Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 525 | 526 | (Page 527) | 528 | 529 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Na Daniel Mbega, Mwanza.

  SHAHIDI wa sita katika kesi ya mauaji ya Aaron Nongo mwenye ulemavu wa ngozi (albino), Mkaguzi wa Polisi (Inspector) David Mhanaya, ameanza kutoa ushahidi wake leo hii katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
  Mbele ya Jaji Robert Makaramba anayesikiliza Shauri hilo namba 213 la mwaka 2014, shahidi huyo ametumia siku nzima kutoa ushahidi wake akiongozwa na mawakili wa serikali Emil Kiria, Esther Majaliwa na Robert Kilando.

  Hata hivyo, Jaji Makaramba aliahirisha kesi hiyo hadi keshokutwa Mei 14, 2015 baada ya kutokea mgongano wa kisheria katika masuala ya vidhibiti kufuatia pingamizi la Wakili Makwega wa upande wa utetezi, hivyo siku hiyo atatoa uamuzi kuhusiana na pingamizi hilo.

  Washtakiwa katika kesi hiyo ni Chacha Jeremia, Mathew Jeremia Mlimi, Paschal Lugoye Mashiku na Alex Joseph maarufu kama Bugwema Silola Jangalu.

  Marehemu Nongo aliuawa Juni 26, 2009 majira ya saa tatu usiku akiwa nyumbani kwake Ibanda Relini, jijini Mwanza ambapo wauaji hao walimkata usoni na kisha kumkata miguu yake yote miwili na kutoweka nayo pamoja na meno mawili ya mbele.

  0 0


  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo leo asubuhi nyumbani kwa Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye John Nyerere kilichotokea hivi karibuni.Aliyesimama pembeni ya Rais ni mdogo wa marehemu Makongoro Nyerere.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya marehemu John Nyerere nyumbani kwao Msasani jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye John Nyerere kilichotokea juzi .Mwili wa Marehemu John Nyerere rubani wa zamani wa ndege za kivita nchini aliyeshiriki kikamilifu vita vya Uganda kati ya mwaka 1978 na 1979, unatarajiwa kusafirishwa leo kwenda kijijini Butiama mkoani Mara kwa maziko.(picha na Freddy Maro).

  0 0

  KATIBU wa wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM ,mkoa wa Arusha,Mayasa
  Kimbau,amewataka wanafunzi  kuzingatia kilichowapeleka masomoni na
  kuacha kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya na uvutaji wa
  bangi.
   


  Kimbau alitoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye
  mahafali ya 24 ya  chuo cha Ualimu na ufundi stadi Sinoni ,ambapo
  jumla ya walimu 90 wahitimu masomo ya ngazi ya cheti na kutunukiwa
  vyeti.
   


  ‘’Hivi sasa wanafunzi wengi wanapokuwa masomoni wengi wao wamekuwa
  wakijihusisha na makundi ya ajabu na kujikuta wakisahau
  kilichowapeleka na wengi wao wakijitumbukiza kwenye utumiaji wa dawa
  za kulevya na uvutaji wa bangi’’alisema
   .


  Aliongeza kwa kuwataka wanafunzi na wanavyuo  ,kuwa na uchungu wa
  fedha za ada zinazotolewa na wazazi wao wanaowasomesha  na wajikite
  kwenye ubunifu wa kuanzisha miradi kwa lengo la kujiajiri kwani suala
  la ajira serikalini bado ni ngumu.
   


  Pia alitoa rai kwa wahitimu kuzingatia maadili katika shughuli zao
  huku wakijua wazi kuwa wao ni kioo cha jamii na wasibweteke na elimu
  walioipata bali wajiendeleze zaidi .
   


  Awali mkurugenzi wa chuo hicho,Edward Laizer,alitoa rai kwa kuiomba
  serikali ibadili mitaala na kuweka mtaala wa kujasiliamali .

  Alisema hatua hiyo itasaidia kukabiliana na soko la ajira kwa nchi za
  afrika mashariki tofauti na sasa ambapo wahitimu wengi hapa nchini
  wamekuwa wakikosa ajira kwenye nchi hizo baada ya kumezwa kielimu.
   


  Akizungumzia ufanisi wa chuo chake alisema hadi sasa jumla ya wahitimu
  96,000 wamehitimu katika chuo hicho na matawi yake hapa nchini huku
  baadhi ya wahitimu wakipata ajira mbalimbali.
   


  Aidha alisema changamoto kubwa inayowakabili wahitimu wengi ni suala
  la ukosefu wa ajira hivyo alisema iwapo serikali itabadili mtaala na
  kuweka suala la ujasiriamali ,suala hilo linaweza kuwa historia hapa
  nchini.

  0 0

  Nianze mada hii kwa kurudia pongezi kwa rafiki yangu Bwana Joe, Kwa kuongezewa nguvu na Nchi yake ya Marekani. Tayari taarifa rasmi ya hili nimeiandikia, na inaweza kusomeka zaidi kwa “KUBOFYA HAPA”. Bwana Joe amekua na imani inayofanana sana na yangu kwa muda mrefu ya kua uhalifu mtandao ni mbio za sakafuni endapo hapatakua na ushirikiano thabiti.

  Kume kua na hoja nyingi kutoka mataifa mbali mbali juu ya kusua sua katika ushirikiano unao vuka mipaka huku uhalifu mtandao kutotambua mipaka iliyopo katika mataifa yetu. Uhalifu mtandao umeendelea kufanyika huku ukivuka mipaka na athari kuendelea kushika kasi ya aina yake hivi sasa.

  Nategemewa kuangazia changamoto kadhaa tulizo nazo katika bara la Afrika na nini kifanyike katika hotuba yangu kwa wataalam mbali mbali wa usalama mitandao baadae mwezi huu jijini Johannesburg ambapo changamoto kubwa iliyoafikiwa na wanausalama kutokea maeneo yote duniani ni kukosekana kwa ushirikiano wa dhati na endelevu katika kupambana na uhalifu mtandao.

  Hili limekua ni tatizo zaidi nchini Tanzania kwani hata ushirikiano wa ndani umekua ukiyumba sana baina ya vitengo mbali mbali vinavyo husiana na usalama mitandao nchini licha ya kua na malengo yananyofanana ya kutokomeza uhalifu mitandao. Kuna kila haja ya kujiangalia zaidi kwenye hili hasa kwa sasa tunapo hitaji zaidi kua na mipango pamoja na mikakati madhubuti ya kuweza kufikia malengo ainishwa.


  0 0

  Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar.

  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kuanzisha Utalii wa Utamaduni wa Zanzibar ambao utakuwa ni kivutio kwa Wenyeji na Wageni mbalimbali nchini. Hatua hiyo ni miongoni mwa jitihada mbali mbali zinazofanywa na Serikali katika kuimarisha Sekta hiyo ambayo ndio tegemeo la Uchumi wa nchi.

  Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Joseph Kilangi wakati alipokuwa akifungua Semina ya majadiliano ya ‘Rasimu ya Sera ya Urithi wa Utamaduni’ iliyofanyika Forodhani Mjini Zanzibar.

  Amesema Zanzibar ina utamaduni wake ambao unatofautiana na Nchi nyingine hivyo ipo haja ya Utamaduni huo kuenziwa na kufanywa uwe kivutio kwa Wageni ili waweze kuja nchini kwa ajili ya kujionea.

  ‘’Zanzibar tuna utamaduni wetu wa Asili ikiwemo Mavazi, Tabia njema, Ukarimu, kupendana,amani na utulivu,mambo ambayo tukiyaratibu vyema katika Sera hii itakuwa kivutio cha Utalii’’ Alisema Mkurugenzi Kilangi
  Amewataka Washiriki wa Semina hiyo kuijadili vyema Rasimu hiyo na kutoa mapendekezo ya kuiboresha kwa lengo la kuvisaidia Vizazi vya sasa na Vijavyo.


  Kwa upande wao Washiriki wa Semina hiyo wameipongeza Serikali kwa uamuzi wake na kuomba kufanyika kwa majadiliano mapana  kutoka kwa Wadau mbali mbali hasa wa Vijijini ambao pia Sera hiyo inawahusu.
   Awali Mwenyekiti wa Semina hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale Dkt. Amina Ameir Issa amewaomba Wananchi kushirikiana na Serikali yao katika kuyahifadhi Maeneo ya Kihistoria ili kuwa chanzo cha Maendeleo kwa Taifa.

  Akielezea lengo la Sera hiyo amesema ni kuweka wigo wa pamoja baina ya Utamduni na Utalii ili kuona mambo hayo yanaendana bila ya kuathiriana. Dkt Amina amefahamisha kuwa ili Sera ya Utalii wa Utamaduni itimie ni lazima Serikali kwa kushirikiana na Jamii ihakikishe inazihifadhi Mila na Silka za Zanzibar sambamba na kuhifadhi Makumbusho ambayo ni kielelezo tosha cha Utamaduni wa Zanzibar.

   Dkt Amina amesema Idara yake ambayo ndio Waratibu wa Sera hiyo itashirikiana na Taasisi za Umma na Binafsi katika kuiboresha ili kutimiza lengo lililokusudiwa. Mjadala huo utaendelea kwa siku mbili ambapo umewashirikisha Wadau kutoka Taasisi mbalimbali ikiwemo za Kibinafsi na Serikali kwa lengo la kuichangia Rasimu hiyo kabla ya kupelekwa mbele kwa hatua zaidi.

  0 0

  Na Scola Milinga. Wizara ya Fedha.


  Tanzania imetoa Ripoti ya Tathimini ya Umasikini kwa upande wa Tanzania bara kwa mwaka 2015, ambayo ni haua muhimu kwa Serikali, wadau wa maendeleo na asasi za kiraia nchini. 


  Hayo  yalisema Waziri wa Fedha Saada Mkuya jana alipokuwa akizindua ripoti hiyo jijini Dar es salaam.

    
  Akitoa shukrani zake kwa niaba ya Serikali kwa Benki ya Dunia, Waziri Saada alisema kuwa kuzinduliwa kwa ripoti hiyo ni ya muhimu kwa Serikali, wadau wa maendeleo na asasi za kiraia ambazo wamekuwa mstari wa mbele katika kuambana na umaskini nchini. 


  Waziri Mkuya alisema kuwa ripoti hiyo inaonesha mambo mengi ikiwemo sera na ufumbuzi wa kiufundi, ambavyo vinapaswa kuwa sehemu ya Serikali katika kutekeleza mikakati mbalimbali katika miaka ijayo.


  “Inatia moyo sote kujua kwamba umaskini, kama inavyoelezwa katika maana yake pana nchini, umeanza kupungua kwa jumla” alisema Waziri Saada. Kupungua huko kunatokana na wigo mpana wa uchumi kama ilivyojitokeza katika ukuaji katika Pato halisi la Taifa kwa asilimia saba kwa mwaka tangu mwaka 2001. 

  Ukuaji huo ni matokeo ya jitihada za kitaifa iliyojengwa kupitia Mkakati wa Kupunguza Umaskini nchini (MKUKUTA I & II na FYDP I).  Kiuhalisia, Watanzania wanaoishi chini ya mstari wa umaskini idadi yao imepungua kutoka 34 asilimia mwaka 2007 hadi asilimia 28.2 mwaka 2011/12.

  Ripoti hiyo inaonesha kuwa idadi ya watu maskini bado ni kubwa kutokana na kiwango cha juu hali ya halisi ya maisha ikilinganishwa na kasi ya ongezeko la watu wengi maskini walioko vijijini wenye kipato cha chini.


  Ili kuhakikisha mchakato wa ukuaji wa uchumi unakuwa na faida nchini katika ustawi wa jamii katika siku za karibuni, yapo mafanikio katika uboreshaji wa hali ya makazi ya kuishi wananchi ambapo mafanikio hayo yamebainishwa kwa kaya kuboresha nyumba na kuwa na nyumba bora ambazo zimeongezeka kutoka asilimia 34 mwaka 2007 hadi 46 katika 2011/12. 


  Mafanikio mengine ni watumiaji wa vifaa mbalimbali wameongezeka ikiwemo watumiaji wa simu ya mkononi, majiko ya gesi na umeme, televisheni na redio, majokofu na kompyuta.  Tathmini ya Umaskini Tanzania Bara inaonesha na kupungua kama ambapo ukuaji wa uchumi umekuwa ni kichocheo cha kasi hiyo. 

  Ili kuifanya Tanzania kufikia kuwa nchi uchumi wa kati kama ilivyoelezwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025,  kama nchi, uvumbuzi wa gesi  asilia itasaidia kukuza sekta za viwanda, uchimbaji wa madini ambazo ndiyo kichocheo kikuu cha kufikia malengo hayo nchini. 

  0 0

  Mwandishi wa habari mzoefu, Luqman Maloto akikitambulisha kitabu chake kijulikanacho kwa jina la “The Special One 2015 Nani Ajaye?” wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
  Mwandishi wa habari mzoefu, Luqman Maloto akimkabidhi mwandishi wa habari wa televisheni ya TBC, Angella Msangi kitabu chake kijulikanacho kwa jina la “The Special One 2015 Nani Ajaye?”.
  Mwandishi wa habari mzoefu, Luqman Maloto akimkabidhi mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, Tatu Mohamed kitabu chake kijulikanacho kwa jina la “The Special One 2015 Nani Ajaye?”.
  Mwandishi wa habari mzoefu, Luqman Maloto akimkabidhi mwandishi wa habari wa televisheni ya Azam, Temeluge Kasuga kitabu chake kijulikanacho kwa jina la “The Special One 2015 Nani Ajaye?”

  Mwanahabari mzoefu nchini, Luqman Maloto amezindua kitabu kinachoelezea wasifu wa wagombea Urais wa uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba kijulikanacho kwa jina la ‘The Special One 2015 Nani Ajaye?’ ambacho kwa sasa kipo mitaani.

  Akizungumza jijini, Maloto amesema kuwa ameamua kuandika kitabu hicho kutokana na kutambua wajibu wake na kutoa mchango kwa nchi yake kama raia hasa kwa kutumia taaluma yake ya uandishi wa habari ili kuwawezesha wapiga kura kumchagua kiongozi bora.


  0 0

   Baadhi ya wananchi wakilazimika kubeba mizigo mizito kichwani kutokana na magari kusitisha shughuli zao kutoka Ifakara kwenda kata ya Mofu.
   Dismas akiteta na jambo na mkewe Rightness, nyuma ni mtoto wao Grace.
   Dismas Lyassa akizungumza na baadhi ya vijana katika kijiji cha Ihenga ambao wamekuwa wakifanya shughuli za kuvusha watu baada ya barabara kujaa maji,

  Ndugu Wanahabari 
  Uchaguzi Mkuu wenye lengo la kuwapata Madiwani, Wabunge na Rais nchini unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu nchini.


  Nimekuwa nikitembelea vijiji na kata mbalimbali za Wilaya ya Kilombero. Hivi karibuni nilitembelea kata zote za wilaya, nilizungumza na wananchi, wengi wao walinishauri kugombea Ubunge. Wananchi wanaamini kuwa kwa pamoja tutaweza kuendeleza vema gurudumu la maendeleo kwa kasi zaidi.

  Wananifahamu kama mtoto wa masikini mwenzao niliyewahi kuzunguka mitaani kupiga picha ili kuendesha maisha, mtoto wa masikini niliyewahi kuwa na ofisi ya kusafisha viatu vya watu eneo la Ubungo Maziwa kwa mzee Mrisho ili niweze kupata nauli ya kwenda shule wakati huo nasoma Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).

  Maisha nayafahamu vizuri na nina uchungu nayo, natamani kushirikiana na wananchi ili kuepukana na maisha duni. Katika maisha yangu kutokula au wakati fulani kutembea kwa miguu kwenda chuo CBE na kurudi nyumbani Ubungo Maziwa (nilikuwa naishi kwa dada), lilikuwa ni jambo la kawaida, kwani maisha yalikuwa magumu mno.


  Sauti ya wananchi wa Kilombero


  Kilio cha wananchi pamoja na mambo mengine ni kwamba wanahitaji kiongozi kijana mwenye nguvu za kuongoza, kiongozi mwenye ujuzi wa namna ya kuongoza na kutawala, kiongozi ambaye atakuwa bega kwa bega na wananchi katika harakati za kuwaletea maendeleo wananchi. Kiongozi ambaye anajua namna ya kuongoza, siyo namna ya kuhonga au kuwalisha yamini wapiga kura, kwani wanachohitaji watu wa Kilombero ni maendeleo, siyo zaidi. Hawahitaji kiongozi ambaye ni maarufu kwa kutembelea magari ya kifahari, wanahitaji huduma za kijamii kama shule, hospitali na wao wenyewe kusaidiwa namna ya kubuni miradi ya maendeleo.

  Elimu yangu ya juu ni Stashahada ya Uzamili katika Uongozi na Utawala (Postgraduate Diploma in Leadership and Governance), kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma-Dar es Salaam niliyohitimu Aprili 22, 2014. Hata hivyo nje ya elimu nimekuwa nikishughulika na masuala ya kijamii kupitia kufanya mikutano ya ana kwa ana na jamii katika masuala ya ujasiriamali, uchumba/ndoa na kadhalika.

  Mojawapo sababu za wananchi kuamini kwamba ninaweza kushirikiana nao kwa ufanisi ni rekodi ambazo wananchi wenyewe wanazo juu yangu, kwani nimekuwa nao karibu katika mambo mengi ya maendeleo ikiwamo kushirikiana nao moja kwa moja au vikundi vyao hasa  vya walemavu, kina mama, vijana na kadhalika kama mshauri wao katika suala zima la namna ya kuviendesha na kuwaunganisha na taasisi au watu wa kusaidiana nao.

  Kwa hivi sasa maeneo kadhaa ya Kilombero yanasaidiwa na mashirika mbalimbali yakiwamo ya nje, baadhi yake ni kutokana na jitihada zangu….nje ya uandishi wa habari, pia nimekuwa nikimiliki kampuni ya kuwaunganisha watu na vyuo vya nje ya Global Source Watch (GSW), ambayo imekuwa ikinipa fursa ya kujuana na watu wengi wa nje.

  Nachukua fursa hii kutangaza rasmi kwamba nitachukua fomu ya kugombea Ubunge kutokana na kukidhi vigezo vyote ya kugombea nafasi hii kama ilivyojieleza katika Katiba ya Tanzania ibara ya 67.-(1) ambayo pamoja na mambo mengine inasema  “Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-

  (a)    ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;

  Mimi ni mzaliwa wa Kijiji cha Mofu, wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, Juni 26, 1976. Nimewahi kufanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi ikiwamo the Guardian Limited kama mwandishi wa kujitegemea, Uwazi kama Mhariri, Leo ni Leo kama Mhariri wa Makala, Mwananchi kama Mwandishi wa makala baadaye mhariri wa jarida la ndani ya biashara, the Media Project (Marekani) kama mchangiaji nk.

  Kwa sasa ni Kiongozi wa Utafiti hapa nchini (National Lead Researcher) wa taasisi ya kimataifa iitwayo Global Integrity yenye makazi yake Marekani, pia ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwanahabari, lakini maamuzi haya ya kugombea ubunge ni yangu binafsi hayana uhusiano wala hayataingiliana na sehemu yoyote ninayofanyia kazi.

  Nimewahi kutembea katika nchi mbalimbali kwa lengo la kwa kusoma na kutembea, baadhi yake ni Marekani, Kenya, Uganda, Dubai, Thailand, India.

  OMBI KWA WASAMARIA WEMA
  Napenda kuchukua fursa hii pia kuwaomba wasamaria wema kuangalia namna ya kusaidiana na wananchi wa Kilombero kwani wakati huu njia nyingi hazipitiki kwa sababu barabara zimejaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Magari yamekuwa hayapitiki katika maeneo mengi ya Kilombero kwa sasa.

  Kwa mfano sehemu kubwa ya barabara ya kutoka  Ifakara kwenda Mofu haipitiki, kiasi kwamba wagonjwa wamekuwa hawawezi kubebwa kupelekwa Ifakara ambako ndiko pekee kuna hospitali ya Wilaya, St Francis. Wapo baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakibebwa kwa kutumia baiskeli na hata pikipiki, jambo ambalo limekuwa gumu hasa kwa wajawazito.

  Magari ya abiriia hasa Noah zilizokuwa zikifanya safari kutoka na kuingia Ifakara kutoka vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Kilombero yamesitisha safari kutokana na barabara kujaa maji. Yapo magari machache hasa ya mizigo ambayo nayo yanafika baadhi ya vijijini kwa shida yakiwa yamebeba mizigo na abiria hivyo kuhatarisha usalama wa wananchi.

  Mvua zimeathiri pia kilimo, kwani mashamba mengi yamefurika maji, huku kukiwa na njaa kwa baadhi ya wanavijiji. Hivyo nachukua fursa hii kuiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kusaidia wananchi wakiwamo wa vijiji vya Mofu, Ihenga, Mlimba, Chisano, Chita,  Mkula, Sanje, Uchindile na Utengule

  Imetolewa leo Mei 12, 2015, saa saba mchana
  na Dismas Lyassa                                 
  (Mtangaza nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Kilombero kwa tiketi ya CCM) 
  0754 49 8972/0712183282 

  0 0


  Na Takdir Ali-Maelezo.  

  Wafanyakazi 38 waliodai kuachishwa kazi katika hoteli ya Rezidensi iliopo Kizimkazi Wilaya ya kusini Unguja  wameiomba  Serikali ya Mapindyuzi Zanzibar kuingilia kati mgogoro wa kuachishwa kazi na Mmiliki wa Hoteli hiyo.

  Wamesema wamesikitiswa na Uongozi wa Hoteli hiyo kuwaachisha kazi wafanyakazi bila kuwepo kwa sababu yoyote ya msingi jambo ambalo ni kinyume na Mikataba ya ajira waliokubaliana wakati wa uajiri.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) kiongozi wa Wafanyakazi hao Mary Laurence Frank amesema wakati wakiwa  katika likizo walipata barua za kuachishwa kazi bila ya kujua sababu za msingi.

  Amefafanua kuwa mara baada ya kupata barua za kuachishwa kazi tarehe 4/5/2015 na kutakiwa kufanya makubaliano (cliarence)na Muajiri wao tarehe 8/5/2015 lakini cha  kusikitisha wamekwenda Hotelini hapo  kuanzia saa mbili hadi saa kumi na mbili bila kuonana na kiongozi yoyote wa Hoteli hiyo.

  “Tulikwenda kufanya makubaliano (cliarence) ili watukabidhi mafao yetu ya kuvunja mkataba na sisi tuwape vifaa vyao lakini wlifunga milango na hawakuturuhusu kuingia ndani”Alisema Mary.

  Amefafanua kuwa madai ya kuachishwa kazi kutokana na msimu mdogo wa biashara (low season) ni kinyume na makubaliano ya mikataba waliokubaliana  na alisema madai hayo hayana ukweli ndani yake.

  Kwa upande wake Mohd Ali Abdallah,  ambae ni miongoni mwa waliochishwa kazi, alisema wamiliki wa Hoteli hiyo wamekuwa wakiwadhalilisha kwa kiasi kikubwa wafanyakazi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla ikiwemo kuwatolea maneno ya kashfa.

  Amesema wanachohitaji ni kukaa pamoja na Uongozi wa Hoteli na kuwapatia haki zao za msingi kwa mujibu wa sheria na taratibu za Ajira ili haki iweze kufanyika na kuiomba serikali kuwabana zaidi Wawekezaji wenye tabia ya kuwadhalilisha wafanyakazi Wazalendo.

  0 0

  Waziri mkuu,Miengo Pinda akizungumza na wawekezaji na watalaamu wa kujenga vihenge vya kisasa na vyenye uwezo wa kuhifadhi tani nyingi za nafaka hasa mahindi  ambao wanatarajia kujenga vihenge hivyo hapa nchini. Watalaamu na wakezaji hao kutoka Plland ambao wakulikutana na Waziri Mkuu mjini Dodoma Mei 12, kutoka kushoto ni Honorta Maslowsk,  Witold Karczewski ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara waPolland na Aleksandar Zingman. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  HOTUBA YA WAZIRI MKUU, MHESHIMIWA  MIZENGO  PETER  PINDA (MB), KUHUSU MAPITIO NA MWELEKEO WA KAZI ZA SERIKALI NA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA FEDHA YA OFISI YA WAZIRI MKUU NA OFISI YA BUNGE KWA MWAKA 2015/2016

                                                                                                 

  UTANGULIZI


  1.            Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba kutokana na Taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lako Tukufu na Wenyeviti wa Kamati za Katiba, Sheria na Utawala; Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; Uchumi, Viwanda na Biashara na Kamati ya Masuala ya UKIMWI zilizochambua Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge lako sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2014/2015 na Mwelekeo kwa Mwaka 2015/2016. Aidha, naliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Bunge, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Mafungu ya Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambazo ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya na Msajili wa Vyama vya Siasa kwa mwaka 2015/2016.


  2.            Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/2015, kumekuwepo na matukio mbalimbali ambayo yamewagusa Watanzania. Katika kipindi hiki Bunge lilipata msiba wa Mheshimiwa Kapteni John Damiano Komba aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi, aliyefariki dunia tarehe 28 Machi, 2015. Tutamkumbuka marehemu kwa utendaji wake mzuri wa kazi na pia kwa nyimbo zake zenye mafundisho na kuvuta hisia za watu wengi pamoja na michango  yake  mizuri kwa Bunge lako Tukufu. Aidha, tarehe 20 Aprili 2015, tulipata msiba wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Mheshimiwa Luteni Kanali Mstaafu, Benedict Kitenga.

   Vilevile, tarehe 26 Aprili 2015 tulimpoteza ndugu yetu, mpigania haki na maendeleo kwa nchi za Afrika, Brigedia  Jenerali Hashim Mbita, ambaye aliwahi kuwa Katibu Mtendaji  wa  Kamati ya Ukombozi Kusini mwa Afrika. Pia, kumetokea vifo, majeruhi na uharibifu wa mali kutokana na ajali za barabarani pamoja na maafa ya mvua na mafuriko.Tunamwomba Mwenyezi Mungu awaponye haraka Majeruhi wote na aziweke Roho za Marehemu Mahali Pema Peponi. Amina!Nitumie fursa hii pia kuwashukuru kwa dhati wale wote waliotoa misaada ya hali na mali kwa walioathirika na matukio hayo.


  3.            Mheshimiwa Spika, ninawashukuru Wajumbe wa Kamati zote za Kudumu za Bunge lako Tukufu kwa michango na ushauri waliotoa wakati wa kupitia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara, Mikoa, Wakala, Idara za Serikali  Zinazojitegemea  na  Mamlaka  za Serikali za Mitaa. Kipekee, nitumie fursa hii  kuwashukuru Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala chini ya Uenyekiti  wa Mheshimiwa Jason Samson Rweikiza, Mbunge wa Bukoba Vijijini ; Kamati ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa chini ya Uenyekiti  wa Mheshimiwa  Dkt. Hamisi Andrea Kigwangala, Mbunge wa Nzega; Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara chini ya Uenyekiti  wa Mheshimiwa  Joelson Luhaga Mpina, Mbunge wa Kisesa na Kamati ya Masuala ya UKIMWI chini ya Uenyekiti  wa Mheshimiwa Lediana Mafuru Mng’ong’o, Mbunge wa Viti Maalum, kwa mchango wao mkubwa wakati wa uchambuzi wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na  Serikali za Mitaa, Ofisi ya Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Maoni na Ushauri wao umesaidia sana kuboresha Makadirio ya Bajeti ninayowasilisha leo.


  4.            Mheshimiwa Spika, mwaka huu, Serikali ya Awamu ya Nne inahitimisha kipindi chake cha miaka kumi kuanzia mwaka 2005. Hivyo, katika Hotuba yangu, nitaelezea kwa muhtasari baadhi ya Mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha  takribani miaka 10 ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2005 na 2010. Aidha, Hotuba hii imeainisha baadhi ya kazi zilizotekelezwa na Sekta mbalimbali kwa kuzingatia MKUKUTA, Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa Mwaka 2011/2012 hadi 2015/2016 na Malengo ya Milenia katika kufikia Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ya kuwa nchi ya kipato cha kati.  5.            Mheshimiwa Spika, Serikali imepata mafanikio makubwa ambayo matokeo yanaonekana katika Ukuaji Uchumi, Kuimarika kwa Huduma za Kiuchumi na Kijamii na Utawala Bora. Nitumie fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wake mahiri katika kusimamia vizuri Serikali ya Awamu ya Nne na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 na 2010. Ninawapongeza pia Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumsaidia Mheshimiwa Rais kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Pia, ninampongeza Mheshimwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kusimamia vizuri utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa upande wa Zanzibar. Aidha, ninawashukuru Viongozi na Watendaji wa Wizara, Taasisi za Serikali, Mikoa, Wilaya na Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na Wananchi wote kwa kutekeleza Ilani kwa mafanikio makubwa.Ni dhahiri kwamba, mafanikio yaliyopatikana yametokana na wananchi kuikubali na kushiriki kikamilifu kuitekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

                                                 

  HALI YA SIASA

  6.            Mheshimiwa Spika, hali ya kisiasa nchini imeendelea kuimarika, demokrasia imekua na mwamko wa Wananchi kushiriki katika shughuli za siasa umeongezeka. Idadi ya Vyama vya Siasa vyenye usajili wa kudumu imeongezeka kutoka 17 mwaka 2005/2006 hadi  22 mwaka 2014/2015. Katika mwaka 2014/2015, Chama cha Wananchi na Demokrasia (CHAWADE), Chama cha Maridhiano na Uwiano (CMU) na Chama cha Kijamaa na Uzalendo Tanzania (CKUT) vimepata usajili wa muda. Aidha, hadi kufikia mwezi Februari 2015, vyama vingine nane vimewasilisha maombi ya usajili wa muda.


  7.            Mheshimiwa Spika, kukua kwa demokrasia nchini kumeambatana na changamoto mbalimbali zinazotokana na ukuaji wa Mfumo wa Demokrasia na matumizi yasiyo sahihi ya demokrasia iliyopo. Ni muhimu sote tukumbuke kwamba, demokrasia ya vyama vingi inatoa fursa kwa Viongozi na Wanachama wa Vyama vya Siasa  kujenga hoja za kunadi sera za vyama vyao ili Wananchi wafanye uamuzi sahihi. Katika kunadi Sera hizo, ni lazima kuheshimiana, kuvumiliana na kuzingatia misingi ya Sheria na Utawala Bora. Maana ya haya yote ni kupingana kwa hoja bila kupigana. Hivyo, tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu natoa wito kwa Viongozi na Wanachama wa Vyama vya Siasa na Wananchi kwa ujumla kuzingatia utii wa Katiba ya Nchi, Sheria za Nchi ikiwemo Sheria ya Vyama vya Siasa na Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa ili kuhakikisha kwamba amani na utulivu uliopo nchini unaendelea kudumishwa.

  ULINZI NA USALAMA


  Jeshi la Wananchi wa Tanzania

  Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2015, Serikali imeliimarisha na kuliboresha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kulipatia zana na vifaa mbalimbali vya kijeshi pamoja na mafunzo. Jeshi limehakikisha kuwa mipaka ya nchi yetu inakuwa shwari na pia limeshiriki katika shughuli za uokozi wakati wa maafa na kuwasaidia wananchi kurejea katika hali ya awali. Pia, Serikali imekarabati miundombinu katika makambi ya jeshi na kujenga Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College). Aidha, Serikali imekamilisha ujenzi wa nyumba 3,096 kati ya nyum

  0 0

  se2
  Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Said akitoa maelezo mafupi kuhusu Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo katika ukumbi wa Hazina ndogo Dodoma.
  se3
  Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Galawa akiwahutubia washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo katika ukumbi wa Hazina ndogo Dodoma.se4
  Mmoja wa washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 akisoma Chati inayoonesha viashiria mbalimbali vinavyotokana na Sensa hiyo. Semina hiyo imefanyika leo  katika ukumbi wa Hazina ndogo Dodoma.se5
  ……………………………………………………………………
  Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo mkoani Dodoma imeendesha semina ya usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi 2012 kwa viongozi na watendaji wa ngazi mbalimbali wa mkoa huo kwa lengo la kuwajengea uelewa viongozi hao waweze kuyatumia matokeo ya Sensa hiyo kupanga mipango ya maendeleo.
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa Semina hiyo viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akiwemo Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Bw.Ephraim Kwesigabo na Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi 2012 Hajjat Amina Mrisho Said wamesema viongozi na watendaji hao wanayo kubwa ya kusimamia matumizi ya takwimu sahihi za Sensa hiyo.

  Wamewasisitiza viongozi na watendaji hao kuzitumia takwimu za Sensa ya Watu na Makazi 2012 katika kupanga mipango yao ya maendeleo ili waweze kutatua changamoto balimbali zinazowakabili wananchi wa maeneo wanayoyasimamia.

  Aidha, wametoa wito kwa viongozi hao kuzingatia matumizi ya takwimu sahihi pindi wanapotenga fedha za bajeti kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya afya, maji, elimu, kilimo,mifugo na biashara ili bajeti zao ziweze kukidhi mahitaji halisi ya idadi ya wananchi wanaowahudumia.

  Zoezi la Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi 2012 mbali na mkoa wa Dodoma limeshafanyika katika mkoa wa Pwani na Morogoro.

  0 0
 • 05/12/15--11:08: HARAMBEE YA ZANCANA YAFANA
 • Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Canada (ZANCANA), imechangisha zaidi ya Dola 1500 za Canada kwa ajili ya waathirika wa hali ya hewa nchini Tanzania.
  Wanajumuiya ya ZANCANA wakipata picha ya pamoja baada ya ibada ya dua maalum ya kuwaombea walioathirika na mvua za masika, nchini Tanzania.

  Katika taarifa yake ambayo Swahilivilla imeipata nakala yake, Zancana imesema kwamba mnamo tarehe 9 Mei, 2015, jumuiya hiyo iliandaa mkutano maalum wa wanachama wake katika jiji la Toronto nchini Canada.

  Mkusanyika huo uliofanyika katika ukumbi wa Zancana, ulifunguliwa kwa ibada maalum ya kuwaombea na kuwakumbuka ndugu jamaa na marafiki waliokumbwa na maafa ya hali ya hewa katika maeneo ya Pemba, Unguja na Dar-es -Salaam.

  Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa, baada ya ibada, mawaidha na dua, kilifuatia chakula maalum kilichoandaliwa kwa ajili ya uchangishaji wa fedha kwa lengo la kuwasaidia wahanga wa mvua za masika katika maeneo ya Unguja na Dar, na waathirika wa kimbunga katika eneo la Kisiwapanza kisiwani Pemba.

  Taarifa ya Zancana imemalizia kwa kusema kuwa, bado michango inaendelea kupokelewa, na kuwaomba wale wote wenye moyo na uwezo kuchangia kwa kupitia accounti inayopatikana katika tovuti yao ya www.zancana.org

  0 0


  0 0

  Meza kuu. (Picha zote na Geofrey Adroph wa Pamoja blog).
  Mshehereshaji wa Semina Bi. Rose Mwalongo akiwakaribisha washiriki wote waliofika kwenye semina ya siku mbili iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali nchini la International Association of women in radio and television (AWRTT) kwa kushirikiana na Ethical Journalism Network ambapo wamewakutanisha wanahabari mbalimbali kutoka nchini Tanzania pamoja na nchi za Afrika.
  Bi. Rose Haji Mwalimu kutoka IAWRT Tanzania akifungua semina kwa kwa washiriki ambao walikuwa ni wanahabari (hawapo pichani) mbalimbali kutoka nchini Tanzania pamoja na nchi za Afrika wa pili kutoka kushoto ni Rais wa IAWRT Bi. Rachael Nakitare, wa pili kutoka kulia ni Bi. Elisabeth Scwabe-Hansen pamoja na Mkurugenzi wa Ethical Journalism Network (EJN).
  Rais wa IAWRT Bi. Rachael Nakitare akitoa semina kwa wanahabari namna ya kusimama katika ukweli na uwazi na pia kuepuka lugha ambazo zinaweza kuleta chuki kwa jamii, na baadae kusababisha machafuko kwenye Uchaguzi mkuu wa 2015.
  Bi. Elisabeth Scwabe-Hansen kutoka ubalozi wa Norway akiwasisitiza washiriki wa semina hiyo kuwa makini kipindi chote wanapochukua au kutafuta taarifa ili kuondoa vurugu kwa nchi hasa Tanzania inayotegemea kufanya uchaguzi mwaka huu.
  Mkurugenzi wa Ethical Journalism Network (EJN), Aidan White akitoa semina kwa wanahabari pamoja na wadau wa habari (hawapo pichani) kuhusu matumizi mazuri ya uandishi hasa kwenye hiki kipindi cha Uchaguzi.
  Baadhi ya washiriki wa semina.
  Rais wa Shirikisho la waandishi wa Habari Afrika (FAJ), Mohamed Garba.
  Mkurugenzi wa Uwezeshashi na Uwajibikaji wa LHRC, Bi. Imelda Lulu Urio akielezea kuhusu vyombo vya habari vya Tanzania vilivyoanza kuonekana kama kuna aina ya lugha ambazo hazikuwepo hapo awali ambapo amesema kuwa ni wakati sasa wa kuanza kuzuia maana zinaleta chuki kwa taifa hasa suala la udini ambalo limeonekana kushika kasi hapa chini Tanzania.
  Bi. Irene Burungi Mugisha kutoka IAWRT nchini Uganda akizungumza jambo.
  Wadau wakifuatilia mada kwa umakini.
  Mhariri mkuu wa gazeti la The New Times la nchini Rwanda, Bw. Kennedy Ndahiro akitoa mada kwa wanahabari pamoja na wadau wa habari waliohudhuria kwenye semina ya matumizi mazuri ya vyombo vya habari kuelekea uchaguzi mkuu unaotegemea kufanyika mwaka huu.
  Rais wa Umoja wa waandishi nchini Uganda, Bi. Lucy Ekadu akiwaasa waandishi wa habari kuwa makini katika utoaji wa habari katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu unaotegemea kufanyika mwaka huu na pia kutoa elimu ya msingi kwa wanahabari ili kutochochea vurugu.
  Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Ayoub Rioba akitoa semina kwa washiriki (hawapo pichani) akiwasilisha mada yake kwenye semina iliyofanyika kwenye hoteli ya Peacock jijini Dar.
  Mshiriki Borry Mbaraka akiuliza swali kwa watoa mada.
  Rais wa IAWRT, Bi. Rachael Nakitare (wa tatu kutoka kushoto) akiuliza swali kwa mtoa mada (hayupo pichani).
  Mtafiti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Patience Mlowe akiwasilisha mada yake kwa wanahabari(hawapo pichani).
  Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena akiuliza swali kwa mmoja wa watoa mada wakati wa semina iliyofanyika jana katika hoteli ya Peacock jijini Dar.
  Mweka hazina kutoka IAWRT Tanzania, Razia Mwawanga akikazia jambo kwenye semina ya wanahabari.

  Wadau wakifuatilia kwa umakini mada.
  Washiriki wa Semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja.Na Mwandishi wetuIkiwa Tanzania inajiandaa kwa ajili ya zoezi la uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, waandishi wa habari nchini wameaswa kujiepusha na lugha za chuki pamoja na uchochezi kipindi chote cha uchaguzi jambo ambalo linaweza kusababisha machafuko kama inavyoonekana katika nchi mbalimbali barani Africa na duniani.Rai hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam katika semina ya siku mbili iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali nchini la International Association of Women in Radio and Television (IAWRT) kwa kushirikiana na Ethical Journalism Network (EJN) ambapo wamewakutanisha wanahabari mbalimbali kutoka nchini Tanzania pamoja na nchi za Afrika mashariki kwa lengo la kujadili masuala yanayohusiana na lugha za chuki kwa vyombo vya habari vya Afrika pamoja na madhara yake kwa wananchi.Akifungua warsha hiyo mgeni rasmi ambaye ni Raisi wa shirikisho la wanahabari Africa (FAJ) Bw. Mohamed Gabra amesema kuwa moja ya mambo ambayo yamekuwa yakisababisha machafuko makubwa katika nchi nyingi za Afrika na duniani kwa ujumla ni lugha zinazotumika na wanahabari wakati wakiripori baadhi ya habari lugha ambazo amesema kuwa zimekuwa zikileta chuki baina ya watu na mwisho wake kusababisha madhara makubwa ambayo yangeweza kuepukika kama hatua zingechukuliwa mapema.Ametolea mifano kwa nchi kama Rwanda, Kenya, na nchi nyingine za ulaya ambazo zimewahi kuingia katika machafuko ya kisiasa katika kipindi cha uchaguzi kutokana na vyombo vya habari pamoja na wanahabari wenyewe kutumia kalamu zao kuwajengea chuki wananchi na mwisho kusababisha kuibuka kwa machafuko makubwa.Amesema kuwa ili kuhakikisha kuwa Tanzania inafanya uchaguzi mkuu kwa mafanikio na amani ni lazima wanahabari wahakikishe kuwa wanasimama kwenye ukweli na kuhakikisha kuwa wanawaambia wananchi kile ambacho kinatokea na sio kujenga na kutengezeza maneno ambayo mwisho yatasababisha chuki kwa watanzania.Awali akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo Rais wa (IAWRT) Bi. Rachael Nakitare amesema kuwa ni lazima kipindi hiki cha Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu ni kipindi cha wanahabari kusimama katika ukweli,uwazi na kuepuka lugha ambazo zinaweza kuleta chuki kwa jamii,na baadae kusababisha machafuko.Baadhi ya watu waliotoa mada katika warsha hiyo ni pamoja na wakili na Mkurugenzi wa uwezeshaji na uwajibikaji kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC Bi. Imelda Lulu Urio ambapo pamoja na mambo mengine ameelezea jinsi vyombo vya habari vya Tanzania vimeanza kuonekana kama kuna aina ya lugha ambazo hazikuwepo hapo awali ambapo amesema kuwa ni wakati sasa wa kuanza kuzuia mambo hayo ili kuepuka mambo makubwa ambayo yanaweza kujitokeza hapo baadae.Wengine waliopata nafasi ya kuchangia katika warsha hiyo ni mwandishi mkongwe nchini ambaye ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Dk. Ayoub Rioba ambapo amesema kuwa katika chaguzi mbalimbali katika nchi za Afrika kwa sasa wanasiasa wamekuwa wakiwatumia wanahabari kutaka kujinufaisha wao kisiasa bila kujali madhara ambayo yanaweze kutokea endapo wanahabari watakiuka maadili ya taaluma zao.Baadhi ya wanahabari kutoka mataifa ya nje ya Tanzania kama Kenya, Uganda,wamesema kuwa hakuna tofauti kubwa sana kati ya ufanyaji wa kazi za wanahabari zinazofanywa nchini Tanzania na mataifa yao bali tofauti iliyopo ni sheria zinazowaongoza wanahari katika mataifa hayo.

  0 0

  Mbunge wa kuteuliwa na rais,Jmaes Mbatia akizungumza jambo na mbunge wa jimbo la Vunjo ,Agustino Mrema mara baada ya kukutana kwa mara ya kwanza jimboni humo katika ibada ya kumbukumbu ya askofu wa kwanza wa KKKT dayosisi ya Kaskazini iliyofanyika mwishoni mwa wiki/
  Kanisala la KKKT ,Usharika wa Mamba Kotelailokofanyika ibada hiyo
  Mbunge Mbatia akiingia kanisani humo.
  Ujenzi wa taasisi ya saratani ya Bishop Moshiunaofanyika kando ya Usharika huo.
  Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bishop Moshi wakiwa katika ibada hiyo.
  Viongozi mbalimbali wa dini pia walikuwepo.
  Mbunge Mrema akiwa ameketi na mbunge mwenzake Mbatia wakifuatilia ibada hiyo.
  Askofu mstaafu Dkt Martin Shao akizungumza wakati wa ibada hiyo.
  BabaAskofu Dkt Fredrick Shoo akiongoza ibada hiyo ya kumbukumbu ya miaka 29 ya kifo cha aliyekuwa askofu wa kwanza wa KKKT dayosisi ya Kaskazini,Stephano Moshi.
  Askofu mstaafu Dkt Erasto Kweka akimzungumzia marehemu Baba Askofu Stephano Moshi jinsi alivyo mfahamu.
  Baba Askofu Dkt Shoo akitoa hotuba yake .
  Ikafika wakati wa kuchangia ujenzi wa taasisi ya saratani ya Bishop Moshi na aliyealikwamwanzo alikuwa ni Mbunge wa jimbo hilo Dkt  Mrema .
  Dkt Mrema akimtizama mkewe Rose Mrema wakati akitoa pesa kwa ajili ya mchango wa harambee ya kuchangia taasisi hiyo ambapo alitoa kiasi cha sh 500,000.
  Baadae ikafika zamu ya Mbatia ambaye alipata nafasi ya kuzungumzakido huku akieleza kuwa tayari amekwisha changia kiasi cha Sh Mil 10 kwa ajili ya shule ya sekondari ya Bishop Moshi na pia alitoa kiasi cha sh Mil 2 kwa ajii ya ujenzi wa taasisi hiyo.
  Baba Askofu ,Dkt Shoo akimhukuru Mbatia kwa mchango anaoendelea kutoa kwa kanisa.
  Baba Askofu Dkt Shoo akizindua rasmi jengo la kuweka kumbukumbu za Askofu wa Kwanza wa KKKT dayosisi ya Kaskazini Stephano Moshi.
  Baba Askofu Dkt Shoo akiingia katika jengo hilo.
  Baba Askofu Dkt Shoo akitia saini katika kitabu cha kumbukumbu.
  Askofu mstaafu ,Dkt  Martin Shao akitia saini katika kitabu cha kumbukumbu.
  Baba Askofu,Dkt Shoo akiweka shada la maua katika kaburi la askofu wa kwanza wa KKKT dayosisi ya Kaskazini na kufanya maombi katika kaburi hilo.
  Mbunge wa kuteuliwa na rais,James Mbatia akitia saini katika kitabu cha kumbukumbu ya askofu wa kwanza wa KKKT dayosisi ya Kaslazini mStephano Moshi .
  Mbunge wa kuteuliwa ,James Mbatia akiweka shada la mauakatika kaburi la Askofu wa kwanza wa KKKT dayosisi ya kasakzini ,hayati Stephano Moshi.
  Mbatia akizungumzajambo na askofu msataafu Dkt Martin Shao mara baadaya kumalizika kwa ibada hiyo/
  Maaskofu wastaafu ,Dkt Erasto Kweka na Dkt Martini Shao wakiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa kuteuliwa James Mbatia mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kumbu kumbu ya asakofo wa kwanza wa KKKT ,Stephano Moshi. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kasakazini.

  0 0

  Edwin Bruno, Founder and CEO at SMART CODES

  Tanzania’s leading digital marketing agency has revamped its new website at www.smartcodes.co.tz

  The agency, which is based in Dar es Salaam, has worked on a wide variety of Tanzania’s leading brands in number of campaigns from developing its’ Digital Strategy to Creativity & Designing to Technology & Development.

  To introduce what they do, SmartCodes released this video which is one of its kind and probably the first company profile video ever in Tanzania. 

  See the video below YouTube link: https://www.youtube.com/watch?v=qwzzF2J-2QU.

  When asked about their secret CEO and Founder Mr. Edwin Bruno said that “We have simple road map on how to serve our prestigious customers, first we meet as face to face talk has proven to be the best way of communication to hear discuss customer’s needs. Then we research proper ways to meet the needs of customers and also his current position.

  From there we prepare a unique pitch, then we develop the big ideas into action and then we launch customer’s site, or mobile app, or social media campaign or both. We don’t end there; we provide all technical and business support to our customers”

  With special skills and technology, Smartcodes has served a handful of big brands in Tanzania including telecommunication giant Huawei, super TV show Mkasi, leading Technology company StarTimes, luxurious Giraffe Ocean View Hotel, Tanzania Postal Bank and many more.

  You can catch more about SmartCodes in below links  0 0

  Wiki hii bwana Costantine Magavilla anaongelea maana nyingine ya shule. Je unajua maana nyingine ya shule zaidi ya kusoma. Bofya hapo kati tuendelee...

  0 0

  3
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Ayoub Mohammed Mahmoud kuwa Mkuu wa Wilaya Mpya ya Magharibi “B” katika Mkoa wa Mjini Magharibi hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali.
  4
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi hati ya kiapo   Ayoub Mohammed Mahmoud baada ya kumuapisha kuwa Mkuu wa Wilaya Mpya ya Magharibi “B” katika Mkoa wa Mjini Magharibi hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali,
  1
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum Haji Omar Kheir (kushoto) akiwa na Washauri wa Rais Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa,Abrahman Mwinyi Jumbe na Burhani Saadat Haji wakiwa ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mkuu wa Wilaya mpya ya Magharibi “B” Ayoub Mohammed Mahmoud Ikulu Mjini Unguja leo.
  2 
  Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu (katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis wakiwa hafla ya kuapishwa Mkuu wa Wilaya mpya ya Magharibi “B” Ayoub Mohammed Mahmoud Ikulu Mjini Unguja leo kazi iliyofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

  0 0

  10
  Mgeni Rasmi ,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Benson Mpesya akisisitiza jambo kwa wadau kuhusiana na umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) katika uzinduzi wa sheria ndogo ya Mfuko huo wilaya Usheto.2
  Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Constantine Makala akiwasalimia wadau wa Wilaya ya Ushetu baada ya kukaribishwa na mwenyeji wake Mkurugenzi wa Wilaya ya Ushetu.
  3
  Afisa Masoko na Elimu kwa Umma kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Hawa Duguza, akiwasilisha mada ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa wadau katika uzinduzi wa sheria ndogo ya Mfuko wa Afya Ya Jamii wilyani Usheto.
  1
  Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Shinyanga, Bwana Imanuel Amani akisisitiza umuhimu wa wana ushetu kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) katika shughuli ya wadau wa Mfuko huo wilayani Usheto.
  6
  Wadau wakifuatilia kwa makini mada iliyokua ikiwasilishwa na Afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
  …………………………………………………………………….
  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha wananchi wengi wananufaika na bima ya Afya umeshirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga kuanzisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF)
  Uzinduzi wa mchakato wa kuanzisha sheria ndogo uliambatana na siku ya wadau wa afya wilayani ushetu ambao umefanyika katika ukumbi wa halmshauri ya wilaya na mgeni rasmi alikuwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Benson Mpesya.
  Katika uzinduzi huo kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mh.Benson Mpesya alisitiza kuhusu umuhimu wa viongozi wa mkoa na wadau wa afya kuhakikisha wananchi wanajiunga kwa wingi kwenye mfuko huu kwani ndio mkombozi wa Afya zao.

older | 1 | .... | 525 | 526 | (Page 527) | 528 | 529 | .... | 1897 | newer