Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 49 | 50 | (Page 51) | 52 | 53 | .... | 1897 | newer

  0 0
 • 03/18/13--23:52: kutoka zanzibar leo.
 •  Usalama wa Abiria na kufuata sheria ni suala muhimu na linalopaswa kuzingatiwa kwa madereva,pichani Askari wa usalama barabarani wakifanya ukaguzi wa magari yaendayo shamba kuhakikisha usalama kwa abiria.
  Haki za Wanyama zinapaswa kulindwa na kila mtu,kuwatesa Wanyama ni kuvunja maadili na haki za wanyama,pichani vijana wakimlazimisha Ng'ombe kumvisha gari baada ya kugoma.PICHA NA YUSUF SIMAI-MAELEZO.

  0 0
 • 03/19/13--03:04: toto day


 • 0 0


  TAMASHA la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Machi 31, mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, linatarajia kuwanufaisha zaidi watu wenye ulemavu, imeelezwa.

  Akizungumza jijini leo, Mkurugenzi wa Msama Promotions ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama, alisema kuwa malengo yake kwa mwaka huu ni kuhakikisha tamasha hilo linawasaidia walemavu wengi tofauti na miaka iliyopita.

  Msama alisema kuwa nia kuu ya tamasha la mwaka huu ambalo pia litahudhuriwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ni kuhubiri amani na upendo, lakini nchi haiwezi kuwa na amani na upendo kama kuna baadhi ya watu wanataabika.

  “Kauli mbiu ya tamasha la mwaka huu ni amani na upendo, lakini wote tunajua ni ngumu kumuhubiria amani na upendo mtu ambaye anataabika, sasa katika kuhakikisha watanzania wote wanaifurahia amani yao na kuongeza mapendo baina yao, nimepanga kuwasaidia kwa namna yeyote walemavu ili kuwapa nguvu za kuifurahia nchi yao yenye amani,”alisema Msama. Aidha aliongeza kuwa wigo wa kuwasaidia walemavu utaongezeka kulingana na kiasi cha fedha kitakachopatikana.

  Tamasha la mwaka huu limeonekana kukubalika na jamii kubwa ya watanzania kutokana na kauli mbiu yake, lakini pia utaratibu wa kuwapa nafasi watanzania kuchagua mikoa na wasanii watakaopamba tamasha umekubalika na wengi hali iliyolifanya tamasha hilo kuwa la watu wote bila kujali dini, rangi ama kabila.

  Wanamuziki wa Injili wanaotarajiwa kupamba tamasha hilo ni  Sipho Makhabane wa Afrika Kusini, Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa ambaye raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi nchini  Kenya, pamoja na kwaya ya Ambassadors of Christ yenye makazi yake Kigali nchini Rwanda.

  Kwa upande wa wasanii wa hapa nchini watakaotumbuiza ni Upendo Kilahiro,  Rose Muhando, Upendo Nkone, John Lissu, kwaya ya Kinondoni Revival na kundi la Glorious Celebration.

  Tamasha la Pasaka hilo pia litafanyika katika mikoa ya Mbeya ambapo litaendelea Aprili Mosi kwenye Uwanja wa Sokoine, Aprili 3 litafanyika katika Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 litakuwa kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. 

  0 0

   Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabia nchi kwa Njia ya Asili kwenye ukumbi wa Mkutano Ofisini Mtaa wa Luthuli Mjijini Dar es Salaam, Kulia Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Sazi Salula kushoto Mkurugenzi Msaidizi Mazingira Bw Richard Muyungi
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Kuhimili  Mabadiliko ya Tabianchi kwa Njia ya Asili Mkutano huo Umefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisini Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam, Kulia Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Sazi Salula. [Picha na Ali Meja]

  0 0  Ofisa wa polisi jamii Tarafa ya Moipo Mkoani Manyara,Amiri Mlemba akikabidhi mpira kwa mabingwa wa soka wa Wilaya ya Simanjiro,timu ya Middle Age ya Mji mdogo wa Mirerani kwenye uwanja wa Barafu.(picha na woinde shizza,manyara.

  0 0
 • 03/19/13--06:03: Tuzo ya shukurani
 • Waziri mkuu mh.Mizengo Pinda akimkabidhi tuzo ya shukrani mkurugenzi wa Tigo Tanzania Diego Gutierrez kwa ajili ya mchango wao katika kuwaletea wananchi huduma ya sms ambayo itawawezesha wananchi kujua hali za figo zao popote walipo kupitia simu zao za mkononi

  0 0


  Rais Jakaya Kikwete akimwagilia maji mti baada ya kuzindua Chuo cha Tehama cha VETA Kipawa jijini Dar es Salaam.


   Picha ya pamoja.
  Rais Kikwete akipewa maelezo ya kazi katika Chuo cha Veta Kipawa.
   Baadhi ya vifaa vinavyotumiwa kufundishia wanafunzi.
   Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Zebadia Moshi akimuonesha Rais Jakaya Kikwete mashine za kisasa zinazotumiwa chuoni hapo.   Mwalimu wa Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Veta Kipawa, Adrian Aloyce akimpa maelezo Rais Jakaya Kikwete wakati wa uzinduzi wa chuo hicho jijini Dar es Salaam.
  Mwalimu wa Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Veta Kipawa, Adrian Aloyce akimpa maelezo Rais Jakaya Kikwete wakati wa uzinduzi wa chuo hicho jijini Dar es Salaam.

   Rais Jakaya Kikwete akibonyeza kitufe wakati wa uzinduzi wa Chuo cha Tehama cha VETA Kipawa jijini Dar es Salaam jana. Kushoto Bolozi wa Korea, Young-Hoon. Kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Shukuru Kawambwa.
   Rais Jakaya Kikwete akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Chuo cha Tehama cha VETA Kipawa jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kulia ni Balozi wa Korea, Young-Hoon na kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Shukuru Kawambwa.   Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Jengo la Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Veta Kipawa jijini Dar es Salaam.

  0 0
 • 03/19/13--06:44: kumbukumbu


 • 0 0


  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) na ujumbe wake wakiwa kwenye semina kuhusu uzoefu wa China katika kupunguza umasikini  vijijini, semina hiyo iliendeshwa na Mkurugenzi wa  Kituo cha Kimataifa cha kupambana na umasikini, Profesa  Huang Chenwei (kushoto), katika hoteli ya Wanshou, Beijing, China, Machi 19, 2013. Wengine ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia), Kulia kwa Kinana ni, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Yusuf Yusuf na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China  kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC. (Picha na Bashir Nkoromo).

  MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Ai Ping, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa China ( kulia) akiendesha semina kwa kuhusu ujenzi wa vyama vingi katika mazingira ya utandawazi, kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kushoto) na ujumbe wake wa viongozi 14 wa CCM, leo Machi 19, 2013. Semina hiyo ilifanyika katika Ofisi za Mambo ya Nje ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC). Viongozi wa CCM kutoka kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Yusuf Mohamed Yusuf, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela na Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi.  Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China  kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC.

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP), Ai Ping, Kinana alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Mambo ya Nje ya chama cha CPC, mjini Beijing, China, Machi 19, 2013. Kinana ambaye aliwasili kwenye Ofisi hizo na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China  kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC. 
  Katibu wa NEC ya CCM,  Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP), Ai Ping, alipowasili na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Mambo ya Nje ya chama cha CPC, mjini Beijing, China, Machi 19, 2013. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China  kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, wakibadilishana mawazo, baada ya semina kuhusu uzoefu wa China katika kupunguza umasikini, iliendeshwa na Mkurugenzi wa  Kituo cha Kimataifa cha kupambana na umasikini, Profesa  Huang Chenwei, katika hoteli ya Wanshou, Beijing, China, Machi 19, 2013. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China  kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC. (Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0


  WANAJUMUIYA WA AFRIKA MASHARIKI WACHUANA KWENYE KIPINDI CHA KWANZA KABISA CHA GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™!
  *KIPINDI CHA KWANZA CHA MCHEZO HUU WA KUSISIMUA WAANZA TAREHE 20 MWEZI HUU*

  MACHI 19, 2013 Dar es Salaam – Wakati umewadia tena wa kushuhudia mapambano katika kipindi ukipendacho cha Televisheni na kinachotambulika kama, “The GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™”, ambacho kinarudi kwenye runinga yako wiki hiii tarehe 20 mwezi huu wa tatu.

  Mwaka huu watazamaji watapata nafasi ya kuangalia mchuano huu wa kipindi hiki katika televisheni mbili ikiwemo televisheni ya ITV na Clouds TV ambazo zitarusha kipindi hiki kwa muda tofauti tofauti siku hiyo ya Jumatano.

  Ikumbukwe kwamba mamia ya vijana kutoka kona mbali mbali nchini walichuana vikali hapo leaders club ambapo walikua na nafasi ya kuweza kuingia kwenye shindano ambalo lingewawezesha kujishidia kitita cha dola za kimarekani $250,000. Kipindi hiki cha televisheni kinachotazamwa na wengi barani Afrika kimerudi tena kwa kishindo na kwa sasa kitakuwa kinashirikisha nchi za barani Africa. Washiriki watakuwa kutoka nchi za Cameroun, Ghana, Kenya, Tanzania and Uganda na washindi wa mwisho
  kabisa watajipatia tuzo ya ‘Pan-African champions.’

  Washiriki wote watapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na kwamba wanaweza kuwakilisha nchi zao ipasavyo . GUINNESS ilipigania kutafuta kwa hali ya juu washiriki walio na uwezo mkubwa na waliokuwa tayari kuonyesha vipaji vyao na ujasiri kwenye mchezo wa soka. Timu zote zitashiriki kwa vipaji na kwa uelewa wa soka yaani kwa kiingereza, ‘Skill and Knowledge’ . Kwa hivyo kila timu ina washiriki wawili. Mmoja kwa maswala ya uelewa na mwingine kwa suala zima la kipaji.

  Kwa kuanza kabisa, watanzania waliofuzu kusafiri watakutanishwa wenyewe kwa wenyewe jukwaani, na kupewa maswali na nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kwenye soka. Baada ya hapo watakaothibitisha kuwa wapo juu zaidi kwa asilimia mia, watapata nafasi ya kuingia kwenye shindano lenyewe wakipewa dhamana ya kubeba bendera ya nchi yao. Wengine watarudi nyumbani.

  Usikose kipindi cha kwanza kabisa ambacho kitarushwa hewani na televisheni ya ITV saa tatu na dakika kumi na tano usiku na Clouds TV saa mbili na dakika kumi na tano usiku siku ya jumatano tarehe 20 machi mwaka huu. Katika kipindi hiki, tutapata nafasi ya kushuhudia timu yetu ikichuana vikali katika raundi ya kwanza.  Timu kwenye raundi ya kwanza :

  Timu ya bluu – Tanzania:
  • Kutoka Dar es Salaam, Daniel Msekwa, ndiye kiongozi kwenye maswala ya maswali
  yanayohusiana na soka, Mwalimu Akida Hamad, naye ataonyesha kipaji kwa kucheza . Daniel
  ni mfanyakazi wa shirika la bandari Tanzania yaani TPA na Mwalimu bado ni mwanafunzi wa
  chuo cha elimu ya juu. Wote wanakubali kwamba mchezo huu umewapa nafasi vijana wengi
  kuonyesha vipaji vyao na kwamba unainua soka sio kwa kucheza tu bali na kuwa na uelewa
  kuhusu mchezo mwenyewe. Je wataweza kuendelea kwenye hatua ya pili?
  Timu Nyekundu – Kenya:
  • Hawa wapenzi wa michezo mmoja ni Michael Kirwa, na mwenzake ni mwalimu wa mazoezi
  yaani ‘fitness trainer’ Stephen Githinji, wote wa jiji la Nairobi. Michael yupo hapa kwa
  maswala ya kujibu maswali yani uelewa wa soka naye Stephen ndiye atakayeonyesha vipaji
  kwa kucheza .
  Timu ya kijani – Uganda:
  • Oscar Boban na Kennedy Andindu, wanatokea kampala na ndio watakaoakilisha Uganda
  katika hiki kipindi cha kwanza. Oscar ni mfanyabiashara na ndiye atakayekuwa mshiriki wa
  uelewa na kennedy ambaye ni mpenzi wa Arsenal .Yeye atakuwa jukwaani kuonyesha kipaji
  chake.
  Timu Nyeusi – Kenya:
  • Daniel Muthendu, ni mhasibu na amekili ni mpenzi mkubwa wa soka na kujiamini kuchuana
  kwenye maswali yote yanayohusu mpira huu wa miguu. Mwenzake ni Oscar Litonde, ambaye
  ni mchezaji wa mpira, mechi za kirafiki jijini Nairobi. Hawa nao pia watachuana vikali na timu
  tajwa hapo juu.

  Wapenzi wa kipindi hiki cha Guiness football challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba nao
  wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa
  katika tovuti ya m.guinnessvip.com kwa kupitia simu ya mkononi na kompyuta zao.

  Pia GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ina kurasa ya Facebook page www.facebook.com/guinnesskenya
  Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri, unatakiwa kuupenda ukurasa huu yaani ‘like’ na utakuwa unapata
  habari zote kama zinavyotiririka.

  GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya
  kimataifa ya Endemol iliyopo Afrika Kusini. Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga
  yako.

  Usisahau kuwa na kinywaji chako ukipendacho cha Guiness wakati unaangalia kipindi hiki.

  *Haiuzwi kwa walio na Umri chini ya miaka kumi na nane. Tafadhali Kunywa kistarabu.

  *MWISHO*

  0 0   Tunu Kavishe head corporate affairs barclays adressed press conference today acompanied by Samuel Mkuyu head of Products and channels on her left and on her right is mr Valence Luteganya Liability and products development manager
  ========  ========  ======= =======
  Barclays Tanzania today launched Barclays Internet banking, tabloid banking and mobile banking.

  Speaking at the press conference today, Mr Samuel Mkuyu, Head of Products at Barclays Bank Tanzania said Barclays Internet Banking is a unique online platform that enables our customers to carry out their everyday banking transactions and pay for their utility bills over the Internet anytime, anywhere conveniently and securely.

  Barclays Internet Banking can be accessed via www.barclays.co.tz.  Another services launched today is Barclays Tabloid Banking (BTB) which is Internet Banking provided via Applications supported by Android (Samsung Galaxy tabs) and i-OS (iPads).

  BTB bears the same functionality as Barclays Internet for Retail (BIR) except, that it does not allow self registration and only supports payments to billers and, or beneficiaries already added as payees in the users profile.

  The third services launched today is the Barclays Mobile Banking (BMB) this is Internet Banking that is provided via Applications supported by Android (Samsung Galaxy phones) and i-OS (iPhones). BTB bears the same functionality as BIR except, that it does not allow self registration and only supports payments to billers and, or beneficiaries already added as payees in the users profile…he added….

  Commenting on these new services offered by Barclays Tanzania, Barclays Tanzania Corporate Affairs Head Mrs Tunu Kavishe said with the features/Benefits outlined above, Barclays Internet Banking takes the lead in the market in provision of the most innovative digital banking solutions in Tanzania.

  This is not to mention that it is free. It goes without saying that Internet banking forms our Unique Selling Proposition as Retail. To support Internet banking, Barclays Operation Client (BOC) has been deployed for use at the branches and with customer service. With this in place, Branches can capably attend to all customer queries and complaints and resolve them.

  Barclays Bank Tanzania Managing Director, Kihara Maina said: “As part of the Barclays Africa Group, we will continue to play an important role in the country to ensure that the benefits of Africa’s growth story are realised by the people of Tanzania.”

  0 0


  Sensei Rumadha Fundi (Romi)( ( 3rd Dan black belt)
  Sensei Rumadha Fundi (Romi)( 3rd Dan black belt), akiwajibika katika semina ya karate Dojo ya Sugarland, Texas USA katika seminar ya walimu wa karate (ma-sensei) wiki iliyopita chini ya uongozi wake Sensei Ramon Veras (7th Dan), wa Traditional Okinawan Goju Ryu Karate-Do.  Sensei Rumadha ni mmoja wa walimu wa Kitanzania wa karate ambao wanafanya vizuri katika fani hii ughaibuni, ni matumaini yetu wahusika katika sekta ya michezo hasa upande wa mapambano kama ngumi, kick boxing, judo nk wataangalia uwezekano wa kupata mchango wao ambao unaweza kusaidia katika kuboresha wanamichezo wetu kufikia kiwango cha kimataifa na kuliletea sifa taifa letu. GFAMILY Blogger.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau (wa pili kushoto) akiangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni wakati Kamati ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea mradi huo leo. Kushoto ni Mhandisi wa NSSF, John Msemwa.

   Kamati ya Bunge ya Miundombinu ikiangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.
   Mafundi wakiwa kazini.
   Mafundi kazini.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Peter Selukamba (kushoto) akiwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi wa Ujenzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.

   Hapa moja ya za daraja la Kigamboni itawekwa hapa.
   Mhandisi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Karim Mattaka akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi wa daraja la Kigamboni. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Peter Selukamba. 

   Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu akiwa na Ofisa wa Trafic, Peter.
   Mhandisi wa NSSF, John Msemwa akitoa ufafanuzi wa maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni kwa Mkufugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhan Dau (kulia)
   Zege ikimiminwa katika moja ya nguzo za daraja hilo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Peter Selukamba (kushoto) akiwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi wa Ujenzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam leo.


  Mkurgenzi Mkuu wa Shirika la taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhani Dau akifafanua jambo mbele ya wajumbwe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu walipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi wa daraja la Kingamboni jijini Dar es Salaam leo. 
   Mhandisi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), John Msemwa akitoa mada wakati Kamati ya Bunge ya miundombinu ilipotembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni..
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge akizungumza wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi wa Ujenzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

   Picha ya Marehemu enzi za uhai wake.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa askari wa Usalama Barabarani, WP Elikizaeli Lokisa Nnko, aliyefariki dunia kwa kugongwa na gari na dereva ambaye hadi sasa hajajulikana wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi eneo la Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam leo. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Prince David, mtoto wa aliyekuwa askari wa Usalama Barabarani, marehemu WP Elikizaeli Lokisa Nnko, aliyefariki dunia kwa kugongwa na gari na dereva ambaye hadi sasa hajajulikana wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi eneo la Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam leo.
   Kutoka (kulia) ni Mume wa Marehemu, David Erasto Luharara, watoto wa marehem, Prince David na Abdulhaman David, wakiwa na huzuni.

  Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu kuomboleza msiba huo.

  0 0

  Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde zinaeleza kuwa  yule dereva aliyemgonga askari polisi wa usalama barabarani WP 2493 CPL-Elikiza  Lokisa Nko na kutokomea, amekamatwa jana usiku masaa kadhaa baada ya kupoteza uhai wa askari huyo maeneo ya Bamaga mapema jana mchana.

  Kwa Mujibu wa Mkuu wa Kikosi cha Polisi cha Usalama barabarani nchini, Kamanda Mohamed  Mpinga amesema leo kuwa gari lilohusika kwenye ajali hiyo aina ya Landlover Discovery rangi nyeusi limepatikana likiwa limefichwa maeneo ya Tabata dampo jijini Dar.

  Kupatikana kwa gari hilo kumekuja baada ya Polisi kufuatilia na kujua mmiliki wa gari hilo kuwa ni kanisa la TAG chini ya Mchungaji Wambura, ambaye kwa ushirikiano alioutoa dereva aliyetambuliwa kama Jackson Stephen, alijulikana na hatimaye kupatikana

  Kamanda Mpiga ametoa taarifa hiyo mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete jioni hii nyumbani kwa Marehemu hukoUnunio kiasi cha kilomita 25 hivi Kaskazini mwa jiji la Dar. 
  Rais Kikwete pamoja na uongozi wa juuu wa jesgi la polisi walifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu ambaye ameacha  Mume na watoto watatu. Mume wa marehemu pia ni askari polisi.

  Pichani juu Rais Kikwete akimfariji mume wa marehemu na watoto wake pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saidi Mwema.

  0 0

    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha historia ya Uuguzi na Ukunga nchini wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania  katika bustani ya Mnazi Mmoja leo Machi 19, 2013
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiondoka kufungua rasmi Maabadara ya kisasa ua Uhandisi Jeni (Genetic Engineering) katika kituo cha utafiti wa Kilimo cha Mikocheni jijini Dar es salaam leo Machi 19, 103. Kushoto ni Dkt Chrtistopher Chiiza na wa pili kulia ni Mku wa kituo hicho Bw. Joseph Ndunguru

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku medali mmoja ya wauguzi wakongwe nchini aliyewahi pia kuwa Mbunge na Msajili wa Wauguzi na Wakunga Mama Jitto Ram  wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya Baraza la Uuguzi na Ukunga katika bustani ya Mnazi Mmoja leo Machi 19, 2013.

  PICHA NA IKULU

  0 0
 • 03/19/13--14:09: Article 11

 • 0 0

  Prof Japhet Killewo, a medical doctor and Epidemiologist from Muhimbili University, speaks to experts who convened on Monday to share research findings and discuss meaningful policies to address maternal and newborn health in Tanzania. The meeting was sponsored by the United States Agency for International Development (USAID) and organized by partners within the Ministry of Health and Social Welfare, Muhimbili University, Johns Hopkins University and Jhpiego. The workshop was held in Dar es Salaam from Monday. 
  Assistant director, Reproductive and Child Division in the ministry of Health and Social Welfare, Dr Neema Rusibamayila specks during a two days workshop on evaluation of the integrated maternal and newborn healthcare programme in Morogoro by the Muhimbili University of Health and Allied Sciences and the Johns Hopkins University in partnership with the Ministry of Health and Social Welfare, whose target is to reduce maternal and infant mortality. The workshop was held in Dar es Salaam from Monday.
  Mainen Moshi, Director of research and publications at Muhimbili University of Health and Allied Sciences specks during a two days workshop on evaluation of the integrated maternal and newborn healthcare programme in Morogoro by the Muhimbili University of Health and Allied Sciences and the Johns Hopkins University in partnership with the Ministry of Health and Social Welfare, whose target is to reduce maternal and infant mortality. The workshop was held in Dar es Salaam from Monday.
  Jackie Gayle, USAID/Tanzania Community Care Advisor, giving a keynote address on behalf of USAID, during a two days workshop on evaluation of the integrated maternal and newborn healthcare programme in Morogoro by the Muhimbili University of Health and Allied Sciences and the Johns Hopkins University in partnership with the Ministry of Health and Social Welfare, whose target is to reduce maternal and infant mortality. The workshop was held in Dar es Salaam from Monday.
  A section of experts who convened on Monday and Tuesday to share research findings and discuss meaningful policies to address maternal and newborn health in Tanzania, follows the proceedings keenly. The meeting was sponsored by the United States Agency for International Development (USAID) and organized by partners within the Ministry of Health and Social Welfare, Muhimbili University, Johns Hopkins University and Jhpiego. The workshop was held in Dar es Salaam from Monday.
  =========  =======  ========
  By Correspondent

  Though the government is making significant efforts to reduce maternal and child mortality, expectant mothers have continued to die, a situation that delays the country from attaining the fifth Millennium Development Goal (MDG5)
  .
  This was revealed on Monday by the assistant director, Reproductive and Child Division in the ministry of Health and Social Welfare, Dr Neema Rusibamayila, during a two days workshop on evaluation of the integrated maternal and newborn healthcare programme in Morogoro by the Muhimbili University of Health and Allied Sciences and the Johns Hopkins University, whose target is to reduce maternal and infant mortality.

  According to the Tanzania demographic and health survey, more than 454 mothers die from pregnancy-related complications for every 100,000 live births. However, Dr Rusibamayila said this is because women have not considered the importance of visiting health facilities during pregnancy, at delivery and afterwards.

  She said, so far, it is only 43 per cent of expectants who visit clinics at least four times before delivery and that only 50 per cent give birth at health facilities and under the supervision of a professional midwife. But this is due to the fact that still only 43 per cent repeat the visits up to four times.

  However, even for women who feel they do not have any sign of complication during pregnancy, there are still unexpected conditions which can arise during delivery and that could lead to death. But only 50 per cent of mothers give birth at health facilities,” said Dr Rusibamayila. Reading a speech to launch the workshop on behalf of deputy minister for Health Seif Rashid, Dr Rusibamayila said the government would continue to demonstrate a strong political commitment to achieving health-related millennium development goals 4 and 5.

  However, there is still significant work that needs to be done to achieve these goals. She said, though the under-five mortality has declined to 122 deaths per 1, 000 live births, up to 47 per cent of children that die in the country do so at the neonatal period or within the first month of life.

  For her part, the principal investigator on evaluation of integrated maternal and newborn healthcare programme in Morogoro, Prof Japhet Killewo, a medical doctor and Epidemiologist who is overseeing the study on behalf of Muhimbili University, said pregnant women make their first visits to facilities later than recommended.

  However, many are discouraged by the long times they need to spend waiting to be seen, lack of drugs and test kits in some health facilities. As a result, many of them do not return to clinics to receive valuable services that could be beneficial for their health and that of their unborn babies.

  “We have discussed extensive research and valuable policies,” said Prof. Killewo adding,  “Today we have presented findings that we hope will spark countrywide discussion on how to best address opportunities in meeting women’s needs during pregnancy, at birth in the months following birth.”
  “There are also positive points that merit mention,” said Dr. Rose Mpembeni of Muhimbili University, who presented at the conference.

  “We see that women generally report good feelings about the integration of many services – including HIV services – during antenatal visits. Among HIV-positive women, we have noted that patient-provider relationships are strong. In terms of supplies within facilities, we observed that supplies of commodities such as family planning products and HIV test kits are, in many facilities, good,” she said.

  0 0


   Mkurugenzi wa Programu na Miradi toka TANEXA, Nyandallo Mboyi akiwa katika semina hiyo
   Moja ya gari la mizigo likifanyiwa ukaguzi wa nyaraka kwenye beria kabla ya kuingia Tanzania.
  Moja ya beria zilizopo eneo la Kyaka
  ======  ======  ======
  Na Mwandishi Wetu, Bukoba

  SHIRIKISHO la Wasafirishaji Bidhaa nje ya nchi (TANEXA) wamelalamikia kukithiri kwa vituo vya ukaguzi wa magari (beria) na mizigo vilivyopo barabarani, unapoingia na kutoka Tanzania kupitia mpaka wa Tanzania na Uganda (Mtukula). Eneo lilalolalamikiwa zaidi ni kutokea Mtukula hadi Bukoba mjini ambapo kuna wingi wa vituo njiani. 

  Akizungumza katika semina ya wadau wa biashara juzi mjini Bukoba, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wasafirishaji Bidhaa Nje ya nchini (TANEXA), Mtemi Naluyaga alisema wingi wa beria umekuwa kikwazo cha wafanyabiashara huku baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu wanaohudumia katika vituo hivyo wakijenga mazingira ya rushwa kwa wanachama wao.

  Akifafanua zaidi alisema baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) wanaohudumu katika vituo hivyo nao wamekuwa wakivitumia vituo hivyo vibaya kwa kutoza faini za juu pale wasafirishaji wa bidhaa na abiria wanapobainika kuwa na makosa, jambo ambalo humlazimu mtozwa faini kutafuta mbadala wa kukwepa faini hivyo kujengeka mazingira ya rushwa kirahisi.

  Aliishauri Serikali kuifanya Mtukula kuwa kituo Kikuu cha Ukaguzi wa Bidhaa zinapoingia na kutoka nchini na kukifuta kile cha Kyaka ambacho kwa sasa kinafanya kazi moja na inayofanywa na kile cha Mtukula mpakani, jambo ambalo alisema ni usumbufu kwa wafanyabiashara wanaotumia mpaka huo.

  "Kutokea Mtukula hadi Bukoba Mjini kuna beria 9 upande wa Tanzania, lakini ukiingia Uganda hadi mjini kuna beria moja...na kibaya zaidi ukiangalia beria hizi nyingine zinafanya kazi sawa na beria zingine huu ni usumbufu kwa wafanyabiashara. Alishauri Serikali kupitia mamlaka husika kujipanga na kuweka beria moja eneo la Mtukula na kuimarisha uteandaji ili kituo hicho kifanye kazi ya beria zote.

  Kwaupande wake Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wanawake Mpakani mwa Tanzania na Uganda (IWCBTA), Mtukula, Jane Charles alisema akinamama wamekuwa wakinyanyaswa na kutishiwa na baadhi ya watendaji katika beria hizo jambo ambalo limekuwa vikwazo katika ufanyaji biashara zao.

  Akizungumza katika semina hiyo, Mjumbe wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi ya mikoani (TABOA), Wilaya ya Bukoba, Eliud Rumanyika alipinga kitendo cha wafanyakazi wa TRA kuyashikilia baadhi ya magari ya wanachama wao kwa makosa ya abiria pindi inapotokea abiria kaingia na mzigo ambao umekuwa na tatizo mpakani. "...Sisi tunaona si haki kwa baadhi ya watendaji wa TRA kwenye vituo vya ukaguzi kuamua kuyashikilia magari yetu kwa kosa la abiria, abiria anapokutwa na kosa mpakani atozwe faini mwenyewe na si kushikilia gari la abiria hii ni usumbufu kwa wengine na wamiliki," alisema Mjumbe Rumanyika.

  Akijibu baadhi ya hoja katika semina hiyo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Nassoro Mnambila alisema Serikali ya Mkoa wa Kagera haiungi mkono hoja ya baadhi ya wafanyabiashara wanaotaka kuhamishwa kwa beria ya Kyaka kwenda Mtukula kwani uamuzi wa awali ulizingatia masuala mengi ya muhimu katika nyanja anuai.

  "Serikali ya Mkoa wa Kagera haishauri kabisha kuvunjwa kwa kituo cha Kyaka...sisi tunaona ipo haja ya kuangalia namna ya kufanya marekebisho kimaboresho zaidi. Watu wachache wasituharibie maana ya kuweka kituo kile (Kyaka) eneo lile," alisema Mnambila.
  *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0

  Awatungia wimbo maalum watanzania katika tamasha la Pasaka


  HISTORIA ya muziki Duniani, inaonesha kuwa muziki wa makanisani, ambao unajulikana kama muziki wa Injili ndio chimbuko la aina zote za muziki ulimwenguni.

  Hakuna ubishi kuwa kila mwanamuziki mwenye kuujua muziki, ukimuuliza chanzo cha yeye kujihusisha na muziki ni lazima atakueleza kuwa alianzia kwenye kwaya ama kaswida. 
  Hata hivyo pamoja na ukongwe wa muziki huo, bado unaonekana kutopewa nafasi sana kwenye vituo vya redio na Televisheni, labda kutokana na kuegemea dini fulani.

  Pamoja na hilo, lakini pia haujaweza kuwanufaisha wanamuziki wa muziki huo hapa nchini tofauti na wanavyofaidika wanamuziki wa mataifa mengine kama ilivyo nchini Afrika Kusini.  
  Sipho Makhabane ambaye anajihusisha na muziki huo nchini Afrika Kusini  ni mmoja wa wanamuziki wa Injili wenye mafanikio makubwa.


  Makhabane ambaye pia ametajwa kuja nchini kushiriki tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Machi 31, mwaka huu, anamiliki kampuni kubwa ya Big Fish, ambapo kazi yake kubwa ni kukuza na kuibua vipaji vipya vya wanamuziki wa Injili.

  Jina la mwanamuziki huyo ni kubwa barani Afrika, ambapo umaarufu wake umepatikana kutokana na uwezo wake wa kutunga nyimbo zenye ujumbe wa hali ya juu wa kumsifu na kumuabudu mungu.  
  Kutokana na uwezo wake huo mashabiki wengi wa muziki wa Injili wamekuwa wakimfananisha na wanamuziki mahiri kama Joyous Celebration ama Sfiso Ncwane. 


  Makhabane mwenye umri wa miaka 45 ni mmoja wa magwiji wa uimbaji nchini Afrika Kusini, ameshiriki katika shughuli mbalimbali za kiroho na kijamii.  
  Kutokana na kutingwa na shughuli zake mwaka 2010 alitangaza kuachana na kazi ya kuimba, hata hivyo mwaka 2012 aliushangaza ulimwengu kwa kuachia albamu yake mpya iliyokubalika na watu wengi. Historia ya maisha yake inaonesha kuwa ni mtu aliyekulia katika muziki huo.


  Kutokana na ugumu wa maisha uliokuwa ukiikabili familia yake, Makhabane alilazimika kuacha shule akiwa darasa la tano na akiamua kufanya kazi katika shamba la miwa la Kaaruls huko Mpumalanga kama ilivyokuwa kwa mwimbaji mwingine nguli Rebecca Malope.  
  Makhabane alifanya hivyo walau aweze kupata fedha ya kuwasaidia wazazi wake pamoja na ndugu zake ambao walikuwa wakimtegemea yeye.

   Alipotimiza  miaka 17, alihamia kwenye kazi za ujenzi kwenye Hifadhi ya Taifa ya Afrika Kusini ya Kruger. 
  Akiwa huko alifanya kazi ya kuwasaidia mafundi waliokuwa wakijenga nyumba kambini hapo na alipotimiza miaka 21 alikuwa tayari na ujuzi wa kutosha katika kazi ya ujenzi na akapata kazi katika eneo la Pienaar. 

  Mwaka 1986, Makhabane alipata ofa nzuri katika kampuni ya Telkom kama fundi, lakini katika kuhangaika kwake alijikuta akiishia kwenye muziki wa Injili. 
  Hata hivyo hakuwa akijua kuwa nyota ya mafanikio yake ilikuwa kwenye huduma hiyo ya uimbaji na badala yake alikuwa akifanya muziki wa kujifurahisha zaidi na si wa biashara. 

  Mwaka 1990, wakati huo akiwa na umri wa miaka 25, Makhabane alifunga ndoa na binti aliyekuwa na umri wa miaka 18.  Baada ya hapo ndipo alianza kazi ya kununua na kuuza kazi za muziki ndani na nje ya nchi ya Afrika Kusini.  
  Kutokana na kuona muziki umeanza kuingia kwa kasi kwenye akili yake, Makhabane aliamua kuachana na kazi ya ufundi mitambo ya simu na kujikita kwenye muziki.

  Katika kuhakikisha anaingiza kipato mwanamuziki huyo aliamua kusambaza kazi zake mwenyewe , lakini kikwazo kwake kikawa ni namna ya kuwavutia wasambazaji waliokuwa tayari kununua kazi kutoka kwake. 
  Kazi yake iliyomfanya kukubalika ilianza kusikika kwenye redio ya Swazi ambayo inajulikana zaidi kwa jina la Ligwalagwala FM, ambapo kibao kilichomtambulisha ni kile cha Ngitinikela Kuwe.

  Hatimaye mwaka 1996, Makhabane aliamua rasmi kuifanya kazi hiyo ya muziki wa Injili na kuacha kazi aliyokuwa akiifanya kwenye kampuni ya simu.

   Mwaka huo huo aliachia album yake iitwayo “Yek’intokozo” wimbo ambao mpaka leo unakumbukwa na mashabiki wake kwani ndio ulimtambulisha vema, ingawa tayari alishatoa album nyingine mbili miaka ya 1993 hadi 1999 za ‘THUM’UMLOLO” na “JESU ULIQHAWE”. 

  Mwaka 1998, kupitia kampuni ya CCP Records aliachia album yake ya nne iitwayo “Uyigugu” iliyofanya vema kabla ya mwaka uliofuata kuachia nyingine iitwayo “Makadunyiswe,”. 

  Mwaka 2001, alifyatua album ya Calvary ambayo iliuza kufikia kiwango cha juu na mwaka uliofuata  (2002), aliachia albamu  nyingine ya ‘Akukhalwa’ ambayo ilitikisa kama album ya “Yek’intokozo,” akiuza zaidi ya nakala 70,000.  Mwaka 2003, Makhabane aliachia album ya ‘Moya wami’ ambayo pia iliuza zaidi ya nakala 70,000. 

  Kutokana na umahiri wake, Makhabane ameweza kushirikishwa katika album na waimbaji wakongwe wa nchini kwake kama Jabu Hlongwane, Marehemu Vuyo Mokoena, Lundi, Hlengiwe Mhlaba na wengine wengi. 

  Pia akiwa nyuma ya mafanikio ya waimbaji lukuki kama Hlengiwe Mhlaba, Ncandweni Christ Ambassadors, Shongwe na Khuphuka Saved Group. 

  Nje ya uimbaji, Makhabane ni mtayarishaji wa kazi za muziki wa injili akiwa daraja la waimbaji wengine kutokana na kuwika vilivyo kupitia kazi zao zilizoandaliwa na gwiji huyo. 
  Makhabane ametunga wimbo maalum kwa ajili ya mashabiki wake wa Tanzania.

  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa amezungumza na msanii huyo na amemueleza kuwa amewaandalia zawadi Watanzania kwa ajili ya tamasha hilo.

  “Sipho amefurahi sana kumualika kwenye tamasha letu, amenihakikishia licha ya nyimbo zake za kawaida, lakini pia atakuwa na wimbo maalum kwa Watanzania, amesema anawapenda Watanzania na ameandaa wimbo mzuri ambao ana uhakika mashabiki wataupenda.

  “Mashabiki watakaokuja kwenye tamasha Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Machi 31 watapata fursa ya kumsikiliza msanii huyo pamoja na wimbo wake mpya ambao jina hakunambia lakini amesema ni zawadi nzuri kwa Watanzania,” alisema Msama na kuzitaja baadhi ya nyimbo za msanii huyo kuwa ni Moya Wami, Indonga, Akukhalwa, Over&Over, Nguy’zolo, Yizwa Nkosiseju, Hlalanami Nkosi Jesu, Yek’intokozo, Injabulo, Hlalanami Jesu, Makadunyiswe, Vuka Mphemlo, Mphefumlo na Moya Wami.

  Kuhusiana na maandalizi mengine ya tamasha hilo alisema yanaenda vizuri na kwamba mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kwamba ni matumaini yake mashabiki watajitokeza kwa wingi.

  Licha ya Sipho Makhabane, wasanii wengine wa nje ya Tanzania ambao tayari wamethibitisha kushiriki tamasha hilo ni , Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya na kwaya ya Ambassadors of Christ ya Kigali Rwanda inayotamba na albamu ya Mtegemee Yesu. Wasanii wa Tanzania waliothibitisha hadi sasa ni Rose Muhando, Upendo Nkone na John Lissu, kwaya ya Kinondoni Revival na kundi la Glorious Celebration.

older | 1 | .... | 49 | 50 | (Page 51) | 52 | 53 | .... | 1897 | newer