja ama nyingine itasaidia kuongeza ajira kwa vijana,kwakuwa kilimo kinahitaji watu wengine na sio wao wenyewe watakao weza kuendesha Matrekta hayo mashambani.


  Kundi hilo la Origino Komedi  linaundwa na vijana 7 ambao ni Alex Chalamila(Mackregani),Josef Shamba(Vengu),Mjuni Sylivery(Mpoki,nyani Mzee),Lucacy Mhavile(Joti), Isaya Mwakilasa(Wakuvanga),Emmanuel Mgaya(Masanja mkandamizaji) na Davidi Seki.


   Waigizaji hao wameahidi kupoleka Matrekta yao kwenda kubeba takataka katika Wilaya ya Kinondoni ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda atazindua  kampeni ya Ona aibu, ambayo itahamasisha usafi katika Wilaya ya Kinondoni.

  0 0

   Wanafunzi wenye ulemavu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Abisina Rashid (kulia) na Rozalia Polycarp (wa pili kulia), wakishiriki katika uzinduzi wa kisima cha maji kwa kufungua maji baada ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kukabidhi msaada wa kisima hicho kwa shule hiyo Dar es Salaam jana. Kisima hicho kitakachohudumia pia Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa ujenzi wake ulisimamiwa na Kampuni ya Winners. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Winners iliyosimamia ujenzi wa kisima hicho, Balozi mstaafu,Herman Mkwizu, Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (wa pili kushoto),Ofisa Elimu Taaluma Manispaa ya Ilala, Rehema Msogoloni na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Anna Mshana.
   Ofisa Elimu Taaluma Manispaa ya Ilala, Rehema Msogoloni (wa pili kulia) akisaidia kumtwisha ndoo ya maji Zarina Kigoma baada ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kukabidhi msaada wa kisima cha maji kwa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam jana.Anayeshangilia kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Anna Mshana.Kisima hicho kitakuwa kinahudumia pia Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa.
   Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kulia) akinywa maji ya bomba baada ya kukabidhi msaada wa kisima kwa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Ofisa Elimu Taaluma wa Manispaa ya Ilala, Rehema Msologoni na Mkurugenzi wa Kampuni ya Winners iliyosimamia ujenzi wa kisima hicho.
  Mwanafunzi mwenye ulemavu wa kuona akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwapatia msaada huo muhimu kwao.


   Ofisa Elimu Taaluma Manispaa ya Ilala, Rehema Msogoloni (wa pili kulia) akisaidiana na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (wa pili kushoto), kufunua kitambaa ikiwa ni ishara ya makabidhiano ya kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa TBL katika Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Winners iliyosimamia ujenzi huo, Balozi mstaafu Herman Mkwizu na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Anna Mshana.
   Ofisa Elimu Taaluma Manispaa ya Ilala, Rehema Msogoloni (wa pili kulia) akisaidiana na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (wa pili kushoto), kufunua kitambaa ikiwa ni ishara ya makabidhiano ya kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa TBL katika Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Winners iliyosimamia ujenzi huo, Balozi mstaafu Herman Mkwizu na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Anna Mshana.
   Viongozi hao wakipongezana baada ya makabidhiano ya kisima hicho
   Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Kilindo akielezea mikakati mbalimbali ya kampuni hiyo katika kusaidia jamii hasa katika sekta ya maji kutokana na faida ya mauzo ya vinywaji vyao.
   Herman Mkwizu ambaye Kampuni yake ya Winners inajishughulisha na uboreshaji wa miundombinu ya maji akielezea jinsi watakavyoendelea kuusimamia mradi huo wa maji.
   Ofisa Elimu Taaluma wa Manispaa ya Ilala, Rehema Msologoni akishukuru kwa niaba ya Serikali baada ya kupokea msaada wa kisima hicho kutoka TBL.
   Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Anna Mshana akiishukuru  TBL kwa msaada huo wa kisima ambao ni muhimu mno hasa kwa wanafunzi wenye ulemavu wa shule hiyo waliokuwa wakiteseka kutafuta maji.
   Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu  akizungmza wakati wa hafla hiyo
   Wanafunzi wakifurahia kukabidhiwa mradi huo

  0 0

  Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum akiwa ameshika mwenge baada ya kufika mtaa wa Kisutu jijini Dar kwenye uzinduzi wa magari mapya ya kuzoa taka katika manispaa ya Ilala yanayomilikiwa na na kampuni ya Green WastePro ltd. Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog 
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akizungumza jambo mara baada ya Mwenge wa Uhuru kufika eneo la Kisutu jijini Dar kwa ajili ya ufunguzi wa Magari ya kisasa ya kuzoa taka.
  Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa magari ya kufanyia usafi yanayomilikiwa na Kampuni ya Green Waste Pro ltd.
  Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw.Abdallah Mbena akisoma risala kwa mgeni rasmi ambaye ni kiongonzi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2015 , Bw. Juma Khatibu Chum (hayupo pichani).
  Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum (kushoto) akikabidhiwa risala na Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw.Abdallah Mbena iliyosomwa wakati wa uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi katika manispaa ya Ilala jijini Dar.
  9
  Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo (katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wakiwa kwenye zoezi la kuweka uchafu kwenye moja ya gari la kufanyia usafi lililozinduliwa na Mwenge wa Uhuru.
  Mmoja wa viongozi wa Mbio za Mwenge akizungumza mara baada ya uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi katika manispaa ya Ilala yanayomilikiwa na Kampuni ya Green Waste Pro Ltd aliwasisitiza wananchi kuendelea kutumia kampuni hiyo kwani usafi utaendelea kuimarika zaidi na zaidi.
  Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum(wa kwanza kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (wa pili kutoka kushoto), Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Kheri Kessy(katikati) Mkurugenzi wa Green WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo( wa pili kutoka kulia) pamoja na Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw. Abdallah Mbena wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi katika eneo la Kisutu jijini Dar.
  Mmoja wa viongozi wa mbio za mwenge akiwa ameshikiria Mwenge wa Uhuru tayari kwa kuondoka mara baada ya kumaliza uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi mali ya kampuni ya Green Waste Pro Ltd inayofanya kazi za usafi katika manispaa ya Ilala jijini Dar.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Ndugu Isaya M. Mngurumi (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo akiwa na Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw.Abdallah Mbena wakiwa wanatoa maelezo juu ya uzoaji na usindikaji wa Taka zinazokusanywa katika sehemu mbalimbali za Manispaa ya Ilala na jinsi ya watakavyoyatumia magari hayo yaliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru. 

    Akizungumza wakati wakati wa tukio la uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi ya Kampuni iliyopewa zabuni kusafisha manispaa ya Ilala, Green Waste Pro Ltd Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi amesema kushirikiana vyema kwa kampuni Green Waste Pro Ltd ndiko kunako pelekea maendeleo na afya bora katika manispaa ya Ilala hivyo tuwaunge mkono wenzetu kwa kuwapa ushirikiano wa kuto tupa taka hovyo bali maeneo husika yaliyo wekwa kwaajili ya kuhifadhi taka hizo ili waweze kuzipitia kwa urahisi na kuzipeleka mahala panapo husika.

  0 0

  Viongozi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA) walioko madarakani sasa ambao wanaolalamikiwa kuingia madarakani kinyume na katiba ya chama hicho wakizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mjini Dodoma kuzungumzia mkutano wao mkuu unaoanza leo mjini Dodoma. Viongozi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA) walioko madarakani sasa ambao wanaolalamikiwa kuingia madarakani kinyume na katiba ya chama hicho wakizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mjini Dodoma kuzungumzia mkutano wao mkuu unaoanza leo mjini Dodoma.Viongozi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA) walioko madarakani sasa ambao wanaolalamikiwa kuingia madarakani kinyume na katiba ya chama hicho wakizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mjini Dodoma kuzungumzia mkutano wao mkuu unaoanza leo mjini Dodoma. Viongozi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA) walioko madarakani sasa ambao wanaolalamikiwa kuingia madarakani kinyume na katiba ya chama hicho wakizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mjini Dodoma kuzungumzia mkutano wao mkuu unaoanza leo mjini Dodoma.

  MGOGORO wa uongozi ndani ya Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA) umeingia katika hatua tata baada ya viongozi waanzilishi wa chama hicho kulalamikia uchaguzi uliopangwa kufanyika Mei 30, 2015 mjini Dodoma ilhali kuna mgogoro wa uongozi ndani ya chama hicho ukiendelea. 

  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa niaba ya viongozi wenzake Mwenyekiti wa TAPSEA, Pili Mpenda ambaye pia ni miongoni mwa waanzilishi wa chama hicho jana jijini Dar es Salaam alisema anasikitishwa na kitendo cha viongozi walioingia kinyume na katiba ya chama hicho kujipanga kufanya uchaguzi ilhali kuna kesi ya msingi ipo mahakamani kulalamikia wao kuondolewa madarakani. 

  Alisema viongozi waliopo madarakani sasa wameingia kwa nguvu za Msajili wa Vyama vya Siasa nchini baada ya kushinikiza uchaguzi kinyume na maelekezo ya Mkutano Mkuu wa kwanza wa TAPSEA uliofanyika Arusha Mai 18, 2013 wa chama hicho ambao ulielekeza maboresho ya katiba ya chama kabla ya chochote kufanyika. 

   Alisema mkutano mkuu wa pili uliofanyika mkoani Mwanza 2014 uliitishwa ili kuwaeleza wananchama juu ya shinikizo la msajili na wanachama wachache (7) kufanyika uchaguzi na kuwaeleza mwenendo wa marekebisho ya katiba ya TAPSEA lakini Ofisa msajili alishinikiza ufanyike uchaguzi ambao uliwagawa wanachama na wengine kususia uchaguzi huo kutokana na mvutano. 

  Bi. Mpenda alisema uchaguzi uliofanyika haukuwa halali kwani mbali na kufanyika kinyume na katiba ya TAPSEA na maelekezo ya Mkutano Mkuu wa kwanza haukushirikisha wanachama wote. Aliongeza kuwa kati ya wanachama halali 815 waliokuwa wamejisajili ni wanachama 200 tu ndio walioshiriki katika uchaguzi huo. 

  "...Uchaguzi huu ni kinyume na katiba ya TAPSEA na kinyume na maelekezo ya Mkutano Mkuu wa kwanza na ulifanyika kwa shinikizo la Msajili wa Vyama vya Siasa...sisi hatujui alitumia kifungu gani kuja kushinikiza uchaguzi na kuusimamia kinyume na katiba yetu," alisema Bi Mpenda katika mazungumzo.

   Aidha alisema tayari viongozi waliopinduliwa wameenda mahakamani kupinga kitendo hicho na msajili anafahamu lakini wanashangaa kuona viongozi wanaolalamikia wamejipanga kufanya uchaguzi mpya wa chama hicho Mai 30, 2015 mjini Dodoma. Hata hivyo taarifa kutoka kwa viongozi waliopo madarakani kwa sasa wamekiri kujiandaa na uchaguzi mkuu mpya kwa nafasi za juu za chama hicho pamoja na wajumbe 9 wa Kamati ya Utendaji. 

  Akizungumza leo mjini Dodoma na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa TAPSEA aliyepo madarakani kwa sasa, Festo Emmanuel amesema chama hicho kinaendelea na mkutano mkuu unaoanza leo mjini hapo na wamesajili upya wanachama ambapo imefikia jumla ya wanachama 1500. Na alikiri watafanya uchaguzi katika nafasi za juu za chama hicho. Viongozi wa TAPSEA walioko madarakani sasa ambao wanaolalamikiwa kuingia madarakani kinyume na katiba ya chama hicho wakizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mjini Dodoma kuzungumzia mkutano wao mkuu unaoanza leo mjini Dodoma.  

  0 0

    Abiria wakishuka kwenye  Ndege ya Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) aina ya CRJ 100. Picha ya Maktaba

  SHIRIKA la ndege la taifa (ATCL) limetangaza  uamuzi wake wa kuongeza idadi ya safari zake kuelekea visiwa vya Comoro hatua inayolenga kuendana  na ongezeko la mahitaji ya huduma za shirika hilo hususani katika kuelekea kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

  Kwa sasa shirika hilo linatoa huduma zake kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma na Mtwara kila siku. Sambamba na kutoa huduma hizo hapa nchini, shirika hilo lina mpango mpya utakaoanza rasmi tarehe mosi ya mwezi Juni mwaka huu kwa kuongeza safari zake kuelekea visiwa vya Comoro hadi kufikia mara nane kwa wiki ikiwemo mara mbili siku za Alhamisi.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Bw. Johnson Mfinanga alisema shirika hilo ndilo pekee linalotoa huduma ya safari za anga kati ya Tanzania na Visiwa vya Comoro huku akibainisha fursa za kibiashara zilizopo kati ya nchi hizi mbili jambo linalosababisha uwepo wa ongezeko la mahitaji ya huduma za ATCL.

  Pia amewaasa watanzania hususan wakazi wa mtwara kuchangamkia fursa hizo kwa kuwa shirika hilo kwa sasa linatoa huduma zake kati ya Mtwara na visiwa vya Comoro kwa siku za Jumatano na Ijumaa kila wiki.
  “Siku zote tumekuwa tukihakikisha kwamba tunabadilika kuendana na mahitaji ya wateja wetu.

   Ni dhahiri kwamba katika kipindi hiki kuna hitaji kubwa la usafiri wa anga kuelekea visiwa vya Comoro kwa sababu za  kibiashara, mapumziko na sherehe mbalimbali, hivyo ATCL imejipanga kuchangamkia fursa hiyo,’’ alibainisha.

  Akizungumzia ufanisi wa shirika hilo katika safari nyingine ikiwemo zile za Kigoma na Mtwara, Bw. Mfinanga alisema wamekuwa wakihudumia idadi kubwa ya abiria kutokana na ndege za shirika hilo kusafiri kwa mwendo kasi wa kuridhisha sambamba na huduma nzuri zinazotolewa kwa wateja wakati wa safari.

  “Zaidi tunaamini kwamba huduma tunazozitoa kati ya Tanzania na Comoro zimekuwa zikichangia kuongeza ushirikiano baina ya nchi hizi mbili na tunaamini kuwa hata hili ongezeko la safari zetu kwenye mataifa haya mawili zitatoa fursa kwa wateja wetu kufaidi fursa zinazopatikana ndani ya nchi hizi,’’ aliongeza Bw. Mfinanga.

  Kuhusu mpango wa shirika hilo kujipanua zaidi kihuduma, Bw. Mfinanga alisema:  “Ndege yetu aina ya De-Havilland Dash 8 Q300 kwa sasa inafanyiwa marekebisho makubwa kwenye karakana yetu iliyopo kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa  wa Julius Nyerere (JNIA) na itakapokamilika tutaendelea na huduma zetu katika mikoa ya Mwanza, Tabora, Kilimanjaro na Mbeya,’’

  Bw. Mfinanga aliongeza kuwa kwa kufanya safari zake kuelekea visiwa hivyo shirika hilo limekuwa likiwezesha wateja wake kunufaika na fursa zilizopo kwenye visiwa hivyo huku pia akitoa wito kwa watanzania wengine kujitokeza kushiriki katika kuchangamkia fursa hizo.

  0 0  Four Years in Heaven  It is now four years since God took you away on 31st May 2011  The vacant place you left in our home, will never be filled   Our darling mother, wife, sister, grandmother, we will always remember you  Time is a healer so people say  You went into a sleep that was long and deep  Your special smile  Your caring heart  That warm embrace, you always gave us  And most importantly, the astounding legacy you left behind  In our heart you will forever remain, Prof Helen IgobekoLugina  Helen, the bole of our family tree you are dearly missed by:  Husband – MaxmillianLugina

  Son – Dr. Emmanuel Lugina, Daughter – Mary Lugina Zangira

  Son in law – Richard Zangira, Daughter – RoselindaLugina Reuben

  Son in law – Kelvin Reuben, Granddaughter – Gabriella Zangira

  Grandson – Nathan Zangira, Granddaughter – Joanna Reuben

  0 0

  Tanzania imeadhimisha siku ya hedhi duniani, ambapo wizara ya elimu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamekubaliana kuandaa na kusimamia sera inayoondoa vikwazo kwa watoto wa kike katika masomo yao.

  Akizungumza katika maadhimisho hayo jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Elimu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Madina Kemilembe, alisema kukosekana kwa miundombinu rafiki mashuleni kunasababisha wanafunzi kutohudhuria masomo.

  Alisema ukosefu wa mazingira bora kama vyoo, maji safi na salama pamoja na vyumba mahsusi vya kubadilishia nguo , hasa kwa watoto wa kike wanapokua katika hedhi mashuleni kunachangia utoro. 

  “Nawashukuru wadau Water Aid, Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV), Kasole Secrets pamoja na wengine kwa kuisaidia serikali kuandaa mazingira rafiki kwa watoto wetu kwa kuwajengea vyumba vya kubadilishia na kuhakikisha upatikanaji wa pedi kwa baadhi ya shule,” alisema Kemilembe.

  Alisisitiza juu ya utoaji wa elimu kwa wazazi na wanafunzi wa jinsia zote ili kuondoa unyanyapaa ili kuboresha mazingira ya kusoma kwa mtoto wa kike. Naye Mkurugenzi wa Water Aid, Ibrahim Kabole, alisema kuna uelewa mdogo pamoja na mila potofu zinazofanya jambo la hedhi kuonekana ni la aibu.
   Afisa Elimu Mkuu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi Madina Juma, akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya hedhi duniani yaliyofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya mnazi mmoja. Kauli Mbiu ya mwaka huu inaeleza "Usisite kuzungumzia hedhi".
   Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye maandamano ya kuadhimisha siku ya hedhi duniani yaliyofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania jana jijini Dar es Salaam.Kauli Mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inaeleza "Usisite kuzungumzia hedhi".

  0 0
 • 05/29/15--01:54: Article 16


 • 0 0
 • 05/29/15--02:26: Article 15


 • 0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera (kushoto) akipokea msaada wa mashuka 150 yatakayotumika jana mjini Babati kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa huo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) Michael Mhando.
   Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) Michael Mhando (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera kifaa tiba cha mama mjamzito jana mjini Babati ili kitumiwe na wanawake watakaopata huduma ya matibabu kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa huo.
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akionyesha dawa zilizotolewa na Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) Michael Mhando jana mjini Babati, ambapo NHIF ilitoa msaada wa vifaa tiba na dawa zenye thamani ya shilingi milioni 5.5. 

  0 0

  01
  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo leo bungeni mjini Dodoma.
  02
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Said Mtanda akiwasilisha mapendekezo ya kamati yake kuhusu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa bajeti ya wizara hiyo leo mjini Dodoma.
  03
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na Naibu Katibu Mkuu Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kutoka kushoto) wakifuatilia kwa makini bajeti ya Wizara hiyo leo mjini Dodoma.
  04
  Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi kwenye viwanja vya bunge leo mjini Dodoma.
  PICHA ZOTE NA FATMA SALUM – MAELEZO
  ……………………………………………….
  Abraham Nyantori MAELEZO, Bungeni, Dodoma
  Serikali imeshauriwa kutenga fedha za kutosha ili kuiwezesha Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. 
  Ushauri huo umetolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakati wa kuwasilisha mapendekezo yake leo bungeni mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa kamati Mhe. Said Mtanda amesema Wizara hiyo ina jukumu la kuratibu na kusimamia maendeleo ya vijana, utamaduni, michezo na habari hivyo ikipewa fungu la kutosha itaweza kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta hizo. 
  Akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake bungeni leo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara ameliomba Bunge kuidhinisha bajeti ya wizara hiyo ya shilingi bilioni 29.4 ambapo shilingi bilioni 5 ni kwa ajili ya maendeleo na shilingi bilioni 24.4 ni matumizi ya kawaida.
  Aidha Waziri Mukangara ameeleza jitihada mbalimbali zinazofanywa na wizara yake zikiwemo kuratibu na kuwajengea vijana uwezo wa kubuni mawazo bora ya kujiajiri, kuhamasisha halmashauri kutenga asilimia 5 ya bajeti yao kuboresha mifuko ya vijana na kuhamasisha uanzishaji wa SACCOS.
  Katika mwaka wa fedha uliopita wa 2014/2015, Waziri Mukangara amesema wizara yake ilitoa mafunzo kwa vijana 1550 katika kujenga dhana ya kujiajiri, na jumla ya shilingi bilioni 2 zilikopeshwa kwa vikundi mbalimbali vya vijana kote nchini.
  Kwa upande mwingine Dkt Mukangara amesema wizara yake imekamilisha miradi kadhaa ukiwemo mradi wa Mawasiliano na kukamilisha lengo la milenia la kubadili matumizi ya analojia kwenda dijitali, mradi huo ulikamilika mwezi Aprili mwaka huu. Miradi mingine katika mwaka wa fedha uliopita ilikuwa ni ya utafiti ukiwemo wa msamiati wa lugha za jamii, utafiti wa majina fiche 1800 ya lugha za asili.
  Wizara katika mwaka huu wa fedha imeahidi kuongeza ufanisi ikiwemo kuongeza ajira kwa vijana, kulinda mazingira, kutoa habari, kulinda mila na desturi kudumisha amani na mshikamano wa katika jamii ya watanzania.
  Leo ni siku ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Wizara ya Maliasili na Utalii ambazo zimewasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara zao na hatimaye kuruhusu Bunge kuendelea kuzijadili bajeti hizo.
  / mitambo ya kukodi TBC na uchaakavu wa majengo, madeni 3.2 /1.3 serikali.
  Katika kipindi cha 2014/15 wizara ipanga kukusanya sh. 1,149,008,000 kutoka vyanzo mbalimbali zilizokusanywa ni sh. 811,616,116 sawa 71% 
  Wizara ilitengewa (2014/2015) 19,806,611,000 zilipokelewa sh. 14,446,963,490 sawa na 73% ya bajeti ya matumizi ya kawaida. 
  Fedha za maendeleo wizara 2014/15 ilitengewa 16,850,000,000 ilipokea hadi april 2015 >7,000,000,000 sawa 42% upanuzi wa usikivu wa shirika la utangazaji la Tanzania TBC Moja ya changamoto ni kuongezeka kwa mifumo na njia za mawasiliano kwa umma kama mitandao ya jamii kwenye intanet kunakoadhiri maudhui ya taarifa zinazotolewa  Wizara kukabiliana na changamoto hizo imetoa elimu na kutembelea vituo kwa kushirikia na kamati ya maudhui (TCRA)

  0 0

   Since December 31, 2012 Tanzania started migrating from analogue to digital broadcasting. The implementation has been successful by 100% which makes Tanzania the first country in the East African Community (EAC) and Southern Africa Development Community (SADC) to meet the deadline imposed by the International Telecommunication Unity (ITU). In fostering this process StarTimes in partnership with SmartCodes is now running a campaign which offers an added value to digital broadcasting.  

  Digital broadcasting which allows the consumers to choose from multiple methods of receiving television signals has given innovators at SmartCodes and Startimes the opportunity to make TV more private and personalized. Tenbre a mobile application that can be downloaded for free allows the user to access StarTimes guide wherever they are and share it.


  With this mobile application the user can; find out what are showing in the next 7 days; sort all channels according to countries, regions, genres and bouquets; create their own favorite channel list; search shows or channels by the title; see what shows are on air; see the ranking order of the coming shows; see recommended shows and channels; set reminders for any show they like; view their wallet; receive their tasks and gain coins; alert setting; view their reminders and favorites; invite friends and get free coupon for recharging; access user friendly chat room; top post in each chat room for easy viewing of up-to-date information; support long press to copy text in chat room; support directing web links by clicking on the link; view number of people currently online in each chat room hence the number of people who are watching particular TV at that particular moment. All this has been made possible on the hand of the consumer.


  It is of great honor that SmartCodes and StarTimes have pioneered in digitizing Tanzania. The big idea here is merging tradition with modern which is what SmartCodes envision. SmartCodes believes that if the government of the United Republic of Tanzania continues to support such initiatives by making them more accessible and affordable by year 2020 Tanzania will be the hub of technological innovation in Africa.  As we say in SmartCodes technology is for everyone and so it ought to be.


  SmartCodes is the awards winning Tanzanian full service digital agency. SmartCodes is a single stop for all digital pursuits. Over the past 5 years, the commitment of the innovative minds you could find in the industry has contributed to the dynamic growth of Digital Industry not only in Tanzania but Africa. SmartCodes has contributed immensely on the exponential growth of digital products consumption in Tanzania. 

  Currently Tanzania has about 31.86million mobile phone users and of that about 40% uses smartphones. With that rapid growth SmartCodes is now servicing a vast portfolio of clients across the sub-Saharan Africa. Quality, on time delivery and on budget has been their strongest reputation.  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA) Dkt.Joseph .M.Kihanda mwenye suti nyeusi(waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Mafunzo maalum kuhusu sheria mpya ya manunuzi ya umma yaani PPA 2011 na kanuni zake PPR.2013 ambao ni wadau wa kitengo cha manunuzi kinachosimamiwa na Bi.Juliana Musomi,Pius Seda,Salha Tego,Dickson Biya,Ezra Obilla,Kennedy Ndosi,Zubeda Mohamed,Alton Kumburu  na Stephen Mahinya),wajumbe wa bodi ya zabuni ya Taasisi hiyo ambao ni Bw.Zodo .M.Zodo,Bi.Linah Tumwidike,Bajjet Naresho,Anthony Mzurikwao,Said Mayunga,Lucina Comino na Burkad Haule pamoja  na wawezeshaji toka Mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa umma (PPRA) ambao ni Bw.Gilbert Kamnde akishirikiana na ,Onesmo France,pia washiriki wengine walikuwa ni mkurugenzi wa biashara wa Taasisi hiyo Bw.Mzee Boma na  mameneja wote wa matawi ya Taasisi hiyo ambao ni  Ndugu John Boneka(Kigoma)Bw.Emmanuel Kingu (Singida),Luciana Hembe Mwanza)Bw.Mugisha Kamala (Mbeya na Bw.Matei Mapunda(Mtwara).
  Wasiriki wakiwasikiliza wawezeshaji kabla ya kumalizika kwa mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa baraza la maaskofu wa kanisa katoliki Tanzania T.E.C Kurasini jijini Dar es Salaama kwa siku tano kuanzia tarehe 25/5/2015 hadi tarehe 29/5/2015 ambapo washiriki watatunukiwa vyeti vya mahudhurio toka PPRA.
  Mkuu wa kitengo cha Manunuzi wa Taasisi hiyo akiwa anaendelea kufuatilia kwa makini mafunzo hayo ambapo amekiri yatasiadia kuongeza ufanisi katika kitengo chake na Taasisi kwa ujumla hivyo kuomba Afisa mtendaji mkuu kuwawezesha mafunzo mbalimbali yanayohusu manunuzi ili Taasisi iendelee kufanya manunuzi kwa kuzingatia thamani ya pesa yaani '' Value for Money Procurement'' na kuiletea Taasisi Sifa nje na ndani ya Nchi kwani inatoa pia mafunzo katika ngazi ya cheti hadi Postgraduate kwa masomo hyo ya ugavi,ughasibu na mengine mengi katika nynja ya biashara.Hivyo ni wito pia kwa watanzania wote wanaohitaji kusomesha watotot wao katika chuo kinachotambuliwa na serikali kuwaleta watoto wao waje kusoma TIA...kwa maelezo zaidi na form za kujiunga chuo bonyeza hapa chini..

  0 0


  Dkt Fidelis Owenya akikabidhi jezi kwa vilabu nane vilivyo fuzu kucheza hatua ya robo fainali katika mashindano ya kombe la Mbunge lijulikanalo kama Lucy Owenya Cup 2015 yanayofanyika katika jimbo la Moshi vijijini.
  Jezi maalumu kwa ajili ya timu zilizo fuzu hatua ya robo fainali katika mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015.
  Baadhi ya iongozi wa timu zilizofuzu hatua ya robo fainali wakifunga jezi zao mara baada ya kukabidhiwa kwa ajili ya hatua ya robo fainali. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
older | 1 | .... | 538 | 539 | (Page 540) | 541 | 542 | .... | 1897 | newer