Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 529 | 530 | (Page 531) | 532 | 533 | .... | 1897 | newer

  0 0  Kibiki azizungumza na kijana, fundi viatu wa mjini Iringa!


  Na mwandishi wetu, Iringa
  VIJANA wa stendi kuu ya mabasi ya mjini Iringa, wameanzisha timu ya mpira wa miguu ya ‘Kibiki Football Club’ili kuunga mkono harakati za mwanahabari wa gazeti la Uhuru na mzalendo, baada ya kutangaza nia kuwania jimbo hilo.
   
  Katibu wa timu hiyo, Charles Manet alisema wameamua kuanzisha timu ya mpira wa miguu inayoitwa Kibiki, ili kuonyesha dhamira yao ya dhati katika kumsaidia kijana mwenzao.


  “Yeye mwenyewe hakujua kama tumetumia jina lake kwenye timu yetu, tayari tumeshacheza mechi mbili tangu timu yetu ianze kuitwa Kibiki FC na tunatarajia kuendelea kucheza mechi za kirafiki, tukianza na timu ya Wambi ya stendi kuu ya mjini Mafinga,”alisema.


  Maneti alisema wamekuwa wakisafiri kwa kuchangishana fedha na kwamba tayari wamepata jezi seti moja, kutoka kwa wadau mbali mbali wa michezo mjini Iringa. Aliwataka wapenzi wa soka la mjini Iringa kuunga mkono jitihada za vijana hao katika kuhakikisha, timu hiyo inasonga mbele badala ya kuikatisha tama.


  “Pamoja na kukatishwa tama tangu tuunde timu hii lakini ukweli ni kwamba, hatutaacha kwa sababu Kibiki ni kiongozi na tusipomuunga mkono kijana mwenzetu tutakuwa hatujamtendea haki hata kidogo,”alifafanua.


  Kabla ya kuunda timu hiyo vijana hao, walichangishana fedha zaidi y ash laki moja na kumkabidhi Kibiki, wakimtaka azitunze kwa ajili ya kuchukulia fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Iringa, muda ukifika.


  Wakizungumzia ubunge, vijana hao walisema kuwa jamii ya wana Iringa inatarajia kumpata kiongozi anayetokana na wenyewe, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ili wampigie kura ya kuwa mbunge wa jimbo hilo na sio vinginevyo. Tangu alipotangaza nia ya kuwania jimbo hilo, Kibiki amekuwa akikubaliwa na makundi mbalimbali wakiwemo vijana, walemavu, wanawake na wazee.

  0 0

   Msanii wa kikundi cha ngoma ya Mganda akitumbuiza  wakati wa mapokezi ya Rais wa Msumbiji Mhe Filipe Nyusi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere
   Ngoma ya mganda 
   Sindimba 
   Kinamama wa kikundi cha Mount Usambara hawako nyuma
   Rais Kikwete akisogea sehemu ya kumpokea mgeni
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernad Membe akisalimiana na balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Mhe  Shamim Nyanduga. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Mhe Hawa Ghasia
   Rais Kikwete akiongea na Flower girl Elizabeth Jackson aliye tayari kumkabidhi mgeni shada
   Rais Nyuzi akitelemka katika ndege baada ya kuwasili
   "....Karibu nyumbani..." anasema Rais Kikwete anapomlaki Rais Nyusi
   Wanakumbatiana kwa furaha
   Rais Nyusi anapokea shada la maua kutoka kwa mtoto Elizabeth
   Rais Nyusi anamshukuru Elizabeth kwa maua
   Rais Nyusi akitambulishwa kwa balozi Shamim Nyanduga
   Rais Nyusi akitambulishwa kwa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Saidi Mwambungu
   Rais Nyusi akitambulishwa kwa wasaidizi wa Rais

   Rais Kikwete na Mgeni wake wanasimama jukwaa maalumu wakati wa nyimbo za Taifa zikipigwa
   Askari hodari wakipiga mizinga 21 kwa mbali kule
   Rais Nyusi anakaribishwa kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa heshima yake
   Rais Nyusi anakagua gwaride 
   Rais Nyusi anaendelea kukagua gwaride 
   Rais Kikwete anatambulishwa wa ujumbe alioongozana nao Rais Nyusi
   Rais Nyusi anafurahia ngoma
   Rais Nyusi anawasili hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro na kulakiwa na meneja mkuu wake
   Rais Kikwete akitambulishwa kwa maafisa waliooongozana na Rais Nyusi
   Mamia ya wananchi wakimsubiri mgeni Ikulu
   Rais Kikwete akiongea na badhi ya vijana waliojitokeza kumpokea Rais Nyusi Ikulu
    Rais Kikwete akiongea na badhi ya vijana waliojitokeza kumpokea Rais Nyusi Ikulu
    Rais Kikwete akiongea na badhi ya vijana waliojitokeza kumpokea Rais Nyusi Ikulu
    Rais Kikwete akiongea na badhi ya vijana waliojitokeza kumpokea Rais Nyusi Ikulu
   Zuria jekundu na wananchi vikimsubiri mgeni
   Rais Nyusi alakiwa kwa nderemo
    Rais Nyusi akilakiwa kwa shangwe
   Rais Kikwete akipeana mkono na mgeni wake baada ya mapokezi makubwa
   Sehemu ya wanahabari wa Tanzania na Msumbiji wakiwa kazini 
   Rais Kikwete katika mazungumzo rasmi na mgeni wake 
   Rais Nyusi akimkabidhi mwenyeji wake zawadi
   Rais Kikwete akimkabidhi mgeni zawadi yake
   Rais Kikwete na mgeni wake wakiongea kabla ya dhifa ya kitaifa aliyomwandalia
   Rais Kikwete na mgeni wake na mawaziri wa nchi zao wakiongea kabla ya dhifa ya kitaifa aliyomwandalia
    Rais Kikwete na mgeni wake katika dhifa ya kitaifa aliyomwandalia
    Rais Kikwete akihutubia wakati wa  dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais Nyusi
   Rais Kikwete agonganishwa glasi na mgeni wake wakati wa  dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais Nyusi
   Rais Nyusi akitoa hotuba yake
   Sehemu ya mawaziri na mabalozi
   Sehemu ya viongozi mbalimbali
   Mabalozi wa nchi mbalimbali walioalikwa
   Mabalozi
   Mawaziri na mabalozi
   Rais Kikwete akigonganisha glasi na mgeni wake
   Mawaziri wakigonganisha glasi
   Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na waalikwa wengine
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Paul Makonda (kushoto), Mbunge wa Singida Mhe. Mo Dewji, Mwenyekiti wa Yanga Bw. Yusuf Manji na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye
  Baadhi ya maafisa wa protokali wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa. Picha zote na IKULU

  0 0


  0 0  0 0

  Q1
  Jumanne Ali Ligopora Mkurugenzi wa Taasisi ya Ulamaa Qaswida Promotion Centre akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Traveltine Magomeni jijini Dar es salaam wakati akizungumzia mashindano ya kuimba Qaswida yatakayofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa,ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernald Membe.Tamasha hilo litafanyikaMei 25 kuanzia saa saba mchana, Kulia ni Sheikh Muharami Pembe na kushoto ni Ustaadhi Jumanne Gereza.
  Q2
  Jumanne Ali Ligopora Mkurugenzi wa Taasisi ya Ulamaa Qaswida Promotion Centre akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wa taasisi hiyo wakizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Traveltine Magomeni jijini Dar es salaam kuhusu Tamasha la Qaswida litakalofanyika Mei 25 kwenye viwanja vya Sekondari ya Benjamin Wiliam Mkapa Kariakoo.
  Q3
  Jumanne Ali Ligopora Mkurugenzi wa Taasisi ya Ulamaa Qaswida Promotion Centre akisisitiza jambo katika mkutano huo.

  0 0

  Karibu kwenye sehemu ya kwanza kati ya mbili za mahojiano yetu na Katibu Uenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania.
  Ameeleza mengi akianza na Hali ya chama hivi sasa.
  KARIBU

  0 0

  Na Abou Shatry Washington DC Watanzania walioko nchini Marekani, wamechangisha zaidi ya Dola 3,550 kwa ajili ya kumsaidia ndugu Moh'd Said Moh'd anayehitaji kwenda nchini India kwa matibabu.
  Bi Moza Moh'd Khamis akitoa maelezo machache, Maryam Shaaban kulia, pamoja na Bi Asha Haris, Picha zote na (swahilivilla.blogspot.com) Akifungua shughuli hiyo iliyofanyika May 17, katika Jimbo la Meryland nchini Marekani na kuzijumuisha jumuiya mbali mbali za Kitanzania, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari nchini humo (ZADIA) Bwana Omar Haji Ali, alisema kwamba mkusanyiko huo ni kielelezo cha umoja, upendo na mshikamano miongoni mwa Watanzania. Katika maelzo yake ya ufunguzi yaliyokamilishwa na dua, Bwana Omar alisisitiza kuwa harambee hiyo iliyofanykika nchini Marekani kwa ajili ya kumsaidia kijana aliyeko Zanzibar, ni uthibitisho kuwa jumuiya za Kitanzania nchini humo zina azma ya kuchangia kidhati katika ustawi wa Tanzania na watu wake.
  Mwenyekiti wa Zanzibar Diaspora Association (ZADIA) ndugu Omar Haji Ally akifungua harambee kwa dua.

  Mbali na fedha taslimu, baadhi ya wasamaria wema, walichangia vitu vya aina mbalimbali vya Kitanzania ambavyo viliuzwa kwa mnada na kuweka nyongeza kwenye fungu hilo.

  Miongoni mwa vitu hivyo ni pamoja na mavazi kama vile kanga, vikoi, kanzu na vyenginevyo, ambavyo vilisasambuliwa chini ya MC Mayor Mlima, Abou Shatry, pamoja na washika fedha katika harambe hiyo Bi Asha  Haris na Bi Sarah Towa.

  Akizungmza katika shughuli hiyo, mama mzazi wa Moh'd, Bi Moza Moh'd Khamis alielezea shukurani zake za dhati kwa wale wote walioitikia wito wa harambee hiyo. "Nawashukuru ndugu zangu muliokuja hapa kuniunga mkono juu ya swala la huyu mtoto", alisema Bi Moza katika sauti iliyochanganyika na kilio na huzuni za uchungu wa uzazi.
  Bi Moza Moh'd Khamis na mumewe Sarai Mfaume Sarai, walipoungana  na waTanzania wa DMV katika harambee ya kumsaidia Moh'd Said Moh'd anayehitaji kwenda nchini India kwa matibabu.

  Aliendelea kusema kuwa, mtoto wake amekuwa akisumbuliwa na maradhi tangu akiwa na umri wa miaka mitano, na hivi sasa akiwa na umri wa miaka 25, imebainika kuwa mafigo yake yameharibika. Kutokana na hali hiyo, Moh'd aliyeko hospitalini nchini Tanzania, anahitaji kwenda nchini India kwa ajili ya upandikizaji wa figo.

  Naye babu wa kijana Moh'd mzee Shaaban Kassim Said, alielezea shukurani zake kwa wale wote walijitokeza katika mkusanyiko huo. Katika dua aliyoitoa ufungaji wa shughuli hiyo, mzee Shaaban alisema kuwa, kamwe hawezi kuwalipa wale wote waliochangia, na kwamba malipo yao yako kwa Mungu.

  Mbali na michango iliyokusanywa hapo, Katibu mkuu wa ZADIA Shamis Al Khatry amesema kuwa, bado michango inaendelea kupokelewa, na kwamba wale wote wanaotaka kufanya hivyo wanaweza kuchangia ama kwa fedha taslimu au kwa kupiti gofundme.com
   Mzee Shaaban Kassim Said akisoma dua pamoja na shukuran
   Katibu mkuu wa ZADIA Shamis Al Khatry akipongeza wanakamati pamoja na kusisitiza michango
    Bi Asha  Haris pamoja na Bi Sarah Towa wakifanya hesabu za michango

  0 0
 • 05/18/15--01:40: MCHUMA UNAUZWA

 • YEAR ; 2005

  MILEAGE ;78789

  ENGINE ;PETROL 2.5

  GEAR; AUTOMATIC / MANUAL

  SEAT; LEATHER

  WHEELS;ALLOY / NEW TYRES

  ROOF;SUN ROOF

  DUTY; FULLY PAID

  STERLING ; RIGHT HAND DRIVE 


  FOR MORE INFO;
  CONTACT  0713250594 CALL /WHATSAPP
  KAWAIDA;

  0 0

  Balozi wa Heshima wa Djibhout nchini Tanzania Balozi Said Amin Shamo akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha mazoezi Universal Body Fitness kilichopo ndani ya jengo la Shamo Tower,Mbezi beach jijini dar,hafla hiyo imefanyika mwishoni mwa wiki.
  Makofi na shangwe za furaha zilisikika mara baada ya Balozi wa Heshima wa Djibhout nchini Tanzania Balozi Said Amin Shamo kukata utepe wa kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha mazoezi Universal Body Fitness kilichopo ndani ya jengo la Shamo Tower,Mbezi beach jijini dar,hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
   Mkurugenzi wa Universal Body Fitness Bi.Mariam Shamo wa kwanza kulia akiwa na wageni waliohudhuria ufunguzi huo.
   Sehemu ya mazoezi yakiendelea kwa wshiriki wa Universal Body Fitness
  Pichani shoto ni  Mkurugenzi wa Universal Body Fitness Bi.Mariam Shamo akiwa na baadhi ya wafanyakazi,mara baada ya kufanyika uzinduzi wa kituo hucho kilicho na vifaa vya kisasa.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA 

  0 0

   Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi Dorothy Mwanyika akifungua Warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari kuhusu wajibu wa vyombo vya habari katika kutoa mchango wake kwenye manunuzi ya umma, katika maadhimisho ya miaka kumi ya  Mamlaka ya Udhibiti na Manunuzi ya Umma (PPRA) iliyoanzishwa mwaka 2005, iliyofanyika leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee VIP, jijini Dar es salaam. Uzinduzi rasmi wa Maadhimisho hayo unataraji kufanyika Kesho Mei 19, 2015 katika ukumbu huo huo wa Diamond Jubilee, Huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa, Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya. 
  Mwenyekiti wa bodi ya  Mamlaka ya Udhibiti na Manunuzi wa Umma (PPRA), Balozi Dkt. Matern Lumbanga akifafanua jambo kwa
  baadhi ya Wadau wa habari (hawapo pichani),kwenye semina ya Wadau wa Habari na PPRA kuhusiana na wajibu wa vyombo vya habari katika kutoa mchango wake kwenye manunuzi ya umma,ambayo imefanyika leo ndani ya ukumbi wa Diamond VIP jijini Dar es salaam.
   Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Manunuzi ya Umma (PPRA), Dkt. Laurent Shirima akizungumza mbele ya baadhi ya Wadau wa habari (hawapo pichani),kwenye semina ya Wadau wa Habari na PPRA kuhusiana na wajibu wa vyombo vya habari katika kutoa mchango wake kwenye manunuzi ya umma,ambayo inafanyika leo ndani ya ukumbi wa Diamond VIP jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya Wadau wa habari wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi.  Dorothy Mwanyika (wa tano kulia) na baadhi ya viongozi wakuu wa Mamlaka hiyo kwenye semina ya Wadau wa Habari na PPRA kuhusiana na wajibu wa vyombo vya habari katika kutoa mchango wake kwenye manunuzi ya umma,ambayo inafanyika leo ndani ya ukumbi wa Diamond VIP jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa PPRA wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Dorothy Mwanyika (wa tano kulia) na baadhi ya viongozi wakuu wa Mamlaka hiyo kwenye semina ya Wadau wa Habari na PPRA kuhusiana na wajibu wa vyombo vya habari katika kutoa mchango wake kwenye manunuzi ya umma,ambayo inafanyika leo ndani ya ukumbi wa Diamond VIP jijini Dar es salaam.Picha na Michuzi Jr.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Kamati ya maandalizi ya Maonyesho ya Biashara ya China 'Expo Central China 2015', wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa 'Wuhan International Exhibition Centre VVIP Room'. Mkutano huo umeanza leo Mei 18 2015 jijini Wuhan, Jiombo la Hubei.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akiwa na baadhi ya Viongozi wa nchini China, Katibu wa Chama Tawala cha CPC cha Nchini China, Jimbo la Hubei, Li Hongzhong (kushoto) na wengine, wakati alipofungua Maonesho ya Biashara ya China 'Expo Central China 2015', yaliyoanza leo Mei 18, 2015, Jimbo la Hubei, Jijini Wuhan nchini China.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na Katibu wa Chama Tawala cha CPC cha Nchini China, Jimbo la Hubei, Li Hongzhong (kushoto) wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara ya China 'Expo Central China 2015'.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza wa na Katibu wa Chama Tawala cha CPC cha Nchini China, Jimbo la Hubei, Li Hongzhong, baada ya kuzungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa China, Wang Yang, wakati walipokutana kwa mazungumzo baada ya Makamu kufungua rasmi Maonesho ya Biashara ya China, leo Mei 18, 2015 kwenye Ukumbi Mikutano wa 'Wuhan International Exhibition Centre, jijini Wuhan Jimbo la Hubei nchini China.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Maonesho ya Biashara ya China, 'Expo Central China 2015', ulioanza leo Mei 19, 2015 kwenye ukumbi wa mikutano wa 'Wuhan International Exhibition Centre, uliopo Jijini Wuhan Jimbo la Hubei nchini China. Picha na OMR.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mh. Dk. Rehema Nchimbi akifungua kikao kazi cha biashara ya kilimo kwa kongani ya Ihemi iliyoandaliwa na SAGCOT (Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania) kwa ushirikiano na UONGOZI Institute (Taasisi ya Uongozi Afrika kwa Maendeleo Endelevu) mapema leo Iringa mjini. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kilimo wa TCCIA Bi. Magadalena Mkocha, Mwenyikiti wa Bodi ya Agricultural Council of Tanzania Dk. Sinare Y. Sinare, DC wa Iringa Mh. Angeline Mabula, DC wa Mufindi Mh. Mboni Mhita na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Philemon Luhanjo.
  Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Philemon Luhanjo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa bodi ya UONGOZI Institute akitoa salaam kwa niaba ya taasisi hiyo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha biashara ya kilimo kwa kongani ya Ihemi inayoendelea Iringa mjini. UONGOZI Institute imeshiriki katika kuwezesha kikao kazi hicho.
  Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT, Bw. Geoffrey Kirenga akitoa utangulizi wa mada ya biashara ya kilimo kwa nyanda za juu kusini. Mkutano huu wa siku mbili unakutanisha viongozi wa serikalini, sekta binafsi, mashirika ya kimataifa pamoja na wakulima kwa ajili ya kujadili kuhusu kuboresha biashara ya kilimo nchini kwa nyanda za juu kusini.
  Picha ya pamoja ya wageni waalikwa na washiriki wa kikao kazi cha biashara ya kilimo inayoendelea Iringa mjini. Mada zinazojadiliwa ni pamoja na wajibu wa viongozi katika kuleta mageuzi katika kilimo.

  0 0

  1
  Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Ester Riwa akiongea na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Bw. Martin Mtani wakati wa ziara ya mafunzo ya ujasiriamali na jinsi ya kujikomboa kiuchumi kwa Vijana wa Halmashauri hiyo mkoani Ruvuma.wa kwanza kushoto ni AfisaVijana kutokaWizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. AminaSanga. (Pichana Benjamin Sawe-WHVUM)
  2
  Mkuu wa Kitengo cha SheriaWizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Ester Riwa akiongea na Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo juu ya umuhimu wao wakujishughulisha naujasiriamali ili kukuza uchumi wa taifa na kujikomboa kiuchumi.
  3
  Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akitoa mada ya jinsi ya mfuko wa Vijana unavyoweza kuwasaidia vijana wa Halmashauri ya Namtumbo Mkoani Ruvuma wanaokidhi vigezo vya ujasiliamali ili kujiinua Kiuchumi.4
  Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Namtumbo akitoa mada kwa vijana wa Halmashauri hiyo juu ya uanzishwaji wa Saccos ikiwa ni juhudi za Serikali kuwainua vijana kiuchumi

  ……………………………………………………………………
  Benjamin Sawe Namtumbo-WHVUM
  Serikali imewaasa vijana kujiepusha na ngono zembe ikiwa ni pamoja na kujiepusha na matumizi ya  dawa zakulevya ili waweze kujiletea maendeleo yao na kujiinua kiuchumi.
  Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa mafunzo elekezi ya jinsi ya kujikwamua kiuchumi kwa vijana  wa halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo.
  Alisema vijana kujihusisha na ngono zembe na matumizi ya dawa za kulevya kutawafanya kuwa dhaifu na kushindwa kuchangia katika ujenzi wa taifa na kujiinua kiuchumi.
  “Nawashauri msijihusishe na ngono zembe na matumizi ya dawa za kulevya kwani mikopo mtakayoipata mtashindwa kuirejesha kwa wakati hivyo mtaisababishia serikali hasara kubwa”.Alisema.
  Bibi.Riwa amesema kuwa jitihada za awali zifanywe na vijana wenyewe kwa kuwa na mwamko wa kuleta maendeleo yatakayotokana na miradi endelevu na yenye malengo kwani kwakufanya hivyo wataweza kukabiliana na hali ya maisha ya dunini kuwa mfano katika jamii na taifa kwaujumla.
  Aidha Afisa Maendeleo ya Vijana Wilaya ya Namtumbo Bi.Rahiya Nasser.amewataka vijana wa Namtumbo kutokupenda kubebwa kwakupewa fedhaza bure kwa kununuliwa na wanasiasa bali wazidi kujijengea mazoea ya kuwekeza na kuchukua mikopo inayotolewa na Serikali kwa vijana yenyeriba nafuu na kurejesha fedha hizo kwa wakati ili vijana wengine waweze kufikiwa na fursahiyo.
  Akizungumza na vijana wakati wa semina hiyo Afisa Ushirika Halmashauri ya Wilaya  hiyo Bw. Theophily Ngonyani amewataka vijana kutokuwa watu wakusukumwa kutafuta maendeleo yao bali wawajibike na kutafuta fursa zilizopo ili kuweza kuondokana na hali duni ya maisha.
  “Vijana wenzangu hamjazaliwa kuishia hapo mlipo, msipende kusukumwa na watu kutafuta maendeleo yenu ,changamkieni fursa zilizopo na kuwajibika katika jamii zenu bila ya kuwa na ubaguzi wakijinsia kwani Namtumbo haitakiwi kuwa kama ilivyosasa” alisemaBw. Ngonyani

  0 0

  Aliyewahi kuwania jimbo la Arumeru Mashariki kupitia CCM  Sioi Sumari akijinadi mbele ya Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha Edward Lowassa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo Mh. Lowassa alikuwa mgeni rasmi. (Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
  SAM_2676 
  Mbunge wa Viti Maalum, Namelock Sokoine akinadaiwa na Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha Edward Lowassa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo Mh. Lowassa alikuwa mgeni rasmi.
  ………………………………
  Baadhi ya wagombea waliotangaza nia kuwania ubunge katika majimbo mbalimbali mkoani Arusha  kupitia CCM juzi walionekana kupigana vikumbo na wengine wakijinadi mbele ya waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani hapa Edward Lowassa.

  Lowasa,ambaye anatajwa kuwania urais kupitia CCM mwaka huu mwishoni mwa wiki iliyopita aliendesha harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi uliopo wilayani Arumeru mkoani Arusha akimwakilisha makanu wa Rais,Dk Mohammed Billal na kufanikiwa kukusanya zaidi ya kiasi cha sh,235 milioni ikiwa ni zaidi ya makisio ya msikiti huo kukusanya sh,200 milioni .

  Baadhi ya watia nia wa CCM walionekana wakichangia fedha katika harambee hiyo huku wengine wakitumia mwanya wa kunadi sera pindi walipokaribishwa jukwaa kuu.

  Wagombea hao watarajiwa wa ubunge ni Mustapha Panju alitoa Sh6 milioni, Sioi Sumari (Sh7 milioni), Kim Fute (Sh3 milioni), Philemon Mollel (Sh5 milioni), mbunge Peter Serukamba (Sh3 milioni) na mjumbe wa NEC kutoka jimbo la Busega, Dk Raphael Chegeni alichanga Sh1 milioni sawa na mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Namelock Sokoine.

  Hatahivyo,wakati wagombea hao kwa nyakati tofauti mara walipofika kuchangia harambee hiyo na kupewa nafasi ya kusema neno ndipo badhi yao walisikika wakinadi sera kitendo kilichopelekea kuibua shangwe kwa wahudhuriaji.

  Mke wa mtia nia wa CCM,Violet Mfuko ambaye mmewe ametangaza nia,Kim Fute alifika jukwaa kuu na kumnadi mmewe kwa kumwambia Lowasa kwamba ametangaza nia na kuwataka makada wa CCM kumuunga mkono.

  “Mheshimiwa waziri mkuu mme wangu ametangaza nia jimbo la Arusha mjini,mimi ni mke wake nawaomba jamani mumuunge mkono”alisema Mfuko na kuibua shangwe

  Hatahivyo,mtia nia mwingine wa CCM jimbo la Monduli mkoani Arusha,Sokoine naye alipopanda jukwaani Lowasa alitumia nafasi hiyo kumnadi kwa kuwataka makada wa CCM kumuombea kwa Mungu mambo yake yaende vizuri.

  “Jamani huyu naye ametangaza nia huko Monduli tumuombee kwa Mungu mambo yake yaende vizuri “alisema Lowasa

  Hatahivyo,Sumari,Monaban,Panju na baadhi ya wagombea wengine walipanda jukwaa kuu na kisha kujitambulisha kabla ya kuchangia fedha huku wakitamka ya kwamba wanaomba mambo yao yaende vizuri  ili wapitishwe kugombea ndani ya CCM.

  0 0

  Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi kwa kipindi cha miaka 15 kwa tiketi wa CCM,Elisa Mollel akizungumza na waandishi wa habari kuhusu nia yake ya kuwa Mbunge jimbo la Magharibi
  (Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog).
  SAM_2643Mwaandishi wa habari mwandamizi wa gazeti la Mwananchi kulia Mosses Mashala akifanya mahojiano na aliyewahi kuwa mbunge jimbo la Arumeru Magharibi Elisa Mollel,kulia ni anayetajwa kuwania jimbo la Arusha mjini Victor Njau.
  ……………………………………………………..
  Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi kwa tiketi wa CCM,Elisa Mollel ametamka ya kwamba atatangaza uamuzi wa kugombea jimbo hilo au la pindi muda utakapowadia kwa kuwa ana uzoefu mkubwa na siasa za jimbo hilo.
   
  Mbali na kauli hiyo Mollel amesema kuwa kwa muda mrefu amekuwa akifuatwa na makundi ya watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa mila maarufu kama Malaigwanani,viongozi wa dini,wakinamama wakimshawishi agombee ubunge mwaka huu.
   
  Hadi sasa makada mbalimbali kupitia CCM wilayani Arumeru Magharibi wametangaza nia ambao ni Mathias Manga,Robinson Meitinyiku,Thomas Ole Sabaya pamoja na mbunge wa sasa wa jimbo hilo,Goodluck Ole Medeye.
   
  Akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini Arusha Mollel alisema kuwa tangu alipong”atuka katika utumishi wake baadhi ya wananchi wilayani humo wamekuwa wakimfuata na kumtaka achukue fomu kwa madai mambo hayaendi sawa.
   
  “Wananchi wananifuata na kuniambia mzee mambo ni hovyo tangu ulipoondoka,nimefuatwa na makundi mengi tu na mimi nasema muda ukifika nitasema jambo”alisema Mollel
   
  Hatahivyo,alisisitiza ya kwamba tangu ang”atuke miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakimsikitisha ni pamoja na ubovu wa miundombinu,kero ya maji sanjari na kero ya migogoro ya ardhi matatizo aliyodai yameshindwa kutatuliwa na mrithi wake.
   
  Hatahivyo,alisema kuwa miongoni mwa mambo ambayo anajivunia hadi sasa ni pamoja na rekodi yake ya kuboresha sekta ya elimu wilayani humo ambapo aliondoka huku akiwa amefanikiwa kuacha shule za sekondari 26 tofauti na alipoingia madarakani.
   
  “Hapo awali tulikuwa na watoto wengi sana wanamaliza elimu ya msingi lakini hawaendi sekondari nimeondoka na kuacha shule za sekondari 26 katika kila kata najivunia kwa hili”alisema kwa kujiamini

  0 0

  Mwonekano wa jengo la kushushia na kupandiashia abiria linaloendelea kujengwa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.2
  Mshauri Mkaazi wa ujenzi wa jengo la kufikia abiria  katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere akimwonyesha Naibu Katibu Mtendaji- Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Bibi. Florance Mwanri (Kulia) maendeleo mradi huo.3
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Bw. Suleiman S. Suleiman akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo la kupikia na kushushia abiria kwa Naibu Katibu Mtendaji- Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Bibi. Florance Mwanri alipotembelea mradi huo.4
  Mafundi wakiendelea na shughuli za ujenzi wa jengo jipya katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.5
  Hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo hilo. 

  ………………………………………………………………………
  Uongozi wa Mamlaka za Viwanja vya Ndege Tanzania wameshauriwa kuwa makini katika ujenzi unaoendelea wa jengo la kutua na kupaa ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyere (JNIA).
  Ujenzi huo unaotarajiwa kuongeza uwezo wa uwanja wa mara tatu zaidi umejikita katika sehemu za maegesho ya magari, sehemu ya abiria kupumzika, sehemu za abiria kupandia na kushuka kwenye ndege, ofisi za uhamiaji na huduma zingine muhimu.
  Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Suleiman S. Suleiman amesema kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) hapo awali kilikuwa na uwezo wa kuruhusu ndege sita tu kutua kwa saa lakini kwa sasa unaweza kuruhusu ndege hadi 30. Tunatarajia kuongeza ndege zaidi na hivyo kuufanya kiwanja hiki kuhimili 2500 tofauti na abira 700 wa awali pindi ujenzi huu utakamilaka.
  Kwa sasa ujenzi umefikia asilimia 85, katika awamu ya kwanza ambayo inategemewa kukamilika Juni mwaka 2016 na itakiwezesha JNIA kuhudumia abiria milioni tatu na nusu kwa mwaka. Iwapo ujenzi wa awamu ya pili utakamilika mwaka 2017 JNIA kitakuwa na uwezo wa kuhudumia jumla ya abiria milioni sita kwa mwaka.
  Alipokuwa akitembelea mradi huo, Naibu Katibu Mtendaji- Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Bibi. Florance Mwanri, aliuambia uongozi wa Mamlaka hiyo kuzingatia wazo la kuwa na huduma zote za msingi katika kiwanja cha Julius Nyerere ili kuweza kushindana viwanja vya nchi jirani na barani Afrika kwa ujumla.
  “Ni vema kuwa kiwanja chetu cha ndege kinapanuliwa ili kiweze kuhudumia watu wengi zaidi, lakini nimegundua kuna vitu muhimu vimesahaulika katika usanifu wa upanuzi huu, kuna vitu kama hoteli, jengo la hospitali, sehemu za kupata huduma za kibenki na pia namna nzuri ya kuwapatia abiria watuao usafiri wa kwenda mjini na sehemu nyinginezo, nadhani haya pia yazingatiwe, alisema Bibi. Mwanri.
  Uwepo wa huduma hizi utawavutia abiria kutumia kiwanja chetu kuliko vya majira zetu na pia kutakuza mapto ya TAA na taifa kwa ujumla. Ujenzi huu unaoendelea umezingatia haja ya kuunganisha majengo yote matatu ili kurahisisha uunganishaji wa ndege za ndani na za nje pia upokeaji wa mizigo.
  Serikali kupitia Tume ya Mipango, imeshaanza kuandaa Mpango wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 wenye dhima ya kukuza uchumi wa kiviwanda hivyo basi Mamlaka ya  Viwanja vya Ndege inapaswa kuwa chachu ya mpango huu kwa kusafirisha watu na bidhaa zitakazozalishwa na viwanda hivyo”alisema Bibi. Mwanri

  0 0

  Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Bi Amina Shabani akifungua semina ya siku moja ya kujadili mpango utekelezaji wa Maendeleo ya Malengo ya Millenia MDG’s, iliyofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar na kuwashirikisha Maofisa Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Viongozi wa Taasisi zisizo za Kiserekali, ulioandaliwa na Tume ya Mipango Zanzibar na Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania na kufadhiliwa na UNDP.
  Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia hutuba ya Katibu Mtendaji Bi Amina Shabani akifungua mkutano huo.
  Mwakilishi wa UN Zanzibar Bi. Anna Senga akitoa salamu za Umoja wa Mataifa (UN) wakati wa mkutano wa kupitia mafanikio ya Maendeleo ya Malengo ya Millenia MDG’s.
  Washiriki wakiwa katika ukumbi wa Mkutano hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar. wakifuatilia mada zinazotolewa wakati wa mkutano huo.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi (ESRF), Dk Oswald Mashindano akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kupitia mafanikio ya Maendeleo ya Malengo ya Millenia MDG’s Tanzania uliofanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
  Washiriki wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakifuatilia kwa utulivu michango na mada zilizoku zikiwasilishwa.
  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano Wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy akiwasilisha mada jinsi mataifa yalivyofikia SDGs, michakato inayoendelea na namna ambavyo Tanzania inaweza kunufaika na mkakati mzima wa maendeleo.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi (ESRF), Dk Oswald Mashindano akiwasilisha mada ya “Elucidating SDG 17 on means of implementation and Global Partnership for Development and Financing of Post MDG’s Development Agenda”.
  Washiriki wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakifuatilia mada zinazowasilishwa na wahusika.
   
  Dk. Kenneth Mdadila, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam Idara ya Uchumi akiwasilisha mada ya “Tanzania’s preparedness in Monitoring Sustainable Development Goals- Analysis Based on Global Indicator Framework” katika semina hiyo..
   
  Pichani juu na chini ni washiriki wa semina ya siku moja ya kujadili Malengo ya Millenia baada ya 2015 iliyofanyika mwishoni mwa wiki visiwani Zanzibar.
  Pichani juu na chini ni Maofisa mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na viongozi wa taasisi zisizo za Kiserikali wakishiriki kuchangia mada katika semina hiyo ya siku moja iliyofadhiliwa na UNDP.
  Mdau Yasser Manu kutoka ESRF.
  Washiriki wakichangia mada zilizowakilishwa wakati wa semina ya siku moja iliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.

  ……………………………………………..
  Na Mwandishi wetu, Zanzibar
  UKOSEFU wa takwimu sahihi katika masuala mbalimbali umeelezwa kuchangia kutopiga hatua kwenye mipango ya kimaendeleo inayopangwa na serikali juu ya wananchi.
  Aidha upotoshaji wa takwimu hizo unaofanywa na baadhi ya watendaji kwa kutaka kujinufaisha wao wenyewe pia umekuwa ukichangia kuchelewa hatua za kimaendeleo.
  Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Zanzibar, Amina Shaaban wakati akifungua semina ya siku moja ya kujadili Malengo ya Millenia baada ya 2015 iliyofanyika mjini hapa.
  Amina alisema, kuwa takwimu ndiyo zinaonesha hali halisi na pia zinawezesha fedha kutoka kulingana na mahitaji, hivyo ni muhimu kuzingatiwa kwa jambo hilo ili mipango ya maendelo iweze kufanyika kwa wakati.
  “Kulikuwa na kamati ile ya ufundi na ya muda, siku hizi hazipo kama zimekufa ni vyema zikarudishwe tena maana zilikuwa na jukumu la ufuatiliaji na kutukumbusha mara kwa mara,” alisema Amina.
  Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi (ESRF), Dk. Oswald Mashindano alisema, semina hiyo inalenga kujadaili utekelezaji wa malengo ya millenia kabla ya kumalizika Septemba, mwaka huu na ajenda mpya ya maendeleo baada ya Septemba, mwaka huu.
  Aidha alisema, nchi nyingi hazijakuwa na uwezo wa kutekeleza malengo ya millenia ikiwemo Tanzania, hivyo kutokana na hali hiyo ilikubalika kuwepo kwa ajenda mpya ya maendeleo baada ya Septemba, mwaka huu.
  “Kwa sisi Tanzania kidogo tuna bahati ya kuiga hatua kidogo, lakini pamoja na kutimiza baadhi ya malengo, bado kuna maeneo ambayo hatujafanikiwa sana na moja kati ya sababu iliyofanya tukwame ni pamoja na ukuaji wetu wa uchumi,” alisema.
  Akizungumzia kuhusu kamati za ufundi na ya muda, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kiamatifa wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy alisema, kuwa suala hilo atalirudisha kwenye tume ya mipango ya Tanzania Bara ili liweze kushughulikiwa kwa wakati.
  Hata hivyo alisema, ili nchi iweze kupiga hatua katika mikakati ya maendeleo ni muhimu kwa sekta binafsi kushiriki kwa mstari wa mbele kutokana na kuwa nafasi kubwa katika kuendeleza maendeleo na uchumi wa taifa.
  “Sekta binafsi wao ndiyo wenye pesa nyingi sana kuliko serikali, ukiangalia hata katika nchi zilizoendelea sekta binafsi kwa kiasi kikubwa zimechangia sehemu kubwa ya maendeleo yao,” alisema Balozi Mushy.
  Balozi Mushy alisisitiza umuhimu wa takwimu sahihi kwa kuwa ndiyo silaha pekee katika kufanikisha mipango ya kimaendeleo kukamilika kwa wakati.
  Semina hiyo iliwashirikisha wataalamu wa tume ya mipango ya Zanzibar na tasisi zingine za serikali ilikuwa inalenga kuwajengea uwezo na kujadili ajenda 17 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na mipango ya maendeleo baada ya kukamilika kwa Malengo ya Maendeleo ya Millenia (MDGs) Septemba, mwaka huu.

  0 0

  IMG-20150518-WA0054
  CEO wa Makampuni ya MeTL Group na Mbunge wa Jimbo la Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji (kulia) katika picha ya pamoja na Rais wa Mozambique, Mh. Filipe Nyusi walipokutana jijini Dar es Salaam. Rais huyo anayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama Rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu nchini Tanzania.

  0 0

  Na Anitha Jonas – MAELEZO.

  Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation imeandaa  mkutano wa mashauriano  unaotarajia kufanyika tarehe Mei 19-20 mwaka huu, ambapo watajadili mambo mbalimbali kuhusu amani na utulivu wanchi ya Tanzania.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi  Mtendaji wa  Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation Bw.Joseph Butiku alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es  Salaam kuhusu maandalizi ya mkutano  huo na agenda za  mkutano huo.

  “Mkutano huu utahusisha viongozi wakuu wa Serikali  ikiwemo walioko madarakani na waliokwisha kustaafu,viongozi wakuu wa  Siasa na viongozi wa wakuu wa Dini na lengo kuu la kushirikisha viongozi  hao ni kutafakari na kujadili hali ya amani,umoja,na utulivu wanchi yetu kwa kuzingatia kuwa viongozi hao ndiyo wenye jukumu na wajibu wa kwanza wa kusimamia amani na umoja”,alisema Bw.Butiku.

  Mbali na hayo Bw.Butiku aliendelea kusema mkutano huo utajadili hoja mbalimbali  ikiwemo masuala ya ukosefu ya ajira kwa vijana,kutoa ufafanuzi wa kuhusu Muungano,muongozo wa elimu kwa taifa letu pamoja na uanzishwaji wa vikundi vya ulinzi ndani ya vyama vya siasa.

  Aidha hoja hizo ziliwasilishwa kwa wadau hao watakaoshiriki mkutano huo kwa ajili ya kutoa mapendekezo yao juu ya  hoja hizo na zaidi ya washiriki kumi na nne wametoa mapendekezo yao katika hoja hizo na zitakazojadiliwa
  .
  Kwa upande mwingine Bw.Butiku alisema muasisi  ya Mwalimu Nyerere  Foundation  Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alianzisha taasisi hiyo kwa lengo la kusimamia mwenendo wa amani na umoja kwa taifa na hivyo ndiyo maana wameandaa mkutano huo ilikujadili hatma ya taifa baada ya kuona uwepo kwa viashiria vinavyotishia amani na umoja. 

  Hata hivyo mkutano huo unatarajiwa kuwahudhiriwa na viongozi mbalimbali wakisiasa na wadini akiwemo Bw.Ibrahimu Lipumba (CUF),Bw.Wilbroad Slaa (CHADEMA),Bw.James Mbatia (NCCR) na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Taifa Bw.Abraham Kinana,Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Bw.Philip Mangula,Katibu Mwenezi (CCM) Bw.Nape Nauye na viongozi wa dini ni uongozi.

  0 0


  Maisha Lab ya Uganda wametangaza kuwa warsha yao nyingine itafanyika Zanzibar wakati wa ZIFF 2015 mwezi Julai kuanzia tarehe 18 hadi 25. Maombi toka kwa wanaotaka kushiriki katika warsha hii yameanza kupokewa na mwisho wa maombi ni tarehe 13 Juni.


  Warsha za Maisha Lab zimekuza vipaji vya waandishi wa filamu na wakurugenzi wa filamu wengi hapa Afrika Mashariki. Tayari warsha hizo zimefundisha zaidi ya watu 1000 tangu Maisha Lab ianzishwe.


  Mkurugenzi wa Maisha Lab aliyeko Kampala Uganda alisema kuwa wanataraji kutoa skolaship 60 kwa wanafunzi kwa mwaka kwa washiriki toka nchi zote za Afrika Mashariki. “Katika warsha zetu watu 60 (15 toka kila nchi) watachaguliwa kuhudhuria mafunzo hayo yatakayoongozwa na wakufunzi waliobobea katika fani za uandishi wa filamu. Nia ni kuongeza  ujuzi na kupanuwa wigo wa biashara ya utengenezaji filamu hapa Afrika Mashariki.” Alisema Fibby Kioria Mkurugenzi wa Maisha lab.


  Katika kila Warsha script zitashindanishwa na mshindi atapatiwa $5000 ili kumwezesha kutengeneza filamu fupi katika mwaka unaofuata. Mwaka jana Nassir Qassim wa Tanzania ndiye aliyeibuka mshindi.


  Hii ni warsha ya 3 itakayofanyika Zanzibar na ZIFF ndio mdhamini wake ili kuwapa washiriki nafasi ya kushiriki katika tamasha na hivyo kuweza kukutana na watengeneza filamu wengine toka nje wanaokuja kwa ZIFF. Pia wanapata nafasi ya kuangalia filamu tele zinazoonyeshwa wakati wa Tamasha.


  Lakini Mkurugenzi wa ZIFF aliharakisha kusema kuwa anasikitishwa sana kuona kuwa washiriki toka Zanzibar huwa wachache kila mwaka. “Tunajuwa kuwa waandishi wa filamu toka zanzibar wanahitaji sana mafunzo haya maana yanawapa ujuzi na pia nafasi ya kujuana na watengeneza filamu wengine wa kimataifa”, alisema Mkurugenzi huyo.


  Tasnia ya filamu ya Bongo Movies imesemwa sana kwa kuwa na hadithi dhaifu kimataifa. Kwa kutumia warsha kama hizi wadau wanaweza kukuza vipaji vyao na kufikia hadhi ya kimataifa.


  ZIFF mwaka huu imejitolea kuwasaidia wale wote ambao wangependa kutuma maombi yao ili kuwasaidia kufuata malekezo ya usaili, kuwapa miongozo ya uandishi wa skripti na kuwaongezea nafasi za kuchaguliwa kuhudhuria warsha hii muhimu. Wanaotaka kusaidiwa katika hili wanatakiwa kufika ZIFF, Ngme Kongwe Zanzibar, au kutuma maombi yao ya kusaidiwa kwa barua pepe workshop@ziff.or.tz  Wanaotaka kujua zaidi kuhusu warsha hii waingie kwenye tovuti hii: www.maishafilmlab.org   au wawasiliane na fibby@maishafilmlab.org


older | 1 | .... | 529 | 530 | (Page 531) | 532 | 533 | .... | 1897 | newer