Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 513 | 514 | (Page 515) | 516 | 517 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi leo amefungua kozi ya walimu wakufunzi wa mpira wa miguu chini inayofanyika katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

  Malinzi amesema kozi hiyo ni muhimu kwa mustakabali wa soka la Tanzania, walimu wakufunzi watasaidia kuwafundisha walimu wengine wa mpira, ili kuweza kufundisha mpira kwa watoto wadogo ambao ndio hazina ya baadae.

  Malengo ya TFF ni kuhakikisha timu ya vijana ya U17 inafuzu kwa fainali za Mataifa Afrika 2017 nchini Madagscar, na baadae kuwa na kikosi bora wakati tunapotarajia kuwa wenyeji wa fainali za U17 Afrika mwaka 2019 "alisema Malinzi".

  TFF ina program mbili za kuwaandaa vijana wenye umri chini ya miaka 13, 15 kwa kuwaweka kambini na kucheza michezo ya kirafiki mikoani na kufanya ziara katika nchi za Malawi, Zambia, Zimbabwe, Bostwana na Afrika Kusini.

  Aidha Malinzi amewaomba walimu wakufunzi kuwa karibu na makocha wa timu za Taifa, na kuwapa ushauri makocha hao ili kuweza kuwasaidia katika kuboresha vikosi vyao na maendeleo ya soka la Tanzania kwa ujumla.

  Naye Rais wa CECAFA na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, Leodgar Tenga alimshukuru Malinzi kwa kuweza kufungua kozi hiyo ambayo inawakutansisha walimu wakufunzi wa mpira miguu kutoka sehemu mbalimbali nchini.

   Akiongea kwa niaba wa walimu wakufunzi, Dr. Mshindo Msolla alisema wanaishukuru TFF kwa kuandaa kozi na kuomba kuendelea kushirikishwa katika mipango mbalimbali ya soka nchini ikiwa ni pamoja na kutambulika kuanzia katika ngazi za juu mpaka katika maeneo waliyopo.

  Kozi hiyoiliyoanza leo jumatatu itamalizika Mei 2 mwaka huu, inawajumuisha walimu 18, wenye leseni A, B na C za CAF kutoka mikoa mbalimbali Tanzania bara na Zanzibar.

   IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0

   Wanajeshi wa nchini Nepal wakiendelea kutafuta miili ya watu waliopoteza maisha katika tetemeko la ardhi  mjini Kathmand nchini Nepal.
   Baadhi ya miili ya watu waliopoteza maisha katika
  katika tetemeko la ardhi  mjini Kathmand nchini Nepal.
  Kwa msaada wa mtandao
  MAMLAKA ya nchini Nepal imesema kuwa zaidi ya watu 3300 wamesemekana kufairki dunia kutokana na Tetemeko kubwa la ardhi lililotokea jumamosi katika mji wa Kathmandu nchini  humo.
  Waokoaji wanchi hiyo wamesema wanaendelea kuchunguza zaidi kwa kuyafikia maeneo ya mashamba mbalimbali katika mji Kathmandu, inawezekana Idadi ya watu waliopoteza maisha kuwa kubwa zaidi jinsi muda unavyozidi kwenda.
  Mamia ya watu wanaoishi karibu na milima inasemekana kuwa wameachwa bila makazi kutokana na tetemeko la ardhi katika nchi hiyo.
  Shirika la umoja wa mataifa linalosimamia watoto (UNICEF) limesema kuwa kalibia watoto milioni moja hawana mahala pakulala, wanakabiliwa na ukosefu wa maji  safi pamoja na mazingira safi katika nchi hiyo.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la siku mbili la Kimataifa la Mafunzo ya pamoja kwa Mabadiliko ya Kisayansi na Teknolojia, yaliyoanza leo jijini Arusha. Mafunzo hayo yameshirikisha washiriki kutoka Nchi 14 za Afrika na washiriki kutoka Vyuo 15 vya nchini Sweden.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Swiden Nchini Tanzania, Lennarth Hjelmaker, wakati alipowasili kwenye Taasisi ya ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, jijini Arusha kwa ajili ya kufungua Kongamano la siku mbili la Kimataifa la Mafunzo ya pamoja kwa Mabadiliko ya Kisayansi na Teknolojia, yaliyoanza leo jijini Arusha. Mafunzo hayo yameshirikisha washiriki kutoka Nchi 14 za Afrika na washiriki kutoka Vyuo 15 vya nchini Sweden.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kwenye ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, jijini Arusha kwa ajili ya kufungua Kongamano la siku mbili la Kimataifa la Mafunzo ya pamoja kwa Mabadiliko ya Kisayansi na Teknolojia, yaliyoanza leo jijini Arusha. Mafunzo hayo yameshirikisha washiriki kutoka Nchi 14 za Afrika na washiriki kutoka Vyuo 15 vya nchini Sweden.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo, baada ya ufunguzi rasimi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, baada ya ufunguzi . Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela, Prof. Burton Mwamila (wa pili kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Hasna Mwilima, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, katika hafla hiyo. Picha na OMR

  0 0

   Ofisa wa Kitengo cha Udhibiti Ubora wa MSD, Richard Makalla (kulia), akimuelekeza jambo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki alipotembelea banda la MSD katika maadhimisho hayo. Kushoto ni Ofisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Dar es Salaam wa MSD, Florida Sianga na ofisa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa.
   Muenekano wa banda la MSD katika maadhimisho hayo.
   Maofisa wa MSD wakiwa kwenye maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Ofisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Dar es Salaam wa MSD, Florida Sianga, Ofisa wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa MSD, Emmanuel Kais, Ofisa wa Kitengo cha Udhibiti Ubora wa MSD, Richard Makalla, Ofisa Habari, Benjamin Massangya na Dereva, Said Tindwa. 
   Baadhi ya vifaa mbalimbali vilivyokuwa vinaoneshwa.
   Ofisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Dar es Salaam wa MSD, Florida Sianga (kushoto), akimuelekeza jambo kijana aliyetembelea banda la MSD katika maadhimisho hayo.


  Na Mwandishi Wetu
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick, ameitaka  Bohari ya Dawa MSD kuendeleza kasi ya huduma zake za kupambana na ugonjwa wa malaria kwakuwa ni  moja ya taasisi  zilizo mstari wa mbele kupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa huo.
  Akizungumza jana katika banda la MSD ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Malaria duniani Sadick alisema MSD imekuwa ikifanya jitihada kuhakikisha ugonjwa wa malaria unakoma na vifo vitokanavyo na ugonjwa huo vinapungua.
  Alisema jitihada hizo za MSD zimechangia matokeo ya kupungua takwimu za vifo vya mama na mtoto mchanga chini ya miaka mitano vitokanavyo na ugonjwa wa malaria hivyo jitihada zaidi zinahitajika kuhakikisha malengo ya millennia ya kupunguza vifo hivyo yanafikiwa.
  Alisema kutokana na MSD kuhakikisha dawa za malaria zinapatikana katika kila kituo cha afya, Zahanati na Hospitali ni wajibu wa wananchi kuhakikisha wanafanya  matumizi sahihi ya dawa hizo ili kutibu ugonjwa huo.
  “MSD inasaidia serikali kufikia lengo la kupunguza ugonjwa wa malaria tumeelezwa jinsi gani MSD inahakikisha dawa za malaria hazikosekani katika vituo vya kutolea huduma lakini pia imepanua  wigo kwa kutoa elimu kwa vitendo jinsi ya kupambana na ugonjwa huo kwa  kuhakikisha kinga dhidi ya malaria   inaanzia kwa wafanyakazi wake na wanapewa vyandarua vyenye dawa wao na familia zao,”alisema
  Sadick aliwataka wananchi kuacha kutumia dawa hizo katika matumizi yasiyo sahihi ikiwemo dozi moja ya dawa kutumiwa na watu zaidi ya mmoja kwakuwa kufanya hivyo kunasababisha matibabu ya wagonjwa wa malaria kutokukamilika na kusababisha vifo.
  Alisema pia kumekuwepo na matumizi yasiyo sahihi  katika vyandarua vya msaada ambapo utumika kwa ajili ya kufugia Kuku au kuvulia Samaki hivyo mapambano dhidi ya ugonjwa huo kutokufanikiwa.
  “ Jitihada hizi za MSD na wafadhili mbalimbali katika kuweka  nguvu ya  kupambana na Malaria ni wajibu wa  jamii kuziunga mkono kwakuwa matumizi ya misaada hiyo ikiwemo Vyandarua ikitumiwa  kwa malengo yaliyokusudiwa  kutaongeza uzalishaji wa uchumi katika nchi kutokana na kuimarika kwa afya ya wananchi wake,”alisema.
  Katika maadhimisho hayo Mkuu Mkoa huyo alizindua mpango wa ugawaji wa Vyandarua milioni 24 kwa nchi mzima ikiwa ni jitihada za Serikali na wadau mbalimbali kupambana na ugonjwa wa Malaria. (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)

  0 0

   Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiangalia moja ya kompyuta maalum zinazotumiwa wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa jili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akijaribu akikagua moja ya vitanda na hema linazotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akishuka kutoka basi linalotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akicheza na mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.

  Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza wakinyanyua juu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu jana,alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akikwagua gwaride la heshima jana alipowasili Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa jili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akijaribu moja ya darubini zinazotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiangalia moja ya darubini zinazotumiw ana wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa jili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.
  Picha  ya pamoja ya wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza.

  Serikali imesema kwamba itaanza kuwaajiri moja kwa moja askari wa wanyamapori kama inavyofanyika kwa jeshi la polisi na Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ).

  Akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Wanyamapori cha Pasiansi jijini Mwanza jana Waziri a  Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amesema utaratibu unaotumika kw asasa unaleta usumbufu kwani urasimu unasababisha askari hao wanapomaliza mafunzo kusubiri kusailiwa wakati wa ajira wakati kuna upungufu mkubwa wa askari hao.

  “Hatuwezi kukaa na kusubiri kupata kibali cha sekritarieti ya ajira kwa maana sasa hivi tumeanzisha Mamlaka ya Wanayamapori na kwa hiyo watakuwa na uwezo wa kuajiri mojakwa moja kuliko utaratibu wa sasa unaofanya mwanafunzi akimaliza chuo asubiri kusailiwa mbona polisi na jeshi hawafanyi hivyo?”

  Waziri Nyalandu alisema kwa sasa kuna tatizookubwa kla ujangili na kuahidi kuwa vijana wengi watakaopata mafunzo wataajiriwa ili vita ya kupambana na majangili nchini ielekezwe sehemu zote ili kuweza kulinda na kuhifadhi rasilimali nchini kwa ajili ya vizazi vijavyo.

  “Tumefanikiwa Serengeti na Selous lakini kwa sasa janga kubwa limekuwa katika pori la Rungwa ambalo limeungana na Ruaha, Tembo wengi wamekuwa wakiuawa na sasa vita tunaelekeza huko, ili kumaliza tatizo la ujangili”.

  Alisema kuwa majangili watatafutwa popote wqlipo na kwamba wananchi wanatakiwa kuingia katika vita hiyo na kutoa taarifa zitakazosababisha majangili kukamatwa sehemu yoyote walipo ikiwa ni pamoja na ndugu zao na wafadhili wao.

  Nyalandu ambaye alitembelea chuo hicho kukagua maendeleo ya mradi wa maboresho ya chuo unaofadhiliwa na Howard Buffet Foundation (HGBF) kwa kupitia taasisi yake ya uhifadhi ya Nature Conservation Trust aliagiza ujenzi wa bweni la wanafunzi 300 ukamilike katika kipindi kifupi kwa kuwa pesa za mradi zipo tayari.

  Mkuu wa chuo hicho, Lowaeli Damalu alimshukuru Waziri Nyalandu kwa kutafuta mfadhili huyo na kusema kuwa kwa sasa chuo kimekuwa ch kisasa na vifaa vya kutosha kw akufundishia.

  Alisema kwamba msaada huo unaokaribia Sh4bilioni umewezesha kununua vitabu magari, mahema darubini na kompyupa ambavyo unaweza kuwajenga wanafunzi kufanya kazi watakapoajiriwa kwa weredi mkubwa.

  Dumalu alisema kwamba kwa sasa bwalo la chakula limekamilika na fedha kwa jaili ya ujenzi wa bweni ziko tayari lakini tatizo limekuwa ni kwa mkandarasi ambaye aliweka bei kubwa kupita bajeti na hivyo kumwahidi waziri kuwa mkandarasi ataletwa na mfadhili ili kukamilisha mradi huo kabla ya mwisho wa mwaka.
  Alisema mbali na kuboresha mafunzo kwa wanafunzi lakini pia walimu wamepata fedha kutoka HGBF kwa ajili ya mafunzo kwa walimu na wafanyakazi ambao wamekuwa wakiendelea na mafunzo hayo kazini ili kuweza kupambana na ujangili na kwamba mradi huo bado unaendelea na kuwa mfadhili huyo tajiri namba mbili Marekani yuko tayari kuendelea kusaidia chuo hicho.

  0 0

   Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akionyesha kitabu kinachoeleza Maendeleo na historia ya Takwimu katika Bara la Afrika alichokizindua leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
   Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akizindua kitabu kinachoeleza Maendeleo na historia ya Takwimu katika Bara la Afrika alichokizindua leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kushoto kwa Waziri Mkuu na Prof. Ben Kiregyeza (kulia) ambaye ndiye mwandishi wa kitabu hicho.

    Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akifungua  Kongamano la Kimataifa la Siku 3 la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika leo jijini Dar es salaam.

   Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa awali akizungumza na Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika waliohudhuria Kongamano la Siku 3 la Kimataifa kujadili Matumizi ya Takwimu leo jijini Dar es salaam.

   Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair akizungumza kabla ya uzinduzi wa  Kongamano  la Kimataifa la masuala ya Takwimu la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa  kutoka Afrika na nje ya Afrika.

   Waziri Mkuu akizungumza jambo na Makamu wa Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bi. Irena Krizman leo jijini Dar es salaam mara baada ya kufungua  kongamano la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika. Katikati ni mjumbe kutoka ya Kusini Bw. Pali Lihohla.
   Waziri Mkuu akizungumza akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya kufungua  kongamano la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 32 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika.
   Waziri Mkuu akizungumza akizungumza akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kufungua  kongamano la Kimataifa la Wakuu wa Taasisi za Takwimu kutoka  nchi 32 za Afrika na 18 za nje ya Bara la Afrika.
  Waziri Mkuu akizungumza akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Taasisi za Takwimu kutoka  nchi 32 za Afrika na 18 za nje ya Bara la Afrika waliohudhuria Mkutano wa siku 3 wa Takwimu  jijini Dar es salaam.  Na Aron Msigwa,Dar es salaam.
  Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda amesema kuwa Serikali itaendelea  kutoa kipaumbele katika matumizi ya takwimu sahihi na kuweka mifumo mizuri ya kuwarahisishia  wananchi na taasisi mbalimbali kupata takwimu za masuala mbalimbali kutoka Serikalini ili  ili waweze kupanga mpango ya maendeleo.

  Akifungua  Kongamano la Kimataifa la Siku 3 la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika leo jijini Dar es salaam Mhe. Pinda amesema kuwa nchi za Bara la Afrika ili ziweze kuwa na maendeleo endelevu yanayotafsiriwa lazima zitoe kipaumbele katika matumizi ya Takwimu sahihi.

  Amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi za Bara la Afrika zilizopiga hatua kubwa katika kuweka mifumo ya kurahisisha upatikanaji wa takwimu za masuala mbalimbali yakiwemo ya Idadi ya watu, takwimu za masuala ya Afya na masuala mbalimbali yanayohusu shughuli mbalimbali za uchumi wa Kaya binafsi.

  “ Mpango wowote ambao hautumii takwimu sahihi  hauwezi kuzaa matunda, Lengo letu Serikali ni kuhakikisha kwamba tunakuwa na takwimu sahihi kuhusu idadi ya wananchi wetu, sekta ya afya, Elimu, Biashara, Kilimo na mifugo yetu ili tuweze kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili” Amesisitiza.

  Ameeleza kuwa upatikanaji wa Takwimu sahihi katika Bara la Afrika hususani nchini Tanzania  katika masuala ya Kilimo, Chakula na Mifugo kutasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima na wafugaji  na kuwawezesha  kupunguza idadi ya mifugo waliyonayo kwa  kuwa na ufugaji wenye manufaa na endelevu.

  Ametoa wito kwa nchi za Afrika kuendelea kujenga taasisi imara za Takwimu na kuongeza bajeti za kugharamia uwekaji wa mifumo rafiki ya upataji wa takwimu za masuala mbalimbali ili kuwawezesha wananchi  kupata takwimu bila vikwazo na kuweka wazi kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuijengea uwezo Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ili iweze kutekeleza kikamilifu majukumu yake.

  Aidha, ameitaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoa takwimu rahisi zinazoeleweka na kundi kubwa la watumiaji ametoa na kutoa wito kwa  wadau mbalimbali kutoka sekta ya Umma na Binafsi, viongozi  na wanasiasa kujenga utamaduni wa kutumia takwimu kutoka vyanzo sahihi ili taasisi wanazoziongoza ziwe imara na zenye matokeo.

  Kwa upande wake Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair akizungumza kabla ya uzinduzi wa  Kongamano hilo la Kimataifa amesema kuwa ili kujenga jamii Imara yenye Ubunifu na inayolenga kupata mabadiliko lazima matumizi ya takwimu sahihi yazingatiwe.

  Amesema kuwa Taasisi anayoiongoza ya ISI imekuwa mstari wa mbele katika kuhimiza matumizi ya Takwimu sahihi, kujenga taasisi imara zenye wataalam wenye weledi katika masuala ya Takwimu katika nchi mbalimbali za Afrika.

  Ameeleza kuwa taasisi yake imekuwa ikifanya kazi ya kuendesha Warsha na Makongamano katika nchi mbalimbali duniani hasa zile zinazungumza lugha ya Kiingereza na Kifaransa kwa kuwakutanisha wakuu wa taasisi na viongozi wengine wakuu wa ngazi ya mawaziri ambao hukutana kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu umuhimu wa matumizi ya takwimu kwa maendeleo ya nchi zao.

   Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua Kongamano hilo la Kimataifa amesema kuwa Tanzania inaendelea kufanya vizuri katika kuimarisha uwazi katika matumizi ya Takwimu sahihi.

  Amesema kuwa licha ya kuwepo kwa tafsiri tofauti ya neon masikini kati ya nchi moja na nyingine,  Ofisi ya Taifa ya Takwimu  inaendelea kuhuisha takwimu mbalimbali ili ziweze kuakisi na kukidhi mahitaji  ya sasa ya matumizi ya wadau mbalimbali kitaifa na Kimataifa.

  “Sisi kama Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini Tanzania tunaendelea kuimarisha shughuli zetu ili kuendelea kujenga uchumi imara kwa takwimu sahihi, tumeendelea kutoa na kubainisha viashiria  vya ukuaji wa uchumi wetu kwa ngazi ya taifa, kutoa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi pamoja na taarifa za Sekta mbalimbali nchini” Amesema.

  0 0

   Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa watatu raia wa kigeni kwa makosa yanayohusiana na wizi wa mtandao kwa lengo la kuiba  katika vyombo vya fedha kama mabenki, maduka ya kubadilishia fedha (Bureau de Change) au kuingilia miamala ya fedha zinazosafirishwa na wateja kutoka nje na ndani ya nchi. 

  Polisi wa kikosi Maalum cha kupambana na wizi wa mtandao (Cyber Crime) walipata taarifa za kuaminika kwamba watu hao watatu walikuwa katika mazingira ya kutiliwa mashaka na ndipo Polisi walienda Mtaa wa Mindu eneo la Upanga na kuwakamata. Watu hao walikutwa katika nyumba namba 416 iliyopo katika ghorofa ya nne na walitambuliwa kwa majina yafuatayo:

  1.    FOTIOS S/O VOGIATZIS, Miaka 32, Mfanyabiashara, Mkazi wa Upanga, Raia wa nchini UGIRIKI mwenye Passport namba AK2669977.

  2.   ATHANASIOS S/O VOGIATZIS, Miaka 30, Mfanyabiashara, Mkazi wa Upanga, Mkazi wa Ugiriki mwenye Passport namba AK3049876.

  3.   PANAGIOTIS S/O ANGELIDIS,   Miaka 25, Mkazi wa Upanga, Raia wa UGIRIKI mwenye Passport namba AK2644930.

  Watu hao watatu ambao ni raia wa nchini Ugiriki kumbukumbu zao zinaonyesha kwamba wamekuwa wakiingia na kutoka nchini Tanzania na kwenda nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya katika namna ambayo inaonyesha kuwa ni wahalifu wa kimataifa kupitia mitandao.

  Katika upekuzi watu hao wamekamatwa na vielelezo mbalimbali vinavyopashiria njama zao kama ifuatavyo:
  1.    Muhuri mmoja wa kughushi ulioandikwa “Inspector General of Police DSM”

  2.   Nyaraka mbalimbali za kughushi za Polisi Tanzania zinazowasaidia  kwa lengo la kupata malipo ya bima nje ya nchi ambazo zina mihuri ya kughushi.

  3.   Zimepatikana Kompyuta Mpakato (Laptops) zipatazo tisa ambazo watuhumiwa hawa huzitumia kwa ajili ya mawasilisano pamoja na uhalifu huo wa kimataifa.

  4.   Zimekamatwa laini za simu za mkononi (Cheap) za kampuni ya simu ya Airtel ambazo baadhi zimetumika na nyingine hazijatumika.

  5.   Aidha, zimekamatwa kadi mbalimbali za benki (Credit Cards) zipatazo 13 zinazotumika kutoa fedha, kuingiza fedha, au manunuzi mengine za ATM.
  Pia watuhumiwa hao wamekamatwa na vitabu vitano vyenye kumbukumbu za majina, anwani, pamoja na namba za siri za wateja mbalimbali wa mabenki mbalimbali kutoka nchi za Tanzania, Zambia, Afrika Kusini, Kenya, Uingereza na Nigeria.

  Uchunguzi ziadi unaendelea kuhusu raia hao watatu kutoka nchi ya Ugiriki ili kubaini mtandao wao na kugundua matukio mbalimbali ambayo wameyafanya.

  TAHADHARI KWA WANANCHI NA WAGENI WENGINE
  Pamoja na kuibuka na wimbi hili la wezi wa mtandao bado ni salama kuweka na kutoa fedha katika mabenki hapa nchini. Hata hivyo kutokana na wimbi hili la wizi kwa njia ya mtandao, ni muhimu sasa kuzuia uhalifu wa aina hii kwa ushirikiano kati ya wamiliki wa mabenki  na wateja wao.  

   Jeshi la Polisi linashauri (pamoja na maelekezo mengine ya benki) njia sahihi ya kwanza ya kuzuia ni kuhakikisha kwamba miamala yote inayofanyika katika akaunti za benki ni lazima ifahamike kwa mteja kwa njia zifuatazo:

  1.    Mteja ajulishwe kwa simu ya mdomo ili kuthibitisha muamala.
  2.   Mteja atumiwe ujumbe kwa kila muamala unaofanyika kupitia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kumjulisha mteja kiasi kilichotolewa, kiasi kilichoingizwa au makato au maingizo yoyote kwa muda ule ule.

  Aidha tunawaomba wananchi waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi na wasikubali kutoa nambari za akaunti zao kwa watu wasiohusika au nambari zao za siri hata kwa mtu ambaye ni ndugu wa karibu sana.
  Mara baada ya upelelezi kukamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.

  S. H. KOVA,  KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
  DAR ES SALAAM.

  0 0

   Simon Msuva (kushoto) akishangilia na Amis Tambwe baada ya Tabwe kuipatia timu yake bao la katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshida 4-1. (Picha na Francis Dande)
   Mashabiki wa Yanga wakishangilia bao lililofungwa na Amis Tambwe.
   Mshambuliaji Wa Yanga, Simon Msuva akimtoka beki wa Polisi Moro, Hassan Mganga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  Shabiki wa Yanga akifurahia bao la pili la timu yake.
   Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya kumalizika kwa mchezona Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.
   Amis Tambwe akipokea mpira baada ya kufunga"Hat Trick"
   Kocha wa Yanga, Hans Pluijm akishangilia baada ya timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.
   Mashabiki wakishangilia.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuifariji 
  familia ya Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo April 27, 2015.  Marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam baada ya Swala ya Alasiri katika msikito wa Mtoro,  baada ya kupata heshima zote za kijeshi asubuhi yake katika makao makuu ya Jeshi Upanga, Dar es salaam.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia wakati Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha 
  maombolezo alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo April 27, 2015. Marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam baada ya Swala ya Alasiri katika msikito wa Mtoro, 
  baada ya kupata heshima zote za kijeshi asubuhi yake katika makao makuu ya Jeshi Upanga, Dar es salaam.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma kikwete wakimsikiliza mtoto wa Marehemu Bw. Iddi Mbita kuhusu taratibu za mazishi walipokwenda kuifariji familia ya  Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo April 27, 2015.  Marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam baada ya Swala ya Alasiri katika msikito wa Mtoro,  baada ya kupata heshima zote za kijeshi asubuhi yake katika makao makuu ya Jeshi Upanga, Dar es salaam.
  Rais Kikwete akiondoka msibani .Picha na IKULU

  0 0


  Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdala Ulega amewakata watendaji na watoa huduma wilayani humo kuhakikisha huduma muhimu za matibabu hasa dawa zinapatina muda wote ili kuboresha huduma wilayani hapo.

  Ulega ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya uhamasiahaji wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa taifa wa bima ya afya katika halmashauri kumi nchi nzima iliyozinduliwa kata ya Tingi njia nne wilayani kilwa.

  Ulega amesema Serikali kupitia mfuko wa uchangiaji wa bima ya afya (NHIF) na mfuko wa afya ya jamii (CHF) imetoa fursa kwa wamiliki wa vituo vya matibabu na watoa huduma kutumia fedha za uchangiaji huduma kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vitendanishi kwa ajili ya kuboresha huduma kwa wananchi na kwamba fedha hizo sio za kulipana posho katika vikao.

  Awali, Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Bima ya Afya, Rehani Athumani alimweleza Mkuu huyo wa Wilaya kuwa kampeni hiyo iliyozinduliwa leo itafanyika katika halmashauri nyingine kumi na hivyo kufanya jumla ya halmashauri zilizohamasishwa nchi nzima kufikia 74 katika mwaka wa fedha wa 2014/15.

  Rehani alizitaja halmashauri hizo kuwa ni Kilwa, Ruangwa, Ulanga, Korogwe na Rufiji. Nyingine tano ambazo huduma za mfuko wa CHF zitaanzishwa na kuhamasishwa katika kampeni hii ni Halmashauri ya Kaliua, Kakonko, Ushetu na Itirima.

  Naye mwakilishi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Mtandao wa Mifuko ya Afya ya Jamiii nchini (TNCHF), Kidani Mhenga aliwaahidi wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kuendelea kushirikiana nao katika kutatua changamoto mbalimbali ili kuboresha huduma za matibabu kupitia Mfuko wa Afya wa Jamii katika mikoa hiyo. 

  Aliomba ushirikiano wa wananchi kwa ujumla kwani mafanikio ya utekelezaji wa huduma za mfuko huo zinategemea ushiriki wa wananchi katika kuchangia na kusimamia huduma.

  Hadi tarehe 31 machi, 2015 mfuko wa afya ya jamii ulikuwa umeandikisha jumla ya kaya 930,879 sawa na wanufaika 5,85,274.
  Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdallah Ulega akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Njia Nne, Kata ya Tingi wilayani Kilwa, wakati uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya uhamasiahaji kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika halmashauri kumi nchi nzima.
  Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),  Rehani Athumani akielezea namna kampeni hiyo inavyofanyika katika halmashauri nyingine kumi na hivyo kufanya jumla ya halmashauri zilizohamasishwa nchi nzima kufikia halmashauri 74 katika mwaka wa fedha wa 2014/15, katika uzinduzi uliofanyika leo katika Kijiji cha Njia Nne, Kata ya Tingi wilaya ya Kilwa, Mkoani Lindi.


  0 0

  ·       Iwapo kutakuwepo ushirikishwaji wa wananchi
  ·       Wataalamu nao watoa yao ya moyoni


  Dar es salaam, Jumatatu Aprili 24, 2015 --KUTOKANA na kugundulika kwa hazina kubwa ya gesi nchini  ambayo inategemewa kukuza pato la taifa zaidi ya mara 15 ya sasa, kiasi cha kuiwezesha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.


  Hata hivyo, dhana ya kwamba Rais ajaye baada ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kumaliza muda wake, anaweza akaikuta Tanzania ikiwa ni nchi tajiri tayari kutokana na rasilimali hiyo ya gesi asili, inaweza isiwe sahihi kama hautawekwa mfumo madhubuti wa ushirikishwaji wa wananchi katika fursa zilizopo katika rasilimali hiyo, sera, sheria na usimamiaji mzuri wa raslimali hiyo.


  Pia itawezekana tu iwapo viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali hiyo watahakikisha wanaisimamia kikamilifu kwa mujibu wa sera na sheria zitakazotungwa na kusimamiwa na viongozi wenye dhamira ya dhati ya kuwatumikia Watanzania na nchi yao kwanza.


  Hayo pamoja na mengine yalijadiliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Watanzania wapatao 400 kutoka wilaya mbalimbali ambapo walitoa maoni yao kuhusu ni jinsi gani mapato yatakayotokana na gesi yatawanufaisha wananchi wote wa Tanzania.


  Mkutano huo uliowakutanisha Watanzania na kuwawezesha kutoa mawazo na maoni yao kama wawakilishi wa maeneo watokayo uliandaliwa na taasisi za  utafiti kuhusiana na kuondokana na umaskini nchini za REPOA  na Center for Global Development (CGD).

  Dr Abel Kinyondo & Invited Expert Innocent Bash from TEITI addressing the media  
   Dr Abel Kinyondo Opening Speech . 
   Expert Mr Dennis Rweyemamu (Head - Policy and Research, UONGOZI INSTITUTE) answering questions
   January Makamba and Mujobu Moyo listening to participants
  January Makamba answering questions from participants 
  Moderator discussing topics with participants 


  Utafiti huu ni wa kwanza wa aina yake wa kuwashirikisha wananchi wa kawaida katika utafiti unaohusiana na jinsi sera mbalimbali zinatungwa na kutekelezwa kwa matakwa ya matajiri katika nchi zinazoendelea bila kuwaangalia wananchi wa kawaida  wa hali ya chini.


  Mtafiti Mwandamizi kutoka taasisi ya CGD, Mujobu Moyo anasema kuwa udhibiti na usimamizi mzuri wa mapato yatakayotokana na gesi yatatoa mustakabali wa nchi yetu utakavyokuwa katika siku zijazo na kuongeza kuwa Tanzania kama zilivyo nchi nyingine zinazoendelea inakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazoweza kupelekea gesi iliyogunduliwa isinufaishe wananchi wote.


  Moyo alizitaja baadhi ya changamoto hizo, kuwa ni rushwa, ubadhirifu na vurugu za kisiasa.


  “Wananchi wanapaswa kwanza kueleweshwa juu ya mchakato mzima na kushirikishwa kutoa maoni yao ni jinsi gani mapato yatakayotokana na raslimali hii yataleta manufaa kwa wote ili kuepuka makosa yaliyojitokeza kwenye nchi nyingine kwa kosa la kutowashirikisha wananchi katika masuala yanayohusu raslimali za Taifa,” Moyo anasema.


  Aidha anaeleza kuwa mradi  huu wa utafiti wa CGD, unalenga kufuta dhana iliyozoeleka kuwa Watanzania wa kawaida, kuwa hawana haki ya  kutoa mawazo katika masuala ya kitaifa kama lilivyo suala hili la gesi ambalo limekuwa likijadiliwa na wasomi na wanasiasa.


  Moyo anaongeza kuwa ushirikishwaji wa Watanzania wa kawaida, utawawezesha kuelewa suala zima la kugundulika kwa gesi nchini na kupata maoni yao ya jinsi gani ya kusimamia mapato yatakayotokana na gesi kwa manufaa ya wote na hivyo kuongeza uwazi kuhusiana na sula hili.


  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya REPOA, Prof. Samwel Wangwe, anasema kuongezeka ghafla kwa mapato kutokana na raslimali hizi kunaweza kuleta athari mbalimbali  kwa Tanzania badala ya faida.


  Prof. Wangwe, anatoa sababu ya kauli yake hiyo uwezekano wa kuibuka kwa athari mbalimbali kuwa ni pamoja na; kuongezeka kwa vitendo vya rushwa, kuvurugika kwa uchumi, kuongezeka kwa umaskini na kupunguza kukuwa kwa demokrasia.


  "Haya yote yanajitokeza iwapo nchi inakuwa na raslimali nyingi na kundi la wananchi wa hali ya chini na wasio na elimu kutopewa taarifa sahihi na za kutosha juu ya kinachoendelea," Prof. Wangwe anatahadharisha.


  Akieleza nini kifanyike ili kuondoka na changamoto hizi, Prof. Wangwe anasema: “ Tanzania inaweza kunufaika iwapo itajitayarisha kuingia katika gesi ikiwa imehakikisha kuwa mawazo ya walio wengi yanaingizwa katika utungaji wa sera na hii itasaidia katika mchakato wa wanasiasa kufanya maamuzi na utekelezaji kwa ujumla.”


  Mtafiti Mwandamizi kutoka REPOA, Dk. Abel Kinyondo, anasema, “ Kwa zaidi ya miongo minne sasa, Tanzania imeshuhudia ukuaji mzuri wa uchumi licha ya watanzania kuzidi kuwa maskini. Lakini kugundulika kwa hazina kubwa ya gesi nchini kunatoa fursa ya kusahihisha makosa ya nyuma na kubadilisha hali hii.”


  Dk. Kinyondo, anaongeza kuwa ili uchumi wa nchi uzidi kukua zaidi kunatakiwa kwanza kujua ni jinsi gani mapato yatakayotokana na raslimali ya mafuta na gesi yatawanufaisha watanzania wote na ndio sababu REPOA na CGD wameamua kuwakutanisha wananchi kutoka sehemu mbalimbali ili watoe mawazo yao kwenye jambo hili muhimu kwa taifa la Tanzania.


  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba: "Wananchi wana uwezo wa kuchagua viongozi ambao wanaweza kuweka maslahi yao katika akili na ambao wataweza kusimamia vizuri mapato ambayo yatakayo kuwa yakipatikana kutokana na sekta ya mafuta na gesi."


  Mkutano huu ni wa pili katika mwendelezo wa utafiti wa suala hili ambapo mwanzoni wananchi 2,000 kutoka wilaya zote za Tanzania wamehusishwa kutoa maoni yao na wawakilishi 400 waliohudhuria mkutano uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam walipata fursa ya kutoa maoni yao na kupata taarifa mbalimbali kutoka kwa wataalamu.


  Utafiti huu unatoa tathmini kuhusu uelewa wa  Watanzania juu ya mchakato mzima wa mafuta na gesi nchini na nini matarajio yao kutokana na raslimali hizi na taarifa za utafiti huu zitasaidia kufanya maamuzi mbalimbali.


  Taarifa za mwisho za utafiti huu ziliwasilishwa kwa watungaji wa sera nchini.


  Ugunduzi wa kwanza wa gesi katika ukanda wa bahari ya Hindi ulikuwa ni mwaka 2010, ingawa bado utafiti unaendelea katika hatua mbalimbali. Ripoti ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) imebainisha kuwa mapato yatakayotokana na gesi kwa mwaka inakadiriwa yatakuwa kati ya Dola za Kimarekani bilioni 3 na bilioni 6.


  Mwaka 1999, Tanzania ilitangazwa na Benki ya Dunia (WB) kuwa moja ya nchi masikini duniani, jambo ambalo wachambuzi wa masuala ya kiuchumi wanaliita la aibu kwa nchi yenye rasilimali nyingi kama Tanzania kutangazwa kuwa miongoni mwa nchi masikini na zinazohitaji misaada ya hali na mali duniani.


  Takwimu zinazopatikana kutoka TPDC zinaonyesha kwamba kati ya futi zaidi ya ujazo wa trilioni 53 za gesi asilia zilizogundulika nchini, ni futi za ujazo za gesi milioni nne hadi nane zinazotumika kwa sasa kwa ajili ya kuzalishia umeme, kupikia pamoja na magari kama mbadala wa mafuta aina ya petroli.


  Kwa mujibu wa TPDC, nchi inapoteza takriban Shilingi trilioni 1.6 kila mwaka kutokana na kutumia mafuta ya kuzalisha umeme pamoja na kununua umeme unaozalishwa na makampuni binafsi kulingana na mikataba iliyopo inayolitafuna Taifa. 


  Wataalamu wa TPDC wanasema kuwa kiasi cha gesi asilia kinachotumika kwa sasa nchini, ni sawa na asilimia 16 tu ya gesi asilia yote iliyogundulika.


  Nchi ya Norway, ambayo kwa sasa ina idadi ya watu wasiozidi milioni tano, inapata neema kubwa kutokana na sekta ya mafuta na gesi asilia. Mfuko ulioundwa kwa ajili ya kuweka fedha za rasilimali hizo katika nchi hiyo, unatajwa kuwa na kiasi cha dola za Marekani bilioni 500, ambazo hata Serikali ya nchi hiyo haijui itazitumia wapi kutokana na wingi wa fedha hizo.


  Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, anasema "Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizobarikiwa kuwa na rasiliamali nyingi na kwa hilo tunamshukuru Mungu sana na hizi raslimali lazima zitumike na katika hili ni lazima kushirikiana na nchi nyingine zenye uwezo. Lakini kinachotakiwa lazima zitumike kwa faida ya nchi na watanzania kwanza."


  Mh. Sumaye anaongeza kuwa Kampuni za nje zije zichimbe lakini lazima kuwekeana utaratibu mzuri wa Watanzania kufaidika zaidi kuliko wao, na kuongeza kuwa hali hii ipo katika nchi nyingi za Afrika kwasababu bado hatujawa na utaalamu mkubwa katika suala zima la kuwekeana mikataba hii, kwani wataalamu hao wanatuzidi sana. Hivyo Afrika inatubidi tuinuke sana.


  "Hivi karibuni nilikuwa katika mkutano World Energy Forum uliofanyika Afrika Kusini ambapo nilikuwa mgeni rasmi katika kufunga mkutano huo na nieleza Afrika tunavyonyonywa sana inatakiwa tukabiliane na hili na tusipokabiliana na hili basi tutaendelea kufaidisha wengine tukidhani ndio utaratibu wa kuendesha biashara hizo," anasema.


  Mh. Sumaye anatoa wito wa kuwekeza na kusomesha vijana wetu kupata utalaamu kwenye sekta hizi za gesi, mafuta na madini sambamba na kwenye suala zima la sheria za kimataifa zinazohusika na mambo haya. 


  Aidha, amehsauri fedha zinazopatikana kutoka kwenye rasilimali hizi zitumike kuendeleza watu, kuendeleza nchi na miundomnbinu yake na nyingine kwa kadri inavyowezekana kuwekezwa kwa namna ambayo vizazi vijavyo vitafaidika sana kwasababu madini, mafuta ni vitu vinavyokwisha.


  "Basi hizo fedha tuwekeze katika utaratibu ambao watoto wetu wanaokuja watazifaidi. Lakini,hatujawa na utaratibu wa kuwekeza fedha kutokana na rasilimali hizi kwa ajili ya vizazi vijavyo.Tunaweza kuona mifano katika nchi kama Uingereza, Norway ambavyo zinafanya hivyo na wanafanikiwa sana," anaeleza.  0 0

  MISATAN Chairperson Simon Berege addresses the media during a press conference to introduce World Press Freedom Day 2015

  Mwenyekiti wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani (WPFD) yatakayofanyika tarehe 2 mwezi Mei mwaka huu mkoani Morogoro.
  TMF Director Ernest Sungura clarifies a point during the conference
  Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) ambao ni miongoni mwa wadau wa maandalizi ya maadhimisho hayo Bw. Ernest Sungura akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika katika hoteli ya Holiday Inn jijini Dar es Salaam leo. Kulia Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa ambao ni miongoni mwa wadhamini wa maadhimisho hayo, Usia Nkhoma Ledama.
  Ms Jane Mihanji, UTPC Vice President tells why it is important for journalists to be at centre stage during celebrations
  Makamu Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waancdishi wa habari nchini (UTPC), Jane Mihanji akisisitiza umuhimu wa wanahabari kuhudhuria maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani (WPFD) ambayo kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani Morogoro Mei 2 mwaka huu. Katikati ni Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa ambao ni miongoni mwa wadhamini wa maadhimisho hayo, Usia Nkhoma Ledama na kushoto ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) ambao ni miongoni mwa wadau wa maandalizi ya maadhimisho hayo Bw. Ernest Sungura.
  KAS's Richard Shaba and TAMWA's Godrida Jola listen to questions from journalists
  Miongoni mwa wadau wa maandalizi ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani (WPFD) Bw.Richard Shaba kutoka KAS Tanzania na Mwakilishi kutoka TAMWA, Godrida Jola wakisikiliza maswali kutoka kwa wanahabari (hawapo pichani).
  A cross section of journalists covering the press conference
  Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini waliohudhuria mkutano huo.
  Journalists at the press conference


  Na Modewjiblog team
  Wanahabari na wadau wa habari wanatarajiwa kukutana Mkoani Morogoro  kwa siku mbili kwa kusanyiko la maadhimisho ya siku ya Uhuru wa habari duniani (WPFD), litakalofanyika katika hoteli ya Nasheera, Mjini Morogoro. Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika), Ndugu Simon Berege alieleza kuwa, kusanyiko hilo la wandishi wa habari na wadau wa habari litafanyika mjini humo Mei 2-3, mwaka huu.

  “Hii ni mara ya kwanza WPFD kuadhimishwa mkoani Morogoro na mwakani itafanyika mkoa mwingine nia ni kufanya kila mkoa kupata nafasi ya kuadhimisha siku hiyo. Wakati wa maadhimisho hayo wadau watakumbuka gharama za waandishi wa habari kukusanya taarifa mbalimbali na kuwapatia wananchi, gharama ambazo wakati mwingine ni uhai wao au hata kunyimwa uhuru’ alieleza Berege. Aidha siku hiyo watakumbukwa wale waliopoteza maisha kutokana na harakati za kutafuta habari kwa ajili ya umma.

  Siku ya WPFD, ambayo huadhimishwa duniani kote kila mwaka ilianzishwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuadhimisha kanuni za uhuru wa habari na kuwakumbuka wale waliokufa wakijaribu kutekeleza kanuni hizo. Kwa maneno mengine WPFD ni jukwaa linalotumika na waandishi wa habari na wadau wengine katika kutoa kauli za kushawishi serikali mbalimbali kutunga sheria rafiki za vyombo vya habari ambazo zitahakikisha uwapo wa uhuru wa habari.

  Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Usalama wa habari katika ulimwenguj wa dijiti: Uandishi bora, Usawa wa jinsia na faragha’. Berege alibainisha kuwa, kwa kuzingatia kauli mbiu hiyo, WPFD 2015 itaangalia masuala matatu muhimu: Ikiwemo Uandishi bora na ulio huru katika dunia ya dijiti. Humu itajadiliwa uwingi wa vyombo vya habari na athari zake katika majukumu ya uandishi na uwajibikaji kwa umma, masuala ya kujiwabisha wenyewe, changamoto katika habari za uchunguzi, kauli za uchochezi na vyombo vya habari na mafunzo ya habari.

  Pia suala lingine ni juu ya Wanawake na menejimenti ya vyombo vya habari; na namna vyombo vya habari vinavyomuona mwanamke huku la mwisho likiwa ni suala la Usalama wa waandishi wa habari hasa katika maeneo yenye vurugu na jinsi ya kuhami vyanzo vya habari dhidi ya ufichuaji wa kidijiti. Katika kongamano hilo pia litatoa nafasi ya kujadili na kutoa maazimio kuhusu sheria zilizopitishwa na bunge na zile ambazo zimetamkwa kwa mara ya kwanza. Sheria hizo ni pamoja na za Cybercrime Act, Statistics Act, Media Services Bill and the Access to Information Law.

  Hata hivyo, imeelezwa kuwa, Wakati wa kongamano hilo walioathirika kwa kuvunjwa kwa uhuru wa habari watatoa ushuhuda wao. Pia taarifa ya hali ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika iliyoandaliwa na MISA itazinduliwa rasmi.

  Aidha, katika tukio hilo, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez huku wadau zaidi ya 200 wakiwemo wadau wa habari na maendeleo pamoja na wawakilishi kutoka serikalini na mashirika mbalimbali ya kimataifa, mabalozi, wabunge, vyama vya kijamii, asasi zisizokuwa za kiserikali, waandishi maveterani,wakuu wa vyuo vya habari na waandishi wa habari.

  Tukio hilo limeandaliwa kwa pamoja na Media Institute of Southern Africa-Tanzania Chapter [MISA (T) Chapter], Media Council of Tanzania [MCT], Tanzania Media Fund [TMF], Union of Tanzania Press Clubs [UTPC], United Nations Tanzania Office, UNESCO.

  Wengine ni Konrad-Adenauer-Stiftung Tanzania [KAS], Media Owners Association of Tanzania [MOAT], Tanzania Editors’ Forum [TEF], Tanzania Media Women’s Association [TAMWA), Morogoro Press Club na Tanzania Communication Regulatory Authority [TCRA).

  Aidha kamati ya maandalizi ya WPFD 2015 imewezesha tukio hilo kwa kushirikisha pia Government Employees Pensions Fund [GEPF], Alliance One Tanzania, IPP Group of Companies, European Union (EU) na Tanzania National Parks [TANAPA].

  0 0
 • 04/27/15--21:37: Article 7
 • "The burden of Dumah. He calleth to me out of Seir, Watchman, what of the night? Watchman, what of the night?  The watchman said, The morning cometh, and also the night: if ye will enquire, enquire ye: return, come."

  0 0

   Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta (aliyesimama) akifungua Mkutano wa wafanyakazi wa Wizara hiyo mapema jana jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo Dkt. Shaaban Mwinjaka na kulia ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo Bwana Hassan Mabula.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka akimshukuru Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta mara baada ya kufungua rasmi mkutano wa wafanyakazi wa wizara hiyo na taasisi zilizo chini yaka.
   Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo Dkt. Shaaban Mwinjaka mapema jana jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa wafanyakazi wa Wizara hiyo.
   Baadhi ya watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi wakiwa katika mkutano wa wafanyakazi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.  Waziri wa uchukuzi Mh,Samuel Sitta akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Uchukuzi na Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo mapema jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa wafanyakazi. Picha na Eliphace Marwa – MAELEZO

  0 0

  Mbunge wa viti Maalumumkoa wa Kilimanjaro,Lucy Owenya akiwasili katika uwanja wa michezo wa shule ya sekondari Singhiti kwa ajili ya ufunguzi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015 yanayofanyika katika jimbo la Moshi vijijini na kushirikisha kata 16 za jimbo hilo.
  Baadhi ya wananchi waliohudhulia ufunguzi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015.
  Mbunge Owenya akicheza ngoma katika shrehe za ufunguzi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup.
  Baadhi ya timu zinazoshiriki mashindano hayo zikiwakatika uwanja wa shule ya sekondari Singhiti kwa ajili ya uunguzi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015.
  Mratibu wa mashindano hayo,Charles Mchau akizungumza jambo katika ufunguzi wa mashindano hayo.
  Mbunge wa Vitimaalumu mkoa wa Kilimanjaro ,Lucy Owenya akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015 ,Mashindano yaliyoanza katika jimbo la Moshi vijijini yakishirikisha kata za Jimbo hilo.
  Mbunge wa Viti Maalum Lucy Owenya akisalimianana mwamuzi Batista Mihafu wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo.
  Mbunge wa Viti maalumu ,Lucy Owenya akikagua baadhi ya timu zinazpshiriki mashindano hayo .
  Mbunge Lucy Owenya akipiga mpira kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup.


  Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Kilimanjaro ,Lucy Owenya akisalimiana na mmoja wa wachezaji wanaoshiriki mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015 yaliyozinduliwa juzi katika jimbo la Moshi vijijini na kushirikisha timu kutoka kata 16 za jimbo hilo.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

    Balozi wa Kampeni  ya Malaria wa Tanzania na aliye kuwa Rais wa Shilikisho la Mpira  TFF Tenga akizungumza na washiriki mbalimbali baada ya matembezi hayo ya  Maadhimisho ya Kutokomeza Ugonjwa wa Malaria Duniani   viwanja vya Farasi Dar es Salaam juzi
    Balozi wa Kampeni ya Malaria wa Tanzania na aliye kuwa Rais wa Shilikisho la Mpira  TFF Tenga (wanne kushoto) katika picha ya pamoja na wafanyakazi mbalimbali wa kiwanda cha Bia Dar es Salaam Tanzania  katika  Maadhimisho ya Kutokomeza Ugonjwa wa Malaria  viwanja vya Farasi Dar es Salaam juzi
  Meneja Rasilimali watu kiwanda cha Bia Dar es Salaam Emmanuel Christopher ( wakwanza kulia) akimkabidhi Vyandarua 50  kwaniaba ya TBL  Balozi wa Kampeni  ya Malaria  Tanzania na aliye kuwa Rais wa Shilikisho la Mpira  TFF Tenga (wanne kushoto) katika Maadhimisho ya Kutokomeza Ugonjwa wa Malaria Duniani  viwanja vya Farasi ambapo  Dar es Salaam juzi.


   Picha ya baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika banda lao kabla ya  Maadhimisho ya Kutokomeza Ugonjwa wa Malaria Duniani   viwanja vya Farasi Dar es Salaam juzi  Oysterbay.
   Matembezi
   Matembezi
   Matembezi
   Matembezi barabara ya Coco Beach
   Matembezi
   Baadhi ya washiriki wakipata vinywaji katika moja ya kituo kilicho andaliwa eneo la Morogoro Stoo eneo la Oysterbay  wakati walipokua katika matembezi hayo yaliyoanzia viwanja vya Farasi
   Baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda cha Bia Dar es Salaa Tanzani wakifuatilia jambo wakati Balozi wa Malaria Tenga alipokuwa akizungumza na washiriki mbalimbali baada ya matembezi hayo katika Maadhimisho ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria Duniani yaliyofanyika  Dar es Salaam  juzi
   Picha ya baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika banda lao wakitowa huduma kwa washiriki kwenye Maadhimisho ya Kutokomeza Ugonjwa wa Malaria Duniani   viwanja vya Farasi Dar es Salaam juzi

  0 0


  0 0

  MALINZI AWAPONGEZA YANGA.

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans, Yusuf Manji kufuatia timu yake kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015.

  Katika salamu zake za pongezi, Malinzi amesema kutwaa Ubingwa wa VPL ni jambo muhimu na sasa wanapaswa kuanza maaandalizi kwa ajili ya michuano ya kimataifa barani Afrika mwakani.

  Klabu ya Young Africans imetwaa Ubingwa wa Ligi Kuu nchini kwa mara ya 25 (ishirini na tano) jana, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya timu ya Polisi Morogoro katika uwanja wa Taifa huku ikiwa na michezo miwili mikononi kabla ya ligi kumalizika.

  Waziri wa Habari, Vijana Utamuduni na Michezo, Dr. Fennela Mkangara anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kukabidhi Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Mei 6, 2015 katika mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Young Africans.


  VILABU VPL VYAPIGWA FAINI, WAAMUZI WAFUNGIWA
  Ruvu Shooting imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa kuzingatia Kanuni ya 14(9) ya Ligi Kuu kwa kutoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo (changing room) katika mechi namba 149 dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga

   Pia Ruvu Shooting imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kutoingia vyumbani wakati wa mapumziko kwenye mechi hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu.

  Stand United imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya washabiki wake kuwatupia chupa za maji wachezaji wa akiba wa timu ya Polisi Morogoro katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu.

  Naye Meneja wa Polisi Morogoro, Manfred Luambano alitolewa kwenye benchi la Polisi Morogoro kwa kosa la kutoa lugha za kashfa kwa mwamuzi msaidizi namba moja Martin Mwalyanje. Suala lake linapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya hatua za kinidhamu.

  Kipa wa Ndanda SC, Wilbert Mweta amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kumkanyanga na kutaka kumpiga mwamuzi Eric Onoka kwenye mechi namba 155 dhidi ya Polisi Morogoro iliyochezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 37(5) ya Ligi Kuu. Kabla ya kufanya kitendo hicho alikuwa ameonyeshwa kadi nyekundu.

  Meneja wa Kagera Sugar, Mohamed Hussein anapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kutoa lugha ya matusi kwa waamuzi na kutaka kumpiga mwamuzi msaidizi namba 2, Said Mnonga kwenye mechi namba 158 dhidi ya Azam FC iliyochezwa Uwanja wa Azam Compex jijini Dar es Salaam.

  Naye Kipa Andrew Ntala wa Kagera Sugar amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kuingia kwenye vyumba vya waamuzi na kuwatolea lugha ya matusi mazito ya nguoni baada ya mechi hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 37(5)(c) ya Ligi Kuu.

  Mwamuzi wa mechi kati ya Azam FC na Kagera Sugar, Stephen Makuka na mwamuzi msaidizi namba mbili Said Mnonga wameondolewa kwenye orodha za waamuzi wa Ligi Kuu na kufungiwa miezi 12 kwa kushindwa kumudu mchezo kwa uzembe. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 38(1) ya Ligi Kuu.

  Pia Kamishna wa mechi hiyo Bevin Kapufi amefungiwa mwaka mmoja kwa kutoa taarifa isiyo sahihi. Adhabu hiyo imetolewa kwa uzingativu wa Kanuni ya 39(1) ya Ligi Kuu. Naye Kamishna wa mechi namba 159 kati ya Mbeya City na Simba, Joseph Mapunda amepewa onyo kutokana na ripoti yake kuwa na upungufu.

  Simba imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa kuzingatia Kanuni ya 14(9) ya Ligi Kuu kwa kutoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo (changing room) katika mechi namba 159 dhidi ya Mbeya City iliyochezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Pia Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kutoingia vyumbani wakati wa mapumziko kwenye mechi hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu.

  Mgambo Shooting imepigwa faini ya sh. 100,000 (laki moja) kwa kuchelewa kufika kwenye kikao cha kitaalamu cha maandalizi ya mechi (technical meeting) dhidi ya Ruvu Shooting. Mechi hiyo namba 161 ilichezwa Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, na adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(2)(a) ya Ligi Kuu.

  LIGI YA MABINGWA WA MIKOA SASA MEI 9
  Michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) sasa itaanza Jumamosi Mei 9, 2015 badala ya Jumamosi Mei 2, 2015 kama ilivyokua imetangazwa awali.

  Uamuzi huo umefanyika ili kutoa fursa kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kukamilisha maandalizi ya mwisho ikiwemo ukaguzi wa viwanja ambavyo vitatumika katika RCL na masuala mengine ya kumsingi.

  Tunaomba radhi kwa usumbufu ambao utakuwa umejitokeza kutokana na taarifa hii ya kusogeza mbele kuanza kwa ligi, lakni pia kuzitakia kila la kheri timu zinazoshiriki katika maandalizi yao.

  Ratiba ya mashindano itatolewa/kutumwa leo kama ilivyopangwa awali.


  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


  0 0

  imagesKIKUNDI cha Wasanii 50 wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) wanatarajiwa kuondoka Mei 10, mwaka huu kwenda kuanza maisha mapya ya kijijini ya kulima, kufuga na kuandaa filamu.

  Akizungumza katika mkutano wa wanachama uliofanyika mwishoni mwa wiki Dar es Salaam, Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema maandalizi ya wasanii hao kuhamia kijijini yamekamilika  na akiwemo yeye ataongoza msafara huo.

  Alisema kati ya wasanii watakaohamia kijijini ni mchezaji wa zamani wa Simba, Dua Said na mwigizaji wa Bongo Movie, Lumola Matovola ‘Big’ na wengine. Taalib alisema wasanii wengine katika kikosi chao wapo wapiga picha, walimu wa kutunga hadithi na wasanii watakaocheza filamu na tamthilia hizo. Alisema wasanii hao pia watagaiwa mashamba ya kulima bustani za mboga mboga, matikiti maji, pilipili na kufuga kuku, bata na mbuzi.

  Katika mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama zaidi ya 200 ilitolewa ofa ya kuingia wanachama katika kusherekea miaka 10 ya SHIWATA ambayo kilele chake kinafanyika Juni mwaka huu ambako nyumba 30 zitagaiwa.Kijiji cha Wasanii Mkuranga mpaka sasa kimejengwa nyumba 134.

  Wanachama hao pia waliwataka wenzao zaidi ya 8,000 kupiga ndiyo za kwenye kura ya maoni ya katiba mpya kwa vile imelenga kuwakomboa wasanii kutoka kwenye wimbi la umasikini.


  Mkutano huo pia ulipitisha adhabu ya kuwafukuza wanachama ambao watakwenda kinyume na utaratibu wa uliowekwa wakati wa kujiunga uanachama, usimamizi wa mashamba na kukiukwa kwa sheria za kijiji cha wasanii Mwanzega, Mkuranga.

  0 0

   ZANTEL, a Malaria Safe Company joined hands with the Ministry of Health and Social Welfare, other Malaria Safe Companies, donors and civil society to commemorate the World Malaria Day (WMD) on April 25th, 2015.
   
  The World Malaria Day theme provides a common platform for all malaria partners to showcase their successes in malaria control and unify diverse initiatives in the changing global context. 

  Malaria-endemic countries have made incredible gains in malaria in the last decade, but sustaining them will take extra efforts until the job is finished and malaria is eliminated worldwide. The theme for 2015 is Invest in the future, Defeat malaria calling attention to the need to increase commitments in the new era of development, with Sustainable Development Goals.
   
  In this year’s climax, we had a 5Km walk that started and ended at the Goat Race Grounds and the National World Malaria Day (NMWD) at the Mnazi Mmoja Grounds. The occasion of the NWMD was graced by the Dar es Salaam Regional Commissioner, Hon. Mr. Said Meck Sadick. 
   Hon. Mr. Said Meck Sadick, giving his remarks on the National World Malaria Day at Mnazi Mmoja Grounds in Dar es Salaam. 
   ZANTEL Chief Human Resources Officer, Mr. Francis Kiaga (L) and ZANTEL Marketing Director, Ms. Progress Chisenga. 
   Mr. Alex Royd, ZANTEL Staff, taking a Malaria Test and diagnosed NEGATIVE.
   Ms. Winnes Lyaro, Specialist Media, ZANTEL, taking a Malaria Test at the Mnazi Mmoja Grounds and diagnosed NEGATIVE.
   ZANTEL Staff on the walk
   Photos below are showing the 5Km walk activities.


older | 1 | .... | 513 | 514 | (Page 515) | 516 | 517 | .... | 1897 | newer