
More Channels
Showcase
Articles on this Page
(showing articles 10481 to 10500 of 37921)
- 05/10/15--00:26: _MV MAENDELEO YATIA ...
- 05/10/15--04:31: _NAPE ASHIRIKI JOGGI...
- 05/10/15--05:20: _RIDHIWANI ATOA MSAA...
- 05/10/15--05:43: _MAONYESHO YA KUUNGA...
- 05/10/15--05:58: _CCM ARUSHA YATOA ON...
- 05/10/15--12:00: _MANGULA NA NAPE WAH...
- 05/10/15--12:05: _RAIS KIKWETE AWEKA ...
- 05/10/15--12:34: _Taasisi ya Imetosha...
- 05/10/15--12:42: _FILIKUNJOMBE AKABID...
- 05/10/15--12:48: _PROFESA HERMAS MWAN...
- 05/10/15--22:25: _Hospitali ya AMI ha...
- 05/10/15--22:28: _KIJANA DAUDI BABU M...
- 05/10/15--22:29: _RAIS KIKWETE KATIKA...
- 05/10/15--22:33: _Mahojiano na Mhe. A...
- 05/10/15--22:43: _“NIPO STUDIO” YA JE...
- 05/11/15--01:46: _SHERIA YA MAKOSA YA...
- 05/11/15--02:27: _Uzinduzi wa Huduma ...
- 05/11/15--02:59: _WAKUU WA TAASISI ZA...
- 05/11/15--03:05: _Rais Kikwete akutan...
- 05/11/15--04:11: _KATIBU WA BARAZA LA...
(showing articles 10481 to 10500 of 37921)
Channel Description:
Karibuni Jamvini Wanajamii
Na Mwandishi Wetu, Swahilivilla.
Meli ya Mv Maendeleo imetia nanga salama katika bandari ya Unguja ikitokea kisiwani Pemba baada ya kukwama kwa muda wa masaa kadha katika eneo la bandari ya Mkoani.

Mv Maendeleo ikiwa imetegesha katika katika eneo la bandari ya Mkoani Pemba.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka bandarini Unguja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari nchini Marekani (ZADIA) Bwana Omar Haji Ali, Afisa wa ngazi za juu katika MV Maendeleo alithibitsha kuwa meli hiyo imetia nanga ikiwa na abiria wote salama.
"Siwezi kuzungumza sana kwa sasa kwa vile bado tumo katika harakati za kushusha abiria", alisema afisa huyo na kuongeza kuwa atakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuongea baadaya mkutano na maofisa wa ngazi za juu wa Serikali ya Zanzibar utakaofanyika mara tu baada ya kumaliza ushushaji wa abiria hao.
Mawasiliano ya Ndugu Omar Ali na maofisa wa ngazi za juu katika Serikali ya Zanzibar na MV Maendeleo, yankuja katika juhudi za kuwapatia taarifa za uhakika wanachama wa ZADIA na Wazanzibari kwa ujumla nchini Marekani, kufutia khofu na mtafaruku vilivyojitokeza miongoni mwa wanajumuiya hiyo baada ya habari za kukwama kwa meli hiyo kisiwani Pemba.
Bwana Ali amewataka wanajumiya hiyo kutokuwa na khofu yoyote juu ya ndugu na jamaa zao waliokuwa katika meli hiyo, kwani abiria wote wamefika salama salmini.
Meli ya Mv Maendeleo ilikwama baada ya kukosea njia wakati ikitoka katika banndari ya Mkoani kisiwani Pemba ikiwa na abiria zaidi ya 260.
Bado haijajulikana rasmi ni hasara gani za kiuchumi zilizosababishwa na mkwamo huo wa abiria ambao baadhi yao walikuwa katika safari za kibiashara.
Taarifa zaidi baada ya mazungumzo na maofisa wa ngazi za juu wa MV maendeleo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza wakati wa uzinduzi wa kikundi cha michezo cha Tegeta Jogging and sports club ambapo aliwaambia vijana wajiandikishe kwenye daftari la kupiga kura kwanza na kuweka itikadi za vyama pembeni, pia alitoa pongezi kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo na Makazi William Lukuvi kwa kazi nzuri ya kusimamia viwanja vya wazi vilivyovamiwa hasa katika wilaya ya kindondoni virudi visaidie katika kukuza michezo.
Kada wa CCM Gabriel Munasa akiwasalimia wana vikundi vya Jogging na kuahidi kuvisaidia katika kila hali katika kufanikisha malengo yao.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akishiriki mazoezi ya kukimbia mchaka mchaka yalioandaliwa na kikundi cha Tegeta Jogging and Sports Club .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye pamoja na viongozi wengine na makada wa CCM wakishiriki mazoezi ya kukimbia mchaka mchaka yalioandaliwa na kikundi cha Tegeta Jogging and Sports Clubikiwa sehemu ya uzinduzi wa klabu hiyo ya michezo na mazoezi ya Tegeta.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akikatiza mitaa ya Tegeta shule wakati wa kuhitimisha mazoezi ya kukimbia mchaka mchaka yalioanzia Tegeta kwa ndevu kupita njia panda ya kiwanda cha saruji Wazo na kuhitimishwa kwenye viwanja vya Tegeta shule .
Kikundi cha Msasani Jogging kikishiriki mazoezi ya viungo kwenye uwanja wa Tegeta shule wakati wa sherehe za uzindiz wa klabu ya michezo na mazoezi ya Tegeta Jogging and Sports Club ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kishiriki mazoezi ya viungo wakati wa uzinduzi wa klabu ya mazoezi na michezo Tegeta.
Mazoezi ya viungo
Watoto hawakuwa nyuma wakati wa kushiriki mazoezi.
Kutoka kushoto ni Diwani wa Viti maalum Kinondoni Florence Wasira, Diwani mwingine wa Viti maalum Bernadette Ritti kutoka Kinondoni pamoja na kada wa CCM Gabriel Munasa wakiwa sehemu ya wageni walioshiriki katika kufanikisha uzinduzi wa kikundi cha Tegeta Jogging and Sports Club.
Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Dar es salaam Juma Simba Gadafi akiwasalimia vikundi vilivyoshiriki sherehe hizo za uzinduzi wa klabu ya michezo na mazoezi ya Tegeta.
Katibu wa Kikundi cha Tegeta Jogging and Sports Club Mariam Said akisoma risala mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nauye wakati wa sherehe wa uzinduzi wa kikundi chao.
Mariam Said akihamasika wakati wa mazoezi kwenye uwanja wa shule Tegeta.
Watoto Mohamed Said nwenye umri wa miaka 14 (kushoto) Mbwana Sharifu mwenye umri wa miaka 13 kutoka Fanja Jogging wakipasha misuli kabla ya kuanza mchaka mchaka.
Wadada wakiruka kamba kabla ya kuanza jogging
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipata kifungua kinywa baada ya kumaliza kushiriki jogging
(Picha zote na Adam Mzee)
Mwenyekiti wa Kijiji cha Pongwekiona Rajab Mgaya kushoto akipokea fedha kiasi cha shilingi milioni moja na mifuko 70 ya Saruji toka kwa katibu wa Mbunge wa Chalinze Iddy Swala ambaye alimwakilisha Mbunge wa Jimbo hilo Ridhiwani Kikwete, fedha hizo ni kwa ajili ya ujenzi wa wodi mbili kwenye zahanati ya Kijiji hicho.
Diwani wa kata ya Kimange Hussein Hadingoka kushoto akipokea fedha kiasi cha shilingi milioni moja toka kwa katibu wa Mbunge wa Chalinze Iddy Swala kwa niaba ya Mbunge kwa ajili ya ofisi ya kata fedha zilizotolewa na Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete.
Na John Gagarini, Chalinze
ADHA ya akinamama wajawazito kujifungua mbele za wanaume kutokana na zahanati ya Kijiji cha Pongwe Kiona wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kuwa na chumba kimoja cha matibabu huenda ikaondoka baada ya kuchangiwa kiasi cha shilingi milioni moja na mifuko 70 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wanawake na wanaume.
Kutokana na zahanati hiyo kuwa na chumba kimoja imesababisha akinamama kujifungua huku kukiwa na wanaume jambo ambalo limesababisha kutokuwa na usiri hivyo utu wa mwanamke kutokuwepo. Msaada huo umetolewa na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambapo fedha na Saruji vilikabidhiwa na Katibu wa Mbunge huyo Iddy Swala kwa niaba ya Mbunge.
Akizungumzia changamoto hiyo mwenyekiti wa kijiji hicho Rajab Mgaya alisema kuwa zahanati hiyo ilijengwa mwaka 1964 na ina wodi moja tu.
“Tunamshukuru Mbunge kwani hii ilikuwa changamoto kubwa kwa akinamama wanaojifungua huku kukiwa na akinababa nao wanapata matibabu humo hivyo usiri kutokuwepo kutokana na hali hiyo,” alisema Mgaya. Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kimange Husein Hadingoka alisema kuwa mbunge huyo ameonyesha upendo wa hali ya juu kwa kutoa vitu hivyo ambavyo vitasaidia ujenzi huo.
Hadingoka alisema kuwa wananchi watafanya ujenzi huo ambapo yeye alitoa 100,000 kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo na kusema atafurahi kuona uujenzi huo unakamilika mapema.
Naye moja ya wakazi wa Kijiji hicho ambaye ni mwanamama Sikudhani Ally alisema kuwa kujifungua huku wanaume wakiwepo ni mtihani mkubwa lakini kwa mpango huo utakuwa umeweka stara ya mwanamke.
Kwa upande wake katibu wa Mbunge Swala alisema kuwa mbunge ametoa msaada huo baada ya kutemebelea hivi karibuni akiwa kwenye ziara zake za kikazi na wananchi kutoa kilio chao juu ya hali hiyo.
Asasi zisizo za kiserikali zinazojishughulisha na shughuli za Kilimo biashara za masharika ya TAHA, SNV,MVIWATA, AGRO PRO FOCUS,HIVOS, TCCIA na TRIAS leo zimefanikisha kufanya maonesho ya Kuunganisha Wakulima na Fursa za Mikopo ambayo yamelenga kuwakutanisha wakulima na wafanya biashara wa mazao ya kilimo pamoja na Taasisi za kifedha na zile zinazotoa mikopo kwa ajili ya shughuli za Kilimo Biashara. Katika picha ni Eneo la viwanja vya Kwaraa Halmashauri ya Wilaya ya Babati ambavyo vinatumika kwa ajili ya kuwakutanisha wakulima na taasisi za kifedha zinazotoa mikopo kwa wakulima(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Afisa wa NMB akifafanua jambo kwa mkulima wakati wa maonesho hayo yaliyofanyika Katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwenye Viwanja vya Kwaraa na yamefunguliwa na Mwenyekiti wa chemba ya biashara Mkoa wa Manyara ndugu Athumani Karunde.
Kulia Mkurugenzi wa TAHA Bi. Jacqueline Mkindi akiwa na Mgeni rasmi ndugu Athumani Karunde wakati wa kutembelea mabanda ya waoneshaji
Eneo la maonesho
Wakulima wakifuatilia hotuba na semina elekezi za wataalamu wa masuala ya biashara
Tom Olesika, Mkurugenzi wa Agri Pro Focus akinena jambo wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Arusha,Feruz Bano (kushoto) akimkabidhi kitabu cha kanuni za uchaguzi wa CCM mgombea aliyetangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Arusha mjini,Kim Fute jana ofisini kwake mara alipofika kujitambulisha na kutangaza nia.
mgombea aliyetangaza kuwania nafasi ya ubunge kupitia CCM katika jimbo la Arusha mjini,Kim Fute akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya katibu wa chama hicho wilayani Arusha jana alipofika kujitambulisha na kutangaza nia(picha na moses mashalla).
Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilayani Arusha kimetoa onyo kwa wagombea waliojitokeza kutangaza nia ya kugombea jimbo la Arusha mjini kupiti chama hicho kuacha tabia ya kuchafuana na kuanza kampeni kabla ya muda.
Onyo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na katibu wa chama hicho wilayani Arusha,Ferooz Bano wakati akimkabidhi kanuni za uchaguzi wa CCM mgombea alliyetia nia ya kugombea jimbo la Arusha mjini kupitia chama hicho,Kim Fute .
Mgombea huyo alifika mbele ya ofisi za CCM wilayani hapa kujitambulisha na kutia nia ambapo mbali na kufanyiwa ukaguzi wa kadi zake za uanachama pia alikabidhiwa kitabu chenye kanuni hizo na kupewa agizo la kutoshiriki kampeni kabla ya muda.
Hadi sasa jumla ya wagombea saba ambao ni Kim Fute,Phillemon Mollel”Monaban”,Mustapha Panju”Bushbuck”,Victor Njau,David Rwenyagira,Deo Mtui,Francis Laiser pamoja na mbunge mstaafu wa jimbo la Arusha mjini,Felix Mrema wamejitokeza kutia nia kuwania jimbo la Arusha mjini.
Akizungumza mara baada kumkabidhi kanuni hizo katibu huyo wa wilaya aliwataka wagombea wote waliojitokeza kutia nia kupitia chama hicho kuacha tabia chafu ya kupakana kuandaa sherehe kwa wapiga kura.
“Muda wa kampeni bado haujafika hatutaki nyinyi wagombea muanze kuchafuana huko mitaani na wala kuandaa vijisherehe”alisema Bano
Hatahivyo,kwa upande wake mgombea huyo mbali na kushukuru mapokezi ofisini hapo pia alihaidi kufuata maagizo ya chama hicho na kusisitiz kwamba atafuata maagizo ya kanuni hizo kwa umakini mkubwa.
Fute,alitangaza rasmi kuinga katika kinyang”anyiro hicho kupitia CCM huku akijitapa kwamba amejipima na kubaini anatosha kuwa mwakilishi wa jimbo la Arusha mjini kwa kuwa amegundua kuna ombwe la uongozi.
Picha ya Marehemu John Nyerere aliyefariki dunia jana akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa.
Marehemu John alizaliwa mwaka 1957 jijini Dar es Salaam na enzi za uhai wake alikuwa Kapteni wa Jeshi la WananchiTanzania (JWTZ) akiwa rubani wa kurusha ndege za kivita.
Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia ni kwamba marehemu amefariki baada ya kusumbuliwa na maradhi ya mapafu na kisukari kwa muda mrefu.
Enzi za uhai wake John alishiriki vita ya kumng’oa Nduli Idd Amini nchini Uganda. Mungu ailaze roho ya marehemu John mahali pema peponi.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akizungumza na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye walipokutana nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani jijini Dar es Salaam kuhani msiba wa John Nyerere.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisaini kitabu cha rambirambi ya msiba wa John Nyerere.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Makongoro Nyerere Msasani nyumbani kwa Baba wa Taifa wakati wa kuhani msiba wa John Nyerere. (Picha zote na Adam Mzee)
0 |
|
0 |
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua kwenye kaburi la Mashujaa wa Algeria, leo Jumapili, Mei 10, 2015. Rais Kikwete yupo nchini Algeria kwa ziara ya siku tatu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo wakati alipotembelea Makumbusho ya Taifa la Algeria, Mjini Algiers, leo Jumapili, Mei 10, 2015. Rais Kikwete yupo nchini Algeria kwa ziara ya siku tatu. PICHA NA IKULU.
Toka kushoto ni Kathrin Hoff, kijana Paulo, Masoud Kipanya na Balozi Henry Mdimu.
Taasisis ya Imetosha ya jijini Dar es Salaam leo hii imepeleka misaada mbali mbali katika kijiji cha watoto wasioona cha Buhangija, Shinyanga ambacho kwa sasa kinahifadhi pia watoto na vijana wenye ualbino takriban 300.
Misaada hiyo ikiwemo mabelo ya mitumba 2 moja la masweta na jingine la suruali za jeans, unga, mchele, maharage, sukari, chumvi, ndoo 3 za mafuta ya kupikia, sabuni za kufulia box 8, vile vile box 3 za vifaa vya hedhi vitakavyodumu miezi miwili pamoja na nguo za ndani dazeni 12 vyote hivo imegharimu Tsh milioni mbili na elfu sitini(2,060,000) ambazo zimetolewa na wanachama wa taasisi hiyo iliyojikita kupambana na mauaji ya watu wenye ualbino kwa njia ya elimu. Akiongea na watoto na vijana hao Mwenyekiti Masoud Kipanya alisema taasisi hiyo inaangalia jinsi ya kutengeneza mazingira kwa kituo hicho kujijengea uwezo wa kujipatia chakula badala ya kutegemea wasamaria wema huja pale watakapojisikia wakati watoto katika kituo hicho wanahitaji kula kila siku.
Mkuu wa kituo hicho alisema anashukuru taasisi ya Imetosha kwa kuonesha mapenzi ya dhati na watoto wa kituo hicho na kuguswa na changamoto zinazowakuta, kwani si mara nyingi sana watu au taasisi kurudia kupeleka misaada kituoni hapo kitu ambacho Imetosha wamekifanya. Wiki 3 zilizopita taasisi hiyo ilipeleka msaada wa chakula kituoni hapo.
Awali mtafiti wa masuala yahusuyo watu wenye ualbino mJerumani Bi Kathrin Hoff alielezwa kufurahishwa na jitihada zinazooneshwa na Imetosha kwa uhamasishaji inayoufanya kwa jamii ya Ki Tanzania, pia amepongeza sana hatua ya Imetosha kutaka kukifanya kituo cha Buhangija kujitegemea badala ya kubaki tegemezi kama ilivyo sasa. Kathrin Hoff ni mhitimu toka chuo kikuu cha Mainz nchini Ujerumani.
|
Baadhi ya missada iliyotolewa na Imetosha pembeni kulia ni mabelo mawili ya mguo. |
Mkuu wa kituo hicho Bw Peter Ajali akiongea na watoto wa kituo hicho akieleza dhamira ya ya asasi ya Imetosha kwao. |
Hapa wakimsikiliza Masoud Kipanya |
Baadhi ya wasichana wa kituoni hapo wakifurahia msaada wa nguo za ndani na vifaa vya hedhi walivyokabidhiwa na mjumbe wa Imetosha aishiye Shinyanga Bibi Herriet |
Picha na habari kwa hisani ya TBN kanda ya kati.
0 |
|
0 |
|
Paroko wa kanisa la Anglicana kushoto akipokea msaada wa bati 300 kutoka kwa mbunge Deo Filikunjombe
Mbunge Filikunjombe kati akikabidhi saruji kwa ajili ya shule ya msingi kijiji cha Mavanga
Saruji iliyotolewa na mbunge Filikunjombe Mavanga
Mbunge Filikunjombe akikabidhi kitanda cha wanawake wajawazito kujifungulia
Mbunge Filikunjombe akiwakabidhi wajawazito kitanda cha kujifungulia
Mwenyekiti wa kijiji cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )akiwa amepokea msaada wa Darubini toka kwa mbunge Deo Filikunjombe
Filikunjombe akiwahutubia wananchi wa Mavanga.
Wananchi Mavanga wakiwa katika foleni ya kuuliza maswali na kumpongeza mbunge wao
Mbunge Filikunjombe akimkabidhi mpira kijana wa Chadema kijiji cha Mavanga
Kijana wa Chadema akimpongeza mbunge Filikunjombe
Wananchi Mavanga wakimkabidhi zawadi ya kuku mbunge wao Filikunjombe
Mbunge Filikunjombe akipokea zawadi ya mbuzi toka kwa vingozi wa kanisa la Anglicana baada ya kuwasaidia bati 300 za ujenzi wa kanisa
Mwenyekiti wa kijiji cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )akimongeza mbunge Filikunjombe
Filikunjombe akizungumza na mlemavu aliyefika katika mkutano wake
Wananchi wa kijiji cha Mavanga wakiwa wamembeba mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe
Msafara wa mbunge Filikunjombe kijiji cha Mavanga
Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akiwapungia mikono wananchi wa kata ya Mavanga
Waendesha boda boda wakiongoza msafara wa mbunge Filikunjombe kwa mbwembwe
Mbunge Filikunjombe akiwasikiliza wanafunzi katika kijiji cha Mavanga
Mbunge Filikunjombe akicheza mpira na wanafunzi hao baada ya kuwapa msaada wa mpira na sukari kwa mwaka mzima
Wasanii wa ngoma katika kijiji cha Mavanga wakishiriki kupiga ngoma na mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe kushoto
Katibu mwenezi mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya akishiriki kucheza ngoma
..............................................................................................................................................................
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe asema baadhi ya wabunge ,mawaziri na watendaji wabovu serikalini wanakichafua chama cha mapinduzi ( CCM )
Filikunjombe alisema kuwa Ccm ni chama makini na kinachopendwa sana ila shida ipo kwa baadhi ya watu waliopo ndani ya Ccm na serikali ni bomu
mbunge huyo alitoa kauli hiyo leo katika kijiji cha Mavanga wakati akijibu maswali ya wananchi na viongozi wa vyama vinavyounda katiba ya wananchi ( Ukawa) kuhusiana na Ccm kuwateulia wananchi viongozi wasio na sifa kugombea nafasi mbali mbali.
Alisema kama kila mmoja angetimiza wajibu wake katika nafasi yake hakuna mpinzani ambae angechaguliwa ila kuchaguliwa kwa wapinzani ni kushindwa kwa wale waliowaamini kutoka Ccm kushindwa kuwajibika kwa wananchi waliowaamini
Filikunjombe alisema atakuwa mbunge wa mwisho kunyoshewa kidole na watanzania wakiwemo wananchi wake wa Ludewa kwa kushindwa kuwatumikia wananchi na chama chake cha Ccm .
Kwani alisema hakuomba ubunge kwa ajili ya kujinufaisha binafsi ila aliamua kugombea ili kuwatumikia wana Ludewa kwa kuwapelekea maendeleo hivyo Kazi Yake kwa sasa hadi mwisho wa ubunge wake ni kuleta maendeleo kwa wananchi wake na kuona ahadi zake zinatimia kwa muda uliopangwa na si kujinufaisha kwa wakati.
" Naomba kwanza mtambue kuwa wabunge wote tulipo fika bungeni kwa mara ya kwanza tulikopeshwa Tsh milioni 90 kwa ajili ya kununua gari la kutembelea na Mimi kwa kuwa nilikuwa na gari pesa hizo niliamua kununua gari la wagonjwa Mlangali ambao hawakuwa na gari la wagonjwa ....lengo langu kutumikia wananchi na kuwatatulia kero zao si vinginevyo"
Akielezea msaada huo wa vitu mbali mbali vyenye thamani ya Tsh milioni 40 alivyotoa alisema ni pamoja na kitanda cha kujifungulia wajawazito chenye thamani ya Tsh milioni 5.2,Darubini ,pesa ya taslimu Tsh milioni 1 bati zaidi ya 500 ,rangi debe 20 ,saruji zaidi 525 na vifaa vingine vingi kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa miradi mbali mbali ya kijiji na ujenzi wa makanisa,shule na wodi la wazazi
Awali viongozi ukawa wa kijiji cha Mavanga kata kata ya Mavanga walimpingeza mbunge Filikunjombe kwa kuwa mbunge wa mfano Ludewa japo wapo viongozi wengi ndani ya chama chake ni wabovu.
Mwenyekiti wa Ukawa Mavanga John Mligo akishukuru kwa msaada huo wa vifaa na fedha toka kwa mbunge Filikunjombe alisema kama wabunge na viongozi wote wangefanya kama Filikunjombe kamwe wananchi wasingechukia chama hicho.
Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti huyo wa Ukawa na mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema ) walisema wao kama viongozi wa upinzani hawana shaka na uwakilishi wa mbunge Filikunjombe ndani ya jimbo hilo na nje ya jimbo hilo
" Tumekuwa na wabunge 7 ambao wametangulia kabla ya Filikunjombe ila uwakilishi wake umekuwa wa kuigwa na wabunge wengine na kama wabunge kote nchini wangekuwa watendaji hivyo huenda upinzani nchini usingekuwepo"alisema Mligo
Kwani alisema kuwa Chanzo cha kijiji hicho kuchagua mwenyekiti wa Serikali ya kijiji kutoka Chadema ni baada ya viongozi wa ccm kuonyesha kuwa mbali na wananchi na baadhi Yao kutafuna pesa za michango ya wananchi .
Bw Mligo alisema shida ndani ya Ccm ni vita ya wenyewe kwa wenyewe ndio ambayo imekuwa ikiwachanganya wananchi na kujikuta wananchi wanaingia katika mgawanyiko na kuchagua wapinzani
Alisema wakati wa kampeni hata wasio na sifa wanataka kuchaguliwa kwa kutumia rushwa ,hivyo kutaka kwa Ludewa kutambua wazi mbunge anayekubalika ni Filikunjombe pekee na kuwa hawahitaji mtu zaidi ya mbunge wao aliyewavusha katika maendeleo
Huku mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Bw Mpambichaka akiwataka wananchi wa Ludewa kuacha kuonja sumu kwa kubadili wabunge na kuwa utendaji wa Filikunjombe hakuna wa kumfananisha nae
Alisema kuwa wamepata kushuhudia utendaji wake ndani ya bunge kupitia kamati ya PAC kwa kupambana na ufisadi kupitia Escrow na kuwafanya mawaziri zaidi ya watatu kujiuzulu
Pia kupitia utendaji wake ndani ya jimbo amefanikiwa kuwavuta wana Ludewa ambao siku zote walikuwa wakiona aibu kuweka wazi kuwa ni wakazi wa Ludewa na badala Yake kudanganya kuwa wao ni wazaliwa wa Mkoa wa Ruvuma kutokana na awali Ludewa kuwa nyuma kwa maendeleo .
" Toka Filikunjombe ameingia madarakani mwaka 2010 na kuwepo kwa kasi ya maendeleo ndio tunashuhudia wana Ludewa wakirejea Nyumbani na kujitangaza kuwa wao ni wakazi wa Ludewa tofauti na zamani wengi walikuwa wakijificha kwa aibu "
Hata hivyo alisema wapo wabunge ambao wamekaa majimboni muda mwingi kama akina Mzindakaya huko Sumbawanga ila siku zote ni mtu wa kueleza jinsi alivyofanya Kazi na Mwl Julius Nyerere ila si kujipambanua namna gani alivyoleta maendeleo jimboni
Kuhusu misaada mbali mbali iliyotolewa na mbunge huyo kijijini hapo mwenyekiti huyo alisema kwa mara ya kwanza toka wabunge 7 waliopita kijiji hicho kimepata kupata misaada mingi kutoka kwa mbunge.
Viongozi wa kijiji cha Mavanga akiwemo mwenyekiti wa kijiji Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )kulia wakipokea misaada ya vifaa vya ujenzi toka kwa mbunge Filikunjombe kushoto
Wananchi wa Mavanga wakiwa wamepanda juu ya magari na miti kumwona mbunge Filikunjombe
Wananchi wakiwa juu ya miti wakifuatilia hotuba ya mbunge wao Deo Filikunjombe
Mbunge Filikunjombe akifurahia jambo wakati mkazi wa Mavanga akimtaka kuwa mbunge hadi atakapochoka yeye
Mwanahabari wa kituo cha Radio Best Ludewa Deo Nyoni akiwa makini kufuatilia matukio
Wananchi wa Mavanga wakiwa wamebeba kitanda cha kujifungulia wanawake wajawazito kilichotolewa na mbunge Filikunjombe kitanda chenye thamani ya Tsh milioni 5.2
Mwenyekiti wa kijiji Cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )akimpongeza mbunge Filikunjombe kwa misaada yake
0 |
|
0 |
|
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko akizungumza wakati wa hafla uzinduzi wa Tawi la Chama cha Wanafunzi wanaosoma KiswahiliAfrika Mashariki (CHAWAKAMA) katika Chuo cha Kumukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam jana.

Mwanafunzi wa mwaka wa Kwanza katika fani yaKiingereza na Kishwahili Bi. Fatma Amour Hamad akiimba shairi wakati wa hafla uzinduzi wa Tawi la Chama cha Wanafunzi wanaosoma KiswahiliAfrika Mashariki (CHAWAKAMA) katika Chuo cha Kumukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko akimlisha keki Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dkt. Magreth Shawa wakati wa hafla uzinduzi wa Tawi la Chama cha Wanafunzi wanaosoma Kiswahili Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) chuoni hapo jana.

Baadhi ya wageni waalika wakifuatilia burudani mbalimbali wakati wa hafla uzinduzi wa Tawi la Chama cha Wanafunzi wanaosoma Kiswahili Afrika Mashariki(CHAWAKAMA) katika Chuo cha Kumukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko akipanda mti kamakukmbukumbu ya ya kuzinduliwa kwa tawi la CHAWAKAMA katika Chuo chaKumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jana jijini Dar es Salaam. Mti huo umepewa jina la CHAWAKAMA.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Wanafunzi wanaosoma Kiswahili Afika Mashariki Tawi la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere-CHAWAKAMA – MNMA jana jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija, WHVUM
0 |
|
0 |
|
Mahakama Kuu, Kitengo cha Biashara imeamuru kufurushwa kwenye jengo hospitali ya African Medical Investment Ltd (AMI) maarufu kama Trauma Center ya Msasani Jijini Dar es Salaam, baada ya kushindwa kulipa kodi ya pango kwa zaidi ya miezi 26, inayofikia zaidi ya dola za kimarekani milioni 1.6 (zaidi ya Shilingi Bilioni tatu za Kitanzania).
Hatua hii imefikiwa baada ya mabishano ya muda mrefu ya kisheria baina ya AMI na mfanyabiashara ambaye pia ni mmiliki wa jengo hilo, Bw. Navtej Singh Bains. Akaunti za Benki za Hospitali hiyo ya AMI katika Benki ya EXIM zilizoambatanishwa na Mahakama zimekutwa zikiwa zimefungwa na fedha zote zikiwa zimetolewa.
Amri hiyo iliyotolewa wiki iliyopita (tarehe 7 Mei, 2015) na kusainiwa na Makamu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, imeipa mamlaka kampuni ya mnada ya MEM (MEM Auctioneers and General Brokers Limited) kuifurusha Hospitali ya AMI kutoka kwenye jingo ambapo kampuni hiyo inafanya biashara yake.
Amri hiyo ya kutoka kwenye jengo itaanza mara baada ya kuisha kwa kipindi cha notisi cha siku kumi na nne ambacho kimeshatumiwa na AMI. “Ikiwa mdeni aliyetajwa katika hukumu hapo juu (African Medical Investment Limited –AMI) ameamuriwa kwa amri ya mahakama hii ya tarehe 9 mwezi Septemba, 2014 kuondoka na kukabidhi jengo, na ikiwa bado hajaondoka na kukabidhi jengo lenyewe.
“Unaelekezwa kumwondoa mdaiwa/wadaiwa au mtu yeyote anaefanyakazi chini yake atakayekataa kuondoka kwenye jengo na kumuweka anaemiliki amri hii ya mahakama (Navtej Singh Bains- Mwenyenyumba) kwenye nyumba yake,” inasomeka sehemu ya amri ya mahakama iliyoelekezwa kwa kampuni ya mnada ya MEM (MEM Auctioneers).
Amri hii sasa inapelekea kufungwa kwa Hospitali ya AMI, licha ya rufaa zake za kujaribu kuzuia kufukuzwa, imefikiwa baada ya hospitali hiyo kushindwa kutimiza amri ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania iliyoamuru kulipwa kwa dola za kimarekani milioni 1.514 mahakamani pamoja na kodi ya kila mwezi ya kiasi cha dola za kimarekani 64,000 kila mwezi kufuatia mgogoro wa kodi ya jengo.
Jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Mbarouk, Salum Massati na Katherine Oriyo waliiamuru Hospitali ya AMI kufanya malipo hayo ndani ya mwezi mmoja baada ya hukumu iliyotolewa Februari 12, 2015, agizo ambalo halijatekelezwa.
Mahakama ilitoa uamuzi huo kwenye kesi No. 185 ya mwaka 2014 iliyofunguliwa na AMI kupinga utekelezaji wa amri iliyotolewa kwenye kesi No. 104 ya mwaka 2013 ambapo ilishindwa kesi na mwenye nyumba wao (Mfanyabiashara wa ndani Navtej Singh Bains) iliyohusiana na jengo ambalo kampuni hiyo inaendesha biashara yake.
Hospitali ya AMI ilishindwa katika kesi iliyofunguliwa na mwenye nyumba wao baada ya kushindwa kulipa kodi kwa kipindi cha miezi 26 iliyopita katika malumbano/mabishano ya kisheria kwenye Mahakama ya Biashara ya Tanzania Novemba 2014 na walipewa notisi ya kuhama na mwenye nyumba huyo.
Kufuatia hukumu hiyo, AMI ilipeleka ombi la kuwa imefilisika katika Mahakama Kuu ya Tanzania ikieleza kuwa imekuwa ikijiendesha kwa madeni baada na kupata hasara katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa AMI Plc, Bw. Theunis Peter Botha, ambaye pia ni Mkurugenzi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya AMI Tanzania, aliwasilisha ombi hilo kuwa imefilisika katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Katika shauri hilo la ufilisi lililofunguliwa wiki iliyopita kwa Msajili wa Mahakama Kuu, kampuni hiyo inadai kuwa imekuwa ikikumbana na hasara za mabilioni ya shilingi jambo lililopelekea kuwepo kwa madeni yaliyokithiri ambayo kwa sasa yako nje ya uwezo wa kampuni kulipa.
“Mlalamikaji (AMI) anadai kuwa alipata hasara halisi ya Dola za kimarekani 1.146 katika mwaka uliomalizika Februari 28, 2013, huku kwa mwaka uliomalizika Februari 28, 2014, mlalamikaji alipata hasara halisi ya Dola za Kimarekani 775,000,” inasomeka sehemu ya hati ya malalamiko.
AMI Tanzania inamilikiwa na Kampuni mama ya AMI Plc ya London ambayo iliondolewa kwenye Soko la Hisa la London mnamo Februari 2014 baada ya jaribio la kuuza mali zake zilizopo nchini Maputo bila kibali kutoka kwa wanahisa.
Inaelezwa kuwa kampuni hiyo ilitakiwa pia kufanya malipo kwa taasisi mbalimbali, zikiwemo Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na watu na makampuni binafsi.
Kwa mujibu wa shauri hilo, ukichukulia thamani ya mali za kampuni na kiasi cha fedha zinazodaiwa na wadai, kulikuwa hakuna njia ya kuweza kupata fedha za kutosha kuwalipa sambamba na kutekeleza majukumu yake.
Pia kuna kumbukumbu zinazoonyesha kuwa Lancet Laboratory (T) Ltd iliwasilisha ombi la dharura dhidi ya kufungiwa kwa Hospitali ya AMI ikiwa inaidai hospitali hiyo zaidi ya Shilingi Milioni 150.
Taarifa za ndani zinaeleza kuwa wadai mbalimbali wako njia panda kutokana na deni kubwa la Dola za Kimarekani Milioni 4 wanaloidai hospitali hiyo. Wadai wakubwa ni pamoja na mmiliki wa jengo Bw. N Bains, Madaktari, Wafanyakazi, TRA, Wasambazaji wa madawa na Wasambazaji wengine.
0 |
|
0 |
|

Amesema endapo atatimiza hayo basi yeye kama mjumbe wa kamati kuu atamuunga mkono na pia amewataka wananchi wa jimbo la Moshi mjini kumuunga mkono.
Kijana Daudi Babu Mrindoko alimaarufu kama “Obama wa Moshi” ni kijana ambaye mwenye mvuto mkubwa na kushawishiwa na wakazi wa jimbo la Moshi mjini achukue fomu ya kugombea ubunge 2015 wa jimbo la Moshi Mjini.
Kijana huyo mkazi wa Moshi mjini anaonekana kukubalika kwa jamii yote wazee na vijana,wanawake na wanaume,baadhi ya wakazi wa moshi mjini wanamedai kuwa wao awajali chama gani atagamboe bali wanachotaka ni kumuona kijana huyo analiwakirisha jimbo la Moshi mjini bungeni.wengine wamedai sababu kubwa za kumuunga mkono ni kuwa wanauhakika kuwa Daudi Mrindoko ni mchapa kazi mwenye kuyaelewa mahitaji ya wapiga kura wa Moshi Mjini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelaziz Bouteflika katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na waandishi wa habari baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na Rais wa Baraza la Nchi ya Algeria Mhe. Abdulkhader Bensalah akiwasili katika ukumbi wa El-Mithak Residency jijini Algiers kwa dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelaziz Bouteflika katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Baraza la Nchi ya Algeria Mhe. Abdulkhader Bensalah na viongozi wengine wakipata picha ya kumbukumbu na kikundi cha utamaduni katika ukumbi wa El-Mithak Residency jijini Algiers baada ya dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelaziz Bouteflika katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mabalozi wa nchi za Kiafrika katika ukumbi wa El-Mithak Residency jijini Algiers baada ya dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelaziz Bouteflika katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelmalik Sellal katika kiunga cha Ikulu ya nchi hiyo cha Zeralda Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa viongozi mbalimbali na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelmalik Sellal katika kiunga cha Ikulu ya nchi hiyo cha Zeralda Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelmalik Sellal katika kiunga cha Ikulu ya nchi hiyo cha Zeralda Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
PICHA NA IKULU
Kiswahili inaaminika kuwa lugha asili ya Afrika inayozungumzwa na watu wengi zaidi kusini mwa jangwa la Sahara.
Ni lugha ya taifa kwa nchi za Kenya na Tanzania na pia yazungumzwa kwenye nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Rwanda, Uganda, Visiwa vya Comoro na nchi nyingine
Ikizungumzwa na watu wanaokadiriwa kufikia milioni 100 hivi sasa, Kiswahili ndio lugha pekee ya kiAfrika iliyo miongoni mwa lugha rasmi za Umoja wa Afrika.
Ni lugha muhimu katika habari, shule, kazi za kiofisi, kidiplomasia na hata usalama miongoni mwa mataifa. Lakini , licha ya ukubwa wake, lugha hii inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Hivi karibuni, Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) kilifanya mkutano wake wa nne, ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi. Na amekuwa mkarimu sana kujiunga nasi kuzungumzia juu ya lugha ya Kiswahili na changamoto zake.
KARIBU
Mtayarishaji wa filamu na mwimbaji wa siku nyingi Jennifer Mgendi anakusudia kuachia filamu yake ya “Nipo Studio” mapema wiki hii. Akiongea na blogu hii Jennifer amesema filamu hiyo imekamilika kwa kila kitu na itaingia sokoni wiki hii ikiwa imewashirikisha wasanii mbalimbali akiwamo shosti wake wa siku nyingi Bahati Bukuku, Bibi Esta, Hassan Mbangwa, Gwamaka Kametta na wengine wengi.
Jennifer amesema filamu hii inazungumzia changamoto mbalimbali anazokutana nazo Bibi Esta pale anapokuwa na ndoto ya kuwa mwimbaji huku umri na kipato vikiwa kikwazo kwake.
Wakati huo huo Jennifer amesema maandalizi ya tamasha lake la uzinduzi wa video ya Wema ni akiba yanaendelea vizuri na tamasha hilo litafanyika kama ilivyopangwa tarehe 28 Juni katika kanisa la DCT Tabata Shule huku Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Askofu Mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God , Dr. Barnabas Mtokambali.
Mkuu wa kitengo cha Biashara Maxcom Africa Bw. Deogratius Lazari (Katikati) Akifafanua Jambo kwa waandishi wa habari ambao hawapo katika picha wakati wa Uzinduzi wa Mfumo Mpya wa kutoa huduma za Maxmalipo kwa kutumia simu ya kiganjani, wengine katika picha ni Maasifisa wa Kampuni Kulia msimamizi mauzo na Usambazaji kanda ya mashariki Bwan Bw. Thomas Mwakalembile na Geofrey Mwakamyanda
Maxcom Africa maarufu kama MaxMalipo ni kampuni ya kitanzania iliyoanzishwa mwaka 2010 ambayo imewekeza katika kurahisisha maisha ya Watanzania na Waafrika kwa ujumla kiuchumi na kijamii kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano (ICT Technology).
Ili kufikia malengo na Sera ya Taifa ya kutumia mifumo ya kielekroniki kutoa huduma na pia kuwezesha Watanzania walio wengi kufikiwa na huduma hizi (Financial Inclusion) na pia kurahisisha ukusanyaji wa kodi na kuongeza ajira, MaxMalipo imeanzisha huduma mpya itakayomuwezesha mtanzania kulipa bili zote kwa kutumia simu ya kiganjani aina ya Smart phone yenye Mfumo utakaojulikana kama SmartMalipo.
Huduma hii inatarajiwa kutoa ajira kwa watanzania takribani laki mbili (200,000) nchi nzima kufikia mwaka 2016 na hivyo kuchangia ukuaji wa sekta isiyo rasmi ya ajira na kunyanyua uchumi wa Nchi. Mfumo huu utaweza kurahisisha ulipaji wa bili mbalimbali Mfano; Umeme (Luku), Ving’amuzi vya Televisheni, Vocha za Mitandao yote, Kulipia Kodi za TRA na Baadae Kufanya Miamala ya Kibenki inayohusisha Kuweka na Kutoa fedha, huduma ambazo kwa sasa zinalipwa kupitia mashine za MaxMalipo.
Huduma hiyo inapatikana kwenye mfumo wa simu ya kiganjani ambapo mtumiaji atalazimika kuweka mfumo wa SmartMalipo (Download Smart Wakala Application) kutoka tovuti ya Google play au tovuti ya Maxmalipo kwa kuandika neno ‘SmartMalipo au Maxmalipo’. Kisha mtumiaji atapata maelekezo ya jinsi ya ku-install mfumo huu kwenye simu yake na jinsi ya kutumia. Mfumo huu utamwezesha mtumiaji yeyote kuwa Wakala na kulipia huduma zilizo orodheshwa. Mtumiaji wa mfumo huu atajipatia kamisheni kama alivyo wakala mwingine wa Maxmalipo kwa Huduma atakazofanya.
Watumiaji wa mfumo huu wa SmartMalipo watatambulika kwa jina la ‘Smart Wakala’ popote walipo na kufanya biashara kupitia simu zao za kiganjani. MaxMalipo imeanzisha huduma hii mpya kwa lengo la kuwawezesha watanzania walio wengi kufikiwa zaidi na huduma za malipo kwa haraka wakiwemo wafanyabiashara wadogo na wenye mitaji midogo ambao kwa mazingira yao ni vigumu kuwa na Mashine za Maxmalipo.
MaxMalipo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza matatizo ya foleni kwenye malipo ya huduma mbalimbali kama bili za TRA, LUKU, DAWASCO, huduma za kibenki na hata katika mifuko ya Hifadhi ya jamii Mfano PSPF.
Mwisho kampuni ya Maxcom Africa - Maxmalipo inatoa rai kwa watanzania hasa wafanyabiashara kuchangamkia huduma zinazotolewa na kampuni hii ili kuendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia katika mifumo ya utoaji huduma.
Wakuu wa taasisi za kuzuia Ruswa barani Africa wamekutana katika ukumbi wa mikutano AICC katika kuangalia jinsi gani wataweza kupambana na kufikia malengo ya kutokomeza Rushwa ndani ya Bara La Africa.
Wakuu hao ambao ni wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa barani Afrika AUABC iliyopo chini ya jumuia ya muungano wa nchi za Afrika ambapo mwenyekiti wa Taasisi ya AUABC Jaji Daniel Batidam amesema kuwa wanatarajia kwa mkutano huu utasaidi kupunguza makali ya Ruswa ndani ya bara hili. Amesema kuwa kiwango kikubwa wanaangalia jinsi gani wataweza kuondoa ruswa katika taasisi za jamii kwa maana ndio zinazochangia kwa kiasi kikubwa maenbdeleo ya nchi zetu za kiafrika.
Pamoja na hayo amesema kuwa tatizo kubwa la Rushwa ndani ya bara la Afrika ni mfumo uliopo ambao unakuwa unaweka mianya ya rushwa pamoja na hayo alisisistiza kwa wananchi kuacha kutoa rushwa ili kuiondoa kabisa. Bodi hiyo imeundwa na watu 11 kutoka nchi mbalimbali barani Africa.

Makamu Mwenyekiti bodi ya ushauri ya kupambana na maswala ya rushwa katika umoja wa Africa Mh.Florince Ziyambi kutoka Zimbabwe.
0 |
|
0 |
|

Katika Mkutano huo kutakuwa na Majadiliano ya Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka 2015/2016.
Akitoa Muhutasari wa Mkutano huo leo Katibu wa Baraza la Wawakilishi Yahya Khamis Hamad amesema Wajumbe wa Baraza hilo watapata nafasi pana ya kujadili Bajeti hiyo ambayo ndio mwelekeo mzima wa Shughuli zote za kiserikali.
Amesema frusa hiyo nimuhimu kwa Wajumbe hao kuitumia vyema kujadili mambo ya msingi yanayowahusu Wananchi wao badala ya kujadili mambo ambayo hayatakuwa na faida kwao.
Aidha Katibu huyo amewashauri Wananchi wa Zanzibar kushirikiana na wakilishi wao na kujadili masuala yenye kipau mbele nao ili kutatua changamoto zinazo wakabili katika Majimbo yao.
Katibu Yahya amesema Miswaada Miwili ya Sheria itawasilishwa na kujadiliwa ikiwemo mswada wa Sheria ya Fedha na Mswada wa Sheria wa kuidhinisha matumizi ya Serikali kwa mwaka 2015/2016
Aidha amefahamisha kuwa Jumla ya Maswali 81 yataulizwa na kujibiwa katika Mkutano huo.
MWISHO IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR.