Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

Ujumbe wa metosha ukiwa Metro fm 99.4 Mwanza!

0
0

Kutoka kushoto ni Juma Herman(meneja wa Green Palm Hotel, Issaya Mwakilasa aka Wakuvwanga, Jhikolabwino Manyika, Kelvina John, Mwenyekiti Masoud Kipanya na Tonny Alphonce(Mtangazaji Metro fm 99.4

Siku ya Ijumaa ya tarehe 17/04/2015 ujumbe wa Imetosha Foundation ukiongozwa na Mwenyekiti Masoud Kipanya ulifanya mahojiano katika kituo cha redio cha Metro Fm 99.4 kwenye kipindi cha Pambazuko la Metro fm 99.4 ikiwa ni katika mfululizo wa kujitambulisha kanda ya ziwa kwa taasisi hiyo inayopinga mauaji kwa watu wenye ualbino kwa njia ya elimu. 

Msanii wa vichekesho (comedian) Wakuvwanga ambaye ni mjumbe wa taasisi hiyo alitoa kali alipoulizwa angependekeza adhabu gani kwa watakaopatikana na hatia ya kuua watu wenye ualbino? akajibu "Kwa kuwa hawa si watu bali ni wanyama kutokana na vitendo vyao viovu basi napendekeza serikali iwapeleke Mikumi national park iwafungie ndani ya senyenge ili watalii wawe wanaenda kuwaona kama wanavyoenda kuwaona Simba na wanyama wengine! Kipindi hicho maridhawa kiliendeshwa na watangazaji Tonny Alphonce na Katumba Madua
Mtangazaji wa kipindi cha Pambazuko la Metro Fm, Tonny Alphonce akimuuliza swali Masoud Kipanya.
Masoud Kipanya akijibu swali toka kwa mtangazaji wa Metro Fm 99.4zaji Tonny Alphonce.
Tonny akimpiga swali Wakuvwanga, anayesikiliza kwa umakini wa hali ya juu, soma uone jibu lake!
Kutoka kushoto ni Katumba Madua, Wakuvwanga na  msanii wa muziki wa Reggae Jhikoman

Moja ya studio za Metro Fm 99.4 ambazo wanazo tatu katika jengo hilo lililopo kati kati ya jiji la Mwanza
Picha ya Pamoja ndani ya Metro fm 99.4 toka kushoto ni Juma Herman, Mkala Fundikira, Kelvina John, George Binagi, Tonny Alphonce, Rosier, Sophia George, Wakuvwanga Masoud na Katumba Madua.
Jhikoman kushoto, Rosier(receiptionist) na Masoud.
Masoud akibadilishana mawazo na Sphia George wa Metro fm 99.4 ya Mwanza wiki iliyopita ujumbe wa Imetosha Foundation ulipotembelea studio za kituo hicho cha redio.

ESAURP, FSDT launches a project of formalization and capacity building of MSMEs in Tanzania.

0
0

 Eastern and Southern African Universities Research Programme (ESAURP) has today launched a project geared on formalizing of Micro, Small and Medium entrepreneurs (MSMEs) covering ten (10) regions of mainland Tanzania; Arusha, Kilimanajaro, Mbeya, Iringa, Kagera, Mtwara, Kigoma, Singida, Morogoro, Dodoma.  

The project, sponsored by Financial Sector Deepening Trust (FSDT) will target a total of 1,500 (150 from each region) businesses/ entrepreneurs.
Speaking to reporters, ESAURP Executive Director Professor Ted Maliyamkono said the project aims to help micro and small businesses in the informal sector acquire business skills to help them grow and cross over to the formal economy, enable them to have access to financial services and also to work with partner banks to create a shift in banking culture in the way they assess informal sector projects seeking financial services; particularly loans.

‘The underlying purpose of the project is to build the capacity of 1,500 micro and small businesses in order to grow.  This will be done by creating a replicable training programme aimed at helping small businesses integrate into the formal economy’ said Prof Maliyamkono

Prof Maliyamkono further noted that the project will also create a cadre of experienced trainers who will be able to deliver courses or programs to develop business skills to small businesses throughout the country thus increase the number of business service providers in the country, and expand the country’s business development capacity.

Also speaking at the event, FSDT Technical Director, Sosthenes Kewe said his organization support to this project aligns with their mission of empowering Micro, Small and Medium entrepreneurs to access financial services.

‘Small and medium sized enterprises (SMEs) are increasingly being recognized as a key drivers of economic growth and development for African countries. As contributors to both income generation and job creation, SMEs have the potential to significantly boost private sector growth’ said Mr. Omari Issa, CEO of the President’s Delivery Bureau (PDB) and who was the Chief Guest of Honors.

The project involve conducting business environment formalization review and capacity building programme by way of delivery of a 5 days training sessions to selected entrepreneurs in each region (general business management, financial management, record keeping, governance/business registration, tax matters etc) and a three month mentorship and setting up of business support centers that will operate for three months.

The project is a joint initiative of the FSDT, Eastern and Southern African Universities Research Programme (ESAURP) and committed participating financial institutions.

Dog For Sale

0
0
 Puppies Details:
Specie: German Shepherd
Gender: Female
Age: 2 Month (Puppies)
Immunization: Distemper; Canine Viral Hepatitis;  Leptospirosis;  Parvovirus and Rabies
Clinic card: Available
Pedigree: Very Good
Contact: 0713353939




WATOTO WATAKIWA KUSHIRIKISHWA MASUALA YA HISTORIA YA NCHI

0
0
 Ofisa usitawi wa Jamii,OMR-Muungano,Elimida Kashumba akizungu akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari katika viwanja vya Makumbusho ya taifa jijini Dar es Salaam leo.
 Mwanafunzi wa shule ya msingi Gerezani-Kariakoo jijini Dar es Salaam,Monica Samwel akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari kuhusiana na alichojifunza leokatika viwanja vya Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Mwalimu wa shule ya msingi Mnazi Mmoja Bora Makwaya akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari leo katika viwanja vya Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali waliokuwepo katika viwanja vya Makumbusho jijini Dar es salaam leo.(Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WATOTO wanatakiwa kushirikishwa katika masuala mbalimbali ya nchi ili waweze kujua historia na kuwa mabalozi wa kuelimisha jamii.


Hayo ameyasema leo Afisa Elimu wa Makumbusho ya Taifa,Annamary Baganyi wakati warsha  ya wanafunzi 1500 katika Mkoa wa Dar es Salaam iliyondaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais –Muungano pamoja na Makobusho ya Taifa iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.


Annamary amesema wameanza kutoa elimu wanafunzi wa shule ya msingi ili waweze kujua historia ya Muungano na kuweza kuwa mabalozi kwa kuelimisha jamii.


Amesema watoto wakishirikishwa katika masuala ya nchi wanaweza kujua historia kutokana na kizazi hicho hakikuwepo katika muungano.


Aidha amesema watu wataendelea kutoa elimu katika mambo mbalimbali ambayo wamekuwa hawajui lakini wamekuwa wakipumzika na kusema ni siku mapumbuziko.

MWENDO NA STORI BILA KUOVERTAKE

0
0

HAPA KAZI TUU

0
0
Mwendo wa kutafuta fwezaaa akiwa na speya taili chini ya toroli ikitumika kama sehemu ya breki eneo la Salenda.
(Picha na Avila Kakingo)

BILLIONAIRE MO TO GIVE AWAY $100M THROUGH MODEWJI FOUNDATION

0
0
Mo-Dewji_0310-780x350
Mohammed Dewji, head of the $1.25bn MeTL Group and an MP in Tanzania, is set to launch a foundation in May to give away $100m of his fortune.

Dewji – ranked 31st richest person in Africa last year by Forbes – plans to gift around $2m from his fortune to the Mo Dewji Foundation on its launch, gradually building up the endowment fund to some $100m, he told Philanthropy Age. “I earned my money in Africa,” said Dewji. “It is my responsibility and priority to give back. 

The foundation will start with work across Tanzania, with the aim of extending its reach into other African countries. The focus areas of the foundation are still being developed, but education, healthcare, water access and enhancing purchasing power for the very poor are all being considered. The timeframe by which the foundation will reach its $100m target is still being decided, he added.

Dewji, 39, heads the Mohammed Enterprises Tanzania (MeTL) Group, an industrial conglomerate. Involved in local development for more than a decade through his political office, Dewji wants to use his foundation to extend his philanthropic reach throughout his country.

Dewji has worked to improve quality and access to education, water, healthcare and agriculture in his constituency of Singida, central Tanzania, since becoming its MP in 2005.

“Just giving money is not enough,” said Dewji, who grew his father’s successful import-export operation into a sprawling business with interests in manufacturing, agriculture, real estate and textiles. “I’m planning to devote at least 10 per cent of my time to [my foundation] to start with.”


Dewji’s own philanthropic journey started in 2000, when he first sought the nomination for MP from his ruling Chama Cha Mapinduzi party. It was an old man’s hunt for water that prompted him to run for parliament, according to Dewji. “There was a puddle of yellow water and the old man had a bucket and a plate and he was scooping up the water and sand with it,” he said. “I went to see and just 5km outside of Singida I saw young children drinking yellow water from used PET [plastic] bottles.”

Elected in 2005 and again in 2010, to represent Singida district, Dewji has used his MP’s fund to build infrastructure in his constituency, including new bore wells, schools and eye care centres. He has worked with organisations such as the Bilal Muslim Mission, Lions Club and the Helen Keller Foundation to combat cataracts and preventable eye diseases.

Named a young global leader by the World Economic Forum, the billionaire is inspired by philanthropists such as Bill Gates, Warren Buffett and the Aga Khan he said. While he has not ruled out signing the Gates and Warren-backed Giving Pledge – where wealthy individuals commit to giving away more than half of their wealth to philanthropy – Dewji is clear he wants to strike out on his own and focus his efforts on Africa.

“The number of [African philanthropists in Africa] is growing,” said Dewji. “[But] we need the wave to get bigger and bigger and it has to trickle down.” There has been a shift in thinking on the continent as wealthy individuals start to consider giving much earlier on, he adds.
Since 2000, he has become more strategic in the way he uses funds, and says he is keen to apply some of the rigours of running a business to his foundation: “Whatever you do has to be viable, sustainable and for the long-term,” he said.
Source click here

DUKA LA NAKIETE LATOA MSAADA HOSPITALI YA SINZA

0
0

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akipokea Msaada kutoka Kwa  Mkurugenzi wa Duka la Dawa la Nakiete Bi Batilda.
Duka la Dawa la Nakiete Limetoa msaada katika Hospitali ya Sinza.Vitu Mbalimbali vilitolewa na duka hilo vyenye Dhamani ya Shilingi milioni 6.Mkurugenzi wa Nakiete Akieleza zaidi kuhusu msaada huo amesema hiyo ni sehemu ya faida waliyopata kwa Mwaka uliopita wakaona ni vema kurudisha sehemu ya faida hiyo kwa jamii.Alisema Hospitali inakabiliwa na changaamoto nyingi lakini wao wameona wasaidie kile kidogo walichopata. 
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akipokea Msaada 

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akiwa katikati ya wakinamama alipowatembelea kuwajulia hali na kuwapa zawadi.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda akiwa wodi ya wazazi Akimpa Mmoja wa wakinamama waliojifungua jana sehemu ya zawadi zilizotolewa na Duka la Nakiete Ambapo zaidi ya wakinamama 40 waliokuwa wamelezwa katika wodi hiyo walinufaika
Baadhi ya wakina mama waliotembelewa na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh Makonda 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda akishukuru kwa Msaada huo amewapongeza kwa moyo waliouonyesha wa kujitolea kwajili ya wananchi maskini wa tanzania.Aidha Mkuu wa wilaya amesema Nakiete wameonyesha mfano kwa kujitolea kwasababu wa Pamoja na kulipa kodi bado wameona umuhimu wa kujitolea kwa jamii ya tanzania tofauti na wachache wanaoikosesha serikali kwa kukwepa kodi na bado hata hawawakumbuki hata Wananchi maskini wa tanzania.

UTIAJI SAINI MANUNUZI YA ENEO LA OFISI KWENYE JENGO LA MOROCCO SQUARE KATI YA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) NA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

0
0
hc1Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa wakitiliana saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea. (Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii)hc2Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo.hc3Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo.hc4
hc5Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhudua NHC na DSE wakitiliana saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea
hc6Watendaji wa NHC na DSE wakibadilishana mawazo wakati wa utiaji saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea.hc7 Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa Tuntufye Mwambusi na Meneja wa Uendelezaji Biashara wa NHC, Willia Genya wakibadiliashana mawazo katika hafla hiyo.hc8Mchechu akibadilishana mawazo na watendaji wa DSE wakati wa utiaji saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea.hc9 Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa, David Misonge Shambwe akiwakaribisha wageni katika hafla hiyo.
hc10 Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa wakifuatilia jambo katika hafla hiyo ya utiaji saini. hc11 Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla hiyo.hc12 Watendaji wa DSE wakibadilishana mawazo wakati wa utiaji saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea.hc13Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa akizungumza katika hafla hiyo.hc14hc15 Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo.hc16Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo.hc17Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo.
............................................................................
Kwa mara nyingine Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo Jumatano, 22 Aprili 2015 tumefikia makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea.

Mkataba unaosainiwa leo baina ya pande hizi mbili utagharimu kiasi cha dola za kimarekani 1,800,000 (bila VAT) kiasi cha shilingi za kitanzania 3.366 bilioni malipo yatakayofanyika kwa awamu nne katika kipindi cha miaka mitatu.

Mradi wa kipee na wa kwanza Tanzania wa Morocco Square wenye ukubwa wa mita za mraba 105,000 unaotarajia kukamilika ndani ya kipindi cha Miaka Mitatu, ni unaotekelezwa kwa kutumia mfumo mpya kabisa wa ujenzi wa (Design and Building). Umebuniwa kwa makini kabisa kulingana na mahitaji ya majengo ya sasa na ya baadae na vile vile unajengwa na mkandarasi wa kitanzania. Sambamba na haya, utekelezaji wa mradi huu umezingatia uwepo wa huduma zote muhimu sambamba na miundo mbadala yakujitosheleza.
Sifa nyingine za ziada za mradi huu ni pamoja na uwepo wa majengo pacha mawili makubwa ya ghorofa, moja likiwa na ghorofa 17 na 19.

Jengo hili limebiniwa likiwa na mahitaji muhimu yakiwa sehemu moja (Mixed Development) ikiwepo maeneo maalum ya Maofisi ya kimataifa, Sehemu ya hotel kwa ajili ya wafanyabiashara, nyumba za makazi (Residential apartment), maeneo ya maegesho ya magari, huduma za kibenki, pamoja na sehemu ya huduma za masoko ( shopping mall).

Mradi huu unatarajiwa kuboresha mazingira ya biashara katika jiji la Dar Es Salaam vile vile ukizingatia mahitaji ya ukuaji na upanukaji wa jiji la Dar Es Salaam. Jengo la Morocco Square lipo karibu kabisa na kitovu cha jiji likiwa limezungukwa na maofisi na makazi muhimu kabisa. Eneo la Morocco Square linatoa fursa kwa mkazi kuweza kufika kwa karibu kabisa sehemu mbalimbali muhimu za jiji la Dar Es Salaam kama vile Mikocheni, Oystebay, Masaki,Mikocheni, katikati ya jiji la Dar Es Salaam,Kinondoni, Kawe na Mlimani City.

Makubaliano haya kati ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na Soko la Hisa la Dar Es Salaam ( Dar Es Salaam Stock Exchange (DSE) yanatoa fursa za kipekee kwa (DSE) pamoja na mawakala wake wa soko la mitaji na tunapenda kulipongeza soko la hisa kwa kuwahi kabla ya mashirika yote ili kuweza kupata fursa ya kipekee katika jengo hili la kisasa kabisa na la kwanza Tanzania.

Tunapenda kutoa wito kwa Mashirika ya kimataifa, yakati ( Medium Enterprises) kuchanmkia fursa hii ya kipekee ususani ukizingatia kwamba miji yote Duniani soko la hisa huwa chachu ya maendeleo ya wadau wote wanaofanya biashara kuzunguka eneo husika.

Sifa za ziada za mradi huu ni kuwa na eneo maalumu linalowezesha kutua helikopta, eneo kubwa la maegesho ya magari ya ziada, Ofisi ya Meneja wa Usimamizi wa Milki, eneo maalumu la kukusanyia taka, nyumba ya mlinzi, umeme wa uhakika, miundombinu ya zimamoto, mfumo wa vipoza joto, kebo za mtandao wa mawasiliano, lifti, ulinzi wa saa 24 wa Kamera za CCTV na kisima kirefu cha maji chenye mfumo wa kusukuma maji ya kutosha.
Tunawahamasisha wenye kuhitaji maeneo ya ofisi, biashara na nyumba za kuishi wafanye mawasiliano na Makao Makuu ya Shirika na kukamilisha taratibu mapema kwa ajili ya kuweza kuingia kwenye mchakato ulio wazi wa manunuzi.

Ukiwa mdau na mnunuzi mtarajiwa, ama una ndugu/rafiki anayetamani kununua ofisi au kuwekeza katika mradi huu, tafadhali wasiliana na Kitengo cha Mauzo, Makao Makuu ya NHC au piga simu namba 0754 444 333; baruapepe: sales@nhctz.com na pia tembelea tovuti ya Shirika www.nhctz.com kwa maelezo zaidi.

AIRTEL YAZINDUA HUDUMA YA UNI WI-FI

0
0
Wakwanza kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Tanzania Aneth Muga akiwa ameshilia bango linaloonyesha huduma mpya ya Airtel Wi-Fi intaneti maalum kwa wanavyuo iliyozinduliwa rasmi kwa mara ya kwanza Mwanza katika chuo cha St Augustine (SAUT) pamoja nae anaefuata ni raisi wa serikali ya wanafunzi Sogone Wambura, Mshauri wa wanafunzi chuoni hapo bw,Liberates Ndegeulaya na Afisa masoko wa Airtel Mwanza Bw, Emanuel Raphael
Afisa masoko wa Airtel bw, Prospa Mwanda akitoa maelekezo ya jinsi huduma mpya ya Airtel Wi-Fi inavyofanyaka kazi kwa kasi kwa Raisi wa wanafunzi chuo kikuu cha SAUT mwanza Bw, Sogone Wambura (wakwanza kulia) na Makamu wa Raisi wa chuo hicho Bi, Pearl Mecar (kati) mara baada ya Airtel kuzindua huduma hiyo chuoni hapo jana.
Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga akionyesha kwa wanafunzi wa SAUT Mwanza (hawapo pichani) muonekano wa vocha za huduma mpya ya Airtel Wi-Fi intaneti iliyozinduliwa chuoni hapo jana maalumu kwaajili ya kuwapa wanafunzi intaneti nafuu na yenye kasi zaidi.

PINDA AKUTANA NA MAKAMU MWENYEKITI WA BARAZA LA BIASHARA LA CHINA AFRIKA

0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara  la China na Afrika ( Vice Chairman of China Africa Business Council, Bw. Huarong Zhang kabla ya mazungumzo yao Ofisini  kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam,Aprili 21, 2015.Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha  Tanzania – China Promotion Centre, Bw. Xian Ding. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)MZ01WAziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara  la China na Afrika ( Vice Chairman of China Africa Business Council, Bw. Huarong Zhang kabla ya mazungumzo yao Ofisini  kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam,Aprili 21, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI YA TANZANIA NA KOREA YA KUSINI ZAKUBADILISHANA UZOEFU KATIKA MASUALA YA UWEKEZAJI.

0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda akifungua kongamano kongamano la siku moja lililofanyika leo jijini Dar es salaam kuhusu masuala ya uwekezaji kati ya Tanzania na Korea ya Kusini ili kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi zote mbili kwa kushirikisha sekta ya Umma na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo endelevu.
02
Baadhi ya wajummbe kutoka nchini Korea ya Kusini wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati alipokuwa fungua kongamano la siku moja lililofanyika leo jijini Dar es salaam kuhusu masuala ya uwekezaji kati ya Tanzania na Korea ya Kusini ili kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi zote mbili kwa kushirikisha sekta ya Umma na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo endelevu.
03
Baadhi ya wajummbe kutoka Tanzania wakifuatilia mjadala wakati wa kongamano la siku moja lililofanyika leo jijini Dar es salaam kuhusu masuala ya uwekezaji kati ya Tanzania na Korea ya Kusini ili kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi zote mbili kwa kushirikisha sekta ya Umma na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo endelevu.
04
Picha ya pamoja ya wajumbe kutoka Tanzania na Korea ya Kusini walioshiriki kongamano la siku moja lililofanyika leo jijini Dar es salaam kuhusu masuala ya uwekezaji ili kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi zote mbili kwa kushirikisha sekta ya Umma na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo endelevu. Kutoka kushoto walioketi ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda. (Picha na Wizara ya Fedha).

Serikali ya Tanzania na Korea ya Kusini zimefanya kongamano la siku moja kuhusu masuala ya kiuchumi ili kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi zote mbili kwa kushirikisha sekta ya Umma pamoja na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo endelevu. Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda alipokuwa akifungua kongamano hilo lililofanyika leo jijini Dar es salaam.
Kongamano hilo lilikuwa na lengo kuiwezesha Tanzania kujifunza namna ya kuendesha masuala ya bajeti ya nchi na namna ya kushirikisha sekta binafsi na sekta ya Umma katika kuinua uchumi wa nchi.
Prof. Adolf Mkenda alisema kuwa kupitia kongamano hilo Tanzania imejifunza kutoka Korea ya Kusini namna ya kushirikisha sekta binafsi na sekta ya Umma katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu na ya nchi kwa ujumla.
“Kama nchi, tumeona ni vema kujifunza kutoka kwa wenzetu wa Korea ya Kusini ili kupata fursa na uzoefu katika kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuwa Korea ya Kusini ni miongoni mwa nchi zinzoongoza duniani kwa kuwa na uchumi imara walionao kwa kushirikisha sekta binafsi” alisema Prof. Mkenda.
Ili kupata maendeleo endelevu, Prof. Mkenda alisema kuwa jukumu la Serikali ni kushirikiana na sekta binafsi na kujiwekea mikakati mbalimbli itakayosaidia kuibua miradi ambayo itakuwa na ushindani ambapo kwa namna hiyo itasaidia nchi kuwa na maendeleo na hivyo kupata faida na kuinua uchumi wa nchi na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. 
Aidha, Prof. Mkenda alisema kuwa fursa hiyo ya kushirikisha sekta binafsi imeanza kuwa na mafanikio nchini ambapo tayari Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepisha mswada wa namna ya Serikali kushirikiana na sekta binafsi (PPP) katika kuleta maendeleo nchini.
Kwa upande wake mwakilishi wa Korea ya Kusini Dkt. Cae One Kim aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwa na ushirikiano mzuri katika kukuza na kuinua uchumi kati ya nchi hizo mbili ambapo Serikali zote mbili zinaimarisha na kujenga ushirikiano na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo. Dkt. Kim alisema kuwa uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya pande hizo mbili ndiyo umekuwa ni msingi wenye manufaa ambapo utaendelea kukuza sekta za kiuchumi, kibiashara, teknolojia na masuala ya kiutamaduni kati ya nchi hizo.
“Serikali ya Korea imetambua na kuiona Tanzania ni sehemu muhimu katika kukuza mahusiano ya kiuchumi ambayo yatasidia nchi hizi mbili kunufaika, kukuza na kuimarisha uhusiano uliopo baina yetu” alisema Dkt. Kim.
Mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Korea ya Kusini siyo ya muda mrefu kama ilivyo kwa Korea ya Kaskazini. 
Uhusiano huo kihistoria umeanza katika miaka ya 1990 ambapo Korea ya Kusini imekuwa nchi ya matumaini kwa kuwa imepata maendeleo makubwa duniani ambapo Tanzania itaendelea kunufaika na kujifunza ili kuimarisha uchumi wake hasa katika kipindi hiki cha ushindani katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.

MUNGU TUNUSURU YARABI TOBA....AJALI INGINE SHINYANGA, 10 WAPOTEZA MAISHA 40 WAJERUHIWA VIBAYA

0
0
Pichani juu ni Winchi likinyanyua basi baada ya ajali ambapo watu 10 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa kutokana na ajali ya basi la Unique na lori la Cocacola kugongana uso kwa uso  mkoani Shinyanga leo.Sababu kubwa ya ajali hiyo inaelezwa kuwa ni mwendo kasi.
 Zoezi la kunyanyua mabaki ya basi hilo likiendelea
 Simanzi yatawala eneo la ajali
Winchi likiwa kazini huku wanahabari wkirekodi tukio la kunyanyuliwa basi hilo

KAMATI YA MAWASILIANO NA UJENZI YA BARAZA LA WAWAKILISHI YATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA NA IDARA YA NJIA ZANZIBAR.

0
0
Wajumbe wa kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi wakitembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa  na Idara ya Ujenzi wa Barabara (UUB).  Mwenyekiti wa Kamati hiyo wakwanza  (kushoto) Mahmoud Muhammed Mussa akiwa na wajumbe wenzake na watendaji wakuu wa UUB wakikagua barabara ya Chaani iliopo Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
2
Mhandisi Mkuu  wa UUB  Eng. Cosmas Masolwa akitoa maelezo  kwa wajumbe wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi  ya Baraza la Wawakilishi juu ya ukarabati unaoendelea wa  kuihami njia ya Chaani kwa kuwekewa kifusi kabla ya kukamilishwa  ujenzi wake kwa kiwango cha lami hap baadae.
3
Sehemu ya barabara ya Chaani  iliyotembelewa na Kamati  hiyo  ambayo inafanyiwa matengenezo ya kutiwa kifusi  ili weze kupitika huku ikisubiri ujenzi wake kwa kiwango cha lami hapo baadae.

Vijana washauriwa kujali afya zao kwa kujiunga na Mfuko wa afya wa Jamii (CHF)

0
0
 Mhamasishaji kutoka Wizara ya habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa akifungua semina ya vijana wa Kata ya Lepurko na Sepeko kuhusu Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo katika Kata ya Lepurko Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha. Kushoto ni Afisa Vijana kutoka Wizara hiyo Bi. Amina Sanga, wa kwanza kulia ni Afisa Mtendaji Kata ya Lepurko Bw. Sambeta Moikan na wapili kulia ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele.

 Afisa Maendeleo ya Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Mesha Singoyo kulia akifafanua jambo wakati wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana katika Kata ya Lepurko Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha.

 Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga kulia akimsikiliza kwa makini kijana kutoka Kata ya Lepurko aliyekua akielezea kuhusu ufahamu juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wakati wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana katika Kata ya Lepurko Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha.

 Mhamasishaji kutoka Wizara ya habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa akiwaonyesha vijana wa Kata ya Lepurko na Sepeko mfano wa andiko la mradi linavyotakiwa kuwa wakati wa semina ya vijana wa Kata hizo katika Halmashauri ya Wilaya ya  Monduli Mkoa wa Arusha.

Dkt. Machuman Kiwanga kutoka Hospitali ya Wilaya ya Monduli akiwaonyesha vijana wa Kata ya Lepurko na Sepeko kadi za uanachama wa mfuko wa afya wa jamii (CHF) kuwahamasisha vijana hao kujiunga na mfuko huo kupata huduma za afya kwa bei nafuu wakati wa semina ya vijana katika kata ya Lepurko Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha.

Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele akitoa mada wakati wa Semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa vijana wa Kata ya Lepurko na Sepeko katika Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha.


Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo, Monduli.



Na: Ganofeva Matemu – Maelezo, Monduli.


Vijana wameshauriwa kujiunga na Mfuko wa afya wa jamii (CHF) unaotoa huduma rafiki ya afya katika jamii ili kuweza kuwa na afya bora itakayopelekea kuleta uchumi imara ndani na nje ya jamii ya kimasai.


Hayo yamesemwa na Dkt. Machuman Kiwanga kutoka Hospitali ya Wilaya ya Monduli wakati wa semina ya vijana wa Kata ya Lepurko na Sepeko kuhusu Ujasiriamali, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo katika kata ya Lepurko Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha.


Akifafanua masuala ya afya katika Sera ya Taifa ya Vijana ya mwaka 2007 Dkt. Kiwanga amesema kuwa kama vijana watajitambua na kuhimili mihemko ya miili yao watafanikiwa kupunguza tatizo la magonjwa ya zinaa likiwemo ngonjwa la ukimwi linalowakumba vijana wengi wakiwemo wa kike wenye umri kati ya miaka 15 hadi 20 kutokana na ngoma ya esoto inayomuandaa mtoto wa kike kabla ya kufunga ndoa pamoja na ukeketaji wa watoto wa kike.


“Serikali ina mpango wa Kujenga zahanati katika kila Kijiji na Vituo vya Afya katika kila Kata ikiwa ni mkakati wa kuboresha afya haswa kwa vijana katika masuala ya uzazi salama na ukimwi ili kuweza kuwa na uchumi imara katika jamii zetu” amesema Dkt. Kiwanga.


Aidha Mhamasishaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa amesema kuwa vijana wa Monduli wamepata fursa ya pekee ya kupata elimu ya afya uzazi na ukimwi itakayowawezesha kubadilika na kujali afya zao kwa kuachana na mila na desturi zinazowakosesha fursa za kiujasiriamali.


Bibi Riwa amesema kuwa ujana ni kipindi cha mpito ambacho kama kitatumika vibaya kitapoteza ndoto za vijana wengi hivyo kuwataka vijana wa Monduli kuwa na dira inayojali maamuzi yao kama vijana na kuwaongoza katika maisha bora kwa kutumia nguvu walizonazo.


Naye mshiriki wa semina hiyo Bibi. Naparakwo Leiio ameishukuru serikali kuwakumbuka vijana wa Monduli kwa kuwafikia na kuwapa elimu ambayo hawakuwa nayo hivyo kuhaidi kutumia elimu aliyoipata katika semina hiyo kuhamasisha vijana wengine katika vikundi vyao na kujenga umoja kati yao kwani umoja ndio suluhisho la unyanyasaji na ngao ya kuondokana na umasikini.




BILIONEA DANGOTE AKAGUA UFUKWE ATAKAOJENGA BANDARI YAKE YA KISASA MTWARA

0
0
 Mfanyabiashara maarufu Afrika, ambaye ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote Group of Industries, Alhaji Aliko Dabgote akinyoosha mkono kuangalia eneo la ufukwe wa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Mgao, Kata ya Maumbu, Tarafa ya Mayanga, Mtwara Vijijini, ambapo atajenga bandari yake ya kisasa kwa ajili kusafirisha saruji itakayozalishwa kwenye kiwanda chake kikubwa kinachojengwa katika Kijiji cha Msijute.
 Alhaji Dangote akipata maelezo kuhusu eneo alilopewa na Serikali ya Kijiji cha Mgao lenye ukubwa wa heka 2500 sawa na hekta 1000. Anatarajia kuanza kujenga bbandari hiyo mapema mwaka huu.
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dedengu akimtambulisha Alhaji Dangote kwa wananchi alipowasili katika Kijiji cha Mgao, ambapo amepewa Dangote  eneo la ujenzi wa Bandari.

 Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao, Shaa akihojiwa na wananchi kuhusu maufaa watakayopata wanakijiji endapo Nadari hiyo ikijengwa..PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Msafara wa Alhaji Dangote ukitoka eneo atakalojenga bandari katika Kijiji cha Mgao
 Ndege iliyomleta Dangote ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara tayari kwenda kukagua eneo atakapojenga bandari yake.
 Alhaji Dangote akishuka kwenye ndege na kulakiwa na Mwakilishi Mkazi wake hapa nchini, Esther Baruti
 Dangote akilakiwa na Esther Baruti
 Alhaji Dangote akilakiwa na Balozi wa Nigeria nchini, Dk. Ishaya Majanbu
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akisalimiana na Alhaji Dangote
 Alhaji Dangote akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu (kushoto) Mwakilishi wake hapa nchini, Esther Baruti na Balozi Dk, Majanbu
 Alhaji Dangote akizungumza na Esther Batuti
 Alhaji Dangote akisaini katika kitabu cha wageni alipowasili katika Kijiji cha Mgfao kukagua eneo la ujenzi wa Bandari pamoja na kiwanja alichopewa na wanakijiji kujenga makazi yake.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Abdulrahman Shaa
 Wananchi wakiangalia msafatra wa Alhaji Dangote uliokuwa unakwenda eneo asmbapo bandari itajengwa.
 Alhaji Dangote akiwa na viongozi wa Kijiji cha Mgao pamoja na wananchi akikagua uwanja heka mbili na nusu aliyopewa kwa ajili ya kujenga makazi yake katika kijiji hicho
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao, Shaa (kushoto) akimuonesha Dangote eneo la uwanja aliopewa  na wanakijiji kwa ajili ya ujenzi wa mkazi yake. Kijiji nacho kitanufaika na Dangote ambaye atawajengea shule, hospitali pamoja na miradi mingine ya maendeleo.
 Msafara wa Alhaji Dangote ukielekea eneo patakapojengwa Bandari
 Alhaji Dangote akizungumza na wanahabari kuhusu ujenzi wa bandari hiyo

 Msafara wa Dangote ukitumia magari kutembelea kiwanda cha saruji kinachojengwa





 Alhaji akijadiliana jambo na Meneja wa Mradi wa ujenzi wa kiwanda cha saruji, Kushoto ni Paschasia Ngaiza Mama Mzazi wa Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais wa Tanzania, Premy Kibanga ambaye pia alikuwepo kwenye ziara hiyo.
 Alhaji Dangote akizungumza na Balozi wa Nigeria nchini, Dk. Majanbu muda mfupi kabla ya kuondoka jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akimuaga Alhaji Dangote uwanjani hapo
 Alhaji Dangote akiteta jambo na mwakilishi wake hapa nchini, Esther muda mfupi kabla ya kupanda ndege kwenda Ethiopia na hatimaye Lagos, Nigeria.
 Alhaji Dangote akiaga
 Dedengu akijadiliana jambo na Esther
 Balozi wa Nigeria nchini, akizungumza jambo na Dendengu pamoja na Esther. Kulia ni Paschasia Ngaiza
Ndege iliyombeba Alhaji Dangote na ujumbe wake ikiondoka Uwanja wa Ndege wa Mtwara

Usikae kimya! Wafanye wabadilike

0
0

WAZIRI WA FEDHA MHE. SAADA SALUM MKUYA KATIK MKUTANO WA MAJUMUISHO NA IMF, BENKI YA DUNIA WASHINGTON DC MAREKANI

0
0
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya  akitoa ufafanuzi na majibu kwaswali aliloulizwa na Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki Bw.Herve’ Joly kwenye mkutano wa majumuisho kati yao na maafisa waandamizi wa  Shirika la fedha la Kimataifa (IMF) mjini Washington DC.
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile wakiwa kwenye mkutano wa majumuisho kati yao na maafisa waandamizi wa  Shirika la fedha la Kimataifa  (IMF) mjini Washington DC.
 Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki Bw.Herve’ Joly  (wa katikati mwenye Tai ya rangi ya chungwa)  akiwa kwenye mkutano wa majumuisho kati ya Shirika la fedha la Kimataifa na  ujumbe kutoka Tanzania( hawapo kwenye picha)mjini Washington DC.
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum akizungumza na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia  wa kundi namba 1 Afrika Bw. Louis Rene Peter Larose wakiagana mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya  akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia  wa kundi namba 1 Afrika Bw. Louis Rene Peter Larose kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile , Bw. Beda Shallanda Kamishina wa Sera na Bw. Paul  Mwafongo ambaye ni Afisa katika ubalozi wa Tanzania na kutoka kushoto ni Bw.Ngosha Said Magonya Kamishina wa Fedha za nje Bw. John Cheyo Kamishina wa Bajeti na wa pembeni ni mfanyakazi wa Benki ya Dunia. Picha zaidi BOFYA HAPA

Benki ya Exim yapiga jeki mbio za marathon Ngorongoro

0
0
 Afisa Masoko wa Benki ya Exim (Tawi la Karatu), Bi. Rosemary Meglan (kulia) akikabidhi kasha la gurudumu kwa Waziri Mkuu mstaafu Mh. Frederick Sumaye ambaye alikua mgeni rasmi katika mbio za Ngorongoro Marathon zilizofanyika Karatu, Manyara hivi karibuni. Benki ya Exim ilikua miongoni mwa wadhamini wa mbio hizo. Wengine ni wafanyakazi wa benki hiyo.
Afisa Masoko wa Benki ya Exim (Tawi la Karatu), Bi. Rosemary Meglan (kulia) akikabidhi vipeperushi vyenye taarifa za huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa Waziri Mkuu mstaafu Mh. Frederick Sumaye ambaye alikua mgeni rasmi katika mbio za Ngorongoro Marathon zilizofanyika Karatu, Manyara hivi karibuni. Benki ya Exim ilikua miongoni mwa wadhamini wa mbio hizo. Wengine ni wafanyakazi wa benki hiyo

KITABU CHA 'THE 7 HABITS OF HIGHLY EFFECTIVE PEOPLE' CHAZINDULIWA UPYA KWA LUGHA YA KISWAHILI

0
0
DSC_0308
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akipokea kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kwa ajili ya mafunzo ya kuongeza manufaa binafsi na maeneo ya kazi kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege (kulia). Katikati anayeshuhudia tukio hilo ni Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ambao wameshiriki kuandaa tafsiri ya kitabu hicho kwa lugha fasaha ya Kiswahili, Vida Mutasa
DSC_0313
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akionyesha kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kwa ajili ya mafunzo ya kuongeza manufaa binafsi na maeneo ya kazi kwa waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo pichani).
DSC_0316
Kutoka kushoto ni Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu, Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), Vida Mutasa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege, Mkurugenzi wa NFT Consult, Nambie Kiwanuka pamoja na Meneja biashara mkazi wa NFT Consult/Franklin Covey Tanzania, Joan Ajilong.
DSC_0339
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NFT Consult/Franklin Covey Tanzania.

DSC_0081
Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na wageni waalikwa.
DSC_0248
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania ambapo alitoa rai kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu mbalimbali vinavyotoa mwanga wa kujituma na kuwajibika.
DSC_0149
Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ambao wameshiriki kuandaa tafsiri ya kitabu hicho kwa lugha fasaha ya Kiswahili, Vida Mutasa akielezea changamoto alizokutana nazo wakati wa kutafsiri kitabu hicho.
DSC_0115
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kulia) na Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ambao wameshiriki kuandaa tafsiri ya kitabu hicho kwa lugha fasaha ya Kiswahili, Vida Mutasa (wa pili kushoto) pamoja na wadau wengine wakifuatilia uchambuzi wa kitabu hicho.
DSC_0006
Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege (kulia) akimwonyesha kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu mara baada ya kuwasili kwenye uzinduzi huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Serena.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
DSC_0007
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto) akipitia kurasa mbalimbali za kitabu hicho kabla ya uzinduzi rasmi. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege.
DSC_0053
Mwezeshaji wa Franklin Covey, Alice Levora akichambua kwa ufupi tabia 7 zilizomo kwenye kitabu hicho kwa wageni waalikuwa (hawapo pichani) kabla ya uzinduzi rasmi.


UWEKEZAJI mkubwa unatakiwa kufanywa katika eneo la raslimali watu, kama taifa hili linahitaji kuondokana na malalamiko kuhusu maendeleo na ajira.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemia Mchechu wakati akizindua tafsiri ya kiswahili ya kitabu cha “The 7 Habits of Highly effective people” kilichoandikwa na Mmarekani, Stephen Covey.

Hii inakuwa tafsiri ya kwanza ya kitabu hiki kwa lugha za asili zinazotumika bara la Afrika . Alisema malalamiko mengi kuhusiana na taifa kuwa na raslimali nyingi na umaskini kuendelea kuwepo yanatokana na kutoendelezwa kwa raslimali watu kwa lengo la watu kujitambua, kutambua wanachotaka na kusababisha kiwepo.

Alisema inasikitisha kuona kwamba watanzania wengi wanalalamika kuhusu hali ngumu kumbe ilhali wao huenda ndio wakawa sababu za matatizo hayo ya ukosefu wa maendeleo.
Alisema ni vyema watanzania wakajenga utamaduni wa kujisomea vitabu mbalimbali vinavyotoa mwanga wa kujituma na kuwajibika kwa kuwa vitabu hivyo vina tafiti nyingi za miaka mingi ambazo watanzania wakitumia kwa muda mfupi watafanya mabadiliko katika maisha yao.

Alisema uwapo kwa tafsiri ya Kiswahili kwa moja ya vitabu vyenye sifa kubwa duniani katika masuala ya menejimenti na ambacho kimekuwa katika 20 bora za vitabu duniani kwa miaka 20, kutasaidia watanzania wengi kujiangalia na kujifunza kuwa na dira na nidhamu ya kutekeleza yale ambayo wanayafikiria.

Alisema kwamba ari ya kusoma kazi mbalimbali kutasaidia watanzania kuwa na upeo mpana wa kujituma na kuwa na nidhamu ya malengo wanayostahili ya kufikia kwa muda mfupi na kwa ufanisi mkubwa. Tafsiri hiyo ya kitabu ambayo imewezeshwa na Baraza la Kiswahili nchini Tanzania (BAKITA) na imeandaliwa taasisi ya ushauri wa masuala ya maendeleo ya raslimali watu (NFT).

NFT ambayo makao makuu yake yapo mjini Kampala, Uganda ina matawi Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.
Wajibu wake mkubwa taasisi hiyo ni kukabilina na changamoto mbalimbali za wafanyakazi kwa kutoa mafunzo yenye kutengeneza manufaa kwao na kwa menejimenti ya uhuru na kutegemeana katika kufanikisha maono ya taasisi husika.

Kutumika kwa kitabu hicho chenye kurasa 380 kwa kuangalia tabia zenye manufaa kunatokana na haja ya kubadilisha mfumo wa uongozi na ushirikishaji wenye lengo la kuchochea kutegemeana katika kuleta ufanisi.
DSC_0278
Pichani ni kikundi cha burudani kutoka Tanzania House of Talent (THT) wakitumia sanaa "Choreograph" kuzindua rasmi kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
DSC_0291
DSC_0303
Sasa kimezinduliwa rasmi.
DSC_0252
Mratibu wa shughuli ya uzinduzi wa kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People"kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kutoka JB's PR & Events, Babbie Kabae akifafanua jambo kwa wageni waalikwa (hawapo pichani).
DSC_0061
Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa ambao ni maafisa rasilimali watu na wadau kutoka makampuni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo.
DSC_0055
DSC_0100
DSC_0103
DSC_0106
DSC_0379
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images