Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

MBUNGE NATSE AWATAKA WANANCHI WA KARATU KUJITOKEZA KWA WINGI KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

0
0
Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ambaye pia Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini akihutubia wananchi wake katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa mazingira bora karatu mjini jana,amewataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu  la wapiga kura ambayo itawapa  fursa ya kuwachagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika ockoba mwaka huu. (Habari picha na Jamiiblog).
SAM_2311
Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ambaye pia Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini akiwa anateta jambo meza kuu.
SAM_2293
Wananchi waliojitokeza kwa wingi wakiwa wanamsikiliza Mbunge wao akihutubia mkutano wa hadharakatika uwanja wa mazingira bora karatu mjini
SAM_2292
Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse akiwa anasisitiza jambo jukwaani ambapo alisema njia bora ya kuwapiga chini chama cha mapinduzi CCM ni kwa kuhakikisha wananchi wanajiandikisha katika daftari la kudumu huku akidai safari hii ni jino kwa jino hadi ikulu.
SAM_2279
Mwenyekiti wa vijana Wilaya ya Karatu John Male alisema lengo lao ni kuwaelimisha wananchi hata wasio wanachama kuhusu umuhimu wakujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
SAM_2282
Diwani wa kata ya Karatu mjini Jublate Mnyenye aonya Redio mbao zinazosambaza habari kuwa anampango wa kuihama chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA)adai yeye na chama hicho ni damu damu.
SAM_2265
Wananchi wakimshangilia Mbunge wao.
SAM_2296
Mzee Peter akijichukulia matukio mbalimbali na simu yake ya mkononi
SAM_2294
Wananchi wa Karatu wakiwa makini kusikiliza
SAM_2304
Mwananchi akieleza kero yake kwa Mbunge wake
SAM_2312
Jackine ambaye aliwakilisha wanawake akiuliza swali kwa Mbunge wake juu ya Hospitali za serikali kukosa dawa

Tanzania yawa Mwenyeji wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Vyuo vya Kodi Afrika.

0
0
01
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo akitoa neno kuwakaribisha wageni katika mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Vyuo vya Kodi Afrika uliohudhuriwa na wajumbe zaidi ya 50 kutoka katika taasisi za kodi barani Afrika, Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Taasisi za Kodi Afrika (ATAF), leo Jijini Dar es Salaam.
02
Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Kodi Tanzani (ITA) Prof. Isaiah Jairo akiongea na wajumbe wa mkutano huo na kueleza namna utakavyosaidia katika kuzijengea uwezo Taasisi za ukusanyaji kodi Afrika hivyo kuweza kuinua uchumi wa Mataifa mengi ya Afrika.
03
Mkurugenzi wa Ujengaji Uwezo kutoka Taasisi za Kodi Afrika (ATAF) Bw. Kennedy Onyonyi akiwaeleza wajumbe wa Mkutano huo namna Kamati hiyo inavyoshirikiana na Taasisi za Kodi Afrika katika kuzijengea Taasisi hizo uwezo wa Kiutendaji na kusaidia nchi wanachama kushiriki kuwa na sera ya pamoja ya masuala ya Kodi ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji kodi.
04
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Lusekelo Mwaseba Akiongea na wajumbe waliohudhuria Mkutano huo namna Tanzania ilivyofurahishwa na kuwa mwenyeji wa Mkutano huo wa Kwanza wa wakuu wa vyuo vya uongozi wa Kodi Afrika na kuwataka wajumbe kutumia fursa hiyo kujifunza masuala mbalimbali katika sekta hiyo ya ukusanyaji kodi kwani ni moja ya mhimili muhimu wa maendeleo kwa Mataifa mengi duniani.

06
Mkurugenzi Ujengeaji Uwezo kutoka Taasisi za Kodi Afrika (ATAF) Bw. Kennedy Onyonyi akiwasilisha Mada wakati wa Mkutano huo wa kwanza unaofanyika Nchini Tanzania.
07
Mkurugenzi Ujengeaji Uwezo kutoka Taasisi za Kodi Afrika (ATAF) Bw. Kennedy Onyonyi akiwasilisha Mada wakati wa Mkutano huo wa kwanza unaofanyika Nchini Tanzania.
05 
Wakuu wa vyuo vya uongozi wa Kodi Barani Afrika wakiwa katika picha ya pamoja

Download App Ya Mjengwablog Upate Mengi Kwenye Simu Yako...!

0
0
Matukio mbalimbali, Habari za magazetini, Uchambuzi wa Habari, picha, burudani na kusikiliza live Kwanza Jamii  Radio.. http://mjengwablog.com

Waziri Membe amuenzi Marehemu Brigedia Generali Hashim Mbita

0
0



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Bregedia Generali Hashim Mbita, kilichotokea hivi karibuni katika Hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam. Marehemu Brigedia Generali Mbita aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambabwe pia atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwenye harakati za ukombozi Barani Afrika.
Waziri Membe akimpa pole Mjane wa Marehemu Bregedia Generali Mbita, Bi. Ngeme Mbita  
Mhe. Membe akimpa pole mtoto wa Marehemu Brigedia Generali Mbita Bi. Sheilla Mbitta
Waziri Membe akizungumza na wafiwa 
Waziri Membe akisalimiana na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini mara baada ya kuwasili kwenye  Msiba wa Brigedia Generali Hashim Mbita
Waziri Membe akisalimiana na aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zuberi Zitto Kabwe walipokutana kwenye msiba wa Brigenida Generali Mbita 
Waziri Membe akiwa amejumuika  na Waombolezaji wengine kwenye msiba wa Brigedia Generali Mbitta nyumbani kwake Chang'ombe Jijini Dar es Salaam.
Waziri Membe akizungumza na waandishi wa Habari juu ya kifo cha Brigedia Generali Mbita. Waziri Membe alimwelezea Balozi Mbita kama kiongozi makini na mwadilifu na pia alikuwa mwanaharakati mahiri ambaye alihakikisha Bara lote la Afrika linakuwa huru. Picha na Reginald Philip

Taarifa ya kifo kwa vyombo vya habari kutoka JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ).

0
0


Brigedia Jenerali Hashim Iddi Mbita (mstaafu) enzi za uhai wake.


JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

Simu ya Upepo   : “N G O M E”             Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM  22150463         Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                          DAR ESSALAAM,  28 Aprili, 2015.
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz
                  
Taarifa ya kifo kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha Brigedia Jenerali Hashim Iddi Mbita(mstaafu) kilichotokea tarehe 26 Aprili 2015, 
Brigedia Jenerali Hashim Mbita(mstaafu) alizaliwa tarehe 02 Novemba 1933 katika mtaa wa Songoro, Kata ya Gongoni, Wilaya ya Tabora Mjini, katika Mkoa wa Tabora.  Alisoma shule ya Msingi ya Government Town Primary School Mkoani Tabora kuanzia mwaka 1946 hadi 1949. Alijiunga na Government Secondary School Tabora Mwaka 1950 hadi alipohitimu kidato cha sita Mwaka 1957. Mwaka 1960 alijiunga na Chuo cha East African School of Co-operatives kilichopo Nchini Kenya.  

Marehemu Brigedia Jenerali Hashim Mbita baada ya masomo yake alijiunga na JWTZ tarehe 01 Novemba, 1968 na kutunukiwa Kamisheni tarehe 26 Aprili, 1969.  Alistaafu Utumishi Jeshini kwa Heshima tarehe 31 Desemba 1992.
 
Katika utumishi wake marehemu alishika Madaraka mbalimbali Ikiwemo Mkaguzi msaidizi Mkoa wa Mwanza mwaka 1958 hadi 1960, Afisa Habari Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 1960 hadi 1962, Afisa Habari Mkuu wa Serikali mwaka 1962 hadi 1965, Mwandishi wa Habari wa Rais mwaka 1965 hadi 1967, Katibu mwenezi wa TANU Mkoa wa    Dar es Salaam mwaka 1967 hadi 1968,


Mwalimu wa Siasa Chuo cha Maafisa Monduli 1969 hadi 1970, Katibu Mtendaji wa OAU Kamati ya Ukombozi mwaka 1972 hadi 1989 na Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe mwaka 2003 hadi 2006.

Marehemu Brigedia Hashim Mbita ameacha mke na watoto.  Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa rasmi tarehe 29 Aprili, 2015 kuanzia saa 1:30 hadi 5:00 asubuhi katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na mazishi yatafanyika katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, saa 10:00 jioini baada ya Sala ya adhuhuri.


MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU
BRIGEDIA JENERALI HASHIM IDDI MBITA (MSTAAFU)
AMINA


 Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 – 309963




WANAFUNZI WA CHUO CHA UALIMU PATANDI WAZUIA BARABARA YA ARUSHA MOSHI KWA SAA MBILI

0
0

kamanda wa polisi mkoa wa Arusha
Hali ya Sintofahamu imeukumba mji wa Tengeru leo Asubuhi baada ya wanafunzi wa chuo cha ualimu Patandi Kufunga barabara kwa muda wa masaa mawili na kuacha shughuli za maendeleo kusimama kwa muda huku magari  ya abiria yanayokwenda katika mikoa ya Kilimanjaro,Tanga na Dar es salaam na mji mdogo wa usa river na maeneo mengine kupata adha hiyo.

Wanafunzi hao walizuia bara bara hiyo  wakishinikiza madai yao kusikiliza kwani wameshatoa malalamiko yao kwa uongozi wa chuo hicho bila ya kushughulikiwa kwa muda sasa wakiainisha kuwa wamekuwa wakipatiwa adhabu zisizo stahiki ikiwemo kurushwa kichura kuchapwa makofi huku kanuni za utumishi zikivunjwa na uongozi wa chuo hicho cha ualimu Patandi kilichopo wilayani Meru..

Wakizungumza kwa nyakati Tofauti na libeneke la kaskazini  blog  Mmoja wa wanafunzi  Jenny Mlay  alisema kuwa leo Asubuhi mkuu wa chuo alimkuta mwanafunzi mwenzao amelala bwenini akiumwa na kuacha taa ikiwa inawaka na ndipo alimpiga makofi na wao kwa umoja wao wakaamua kuingia barabarani ilikufikisha kilio chao cha muda mrefu.

Alisema kuwa kumekuwepo na unyanyasaji wa wanafunzi kwa kupewa adhabu zisizoendana na maadili ya vyuo ikiwemo kupiga magoti,kuruka kichura, na nyingine kama hizo ambazo ni kinyume na haki za binadamu na kanuni za chuo.

“Utakuta mtu anarukishwa kichura tena muajiriwa ambaye amekuja kuongeza daraja hapa chuoni huyu sio mwanafunzi wa darasa la kwanza hivyo tumefikisha ujumbe wetu mara nyingi kwa uongozi lakini hatupatiwi majibu ndio tukaamua kufunga barabara ilikufikisha ujumbe wetu kuwafikia walengwa”alisema Mlay


Mlay alisema kuwa kufuatia malalamiko yao kupuuzwa na tukio la Asubuhi la kupigwa kwa mwenzao wao wanautaka uongozi akiwemo mkuu wa chuo hicho kuachia ngazi kwani amekuwa ndio tatizo la migogoro hapo chuoni.

Nae Mkuu wa chuo hicho cha ualimu patandi Zaina Kabelwa akijibu hoja zilizotolewa na wanafunzi hao alisema kuwa ualimu wao unaishia Geti la chuo na wakishaingia chuoni hapo wanakuwa kama wanafunzi wengine wa vyuo na wanatakiwa kufuata kanuni na sheria za chuo.


Kabelwa alisema kuwa matumizi ya vifaa vya chuo yakiwemo majengo na usafi wa mazingira ni kwa kila mwanafunzi bila ya kujali huyu ni mwajiriwa au la wote wananafasi sawa kwa mujibu wa kanuni za chuo hicho

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wale wote wenye kuvunja sheria kufuata mikondo ya sheria ikiwemo kufuata mamlaka husika ili malalamiko yao yaeweze kupatiwa ufumbuzi na sio kuchukuwa sheria mkononi.

Kamanda Sabas alisema kuwa wanafunzi hao walisimamisha msafara wa magari kwa saa mbili hadi walipotawanya na askari wake wa kituo cha usa river baada ya kukaidi amri ya mkuu wa chuo hicho aliewataka warudi chuoni hapo iliwaweze kukaa na kujadili mamalamiko yao.

"Nawasihi wote wanajichukulia sheria mikononi kufuata sheria bila shuruti kwani jeshi hilo lipo macho kwa wote wanaovunja sheria kwani sheria itachukuwa mkondo wake bila ya kumuonea mtu"alisisitiza Sabas

Wanafunzi 60,000 wa UDOM kufurahia Airtel WI-FI

0
0
  Afisa masoko wa Airtel tanzania Prospa Mwanda akionyesha kwa wanafunzi wa chuo Kikuu dodoma (UDOM) jinsi huduma mpya ya Airtel Wi-Fi Intaneti  inavyofanya kazi mara baada ya uzinduzi wa huduma hiyo chuoni hapo jana. Airtel Tanzania chuoni hupo imezindua huduma ya UNI Wi-Fi Intaneti yenye ubora zaidi na itakayopatikana kwa wananfunzi kwa gharama nafuu. 
 Meneja masoko wa Airtel Uni Wi-Fi Bi Aneth Muga anaepiga picha ya selfie ili waitume kwa kutumia huduma ya Airtel Wi-Fi intaneti kwa baadhi ya uongozi wa wanafunzi na mshauri wa wanafunzi chuoni hapo mara baada ya Airtel kuzindua huduma yao ya  intaneti Wi-Fi yenye kasi zaidi  maalum kwa wanafunzi wa chuo hicho jana. 
 Mshauri wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) bw, Dick Manong akiongea na wanafunzi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel UNI Wi-Fi jana chuoni hapo ambapo itawasaidia wanafunzi kupata intaneti kwa gaharama nafuu ya yenye kasi zaidi.
 Wanafunzi 60,000 wa UDOM kufurahia Airtel WI-FI
• Pia Airtel yazinduzi mnara wa pili UDOM

Dodoma, Aprili 27, 2015, kutokana na ukweli kwamba Dodoma ni mji mteule na wenye kuendelea kwa kasi hapa nchini na pia ni mji uliobahatika kuwa miongoni mwa mji wenye chuo kikubwa hapa Tanzania, Airtel Tanzania mkoani huko imezindua huduma ya UNI Wi-Fi Intaneti yenye ubora zaidi na itakayopatikana kwa wananfunzi kwa gharama nafuu.

UNI WI-FI itawezesha wanafunzi zaidi ya 60,000 katika Chuo Kikuu cha Dodoma kupata huduma ya kimtandao ya Intaneti iliyo bora na nafuu pamoja na  kukidhi mahitaji ya wote waishio chuoni hapo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Airtel Bi , Adriana Lyamba alisema: "Leo hii tunazindua Airtel UNI WI- FI huduma ya internet inayopatikana kwa bei nafuu kwa ajili ya wanafunzi na  pia tumeongeza mnara wa pili  wa simu   ambao tunaamini utaimarisha mtandao wetu hapa UDOM na kuinua uchumi  wa nchi yetu na kwa watu wanaoishi karibu na maeneo haya ".

Tunafuraha kubwa kwa Airtel kuweza kuboresha Maisha ya wanafunzi hapa chuoni  kwani spidi hii itawawezesha wanafunzi kuweza kufanya utafiti wao, kupata habari mbalimbali za  taaluma au kijamii  kupitia mtandao wetu wa Airtel "

Meneja Masoko wa Airtel UNI WI-FI, Bi, Aneth Muga, alisema "Airtel wifi itakuwa inapatikana kwa mwanafunzi yoyote hapa  UDOM, kwa kutumia simu zao za mkononi, laptop, kamera na kwa mwanafunzi yoyote aliyepo UDOM bila kujali mtandao wa simu wanaoutumia.

Wanaweza kununua UNI Wi-FI vocha ambayo inapatikana  masaa 24 , kwa kifurushi cha siku , wiki,  mwezi na kifurushi cha usiku mzima.
Fikiria! Unaweza kufurahia kifurushi cha 1 GB kwa shilingi  500 tu! Alisisitiza Bi, Muga

Kwa upande wake mgeni rasmi ambae ni mshauri wawanafunzi chuoni hapo (UDOM) Bw, Dick Manongi   alisema: ". Tunawashukuru sana Airtel Tanzania kwa ajili ya uzinduzi wa huduma hii kubwa na ya bei nafuu hapa chuoni. Nina hakika kwamba, huduma hii itaimarisha uwezo wa kujifunza na kuendelezea wanafunzi  urahisi wa kujipatia Habari mbalimbali zinazoendelea hapa nchini na hata nje ya nchi ".

Ningependa kuwaomba wanafunzi wote kutumia fursa hii kubwa ili kuweza kuongeza ujuzi wao kitaaluma na katika Maisha yao ya baadae.

Uzinduzi wa Airtel Uni Wi- Fi katika chuo kikuu cha Dodoma umekuja mara baada ya Airtel Tanzania kuzindua huduma kama hiyo katika chuo kikuu cha Saint Augustine (SAUT) jijini Mwanza na mipango mingine inaendelea kufikia vyoo vingine hapa nchini.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, LAZARO NYALANDU AFANYA ZIARA KATIKA VIJIJI VINAVYOZUNGUKA HIFADHI YA RUAHA KUTATUA MIGOGORO YA WANANCHI NA WAWEKEZAJI

0
0
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kuhusu eneo la hifadhi  lililoombwa kwa ajili ya upanuzi wa manispaa ya Iringa wakati wa ziara ya waziri wa maliasili na utalii mkoani Iringa leo. (Picha zote na Loveness Bernard)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu  akifafanua jambo katika mkutano wa kutatua mgogoro kati ya wawekezaji na wananchi wanaozunguka hifadhi ya Ruaha (mbomipa). Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

Na Loveness Bernard

SERIKAli imeagiza Jumuia zote za hifadhi za jamii (WMA) nchini kutoingia mikataba na wawekezaji mpaka wanasheria wa wizara ya Maliasili na Utalii kuiidhinisha.

Akizungumza mjini Iringa, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amesema kuwa jumuia hizo zimekuwa zikiingia mikataba ambayo inasababisha wananchi kushindwa kunufaika na rasilimali za maliasili zilizoko katika maeneo yao.

“Migogoro katika hizi jumuia imekuwa mingi karibu nchi nzima, na kwa sasa nadhani imefika wakati kila mikataba lazima iangaliwe na wanasheria katika wizara yangu ili tuweze kujua kama mikataba imekaa sawa”.

Nyalandu ambaye alikuwa mkoani Iringa kwa ajili ya kusikiliza mgogoro wa WMA ya Mbomipa alisema kwamba kwa kipindi kirefu wananchi wa zaidi ya vijiji 20 wilayani Iringa wameshindwa kunufaika na rasilimali hizo.

‘’Wananchi waishio katika vijiji zaidi ya 20 Iringa hawajanufaika na rasilimali zilizoko katika hifadhi ya Ruaha kutokana na mfumo ambao haujawa rahisi kwa watumiaji wa WMA wote nchini , wizara wameamua kurekebisha ili waweze kuepuka migogoro kama hiyo na mikataba yote itakaguliwa na wizara’’

Aidha waziri huyo amekubali ombi la manispaa ya Iringa la kuongeza eneo la iliyokuwa hifadhi ya taifa ya Kihesa kilolo kuwa eneo la Manispaa hiyo kwa jili ya upanuzi wa mji wa Iringa.

 Ombi hilo lilitolewa na Manispaa ya Iringa ikiwa ni ombi la kutaka kubadilisha matumizi ya eneo hilo lililokuwa hifadhi kuw amakazi ya watu kwa ajili ya upanuzi wa mji ombo walilotoa kupitia kwa Waziri wa Ardhi Willia Lukuvi.

MBUNGE NDESAMBURO NA MEYA WA MOSHI JAFARY MICHAEL WAENDELEA NA MIKUTANO KATIKA JIMBO LA MOSHI MJINI.

0
0
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika jirani na Super Market ya Nakumat.
Baadhi ya wananchi waliofika katika mkutano huo wakimsikiliza Ndesamburo.
Ndesamburo akizungumza.
Baadhi ya viongozi wa Chadema akiwemo mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi ,Jafary Michael wakimsilikiza Ndesamburo.
Msatahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Jafary Michael akizungumza katika mkutano wa hadhara .
Mbunge waMoshi mjini Philemoni Ndesamburo akimsikiliza Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi.(hayuko pichani) akiwa na viongozi wengine wa Chadema.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Moshi.

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MLIMANI WAPATIWA MAFUNZO.

0
0
Na Loveness Bernard

SERIKAli imeagiza Jumuia zote za hifadhi za jamii (WMA) nchini kutoingia mikataba na wawekezaji mpaka wanasheria wa wizara ya Maliasili na Utalii kuiidhinisha.

Akizungumza mjini Iringa, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amesema kuwa jumuia hizo zimekuwa zikiingia mikataba ambayo inasababisha wananchi kushindwa kunufaika na rasilimali za maliasili zilizoko katika maeneo yao.

“Migogoro katika hizi jumuia imekuwa mingi karibu nchi nzima, na kwa sasa nadhani imefika wakati kila mikataba lazima iangaliwe na wanasheria katika wizara yangu ili tuweze kujua kama mikataba imekaa sawa”.

Nyalandu ambaye alikuwa mkoani Iringa kwa ajili ya kusikiliza mgogoro wa WMA ya Mbomipa alisema kwamba kwa kipindi kirefu wananchi wa zaidi ya vijiji 20 wilayani Iringa wameshindwa kunufaika na rasilimali hizo.

‘’Wananchi waishio katika vijiji zaidi ya 20 Iringa hawajanufaika na rasilimali zilizoko katika hifadhi ya Ruaha kutokana na mfumo ambao haujawa rahisi kwa watumiaji wa WMA wote nchini , wizara wameamua kurekebisha ili waweze kuepuka migogoro kama hiyo na mikataba yote itakaguliwa na wizara’’

Aidha waziri huyo amekubali ombi la manispaa ya Iringa la kuongeza eneo la iliyokuwa hifadhi ya taifa ya Kihesa kilolo kuwa eneo la Manispaa hiyo kwa jili ya upanuzi wa mji wa Iringa.

 Ombi hilo lilitolewa na Manispaa ya Iringa ikiwa ni ombi la kutaka kubadilisha matumizi ya eneo hilo lililokuwa hifadhi kuw amakazi ya watu kwa ajili ya upanuzi wa mji ombo walilotoa kupitia kwa Waziri wa Ardhi Willia Lukuvi.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kuhusu eneo la hifadhi  lililoombwa kwa ajili ya upanuzi wa manispaa ya Iringa wakati wa ziara ya waziri wa maliasili na utalii mkoani Iringa leo. (Picha zote na Loveness Bernard)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu  akifafanua jambo katika mkutano wa kutatua mgogoro kati ya wawekezaji na wananchi wanaozunguka hifadhi ya Ruaha (mbomipa). Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

UWASILISHWAJI WA MPANGO NA UKOMO WA BAJETI KWA MWAKA 2015/16

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
 TAARIFA KWA UMMA
YAH: UWASILISHWAJI WA MPANGO NA UKOMO
WA BAJETI KWA MWAKA 2015/16
_______________

Kesho Jumatano tarehe 29 Aprili, 2015 Wabunge wote kwa ujumla wao watakutana katika Ukumbi wa Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam kupokea Mapendekezo ya Mpango, Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2015/2016 kwa mujibu ya matakwa ya Kanuni ya 97 ya kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la 2013.

Shughuli hiyo itaanza rasmi saa tatu na nusu asubuhi kwa Waheshimiwa Wabunge na Washiriki wote kuwasili na kuketi Ukumbini kabla ya ukaribisho utakaotolewa na Naibu Spika amabaye pia atakuwa mwenyekiti wa Mkutano huo na kufuatiwa na neno la utangulizi kutoka kwa Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda.

Aidha, Uwasilishwaji wa Mapendekezo ya Mpango wa Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016 yatafanyika kuanzia saa nne asubuhi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahususiano na Uratibu) Mhe. Dkt. Mary Nagu (Mb) na kufuatiwa na uwasilishwaji wa mapendekezo ya kiwango na ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (Mb).

Shughuli hiyo inatarajiwa kumalizika saa sita mchana, na baadae kamati za Bunge kuendelea na utekelezaji Majukumu yake kulingana na ratiba za kamati.


Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
28 Aprili 2015



Mama wa Mitindo Asya Idarous, Gusagusa Min band kufanya maonyesho Uingereza

0
0
11169017_958488377518759_1048095244_n
Bana ya shoo hiyo ya Gusagusa Min band na Asia Idarous Khamsin itakayofanyika nchini Uingereza

London, Uingereza
Mbunifu wa mavazi nchini ‘Mama wa Mitindo’, Asia Idarous Khamsin yupo nchini Uingereza akiwa ameambatana na magwiji wa muziki wa taarab kutoka Tanzania, Gusagusa Min Band ambao watafanya maonyesho makubwa ndani ya miji ya nchi hiyo ikiwemo London na Northampton.
Kwa mujibu wa wandaaji wa shoo hiyo nchini humo, Kampuni ya Didas Entertainment ya Uingereza walieleza kuwa, shoo ya kwanza itakuwa Mei 2, katika viunga vya mji wa London na shoo nyingine ni Mei 3 katika mji wa Northampton ambapo kutakuwa na fashion shoo ‘Divas Catwalk’ itakayopambwa na Mama wa Mitindo, Asia Idarous.
11069501_10152884668557684_7139946682781219300_n
Magwji Afua, Mwanahawa, Asya Idarous na Achun Baa meneja wa Gusagusa min Band ndani ya UK.

“Gusagusa Min Band na Mama wa Mitindo, Asia Idarous, Tayari wapo ndani ya viunga vya Uingereza na wapo kamili kwa shoo kabambe Mei 2 ndani ya Empire Suite, London na shoo ya Mei 3, ndani ya Academy, mji wa Northampton. Gusagusa ipo full band nzima ikijumuisha wapiga vyombo wao” ilieleza taarifa hiyo kutoka Didas Entertainment.

Aidha, katika safari hiyo, Asia Idarous ameongozana na wadau wengine wakiwemo Mkurugenzi wa Gusagusa Mind Band, Hasan Farouk, gwiji wa taarab, Bi Afua Suleiman (muimbaji), Bi Mwanahawa Ally (muimbaji), Jaffer bhai (muimbaji), Khamis Chizi (master keyboard ) na Abdulla Ngonda (mpiga base) na wengineo wengi.
11178372_957991814235082_5347065811729573025_n
Mama wa Mitindo, Asya Idarous Khamsin (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Gusagusa Min Ban, Achun Baa na Hamis chizi 'Master keyboard' ndani ya viunga vya Milton Keynes UK (Uingereza).
Didas Entertainment imekuwa ikifanya shughuli mbalimbali za burudani ikiwemo kupeleka wasanii kutoka Tanzania na kupiga shoo nchini Uingereza pamoja na shughuli zingjne za Sanaa ikiwemo filamu, wasanii wa filamu na uandaaji wa filamu, ambapo hadi mwaka huu imeweza kutimiza miaka 10, tokea kuanzishwa kwake.
11009174_10152877662767684_2829549992663885067_n
Asia Idarous na waimbaji gwiji
11188171_957971547570442_5616187021648209676_n
Asya Idarous ndani ya pozi kweney viunga vya Milton Keynes United kingdom
11178232_10152886994017684_7247829965855112253_n
Kwa kuweka oda ya kupata tiketi ndani ya UK, whatsapp +447556171941 kwa ku reserve tables.
With Didas fashions and Mwanahawa ally
Asya Idarous na Didas fashions pamoja na Mwanahawa ally
1375172_10152872390352684_5056457734253432038_n
Achuu Baa meneja wa Gusagusa akiwa ndani ya ndege wakati wa kuwasili kwake ndani ya UK tayari kwa shoo hiyo Mei 2 na Mei 3.
11149355_842666905806201_697106551785747428_n
Gusagusa Mind Band ndani ya UK wakiwa kamili na wenyeji wao.

MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KWA MWAKA 2015

0
0

 Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (kulia)akishaurina na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(katikati) leo mjini Songea wakati wa mazoezi ya mwisho ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2015.Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi(mwenye kofia nyeupe) na Katibu wa Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Juma Mswadiki(mwenye tshirt ya bluu bahari)
 Naibu Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia  (wa pili kulia)akishaurina na Katibu Mkuu wa Mkuu wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga leo mjini Songea wakati wa mazoezi ya mwisho ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2015.Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi(mwenye kofia nyeupe) na Waziri wa Uwezeshaji , Ustawi wa Jamii , Vijana ,wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Zainabu Omary Mohamed(kushoto)
 Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (katikati)akishaurina na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kushotoi)  na Waziri wa Uwezeshaji , Ustawi wa Jamii , Vijana ,wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Zainabu Omary Mohamed(kulia) leo mjini Songea wakati wa mazoezi ya mwisho ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2015, utakaozinduliwa tarehe 29.4.2015 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
 Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangaraakizunguza na wandishi wa habari leo mjini Songea.
Kikundi cha sanaa cha Mlale JKT mkoani Ruvuna kikitumbuiza leo mjini Songea wakati wa mazoezi ya mwisho ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2015 ,utakaozinduliwa tarehe 29.4.2015 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA MAREKANI BILL CLINTON JIJINI DAR ES SALAAM APRIL 28, 2015.

0
0
01
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Mstaafu wa Marekani Mhe Bill Clinton Ikulu jijini Dar es salaam leo April 28, 2015.na kisha kufanya mazungumzo na rais huyo wa 42 wa Marekani yuko nchini  kukagua miradi ya maendeleo na afya inayofadhiriwa na taasisi za Clinto Development Initiative (CDI) na Clinto Health Access Initiative (CHAI).
2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe Bill Clinton Ikulu jijini Dar es salaam leo April 28, 2015.rais huyo wa 42 wa Marekani yuko nchini  kukagua miradi ya maendeleo na afya inayofadhiriwa na taasisi za Clinto Development Initiative (CDI) na Clinto Health Access Initiative (CHAI).PICHA NA IKULU

AMIRI JESHI MKUU NA RAIS WA TANZANIA DKT. JAKAYA KIKWETE AZINDUA MELI VITA ZA JESHI LA WANAMAJI

0
0

1
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa amri kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015
2
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mara baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015
34
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na makamanda wa meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015
5
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Chifu Edward Wanzagi wa kabila la Wazanaki (kati) pamoja na Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe Makongoro Nyerere baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015
PICHA NA IKULU

Dkt. Shein mgeni rasmi uzinduzi wa Mbio za Mwengi wa Uhuru mkoani Ruvuma.

0
0
Na: Frank Shija, WHVUM

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2015 ambazo Kitaifa zinafanyika Mkoani Ruvuma.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waizri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara wakati wa mazoezi ya ya mwisho yaliyofanyika katika Uwanja wa mpira wa Majimaji mjini Songea.

Waziri Fenella amesema kuwa maandalizi yameenda vizuri na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika sherehe hizo za uzinduzi wa mbuio za Mwenge na kutoa hamasa zaidi kwa Vijana wotye nchini kushuhudia uzinduzi huo ata kwa vile utaonyeshwa moja kwa moja kupitia Televisheni ya Taifa (TBC).

"Nisema tu kuwa maandalizi yamekwenda vizuri sana mmejionea vijana wa Halaiki walivyo onyesha umahiri wao, niwatate tu wakazi wa mjini wa Songea mjitokeze kwa wingi kuja kushuhudia sherehe hizi za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru lakini pia VIjana nchini kote shuhudieni tukio hili muhumu kwa kuwa litaonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa TBC" Alisema Dkt.Fenella

Aidha Waziri Fenella alitoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi katika zoezi a kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura na baadaye watumie demokrasia kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka 2015 zinazindulia rasmi tarehe 29 Aprili 2015 mkoani Ruvuma na kilele chake kitakuwa tarehe 14 Oktoba mkoani Dodoma ambapo mbo hizo kwa mwaka huu zimebeba kauli mbiu ya "Tumia Haki yako ya Kidemokrasia" Jiandikishe na kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. 

Mwenge huo wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa katika halmashauri 168 za mikoa 30 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

WAZIRI WA MEMBE AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA MAREKANI BILL CLINTON JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe Membe akimkaribisha Rais Mstaafu wa Marekani Mhe Bill Clinton Ikulu jijini Dar es salaam Aprili 28, 2015. Rais huyo wa 42 wa Marekani yuko nchini kukagua miradi ya maendeleo na afya inayofadhiriwa na taasisi za Clinton Development Initiative (CDI) na Clinto Health Access Initiative (CHAI).

FANYENI REDIO ZENU ZITAMANIKE, WAMILIKI REDIO JAMII WAAMBIWA

0
0
DSC_0088
Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Bw. Ramadhan Ahungu akiendesha mafunzo ya masoko na mpango biashara kwa viongozi wa redio jamii nchini wakati kuhitimisho la warsha ya awamu ya kwanza ya mradi wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kuzipa uwezo Redio hizo katika matumizi ya Tehama na Mawasiliano iliyoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO ambayo imefanyika katika kituo cha Redio jamii Sengerema Telecentre mkoani Mwanza.

DSC_0219
Meneja wa kituo cha Redio Jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Adelina Lweramula akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo yaliyomalizika jana kwenye kituo cha Redio Jamii Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.
DSC_0229 
Meneja wa kituo cha Redio Jamii Kahama FM ya Shinyanga, Marco Mipawa akiuliza swali kwa mkufunzi wa warsha ya mafunzo ya masoko na mpango biashara (hayupo pichani) wakati wa kuhitimisha warsha ya awamu ya kwanza inayofadhiliwa na mradi wa SIDA kwa kushirikiana na UNESCO iliyomalizika jana katika kituo cha Redio Jamii cha Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.
  DSC_0067
Pichani juu na chini ni Viongozi wa Redio Jamii nchini walioshiriki mafunzo ya masoko na mpango biashara yanayofadhiliwa na mradi wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kuzipa uwezo Redio hizo katika matumizi ya Tehama na Mawasiliano na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO ikiwa ni hitimisho la warsha ya awamu ya kwanza ya mradi huo yaliyofanyika katika kituo cha Redio Jamii Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.
DSC_0064DSC_0082
Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Ramadhan Ahungu akiendelea kuwapiga msasa viongozi hao namna ya kutafuta masoko na kuboresha mpango biashara.
DSC_0236
Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Ramadhan Ahungu (kulia) akibadilishana mawazo na Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph (wa pili kulia) wakati wakijiandaa kwa zoezi la picha ya pamoja. Kushoto ni Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa vituo vya Redio Jamii nchini.
DSC_0246
Picha ya pamoja ya Wakufunzi na washiriki wa warsha ya mafunzo ya masoko na mpango biashara iliyomalizika jana katika kituo cha Redio Jamii Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.

Na Mwandishi wetu, Mwanza
WAMILIKI wa redio za jamii wametakiwa kujenga taswira njema za redio zao ikiwa wanataka redio zao zitamanike na kutumiwa na wadua mbalimbali wa maendeleo nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Ramadhan Ahungu.

Akizungumzia malengo ya warsha hiyo na madhumuni yake alisema kwamba kuwapo kwa mpango wa biashara ndani ya redio hizo hakutakuwa na maana kama wasipozingatia ujenzi wa taswira utakaowafanya wadau kuvutiwa na redio hizo. Alisema kuna umuhimu wa suala hilo kwani kusipojengeka kwa mahusiano bora kati yake na jamii, watu binafsi na taasisi za kiraia zenye malengo tofauti katika kuhudumia wananchi, redio hizo hazitakuwa na biashara ya kufanya.

Ahungu pamoja na kusifia mtindo uliotumika kuwezesha redio hizo kuandaa mipango kazi ya biashara yenye lengo la kusimamia masoko na fedha alisema warsha imefanikiwa kuwaweka karibu zaidi na wadau wamiliki wa vyombo hivyo. Warsha hiyo ni hitimisho ya awamu ya kwanza kwa ufadhili wa mradi wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kuzipa uwezo redio za jamii katika matumizi ya Tehama na mawasiliano inayoratibiwa na Shirika la Kimataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO iliyofanyika katika kituo redio cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza.

Alisema katika warsha hiyo wamiliki hao walijifunza uandaaji wa mipango ya biashara, kutunza fedha, utafutaji masoko, uhakiki wa mipango ya biashara na vipindi vya redio kwa lengo la kuona namna ya kuvifanya kuleta biashara. Naye Meneja wa kituo cha Redio Jamii Kahama FM ya Shinyanga, Marco Mipawa akizungumzia mafunzo hayo alisema yamemsaidia sana katika kuhakikisha kwamba kituo chake kinakuwa bora na kinachovutia watangazaji.Alisema mafunzo hayo yamewafanya wajitambue kwani yamefanyika mfululizo kwa mara 5 na kuwafanya wabadilike.

Aidha Meneja wa kituo cha Redio Jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Adelina Lweramula alisema kwamba anashukuru mafunzo kwa kuwa yamewafanya kuondoa mawazo vichwani na kuweka mipango kazi katika karatasi na kuwezesha wafanyakazi nao kufuatilia.

BENKI YA EXIM YAJIDHATITI KUIUNGA MKONO SERIKALI KATIKA VITA DHIDI YA MALARIA

0
0
 Meneja Mkuu wa Benki ya Exim tawi la Arusha Bw. Fredrick Umiro (kulia) akikabidhi vyandarua vyenye dawa kwa Mtaalamu wa masuala ya upasuaji katika hospitali ya  Mount Meru iliyopo jijini Arusha,  Dkt. Zubera Mtengwa (wa pili kushoto).Wakishuhudia pembeni ni Meneja Mauzo wa benki ya Exim Arusha Bw Bw. Assed Ali Naqvi (kushoto)na wawakilishi kutoka hospitali hiyo.Msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani inayoadhimishwa kote ulimwenguni Aprili 25 ya kila mwaka
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula iliyopo Mkoani Mtwara Dkt. Mohamed Gwao (wa pili kulia) pamoja na Meneja Huduma kwa Wateja na Uendeshaji wa Benki ya Exim Tawi la Mtwara Bw. Chande S. Chande (kulia) wakionyesha baadhi ya vyandarua vilivyowekewa dawa ikiwa ni msaada kutoka benki hiyo. Wakishuhudia tukio hilo ni baadhi ya wawakilishi kutoka benki ya Exim Mtwara na hospiatali hiyo. Msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani inayoadhimishwa kote ulimwenguni Aprili 25 ya kila mwaka.

WAKANDARASI NCHINI WATAKIWA KUZINGATIA UBORA WA KAZI ZAO

0
0
picha maktaba 

Na Woinde shizza wa libeneke la kaskazini blog.
 
Wakandarasi nchini wametakiwa   kuzingatia ubora ,viwango  vya kazi zao ili kuweza kutekeleza kazi zao kwa ufanisi zaidi na kuweza kufanya bkazi yenye viwango vya hali ya juu pindi wanapo tekeleza miradi mbalimbali nchini.


Endapo wakandarasi wazawa wataweza kuzingatia taratibu za viwango vya ujenzi  pindio wanapopata zabuni za miradi ya ujenzi hali hiyo itaongeza chachu ya mabadiliko na kuweza kushasishi serikali kuyweza kuwa wanawatumia wakandarasi wazawa ili kuepuka gharama za kutoa zabuni kwa wakandarasi wageni  ili kuweza kutumia ghara ma ndogo na pesa  ziweze kubaki nchini na kutopelekwa kwa nchi za wakandarasi wageni.




Hayo yameelezwa leo na Mhandisi   Omari Kiure  kutoka kampuni ya Kiure Engineering Limited kutoka mkoani hapa  wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi  jengo la kituo cha jimolojia  Tanzania  ambapio kituo hicho kiko chini  ya Wizara ya nishati na madini ambacho kimejengwa eneo la njiro mkoani Arusha. 


Hata hivyo jengo hilo limegharimu zaidi ya shilingi bilioni moja ambalo nikituo cha kutoa mafunzo kwa wanafunzi namna ya kuongeza thamani madini ya vito,mafunzo ya ukataji  madini ,utengenmezaji   bizaa za mapambo  sambamba na uchongaji vinyago vya mawe ili kuweza kuongeza ajira kwa vijana walio wengi ambalo ndilo kundi kubwa nchini ambalo halina ajira.


Aidha aliongeza kuwa  endapo wkandarasi watajizatiti  na kuboresha kazi zao wataweza  kufanya kazi  ambazo zinzonekana katika viwango vya hali ya juu ili kuwezaa kushawishi wadau mbalimbali kuweza kuwapa miradi ya ujenzi pindi inapohitajika na kuweza kutokuwepo dosari ama kuanguka kwa magorofa baada ya muda mchache hali inayogharimu Serikali fedha nyingi ambazo bni kodi za wananchi.


Kwa upande wake mhitimu wea kituo hicho Bi,Salome Mollel  alisema kuwa  ujenzi wa kituo hicho kitakuwa mkombazi wa vijana kupata mafunzo hayo na kuweza kupata ajira kwa wafanyabiashara wa mawe  kwani kulikuwa na changamoto kubwa sana ya kituo cha mafunzo ya uongezaji thamani ya vito vya madini hali iliyokuwa inawalazimu wafanyabiahsra hao kuuza madini yakiwa ghafi nsa kuuza kwa bei ya hasara  na fedha nyingi kuenda nchi nyingine.

Ambapo kupitia kituo hicho kitawasaidia vijana kupata ajira na kuongeza thamani ya madini hayo na itawawezewsha wafanyabiahsra hao kuuza madini yakiwa yameongezwa thamani ili kupata bei nzuri na fedha kubaki na kuomgeza uchumi wan chi.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images