Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

Rais Kikwete afungua Mkutano wa Mabalozi wa Tanzania

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa Mabalozi wa Tanzania unaofanyika katika hoteli ya Ramada jijini Dar es Salaam. Mkutano huo unajadili kwa kina namna ya kutekeleza dira mpya ya Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania ili kuendana na mabadiliko ya Uchumi na Diplomasia Duniani na kuleta tija nchini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wakati wa mkutano wa mabalozi wa Tanzania.Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Watatu Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje Mh.Bernard Membe,Wanne kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Liberata Mulamula.(picha na Freddy Maro)

AKI NA UKWA WA BONGO WAELEZEA MAFANIKIO YAO KWENYE TASNIA YA FILAMU

$
0
0
Kushoto ni Meya Shabani a.k.a Aki akiwa na Mwenzake Nicholaus Ngoda a.k.a Ukwa nje ya ofisi yao
 Aki na Ukwa wa Bongo wakipiga kazi ...
 Hapa wakionesha upande mwengine wa ofisi yao ya International Film Angels

Wasanii wa komedi maarufu kama Aki na Ukwa wa Bongo Muvi wameelezea mafaniko yao kwenye tasnia ya filamu za vichekesho nchini kwa mara ya kwanza tangu wajiingize kwenye filamu mwaka 2010.

Wakizungumza na Komedi Zone, Meya Shabani ambaye ni 'Aki' na Nicholaus Ngoda 'Ukwa' wamesema kuwa moja ya mafanikio waliyoyapata mpaka sasa ni kufanya kazi chini ya kampuni yao ya International Film Angels iliyopo Mwananyamala Visiwani jijini Dar na kuigiza muvi nzuri za vichekesho ambazo zina hadhi ya kipekee kimwonekano na hata simulizi zake tofauti na muvi nyingi za komedi ambazo hukosa ubora unaostahiki.

Baadhi ya muvi zao za komedi walizozifanya ni kama vile; Sometimes Yes Sometimes No, Zero Brain, Lost Sons, Crazy in Hospital, Ayubu wa Leo na Pastor Miyamba's Trial huku wakisema kuwa kuna utitiri wa muvi kali zaidi zipo katika matengenezo.

Mbali na muvi hizo wasanii hao wa Komedi waliongeza kuwa kupitia sanaa wameweza kujiendeleza kimasomo katika kozi za kuongoza filamu, kuedit na kuigiza huku muvi zao zikiwatambulisha vyema kiasi cha kufahamika na watu wengi na kupata dili mbalimbali za kuelimisha jamii kupitia kuigiza na kuimba.

"Kwa sasa tunajiita kama 'Edutainmenter' tukiwa na maana ya kuwa ni waburudishaji na waelimishaji kutokana na uwezo wetu wa kuimba na kuigiza hivyo hayo yote kwetu ni mafanikio japo malengo yetu bado ni kufika mbali zaidi," walisema mastaa hao.

Pia kupata taarifa zaidi za wasanii wa Komedi Tanzania  tembelea mtandao wao wa www.komedizonetz.blogspot.com

TANZIA

$
0
0
Familia ya Mchungaji Fanuel Solomon wa Mruma Ugweno – Kilimanjaro wanasikitika kutangaza kifo cha Mama yao mpendwa, Mama Salome Fanuel Solomon kilichotokea Ugweno siku ya Ijumaa tarehe 22/05/2015. Mazishi yatafanyika kijijini Mruma, Ugweno siku ya Ijumaa 29/05/2015.Taratibu za mazishi zinafanyika kwa mtoto wa marehemu Mbazi Fanuel Solomon Kunduchi Beach, Dar es salaam. 

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA – JINA LAKE LIHIMIDIWE  

katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa Elisha Mwampashi awataka vijana kujituma kufanya kazi na kuacha kukaa vijiweni

$
0
0
 katibu  wa  UVCCM mkoa  wa  Iringa Elisha Mwampashi wa  pili  kulia akiwa na katibu  mkuu  wa UVCCM Taifa Bw  Sixtus Mapunda

 na fredy mgunda,iringa


Akizungumza na mtandao huu katibu wa uvccm mkoa wa iringa ELISHA MWAMPASHE alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wakibweteka kwa kutojituma kufanya kazi na kuendelea kuilaumu serikali.

“Eti asubuhi unawakuta vijana wamekaa kwenye vijiwe wakizungumza siasa na kucheza mabao wakati hawajui mchana watakula wapi na jioni watarudi na nini nyumbani”alisema  ELISHA MWAMPASHE

ELISHA MWAMPASHE ameendelea kuwaomba vijana wengi wenye fursa ya kurudi au kuingia shuleni upya warudi kwa kuwa dunia ya sasa inataka wasomi wengi kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na sayansi na teknolojia na ndio sababu inayopelekea hata watu wazima kurudi shuleni.

“Vijana mnatakiwakujifunza kutoka kwa watu wazima ambavyo wamekuwa wakijituma kufanya kazi kwa bidii na kujituma ilimradi kuwatengenezea watoto maisha mazuri pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla”alisema  ELISHA MWAMPASHE

Lakini ELISHA MWAMPASHE amewataka wakinamama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.

ELISHA MWAMPASHE  ameeleza kuwa wanawake waondoe hofu ya kugombea hasa kukiwa na ushindani wa wagombea wanaume kwa kuogopa kuchafuliwa kwa mambo yasiyokuwepo.

Ameendelea kusema kuwa wananchi wasishawishiwe na propaganda za wanasiasa na badala yake wachague viongozi bora wenye uwezo wa kuongoza kutoka katika chama chochote.

Aidha ameongeza kuwa viongozi wawe na sera za kutekelezeka ili kuwatendea haki wapiga kura wao hali itakayowafanya waaminike katika jamii.

Mbali na hayo ELISHA MWAMPASHE amewakumbusha vijana kutokubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa katika kuleta vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na badala yake wachague kiongozi mwenye weredi na sifa za kuwa kiongozi kutokana na sera za chama chake.

Ameendelea kusema kuwa vijana wajitokeze kwa wingi katika kupiga kura ndiyo katika katiba iliyopendekezwa ili kuweza kufanya uchaguzi ulio wa haki na amani pia kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura pamoja na kupiga kura.

Aidha ELISHA MWAMPASHE amewataka vijana wa Manispaa ya Iringa, wametakiwa kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali na kutumia fursa zilizopo kwenye maeneo yao ili waweze kujiajiri na hivyo kujikwamua na hali ngumu ya maisha.



“Tukiungana pamoja ni rahisi kufanikiwa kiuchumi, hakuna njia njia nyingine kwa sababu dhamana yetu vijana ni umoja tu, jiungeni kwenye vikundi vya ujasiriamali,”alisema ELISHA MWAMPASHE



Alisema maeneo mengi ambayo vijana wameungana wameweza kukopeshwa, na wanaendesha shughuli zao za kiuchumi bila wasi wasi, jambo hilo linawezekana.
 


Alisema mpaka sasa wanayo zaidi ya Sh Milioni 10, ambazo wamekuwa wakikopeshana kwa riba naafuu. Alifafanua kuwa mara nyingi vijana wa stendi wamekuwa wakiachwa nyuma kwenye shughuli za kimaendeleo jambo ambalo, limewafanya waungane.

Wiki ya Ukombozi wa Afrika na Uzinduzi Mradi Uhifadhi Urithi Nyaraka Tanzania

$
0
0
Profesa Issa Shivji akichokoza mada katika mjadala wa Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Profesa Issa Shivji akichokoza mada katika mjadala wa Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Silima akisoma hotuba ya uzinduzi akimuwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe kwenye Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Silima akisoma hotuba ya uzinduzi akimuwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe kwenye Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.Ofisa Mkuu na Mwakilishi Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania, Mzulmira Rodrigues akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Ofisa Mkuu na Mwakilishi Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania, Mzulmira Rodrigues akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Mkinga akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Mkinga akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Silima akisoma hotuba ya uzinduzi akimuwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe kwenye Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Profesa Audax Mabulla akisoma hotuba yake na kuwakaribisha wageni kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana.Meza kuu katika uzinduzi wa Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa imesimama kuimba wimbo wa taifa kabla ya hafla hiyo kuanza. Meza kuu katika uzinduzi wa Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa imesimama kuimba wimbo wa taifa kabla ya hafla hiyo kuanza.Baadhi ya mabalozi na viongozi wa taasisi anuai waandamizi wakishiriki katika mjadala wa Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Mijadala hiyo imeanza tarehe 25 na inatarajia kumalizika tarehe 29 Mai, 2015. Baadhi ya mabalozi na viongozi wa taasisi anuai waandamizi wakishiriki katika mjadala wa Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Mijadala hiyo imeanza tarehe 25 na inatarajia kumalizika tarehe 29 Mai, 2015.Profesa Issa Shivji akichokoza mada katika mjadala wa Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Profesa Issa Shivji akiwasilisha mada yake katika mjadala wa Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.Meza kuu ya wawasilishaji mada na mwenyekiti wa mjadala katika Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Meza kuu ya wawasilishaji mada na mwenyekiti wa mjadala katika Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es SalaamBaadhi ya washiriki wa mijadala ya Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada mbalimbali zinazowa wasilishwa kwenye mjadala wa Wiki ya Ukombozi wa Afrika. Mijadala hiyo imeanza tarehe 25 na inatarajia kumalizika tarehe 29 Mai, 2015. Baadhi ya washiriki wa mijadala ya Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada mbalimbali zinazowa wasilishwa kwenye mjadala wa Wiki ya Ukombozi wa Afrika. Mijadala hiyo imeanza tarehe 25 na inatarajia kumalizika tarehe 29 Mai, 2015.Baadhi ya mabalozi wakishiriki katika mjadala wa Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Mijadala hiyo imeanza tarehe 25 na inatarajia kumalizika tarehe 29 Mai, 2015. Baadhi ya mabalozi wakishiriki katika mjadala wa Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Mijadala hiyo imeanza tarehe 25 na inatarajia kumalizika tarehe 29 Mai, 2015.Meza kuu ya wawasilishaji mada na mwenyekiti wa mjadala katika Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Meza kuu ya wawasilishaji mada na mwenyekiti wa mjadala katika Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam..Baadhi ya washiriki wa mijadala ya Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada mbalimbali zinazowa wasilishwa kwenye mjadala wa Wiki ya Ukombozi wa Afrika. Mijadala hiyo imeanza tarehe 25 na inatarajia kumalizika tarehe 29 Mai, 2015. Baadhi ya washiriki wa mijadala ya Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada mbalimbali zinazowa wasilishwa kwenye mjadala wa Wiki ya Ukombozi wa Afrika. Mijadala hiyo imeanza tarehe 25 na inatarajia kumalizika tarehe 29 Mai, 2015..Baadhi ya washiriki wa mijadala ya Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam wakiuliza maswali kwa wawasilishaji mada. Mijadala hiyo imeanza tarehe 25 na inatarajia kumalizika tarehe 29 Mai, 2015. Baadhi ya washiriki wa mijadala ya Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam wakiuliza maswali kwa wawasilishaji mada. Mijadala hiyo imeanza tarehe 25 na inatarajia kumalizika tarehe 29 Mai, 2015..Baadhi ya washiriki wa mijadala ya Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam wakiuliza maswali kwa wawasilishaji mada. Mijadala hiyo imeanza tarehe 25 na inatarajia kumalizika tarehe 29 Mai, 2015. Baadhi ya washiriki wa mijadala ya Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam wakiuliza maswali kwa wawasilishaji mada. Mijadala hiyo imeanza tarehe 25 na inatarajia kumalizika tarehe 29 Mai, 2015..Baadhi ya washiriki wa mijadala ya Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam wakiuliza maswali kwa wawasilishaji mada. Mijadala hiyo imeanza tarehe 25 na inatarajia kumalizika tarehe 29 Mai, 2015. Baadhi ya washiriki wa mijadala ya Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam wakiuliza maswali kwa wawasilishaji mada. Mijadala hiyo imeanza tarehe 25 na inatarajia kumalizika tarehe 29 Mai, 2015..Baadhi ya washiriki wa mijadala ya Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada mbalimbali zinazowa wasilishwa kwenye mjadala wa Wiki ya Ukombozi wa Afrika. Mijadala hiyo imeanza tarehe 25 na inatarajia kumalizika tarehe 29 Mai, 2015. Baadhi ya washiriki wa mijadala ya Wiki ya Ukombozi wa Afrika inayofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada mbalimbali zinazowa wasilishwa kwenye mjadala wa Wiki ya Ukombozi wa Afrika. Mijadala hiyo imeanza tarehe 25 na inatarajia kumalizika tarehe 29 Mai, 2015.Profesa Issa Shivji akichokoza mada katika mjadala wa Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Profesa Issa Shivji akichokoza mada katika mjadala wa Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Afrika inayofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

KIKAO CHA BARAZA LA WAWAKILISHI CHAFANYIKA CHUKWANI NJE KIDOGO WA MJI WA ZANZIBAR

$
0
0
index11
Wizara ya Afya  imesema  Wagojwa wa Ukoma hawatengwi na Familia zao kasababu Dawa wanazotumia zinauwezo mkubwa za kutibu na kuuwa vimelea kwa wingi na kwa muda na hatimae kupungua maambukizi.
Akijibu swali la muwakilishi  Mohammed Haji Khalid ( Jimbo la mtambile )katika kikao cha Baraza la Wawakilishi Chukwani  nje kidogo wa Mji wa Zanzibar Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe Mahmoud Thabit Kombo .
Alisema kuwa hapo zamani Watu waligunduliwa na maradhi ya Ukoma walikuwa wakipelekwa katika Kambi maalum kwa ajili ya kupatiwa matibabu, Kambi hizo kwa Unguja walipelekwa Welezo na Pemba Makondeni.
Aidha alisema kwa zamani walipokuwa wakitegwa walikuwa wanatumia Dawa kwa muda usiopunguwa miaka mitano au zaidi ya hali ya uponeshaji ulikuwa mdogo. Alisema kuwa baada ya hapo palitumika Dawa mseto aina ya (MDT) zilitumika ambazo zinauwezo wa kukatisha maambukizi kwa muda mfupi ;Sambamba na hayo Naibu Waziri huyo ameishauri Jamii kutowatenga au kuwanyanyapaa Wagojwa wa maradhi ya Ukoma au wale wenye ulemavu uliotokana na Ugojwa huo.
Hata hivyo amewataka Baadhi ya Watu  kuwaelimisha  wale wenye dalili kujitokeza katika Vituo vya Afya ili watibiwe mapema na kuepuka  Ulemavu utokanao na Ugonjwa huo.
                   IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

WORLD LUNG FOUNDATION YAZINDUA KAMPENI MPYA YA KUHAMASISHA MATUMIZI YA UZAZI WA MPANGO

$
0
0
 
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dk.Leonard Subi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kuhamasisha faida na matumizi ya uzazi wa mpango  jijini Dar es Salaam jana, mpango utakaotekelezwa mkoani Kigoma chini ya Shirika la World Lung Foundation (WLF).

 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Cosmas  Swai, akizindua kampeni mpya ya kuhamasisha Faida na Matumizi ya Uzazi wa Mpango jijini Dar es Salaam jana, kampeni itakayotekelezwa mkoani Kigoma. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la, World Lung Foundation (WLF), Nduke Mwakatundu (mwenye tai) na  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dk.Leonard Subi (watatu kulia) na baadhi ya wafanyakazi wa (WLF).

  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la, World Lung Foundation (WLF), Nduke Mwakatundu, akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kuhamasisha faida na matumizi ya uzazi wa mpango  jijini Dar es Salaam jana, mpango utakaotekelezwa mkoani Kigoma. Kushoto ni Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya, Dk.Cosmas Swai na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dk.Leonard Subi.

TAMASHA LA KWANZA LA STARA KUZINDULIWA JIJINI DAR

$
0
0
Pazia la Tamasha la kwanza la Mavazi ya Heshima STARA limezinduliwa hivi "Stara Street Fashion"

Tamasha hili la aina yake linatazamiwa kufanyika tarehe  13th June 2015 katika ukumbi wa City Garden, kuanzia saa moja usiku hadi saa nne usiku kwa kiingilio cha shilling elfu 20 tu.

Pazia  la Tamasha hili litafunguliwa wiki moja kabla ya Tamasha kwa Exhibition ya bidhaa ya vitu mbalimbali... vitakavyouzwa kama vile Mabaibui, Udi Hena na vitu vingine kuanzia saa mbii asubuhi hadi saa 1usiku na hakuta kuwa na kiingilio, ni Buree

Tamasha hilo ambalo litafanyika kwa mara ya kwanza katika historia linatarajiwa kupambwa na Mavazi ya STARA. pamoja na mada mbalimbali kuhusu Nafasi ya Mwanamke katika Ndoa, Ujasriamali, Utunzaji wa Fedha na Mazungumzo kuhusu Mavazi ya Heshima sehemu za kazi. 

Akizungumzia kuhusu tamasha hilo Mratibu wa tamasha Latifah Makau Shekhoza alisema Wahudhuriaji watatakiwa kuwa wamejistiri na watoto wataruhusiwa.

Latifah Alisema ingawa Fashion show itahudhuriwa na wnawake pekee, exhibition itakuwa wazi wa watu wote.

Aliwataja wadhamini wa Tamasha hilo kuwa ni I-view Studio, Vayle Springs, AA Shekhozah co. Ltd, City Garden, Event Lights, Sofia Production, Gs1, Tanzania Women Bank, Clouds FM, Rehema Samo  na wengine.


Memorial Day 2015: Taswira mbalimbali za Mamia ya wananchi walivyohudhuria gwaride kitaifa kwaajili ya mashujaa wa Marekan

$
0
0
Joe Mantegna na Gary Sinise  kwenye gari la Pili kushoto wakiwa katika ufunguzi wa Sherehe za National Memorial Day Parade Siku ya Jumatatu May 25, 2015 Jijini Washington DC. (Picha zote na Swahilivilla.Blog)
Kushoto: Joe Mantegna akiwa katika mwendo wa National Memorial Day Parade Siku ya Jumatatu May 25, 2015 katika barabara ya Pennsylvania Avenue Jijini Washington DC
 Mmoja katika ya wageni rasmi katika Parade 2015 Chef Robert Irvine pia alikuepo katika National Memorial Day Parade Siku ya Jumatatu May 25, 2015 katika barabara ya Pennsylvania Avenue Jijini Washington D.C 
Cheif wa Swahilivilla Abou Shatry  Swahilivilla akisalimiana  na kamanda wa Naval Wilaya Washington DC,  Adm. Markham K. Rich, baada ya  gwaride la kitaifa kwaajili kuwapongeza mashujaa wa Marekani 
 Cheif wa Swahilivilla Abou Shatry alipoungana na Mamia ya wananchi waliokusanyika katika jengo la National Archives North Side, Washington, D.C. kuangalia gwaride la kitaifa kwaajili ya mashujaa wa Marekani,  Siku ya Jumatatu May 25, 2015 katika barabara ya Pennsylvania Avenue Jijini Washington D.C  

Mami ya wananchi waliokusanyika kuangalia National Parade honors American heroes. katika jengo la National Archives North Side, liliopo barabara Pennsylvania Avenue Jijini Washington DC 

Baadhi ya wananchi kutoka sehemu mbalimbali wakusanyika kuangalia  gwaride la kitaifa kwaajili ya mashujaa wa Marekan     Parade  katika jengo la National Archives North Side, liliopo barabara Pennsylvania Avenue Jijini Washington DC

Cheif wa Swahilivilla Blog Abou Shatry akionyesha jambo katika   gwaride la kitaifa lilifanyika, Siku ya Jumapili Mei 26 katika barabara barabara Pennsylvania Avenue Jijini Washington DC 

Ufunguzi wa Gwaride yakiandaliwa huku mamia ya wanachi waliotoka majimbo tafauti wakiwa wamebeba bendera za U.S.A kwaajili ya kutoa heshima kwa mashujaa wa Marekan.

Kina mama wakiwa wamevalia mashati ya bendera ya Marekan yao ili kuja kuona gwaride kitaifa kwaajili ya mashujaa wao
    

Mpangilio wa heshima wa Polisi Pikipiki waliojipanga kuaza ufunguzi rasmi wa gwaride la kitaifa kwaajili ya mashujaa wa Marekan.           

Polisi Pikipiki waliojipanga kuaza ufunguzi rasmi wa gwaride la kitaifa kwaajili ya mashujaa wa Marekan. Kwapicha zaidi BOFYA HAPA 
           

Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

SERIKALI YAMKARIBISHA MWAKILISHI MKAZI MPYA WA JICA NCHINI

$
0
0
 Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA nchini aliyemaliza muda wake Bw. Tomonari Shinya (kushoto) na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi mpya wa JICA nchini Bw. Takizawa Koichi (kulia) wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumuaga  Bw. Tomonari Shinya iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo .
 Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi mpya wa JICA nchini Bw. Takizawa Koichi (kulia) na aliyemaliza muda wake Bw. Tomonari Shinya (wa pili kutoka kulia) katika hafla fupi ya kumuaga Bw. Shinya iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.Wengine ni Afisa Tawala Msaidizi wa JICA Bw. Nasibu Hamisi (wa tatu kutoka kulia) na Afisa Tawala  wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bi. Mwanamridu Jumaa (wa nne kutoka kulia).
 Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) akisalimiana na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi mpya wa JICA nchini Bw. Takizawa Koichi (kushoto) alipoitembelea Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.
 Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) akipeana kadi za mawasiliano na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA nchini aliyemaliza muda wake Bw. Tomonari Shinya (kushoto) wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo. Katikati ni Mwakilishi Mkazi Mwandamizi mpya wa JICA nchini Bw. Takizawa Koichi akishuhudia.
Kaimu katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akimkabidhi zawadi Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA nchini aliyemaliza muda wake Bw. Tomonari Shinya (kulia) katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.

MOAT YAUPINGA MSWADA WA SHERIA YA VYOMBO VYA HABARI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mswada wa sheria ya vyombo vya habari ambao ulitaka kuwasilishwa bungeni kwa dharula. Kulia ni Mwanasheria, Godfrey Mpandikizi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Sahara Comminication, Samuel Nyalla (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Saed Kubenea kutoka Mwanahalisi Publishers na Mwanasheria, Godfrey Mpandikizi.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (kushoto), akisalimiana kwa kumbatiana na Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Azizi ambaye pia ni mmoja wa wamiliki wa vyombo vya habari.
 Wadau na wamiliki wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wanahabari na wadau wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo.
wadau wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo.



Na Dotto Mwaibale
WAMILIKI wa Vyombo vya habari nchini (MOAT) wameitaka serikali kutosaini muswada wa vyombo vya habari kutokana na kutokuwa wa haki na kwamba unavibana vyombo vya habari.

Pia wamiliki hao wamesema kama serikali inataka kuupitisha isubiri Rais ajaye ndiyo aupitishe wakati huohuo wameunda kamati maalumu itakayoenda Mjini Dodoma kuuzuia usipitishwe wala kujadiliwa bungeni.

Akizungumza Dar es Salaam leo mchana Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Regnald Mengi  alisema anashangazwa sana na wanasisa kusahau walipotoka kutokana na kusapoti muswada huo kupitishwa.

Alisema serikali imeamua kufanya hivyo kutokana na kusahau waliowasababishia kupata madaraka kutokana na shida yao kuisha hivyo vyomba vya habari vimejifunza.

"Tumejifunza kuwa sisi ni8 watu wa kutumika  wanapotaka kututumia hivyo wanataka kutumaliza na muswada huu hivyo sioni kama wana nia njema na sisi, "Alisema Mengi.

Aliongeza nia ya kupitishwa kwa muswada huo so njema na kwamba haki ya kupata habari sio tuu haki ya msingio bali ni ya kikatiba hivyo serikali isije ikajihusiasha na kuvunja katiba ya nchi bali inatakiwa kuonesha mfano bora.

Akizungumzia kuhusu Demokrasia alisema mtu hawezi kufanya vitu visivyozingatia demokrasia ili kudhibiti demokrasia au kuhakikisha unapata demokrasia kwa kutumia njia za kidemopkrasia bali anapaswa kutumia amani.

"Huwezio kuheshimu sheria kwa kutumia nguvu, hivyo muswada ukiwa na sheria onevu na isiyokubalika au kukiuka katiba ya nchi lazima hali itakuwa mbaya nchini,"

Kwa upande wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu alisema watanzania tunaelekea kwenye mchakato huo lakini hatuwezi kuwa na uchaguzi huru ikiwa vyombo vya habari havina uhuru wa kupokea na kuandika habari ili watanzania waweze kuelewa hivyo serikali inatakiwa kujadili kwa makini ili kunusuru machafuko yanayoweza kujitokeza.

"Hatuwezi kuficha vitu wakati mambo yanatakiwa yawe wazi, na kama tungekuwa tunataka uwazi tusingeruhusu vyombo vya habari kuwa wazi, hivyo muswada huo utatupa matatizo kwenye uchaguzi na hauwezi kluwa huru pasipo wananchi kujua nuini kinaendelea kupitia vyombo hivyo,"alisema Mengi. 

Hata hivyo mengi aliongeza kuwa hakuna amani endelevu bila kuwepo uhuru na haki kwa kuwa ni rasilimali kubwa ya taifa na kwamba si ya mtu mmoja, kikundi wala chama bali ni yetu sote hivyo serikali ikijaribu kuichezea itakuwa inacjhezea wananchi wa tanzania.

Kwa upande wake Wakili wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Godfrey Mpandikizi  akizungumzia changamoto zilizopo kwenye muswada huo,alisema vitu vilivyopo kwenye muswada huo vinakinzana na katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania hivyo aliwataka wahariri kwenda Dodoma kuuzuia.

Alisema muswada huo pia unazuia jamii kujua mambo yanayoendelea hivyo itasababisha hali ya nchi kuwa mbaya kwa siku zijazo kurtokana na kuwa na mapungufu zaidi ya 10 katika kila kifungu pamoja na tafsiri zaidi ya 20.

"Sheria hiyo ni chafu, na hairuhusiwi kwenda bungeni hivyo isubiri Rais ajaye na katiba mpya ndiyo ujadiliwe ili uwe na haki hivyo wamiliki nendeni Dodoma mkauzuie usijadiliwe na wabunge waka kupitishwa,"alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mwananchi, Francis Nanai aliwataka wamiliki hao kuonana na wanasheria, wabunge na mashirika mengine kwenda mahakani kupinga sheria hiyo chafu.

Abdala Majura alisema anaungana na vyombo mablimbali vya habari kuukataa muswada huo usijadiliwe bungeni na kwamba utasababisha kufa kwa taaluma za uandishi wa habari. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com).


BENKI YA CRDB YAKABIDHI HUNDI YA SH. MILIONI 20 KWA MEYA WA KINONDONI

$
0
0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi hundi ya sh. milioni 20 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda zilizotolewa na benki hiyo baada ya  meya huyo kupata tuzo ya Meya Bora Afrika iliyotolewa na Rais Jose Eduardo do Santos wa Angola. Hafla hiyo ilifanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Meya, Songoro Mnyonge.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi hundi ya sh. milioni 20 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda zilizotolewa na benki hiyo baada ya  meya huyo kupata tuzo ya Meya Bora Afrika iliyotolewa na Rais Jose Eduardo do Santos wa Angola. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
 Meya wa Kinondoni Yusuf Mwenda akitoa shukrani zake kwa uongozi wa Benki ya CRDB kwa kutambua juhudi wanazofanya katika utendaji kazi na masuala ya usafi na ukusanyaji wa mapato.
 Meya wa Kinondoni Yusuf Mwenda akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
 Picha ya pamoja.
 Dk. Charles Kimei akimpongeza Meya wa Kinondoni kwa tuzo aliyopata.
 Picha ya pamoja.

 Dk. Charles Kimei akiambatana na Meya wa Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto) na Naibu Meya, Songoro Mnyonge.
 Dk. Kimei akibadilishana mawazo na Meya wa Kinondoni.
Meya wa Kinondoni, Yusuf Mwenda akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisaini kitabu cha wageni alipowasili ofisini kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda, (katikati). Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa. 
  Meya wa Manispaaya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei muda mufupi kabla hajakabidhi hundi ya sh. milioni 20 baada ya meya huyo kupata tuzo ya Meya Bora Afrika iliyotolewa na Rais Jose Eduardo do Santos wa Angola.

   Meya wa Manispaaya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto) akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.

 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.
Meya wa Kinondoni, Yusuf Mwenda akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mussa Natty. 
 Dk. Charles Kimei akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi.

RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGUA RASMI MKUTANO WA NNE WA MABALOZI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mhe. Rais Kikwete akizungumza huku Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakimsikiliza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano wa Nne wa Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi. Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam ukiwa umebeba Kaulimbiu isemayo "Diplomasia ya Tanzania Kuelekea Dira ya Taifa 2025".Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ya Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani)Wajumbe wengine wakiwemo Wakuu wa Vitengo katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifutilia hotuba ya Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani.)
Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine aliwakumbusha Mabalozi  kuwathamini Watanzania waishio nje ya nchi, kuendelea kusaidia upatikanaji wa misaada ya maendeleo, masoko ya bidhaa za Tanzania, wawekezaji na teknolojia bora. 
Mhe. Rais Kikwete akiteta jambo na Waziri Membe kabla ya kuwahutubia MabaloziWaziri Membe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu, Balozi Mulamula huku Balozi Sefue akisikiliza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Sekretarieti ya Mkutano wa Nne wa Mabalozi Mhe. Rais Kikwete akiongozana na Balozi Mulamula kuelekea eneo la kupata picha ya pamoja.
Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja na Waziri Membe, Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Balozi Sefue,  Balozi Mulamula, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Simba Yahya, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Mhe. Mussa  Zungu, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wote.
Mhe. Rais Kikwete na Viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi Wanawake.
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MANJANO FOUNDATION YAKAMILIKA

$
0
0
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama  Shekha Nasser Katikati  akiongea na Vyombo vya Habari leo wakati akelezea Mandalizi ya Uzinduzi wa Manjano Foundation Ambao ni Mpango unaolenga kuwawezesha Kutoa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa Wasichana wa Kitanzania.Mpango Uzinduzi huu utafanyika tarehe 31 Mei 2015 kuanzia saa 6 mchana kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee VIP Hall. Utatoa fursa kwa kuendeleza mtandao wa kibiashara kwa kina mama na pia mada mbali mbali ya jinsi ya kujikwamua kimaisha itatolewa. Bila ya kusahau mafunzo ya jinsi ya kutumia vipodozi..Mgeni Rasmi anategemewa Kuwa Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda
 Meneja Mradi wa Manjano Foundation Mama Gugu Ndolvu Akieleza jambo leo wakati wakiongea na wanahabari kuhusu Mradi huo ambao ni Mkombozi kwa wakinamama wasio na Ajira Akiwa samabamba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama  Shekha Nasser  Pamoja na  Aunty Sadaka Gandi
 Aunty Sadaka Gandi akiwa ni dada mkuu wa Atakayewashauri wasichana watakaopata mafunzo ya ujasiriamali kupitia Manjano Foundation. 

Wasichana waliochaguliwa kunufaika na Mpango hup wakiwa Katika Picha ya Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama  Shekha Nasser  

Shear Illusions inasherehekea mwongo mmoja wa urembo nchini Tanzania kwa kuzindua vipodozi vyake ijulikanayo kama LuvTouch Manjano!

Uzinduzi huu utafanyika tarehe 31 Mei 2015 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee VIP Hall. Shamrashamra hizi pia itatoa fursa kwa kuendeleza mtandao wa kibiashara kwa kina mama na pia mada mbali mbali ya jinsi ya kujikwamua kimaisha itatolewa. Bila ya kusahau mafunzo ya jinsi ya kutumia vipodozi.



Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda na mtoa mada mkuu atakuwa ni Balozi Mwanaidi Majaar.

Shear Illusions, imeweza kutambulisha urembo na muonekano wa mwanamke wa kitanzania kwa Zaidi ya miaka kumi. Wamebaisha urembo kuanzia kujipodoa, nywele, vipodozi na vito hadi blog na jarida inayoelezea masuala ya urembo. Baada ya kuuza bidhaa mbali mbali ya urembo toka nchi mbali mbali, Shear Illusions inazindua rasmi bidhaa yake ya LuvTouch Manjano.


LuvTouch Manjano ni maalum kwa ajili ya kumpendezesha mwanamke wa kitanzania. Kuna aina kumi ya vipodozi msingi kuanzia Mwanzi na Mpodo hadi kahawa na ardhi. Bidhaa hizi zimezingatia hali ya hewa ya joto. Vipodozi hivi vinalengo la kuongeza muonekano wako kwa hali yoyote.



Shear Illusions inazishukuru kampuni zifuatazo waliojitokeza kusaidia hafla hii ya kuwawezesha wanawake; NSSF, TCRA, Clouds Media, Maxcom, A1 Outdoor, Mr. Price, Cassandra Lingerie, Amina Design, Maznat Bridal, Advertising Dar, Beauty Point, Hugo Domingo, I-View Media, FAIDIKA, Benchmark Productions, Fasta Fasta, TENSHI, Jardin Modeling Agency na mashirika mbali mbali hapa Dar es Salaam.

Bayport: Wa mikoani nao wanaweza kukopa viwanja vya Kibaha

$
0
0
TAASISI ya Kifedha ya Bayaport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo,imesema hata Watanzania wanaoishi mikoani wanaweza kutumia fursa ya kukopeshwa viwanja katika mradi wa Vikuruti, uliopo Kibaha, mkoani Pwani. Unaweza kuptata fomu hapa.
Afisa Mipango wa Wilaya ya Kibaha, Obed Katonge, akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya mikopo ya viwanja, uliyofanyika mwishoni mwa wiki, katika hoteli ya Serena.

Bonyeza hapa kupata fomu ya mkopo wa viwanja kutoka Bayport Financial Serviceshttp://www.kopabayport.co.tz/RESERVATION%20FORM.pdf

Kauli hiyo imetolewa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa taasisi hiyo, Ngula Cheyo, ikiwa ni siku chache baada ya kuzindua huduma ya mikopo ya viwanja katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, huku akisisitiza kwamba si lazima mkopaji wa viwanja hivyyo atoke Dar es Salaam au Kibaha.
Kicheko cha furaha. Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, kulia akifurahia jambo na Meneja Masoko na Mawasiliaano wa Bayport Financial Services, jijini Dar es Salaam.

Habari; Watanzania wengi wanaoishi mikoani wamekuwa wakiulizia kama nao wana weza kukopeshwa viwanja hivyo,hivyo Bayport imeona itowe ufafanuzi huu. Kwamba ni ruhusa. Kilaa mtu anaweza kukopa.

Cheyo alisema kwamba huduma hiyo ni ya Watanzania wote, ndio maana wamesambaza fomu za kuomba mkopo wa viwanja katika matawi yao mbalimbali, bila kusahau wale wanaoweza kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz.

“Nafasi ni chache, maana maombi yetu yanafanyika kwa siku (20), kuanzia ile Mei 22 hadi Juni 10, huku fomu za maombi zikipatikana katika matawi yao yote ya Bayport Financial Services, bila kusahau kupitia bank of Africa (BOA), ambapo malilipo ya awali yakianzia Sh 150,000 na yatakuwa yakilipwa kwa akaunti yao ya Bayport iliyopo BOA.

“Fomu ya maombi na nakala ya malipo ya awali yarejeshwe katika matawi BOA au ofisi za taasisi yetu ya Bayport zilizoenea nchi nzima, huku baada ya Juni 10, mteja akitakiwa kulipia kiwanja kwa fedha taslimu au mkopo kutoka Bayport, ambapo watumishi wa umma na wa kampuni wanaweza kukopeshwa kiwanja na wakikabidhiwa hati miliki ndani ya siku (90), baada ya kukamilisha mkopo wake kwa wateja wa fedha taslimu na wengineo wakipewa baada ya kumaliza mkopo wao,” alisema Cheyo.

Kwa mujibu wa Cheyo, huduma ya mikopo ya viwanja ni maalum kwa ajili ya kuwakomboa Watanzania wote waliokuwa wakitatizwa na suala zima la makazi, hususan kutokana na ugumu wa maisha unaowakumba Watanzania wengi nchini.

Ngula alisema kukaa mikoani si sababu ya kushindwa kukopa kiwanja kwa sababu wamefungua matawi katika wilaya na mikoa mbalimbali, hivyo ni jukumu la mjasiriamali, mtumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi wanatumia nafasi hiyo kujiendeleza kwa kupata viwanja hivyo.

Naye Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, aliliambia gazeti hili kuwa ukubwa wa viwanja hivyo unaanzia hatua 15 kwa 16, huku thamani yake ikianzia Sh 1,400,000 bila riba (mortgage), ambapo pia fomu zao zimejieleza na kujifafanua vizuri kwa ajili ya kutoa urahisi wa kuwahudumia Watanzania wote.

Mndeme alimaliza kwa kuwataka wateja wao na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kuchangamkia viwanja hivyo vinavyokadiliwa kuwa 1878 vilivyokuwa katika eneo zuri, kilomita 50 kutoka Kisutu, jijini Dar es Salaam na kilomita 6.5 kutoka barabara Kuu ya Morogoro.


Article 20

WAZIRI LUKUVI AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI TABORA

$
0
0
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akisisitiza jambo wakati alipozungumza na Wakuu wa sekta mbalimbali mkoani Tabora leo kuhusiana na masuala yanayohusu sekta ya ardhi mkoani humo katika ukumbni wa mikutano wa Isike. Kulia ni mkuu wa Wilaya ya Tabora Mh Suleiman Kumchaya  na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Bi Kudra Mwinyimvua. 
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akizungumza na Wananchi wa Eneo la Malabi katika Manispaa ya Tabora, kuhusiana na mgogoro wa Ardhi unaowakabili wananchi hao ambao unaotokana na Manisapaa kutowalipa fidia ya maeneo yao.

Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mh Suleiman Kumchaya akijadiliana jambo wakati Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvu alipotembelea eneo la Malabi katika Manispaa ya Tabora kusikiliza matatizo ya Ardhi yanayo wakabili wananchi wa eneo hilo leo.  

Picha/Clarence Nanyaro

MAOMBI YA MCHANGO WA UJENZI WA MSIKITI

$
0
0

Katika Maisha yetu Wanaadamu Ibada ni Jambo Muhimu saana. 
Uzuri , Usafi wa sehemu ya kuabudu ni Moja katika mambo mazuri yenye kupendeza katika kila Nafsi ya Binaadamu.

Katika Nyumba (Msikiti)  huu , Ndugu zetu wanafanya Ibada ya Swala 5 kwa siku , Msikiti huu upo Mkoa wa Pwani , Wilaya ya Mkuranga , Kijiji cha Mlamleni Kitongoji cha Kimbangulile. 

Wenzetu wameanza kwa Nguvu zao  Ujenzi wa Msikiti kama Mnavyo uona.
Jitihada nyengine wameweza kuwa na Matofali yasiyo pungua 300 kwa Ajili ya kuanza Ujenzi Mpya. 

Ukiwa Umeguswa na hili tunaomba kutoka kwako MCHANGO WAKO WA VIFAA VYA UJENZI.

Kwa Mwanzo Tunahitaji 
1.Cement 
2.Tofali
3.mchanga
4.Vifaa vya Kuchimbia Majembe, Panga , chepe N.k

Maazimio yetu tuanze Ujenzi pale tu tutakapo pata uwezo wa kulifanya hili.

Tunawakaribisha mtembelee eneo la tukio kwa wale ambao Mtakuwa na  Na Muda wa kufanya hivyo.

Michango yenu tunaomba muwasilishe kwa Namba ya Simu.
0715800772( Tigo Pesa ) GHALIB MONERO.

Kwa wale waliopo Nje ya Tanzania : WESTERN UNION : GHALIB NASSOR MONERO 

Waliopo KENYA tafadhali wasiliana ALI BAJIY NASOR no' 0725113783 M-PESA.

More Update kuhusu Michango ya Msikiti huu Tafadhali Tutembelee : facebook : Kijana wa Kiislam Dsm or Whatssap Number : +255689604780

Au Piga Simu : +255715800772

Tunawashukuru kwa Michango yenu na Ubalozi wenu Mzuri wa kuitangaza kheri hii . 

WABILLAHI TAUFIQ WENU KATIKA UTUMISHI WA DINI KATIKA JAMII.

GHALIB N MONERO.

PATAKUWA HAPATOSHI DAR LIVE SIKU HIYO.

WAZIRI NYALANDU ASAINI MKATABA MSUMBIJI KULINDA SELOUS

$
0
0
 Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akibadilishana hati za makubaliano ya  kuhifadhi Pori la akiba la selous nchini Tanzania lililoungana na Hifadhi ya Nnyasa nchini Msumbiji na waziri wa Ardhi na Maendeleo vijijini Celso Coreia, ambapo mbali na uhifadhi watashirikiana kupambana na ujangili , utaalamu na vifaa, jana mjini Maputo Msumbiji.
  Waziri wa maliasili na Utalii, lazaro Nyalandu akimsikiliza waziri wa Ardhi na Maendeleo vijijini, Celso Coreia jana mjini Maputo kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kuhifadhi Pori la akiba la selous nchini Tanzania lililoungana na Hifadhi ya Nnyasa nchini Msumbiji ambapo mbali na uhifadhi watashirikiana kupambana na ujangili , utaalamu na vifaa.
 Waziri wa Maliasii na Utalii, Lazaro Nyalandu na waziri wa Ardhi na Maendeleo vijijini wa Msumbiji Celso Coreia wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kuhifadhi Pori la akiba la selous nchini Tanzania lililoungana na Hifadhi ya Nnyasa nchini Msumbiji ambapo  mbali na uhifadhi watashirikiana kupambana na ujangili, utaalamu na vifaa. 
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images