Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 537 | 538 | (Page 539) | 540 | 541 | .... | 1896 | newer

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha   na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akiwaeleza Mawaziri wa Fedha kuhusu serikali ya Tanzania ilivyonufaika na fedha za Benki ya Maendeleo katika kutekeleza mipango yake hasa  kwenye miundombinu. Kutoka kulia ni Waziri wa Fedha wa Rwanda Bw. Claver Gatete  na kushoto kwake ni  Mchumi Mkuu Rugwabiza Minega Leonard.  Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha   na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akitoa ufafanuzi kuhusu Tanzania inavyoshirikiana na Benki ya Afrika kwa Mawaziri wa Fedha kutoka  nchini Rwanda, Ethiophia, Kenya na Visiwa vya Shelisheli wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya utekelezaji wa mazimio ambayo kila nchi imejiwekea.
   Waziri wa Fedha wa Rwanda Mhe. Claver Gatete akitoa ufafanua wa masuala mbalimbali yanayohusu nchi za Afrika. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile ambaye amemwakilisha Waziri wa fedha na kulia kwake ni Waziri wa Fedha wa Ethiophia Mhe. Fisseha Aberra.

   Kamishna wa Fedha za Nje Bwana Ngosha Manyoga akiwa katika majadiliano yanayohusu ya ripoti ya utekelezaji wa mpango wa mafanikio  katika nchi za Africa.
   Wajumbe waliohudhuria Mkutano wa Kanda ya Afrika  wakimsikiliza na kufuatilia kwa makini Dkt. Mulu Ketsela ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika alipokuwa akiwasilisha ripoti ya Benki hiyo.

  0 0  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na mtoto Albert Kanan wa darasa la tatu katika shule ya msingi ya Ilalangulu wilayani Mlele ambaye alikwenda nyumbani kwa Waziri Mkuu katika kijiji cha Kibaoni akiomba kupiga naye picha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0


  0 0


  Mkurugenzi wa VETA,Mhandisi Zebadiah Moshi (kushoto) akitia saini ya makubaliano kati ya Veta na Serikali ya Australia na Kulia ni Naibu Waziri Mkuu wa Jimbo la Australia Magharibi na Waziri wa Afya na Utalii Dk.Kim Hames wanaoshudia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Consolata Mgimba,Balozi wa Australia nchini,John Feakes katika hafla ya makubaliano kati ya VETA na Serikali ya Australia iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam.  
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Consolata Mgimba akizungumza na waandishi habari katika hafla ya kusaini makubaliano kati ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA),iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam.  
  Mkurugenzi Mkuu wa VETA,Mhandisi Zebadiah Moshi na akizungumza na waandishi habari katika hafla ya kusaini makubaliano kati ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA),iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri Mkuu wa Jimbo la Australia Magharibi na Waziri wa Afya na Utalii Dk.Kim Hames  akizungumza na waandishi habari katika hafla ya kusaini makubaliano kati ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA),iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam.  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Consolata Mgimba (Katikati),Kushoto ni Mkurugenzi  Mkuu wa VETA,Mhandisi Zebadiah Moshi,kulia ni Naibu Makamu,Magharibi wa Australia,Waziri wa  Afya na Utalii,Dk.Kim Hames pamoja na watendaji wa VETA na Ubalozi wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya kusaini makubaliano kati ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA),iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam.


  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

  MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)imeanzisha mfumo wa mafunzo stadi katika sekta ya madini na gesi ambao utasaidia watu wanaohitimu katika mafunzo hayo duniani.

  Hayo ameyasema leo Mkurugenzi Mkuu wa VETA,Mhandisi Zebadiah Moshi wakati wakisaini makubaliano na serikali ya Australia kuptia shirika la Idara ya Mambo ya Nje na Biashara (DFAT)iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam.

  Amesema katika makubaliano hayo,Serikali ya Australia imekubali kutoa Sh.milioni 330  kwa ajili mfumo huo ambao utatengenezwa na wataalam wa nchi hiyo.

  Mhandisi Moshi amesema manufaa ya mfumo huo kwa VETA kuimarisha ushirikiano na viwanda au waajiri mbalimbali, kulenga kutoa mafunzo ambayo yanaendana na mahitaji ya soko la ajira,uboreshaji wa viwango vya mafunzo yanayotolewa na viwanda,kuipunguzia mzigo serikali katika kuilea VETA kwa kuchangia gharama za mafunzo kwa njia ya vifaa au kutoa wataalam wa kufundisha.

  Naibu Waziri Mkuu wa Jimbo la Australia Magharibi na Waziri wa Afya na Utalii Dk.Kim Hemes  amesema nchi yao imepiga hatua katika utoaji wa mafunzo na viwango vyake vinatambulika duniani  katika madini,mafuta,gesi pamoja na Utalii.

  0 0


  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amepokea msaada wa vitabu 895 vyenye thamani ya sh. milioni 6.5/- ikiwa ni jitihada ya wadau mbalimbali kuchangia shule ya msingi aliyosoma ya Kakuni iliyoko kijiji cha Kibaoni, wilayani Mlele, mkoani Katavi.  Waziri Mkuu amepokea msaada huo jana mchana (Jumanne, Mei 26, 2015) kwenye shule mpya ya msingi Kakuni ambayo bado inaendelea kujengwa kwenye kijiji cha Kibaoni.  Akizungumza katika hafla hiyo fupi mara baada ya kupokea msaada huo, Waziri Mkuu Pinda aliishukuru kampuni ya General Booksellers Ltd ya kutoka Dar es Salaam kwa msaada huo ambao alisema utachangia kwa kiasi kikubwa kuitimiza ndoto yake aliyokuwa nayo ya kuisaidia jamii iliyomsomesha.  “Wazo la ujenzi wa shule mpya ya msingi Kibaoni lilitokana na ukweli kwamba nilisoma na kumaliza kwenye shule hii ya Kakuni. Nikiwa ni mtumishi wa Serikali, ni Mbunge na sasa hivi ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nilijiuliza hivi shule hii ninaweza kuiacha hivi hivi?”  “Nilijiuliza sana ni jambo gani ambalo naweza kulifanya la kusaidia wanakijiji wenzangu na kata nzima ya Kibaoni kama shukrani kwa kunilea na kunifikisha hapa nilipo. Ndipo wazo la kujenga shule niliyosoma likazaliwa kama mwaka mmoja na nusu uliopita,” alisema Waziri Mkuu wakati akiwahutubia wazazi, walimu na wanafunzi.  Mapema, akiwasilisha msaada huo, mwakilishi wa kampuni ya General Booksellers Ltd, Bw. Joachim Masaburi alisema wameamua kuchangia vitabu hivyo kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto lakini pia wanatambua juhudi za Serikali za kutoa elimu bora.  Akitoa mchanganuo wa vitabu hivyo, Bw. Masaburi alisema: “Kuna vitabu 600 kwa ajili ya shule ya awali ambavyo kati yake 300 ni vya ngazi ya chini (nursery) na vitabu vingine 300 ni vya ngazi ya juu (pre-school). Vyote ni vya hisabati, Kiingereza na sayansi”.  “Kwa shule ya msingi wao tunawapatia kivunge cha kufundishia mfumo wa mwili wa binadamu kama sehemu ya masomo ya sayansi, hiki kina thamani ya sh. 550,000/-,” alisema.  Pia kampuni hiyo ilitoa msaada wa vitabu vingine 295 vya Baiolojia, Fizikia, Uraia, Kiswahili kwa ajili ya shule ya sekondari ya Mizengo Pinda iliyoko kijijini hapo.  Hadi sasa majengo yaliyokamilika kwenye shule hiyo ni madarasa 14, jengo la utawala lenye ofisi za walimu na maktaba mbili (wanafunzi na walimu), jengo la TEHAMA la wanafunzi lenye darasa moja, ukumbi mdogo na ofisi za walimu na jengo moja la choo lenye matundu 48. Pia ujenzi wa nyumba sita za walimu uko kwenye hatua ya kuezeka. Nyumba hizo zinajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Ujenzi wa choo kingine chenye matundu 48 umeanza.  Waziri Mkuu aliwaomba wananchi wengine wamsaidie kutimiza ndoto yake kwani bado anakabiliwa na kazi ya kuweka umeme, maji, kujenga nyumba nane za walimu, bwalo na jiko, karakana nne za ufundi, ujenzi wa kituo cha walimu cha mafunzo ya muda mfupi na utunzaji taarifa (Resource Centre), viwanja vya michezo vya kisasa vinavyozingatia michezo yote, mfumo wa uvunaji maji ya mvua, mfumo wa maji safi na maji taka, nyumba mbili za walinzi na uzio wa shule.  Alitaja vitu vingine ambavyo bado vinahitaji kuchangiwa ni meza za walimu – za ofisini na darasani, viti vya walimu – vya ofisini na darasani, madawati ya shule ya msingi na ya awali, meza na viti vya maktaba zote mbili, meza na viti vya bwalo – shule ya msingi na shule ya awali.  IMETOLEWA NA

  OFISI YA WAZIRI MKUU,

  JUMATANO, MEI 27, 2015.

  0 0


  IMG_3895

  MBUNIFU mkongwe wa mavazi, Mama wa mitindo nchini, Asia Idarous Khamsin amepata pigo kufuatia kufiwa na Mama yake mkubwa, Aliyefahamika kwa jina la Fatma Juma, Msiba uliotokea Kisiwa Ndui, Unguja.

  Kwa mujibu wa taarifa za msiba huo ambao hata hivyo tayari mazishi yake yamefanyika siku ya Jumatatu ya Mei 25, Kisiwa Ndui, na leo Jumatano ya Mei 27 wanatarajia kufanya kisomo maalum.

  Ratiba ya Kisomo:
  Leo Jumatano ya Mei 27, saa 10, Alasiri wanatarajia kufanya kisomo maalum kwa wanawake wote nyumbani kwa marehemu, Kisiwa Ndui na kwa upande wa Wanaume wao wanatarajia kufanya kisomo, majira ya saa mbili usiku.

  Tunampa pole Mamaa wa Mitindo Asia Idarous Khamsin kwa kufiwa na Mama yake mkubwa na mlezi. 

  "Inna lillahi wa inna ilayhi rajiiun, mwenyezi mungu amlaze pema peponi".

  0 0


   Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Salum Mwalim akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika hivi karibuni mjini Magu, mkoani Mwanza, ikiwa ni sehemu ya mfululizo wa mikutano ya chama kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kujiandaa kupiga kura uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
  Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika hivi karibuni katika Uwanja wa Halmashauri, mjini Bariadi, mkoani Simiyu hivi karibuni alipokuwa mkoani humo kwa ajili yakuzindua mpango maalum uitwao 'Changia Chadema Kanda ya Serengeti ili Kushinda Uchaguzi 2015' unaolenga kukusanya fedha kampeni za wagombea wa ubunge na udiwani mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya, John Michael Haule, wakati Balozi huyo alipofika Osifini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kumuaga leo Mei 27 2015. Picha na OMR

  0 0

   
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Chama Cha Waalimu TANZANIA( CWT) uliofanyika katika hoteli ya Ngurdoto nje kidogo ya mji wa Arusha jana.Wakati wa mkutano huo wanachama wa CWT ulitarajia kuwachagua viongozi wapya wa chama Hicho.Akizungumza katika  mkutano huo Rais Kikwete ameahidi kutatua changamoto moto mbalimbali zinazowakabili waalimu nchini(picha na Freddy Maro).

  0 0  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  Telephone:255-22-2114512, 2116898
  Website : www.ikulu.go.tz              

  Fax: 255-22-2113425  PRESIDENT’S OFFICE,
        STATE HOUSE,
                1 BARACK OBAMA ROAD,  
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa masikitiko na huzuni nyingi taarifa ya kifo cha mwanasiasa mkongwe nchini na aliyepigania uhuru wa Tanganyika, Ndugu Samwel Ntambala Ruangisa, ambaye aliaga dunia mwanzoni mwa wiki hii nchini Marekani ambako alikuwa anatibiwa.

  Katika salamu za rambirambi ambazo amempelekea Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mheshimiwa John Mongella kuomboleza kifo cha Mzee Ruangisa, ambaye pia alikuwa bado diwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Rais Kikwete amesema:

  “Nimepokea taarifa za kifo cha Mzee Ruangisa kwa masikitiko na huzuni nyingi. Kwa zaidi ya nusu karne, Mzee Ruangisa amekuwa kiongozi wa kuigwa mfano katika nafasi zote ambazo zimepata kuzishikilia katika maisha yake kuanzia Ukuu wa Mkoa wa Ziwa Magharibi (sasa Kagera) na baadaye Mkoa wa Mara tu baada ya Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, Ubalozi, Uwaziri, Ubunge, Umeya na Udiwani. Katika kila nafasi aliyoishikilia, Mzee Ruangisa alionyesha uongozi wa kiwango cha juu. Kwa hakika, tumepoteza kisima cha uzoefu wa uongozi.”

  Rais Kikwete ameongeza katika salamu zake za rambirambi: “Mkuu wa Mkoa nakutumia salamu zangu za rambirambi kuomboleza msiba huu na kupitia kwako naomba uwape pole wana-Kagera wote kwa kuondokewa na mzee wao wa siku nyingi. 

  Aidha, naomba unifikishe pole zangu nyingi kwa wanafamilia wote ambao wamepoteza baba, babu na mhimili wa familia. Wajulishe kuwa niko nao katika kipindi hiki kigumu. Waambie naelewa machungu yao kwa sababu machungu yao ni machungu yangu. Vile vile, naungana nao katika kumwomba Mwenyeji Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi roho ya Marehemu Samwel Ntambala Ruangisa. Amina.”

  Imetolewa na;
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  IKULU,
  DAR ES SALAAM.

  27 Mei, 2015

  0 0


   On May 28th at 17:30 BST, as part of the Homestrings Webinars Investor Series, we’re pleased to invite you to the webinar on “Homestrings Product: Innovare Agriculture Leasing Bond”.
  The Innovare Agriculture Leasing Bond is designed to increase the availability of capital for African agriculture value chain companies to grow their businesses and increase food and feed production. It has been created to provide attractive, risk-mitigated market-rate returns which include a 50% credit guarantee by the African Guarantee Fund, who will be featured in the webinar.

  During this LIVE webinar, you will be able to find out more about the promoter behind this investment product - Innovare Advisors, who works with innovative companies that utilize “best practices” in the global alternative agribusiness sector.  Topics will include:
  1. How innovation and capital can address food security by improving agriculture
  2. value chain efficiency
  3. How interests in the agriculture value chain can be aligned so all parties benefit;
  4. Investors, SMEs, Small holders, consumers, equipment manufacturers and
  5. leasing companies
  6. Innovative risk-mitigation strategies to protect investors while providing attractive
  7. financial and social returns
  8. African Guarantee Fund tools, strategies and partners to facilitate capital flows  
  9. How Diaspora can get involved
  Webinar Panellists:
  1. Innovare Advisors: John Riggan, CEO; Mary Jane Potter, CIO; Roger Frank, CMO
  2. African Guarantee Fund, John Kimathi, Senior Business Development Officer, Eastern & Southern Africa
  Moderated by: Ruby Alcantara, Chief Marketing Officer, Homestrings

  Webinar Details:
  During the webinar, attendees will be able to ask questions to the panellists enabling a highly engaging and interactive webinar. African Guarantee Fund was officially launched on June 2nd, 2012, in Arusha, Tanzania, by Dr. Donald Kaberuka, the President of the African Development Bank (AfDB), which together with the governments of Denmark (through Danida) and Spain (through aecid), are the founding shareholders.

  Innovare is an alternative investment management company focused on food and agriculture. We facilitate the capital flow to small and medium enterprises (SMEs) involved in all aspects of food and fiber production and processing in emerging and frontier markets.

  To Register:
  The webinar is limited to Homestrings members only, but don’t worry if you’re not a member. Membership is FREE and will give you access to the catalogue of investments, advance and exclusive invites for upcoming events, as well as a community of like-minded professionals and investors interested in these dynamic markets. If you’re not a member you’ll be directed to the Homestrings.com registration page then will receive confirmation with access to attend the webinar.

  For more Info, click HERE

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha  Balozi Liberata Mulamula kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Balozi Mulamula anakuwa Katibu Mkuu wa kwanza mwanamke kuongoza Wizara hiyo na kabla ya uteuzi huo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani. Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei, 2015.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi  Mulamula  akisaini Hati ya Kiapo mara baada ya kumwapisha. 

  Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi Balozi Mulamula Vitendea Kazi mara baada ya kumwapisha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Balozi Hassan Simba Yahya  kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kabla ya uteuzi huo Balozi Yahya alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei, 2015.

   Mhe. Rais Kikwete akishuhudia Naibu Katibu Mkuu  mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi Yahya  akisaini Hati ya Kiapo mara baada ya kumwapisha. 
  Mhe. Rais Kikwete akimpongeza Balozi Yahya mara baada ya kumwapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha, Mhe. Hemed Iddi Mgaza kuwa Balozi  wa Tanzania nchini Saudi Arabia. Kabla ya uteuzi huo Balozi Mgaza alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu  na Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei, 2015.
  Rais  Kikwete akishuhudia Balozi  Mgaza  akisaini Hati ya Kiapo mara baada ya kumwapisha.
  Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi Balozi Mgaza Vitendea Kazi mara baada ya kumwapisha.
  Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mulamula, Balozi Yahya na Balozi Mgaza mara baada ya kuwaapisha katika nyadhifa zao mpya
  Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja  na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Mohamed Gharib Bilal (wa nne kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (wa tatu kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (wa tatu kutoka kulia), Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (wa pili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mulamula, Balozi Yahya na Balozi Mgaza muda mfupi baada ya kuapishwa.
  Mhe. Rais Kikwete akiwa katika Picha ya Pamoja na Balozi Mulamula, Balozi Yahya,  Balozi Mgaza na baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mabalozi wa Tanzania.
  Mhe. Rais Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi aliowaapisha pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Idara za Mambo ya Nje na Watumishi wa Wizara hiyo
  Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mulamula (kushoto) na mumewe, Bw. George Mulamula (kulia) Picha na Reginald Philip

  0 0

    Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (wa pilikulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi Juma Mwapachu (wapili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso (kulia) na Menejawa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi wakiwa wameshika bango kamaishara ya uzinduzi wa mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’, katika haflailiyofanyika jijini Dar es Salaam  jana.
    Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (wa pili kulia), akikabidhi zawadi ya pasi na meza yake kwa muuza mitumba RashidSeleman (wa pili kushoto), ambaye ni mmoja wa vijana waliowezeshwa na  mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’ katika hafla ya uzinduzi wa mpango  huo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji   wa Airtel Sunil Colaso, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi Juma  Mwapachu (wa tatu kushoto) na Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.
   Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (wa pili kulia), akikabidhi zawadi ya mashine ya kutengeneza juisi kwa Abdulkarim  Ramadhan (wa tatu kushoto), ambaye ni mmoja wa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’ katika hafla ya uzinduzi wa mpango huo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi Juma Mwapachu na Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.
   Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
   Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi
  akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa Airtel Fursa
  ‘Tunakuwezesha’, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
    Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi Juma Mwapachu akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Sunil Colaso akizungumza katika hafla ya
  uzinduzi wa mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

  Baadhi ya vijana waliohudhulia katika hafla ya kuzindua Program mpya iitwayo Airtel Fursa , wakisalimiana na Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi jana jijini Dar es Salaam.

  AIRTELTanzania imezindua programu mpya iitwayo Airtel Fursa itakayowawezesha vijana kiuchumi ikiwemo kuwapa mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kupata maendeleo zaidi katika shughuli zao.

  Akizungumza katika uzinduzi wa programu hiyo, Mgeni wa heshima na  mfanyabiashara mkubwa nchini Dokta Reginald Mengi aliipongeza Airtel kwa kubuni program hiyo itakayosaidia vijana nchini huku akitoa wito kwa vijana wote nchini kuikumbatia fursa hiyo ili kuweza kutimiza malengo yao.


  “Hii ni Fursa ambayo vijana wanatakiwa kuikumbatia kwa nguvu zote ili wale wote watakaofaidika waweze kuwashawishi wenzao pia katika miaka ijayo,” alisema”

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema vijana watanufaika kwa njia mbalimbali na wataweza kujiendeleza kiuchumi na kupunguza suala la ukosefu wa ajira.


  “Airtel FURSA itawawezesha vijana toka sehemu mbalimbali nchini, Fursa zitawafikia vijana wengi wenye kiu na ari ya kufanya ambacho wanakiamini na ambao wako tayari kukabili changamoto mbalimbali ili waweze kufikia malengo yao na kubadilisha hali yao kimaisha,” alisema Colaso.


  Alisema program hiyo inawalenga vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 ambao watapokea misaada ya vifaa au thamani ili kuweza kutimiza malengo yao.


  Mbali na kutoa vifaa hivyo, Bw, Colaso alisema zaidi ya vijana wapatao 1500 watapata mafunzo mbalimbali ya kibiashara kila mwaka kupitia program hiyo.


  “Watafundishwa kuhusu usimamizi bora wa fedha, namna ya kupata mikopo, namna ya kufugua akaunti benki na mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa biashara,” alisema Colaso.

  Alisema program hiyo itahusisha vijana kutoka Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya na Mtwara.Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Airtel Balozi Juma Mwapachu, aliwataka vijana kutumia program hiyo ya Airtel Fursa kujiendeleza. Huku akiwaomba watanzania kuwapendekeza vijana wote wanaoona wanafaa kufaidika kwa mradi huo kwa manufaa ya jamii zao.

  Ili kijana kushiriki au kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- JIna, Umri, aina ya biashara na eneo.

  Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com.  ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, aina ya biashara na sababu ya kuomba msaada kutoka Airtel.


  Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com.


  “Programu hii itanufaisha vijana ambao tayari wana miradi mbalimbali na sio ambao wanataka kuanzisha,” alisema.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Nkaya Bendera (kushoto) akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Ally Uredi vifaa tiba na dawa zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF) ambazo gharama zake ni shilingi milioni 5.5.
   Ofisa mawasiliano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) Luhende Singu akizungumza wakati wa zoezi la kuzindua mpango wa huduma za madaktari bingwa Mkoani Manyara, asubuhi ya leo.
   Meneja wa NHIF Mkoa wa Manyara, Innocent Mauki akiwakaribisha viongozi wa NHIF makao makuu na uongozi wa Mkoa wa Manyara, kwenye uzinduzi wa mpango wa huduma za madaktari bingwa Mkoani Manyara. 
  Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wakishuhudia Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Nkaya akizindua mpango wa huduma za madaktari bingwa mkoani humo, zilizowezeshwa na NHIF
   Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Nkaya Bendera akizungumza asubhi ya leo kwa kuwa mkoa huo kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) kwenye uzinduzi wa mpango wa huduma za madaktari bingwa mkoani Manyara uliowezeshwa na NHIF.
   Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara wakiwa kwenye hospitali ya rufaa ya Mkoa huo ambapo leo asubuhi Mkuu wa Mkoa huo Dk Joel Nkaya Bendera alizindua mpango wa huduma za madaktari bingwa uliondaliwa na NHIF.
  Bibi Cecilia Tluway wa Wilaya ya Babati akikabidhiwa msaada wa shilingi 10,000 na Ofisa mawasiliano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) Luhende Singu, za kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii nchini CHF wakati wa zoezi la kuzindua mpango wa huduma za madaktari bingwa Mkoani Manyara, asubuhi ya leo.

  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar Bi. Maryam Hamdani akifungua mafunzo ya siku mbili ya waandishi wa habari kuhusu Haki za binaadamu na sheria za waandishi wa Habari katika kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kiliopo Migombani.
  hg2
  Kamishna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mohd Khamis akiwasilisha mada ya Chimbuko, Historia na Maendeleo ya Haki za Binadamu Kimataifa, Kikanda na Tanzania katika mafunzo ya waandishi wa Habari yaliyofanyika Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Migombani.
  hg3
  Mwenyekiti wa mafunzo hayo Salma Saidi akitoa muongozi kwa washiriki wa mafunzo hayo.
  hg4
  Mwandishi Mkongwe wa habari Tanzania Salim Said Salim akiwasilisha mada ya Kanuni, Miiko na Maadili ya Waandishi wa Habari Kimataifa na kitaifa katika semina ya waandishi wa Habari iliyoandaliwa na Kituo cha Sheria Zanzibar.

  hg5
  Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo
  hg6
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Rafii Haji akiwasilisha mada juu ya Mapitio ya sheria za uandishi wa Habari Zanzibar.
  hg7
   Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo Bi. Maryam Hamdani (wa pili kulia) na washiriki wa mafunzo hayo. Picha Na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Balozi Seif kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein akiufunga Mkutano wa Nne wa siku Tatu wa Mabalozi wa Tanzania uliokuwa ukifanyika katika Hoteli ya Ramada Mjini Dar es Salaam.Baadhi ya Mabalozi wa Tanzania katika Mataifa mbali mbali Duniani walioshiriki Mkutano wao wakifuatilia Hotuba ya Ufungaji wa Mkutano huo iliyosomwa na Balozi Seif kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. ASli Mohammed Shein.Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Tanzania Nchi mbali mbali Duniani mara baada ya kufunga Mkutano wao wa Nne ulifanyika Ramada Hoteli Jijini Dar es Salaam. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mh. Bernard Membe, Katibu Mkuu Mpya wa Wizara hiyo Balozi Lebereta Mula mula na kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Mhadhi Juma Maalim. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Jamuhuri ya Watu wa China Balozi Abrahaman Nyimbo mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mabalozi wa Tanzania Mjini Dar es salaam. Picha na – OMPR – ZNZ. 
  ---
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein alisema Mabalozi wanayoiwakilisha Tanzania katika Mataifa tofauti Duniani wanapaswa kuitekeleza vilivyo Sera ya Mambo ya Nje inayolenga katika Diplomasia ya uchumi ambayo ndiyo muongozo wao katika utekelezaji wa jukumu lao la msingi.
  Alisema Sera hiyo ni vyema ikatumika vizuri wakati huu ambao Taifa la Tanzania linatekeleza Dira ya kuelekea uchumi wa Kati na kati ifikapo mwaka 2020 kwa upande wa Zanzibar na Mwaka 2025 kwa Tanzania Bara.
  Dr. Ali Mohammed Shein alisema hayo wakati akiufunga Mkutano wa Nne wa siku Tatu wa Mabalozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo katika Ukumbi wa Hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam.
  Alisema katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi ya utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje yenye kuweka msisitizo katika Diplomasia ya Uchumi Tanzania imepiga hatua kubwa vikiwemo Visiwa vya Zanzibar.
  Dr. Shein alifahamisha kwamba matunda ya Sera hii yanadhihirisha wazi ukuaji wa sekta ya Utalii, miradi mengine ya kiuchumi ikiwemo pia ile mikubwa inayotekelezwa na wahisani kwa upande wa Zanzibar.
  “ Mikakati mipya ya muda mfupi na mrefu mliowekeana katika Mkutano huu ni msingi mzuri kabisa kufuatana na mabadiliko ya uchumi yanayotokea Duniani na kufikia malengo ya Dira ya 2020 na 2025 “. Alisema Dr. Shein.
  “ Nina hakika kuwa katika Mkutano huu mmeweza kuziba nyufa zote zilizojitokeza katika utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 inayolenga katika Diplomasia ya Uchumi ambayo ndio muongozo wetu katika utekelezaji wake na ni jukumu letu la msingi “. Alisisitiza Dr. Shein.
  Rais wa Zanzibar alieleza kwamba licha ya mafanikio makubwa ya kiuchumi na maendeleo yanayoendelea kushuhudiwa kwa upande wa Zanzibar lakini bado iko haja kwa Mabalozi hao wa Tanzania kuongeza juhudi za kuitangaza Zanzibar katika Mataifa waliyopangiwa kutekeleza majukumu yao ya Kidiplomasia.
  Alisema mafanikio ya Zanzibar katika kukuza sekta ya Utalii , uwekezaji na utekelezaji wa mipango mengine ya maendeleo hutegemea sana juhudi za Ofisi za Kibalozi katika kuitangaza Zanzibar nchi za Nje.
  Dr. Shein alifahamisha kwamba baadhi ya wakati Serikali imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wawekezaji, watalii na wageni wanaofika Zanzibar juu ya ukosefu wa taarifa za kutosha kuhusu Zanzibar katika Ofisi za Kibalozi za Tanzania.
  Aliwakumbusha Mabalozi hao kwamba katika kutekeleza majukumu yao ni vyema kila wakati wakazingatia kuwa Ofisi zao zinaweka taarifa za kutosha juu ya sekta zote muhimu za kiuchumi na kijamii za pande zote mbili za Jamuhuri hasa zile fursa za uwekezaji vivutio vya utalii.
  “ Suala hili nimekuwa nikilikumbusha kila ninapopata fursa ya kuzungumza nanyi, hasa wakatia mbao Mabalozi huja kunitembelea na kuniaga kabla ya kuripoti katika vituo vyao vya kazi “. Alifafanua Dr. Shein.
  Alifahamisha kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kupokea mawazo ya Mabalozi hao ili kupata fursa nzuri ya nini Wanadipomasia hao wakitangaze kuhusu Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar alihimiza kwamba katika kipindi hichi ambapo Nchi mbali mbali Duniani zimekumbwa na misukosuko ya kutetereka kwa hali ya amani na utulivu Mbalozi hao wanapaswa kuzitangaza fursa ya kiuchumi zilizopo Nchini na kuzihusisha na hali ya amani na utulivu uliopo Nchini Tanzania.
  Alieleza kuwa amani na utulivu ni miongoni mwa vigezo muhimu vya awali vinavyozingatiwa na wawekezaji pamoja na wageni wanaotaka kwenda nje ya nchi zao kwa nia ya kuwekeza na kufanya biashara.
  Mapema Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mh. Bernard Membe alisema utekelezaji wa sera ya mambo ya nje inayolenga katika Diplomasia ya Uchumi umeleta faida kubwa katika uchumi wa Taifa ndani ya kipindi cha miaka kumi iliyopita.
  Waziri Membe alisema ipo miradi kadhaa ya kiuchumi iliyotokana na sera hiyo kufuatiwa kutanganzwa na Ofisi za Kibalozi za Tanzania akiitaja kuwa ni pamoja na misaada ya maendeleo iliyofadhiliwa na mpango wa Milenia wa Marekani MCC na mradi wa chuma wa Mchuchuma.
  Mh. Membe alisisitiza pia kuwa ipo miradi ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, Tanzania kusamehewa mikopo tofauti kutoka kwa baadhi ya wafadhili, mradi wa huduma za maji safi unafadhiiwa na Serikali ya Japan pamoja na mradi wa Kilimo kwa upande wa Visiwa vya Zanzibar.
  Alisisitiza kwamba Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya nje itahakikisha kwamba inaendelea kuchangia vikosi vya kulinda amani Barani Afrika.

   Akitoa shukrani kwa niaba ya washiriki wa Mkutano huo wa Nne wa Mabalozi wa Tanzania Nchi Mbali mbali Duniani Dini wa Mabalozi hao Balozi Kijazi alisema Maalozi hao wakirudi vituoni mwao watakuwa na kazi moja tu ya kutekeleza yale waliyoyajadili na kukuibaliana katika Mkutano huo.
  Balozi Kijazi alilihakikishia Taifa kwamba Mabalozi hao wana nia safi ya kutekeleza majukumu yao kwa ufasini uliotukuka, lakini lakuzingatia zaidi ni uwezeshwaji wao ili kutekeleza vyema kazi yao hiyo ya Kidiplomasia.
  Othman Khamis Ame


  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

  0 0

  MZEE SAMUEL NTAMBALA LUANGISA

  Familia ya Marehemu Mzee Luangisa na New York Tanzania Community, inawakaribisha kwenye MISA ya kumuaga Marehemu Mzee wetu, Baba yetu na Kiongozi wetu Mzee Samuel Ntambala Luangisa (83), kabla ya kwenda Bukoba kwa mazishi Siku Jumamosi MAY 30th, 2015
  kuanzia Saa: 1pm - 5pm

  Address: LEE'S Funeral Home L.L.C
  160 Fisher Avenue
  White Plains, NY 10606

  Baada ya Misa sote tutajumuika nyumbani kwa Wafia The Luangisa Residence: 

  374 Hawthorne Terrace, 
  Mt. Vernon, NY 10552

  Mpe taarifa mwenzako wote karibuni. 

  Kwa taarifa zaidi wasikiana na:

  1. Prof. K. Lwiza 631-273-3859
  2. Dr. Abas Byabusha 914-584-7502
  3. Shabani Mseba 347-712-8539
  4. Hajj Khamis 347-623-8965

  Ukitaka kutoa rambirambi yako unaweza kutumia number hizi hapa chini.
  Luangisa na Kwame Luangisa. Bank ni Bank of America. Account# 9504210977. Routing# 021000322. Swift code ni BOFAUS3N. 

  Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake la Bwana litukuzwe. Amen!

  0 0

  DSC_0099
  Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Dkt. John Ndunguru akisoma taarifa fupi ya hali ya Wakimbizi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe aliyeambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa mjini Kigoma.
  DSC_0113
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akizungumza kwenye mkutano wa kupokea taarifa fupi ya hali ya wakimbizi katika mji wa Kigoma na changamoto wanazokabiliana nazo mbele ya wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini.
  DSC_0128
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumzia jitihada zilizofanywa na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika lake la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengi katika kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatikana kwa haraka zaidi ili wakimbizi nao wafarijike kama binadamu wengine sambamba na sheria za Umoja wa Mataifa zinavyotaka. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na watatu kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole.
  DSC_0134
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea na mazungumzo na viongozi mbalimbali wa ulinzi na usalama wa mkoa wa Kigoma.
  DSC_0146
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole akizungumza katika mkutano huo ambapo ameipongeza serikali ya Tanzania kwa moyo wake wa upendo na kutenga maeneo maalum ya kuhifadhi Wakimbizi kutoka nchi za jirani.
  DSC_0163
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe katika picha ya pamoja ya viongozi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wa mkoa wa Kigoma sambamba wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yaliyopiga kambi mkoani Kigoma kuhudumia Wakimbizi.


  DSC_0009
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (kulia) akiwasili kwenye uwanja wa ndege Kigoma akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wa pili kulia) na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Dkt. John Ndunguru (wa pili kushoto) kwa ajili ya kutembelea na kuona changamoto katika maeneo maalum wanapohifadhiwa Wakimbizi. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Juma Abdulla Saadala.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

  Na Modewjiblog team, Kigoma
  Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe amesema Tanzania itatoa nafasi zaidi kuliko ya sasa ili kuweza kuwaweka wakimbizi wa Burundi wanaoingia nchini katika mazingira ya kuishi maisha ya kawaida.Kauli hiyo ameitoa ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma jana kabla ya kuelekea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu na kujionea hali ilivyo akiambatana na watendaji wa mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini.

  Alisema kama taifa wameona uwingi wa Wakimbizi na watatoa nafasi zaidi ili kuwezesha Wakimbizi hao kupata mahitaji yao ya msingi kwa mujibu wa taratibu za Umoja wa Mataifa kuhusu Wakimbizi. Alisema katika kufanikisha suala la kuhudumia Wakimbizi wanaomiminika kwa sasa serikali itashirikiana na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kuhakikisha mahitaji ya msingi kwa Wakimnbizi hao yanapatikana.

  “Wakimbizi wanahaki ya kulindwa na kuthaminiwa kama wananchi wa Tanzania, kwa hiyo serikali itatoa nafasi zaidi na tunashukuru msaada tunaopata kutoka kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa kukabiliana na tatizo hili …,” alisema.Naye Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez alisema kwamba Umoja wa Mataifa unatiwa shaka na hali ya kisiasa ilivyo nchini Burundi na kusema kuyumba kwa hali ya kisiasa kunaweza kuleta Wakimbizi wengi nchini.

  Alisema kwa sasa Umoja wa Mataifa unafanya kazi na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Umoja wa Afrika na wanachama wengine wa jumuiya za kimataifa kuhakikisha kwamba hali ya usalama inarejea nchini Burundi. Aidha aliipongeza Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia kutatuliwa kwa mgogoro wa Burundi.

  Rodriguez alisema Tanzania ni mfano wa kuigwa kwa namna inavyoshughulikia Wakimbizi na kusema Umoja wa Mataifa unaangalia hali inayojitokeza Burundi kwa makini ili kusaidia Tanzania isilemewe na Wakimbizi. Aidha alisema kwamba kitendo cha serikali ya Tanzania kutoa nafasi zaidi ya kuwezesha kusiwepo na msongamano wa Wakimbizi Nyarugusu kunaonesha ushirika wa kweli kati ya serikali ya Tanzania na jumuiya ya Kimataifa katika kushughulikia matatizo ya Wakimbizi.

  Alisema hata hivyo kuanzishwa kwa kambi hiyo mpya ni gharama kubwa na kuitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia kuanzishwa kwa kambi hiyo mpya. Aidha alisema kwamba Mashirika ya Umoja wa Mataifa yakifanyakazi kama shirika moja, chini ya uongozi wa Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia Wakimbizi duniani (UNHCR) wameitikia wanavyostahili pamoja na changamoto nyingi walizokumbana nazo.
  DSC_0014
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akisamiana na Waziri wa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma Kamishina mwandamizi, Ferdinand Mtui (kulia) pamoja na viongozi wengine wa usalama wa mkoa wa Kigoma mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Kigoma akiwa na mwenyeji wake Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Dkt. John Ndunguru (wa pili kushoto).
  Changamnoto hizo ni pamoja na uwingi wa Wakimbizi waliokuwa wakimiminika, umbali uliopo wa kambi ya Kagunga ambako walikuwa wanafikia huku waliowengi wakiwa wanawake na watoto.

  Alisema hata hivyo UNHCR walifanikiwa kuwasajili Wakimbizi hao na kuandaa mazingira ya ukazi wao katika kambi ya Nyarugusu. Aidha wamewezesha usafiri kwa Wakimbizi kutoka Kagunga hadi Kigoma. Pia alisema IOM walifungua njia kutoka Kagunga hadi eneo jirani ambako Wakimbizi walipakia katika mabasi na kufika katika vituo walivyotakiwa kuwepo.
  Pia UNICEF waliweza kusaidia maji na vifaa vya usafi kwa watoto na WFP wao walihakikisha chakula kinafikishwa hasa biskuti za kuongeza nguvu.

  Aidha WHO wao walikuwa wanaisaidia serikali katika kukabiliana na mlipuko wa Kipindupindu. Aidha UNFPA walishughulikia mahitaji ya wanawake hasa wale waliokuwa wajawazito. Mratibu huyo alisema kwamba hata hivyo mambo yote hayo yasingefanikiwa kama si kwa msaada wa serikali ya Tanzania na jumuiya ya kimataifa.

  Mratibu huyo alisema kuwa Mashriika ya Umoja wa Mataifa yameanza kupata fedha za kusaidia katika shughuli zao na kwamba kuna ahadi ya dola za Marekani milioni 12.
  Alisema kwamba Umoja wa Mataifa umeona kwamba kutitirika kwa Wakimbizi hao kumeleta hali ngumu kwa serikali ya Tanzania na wakazi wa Kigoma.Alisema wanatambua changamoto zinazoambatana na kuwa na kundi kubwa la Wakimbizi lakini wataendelea kuhitaji msaada wa serikali ya Tanzania na jumuiya ya kimataifa katika kipindi hiki kigumu.
  DSC_0016
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akiendelea kusamiana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Kigoma waliofika kumlaki katika uwanja wa ndege wa mjini Kigoma.
  DSC_0019
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma Kamishina mwandamizi, Ferdinand Mtui mara tu baada ya kuwasili akiwa amefuatana na Waziri Chikawe (hayupo pichani).
  DSC_0018
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (kulia) akifurahi jambo na Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner kwenye uwanja wa ndege mjini Kigoma mara tu baada ya kuwasili.
  DSC_0024
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Bw. Damien Thuriaux (kulia) mara tu baada ya kuwasili mjini Kigoma tayari kuelekea kambi ya Wakimbizi Nyarugusu.
  DSC_0027
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole akifafanua jambo kwa viongozi wenzake mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Kigoma. Wa pili kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Bw. Damien Thuriaux.
  DSC_0036
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) akiongozana na Mkuu wa Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Bw. Damien Thuriaux kuelekea chumba maalum cha mapumziko mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Kigoma.
  DSC_0049
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) akisaini kitabu cha wageni kwenye chumba maalum cha wageni mashuhuri katika uwanja wa ndege wa mjini Kigoma. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akimsikiliza Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (katikati) walipokuwa kwenye chumba cha mapumziko.
  DSC_0071
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma kabla ya kusomewa kwa taarifa fupi ya hali ya Wakimbizi mkoani Kigoma.

  0 0

  Kama utakuwa na kumbukubu nzuri kipindi cha nyuma kidogo ulikuwa ukiingia kwenye mtandao utakuta domain nyingi ziko kwa namna ya jinafulani.com alafu baada ya muda tukaanza kuona jinafulani.co.uk ila hapakuwa na jinafulani.co.tz. Hilo lime badilika na kwa takwimu za sasa kuna takribani domain 10,000 zinazoishia na .tz ambazo zimesajiliwa na tzNIC moja kwa moja au kupitia wakala wao. 

  Tanzania Network Information Centre (tzNIC) ni msajili wa domain zinazo ishia na .tz. Hivyo pale unapo taka kusajili domain ambayo inaishia na .tz hawa ndio wahusika wakuu. tzNIC wanasimamia mfumo ambao una onyesha barua pepe yani email na servers zote zinazo ishia na .tz na zilipo. Tanzania Network Information Centre nishirika lisilo la kutafuta faida (nonprofit) ambalo lilianzishwa na kusajiliwa mwaka 2006 kwaajili ya kusimamia na kutekeleza shuguli zote zinazo husiana na Tanzania country code Top Level Domain (.tz ccTLD). 

  tzNIC ni limited company (kwa dhamana) ambayo ina waanzilishi wawili ambao ni TCRA ambae ni mdhibiti mkuu wa maswala ya mitandao Tanzania na TISPA (Tanzania Internet Service Provider Association) ambae ni sehemu ya chama cha ISP (Internet Service Provers Association).

  Lengo la tzNIC

  Lengo kuu la tzNIC ni kukuza matumizi ya majina ya domain yanayo ishia na .tz pamoja na kulinda maslahi ya walio sajiliwa kwa kuwapa database ambayo ina ulinzi wa kutosha na unafuu. Kwa kufanya hivyo huwapa watumiaji fursa ya kuonekana dunia nzima, wana brand huduma yako na muonekano wa kitanzania, kuongeza ushindani wa biashara yako ndani na nje ya Tanzania, kuwezesha domain yako ulio sajili kupata watembeleaji wengi wa ndani ya nchi ya Tanzania, na kukuza utumiaji wa mtandao katika biashara.

  Wako wapi
  Head office za tzNIC (Tanzania Network Information Cetre) ziko Suite #4 Ground Floor, of LAPF Millenium Towers, at the New Bagamoyo Road, Dar es Salaam na namba zao za simu ni +255 22 2772659 fax: +255 22 2772660 na email address ni: info@tznic.or.tzhivyo pale unapo taka ku register domain yako au una tatizo linalo husiana na usajili wa domain usisite kuwasiliana nao au kuwatembelea.older | 1 | .... | 537 | 538 | (Page 539) | 540 | 541 | .... | 1896 | newer