Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 534 | 535 | (Page 536) | 537 | 538 | .... | 1903 | newer

  0 0

  PR1
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya nUtamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko (kushoto) akiwa katika maandanano ya kuadhimisha siku ya Uanuai wa Utamaduni Dunia jijini Dar es Salaam juzi ambapo maaandamano hayo yalianzia katika viwanja vya maonyesho ya Biashara vya Mwalimu Nyererere Sabasabasa kupitia mtongani kwa Aziz Aly na kurudi kiatika viwanja hivyo.Kulia ni balozi wa India nchini Mhe.Debnath Shaw.
  PR2
  Baadhi ya vikundi vya sanaa na wananchi wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya uanuai wa Utamaduni Dunia maandamano hayo yalianzia katika viwanja vya maonyesho ya Biashara vya Mwalimu Nyererere Sabasabasa jijini Dar es Salaam kupitia mtongani kwa Aziz Aly na kurudi kiatika viwanja hivyo.Siku hiyo ya Uanuai wa Utamaduni uadhimishwa tarehe 21 May kila mwaka Duniani kote ikiwa na lengo la kukukuza na kuibua kazi za sanaa na utamaduni.
  PR3
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tan Trade) Bibi. Jacqueline Maleko akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Uanuai wa Utamaduni Duniani. Hafla iliyofanyika mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko na wa mwisho kushoto ni Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Debnath Shaw.
  PR4
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko Mkurugenzi kizungumza wakiti wa ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Uanuai wa Utamaduni Duniani. Hafla iliyofanyika mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tan Trade) Bibi. Jacqueline Maleko na mwisho kushoto ni Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Debnath Shaw.
  PR5
  Wapiga vyombo vya muziki na ngoma kutoksa kikundi cha Tanzania wkichakarika wakati wa zoezi la kutumbia kwenye hafla ya ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya uanuai wa Utamaduni.

  PR6
  Wanakikundi cha sanaa kutoka nchini India wakitumbuiza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uanuai wa Utamaduni Duniaa ambayo nufanyika kila tarehe 21 mwezi wa tano kila mwaka.
  PR7
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermsa Mwansoko akicheza Bao na Balozi wa India nchini Bw. Debnath Shaw wakati wa maadhimisho ya siku ya Uanuai wa Utamaduni Duniani ambapo kitaifa imefanyika jijini Dar es Salaam.Maadhimisho hayo yameambatana na maonyesho ya wajisariamali wa bidhaa za kiutamaduni na kuratibiwa kwa ushirikianao baiona ya Wizara yenye dhamana ya Utamaduni na Tan Trade.
  PR8
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya nUtamaduni KUTOKA Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko akiwa akiangalia namna wanafunzi wa shule
  …………………………………………………………………
  Na: Genofeva Matemu – Maelezo
  Wadau mbalimbali wa sekta ya Utamaduni nchini wameiomba jamii kuuenzi utamaduni wa Mtanzania kwa kuzingatia matumizi ya vitu vinavyoendana na tamaduni za Tanzania ili kudumisha na kuenzi mila na desturi za Tanzania.
  Kauli hiyo imeibuliwa na wadau wa sekta ya Utamaduni walioshiriki katika ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Uanuai wa Utamaduni Duniani inayoadhimishwa kila tarehe 21 ya mwezi Mei ambapo Tanzania imeadhimisha siku hiyo katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere Sabasaba jana jijini Dar es Salaam.
  Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bibi. Jacqueline Maleko ameiomba serikali kujenga kituo cha Utamaduni kitakachotumika kuendeleza, kudumisha na kuhamasisha matumizi ya vitu vya asili ya Tanzania hivyo kuendeleza tamaduni zetu.
  “Utamaduni wa mtanzania ni urithi wenye mashiko kama utadumishwa na kuhamasisha jamii kutumia vitu vya asili kama vile nyimbo, ngoma, uchongaji, mashahiri, uchoraji, filamu Sanaa, vyakula na mavazi kwa kuviendeleza na kuvinadi ndani na nje ya Tanzania” Amesema Bibi Maleko.
  Akitoa maoni yake kuhusu utamaduni wa Tanzania Mwalimu Gasper Maro kutoka Shule ya Msingi Magomeni amesema kuwa shule za msingi zimekuwa zikijitahidi kuuenzi utamaduni wa Tanzania kwa kuwahamasisha wanafunzi kuimba nyimbo za jadi na kucheza ngo ma za makabila mbalimbali ili kuweza kujua tamaduni za kila kabila lililopo nchini Tanzania,
  Hata hivyo mwalimu Maro amesema kuwa utamaduni wa Tanzania kwa sasa unashuka kutokana na kizazi cha sasa kuiga tamaduni za nchi nyingine na kudharau tamaduni zao hivyo kuwaomba maafisa utamaduni nchini kuandaa programu mbalimbali zitakazokuwa zikihamasisha jamii kuishi kwa kufuata tamaduni za Tanzania.
  Kwa upande wake mwanafunzi Agustino George Pius kutoka Shule ya Msingi Magomeni amesema kuwa utamaduni wa Tanzania umekua ukibadilishwa na vijana kutokana na maendeleo ya teknolojia hasa katika upande wa mavazi, vyakula, pamoja na staili ya maisha wanayoishi vijana wa sasa.
  Naye Afisa Utumishi kutoka Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bw. Elius Ngemela ameitaka jamii kutambua kuwa utamaduni ni utambulisho wa nchi ambao kama utatumika vizuri utasaidia kukuza uchumi wa nchi na kutoa ajira katika jamii hivyo kuuthamini na kuudumisha kwa maendeleo ya nchi yetu.

  0 0

  Diwani wa Nhavila, wilayani Masasi Meja Ramadhan Chilumba akimsaidia Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kupanda kingo za mto, alipotembelea mto Ruvuma mpakani na Msumbiji kutoa kifutajasho kwa watu waliojeruhiwa na kuuawa na mamba katika mto huo.
  ny3
  Diwani wa Nhavila, wilayani Masasi Meja Ramadhan Chilumba akimwongoza Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alipotembelea mto Ruvuma katika kijiji cha Manyuli wilayani Masasi, mpakani na Msumbiji alikokwenda kutoa kifutajasho kwa watu waliojeruhiwa na kuuawa na mamba katika mto huo.
  ny4
  Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na wanakijiji wa Manyuli wilayani Masasi ambako alitembelea watu waliojeruhiwa na wengine kuuawa na mamba, alipokwenda kutoa kifuta machozi kutoka wizarani kwake.
  ny5
  Wanakijiji wa Manyuli, wilayani Masasi wakimsikiliza Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alipozungumza nao jana, alitembelea watu waliojeruhiwa na wengine kuuawa na mamba, alipokwenda kutoa kifuta machozi kutoka wizarani kwake.
  ny6
  Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na wanakijiji wa Manyuli wilayani Masasi ambako alitembelea watu waliojeruhiwa na wengine kuuawa na mamba, alipokwenda kutoa kifuta machozi kutoka wizarani kwake.

  0 0


  0 0


  Mwimbaji mahili wa nyimbo za injili kutoka Tanzania Upendo Nkone akiimba moja ya nyimbo zilizowainua watu vitin kwenye tamasha la Gospel linaloendelea mjini Columbus tangia siku ya Ijumaa May 22 na kuhitimishwa leo siku ya Jumapili May 24. Tamasha lilihudhuriwa na watu kutoka mataifa mbalimbali wengine wakiwa wamesafiri kutoka majimbo ya mbali na Ohio.

  Mwimbaji kutoka Jamhuri ya Congo akienda sambamba na mwimbaji mahili wa nyimbo za injili Upendo Nkone kwenye tamasha la Gospel lililofanyika siku ya Jumamosi May 23, 2015 6230 Busch Blvd suit 260, Columbus, OH 43229.

   Nnunu Nkone akitoa neno la Mungu na kuimba kwenye Tamasha la Gospel lililofanyika
  Mchungaji Donis Nkone ambaye ni kaka ya mwimbaji Upendo Nkone akitoa ukifanya utambulisho kwa bendi iliyokuwa ikitumbuiza nyimbo za injili kwenye tamasha la Gospel lililofanyika siku ya Jumamosi May 23, 2015 mjini Columbus.

  Mchungaji Donis Nkone na mkewe Nnunu Nkone wakifuatilia tamasha la Gospel. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  WATU sita, akiwemo Mwalimu wa Shule ya Msingi Katunguru iliyoko Kata ya Wendele, Tarafa ya Msalala wilayani Kahama, wamekamatwa mjini hapa wakiwa na vipande sita vya mifupa inayodhaniwa kuwa ya albino. 

   Taarifa zilizopatikana mjini Kahama zimeeleza kwamba, mwalimu huyo Bahati Kilungu Maziku (56), Msukuma na mkazi wa Mtaa wa Mbulu katika Halmashauri ya Mji wa Kahama, amekamatwa akiwa na watu watano, wakiwemo waganga wa jadi watatu, katika harakati za kuuziana mifupa hiyo.
  Wengine waliokamatwa ni mganga wa jadi Bi. Elizabeth au Shija Makandi Sweya (42), mkazi wa Busongwahala, Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Bilia Masanja Mhalala (39), Msukuma, mkulima na mkazi wa Mogwa wilayani Nzega, mke wa Biria ambaye ni mganga wa jadi Regina au Tatu Kashinje Nhende (40), Msukuma na mkazi wa Mogwa. 

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, SACP Justus Kamugisha, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Mei 21, 2015 na kwamba watu hao walikamatwa saa 7:00 mchana katika nyumba moja ya kulala wageni inayofahamika kwa jina la Maji Hoteli iliyopo Phantom, Kata ya Nyasubi mjini Kahama baada ya Polisi kuweka mtego kufuatia taarifa za wasamaria wema. 

  Taarifa ya Kamanda Kamugisha imesema kwamba, mnamo Mei 19, asubuhi, mkuu wa upelelezi wa Wilaya ya Nzega alipata taarifa kuwa kuna mtu anauza viungo vya albino, ndipo walipoweka mtego. Hata hivyo, alisema kuwa walishindwa kuwakamata na baadaye mtu huyo alihamishia biashara hiyo wilayani Kahama. 

   Aidha, watuhumiwa wengine waliokamatwa ni Muhoja John Shija (24), Mnyamwezi na mkazi wa Isagenhe wilayani Nzega pamoja na mganga wa jadi na mfanyabiashara Abubakar Ally Magazi (25), Mrundi na mkazi wa Nzega. Taarifa za uchunguzi wa awali zinaeleza kwamba, Mwalimu Bahati ndiye aliyesuka mpango mzima akishirikiana na waganga wa jadi Bi. Shija Makandi ambaye ndiye aliyeitafuta mifupa hiyo na Abubakar Magazi ambaye alikuwa apelekewe ili ‘kuibetua’ (kuitengeneza) na kuzalisha fedha. 

   Watuhumiwa watano wanadaiwa kwamba walifunga safari kutoka Nzega hadi Kahama kwa Mwalimu Bahati, ambaye kwa mujibu wa maelezo ya awali, ndiye aliyejua ni wapi ambako mifupa hiyo ingeuzwa, hivyo walikuwa wanakutana hapo kwa ajili ya kugawana fedha.
   Mifupa hiyo inadawa kuhusishwa na tukio la kukatwa mkono wa kulia Bi. Muungu Masaga Gedi (35) mwenye albinism, mkazi wa Kitongoji cha Mkuyuni, Kijiji cha Buhekela, Kata ya Igoweko wilayani Igunga, ambalo lilitokea Mei 16, 2014 na kufunguliwa Jalada Namba IGU/IR/1070/2014. 
   Katika tukio hilo, mume wa majeruhi huyo, Mapambo Mashili, aliuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiofahamika wakati akipambana na watu hao wasimdhuru mkewe.  

   Hata hivyo, amesema, jeshi la polisi bado linaendelea na msako dhidi ya watu wengine wanaotajwa kwamba ndio walioitafuta mifupa hiyo, na kwa mujibu wa taarifa za awali, ndio waliohusika na mauaji pamoja na kumjeruhi mama huyo. Picha zote za watuhumiwa hao 
  zimepigwa na Daniel Mbega, Kahama

  Bilia Masanja Mhalala.  Mwalimu wa Shule ya Msingi Katunguru wilayani Kahama, Bahati Kilungu Maziku.


  Abubakar Ally Magazi.  Elizabeth au Shija Makandi Sweya na Regina au Tatu Kashinje Nhende.


  Muhoja John Shija


  0 0

  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala pamoja na viongozi mbalimbali wa meza kuu kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 wakipiga picha na baadhi ya washindi wa Tuzo za Filamu 2015 jana zilizofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala pamoja na viongozi mbalimbali wa meza kuu kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 wakipiga picha na baadhi ya washindi wa Tuzo za Filamu 2015 jana zilizofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala akitoa shukrani baada ya kupokea tuzo aliyopewa Rais Jakaya Kikwete na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFA) kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala akitoa shukrani baada ya kupokea tuzo aliyopewa Rais Jakaya Kikwete na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFA) kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015.Mama yake na Steven Kanumba akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo ya mwanaye kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.Mama yake na Steven Kanumba akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo ya mwanaye kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.

  0 0

   Katibu Tawala wilaya ya Masasi, Dunford Peter akimwonyesha ramani Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ya sehemu ya mto huo, wakati waziri huyo alipotembelea mto Ruvuma katika kijiji cha Manyuli ambako alitembelea.
   Diwani wa Nhavila, wilayani Masasi Meja Ramadhan Chilumba akimwongoza Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alipotembelea mto Ruvuma katika kijiji cha Manyuli wilayani Masasi, mpakani na Msumbiji alikokwenda kutoa kifutajasho kwa watu waliojeruhiwa na kuuawa na mamba katika mto huo.
  Wanakijiji wa Manyuli, wilayani Masasi wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alipozungumza nao jana, alitembelea watu waliojeruhiwa na wengine kuuawa na mamba, alipokwenda kutoa kifuta machozi kutoka wizarani kwake.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na wanakijiji wa Manyuli wilayani Masasi ambako alitembelea watu waliojeruhiwa na wengine kuuawa na mamba, alipokwenda kutoa kifuta machozi kutoka wizarani kwake.


  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amewaagiza askari na maofisa wa wanyamapori nchini kuwavuna mamba wanaoua na kujeruhi wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.


  Alitoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Manyuli wilayani Masasi mkoani Mtwara, alipokwenda kukagua madhara yatokanayo na mamba katika Mto Ruvuma.  Kauli ya Nyalandu imetokana na kilio cha Mbunge wa Masasi, Mariam Masembe na wananchi wake kuwa mamba hao mbali na kuua na kujeruhi wananchi, pia wamekuwa kero kubwa na kusababisha shughuli za uzalishaji mali kuzorota.


  Amesema serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imesikia kilio cha wananchi na imeanza kuchukua hatua ili kuhakikisha usalama wa wananchi unakuwepo muda wote na kwamba, jukumu la kuwavuna wanyama hao litasimamiwa na maofisa na askari wa wanyamapori.


  “Nimekuja hapa kuwajulia hali na kuwapa pole kutokana na uharibifu wa wanyama hawa ambao wamekuwa wakiwasumbua kwa muda mrefu… nimewaona na kuzungumza na watu waliojeruhiwa na mamba wakati wakiwa kwenye shughuli za uzalishaji mali jirani na mto.


  “Watendaji na askari wa wanyamapori kukagua maeneo yote ambayo yana wanyama wanaoshambulia wananchi na kuwajeruhi ili wavunwe. Serikali ya CCM ipo kwa ajili ya maendeleo na kulinda maisha ya watu wake hivyo, wanyama hawa watavunwa haraka iwezekanavyo,” alisema Nyalandu.


  Nyalandu amesema kuwa mapato yatakayopatikana kwa kuvunwa mamba hao zitatumika katika mapambano dhidi ya ujangili na huduma zingine za kijamii.


  Awali, alikabidhi hundi ya sh. milioni 11.7 ikiwa ni malipo ya kifuta jasho na pole kwa watu walioshambuliwa na mamba wilayani humo, ambapo uongozi wa wilaya utakuwa na jukumu la kugawa kwa utaratibu uliopangwa.


  “Kwa kutambua na kuthamini wananchi wetu, serikali yenu ya CCM imetoa fedha kama pole na kifuta jasho kwa ndugu zetu walioshambuliwa na wanyama hawa…fedha hizi haziwezi kuponya machungu ama kurejesha kiungo kilichopotea, lakini ni ubinadamu na kuonyesha kuguswa kwetu na matukio haya,” aliongeza.


  Kwa upande wake, Katibu Tawala Wilaya ya Masasi, Dunford Peter, alimpongeza Nyalandu kwa kutimiza ahadi ya kukutana na kuzungumza na wananchi na kutoa kifuta jasho kwa waathirika.


  Diwani wa Kata ya Mhavila, Meja Ramadhani Chilumba, alisema Nyalandu ni kiongozi wa aina yake na kwamba, utendaji kazi wake umedhihirisha serikali ya CCM inawajali wananchi wake.


  Pia alipongeza uamuzi wa serikali kuvuna mamba katika mto huo kuwa itaongeza ari na hamasa ya wananchi kufanya shughuli za uzalishaji mali bila hofu tofauti na ilivyo sasa.

  0 0

  index
  * Mbwembwe,sherehe marufuku
  *Idadi ya wadhamini, mikoa sasa yaongezwa
  *Wajumbe NEC, marufuku kudhamini wagombea
   
  Chama  cha Mapinduzi(CCM), kimetangaza rasmi ratiba ya kuchukua na kurejesha fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo ya urais, huku kikitoa masharti magumu kwa wanaotaka kuwania urais kupitia chama hicho.

   Chama hicho kimetoa msimamo wake kuwa wagombea wanatakia kuheshimu kanuni na misingi ya chama hicho na ni marufuku kwa wagombea kufanya mbwembwe, madoido na kukodi watu kwa ajili ya kukushangilia wakati wa kuchukua fomu au kurudisha ni marufuku.
  Akitangaza uamuzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu(NEC) ya chama hicho, leo mjini Dodoma,Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema fomu ya kugombea urais itaanza kutolewa Juni 3 mwaka huu na kuzidurisha Julai 2 mwaka huu saa 10 jioni.

  Amesema kuanzia Juni 3 wanaruhusiwa kuanza kuchukua fomu na kuzirudisha Julai 2 mwaka huu. Wakishachukua fomu watafanya kazi ya kutafuta wadhamini mikoani. Amesema mwaka huu idadi ya wadhamini imeongezeka kutoka wadhamini 250 hadi wadhamini 450 huku idadi ya mikoa nayo ikiongezeka kutoka 10 hadi 15.

  Nape amesema  kuongeza kwa wadhamini hao ni kutokana na idadi ya wanachama wao kuongezeka na wakati huo huo mikoa nayo imeongezeka.Hivyo lazima wagombea waende kwenye mikoa hiyo ambapo mikoa 12 kwa Tanzania Bara na mikoa mitatu Zanzibar na moja ya mkoa uwe Pemba au Unguja.

  Amesema moja ya sharti ni kuhakikisha wadhamini wa mgombea mmoja wa ngazi ya urais hawatakiwi kuwa wadhamini wa mgombe mwingine .Hivyo kila mdhamini mmoja anatakiwa kumdhamini mgombea mmoja na si zaidi.
  “Tumekubaliana kwenye NEC mwanachama mmoja anatakiwa kumdhaminni mgombea mmoja tu.Haitaruhusiwa mwachama mmoja kuwadhamini wagombea wawili.

  Pia amesema wakati wa kuchukua fomu na kurejesha ni marufuku mgombea kufanya mbwembwe za aina yoyote huku akifafanua ni muhimu wagomba kusoma kanuni na kuzielewa mapema. Kwa mujibu wa Nape ni kwamba vikao vya uchuchaji ni kwamba Kamati ya Maadili na Usalama itachuja majina ya wagombea urais Julai 8 mwaka huu, Kamati Kuu(CC) itachuja majina Julai 9 mwaka huu na Halmashauri Kuu nayo itapitisha jina la mgombea Urais Zanzibar.

  Wakati kwa jina la mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jina litapitishwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu Julai 11 mwaka huu mjini hapa. Alisisitiza wagombea urais wanatakiwa kuheshimu kanuni za chama hicho katika mchakato mzima wa kuchukua fomu, kurudisha na hata wakati wa  kutafuta wadhamini na mwaka huu masharti yameongezeka kidogo likiwemo la idadi ya wadhamini na wagombea kuhakikisha hawakiuki kanuni za maadili.

  “Sharti ambalo limetolewa na NEC ni kwamba marufuku wajumbe wa NEC na Kamati kuu kuwadhamini wagombea urais kwani wao ndio watakaopitisha jina la mgombe, hivyo hawatakiwi kua sehemu ya wadhamini.
  .
  Kuhusu  kuchukua fomu ya udiwani, ubunge na uwakilishi, Nape amesema fomu zitaanza kutotolea Julai 15 mwaka huu na kurudishwa Julai 19 mwaka huu wakati mikutano ya kempeni itaanza Julai 20 hadi Julai 31 mwaka huu.
  Nape alisema kura ya maoni itafanyika Agosti 1 mwaka huu wakati wabunge wa viti maalumu nayo itakuwa Julai 15 mwaka huu na kurudisha fomu Julai 19 na kufafanua uchujaji wa majina utafanywa na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake(UWT), Taifa licha ya kwamba mchakato wake utapita Baraza la Vijana.

  Kwa upande wa gharama za fomu kwa ajili ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye chama hicho,Nape alisema fomu ya kugombea urais itakuwa sh.milioni moja, wakati fomu ya kugombea ubunge ni sh.100,000 na fomu ya udiwani sh.50,000.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiikabidhi timu ya soka ya Kilimani Sports Club jezi na mipira katika ikulu ndogo ya mjini Dodoma leo asubuhi.Rais Kikwete alitoa msaada kwa timu hiyo baada ya kuwakuta vijana hao wakifanya mazoezi bila zana bora katika uwanja wa mpira ulioko eneo la Kilimani karibu na Ikulu wakati Rais alipokuwa akifanya mazoezi ya kutembea katika eneo hilo.

  Wakiongea mara baada ya kupokea msaada huo vijana hao walimshukuru Rais Kwa moyo wake wa upendo na nia yake ya kukuza vipaji kwa vijana na kuahidi kufanya vyema katika ligi ya Wilaya ya Dodoma mjini. Picha na Freddy Maro

  0 0


  MALI MUPYA IMEINGIA @AK CLASSIC COSMETICS WAPI WAREMBO WA MUJINI!!?
  WADADA WOTE WANAOTAKA KUPIGA MSASA NGOZI ZAO NA BIDHAA ZENYE VIWANGO BASI KIJIWE NDIO HIKI...   @AKCLASSIC WANA MZIGO MUPYAA  KWA AJILI YAKO KUANZIA UNYAYONI MPAKA UTOSINI!!

   NINI KINAKUPA STRESS WEWE? JE WATAKA KUNG'AA?AU UNYWELE HAUJAI AMA KUNYONYOKA?UNASWEAT SANA KULIKO KAWAIDA? UNA CHUNUSI NA MABAKA?UNATAFUTA MAKE UP NZURI KWA GHARAMA NAFUU?UNATAKA KUPUNGUZA TUMBO? UNA DARK CIRCLE (MIWANI) AMA MICHIRIZI?AU WEUSI WA MAPAJANI ULEEE?AMA UNATAKA KUWA NA RANGI MOJA MWILI MZIMA? 
  PITIA BAADHI YA MAMBO YAO HAPA....  TUNAPATIKANA KINONDONI KWA MANYANYA NA MLIMANI CITY MKABALA NA SUBWAY.
   TUPIGIE  TUPIGIE /0753482909

  BIDHAA ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO!!
  0 0


  0 0

  DSC_0569

  Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bi. Zulmira Rodgrigues, akiwasilisha mada katika warsha ya siku tatu iliyofanyika katika kijiji cha Nyakahungwa wilayani Sengerema mkoani Mwanza kuhusu ushirikishaji jamii katika kuandaa na kutekeleza mikakati itakayochangia kuzuia na kutokomeza unyanyasaji na dhulma zinazofanywa dhidi ya watu wenye albinism iliyoshirikisha waganga wa asili, wauguzi na wakunga, viongozi wa dini, walimu pamoja na watu maarufu iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

  Na Modewjiblog team, Mwanza
  Mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) yanayoendelea nchini yanatokana na mitazamo hasi kitamaduni miongoni mwa wanajamii. Hayo yameelezwa na washiriki wa warsha ya siku tatu inayoendelea katika kijiji cha Nyakahungwa kata ya Nyakahungwa wilayani Sengerema yenye lengo la kubadili mitazamo iliyojengeka katika jamii na kusababisha madhara makubwa kwa watu wenye albinism iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

  Warsha hiyo ni miongoni mwa mlolongo wa warsha nne zitakazofanyika katika wilaya za Sengerema, Mwanza, Kahama na Bariadi kwa kuzishirikisha jamii kuibua masuala mbalimbali yanayobagua, kunyanyapaa na kuwatenga watu wenye albinism katika maeneo husika. Warsha hizo zinafanyika katika kipindi ambacho kumetokea mauaji ya mtoto wa kike, msichana na kijana wenye albinism wilayani Sengerema wakati tarehe 14 Mei 2015 mwanamke mmoja alikatwa mkono wilayani Bariadi.
  DSC_0522
  DSC_0532
  Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Sengerema, Bw. Bushaija Vicent (kulia), akitoa takwimu za idadi ya za wanafunzi wenye albinism katika wilaya yake kwa Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO Bi. Zulmira Rodgrigues.

  Kwa mujibu wa Afisa Maendeleo Jamii wilayani Sengerema Bwana Bushaija Vicent kati ya shule za msingi 191 wilayani humo ni Shule zenye watoto wenye albinism ni 14, Idadi yao ni 16 katika shule ya awali watoto 4 wana albinisim, vyuo mbalimbali Sengerema vijana 4 wana albinism na katika Shule za sekondari 48, watoto wenye albinism 4.


  Akitoa mada kuhusu uhamasishaji jamii katika masuala ya albinism, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO Bi Zulmira Rodgrigues amesema miongoni mwa masuala ambayo warsha italenga ni kutafakari kwa kina kwa nini watu wenye albinism wanauawa, kubaguliwa, kutengwa na mambo yanayosababisha Tanzania kuongoza katika mauaji hayo ikilinganishwa na nchi nyingine ambazo pia zina watu wenye albinism.

  “Watu wenye albinism hawauwawi katika sehemu nyingine duniani, kwa nini Tanzania? Ikiwa mauaji hayo yako kwa wingi nchini Tanzania basi kuna tatizo kubwa ambalo linatakiwa kufanyiwa kazi, na si serikali, UNESCO wala taasisi yoyote ambayo inaweza kuleta mabadiliko hayo isipokuwa jamii yenyewe,” alisema Rodrigues.

  Tatizo kubwa lililotajwa kuhusiana na mauaji ya watu wenye albinism ni utamaduni uliojengeka katika fikra za watu na kuwa na imani kwamba watu wenye albinism si watu wa kawaida, hawana hadhi na hawastahili kuishi.

  Watu wenye albinism ni watu wa kawaida wanaostahili heshima na kulindwa kama binadamu wengine kulingana na kanuni na sheria za nchi na za kimataifa zinazopinga ubaguzi wa rangi, jinsia, tabaka na kukatisha maisha ya mtu. Tofauti ni kwamba rangi yao inatokana na ukosefu wa vinasaba asili vijulikanavyo kama melanin, vyenye uwezo wa kuzalisha rangi ya nywele, macho na ngozi.

  Utamaduni uliojengeka katika jamii wa kuwabagua, kuwatenga na kuwapuuza watu wenye ulemavu wa ngozi kumehalalisha mauaji ambayo kwa hivi sasa imekuwa biashara ya kuuza viungo vya watu wenye albinism kwa waganga wa asili kwa lengo la kupata utajiri, cheo na madaraka.

  “Mara nyingi waganga wa asili wamekuwa wakitajwa kuwa ndio chanzo cha mauaji hayo kwa ajili ya imani potofu ya kujipatia utajiri, vyeo na madaraka. Biashara hiyo inaonekana kushamiri kwa kuwa hakuna mifumo mahsusi kudhibiti maafa hayo,” alisema mmoja wa washiriki anayeshughulikia masuala ya usalama.
  DSC_0545
  Mratibu na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO Bi. Rose Haji Mwalimu, akichangia mada kuhusu ushirikishaji jamii katika kuandaa na kutekeleza mikakati itakayochangia kuzuia na kutokomeza unyanyasaji na dhulma zinazofanywa dhidi ya watu wenye albinism iliyoshirikisha waganga wa asili, wauguzi na wakunga, viongozi wa dini, walimu pamoja na watu maarufu iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Katikati ni Mratibu ambaye pia ni Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias na Kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bi. Zulmira Rodgrigues.
  Akichangia mada wakati wa majadiliano yanayokusudiwa kuzalisha mikakati ya kukomesha maovu hayo, Mratibu na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO Bi Rose Haji Mwalimu alisema kwamba wakati umefika wa kutambua kitu gani kizuri katika tamaduni zilizopo zitakazoweza kusaidia kuleta mafanikio na kuachana na zile ambazo hazina tija na zinasababisha maafa katika maendeleo na ustawi wa jamii.
  “Ni kweli kuna changamoto nyingi katika jamii zinazosababishwa na kuhalalisha tamaduni zinazolenga kupotosha badala ya kujenga. Tukiendelea kuzikumbatia tutajikuta tunajenga taifa lisiloona mbali kimaendeleo kuhadaiwa na watu wenye ubinafsi kutoka nje na ndio maana Tanzania imekuwa soko kubwa au shamba lenye rutuba ya kupandikiza mbegu ambazo mavuno yake hupatikana kwa urahisi”, alisema Bi Mwalimu.
  Katika warsha hiyo washiriki walibaini maeneo makuu matatu ya kuyawekea mpango kazi. Maeneo hayo ni Kuzuia mauaji, ubaguzi, unyanyapaa na kuwatenga, eneo la pili ni kuwalinda watu wenye albinism katika maeneo ya makazi, mashuleni, katika jamii na familia zao na la tatu ni hatua za kisheria wale wote watakaoonekana kuhusika moja kwa moja au kwa namna nyingine katika kuwatendea maovu watu wenye ulemavu wa ngozi kuanzia ngazi za kimataifa, kitaifa, kifamilia na shuleni.
  DSC_0553
  Mganga wa jadi kutoka kijiji Nyanzenda, wilayani Sengerema, Maimuna Musa akizungumzia jinsi anavyotoa huduma za kutibu watoto magonjwa mbalimbali ya watoto ikiwemo na huduma ya kuzuia mwanamke asizae mtoto mwenye ulemavu wa ngozi.
  DSC_0549
  Mganga wa jadi kutoka kijiji cha Nyakasungwa, Omary Mongongwa akitoa msimamo kuhusu uwezo wa tiba kwa waganga wa jadi unavyotofautiana na kuwasihi waganga wenzake wa jadi wanapojadili wazungumzie kazi za mtu binafsi na utendaji wake na si kuusemea moyo wa mganga mwingine.
  DSC_0596
  Mzee maarufu kutoka kijiji cha Bukokwa, Felician Buhumbi, akifafanua hatua zilizokuwa zikichukuliwa wakati wa Ukoloni dhidi ya waganga asili wenye kupiga ramli chonganishi wakati wa warsha ya siku tatu iliyofanyika katika kijiji cha Nyakahungwa wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
  DSC_0511
  Sehemu ya washiriki wa warsha hiyo ya siku tatu iliyowashirikisha, Waganga wa Jadi, Viongozi wa dini, walimu shule za msingi na sekondari, wazee maarufu, Wakunga, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Shirika la Under the Same Sun, Baraza la taifa la dawa asilia, Afisa wa polisi wa dawati la jinsia pamoja na Maafisa wa mkoa wa Mwanza na wa wilaya ya Sengerema.
  DSC_0652
  Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bi. Zulmira Rodgrigues aliyeambatana na mbunge wa viti maalum CCM anayetetea maslahi ya watu wenye albinism, Mh. Al-Shaymaa Kwegyir wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki.

  0 0

  0029Na: GenofevaMatemu – Maelezo
  ……………………………………………….
  Wadau waTasniaya Sanaa na Utamaduni wametakiwa kutumia Sanaa kuendeleza upendo, amani na uvumilivu wa nchi hasa katika kipindi hiki tunapoelekea kwenye uchaguzi makuu.
  Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Prof. Helmas Mwansoko alipokua akimwakilisha Mhe.Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni kwenye maadhimisho ya siku ya Uanuai wa Utamaduni yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Prof. Mwansoko amesema kuwa suala la upendo linasisitizwa katika vitabu mbalimbali vya dini ulimwenguni kote kwani palipo na upendo amani na utulivu vinatawala hivyo kuwaomba wadau wa Sanaa na utamaduni kutumia mbinu mbalimbali za sanaa kuendeleza upendo na amani nchini.
  “Nikinukuu kwenye katiba inayopendekezwa sura ya kwanza Ibara ya tano inasema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaenzi na kuzingatia Tunu za Taifa ambapo moja ya tunu hizo ni Amani nautulivu pia sera ya Utamaduni ya mwaka 1997 kipengele cha dhima ya utamaduni kimeeleza kuwa watanzani awanajivunia kuwa kielelezo cha Uhuru na utaifa wao kwakuwa na umoja, amani na utulivu hivyo ni vyema tukaendeleza amani ya nchi yetu kupitia sanaa”, alisema Prof. Mwansoko.
  Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bibi Jacqueline Maleko amesema kuwa TanTrade imeandaa mpango mkakati wa kukuza na kuendeleza biashara ya bidhaa za asili za Tanzania kuweza kupata masoko ndani na nje ya nchi hivyo kuchangia katika kukuza kipato kwa wadau na uchumi waTaifaletu.
  Bibi. Maleko amesema kuwa vitu vya asili kutoka Tanzania vinapendwa na watu kutoka nchi nyingine hivyo kuwataka wadau wa Tasnia ya Sanaa na Utamaduni kuchangamkia fursa zinazo jitokeza na kupigania kupata masoko endelevu ya bidhaa nakujitokeza kushiriki katika maonyesho mbalimbali ya Sanaa na utamaduni yatakayo wawezesha kupata mbinu mpya za kiujasiriamali.
  Siku ya uanuaiwa utamaduni uadhimishwa duniani kote kila tarehe 21 ya mwezi wa tano ambapo nchini Tanzania siku hiyo imeadhimishwa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba na kubeba kaulimbiu iliyosema “Tuuenzi Utamaduni wetu kwakudumisha Amani na Upendo wakati wa Uchaguzi Mkuu” na kushirikisha wajasiriamali mbalimbali wabidhaa za utamaduni pamoja wasanii kutoka Kituo cha Utamaduni cha India kilichopo nchini Tanzania.

  0 0

   Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Mh.Freeman Mbowe akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Parkers Jana, ambapo pia alizindua kitabu cha Mbunge wa jimbo la Kawe Mh. Halima Mdee.
   Mh Freeman Mbowe, Halima Mdee na John Mnyika wakizindua kitabu cha Mbunge wa Kawe Mh Halima Mdee
   Gwajima akiwa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA
   Mchungaji Gwajima akiongozwa na Halima Mdee kwenye jukwaa kuu
   Wafuasi wa CHADEMA wakisikiliza hotuba ya mwenyekiti wao, Freeman Mbowe
  Umati wa watu waliohudhuria mkutano wa CHADEMA uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers.

  0 0

  Naibu Kamanda wa UVCCM ,Innocent Melleck akiwa na mama mzazi wa mtoto Felista ,Beatrice Shirima mara baada ya kukabidhi kiti cha walemavu cha magurudumu kwa ajili ya kusaidia kutoka eneo moja hadi jingine.
  Naibu kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi vijijini ,Innocent Melleck akikabidhi Pempers kwa mama wa mtoto Felista ,Beatrice Shirima kwa ajili ya kumsaidia mtoto huyo aliyepata ulemavu wa miguu miwli baada ya kugongwa na gari aina ya Fuso.(Na Dixon Busagaga).
  Naibu kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi Vijijini ,Innocent Melleck akiwa amembeba mtoto Felista Shirima(3) aliyekatwa miguu yote miwili baada ya kugongwa na gari aina ya Fuso jirani na nyubani kwao.

  Akizungumzia sakata la mtoto huyo Naibu kamanda huyo alisema kuwa ataumia kila aina ya uwezo na nguvu zake kwa kushirikiana na ofisi ya umoja wa vijana wa chama chama mapinduzi UVCCM ili kuhakikisha kuwa  haki ya mtoto huyo inapatikana.

  Awali akizungumza mara baada ya kukabidhiwa msaada wa baiskeli  ya magurudumu matatu na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki saba na kamanda huyo, mama mzazi wa mtoto huyo Beatrice Kelvin,aliiomba serikali na wadau mbalimbali kujitokeza na kumsaida mwanae ili kuhakikisha haki inapatikana. 


  Alisema kesi iliyokuwepo mahakama kwa ajili ya kudai haki za msingi za mwanae imeisha bila haki yake kupatikana licha ya kuhangaika sehemu mbalimba na kuomba vyombo husika vinavyo jishughulisaha na haki za binadamu kuingilia kati suala hilo hatua ambayo itasaida kupata haki.


  0 0
 • 05/24/15--23:16: RATIBA YA NAFASI ZA UBUNGE

 • 0 0

  Acacia’s top leadership,DeoMwanyika, (First-L), Peter Gelete, (2rd-L), Andrey Wrey, (3rd-R), Asa Mwaipopo, (2nd-R), and Janet Reuben Lekashingo, (First-R),  pose for a group photo with two awards’ recipients of 15 years of service, Hamisi Hussein Juma, (3rd-L), and Omary Ally, (4th-L), during the awards giving ceremony held at the main office off Bagamoyo road in Dar es Salaam

   ACACIA has been operating in Tanzania for over a decade and during that time the company has made a significant progress in mining industry in the country. To value this achievements, in the beginning of this year 2015, Acacia has recognized it's employees by rewarding them, some for long service and others for their outstanding performance under the company's six desired behaviors' culture.

  All team members are exposed to a unique world class Cultural Transformation Programme, called Tufanikiwe Pamoja. The Programme embeds the Company's expectations and the accountabilities of every leader and team member with respect to their behavior and approach to work.  To ensure a high performance culture and become the best Company in Africa, the company has articulated six desired behaviors which all team member  are expected to practice. These including, "We plan the work and work to  plan, We hold people accountable and recognise performance, We work as a team (collaborate) and communicate openly, We do what we say we will do, We act with a sense of urgency, We develop our people to do their best".  At the end of this week it was the turn of Acacia Dar office employees, where 46 employees were awarded for a long service at a colorful event  held on Friday evening at the company's main office along Bagamoyo road. Long servicing employees is the company's Buzwagi, North Mara and Bulyanhulu gold mine sites have also been rewarded since last month.  Those recognized on Friday were the staff who worked for 5, 10 and 15 years, since the company commenced it's operation in Tanzania. The awards were meant to show the company's appreciation for the workers commitment and loyalty that's reflected by their long years of service.

  Acacia’s Executive General Manager, Organisational Effectiveness, Peter Geleta, (L), presents a certificate of appricietion for long service, to the company’s Head of Government Relations, Alex Lugendo, during the awards giving ceremony held at the main office along Bagamoyo road, Friday May 22, 2015. Lugando joined the company 5 years ago.


  Acacia’s Vice President, (Corporate Affairs), Deo Mwanyika, delivers his speech during the awards giving ceremony held at the company’s main office in Dar es Salaam  Acacia’s Chief Financial Officer, (CFO), Andrew Wrey, makes his speech


  Acacia’s General Manager, Organizational Effectiveness Janet Reuben Lekashingo, (L), presents a certificate of appreciation to Bonifacia Bernard Mlenga, from aviation department during award giving ceremony for long service.


  Acacia’s Vice President (Corporate Affairs), Deo Mwanyika, (L), presents a certificate of appreciation to the company’s Chief Advisor Occupational Health and Safety Zumbi Musiba, who joined the company 10 years back


  Vice President Corporate Affairs, Deo Mwanyika, (R), joins the representatives from all three groups, to cut a cake to signify the award giving ceremony success.


  Acacia’s Vice President, (Corporate Affairs), Deo Mwanyika, (C), Chief Financial Officer, Andrew Wrey, (4th-R), Executive General Manager, Organisational Effectiveness, Peter Geleta,, (3rd-L),  GM Sustainability Asa Mwaipopo, (3rd-R), GM Organizational Effectiveness, Janet Reuben Lekashingo(First-R), pose for a group photo with awards’ recipients of 10 years of service, left to right, Caroline Lucas Materu, Ritesh Divecha, Joseph Mbanya, and the company’s Chief Advisor Occupational Health and Safety, Dr.  Zumbi Musiba


  Acacia’s employees, carry a balloon named Acacia, to show the spirit of working as a team (collaborate), during the event  Elated awards’ recipients display they certificates to a photographer


  Acacia’s top leadership poses for a group photo with awards’ recipients of 5 years of service

  Acacia’s Sustainability General Manager Asa Mwaipopo, presents a certificate of appreciation to the company’s Corporate Community Relations Manager Stephen Kisakye for long service
  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ratiba rasmi kwa vyama vya Siasa na wananchi wote itakayotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Serikali  unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
  Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo  Jaji wa Rufaa (Mst.) Damian  Lubuva imesema kuwa kwa Mamlaka waliyopewa kwa mujibu wa vifungu vya 35B(1), (3) (a), 37 (1) (a) na 46 (1) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,  Sura ya 343, shughuli za uchaguzi zinatarajia kuanza hivi karibuni.
  Taarifa hiyo imefafanua kuwa  Uteuzi wa wagombea Urais, Ubunge na Udiwani unatarajia kufanyika Agosti 21, 2015, na  kampeni za Uchaguzi kwa wagombea hao zitatarajia kuanza Agosti 22 mpaka - Oktoba 24 mwaka huu.
  Halikadhalika siku ya kupiga kura kwa wananchi wote inatarajiwa kuwa Oktoba 25, 2015 kwa wale waliojitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO


  IDARA YA HABARI (MAELEZO)

  S.L.P.  8031, Dar es Salaam, Simu: 2110585, 2122771/3, Fax: 2113814, e-mail: maelezopress@yahoo.com

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  SERIKALI YA TANZANIA NA UNESCO KUADHIMISHA WIKI YA

  UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA NA KUZINDUA MRADI WA NYARAKA ZA URITHI WA TANZANIA


  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalo shughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) itaadhimisha Wiki ya Ukombozi wa Bara la Afrika kuanzia tarehe 25 hadi 29 Mei, 2015 kwa kufanya maonesho ya picha na kumbukumbu mbalimbali zinazoonesha na kuelezea harakati za ukombozi wa bara la Afrika pamoja na midahalo mbalimbali itakayowahusisha wasomi na baadhi wa watu mashuhuri walioshiriki katika harakati za ukombozi.


  Maadhimisho hayo yatatanguliwa na uzinduzi wa Mradi wa Nyaraka za Urithi wa Tanzania (TAHAP) utakaofanyika tarehe 25 Mei, 2015 katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam. Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Mhe. Bernard Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


  Mradi wa Nyaraka za Urithi wa Tanzania unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na UNESCO ukikamilika unaatarajia kuweka na kutunza  kumbukumbu na nyaraka mbalimbali zinazohusu harakati za ukombozi wa bara la Afrika na ushiriki wa Tanzania kama mwenyekiti wa iliyokuwa Kamati ya nchi za mstari wa Mbele katika kuzikomboa nchi na kuvijengea uwezo vyama vya wapigania uhuru kusini mwa bara la Afrika.


  Miongoni mwa matukio muhimu katika maadhimisho hayo ni mdahalo utakaohusu Mchango wa vyama vya Siasa katika harakati za Ukombozi utakaoongozwa na Mhe. Salim Ahmed Salim na Wazungumzaji Wakuu watakuwa ni Prof. Issa Shivji na Mhe. Ibrahimu Kaduma, aliyewahi kuwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


  Mdahalo mwingine Utajikita katika kuangalia "Mchango wa Wapiganaji/Wanajeshi katika harakati za Ukombozi" tarehe 26 Mei, 2015 utakaofanyika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam utakaoongozwa na Prof. Penina Mlama na Wazungumzaji Wakuu watakuwa Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Brigedia Jenerali Ananias Mwanga.


  Tarehe 27 Mei, 2015 kutakuwa na mdahalo mwingine kuhusu "Mchango wa Wanawake katika harakati za ukombozi" utakaoongozwa na Prof. Ruth Meena na wazungmzaji wakuu watakuwa ni Dkt. Alexander Mkulilo na Mhe. Balozi Getrude Mongela (MB). Mdahalo huu utafanyika katika ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu Cha Dar es salaam.


  Mdahalo kuhusu "Mchango wa vyombo vya habari Wakati wa Harakati za ukombozi" utafanyika Chuo Kikuu  Huria Cha Tanzania tarehe 28 Mei, 2015 na kufuatiwa na  mdahalo kuhusu "Mchango wa Wasanii na Watunzi katika Harakati za Ukombozi" tarehe 29 Mei, 2015 utakaofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa. Mdahalo huo utaongozwa na Mzee Walter Bgoya. Wazungumzaji wakuu katika mdahalo huo watakuwa Prof. Penina Mlama na Bw. Zahiri Zahoro.


  Maadhimisho hayo yatafungwa Rasmi na Mhe. Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo tarehe 29 Mei, 2015.


  Vyombo vya habari vinaombwa kushiriki kwa kuandika na kutangaza Matukio hayo muhimu katika kutunza kumbukumbu za ukombozi wa bara la Afrika katika mikono ya wakoloni na utawala dhalimu wa Afrika Kusini.   MKURUGENZI IDARA YA HABARI (MAELEZO)


  0 0

   Katibu Mkuu wa Sirika la Dawa Asili na Ulizi wa Mazingira Boniventure Mwalongo akifafanuaa jambo mbele ya waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusiana na Maadhimisho ya kimataifa ya kuongeza ufahamu juu ya Ualbino katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam Leo katikati ni Mwenyekita wa Chama Cha Maalbino Tanzania (TAS), Kassimu Kirwe na Katibu Mkuu Ziada Nsembo.
  Katibu Mkuu wa TAS, Ziada Nsembo akizungumza na waandishi wa habari Hawapo pichani katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo,kushoto ni Mwenyekita wa Chama Cha Maalbino Tanzania (TAS), Kassimu Kirwe.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia kwenye Mkutno  wa TAS  jijini Dar es Salaam leo katika Ukumbi wa Idara Habari MAELEZO. PICHA NA EMMENUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.

  Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya kimataifa ya kuongeza ufahamu juu ya Ualbino ambayo yameandaliwa na Chama Cha Maalbino Tanzania yatayofanyika Juni 13 mwaka huu  jijini Arusha.


   Hayo yamesemwa na Mwenyekita wa Chama Cha Maalbino Tanzania (TAS), Kassimu Kirwe wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.


  Kirwe, amesema kuwa  maadhimisho hayo yanalengo la kuwaelimisha wananchi juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) kuwa ni watu wa kawaida kasoro yao ni upungufu wa baadhi ya seli zinazosaidia kutengeneza rangi ya ngozi tuu na sio kitu kingine.


  Ameongeza kuwa watu wenye ualbino  ukiwaua au kukata viongo vyao huo ni upotofu wa imani tuu na ni imani za kishirikina  inatakiwa kuepukana na tabia ambazo hazituletei faida yoyote.


  Nae Katibu Mkuu wa TAS, Ziada Nsembo amesema kuwa nchi zitakazo shiriki katika  maadhimisho hayo  ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda Malawi, Uingereza,Marekani na Swideni pia nchi nyingine zinaendelea kujiandikisha ili kuungana ili kutokomeza na kutoa Elimu juu ya watu wenye ualbino.


   Maadhimisho hayo hapa nchini yanaratibiwa na Chama Cha Maalbino Tanzania (TAS),Serikali chini ya Ustawi wa Jamii,Jukwaa la Tiba Asili Tanzania shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania New hope Family, Upendo Daima, Shirika la Dawa Asili na Ulizi wa Mazingira.

older | 1 | .... | 534 | 535 | (Page 536) | 537 | 538 | .... | 1903 | newer